Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

KAMBI TIBA YA GSM NA MOI: OPARESHENI 55 ZA VICHWA VIKUBWA ZAFANIKIWA BUGANDOKA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Jumla ya watoto 55 wamefanyiwa upasuaji katika kambi ya tiba ya watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi, iliyowekwa katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza siku nne mfululizo, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa nalo, chini ya udhamini wa taasisi ya GSM Foundation. Zoezi litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne zinazotarajiwa kufanyika Tanzania nzima. 

Akiongea wakati wa kufunga kambi hiyo rasmi jioni ya leo, Daktari Bingwa wa upasuaji na mifupa kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, Dk Othman Kiloloma(Pichani Juu) ambaye pia ni mratibu wa kambi hiyo aliishukuru taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.

Dk Kiloloma aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima, wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu.

Cha kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za matibabu.

Mpaka jioni ya leo, ambayo ni siku ya nne tangu kuanza kwa kambi hii, jumla ya watoto 55 walikuwa wameshafanyiwa upasuaji, ambapo siku ya kwanza, walifanyiwa watoto 16, siku ya pili wakafanyiwa watoto 17, siku ya tatu wakafanyiwa watoto 12, na leo wamefanyiwa watoto 10.

Mratibu huyo ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI), Dk Othman Kiloloma, amebainisha kwamba changamoto kubwa inayotokea kwa jamii linapokuja suala la watoto wenye vichwa vukubwa na mgongo wazi ni gharama za upasuaji, ambapo gharama ya upasuaji kwa mtoto mmoja ni kati ya shilingi laki saba za kitanzania mpaka Milioni moja.
“Watoto wengi huzaliwa katika mazingira duni na wazazi wasiokuwa na nguvu ya kiuchumi, hali inayosababisha wengi wao kuwaficha ndani huku wakiwahusisha na imani za kishirikina”, alifafanua Dk Kiloloma.

Dk Kiloloma amesema zaidi ya watoto 4000 huzaliwa kila mwaka wakiwa na tatizo la kichwa kikubwa, lakini wanaorudi Hospitali kwa ajili ya tiba nhawazidi laki nne, swali kubwa ambalo jamii hujiuliza ni kuhusiana na watoto ambao hawafiki hospitalini huishia wapi?
Kwa upande wake, Halfan Kiwamba, Afisa Mawasiliano wa Taasisi ya GSM Foundation ambao ndio washamini wakuu wa kambi hizo amesema, taasisi yake imeamua kuokoa maisha y watoto hao ambao ni nguvukazi ya taifa la kesho na inalifanya hilo ikiwa ni moja ya mikakati yake katika kurudisha fadhila kwa jamii ya kitanzania ambao ni wateja wakubwa wa bidhaa za GSM. 

Kiwamba amesema taasisi yake ina lengo la kuhakikisha kwamba wananchi wa Tanzania hasa watoto ambao ni wa taifa ya kesho wanao msingi wa nguvu kazi kwa ajili ya maisha yao ambapo vitu vikubwa ni elimu boira pamoja na Afya.

Kwa upande wake Meneja wa Taasisi ya GSM Shannon Kiwamba amesema wakati mwingine ni vigumu kuingia katika maisha ya kila mwananchi na kumsaidia mahitaji yake, lakini akiwa na uhakika wa Afya na elimu anaweza kwenda mbali akijumlisha na jitihada zake.

Hivyo amewaomba watanzania kujitokeza wanaposikia taasisi yake inatoa huduma ili kufaidika nayo.Kambi ya tiba ya GSM inaondoka kesho juijini Mwanza kuelekea Shinyanga ambapo itaweka kambi kwa siku tatu.

Waziri Mhagama atoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (kulia) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 na jinsi dawa hizo zinavyoathiri afya na nguvu kazi ya taifa. Kushoto ni Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya nchini Keneth Kiseke.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (kushoto) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 na jinsi dawa hizo zinavyoathiri afya na nguvu kazi ya taifa. Kulia ni Mfamasia Sehemu Elimu, Habari na Takwimu Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za kulevya nchini Amani Masami.



Waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini ya mwaka 2014 kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma)

Article 22

$
0
0
FUATILIA HOTUBA YA MHE.RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ''LIVE'' KUPITIA TOVUTI RASMI YA RAIS WWW.IKULU.GO.TZ KUANZIA SAA 3:30.

NI SHEREHE ZA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI KITAIFA ZINAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA JAMHURI MKOANI DODOMA LEO  (MEI MOSI).




WABUNGE WAFANYE KAZI WALIOTUMWA NA WANANCHI NA SIO KUTOKA NJE YA BUNGE-SHAKA

$
0
0
 kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anaonyeshwa moja ya miradi ya UVCCM wilaya ya Same.

Na Woinde Shizza, Same

Wabunge wa upinzani wametakiwa kuwatetea wananchi, kutatua kero zao pamoja na kuwawakilisha vyema wanapokuwa bungeni na sio kufanya kazi ya kutoka nje ya bunge kwa mambo ya siyokuwa ya msingi.

Hayo yamebainishwa leo na kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wakati akiongea na wananchi wa wilaya ya Same katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa standi ya Same.

Alisema kuwa ni jambo la kuchekesha na kushangaza kuona kiongozi ambaye amechaguliwa na mwananchi ili akamuwakilishe kwa kupeleka kero zao bungeni anafika bungeni na kutoka nje kutokana na sababu zisizo za msingi.

"unajua ni jambo la kushangaza kuona mbunge anasusia kikao cha bunge kisa eti serekali imekata a kurusha vikao vya bunge live sasa jamani uyu mbunge katumwa kuuza sura kwenye televisheni au kupeleka kero za wananchi, mbona awa Wabunge watakuwa kama harusi iliyokosa Vyombo "alisema shaka

Alibainisha kuwa wananchi wa nataka kutekelezewa ahadi zao na sio kuona sura zao kwenye tv, na kuaidiwa ahadi zisizo tekelezwa.

Alisema kuwa wananchi wa sasa hivi wanataka maendeleo, na viongozi kuona Sura zao bungeni wakiwa wanafanya mambo ya ajabu na ya kutia aibu wanapokuwa bungeni.

Aliongeza kuwa iwapo kama viongozi wa upinzani wameshidwa kufanya kazi waliotumwa na wananchi wao basi waachie ngazi kwa kujiuzuru ili waweza kufanya kazi na wanaotambua nini wajibu wao bungeni.

