Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 844 | 845 | (Page 846) | 847 | 848 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mtaalam Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti akieleza jambo kwa waandishi wa habari juu ya kushiriki shindano la kuongeza kipato lijulikanalo kama “Scaling Competition” kwa makundi yanayoruhusiwa kushiriki shindano hilo kuwa ni pamoja na vikundi vya akiba, bima ndogo ndogo na mifumo ya umoja wa fedha, fomu za maombi na mwongozo wa kushiriki shindano hilo zinapatikana katika tovuti ya www.frp.org .
  Mtaalam Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti akifafanua jambo katika semina ya namna shirika hilo linavyofanya kazi na jinsi ya kushiriki shindano la mwaka 2016 ili kupata washindi watakaopata msaada wa kifedha na kuboresha ushirikishwaji wa kifedha kwa wakulima wadogo Afrika.

  Na: Lilian Lundo – Maelezo

  Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano la kuongeza kipato lijulikanalo kama “Scaling Competition” kwa kutuma maombi yao shirika la “Master Card Foundation, Fund For Rural Prosperity” ili kupanua na kuimarisha upatikanaji wa fedha Vijijini Tanzania.

  Hayo yalisemwa na Mtaalam Mshauri wa Master Card Foundation Gabriel Kivuti leo, jijini Dar es Salaam katika semina ya namna shirika hilo linavyofanya kazi na jinsi ya kushiriki shindano la mwaka 2016 ili kupata washindi watakaopata msaada wa kifedha na kuboresha ushirikishwaji wa kifedha kwa wakulima wadogo Afrika.

  “Master Card Foundation inafanya kazi na mashirika yenye maono ili kuleta zaidi upatikanaji wa elimu, mafunzo ya ujuzi na huduma za kifedha kwa watu wanaoishi katika umaskini barani Afrika, ikiongozwa na dira ya kuboresha mafunzo na kuongeza ushirikishwaji wa upatikanaji wa kifedha ili kupunguza umaskini,” alisema Kivuti.

  Kivuti alisema kuwa, kaya nyingi za vijijini barani Afrika hazishirikishwi katika masuala ya kifedha na zaidi ya asilimia 70 za familia Kusini mwa Jangwa la Sahara sehemu kubwa ya mapato yao yanatokana na shughuli za kilimo, wakati huohuo watoa huduma za kifedha wanakabiliana na changamoto kadhaa katika kuifikia jamii, hivyo Master Card likaamua kusaidia miradi ambayo ina uwezo wa kuleta mabadiliko chanya.

  Aidha, Kivuti alitaja makundi yanayoruhusiwa kushiriki shindano hilo kuwa ni pamoja na vikundi vya akiba, bima ndogo ndogo na mifumo ya umoja wa fedha, fomu za maombi na mwongozo wa kushiriki shindano hilo zinapatikana katika tovuti ya www.frp.org .

  Jumla ya dola za Kimarekani milioni 10.6 zimetolewa kwa washindi wa mwaka 2015 kwa ajili ya maendeleo Vijijini, kampuni zilizoshinda ni APA Insurance Ltd kutoka Kenya, Finserve Afrika Ltd/Equitel kutoka Uganda, M-KOPA LLC kutoka Tanzania, Musoni Kenya Ltd kutoka Kenya na Olam Uganda Ltd kutoka Uganda. Kupitia kampuni hizo takribani watu milioni nane wanaoishi maeneo ya Vijijini watakuwa na fursa ya kupata huduma za kifedha ifikapo mwaka 2020

  0 0

  Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kupambana na Ukimwi nchini (TACAIDS) imemteua msanii maarufu Mrisho Mpoto kuwa balozi wa kampeni ya Kili Challenge.

  Kili Chalenge ni kampeni inayolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kutunisha mfuko wa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI. Kampeni hiyo ilianzishwa miaka 15 iliyopita na hufanyika kila mwaka kwa wadau mbalimbali kupanda mlima Kilimanjaro.Mwaka uliopita 2015 watu 39 walifanikiwa kupanda Mlima na kuchangisha fedha zaidi ya Sh bilioni 1.2  ambazo zitagawiwa kwa Asasi mbalimbali tarehe 20 Mwezi huu pale Hyatt Regency Dar es Salaam,Mgeni rasmi atakuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

  Mrisho Mpoto ameteuliwa kuiwakilisha na kuitangaza kampeni hii ili kusaidiana na serikali pamoja na wadau mbalimbali ndani na nje ya Tanzania kupambana na janga hili la Taifa. Mrisho Mpoto anakuwa Balozi mpya katika Kampeni hii kwa sababu ni msanii mwenye ushawishi ndani ya jamii na kupitia kazi zake za kisanaa tunaamini ataweza kuihamasisha jamii ipasavyo kuona umuhimu wa kumaliza tatizo la VVU na UKIMWI hasa katika masuala ya unyanyapaa.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Fatma Mrisho, “Inakadiriwa kuwa watu milioni 1.6 nchini wanaishi na VVU & Ukimwi. Ugonjwa huo umewaathiri zaidi vijana na watoto yatima zaidi ya milioni 1.3. Tunahitaji kubadilisha hali hii.  TACAIDS kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na wadau wengine kwa kupitia mpango huu wa Kilimanjaro Challenge tunapenda kutoa mchango na ushirikiano wetu kwa Taifa ili kutunisha mfuko utakaowezesha kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo”.

