Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 843 | 844 | (Page 845) | 846 | 847 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akipeana mkono na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akipeana mkono na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akipeana mkono na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akipeana mkono na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na wanahabari hawapo pichani katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Kushoto ni Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia). Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na wanahabari hawapo pichani katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Kushoto ni Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia).Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza jambo na Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas (kushoto), katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza jambo na Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas (kushoto), katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.
  Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas (kushoto) akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati benki hiyo ilipozinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akiwa na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia). Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas (kushoto) akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati benki hiyo ilipozinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akiwa na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia).Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kushoto) mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Kushoto ni Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas akishuhudia. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kushoto) mara baada ya benki hiyo kuzinduwa hati fungani zinazoanza kuuzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Kushoto ni Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas akishuhudia.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na wanahabari hawapo pichani katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Kulia ni Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa akifuatilia tukio hilo. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) akizungumza na wanahabari hawapo pichani katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Kulia ni Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa akifuatilia tukio hilo.Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia) akizungumza na wanahabari kufafanua hali ya hisa nchini na kuipongeza NMB kwa hatua ya kuwashirikisha wananchi kwenye uwekezaji. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker. Meneja Miradi na Maendeleo ya Biashara kutoka Soko la Hisa Tanzania, Patrick Mususa (kulia) akizungumza na wanahabari kufafanua hali ya hisa nchini na kuipongeza NMB kwa hatua ya kuwashirikisha wananchi kwenye uwekezaji. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker.[/caption]   BENKI ya NMB imetoa ofa ya hati fungani kwa wananchi wanaotaka kuwekeza kwa muda wa miaka mitatu katika mtaji wa benki hiyo, huku wakijipatia faida ya asilimia 13 ya fedha waliyowekeza kwa kila miezi sita. Ofa hiyo imefunguliwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker. Alisema NMB itauza hati fungani ya thamani ya shilingi bilioni 20 ikiwa ni njia ya kuwashirikisha wananchi kuwekeza fedha zao na kujipatia faida. Akifafanua zaidi, Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha wa NMB, Waziri Barnabas alisema ofa ya chini kwa kila anayetaka nunua hati fungani hizo ni kuanzia shilingi 500,000 na kuendelea kulingana na uwezo wa mtu kwa kiasi atakachoitaji kukiweka katika mtaji wa NMB..Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) akizungumza na wanahabari katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) akizungumza na wanahabari katika hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wanahabari wakifuatilia hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wanahabari wakifuatilia hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.[/caption]   Alisema wawekezaji hao wataanza kupata gawio lao la asilimia 13 kwa kiasi ulichowekeza baada ya miezi sita na litaendelea kutolewa kila baada ya miezi sita kwa kipindi cha miaka mitatu. Aliongeza kuwa baada ya kutimia miaka mitatu mwekezaji atalipwa fedha yake pamoja na asilimia 13 ya kiasi alichowekeza. Hati fungani hizo zitaanza kuuzwa kwa wananchi kuanzia Mai 10 hadi Juni 8, 2016 ambapo ofa itafungwa na utaratibu wa kupangwa kwa hati hizo kuanza. Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuwekeza fedha zao hasa wale wanaohifadhi fedha bila kuzizalisha kwani wataziongezea thamani.Mmiliki wa Blogu ya Father Kidevu, Mroki Mroki (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) mara baada ya hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Mmiliki wa Blogu ya Father Kidevu, Mroki Mroki (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (kushoto) mara baada ya hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wanahabari wakifuatilia hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB. Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wanahabari wakifuatilia hafla ya uzinduzi uuzaji wa hati fungani zitakazouzwa kwa Watanzania wanaoitaji kuwekeza katika mtaji wa benki ya NMB.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter  Muhongo (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, baadhi ya Wabunge na  Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika mjini Geita. Wa Pili kulia ni Mkuu  wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Wa Pili kulia) akiwa na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Geita, waliohudhuria kikao baina ya Waziri na Watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, baadhi ya Wabunge na  Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika mjini Geita. Kikao kililenga katika kujadili suala la magwangala na maeneo ya wachimbaji wadogo nchini.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter  Muhongo (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, baadhi ya Wabunge na  Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika mjini Geita. Wa Pili kulia ni Mkuu  wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga.

  Na Teresia Mhagama, Geita.
  MGODI wa Dhahabu wa Geita (GGM) uliopo mkoani Geita umeridhia ombi la Serikali la kutoa mabaki ya mawe ya  dhahabu kwa wananchi ili kuweza kuyachenjua na kupata dhahabu.

  Hayo yameelezwa mjini Geita na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kumaliza vikao vya majadiliano kati ya watendaji wa GGM, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, baadhi ya Wabunge na Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

  “Tatizo la Magwangala sasa limetatuliwa kwani Mgodi umekubali kuyatoa kwa wananchi ila kinachotakiwa kufanywa kabla ya kuyatoa magwangala hayo ni Serikali ya Mkoa huu kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa kwanza wanapata eneo ambalo uchenjuaji wa magwangala utafanyika,” alisema Profesa Muhongo.

  Aidha aliongeza kuwa eneo hilo litakalotengwa na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita lazima lifanyiwe tathmini ya mazingira na Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kuweza kuthibitika kama eneo hilo linafaa kwa shughuli hizo bila kuleta athari kwa wananchi na mazingira.

  Profesa Muhongo alitoa agizo kuwa  kazi hizo zinatakiwa kukamilika tarehe 30 Juni, mwaka huu ambapo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itafanya kikao kitakachohudhuriwa na watendaji wa  Mgodi na Wabunge wa mkoa huo na kutoa uthibitisho wa kimaandishi kuhusu eneo lililotengwa kwa shughuli hiyo pamoja na Cheti kutoka NEMC cha uthibitisho kuwa eneo hilo linafaa au halifai kwa shughuli za uchenjuaji madini kufanyika.

  Aidha alieleza kuwa katika kikao hicho cha tarehe 30 Juni GGM itapaswa pia kutoa uthibitisho wa kimaandishi kuwa imekubali kutoa magwangala hayo kwa wananchi.

  “Baada ya Eneo hilo na Cheti cha mazingira kupatikana,  sasa katika kikao hicho mtaweza kujadiliana kuhusu  usafirishaji wa magwangala  hayo kutoka eneo la Mgodi hadi eneo lililotengwa, hapo mtakubaliana nani atachukua jukumu la kusafirisha magwangala hayo,”alisema Profesa Muhongo.

  Aliongeza kuwa Leseni za uchenjuaji madini zitakazotolewa mara baada ya eneo  hilo kupatikana, zitakuwa katika vikundi na si mtu mmoja mmoja  ambapo  Ofisi ya Mkuu wa mkoa ndiyo itakayoratibu suala hilo huku jukumu la Wizara likiwa ni kutoa Leseni hizo.

  “Ni vizuri pia mkashirikiana na viongozi wa Wachimbaji Wadogo katika kuratibu uundaji wa vikundi hivyo na lazima vikundi hivyo vielezwe kuwa ni lazima walipe kodi stahiki kwa Serikali kama ilivyo kwa shughuli nyingine za uchenjuaji madini,” alisema Profesa Muhongo.

  Kwa nyakati tofauti Wabunge wa mkoa huo walieleza kuwa utoaji wa Magwangala hayo kwa wananchi, utasaidia wanachi hao kujiajiri, kujiongezea kipato na kuwaepusha katika kushiriki matendo ya uhalifu.

  0 0

  Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma.
  Kufuatia majadiliano na vikao mbalimbali vilivyofanyika mwaka 2005-2010, kumbukumbu zinaonyesha kuwa suala la uanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) lilifanyiwa kazi kwa ukamilifu na Serikali za pande zote mbili kwa ushirikiano na Vyama vyote viwili.

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Nape Nnauye (Mb) wakati akijibu swali la Mhe. Mbunge wa Dimani Hafidh Ali Tahir lenye kipengele a,b na c lililotaka kujua ni nini matokeo ya Kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu.