Aidha Alibainisha kuwa viongozi wa CCM pamoja na serekali wamejipanga vyema kuhakikisha wanatatua kero za wananchi na kuwatimizia yale  yote ambayo waliahidi kwa wananchi wakati wa kipindi cha kampeni.

SIMIYU YAHAMASISHWA USAFI WA MAZINGIRA NA KUTUNZA MITI

$
0
0
NA EVELYN MKOKOI

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano za Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameshiriki usafi wa mazingira wa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, mara hii mkoani Simiyu katika wilaya ya Meatu jimboni Kisesa.

Akizungumza na wananchi wa eneo la Mwandoya wilayani Meatu, Mhe. Mpina amewaasa wananchi wa mkoa wa Simiyu kwa ujumla kuitunza miti 4820 iliyopokelewa na kupandwa wilayani hapo baada ya serikali ya awamu ya tano kutekeleza ahadi yake ya kuupatia Mkoa wa Simiyu idadi hiyo ya miti.

Naibu Waziri Mpina, alisema kuwa kwa kuwamkoa wa simiyu huko kwenye hatari kubwa ya kuwa janga na umesha wahi kukabiliwa na tatizo la uhaba wa chakula, kabla ya uchaguzi uliopita, kwa kuitunza miti hiyo ya matunda wakazi wa mkoa huo watanufaika na miti ya matunda hayo ya muda mfupi kwa kufanya biashara ili kuweza kukuza uchumi na kuongeza kipato cha kila mmoja.
Aliongeza kuwa, zoezi la upandaji miti mkoani simiyu katika ma shule, maeneo ya makazi ya watu na mashamba yanahitaji utunzani mkubwa kwani miti hiyo ina uwezo mkubwa wa kuboresha uoto wa asili ambao mpaka hivi sasa umetoweka.

Aidha Mhe. Mpina amewataka viongozi wa mkoa wa Simiyu kuchukua nafasi yao kusimamia wanachi wafanye usafi ikiwa ni agizo la serikali la kila mwisho wa mwezi kuwa siku ya usafi na kuwa viongozi ambao watakuwa wazembe katika suala zima la usimamiaji wa usafi wa mazingira watachukuliwa hatua.

Alipoongea na wanachi wa Jimbo La Kisesa, Naibu Waziri Mpina aliwaasa wananchi wa Kisesa wa sapoti jitihada za serikali za kupanda miti na kutunza mazingira, na kuwa hakikishia wapiga kura wake kuwa pamoja na kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, nafasi za kazi yake kama Mbunge wa jimbo hilo ipo pale pale na ataendelea kuwapigania wana Kisesa.

Aliwaomba wana Kisesa wawe mfano wa kupanda miti iliyotolewa na serikali na kuitunza na kwa aliokosa miche ya miti hiyo iliyogawiwa ame ahidi kuwapatia miche mingine kwani shabaya yake kubwa ni kuwezesha mkoa wa simiyu kupata miti hasa ya matunza na mbao ili kuboresha uchumi binafsi na pato la taifa.

Mhe. Mpina Amefanya usafi wa mazingira leo katika eneo la hospital ya Mwandoya pamoja na kupanda miti ikiwa ni sehemu ya utekekezaji wa kampeni ya kitaifa ya kupanda miti.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAMUAGA KATIBU MKUU DKT. MOHAMED JIDAWI NA KUMKARIBISHA KATIBU MPYA DKT. JUMA MALIK AKILI.

$
0
0
Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo, Katibu Mkuu mstaafu na Katibu Mkuu mpya katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi walioshiriki katika hafla hiyo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wafanyakazi katika hafla ya kuamuaga Katibu Mkuu aliemaliza muda wake Dkt. Mohd Jidawi (kushoto) na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya (kulia) Dkt. Juma Malik Akili alievaa kofia katika Ofisi ya Wizara hiyo Mnazimmoja, Mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Afya Dkt. Mohd Jidawi akiwashukuru wafanyakazi wa Wizara hiyo kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati wa kutekeleza majukumu yake.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Dkt. Juma Malik Akili wakimsikiliza katibu Mkuu mstaafu Dkt. Mohd Jidawi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi cheti cha heshima Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara hiyo Dkt. Mohd Jidawi katika hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizarani, Mnazimmoja. Wa kwanza (kushoto) ni mke wa Dkt. Jidawi, Dkt. Mwanaheri Jidawi.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi meza yenye mlango wa Zanzibar (Zanzibar Door), Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara hiyo Dkt. Mohd Jidawi katika hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizarani, Mnazimmoja. Wa kwanza (kushoto) ni mke wa Dkt. Jidawi, Dkt. Mwanaheri Jidawi.

VYAMA VYA SIASA VIMEKUTANA KUJADILI MAPENDEKEZO YA MFUMO WA UTATUZI WA MIGOGORO NDANI NA BAINA YA VYAMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini Mhe. Peter Kuga Mziray akifafanua jambo wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam . Kulia ni Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa na Mhe. Vuai Ali Vuai, Makamu Mwenyekiti wa Baraza .
Bw. John Cheyo mmoja wa wajumbe wa Baraza la vyama vya siasa akichangia hoja wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam. 
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam. 
Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Baraza la vyama vya Siasa baada ya kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam


Na Monica Laurent -Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini ambalo linaundwa na wawakilishi wawili kutoka kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu wamekutana mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa GEPF uliopo Victoria Jijini Dar es salam kujadili mapendekezo ya mfumo wa utatuzi wa migogoro ya ndani na baina ya vyama vya siasa .

Mapendekezo hayo yalitolewa na Mtaalamu wa utatuzi wa Migogoro Bw. Ghalib Galant ambaye awali alifanya utafiti wa utatuzi wa migogoro ya ndani na baina ya vyama vya siasa nchini chini ya usimamizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na kwa udhamini wa UNDP kupitia mradi wake wa “Democratic Project” ukiwa na lengo la kuiboresha sura namba 258 ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ili kuendana na mahitaji ya ukuaji wa demokrasia nchini. Utafiti huo ulishirikisha wadau mbalimbali wa demokrasia ya vyama vingi nchini vikiwemo vyama vya siasa.

