Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

NJIA YA KIELETRONIKI YAANZA KUTUMIKA KUKUSANYA ADA ZA USAJILI.

$
0
0
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.
SERIKALI inaendelea kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ili kuchangia upatikanaji wa fedha za kusaidia kuimarisha na kuendeleza miradi ya maendeleo nchini. 

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imekuwa miongoni mwa taasisi za Serikali ambayo imeanza kukusanya ada zote zitokanazo na huduma inazotoa kwa njia ya kielekroniki kwa wadau wake kufanya malipo kwa njia ya simu au benki kabala ya kupata huduma wanayohitaji.

Hayo yamebainishwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harisson Mwakyembe alipokuwa akiwasilisha mpango wa makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

“Tayari wilaya 114 kati ya 139 zinakusanya maduhuli kwa njia ya kielekroniki na kwamba ifikapo Juni, 2016 wilaya zote Tanzania Bara zitakuwa zinatumia njia ya kielekroniki kukusanya maduhuli” alisema Dkt. Mwakyembe.

Katika kuongeza mapato, Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa upo mkakati wa kuongeza kiwango cha usajili wa vizazi na vifo nchini, ambapo RITA imeanzisha kampeni ya usajili inayoambatana na uboreshaji wa mfumo wa usajili kwa kuweka mfumo wa kompyuta kila wilaya ambapo kampeni hizo zilifanyika.

Wilaya ambazo kampeni hizo zimefanyika ni Arusha na Arumeru ambapo jumla ya watu 49,548 wamesajiliwa na kupewa vyeti vyao vya kuzaliwa.

Zoezi hilo la usajili linaendelea katika wilaya ya Kahama na baadaye litaendelea katika wilaya 16 nchini ambazo ni Bariadi, Chato, Dodoma, Igunga, Kilombero, Kilosa, Lushoto, Maswa, Mbinga, Misungwi, Mtwara, Muleba, Nzega, Shinyanga, Sumbawanga na Tunduru.

Waziri Mwakyembe alibainisha kuwa Wizara hiyo kupitia RITA imekusudia kusajili zaidi ya watu 500,000 katika maeneo hayo na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.

Kwa mujibu wa utafiti wa afya uliofanyika 2010, asilimia 16 ya watoto wenye umri wa miaka mitano ndio wenye usajili na vyeti vya kuzaliwa Tanzania Bara ikilinganishwa na Tanzania Zanzibar ambapo usajili ulikuwa ni asilimia 79.

Ili kukabiliana na hali hiyo, RITA kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) wamebaini mradi wa kusajili watoto chini ya umri wa miaka mitano uliofanyiwa majaribio wilaya ya Temeke mwaka 2012 na kuzinduliwa rasmi mwaka 2014 mkoani Mbeya.

Kampeni hiyo imeonesha mafanikio na tija kwa taifa ambapo usajili umeongezeka na kufikia asilimia 58 ambapo awali mkoa wa Mbeya usajili ulikuwa asilimia 8.7.

Kampeni hiyo ni endelevu kwa nchi nzima ambapo mikoa itakayoanza kufanya usajili ni Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Iringa, Njombe, Tabora, Kagera na Dodoma.

CCM YAKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA KWA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI KUKUHUS KUKABIDHIANA KIJITI CHA UENYEKITI.

$
0
0


 Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinatoa taarifa potofu kuhusu mchakato wa Mwenyekiti wa sasa wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti cha uongozi wa CCM kwa Rais John Pombe Magufuli kama ilivyo mila na desturi ya Chama Cha Mapinduzi. Yamekuwepo madai eti Mwenyekiti amekataa au anachelewesha kukabidhi kijiti.


Habari hiyo sio kweli kabisa na ni kinyume chake, kwani Dkt. Kikwete amekuwa akisisitiza kukabidhi madaraka mapema iwezekanavyo. Kwa ajili hiyo kwenye kikao cha Mei 3, 2016 alikataa kusiongezwe agenda nyingine ambazo zitalazimisha Mkutano Mkuu Maalum kuchelewa kufanyika kwa sababu ya kukamilisha maandalizi ya agenda hizo. Alisisitiza agenda iwe moja tu.

Dhamira ya kufanyika Mkutano Mkuu maalum mwezi Juni, 2016 iko pale pale. Kilichoelezwa kwenye kikao ni kutaka kukamilisha utaratibu wa kupata fedha za kugharamia mkutano huo. Taratibu zikikamilika tarehe itapangwa. Mipango ya kutafuta pesa inaendelea na ikikamilika tarehe itatangazwa.

Tunawataka wana-CCM wasihamanike wala kubabaishwa na taarifa za upotoshaji zinazofanywa na watu wenye nia mbaya na CCM. Hawa ni wale wale ambao wamekuwa wakiiombea mabaya CCM bila ya mafanikio.

Pia tunapenda kukanusha madai ati kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwatahadharisha Wajumbe wa Kamati Kuu kuhusu ukimya wa Ndugu Edward Lowassa. Hakuna wakati wowote kauli kama hiyo aliitoa. Ni uzushi mtupu. Jina la Ndugu Lowassa halikutajwa kabisa.