  Nnauye ameeleza kwamba, kwa kutambua umuhimu wa ZFA kupata uanchama wa FIFA, mwaka 2010 ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwamba, ukiongozwa na aliyekuwa Naibu Waziri Kiongozi, Mhe. Juma Shamhuna pamoja na aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Mhe. Joel Bendera walikwenda Zurich, Switzerland ambako walikutana na Rais wa FIFA wa wakati huo.

  Aidha, Nnauye amefafanua kuwa, katika msafara huo walifuatana na viongpozi wa TFF na ZFA na madhumuni ya safari hiyo ilikuwa ni kuwasilisha maombi ya ZFA kupewa uanachama wa FIFA.

  "Mwezi Juni 2011, FIFA iliiandikia ZFA ikiwajulisha kuwa kwa mujibu wa taratibu zilizopo, isingewezekana Zanzibar kupata Uanachama wa FIFA kwa kuwa wananchama wao ni nchi zinazotambuliwa na Jumuiya ya Kimataifa kama ilivyoelezwa katika aya ya 10 ya Katiba yao", alisema  Nnauye.

  Nnauye aliongeza kuwa, suala la usajili wa TFF au ZFA linafahamika vyema ndani ya Serikali ya Mapinduzi pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  "Hata hivyo, naomba kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa, uanachama wa TFF katika FIFA upo kwa mujibu wa muafaka wa pande zote mbili.

  Kwa kuzingatia utaratibu wa FIFA kuhusiana na suala hilo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imewaelekeza TFF nao wako tayari kufanya maridhiano na ZFA ili kukamilisha utaratibu wa wazi wa kukidhi mahitaji ya Zanzibar kushiriki katika masuala ya FIFA kupitia TFF bila kuathiri ushiriki wa klabu za Zanzibar katika mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).

  0 0

  Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.

  SERIKALI imepiga marufuku upakiaji wa mizigo kupita kiasi (lumbesa) katika magunia kuanzia mwaka ujao wa fedha.

  Kauli hiyo imetolewa jana Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb) wakati akijibu hoja mbalimbali za Wabunge wakiochangia hotuba ya Wizara yake.

  Amesema kuwa, kuanzia mwaka ujao wa fedha, Vyombo vy Dola vitakamata wafanyabiashara wote watakaokuwa wanapakia lumbesa.

  Mhe. Mwijage alisema kuwam upakiaji huo wa mizigi kupita kiasi unawasababishia wizi kwa wakulima ambapo ametoa wito kwa wakulima na wafanyabiashara nchini kutumia vipimo halali wakati wanaponunua na kuuza mazao yao mbalimbali.

  Katika hatua nyingine, Waziri huyo ametoa wito kwa wakulima kuacha tabia ya kuuza mazao yao yakiwa shambani au kabla ya kukomaa.

  Alisema kuwa hali hiyo inawarudisha nyuma na kuwapunja wakati wangesubiri mazao yakomae wangepata fedha za kutosha.

  0 0


  Mhandisi Cyprian Luhemeja. 
  Katika kutekeleza agizo la serikali la kuwafikia wateja laki 4 (400,000) ifikapo June 2016 ,Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco) ,linaendelea na zoezi la uunganishaji wa huduma ya Maji kwa wananchi wote wa jiji la Dar es salaam pamoja na miji ya Bagamoyo na Kibaha mkoani Pwani huku ikigharamia gharama zote za uunganishaji ambazo awali zilikuwa zikilipwa na mteja.

  Akiongea na waandishi wa habari hivi Afisa mtendaji mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameeleza kuwa kwenye awamu hii ya zoezi la uunganishaji wateja wapya shirika litagharamia gharama zote za maunganisho ambazo ni gharama za uunganishaji, mabomba na vifaa vya uunganishaji ambapo mteja atawajibika kurudisha gharama hizo za maunganisho kidogo kidogo kila mwezi kwa kipindi cha miezi 12 baada ya kupata huduma ya Maji.

  “Dawasco itamuunganishia huduma ya maji na kugharamia gharama zote uunganishaji ila mteja atawajibika kurudisha ile gharama kidogokidogo kila mwezi kwa kipindi cha miezi 12 baada ya kupata huduma ya Maji hii itasaidia hata wale ambao kipato chao ni cha chini kuweza kuunganishiwa huduma ya Maji” alisema Luhemeja.
  Pia Mhandisi Cyprian Luhemeja ameleeza kuwa zoezi hili la uunganishia wateja wapya ni la kipindi cha miezi miwili tu cha Mei na Juni 2016 hivyo wananchi wote watumie fursa hii kwa kufika katika ofisi za Dawasco za kanda ili kupata huduma hiyo. 

  “Zoezi hili la kugharamia gharama za uunganishaji huduma ya maji kwa wateja ni kwa kipindi maalum cha miezi miwili tu ambacho ni Mei na Juni hivyo wananchi watumie fursa hii kujitokeza iliwaweze kuunganishiwa na katika kipindi chote cha zoezi Ofisi za Dawasco zitakuwa wazi kuanzia jumatatu hadi jumapili” alisema Luhemeja.

  Hata hivyo Dawasco imeeleza kuwa wananchi pamoja wateja wake wameweza kuwasiliana na kituo cha huduma kwa wateja kupitia namba 022-2194800 au 0800110064 (bure) ili waweze kupata huduma na maelezo zaidi kuhusiana na zoezi hilo la uunganishaji huduma ya Maji.

  Mapema mwaka huu serikali kupitia kwa waziri mwenye dhamana ya kusimamia Wizara ya Maji, Mh Mhandisi Gerson iliagiza Shirika la Dawasco kuongeza idadi ya wananchi wanaopata huduma ya Majisafi kutoka 156,000 waliopo sasa kufikia wateja 400,000 (laki nne) ili kwenda sambamba na ongezeko la watu pamoja na mahitaji makubwa ya Maji yanayohitajika katika jiji la Dar es salaam.

  0 0

  Timu ya wataalamu kutoka shirika la ndege la Etihad leo wametembelea abiria tisa waliolazwa baada ya Ndege aina ya EY474 ya shirika hilo kupatwa na msukosuko mkali katika anga la wazi ambapo walitoa huduma endelevu, ushirikiano na msaada.


  Vile vile walikutana na wanafamilia kadhaa wa majeruhi na kuthibitisha kuwa shirika la ndege la Etihad litagharamia gharama zote za matibabu.

  Kati ya majeruhi tisa ambao walikuwa wamelazwa, wengi wao wataruhusiwa kuondoka leo. Rais wa shirika la ndege la Etihad na Mkurugenzi Mkuu Bwana James Hogan amesema: “Rubani wetu na wafanyakazi wa ndege wanapaswa kupongezwa sana kwa utulivu wao na namna ambavyo walishughulikia tukio hili la aina yake kwa utaalamu mkubwa, na huduma waliyoionesha kwa abiria japo kuwa wengi wao walikuwa wamejeruhiwa. Ni ushahidi wa mafunzo ya kiwango cha juu yanayotolewa kwa wafanyakazi wetu ndio sababu athari za msukosuko ulipunguzwa. Wakati huo hakuna kabisa usalama wa ndege,abiria au wafanyakazi walioathirika.”

  Shirika la ndege la Etihad linashirikiana kikamilifu na Mamlaka za Indonesia katika uchunguzi wao.

