Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 840 | 841 | (Page 842) | 843 | 844 | .... | 1904 | newer

  0 0

  RC Mwanza, John Mongella

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) akisalimiana na kumkaribisha ofisini kwake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale (katikati) walipowasili jijini Mwanza kabla ya ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Ulaya.

  MRATIBU Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale, wamesema wameridhishwa na miradi inayofadhili maeneo kadhaa jijini Mwanza.

  Wakizungumza baada ya kutembelea Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Mwauwasa), Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC), Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) na Radio ya Kijamii (Saut), walisema utekelezaji wa miradi hiyo imewatia hamasa kubwa.

  Awali akizungumza katika ofisi za Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Anthony Sanga, alisema mradi unaoendelea sasa wa kusambaza maji safi utakapokamilika utaweza kuwafikia wakazi 54,000 badala ya 23,000 wa sasa.Sanga alisema mradi huo utakapokamilika Mei mwaka huu, utawafikia wakazi kwa asilimia 90 badala ya 68 za sasa.

  “Mradi ukishakamilika utafanikisha makusanyo ya Sh. Bilioni 1.4 kwa mwezi badala ya kukusanya Sh. milioni 316 za sasa kwa mwezi, ukiwa na matanki ya ujazo wa lita 33,400,” alisema Sanga.Akizungumzia hilo, Rodriguez alisema baada ya kushuhudia miradi hiyo ukiwamo wa maji taka chini ya ufadhili wa EU, amefurahishwa na hali ya miradi hiyo.

  “Timu yetu imetembelea Mwauwasa na kushuhudia miradi hiyo inayofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya kwa ajili ya huduma ya maji kwa wananchi, pia tumeenda kuangalia chanzo cha maji na yanapowekwa maji taka,” alisema Rodriguez.Naye Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Prof. Kien Mteta, alishukuru UN na EU kwa miradi hiyo na kuja kushuhudia ufadhili wao.

  “Ufadhili umelenga katika mambo matatu, moja kwenye maabara ambako vilinunuliwa vifaa vya mbalimbali vikiwamo vya kutambua kansa, pili vifaa vya mionzi kwa ajili kutambua vyanzo vya magonjwa,” alisema Prof. Mteta.Aidha, alisema pia wafadhili hao walitembelea kitengo cha kutoa matibabu ya mionzi ya kansa, ambacho kinawafunza baadhi ya watumishi wake na upatikanaji wa mashine.
  Luana Reale, EU Tanzania
  Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella mara baada ya kuwasili ofisini kwake mwishoni mwa wiki.

  Hospitali ya Bungando yenye uwezo wa vitanda 950 iliyoanzishwa mwaka 1972 ni miongoni mwa hospitali nne kubwa nchini ambazo hutoa tiba maalumu ikihudumia watu milioni 16 katika mikoa minane ya kanda ya ziwa.Hospitali hii inatoa tiba ya ugonjwa wa saratani kwa mifumo miwili. Moja kwa kutumia onkolojia au patholojia na tiba kwa kutumia mionzi.
  Toka mwaka 2000 hospitali ya Bugando imekuwa ikifanyakazi kwa karibu na kampuni ya kitaliano ya TISSON ASSOCIATION ili kuboresha huduma zake patholiojia na pia kuanza kutibu kansa mwaka 2009.

  Wataliano wamewezesha kufundishwa kwa wataalamu wa patholojia na onkolojia ya tiba, vifaa tiba, dawa na kuwezesha ziara za za kifundi za watu wa patholojia na utafiti.Uangalizi wa wagonjwa wa kansa na matibabu yao ulianza mwaka 2009 na kuelezwa kuwa kwa mwaka wagonjwa 3500 wa kansa huangaliwa.Huduma ya uangalizi ni pamoja na kufanya utambuzi, upasuaji na utoaji wa tiba ya kemo.
  Hoyce Temu
  Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akitoa utambulisho wa ujumbe alioambatana nao kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.Hata hivyo wagonjwa wanaohitaji huduma ya mionzi hukatiwa rufaa hospitali ya kansa ya Ocean (ORCI).

  Kutokana na kuzidiwa kwa hospitali ya Ocean Road katika tiba ya mionzi, serikali iliamua kutanua huduma zake na kuzifikisha Bugando.Ili kuwezesha haja ya serikali taasisi ya nguvu za atomiki duniani na ile ya hapa nchini kupitia mpango wa ushirikiano wa kiufundi walianzisha miradi kadha yenye lengo la kuwezesha huduma yenye tija kwa wagonjwa wa kansa.Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo yanachangia miradi hiyo imekuwa ikisaidia serikali ya Tanzania kuwezesha tiba ya mionzi katika hospitali ya Bugando.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale katika ziara maalum ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na UN pamoja na EU jijini humo.