Aidha, tunapenda kukanusha madai ya kufanyika mkutano baina ya Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa CCM kuhusu uchaguzi wa Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM. Hapajawahi kufanyika mkutano wa aina hiyo siku yoyote na mahali popote. Hivyo madai ya kuwepo kwa tofauti baina ya Viongozi wakuu kuhusu nani achaguliwe kuwa Katibu wa Wabunge wa CCM hayana msingi wowote. 

Kamati Kuu iliteua Wabunge wanne kugombea na kuwaachia Wabunge wa CCM kuamua. Kuhusisha Viongozi na hasa kuzua kuwepo kutokuelewana ni jambo la kusikitisha. Ni taarifa ya uongo yenye nia ovu kwa CCM na Viongozi wake.

Tunapenda kuwatahadharisha waandishi wa habari kuandika habari za ukweli. Waache kuzua mambo yenye kupandikiza chuki na mgawanyiko usiostahili kuwepo ndani ya CCM na kuyaeneza kwa watu. Waheshimu maadili ya kazi zao.

Napenda kuwahakikishia na kusisitiza kuwa hakuna mgogoro wa kukabidhi kijiti cha uenyekiti katika CCM na wala hautakuwepo.


Imetolewa na;
  
Ndugu Christopher Ole Sendeka   
                  MSEMAJI WA CCM                  
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,




05/05/2016

RITA yaanza kukusanya ada za Usajili kwa njia ya kielekroniki.

$
0
0
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.

Serikali inaendelea kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ili kuchangia upatikanaji wa fedha za kusaidia kuimarisha na kuendeleza miradi ya maendeleo nchini. 

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imekuwa miongoni mwa taasisi za Serikali ambayo imeanza kukusanya ada zote zitokanazo na huduma inazotoa kwa njia ya kielekroniki kwa wadau wake kufanya malipo kwa njia ya simu au benki kabala ya kupata huduma wanayohitaji.

Hayo yamebainishwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harisson Mwakyembe alipokuwa akiwasilisha mpango wa makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

“Tayari wilaya 114 kati ya 139 zinakusanya maduhuli kwa njia ya kielekroniki na kwamba ifikapo Juni, 2016 wilaya zote Tanzania Bara zitakuwa zinatumia njia ya kielekroniki kukusanya maduhuli” alisema Dkt. Mwakyembe.

Katika kuongeza mapato, Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa upo mkakati wa kuongeza kiwango cha usajili wa vizazi na vifo nchini, ambapo RITA imeanzisha kampeni ya usajili inayoambatana na uboreshaji wa mfumo wa usajili kwa kuweka mfumo wa kompyuta kila wilaya ambapo kampeni hizo zilifanyika.

Wilaya ambazo kampeni hizo zimefanyika ni Arusha na Arumeru ambapo jumla ya watu 49,548 wamesajiliwa na kupewa vyeti vyao vya kuzaliwa.

Zoezi hilo la usajili linaendelea katika wilaya ya Kahama na baadaye litaendelea katika wilaya 16 nchini ambazo ni Bariadi, Chato, Dodoma, Igunga, Kilombero, Kilosa, Lushoto, Maswa, Mbinga, Misungwi, Mtwara, Muleba, Nzega, Shinyanga, Sumbawanga na Tunduru.

Waziri Mwakyembe alibainisha kuwa Wizara hiyo kupitia RITA imekusudia kusajili zaidi ya watu 500,000 katika maeneo hayo na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa.

Kwa mujibu wa utafiti wa afya uliofanyika 2010, asilimia 16 ya watoto wenye umri wa miaka mitano ndio wenye usajili na vyeti vya kuzaliwa Tanzania Bara ikilinganishwa na Tanzania Zanzibar ambapo usajili ulikuwa ni asilimia 79.

Ili kukabiliana na hali hiyo, RITA kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) wamebaini mradi wa kusajili watoto chini ya umri wa miaka mitano uliofanyiwa majaribio wilaya ya Temeke mwaka 2012 na kuzinduliwa rasmi mwaka 2014 mkoani Mbeya.

Kampeni hiyo imeonesha mafanikio na tija kwa taifa ambapo usajili umeongezeka na kufikia asilimia 58 ambapo awali mkoa wa Mbeya usajili ulikuwa asilimia 8.7.

Kampeni hiyo ni endelevu kwa nchi nzima ambapo mikoa itakayoanza kufanya usajili ni Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Iringa, Njombe, Tabora, Kagera na Dodoma.

MAJALIWA:WANAVYUO WAFUATE TARATIBU NA SHERIA ZILIZOPO VYUONI

$
0
0
SERIKALI imekanusha madai ya kutoa maelekezo kwa Uongozi wa vyuo vya elimu ya juu ya kuwanyanyasa wanafunzi wa vyuo hivyo wanaojihusisha na masuala ya siasa na badala yake imewataka wafuate kanuni na taratibu zilizowekwa sehemu husika.

