Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

ZANTEL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MSINGI KWA AJILI YA KAMBI YA WAGONJWA WA KIPINDIPINDU ZANZIBAR

$
0
0
Mkuu wa Kampuni ya Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya Kambi ya wagonjwa wa kipindupindu iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja (kushoto) Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (kulia) daktari dhamana kanda ya Unguja Dkt. Fadhil Mohammed.
Mkuu wa Kampuni ya Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha akimkabidhi Waziri wa Afya baadhi ya vifaa vilivyotolewa na Kampuni hiyo kwa ajili ya Kmbi ya wagonjwa wa kipindupindu (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Juma Malik Akili.
Shehena ya msaada wa vifaa vilivyotolewa na Kampuni ya Zantel kwa ajili ya kambi ya kipindupindu Zanzibar.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni kumi na moja. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
 
Kampuni ya simu ya mikononi ya Zantel leo imetoa msaada wa vifaa vya usafi kwa ajili ya kusaidia juhudi za kupambana na kipindupindu za Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kambi za kipindupindu visiwani humo.


Vifaa hivyo ambavyo vimekabidhiwa kwa Wizara ya Afya vimegharimu jumla ya shlingi milioni 11, ni pamoja na matanki ya kuhifadhia maji, vitanda vya kamba, pampu ya kisima, mabomba ya kunyunyizia dawa, maturubali mazito, maboksi ya gloves na mafuta ya petroli lita 3,000 kwa ajili ya magari ya kuhudumia kambi za kipindupindu.


Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo, Waziri wa Afya, Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo amesema ugonjwa wa kipindupindu ambao mpaka sasa umesabababisha vifo vya watu 53 utatoweka visiwani Zanzibar baada ya wiki tatu zijazo.


‘Kwa kiasi kikubwa juhudi zetu za kupambana na kipindupindu kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali zimeanza kufanikiwa, na tunaomba wadau wengine wazidi kujitokeza kutuunga mkono’ alisema Mahmoud.


Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya kampuni ya Zantel, Mkuu wa kampuni ya Zantel upande wa Zanzibar, Mohammed Mussa amesema kampuni yake inajivunia kushirikiana na serikali ya Zanzibar kupambana na ugonjwa wa kipindupindu ambapo ameeleza kuwa tarehe 23 na 24 mwezi uliopita kampuni ya Zantel imetuma ujumbe kwa wateja wake zaidi ya laki sita na nusu juu ya kujikinga na ugonjwa huo.


‘Tunawaomba wananchi waendelee kudumisha kanuni za usafi ikiwemo kuweka mazingira safi, kuchemsha maji ya kunywa, kunawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka kufanya haja ili kujikinga na janga la kipindupindu’ alisema Mussa.


KUTANA NA ‘GREEN VOICES’, SAUTI ZA AKINAMAMA WAPAMBANAO NA MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0
Akinamama wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na viongozi wa Foundation For Women of Africa na wafadhili wa mradi huo, mara baada ya uzinduzi wa mradi huo Madrid, Spain hivi karibuni.
Mama Maria Tereza (katikati) - Rais wa taasisi ya Foundation for Women of Africa akiwa na waandishi wa habari wanaotekelza mradi wa Green Voices wakati wa hafla ya kuwakaribisha kinamama nchini Spain. Kutoka kushoto ni Secelela Balisidya, Tukuswiga Mwaisumbe, Farida Hamis, Siddy Mgumia na aliyechuchumaa Judica Losai.
Akinamama wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo kikuu cha Universitad Automous De Madrid, mara baada ya kutembelea mazingira ya chuo hicho Madrid, Spain hivi karibuni.
Ziara ya mafunzo kujifunza jinsi ya kutengeneza mbolea ya mboji.
Ziara ya mafunzo kujifunza majiko yanayotumia nishati ya jua.
Ziara ya mafunzo katika chumba cha habari cha gazeti la El Pais.
Akimama na wawezeshaji wa mafunzo katika picha ya pamoja darasani.



WANAWAKE wapatao 15 hivi karibuni walihudhuria mafunzo ya kuongeza ujuzi wa jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini Spain. Mafunzo na mradi huo vinafadhiliwa na Taasisi inayojihusisha na maendeleo ya wanawake wa Afrika, ijulikanayo kama Foundation for Women of Africa  inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu waSpain Mama  María Teresa Fernández de laVega.


Taasisi hiyo itafanya kazi na wanawake hao 15 wa kitanzania kupitia miradi inayosaidia nchi kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Wanawake hao ambao kati yao watano ni waandishi wa habari kila mmoja atatekeleza mradi mmoja, huku waandishi wa habari wakisaidia kupaza sauti za akinamama hao kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Mradi huu unaojulikana kama GREEN VOICES una lengo la kupaza sauti za akinamama kueneza ujuzi wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili jamii nzima ya kitanzania iweze kujifunza zaidi na kuzitumia mbinu hizo katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.


Mradi huo unaoratibiwa hapa nchini na Mtandao wa wanahabari wa Mazingira (EMNet) kwa niaba ya Foundation for Women of Africa unatekelezwa katika mikoa sita ya Kigoma, Kilimanjaro, Mwanza, Morogoro, Dar es Salaam na Pwani ukihusisha miradi ya kilimo, usindikaji, ufugaji na utafiti.


