Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 841 | 842 | (Page 843) | 844 | 845 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akitoa mada kwenye Kongamano la siku Nne la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls Zimbambwe lilianza tarehe 4 – 8 Mei, 2016. Vyama hivyo ni ANC ya Afrika Kusini, FRELIMO ya Msumbiji, MPLA ya Angola, SWAPO Party ya Namibia na CCM ya Tanzania.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akimpongeza Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF Ndugu Ignatius Morgen Chombo kwa kufanikisha Kongamano la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika na anaeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu wa FRELIMO Ndugu Eliseu Machava. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016
  Picha ya pamoja ya Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) wanaoshiriki Kongamano la siku Nne la kutafakari uimarishaji na uendelezaji wa ushirikiano wao na namna ya kukabiliana na changamoto walizonazo. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini Ndugu Ndugu Gwede Mantashe, Katibu Mkuu wa FRELIMO ya Msumbiji Ndugu Eliseu Machava, Katibu Mkuu wa CCM ya Tanzania Ndugu Abdulrahaman Kinana, Makamu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomnisti cha China (CPC) Ndugu Guo Yezhou, Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF ya Zimbabwe Ndugu Ignatius Morgen Chombo, Katibu Mkuu wa MPLA ya Angola Ndugu Juliao Mateus Paulo na Katibu Mkuu wa SWAPO Party ya Namibia Ndugu Nangolo Mbumba. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini, Ndugu Gwede Mantashe kwenye Kongamano la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) linalofanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016


  0 0

  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa inafanya uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowahusu wafanyabiashara wa sukari nchini kwa kuficha bidhaa hiyo ili kusababisha upungufu katika soko na hivyo kuleta usumbufu kwa jamii ya watanzania wanaohitaji bidhaa hiyo kwa matumizi jambo ambalo limesababisha kupanda kwa bei hadi kufikia shilingi elfu nne kwa kilo moja ya sukari. 

  Taasisi imeanza uchunguzi dhidi ya Tuhuma hizi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na tayari tumeweza kutembelea Maghala ya mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa nchini wa sukari na anayetuhumiwa kuficha bidhaa hii. 

  Mnamo tarehe 05 Mei, 2016 timu ya uchunguzi ilitembelea maghala ya Tabata na kubaini uwepo wa sukari yenye jumla ya tani 4,579.2 iliyonunuliwa toka Kiwanda cha Kilombero Sugar Company. 

  Aidha uchunguzi ulibaini kuwepo kwa njama za dhati za kutouza kwa sukari kulikofanywa na mfanyabiashara huyu kwani hata sehemu ya Maghala ilipo sukari hapa kuwepo dalili za upakiaji wa sukari na baada ya kufika Kitumbini tulibaini uwepo wa wananchi wengi waliokuwa wakihitaji bidhaa hiyo na wachache sana waliweza kuuziwa tena kwa kiwango kidogo sana kuliko mahitaji yao. Wananchi wengi walikosa huduma hiyo licha ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo. 

  Uchunguzi uliofanyika umebaini kuwepo kwa mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiashar huyu kwa kununua sukari yote toka viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko. Kuficha bidhaa ni kosa la uhujumu uchumi na ni kinyume na Aya ya 3 Jedwali la kwanza Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 [Chapisho la Mwaka 2002]. Serikali haitavumilia hujuma za namna hii na itachukua hatua kali dhidi ya mfanyabiashara yeyote ataekwenda kinyume na sheria hii. 

  Kuanzia sasa TAKUKURU inatoa wito kwa wafanyabiashara wote wa sukari kuacha vitendo vya kuficha sukari na vyombo vya uchunguzi vinafuatilia kote nchini na yeyote atakayebainika kufanya hujuma hizo atakabiliwa na mkondo wa Sheria. 