Hata hivyo imesema itaendelea kuwahudumia Watanzania wote ikiwemo kutoa elimu kuanzia ngazi awali hadi elimu ya juu bila kujali ya itikadi za dini wala vyama vyao vya siasa.Waziri Mkuu,Kassm Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 5, 2016) wakati akijibu swali la papo kwa papo la Mheshimiwa Ester Matiko (Viti maalum Chadema) aliyetaka kujua kama Serikali imetoa maelekezo kwa uongozi wa vyuo vikuu kunyanyasa wanafunzi wanaojihusisha na masuala ya siasa.

“Nakanusha si kweli kwamba kuna maelekezo kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu na pia hakuna unyanyasaji wowote wa vyuo na Watanzania wote wanao uhuru wa kujiunga na vyama vyote wanavyovitaka, lakini kila eneo limeweka utaratibu wake hivyo wafuate taratibu na sheria katika sehemu husika,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imeondoa tozo ya asilimia 15 ya eneo la manunuzi ya vifungashio katika zao la korosho ili kumfanya mkulima kupata tija zaidi.Akijibu swali la papo kwa papo la Mheshimiwa Katani Katani (Tandahimba-CUF) aliyetaka kujua ni lini tozo hiyo itaondolewa, Waziri Mkuu Majaliwa amesema tayari tozo hiyo imeshaondolewa na gharama hizo kwa sasa zipo katika mfuko wa wakfu ulioundwa na wadau wa zao hilo na unachangiwa na asilimia 65 ya tozo za korosho zinazouzwa nje.

Amesema mfuko huo wa wakfu unatakiwa kusimamia upatikanaji wa masoko ya zao la korosho, kununua pembejeo, kusimamia uboreshaji na upanuzi wa mashamba na kugharamia tatifi mbalimbali kwa ajili ya kupata ubora wa zao hilo.Akijibu kuhusu suala la madai ya wakulima ambao korosho zao zimepotea ghallani, amesema mfumo wa uuzwaji wa zao hilo wa stakabadhi ghalani ni wa kiushirika na unasimamiwa na Mrajisi ni vema wakulima wakadai haki yao katika mikutano ya ushirika wao na kama hawaridhiki na majibu waende mahakamani ili kupata haki yao.

Amesema kwa sasa Serikali itahamishia nguvu zake katika kusimamia mazao mengine ya pamba, tumbaku na kahawa kama walivyofanya kwenye zao la korosho ili wakulima wa mazao hayo nao wapate tija.

Akijibu swali la Mheshimiwa Joseph Kekunda (Sikonge-CCM) aliyetaka kujua Serikali inampango gani wa kutatua migogoro ya wakulima na wakulima ,Waziri Mkuu amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha inakomesha migogoro hiyo ambazo ni pamoja na kupima maeneo na kuweka mipango bora ya matumizi ya ardhi.

Pia kuweka mipaka katika maeneo mapya na kutumia ranchi zilizopo kwa ajili ya wafugaji wakubwa na kwamba itatenga maeneo ya kilimo na kuyabainisha kwa wananchi ili kuepuka muingiliano uliopo hivi sasa.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
05 Mei, 2016.

MUFTI,AFUNGUA SEMINA ELEKEZI YA VIONGOZI WA BAKWATA

$
0
0
Shekhe Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar bin Zuberi akizungumza viongozi wakati wa ufunguzi wa semina elekezi ya viongozi wa Bakwata katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
Shekhe wa Mkoa s Dar es Salaam,Alhaji Mussa Salum akitoa neno wakati wa kumkaribisha , Shekhe Mkuu wa Tanzania ,Mufti Abbakari Ally Bin Zuberi katika semina elekezi ya viongozi wa Bakwata iliyofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya viongozi wa Bakwata wakimskiliza Shekhe Mkuu wa Tanzania , Mufti Abbakari Ally Bin Zuberi (hayupo pichani) wakati wa semina elekezi ya viongozi wa Bakwata iliyofanyika katika ukumbi wa Karimjee ,jijini Dar es Salaam.(picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)

BENKI ya Rasilimali nchini (TIB) yatangaza mikopo yenye masharti nafuu kwa wakandarasi wazawa.

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa TIB Corporate Bahati Minja (aliyesimama) akitoa ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na TIB Corporate Bank.

TIB Corporate Bank imesema imekusudia kuwawezesha kifedha wakandarasi wa ndani ili waweze kutekeleza vema majukumu yao ya kikandarasi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB) uliofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Mikopo wa Benki ya TIB, Theresia Soka amesema benki yake imekuja na suluhisho la kutatua changamoto za wakandarasi wazawa.

TIB Corporate Bank imemua kurahisisha taratibu zake za kutoa mikopo kwa wakandarasi wa ndani kwa kuwataka kuwasilisha vielelezo tu vinavyomtambulisha kuwa amesajiliwa kisheria ili aweze kupata mkopo. ‘Tumeamua kurahisisha utaratibu wetu wa utoaji mikopo ili kuwawezesha wakandarasi na hivyo kuchangia ukuaji wa maendeleo nchini katika sekta hii muhimu ya ujenzi’ alisema Bi Soka.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa TIB Corporate Bahati Minja, alisema benki hiyo inayomilikiwa na Serikali, imeboresha huduma zake za kibenki ili kuwawezesha wakandarasi wazawa. ‘Lengo kubwa la Benki ya TIB Corporate ni kuhakikisha wakandarasi wanawezeshwa kifedha ili wawe na vitendeakazi vya ujezi’ alisema Bi Soka.