  Napenda kuupongeza  Mgodi wa Dhahabu wa Geita kwa kushirikiana na wadau wengine kwa kuamua kwa dhati kwa kipindi cha miaka 15 kuwekeza katika mradi huu kwa kuuwezesha kuwa mradi wa kitaifa na si wa GGM, hivyo pamoja na balozi wetu hivi sasa Mrisho Mpoto,  tuungane nao ili kuongeza chachu kwa wadau wengine kujitokeza kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya janga hili” alisisitiza Dkt Fatma Mrisho.

  “Kwa kushirikiana na Mpoto tuna matumaini ya kujenga timu imara yenye hamasa ya kupambana na janga hili. Tunatoa wito kwa makampuni na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, wajitokeza ili tushirikiane kutunisha mfuko wa Kilimanjaro Challenge na mwishowe kufikia ndoto au malengo ya nchi yetu ya kuhakikisha tunakuwa na kizazi kisicho na maambukizi ya VVU na Ukimwi” alisema Bw. Simon Shayo Makamu wa Raisi wa miradi endelevu wa Anglogold Ashanti (GGM).

  Shayo alisisitiza kwa kusema “GGM iko tayari kushirikiana na wadau wengine wenye nia ya dhati, kuungana pamoja kupitia mfuko wa Kili Challenge katika kuhakikisha maambukizi haya hayaendelei kuleta athari kwa jamii yetu kwa sababu serikali yenyewe haitaweza kutokomeza tatizo hili”.

  Naye Balozi mpya wa Kili challenge, Mrisho Mpoto alisema; “Nashukuru sana kwa kupata fursa hii ya kuweza kutoa mchango wangu katika kuisaidia jamii kuepukana na janga hili. Changamoto kubwa inayotokana na janga hili la VVU &UKIMWI ni ongezeko la maambukizi ya VVU kwa vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa letu pasipo kila mmoja wetu kujitoa kwa dhati hatutalimaliza janga hili. Napenda kuwaambia watanzania wenzangu kwamba tushirikiane kwa pamoja ili tuangamize janga hili”

  Pamoja na hatua kubwa zilizopigwa na serikali ikishirikiana na wadau, kumekuwapo na ongezeko la maelfu ya watoto yatima wanaohitaji misaada baada ya wazazi wao kufariki, wajane wasiokuwa na kipato, pamoja na wazee wanaolazimika kuwalea wajukuu walioachwa na watoto wao ambao walifariki kutokana kwa ugonjwa huo alisisitiza Mkurugenzi mtendaji wa TACAIDS.

  Kilimanjaro Challenge ni mradi unaolenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu ugonjwa wa Ukimwi na Virusi Vya Ukimwi (VVU). Pia inalenga kuchangisha fedha ili kujenga timu imara itakayoendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.Ili kuweza kuwa sehemu yawatakaopanda Mlima Kilimanjaro, kwa kupitia Kili Challenge mwaka huu, uwe Mtu binafsi au kupitia shirika kulipia wafanyakazi wake kupanda mlima mchango ni $5,000 tu ambazo zitalipia gharama za upandaji na kuchangia mfuko wa Kili Challenge.

  Kilimanjaro Challenge imebakia kuwa chombo muhimu kinachoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya nchi katika mapambano dhidi ya VVU&Ukimwi kwa jamii ya Kitanzania na dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii inabaki bila kuathiriwa na ugonjwa huo katika miaka ijayo
  Mpango huo pia unalenga kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU & Ukimwi pamoja  na kutoa nafasi kwa watalii wa ndani kuupanda mlima Kilimanjaro.


  KUHUSU Kili Challenge:
  Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.anglogoldashanti.com  na www.geitakilichallenge.com

  0 0


  Na  Bashir  Yakub.


  1.WAKFU  NININI.

  Sheria ya  Mirathi na  Usimamizi  Mali Sura  ya  352  ndiyo  sheria  inayoeleza  masuala  yote  ya  msingi  kuhusu   habari  nzima  ya  Wakfu. 

  Kwa  mujibu  wa  sheria  hiyo kifungu  cha  140  Wakfu  ni  kutoa  mali  kulingana  na    sheria  za  kiislam  kwa  ajili  ya  dini, hisani  au  kwa  ajili  ya watu/mtu  wa  familia  fulani.


  Suala  la  Wakfu  huenda  sambamba   na  suala  la  wadhamini.  Kwa  mujibu  wa  kifungu  hicho  wadhamini  ni  watu/mtu  ambaye  ndiye   hupewa  jukumu  la  kusimamia  mali  ya  wakfu. 


  Kama  ni  nyumba  yenye  wapangaji  basi mtu  au  watu  hao  ambao  ni  wadhamini  ndio  watahusika  na  kukusanya  kodi  pamoja  na  mambo  mengine  yote  yanayohusu   nyumba. Na  kama  kuna  maendelezo  yoyote ya ukarabati  au  vinginevyo   hawa  ndio  watahusika.