  VALENTINO MLOWOLA
  MKURUGENZI MKUU WA TAASISI 
  YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA 

  7 MEI, 2016

  0 0


  0 0

  Mbunge Mbatia akizungumza jambo mara baada ya kufika katika eneo lililokuwa na nyumba iliyobomoka baada ya kuporomokewa na kifusi na kusababisha kifo cha mtoto mmoja katika kijiji cha Manda juu wilayani Rombo.
  Baadhi ya majirani wa familia iliyopoteza mtoto katika kijiji cha Manda wilayani Rombo baada ya nyumba aliyokuwemo mtoto kuporomokewa na kifusi kutokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni.
  Wabunge James Mbatia (Jimbo la Vunjo ) na Joseph Selasini wakiwa ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya alipofika kutembelea wahanga wa mvua zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha maafa.
  Mbunge wa Jimbo la Rombo Joseph Selasini (kulia) akijaribu kutoa maelezo namna ambavyo wakazi wa kijiji cha Manda juu wilyani humo walivyo pata maafa yaliyotokana na kunyesha kwa mvua kubwa Aprili 24 na 25 mwaka huu.
  Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa pole kwa wakazi wa kijiji cha Manda juu wilayani alipokua akielekea kujionea namna ambavyo baadhi ya familia zilivyo athirika na mvua katika kjiji hicho na mtoto mmoja kupoteza maisha baada ya kifusi kuporomoka na kuangusha nyumba aliyokuwemo.
  Mbunge wa Jimbo la Rombo ,Joseph Selasini (kushoto) akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Rombo ,Lembris Kupuyo wakielekea kuijionea athari ya mvua hizo.
  Sehemu ya mabaki ya nyumba iliyoanguka.
  Eneo la Shamba la Migomba kama linavyoonekana baada ya kifusi kuporomoka .
  Mbunge wa Jimbo Rombo,Joseph Selasini akizungumza jambo wakati vongozi wakifika eneo hilo kujionea hali halisi.
  Baadhi ya viongozi walioambatana na wabunge hao wakijaribu kupanda kwenda kujionea hali halisi ya athari zilizotokana na mvua hizo.
  Watoto wakionekana wakiwa wamesimama kwa juu sehemu ambayo ni hatari kwa usalama wao hasa kutokana na maeneo mengi ya muinuko katika eneo hilo udongo kuanza kuporomoka.
  Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa tahadhari kwa wananchi wanaoendelea kusihi katika maeneo hayo huku akiutaka uongozi wa kijiji ,kata na wilaya kuhakikisha hakuna familia inaendele kuishi maeneo hayo hadi pale mvua zitakapo koma.
  Viongozi pamoja na wananchi katika eneo hilo wakifanya sala kabla ya kuondoka katika eneo hilo.
  Viongozi waliofika katika kijiji hicho wakiondoka eneo la tukio.
  Sehemu ya nyumba zilizo athirika hivi ndivyo ilivyoonekana.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0  Mmoja wa waasisi wa muziki wa kufoka foka nchini Chief Rhymson kutoka kundi la Kwanza Unit ambaye kwa sasa anafahamika kwa jina la Zavara ameendelea kufanya kazi zake za kimuziki katika eneo la uandaaji, uongozaji na kutengeneza video na hii moja ya kazi ya mikono yake inayozunguka duniani.

  0 0
 • 05/08/16--01:37: UDONDOZI MAGAZETINI LEO

 • 0 0

  Aaron Ally(Dj Aaron Tanzania)Mratibu wa‘All-stars Students Awards Akiongea Kwenye Kipindi cha Morning Trumpet kuelezea tuzo hizo.
  Dj wa zamani wa Clouds FM, Aaron, yeye na Team yake(Ms Chiku Lweno, Mwl. Dany Mtanga) wameanzisha Tuzo walizoziita All-stars Students Awards. Hizo ni tuzo zitakazotolewa kwa wanafunzi wa shule za sekondari A-level na O-level za Afrika Mashariki.Alhamisi hii Dj Aaron alialikwa kwenye kipindi cha Morning Trumpet cha Azam TV kuongelea tuzo hizo zitakazofanyika jijini Dar es Salaam.


