Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 842 | 843 | (Page 844) | 845 | 846 | .... | 1904 | newer

  0 0

   Meneja Uhusiano na Masoko wa TSN Group, Jahu Kessy akitambulisha Vocha hizo zilizogaiwa Mwanza kwa Wateja. Afisa Mwajiri wa TSN Group Amos Paul akikabidhi Vocha hizo za punguzo la manunuzi ya bidhaa, kwa wateja wa kwanza kufurahia punguzo hilo TSN hypermarket Mwanza. 
  Meneja Uhusiano wa TSN Group, amesema mpango wao wa kuendelea kuboresha biashara kwa kutangaza kwenye mitandao ya kijamii. Sasa unaweza kufollow TSN Group TZ kwenye mitandao ya kijamii kwa promotion mbalimbali zitakazoendelea kutambulishwa. 

  Sasa unaweza ku’bargain’ kwenye supermarket, Meneja Uhusiano na Masoko wa TSN Group, Jahu Kessy ameelezea kuhusu mikakati ya kuboresha biashara za TSN kwa kutambulisha Loyalty Gift Vouchers kwa wateja.

  Wateja sasa wanaweza kuomba na kupata punguzo la bei ya bidhaa walizonunua katika maduka yao yaliyopo, Kibo Complex-Tegeta, Bamaga Petrol station-Mwenge, Baraka Plaza-Mikocheni, Tancon House-Posta, Swiss Tower -Upanga Dar es Salaam pamoja na Rock City Mall-TSN Hyprmarket Mwanza iliyofunguliwa hivi karibuni.

  Meneja Uhusiano huyo ambaye alizitambulisha Voucher hizo kwa mara ya kwanza Mwanza amewataka wateja kumiminika katika maduka yao kupata punguzo hilo la kwanza kufanyika katika supermartket. 

  Alisema TSN inatoa punguzo la manunuzi kwa wateja wanaonunua bidhaa zisizopungua chini ya laki tatu ndani ya wiki moja. Alisema kupata punguzo la bei mteja atalazimika kujisajili na kuacha mawasiliano yake ya simu na kuhakiki mauzo yake kwa wiki. 

  Katika promotion hiyo ambayo itadumu  miezi mitatu kuanzia sasa hadi mwezi wa saba, kwenye checkout point ya maduka ya TSN, utatakiwa kuomba kitabu na ujisajili kwa kuandika jina lako, kiasi cha manunizi uliyofanya na mawasiliano yako ukisubiri kufikia kiwango kinachostahiki ili uweze kukabidhiwa vocha hiyo.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akihutubia wakazi wa arusha na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati alipozindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.
  Sehemu ya wadau kutoka NSSF waliohudhuria uzinduzi huo wa wenzao wa PPF.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akikata utepe kuzindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016. Wa pili (kushoto) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama, (kushoto) ni Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro (wa kwanza kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Ramadhan Kijjah, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango. Picha zote na Mafoto Blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la uzinduai wa Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.
  Jengo hilo lililozinduliwa leo.
  Sehemu ya wadau wakimsikiliza Mhe. Rais Dkt. Magufuli.....
  Baadhi ya wafanyakazi wa PPF Kanda yas Arusha wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
  Sehemu ya wananchi wa Jiji la Arusha wakimsikiliza Mhe. Rais Dkt. Magufuli.....
  Wananchi wakimshangilia Mhe Rais wakati akihutubia.....
  Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mhe Rais.
  Baadhi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
  Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni PPF na Wakurugenzi wa Mfuko wa huo wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
  Baadhi ya viongozi na wadau wa Mfuko huo na Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro (kushoto) wakimsikiliza Mhe Rais.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PPF, Ramadhan Kijjah, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na baadhi ya Wadau wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
  Wakifurahia baada ya uzinduzi huo....
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Meneja wa PPF Kanda ya Arusha, Onesmo Ruhasha, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
  Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
  Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
  Viongozi wakiwa meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa
  Wadau wakiimba wimbo wa Taifa.

  Wadau wakiimba wimbo wa Taifa

  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Said Mecki Sadiki akizungumza na maafisa wa TFDA ofisini kwake walipokwenda kumtembelea ofisini kwake na kujadili masuala ya udhibiti wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba katika mkoa wake.
  Picha ya Pamoja.


   Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Daud Ntibenda akifungua kikao kazi cha wadau wa TFDA katika sekta ya Habari mkoani Arusha.
  Wadau wa Habari mkoani Arusha wakifuatilia mada mbalimbali.  
  Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TFDA bi. Charys Ugulum akitoa Maelezo ya utangulizi katika kikao kazi mkoani Arusha.

  0 0

   Mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja akifafanua  jambo  kwa waandishi wa Habari kuhusu mwenendo wa uchumi wa Tanzania.kushoto ni Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo.
   Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka kidogo kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Aprili 2016 leo jijini Dar es salaam, Kulia ni Mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja.Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Aprili 2016 umepungua hadi asilimia  5.1  kutoka asilimia 5.4.
  Waandishi wa Habari wakimsikiliza  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.
  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu, ya Jamii). 

  Na. Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
  OFISI ya Taifa ya Takwimu imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Aprili 2016 na kusema kuwa umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.4 iliyokuwepo mwezi Machi, 2016.

  Hii inamaanisha kuwa  kasi ya upandaji wa bei ya  bidhaa na huduma kwa mwezi Aprili 2016 imepungua kidogo ikilinganishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma  iliyokuwepo mwezi Machi mwaka huu.


  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo ametoa taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam na kueleza kuwa kupungua kwa mfumuko huo kumesababishwa na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali nchini.

  Amesema Takwimu zilizokusanywa katika mikoa yote ya Tanzania Bara kwenye bidhaa zinazotumika kupima mfumuko wa bei kwa mwezi Aprili 2016 zimeainisha kuwa bidhaa zisizo za vyakula katika soko zikiwemo Gesi , dizeli na mafuta ya taa zimechangia kupungua kwa mfumuko huo.

  Amesema kuwa pamoja na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa hizo kwa mwezi Aprili 2016, baadhi ya bidhaa za vyakula ikiwemo mchele, unga wa Mahindi na mkaa ilionyesha kuongezeka katika kipindi hicho.

  Akizungumzia Kuhusu Fahirisi za Bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya binafsi hapa Tanzania kwa mwezi Machi na Aprili Bw. Kwesigabo amesema kuwa zimeongezeka hadi kufikia 102.46 kutoka 101:93 za mwezi Aprili.

  Amesema kuwa tofauti na mwezi Machi bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi kwa mwezi Aprili ni unga wa muhogo, dagaa, choroko, maziwa ya ungana na matunda aina ya machungwa.

  Aidha,bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na mvinyo, bia kuni na mazulia.

  Kwa upande wa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Aprili, 2016 umefikia shilingi 97 na senti 60 ikilinganishwa na uwezo wa shilingi 98 na senti 11  wa mwezi Machi 2016.

  “Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Aprili 2016 umepungua, hii ina maana kuwa sasa mtu anahitaji kuongeza  ya shilingi 2.40 ili aweze kununua bidhaa na huduma sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua mwezi Machi " Amesema Kwesigabo.

  Kwa upande wa mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki mwezi Machi, 2016, Kwesigabo amesema una mwelekeo unaofanana; Kenya umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 5.27 kutoka 6.45 huku Uganda ukifikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 6.2 zIlizokuwepo mwezi Machi 2016.

  0 0

   Maoneshi ya Mavazi yakiendela.
  TAMASHA la pili la Stara, Stara fashion Week 2016 linatazamiwa kuchukua nafasi yake tena mwaka huu katika ukumbi wa City Garden Restaurant Kamata, June 1 hadi 5.

  Tamasha hilo ambalo litafunguliwa na Exhibition ya bure, linakaribisha watu mbalimbali wanawake wanaume na watoto kwa manunuzi ya vitu mbalimbali, kama vile Mabaibui,Mitandio Madera kwa ajila ya Mwezi mtufu wa Ramadhani, evening dresses, kanzu, Udi Hena na vitu vingine pia kutakuwa na wachora heena kwa bei nafuu.

  Exhibition hiyo ambayo itakuwa inaanza tarehe 1 June asubuhi ya saa nne hadi saa 12 jioni, itafungwa na maonyesho ya mavazi ya stara kwa wanawake pekee siku ya Jumapili ya tarehe 5 kuanzia saa nne hadi saa 11 jioni.