  2.  MAELEKEZO YA  MTOA  WAKFU LAZIMA YAFUATWE.

  Siku  zote  mtoa  wakfu  hutoa  mali  kwa  malengo  maalum. Yaweza  kuwa  malengo  ya  kiimani  au  vinginevyo. Mtoa  wakfu  anapotoa  nyumba/kiwanja  kama  wakfu  hutoa  kwa  maelekezo  ya  namna  na  jinsi  kitakavyotumika. Kwa  namna  mtoa  wakfu  atakavyotoa  maelekezo  ndivyo  hivyo  inavyotakiwa  kuwa.


  Ni  kosa  mali  ya  wakfu  kutumika   kinyume  na  maagizo  ya  mtoa  wakfu. Ikiwa  itatumika  kinyume  basi  kuwe  na  sababu  za  msingi  ambazo  zinalazimisha  hivyo. Ziwe  ni sababu  ambazo hakuna  namna  isipokuwa  ni  lazima kufanyika  hivyo.  Kifungu  cha  150(  1  ) cha  sheria  ya  mirathi  na  usimamizi  wa  mali  kinasema  kuwa  matumizi  ya  mali  za  wakfu  ni  lazima  yazingatie  nia  na  malengo  ya  mtoa  wakfu.


  Isipokuwa  kifungu  hicho  kinasisitiza  kuwa  nia  na  malengo  ya  mtoa  wakfu  yatafuatwa  tu  pale  ambapo   nia  na  malengo  hayo  yatakuwa  halali  kisheria. Ikiwa  mtoa  wakfu  ameelekeza  matumizi  ambayo   hayakubaliki  kisheria  basi  maelekezo   hayo hayatafuatwa.  Lakini ikiwa  hayapingani   na  sheria  yoyote  basi  ni  sharti  kuyafuata.
  0 0

  Na Benedict Liwenga, MAELEZO, Dodoma.

  Serikali imewaunga mkono Wachimbaji Wadogo wa Madini wa Busiri kwa kuwatafutia maeneo ya uchimbaji wa madini, ambapo Wizara ya Nishati na Madini imetenga eneo lenye ukubwa wa hekta 11,031 lililokuwa chini ya Leseni za Utafutaji namba PL 3220/2005 ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Bw. Daudi Mbaga pamoja na PL 5853/2009 iliyokuwa ikimilikiwa na na Meru Minerals Resources Limited ambazo zilizoisha muda wake.

  Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Medard Kalemani wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi kuhusu mikakati ya Serikali ya kuwaunga mkono Wachimbaji wadogo wadogo wa Busiri.

  Mhe. Kalemani ameeleza kuwa, hadi mwishoni mwa mwezi Machi, 2016, Wizara yake imegawa kwa wananchi wa Busiri leseni 81 za Uchimbaji Mdogo wa Madini (PMLs) katika eneo hilo, sawa na takribani hekta 810 kati ya hekta 11,031 za eneo lililoachwa kwa ajili ya Wachimbaji Wadogo.

  “Wizara imegawa leseni nyingine 30 za uchimbaji mdogo (PMLs) katika eneo lililopo katika kijiji cha Kuntakama takribani kilomita moja eneo la uchimbaji mdogo wa madini la Busiri”, alisema, Mhe. Kalemani.

  Ameongeza kuwa, mkakati mwingine wa Serikali ni kuendelea kulitumia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kutoa huduma ya ugani kwa wachimbaji madini wadogo wa kijiji cha Busiri na wengine wote nchini ikiwemo kutoa ruzuku kupitia Mfuko wa Wachimbaji Wadogo.“STAMICO pia itaendelea kuwapa elimu wachimbaji wadogo na kuwahamasisha kuunda Vikundi vya Uchimbaji ili waweze kusaidiwa kwa pamoja”, alisema Mhe. Kalemani.

  Aidha, Serikali imekuwa ikiwatembelea wachimbaji madini wa eneo tajwa mara kwa mara kwa kutumia Maafisa na Wataalamu wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi-Bukoba.Amefafanua kuwa, tarehe 11 Machi, 2016 Afisa Madini Mkazi wa Bukoba alifika na kufanya mkutano na kikundi cha Busiri Mining Co-operative Society Limited chenye Leseni Na. PML 001712WLZ.

  “Ili kutekeleza ombi la sasa la Mheshimiwa Mbunge, Wizara yangu itamtuma Afisa Madini wa Kanda ili awatembelee tena na kuwaelimisha juu ya fursa zilizopo za kuendeleza wachimbaji wadogo ili uchimbaji uwe wenye tija na kutoa ajira na kuondoa umaskini kupitia uchimbaji wa madini”, aliongeza, Mhe. Kalemani.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Entebbe, nchini Uganda kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni, kesho.


  0 0
 • 05/11/16--03:58: MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO
 • Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Mhe. Ummy Mwalimu (IMb) akisoma taarifa ya Bajeti ya Wizara yake Bungeni mjini Dodoma, 11 Mei, 2016.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bungeni mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) akifurahi na Wabunge wenzie nje ya Bunge mjini Dodoma.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DODOMA.