  Aaron amesema tuzo hizo zina dhumuni la kuwapa hamasa wanafunzi wa shule za Afrika Mashariki. Tuzo hizo zitatolewa kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne na sita. pia na walimu husika ambao ni chachu ya wanafuzi ambao wamefanya vizuri kwenye hayo masomo.

  Tuzo hizo zitaaangalia namba moja wote waliongoza katika nchi zote za Africa Mashariki,
  Masomo yakayotolewa tuzo ni Kiswahili, Hesabu, Fizikia, Kemia, Bailojia na Kiingereza. Mchakato wa tuzo utaanza katikati ya mwezi wa sita.pia Special Talents, Michezo na Shule bora

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Amani K. Mwenegoha ameagiza maafisa tarafa kusimamia kwa karibu shughuli za hifadhi ya mavuno yaliyopatikana katika Mvua za vuli Msimu wa 2015/2016 kwa kuhamasisha wananchi wenye mavuno mengi kila mahali kuhifadhi vizuri ili mavuno hayo yasiharibike na kuweka akiba ya kutosha kwaajili ya kaya zao.

  Pia ameagiza Wakulima washauriwe kuuza ziada tu ya mavuno yao kwaajili ya kukidhi mahitaji yao muhimu na kila kaya isimamiwe kuhakikisha imehifadhi mazao ya chakula cha kuwatosha huku akiagiza Wafugaji washauriwe kuvuna sehemu ya mifugo yao kwaajili ya kukidhi mahitaji yao muhimu na kununua nafaka kwaajili ya kaya zao.

  Amesisitiza maelezo haya yawafikie viongozi ngazi za kata,vijiji na vitongoji kwaajili ya utekelezaji na taarifa iwasilishwe kwa Mkuu wa Wilaya kabla ya 13/05/2016.

  Imetolewa na

  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bukombe
  Geita 
  06 Mei, 2016

  0 0

  Na Editha Karlo blog ya Jamii, Kagera.

  WAKAZI wawili wa Mkoa wa Kagera wameshinda fedha taslimu kupitia shindano la pata patia linaloendeshwa na bank ya NMB katika matawi yake yote nchini.

  Wakiongea na mtandao huu mara baada ya kushinda fedha hizo mmoja wa washindi hao Jafram Mohamed ambaye ni askari polisi Wilayani Ngara alisema kuwa anaupongeza uongozi wa NMB kwa kuanzisha shindano hilo kwa wateja wao kwani lina lenga kuwahamasisha kujiwekea akiba mara kwa mara.

  Mohamed alisema kuwa yeye ni mtumishi wa serekali lakini amekuwa akijiwekea akiba mara nyingi kadiri awezavyo katika akaunti yake hali iliyopelekea kuingia katika droo ya kucheza bahati nasibu hiyo.

  "Nilifurahi sana baada ya meneja kunipigia simu na kuniambia nimeingia faini za bahati nasibu ya shindano la pata patia, hizi fedha nilizoshinda shilingi laki nane ntazifanyia jambo la msingi na ambalo ni kumbukumbu kwangu na familia yangu"alisema Mohamed.Naye mshindi mwingine Philbert Robart mjasiliamali na mkazi wa Wilaya ya Muleba alisema kuwa amefarijika kushinda kiasi cha shilingi laki nne katika bahati nasibu ya pata patia toka bank ya NMB.

  "Kwakweli bank ya NMB unatujali sana wateja wake, hizi fedha nilizoshinda leo zitanisaidia katila biashara zangu, nina wasihi wateja wote wa bank ya NMB nchi nzima wale wapya na wazamani kujiwekea fedha mara kwa mara katika akaunti yao itawapa nafasi ya kuingia katika shindano hili"alisema Rogati

  Meneja wa NMB Mkoa wa Kagera Victorine Kimario alisema kuwa shindano hilo la pata patia kwa wateja wao ni endelevu hivo amewataka wateja kujiwekea fedha kwenye akaunti zao mara kwa mara ili waweze kupata nafasi ya kuingia kwenye droo ya kushinda.