  0 0

    Katibu wa CCM Tawi la Makangira Kata ya Msasani Nd. Epi Fania Ngonyani akibadilishana mawazo na Balozi Seif akijiandaa na ujumbe wake kuondoka Bandarini Malindi kurejea Mjini Dar es salaam baada ya kumaliza ziara yao ya ujirani mwema. Nyuma ya Ndugu Ngonyaji ni Mwenyekiti wa CCM wa Tawi hilo Ndugu Haroub Othman Mberwa.
   Balozi Seif akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Makangira Ndugu Haroub Othman Mberwa aliyeuongoza ujumbe wa Viongozi kumi wa Kata hiyo waliofanya ziara ya ujirani mwema hapa Zanzibar.
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Ujumbe Viongozi wa CCM Tawi la Makangira Kata ya Msasani, Wilaya ya Kinondoni Mjini Dar es salaam katika Banadari ya Malindi baada ya kumaliza ziara yao ya ujirani mwema Visiwani Zanzibar wakiwa wenyeji wa Tawi la CCM Vikokotoni Mjini Zanzibar.

  Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Matawi mbali mbali Nchini Tanzania wanapaswa kuwa makini katika kuwachangua viongozi imara wakati utakapowadia wa chaguzi za Chama hicho ili kuirahisisha kazi ya ushindi CCM mwaka 2020.

  Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Makangira Kata ya Msasani Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Haroub Othman Mberwa wakati akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi hapo Bandarini Malindi Mjini Zanzibar.

  Mwenyekiti Mberwa na Ujumbe wake wa Viongozi Kumi wa Kata ya Makangira Msasani ulikuwepo Zanzibar kwa ziara ya kuimarisha uhusiano mwema kati ya kata hiyo na wenyeji wao wa Tawi la CCM Vikokotoni lilioko Mji Mkongwe Zanzibar.

  Ndugu Mberwa alisema wakati umefika kwa wana CCM kuendelea kuongozwa na Viongozi makini waliobobea hekima na busara kuanzia Matawi maeneo ambayo ni chimbuko halisi la upatikanaji wa Viongozi katika ngazi za Majimbo, Wilaya, Mkoa hadi Taifa.

  Alisema Chama cha Mapinduzi kimepata misukosuko mingi katika awamu tofauti za Uongozi zilizopita iliyosababishwa na baadhi ya Viongozi wenye sura mbili za maamuzi jambo ambalo lilipelekea kuwa na mgawanyiko na hatimae kuzalisha makundi yaliyozaa ufa ndani ya chama hicho.
  Ndugu Mberwa alitahadharisha kwamba Wanachama wa CCM Matawini ndio wenye kauli na rungu za kuwachagua Viongozi watakaokuwa tayari kuwatumikia katika misingi ya uadilifu na ni vyema kuachana na tabia ya kubebana kwa kisingizio cha ukabila, uzawa na urafiki.

  Alieleza kwamba tabia kama hizo ndizo zinazopelekea Viongozi wa Kitaifa kukumbana na wakati mgumu katika kutoa maamuzi ya hatma ya muelekeo wa kumpata Kiongozi wa kubeba dhamana ya kuwatumikia katika masuala yao ya Chama.

  Naye Katibu wa Tawi la CCM la Makangira Kata ya Msasani, Wilaya ya Kiondoni Mkoa wa Dar es salaam Nd. Epi Fania Ngonyani alisema uwepo wa ujumbe wao hapa Zanzibar umejifunza mambo mengi yatakayosaidia kuimarisha chama chao kwa upande wa Tanzania Bara.

  Nd. Ngonyani alisema matembezi ya sehemu za kihistoria pamoja na Mikutano ya hadhara ya kukutana na wanachama wenzao wa baadhi ya Matawi na hata Wilaya za Tanzania Zanzibar imewajengea heshima na upendo kati yao na wenyeji wao iliyopelekea pia kujadili mapungufu yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

  Alieleza kwamba katika mikutano hiyo ya uhusiano mwema pande hizo mbili zilipendekeza uwepo wa mikakati ya makusudi ya kujengewa uwezo zaidi wa uwezeshaji makundi makubwa ya vijana na wanawake ili washiriki vyema kwenye shughuli za uzalishaji.

  Ziara hizo za kuimarisha uhusiano mwema kati  ya Matawi ya Chama cha Mapinduzi ya Vikokotoni Mjini Zanzibar na Makangira Msasani Dar es salaam hufanyika kwa kutembeleana kila mwaka.

  0 0


  Dk. Sophia Mlote, mkazi wa Kinyerezi Zimbili jijini Dar es Salaam akiweka sawa vifaa mbalimbali kwenye banda lake la kilimo ambamo amepanda nyanya. Dk. Mlote anatekeleza kilimo hai kupitia mradi wa Green Voices unaofadhiliwa na taasisi ya Foundation for Women of Africa ambayo inaongozwa na Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega. (Makala na Picha zimeandaliwa na www.brotherdanny.com
  Bw. Abdon Hamaro, Ofisa Kilimo kutoka TAHA na mwezeshaji wa mafunzo ya akinamama wa kikundi cha ‘Green Voices  Kinyerezi’, akiendelea kuwaelekeza wanakikundi (hawapo pichani) namna ya kuendesha kilimo hai cha nyanya. Mafunzo hayo yalifanyika hivi karibuni Kinyerezi, jijini Dar es Salaam.


  Mratibu wa mradi wa Green Voices, Bi. Secelela Balisidya (kulia), akiwa makini kuangalia Bw. Hamaro akiandaa mambo mbalimbali kwa ajili ya kuwaelekeza wanakikundi namna bora ya kuendesha kilimo hai cha nyanya.

  Wanakikundi cha Green Vocies Kinyerezi wakifuatilia mafunzo hayo.


  Christina Lwiza (kushoto) akipokea pakiti ya mbegu ya nyanya kutoka kwa Dk. Sophia Mlote tayari kwa kuwatika ili kuanzisha kilimo hai cha nyanya.


  Bw. Hamaro akiandaa tray maalum kwa ajili ya kuwapa wanakikundi kupandikiza mbegu kabla ya kupeleka kwenye vitalu vyao. Hii ilikuwa ni sehemu ya mafunzo ya vitendo.


  Wanakikundi wakijaza udongo maalum kwenye tray kabla ya kuanza kupandikiza mbegu.


  Bw. Hamaro akiwaelekeza kwa vitendo wanakikundi namna ya kupandikiza mbegu hizo.
  Hapa wanakikundi wakiendelea kupandikiza mbegu kwenye tray.


  10. Banda maalum ambalo ni shamba muhimu kwa ajili ya kilimo hai (green house) ambamo ndani yake nyanya zimestawi.


  Picha ya pamoja ya wanakikundi cha Green Voices Kinyerezi.

  NDANI ya banda kubwa lililoezekwa na kuzungushiwa plastiki maalum katika Mtaa wa Kinyerezi Zimbili jijini Dar es Salaam, Dk. Sophia Mlote akiwa ameongozana na mtaalamu wa kilimo, Bw. Abdon Hamaro, anaonekana akipanga vizuri vifaa vya kilimo pembeni ya matuta yaliyostawisha vizuri nyanya.

  Pembeni ya banda hili lenye ukubwa unaokadiriwa kuwa wa meta 8 kwa 12, akinamama kadhaa wamezunguka wakitazama ustawi wa zao hilo huku Bw. Hamaro akiendelea kutoa maelekezo ya namna ya kuendesha kilimo hai  kinacholimwa katika mabanda maalum yajulikanayo kama green houses ikiwa ni sehemu ya mafunzo ya vitendo ya akinamama hao katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuongeza kipato.

  Tofauti na nyanya ambazo watu wamezoea kuziona zikilimwa katika mashamba makubwa na bustani za wazi, nyanya hizi zinalimwa ndani ya banda ambao ukubwa wake utategemea pia na eneo lililopo pamoja na uwezo wa mhusika katika kulijenga banda hilo.

  Hiki ni kilimo hifadhi ambacho kinahimizwa kwa sasa ulimwenguni kote ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji.