  0 0

  AccessBank yaendelea kuwakumbusha wateja kuweka fedha kwenye akaunti zao za”RAHISI inayowezeshwa na AccessMobile” na kisha wafanye miamala mingi ili waokoe muda na pesa zao.Sambamba na hilo, pindi mteja afanyapo miamala mingi, unaweza kujishindia simu mpya ya kisasa”brand new smart phone”.

  Pichani (kushoto) ni mmoja wa wateja ambao wamewahi kujishindia zawadi ya simu mpya na ya kisasa aina ya Huawei P8 kwa kufanya miamala mingi zaidi kupitia huduma maridhawa ya “RAHISI inayoweshwa na AccessMobile.

  Mr Amos Masunga (mmoja wa wateja ambao wamewahi kujishindia zawadi ya simu mpya na ya kisasa), akipongezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa AccessBank Tanzania, Mr. Roland Coulon.

  Akitoa maonijuu ya hili, Meneja Masoko wa AccessBank, Bw. Muganyizi Bisheko, alisema kuwa, “inafurahisha sana kuona huduma hii inafanya vizuri na imeweza kukidhi kisawa sawa mahitaji ya wateja. tutaendelea kuwaweka wateja wetu mbele na kuwazadia kwa uzalendo wao na uaminifu wao katika kutumia huduma zetu.”

  “Ningependa kuwashauri wateja waendelee kutumia mfumo wetu wa bure wa huduma za kibenki kwa njia ya simu, wafanye miamala mingi na wawashauri ndugu na jamaa kujiunga na mfumo huu kwa kutembelea tawi lolote la AccessBank huu ili nao waweze kufurahia miamala ya bure na kufuzu kwenye mfumo huu wa zawadi.”

  Mnamo 1/5/2015 AccessBank ilizindua huduma maridhawa ya “RAHISI inayowezeshwa na AccessMobile”, huduma inayomuwezesha mteja kupata huduma zote za kibenki bure kupitia simu ya mkononi  kama ifuatavyo;

  ·         kupata akaunti Bure isiyo na gharama za uendeshaji

  ·         kuweka na kutoa fedha Bure kwenye tawi lolote la AccessBank
  ·        Kuhamisha Fedha Bure: Kwenda Akaunti ya Benki/M-pesa/Airtel Money/Tigo Pesa.
  ·                    ·        Kulipia Bili Bure: Luku/Dawasco/DSTV na nyinginezo.
              ·        Kupata taarifa za akaunti Bure: Kujua salio, kupata taarifa fupi.
  ·                     ·        Kuongeza salio Bure: Vodacom/Airtel/Tigo/Zantel.

  Ili kujiunga na huduma hii mteja anatakiwa kutembelea tawi lolote la AccessBank lililo karibu nae na kisha atakua anapiga * 150*43# kufurahia huduma mbalimbali za Bure za kibenki mahali popote kupitia simu ya mkononi. Kwa maelezo zaidi mteja anaweza kupiga; 0659 074000, 0784 108500  AccessBank Tanzania ni Taasisi ya Kifedha inayolenga kutoa huduma za kibenki kwa wajasiriamali wadogo na wa kati. kupitia wanahisa wake wa kimataifa amabao ni AccessHolding, International Finance Corporation (Word Bank), KfW, African Development Bank na MicroVest, maono ya benki ni kujidhatiti katika uanzishaji wa mifumo ya kifedha unayochochea maendeleo ya jamii kwa kutoa huduma zilizobora kwa watu wote. 

  0 0


  TAARIFA KWA WADAU WA HABARI MKOA WA SHINYANGA KUHUSU WATU WASIO WAANDISHI WA HABARI KUTUMIA JINA LA UANDISHI WA HABARI KWA MANUFAA YAO BINAFSI.

  Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club-SPC) inapenda kuwataarifu wadau wa habari mkoa wa Shinyanga kuwa makini na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakidanganya kuwa ni waandishi wa habari wakati siyo waandishi wa habari.

  Miongoni mwa watu wanaotumia majina ya vyombo vya habari kutapeli na kujipatia fedha ni Emmanuel Mpanda ambaye kwa nyakati tofauti amelalamikiwa na wadau wa habari pamoja na baadhi ya waandishi wa habari kuwa amekuwa akijiita mwandishi wa habari akitumia majina mbalimbali ya vyombo vya habari hasa Televisheni na kusababisha usumbufu pale wadau wanapohitaji kuona habari zao.

  Klabu hii pia inafuatilia mienendo ya watu wengine wawili ambao pindi uchunguzi wetu utakapokamilika na kubaini udanganyifu wanaoufanya kwa wadau wa habari kwa kuwahadaa kuwa ni waandishi wa habari nao tutawaweka hadharani na kuviomba vyombo vya dola kuwachukulia hatua za kisheria.

  Tunapenda kuwatahadharisha kuwa makini na watu wa namna hiyo ambao wanajiita waandishi wa habari wakati siyo waandishi wa habari kwani mbali na kuvichafulia majina vyombo vya habari pia wanashusha thamani taaluma ya Habari,huku wakitutia doa tunaohusika na tasnia hii kwa  kuonekana sote hatufai.

  Ili kuhakikisha kuwa jamii inapata taarifa sahihi na kwa wakati muafaka tunaomba wadau wote wa habari muendelee kushirikiana na waandishi wa habari kwani jamii bila habari ni sawa na usiku wa giza.