  ''Kampeni hii ya pata patia ya kuwataka wateja wetu kuweka fedha katika akaunti zao imeanza mwezi wa pili mwaka huu, wateja wanatakiwa kuweka fedha katika akaunti zao kuanzia kiasi cha shilingi elf hamsini na kuendelea mara kwa mara ili aweze kuingia katika faini za kushinda"alisema Meneja

  Alisema kila mteja ambaye anaingia fainali lazima ashinde sababu atatakiwa kuzungusha gurudumu lenye lenye nba kuanzia laki moja hadi milioni tatu na mshale wa gurudumu utakaposimama ndiyo kiasi ambacho atakuwa kashinda.Meneja Kimario amewataka wateja wapya na wazamani wa bank ya NMB kuendelea kuweka fedha kwenye akaunti zao mara kwa mara ili kujiweka katika nafasi ya kushinda bahati nasibu ya pata patia.
  Mshindi wa shindano la pata patia linaloendeshwa na bank ya NMB matawi yote nchini Jofram Mohamed akizungusha gurudumu na kushinda shilingi laki 8 taslimu.
  Mshindi mwingine wa shindano la pata patia linaloendeshwa na bank ys NMB kwa matawi yote nchini kutoka Mkoa wa Kagera Filbert Rogati akizungusha gurudumu  na kushinda shilingi laki 4
  Washindi wa shindano la pata patia wakisikiliza maelekezo toka kwa meneja wa NMB Mkoa wa Kagera kabla ya kuzungusha gurudumu la bahati nasibu
  Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa bank ya NMB tawi la bukoba mjini wakishuhudia washindi wanavyojipatia fedha zao kwa kuzungusha gurudumu. 

  0 0


  0 0  Mwili wa mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki ukiwasili kwa ajili ya maziko hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya. 
  Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Kenya Mh.Mwai Kibaki kufuatia kufiwa na mke wake mpendwa Mama Lucy Kibaki mjini Nairobi,nchini Kenya anaeshuhudia kulia ni Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta.
  Naibu Rais wa Kenya Mh.William Rutto na Mkewe wakimfariji Rais Mstaafu wa Kenya Mh.Mwai Kibaki wakati wa mazishi ya Mkewe Lucy Kibaki yaliyofanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya,Pichani shoto ni Rais Mstaafu awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akishuhudia tukio hilo.
  Rais wa Kenya Mh Uhuru Kenyatta akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete wakati wa mazishi ya Mama Lucy Kibaki hapo jana mjini Nairobi,kulia ni mke wa Rais Uhuru Kenyatta,Bi Margaret Kenyatta. 
  Rais Mstaafu wa Kenya,Mh.Mwai Kibaki akiweka udogo kwenye kaburi la Mke wake Mama Lucy Kibaki,wakati wa mazishi yaliyofanyika hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya.
  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka udogo kwenye kaburi la mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki .Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya. 
  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki .Mazishi hayo yamefanyika jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya,ambapo nchini Tanzania iliwakilishwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

  Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.

  Marehemu Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na wema katika familia.

  Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki.

  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.

  0 0


  Kwa mara nyingine tena Tanzania inashiriki katika onesho la kimataifa la Utalii la INDABA yanayofanyika huko Afrika Kusini maonesho hayo yalianza jana tarehe 7 Mei na yanatarajiwa kumalizika tarehe 9 Mei, 2016. jijini Durdan, Bodi ya Utalii (TTB) ndio waratibu wa onesho kwa upande wa Tanzania. Katika onesho hili TTB inashirki pamoja na taasisi za TANAPA na Mamlaka na Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na makampuni mbalimbali binafsi Zaidi ya 30 ya sekta ya Utalii .