  Alvaro Rodriguez
  Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza CP. Clodwig Mtweve, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella pamoja na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale wakiwa wameshilikilia kuhamasisha utekelezaji wa malengo mapya ya maendeleo endelevu (SDGs) ambayo yamewafikia wakazi wa jiji la Mwanza.
  Luana Reale
  Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa) mara baada ya kuwasili katika ofisi hizo jijini Mwanza.
  Eng. Anthony Sanga
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony Sanga, akitoa 'power point presentation' ya maendeleo ya mradi wa maji unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya jijini Mwanza kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
  Anthony Sanga
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony Sanga akitoa maelezo ya mradi kwa ugeni ulioambata na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
  Mwauwasa 1
  Maji yakiwa kwenye hatua ya kutakatishwa ili yawe salama kwa watumiaji.
  Godadi Mgwatu
  Mhandisi wa ubora wa maji Mwauwasa, Godadi Mgwatu akitoa maelezo kwa mgeni ugeni huo ulioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kukagua mradi wa maji wa Mwauwasa jijini Mwanza.
  Mhandisi, Anthony Sanga-Mwauwasa Mwanza
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony Sanga akitoa maelezo kwa ugeni huo ya namna ya maji yanavyochujwa na kusafisha kwa kutumia mtambo maalum uliopo mbele yao. (Picha zaidi za ziara hii Bofya hapa)

  0 0


    Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata  akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato nchini kulia ni Kamishna wa kodi za ndani Bw. Yusufu Salum.(Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO).

  Na Lilian Lundo MAELEZO

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imejipanga kugawa jumla ya mashine 5700 za (Electronic Fiscal Devices) EFD’s kwa wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ikiwa ni jitihada za Serikali katika kukusanya mapato nchini.Akizungumzia mipango hiyo leo, Jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Alphayo Kidata amesema wameamua kuanza kugawa mashine hizo kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao wengi wao hawana uwezo wa kugharamia manunuzi ya mashine hizo.

  “ Mamlaka imeona changamoto wanayoipata wafanyabiashara wadogo hivyo imeamua kuanza kugawa mashine hizi ili kuondokana na tatizo la kutotoa risiti za mauzo kwa wafanyabiashara hao ambao walio wengi walikuwa na kisingizio cha kutokuwa na mashine hizo”. Alisema Kidata.

  Kamishna Kidata ameongeza kuwa Mamlaka yake imeshaagiza mashine hizo na zipo tayari kuanza kugawiwa mwezi huu kwa wafanyabiashara  hao ikiwa ni awamu ya kwanza ya ugawagaji wa mashine hizo ambao utafanyika nchi nzima.

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeazimia kugawa mashine laki mbili kwa wafanyabiashara wadogo wadogo nchini ikiwa ni jitihada za kuweza kukusanya mapato yatokanayo na kodi za biashara kwa urahisi na ufanisi mkubwa.

  0 0


  Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) akiongea na Waandishi wa Habari leo 6 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam kuhusu msaada walioupokea toka Shirika la Afya Duniani (WHO) wenye thamani ya shilingi bilioni 1.4.
  Mkurugenzi wa Huduma za Kinga,Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa tiba leo 6 Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro wakikabidhiana hati za makabidhiano ya vifaa tiba leo 6 Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.

  Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro (kulia) akikabidhi jokofu kwa kwa jaili ya huduma za chanjo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Neema Rusibimayila leo 6 Mei, 2016 jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa juu ya makabdhiano ya vifaa tiba toka Shirika la Afya Duniani (WHO) pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo 6 Mei, 2016 Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Benedict Liwenga)


  Na Benedict Liwenga-MAELEZO.

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kutoa chanjo kwa akina mama na watoto dhidi ya magonjwa mbalimbali nchini.

  Akiongea na waandishi wa habari Wizarani hapo, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Dkt. Neema Rusibimayila ameeleza kuwa vifaa tiba hivyo vitasaidia uhifadhi wa chanjo katika mikoa mbalimbali pamoja halmashauri nchini.

  ‘’Ni msaada mkubwa tulioupata toka WHO na nina amini kuwa utatusaidia sana katika kufanikisha suala la chanjo kwa akina mama na watoto nchini na pia tunaamini wataendela kushirikiana na Wizara ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea’’, alisema Dkt. Rusibimayila.

