Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ATUNUKU VYETI KWA WASHIRIKI WA KAMPENI YA SIKU 10 YA USAFI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO (KINAPA)

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akitoa vyeti kwa wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zilizosaidia katika kampeni ya siku 10 ya kufanya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro  (KINAPA),Zoezi la utoaji Vyeti limefanyika katika lango la Marangu wakati wa hafla fupi ya kuwapokea washiriki wa zoezi hilo la usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza na washiriki wa kampeni ya siku 10 ya kufanya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) muda mfupi mara baada ya kurejea. 

Washiriki wa zoezi la usafi katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick huku wakionesha vyeti walivyotunukiwa baada ya kufanikisha zoezi hilo.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akiliongoza kundi la watu waliopanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kufanya usafi muda mfupi baada ya kurejea kutoka katika kilele cha mlima huo.
 

BWANA SAMWEL MILEGO AFUNGA NDOA NA BI. FLORIDA KAHATANO JIJINI DAR

0
0
Bwana harusi Samwel Milego na Bi. Florida Kahatano wakionyesha vyeti vyao mara baada ya kumaliza kufunga ndoa yao takatifu Jerusalem church of God lililoko Yombo Vituka jijini Dar es Salaam Jumamosi Aprili 30, 2016. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Bwana harusi Samwel Milego akimvalisha pete Bibi harusi Florida Kahatano wakati wakifunga ndoa takatifu Jerusalem church of God lililoko Yombo Vituka jijini Dar es Salaam Jumamosi Aprili 30, 2016.
Bwana harusi Samwel Milego akila kiapo mbele ya mkewe Bi. Florida Kahatano wakati wakifunga ndoa takatifu Jerusalem church of God lililoko Yombo Vituka jijini Dar es Salaam Jumamosi Aprili 30, 2016.

MFUKO WA PENSHENI WA PPF WATOA MFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2015, RAIS MAGUFULI AMKABIDHI CHETI NA KITITA CHA SH. MILIONI TANO

0
0
Rais Dkt. John Magufuli, akimkabidhi cheti cha mfanyakazi bora wa mwaka 2015 Enock Kalege, na zawadi ya Sh. milioni 5 iliyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa mfanyakazi huyo bora wa mwaka, wakati wa Kilele cha sherehe za Mei Mosi zilizofanyika Kitaifa mkoani Dodoma leo,Mei 1,2016.Kutoka kushoto, ni Kaimu Murugenzi wa Bernard Konga,Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni PPF, William Erio na Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Eliud Sanga, wakiwa katika sherehe za Mei Mosi Mkoani Dodoma leo,

SHULE YA MSINGI GONGOLAMBOTO JESHINI YAIBUKA MSHINDI SHINDANO LA PUMA ENERGY TANZANIA.

0
0
KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania yawakabidhi zawadi washindi wa shindano la kampeni ya Usalama barabarani lililoshindanisha shule sita za jijini Dar es Salaam ambazo ni Maweni, Kimara Baruti, Oysterbay, Gongolamboto Jeshini na Mji Mwema.

Ndoto kubwa ya kampuni ya Puma Energy Tanzania  katika kuhakikisha usalama wa wanafunzi wakati wa kuvuka barabara ni kushirikisha shule zote za msingi Tanzania ili kuhakikisha watoto wako salama na ajali za barabarani.

 hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti  wakati akizungumza na wanafunzi wa shule za Msingi sita za jijini Dar es Salaam katika wa hafla fupi ya kutafuta mshindi na kumtangaza kutokana na mchoro alioutoa kama unahamasisha uasalama barabarani, katika shindano hilo shule ya Gongolamboto Jeshini iliibuka mshindi baada ya kushinda wanafunzi wawili wa mchoro bora zaidi ya wengine na shule ya msingi Oysterbay kuwa na mshindi mmoja.

Nae Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu 
 amewaasa madereva watakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali na madhara yanayojitokeza barabarani hasa wakiona wanafunzi wanavuka barabara, ikiwa takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa wanafunzi  78 walipoteza  na majeruhi  191 katika matukio tofauti hapa nchini 


 Maeneo hatari sana kwa wanafunzi kwa jijini la Dar es Salaam  amesema kuwa ni Lumumba, Mikumi, Mtambani, Boko-Basihaya Bunju na Kongowe.
.

 Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu  akionyesha mchoro wa Mwanafunzi Christina Christopher wa Darasa la saba shule ya Msingi Gongolamboto Jeshini (aliyeshika kikombe) mara baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililoandaliwa na kampuni ya mafuta ya Puma Energy Tanzania lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.



Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti akizungumza katika hafla ya kuwatangaza washindi wa kampeni ya Uasalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo jijini Dar es Salaam. Shindano hilo lililoshirikisha shule sita za jijini Dar es Salaam kama, Shule ya Msingi Maweni, Kimara Baruti, Oysterbay, Gongolamboto Jeshini na Mji Mwema. Katika shindano hilo shule ya Msingi Gongolamboto Jeshini iliyopo manispaa ya Ilala iliibuka mshindi kwa kuwa na wanafunzi wawili kwa kufanikiwa kuchora mchoro unaoweza kutoa tahadhari katika usalama barabarani.
 Mkurugenzi wa Afrika wa kampuni ya AMENDI, Tom Bishop akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi washindi wa shindano la kampeni ya usalama barabarani lililoandaliwa na kampuni ya Puma Enegy Tanzania jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu akizungumza na wanafunzi wa shule sita za jijini Dar es Salaam katika kutangaza mshindi wa shindano la Kapeni ya Usalama barabaranu kwa shule za msingi na kutangaza mshindi wa shindano hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Kauli mbiu ya kuwalinda watoto na ajali za barabarani ambayo ni "Kwa pamoja hatutaki ajali tunataka kuishi na maendeleo" alisema Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) huyo.

Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi za jijini Dar es Salaam wakiwa katika hafla ya kuwatafuta washindi wa shindano la kampeni ya usalama barabarani kwa shule za msingi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meza kuu wakiwa katika hafla ya kuwatafuta na kuwakabidhi washindi wa shindano la kampeni ya Usalama barabarani kwa shule za msingi sita za jijini Dra es Salaam.
 Mwalimu akiwaelezea wanafunzi wake igizo la jinsi ya kuepukana na ajali za barabarani.
 Mshehereshaji akiwasaidia wanafunzi kuimba wimbo wa kuhamasisha usalama barabarani wakati wanafunzi wanavuka barabara.

 Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu akionyesha picha ya mshindi wa tatu katika shindano la Kampeni ya Usalama Barabarani kwa shule za msingi shindano lililodhaminiwa na kampuni ya Puma Energy Tanzania. Mshindi wa Tatu ni Shaib Abdala darasa la 5 wa shule ya msingi, Gongolamboto Jeshini. kushoto aliyeshika begi ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti.

 Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu akionyesha picha ya mshindi wa pili katika shindano la kuchora mchoro unaotoa taarifa ya usalama barabarani, Abdala Husein wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
 Mshindi wa Kwanza wa shindano la Kampeni ya usalama Barabarani kwa shule za Msingi, Christina Christopher Darasa la Saba Shule ya Msingi, Gongolamboto Jeshini akisaidiwa  kutembea mara baada ya kutangazwa ndiye aliyechora mchoro mzuri zaidi ya wengine na kutangazwa kuwa mshindi wa shindano hilo na kupata mfano wa hundi ya shilingi milioni mbili kwaajili ya vitabu vya shule anayesoma.
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti akimkabidhi mwalimu wa shule ya Msingi ya ongolamboto Jeshini, Hashim Kalya akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni mbili mara baada ya  wanafunzi wa Darasa la saba wa shule hiyo Christina Christopher Kushoto mbele aliyeshika kombe ambaye ni mshindi wa kwanza wa shindano la Usalama barabarani kwa shule za Msingi.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsalrtti na  Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP), Fortunatus Musilimu wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa manispaa ya Ilala na Kinondoni pamoja na wanafunzi walioshinda katika shindano la usaama barabarani kwa shule za msingi za jijini Dar es Salaam.

SIKU YA MADANSA DUNIANI KUDHAMINIWA NA NSSF

0
0

 Wafanyakazi wa NSSF wakimkabidhi fulana mteja wao, Antela Salumu (katikati).
Ofisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim Kimaro, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya madansa duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na NSSF.  (Na Mpiga Picha Wetu)
 Ofisa Mwandamizi  Masoko na Uhusiano NSSF, Amina Mbaga, (kushoto) akimkabidhi fulana,  Jumanne Mnola alipotembelea banda la NSSF wakati wa uzinduzi wa siku ya madansa duniani iliyofanyika viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF.

 Ofisa Mwandamizi  Masoko na Uhusiano NSSF, Amina Mbaga, (kushoto), akimkabidhi fulana mmoja wa wateja wao, Said Ally, alipotembelea banda lao wakati wa uzinduzi wa siku ya madansa duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya TCC Club jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na NSSF.
 Ofisa Mwandamizi  Masoko na Uhusiano (Nssf), Amina Mbaga akigawa vipeperushi kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda lao.

 Ofisa Uhusiano wa NSSF, Faides Mdee, akigawa vipeperushi kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda lao katika uzinduzi wa siku ya madansa duniani uliofanyika kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe jijini Dares Salaam, mwishoni mwa wiki. Uzinduzi huo ulidhaminiwa na NSSF.

 Ofisa wa NSSF, Innocent Shao, (kulia) akiwaandikisha baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na NSSF walipotembelea banda la NSSF katika uzinduzi wa siku ya madansa duniani iliyoadhimishwa kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe na kudhaminiwa na NSSF.

