Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRIL 30


MKUTANO WA WATAALAM WA UTHAMINI WA KUPITIA VIWANGO ELEKEZI VYA BEI YA SOKO LA ARDHI NCHINI 2016

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila pamoja na Kaimu Mthamini Mkuu wa Serikali Bi. Evelyin Mugashwa wakifuatilia taarifa ya viwango elekezi vya bei ya soko la Ardhi nchini katika mkutano na wataalam wa Uthamini Aprili 29, 2016.
Watalaam wa uthamini wa Serikali, Mashirika ya Umma na binafsi wakijadili taarifa ya viwango elekezi vya bei ya soko la Ardhi nchini iliyowasilishwa kwao na ofisi ya mthamini mkuu wa Serikali Aprili 29, 2016.

KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI CHAFUNGUA MAFUNZO YA KUPUNGUZA AJALI,VIFO NA MAJERUHI BARABARANI

$
0
0
Mwenyekiti wa kamati ya Bloomberg Initiative Global Road Safety Tanzania,Mrakibu Msaidizi wa Polisi Mathew Msuyale akimkaribisha mgeni rasmi(hayupo pichani)pamoja na wadau wa mafunzo hayo.
Kaimu kamanda kikosi cha usalama barabarani Tanzania,Kamishna Msaidizi wa Polisi Fortunatus Musilimu akifungua mafunzo kwa mawakili,waendesha mashitaka na askari wapelelezi wa kesi za ajali barabarani iliyoandaliwa na wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto kwa kushirikiana na shirika la afya Duniani kupitia mpango wa Bloomberg Initiative Global Road Safety,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mawakili,waendesha mashitaka na askari wapelelezi wa kesi za ajali barabarani wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani)wakati wa ufunguzi huo.Mradi wa Bloomberg una nia ya kupunguza ajali,vifo na majeruhi barabarani pamoja na kuweka vipaumbele kuzuia vyanzo hatarishi vya ajali kama mwendokasi,kutovaa kofia ngumu,kutofunga mikanda,vifaa maalum vya kuwakinga watoto kwenye magari na ulevi.
Baadhi ya wadau na askari wapelelezi wa kesi za a halo za barabarani wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo.Nchini takwimu zinaonesha ukubwa wa tatizo la ajali ni kubwa ambapo mwaka 2014 zilitokea ajali 14,360,vifo 3,760 na majeruhi 14,530 ukilinganisha na mwaka 2015 zilitokea ajali 8,337,vifo 3,468 na majeruhi 9,383.


Na. Catherine Sungura,WAMJW 

Wazazi nchini wametakiwa kuwakinga watoto wao wakati waendeshapo magari kwa kuhakikisha wanawafunga mikanda ili kuwaepusha na ajali za barabarani na kudhibiti madhara yatokanayo na ajali.

Rai hiyo imetolewa leo jijini hapa na kaimu kamanda kikosi cha usalama barabarani Tanzania,Kamishna Msaidizi wa Polisi Fortunatus Musilimu wakati akifungua mafunzo kwa Mawakili,Mahakimu ,Waendesha Mashitaka na Askari wapelelezi wa kesi za ajali za barabarani,iliyoandaliwa na wizara ya afya kwa kushirikiana na shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia mpango wa Bloomberg Initiative Global Road Safety.

Alisema wazazi wengi wanapokuwa wanaendesha magari hawawafungi mikanda watoto wao na hivyo ajali inapotokea watoto wanakuwa ni wahanga wakubwa kwa kupoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu

?Wazazi mnawalindaje watoto,baba anaendesha gari,mtoto yupo kwenye usukani anaendesha nae gari,hiyo siyo sahihi ,tuwalinde watoto wawe salama kwa kuvaa mikanda?

Aidha, Kamanda Musilimu alisema tatizo la ajali barabarani nchini imekua ikiongezeka kila mwaka na hii ni kutokana na wananchi kutokuona kama ajali ni tatizo kubwa na la haraka ambalo linafanya kuongezeka kwa vifo nchini kulinganisha na magonjwa mengine na hivyo kupoteza nguvu kazi ya taifa kiuchumi

?Watu bado hawaoni kama ajali ni tatizo ,vifo inatokea hapohapo na watoto wanabaki kuwa tegemezi,hizi ni changamoto hivyo mshirikiane kubadilishana uzoefu ili muweze kutatua kesi zote zinazowafikia na kupunguza malalamiko pamoja na kutenda haki,alisema

Takwimu za hapa nchini kwa miaka miwili zinaonesha mwaka 2014 zilitokea ajali 14,360,vifo 3,760 na majeruhi 14,530 na mwaka 2015 zilitokea ajali 8,337,vifo 3,468 na majeruhi 9,383,hata hivyo Ripoti ya Shirika la Afya Duniani ya mwaka 2015 zinaonesha ajali huua watu 1.25 milioni Duniani kila mwaka, watu kati ya 20 na 50 milioni hujeruhuwa kila mwaka na hivyo asilimia 90 ya ajali hizi na vifo hutokea katika nchi zenye uchumi wa kati na wa chini kama Tanzania.