  “Mtu yeyote anaweza kuendesha kilimo cha mazao mbalimbali kwa kutumia Green house hata katikati ya Jiji la Dar es Salaam kama tunavyoona, ni rahisi na rafiki wa mazingira kwa sababu unaweza kuendesha hata kwenye uwa wa nyumba yako kama hivi,” Bw. Hamaro anaendelea kuwaeleza akinamama hao, ambao ni wanakikundi wa mradi wa  ‘Green Voices’ unaofadhiliwa na taasisi ya Foundation for Women of Africa yenye makao yake katika mji wa Madrid, nchini Hispania.

  Mbali ya kutunza mazingira, Bw. Hamaro kutoka Chama cha Wakulima wa Bustani Tanzania (TAHA) anasema, kilimo hai kinasaidia kuzalisha vyakula visivyo na kemikali ambavyo ni rafiki wa afya ya binadamu.

  Katikati ya Jiji la Dar es Salaam watu wamekuwa wakishuhudia kilimo cha mboga mboga kwenye mabonde ya mito midogo, ambacho kinatumia umwagiliaji wa maji machafu na yenye kemikali za kutoka viwandani, ambazo ni hatari kwa afya ya binadamu.

  “Mbegu zinazotumika zimetengenezwa maalum na hazifanani za zile GMO zinazopigiwa kelele, lakini pia unatakiwa kutumia mbolea za asili kama mboji na samadi, kwa sababu ukitumia kemikali nyingi kwenye udongo, mimea inanyonya na kemikali hizo zinabaki kwenye vyakula na hatimaye kuingia miilini mwetu,” anafafanua Hamaro.

  Vile vile, Hamaro anasema kilimo cha Green house kinaweza kutumika hata kwa matunda na kwamba kinatumia maji kidogo huku pia kikimpunguzia gharama mkulima hasa kwa kuepukana na magonjwa mbalimbali ambayo yanasababishwa na wadudu.

  “Kwa kuwa banda limefunikwa na kukingwa, hakuna wadudu waenezao magonjwa ya mimea wanaoweza kuingia, lakini faida nyingine ni kwamba, unaweza kudhibiti hali ya hewa kwa kupunguza ama kuongeza joto ili kuifanya mimea kukua vizuri,” anaongeza.

  Dk. Mlote mwenyewe, ambaye ni Ofisa Mwandamizi katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Mifugo, ni mshiriki wa mradi wa Green Voices ambaye baada ya mafunzo aliyoyapata, sasa anaieneza elimu hiyo kwa wanawake wenzake majirani wa mtaa huo.

  Yeyé ni miongoni mwa wanawake 15 waliopatiwa mafunzo ya kuongeza ujuzi wa jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yaliendeshwa nchini Hispania chini ya ufadhili mkubwa wa taasisi ya Foundation for Women of Africa inayojihusisha na maendeleo ya wanawake wa Afrika, ambayo inaongozwa na Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega.

  “Niliamua kuchagua mradi huu kwa sababu, kwanza ni rahisi kuuendesha kwa kuwa shughuli zote zipo hapa nyumbani na hata kama nitarudi usiku kutoka kazini, bado ninaweza kuingia humu shambani na kuhudumia mimea kwa kuwa banda hili lina taa,” anaeleza.

  Aidha, anasema, kwa kuwa anakaribia kustaafu, na kwa elimu ya kilimo na uchumi aliyonayo pamoja na utaalamu alioupata, ameona ni vyema aanzishe mradi ambao siyo tu utampatia kipato, lakini pia utasaidia kutunza mazingira pamoja na kuwa msaada kwa jamii kutokana na mazao yatakayovunwa.

  “Niliamua kuwaelimisha wanawake wenzangu katika mtaa huu na kuwashawishi waunde kikundi hiki na tayari wamekwishapata mafunzo ya kutosha ambapo kila mmoja amekuja na wazo la kuanzisha bustani ndogo nyumbani kwake ya mtindo huu kwa mazao ambayo anaona yanafaa,” anaongeza Dk. Mlote, ambaye ameeleza kwamba, anakusudia kupanua kilimo hicho kwa kupanda hata miti ya matunda.

  Kikundi hicho cha ‘Green Voices Kinyerezi’ kinaundwa na wanawake 10, ambapo mbali ya kujifunza kwa nadharia namna ya kuendesha kilimo hai kwa njia ya green house, walipata fursa ya kufanya kwa vitendo kwa kupandikiza mbegu za mazao mbalimbali ya mboga mboga kama nyanya, kabichi, hoho, matango na matikiti maji kwenye bando hilo ambapo yatakapoota kila mmoja atakwenda kupanda nyumbani kwake.

  Christina Lwiza, mmoja wa wanakikundi hicho ambaye anajishughulisha na biashara ya uuzaji vinywaji kwenye grocery yake mwenyewe, anasema ameshawishika kuanzisha kilimo cha nyanya nyumbani kwake ambacho kinaweza kumpatia mapato ya nyongeza pamoja na kukidhi mahitaji ya nyumbani.

  “Sijawahi kulima nyanya, lakini kwa mafunzo niliyoyapata, hakika naweza kuendesha kilimo hicho bila shida,” anasema Christina.

  Karibu wanakikundi wote wamehamasika, ambapo kila mmoja ameamua kubuni zao ambalo linaweza kumfaa.

  Mratibu wa mradi huo, Bi. Secelela Balisidya, anasema mradi huo wa kilimo hai cha nyanya kwa kutumia green house ni sehemu ya miradi 10 inayoendeshwa nchini Tanzania kupitia Green Voices ambapo inaendeshwa katika mikoa sita ya Tanzania Bara.

  Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Pwani, Mwanza, Kigoma, Morogoro na Kilimanjaro ambapo inahusisha kilimo, usindikaji, ufugaji na utafiti.

  “Miradi hiyo ni kilimo cha miti ya matunda mkoani Kigoma, kilimo cha viazi lishe visiwani Ukerewe mkoani Mwanza, Ufugaji Nyuki mkoani Morogoro na Pwani, ukaushaji wa mbogamboga kwa kutumia nishati ya jua mkoani Morogoro, usindikaji wa vyakula mbalimbali kutokana na muhogo mkoani Pwani, kilimo hai cha mbogamboga, kilimo cha uyoga mkoani Dar es Salaam, mradi wa majiko banifu mkoani Pwani na mradi wa utafiti wa jiko linalotumia nishati ya jua mkoani Kilimanajro,” amefafanua Secelela Balisidya.

  Aidha, amesema kwamba, lengo kubwa la mradi wa Green Voices ni kupaza sauti za akinamama kueneza ujuzi wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili jamii nzima ya Kitanzania iweze kujifunza zaidi na kuzitumia mbinu hizo katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

  Mradi huo unatarajiwa kutelekezwa kwa mwaka mmoja ili kutoa fursa kwa akinamama kutoa ujuzi wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi na sauti zao kusikika, kwa sababu kazi wanazozifanya kila siku za kilimo na utunzaji wa familia zinahusiana moja kwa moja na mazingira hivyo kuyaelewa zaidi mazingira na jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

  Malengo ya dunia.
  Kilimo hai kinaendana na masuala mtambuka ya mazingira pamoja na kukabiliana na uhaba wa chakula na kupunguza umaskini kama inavyoelezwa kwenye Malengo Endelevu ya Dunia yaliyopitishwa mwaka 2015.

  Kwa mujibu wa malengo hayo, mataifa mbalimbali yamekubaliana kuhakikisha yanatokomeza umaskini kwa namna zote pamoja na kukomesha njaa na kupata uhakika wa usalama wa chakula na kuboresha lishe kwa kuhimiza kilimo endelevu.

  “Kilimo hai ni endelevu kwa sababu unaweza kulima wakati wowote hivyo kinaweza kukabiliana na njaa na uhakika wa chakula ni mkubwa, lakini pia kitasaidia familia kuongeza kipato kwa kuuza ziada ya chakula kitakachozalishwa,” anasema Hamaro.

  Lakini pia kwa kutumia kilimo hai, lengo namba sita la dunia linaweza kutimia, kwani ni kilimo ambacho kinatumia maji kidogo, hivyo kuhakikisha utunzaji mzuri wa vyanzo vya maji na matumizi sahihi ya maji yaliyopo.