Mratibu wa EMNet Secelela Balisidya amesema akinamama hao wanatekeleza miradi ambayo inachangia moja kwa moja aidha kupambana au kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Amesema miradi hiyo ni mradi wa kilimo cha miti ya matunda mkoani Kigoma, kilimo cha viazi lishe visiwani Ukerewe mkoani Mwanza, Ufugaji Nyuki mkoani Morogoro na Pwani na ukaushaji wa mbogamboga kwa kutumia nishati ya jua mkoani Morogoro. 

Miradi mingine ni usindikaji wa vyakula mbalimbali kutokana na muhogo mkoani Pwani, kilimo hai cha mbogamboga na kilimo cha uyoga mkoani Dar es Salaam, mradi wa majiko banifu mkoani Pwani na mradi wa utafiti wa jiko linalotumia nishati ya jua mkoani Kilimanajro.


Mradi huo unaotarajiwa kutelekezwa kwa mwaka mmoja unatoa fursa kwa kinamama kutoa ujuzo wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi na sauti zao kusikika. Hiyo ni kwa sabuabu kinamama wana uhusiano mkubwa na mazingira kutokana na kazi wanazozifanya kila siku za kilimo na utunzaji wa familia kuhusiana moja kwa moja na mazingira hivyo kuyaelewa zaidi mazingira na jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.


Wakiwa Madrid nchini Spain walikopata mafunzo wa wiki mbili katika chuo kikuu cha Autonomus Universitad De Madrid, akinamama hao na waandishi wa habari walijifunza kwa nadharia na vitendo jinsi nchi ya Spain inavyokabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuona njia ambazo na huku nchini zinaweza kutumika kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Mafunzo kwa vitendo pia yalihusisha ziara za mafunzo kujifunza kilimo hai, na jinsi nishati jua inavyoweza kusaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi.


Waandishi wa habari pia walipata nafasi ya kutembelea chumba cha habari cha gazeti la Serikali ya Sapin la El Pais an kujifunza zaidi jinsi waandishi wa huko wanavyoandika habari zihusianazo na mabadiliko ya tabianchi.  


Tovuti: Green Voices.

TATIZO LA AJIRA LINAENDELEA KUWA CHANGAMOTO KWA VIJANA ZANZIBAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Ajira Ameir Ali Ameir

Na Miza Kona Maelezo- Zanzibar 

Mkurugenzi wa Idara ya Ajira Ameir Ali Ameir amesema tatizo la ajira nchini bado ni changamoto kubwa kwa vijana kutokana vijana wengi kukosa sifa za kuajiriwa na baadhi yao kuchagua kazi za kuajiriwa.

Hayo ameyasema leo katika Ukumbi wa Kidongo chekundu wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya Kuwajengea Uwezo wa Kamati za Ajira za Wilaya za Mjini na Magharibi.

Amesema vijana ndio nguvu kazi katika jamii hivyo wana nafasi kubwa katika kulitumika Taifa kwa kufanya kazi lakini mtazamo wa vijana bado ni tatizo na baadhi wamejenga tabia ya uvivu unaopelekea kuwepo kwa vijana wengi wanaomaliza masomo wakiwa wazururaji wasio na ajira.

Mkurugenzi huyo amezitaka kamati za ajira kujipanga vizuri kuyafuatilia matatizo yanayowakabili vijana kupitia vigezo vyao, masheha, waajiri, mtazamo pamoja Utamaduni wao ili kuwanusuru kujiingiza katika vikundi viovu.

“NI kazi ya kamati kupita kwa waajiri ili kuangalia Changamoto, mafanikio attitude na Utamaduni kwa vijana pia unaweza kufahamu matatizo ya vijana kupitia vigezo vyao pia wazee wana nafasi gani katika kuwasaidia vijana,” alifahamisha Mkurugenzi Ameir.

Aidha amezifahamisha kamati hizo kutafuta taarifa yakinifu kwa vijana ili kupata kujua matatizo ya ajira yanayowakabili na kuweza kuwasaidia na kuwaingiza katika soko la ajira.Ameeleza kuwa vijana wanahaki ya kupata kazi yenye heshima inayoendana na mazingira bora ambayo yatamjenga kuweza kufanya kazi kwa ufanisi na kumpatia kipato cha kujikimu kimaisha na kuondokana na utegemezi.

Akiwasilisha Mada ya Mpango Kazi wa Ajira kwa Vijana Afisa Ajira Kutoka Idara ya Ajira Mustafa Hassan Makame amesema serikali imeweka mikakati mbali mbali ili kuhakikisha inakabiliana na tatizo la ajira na kuona kwanba tatizo hilo linapungua nchini.“Ujasiri amali ni njia ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana na sio ajira za serikali peke yake hivyo vijana wana nafasi kubwa ya kujiajiri wenyewe,” ameeleza afisa huyo. 

Nae Mtaalamu kutoka Shirika la Kazi Duniani Edmund Mushy amesema serikali pekee haiwezi kulitatua tatizo la ajira kwa vijana ni lazima pawepo mashirikiano na wadau wengine ikiwemo sekta binafsi na taasisi nyngine kwani nao wana mchango mkubwa katika kukuza ajira nchini.

