Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

kutoka Iringa leo:sakata la mtuhumiwa kuiba bangi mahakamani mjini iringa,lachukua sura mpya.

$
0
0

Kufuatia jeshi la polisI mkoani Iringa kutoa taarifa kuwa inamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kukamatwa na  bangi ambayo ameuziwa na mlinzi wa mahakama ya wilaya kutoka mahakamani,Mahakama imekanusha kuwepo na upotevu wa kielelezo cha bangi  au kielelezo chochote kingine katika mahakama.
 
Akizungumza na wandishi wa habari  kaimu msajili wa mahakama ya wilaya  GODFREY  ISAYA amesema kuwa mahakama inasikitika kuwa polisi imetoa taarifa za kuibiwa kwa vielelezo vya mahakama katika vyombo vya habari kabla ya kuwasiliana na uongozi wa mahakama.
 
ISAYA amesema kuwa vielelezo hivyo havikuwepo katika mahakama tayari vilishateketezwa chini ya uangalizi wa afisa wa jeshi la polisi na kesi ya mtuhumiwa huyo ilikwisha tarehe 13 february na mshitakiwa alihukumiwa kifungo cha miaka miwili.
 
Hata hivyo amesema kuwa polisi hawajafika kuufanya uchunguzi wowote juu ya upotevu wa vielelezo hivyo na wala hawajawapa taarifa juu ya kumshikilia mlinzi wao huku wakisema kuwa na mlinzi huyo si wa mahakama ya wilaya kama walivyosema bali ni mlinzi wa mahakama kuu.
 
Aidha ISAYA ameongeza kwa kusema kuwa jeshi la polis linapaswa kufanya uchunguzi yakinifu kwa kila taarifa inayotolewa na si kutoa taarifa bila uchunguzi wowote kama ilivyotokea sasa kwani hawajamuona askali yoyote mpelelezi aliyefika mahakama kuulizia suala hilo.

wanaume waliofanyiwa tohara kupunguza maambukizi ya vvu kwa asilia 60

$
0
0


Imeelezwa kuwa wanaume waliofanyiwa tohara si kweli kwamba hawatapata virusi vya Ukimwi na badala yake kutawasaidia kupunguza uwezekano wa kupata vvu kwa asilimia 60

Hayo yamesemwa na mratibu wa Ukimwi wilaya ya Makete(DAC) Dkt. Shadrack Sanga(pichani) wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusu umuhimu wa tohara ya wanaume wilayani hapo

Amesema kumekuwa na taarifa zilizozagaa kuwa mwanaume akishafanyiwa tohara hawezi kupata VVU  ambapo  amesema taarifa hizo si za kweli na ukweli ni kwamba mwanaume huyo atapunguza asilimia 60 za kupata vvu kuliko yule ambaye hajatahiriwa

"Naomba hili lieleweke wazi, mwanaume ambaye hajafanyiwa tohara na yule aliyefanyiwa wote wanaweza kupata vvu, lakini aliyefanyiwa tohara anaupungufu wa asilimia 60 kupata vvu lakini si kwamba hatapata" alisema

Katika hatua nyingine Dkt. Sanga amesema tangu kampeni ya tohara ya wanaume maarufu kama dondosha mkono sweta ianze rasmi wilayani Makete mwaka 2011 jumla ya wanaume 9,669 wamefanyiwa tohara

Amesema muitikio ni mzuri lakini bado idadi ya wanaume ambao hawajafanyiwa tohara ni kubwa hivyo anatoa wito kwa wanaume kuacha woga na aibu ya kwenda kufanyiwa tohara ambayo ianatolewa bure

Hivi sasa mkoa wa Njombe unaongoza kitaifa kwa kuwa na maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi, ambapo imegundulika kuwa wanaume wengi wa mkoa huo kutofanyiwa tohara ni miongoni mwa sababu kubwa zinazopelekea maambukizi hayo kuwa juu

MAMA TUNU PINDA AWAASA MAKATIBU MUHTASI WAZINGATIE MAADILI YAO

$
0
0

 MKE WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda amewaasa Makatibu Muhtasi na kuwataka wazingatie maadili ya taaluma yao ya uhazili ili kuongeza ufanisi wa majukumu ya kazi zao.



Ametoa wito huo leo mchana (Alhamisi, Mei 16, 2013) wakati akifungua Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.



Kongamano hilo la siku mbili, limehudhuriwa na Makatibu Muhtasi zaidi ya 1,500 kutoka mikoa yote nchini, na baadhi ya wawezeshaji kutoka Kenya, Uganda na Rwanda.



“Umuhimu wa taaluma ya uhazili katika taasisi tunazofanyia kazi unatokana na nafasi  kubwa ya makatibu muhtasi kama wasimamizi wa ofisi na wasaidizi wa watendaji wakuu. Nafasi yenu inawapa fursa ya kuandaa na kutunza nyaraka mbalimbali za kiofisi zinazohusu menejimenti ya taasisi hizo. Niwaombe makatibu muhtasi wote mzingatie maadili ya kazi ya uhazili katika kutekeleza majukumu yenu,” alisisitiza.



Aliwataka waongeze jitihada za kukimarisha Chama cheo ili hatimaye TAPSEA iweze kuenea Mikoa yote na kuwa Chombo kitakachosimamia miiko na maadili ya fani ya Uhazili.