  Katika kilele cha maonyesho hayo kazi za mikono ya wabunifu wa hapa nyumbani wanaobuni mavazi ya stara zitaonyeshwa pamoja na warsha itakayojadili mada mbalimbali ambazo ni pamoja na
  1. Jinsi ya kumpata mwenza na kudumisha ndoa
  2. Matumizi na Mipango ya Fedha
  3. Ujasiriamali Na nyinginezo
  Kongamano hilo la wanawake, litakuwa na kiingilio cha shilling elfu 35 VIP na Elfu 50 viti maalum Kwa kujumuisha chakula cha mchana kwa wote na zawadi mbalimbali zitatolewa.

  Stara fashion week imedhaminiwa na  Maximalipo, Hijab Couture, Hijabi Central Tz, Kanzu Point, Cordoba School, Speedy Print, I-view Studio, Vayle Springs, AA Shekhozah co. Ltd, City Garden Restaurant, Event Lights, Sofia Production,  Clouds Media na wengineo.

  0 0

  Familia ya Ankal Issa Michuzi iliyopatwa na msiba wa kuondokewa na na Mtoto wa Ankal, Maggid Muhidin kilichotokea jana Jumapili huko Durban, Afrika Kusini.

  Msiba sasa umehamishiwa Tegeta Wazo Hill, Nyumbani kwa Mama Mzazi wa Marehemu (likiwa ni ombi maalum la Mama), na taratibu zote zinafanyika huko.

   Mipango ya kuusafirisha Mwili wa Marehemu kutoka nchini Afrika Kusini na kuja nyumbani kwa mazishi, inafanyika na taratibu za  mazishi zitatolewa mara tu baada ya mwili kuwasili nchini.

  Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.

  Innalillah wa inna ilayhi raajiun

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akikata utepe
  kuzindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni (PPF) lililopo Mtaa
  wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016. Wa pili (kushoto) ni Waziri wa Nchi
  Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira,
  Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama, (kushoto) ni Meya wa jiji
  la Arusha, Calist Lazaro (wa kwanza kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini
  ya PPF, Ramadhan Kijjah, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio na Waziri wa Fedha
  na Mipango, Dkt. Phillip Mpango.Picha zote na Mafoto Blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la uzinduai wa Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo lililopo Mtaa wa Korido
  Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.
  Jengo hilo lililozinduliwa leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akihutubia wakazi wa arusha na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati alipozindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.
  Sehemu ya wadau kutoka NSSF waliohudhuria uzinduzi huo wa wenzao wa PPF.
  Sehemu ya wadau wakimsikiliza Mhe. Rais Dkt. Magufuli…..
  Baadhi ya wafanyakazi wa PPF Kanda yas Arusha wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
  Sehemu ya wananchi wa Jiji la Arusha wakimsikiliza Mhe. Rais Dkt. Magufuli…..
  Wananchi wakimshangilia Mhe Rais wakati akihutubia…..
  Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mhe Rais.
  Baadhi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
  Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni PPF na Wakurugenzi wa Mfuko wa huo wakimsikiliza Mhe Rais wakati akihutubia.
  Baadhi ya viongozi na wadau wa Mfuko huo na Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro (kushoto) wakimsikiliza Mhe Rais.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PPF, Ramadhan Kijjah, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na baadhi ya Wadau wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
  Wakifurahia baada ya uzinduzi huo….
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Meneja wa PPF Kanda ya Arusha, Onesmo Ruhasha, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini
  Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
  Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo leo.
  Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
  Viongozi wakiwa meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa
  Wadau wakiimba wimbo wa Taifa
  Wadau wakiimba wimbo wa Taifa

  0 0

  001
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula akifungua rasmi mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye makao makuu ya shirika hilo Upanga jijini Dar es salaam ambapo alilipongeza shirika hilo kwa kazi nzuri ambayo wafanyakazi wake wanaifanya kwani ndiyo shirika pekee la Serikali linaloendeshwa kwa ufanisi mkubwa na kuiletea heshima serikali, Waziri Mabula amewaambia wafanyakazi wa shirika hilo pamoja na Menejimenti yake kuendelea na kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya ili kuleta maendeleo zaidi nchini katika sekta ya nyumba.PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM
  01Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi katika mkutano uliofanyika mwishoni mwa wiki katikia makao makuu ya shirika hilo Apanga kulia ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na kushoto ni Adolf Kasegenya Katibu wa Baraza la Wafanyakazi TAMICO NHC.
  1
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu kulia na Adolf Kasegenya Katibu wa Baraza la Wafanyakazi TAMICO NHC kushoto wakiimba wimbo wa wafanyakazi kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
  3
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula na Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo.