Wakichangia mada washiriki wa mafunzo hayo wameiomba wizara kuweka mratibu wa ajira katika Wilaya zote atakaeshughulia masuala ya ajira ili kuondosha usumbufu uliopo katika wilaya hizo na kamati ziweze kufanya kazi walizopangiwa kwa ufanisi.

SERIKALI KUENDELEA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA KEMIKALI

$
0
0
Mkuu wa Kitengo Cha Utafiti na Ubora wa Mifumo Bw. Benny Mallya kutoka Ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu utekelezaji wa sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali sura 182 ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kwa wasafirishaji na watumiaji wa kemikali hapa nchini. Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi na kulia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Sylvester Omari.
Mkuu wa Kitengo Cha Utafiti na Ubora wa Mifumo Bw. Benny Mallya kutoka Ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo kutoa mafunzo kwa wasimamizi 61 wa shughuli za usafirishaji wa kemikali na madereva 123 hapa nchini. Kulia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Sylvester Omari.

Frank Mvungi-Maelezo

Serikali itatoa mafunzo kwa wasimamizi 61 wa shughuli za Kemikali na madereva 123 wanaosafirisha Kemikali mbalimbali ili kuzuia athari zinazotokana na matumizi yasiyozingatia sheria na kanuni za kemikali.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na vyombo vya habari Mkuu wa Kitengo Cha Utafiti na ubora wa Mifumo Bw. Benny Mallya kutoka Ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani sura 182.

Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2015 matukio ya kemikali yalisababisha vifo 14.

“Jumla ya matukio 11 ya ajali za Kemikali yalitolewa taarifa katika kipindi cha mwaka jana pekee na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali ikiwemo kuungua moto magari na tani 250 za kemikali”.alisisitiza Mallya.

Akifafanua kuhusu matukio hayo Mallya amesema kuwa ajali hizo zilisababishwa na kukosekana kwa uelewa juu ya athari zinazoweza kusababishwa na kemikali hizo miongoni mwa wasafirishaji na watumiaji.

Kama sehemu ya utekelezaji wa sheria hii,Serikali inatarajia kuendelea kufanya mafunzo ya wadau kuhusiana na kemikali zenye kusababisha mlipuko.

Mafunzo hayo yatatolewa kwa wakuu wa polisi wa Usalama barabarani nchi nzima yanalenga kuongeza uelewa kwa wadau wanaohusika katik a kutumia na kusafirisha kemikali ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza.

Katika kukabiliana na madhara yatokanayo na matumizi yasiliyo salama,ajali na matukio ya kemikali,Serikali iliamua kutunga sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani sura 182 (The Industrial and Consumer Chemicals Management and Control) Act Capt 182).

Lengo kuu la sheria hii ni kuhakikisha kuwa kemikali zinatumika katika hali iliyo salama bila kuleta athari kwa watu na mazingira.

NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI DK. MHANDISI JU.LIANA PALLANGYO AKUTANA NA WATENDAJI KUTOKA TPDC

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dk. James Mataragio (mbele) akielezea mikakati ya shirika hilo katika matumizi ya gesi asilia inayozalishwa kwa ajili ya matumizi ya majumbani na nyingine kuuzwa katika soko la nje katika kikao kilichokutanisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili matumizi ya gesi iliyogunduliwa nchini katika matumizi ya ndani na nyingine kuuzwa nje ya nchi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo (pichani) akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Wataalam kutoka Idara ya Nishati kutoka kushoto, Mussa Abbas na Athur Lyatuu wakinukuu hoja mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa katika kikao hicho.
Wataalam kutoka Idara ya Nishati iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kikao hicho.

MAADHIMISHO YA SIKU MKUNGA DUNIANI KUFANYIKA KESHO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) bi.Feddy Mwanga akizungumza leo na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu maadhimisho ya siku ya mkunga duniani yatakayofanyika kesho , jijini Dar es Salaam, Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wakunga Tanzania Dkt. Sebalola Leshabari .
Katibu Mkuu wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Dk. Sebalola Leshabari akiwasilisha maada katika mkutano wa kuelekea maadhimisho ya Mkunga Duniani, uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau mbalimbali waliofika kwenye mkutano wa kuelekea maadhimisho ya siku ya mkunga duniani, uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu, Jamii)

NHIF yakabidhi kituo cha Uchunguzi na Matibabu Hospitali ya Rufaa Dodoma

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekabidhi kituo cha Uchunguzi na Matibabu kwa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kupata huduma bora za matibabu.

Kituo hicho kimekabidhiwa leo mkoani Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Benard Konga kikiwa na lengo la kuwapa wananchi huduma bora za matibabu na kuweka wataalamu wenye uzoefu ili iwe ni sehemu ya kujifunzia kwa wataalamu wa kada mbalimbali za udaktari.