Alisema majukumu ya makatibu muhtasi siyo kupiga chapa pekee na kuongeza kwamba, kama chama cha kitaaluma, TAPSEA lazima iendeleze jitihada za kubadili mtazamo huo ili jamii iweze kutambua umuhimu wa nafasi ya makatibu muhtasi katika taasisi mbalimbali za umma na za sekta binafsi.



“Hata hivyo, napenda ieleweke kwamba kazi ya kuleta mabadiliko ya kimtazamo inaanzia kwa katibu muhtasi mwenyewe. Nawashauri wanachama wote wa TAPSEA wawe mstari wa mbele katika kubadilika kifikra na kujiendeleza kila wakati ili kujijengea uwezo wa kuzikabili ipasavyo changamoto za taaluma ya uhazili katika mazingira ya sasa,” alisema.



Mama Tunu Pinda alisema kuwekeza katika teknolojia ni jambo muhimu lakini teknolojia pekee haiwezi kuleta mabadiliko chanya katika kuboresha huduma na kuongeza tija. “Jambo hili ni lazima liende sambamba na uwekezaji katika rasilimali watu kwa watumishi kusoma zaidi na kupatiwa fursa za mafunzo zaidi ndani na nje ya nchi,” alisisitiza.



Mama Tunu Pinda pia alizindua TAPSEA SACCOS na kuwataka makatibu muhtasi hao wajiunge kwa wingi ili kutunisha mfuko wa chama chao.


Mapema, akimkaribisha kuzungumza na washiriki wa mkutano, Mlezi wa TAPSEA Dk. Mary Nagu ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Uwekezaji na Uwezeshaji aliwataka wawe waaminifu katika kuijenga TAPSEA SACCOS ili hatimaye ifikie hatua ya kuwa benki yao maalum kama ilivyo kwa Chama cha Walimu nchini.



Naye Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Bi. Angela Kairuki ambaye pia mshauri wa Kisheria wa TAPSEA aliwataka washiriki wa kongamano hilo kuzingatia maadili kwa kutunza siri za ofisi wanazozitumikia.


“Inasikitisha kuona kila mara kunakuwa na taarifa ambazo zinavuja lakini ukifuatilia wapi taarifa hizo zimetokea utabaini kuwa chanzo ni makatibu muhtasi... ninawaomba sana mjitahidi kutunza siri za taasisi zenu,” alisisitiza.



IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

ALHAMISI, MEI 16, 2013.

Kutoka Iringa Leo:Mbunge Peter Msigwa awataka machinga waendelee kufanya biashara eneo la mashine tatu mjini iringa.!

$
0
0

Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amewataka  wafanyabiashara  ndogo ndogo (machinga ) mjini Iringa  kuendelea  kufanya kazi katika  eneo la Mashine  tatu  bila  kufanya  vurugu  zozote na kuzingatia usafi wa mazingira.
 
Akizungumza  katika mkutano alioufanya na wanachi katika kata ya makolongoni maeneo ya standi kuu, mbunge Msigwa amesema  kuwa kamwe  machinga  Iringa  wasikubali  kunyanyasika kwani wanahaki ya kufanya kazi zao ilimradi wasivunje sheria .


Amesema kuwa viongozi wamekuwa wakiwatumia wafanyabiashara hao wakati wa kampeni katika kutafuta kura na wakipata uongozi wanawasahau na kuwaona hawana umuhimu kwao.


Hata hivyo msigwa amesema kuwa viongozi wanapaswa kukaa meza moja nakujadili matatizo ya wananchi na si kurumbana na kuvutana huku akilitaka jeshi la polisi kuacha mara moja kuwabugudhi wafanyabiashara hao na badala yake wamfuate yeye.


Aidha ameongeza kwa kusema kuwa hatobadilisha msimamo wake na wafanyabiashara waendelee kufanya biashara katika eneo hilo la mashine tatu huku akiwataka wananchi kuchagua viongozi wanaojali masilahi yao.


Kwa upande mwingine Mbunge  Msigwa amesema  kuwa katibu mkuu  wa CCM kukimbilia katika  vyombo  vya habari  kutishia  kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika  kupelekewa taarifa  ni  sawa na uoga kwani mpaka sasa yeye hana nakala yoyote ya maandishi taarifa anaipatia katika vyombo vya habari.


Msigwa pia amemtaka katibu huyo kumkamata hata leo kwani yuko tayari na sio kusubili siku 21 kama alivyosema kwani  Chadema  ina  mawakili  waliojitosheleza na  kuwa hawatanyamaza kusema  ukweli kwa  kuogopa vitisho vyovyote


RAIS KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA LISHE LEO

$
0
0
 
 Mama Maria Nyerere akifurahia tuzo maalumu aliyopokea kwa niaba ya Baba wa Taifa aliyotunukiwa na Taasisi ya Chakula na Lishe kwa mchango wake mkubwa kwa kukuza na kuendeleza sera ya lishe nchini wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya Lishe Tanzania leo Machi 16, 2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi tuzo maalum iliyotolewa na Taasisi ya Chakula na Lishe kutambua mchango wake mkubwa katika kusimamia lishe na maendeleo yake  nchini  katika uzinduzi wa kampeni ya lishe nchini  leo Machi 16, 2013  katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na kushoto ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua   kitabu cha kampeni ya Lishe Tanzania baada ya kukizindua leo Machi 16, 2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Peniel Lyimo akifuatiwa na Mkurugenzi wa kwanza wa Taasisi ya Chakula na Lishe Mzee Lema. Kushoto ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akisalimiana  kitabu cha kampeni ya Lishe Tanzania baada ya kukizindua leo Machi 16, 2013  katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na kushoto ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere.PICHA NA IKULU