  4
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula akipitia nyaraka huku Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo kabla ya kumkaribisha ili kufungua rasmi mkutano huo.
  5 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu akizunguma na wafanyakazi wa shirika hilo kabla ya Waziri Angelina Mabula kuufungua rasmi.
  6 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu akisisitiza jambo wakai akizunguma na wafanyakazi wa shirika hilo kabla ya Naibu Waziri Angelina Mabula kuufungua rasmi.
  7Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba wakifuatilia mkutano huo.
  8Wafanyakazi wa shirika la Nyumba wakiimba wimbo wa wafanyakazi kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo.
  9Wafanyakazi wa shirika la Nyumba wakiwa katika mkutano huo.
  11 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na Naibu Waziri Angelina Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.
  12 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na Naibu Waziri Angelina Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.
  13 
  Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na Naibu Waziri Angelina Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.

  0 0

  LAPF imedhamini kongamano la Jeshi la Polisi (Vikosi vya masuala ya tiba) uliofanyika mjini Tabora. Mfuko wa Pensheni wa LAPF umetoa kiasi cha Shilingi milioni 6,200,000/= katika kufanikisha kongamano la Maafisa wa Polisi kutoka mikoa yote Tanzania maalum kwa ajili ya kujipima na kujadili changamoto mbalimbali za kitengo cha tiba ndani ya jeshi la polisi (medical wing) Wawakilishi kutoka mikoa yote Tanzania walishiriki katika kongamoano hilo wakiwa ni maofisa waandamizi wa jeshi hili la polisi. katika kongamano hilo Mfuko ulipata wasaa wa kuwasilisha mada kuhusu fursa mbalimbali zitolewazo na Mfuko lakini pia mada ya maandalizi kabla ya kustaafu ilitolewa katika mkutano huo , udhamini huu una synergy kubwa na mfuko katika kusajili wanachama wapya ndani ya jeshi la polisi.
  Kamanda wa Jeshi la Polisi ACP Paul Kasabago akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya TZS. 6,200,000/= iliyotolewa na Mfuko wa Pensheni LAPF kuwezesha kongamano la Maafisa wa Polisi kutoka mikoa yote Tanzania (medical wing) mjini Tabora. Wanaokabidhi kutoka LAPF ni Mkurugenzi wa Huduma kwa wanachama Bw. Valerian Mablangeti, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Desdery Sigonda pamoja na Meneja Kanda ya Dar es Salaam Bi. Amina Kassim.
  Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Pensheni LAPF Bw. Valerian Mablangeti akitoa mada kuhusu Mfuko ikijumuisha maandalizi kabla ya kustaafu, Maafisa waandamizi wa jeshi la Polisi wakisiliza kwa makini katika kongamano la jeshi hili lililofanyika mjini Tabora hivi karibuni.
  Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi wakifuatilia kwa makini mada toka Mfuko wa Pensheni LAPF kwenye kongamano la Jeshi hili lililofanyika mjini Tabora ambapo maafisa hao walivutiwa na kujiunga na mfuko wa uchangiaji wa hiari ikiwa ni maandalizi kabla ya kustaafu.
  Mmoja ya Maafisa waandamizi walioshiriki kongamamo la jeshi la Polisi mkoani Tabora hivi karibuni akiuliza namna ya kujiunga kwa hiari na Mfuko wa Pensheni wa LAPF mara baada Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama kuwasilisha mada kuhusu fursa mbalimbali zitoleawazo na Mfuko wa Pensheni wa LAPF.