Akiwasilisha mapendekezo, Msajili Msaidizi Bi. Piencia C. Kiure ,alisema kuwa ilipendekezwa kuwa Sheria ya Vyama vya Siasa nchini iweke masharti yanayohusu utaratibu wa kutatua migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa “ migogoro ndani ya chama ni lazima ishughulikiwe kwanza ndani ya chama cha siasa na kufikia tamati kwa mfumo wa utatuzi wa migogoro uliowekwa kwa mujibu wa katiba ya chama, kabla ya kuwasilishwa katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya upatanishi” ilikaririwa sehemu ya mapendekezo

“Upatanishi ukishindikana mgogoro husika uwasilishwe kwenye Baraza la Uamuzi la Migogoro ya Vyama vya Siasa kwa uamuzi. Ikiwa muhusika wa mgogoro asiporidhika na uamuzi wa Baraza la Uamuzi wa migogoro ya vyama vya siasa atawasilisha mgogoro husika Mahakama Kuu mbele ya Majaji watatu kwa mapitio ya uamuzi wa Baraza. Muhusika asiporidhika na uamuzi wa Mahakama Kuu, atakata rufaa Mahakama ya Rufaa” ilifafanua sehemu ya Mapendekezo.

Aidha kumekuwa na msisitizo wa kufuata mtiririko wa hatua katika utatuzi wa migogoro kama ilivyobainishwa hapo juu ili kuepusha migogoro ndani ya vyama kwenda moja kwa moja Mahakamani ambako huchukua muda mrefu na kuathiri ukuaji wa demockaria ndani na nje ya vyama vya siasa hapa nchini.

Wakichangia katika mjadala huo, baadhi ya wajumbe walikubaliana na hoja kuwa vyama vya siasa vitatue kwanza migogoro yake ndani ya vyama na kwamba pale tu itakaposhindikana ndipo ipelekwe kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Wajumbe walishindwa kukubaliana katika hoja ya uwepo wa Baraza la Uamuzi wa Migogoro ya vyama vya siasa, wapo walioona haja ya uwepo wake na wapo walipendekeza kuwa majukumu ya Baraza hilo yafanywe na Baraza la Vyama vya siasa lililopo sasa jambo lililosababisha kutokukubaliana katika hoja hiyo.

Pamoja na michango iliyotolewa , Wajumbe wameishauri Serikali kuona umuhimu wa kuwekeza katika Baraza la Vyama vya Siasa ili kusaidia utatuzi wa migogoro nchini kwa kuwa imebainika kuwa machafuko katika nchi nyingi duniani yamesababishwa na machafuko katika masuala ya siasa.

Akihitaji ufafanuzi wa hatua gani imefikiwa katika uboreshaji wa Sheria ya Vyama vya siasa, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Siasa, Mhe. Peter Kugar Mziray aliiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutoa ufafanuzi. Naye Msajili Msaidizi, Bw. Sisty Nyahoza akitoa ufafanuzi alisema tayari vyama vyote vya siasa vimeshapelekewa barua vikiombwa kuwasilisha mapendekezo kwa ajili ya kuboresha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 na kwamba Ofisi inafanya jitihada za kupokea mapendekezo kutoka kwa wadau wa siasa na ikishakamilisha upokeaji huo, mapendekezo hayo yatawasilishwa kwenye kamati ya Katiba na Sheria.

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF, WASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI KWA MARA YA KWANZA

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, wakishiriki matembezi yakilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani (May day), hapa matembezi yakiwa barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 1, 2016.

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

MFUKO wa Fidia Kwa Wafanyakazi, WCF, kwa mara ya kwanza umeshiriki kwenye matembezi ya kusherehekea siku ya Wafanyakazi, maarufu kama MAY DAY jijini Dar es Salaam leo Mei 1, 2016. 

Matembezi hayo yaliyoshirikisha wafanyakazi kutoka sekta ya Umma na Binafsi, ambazo ndio wadau wakubwa wa Mfuko huo, yalianzia kwenye ofisi za Shirikisho la Vyamavya Wafanyakazi, TUCTA, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kupita barabara ya Nkurumah, Nyerere na kisha kupinda barabara ya Chang’ombe hadi uwanja wa Uhuru ambako
yalipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda.

WCF ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Bunge ya Fidia kwa wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008 ukiwa na wajibu wa kutoa Mafao ya Fidia kwa mfanyakazi apatwapo na madhara mahala pa kazi.

Tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo, juhudi za kutangaza hudumazake kwa wadau zimekuwa zikiendelea mfululizokwa kutoa elimu kupitia semina, maonyeshona makongamano lakini pia kupitia vyombo vyahabari na kwa siku ya Mei Day imekuwa ni fursa kubwa ya WCF kuungana na wadau wake wakubwa.

Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, wakishiriki matembezi ya kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani (May day), hapa matembezi yakiwa barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei 1,
2016.
Wafanyakazi wa WCF wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuruwakati wa matembezi ya kilele chasiku ya wafanyakazi Duniani
Matembezi yakiwa yameingia Uwanja wa Uhuru
Matembezi yakipita barabara ya Chang’ombe
Matembezi yanaendelea, hapa ni barabara ya Uwanja wa Taifa mkabala na ofisi za TAKUKURU wilaya ya Temeke
Matembezi yakiendelea barabara ya Chang’ombe
Matembezi yakiwa barabara ya Uwanaja wa Taifa
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa kwenye matembezi hayo, hapa nibarabara ya Chang’ombe
Baadhi
ya wafanyakazi wa WCF, wakimsikiliza mwenzao aliyevaat-shirtyenye ujumbe maalum
wa Mfuko huo “WCF inatoa Fidia Stahiki kwa Wafanyakazi wote wa Sekta ya Ummana
Binafsi”.


Mkuu wa Mkoa wa Dar esSalaam, Mh. Paul Makonda, (kulia), akiteta jambo na kiongozi
wa Shirikisho la Wafanyakazi mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa kilele cha May
Day uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa WCF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha
matembezi hayo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa WCF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilisha
matembezi hayo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Nyuso za furaha baada ya matembezi

NCCR, CUF NA TLP VIKO ICU- SHAKA

$
0
0
Picha ikionyesha kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anapokea kadi ya chadema na kumkabidhi ya CCM alikuwa mgombea wa udiwani kata ya Kisimani kupitia Tiketi ya chadema Amani John Mgonja Mara baada ya kuhamia Ccm.
Na Woinde Shizza , Kilimanjaro

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM ) umesema muda mfupi ujao Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kitaifuata mahali viliko vyama vya NCCR-Mageuzi, TLP na Chama cha Wananchi (CUF ) kwa sababu kimejidhuru kukubali kukumbatia mafisadi .

Aidha umoja huo umevitaja vyama hivyo sasa vinachechemea, vinaishi kwa matumaini na viko mahututi kwani wakati wowote ugonjwa uliovitafuna vyama hivyo utakishambulia chadema. 

Matamshi hayo yametamkwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na wanachama wa Uvccm na jumuiya zake katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Maendeleo Kata ya Mabogini wilaya ya Moshi vijijini.