Hata hivyo wakandarasi waliohudhuria mkutano huo ambao miongoni mwao wamefadhiliwa na benki hiyo, waliupongeza uongozi wa Benki ya TIB Corporate kwa kuamua kuwawezesha kwa mikopo ya kikandarasi. Wakandarasi hao walisema uwezeshwaji huo wa mikopo nafuu inayotolewa na benki hiyo, itawasaidia kuendesha kampuni zao za ujenzi kwa ufanisi zaidi.

Mkutano huo wawakandarasi wenye kauli mbiu ya ‘Kuwajengea Uwezo Wakandarasi wa Ndani kwa ajili ya Uchumi Endelevu', utafuatiwa na mkutano mwingine utakaofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Daimond Jubilee kuanzia tarehe 26 hadi 27 mwezi huu wa tano.

TIB Corporate Bank imefanya mabadiliko ya kitaasisi ili kuweza kuwa kituo cha huduma zote za kibenki kwa kushughulikia mahitaji ya wawekezaji wa ndani kwa lengo la kusukuma maendeleo ya 
Uchumi Endelevu: Changamoto na Mipango ya baadae’.

Menejimenti ya NHC yatembelea miradi yake jijini Dar es salaam

$
0
0
Meneja Mradi wa Shirika l nyumba la Taifa NHC Kawe unaokwenda kwa jina la 711 Injinia Samwel Metil akitoa maelezo kwa Timu ya Menejimenti ya NHC wote(Directors, Regional Managers & Line Managers) wakati walipotembelea miradi ya 711 Kawe , Morocco Square, Victoria Place, Eco Residence na Kibada ambapo ambapo pia watafanya pia kazi katiia miradi hiyo Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kuwafahamisha juu ya maendeleo na changamoto za miradi hiyo. 
Mmoja wa Mainjinia wa Mradi wa 711 Kawe Bw.Kishor Hirani akimelezea jambo Meneja mradi Injinia Samwel Metil wakati menejimenti ya shirika hilo ilipotembelea katika mradi huo.
Wakuu wa vitengo mbalimbali na mameneja wa mikoa wakitembelea mradi wa 711 Kawe leo.
Mmoja wa Mameneja wa NHC kutoka mkoani Dodoma Bw. Itandula Gambalagi pamoja na wenzake wakiwasili kutembelea mradi wa Morocco Square.
Wakipatiwa maelezo katika mradi wa Morocco SquareMorocco Square.
Mameneja hao wakifuatilia maelezo ya mradi wa Morocco Square.
Muungano Saguya kulia Yahya Charahani kushoti na Itandula Gambalagi wakijadiliana jambo wakati walipotembelea mradi wa 711 Kawe pamoja na wenzao.
Jengo la Mradi wa Eco Residents ambalo limekamilika kwa asilimia 99%.

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMUAPISHA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza huku Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Augustine Mahiga wakisikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kutoka kwenye tukio la kumuapisha Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi mpya nchini Uingereza . PICHA NA IKULU. 





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Hafla ya kuapishwa kwa Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro imefanyika leo tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kallaghe ambaye amerudishwa nyumbani.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Dkt. Migiro ameahidi utumishi uliotukuka na kwamba atahakikisha uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Uingereza unaimarishwa zaidi, hususani katika kuvutia uwekezaji, biashara na utalii baina ya nchi hizi mbili.

Dkt. Migiro pia ametoa wito kwa watanzania waliopo hapa nchini na waishio Uingereza kuitumia ofisi hiyo ya ubalozi ipasavyo, ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali hasa za kiuchumi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
05 Mei, 2016

SHIRIKA LA NDEGE LA NCHINI MAURITIUS LAZINDUA SAFARI ZA NDEGE ZA MAURITIUS KUJA DAR ES SALAAM.

$
0
0
Mwenyekiti wa shirika la ndege la nchini Mauritius, Dr. Arjoon Suddhoo akizunumza katika uzinduzi wa safari za shirika la ndege la nchini Mauritius jijini Dar es Salaam leoikiwa na lengo la kuunganisha ushirikiano kati ya nchi za bara la Afrika hasa Tanzania na Nchi ya Mauritius.Safari hizo ni za kutoka nchini Mauritius kuja Dar es Salaam na Dar es Salaam kwenda nchini Mauritius.
Makamu mkuu wa rais wa shirika la ndege la nchini Mauritius, Dornald Payen(katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kabla ya kuzindua safari za ndege za shirika la ndee la nchini Mauritius, kushoto ni Mwenyekiti wa shirika la ndege la nchini Mauritius, Dr. Arjoon Suddhoo na kulia ni Mrs Kan oye Long akiwa katika mkutano wa waandishi wa habari.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora akizungumza katika uzinduzi wa Safari za ndege za shirika la ndege la nchini Mauritius jijini Dar es Salaam leo. shirika hilo limezindua safari za ndege za kutoka nchini Mauritius kwenda jijini Dar es Salaam na kutoka jijini Dar es Salaam kwenda nchini Mauritius ndege hizo zitaanza safari zake kesho.