  Ameongeza kuwa, kwa sasa vituo vipya vinavyofunguliwa nchini vikiwemo vile ambavyo havikuwa na majokofu vitakuwa na uwezo wa kupata vifaa hivyo kama vile majokofu na vifaa vingine vya tiba ili huduma za chanjo ziweze kutolewa katika kila kituo nchini.

  Akikabidhi vifaa hivyo Wizarani hapo, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Rufaro Chatoro amesema kuwa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 ni pamoja na majokofu 200 pamoja na vifaa vitumikavyo kwa ajili ya kutolea chanjo.


  Kwa upande wake Mratibu Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bwana Emmanuel Yohana ameeleza kuwa, majokofu hayo pia yatapelekewa katika wilaya ambayo yana upungufu wa majokofu pamoja na vituo vipya kwa ajili ya kupunguza umbali kwa wagonjwa wa chanjo na pia ni moja ya kuweka huduma karibu na wananchi nchini.

  Aidha, ameongeza kuwa spesimeni za polio na surua zilizotolewa na WHO zitapalekwa pia katika vituo kwa jili ya kuchukua damu kwa ajili ya vipimo na kuletwa Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi wa maabara.‘’Wanufaika wa huu msaada kutoka WHO ni wananchi wote wa Tanzania kwani utaenda katika vituo vyote vya chini zikiwemo Zahanati’’, alisema Yohana.

  Kupitia wadau mbalimbali Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea kushirikiana na wadau hao katika kutafuta vifaa tiba mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kuwa sekta ya afya nchini inaimarika kwani Tanzania kwa sasa imeweza kudhibiti polio kwa kiasi kikubwa.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan Mhe,Mathias M.Chikawe alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kuonana na Rais,leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan Mhe,Mathias M.Chikawe alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya mazungumzo yao,[Picha na ikulu.].

  0 0

  Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.

  Serikali inaendelea kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ili kuchangia upatikanaji wa fedha za kusaidia kuimarisha na kuendeleza miradi ya maendeleo nchini. 

  Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imekuwa miongoni mwa taasisi za Serikali ambayo imeanza kukusanya ada zote zitokanazo na huduma inazotoa kwa njia ya kielekroniki kwa wadau wake kufanya malipo kwa njia ya simu au benki kabala ya kupata huduma wanayohitaji.

  Hatua hiyo imefikiwa na Wizara Katiba na Sheria ili kuhakikisha Serikali inakusanya mapato kuanzia sasa na mwaka wa fedha 2016/2017 ili kuwahudumia wananchi.

  “Tayari wilaya 114 kati ya 139 zinakusanya maduhuli kwa njia ya kielekroniki na kwamba ifikapo Juni, 2016 wilaya zote Tanzania Bara zitakuwa zinatumia njia ya kielekroniki kukusanya maduhuli” alisema Dkt. Mwakyembe.Katika kuongeza mapato, Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa upo mkakati wa kuongeza kiwango cha usajili wa vizazi na vifo nchini, ambapo RITA imeanzisha kampeni ya usajili inayoambatana na uboreshaji wa mfumo wa usajili kwa kuweka mfumo wa kompyuta kila wilaya ambapo kampeni hizo zilifanyika.

  Wilaya ambazo kampeni hizo zimefanyika ni Arusha na Arumeru ambapo jumla ya watu 49,548 wamesajiliwa na kupewa vyeti vyao vya kuzaliwa.Zoezi hilo la usajili linaendelea katika wilaya ya Kahama na baadaye litaendelea katika wilaya 16 nchini ambazo ni Bariadi, Chato, Dodoma, Igunga, Kilombero, Kilosa, Lushoto, Maswa, Mbinga, Misungwi, Mtwara, Muleba, Nzega, Shinyanga, Sumbawanga na Tunduru.

  Waziri Mwakyembe alibainisha kuwa Wizara hiyo kupitia RITA imekusudia kusajili zaidi ya watu 500,000 katika maeneo hayo na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.Kwa mujibu wa utafiti wa afya uliofanyika 2010, asilimia 16 ya watoto wenye umri wa miaka mitano ndio wenye usajili na vyeti vya kuzaliwa Tanzania Bara ikilinganishwa na Tanzania Zanzibar ambapo usajili ulikuwa ni asilimia 79.

  Ili kukabiliana na hali hiyo, RITA kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) wamebaini mradi wa kusajili watoto chini ya umri wa miaka mitano uliofanyiwa majaribio wilaya ya Temeke mwaka 2012 na kuzinduliwa rasmi mwaka 2014 mkoani Mbeya.