Ofisa uandikishaji NSSF, Amina Kisawaga (kulia) akitoa maelezo kwa mteja alietembelea banda lao Fumbwe Juma, katika uzinduzi wa siku ya madansa duniani uliofanyika kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Dar es Salaam na kudhaminiwa na NSSF.

Picha ya pamoja.

BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR (ZFDB) YAHARIBU TANI 42.2 ZA BIDHAA ZISIZOFAA KWA MATUMIZI YA BINADAMU

0
0
Wafanyakazi wa ZFDB wakipakia shehena ya bidhaa zilizoharibika tayari kwenda kuangamizwa katika Dampo la Kibele Mkoa Kusini Unguja.
Bidhaa mbali mbali zilizoharibika zikiteremshwa kutoka kwenye gari na wafanyakazi wa Bodi ya chakula na Vipodozi katika Dampo la Kibele kwa ajili ya kuangamizwa.Bidhaa mbali mbali zilizoharibika zikiteremshwa kutoka kwenye gari na wafanyakazi wa Bodi ya chakula na Vipodozi katika Dampo la Kibele kwa ajili ya kuangamizwa.
Mkuu wa Idara ya Usalama na Ubora wa chakula wa ZFDB Aisha Suleiman Mubandakazi akizungumza na waandishi wa habari juu ya zoezi la kuangamiza bidhaa mbali mbali zilizoharibika na zilizokatazwa kwa matumizi ya binadamu.Mkuu wa Idara ya Usalama na Ubora wa chakula wa ZFDB Aisha Suleiman Mubandakazi akizungumza na waandishi wa habari juu ya zoezi la kuangamiza bidhaa mbali mbali zilizoharibika na zilizokatazwa kwa matumizi ya binadamu.
Bordoza la Manispaa ya Zanzibar likiwa kazini kuangamiza bidhaa hizo katika eneo la Kibele Mkoa Kusini Unguja.
Wafanyakazi wa ZFDB wakiongozwa na Mkuu wa operesheni ya uangamizaji bidhaa zilizoharibika Abdulaziz Shaib Mohamed (katikati) mwenye shati wakifuatilia uangamizaji wa bidhaa hizo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

TAARIFA KUTOKA MAKAO MAKUU YA JKT.

0
0

Airtel Fursa yasaidia kikundi cha Vijana Wajasiriamali katika mradi wa kutunza mazingira

0
0
 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (Kushoto), akikabidhi vifaa vya usafi kwa mmoja wa wakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (kulia), ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la Dodoma, walivyowakabidhiwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, hapo jana. Wanaoshuhudia (kutoka kulia) ni Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao akifuatiwa na  meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno na  wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.
 Mwakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (kulia), akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa na Airtel Tanzania, msaada wa pikipiki 2 za  magurudumu matatu aina ya Toyo, malighafi na vifaa mbali mbali vya shughuli za usafi, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo lao la biashara Majengo jijini Dodoma hapo jana.Akishuhudiwa na Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kushoto),akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno na Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao.
 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati), akikabidhi vifaa vya usafi kwa mmoja wa wakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (wanne kulia), ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika jiji la Dodoma, walivyowakabidhiwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, waliopo Majengo  jijini Dodoma hapo jana. Wanaoshuhudia (wane kulia) ni Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao na wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.

 Diwani wa kata ya Majengo Dodoma, Msinta Mayaoyao (pili kushoto) akitoa maneno machache katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya usafi ambapo kikundi cha Pambana kilikabidhiwa  msaada wa pikipiki 2 za  magurudumu matatu aina ya Toyo, malighafi na vifaa mbali mbali vya shughuli za usafi, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, hapo jana. Akisikilizwa na afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati), Meneja masoko wa Airtel Dodoma Hendrick Bruno (kulia) na wanakikundi wa Pambana wapatao vijana 30 na walezi wa kikundi hicho.
Mwakilishi wa kikundi cha Pambana Amasha Zuberi (pili kulia) kilichopo Majengo Dodoma akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa funguo ya pikipiki aina ya Toyo na afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki, (tatu kushoto), kwa ajili ya shughuli zao za usafi, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika katika eneo lao la biashara Majengo jijini Dodoma hapo jana.