Mwenyekiti wa shirika la ndege la nchini Mauritius, Dr. Arjoon Suddhoo (wa nane katikati)Picha ya Pamoja na viongozi wa shirika la ndege la nchini Mauritius jijini Dar es Salaam leo.

  Viongozi wa shirika la ndege la nchini Mauritius wakifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mshehereshaji wa uzinduzi wa safari za ndege za shirika la ndege la nchini Mauritius ,Evance Bukuku akizungumza leo katika uzinduzi wa safari za ndege za shirika hilo jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa shirika la ndege la nchini Mauritius, Dr. Arjoon Suddhoo akimkabidhi zawadi mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora leo katika uzinduzi wa safari za ndege za shirikal la ndege la nchini Mauritius katika ukumbi wa Maqee katika hoteli ya Hyatt Rgency jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa shirika la ndege la nchini Mauritius, Dr. Arjoon Suddhoo akimkabidhi sanamu ya ndege ya shirika la ndege la nchini Mauritius Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora jijini Dar es Salaam leo katika uzinduzi wa safari za ndege za shirika hilo za kutoka nchini Mauritius kuja Dar es Salaam na Dar es Salaam kwenda nchini Mauritius.
Mwenyekiti wa shirika la ndege la nchini Mauritius, Dr. Arjoon Suddhoo akigonganisha glass na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora katika uzinduzi wa safari za shirika la ndege la nchini Mauritius jijini Dar es Salaam leo. 
Shamlashamla za uzinduzi wa safari za shirika la ndege la nchini Mauritius jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuzinduasafari za ndege za shirika hilo za kutoka nchini Mauritius kuja Dar es Salaam na Dar es Salaam kwenda nchini Mauritius.
Baadhi ya wadau wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa uzinduzi wa safari za ndege za shirika hilo za kutoka nchini Mauritius kuja Dar es Salaam na Dar es Salaam kwenda nchini Mauritius.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA ALEX MSAMA MKURUGENZI WA MSAMA PROMOTION

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza jambo na  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama  kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma May 5, 2016. pichani kati ni Mbunge wa Urambo, Magreth Sitta .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma May 5, 2016. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO MEI 6

MKUTANO WA WAZIRI UMMY MWALIMU ALIPOHUDHURIA MKUTANO WA VIONGOZI WANAWAKE KUHUS MASUALA YA AFYA

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Wajumbe wa Mkutano wa Viongozi Wanawake katika masuala ya Afya katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam 5 Mei, 2016.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar Hebogard Jensen akiongea na Wajumbe wa Mkutano wa Viongozi Wanawake katika masuala ya Afya katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam, 5 Mei, 2016.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar Hebogard Jensen akiongea na Wajumbe wa Mkutano wa Viongozi Wanawake katika masuala ya Afya katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam, 5 Mei, 2016.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) pamoja na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Einar Hebogard Jensen wakifurahia burudai toka kwa Vijana wakiotumbuiza stejini (hawapo pichani) wkaati wa Mkutano wa Viongozi Wanawake katika masuala ya Afya uliofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam 5 Mei, 2016.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.


Na Jonas Kamaleki- MAELEZO.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakusudia kutoa taarifa ya wanawake wanaofariki Dunia kutokana na matatizo ya uzazi kila baada ya miezi mitatu ili kukabiliana na tatizo la vifo vya wanawake nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Viongozi Wanawake katika masuala ya Afya.

“Nimeamua kuhakikisha wanawake wanapiga hatua na kuthaminiwa katika jamii, na nimeamua kuanza kutoa ripoti ya robo mwaka kwa kila Halmashauri kuhusu taarifa ya wanawake wanaofariki kutokana na matatizo ya uzazi,” alisema Ummy Mwalimu.

Ameeleza kuwa, katika uteuzi atakaoufanya kwenye bodi zilizo chini ya Wizara yake, atahakikisha asilimia 30 ya wajumbe wa bodi hizo ni wanawake. Baadhi ya Bodi zilizo chini ya Wizara yake ni pamoja MSD, TFDA na Bodi ya Wafamasia.

Aidha, Mhe. Ummy amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza sera ya elimu bure ambapo amesema wazazi watalazimika kuwapeleka watoto wa kike shuleni kwa wingi kuliko ilivyokuwa awali.

Katika kutilia mkazo suala la elimu kwa wasichana, Waziri Ummy amasema watoto wa kike hawana budi kujitambua na kuzingatia masomo ambayo ndiyo yatawafanya waweze kuchagulika au kuteuliwa kushika nyadhifa kubwa za uongozi. “Hamsini kwa Hamsini bila elimu ni siasa tu” alisisitiza Mhe. Waziri.