  Kampeni hiyo imeonesha mafanikio na tija kwa taifa ambapo usajili umeongezeka na kufikia asilimia 58 ambapo awali mkoa wa Mbeya usajili ulikuwa asilimia 8.7.Kampeni hiyo ni endelevu kwa nchi nzima ambapo mikoa itakayoanza kufanya usajili ni Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Iringa, Njombe, Tabora, Kagera na Dodoma.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waumini wa Dini ya Kiislam baada ya Sala Ijumaa katika Msikiti Mkuu wa GADAFFI Mkoani Dodoma Leo Mei 6,2016. (Picha na OMR)

  0 0

  Mwenyekiti wa Mbeya City fc, Mussa Mapunda amelipongeza shirikisho la soka Tanzania TFF kwa hatua yake ya kuipoka pointi 3 timu ya Azam Fc na kuziweka kwa timu yake kufutia makosa yaliyofanywa na timu hiyo ya Chamazi Complex kumchezesha mchezaji Erasto Nyoni aliyekuwa na zuio la kadi tatu za njano.

  Muda mfupi uliopita Mapunda ameimbia mbeyacityfc.com kwamba kwa kosa hilo City ilistahili kupata ushindi huo wa bao 3 na pointi 3 kama ambavyo kanuni za ligi zinavyoelekeza na kutoa angalizo kwa vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara kuongeza umakini katika kutunza kumbukumbu za adhabu au makosa mbalimbali kwa wachezaji wake.

  “Kwenye hili nalipongeza shirikisho, hakika wametenda haki, na ninawaomba waendelee kusimama kwenye misingi ya haki, ni haki yetu kupata pointi 3 baada ya Azam fc kuchezesha mchezaji mwenye adhabu ya kadi 3 ambaye ni wazi hakustahili kucheza mchezo ule, hata sisi tumekutana na hali hii katika nyakati tofauti lakini hatukuwahi kuthubutu kumchezesha mchezaji mwenye adhabu hata kama alikuwa ni muhimu kikosini” alisema.

  Akiendelea zaidi Mwenyekiti Mapunda alisisitiza vilabu kuwa makini na matukio ya aina hii huku pia akiikumbusha TFF kuendele kuchukua hatua kama hizi.

  Katika hatua nyingine Mapunda amesema kuwa bado anaamini TFF itaitendea haki City kwa kuchukua hatua kama hizi kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union uliovunjika dakika mwisho za kipindi cha pili baada ya kutokea kwa vurugu kubwa uwanjani zilizosababishwa na mashabiki wa timu hiyo ya Tanga.

  “Naamini TFF watatutendea haki kwenye hili pia,mchezo ule ulikuwa na matukio mengi ya ajabu ambayo yalimfanya mwamuzi kushindwa kumaliza mchezo, risasi za moto zilipigwa uwanjani, , sisi bado tunasubiri pointi tatu zingine kutoka kwenye mchezo ule, kwa sababu mnyonge mnyongeni haki yake mpeni”, alimaliza.

  0 0  Pichani ni Watuhumiwa hao Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry Kitilya (mwisho kulia haonekani pichani), Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic tawi la Tanzania Shose Sinare wakipeana mikono na Mawakili wao,ndugu jamaa na marafiki mahakamani hapo mapema leo mara baada ya Mahakama kuu leo Mei 06 2016 Kusikiliza rufaa ya kufutiwa shitaka lao namba nane la utakatishaji fedha.


  Na JacquilineMrisho - MAELEZO

  Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iliyokuwa ikipinga kuondolewa kwa shitaka la 8 la utakatishaji fedha linalomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Harry Kitilya na wenzake wawili.
   
  Uamuzi huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Moses Mzuna alipokuwa akitoa majibu ya rufaa iliyokuwa imekatwa na DPP.
   
  “Ninafahamu kila kesi inaamuliwa kutokana na mazingira yake lakini nimefuta rufaa hii kwa kuwa hoja zilizotolewa hazina nguvu kisheria” alisema Jaji Mzuna.
   
  Aidha Jaji Mzuna amefafanua kuwa hata kama amefuta rufaa hiyo lakini upande wa Jamuhuri bado una nafasi ya kubadilisha shitaka au hati nzima ya mashtaka inayowakabili washtakiwa hao.
   
  Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali Timony Vitalis amekubaliana na uamuzi uliotolewa na Mahakama hiyo juu ya pingamizi lake ingawa bado anasimamia watuhumiwa kutofutiwa shitaka la utakatishaji wa fedha.
   