  Katika siku yake ya kwanza Banda la Tanzania limetembelewa na wadau wengi wakiwemo watalii, waandishi wa habari za utalii, mawakala wa Utalii nk. Miongoni mwa watu mashuhuri waliotembelea Banda la Tanzania ni Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest ambaye alifurahishwa na vivutio vua utalii nchini Tanzania mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Maofisa wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB.Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian akimuonyesha jambo Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest wakati alipotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini..Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian akimpa maelezo kuhusu vivutio vya utalii nchini Tanzania Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest wakati alipotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini Katikati ni Bi Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB. Baadhi ya wagenimbalimbali waliotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya Utalii ya Indaba yanayofanyika katika jiji la Durban nchini Afrika Kusini.Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian na Bi. Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB. wakiwa na mmoja wa wageni aliyetembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini.
  Baadhi ya wageni wakipata taarifa mbalimbali kutoka katika banda la Tanzania.Wageni mbalimbali wakiwa katika banda la Tanzania.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joyce Hagu (wa pili kushoto), akimkabidhi Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), Stellah Joel, kadi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo kwa waimbaji wa nyimbo za injili uliofanyika Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mlezi wa chama hicho, Askofu Dk. Rejoyce Ndalima na Rais wa chama hicho, Ado Novemba.
  Hapa mwimbaji nguli wa nyimbo za injili Mzee Kitenzogu Makassy akikabidhiwa kadi yake baada ya kujiunga na NHIF.
  Burudani kutoka Kwaya ya Victorous Station ya Mwananyamala ikiendelea.
  Wanakwaya wakibadilishana mawazo katika uzinduzi huo.
  Burudani zikiendelea.
  Waimbaji wa kwaya ya Kanisa la Nabii Flora la Salasala wakitoa burudani.
  Wanakwaya ya Ukombozi ya Kanisa la Anglikana Tegeta wakionesha umahiri wa kumtukuza mungu kwa kuimba.
  Muonekano wa meza kuu katika uzinduzi huo.
  Ushuhuda ukitolewa kuhusu mungu anavyowatendea watu wake miujuzi.
  Mlezi wa chama hicho, Askofu Dk. Rejoyce Ndalima (kushoto), akiwa ameketi na mgeni rasmi mama Joyce Hagu.
  Maofisa wa NHIF kutoka Wilaya ya Kinondoni wakiwa tayari kuwandikisha wanachama wapa katika uzinduzi huo. Kutoka kulia ni Derick Ndyetabula, Margaret Malangalila na Dk.Fortunatus Salala.
  Mchungaji David Nyanda ambaye ni muimbaji (wa pili kulia), akionesha manjonjo wakati akitoa burudani kwa kuimba katika uzinduzi huo.
  Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), Stellah Joel akizungumza kwenye uzinduzi huo.
  Waimbaji na maofisa wa NHIF kutoka Kinondoni wakifuatilia uzinduzi huo.
  Rais wa Chamuita, Ado Novemba akizungumza kwenye uzinduzi huo.
  Furaha na shangwe zikiendelea katika uzinduzi huo watu wote mikono juuu.
  Meneja wa NHIF Wilaya ya Kinondoni, Constantine Makala akitoa darasa kuhusu faida za kujiunga na NHIF na jinsi ya kujiunga.
  Dk.Fortunatus Salala wa NHIF akizungumza kwenye uzinduzi huo.
  Mmoja wa waimbaji wa nyimbo za injili akielezea jinsi alivyonufaika na mfuko huo baada ya kujiunga miezi miwili iliyopita pamoja na mke wake.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joyce Hagu (kushoto), akionesha kadi za wanachama hao baada ya kuzizindua. Kulia ni Maadam Ruti Mwamfupe.

  Na Dotto Mwaibale

  WANACHAMA wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), wamejiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ili waweze kupata matibabi ya uhakika pindi watakapo umwa.

  Katika hatua nyingine Mlezi wa chama hicho Askofu Rejoyce Ndalima amewataka waimbaji wa nyimbo za injili kujianzishia miradi mbalimbali itakayowaingizia kipato badala ya kutegemea uimbaji pekee na amewasihi wanamuziki hao kuachana na utamaduni wa kudurufu (kukopi) kazi za wenzao badala yake wawe wabunifu katika kutunga nyimbo zao.

  Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Afya kwa wanachama wa chama hicho Dar es Salaam jana kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Ndalima alisema kuokoka sio kuwa mjinga hivyo ni vyema kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo.

  “Kuokoka sio kuwa mjinga kwani kuna fursa za biashara ambapo mnatakiwa kuonesha uwezo wenu wa kuzifanyia kazi ili muweze kujikwamua kiuchumi badala ya kung’ang’ania kazi moja tu ya uimbaji,” alisema Ndalima.

  Askofu Ndalima aliwataka waimbaji hao wajiunge na bima ya afya kwani hakuna mtu atakayechangiwa tena pindi atakapoumwa na kama ni msaada mtu husika atasaidia katika masuala mengine.

  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Joyce Hagu kutoka, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri wa wizara hiyo, alisema Serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha mfuko wa wasanii kutokana na kutambua mchango wao katika jamii.

  Hagu aliipongeza NHIF kwa kufikisha huduma hiyo kwa waimbaji hao kwani itawasaidia katika maisha yao hasa pale watakapohitaji kutibiwa katika Hospitali mbalimbali.

  Meneja NHIF Wilaya ya Kinondoni, Constantine Makala alisema kuwa huduma hiyo watalipia 76800 kwa mwaka mzima.
  Alisema watu wote waliojiunga na huduma hiyo wanaweza kupa matibabu katika Hospitali zilizoainishwa pamoja na kupata dawa katika maduka 200 yaliyosajiliwa na NHIF.

  0 0

  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifungua Semina wa Chama cha Wabunge wanaopambana na Rushwa-Tanzania Mjini Dodoma leo tare 8 Mei, 2016.Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifungua Semina wa Chama cha Wabunge wanaopambana na Rushwa-Tanzania Mjini Dodoma leo tare 8 Mei, 2016Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ( katikati pamoja na viongozi wengine wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa Semina wa Chama cha Wabunge wanaopambana na Rushwa-Tanzania. Wengine katika ni , Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki (kushoto) na Cecilia Paresso (Mb) – Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho.Wakili wa kujitegemea Bw. Said Yakubu akiwasilisha mada wakati wa Semina wa Chama cha Wabunge wanaopambana na Rushwa-Tanzania.Picha na Ofisi ya Bunge)

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Bidhaa za aina mbalimbali zinazotengenezwa na Wajasiriamali wadogowadogo kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya Mama na sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yamefanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
  Baadhi ya Wajasiriamali wadogowadogo wakifuatilia maonesho ya maadhimisho ya siku ya Mama na sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yamefanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi cheti mmoja kati waliofanya vizuri kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya Mama na sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yamefanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Tunzo alizokabidhiwa na UWT Taifa kwa ajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa Kwanza Mwanamke kwenye maadhimisho ya siku ya Mama yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yaliyofanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
  Wananchi wa Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,alipokua akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Mama na sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke yaliyofanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Wanawake kwenye maadhimisho ya siku ya Mama na sherehe za kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais Mwanamke wa kwanza yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yaliyofanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.

  Vikundi mbalimbali vya Ngoma Vikitumbuiza kwenye maadhimisho ya siku ya Mama na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yaliyofanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Wanawake na Wananchi wa Dodoma baada ya kuwahutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Mama na kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yaliyofanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.(Picha na OMR)

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Sehemu ya waumini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa akiwsalimia  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia na wanakwaya  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia baadhi ya watawa aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia baadhi ya watawa aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia baadhi ya watawa aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Padri Kiongozi Germin Longio baada ya kushiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016. Kulia ni Pdr. Germin Longio na kushoto kwake ni Padri  wasaidizi Prosper Tesha na Furchong James Luis
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na vijana wa altari katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Sehemu ya waumini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa akiwsalimia  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishiriki katika  ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea zawadi ya Rozari  kutoka kwa Padri Kiongozi Peter Pinto  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akishukuru baada ya kupokea zawadi ya Rozari kutoka kwa Padri Kiongozi Peter Pinto  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea zawadi ya Biblia Takatifu kutoka kwa Padri Kiongozi Peter Pinto  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Mei, 2016 ameungana na waumini wa Parokia ya Toleo la Bwanailiyopo katika Jimbo Katoliki la Arusha kusali ibada ya Jumapili, ambapo katika salamu zake amewaomba watanzania kuendelea kuiombea nchi yao ili kazi anayoifanya ya kukabiliana na matatizo yanayowakabili watanzania wanyonge ifanyike kwa mafanikio.