Shaka alisema jeuri na mbwembwe za NCCR ‘Mgeuzi, CUF na TLP muda umepita na sasa havina mategemeao tena ya kuibuka na kushindana na chama tawala .

Alisema vyama hivyo hupenda kujiita vyama vya siasa jambo ambalo alisema si kweli kwasababu kujiendesha kwake kunamtegemea mtu badala ya kujijenga na kuwa taasisi kamili.

Alisema vyama hivyo vineajua kutegemea makapi yalioachwa na ccm ili yawasaidie kuendesha masuala ya kisiasa .

Akizungumza katika mkutano huo,Shaka  alimtolea mfano mbunge wa Moshi vijijini Anthony Komu (chadema) akisema hana uwezo wala uaminifu katika dhima ya kuwatumikia wananchi kwa sababu historia yake ya kisiasa haionyeshi kama mtu madhubuti na mwenye msimamo.

“Komu alikuwa mwanachama na kiongozi wa NCCR -Mageuzi tokea mwaka 1992 , akahama na kujiunga Chadema akivutiwa na ukabila, wakati fulani akataka aende TLP Mrema akamuwekea ngumu , aina ya kiongozi kama Komu ni ushahidi tosha si kiongozi muaminifu , kesho sivajabu ukasikia amegama chadema kurudi ccm “alisems Shaka

Hata hivyo Kaimu huyo katibu Mkuu aliitaka halmashauri ya wilaya ya Moshi vijijini kufanya kila linalowezekana kupekeka maji katika maeneo ya kata ya Mabogini ili wananchi waondokane na adha ya ukosefu maji.

“Wananchi wa Moshi vijijini nawahakikishia kuwa ujenzi wa barabara yenu umbali wa kilomita 14 toka TPC hadi Chekereni itatekelezwa na serekali ya Dk Magufuli kwa kiwango cha lami “alisema shaka.

Katika kijiji cha Chekereni kata ya mabogini wanachama wapya 34 wamejiunga na Uvccm, 27 CCM na UWT wanachama 12.

WAFANYAKAZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI MKOA WA DAR ES SALAAM.

$
0
0
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakiwa katika maandamano wakipita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (hayupo pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Mafoto Blog

DK. SHEIN AONGOZA SIKU YA KILELE CHA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali wakinyanyua mikono juu kuashiria Mshikamano wakati wa sherehe za kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani,ambazo sherehe zimewajumuisha mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimakabidhi zawadi Musssa Yussuf wa ZSSF Laki Sitafedha taslim akiwa mfanyakazi Bora Chama cha ZAFICOWV katika sherehe za Siku ya wafanyakazi Duniani Zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimakabidhi zawadi Bi.Asya Rajab Said fedha taslim laki tano,kutoka Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwa mfanyakazi Bora Chama cha ZUPHE katika sherehe za Siku ya wafanyakazi Duniani Zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi pamoja na Wananchi wakati wa Kilele cha siku ya Wafayakazi Duniani sherehe zilizofanyika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi, wakipita mbele yake wakati wa sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea maandamano ya Wafanyakazi mbali mbali wa Taasisi za Serikali na Binafsi,(pichani) Vijana waliobeba bango kutoka Ofisi ya Makamo wa Pili ya Rais akipita mbele yake wakati wa sherehe za sikuya Wafanyakazi Duniani katika viwanja vya Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo.
Baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Binafsi wakiwa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo mgeni rasmin akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Baadhi ya Vingozi na Wafanyakazi wa Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi wakiwa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja,mgeni rasmin akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein 
Baadhi ya Vingozi na Wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Binafsi wakiwa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo mgeni rasmin akiwa Baadhi ya Vingozi na Wafanyakazi wa Taasisi za Serikali na Binafsi wakiwa katika sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo mgeni rasmin akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ,

Hospitali zatakiwa kuwalinda wapokea kumbukumbu na maambukizi

$
0
0
Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed A. Mohamed (kulia) aliyemwakilisha Waziri wa wizara hiyo, Bi. Ummy Mwalimu, akizungumza na wanachama wa THERIA kabla ya kufunga mkutano huo. 
Katibu Mkuu wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Rehema Mwaipaja akizungumza na wanachama wa THERIA kabla ya kufungwa kwa Mkutano wao juzi. 
Katibu Mkuu wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA), Rehema Mwaipaja akizungumza na wanachama wa THERIA kabla ya kufungwa kwa Mkutano wao juzi. 


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu ameziagiza hospitali mbalimbali nchini kuhakikisha zinachukua tahadhari za kuwalinda wafanyakazi wake kitengo cha kumbukumbu katika mazingira ya kupata maambukizi hasa wanapokuwa kazini wakitimiza majukumu yao.

Waziri, Mwalimu ametoa maagizo hayo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka wizara hiyo, Dk. Mohamed A. Mohamed alipomwakilisha katika hafla ya kufungwa kwa mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania (THERIA) zilizofanyika juzi jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Mohamed alisema wizara hiyo, inatambua mazingira hatarishi ambayo wafanyakazi wa kitengo cha kumbukumbu wamekuwa wakifanyia kazi hasa ukizingatia wao ndio watu wa kwanza kukutana na wagonjwa kabla ya kufika kwa madaktari jambo ambalo linaweza kuzua maambukizi kwa magonjwa yaambukizwao kwa njia ya hewa.

"..Natambua pia mazingira mnayofanyia kazi wengi wenu yanayowafanya kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza kwani nyie ndo wa kwanza kabisa kukutana na mgonjwa, kabla ya kuonana na daktari au mtaalamu wa vipimo, hivyo kupata maambukizi ya magonjwa hatarishi hasa yaambukizayo kwa njia ya hewa na mengineyo ni rahisi. Woizara yangu inapenda kuwaagiza Wakuu wote wa hospitali nchini kuhakikisha wanarekebisha mazingira mnayofanyia kazi ili kuondoa hali hii," alisema Dk. Mohamed akimwakilisha waziri wake.

Aidha wizara hiyo pia iliahidi kushughulikia kero ya uhaba na ukosefu wa wafanyakazi wa taaluma ya utunzaji kumbukumbu za afya kwenye vituo vya afya na hospitali hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuzitaka hospitali na vituo hivyo kuajiri watu wenye taaluma halisi ya utunzaji kumbukumbu na kuhakikisha kada hiyo inapata muundo, stahili zake na kutambulika kama ilivyo kwa makundi ya kada nyingine.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za Afya Tanzania, Rehema Mwaipaja akizungumza katika mkutano huo alisema kuwa THERIA ina umuhimu mkubwa hasa ukizingatia kuwa takwimu sahihi za afya ndio msingi bora kwa huduma kamilifu kwa jamii. Aliongeza kuwa uboreshaji wa hali ya ukusanyaji, uchambuzi na utunzaji wa takwimu sahihi za afya unachangia kuboresha tafiti mbalimbali za afya ambazo ni matunda ya ukuaji na uboreshaji wa huduma kiujumla.