  • Airtel Fursa imewapatia pikipiki mbili aina ya Guta, na vifaa vya kufanyia usafi kwa kikundi cha Pambana
 Dodoma, Jumapili 1 Mei 2016, Pambana ni kikundi cha vijana 30 wajasiriamali kinachojishughulisha  na shughuli mbalimbali katika jamii kama kukusanya taka, kuzalisha na kusambaza sabuni na kuchomelea vyuma mjini Dodoma, ambao leo wamepokea vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 17 kutoka Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel FURSA. Kundi hili limepokea vifaa mbalimbali vikiwemo pikipiki  mbili aina ya Guta, sare za kufanyia kazi, mabuti, reki ya chuma, ufagio mgumu na  vifaa vingine vya usalama vya kufanyia kazi zao. 
Afisa uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki aliwapongeza kikundi cha Pambana kwa juhudi zao na kufanya kazi kwa bidii. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano alisema, " Tumeamua kutoa vitendea kazi vya usafi ili kuweza kuungana na kikundi hiki katika kufikia lengo kuu la kuhakikisha maeneo yanayozunguka jamii yanakuwa katika hali ya usafi na hivyo kuchangia katika mikakati ya kutunza mazingira kwa ujumla.  Sambaba na hili Airtel imeona nia na juhudi zao kikundi hiki na ndio maana leo imewakabidhi vifaa vitakavyowawezesha kufanya kazi kwa haraka na kukuza biashara yao". 
"Kikundi cha Pambana kimeshapata mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kupitia Airtel FURSA na wataendelea kupata ushauri na uongozi kutoka kwa washauri wa Airtel FURSA ili kuwawezesha kuimarisha biashara yao " aliongeza Kaniki."Kama kampuni ya simu inayojali jamii yake, tumeahidi  kuwawezesha vijana hapa nchini kwa kuwawezesha kwa njia mbalimbali ili waweze kufikia ndoto zao." alisema Kaniki.
Kwa upande mwingine kundi la Pambana waliahidi  kuweka ujuzi wao wote na kutumia kwa umakini vifaa vilivyotolewa  kwao na Airtel kwa matumizi bora na yaliyo sahihi.Kiongozi wa kikundi hicho, Amasha Zuberi, aliishukuru Airtel kwa msaada na kutoa wito kwa mashirika mengine hapa nchini  kuuunga mkono mpango wa Airtel katika kusaidia vijana zaidi katika Jamii.
"Hatukuamini siku moja tutakuwa na uwezo wa kufikia malengo yetu katika biashara hii, tunaahidi kuweka juhudi zaidi na kutumia vifaa hivi na mafunzo tuliyopata kwa umakini zaidi kuhakikisha tunainua zaidi biashara yetu," alisema Amasha.
Kwa upande wake, wakati wa hafla ya makabidhiano, Diwani wa kata ya Majengo, Msinta Mayaoyao alitoa wito kwa vijana kutumia program hiyo ya Airtel Fursa kujiendeleza. Huku akiwaomba watanzania kuwapendekeza vijana wote wanaoona wanafaa kufaidika kwa mradi huo kwa manufaa ya jamii zao kwani Airtel FURSA ipo kwa ajili ya kubadilisha maisha ya vijana hapa nchini.
Airtel FURSA, inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa uwezeshaji kwa vijana ili kuhakikisha kuwa wanafikia ndoto zao.Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo.
Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com.  ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, aina ya biashara na sababu ya kuomba msaada kutoka Airtel.


MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI 2016 YAFANYIKA KITAIFA JIJINI MWANZA.

0
0
Bi.Valerie Msoka kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), akiongoza kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa mwaka 2016 yanayofanyika kitaifa katika hoteli ya ufukweni ya Malaika Jijini Mwanza.

Na George Binagi

Kauli mbiu ya Maadhimisho haya mwaka huu ni "Kupata Taarifa ni Haki yako ya Msingi:Idai'". Maadhimisho haya yanafanyika kitaifa kwa mara ya nne na yanalenga kukumbusha Umma na dunia kwa ujumla umuhimu wa vyombo vya habari kufanya kazi yake bila kuingiliwa na mtu ama chombo chochote. 

Zaidi ya wadau 250 wakihusisha waandishi wa habari wakongwe na wapya, wahariri, viongozi wa mashirika wahisani (ya kimataifa na ya hapa nchini) wawakilishi wa mihili ya nchi, wasomi wa vyuo vikuu na balozi mbalimbali wamekusanyika jijini hapa kwa maadhimisho hayo ambayo kilele chake ni kesho.
Watoa Mada katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2016 yanayofanyika Jijini Mwanza. Kilele cha Maadhimisho hayo kinafanyika kesho Mei 3,2016 ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman. Pia Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Nhaute pamoja na wageni wengine waalikwa wanatarajia kuhudhuria maadhimisho hayo.
Watoa Mada katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2016 yanayofanyika Jijini Mwanza. Kilele cha Maadhimisho hayo kinafanyika kesho Mei 3,2016 ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman. Pia Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Nhaute pamoja na wageni wengine waalikwa wanatarajia kuhudhuria maadhimisho hayo.
Usia Nkhoma Ledama ambae ni Afisa Habari kutoka UN Information Centre (Tanzania) akiwasilisha Mada katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.
Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.
Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.
Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.
Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.
Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.