  Dkt. Magufuli amesema hayo alipokaribishwa na Mwenyekiti wa Parokia hiyo Bw. Philemon Mushi kuwasalimu waumini wa kanisa hilo, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya Jumapili ya kupaa kwa Bwana.


  "Niko pamoja na nyinyi ndugu zangu watanzania na wana Arusha wote, napenda kuwaahidi tena sitawaangusha, nitasimama mbele kuwatetea masikini, siku zote nitakuwa upande wenu, siku zote nitatembea na nyinyi, nasema kwa dhati kabisa na nataka muamini hilo kwamba sitawaangusha" amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa na waumini walioshiriki ibada hiyo.


  Rais Magufuli amewahakikishia watanzania wote kuwa atahakikisha ahadi zote alizoziahidi anazitekeleza na amewaomba watanzania wote kuungana na kushikamana ili kufanikisha juhudi za kuijenga Tanzania bora.


  "Ninajua kuongoza ni kazi kubwa, ninajua kuongoza Taifa lililo masikini kama Tanzania inahitaji mkono wa Mungu, kwa hiyo niwaombe sana ndugu zangu Wakristo na watanzania kwa ujumla, muendelee kuliombea Taifa hili, kuniombea mimi, na pia kujiombea sisi wote ili amani tuliyonayo katika nchi yetu iendelee kudumu katika maisha yote.


  "lakini siku zote katika matendo yetu kila tunapofanya tumtangulize Mungu kwa sababu Mungu ndio kila kitu, lakini tutambue kwamba siku moja tutakufa, kwa hiyo ni vyema katika matendo yetu tutakapokuwa hapa duniani tujitahidi sana kufanya matendo mazuri kwa ajili ya watu na hasa watu wanyonge, ambao kwa kweli watanzania waliowanyonge wanapata shida sana"Amebainisha Rais Magufuli.  Pia Dkt. Magufuli amewasihi watanzania wote kuachana na ushabiki wa vyama vya siasa na badala yake waungane katika ujenzi wa Taifa na kukabiliana na kero zinazowaumiza.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Arusha


  08 Mei, 2016


  0 0

  Chama cha Alliance for Democratic Change ADC kimewafuta uanachama wanachama wake wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Bwana Said Miraaj,Katibu Mkuu Bi.Lydia Bendera,Mkurugenzi wa mipango na uchaguzi Bwana Jumanne Magafu pamoja na Katibu wa Kamati ya ulinzi Bwana Juma Wandwi kwa makosa ya kukiuka katiba ya chama hicho kwa kususia kushiriki uchaguzi mkuu wa marudio wa Zanzibar.

  Maamuzi hayo yamefikiwa katika mkutano mkuu wa chama hicho ambapo akizungumza baada ya ufunguzi aliyekuwa mlezi wa chama cha ADC ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Zanzibar,Mhe.Hamad Rashid amesema katiba ya chama inasisitiza ushiriki katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi,hivyo kutoshiriki ni kukivunja nguvu chama katika mikakati yake ya kuchukua dola.

  Akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa -ADC- Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa Bwana Sisty Nyahoza amesema kitendo cha chama cha siasa kutoshiriki uchaguzi kinakwenda kinyume na sheria ya vyama vya siasa na malengo ya kuanzishwa chama Chochote cha siasa na kusisitiza ipo haja ya kuangalia mfumo wa usajili wa vyama utakaowezesha kutoa adhabu kwa vikavyoonekana kukataa kushiriki katika chaguzi.