  Naye Wakili wa Utetezi Majula Magafu amesema kuwa wao wanasubiri maamuzi yatakayotolewa na Wakili wa Serikali ili wajue namna ya kuikabili kesi hiyo.

  0 0

  MFANYAKAZI wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, akiielekeza ndege ya Shirika la Ndege Mauritius Airlines, kuegesha kwenye daraja la kushukia abiria (Bridge), kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 6, 2016. Ndege hiyo aina ya Airbus 319 yenye uwezo wa kubeba abiria 130, imetua kwa mara ya kwanza na itakuwa ikifanya safari zake kila Ijumaa ikiruka moja kwa moja kutoka Mauritius kuja Dar es Salaam kasha Nairobi, nchini Kenya.
  Magari ya zimamoto yakiipokea ndege hiyo kwa kuimwagia maji ikiwa ni ishara ya ukaribisho

  NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, JNIA

  Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, kupitia uwanja wake wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, imeongeza idadi ya mashirika ya ndege yanayotumia uwanja huo baada ya ndege ya kwanza ya Shirika la Ndege la Mauritius (Mauritus Airlines), kutua kwenye uwanja huo leo Mei 6, 2016.

  Ndege hiyo aina ya Boeng Airbus 319, yenye kubeba abiria 130, ilitua kwenye uwanja huo majira ya saa 5;20 asubuhi ambapo kama ilivyoada ya kupokea ndege mpya inayoanza shughuli zake kwenye uwanja huo, magari mawili ya zimamoto yalipiga (saluti), kumwagilia maji ndege hiyo wakati ikielekea kuegesha kwenye daraja la kushukia abiria.

  Kwa mujibu wa maafisa wa Shirika hilo, ndege hiyo itakuwa ikiruka kutoka Mauritius moja kwa moja na kutua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo itashusha abiria na kuelekea uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.“Safari ya kutoka Mauritius kuja Dar es Slaam ni kiasi ya masaa matatu .”alisema rubani mkuu wa ndege hiyo, Parikshant Nundlol

  Maafisa wa TAA waliiambia K-VIS MEDIA kuwa ndege hiyo itakuwa ikifanya safari yake mara moja kwa wiki kila siku ya Ijumaa.

  Rubani mkuu wa ndege hiyo, Parikshany Nundlol, akizungumza na waandishi wa habari wa Mauritius waliofuatana na ndege hiyo

  Warembo wa Kitanzania walioshiriki kuipokea ndege hiyo  Wafanyaakzi wa shirika la ndege la Mauritius na wale wa Swissport wakiwa katika picha ya pamoja
  Abiria wa kwanza waliowasili na ndege hiyo
  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua karanga kutoka kwa mjasiriamali mara baada ya kuwahutubia mamia ya wakazi wa Babati mkoani Manyara waliojitokeza katika eneo la Stendi ya Mabasi ya Babati Mkoani Manyara.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Magugu mkoani Manyara wakati akielekea  Mkoani Arusha.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyabiashara wa Stendi ya Mabasi ya Singida wakati alipokuwa njiania kuelekea Arusha.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Endasak mkoani Manyara wakati akitokea Dodoma kuelekea Arusha kwa njia ya barabara.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Dareda mkoani Manyara waliojitokeza kumsalimia wakati akitokea Dodoma kuelekea mkoani Arusha. PICHA NA IKULU

  0 0

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto inasikitishwa na inalaani vikali tukio la kuuawa kwa kuchinjwa, mwanamke Oliver Erasto (23) na mtoto wake Emmanuel (3), wakazi wa eneo la Zinga, kata ya Dunda, wilayani Bagamoyo, kutokana na wivu wa kimapenzi.

  Wizara inakemea maauji hayo, yanayodaiwa kutekelezwa na Frowin Mbwale mkazi wa Kawe, Dar es salaam, ambaye ni mme wa marehemu, kwani yamesababisha kukatisha maisha ya mama na mtoto, katika kipindi ambacho Taifa linahimiza uzingatiaji wa mchango na haki za wanawake katika maendeleo ya taifa, na mwitikio wa haki ya kuishi ya Mtoto katika mipango na programu za maendeleo endelevu.

  Wizara inasisitiza kutambua kuwa jukumu la ulinzi na usalama wa wanafamilia liko mikononi mwa kila mwananchi, hivyo jamii inawajibu wa kusaidia udhibiti wa ukatili na mauaji katika familia na jamii zetu. Jamii ikiwa na uelewa wa pamoja katika haki za wanawake na watoto katika jamii, itawezesha kuwekeza katika haki ya kuishi ya Mtoto, na kuendelea kuwaamini wanawake kwamba wanaweza kutoa mchango mkubwa wa kuendeleza familia zao, na taifa likaweza kupiga hatua kufikia maendeleo endelevu. 