UKURASA MPYA WA KIPINDI CHA JOTO LA ASUBUHI CHA EFM 93.7

0
0
Watangazaji mahiri Gerald Hando na Paul James (PJ) wameanza rasmi kutangaza 93.7 Efm redio siku ya leo ya tarehe 02/05/2016 katika kipindi cha Joto la asubuhi kilichoboreshwa wakiwa pamoja na Adela Tilya live nje ya jengo la K- net house zilipo ofisi za E fm. Kipindi hiki kinarushwa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 12:00 hadi saa 3:00 Asubuhi. Usipitwe.
 Kutoka kushoto ni Gerald Hando, Adella Tillya, pamoja na Paul James wakitangaza kipindi cha JOTO LA ASUBUHI live chini ya jendo la K-net house Kawe Beach Dar es salaam leo asubuhi.
  Rdj Spar akisababisha muziki live katika kipindi hicho asubuhi ya leo
  Timu nzima ya Joto la Asubuhi katika picha ya pamoja na baadhi ya mashabiki wa Efm Redio walioshiriki katika kipindi hicho
 Timu nzima ya joto la asubuhi pamoja na Rdj spar,
Gerald Hando akiwa katika picha ya pamoja na Baba yake mzazi  pamoja na dada yake walipofika katika ofisi za EFM  redio kumpongeza.

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM (BARA) MANGULA AKUTANA NA WAZIRI MAMBO YA NJE KUTOKA CHINA MJINI DODOMA

0
0
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara ) Mhe. Philip Mangula akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo wa CPC Mhe. Guo Yezhou mjini Dodoma ambapo walizungumzia mahusiano imara kati ya Tanzania na China pamoja na mipango mbali mbali ya kimaendeleo.
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dodoma Mhe. Adam Kimbisa akifafanua jambo wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Mbao ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha Watu wa China Mhe. Guo Yezhou mjini Dodoma.BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAKONDA AJA NA MBINU MPYA KUTAFUTA WATUMISHI HEWA.

0
0
 Wakuu wa Idara mbalimbali  wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wakiapa kiapo cha mkataba wa kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jijini la Dar es Salaam leo walipo apishwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wakuu wa wilaya, wakurugeni pamoja na wakuu wa idara mabalimbali za manispaa na jiji la Dar es Salaam leo.Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi(katikati) na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
 Wakuu wa Idara mbalimbali  wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wakisaini mkataba wa kutafuta watumishi hewa katika manispaa zao jijini Dar es Salaam, na atakaye shindwa kuwajibika  katika kufanya kazi  na baadae wakija kujulikana atawajibishwa yeye.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapa mkataba wa wiki moja wakuu wa Idara za Manispaa za jiji la Dar es Salaam kutafuta watumishi hewa.

Wakuu wa Idara za Manispaa watakaoshindwa kufanya hivyo wataundiwa tume ambayo itapita katika manispaa hizo kuhakiki watumishi hewa na endapo watumishi hewa wakibainika kuwepo mzigo utabebwa na wakuu wa Idara kulipa mishahara hewa hiyo.

Makonda ameyasema hayo leo wakati alipokutana na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Pamoja na Wakuu Idara mbalimba za manispaa za jiji la Dar es Salaam, amesema kuwa mkataba huo kila mtu lazima afanye kazi  na sio  na  kukimbizana au kuamrishishana.

 Amesema kuwa mara ya kwanza walipatikana watumishi 71 lakini baada ya kuweka mkazo wamefikia 209 ambao wanalipwa zaidi ya sh.bilioni 2.9 ambapo fedha hiyo zingefanya kazi nyingine ya kutoa huduma kwa wananchi.

Aidha amesema kuwa watumishi wamekuwa wakifanya kazi kwa kusukumana wakati kazi hiyo waliomba wenyewe na kuahidi kutekeleza majukumu yao.

Amesema kuwa kwenda kuangalia vitu vya kihuduma kwa wananchi sio yake, lakini inatokana na wale wenye wajibu wa  kutekeleza majukumu yao kufanya uzembe tu.

 Makonda amesema kuwa zoezi la kutafuata watumishi hewa lazima lifike kikomo na kuweza kufanya mambo mengine ya kutatua changamoto za wananchi ambazo zimetokana na watu kujisahau kutimiza wajibu wao.

TADB YAASWA KUTOA ELIMU KUHUSU KILIMO BORA.

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Lephy Gembe (Kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Robert Paschal (Kushoto) wakati akitoa maelezo kuhusu Wajibu wa TADB katika kuendeleza kilimo nchini.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilombero,  Bw. Lephy Gembe (Katikati) akizungumza na maafisa wa kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake. Wanaomsikiliza ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (Wapili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa TADB, Bw. Geofrey Mtawa (Kulia) na Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi wa TADB, Bw. George Nyamrunda (Kushoto).
 Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Robert Paschal (Kushoto) akimsikiliza i Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Lephy Gembe (Kulia) walipomtembela Ofisini kwake.