  0 0

  Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Medard Kalemani akijibu baadhi ya hoja za Wabunge zilizoihusu Wizara ya Nishati na Madini wakati wa kipindi cha jioni Bungeni mjini Dodoma.
  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) (kulia)
  akijibu baadhi ya hoja za baadhi ya Wabunge wakati wa mapitio ya hoja mbalimbali jioni bungeni mjini Dodoma.
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakati wa mapitio ya baadhi ya hoja za Wabunge leo jioni Bungeni mjini Dodoma. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Mhe. Amina Makilagi ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum wakati wa mapitio ya hoja mbalimbali za Wabunge leo mjini Dodoma.
  Naibu Waziri, Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Medard Kalemani (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Ashatu Kijaji (Mb) wakati wa mapitio ya hoja mbalimbali Bungeni mjini Dodoma.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb) akijibu hoja za Wabunge mbalimbali wakiochangia hotuba ya Wizara yake leo jioni Bungeni mjini Dodoma.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mwigulu Nchemba wakati wa mapitio ya hoja za Wabunge jioni Bungeni mjini Dodoma.(Picha zote na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma)

  0 0

  Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anaongea na wananchi wa tanga
  ……………………………………
  Na Woinde Shizza,Tanga

  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM )umevitaka vyama vya
  upinzani wanaopika maneno ya majungu yenye lengo la kuwagonganisha viongozi wa CCM,Waache kumsumbua sumbua Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Kikwete astaafu kwa heshima, kwa sababu ameitumikia nchi yake kwa kutoa jasho jingi miaka kumi iliopita, Aidha umoja huo umesisitiza kuwa kazi aliyoifanya Dk Kikwete katika uongozi wake wa miaka kumi kisiasa na kiserikali utabaki kwenye vitabu vya kumbukumbu ya historia iliotukuka, hususan kila utakapokumbukwa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM mwaka 2015.

  Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ameyasema hayo wakati alipozungumza na viongozi na wanachama wa uvccm na ccm kwenye ukumbi wa TANU Hall mjini Tanga.Alisema baada ya upinzani kubaini kukosa hoja na hawakubaliki katika jamii maadui wa kisiasa wanotimiwa na nafisadi wamekuwa wqkijaribu kupika uzushi na kutaka kuionyesha jamii kwamba viongizi wa chama tawala hawana maelewano.

  “Nakupeni usia viongozi wa Ukawa ambao sasa mmekuwa wakiwa , mambo ya ngoswe waachieni ngoswe wenyewe, viongozi wa ccm hawagombani, hawajawahi kugombana na kamwe hawatagombana milele “alisema shaka Aliwataka viongozi hao kutazama mustakabali wao kisiasa na kuachana na ccm kwa sababu chama hicho tawala haiwezekani kubomoka kwa maneno ya jikoni , vijiweji au vichochoroni.

  Shaka alisisitiza kuwa mwenyekiti wa ccm Dk Kikwete wakati akiwa Rais ameitumikia nchi yake kwa kadri ya uwezo wake kama ambavyo walivyotenda na kuitumikia nchi viongozi watangulizi wake akiwemo baba wa Taifa Mwalimu julius Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na yeye ametenda kwa uwezo wake kama atakavyotenda Rais Dk John Magufuli katika kipindi chake.

  “Mtu mwenye akili timamu kila atakaposafiri akiizunguuka nchi yetu na kupita juu ya barabara za lami, ujenzi wa madaraja, kutanuka kwa mawasiliano, kukua uchumi wa Taifa na wa mtu mojmoja na wananchi kiushi katika nyumba za kisasa lazima utamkunbuka Kikwete taka usitake
  “alieleza Kaimu huyo katibu mkuu . 

  Alisema kila zama ina kitabu na Nabii wake hivyo mema yaliofanywa na kiongozi mmoja aliyemaliza muda wake yanahitaji kuheshimiwa kwa sababu  Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli wote ni watoto wa baba na
  mama mmoja.

  0 0
 • 05/09/16--22:31: Jecha atembelea NEC
 • Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Jecha Salim Jecha akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva ,Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani pamoja na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi walipokutana makao makuu ya NEC kuzungumzia maswala mbali mbali ya Demokrasia na mustakabali wa Siasa za Tanzania hapo jana tarehe 9-5-2016.
   