"Nidhahiri kuwa ukuaji wa taaluma ya afya hutegemea sana tafiti mbalimbali zitokanazo na taarifa zilizokusanywa na kutunzwa kikamilifu kazi ambayo ni ya msingi kwa afisa kumbukumbu wa afya mahali popote anapofanya kazi, hayo yote huleta faida kwa wagonjwa, taasisi na kwa wafanyakazi," alisema Bi. Mwaipaja.

Wanachama wa THERIA kutoka mikoa mbalimbali walikutana kwa siku mbili mfululizo katika wao mkuu uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine mkutano huo ulifanya uchaguzi kupata viongozi wapya wa chama hicho.

Rais Magufuli ahutubia Mei Mosi, atangaza kupunguza kodi ya mishahara kwa 2%

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya Wafanyakazi katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zulizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi TUCTA wakati wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kombe la ushindi wa jumla kwa Rais wa TUCTA Gratian Mukoba katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Cheti cha Mfanyakazi bora kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Ndugu Peter Chisunga katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwa serikali yake itapunguza kodi katika mishahara ya wafanyakazi kutoka asilimia 11 hadi kufikia asilimia 9 kuanzia mwaka ujao wa fedha wa 2016/2017 ili kupunguza mzigo kwa wafanyakazi.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo leo tarehe 01 Mei, 2016 wakati akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya siku ya siku ya wafanyakazi duniani, zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.


"Napenda kuwataarifa kuwa serikali yangu kama nilivyoahidi wakati wa kampeni zangu, nimeamua kupunguza kodi ya mapato ya mishahara kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 9, kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/2017, nikiwa nina mategemeo makubwa waheshimiwa wabunge watapitisha bajeti ya serikali niliyoiwasilisha"Amesema Dkt. Magufuli huku akishangiliwa na maelfu ya wafanyakazi waliojitokeza uwanjani hapo.


Pamoja na uamuzi huo, Rais Magufuli pia amewaahidi wafanyakazi kuwa baada ya kupunguza kodi katika mishahara ya wafanyakazi, serikali yake itafanyia kazi mapendekezo ya kuongeza mishahara.


Katika maadhimisho hayo ambayo pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Akson, Rais Magufuli amewataka wafanyakazi kote nchini kushiriki kufanikisha Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 kwa kufanya kazi kwa bidii, kujituma, weledi na uadilifu.


Amesema Mpango wa Maendeleo ya Taifa utagharimu takribani shilingi Trilioni 107 zikiwemo shilingi Trilioni 59 kutoka serikalini, hivyo amewataka wafanyakazi wote kutambua kuwa wanategemewa kuwaongoza watanzania kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo kwa kuchapa kazi.


Aidha, Rais Magufuli amewataka wafanyakazi kuunga mkono juhudi za kuwafichua wanaozalisha wafanyakazi hewa, huku akibainisha kuwa mpaka kufikia jana tarehe 30 Aprili, 2016 jumla ya wafanyakazi hewa waliobainika walikuwa 10,293 ambao kwa mwezi mmoja tu wamelipwa shilingi bilioni 11.6.


"Kwa hiyo kwa mwaka wafanyakazi hewa hawa wamekuwa wakilipwa shilingi 139,239,285,592.92, ukizidisha kwa miaka mitano kama tungekuwa na wafanyakazi hewa, miaka mitano tu, tusiseme miaka kumi au ishirini au kumi na ngapi, miaka mitano tu, manaake wangelipwa shilingi 696,196,427,964.6.


"Hizi bilioni 696 zinatosha kujenga madaraja kama la Nyerere lililopo Kigamboni, madaraja matatu, hizi bilioni 696 zinatosha kujenga flyover zinazojengwa Dar es salaam kwa msaada na mkopo kutoka Japan, zingekuwa saba, hizi bilioni 696 mjiulize kama zingetumika kulipa mishahara ya wafanyakazi waliopo ndani ya serikali, tungewaongezea mshahara kiasi gani" amesisitiza Rais Magufuli.


Hata hivyo Rais Magufuli amewahakikishia wafanyakazi wote ambao wanatekeleza majukumu yao kihalali kuwa serikali yake itawalinda na kuwatetea huku akitaka wawapuuze wanaodai serikali ya awamu ya tano haiwapendi wafanyakazi.


"Tukumbuke ya kuwa kazi ni utu, kazi sio fursa ya kupata mshahara kwa manufaa ya familia zetu bali ni fursa nzuri ya kutoa mchango kwa taifa lako kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho"amesema Dkt. Magufuli.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dodoma

01 Mei, 2016



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia namna ya uokozi katika majanga mabalimbali yanayotokea Migodini nje ya uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiifurahi picha yake ya kuchora alipokabidhiwa wakati anakagua mabanda ya Maonesho katika katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniania zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwenye banda la mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii SSRA mjini Dodoma .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwenye banda la Wakala wa Afya na Usalama mahala pa kazi OSHA mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi wa Tanzania TUCTA Ndugu Nicholas Mgaya mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa TUCTA Gratian Mukoba wakati alipowasili katika katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wazee wa mkoa wa Dodoma mara baada ya kuhutubia katika kilele cha Maadhimisho hayo ya siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuagana na mamia ya wafanyakazi katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Sehemu ndogo ikionesha wafanyakazi waliojitokeza katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma katika kilele cha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU

Rais Dkt.Magufuli ahutubia Mei Mosi, atangaza kupunguza kodi ya mishahara kwa 2%

Wanadiaspora watakiwa kuekeza nyumbani

$
0
0
Nembo ya ZADIA
Na Mwandishi wetu Washington 

Wazanzibari waishio nchi za nje wametakiwa kuwekeza nyumbani kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya taifa.

Wito huo ulitolewa jana na maofisa kutoka Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zaznzibar (ZSSF) wakati wakizungumza na Wazanzibari waishio nchini Marekani.