  Aidha, kilimo hai pia kinaweza kukidhi lengo namba 13 la dunia linalohimiza kupambana na mabadiliko ya tabianchi na athari zake.

  Sera ya Kilimo
  Kilimo hai ni sehemu ya mapendekezo yanayotajwa kwenye Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2013 ambayo inaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo kuelekea mwaka 2025 kwa kuhimiza kilimo chenye tija pamoja na utumiaji mzuri wa rasilimali zilizopo, hususan ardhi na maji.


  Kwa maana nyingine, kuhamasisha kilimo hai ni sehemu ya utekelezaji wa malengo, dhima na dira ya sera hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na changamoto ya uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi, ambayo serikali pia imeainisha mikakati yake katika Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2007.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka kwenda London Uingereza Mai 10 , 2016, kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi wa kujadili masuala ya kupambana na rushwa duniani.(Picha n Ofisi ya Wziri Mkuu).
   
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuondoka nchini leo jioni (Jumanne, Mei 10, 2016) kwenda London, Uingereza kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi unaojadili suala la kupambana na rushwa (Anti-Corruption Summit 2016) utakaofanyika Mei  12, mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana, Waziri Mkuu alisema anaenda kumwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli kwa sababu siku hiyo hiyo, atalazimika kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni.

  “Mheshimiwa Dk. Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na siku hiyo hiyo, mmoja wa marais wa nchi wanachama anaapishwa. Kwa hiyo amelazimika kwenda kuhudhuria sherehe hizo,” alifafanua Waziri Mkuu.

  Akizungumzia kuhusu mada ya mkutano huo, Waziri Mkuu amesema Tanzania inafanya vema katika mapambano dhidi ya rushwa na kwamba baadhi ya nchi zimeanza kuvutiwa na juhudi ambazo Serikali imekuwa ikichukua.

  “Waziri Mkuu wa Uingereza ameandaa mkutano huu na alimwalika Mheshimiwa Rais Magufuli ili ahudhurie akiwa ni miongoni wa wakuu wa nchi 60 watakaohudhuria mkutano huo. Tanzania ni miongini mwa nchi mbili kutoka bara la Afrika ambazo zimealikwa kushiriki. Nchi nyingine ya kutoka Afrika ni Nigeria,” alisema.

  Waziri Mkuu atafuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Mkurugenzi wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola, wataalamu wa sekta ya rushwa na wanasheria


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMANNE, MEI 10, 2016.

  0 0

  John Marwa Mratibu wa Chama cha Watetezi wa Rasilimali Wasio na Mipaka WARAMI akizungumza na waandishi wa habari Kwenye Hoteli ya Tamarin Mwenge jijini Dar es salaam kuhusu Sakata la Sukari ambapo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa jinsi anavyothubutu kuwatetea watanzania waliowanyonge katika masuala mbalimbali na hasa katika suala zima la uhaba wa sukari.

  Kuna tani nyingi za sukari zimekamatwa katika msako maalum ambao Rais aliamrisha vyombo vya dola kufuatilia wafanyabiashara wasio waaminifu walioficha sukari, baada ya zoezi hilo kuanza sukari nyingi imeendelea kukamatwa maeneo mbalimbali nchini ikiwa imefichwa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.

  WARAMI inapongeza jitihada zote za dhati anazozifanya Rais Magufuli na Serikali yake za kuhakikisha watanzania wanaishi kwenye usawa, lakini pamoja na hayo wanapendekeza mambo kadhaa yafanyika na jeshi la polisi

  Mratibu huyo wa Taasisi ya WARAMI amelitaka jeshi la polisi kutoa taarifa rasmi juu ya wafanyabiashara wanaotamba barabarani kuwa wameliweka jeshi hilo mfukoni kwamba hakuna wa kuwafanya lolote katika nchi hii.

  Taasisi za kiserikali zifafanue juu ya tabia hii ya wafanyabiashara kutumia picha za viongozi kwa maslahi yao kama, ni haki ama si haki.

  Kiongozi huyo wa WARAMI akaongeza kwamba hivi sasa Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli anayo vita kubwa kutokana na kazi anayoifanya ya kuwatetea watanzania waliowanyonge anayo vita ndani ya bunge na nje ya Bunge 

  Kutokana Na Hoja Ambazo Zimekuwa Zikitolewa Na Baadhi Ya Wabunge Zikikosoa Utendaji Wa Rais, kuna baadhi ya watu wamekuwa wakifaidika na baadhi ya mambo hivyo wasingependa mabadiliko ya kumkomboa mwananchi wa kawaida yatokee, katika picha kushoto ni Makdeo Makeja mratibu msaidizi WARAMI
  Makdeo Makeja mratibu msaidizi WARAMI akifafanua jambo wakati viongozi hao wa taasisi ya WARAMI walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam , kulia ni John Marwa Mratibu wa Chama cha Watetezi wa Rasilimali Wasio na Mipaka WARAMI

  0 0

  Katibu mkuu: Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Joseph Nyamhanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kutozwa kwa vyombo vya usafiri vitavyopita katika Daraja la Nyerere kuanzia jumamosi ya Mei 14.(Picha na Raymond Mushumbusi) MAELEZO

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Serikali imetangaza rasmi kuanza kwa tozo kwa vyombo vya usafiri vitakavyopita katika daraja la Nyerere kuanzia Jumamosi tarehe 14 ,mwezi huu.Akizungumzia na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema kuwa kuanzia siku hiyo , vyombo vyote vya usafiri vitatakiwa kulipia ushuru wa kupita katika daraja la Nyerere.

  “ Tumeanza kutoza tozo hii mara baada ya kufunguliwa kwa daraja hili na kuanza kutumika kwa kupita bila kulipa kwa vyombo vya usafiri tangu Aprili 19 mwaka huu na sasa tunaanza rasmi kutoza tozo kwa ajili ya kukusanya gharama za usimamizi, utunzaji na uendeshaji wa daraja hili.” alisema Mhandisi Nyamhanga.

  Mhandisi Nyamhanga amefafanua kwamba watembea kwa miguu watapita bure katika daraja hilo huku wenye baiskeli wakilipia Sh. 300, pikipiki Sh. 600, waendesha maguta ,bajaji na magari ya kawaida(Saloon Cars) watatakiwa kulipia Sh.1500.Mabasi yanayobeba abiria 15 yatalipia Sh. 3,000, yale ya abiria zaidi ya 15 Sh. 5,000 na yale yanayobeba abiria zaidi ya 29 yatalipia Sh. 7,000.

  Aidha magari yenye tani zaidi ya mbili mpaka saba yatalipia Sh. 7,000, tani 7 hadi 15 watalipa Sh.10,000, tani 15 mpaka 20 watalipa Sh.15,000 na yale yenye tani 20 mpaka 30 yatalipia Sh. 20,000.

  Mhandisi Nyamhanga ameongeza kuwa magari yenye namba za Jeshi la Wananchi(JWTZ), Jeshi la Polisi(PT), Jeshi la Magereza(MT), gari za wagonjwa, magari ya zimamoto na magari yenye vibali maalum yataruhusiwa kupita bure.

  0 0

  Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu tathmini ya hali halisi kuelekea ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini ifikapo mwezi june 2016 ambapo kiwango cha simu Bandia Kimepungua kutokana na Elimu inayotolewa na Mamalaka hiyo kwa wananchi. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.
  Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Mawasiliano (TTMS) toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Injinia Gabriel Mruma akiwaeleza waandishi wa habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kutumia simu zenye ubora unaokubalika ili kuepuka athari zinazotokana na matumizi ya simu Bandia. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy .(Picha na Hassan Silayo- MAELEZO ).