  Wizara inapenda kupongeza Polisi mkoa wa Pwani na wananchi walitoa taarifa za kuwakamata watuhumiwa wa mauaji haya, na tunaamini kuwa watakapofikishwa mbele ya vyombo vya sheria haki itaweza kutendeka.

  Wizara inapenda kutoa pole kwa familia za marehemu hao waliopoteza maisha kwa kuchinjwa na kuawa, na kuwaombea kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki cha majonzi makubwa. Wizara inaitaka jamii itambue kuwa hakuna mwenye haki ya kukatisha uhai wa mtu mwingine, na mwanamke na mtoto anahaki ya kuthaminiwa utu wake, bila ubaguzi wowote ambao unaweza kukatisha maisha yao.

  Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee

  0 0

  Mtangazaji wa kipindi cha Rushwa ni Adui wa Haki Bi. Miriam Chisoro (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Mathew Kirama (kulia) wakati wakijadili mada kuhusu Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa umma ofisini kwa mkurugenzi huyo mapema leo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa Maadili wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Mathew Kirama (kulia) akisisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa umma wakati wakijadili mada hiyo na Mtangazaji wa kipindi cha Rushwa ni Adui wa Haki Bi.Miriam Chisoro (kushoto) ofisini kwa mkurugenzi huyo mapema leo.

  0 0  Rais Dkt.John Pombe  Magufuli amewaonya aalioficha Sukari na kutishia  Kuichukua Sukari hiyo na Kuigawa Bure Kwa Wananchi.Rais Magufuli ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara walioficha sukari ili baadae waiuze kwa bei  ya juu.

  Amesema wafanyabiashara hao wenye tamaa ya pesa walikuwa wakifuata sukari iliyo Expire huko Brazili   na kuileta nchini ili watengeneze faida na ndo maana serikali iliwapiga marufuku kuagiza.Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akiwasalimia wananchi wa Katesh, Mkoani Manyara. Rais ametoka Mkoani Dodoma leo, anaelekea Mkoani Arusha kwa usafiri wa gari.

  Akiongea na mamia ya wananchi hao waliojitokeza kumlaki njiani, Rais Magufuli amewatoa hofu wananchi kuhusu uhaba wa sukari kwa kuwa tayari wako  katika mchakato wa kuagiza makontena ya sukari nje ya nchi ili kuwakabili wafanyabiashara walioficha bidhaa hiyo.Amesema kwa taarifa alizonazo kuna mfanyabiashara alienda akanunua sukari pale Kilombero zaidi ya tani 3000 na hataki kuzichukua hadi leo

  Pia amesema kuna mwingine ana godauni huko Mbagala yenye tani 4000  ambazo hataki kuzitoa ili wananchi wakose sukari.Rais Magufuli amesema ameviagiza vyombo vya dola viwafuatilie ili ikithibitika sukari waliificha basi ichukuliwe na kugawiwa bure kwa wananchi na pia watapigwa marufuku kufanya biashara yoyote hapa nchini

  0 0


  0 0

  MADAKTARI wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamefunga kambi ya Madaktari wa tiba ya Moyo wa kutoka Saudi Arabia na Qutar na baaadhi ya madaktari wenye utaalam wa tiba ya matatizo ya moyo hapa nchini.

  Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo  kutoka nchi za Saudi Arabia na Qutar jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa kambi hiyo imejumuisha pamoja taasisi nne kutoka nchi tatu tofauti.

  Abri amesema taasisi zilizoshiriki kambi ya Moyo Muhimbili ni Muntada Aid ya Uingereza, Timu ya Madaktari kutoka Saudi Arabia, Taasisi ya Araf kutoka Qutar na taasisi ya Dhi Nureyn ya hapa nchini na Taasisi ya Jakaya Kikwete.

  Amesema kuwa kambi  hii ya sasa imefanikiwa kuwatibu watoto wenye matatizo ya moyo 66 ambao walikuwa wamepangwa kusafirishwa  nje ya nchi kwaajili ya matibabu sasa wametibiwa hapa nchini na kuokoa mabilioni ya fedha za serikali.

  Kwaupande wake Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala amewashukuru madaktari kutoka taasasisi hizo kwa kuja hapa nchini na kuokoa watoto wenye matatizo ya moyo 200 ambao wametibiwa hapahapa nchini.

  Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala akizungumza hatika hafla ya kufunga kambi ya madakitari wa Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar waliokuwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, haflaa hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam na kuwaaga madaktari wa nchi hizo.
  .

   Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri akizungumza na madaktari wa wa Moyo kutoka Saudi Arabia na Qutar waliokuwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakifanya matibabu ya moyo, haflaa hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa Taasisi yake ndio kiungo cha kuunanisha taasisi zilizoshiriki kuokoa maisha ya watoto wenye matatizo ya moyo.
   Katibu mkuu na mkurugenzi wa Muntada Aid, Sheikh Khalid Sukeir akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari bingwa wa matatizo ya Moyo jijini Dar es Salaam leo.
   Kiongozi wa Madaktari, Jamil Al Ataa akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari bingwa wa matatizo ya Moyo jijini Dar es Salaam leo.
   Mwakilishi wa Balozi wa Qatar, Wajih Al Uteibly akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari bingwa wa matatizo ya Moyo jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri akimkabidhi zawadi ya ngao   Kiongozi wa Madaktari, Jamil Al Ataa wakati wa hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.

  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi akikabidhiwa zawadi katika  hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri.  Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala akikabidhiwa zawadi wakati wa hafla ya kufunga kambi ya Madaktari wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation, Said Abri.


    

   Picha ya pamoja ya madaktari bingwa wa matatizo ya moyo kutoka taasisi nne tofauti za nchi tatu.
  Daktari bingwa wa kufanya oparesheni ya BAY PASS kwa watu wenye matatizo ya moyo(Jina lake halijpatikana mara moja)

  0 0


  0 0

  Hamisi Maduka Kaimu mwenyekiti wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alisistiza ulipaji wa fidia za Ardhi uzingatie uhalisia wa thamani ya eneo husika.Abdallah Moto mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake kwa Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 kuhusu suala la kupewa kipaumbele utoaji wa hati miliki kwa wanavijiji.Shakira Masudi mkazi wa Kijiji cha Kigwa B wilaya ya Uyuwi Mkoani Tabora akitoa maoni yake mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ambaye alitaka Sera itambue wamiliki wa Ardhi wa maeneo wa muda mrefu katika kutoa Hati.Mwl. Hadija Nyembo mkuu wa wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora.Hanifa Selengu Mkuu wa wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kukusanya Maoni ya kuboresha Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 wakati akitoa maoni yake kuhusu Umiliki wa Ardhi mkoani Tabora. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Ardhi.
   
  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la ukusanyaji wa maoni na kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kuiboresha. Zoezi hilo limeanza Mwaka huu wa 2016 ambapo linashirikisha kanda nane za Ardhi ambazo ni Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kusini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini.

  Na kwa sasa kamati maalumu ya kukusanya maoni ipo mkoani Tabora ikikusanya maoni ya wananchi na wadau mbalimbali wa sekta ya Ardhi ili kupata sera iliyoridhiwa na wengi.

  Katika sekta ya Ardhi Serikali ya Tanzania imekuwa ikitekeleza Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 kwa takribani miaka 20 hadi sasa, hata hivyo zimejitokeza changamoto nyingi ambazo zinalazimu kufanya mapitio ya sera hiyo.

  Migogoro na malalamiko yanayotokana na ardhi ni changamoto zinazo chukua nafasi kubwa katika jamii yetu na imekuwa ikiigharimu kwa kiasi kikubwa katika kuitatua.

  Kuongezeka kwa migogoro hii imekuwa ni changamoto zinazoikabili sekta ya ardhi pamoja na watumiaji mbalimbali wa ardhi hususan wakulima na wafugaji, wawekezaji, wananchi, vijiji na hifadhi.

  Hata hivyo, kuongezeka kwa mahitaji ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji hususan katika sekta za kilimo, madini, viwanda na wananchi kutonufaika na uwekezaji unaofanywa katika ardhi na hivyo kusababisha migogoro baina ya wananchi na wawekezaji.

  Aidha kutokuwepo kwa mipango ya matumizi endelevu ya ardhi mijini na vijijini na hata sekta ya ardhi kuvamiwa na madalali ni changamoto iliyoifanya Serikali kuamua kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995.

  Changamoto zote kwa pamoja, zimelazimika kufanyika kwa mapitio ya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kutoa mwelekeo mpya na usimamizi wa ardhi kwa manufaa ya watanzania wote.