Akizungumza kwenye mkutano huo uliondaliwa na Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA), Meneja wa Mipango na Uwekezaji kutoka ZSSF Bwana Khalifa Muumin Hilal alisema kuwa Taasisi yake ina miradi kadhaa ya uwekezaji inayoendeshwa kwa ushirikiano na Benki ya Watu wa Zanzibar, na kwamba inawahamasisha Wazanzibari waishio Ughaibuni kuwekeza katika miradi hiyo.
Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa nyumba za kisasa katika eneo la Mbweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar ambao ujenzi wake tayari umeanza na unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu.

Bwana Hilal alifafanua kuwa eneo hilo litakuwa na majengo ya nyumba za kuishi yenye urefu wa ghorofa saba, ambapo kila ghorofa itakuwa na nyumba mbili."Kutakuwa na nyumba za vyumba viwili, vitatu na vinne" alifafanua Meneja Hilal, na kuongeza kuwa nyumba hizo zitapatikana kwa bei nafuu.
Akijibu swali kukhusu masharti ya upatikanaji wa nyumba hizo, Bwana Hilala alifafanua utaratibu wa upatikanaji wake kwa kusema "Kwanza kabisa tunaangalia vigezo vya fedha, kwa maana ya kipato cha mtu, kuna fomu ya maombi unajaza, kisha tunakupatia fomu ya mkataba ambayo inaelezea masharti yote, na tunaendelea kutoka hapo".Aliendelea kusema kuwa nyumba hizo zitapatikana kwa njia za mkopo au fedha taslim, ambapo ukilipa fedha taslim utapata punguzo lisilozidi asiliam tano (5%).

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tawi la Muamala wa Kiislamu katika Benki ya Watu wa Zanzibar Bwana Said Muhammed Said, alisema "Tumeweka utaratibu ili kila mtu aweze kumudu kununua nyumba hizo, na hapo ndipo inapokuja nafasi ya Benki"Aliendelea kusema kuwa, baada ya kujaza mikataba na ZSSF, mwekezaji ambaye hana uwezo wa kulipa fedha taslim anaweza kwenda kwenye Benki yake na kupata mkopo wenye masharti nafuu.

Akijibu swali kukhusu iwapo mtu atafariki kabla ya kumaliza kuilipia nyumba hiyo, Bwana Said alitoa khofu kwa kusema "Mtu haki yake haipotei". Aliendelea kuwa mtu akifariki kuna hali mbili, ama nyumba itauzwa na haki ya marehemu kupewa warithi wake, au warithi wakiamua kuendelea kulipa basi wataendelea kubaki na nyumba yao.Kukhusu taratibu za malipo, Bwana Hilal alisema, mtu anaweza kulipa kila mwezi, miezi mitatu au kama atakavyojaza kwenye mkataba wa mauzo.

Mbali na nyumba za kuishi, eneo hilo pia litajumuisha viwanja vya watoto, michezoya aina mbalimbali, mabwawa ya kuogelea, kituo cha Mikutano Msikiti na mengineyo.
Akijibu swali iwapo mikopo ya nyumba hizo itakuwa na riba au la, Bwana Said alisema "Unachagua, kama unataka mkopo wenye riba au mkopo kwa kupitia tawi letu la Muamala wa Kiislamu, huo utakuwa hauna riba".

Alendelea kufafanua kuwa kiwango cha riba rubuni vinategemea na hali ya soko kwa wakati ule mteja atakapochukua mkopo ikiwemo thamani ya sarafu kwa wakati ule, viwango vya riba vinavyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania na urefu wa muda wa mkopo wenyewe.
Kukhusiana na khofu ya mtu kupoteza nyumba yake iwapo atapoteza kazi, Bwana Said aliwatoa khofu Wazanzibari kwa kusema "Kutolipa mkopo kwa wakati uliokubaliwa kulaleta athari katika mfumo wa Benki.

Hata hivyo, iwapo mtu atashindwa kulipa kwa mara ya mwanzo na ya pili tunamtumia barua ya ukumbusho. Mara ya tatu ikiwezekana tunakutana naye ana kwa ana na kutafuta ufumbuzi" Ama iwapo mtu atapoteza kazi milele kwa sababu zisizoweza kuepukika kama ugonjwa na mengineyo, Mkurugenzi huyo alisema "Tutazungumza naye ili kuiuza nyumba na kumrejeshea chake".
"Tutakuwa na mkataba maalum, na yote hayo tuliyoyazungumza yatakuwemo humo", alisisitiza Bwana Said.

Mradi wa Makaazi ya Mbweni ni hatua za awali zilizopangwa kutekelezwa na ZSSF, kwani baadaye kutakuwa na mpango wa ujenzi wa nyumba moja moja (bungalow).Hata hivyo, Mkurugenzi Said alisema kuwa mtu akiwa na kiwanja chake binafsi, basi pia PBZ inaweza kutoa huduma za kifedha kugharamia ujenzi wa nyumba binafsi. "Muhimu uwe na hati miliki ya kiwanja, uwe na mkandarasi anaye julikana, na siyo mafundi wa vichochoroni", alifafanua Bwana Said.

Akijibu hoja juu ya sheria inayowazuia raia wa kigeni kumiliki ardhi Zanzibar, Meneja Hilal alifafanua kwa kusema "Ardhi ni milki ya Serikali, lakini serikali inaruhusu ukodishaji wa ardhi kwa wawekezaji. Hata sisi ZSSF tumekodishwa tu ardhi hiyo ya Mbweni, lakini kuna sheria ya umiliki wa nyumba kwenye majengo ya ghorofa, na sheria hii haimbagui mtu yeyote".Aliongeza kuwa kila mtu atapewa hati ya umiliki wa nyumba katika ghorofa hizo bila kujali uraia wake. "Ndiyo maana tumekuja kwenu" alisistiza Bwana Hilal.

Baadhi ya wachangiaji kwenye mkutano huo waliezea wasiwasi wao kuwa nyumba hizo huenda zikatolewa kwa upendeleo kama ilivyotokea kwenye nyumba za eneo linalojuilikana kama "Kwa Mchina". Awali nyumba hizo zilikusudiwa kuwasaidia watu wenye vipato vya chini, lakini badala yake zikatolewa kwa upendeleo na kumalizikia mikononi mwa watoto wa Wakubwa. "Je kuna uhakika gani kuwa mradi wa nyumba za Mbweni hautomalizikia kuwa kama ule wa Kwa Mchina"? aliuliza mchangiaji mmoja.

Akijibu hoja hiyo, Bwana Hilal alisema kuwa, hilo halitotokea. Zitatolewa kwa usawa kwa mtu yoyote yule mwenye uwezo, na ndiyo maana tumekuja Marekani kuunadi mradi huu, ili kila mtu mwenye uwezo akiwa Mzanzibari au laa, ndani au nje ya nchi aweze kununua nyumba hizo.