  Frank Mvungi-MAELEZO

  Serikali imewataka wauzaji wa vifaa vya Mawasiliano vya mkononi (mobile devices) kuacha mara moja tabia ya kubadilisha namba tambulishi (‘kuflash’) za vifaa hivyo kwani watakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka 10 au faini isiyopungua milioni 30 au vyote viwili.Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.

  “Namba tambulishi (IMEI) za vifaa vyote vya Mawasiliano ya mkononi ambavyo vimeibiwa,vimeharibika,kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaruhusiwa kuunganishwa kwenye mitandao ya watoa huduma ifikapo tarehe 16 June 2016. “Aalisema Mungy.

  Akizungumazia kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi ya simu zote zisizokidhi viwango, Mungy alibainisha kuwa idadi ya simu hizo imeshuka kutokana na elimu ambayo wameitoa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.Alisema lengo la elimu hiyo kwa umma ni kujenga uwezo kwa wananchi kutambua simu zisizokidhi vigezo kabla ya kufika ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini.

  Mungy alifafanua kuwa uchambuzi wa IMEI unaonyesha kuwa hadi Februari,2016 idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia 3 ambapo namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 18 na simu halisi zilikuwa sawa na asilimia 79.

  “Kwa mwezi Machi 2016 ulionyesha kuwa Idadi ya namba tambulishi ambazo hazina viwango ni asilimia 4, na idadi ya zile zilizonakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 13 ambapo uchambuzi huu umehusisha taarifa za kampuni zote za simu nchini’’. Alifafanua Mungy.

  Aliongeza kuwa matokeo hayo mazuri ni matunda ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya Mamlaka hiyo, Shirika la viwango Tanzania (TBS),Tume ya ushindani (FCC),kampuni za simu, pamoja na wadau wengine katika kuelimisha umma juu ya uhakiki wa simu walizo azo ikiwa ni pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kununua simu ikiwemo kuzihakiki ubora wake.

  Kwa Upande Wake Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Injinia Gabriel Mruma amesema kuwa ni vyema watanzania wakajenga utamaduni wa kununua simu zenye ubora kuepuka usumbufu wakati Tanzania inapoelekea ukomo wa matumizi ya simu bandia.

  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni Taasisi ya Serikali yenye Dhamana ya kusimamia shughuli za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta hapa nchini.Kuwepo kwa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 na Kanuni zake za mwaka 2011 kumewezesha kutekelezwa kwa mfumo wa rajisi ya namba za Utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi.

  Mfumo huu wa kielektroniki ulizinduliwa tarehe 17 Desemba 2015 na unahifadhi kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi kwa lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vilivyoibiwa,kuharibika au kupotea,bandia vya mawasiliano katika soko.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo (pichani) akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa siku tatu jijini Dar es Salaam uliokutanisha wataalam kutoka nchi mbalimbali kwa ajili ya kujadili taarifa ya mtaalam mwelekezi kuhusu utafiti uliofanywa katika Ziwa Ngozi lililopo mkoani Mbeya ambapo kuna viashiria vya jotoardhi pamoja na eneo la Kibiro nchini Uganda.
  Wataalam mbalimbali wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo ( anayeonekana mbele kwa mbali)
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo (wa nne kutoka kushoto waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo mara baada ya ufunguzi.

  Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

  Imeelezwa kuwa Tanzania inatarajia kuzalisha megawati 100 ndani ya kipindi cha miaka saba ijayo na kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.

  Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk. Juliana Pallangyo katika mkutano uliokutanisha wataalam kutoka nchi mbalimbali kwa ajili ya kujadili taarifa ya mtaalam mwelekezi kuhusu utafiti uliofanywa katika Ziwa Ngozi lililopo mkoani Mbeya ambapo kuna viashiria vya jotoardhi pamoja na eneo la Kibiro nchini Uganda.

  Wataalam katika mkutano huo ulioandaliwa na Kampuni ya Maendeleo ya Jotoardhi Tanzania (TGDC) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje Iceland, wanatoka katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Eritrea, Marekani, New Zealand na Djibouti.

  Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo wa siku tatu Dk. Pallangyo alisema kuwa kutokana na ugunduzi wa nishati ya jotoardhi nchini Tanzania, serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa ndani ya kipindi cha miaka saba ijayo inazalisha megawati 100 zitakazoongezwa kwenye gridi ya taifa na hivyo kupunguza tatizo la upungufu wa umeme nchini.

  Alisema kuwa serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inachangia katika ukuaji wa uchumi na kupelekea nchi kutoka kwenye orodha ya nchi masikini duniani na kuingia katika nchi zenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, kama Dira ya Maendeleo ya Taifa inavyofafanua.Aliongeza kuwa kuwepo kwa nishati ya uhakika kutavutia uwekezaji kwenye viwanda na kuzalisha ajira na nchi kupiga hatua kimaendeleo.

  Alisisitiza kuwa Tanzania ina nishati ya kutosha ya jotoardhi yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 5000 ambayo haijatumika bado ambapo serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Jotoardhi Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  Aliendelea kusema kuwa TGDC ilianzishwa Desemba 2013 kwa madhumuni ya kusimamia maendeleo ya jotoardhi nchini Tanzania na kuanza rasmi shughuli zake Julai 2014 jukumu lake kuu likiwa ni kutafiti, kuchimba na kutumia rasilimali za jotoardhi kwa uzalishaji umeme na matumizi mengine ya moja kwa moja.

  0 0

  Mweneyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipewa maelezo ya awali na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alipowasili kukagua daraja lla Nyerere, leo Mei 10, 2016. Kulia ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph Nyamhanga, akimpokea Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipowasili kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na viongozi mbalimbali waliompokea, kabla ya kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama barabara zinazopishana ya chini na ya juu mwanzoni mwa daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo, leo
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama barabara zinazopishana ya chini na ya juu mwanzoni mwa daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo, leo
  Msafara wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ukipita kwenye daraja la Nyerere kwenda Kigamboni, alipokagua daraja hilo leo
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu jakaya Kikwete akiangaza mandhari ya darala la Nyerere alipokagua daraja hilo leo
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimuuliza jambo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph Nyamhanga (kulia), wakati akikagua daraja la Nyerere leo Kulia kwake ni Mama Salma Kikwete 
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu kwenye daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo leo
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama salma Kikwete wakitembea kwenye daraja hilo leo. ushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipita eneo ambalo magari yatakuwa yakilipia ushuri, alipokagua daraja la Nyerere, leo 
  Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama moja ya ofisi zitakazotumiwa na magari kulipia ushuru wa kutumia daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo leo Mei 10, 2016
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Ofisa Uhusiano wa NSSF, Kiamba Rajabu, alipokagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na akipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Mipango na Ujenzi wa NSSF, Yakub Kidula, kuhusu eneo la magari kulipia ushuru alipokuwa akikagua daraja la Nyerere leo. Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na akipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Mipango na Ujenzi wa NSSF, Yakub Kidula, kuhusu eneo la magari kulipia ushuru alipokuwa akikagua daraja la Nyerere leo. Kulia ni Mama Salma Kikwete
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipanda ngazi kwenda kwenye ofisi za Utawala unaosimamia utoaji huduma za daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo leo
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama salma Kikwete wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na uongozi unaosimamia huduma za daraja la Nyerere baada ya kukagua daraja hilo leo
  Dajala hilo la Nyerere na barabara zake linavyoonekama
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama salma Kikwete wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na uongozi unaosimamia huduma za daraja la Nyerere baada ya kukagua daraja hilo leo. Kushoto kwa Jkk ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph Nyamhanga
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa maneno ya shukurani kabla ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu jakaya Kikwete kuondoka baada ya kukagua Daraja la Nyerere leo. Daraja hilo ambalo lilianza kujengwa wakati Kikwete anamalizia awamu ya mwisho ya uongozi wake wa Urais, limefunguliwa hivi karibuni na Rais wa awamu ya tano Dk. John Magufuli baada ya kukamilika. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

  Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde leo amefanya ziara ya kushtukiza katika kambi tiba ya GSM Foundation inayofanywa na kikosi cha Madaktari bingwa kutoka hospitali ya MOI, ambayo kuanzia leo imepiga kambi Dodoma baada ya kutoka katika mikoa ya Mwanza, Singida, na Shinyanga.