“Kituo hiki kimejengwa kisasa kwa kuwekewa mfumo wa kisasa wa miito ya manesi (Nurse Call System), jengo la jenereta na transfoma kwa ajili ya kuwa na umeme wa uhakika masaa yote, mifumo ya kisasa ya vipooza hewa, sehemu ya mapokezi, sehemu ya kutolea dawa, sehemu ya dharura, maabara, vyumba vya uchunguzi, vyumba vya Madaktari, chumba cha upasuaji, chumba cha wagonjwa mahututi, kliniki mbalimbali,sehemu za kulaza wagonjwazenye jumla ya vitanda 34 pamoja na Jengo la mgahawa kwa ajili ya huduma ya chakula”alisema Konga.

Konga ameongeza kuwa kuna baadhi ya shughuli za ujenzi zinaendelea kukamilishwa lakini haziwezi kuzuia kuanza kufanya kazi kwa kituo hicho kwa sababu huduma hizo zinapatikana katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambayo inasimamia kituo hiko.

Aidha, Konga amezitaja baadhi ya shughuli za ujenzi zinazoendelea zikiwemo jengo la kuhifadhia maiti, ujenzi wa sehemu ya kufulia nguo pamoja na sehemu ya kuchomea taka ambazo amekiri kuwa hazitachukua mda mrefu kukamilika kwakua fedha za ujenzi huo zilishatengwa.

Amefafanua kuwa Mfuko huu una mpango wa kuimarisha huduma kwa kujenga vituo kamahivi katika kila Kanda na kwa mwaka wa fedha 2016/2017 mfuko umepanga kujenga kituo kama hiki mkoani Kigoma.Mradi wa ujenzi wa Kituo hicho ulianza mwezi Oktoba, 2009 ambapo ujenzi wa jengo umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 6.Jumla ya shilingi Bilioni 2 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya vifaa tiba na samani.

Rais Magufuli amteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza

$
0
0
Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza


VYOMBO VYA HABARI ASILIA (wa makaratasini) HOI BIN TAABAN WAKATI VYA digitali (wa mitandaoni) VYAPETA

$
0
0
Vyombo vya habari vya asilia, hususan magazeti,  vinakufa. Hivi sasa vvyombo hivyo vinajikongoja kutokana na  mauzo hafifu  na mdororo wa mapato kutoka matangazo na kupunguza wafanyakazi. 

Ila wakati idadi ya wasomaji wa habari mtandaoni ikizidi kukua, wanaoperuzi mtandaoni  humo hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando, utafiti wa Pew Research Centre unaeleza. 

Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 ("State of the News Media 2015,”) imeonesha kwamba katika vyombo vya habari vya karatasi (print media), Digitali na TV, imeonesha Dhahiri kwamba magazeti yanaelekea kuzimu. 

Utafiti huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa mtandaoni wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa makaratasini, ambapo gazeti kubwa sana la New York Times la Marekani limetangaza kuwa nakala zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali sana na wa mitandaoni .

Hivi sasa kuna mjadala mitandaoni endapo kama Tanzania iko ama itafika huko. Mabishano ni makali ambapo wa makaratasini wanashikilia msimamo wao kuwa nchini hapa tasni ya habari mtandaoni bado ni changa sana kuweza kutishia amani ya magazeti. 

Upande wa digitali unajibu kwamba endapo kama kuna wahariri viburi wanaobeza kasi ya mitandao, basi wakae mkao wa kulala njaa muda si mrefu ujao, maana ni wachache wanaoendelea kupata habari kwa njia asili ya magazeti. 

Upande wa digitali umeyasifia magazeti ya Global Publishers na la Mwananchi  anbayo ni dhahiri yana wahariri wanaokwenda na wakati na wanaojua nini wanachokifanya kwa kuanza na mapema kuogelea bahari ya maendeleo ya tasnia kwa vitendo kwa kuwa na vitengo vya mtandao vinavyopelekesha mbio magazeti yanayobeza technolojia hio kwa kubuni. 

"Ni kweli kwamba Tanzania ni bado sana kiteknolojia na miundombinu kiasi cha habari za mtandaoni zikatishia uhai wa habari za makaratasini, lakini si uwongo kwamba ukizingatia uharaka na gharama pamoja na kwenda na wakati muda si mrefu print media itakwenda na maji", amesema blogger mmoja ambaye pia ni mwanahabari kwenye moja ya magazeti makubwa nchini.

CHURA KUJAKIVINGINE.

$
0
0
Meneja wa msanii Wa Bongo Movie Snura Mushi (Snura), Hemed Kavu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuwaomba radhi wa tanzania kwa video ya wimbo wa Msanii Snura na wimbo wake wa Chura.
Kulia ni Msanii Wa Bongo Movie Snura Mushi (Snura) na Kushoto ni meneja wa msanii huyo, Hemed Kavu.
Snura amesema kuwa yupo tayari kufanya upya video ya Wimbo wake wa chura ambayo itafuata maadili ya kitanzania kwani tayari ameshachukua vibali vya kufanya upya video ya wimbo huo.Msanii Wa Bongo Movie Snura Mushi (Snura) amewaomba radhi watanzania kwaujumla pamoja na vyombo vya serikali vinavyosimamia sekta ya sanaa kwa kutokufuata sheria na kanuni na taratibu zilizopo katika uendeshaji wa sanaa.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, radhi hiyo imekuja mara baada ya Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo jana kufungia video ya wimbo wa msanii huyo wa Chura ikiwa ni pamoja na kutoonyeshwa kwenye Televisheni pamoja na kupigwa kwenye redio. Amesema kuwa tayari  video ya wimbo huo ameshatoa kwenye mtandao wa kijamii wa Youtube.
Msanii Wa Bongo Movie Snura Mushi (Snura) awaomba radhi watanzania kwa kufanya video isiyo na maadili ya kitanzania ya wimbo wake wa Chura ameomba radhi watanzania mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

MATUKIO YA BUNGE LINAENDELEA MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa papo yanayoulizwa na Wabunge leo mjini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai akiingia kwenye ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akiwasili viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.
Wabunge wakiwasili viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma.(Picha na Eleuteri Mangi-MALEZO, Dodoma).