  Ardhi ni Sekta mama na hivyo basi Sera ya ardhi ni sera mama katika masuala yote ya maendeleo ikiwemo kilimo na mifugo, ambayo shughuli zake zinafanyika kwenye ardhi.

  Na sasa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la ukusanyaji wa maoni na kuipitia upya Sera ya Taifa ya Ardhi ya 1995 ili kuiboresha. Zoezi hilo limeanza Mwaka huu wa 2016 ambapo linashirikisha kanda nane za Ardhi ambazo ni Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Kusini, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia ngoma alipowasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM mjini Dodoma leo Mei 7,2016 kwa ajili ya kufungua mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa.
  Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wenye lengo la kukumbushana katika majukumu ya kiutendaji kwenye ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi hiyo Kuu ya kitaifa. Mkutano huo umefunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini.
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la UWT Taifa wakimkabidhi zawadi za aina mbalimbali Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi Kuu ya kitaifa wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa uliofunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wenye lengo la kukumbushana katika majukumu ya kiutendaji kwenye ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi hiyo Kuu ya kitaifa. Mkutano huo umefunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
  Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wenye lengo la kukumbushana katika majukumu ya kiutendaji kwenye ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi hiyo Kuu ya kitaifa. Mkutano huo umefunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma. 
  Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa wenye lengo la kukumbushana katika majukumu ya kiutendaji kwenye ngazi mbalimbali za Jumuiya hiyo pamoja na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi hiyo Kuu ya kitaifa. Mkutano huo umefunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma. 
  Mjumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la UWT Taifa Mama Lupembe akisalimiana na kumpongeza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa Mwanamke wa kwanza katika Ngazi Kuu ya kitaifa wakati wa Mkutano Mkuu wa UWT Taifa uliofunguliwa leo Mei 7,2016 katika ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mjini Dodoma.
  Makamu wa Raisv wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Mhe. Adam Kimbisa kabla ya kufungua Semina ya Mafunzo kwa ajili ya kuwajengea Uwezo Viongozi na Mkada wa Chma cha Mapinduzi iliyofunguliwa leo Mei 7,2016 katika Ukumbi wa MORENA Mjini Dodoma. (Picha na OMR)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Semina ya Mafunzo kwa ajili ya kuwajengea Uwezo Viongozi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM iliyofunguliwa leo Mei 7,2016 katika ukumbi wa MORENA Mjini Dodoma.akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa bkatika picha ya pamoja na Viongozi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM baada ya kufungua Semina ya Mafunzo kwa ajili ya kuwajengea Uwezo Viongozi na Makada wa Chama cha Mapinduzi CCM iliyofunguliwa leo Mei 7,2016 katika ukumbi wa MORENA Mjini Dodoma.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu), Dk Abdallah Possi (kulia), akiwasilisha mada katika semina ya Wabunge kukuza na kuimarisha usawa wa watu wenye ulemavu nchini, kwenye Ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma jana. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bukene, Seleman Zedi (CCM) na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
  Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akifungua semina hiyo
  Baadhi ya wabunge wakihudhuria kwenye semina hiyo

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Afisa Mpya wa cheo cha Luteni Usu, Nasra Rashid ambaye alifanya vizuri zaidi kuliko Maafisa Wanafunzi wanawake katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya wananchi General Davis Mwamunyange mara baada ya kuwasili kwenye chuo cha Mafunzo Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
  Maafisa Wanafunzi wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kutuniwa Kamisheni
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA Meja Jenerali Paul Peter Massao kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 katika chuo hicho cha Monduli.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wapya aliowatunuku Kamisheni katika cha Mafunzo Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya wananchi Jeneral Davis Mwamunyange , Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA Meja Jenerali Paul Peter Massao, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Maafisa wa ngazi za juu katika Jeshi la Ulinzi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Ngarenaro waliomsimamisha wakati akitokea kwenye chuo cha Mafunzo ya Kijenshi cha Monduli mkoani Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitembea kikakamavu mara baada ya kutoka kukagua gwaride katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanaanchi wa kona ya Mbauda mkoani Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mara baada ya kutazama picha za Majenerali wastaafu waliongoza Jeshi la Wananchi katika miaka ya nyuma.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mara baada ya kutazama picha za Majenerali wastaafu waliongoza Jeshi la Wananchi katika miaka ya nyuma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Kona ya Nairobi eneo la Arusha Tech mara baada ya kutoka kutunuku Kamisheni kwa maafisa Wapya katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mkoani Arusha. PICHA NA IKULU

older | 1 | .... | 840 | 841 | (Page 842) | 843 | 844 | .... | 1904 | newer