Thamani ya Fedha Kenya 'Yawaachisha' Shule Wanafunzi Rombo

$
0
0

 Sehemu ya Soko la Tarakea, Rombo. Soko hili ni miongoni mwa masoko yaliopo jirani na mpakani wa Kenya na Tanzania wilayani Rombo ambapo wananchi wa pande zote za mpaka huingia na kujipatia mahitaji yao kama wanavyoonekana.
Hizi ni baadhi ya njia zisizo rasmi kwenda nchini Kenya zilizopo eneo la Rongai, Rombo
Mkuu wa Sekondari ya Tanya, Victus Kiwango akizungumza na mwandishi wa www.thehabari.com hivi karibuni wilayani Rombo. 

==========   ========  ===========
Thamani ya Fedha Kenya 'Yawaachisha' Shule Wanafunzi Rombo

Na Thehabari.com, Rombo

KUFANYA vizuri kwa thamani ya fedha ya Kenya (Kshs) tofauti na ile ya Tanzania (Tshs) kumechangia kwa namna moja kuiathiri Wilaya ya Rombo maeneo ya mpakani mwa Kenya na Tanzania kitaaluma kwa kile baadhi ya wanafunzi wa sekondari kuacha shule na kwenda kufanya vibarua vijiji vya jirani.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni mjini hapa kumebaini kuwepo na idadi kubwa ya wanafunzi wa sekondari wa shule za mpakani wanaotoroka shule, ama wengine kuacha shule kuendelea na shule baada ya kumaliza elimu ya msingi hata kama wamefaulu na kwenda kufanya vibarua mpakani kwa kuvutiwa na thamani ya fedha ya Kenya.

Uchunguzi uliofanywa katika sekondari za Ngaleku, Tanya, Holili, Nduweni na Urauri zote zilizopo maeneo ya mpakani mwa Kenya wilayani Rombo umebaini idadi kubwa ya wanafunzi huzikimbia shule kabisa na wengine kufanya utoro wa rejareja wawapo shuleni kwa malengo ya kufanya vibarua mpakani.

Kwa shule ya Sekondari Urauri kati ya wanafunzi 238 waliopangiwa kujiunga na shule hiyo kwa mwaka huu ni wanafunzi 178 tu ndiyo walioripoti huku idadi kubwa ikidaiwa kukimbilia nchi jirani ya Kenya kufanya vibarua anuai zikiwemo kazi za ndani na mashambani kwa kuvutiwa na thamani ya fedha nchini humo.

Licha ya idadi hiyo kutojiunga na shule na kudaiwa kukimbilia Kenya, baadhi ya wanafunzi waliojiunga na shule nao huendelea na utoro wa rejareja hasa kipindi cha msimu wa kilimo, mavuno na palizi na kwenda kufanya vibarua hali ambayo huathiri maendeleo ya kitaaluma kwa shule na wanafunzi.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Holili, Benson Samizi alisema kati ya wanafunzi 140 waliofaulu na kupangiwa kujiunga na shule hiyo kwa mwaka huu ni wanafunzi 85 tu ndiyo walioripoti. Alifafanua kuwa 30 alipata taarifa waliamua kujiunga na shule nyingine huku idadi iliyobaki wakitokomea kusiko julika na shule inaendelea kuwatafuta.

Kwa upande wa Mkuu wa Sekondari ya Tanya, Victus Kiwango alibainisha kati ya wanafunzi 94 waliopangiwa kujiunga na shule hiyo kwa mwaka huu ni wanafunzi 79 tu ndiyo waliripoti shuleni. Aidha alisema utoro pia umeiathiri shule hiyo kitaaluma kwani matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana jumla ya wanafunzi 71 wamepata sifuri, hakukuwa na ufaulu wa daraja la kwanza wala la pili na wanafunzi wawili walipata daraja la tatu huku wanafunzi 18 wakipata daraja nne.

Mzazi mmoja aliyejitaja kwa jina la Protus Shirima alisema si wanafunzi pekee ambao huvutiwa na thamani kubwa ya fedha ya Kenya kwani hata wapo wazazi ambao hukimbilia kufanya vibarua Kenya vijiji vya mpakani kutokana na thamani ya fedha. Alisema kibaya zaidi wapo baadhi ya wazazi ambao huambatana na watoto wao katika vibarua hivyo ili kuongeza kipato cha familia.