BODI YA WATAALAMU WA MANUNUZI NA UGAVI YANG’ARA KIMATAIFA.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya tuzo ya kimataifa ya viwango iliyotolewa na International Federation of Purchasing and Supply Manangement(IFPSM) kwa bodi hiyo hivi karibuni kulia ni mkurugenzi wa mafunzo Bw. Godfrey Mbanyi.
Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) vitabu vya mtaala mpya wa mafunzo ulioanza na Bodi ya wataalamu ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB)Desemba mwaka 2015 kulia ni mkurugenzi wa mafunzo Bw. Godfrey Mbanyi.
Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) tuzo ya viwango vya kimataifa kutoka International Federation of Purchasing and Supply Manangement(IFPSM) iliyotolewa kwa bodi hiyo hivi karibuni kulia ni mkurugenzi wa mafunzo Bw. Godfrey Mbanyi.

Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Bodi ya wataalam wa manunuzi na ugavi (PSPTB) imetunukiwa tuzo ya viwango vya kitaalamu vya kimataifa na International Federation of Purchasing and Supply Manangement(IFPSM) na kutambulika rasmi kimataifa kwa kuwa na vigezo vya utoaji huduma katika viwango vya kimataifa.

Katika taarifa iliyotolewa na Afisa Masoko na Mahusiano mwandamizi wa (PSPTB)Bi Shamim Mdee imesema tuzo hiyo ilitolewa kwa PSPTB mwezi Februari mwaka 2016 na kuifanya PSPTB kuwa bodi ya kwanza barani Afrika kupata tuzo hiyo ya viwango vya kimataifa kutoka IFPSM.

Taarifa hiyo imesema kuwa upatikanaji wa tuzo hiyo ni matunda ya ushirikiano kati ya watendaji na Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha katika kuiendesha bodi hiyo kufanikisha malengo na mipango yake katika utendaji kazi.

Mara baada ya PSPTB kupata tuzo hiyo Rais wa IFPSM Dkt Paul Davi kwa niaba ya Bodi ya wataalamu wa viwango vya kimataifa ameipongeza PSPTB kwa kazi kubwa walioifanya na kuwa taasisi ya kwanza Barani Afrika kufikia kiwango cha kutambulika kimataifa kwenye taaluma hiyo.

Kabla ya kupata tuzo hiyo, PSPTB ilikuwa mwanachama muhusishwa wa IFPSM tangu mwaka 2015 lakini kutokana na utendaji wa kazi wake, Bodi ya viwango ya kimataifa ikawatunuku tuzo ya kuwa na viwango vya kimataifa katika utoaji wa taaluma hiyo Barani Afrika kwa ujumla.

Aidha ,taarifa hiyo imesema kuwa PSPTB imezindua mtaala mpya wa mafunzo tangu Desemba mwaka 2015 na mtaala huo kwa sasa unaendelea kufundishwa katika vituo mbalimbali vya maandalizi ya mitihani ya Bodi ambapo mtihani wa kwanza chini ya mtaala mpya utafanyika November 2016.

Taarifa imeeleza kuwa umuhimu wa mtaala huo ni pamoja na utaratibu wa kuanzisha masomo ya usimamizi wa manunuzi wa umma kuanzia ngazi za chini hadi juu na pia utaratibu huu utawataka watahiniwa kufaulu ngazi yoyote ya mtihani ndani ya miezi 24 toka kufanyika kwa mtihani husika kwa mara ya kwanza.

Katika kuzingatia utoaji wa taaluma ya manunuzi na ugavi nchini Bodi ya wataalamu wa manunuzi na ugavi itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ili kusaidiana na kupambana na changamoto zilizopo katika kupeleka mbele gurudumu la taaluma hiyo.

RC WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU AMSIMAMISHA KAZI AFISA UTUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA.

$
0
0
 
Mkuu wa mkoa wa RUVUMA SAID MWAMBUNGU amemsimamisha kazi afisa utumishi wa Halamashauri ya wilaya ya SONGEA Mkoani humo PHILBERT MTWEVE kwa kosa kuwalipa mishahara watumishi hewa 8 na kuisababishia hasara serikali zadi ya milioni 27. Soty kamili hii hapa chini kupitia Ruvuma TV

JK AKUTANA NA NAIBU MKURUGENZI WA GATES FOUNDATION YA MAREKANI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Naibu Mkurugenzi Kanda ya Afrika wa  Gates Foundation ya Marekani, Haddis Tadesse, ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, May 5, 2016. (Picha na Bashir Nkoromo).
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiagana na Naibu Mkurugenzi Kanda ya Afrika wa  Gates Foundation ya Marekani, Haddis Tadesse, baada ya mazungumzo yao, ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, May 5, 2016. 