  Tunaomba wadau wa habari pale panapotokea shughuli ama tatizo lolote msisite kuwasiliana na ofisi ya Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kwa kufika moja kwa moja ofisini au kupitia mawasiliano yaliyopo hapo juu.

  Tunatoa rai kwa waandishi wa habari kuwa na uchungu na taaluma yao na kutoruhusu tasnia ya habari kuchezewa kwa kuona haya kuwafichua Makanjanja ama kwa lugha nyingine “Waandishi wa Habari Hewa”,wanaodhalilisha taaluma hii.

   Lakini pia hatutasita kuchukua hatua kwa waandishi wa habari wanaoshirikiana na waandishi hewa kwa shughuli za kiuandishi wa habari.

  Tunaahidi kushirikiana na vyombo vya dola katika kuhakikisha kuwa taaluma ya uandishi wa habari inaheshimika.
  Imetolewa na
  Kadama Malunde
  Mwenyekiti SPC
  11.05.2016

  0 0


  MAADHIMISHO YA MIAKA SITA YA CHAMA CHA WATANZANIA WALIOSOMEA CHINA (CAAT)

  Chama cha Watanzania Waliosoma China kwa kiingereza China Alumni Association of Tanzania (CAAT) kinapenda kukukaribisha katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 6 (2010-2016) tokea kilipozaliwa.

  Sherehe hiyo itafanyika katika ukumbi wa Cardinal Laurian Rugambwa Social Centre pembezoni mwa kanisa la Mtakatifu Peter (St Peter), Oysterbay Ijumaa ya tarehe 20-May-2016 kuanzia saa 8 alasiri.

  Sherehe hiyo itahudhuriwa na viongozi wakubwa kutoka serikalini na baadhi ya wageni kutoka ubalozi wa China.

  Pamoja na burudani mbalimbali, maadhimisho hayo yatakuwa na hotuba kutoka viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wa ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China.

  Kwenye sherehe hiyo pia utafanyika uzinduzi wa tovuti (website) ya CAAT. Baada ya chakula cha pamoja cha jioni, vilevile kutakuwa na fursa ya wafanyabiashara,  wajasiliamali na wafanyakazi waajiriwa kuonyesha bidhaa au matangazo ya bidhaa au huduma wanazotoa.

  Dhima kuu ya tukio hilo ni;
  Utambulisho wa jumuia ya CAAT ambayo inajumuisha wataalam wa taaluma mbalimbali waliohitimu mafunzo yao katika Jamhuri ya Watu wa China
  Kubaini na Kuainisha fursa zinazopatikana Tanzania na China kupitia CAAT
  Maonyesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za biashara za wanajumuia.

  Wote mliopata kusoma China mnakaribishwa. Hakutakuwa na kiingilio.

  Unaweza kushiriki kwa kuthibitisha uwepo wako kwa kupiga simu kwa Katibu Mtendaji wa CAAT kwa kupitia 0783-992020 au 0715-200090 au email gsoreku@yahoo.com

  Asante

  George Oreku
  Katibu Mkuu
  Chama cha Watanzania Waliosoma China (China Alumni Association of Tanzania) 
  05-May-2015

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwenye kikundi cha ngoma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Entebe nchini Uganda. PICHA NA IKULU.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya maua kama ishara ya Ukaribisho kutoka kwa mtoto katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda mara baada ya kuwasili kutokea Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za mataifa mawili pamoja na ule wa Afrika Mashariki ukipigwa katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za mataifa mawili pamoja na ule wa Afrika Mashariki ukipigwa katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Maafisa mbalimbali waku wa vyombo vya Ulinzi wa Serikali ya nchini Uganda mara baada ya kuwasili nchini humo.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika Ikulu nchini Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima wakati kikagua gwaride rasmi la heshima mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwenye kikundi cha ngoma za asili mara baada ya kuwasili kwenye Ikulu ya nchini Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Pongezi wakati alipowasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.

  0 0
 • 05/12/16--00:10: DONDOO ZA MAGAZETI

 • 0 0

   Mstahiki Meya Wa Jiji la Tanga Mustafa Mhina akizungumza na kumhakikishia Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa ya kua kamwe hawezi kuyumbishwa na upinzani na Anawaahidi wana Tanga kufanya kazi kikamilifu ili kuleta maendeleo katika Jiji la Tanga.
  Na Woinde Shizza,Tanga

  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeitaka halmashauri ya Manispaa ya Mji wa Tanga kuitisha vikao vya madiwani kama kawaida na kumtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo atimize wajibu wake ipasavyo kabla hajachukuliwa hatua za kisheria .

  Imeelezwa kuwa haiwezekani kwa mtumishi yeyote  aliyeajiriwa na serikali ya ccm akawa mzandiki, adui na msaliti wa sera za serikali ya chama tawala.

  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ameeleza hayo  wakati akizungumza na wanachama wa uvccm na ccm kwenye ukumbu wa TANU Hall mjini hapa.

  Alisema ni jambo la kushanagaza kuona vikao ambavyo ndivyo vinavyotakiwa kujadili, kupanga mipango na kutekeleza program za maendeleo vikiwa haviitishwi kwa muda mrefu  kwasabahu za kipuuzi zisizo na mashiko.