Maofisa hao wa kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar wapo nchini Marekani kuhudhuria Kongamano la Wanadiaspora wa Tanzania (DICOTA) lilloifanyika katika Jimbo la Texas.

Bwana Hilal alielezea shukurani zake kupata fursa ya kuzungumza na Wazanzibari nchini hapa, na kuelezea matmaini yake kuwa mkutano huo hautokuwa wa mwisho bali wa mwanzo kwa jili ya kuendeleza maslahi ya Zanzibar.

Kwa maelezo zaidi juu ya mradi huo tembelea http://zssf.org/en/, na fomu za maombi zitapatikana hapo katika wakati mwafaka.

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 2

YANGA YAANGUKIA PUA, YACHAPWA 3-1 NA SIMBA UGHAIBUNI

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akikabidhi kombe kwa nahodha wa Simba Bagasa
Mhe. Balozi Wilson Masilingi na mkewe Marystela Masilingi wakiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Simba walioibamiza Yanga kwa bao 3-1 mechi iliyoanaliwa na DICOTA 2016 Dallas Texas.
Kikosi cha Simba Ughaibuni
Kokosi cha Yanga Ughaibuni.
Timu ya Simba iliendeleza ubabe kwa mara ya nne mfululizo nje ya DC baada ya jana Jumamosi April 30, 2016 kuibanjua timu ya Yanga bao 3-1 katika mechi iliyoandaliwa na kongamano la DICOTA 2016 lililomalizika siku ya Juamamosi jijini Dallas, Texas nchini Marekani.

Wanandugu wawili Nico Njohole na Renatus Njohole waliowahi kuichezea Simba ya jijini Dar es Salaam na timu ya Taifa kwa nyakati tofauti, walikua kizingiti kikubwa kwa Yanga ambao jana waliuanza mchezo kwa kasi na kupata bao la kuongoza kupitia mchezaji wao hatari Dulla Makubeli.

Baada ya bao hilo Simba ilitulia na kucheza soka la kitabuni huku ikiongozwa na wakongwe wawili ambao walicheza soka lililowashangaza wengi lililosaidia Simba kusawazisha bao safi katika dakika 44 ya kipindi cha kwanza kupitia mchezaji James Kitia. Bao hilo lillisababishwa na mchezaji Renatus Njohole baada ya kuambaa na mpira wingi ya kushoto na kutia krosi iliyomkuta James Kitia na kufunga goli zuri la kideo kwa kichwa,

Kipindi cha pili Simba walitulia zaidi na kucheza mpira wa kisasa kwa pasi fupi fupi huku wakiwasoma Yanga ambao muda mwingi walifanya mashambulizi ya kushutukiza huku wakitumia mipira mirefu.

Katika dakika ya 74, Renatus Njohole aliifungia Simba bao la tatu baada ya kuwatoka mabeki na kumpiga shuti nayvu ndogo na kumwacha kipa wa Yanga asijue la kufanya.

Bao la tatu la Simba lilifungwa na mchezaji Everist aliyefunga baada ya mabeki wa Yanga kuijisahau.

Mpaka dakika 90 Simba 3 Yanga 1.


Mchezaji Renatus Njohole akiambaa na mpira pembezoni mwa uwanja.

Wachezaji wa Simba wakisimama kwa dakika moja kwa ajili ya misina iliyotokea Houston, Texas kwa Watanzania Henry Kiherile na Andrew Sanga waliopoteza maisha kwa ajali ya kupigwa  risasi. Picha na Vijimambo/Kwanza Production.
Wachezaji wa Yanga wakisimama kwa dakika moja kwa ajili ya misina iliyotokea Houston, Texas kwa Watanzania Henry Kiherile na Andrew Sanga waliopoteza maisha kwa ajali ya kupigwa  risasi

Mchezaji Renatus Njohole akiwatoka mabeki wa Yanga.
Mke wa Balozi Marystela Masilingi akiwa uwanjani kuishabikia Simba.
Michezo si uadui ni furaha baada ya mechi tizu zote zikipiga picha ya pamoja huku kukiwa na bango la Njohole Legend Foundation.
Renatus Njohole akifunga goli la pili.


NSSF YADHAMINI SIKU YA MADANSA DUNIANI

$
0
0
Ofisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim Kimaro, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya madansa duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na NSSF. (Na Mpiga Picha Wetu)
Ofisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano NSSF, Amina Mbaga, (kushoto) akimkabidhi fulana, Jumanne Mnola alipotembelea banda la NSSF wakati wa uzinduzi wa siku ya madansa duniani iliyofanyika viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF.
Ofisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano NSSF, Amina Mbaga, (kushoto), akimkabidhi fulana mmoja wa wateja wao, Said Ally, alipotembelea banda lao wakati wa uzinduzi wa siku ya madansa duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na NSSF.
Ofisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano (Nssf), Amina Mbaga akigawa vipeperushi kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda lao.
Ofisa Uhusiano wa NSSF, Faides Mdee, akigawa vipeperushi kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda lao katika uzinduzi wa siku ya madansa duniani uliofanyika kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe jijini Dares Salaam, mwishoni mwa wiki. Uzinduzi huo ulidhaminiwa na NSSF.
Wafanyakazi wa NSSF wakimkabidhi fulana mteja wao, Antela Salumu (katikati).
Ofisa wa NSSF, Innocent Shao, (kulia) akiwaandikisha baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na NSSF walipotembelea banda la NSSF katika uzinduzi wa siku ya madansa duniani iliyoadhimishwa kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe na kudhaminiwa na NSSF.
Ofisa uandikishaji NSSF, Amina Kisawaga (kulia) akitoa maelezo kwa mteja alietembelea banda lao Fumbwe Juma, katika uzinduzi wa siku ya madansa duniani uliofanyika kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF.
Picha ya pamoja.

MRADI WA KUKUZA TEKNOLOJIA KUPITIA WATOTO XPRIZE WAZINDULIWA DODOMA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila (kulia) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mradi wa kukuza teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues. (Picha na Modewjiblog).

Kwa kutambua uwezo walionao watoto katika kubuni vitu mbalimbali, Taasisi ya XPRIZE iliyo na makazi yake nchini Marekani, imezindua mradi wa XPRIZE nchini ambao utahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao watoto wa miaka 5-12.