ZIFF 2016 Announces Film Selection with Strong East African Presence

$
0
0


ZIFF 2016 Announces Film Selection with Strong East African Presence

Tamasha la filamu la Zanzibar (ZIFF) limetangaza majina ya filamu zitakazoshindanishwa hapo ifikapo Julai 9 hadi 17. Tamasha lilipokea jumla ya filamu 490 kutoka nchi 32 mwaka 2016. 

Jopo la wachaguzi limependekeza filamu 80 ndio zitakazoshindanishwa katika makundi matano maalum: Kundi la Kawaida 59, Sembene Ousmmane 15, filamu 12 Bongo movies. Nyingine 5 ni la kundi jipya kabisa la filamu zinazoizungumzia Zanzibar itakayopata tuzo ya Emerson. 
Kutakuwepo pia mashindano ya Video za Muziki ambazo zitatangazwa mwisho wa mwezi Mei na hizi zitaoneshwa katika maonyesho yanayofanyika katika Ngome Kongwe. 

Jambo la kukumbukwa zaidi mwaka huu nikuongezeka kwa jumla ya filamu za kitanzania katika mashindano. Filamu zaidi ya 40 zilitumwa kwa mashindano kwa ujumla na mwaka huu filamu 5 za kitanzania zitashindanishwa katika jopo la Ousmane Sembene kati ya filamu 17. 

Kwa ujumla filamu toka Afrika mashariki zinazoingia katika mashindano zimeongezeka pia ambapo kuna 8 toka Tanzania, Kenya 5, Uganda 3 na Rwanda 2. Mwaka huu kutakuwa na filamu 3 ambazo zitaoneshwa kwa mara ya kwanza duniani katika tamasha la ZIFF. Filamu hizi zimedhaminiwa na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) wakishirikiana na ZIFF. Washindi watatu wa shindano la Sembene Ousmane mwaka 2015 walipewa $2000 kila mmoja kuwawezesha kutengeneza filamu mpya katika kipindi cha mwaka na kuzituma tena ZIFF kwa kushindanishwa na nyingine. 

Mvuto wa tamasha unazidi kukua ukiangalia kuongezeka kwa nchi zinazotuma filamu. Mwaka huu Estonia na Albania zimetuma filamu zikiungana na nchi nyingine kama Bangladeshi, Finland, Trinidad and Tobago, Bermuda na nyinginezo. 

ZIFF pia inaendeleza mchango wake katika tasnia ya filamu kwa kutayarisha warcha maalum juu ya utengenezaji filamu. Mwaka huu ZIFF imetangaza warsha mbili. Ya kwanza ni juu ya matumizi bora ya Camera ya Canon D5 itakayoendeshwa na Barry Braverman toka Marekani ,aliyeifanyia kazi Panasonic na Sony katika kujaribisha vifaa vyao. 

Warsha nyingine ni ile itakayodhaminiwa na Goethe Institute ya Ujerumani itayofunza watoto wa shule ufundi wa kutengeneza vikaragosi katika filamu. Hii inatokana na kutambua nafasi ya sanaa katika kukuza vipaji na kuwatayarisha watoto wasanii kwa ajira, uadilifu na ubunifu. 

Kwa maelezo zaidi na kupata listi ya filamu zilizochaguliwa tembelea tovuti ya www.ziff.or.tz na pia tafadhali tu-like katika Facebook https://www.facebook.com/ZanzibarInternationalFilmFestival/

IFIKAPO 2030 WAKAZI WA DAR KUWA MILIONI 10.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MKOA wa Dar es Salaam unatarajiwa kuwa watu milioni 10 ifikapo 2030 hivyo kunahitaji uboreshaji wa jiji katika  kuendana na idadi  watu  kuongezeka kwa kiwango kikubwa.

Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda(Pichani) amesema kuwa kutokana kuwepo kwa ongezeko la watu kila mwaka Serikali ilibuni mradi wa uendelezaji wa jiji la Dar es Salaam kwa ufadhili wa Benki ya Dunia na serikali ya Tanzania.

Amesema ukuaji wa jiji la Dar es Salaam unakabiliwa na makazi yasiyopimwa kwa asilimia 70 hadi 80 hivyo kutokana na hali ya ukuaji wa kasi  wa jiji la Dar es Salaam na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoikabili dunia ni pamoja athari ya mafuriko yanatarajiwa kuongezeka katika jiji.

Makonda amesema katika kukabiliana na uongezeko mradi uendelezaji jiji la Dar es Salaam unatarajia kuanza mwaka wa fedha 2016 /2017  kwa kuanza kuboresha miundombinu na kujengea uwezo manispaa katika utoaji wa huduma katika kuweza kukabili changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kukabili majanga ya dharula yanayoweza kutokea katika jiji la Dar es Salaam.

Aidha amesema kuwa katika mradi huo utaangalia maeneo ya watu wenye kipato cha kidogo na maeneo yao yamejengwa kiholela, ujenzi wa miundombinu ya barabara inayoaunganisha Wilaya na Mkoa pamoja kuunganisha maeneo mbalimbali na ukanda wa mabasi haraka.