  Aidha katika mkutano mkuu huo, wajumbe wamemchagua aliyekuwa mlezi wa ADC ambaye kwa sasa ni Waziri wa Kilimo Zanzibar Mhe.Hamad Rashid kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bwana Doyo Hassan Doyo amechaguliwa kushika wadhifa wa katibu mkuu wa chama.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wafanyabiashara wote walioficha sukari katika maghala yao, kuanza kuisambaza mara moja, vinginevyo serikali itachukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kuinyang'anya sukari hiyo na kuisambaza kwa wananchi bure.

  Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 06 Mei, 2016 katika mikoa ya Singida na Manyara wakati akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti waliosimamisha msafara wake uliokuwa ukitoka Dodoma kwenda Arusha.

  Dkt. Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuwafuatilia wafanyabiashara wanaofanya njama za kuficha sukari na kusababisha upungufu wa bidhaa hiyo, na ameapa kuwa serikali yake itawachukulia hatua kali watakaobainika kufanya hivyo.

  Pamoja na kutoa maagizo hayo Rais Magufuli amewaondoa shaka watanzania juu ya upungufu wa sukari, kuwa serikali imeagiza sukari kutoka nje ya nchi ambayo itasambazwa kwa wananchi kwa bei nafuu ili kufidia upungufu uliopo.

  "Wale wote waliokuwa wameficha sukari waiachie, wasipoiachia sukari, huwezi kuificha kama sindano, nimeshaagiza vyombo vya dola, vikague magodown yote, atakayekutwa na sukari ameificha, yule ni mhujumu uchumi kama wahujumu wengine, asije akanilaumu, asijee-akanilaumu, na ninasema kwa dhati, wewe mfanyabiashara uliyepata nafasi ya Tanzania kuleta bidha za sukari,  halafu unanunua unakwenda kuficha ili kusudi wazee hawa wahangaike, ili mwezi mtukufu wa Ramadhani utakapoingia watu wakose sukari, dawa yao ninayo" Amesema Rais Magufuli.

  Aidha, akizungumza katika miji ya Katesh, Babati, Dareda na Magugu Mkoani Manyara Dkt. Magufuli amepokea malalamiko ya wananchi kuhusu kukosa maeneo ya kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji, na amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Bw. Joel Bendera na wakuu wilaya za mkoa huo kukamilisha mchakato wa kuyapitia mashamba yote yaliyotelekezwa na wamiliki wake, kisha wawasilishe taarifa kwake ili afute hati za umiliki wa mashamba hayo na kuamuru wagawiwe wananchi.

  "Kero kubwa katika maeneo haya, pamekuwa na mashamba makubwa ambayo yalichukuliwa na wenye pesa, halafu yale mashamba hawayaendelezi, na wanapoacha kuyaendeleza wanawachukua wananchi masikini na kuanza kuwakodisha, kwa kukusanya fedha, mniachie hili ndugu zangu nitalishughulikia" Amesisitiza Dkt. Magufuli.

  Mjini Babati Rais Magufuli amepokea kilio cha wananchi waliodai kudhulumiwa haki zao na kujikuta wakipoteza mali ikiwemo nyumba za kuishi na mazao na amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Manyara kupanga siku za kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
  Rais Magufuli amewasili Mjini Arusha akitokea Dodoma kwa njia ya barabara na kesho anatarajia kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) kundi la 58/15 katika chuo cha mafunzo ya jeshi Monduli.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Arusha
  06 Mei, 2016.

  0 0

  Kijana mjasiriamali Diana Moshi (Kulia) akimkabidhi keki Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (Kushoto) kama shukrani yake kwa Airtel baada ya kuwezeshwa  kupitia mpango wa Airtel FURSA "Tunakuwezesha" kwa kukabidhiwa vifaa vya kisasa vilivyomsaidia kuboresha biashara yake ya kupika keki na kumsaidia kupata mafanikio. Makabidhiano hayo yalifanyika katika makao makuu ya ofisi za Airtel Morocco jijini Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 841 | 842 | (Page 843) | 844 | 845 | .... | 1903 | newer