  "Tunasikia  Meya wa Manispaa ya Tanga kupitia ccm kwamba CUF wana mpango wa kukununua ili uhame  ccm , tunakwambia kama kuna mkakati huo kataa, CCM  ni chama kikubwa, mikono yake ni mirefu "alisems Shaka.

  Shaka alimtaka Meya wa Manispaa ya Tanga Mustafa Seleboss kuhakikisha vikao hivyo vinaitishwa na chama chochote kitakachojaribu kukwamisha  uvccm watapambana nacho.

  Alisema si haki wala wajibu ikiwa kikao halaki cha madiwani kimemchagua mstahiki  Meya  wa mji Tanga  kwabtaratibu halali kilifanyika na matokeo yakakipa ushindi ccm hivyo tishio lolote la vurugu au la kukwamisha maendeleo ya wananchi  halitakubalika.
  "Wana ccm na uvccm acheni kulalamima kila siku kwamba kuna baadhi ya viongozi na  waliosaliti bila kuwachukulia hatua za kinidhamu na kimaadili, akipatikana msaliti kwa ushahidi kamili mtoseni ili tusonge mbele"alisema.

  Aidha Shaka alisisitiza kuwa kila mtendaji au Mkurugenzi wa halmashauri ana wajibu wa kusimamia maelekezo ya kisera katika utendajikazi  wake pamoja na kufuata taratibu za kisheria husika

  Kwa upande wake mstahiki Meya selebos akijibu  madai ya Sgaka alimhakikishia kuwa hakuna mpinzani au chama vjochote chenye chenye ubavu na jeuri ya kumnunua na kumtoa ccm.

  Mstahiki huyo Meya alikiri kuwa ni kweli wapo baadhi ya watendaji wa ngazi za serikali wanaoonekana kuwa waasi wasiotii matakwa na utashi wa kutoitumikia serikali ya ccm kwa.

  Seleboss alisema hata hivyo pamoja na vikwazo vilivyopo katika baadhi ya maeneo na kuwepo kwa watendaji  watukutu alisema anaamini serikali itachukua nafasi yake kuwakabili na kuwadhibiti.

  Jumla ya wanachama wapya wa uvccm kutoka Chuo cha utumishi Kange mkoani Tanga kwa hiari yao walijiunga na umoja huo pamoja na kumtawaza rasmi kamanda mpya wa uvccm Mkoa wa Tanga Najim Senga.


  Picha ya pamoja ya Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka Wazee Waasisi Mkoa wa Tanga.


  0 0

  The Former President of the United Republic of Tanzania H.E. Benjamin William Mkapa and Madam Anna Mkapa arrived in Washington D.C. yesterday, May, 11 2016. H.E. Benjamin Mkapa is in Washington for meetings with the Board of Trustees of the African Wildlife Foundation (AWF). As a member of the Board of Trustees of the AFW, H.E. Mkapa will participate in efforts to further wildlife conservation efforts.
  Former President of the United Republic of Tanzania H.E. Benjamin William Mkapa greeting the staff of the Embassy after arriving in Washington D.C with Madam Anna Mkapa.

  H.E. Wilson M. Masilingi, the Ambassador of the United Republic of Tanzania,  H.E. Benjamin William Mkapa the Former President of the United Republic of Tanzania with Madam Anna Mkapa and Madam Marystella Masilingi shortly after arriving in Washington D.C.

  Mr. Kaddu Sebunya, President of African Wildlife Foundation with Mr. Felix Otieno, Director of Board Relations at the African Wildlife Foundation. (In the back) Embassy officer Mr. Abbas Missana, H.E. Mkapa’s assistant Mr. Erick Ndobi and Defence attache Col. Adolf Mutta.

  0 0

  Na Tigaya Vincent_MAELEZO-Dodoma.

  Wizara ya Afrika , Maendeleo ya Jamii ,Jinsia Wazee na Watoto ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha maabara nne za Kanda ili kuboresha huduma za vipimo vya upimaji wa kifuu na kifuaa kikuu sugu.Hatua hiyo inalenga kuimarisha na kusogeza huduma karibu za upimaji wa kifuaa kwa wananchi.

  Kauli hiyo imetolewa jana mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha Bungeni hotuba kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka ujao wa fedha 2016/17.

  Amezitaja hospitali hiso ambazo zitakuwa na maabara hizo kuwa ni Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Kibong’oto mkoani Kilimanjaro.Waziri Ummy aliongeza kuwa Wizara hiyo itaendelea matibabu ya kifua kikuu sugu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Bugando.

  Aidha ,Waziri huyo aliongeza kuwa Wizara imefanikiwa kufikia idadi ya vituo 547 vinavyotoa huduma shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI nchini .Hatua hii inalenga kuondoa usumbufu kwa wagonjwa wenye maambukizi mseto ya Kifuua Kikuu na UKIMWI kupata huduma sehemu moja.

  Waziri Ummy aliongeza kuwa chini ya utaratibu huo , Wizara imefanikiwa kutoa huduma watu 692,642 wanaoishi na Virusi vinavyosababisha UKIMWI (WAVIU) ili kubainisha uwepo na kutokuwepo kwa maambukizi ya kifua kikuumiongoni mwao.