Amesema vigezo viliibua miradi kama ujenzi wa barabara zinazoingia katika barabara kuu za manispaa zote zenye urefu wa kilomita  65.6 katika kuweza kupunguza msongamano wa magari, ujenzi wa wa mitaro ya kutiririsha maji ya mvua zenye urefu wa kilomita 31.8 katika maeneo ya Mto Ng’ombe, Msimbazi, Gerezani Greek, Yombo pamoja na Kwashego ili kuweza kutatua changamoto za mafuriko.

Makonda amesema katika mradi watapandisha hadhi makazi yaliyopangwa kiholela katika kata 14 ambazo ni Tandale, Mburahati, Mwanyamala, Gongola Mboto, Kiwalani,Ukonga, Keko , Kilakala, Mbagala Kuu, Mbagala, Mtoni , Yombo Vituka ,Kijichi pamoja na Makangarawe  kwa kujenga barabaza za lami zenye urefu wa kilomita 145.

NHIF yazindua huduma Toto Afya Kadi

$
0
0
 Meneja Huduma za Dawa Michael Kishiwa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF)  akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu huduma mpya ya mfuko huo iitwayo “Toto Afya Kadi” inayohusisha watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane ambao sio wanachama wa kundi la mwajiriwa, Kushoto ni Afisa Masoko wa Mfuko huo Bi. Sabina Komba.
Baadhi ya waandishiwa Habari wakifuatilia mkutano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)  umepanua huduma za mfuko wake kwa kuanzisha huduma mpya iitwayo “Toto Afya Kadi”.Hayo yameelezwa na Meneja Huduma za Dawa NHIF Michael Kishiwa leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.

“Huduma ya Toto Afya Kadi ni huduma ambayo inahusisha watoto chini wenye umri chini ya miaka kumi na nane ambao sio wanachama wa kundi la mwajiriwa kwa mwajiri hasa wale ambao wanalelewa katika vituo vya watoto yatima au wanaolelewa na ndugu waliokosa fursa ya kujiunga na huduma ya Bima ya Afya,” alisema Kishiwa.

Kishiwa alisema kuwa, mwanachama ambaye ni mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 atatakiwa kujaza fomu zinazopatikana nchi nzima chini ya uangalizi wa mdhamini ambaye ni mlezi wake aidha kwenye kituo anacholelewa au mahali anapoishi.

Aidha, Kawishe alisema kuwa mwanachama wa Toto Afya Kadi atapata huduma zote ambazo mwanachama wa huduma ya Bima ya Afya ya NHIF anapata na ambazo zimeorodheshwa katika huduma ambazo zinatolewa na Bima hiyo kwa gharama ya shilingi 50,400 kwa mwaka.

Pia alisema kwa kijana ambaye amepita miaka 18 ili kuweza kuendelea kuwa mwanachama wa Bima ya Afya na hajaajiriwa atatakiwa kujiunga katika vikundi vilivyosajiliwa ili aweze kusajiliwa katika mfumo wa kikoi kwa kuchangia kiasi cha shilingi 76,800 kwa mwaka.

NHIF ina wanachama asilimia 12 ya watanzania huku ikiwa na jumla ya vituo 6700 nchi nzima, na mpaka sasa jumla ya wanachama 2,000 wa Toto Afya kadi wamesajiliwa nchi nzima tangu ianze Machi, 2016.

UVCCM KULA SAHANI MOJA NA WALIOFUJA MALI ZAO

$
0
0
kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka hamdu Shaka 

Na Woinde Shizza,Kilimanjaro 

Jumuiya ya vijana UVCCM imetoa wiki moja kwa wale wote waliouza viwanja na rasilimali za jumuiya hiyo kujiandaa kwa ajili ya kupelekwa mahakamani .

Agizo hilo limetolewa na kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka hamdu Shaka wakati akiongea na viongozi wa umoja huo wakiwemo wenyeviti wa mikoa ,wenyeviti wa wilaya pamoja na makatibu wa umoja huo kutoka katika mikoa ya Arusha ,kilimanjaro pamoja na Manyara waliokutana katika ofisi ya CCM wilaya moshi mjini katika majumuisho ya ziara yake alikuwa akifanya katika mikoa hiyo.

Alisema kuwa baadhi ya watu wamegeuza mali za jumuiya hiyo kama shamba la bibi, kwani kila mtu aliyekuwa akitumia mali hizo na kuzitawanya kama anavyotaka, hivyo atahakikisha anawachukulia hatua kali za kisheria kwa kuwapeleka mahakamani wale wote ambao wamehusika kufanya hivyo.

Alibainisha kuwa kwa sasa hivi katika uongozi wake amezamiria kuimarisha jumuiya hiyo na hatosita kuchukua hatua kwa yeyote yule wala kumuonea huruma yeyote yule ambaye amezifujaa mali hizo za jumuiya kama shamba la bibi.

Pia kwa upande wa utendaji ndani ya Jumuiya hiyo alisema kuwa kwa mtendaji yeyote ambaye anaona hawezi kwenda na mabadiliko na kasi anayoitaka aachie ngazi mapema kabla hajamkuta, maana hatamuonea huruma yeyote kwani hawataki watendaji wavivu wala mizigo ndani ya chama .