"Mi nakushauri jaribu kuja msimu wa kilimo ukichanganya ukae eneo hili (Tarakea) utaona makundi makubwa ya wananchi wakivuka mpakani nyakati za asubuhi kuelekea Kenya kufanya vibarua na kurejea tena jioni...hali hii hufanyika vivyo hivyo wakati wa mavuno na palizi, fedha ya Kenya ipo juu na ndiyo inayotuvutia wengi," alisema Shirima.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rombo, Judethadeus Mboya akizungumzia hali hiyo alikiri kuwepo na wimbi la wananchi kujiushisha na shughuli za mpakani maeneo hayo, japokuwa alisema wameanza utaratibu wa kuwatoza faini baadhi ya wazazi wanaoshindwa kuwazibiti watoto wao kiutoro shuleni kwa kuwatumia viongozi wa vijiji.

Aidha aliongeza kuwa ni vigumu kuwadhibiti wanafunzi kufanya shughuli za mipakani kwa kuwa wanapokwenda maeneo hayo hawaendi na sare za shule, ukiachilia mbali kuwa wapo baadhi ya wanavijiji wa Tanzania pia huendesha shughuli za kilimo nchini Kenya katika vijiji vya jirani.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

MSHINDI WA PROMOSHENI YA VODACOM MAHELA AWASILI JIJINI KUKABIDHIWA KITITA CHAKE CHA SHILINGI MILIONI 100

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu,akimpokea Mshindi wa Droo kubwa ya "MAHELA "Bw.Valelian Nickodemus(22)baada ya kuwasili katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam akitokea Mkoa wa Kigoma kuja kukabidhiwa fedha zake taslimu  kiasi cha shilingi Milioni 100.atakazokabidhiwa hivi karibuni.
 Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu (katikati)akiongea na Mshindi wa Droo kubwa ya "MAHELA "Bw.Valelian Nickodemus(22)(kulia)baada ya kuwasili katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam akitokea Mkoa wa Kigoma kuja kukabidhiwa fedha zake taslimu hivi karibuni kiasi cha shilingi Milioni 100.anaeshuhudia kushoto ni mmoja wa wafanyakazi wa kituo cha mabasi Ubungo.
 Mshindi wa Droo kubwa ya "MAHELA "Bw.Valelian Nickodemus(kushoto) akihojiwa na  mwandishi wa habari wa ITV Emanuel Buhohela mara baada ya kuwasili katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam akitokea Mkoa wa Kigoma mahususi kwa ajili ya makabidhiano rasmi ya fedha zake kiasi cha shilingi Milioni 100 hivi karibuni.Kulia ni  Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakimsikiliza kwa umakiini Mshindi wa Droo kubwa ya "MAHELA "ambaye alijishindia shilingi Milioni 100 Bw.Valelian Nickodemus(22)akiwaelezea jinsi atakavyotumia fedha zake mara baada ya kukabidhiwa rasmi hivi karibuni.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa,akimsikiliza jambo mshindi wa Droo kubwa ya "MAHELA "ambaye alijishindia shilingi Milioni 100 Bw.Valelian Nickodemus(22)baada ya kuwasili makao makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo amekuja kukabidhiwa fedha zake za ushindi.

IMEELEZWA BAADHI YA VIONGOZI NDIYO CHANZO CHA UVUJAJI WA SIRI MAKAZINI NA SI MASEKRETARI.

$
0
0
Mtoa mada iliyohusu Maadili kazini,Bwa.Alex Senzota kutoka Idara ya Usalama Kazini (GSO),akifafanua zaidi kuhusiana na mada iliyohusu Maadili kazini na namna ya kutunza/kuepuka uvujaji wa siri za ofisi husika,mapema leo kwenye Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) uliofanyika ndani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Chama chama cha Makatibu Muhtasi  Nchini Uganda (NASAP),Bi Edith Kutesa Giita akifafanua jambo kuhusiana na mada mojawapo ya iliyohusu Ni namna gani unaweza kuwa Katibu Muhtasi unaekwenda na wakati/wa kisasa,mapema leo kwenye Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) lililofanyika ndani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.

 Mwenyekiti wa chama cha Makatibu Muhtasi  (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA),Bi Pili Mpenda akifafanua jambo mbele ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi  likiendelea ndani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha,kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama chama cha Makatibu Muhtasi  Nchini Uganda (NASAP),Bi Edith Kutesa Giita.


 
Baadhi washiriki wa Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zinazojadiliwa  kwenye kongamano hilo lililofanyika dani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha. 
  Mmoja wa wachangia mada kutoka chuo  cha Sokoine,Bi Teddy Salum akizungumza kuhusiana na mada iliyohusu Maadili kazini na namna ya kutunza/kuepuka uvujaji wa siri za ofisi,wakati Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) likiendelea ndani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
 Mmoja wa wachangia mada kutoka chuo Kikuu cha Dar- Es Salaam (UDSM),akifafanua jambo kuhusiana na mada iliyohusu Maadili kazini na namna ya kutunza/kuepuka uvujaji wa siri za ofisi,wakati Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) likiendelea ndani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zinazojadiliwa  kwenye kongamano hilo lililofanyika dani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.

=============  =======  ===========

IMEELEZWA VIONGOZI NDIYO CHANZO CHA UVUJAJI WA SIRI MAKAZINI NA SI MASEKRETARI.

Suala la uvujaji kwa siri kwa baadhi ya sehemu kubwa ya maofisi makazini,imeelezwa kuwa chanzo kikubwa ni viongozi na si makatibu Muhtasi kama ambavyo baadhi  ya watu  wamekuwa wakieleza.