Mhe. Ummy amewataka wanawake kujituma katika kufanya kazi ili kuibadilisha jamii. Hapa akaja na kauli mbiu kuwa “Mwanamke akitenda, jamii itatenda, Tanzania Itasonga mbele’’.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Bibi Fatuma Mrisho amewasisitiza watoto wa kike kuthamini masomo na kuepuka ndoa za utotoni. Amesema kuwa mtoto anapokuwa shuleni anaepuka Ukimwi kwa asilimia saba. Hivyo amesema ni lazima wasichana kupenda shule na kuacha kurubuniwa na wavulana.

Huu ni mkutano wa utangulizi kabla ya mkutano Mkubwa wa karne kuhusu Afya, Haki na Ustawi wa Wasichana na wanawake ambao wajumbe zaidi ya 5,000 wakiwemo viongozi wa Dunia, Wasomi, Watunga sera, Wanaharakati, Watu wa habari, dini, Vyama vya kijamii na Wawakilishi wa sekta binafsi watashirik

MAMIA WAMZIKA ANDREW NICKY SANGA (KING DREW) DODOMA

$
0
0
Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga Enzi za Uhai wake .
Marafiki wa Andrew Nicky Sanga wakiwa katika Picha ya Pamoja baada ya Mazishi
.


Ibada ikiwa inaanza Baada ya Mwili wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga kuwasili

Familia,Ndugu wa karibu, pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Serikali wakiwa katika ibada ya kumsindikiza Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga.
 

Jarida La Ofisi Ya Taifa Ya Takwimu

JARIDA LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI TOLEO NA. 118


WAFANYAKAZI WA BENKI YA EXIM WASHIRIKI KAMPENI YA USAFI DAR

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania wakishiriki usafi wa mazingira kuunga mkono kampeni ya siku 90 ya usafi iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw Paul Makonda jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kampeni hiyo inalenga kutoa elimu kwa wakazi wa jiji hilo kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira ili kukabiliana na milipuko ya magonjwa.



BRITAM YAZINDUA HUDUMA ZAO NCHINI TANZANIA IKIWA NI HATUA YA KUIMARISHA UWEPO KWENYE KANDA YA AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0
  Mkurugenzi Mkuu wa Britam Tanzania Bw. Stephen Lokonyo (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Biashara ya Bima Britam group Bw. Steven Wandera muda mfupi baada ya mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa shughuli za kampuni hiyo ya Bima hapa nchini, uzinduzi uliofanyika juzi Hyatt Regency hotel jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi wa Biashara za Kimataifa Britam group Bw. Kennedy Aosa (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Mauzo wa Britam Tanzania, Bw. Godfrey Mzee (kushoto) na Afisa Mkuu Uendeshaji Britam Tanzania Bw. Sodson Manatsa (katikati) muda mfupi mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa shughuli za kampuni hiyo hapa nchini. Uzinduzi huo uliofanyika juzi Hyatt Regency hotel jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Biashara ya Bima Britam group Bw. Steven Wandera (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa shughuli za kampuni ya Bima ya Britam Tanzania nchini. Uzinduzi wa kampuni hiyo ulifanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam juzi. (Kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Tanzania Bw. Stephen Lokonyo.

 Meneja Mauzo wa Britam Tanzania, Bw. Godfrey Mzee (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa shughuli za kampuni ya Britam Tanzania hapa nchini ikiwa ni moja ya juhudi zinazofanywa na Britam group kujipanua kikanda.Mkutano huo ulifanyika juzi katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. (Kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Tanzania Bw. Stephen Lokonyo .
 Mkurugenzi wa Biashara za Kimataifa Britam Group Bw. Kennedy Aosa (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampuni ya Britam Tanzania hapa ncnini ambayo inayojishughulisha na masuala ya bima. Katika upanuzi wa soko lake Britam Group imeingia rasmi katika soko la Tanzania ambapo uzinduzi ulifanyika juzi katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi huyo aliwahakikishia watanzania kuwa lengo la Britam ni kuhakikisha kuwa inabadilisha biashara ya bima hapa nchini na kuwa chaguo la watanzania.
 Mgeni rasmi Jaji (mstaafu) Joseph Sinde Warioba akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Group Dk. Benson Wairegi muda mfupi baada ya mheshimiwa huyo kuzindua rasmi Kampuni ya Britam Tanzania inayojishughulisha na masuala ya bima katika soko la Tanzania, uzinduzi huo ulifanyika juzi katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Jaji (mstaafu) Joseph Sinde Warioba (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Group Dk. Benson Wairegi (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo nchini Tanzania Bw. Steven Lukonyo (kushoto) muda mfupi baada ya mheshimiwa huyo kuzindua rasmi Kampuni ya Britam Tanzania inayojishughulisha na masuala ya bima katika soko la Tanzania, uzinduzi huo ulifanyika juzi katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

SHIRKA la Britam Holdings linaloongoza katika huduma za kifedha limefanikiwa kuzindua huduma zake nchini Tanzania baada ya kukamilisha mchakato wa kuunganisha kampuni ya Real Insurance pamoja na shirika la Britam lililopo nchini Kenya.   