  Akieleza sababu za kuitembelea kambi hiyo ambayo iko katika hatua zake za mwisho kumaliza awamu ya kwanza, Mheshimiwa Mavunde amebainisha kwamba kwanza, ni kwa sababu alisikia kambi iko katika jimbo lake, lakini jingine kubwa na la msingi likawa ni kupeleka shukrani zake kwa Maafisa wa Taasisi ya GSM wanaoambatana na madaktari kuweka kambi tiba hizo katika kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na migongo wazi kila mwaka.

  "Nimeshtushwa na takwimu za mwaka juzi, kwamba wanaozaliwa ni 4000 na wanaorudi hospitali kwa ajili ya tiba hawazidi 600. Hii ni hatari, ilipaswa mtu kuchukua jukumu la haraka na nimeshukuru kusikia GSM mmefanya hilo, hongereni sana", alisema Mavunde.

  Mavunde amewataja Maafisa wa GSM na Madaktari kuwa ni watu wenye moyo wa kizalendo ambao wanatakiwa kuigwa na jamii, wameacha familia zao, na wameamua kuokoa maisha ya watoto ambao hata hawawajui, kwa sababu moja tu kubwa na ya msingi ya utanzania.

  PICHANI JUU: Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(Wa Pili kutoka kulia) akikaribishwa eneo la Hospitali na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw Jordan Rugimana(Wa tatu kutoka kulia) na Naibu Mkurugenzi wa MOI ambaye ndio mratibu wa kambi tiba ya GSM DK Othman KIloloma(Wa nne kutoka kulia) na Meneja wa Taasisi ya GSM BI Shannon Kiwamba(kushoto)
  Mh Mavunde akisikiliza maelezo ya mmoja kati ya wagonjwa waliohudhuria kambi tiba ya GSM
   Mratibu wa Kambi Tiba ya GSM, Dk Othman Kiloloma akimpa taarifa za wagonjwa Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini
   Mh Mavunde akiongea na wanahabari waliokuwa hospitalini hapo kufuatilia habari za wagonjwa waliohudhuria kambi tiba ya GSM
  Mh Mavunde akibadilishana mawazo na mratibu wa kambi tiba ya GSM, Dk Othman Kiloloma, wanaosikiliza ni Kibwana Matukio kutoka GSM, na Mganga mkuu wa mkoa Bw Jordan Rugimana

  0 0

  BABA Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Michael Kagondela kulia na Mhasibu wa mtandao huo, Asha Salvador baada ya kumkabidhi kadi ya uanachama na katiba baada ya kikao cha kuthibitisha mwanae kukubali kupewa ekari tano za kujenga kituo cha wanamichezo, Mkuranga
  BABA Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati) akijaza fomu za kukubali masharti ya kujiunga na Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) mbele ya Mhasibu wa mtandao huo Asha Salvador.

  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa sherehe za kumkabidhi eneo la kujenga kituo cha michezo mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta katika sherehe zitakazofanyika Juni 4, 2016 kwenye kijiji cha Wasani Mwanzega Mkuranga.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa maandalizi ya sherehe hizo itaambatana na ugawaji nyumba 31 kati ya hizo moja kubwa, tatu ndogo na misingi 27 ya nyumba hivyo kufikisha jumla ya nyumba 150.

  Alisema baba yake Mbwana Mzee Ali Samatta amethibitisha kuwepo kwa mwanae katika sherehe hizo ambazo naye ametunukiwa kuwa mwanachama wa heshima wa mtandao huo na kukubali kushirikiana kuhakikisha michezo inakuwa nchini.

  “Baba yake Samatt alisema wakati akiwa kijana alikuwa mfungaji mzuri kwa timu alizowahi kuchezea miaka ya sitini kama vile timu ya shele ya Sekondari ya Mzumbe, timu ya mkoa wa Morogoro, timu ya Polisi na badaye aliwahi kuichezea Simba akiwa na akina Hamisi Kilomoni” alisema Taalib.

  Alisema sherehe hizo pia zitapambwa na wasani kutoka vikundi mbalimbali vya ngoma na sarakasi kutoka jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani..

  Alisema SHIWATA ilimzawadia uanachama wa heshima mchezaji huyio baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika na kutangaza kumpatia eneo la ekari tano kwa ajili ya kujenga kituo cha wanamichezo.

  0 0

  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akibadilishana hati za makubaliano na Afisa Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa,Dkt Ellen Mkondya wakati wa hafla ya makabidhiano ya hati hizo iliyofanyika wilayani Kahama.
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu,Graham Crew pamoja na Afisa Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Dkt Ellen Mkondya wakitia saini katika hati za makubaliano ya kuboresha mradi wa huduma ya afya ,Zoezi la utiaji saini ulishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa(kulia) ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala,Patrick Karangwa (nyuma ya mkuu wa wilaya) pamoja na viongozi wa Mgodi wa Bulyanhulu ,Elias Kasitila na Mganga Mkuu wa wilaya ya Msalala Dkt Hamad Nyembea.
  Meneja wa Mgodi wa Bulyanhulu ,Graham Crew akizungumza mara baada ya kutiliana saini makubaliano ya kuboresha huduma za Afya na Taasisi ya Benjamini William Mkapa wakati wa hafla iliyofanyika katika mji wa Kahama.
  Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu kwa michango ambao wameendelea kutoa kwa wilaya ya Kahama na Msalala.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyeko Shinyanga.

  MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilayani Kahama umetiliana saini hatii ya makubaliano ya Dola 200,000 sawa na shilingi Milioni 440 za Tanzania na Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF) kwa ajili ya mradi wa kuboresha huduma za afya ya uzazi kwa mama na mtoto katika wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga

  Mgodi Bulyanhulu kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Acacia na Taasisi ya Benjamin W. Mkapa (BMF) wamesaini hati ya makubaliano ili kushirikiana katika kutekeleza mradi wa miaka miwili unaolenga kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto katika jamii .

  Mgodi wa Bulyanhulu kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Acacia utatoa kiasi cha dola za Kimarekani 200,000 kusaidia awamu ya pili ya mradi wa BMF utakaosaidia kuboresha huduma ya vituo viwili vya afya wilayani humo, Kituo cha Afya cha Bugarama na Zahanati ya Kakola kupitia mradi huo.

  Mradi huo katika vituo tajwa unatarajiwa kunufaisha wananchi 321,852 katika Halmashauri ya Msalala ambapo makubaliano hayo ya miaka miwili yanaanzia, 01 April 2016 hadi 30 Machi 2018.

  “Mgodi wetu unaendesha shughuli zake katika halmashauri ya Msalala hapa mkoani Shinyanga na sehemu ya uwajibikaji wetu kwenye jamii, kupitia mkakati wa mipango endelevu kwenye jamii na kusaidia mikakati ya uboreshaji wa sekta ya afya kwa ajili ya jamii inayozunguka mgodi.”alisema Graham Crew.

  “Ushirikiano huu na Taasisi ya BMF umekuja wakati muafaka ambapo BGML imewekeza katika miundombinu ya kuipandisha hadhi zahanati ya Bugarama kuwa kituo cha afya na pia kumalizia ujenzi wa Zahanati ya Kakola.” Aliongeza meneja huyo mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew.

  Awamu ya pili ya Mradi wa BMF inalenga kutekeleza mradi utakaoboresha huduma za HIV/AIDS, huduma za mama na mtoto kwa kuongeza upatikanaji wa wataalamu wa afya na kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa BMF Dk Ellen Mkondya Senkoro amesema; “Takwimu zinaonyesha kwamba mkoa wa Shinyanga una maambukizi kwa asilimia 7.4% ambapo kiwango kikubwa kipo katika halmashauri ya Msalala kutokana na shughuli za uchimbaji madini hasa uchimbaji mdogo mdogo.”