Hayo yameelezwa leo kwenye siku ya pili ya Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) uliofanyika ndani ya  ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.


Akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali, mtoa mada iliyohusu Maadili kazini,Bwa.Alex Senzota kutoka Idara ya Usalama Kazini (GSO),alipata wakati mgumu wa kujibu maswali kutoka kwa washiriki wa kongamano hilo kuhusiana na mada hiyo iliyozua mjadala mkubwa ukumbini humo.


Mmoja wa washiriki katika kongamano  hilo aliyejitambulisha kwa jina la Teddy Salum kutoka chuo cha Sokoine,alieleza kuwa tatizo kubwa la uvujaji siri kwa asilimia kubwa linatokana na Viongozi wenyewe kutokana na itikadi zao za kisiasa ama ya kutaka umaarufu.


Aidha Mshiriki Mwingine alibainisha kuwa tatizo hilo la uvujaji siri maofisini linatokana na  baadhi ya viongozi a.k.a MABOSS kutozingatia/kupuuza ama kutokuwa na maadili ya kazi katika kuhakikisha siri za ofisi husika zinatunzwa ipasavyo,ili kulinda usalama wa ofisi husika.


Mtoa Mada wa Maadili kazini,Bwa.Alex Senzota alifafanua kuwa kutokana na tatizo hilo kubainika kuwa kubwa katika kongamano hilo,kuna haja ya Serikali kuangalia mfumo mzima wa kuhakikisha maadili ya kazi yanazingatiwa katika Nyanja zote zote,hasa kwa watumishi wa umma.


Kongamano hilo la siku mbili, limehudhuriwa na Makatibu Muhtasi zaidi ya 1,500 kutoka mikoa yote nchini, na baadhi ya wawezeshaji kutoka Kenya, Uganda na Rwanda.

kutoka Iringa leo:waandishi wa habari mkoani iringa waaswa kufanya kazi zao kwa uhuru

$
0
0

Waandishi wa habari mkoani Iringa wameaswa kufanya kazi zao kwa uhuru bila kumuongopa mtu yoyote kufuatia vitisho wanavyovipata katika utendaji wao wa kazi.

Akizungumza,Mbunge wa  jimbo la Iringa Mjini,Mchungaji Peter Msigwa amesema kuwa kwa sasa wandishi wa habari wamekuwa katika wakati mgumu kwenye utendaji wao wa kazi kutokana na vitisho wanavyovipata juu ya kazi wanazofanya kutoka kwa viongozi mbalimbali.


Amesema kuwa mwandishi wa habari wanahaki ya kupata habari mahali popote pale bila kubugudhiwa, kwani ni haki yao ili mradi wanafuate sheria na maadili yanayoendana na kazi yao.


Aidha amesema kuwa kutokana na kuwa amepata taarifa zinazohusu majina ya waandishi saba mkoani Iringa  ambao wako hatarini kutokana na kuandika habari zake,amewataka waandishi hao pia kufanya kazi yao kwa amani na yuko pamoja nao.

Taarifa kutoka jeshi la polisi Iringa leo.lapokea kesi 592 kwa miezi 3

$
0
0

Dawati la jinsia la jeshi la polis mkoani Iringa limepokea kesi 592 kwa mienzi mitatu ndani ya mwaka huu zikiwemo kesi za watoto,wanawake na wanaume.

Akizungumza kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amezitaja kesi hizo kwa upande wa watoto ni kesi za kubaka ni 24,kesi za kufanya mapenzi na wanafunzi 3,kumpa mimba mwanafunzi 5,kutorosha wanafunzi 5,kutupa watoto 4,kulawiti 1,shambulio la kudhuru mwili 13,kujeruhi 1 na shambulio la aibu kesi 1.


Kwa upande wa kesi za wanawake katika dawati hilo ni kubaka 4,kujeruhi 46,kutumia ruga ya matusi 26,kutishia kuua kwa maneno na sms kesi 46,kutishia kuua kwa vitu nyenye ncha kali kesi 22,kutelekeza familia kesi 14 na shambulio la kudhulu mwili kesi 162.


Hata hivyo katika upande wa wanaume kesi walizopokea ni kesi ya kujeruhi 57,kutumia lugha za matusi kesi 20,kutishia kuua kwa maneno na sms kesi 30,kutishia kuua kwa vitu vyenye ncha kali kesi 11 na shambulio la kudhulu mwili kesi 97.


Aidha kamanda ameongeza kwa kusema kuwa mbali na elimu kuendelea kutolewa bado dawati hilo linachangamoto ya mwitikio kwa upande wa wanaume katika kwenda kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa vitendo vya kinyama na wake zao.


MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII PAMOJA NA SSRA YATOA MISAADA KATIKA WODI YA WAZAZI YA CHIKANDE PAMOJA NA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA AKILI CHA MIYUJI

$
0
0

Mkuu wa Kitengo cha uhusiano bi Sara Msika akikabidhi msaada wa shuka 100 na magodoro 30 katika wodi ya wazazi ya chikande

Mkuu wa kitengo cha uhusiano cha SSRA Bi Sara Msika akiwa amembeba mmoja kati ya watoto waliozaliwa katika Hospital ya Genera,  wodi ya wazazi ya Chikande mkoani Dodoma..