   Picha ya pamoja  0 0

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Balozi Mathias Chikawe, Balozi huyo alipofika kumuaga katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam,jana, Mei 9, 2016.Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiagana na Balozi Mpya wa Tanzania nchini Japani, Balozi Mathis Chikawe, baada ya mazungumzo yao, Balozi huyo alipofika kumuaga katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, jana, Mei 9, 2016.Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Balozi Mathew Kisamba akisaini kitabu cha wageni, alipofika kumuaga Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, jana.Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Balozi Mathew Kisamba, Balozi huyo alipofika kumsalimia katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, jana, Mei 9, 2016.(Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0
 • 05/09/16--22:36: TANZIA UK DIASPORA GLASGOW.
 • Tunasikitika kuwatangazia msiba wa Mtanzania mwenzetu 
  Bi Mwasaburi Hajikilichotokea Jumamosi jioni huko Glasgow Scotland.

  Mipango ya mazishi inaendelea na mtajulishwa tarehe ya mazishi.
  Msiba uko nyumbani kwa Marehemu
  2/1, 105 Mcculloch St. Glasgow, G41 1NT.

  Kwa wale mlioguswa mnaweza kutuma rambi rambi zenu kwenye account ya
  ndugu wa marehemu 

  A. AZIZ.
  Nationwide.
  Account No: 01491791
  Sort code: 07 04 36.
  Kwa mawasiliano zaidi mnaweza kumpigia ndugu wa Marehemu


  A. AZIZ - 07411445644

  Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Rajiun.

  0 0

  Na Lilian Lundo – Maelezo

  Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limeazimia kuongeza idadi ya madampo na kurekebisha miundombinu ya dampo la Pugu ili kuhakikisha jiji linakuwa safi.

  Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita alisema Baraza hilo limeazimia kuongeza na kurekebisha miundombinu baada ya ziara walioifanya na kugundua mapungufu katika dampo la Pugu.

  “Tumegundua kuna udhaifu mkubwa katika dampo la Pugu, magari yanayopeleka taka yananasa barabarani hivyo tukaona kuna sababu ya kutengeneza miundombinu, hivyo tumetenga milioni 700 kwenye bajeti hii ili kutengeneza barabara hiyo,”alisema Mhe. Mwita.

  Aidha, alisema kwamba baraza limetenga kiasi cha shilingi milioni 200 katika bajeti ya 2016/17 ili kununua eneo Mkuranga kwa ajili ya dampo, huku wakiendelea na mchakato wa kuongeza madampo mengine Kigamboni na Kisarawe ili kuhakikisha taka zote zinazozalishwa ndani ya jiji la Dar es Salaam zinapelekwa kwenye madampo badala ya kuzagaa mitaani.

  Kwa upande wake, Naibu Meya wa jiji la Dar es Salaam Mhe. Mussa Kafana alisema kuwa, suluhisho la kumaliza taizo la uchafu si kuwa na dampo tu bali ni kuwepo kwa vifaa maalumu vya kuhifadhi taka. Hivyo baraza likaamua kuwepo na vyombo vya kuhifadhia taka katika mitaa yote ya jiji la Dar es Salaam ili kudhibiti uzagaaji wa taka.

  Usafi ni moja ya kipaumbele cha Rais wa Awamu ya Tano Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambapo kwa mara ya kwanza alitangaza siku ya Uhuru wa Tanzania (Tisa Desemba) iazimishwe kwa kufanya usafi nchi nzima ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu pamoja na kuiweka Tanzania katika hali ya usafi.

  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Alexander Ng’winamila (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu uwekezaji kwenye dhamana za Serikali. Kulia ni Meneja Msaidizi Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BOT Bi. Victoria Msina na Kushoto ni Meneja Msaidizi Masoko ya Ndani wa BOT Bw. Genes Kimaro.
  Meneja Msaidizi Masoko ya Ndani wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Genes Kimaro (kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu aina na faida za uwekezaji kwenye dhamana za Serikali.PICHA NA FATMA SALUM-MAELEZO

  0 0  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Japan ya KOYO na   kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited ambazo kwa pamoja  zimekusudia  kushirikiana ili kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. Waziri Mkuu alifanya mazungumzo na viongozi hao  ofisini kwake  jijini Dar es salaam May 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata ufafanuzi wa mikakati ya uwekezaji kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  KOYO ya Japan, Bw.  Norio Shoji wakati alipokutana na ujembe wa kampuni hiyo  ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Kampuni ya Japan ya KOYO na   kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited ambazo kwa pamoja  zimekusudia  kushirikiana ili kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam May 9, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  KOYO ya Japan, Bw.  Norio Shoji  baada ya kukutana na Mtendaji huyo na ujumbe wake ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. Kampuni hiyo ikishirikiana na Kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited inakusudia kuwekeza  kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) .