Akielezea mradi huo, Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, alisema kuwa wameanzisha mradi huo kwa kutambua uwezo ambao wanao watoto na kama wakiwezeshwa wanauwezo wa kufanya mambo makubwa.Alisema dunia ina watoto wengi ambao hawapo shuleni kwa sababu mbalimbali na hivyo mradi huo utakwenda kufanyika kupitia watoto ambao hawapo mashuleni na watawapatia vifaa mbalimbali ili waweze kupimwa uwezo wao katika kazi zinazohusiana na teknolojia.

“Dunia ina watoto Milioni 57 ambao hawapo shuleni tutawatumia kama hao kwa sababu tunaamini watoto wanaweza kufanya mambo mengi lakini wanachohitaji ni kuwezeshwa ili waweze kukamilisha mambo wanayofanya,” alisema Keller.

Nae Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues alisema kuwa ni muda muafaka kwa watoto kusaidiwa kupata elimu kwa njia ya kiteknolojia hasa kwa wakati uliopo ambao teknolojia inatumika zaidi katika kurahisisha kazi mbalimbali.

Alisema ni muhimu kwa Tanzania kuanza kutumia mifumo ya teknolojia hasa katika kipindi hiki ambacho nchi ipo katika hatua za kuelekea uchumi wa kati kwani kwa kufanya hivyo itaweza kurahisha kufikiwa malengo kwa muda muafaka ambao umepangwa.“Ni wakati kwa watoto kupata elimu ya teknolojia, haijalishi hayupo shuleni kwa kipindi hiki teknolojia inatumika zaidi na hii itasaidia wakati huu ambao nchi (Tanzania) inakwenda katika uchumi wa kati,” alisema Bi. Rodrigues.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila alisema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili kuwawezesha watoto kupata elimu ya teknolojia lakini inakuwa ni ngumu kufikia malengo hayo yenyewe hivyo ni tumaini lao mradi huo utafanikiwa.

Alisema ni muhimu kwa watoto kupatiwa elimu ya teknolojia kwa dunia ya sasa na serikali ipo tayari kushirikiana nao kwa pamoja ili mradi huo uweze kufanyika kama jinsi umevyopangwa na Taasisi ya XPRIZE ambao ndiyo waanzilishi wa mradi huo ambao unataraji pia kufanyika nchi mbalimbali duniani.

“Unaposema dunia inakuwa kijiji ina maana unazungumza kuhusu teknolojia kutokana na kusogeza kila jambo karibu na kwa haraka ni ngumu kwa serikali kufanya yenyewe lakini wanapopattikana watu wanaosaidia inakuwa vizuri na pia inasaidia kukuza teknolojia nchini,” alisema Prof. Msanjila.

Nae Afisa Mradi wa Elimu wa UNESCO, Faith Shayo alisema mradi huo nchini utaanza kwa majaribio katika makundi 200 kutoka mkoa wa Tanga katika wilaya ya Lushoro, Korogwe, Muheza, Pangani, Mkinga, Handeni na Kilindi na mkoa wa Arusha utafanyika katika wilaya ya Ngorongoro ambapo watoto hao watapatiwa simu zilizo na muundo wa tablet na sola za kuchajia na watatumia 'tablet' kwa kusoma, kuandika na kuhesabu na baada ya hapo watakuwa wakichaguliwa kutokana na uwezo binafsi.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila.
Naibu wa Programu kutoka Shirika la Chakula Duniani (WFP) nchini, Marina Negroponte (kulia) akizungumzia nafasi ya Shirika lake katika utekelezaji wa mradi wa XPRIZE katika hafla fupi ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Pichani juu na chini ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Mafunzo kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller akizungumzia malengo ya mradi huo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Makamu wa Rais anayeshughulikia uendeshaji wa XPRIZE Foundation, Joel Carnes akifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi wa mradi huo uliofanyika mjini Dodoma, mwishoni mwa wiki.


Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon S. Msanjila (kushoto) akijadili jambo na Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Sarah Mlaki wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kukuza teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.


Kutoka kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila wakifuatilia kwa umakini 'power point presentation' ya jinsi mradi huo utakavyotekelezeka nchini.


Afisa Mradi wa Elimu wa UNESCO, Faith Shayo akizungumzia utekelezaji wa mradi huo wa kukuza teknolojia kupitia watoto XPRIZE na wadau watakaoshirikiana nao katika kutekeleza.


Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila, Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Sarah Mlaki, waandishi wa habari pamoja na wadau wa sekta elimu waliohudhuria uzinduzi huo, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.


Naibu wa Programu wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) nchini, Marina Negroponte akiandika mambo muhimu kwenye uzinduzi wa mradi wa XPRIZE.


Afisa mradi wa Elimu wa Unesco, Dar es Salaam, Faith Shayo akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller wakati wa uzinduzi wa mradi wa XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.


Baadhi ya wadau wa sekta ya elimu, waandishi wa habari na viongozi kutoka Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Hoteli ya Veta, mjini Dodoma.


Baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kwenye uzinduzi wa mradi wa XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.


Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila akiagana na Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller....Kulia Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues na kushoto ni Makamu wa Rais anayeshughulikia uendeshaji wa XPRIZE Foundation, Joel Carnes.


Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa Veta mara baada ya kuzindua rasmi mradi huo.


Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller (katikati) akizungumza na mmoja wa waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Veta mjini Dodoma, mara baada ya uzinduzi wa mradi huo. Kulia ni Makamu wa Rais anayeshughulikia uendeshaji wa XPRIZE Foundation, Joel Carnes.

MBATIA ATEMBELEA BARABARA YA KILEMA NA KUJIONEA ILIVYO HARIBIKA VIBAYA KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitizama barabara ya kuelekea Hospitali ya wilaya ,Kilema Hospital namna ambavyo imeharibika kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha.
Wanafunzi katika shule iliyo jirani na barabara hiyo wakitizama sehemu ya korongo lililopo katika barabara hiyo ambayo ni tegemeo kwa Chuo cha Ualimu Mandaka,Seminari ya Mtakatifu James ,shle za sekondari pamoja na msingi.


Baaadhi ya madreva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wakipita katika barabara hiyo ambapo kwa sasa nauli ya kupandisha abiria kwenda Hospitali ya wilaya ya Moshi,Kilima imepanda kutoka kiasi cha sh 3000 hadi 6000 .
Moja ya Magari yanayotumia barabara hiyo likijaribu kupita katika barabar hiyo ambayo imeharibika vibaya kutokana na maji yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Sehemu ya barabara hiyo likionekana korongo ambalo limeanza kumegwa na maji na kuhatarisha kukatika kwa mawasiliano katika baina ya vijiji 12 ambavyo wakazi wake wanatumia barabara hiyo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images