Wawakilishi wa Mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na SSRA wakikabidhi msaada wa vifaa vya ujenzi katika kituo cha kulea watoto wenye ulemavu wa akili cha Miyuji Cheshire mkoani Dodoma.

rais kikwete aongoza kilele cha maadhimisho Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Dodoma leo

$
0
0
Meneja Uhusiano Mfuko wa PPF Bi Lulu Mengele akimweleza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jinsi mfuko huo unavyosaidi kuendeleza kielimu watoto wa wanachama waliofariki wakati Rais alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali ya mifuko ya Hifadhi za jamii hapa nchini wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya jamii yanayofanyika mjini Dodoma.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio. Picha na Freddy Maro.

PRADO TX FOR SALE

$
0
0



PRADO TX IN GOOD CONDITION
Model: 1997 
Millage: 115,000km
Cc  3000
Engine 1KZ Diesel,
Color: Green 2 tone
Transmission:  AT
5doors, 8passengers, AC, PS, PW, AL, ABS.
Price: Tsh 19m/- Negotiable
TEL: 0712155221/0784587088
E-MAIL:badijohn30@yahoo.co.uk

Taswa FC na Taswa Queens zamwagiwa vifaa vya michezo

$
0
0

Meneja Masoko wa kinywaji cha Chilly Willy kinacho sambazwa na kampuni ya TSN Group, Yohana Manoli  (Kushoto) akimkabidhi jezi mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary (wa kwanza kulia) katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye mgahawa wa Hadees. Kulia ni Meneja Uhusiano wa TSN Group, Meshack Nzowah.
========  ============  ======
Kinywaji maarufu cha kuongeza nguvu, Chilly Willy Energy Drink kimetoa msaada wa jezi  na mipira kwa timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC na timu ya Netiboli, Taswa Queens kwa ajili ya kutumika michezo yake mbali mbali.
Meneja Masoko wa Kampuni ya TSN Group kinachosambaza kinywaji cha Chilly Willy Yohana Manoli alikabidhi vifaa hivyo kwa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary katika hafla fupi iliyopfanyika kwenye mgahawa wa Hadees uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Manoli alisema kuwa sababu kubwa ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Taswa SC ni kutambua mchango wa waandishi wa habari katika kuendeleza michezo nchini na hasa ukizingatia kuwa kinywaji cha Chilly Willy hakina kilevi na ni maalum kwa wanamichezo.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa  TSN Group, Meshack Nzowah alisema kuwa kinywaji chao cha Chilly Willy kina ubora wa kimataifa na wanaamini kuwa wanamichezo na wanajamii wataanza kutumia kinywaji hicho katika shughuli mbalimbali.
“Chilly Willy ni kinywaji ambacho hakina kilevi, kina ubora wa kimataifa na kutokana na hilo, kampuni ya TSN Group ikaamua kukisambaza nchini kwa lengo la kutoa bidhaa iliyobora zaidi, tunaamini wanamichezo wataanza kutumia hiki na vile vile ni maalum kwa waandishi wa habari na wadau wengine nchini,” alisema Nzowah.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliipongeza kampuni inayosambaza kinywaji cha Chilly Willy na kuwaomba waandishi wa habari kuanza kutumia kinywaji hicho. Majuto alisema kuwa Chilly Willy imetambua mchango wa Taswa  SC katika kuendeleza michezo na kutoa msaada huo.
“Ni faraja kubwa kuwa na kinywaji hiki hapa nchini na hasa kwa kutujali wana habari, kwa vifaa hivi, Taswa FC na Taswa Queens zitakuwa na nguvu na ubora kama wa Chilly Willy,” alisema Majuto.  Majuto alisema kuwa jezi hizo watazizindua rasmi Jumapili katika mechi dhidi ya timu ya kombaini ya mabondia wa ngumi za kulipwa nchini itakayochezwa kwenye uwanja wa Leaders Club kuanzania saa 5.00 asubuhi.
Alisema kuwa timu ya mabondia itaongozwa na bondia mkongwe nchini, Rashid “Snake Man” Matumla na mabondia wakali wengine kama Francis “SMG” Cheka, Cosmass  Cheka, Mbwana Matumla, Karama Nyilawila, Maliki Kinyogoli, Hassan Matumla, Daudi Mhunzi, Saidi Yazidu, Francis Miyeyusho , Thomas Mashali, Charles Mashali na wengine wengi.

HALMASHAURI KYELA YALALAMIKIWA KWA UFUJAJI WA FEDHA.

$
0
0

Na Ibrahim Yassin. Kyela

ZIARA ya Madiwani  kutoka Wilayani Kyela Mkoani   Mbeya waliokwenda kusikiliza bajeti iliyosomwa jana na mbunge wa jimbo la Kyela ambaye pia ni waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe imeingia doa  baada ya wananchi wilayani humo kulalamika kuwa kumetokea ufujaji wa fedha za wananch zilizotumika kwa ajili ya safari hiyo.

Wakizungumza  na Mwandishi wa habari hii kwa nyakati tofauti wananchi hao walidai kuwa madiwani hao walialikwa na Mbunge kwenda kusikiliza bajeti  hiyo kwa ufadhili wake na kuwa  wanashangaa kitendo cha Halmashauri kuwasainisha fedha kwa ajili ya safari hiyo wakati aliyewaalika ndiye aliyetoa kila kitu.