  KAMPUNI YA KIJAPAN KUWEKEZA KWENYE UMEME

  SHIRIKA la Koyo la kutoka Japan limepania kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na umeme jua ili kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi waishio vijijini.

  Hayo yamesemwa jana jioni (Jumatatu, Mei 9, 2016) na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa shirika la Koyo, Bw. Norio Shoji wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam.

  “Tumepanga kuwekeza kwenye maeneo matano ambayo mojawapo ni kujenga mtambo wa kuchakata gesi kwa kutumia gesi asilia inayozalishwa hapa nchini. Mtambo huu utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 1,000 za umeme,” alisema.

  "Pia tunao mpango wa kujenga mitambo ya umemejua inayoweza kujiunganisha kwenye gridi (on-grid/off grid solar power plants) kwa ajili ya maeneo vijijini  na yale yasiyofikika kwa urahisi zaidi ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo wa usambazaji umeme kwenye gridi ya Taifa ili Tanzania iweze kuzalisha zaidi nishati hiyo na kuiuza nchi jirani," aliongeza.

  Bw. Shoji alimweleza Waziri Mkuu kwamba wana nia ya kuwekeza pia katika sekta nyingine kama kilimo, sayansi ya tiba (medical science), usafishaji na uyeyushaji madini (refinery-smelting), uzalishaji wa bidhaa za viwandani na teknohama.

  Akifafanua zaidi Bw. Shoji alisema shirika lake kwa kushirikiana na makampuni mengine makubwa ya Japan pamoja na Serikali ya nchi hiyo wamedhamiria kuwekeza kwenye miundombinu hiyo kwa sababu wanataka Tanzania iwe ni kitovu (hub) cha uzalishaji na iweze kulisha nchi jirani katika SADC na EAC.

  Akitolea mfano, Bw. Shoji alisema mbali na miradi mingine wanayotaka kuwekeza, gharama za kuweka mtambo wa kuzalisha megawati 1,000 za umeme hazitapungua kiasi cha dola za marekani bilioni moja (sawa na sh. trilioni 2.2).

  Waziri Mkuu alimshukuru Bw. Shoji kwa nia yake aliyoionyesha na akamtaka achangue eneo mahsusi kwa sababu Tanzania inahitaji umeme wa kutosha katika kutekeleza azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.

  “Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda ili kuongeza ajira na kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi wake. Tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye nishati ya umeme katika mikoa ya Kusini, ya Kaskazini, ya Magharibi na hata mikoa ya kati,” alisema Waziri Mkuu.

  Kwa upande wake, Bw. Suleiman M. Nassor alisema shirika la Koyo litafanya uwekezaji huo kwa kushirikiana na kampuni ya SSF Limited ambayo inajihusisha na masuala ya nishati.

  “Tunashirikiana na shirika la Koyo pamoja na Serikali ya Japan ili kuleta unafuu wa maisha kwa Watanzania wenzetu,” alisema Bw. Nassor.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM

  JUMANNE, MEI 10, 2016.

  0 0

  Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda (katikati) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka. Wengine ni  Afisa Mwandamizi wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (kulia), Meneja Masoko wa benki hiyo, Bw Abdulrahman Nkondo, (kushoto) na Mkaguzi Mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo Bw. George Binde (wa pili kushoto)

  BENKI ya Exim Tanzania imetangaza kupata faida ya sh. bilioni 53. (kabla ya kodi) kwa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka mwaka 2016, sambamba na faida ya kuuza hisa ilizowekeza (capital gain) ya Tsh bilioni 45 mafanikio yanayotajwa kusababishwa na ufanisi wa benki hiyo katika usimamizi mizania.

  Aidha, mapato yatokanayo na uendeshaji wa benki hiyo yaliongezeka na kufikia kiasi cha Tsh bilioni 8.4 yakiakisi ukuaji wa asilimia 67 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka uliopita.