  “Kiwango hiki kimeendelea kuwa hivyo tangu mwaka 2007/2008 hadi 2011/2012 ingawa kiwango cha maambukizi nchini kimepungua kutoka asilimia 5.7% hadi 5.1% hivyo sehemu hii inahitaji hatua maalumu. “alisema Dkt Mkondya.

  Alishukuru Kampuni ya ACACIA kwa msaada huo na kwamba utasaidia kwenye utekelezaji wa uboreshaji wa mifumo ya kukabiliana na tatizo la Virusi vya Ukimwi, huduma za uzazi na watoto kwa kuongeza rasilimali watu ya watalaamu wa afya, uendelezaji wa miundombinu na kujengea uwezo maeneo yanayohitaji ufanisi zaidi.

  Tangu mwaka 2013 Taasisi ya Benjamin William Mkapa (BMF) imekuwa ikishirikiana na Acacia kupitia Mfuko wake wa Acacia Maendeleo Fund katika kutekeleza sehemu ya miradi ya awamu ya pili ya mfuko wa taasisi ya BMF katika wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera na Halmashauri iliyokuwa ya Kahama mkoani Shinyanga.

  Kuhusu Mfuko wa Maendeleo wa Acacia:

  Mfuko wa Maendeleo wa Acacia maarufu kama Acacia Maendeleo Fund ulianzishwa mwaka 2011 kama sehemu ya dhamira katika kuboresha maendeleo endelevu katika jamii kwenye maeneo tunayofanya kazi. Hadi sasa tumefanikiwa kuwekeza dola za kimarekani milioni 35.0 katika miradi 150 kwenye maeneo mbalimbali.

  Misaada kutoka kwenye mfuko huu hutoa kipaumbele kwa vitega uchumi vinavyosaidia maendeleo ya jamii, ujengaji wa uwezo, sekta ya afya, elimu, maji, mazingira katika maeneo tunakoendesha shughuli zetu.

  Taasisi ya Benjamin W. Mkapa 

  Taasisi ya Benjamin W. Mkapa ilianzishwa April 2006 na Rais Mtaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Benjamin W. Mkapa, taasisi hii isiyo ya kiserikali ina dhamira ya kuboresha afya na hali za watanzania hasa katika maeneo yaliyoko vijijini kwa kutekeleza miradi yenye kutoa matokeo.

  0 0

  Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanania Dk. Gharib Bilal wa tatu kutoka kushoto na Mama Salma Kikwete wa kwanza kushoto wakishiriki mazishi ya Merehemu Benadette Izengo mama wa Mkurugenzi wa kampuni ya Montage Limited Teddy Mapunda aliyekaa katikati yao pamoja na wanafamilia wengine wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanis kuu la Mtakatifu Joseph. 
  Mke wa Rais Mstaafu Dk Jakaya Kikwete Mama Salma Kikwete akiweka mchanga kaburini wakati aliposhiriki mazishi ya Marehemu Mama Benadette Izengo yaliyofanyika jana kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
  Balozi Asha Rose Migiro akiweka mchanga kaburini wakati wa maishi ya marehemu mama Benadette Izengo.
  Fathre Matumaini akiongoza ibada ya mazishi ya Marehemu Mama Benadette Izengo iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Josepha jana.
  Wanafamilia wakiwa katika ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph jana jijini Dar es salaam na kufuatiwa na mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni.
  Teddy Mapunda na Ndugu yake wakiwa pembeni mwa jeneza la mama yao mpendwa marehemu Benadette Izengo.
  Mkwe wa Marehemu mama Benadette Izengo akishiriki ibada ya mazishi pamoja na ndugu na jamaa wa familia kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph jana.
  Wajukuu wa marehemu wakishiriki ibada hiyo jana.
  Wana familia wakiwa na majonzi kwa kuondokewa na mpendwa mama yao Marehemu Mama Benadette Izengo.
  Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mzee Jon Momose Cheyi akishiriki sakramenti ya bwana kutoka kwa Father Kaombwe wakati wa ibada hiyo ya mazishi
  Teddy Mapunda na Mumewe Nestor Mapunda wakiwa na majozni huku wakiangalia jeneza la mama yao mpendwa marehemu mama Benadette Izengo.
  Baadhi ya waombolezaji wakishiriki mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
  Kutoka kushoto ni Jeseph Kusaga Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Enertainment, Nandi Mwiyombela, Justin Pamba, Godfrey Kusaga na John Mbele nao walishiriki katika mazishi hayo ya mama Bebadette Izengo.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaagiza kutoka nje ya nchi tani 70,000 za sukari ambapo kati ya hizo, tani 11,957 zimeshawasili nchini na zitaanza kusambazwa kesho (Jumatano).

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 10, 2016) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam.

  Akitoa ufafanuzi wa sukari ambayo imekwishawasili nchini, Waziri Mkuu alisema tani 2,000 zitapelekwa mikoa ya Kaskazini, tani 3,000 (mikoa ya Kanda ya Ziwa), tani 2,000 (mikoa ya Kusini), tani 2,000 (Nyanda za Juu Kusini) na tani 2,000 (mikoa ya Kanda ya Kati).

  “Tani nyingine 24,000 za sukari zitawasili Ijumaa hii na hadi zitoke bandarini itakuwa kama Jumapili kwa hiyo zinaweza kusambazwa kuanzia Jumatatu. Tani nyingine 20,000 zitawasili baadaye, ama mwishoni mwa mwezi huu au mapema mwezi Juni,” alisema Waziri Mkuu.

  Amesema anawataka Watanzania wasihofu kuhusu uhaba wa sukari uliojitokeza hivi karibuni kwani umesababishwa na watu wachache. “Mheshimiwa Rais ameagiza watu waliohodhi bidhaa hii wakamatwe na sukari isambazwe. Lakini pia tunaagiza kwa muda mfupi kwa sababu viwanda vyetu vinatarajia kuanza uzalishaji ifikapo Julai,” alisema.

  Amewataka wasambazaji wa sukari waziuze kwa wafanyabishara wadogo ili wao wawawuzie wananchi kwa bei elekezi ya sh. 1,800. Pia amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi la ukaguzi ili kubaini zaidi wale waliohodhi bidhaa hiyo.

  Akifafanua kuhusu mkakati wa Serikali kuongeza uzalishaji wa sukari nchini, Waziri Mkuu amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha tatizo la uhaba wa sukari nchini linakwisha ifikapo 2019. “Wananchi wasiogope, Serikali imechukua hatua kwa udhibiti mzuri ili tusije kuporomosha soko letu la ndani,” alisema.

  “Tunao mkakati wa kuboresha viwanda vya ndani, wenye viwanda wenyewe au kwa ubia na wawekezaji kutoka nje, wanaweza kufungua mashamba kwenye maeneo matatu tuliyotenga kwa ajili hiyo,” alisema.

  “Serikali imetenga maeneo matatu yanayofaa kwa kilimo cha miwa huko Bagamoyo, Ngerengere na Kigoma. Huko wanaweza kulima na kujenga viwanda vya sukari na uzalishaji ukawa unapanda mwaka kwa mwaka hadi tutakapoweza kuimaliza hii gap iliyopo,” alisema.
    

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMANNE, MEI 10, 2016.

  0 0


  Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve (CCM) akiuliza swali kwa Waziri wa Nnchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), bungeni Dodoma , kwamba ni fedha kiasi gani kimetengwa kwa ajili ya maendeleo ya vijana na wanawake mkoani Iringa. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
   Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde (kushoto), akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve (katikati) pamoja na Mbunge wa Viti Maalum, Kiteto Koshuma kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

older | 1 | .... | 843 | 844 | (Page 845) | 846 | 847 | .... | 1903 | newer