Waliongeza  kuwa hawaoni sababu ya Halmashauri hiyo kutumia fedha hizo kwa ajili ya safari ya Madiwani  kwenda Dodoma  wakati Wilaya ya Kyela inakabiliwa na Changamoto nyingi ikiwamo ya ubovu wa miundombinu ya barabara, maji safi, mifereji ya kupitisha maji taka, kutokamilika kwa stendi kuu, na kutokamilika kwa miradi ya maendeleo na kuwa badara ya fedha hizo kutatulia baadhi ya kero hizo wao wanazitumia kwa matumizi yasiyo kuwa na tija.

‘’Sisi wana Kyela tuna shangaa sana kuona wilaya yetu ikiyumba kimaendeleo ,ambapo changamoto zilizokuwepo ni nyingi lakini Halmashauri badara ya kutatua baadhi ya shangamoto zilizopo wao wanatumia fedha hizo kwa shughuli zisizokuwa na tija kwa wanakyela, ziara hii imedhaminiwa na aliyewaita kwenda bungeni sasa wao wametoa fedha hizo kwa misingi ipi’’ walihoji wamanchi hao.

Mwandishi wa habari hii  ilimtafuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Abdarah Mfaume ili kutoa ufafanuzi kuhusu safari hiyo ya madiwani inayolalamikiwa baada ya mkurugenzi kujurishwa kwa njia ya mtandao hakuweza kulijibia ambapo alikuwa Mkoani kwenye vikao hali iliyo pelekea kufanya mawasiliano na mkuu wa mkoa wa Mbeya ambaye alitoa ufafanuzi.


Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alipoulizwa kwa njia ya mtandao kuhusiana na uhalali wa safari hiyo alisema kuwa yeye kama mkuu wa Mkoa aliombwa ruhusa kuhusu safari ya madiwani kwenda bungeni kuhudhuria usomwaji wa bajeti ya wizara ya uchukuzi kwa ufadhiri wa Mbunge na sio vinginevyo.

‘’Mimi niliombwa ruhusa kuhusu safari hiyo na kujurishwa kuwa safari hiyo imedhaminiwa na Dr.Harrison Mwakyembe mbunge kwa lengo la madiwani hao kwenda kusikiliza bajeti wizara ya uchukuzi ilyosomwa jana na mbunge huyo ambaye ni waziri wa uchukuzi lakini sio vinginevyo.

Kutokana na mjibu hao ya Mkuu wa Mkoa  Tanzania Daima ilienda katika ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela na kumkuta Kaimu Mkurugenzi  Joseph  Njau akiwa na mhasibu wa Halmashauri hiyo Jacob Mbarouk baada ya mahojiano alikili ofisi yake kuwasafirisha madiwani hao kwenda Dodoma bila kutaja kiasi cha fedha kilichotumika.

Njau aliongeza kuwa ni kweli ziara hiyo ya madiwani ilidhaminiwa na mbunge Mwakyembe lakini Halmashauri iliwawezesha madiwani hao kufika Dodoma na kuwa sio dhambi Halmashauri kuwasafirisha madiwani kwa kuwa Madiwani ndiyo wenye Halmashauri.

FAINALI MISS UTALII TANZANIA 2013, KUFANYIKA JUMAPILI MKWAKWANI TANGA.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Galawa akiwasalimia Washiriki wa Miss Utalii 2012/13 wakati wa kuupokea Mwenge wa Uhuru Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga
 Washiriki wa Miss Utalii 2012/13 wakiwa katika picha ya Pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe Halima Denengo (t-shit kijani kati) pamoja na Viongozi wa chama na Serikali.Kushoto ni mwandaaji wa mashindano hayo Gideon Chipungahelo akipungia pamoja na warembo na viongozi hao
Washiriki wa Miss Utalii 2012/13 wakiwa katika picha ya Pamoja na maafisa wa BASATA Taifa.
=========  =============  ========

Hatimaye fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu,zinafanyika mkoani Tanga siku ya Jumapili Tarehe 19-5-2013katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga. Fainali hizo za tano za Taifa za mashindano ya Miss Utalii      Tanzania tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, zitajumuisha jumla ya warembo 30 kutoka mikoa yote ya Tanzania, na vyuo vikuu watapanda jukwaani kuwania taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2012/13.
 Zawadi kwa mshindi wa kwanza ni mkataba wenye thamani ya sh.90, 000,000/=,ambao unajumuisha skolashipu ya kusoma kozi ya Diploma katika chuo cha Dar es Salaam City Collage, safari za kushiriki mashindano ya Dunia,ziara za Tanzania Great Safari and Tour 2013, kugharamiwa usafiri wakati wa shughuli za kutekeleza majukumu yake ya ushindi,na shilingi 5,000,000/= baada ya kutumikia taji lake wakati wa kukabidhi kwa mshindi wa msimu ujao. 

 Aidha mshindi wa pili hadi wa tano, kila mmoja kila mmoja atajipatia mkataba wenye thamani ya shilingi 58,000,000/=, ambao pia unajumuisha skolaship za kusoma chuo cha Dar Es Salaam City Collage na safari za kushiriki mashindano ya kimataifa na ya dunia, pia ushiriki wa safari za Tanzania Great Safari and Tour 2013 na kugharamiwa usafiri wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya ushindi. 