Na Mwandishi wetu.
Benki mpya ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeaswa kutoa elimu kuhusu kilimo bora ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero,  Bw. Lephy Gembe wakati akiongea na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal alipomtembelea Ofisini kwake.

Bw. Gembe alisema kuwa ili kuinua uzalishaji wenye tija katika Sekta ya Kilimo kwa kuendeleza TADB ina wajibu wa kutoa elimu ya kina kuhusu kilimo cha kisasa kwa kutilia mkazo kuhusu miundombinu muhimu ya kilimo mathalani skimu za umwagiliaji za kilimo ili kuongezea tija shughuli hizo za kilimo.

“TADB muna wajibu wa kuhamasisha kilimo cha kisasa na cha kibiashara kwa wakulima wadogo wadogo ili waweze kubadilisha fikra zao kutoka kilimo cha mazoea na kufikiria kilimo cha kisasa chenye tija kitakachoongeza kipato cha wakulima hao,” alisema Bw. Gembe.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Kilombero aliongeza kuwa TADB inapaswa kutekeleza kwa vitendo juhudi za Serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania kupitia kilimo ambacho kwa mujibu wa takwimu kinaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya  asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.

Bw. Gembe alisema kuwa ili kufikia malengo yake TADB inapaswa kuwa na wataalamu wa utafiti na maendeleo ili waweze kuratibu taarifa za utafiti na maendeleo ya Kilimo, hali ya hewa, udongo unaofaa kwa Kilimo, pamoja na hatua nyingine za kuhuisha maendeleo kwenye Kilimo.

Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal alisema kuwa TADB imejipanga kutoa mikopo ya kilimo katika makundi matatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi, Mikopo ya Muda wa Kati na Mikopo ya Muda Mrefu kwa kutumia njia mbalimbali.

Akizitaja njia ambazo TADB inatumia kutoa mikopo hiyo, zinajumuisha pamoja na mambo mengine, mikopo ya moja kwa moja kwa vikundi vya wakulima wadogo wadogo;  kutoa mikopo kwa njia ya marejesho taasisi zinazokopesha; utoaji wa mikopo kwa pamoja na kushirikiana na taasisi/benki zingine; pamoja na mikopo ya miundombinu inayolenga kupunguza mapengo ya upatikanaji wa fedha katika minyororo ya ongezeko la thamani ya kipaumbele.

Bw. Paschal aliongeza kuwa kwa kuanzia, TADB imelenga uwekezaji katika maeneo nane (8) ya minyororo ya uongezaji wa thamani ambayo ni: nafaka, kilimo cha mbogamboga, kilimo cha bidhaa za  viwanda, mbegu za mafuta, ufugaji wa ng’ombe, ufugaji kuku, ufugaji wa samaki na bidhaa za misitu.

Aliongeza kuwa Benki pia inajitahidi kusimamia fedha kutoka kwa wafadhili wengine ambazo zimeelekzwa kwenye kuendeleza kilimo.

Mkurugenzi huyo wa Mikopo alitumia fursa hiyo kumuomba ushirikiano Mhe. Gembe ili kuhakikisha mikopo hiyo inarudishwa kwa wakati.

“Ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, TADB inafanya kazi kwa karibu na washirika mbalimbali wa kimkakati pamoja wadau wengine muhimu kutoka ndani na nje ya nchi, hivyo ukiwa ni mdau muhimu, tunakuomba ushirikiano katika kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa TADB,” aliomba Bw. Paschal.

Kwa mujibu wa Bw. Paschal wadau wengine wa TADB ni pamoja na Serikali, Wizara na Wakala mbalimbali wa Serikali; Mashirika; Serikali za Mitaa, Sekta Binafsi, benki na taasisi za fedha, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Wafadhili wa ndani na wa Kimataifa, Taasisi za Utafiti na Umma kwa ujumla.

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016.PICHA NA IKULU.

MAMIA KUTOKA KILA PANDE ZA MAREKANI WAMUAGA ANDREW SANGA HOUSTON - TEXAS

0
0

Hapa ni mzazi mwenzie Andrew na mtoto wao mpendwa Zoe wakiwa mbele ya mwili wa marehemu.Mwili wa marehemu utawasiri Dar Es Salaam siku ya jumanne  na jumatano ndugu na jamaa wa Dar_Es_Salaam  wata Ibada ya misa na kuaaga mwili ndani ya kanisa la Lutheran nyuma ya Ubungo Plaza siku ya jumatano asubuhi kisha safari ya Dodoma jioni na mazishi yatafanyika siku ya Alhamis May 05.
Mwakilishi wa ubalozi wa Tanzania hapa Marekani angeongea mbele ya watu waliojitokeza ndani ya kanisa kwa ajili ya Ibada ya misa na kuaga mwili wa Andrew.
Mzazi mwenza wa marehemu Andrew akitoa neno mbele  ya watu waliojitokeza kuja kuaga mwili wa marehemu. 
Wash kutoka Ohio akiwa  na majonzi mbele ya mwili wa marehemu 
Majonzi kwa kila mmoja aliepita mbele ya mwili marehemu.