Alibainisha kuwa muda wa majungu ,fitina ,umbea na poroja umeisha na sasa ivi kinachohitajika ni mabadiliko ya utekelezaji wa majukumu ya kazi za kila siku, kufuata vikao vya kikanuni na kubuni miradi ya maendeleo na itayokuza uchumi kwani UVCCM anayohitaji kwa sasa ni ya siasa na uchumi huku akiziagiza wilaya zote na mikoa kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo. 
Baadhi ya wafuasi wa CCM wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo 

Wakazi wa Ilala wahakikishiwa usalama

$
0
0
Jeshi la polisi Mkoa wa kipolisi Ilala limewahakikishia usalama wananchi wa Mkoa wa kipolisi Ilala  na kuachana na taarifa za uvumi kuhusu hali ya usalama katika mkoa huo wa kipolisi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya  amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga ipasavyo kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote na kutoa tahadhari kwa wahalifu kuwa makini kwani jeshi lake limejidhatiti ipasavyo.

“Niwahakishie wananchi kuwa hali ya ulinzi iko vizuri na jeshi la polisi Mkoa wa Ilala limejipanga vizuri hivyo wananchi wawe na amani kwani tunafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha hali ya amani na utulivu inakuwepo wakati wote”, alisema Kamanda Mkondya.

Aidha kuhusiana na malalamiko ya wananchi wa Buguruni kuhusiana na kuwepo kwa kundi la vibaka na waporaji kamanda Mkondya amesema kuwa Jeshi lake linaendelea na operesheni ya kukamata wahalifu usiku na mchana ili kuhakikisha Mkoa wa kipolisi wa Ilala unakuwa salama ambapo mpaka sasa jeshi hilo linawashikilia baadhi ya wahalifu waliokuwa vinara wa uporaji eneo la Buguruni Chama.

“Mpaka sasa tunawashikilia vijana kadhaa ambao walikuwa ni kero katika eneo la Buguruni chama na maeneo mengine ya Mkoa wa Ilala”, aliongeza Kamanda Mkondya.

Kwa upande wake Afisa habari wa Manispaa ya Ilala Bw. David Langa amesema kuwa Manispaa yake kwa kushiriana na Jeshi la Polisi wako katika mkakati wa kuanza operesheni ya kuwaondoa wapiga debe ambao wamekuwa wakishtumiwa na wananchi kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika sehemu mbalimbali za Manispaa ya Ilala.

Aidha Kamanda Mkondya amewataka wakazi wa Ilala kutoa taarifa za kihalifu kwa jeshi lake ili kuweza kuifanya Ilala kuwa salama na kutimiza dhana ya ulinzi shirikishi.

Na Eliphace Marwa MAELEZO

PWANI: WIVU WA KIMAPENZI WASABABISHA KIFO KWA MAMA NA MTOTO

$
0
0
John Gagarini, Kibaha.
JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Frowin Peter Mbwale (26) mkazi wa Kawe Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuwa ua kwa kuwachinja mkewe Oliver Erasto (23) na mtoto wake Emanuel Frowin (3) kutokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Bonaventura Mushongi alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10:30 usiku eneo la Zinga kata ya Dunda Tarafa ya Mwambao wilayani Bagamoyo.

Mushongi alisema kuwa katika hali isiyo kuwa ya kawaida juzi siku ya tukio mtuhumiwa akiwa na mwenzake alijulikana kwa jina la Rajabu Juma (20) Mkazi wa Makongo Jijini Dar es Salaam waliwaua watu hao kwenye vichaka vilivyopo kwenye eneo hilo la Kaole.

“Muda huo mtuhumiwa akiwa na mwenzake alimhadaa mke wake kuwa waende kwenye nyumba yao ambayo inaendelea kujengwa kwa lengo la kuitazama ambapo mke wake alikubali na kumbeba na mtoto wao na kwenda huko ambako aliwachinja shingoni,” alisema Kamanda Mushongi.

Alisema kuwa mtuhumiwa kumbe lengo lake halikuwa kuangalia ujenzi wa nyumba yao huko Kaole kumbe alikuwa na lengo lingine la kufanya unyama huo ambao aliutekeleza akiwa na rafiki yake huyo ambaye walishirikiana kumchinja mke na mtoto wake.

“Chanzo cha mauaji hayo ni mtuhumiwa huyo alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa ana uhusiano na mwanaume mwingine aitwaye Hamza mkazi wa Kawe Jijini Dar es Salaam na kusababisha mauaji hayo ya kusikitisha ambayo yamewaumiza watu wengi,” alisema Mushongi.

Alibainisha kuwa miili ya marehemu hao ilikutwa ikiwa imechinjwa na watu hao umbali wa mita 100 kutoka barabara ya magari itokayo Kaole kwenda eneo la Mbegani.

Aidha alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa majira ya saa 3:30 usiku baada ya wananchi Zinga kuwatilia mashaka walipokuwa wakijaribu kutaka kutoroka na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika, miili ya marehemu imehifadhiw akwenye Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo kusubiri ndugu kwa ajili ya mazishi.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images