Uzinduzi rasmi wa shirika la bima la Britam Tanzania ni moja wapo ya mkakati wa shirika mama la Britam kukuza biashara yake ya bima na kuimarisha uwepo wake katika kanda za kusini na Mashariki mwa Afrika wakilenga makundi ya watu wasio na bima.

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha usajili wa bima Tanzania ni chini ya asilimia moja la pato la taifa, kiashirio cha chini sana ukilinganisha na mataifa yaliyoendelea pamoja na mataifa mengine ya Afrika. Britam inatazamia kupunguza pengo hilo kwa kuleta huduma za bima za kipekee zenye ufumbuzi wa mahitaji ya watanzania.

Britam ni shirika lenye kutoa huduma mbalimbali za kifedha na limesajiliwa nkwenye soko la hisa mjini Nairobi. Shirika lina maslahi kanda nzima ya masharika na kusini mwa Afrika, likitoa huduma zake nchini Kenya, Uganda, Sudan ya Kusini, Mozambique na Malawi. Shirika linatoa huduma mbali mbali za kifedha zikiwemo bima, benki pamoja utunzaji mali.  

Akiongea jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Britam Dk. Benson Wairegi alisema kampuni hiyo itatumia uzoefu wake wa miaka 50 katika masuala ya kifedha, jina lake lina nguvu na kuaminika ndani ya nchi saba barani Afrika, nguvu kazi  kubwa ya waajiriwa wake pamoja na mfumo wake thabiti wa teknolojia.

“Uzinduzi wa Britam nchini Tanzania ni kiashirio cha hatua muhimu iliyopigwa na shirika katika mkakati wake wa kukuza bidhaa na huduma za bima katika soko. Ndani ya Britam kuna huduma na bidhaa nyingi za kifedha katika masuala ya bima, usimamizi wa mali pamoja na benki. Wateja wetu nchini wataweza kupata huduma hizo zote chini ya paa moja” alisema Dk. Wairegi.

Dk. Wairegi alidokeza pia jinsi Britam ni chapa inayoheshimika sana nchini Kenya, likiwa linaendesha shughuli zake kwa miaka zaidi ya 40, shirika limekuwa mstari wa mbele katika huduma wanazotoa.

Bw. Stephen Lukonyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Insurance Tanzania alisema kampuni tayari ina matawi saba nchini, Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya, na Mtwara, huku matawi zaidi yakiwa mbioni kufunguliwa katika siku zijazo.

“Matawi haya yatahudumia maeneo ambayo huduma za bima bado hazijafika vya kutosha. Wananchi sasa wataweza kupata huduma zote kwa urahisi na unafuu” alisema Lokonyo. 

Bw. Lukonyo aliongezea kwa kusema tayari kampuni wamepokelewa vizuri sana na mawakala pamoja na washika dau katika sekta ya bima Tanzania, huku akiomba kuendelea kuungwa mkono ili kuwezesha kampuni yake kutoa huduma bora kwa wateja na hivyo kusaidia kukuza soko la bima nchini.

Alisema kampuni imepiga hatua kuwa mstari wa mbele katika uvumbuzi wa bidhaa na hivi karibuni watazindua bima ya afya na usafiri katika soko la Tanzania. Kampuni pia inatazamia sekta ya mafuta na gesi pamoja na sekta ya kilimo.

JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA AFUNGUA MAFUNZO MAALUMU KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOANI MWANZA.

$
0
0
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba, amewataka watumishi wa Mahama Mkoani Mwanza kutimiza wajibu wao kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na kwa wakati.

Mhe.Makaramba ameyasema hayo hii leo Jijini Mwanza, wakati akifungua Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayoendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza.

Amesema Mafunzo hayo yamekuja kwa wakati ikizingatiwa kwamba Mahakama ya Tanzania kwa sasa inaendelea na maboresho ya Utendaji kazi wake kama sehemu ya kuhakikisha kwamba inatoa huduma iliyo bora kwa wananchi.

Mwenyekiti wa taasisi ya MISA tawi la Tanzania, Simon Berege, amesema mafunzo hayo yanaendeshwa katika Kanda zote za Mahakama nchini, baada ya utafiti uliofanyika mwaka 2014 kuonyesha kwamba kuna ugumu katika upatikanaji wa habari za mahakama kwa umma hata kama habari hizo siyo za siri.

“Tunaipongeza Mahakama kwa hatua hii ya kukubali kutoa mafunzo kwa watumishi wake na kutoa taarifa muhimu kwa wananchi maana mihimili mingine imekuwa ikiminya upatikanaji wa taarifa zake hata kama taarifa hizo siyo za siri”. Amesema Berege.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema wanatarajia kujifunza mambo mengi ikiwemo kuongeza ujuzi zaidi wa namna ya kuwahudumia wateja (Wananchi) ili kuwafanya watambue kwamba Mahakama nchini zinatenda haki.