Ny Ebra kutoka New York nae ni mmoja kati ya watu waliotoka nje ya Houston, Texas kwaajili ya kuaaga mwili wa Andrew, hapa Ebra akipata ukodak na Emmy mzazi mwenza wa marehemu Andrew na mtoto wao Zoe nnje ya kanisa baada ya kuaaga mwili pamoja na Ibada ya misa. 
Mzazi mwenza wa marehemu Emmy Matafu pamoja na mtoto wake Zoe katikati. 
Marafiki kutoka North Carolina na Atalanta .


VYETI VYA KUZALIWA WILAYANI MICHEWENI PEMBA HAVITOLEWI KWA MISINGI YA KISIASA

0
0


Na Masanja Mabula –Pemba

SERIKALI ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba imekanusha taarifa zilizotolewa na wananchi ya kwamba vyeti vya kuzaliwa katika Wilaya hiyo hutolewa kwa misingi ya kisiasa .

Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Abeid Juma Ali aliyaeleza hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara ambao baadhi yao waliodai kwamba kuna ubaguzi juu ya utoaji wa vyeti vya kuzaliwa

Alisema kuwa kwa kipindi cha miezi mitano tangu ashike wadhifa huo tatizo la upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto katika wilaya hiyo limeanza kupatiwa ufumbuzi .

Alifahamisha kuwa kwa kushirikiana na watendaji wa Ofisi ya Vizazi na Vifo , ameanza kulipunguza tatizo hilo , ambapo watoto wengi wameweza kupatiwa vyeti kwa wakati na bila usumbufu .

“Mtoto hana chama iweje basi nimbague kwa misingi ya siasa , natambua wajibu na majukumu yangu kwani mimi ni mtumishi wa umma na ninawatumikia wananchi wote pasi na ubaguzi ”alifahamisha .

Awali mfanyabiashara Ali Salimu Ali (Baraka) wa Wingwi alisema kwamba kunahitaji kuangaliwa upya Ofisi inayohusika na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwani imekuwa ikichelewesha kupatikana kwa vyeti kwa baadhi ya watoto .

Alieleza kwamba wapo watoto wamefikia umri wa kwenda skuli lakini hawana vyeti vya kuzaliwa , licha ya kwamba kumbukumbu zao zipo katika Ofisi ya vizazi na vifo lakini zimeshindwa kufanyiwa kazi .

“Vyeti vya kuzaliwa bado ni tatizo , kwani kuna baadhi ya watoto wamefikia umri wa kuanza skuli , lakini hawana vyeti , tunaomba hii Ofisi inayohusika na utoaji wa vyeti uiangalie upya nahisi kama kuna ubaguzi fulani hivi ”alisema .

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Madiwani wa Wilaya hiyo ambapo Mkuu wa Wilaya alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara kuwapa ushirikiano wakati wanapokusanya mapato yatokanayo na biashara zao.

SERIKALI KUTUMIA DOLA MILIONI 690 KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA BANDARI YA DAR ES SALAAM

0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Injinia Alois Matei akiwaeleza waandishi habari kuhusu mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam utakaogharimu kiasi cha Dola za Marekani milioni 690 ambapo mradi huo unafadhiliwa na Serikali, Benki ya Dunia,Trade Mark East Afrika na DFID, kulia ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka hiyo Bw. Focus Mauki na mwisho Kapteni Abdullah Mwingamno wa TPA Bandari ya Dar es Salaam.
Mhandisi Mkuu wa TPA Bi Mary Mhayaya akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa Flow meter mpya ya Kigamboni ambao umeshakamilika na hivyo kuwezesha mafuta yote yanayoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam kupimwa na kujulikana kiasi halisi kilichoingizwa hapa nchini ili kuiwezesha Serikali kupata mapato stahiki ikiwemo kodi .
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya Mamlaka ya Bandari TPA iliyokuwa ikitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Injinia Alois Matei kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezi leo.

LIFE FORMULA FAMILY MFUMO MPYA WA KUJIKWAMUA KIUCHUMI KATIKA TASNIA YA SANAA

0
0
Beatrice Lyimo-MAELEZO

KAMPUNI ya Dream Success Enterprises kwa kushirikiana na kampuni ya Bid Production wameanzisha mfumo mpya wa kiuchumi ujulikanao kama “Life Formula Family (LFF)” kwa ajili ya kubuni masoko na mtaji katika tasnia ya Sanaa nchini.