  Alisema kuwa kati ya hao watu 26,218 waligundulika kuwa na maambukizi ya kifua kikuu na walipatiwa matibabu.Aidha , Waziri huyo alisema kuwa katika mwaka ujao wa fedha ,Wizara hiyo itaendelea kutoa huduma za matibabu ya kifua kikuu sugu kufikia hospitali kumi za mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Morogoro, Mtwara, Tanga, Shinyanga, Geita na Mara.

  Alisema kuwa Wizara itaongeza uwezo mikoa 16 yenye viwango vya chini kabisa vya uibuaji wagonjwa wa kifua kikuu ili kuongeza kasi ya kudhibiti ugonjwa huo nchini.Katika mwaka ujao wa fedha Wizara hiyo iliomba Bunge likubali kuidhinisha makadirio ya matumizi ya Wizara pamoja na Taasisi zake yenye jumla ys shilingi 845,112,920,056.00.

  Kati ya fedha hizo shilingi 317,752,653,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 527,360,267,056.00 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 

  0 0  0 0

  Miradi yote ya maendeleo nchini Tanzania kuhifadhiwa kwenye kanzi data ili kurahisisha uratibu, upembuzi, ufadhili na utekelezaji wake.Kituo cha kuchakata na kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha Kinyezi I kimekamilika kwa asilimia 88 na kinatarajiwa kuzalisha umeme kuanzia Septemba mwaka huu.

  Akiongea katika ufungunzi wa mkutano wa kupata maoni ya taasisi za serikali zinazotekeleza miradi ya maendeleo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bi. Florance Mwanri alisema uwepo wa taarifa za miradi zitasadia taifa.

  “Uwepo wa kanzi data hii utakuwa na manufaa sana kwa taifa kwa sababu itakuwa ni rahisi kufanya maamuzi katika mchakato mzima wa kutekeleza miradi” alisema Bi. Mwanri.

  Miongoni mwa faida zitakazo tokana na mfumo huu ni kurahisisha upatikanaji wa vipaumbele vya miradi, kufanyika kwa upembuzi yakinifu vilevile upanikanaji wa fedha za kufadhili miradi hiyo. Pia mfumo huu utarahisisa utekelezaji na ufuatiliaji wa miradi iliyoidhinishwa na serikali.
   Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bi. Florance Mwanri akifuatilia utangulizi wa  mapendekezo ya uundaji wa mfumo wa utunzaji wa miradi ya maendeleo – Kanzi data (Data Base), kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Omar  Abdallah.
   Bi. Salome Kingdom akichukua taarifa za mapendekezo ya wadau mbalimbali ya kutoka taasisi za serikali ili kuboresha uundwaji wa wa kanzi data hiyo.
   Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mjadala.
   Kaimu Naibu Katibu Mtendaji – Uzalishaji, Bi. Lorah Madete, akielezea jinsi  taifa litakavyonufaika na mfumo huu. Kushoto kwake ni Bi. Zena Hussein na Bw. Hekima Chengula ambao ni sehemu ya kamati ya maandalizi.
  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bi. Florance Mwanri akiteta jambo na wataalamu kutoka Tume ya Mipango kuhusu mrejesho wa mkutano huo.

  0 0


  Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia Leseni, Mhandisi John Nayopa (katikati), Meneja wa TANESCO Kanda ya ziwa, Mhandisi Amos Maganga (kulia) na Mhandisi Joseph Kumburu (kushoto) wakiwa katika kikao kilichofanyika mjini Geita kilichojumusha watendaji mbalimbali katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, baadhi ya Wabunge na Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Kikao kililenga kujadili suala la magwangala na maeneo ya Wachimbaji Wadogo.

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (kulia) na Katibu Tawala mkoa wa Geita, Selestine Gesimba (kushoto) wakiwa katika kikao kilichofanyika mjini Geita kilichojumusha baadhi ya Wabunge na Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
  Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Geita, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakiwa katika Kikao kilichofanyika mjini Geita ambacho kililenga kujadili suala la magwangala na maeneo ya Wachimbaji Wadogo kilichoongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (hayupo pichani).


  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga (kushoto) na Katibu Tawala mkoa wa Geita, Selestine Gesimba (kushoto kwa Mkuu wa Mkoa) katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa, kabla ya kufanya kikao kilichojumusha baadhi ya Wabunge na Wakuu wa Wilaya za mkoa huo, Wawakilishi wa Wachimbaji Wadogo na Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kilicholenga kujadili suala la Magwangala na Maeneo ya Wachimbaji Wadogo.

  0 0

   Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya  Wilaya ya Chato, Mhandisi; Joel Hari akifafanua jambo kwa mtaalamu wa ufuatiliaji na Tathmini kutoka MIVARF, Wangael Wilfred alipofika ofisini kwake wakati wa ufuatiliaji utekelezaji wa Programu hiyo katika wilaya hiyo.
   Baadhi ya wakazi wa wilayani chato wakifuatilia maelezo ya  mtaalamu wa ufuatiliaji na Tathmini kutoka MIVARF, Wangael Wilfred (hayupo pichani) wilayani hapo wakati wa ufuatiliaji utekelezaji wa Programu hiyo katika wilaya hiyo.
  Sehemu ya ghala la kuhifadhi mazao liliokarabatiwa na MIVARF katika kijiji cha Nyamirembe wilayani Chato.