Mafunzo hayo ambayo yanafadhiriwa na Shirika la Misaada la Ujerumani FES, yamefanyika Mkoani Mwanza baada ya mafunzo kama hayo yaliyofanyika katika Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Tabora kuonyesha yameongeza ufanisi na utendaji wa Watumishi wa Mahakama katika kuwahudumia wananchi hususani katika utoaji wa taarifa kwa umma ambapo yanawajumuisha Mahakimu, Watunza Kumbukumbu pamoja na Maafisa Utumishi wa Mahakama.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba akiongea katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza. Mafunzo hayo yameanza leo na yanatarajia kufikia tamati kesho Mei 07,2016.PICHA NA
BMG
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba akiongea katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Afisa Habari na Utafiti kutoka MISA-Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza katika Mafunzo hayo
Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.

TAHAFE YATANGAZA TAASISI 31 ZITAKAZO PELEKA MAHUJAJI KWENDA KUHIJI MAKKA

$
0
0
Mwenyekiti wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (TAHAFE), Sheikh Abdallah Khalid (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu mchakato wa kwenda kuhiji mwaka huu 2016. Kushoto ni Katibu wa Taasisi hiyo, Dk. Ahmed Twaha na kulia ni Mjumbe, Hassan Ali. 
Katibu wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (TAHAFE), Sheikh Abdallah Khalid , akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

OFISI Kuu ya Hijja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezitangaza taasisi 31 zilizokidhi vigezo vya kupeleka mahujaji kwenda kuhiji kwa mwaka 2016.Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (TAHAFE) Sheikh Abdallah Khalid wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo.

Alisema shughuli zote za utekelezaji wa ibada ya Hijja na Umra hapa nchini zinasimamiwa, kuratibiwa na kuendeshwa chini ya uongozi wa Biita inayoundwa na Shirikisho la Taasisi za Hijja Tanzania (Tahefa) na Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar (Utahiza).

Alisema gharama za mahuja kwa mwaka huu kutoka nchi kwenda kuhiji ni dola 3400 hadi 4700 na kuwa malipo ya huduma stahili yanapaswa kupitia benki zilizoanishwa na Wizara ya Hijja Saudia Arabia.Sheikh Khalidi alisema taasisi zote zinatakiwa kuwapima afya mahujaji watarajiwa mapema kuanzia Agosti 8 au kabla ya hapo na kujaza fomu maalumu zitakazotolewa na Biita na kuingizwa kwenye mtandao.

FILAMU YA NIMEKOSEA WAPI? KURUKA SUNCREST QUALITY CENTRE KATIKA BIG SCREEN 11.MAY.2016!

$
0
0
FILAMU kubwa ya kitanzania ya Nimekosea wapi? ya mtayarishaji na mwigizaji mahiri Swahilihood Salum Saleh ‘Fizo’ itakuwa ni filamu ya kwanza kufungua njia kuonyeshwa katika jumba la sinema la Suncrest Cineplex Cinema lilopo Quality Centre wiki ijayo.

Akiongelea tukio hilo Fizo amesema kwake ni bahati kubwa sana kupata nafasi hiyo kwa filamu yake kuwa ya kwanza kutoka kampuni ya Steps Entertainment kuanza kuonyeshwa katika Jumba la sinema katika Big Screen na kuingia katika hatua nyingine ya biashara.

“Namshukru sana Mwenyezimungu kwa kupata bahati hii nimetengeneza filamu kubwa na inaonyeshwa katika ukumbi wa filamu kwa hadhi kubwa, nipo na wasanii wakubwa Gabo zigamba na wengine,”anasema Man Fizo.

Filamu ya Nimekosea wapi? inatarajia kuonyeshwa tarehe 11.May.2016 kwenye Bongo Movie Premiere kuanzia saa 1:00 ambapo wasanii watapita katika Red Carpet na kuingia ukumbi kwa ajili ya kuona sinema yenye ubora mkubwa.

“Pia tunashukru kwa wapenzi wa kazi zetu kusapoti kwa kila hatua kwani wamekuwa karibu nasi na naamini kuwa katika jambo hili muhimu kwa tasnia ya filamu watatuunga mkono, kiingilio ni 5,000/ tu za Kitanzania msikose,”anasema Man Fizo.

Tarehe 12.may.2016 hadi tarehe 15. May. 2016 saa 2:00 kamili usiku kila siku sinema ya Nimekosea Wapi? itaonyeshwa katika ukumbi wa Suncrest Cineplex Cinemas na wapenzi wa filamu kujionea hatua kubwa kutoka kwa wasanii wa kitanzania wakifanya mambo makubwa.

Na tarehe 16. May. 2016 filamu ya Nimekosea wapi itaingia mtaani kwa maana hatua ya Dvd. Tanzania inaingia katika hatua nyingine kwa filamu zetu kuonyeshwa katika kumbi za sinema hatua muhimu sana katika ukuaji wa tasnia ya filamu Tanzania kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea.

Filamu ya Nimekosea Wapi? inafungua njia kwa kazi za kitanzania kuonyeshwa katika majumba ya sinema kwa kiingilio cha 5,000/ ikiwa ni njia ya kuwafanya watu wapende kazi za ndani na itaonyeshwa kwa siku tano mfululizo.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images