Mfumo huo unatarajia kuzalisha wawekezaji Wazawa na Wafanyabiashara wakubwa na hivyo kuipaisha sanaa ya Tanzania katika ngazi za kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Bid Production, Bw. Fadhili alisema kuwa kampuni hiyo ina lengo la kuhamasisha wahitimu wa vyuo vikuu nchini kuanzisha makampuni na kujiajiri na hivyo kuondokana na tatizo la ajira kwa vijana.Matekela alisema kuwa mfumo huo wa Life Formula Family unatarajia kuanza na Watu Milioni 5, ambapo mwanachama atakejiunga atapatiwa namba maalum ya utambulisho.. 

“Filamu zitakazoingizwa katika mfumo huu zinatarajiwa kuuzwa Tsh. 3,000 kwa wakazi wa jijini dare s salaam na kwa upande wa wakazi wa mikoani itategemea na gharama za usafirishaji” alisema Mateleka.

Aliongeza kuwa kampuni yake pia inatarajia kuendesha kongamano maalum lijulikanalo kama la “Sitaki kuajiriwa” ambalo litawahusisha wahitimu wa vyuo vikuu nchini, ambapo watajadiliana kwa pamoja tatizo la ajira kwa vijana na hatua za kukabiliana na tatizo hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Dream Success Enterprises, Charles Makoba alisema taasisi imeunga mkono kwa vitendo Hatua za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mkakati wa kutumbua majipu, hivyo taasisi yake imekusudia kutumbua jipu la ukosefu wa ajira kwa vijana.

“Tumeamua kuanzisha kampeni ya “Sitaki Kuajiriwa” kwa kuhimiza wahitimu na wanavyuo kuanzisha makampuni yao, na tayari kampuni ya kwanza ya Bid Production imeshajiliwa na tumeungana katika kuendesha kampeni ya Sitaki kuajiliwa” alisema Makoba.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI.

0
0
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI.
Katika Tukio la Kwanza:

Mtoto wa miaka mitatu aliyefahamika kwa jina la JANET PONSIAN mkazi wa Matemela Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na Gari yenye namba za usajili T.957 CWJ aina ya Isuzu Journey ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la ELIABU MYEKO (33) mkazi wa Makambako Mkoa wa Njombe.


Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 01.05.2016 majira ya saa 17:45 jioni huko katika Kijiji cha Matemela, Kata ya Ipwani, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya.


Aidha chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na uzembe wa Dereva wa Gari hilo. Dereva alikimbia mara baada ya tukio na jitihada za kumtafuta kwa kushirikiana na mmiliki wa Gari zinaendelea. Mwili wa marehemu umehifadhi Kituo cha Afya Ipwani Wilayani Mbarali kwa uchunguzi wa kitabibu.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi EMANUEL G. LUKULA anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa dereva huyu azitoe kwa mamlaka husika ili akamatwe.


Katika Misako:

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Matemela aliyefahamika kwa jina la HUSSEIN BAKARI (59) baada ya kukutwa na miche 25 ya Bhangi akiwa amepanda kwenye bustani yake ya mbogamboga.

Mtuhumiwa alikamatwa katika msako uliofanyika mnamo tarehe 01.02.2016 majira ya saa 16:00 jioni katika Kijiji cha Mayota, Kata ya Lugelele, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya.


Aidha katika msako mwingine, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la WILSON PHILIP (19) mwendesha Pikipiki @ bodaboda, mkazi wa Msasani anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya akiwa na Bhangi yenye uzito wa Gram 10.


Mtuhumiwa alikamatwa na askari katika msako uliofanyika mnamo tarehe 01.05.2016 majira ya saa 17:05 jioni huko Mtaa wa msasani, Kata ya Bagamoyo, Tarafa ya Tukuyu Mjini, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.

Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamiliki.

Imesainiwa na:

(EMANUEL G. LUKULA – ACP)

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

WAZIRI MAKAMBA ASOMA BAJETI YA MAZINGIRA LEO BUNGENI MJINI DODOMA.

0
0
 Baadhi ya Wabunge wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
 Mashududa walihusika katika zoezi la kuchanganya udongo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964, wakiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa  mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wao katika kuuenzi na kuulinda Muungano wa Tanzania.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akitoa ufafanuzi kuhusu wizara hiyo leo Bungeni mjini Dodoma. 
 Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Andrea Kigwangalla (kushoto) akiwa Bungeni leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Dkt. Ashatu Kijaji.

 wanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement akiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa  mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wake kwenye  utunzaji wa mazingira. Mwanafunzi huyo alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani.
 Naibu Spika Dkt Tulia Ackson na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe January Makamba wakiwa katika picha ya pamoja na mashuhuda waliohusika katika zoezi la kuchanganya udogo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964. Mashuhuda hao walikuja kutembelea Bunge leo Mei 2, 2016.

(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma)
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images