  Programu ya uboreshaji wa miundombinu ya masoko, uongezaji thamani mazao na huduma za kifedha vijijini (MIVARF) imefanikiwa kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi  endelevu wilayani Chato  kwa kuziwezesha kaya za vijiji hivyo kujiongezea kipato, kuboresha miundo mbinu ya masoko na kuongeza ya thamani ya zao la mpunga.


  Programu hiyo imeweza kuwajengea uwezo wazalishaji wadogo na kuwaunganisha na masoko na Taasisi za kifedha, kutoa mafunzo ya uongezaji wa thamani wa mazao pamoja na ukarabati wa barabara za vijiji hivyo zinazoanzia mashambani pia na ukarabati wa ghala la kuhifadhi mazao na ujenzi wa soko la mchele.


  Akiongea wakati timu ya ufuatiliaji na tathmini ya MIVARF ilipotembelea wilaya hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Mhandisi Joel Hari alieleza kuwa wananchi 3,961  kutoka katika vijiji 12 vya kata tatu za Nyamirembe, Kigongo na Ichwankima tayari wamenufaika na utekelezaji wa Programu hiyo.


  “Programu hii imeweza kukarabati barabara zenye urefu wa kilomita 28.1 za vijijini zinazo anzia mashambani kwa gharama ya  Tsh. 1,118,235,000. Kukarabatiwa kwa barabara hizi kumepunguza gharama za kusafirisha mazao kutoka  mashambani na nyumbani hadi kwa wanunuzi kutoka Tsh 2,000 kwa gunia moja hadi Tsh1,000 kwa gunia moja.” Alisema Hari.


  Hari alifafanua kuwa Programu hiyo imeweza kukarabati ghala la kuhifadhi mazao katika kijiji cha Nyamirembe ambapo ghala hilo litasaidia wakulima kuendesha mfumo wa stakabadhi ya mazao gharani suala ambalo litasaidia kukabiliana na kudorora kwa bei ya zao la mpunga hasa wakati wa mavuno.


  Mmoja wa wakulima wa zao la mpunga katika kata ya Kigongo, Ngavune John alifafanua kuwa kutokana na uwezo wa kilimo cha kisasa waliojengewa na MIVARF kupitia SIDO Kagera  tayari mavuno yameongezeka kutoka gunia 5 kwa ekari moja hadi gunia 25 kwa ekari moja kwa msimu wa mwaka jana  na wameunganishwa na masoko ya uhakika.


  Mratibu wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakulima wilayani humo SIDO Kagera, Abel Beebwa alibainisha kuwa vikundi vya uzalishaji wa mpunga wilayani humo vimeunganishwa na taasisi za kifaedha kwa ajili ya kupata mikopo ya kilimo na kujiwekea akiba.  Naye mtaalumu wa Ufuatiliaji na tathmini kutoka MIVARF, Wangael Wilfred alibainisha kuwa  Programu hiyo inalenga kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa wakulima wadogo wadogo, wajasiriamali wadogo wadogo vijijini na Asasi ndogondogo za kifedha zinazotoa huduma vijijini ili kuweza kufanikisha azma ya serikali ya kupunguza umasikini na kuogeza kasi ya ukuaji wa uchumi endelevu kwa kuziwezesha kaya za vijijini kujiogeza  kipato na usalama wa chakula.


  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Mb) (wa pili kulia) akiwa pamoja na Wasanii wa kizazi kipya ambao walitembelea Bunge mjini Dodoma akiwemo Msanii Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz pamoja na Mafikozolo 12 Mei, 2016. 
  Wasanii wa kizazi kipya, Nasib Abdul (Diamond Platinumz) (wa tatu kushoto) pamoja na Mafikizolo wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Mbunge Dodoma. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Babu Tale (katikati). Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba Bungeni Dodoma. 
  Mhe. Nape Nnauye (wa pili kulia) pamoja na Mhe. January Makamba (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wasanii Nasib Abdul (Diamond Platinumz) (katikati) pamoja na Mafikizolo Bungeni mjini Dodoma. 
  Mhe. Nape Nnauye (kushoto) pamoja na Mhe. January Makamba (kulia) na Mbunge mwingine (mwenye suti nyekundu) wakiwa katika picha ya pamoja na Wasanii Nasib Abdul (Diamond Platinumz) (katikati) pamoja na Mafikizolo Bungeni mjini Dodoma. (Picha zote na Benedict Liwenga, Dodoma).

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bw. Thomas Samkyi akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkakati wa Benki hiyo wa kusaidia utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano kwa kipindi cha kuanzia 2016/17 hadi 2020/21. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti na Sera Bw. Francis Assenga.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bw. Thomas Samkyi akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkakati wa Benki hiyo wa kusaidia utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano kwa kipindi cha kuanzia 2016/17 hadi 2020/21. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti na Sera Bw. Francis Assenga.

older | 1 | .... | 844 | 845 | (Page 846) | 847 | 848 | .... | 1898 | newer