  “Kasi ya mafanikio tuliyomaliza nayo mwaka uliopita ndio tulianza nayo na ndio siri kubwa ya mafanikio haya,’’ alisema Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw Selemani Ponda alipokuwa akitoa ripoti ya awali (kabla ya ukaguzi) ya benki hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  Alisema ongezeko hilo lilipatikana kupitia mchanganyiko linganifu baina ya mapato yatokanayo na faida pamoja na yale yasiyotokana na faida.

  Kwa mujibu wa Bw. Ponda katika kipindi hicho faida kwenye riba ilikuwa kwa asilimia 24 na kufika sh. Bilioni 21 ikilinganishwa na kiasi cha sh. 17 kilichopatikana katika kipindi kama hicho kwa mwaka uliopita. Ongezeko hilo limechagizwa na mkazo wa benki hiyo katika amana za gharama nafuu, wingi wa matawi ya yapatayo 45 ya benki hiyo pamoja na usimamizi mzuri wa mizania.

  Zaidi, tozo mbalimbali za huduma za kibenki katika kipindi cha mwaka ulioipita kiliongezeka kwa asilimia 21 hadi kufikia sh bilioni 9, kutoka kiasi cha sh bilioni 7.5 kilichopatikana mwaka uliopita.

  “Ongezeko hilo pia lilichagizwa na faida katika biashara ya kununua na kuuza fedha za kigeni ambayo mapato yake yaliongezeka kwa asilimia 11 na kufikia kiasi cha Tsh bilioni 2.5 sambamba na mapato mengine ya ada kutokana na ufanisi katika utoaji huduma kwa wateja wakubwa na wale wa kati.,’’ alifafanua.

  Alisema matumizi ya benki hiyo yalliongezeka kwa asilimia 35 kutokana na mabadiliko inayopitia kupitia uwekezaji mkubwa kwenye rasilimali watu, michakato mbalimbali pamoja na teknolojia.

  “ Miradi mingi ya kiteknolojia inatarajia kukamilika kwenye robo ya tatu ya mwaka huu.,’’ alibainisha Bw Ponda.

  Akizungumzia upanuzi wa benki hiyo iliyoufanya nchini Uganda alisema rasilimali za benki ya Exim zimeweza kukua kwa asilimia 14.63 katika kipindi cha robo ya mwaka huu na hivyo kufikia kiasi cha Tsh Trilioni 1.44 ilinganishwa na kiasi cha Tsh Trilioni 1.25 kilichorekodiwa mwishoni mwa mwaka uliopita.

  “Exim tunaahidi kuendelea na muelekeo huu ulio sahihi kwetu na kwa wateja wetu katika kutimiza malengo yetu. Ripoti hii inaonyesha kuwa robo ya kwanza ya mwaka huu ilikuwa na mafanikio makubwa na ya kujivunia,’’ alisema Bw Ponda huku akiwapongeza wafanyakazi na wadau wote waliochangia mafanikio hayo.

  0 0

  Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dodoma.

  SERIKALI imetenga Shilingi bilioni 59.5 katika Bajeti ya mwaka 2016/17 kwa ajili ya kuwawezesha Wananchi vijijini kwa kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa.

  Taarifa hiyo imetolewa leo Bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi (Mb) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Esther Mahawe aliyetaka kujua ni lini fedha zingetolewa na Serikali imejipanga vipi kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wananchi juu ya njia bora ya kutumia fedha hizo.

  Dkt. Possi amesema kuwa, fedha hizo zitatolewa mara baada ya kuidhinishwa na Bunge hilo na baada ya kukamilisha taratibu mahususi zinazolenga kuhakikisha uwepo wa tija katika matumizi ya fedha hizo.

  Ameongeza kuwa, kuhusu mpango bora wa Elimu ya Ujasiriamali kwa wananchi, Serikali inaendelea kukamilisha maandalizi ya utaratibu maalum wa utoaji wa fedha hizo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya Ujasiriamali.

  "Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI imepewa kazi ya kuratibu utekelezaji wa mpango huo", alisema Dkt. Possi.

older | 1 | .... | 842 | 843 | (Page 844) | 845 | 846 | .... | 1904 | newer