Washiriki walio bakia watajipatia tuzo mbalimbali za heshima, za utalii, utamaduni, jamii, uchumi, mitindo, ,wanyama pori,misitu,mazingira,utalii wa ndani,utalii wa kitamaduni,jinsia,utalii wa michezo,utalii wa mikutano,elimu ya jamii,afya ya jamii, urembo na maliasili. 

 Mashindano ya Dunia ambayo washindi hao watashiriki ni Miss Tourism World 2013, Miss Tourism United Nation 2013, Miss Tourism University World 2013, Miss Heritage World 2013, Miss United Nation 2013,Miss Freedom Of The World 2013,na Miss Globe International 2013. 

 Burudani katika fainali za mwaka huu ,zitakazo fanyika kitaifa mkoani tanga jumapili tarehe 19-5-2013, ni pamoja na Bendi ya Msondo Ngoma, Mwana mziki wa kimataifa Che Mundu Gwao, Ngoma za asili na vichekesho kutoka kundi la Majuto Arts Group linalo ongozwa na mwigizaji mahili na mkongwe Mzee Majuto,sarakasi na muziki wa kizazi kipya yani bongo fleva.
Maandalizi yamekamilika, na hali ya kambi ni shwari huku washiriki wote wakiwa katika hali ya kujiamini, kila mmoja akijigamba kupeleka jaji mkoani kwake mwaka huu.

kikosi cha zima moto iringa chatembelea shule na vyuo 12 kutoa elimu ya kupambana na majanga ya moto.

$
0
0
Kikosi cha zima moto mkoani iringa kimefanya ziara  katika vyuo na shule za bweni lengo likiwa ni kutoa elimu ya tahadhari ya kinga ya moto na namna ya kujikinga punde majanga yatokeapo.


Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi,Kamanda mkuu wa kikosi cha zima moto Kenedy Komba, amesema kuwa katika ziara hiyo amebaini kuwa shule nyingi hazina vifaa na nyingine kuwa navyo vichache na  amewapa siku 14 ya kuwa na vifaa hivyo.


Komba amesema kuwa wazazi wanapaswa pale tu wanapowapeleka watoto wao mashulen ni vyema kuuliza juu ya usalama wa shule katika majanga na hata vyeti vya tahadhali ya kinga na moto.


Aidha ametembelea shule na vyuo 12 zilizopo ndani na nje ya manispaa ya iringa.


LOWASSA AZINDUA KITABU CHA MTIKISIKO WA UCHUMI

$
0
0

  Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kushoto), akizindua kitabu kipya kinachoelezea mtikisiko wa uchumi karne ya 2000 na kuendelea, kiitwacho 'The Economic Crisis of the 2000s and Beyond', Dar es Salaam LEO. Katikati ni Mtunzi wa kitabu hicho Dk. Prosper Ngowi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni iliyochapisha kitabu hicho ya Matokeo Publishers &Printers, Rosemary Sokile.
  Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (katikati), akizindua kitabu kipya kinachoelezea mtikisiko wa uchumi karne ya 2000 na kuendelea, kiitwacho 'The Economic Crisis of the 2000s and Beyond', Dar es Salaam jana. Kulia ni Mtunzi wa kitabu hicho Dk. Prosper Ngowi na Mchapishaji, Dk. Charles Sokile.
 Dk. Ngowi akisaini moja ya vitabu vilivyonunuliwa  jana. Kushoto ni Katibu Mkuu mstaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Juma Mwapachu.
Baadhi ya wadau waloshiriki kwenye uzinduzi huo.Picha kwa hisani ya Richard Mwaikenda.

PSPF MKOANI RUKWA YATOA SOMO KWA WADAU JUU YA UMUHIMU WA MFUKO HUO KATIKA KUHITIMISHA WIKI YA HIFADHI YA JAMII NCHINI

$
0
0
Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Mbijima akitoa somo kwa wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa (Rukwa Teacher's College) juu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa na mfuko huo kwa watumishi wa Umma. Semina hiyo imeenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini iliyofanyika kitaifa Mkoani Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ameongoza kilele cha maadhimisho hayo leo tarehe 17.05.213.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa wakimsikiliza mtoa mada kwa umakini mkubwa. Wahitimu hao ni sehemu ya wadau wakubwa wa baadae wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.
Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Mbijima akiendelea na kutoa mada alizoandaa kwa wahitimu hao juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko huo wenye mafao mbalimbali.
Malipo ya uzeeni, Malipo ya ulemavu, Malipo ya mirathi, Malipo ya wategemezi, na Malipo ya mazishi ni sehemu ya mafao muhimu yanayotolewa na mfuko huo kwa watumishi wa umma. 

Wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa wakionekana kukolea na mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Mbijima akiagana na baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu chuoni hapo baada semina ya shughuli na mafao muhimu yanayotolewa na mfuko wa PSPF nchini.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa - rukwareview.blogspot.com)

Rais Kikwete aongoza Sherehe za maadhimisho ya mifuko ya jamii

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wadau na viongozi wa mifuko ya hifadhi ya jamii wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mifuko hifadhi ya ya jamii iliyofanyika mjini Dodoma leo(picha na Freddy Maro)
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>