Kamanda Musilimu alisema kasi hii ya ajali ikiendelea hadi ifikapo mwaka 2030,ajali itashika nafasi ya 5 kwa kusababisha vifo Duniani.

Mradi wa Bloomberg Initiatives ni mradi wa miaka mitano hapa nchini umeanzishwa mwaka 2015 ukiwa na nia ya kuweka vipaumbele vya kuzuia vyanzo vya ajali hatarishi kama vile mwendo kasi,kutokuvaa kofia ngumu,kutokufunga mikanda,vifaa maalumu vya kuwakinga watoto kwenye magari pamoja na ulevi.

BASATA KUAZIMISHA SIKU YA MUZIKI WA JAZZ

$
0
0
\
National Arts Council BASATA

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na Elimu na Sayansi (UNESCO) litaungana na wasanii mbalimbali nchini na wadau wa Sanaa kuazimisha siku ya muziki wa Jazz duniani ambayo kwa mara ya kwanza itaazimishwa nchini Mei 2, 2016.

Maazimisho hayo ambayo yatapambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa Wasanii wa muziki wa jazz hususan Band maarufu ya Das Jazz yanatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ofisi za BASATA Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

Sambamba na burudani hizo, kutakuwa na mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wadau wa muziki huu wa jazz ambazo zitalenga kuamsha ari, thamani na ufahamu wa muziki huu maarufu duniani miongoni mwa wasanii nchini.

Wawasilishaji wa mada hizo pamoja na mada zao kwenye mabano ni pamoja na John Kitime (Matumizi ya neno Jazz), Carola Kinasha (Uhusiano kati ya Elimu ya Muziki na Jazz) na Kurwigira Mareges (Historia ya Muziki wa Jazz) na Masoud Masoud (Ujue Muziki wa Jazz)

Mbali na burudani na mada hizo kuhusu muziki huo wa Jazz kutakuwa na wageni waalikwa kutoka kwenye balozi na vituo vya Utamaduni vya nchi mbalimbali zilizopo hapa Tanzania

BASATA linatoa wito kwa wasanii na wadau wa muziki huu wa jazz kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho haya ambayo yatakuwa yakifanyika kila mwaka sambamba na mataifa mengine duniani.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
Godfrey Mngereza
Katibu Mtendaji – BASATA

CCM MWANGA WAJIVUNIA KUTOVURUGWA NA WAPINZANI

$
0
0
Kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anapanda mti nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Mwanga
kaimu katibu mkuu UVCCM taifa akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Kileo iliopo ndani ya Wilaya ya Mwanga 
kaimu katibu mkuu UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anamkabidhi kiongozi wa timu ya Kileo jezi ambazo UVCCM mkoa wa Kilimanjaro waliaidi timu 
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma akiwa anapanda mti wa ukumbusho nje ya ofisi ya CCM wilaya ya mwanga 
Shaka akiongea na wanachama wa CCM wilaya ya Mwanga hii leo.

Na Woinde Shizza, Mwanga

Wanachama wa chama Mpinduzi wilaya ya Mwanga mkoa kiliimanjaro Wameeleza kuwa pamoja na kupita kimbunga cha siasa za maji taka zilizosheheni ushabiki , ubabaishaji na hujuma,Wana  CCM wilayani humo wamebaki wamoja bila kuyumbishwa na wanasiasa wasaka madaraka kwa njia za hila na fedha .

Wamesema kuwa wale wote ambao walifuata siasa za ushabiki kwa kushabikia mambo bila kupima uzani wa siasa na ubora wa kila chama,  sasa hivi wako katika dimbwi la majuto na fedheha kwani wameshaona hasara za kuhama chama hicho.

Katibu wa CCM wilaya ya Mwanga Mkoa kilimanjaro Mwanaidi Hussein Mbisha aliyasema hayo wakati akitoa neno la shukran mara baada ya Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka kuzungumza na viongozi wa vijiji na kata pamoja na wanachama wa chama hicho wilayani Mwanga mkoani hapa.

Mbisha alisema umadhubuti wa CCM usichukuliwe kama janbo jepesi na rahisi badala yake viongozi wa upinzani na wanachama wanaoshabikia vyama hivyo wakubali ukweli kuwa CCM iko imara .

Alisema CCM iliioachwa na marehemu baba wa Taifa Mwalimu julius Nyerere , Mzee Abeid Karume,Mzee Rashid Kawawa na mzee Thabit Kombo itabaki kuwa kimbilio na tarajio la wananchi katika kufanikisha masuala yao kisiasa, kijamii na kiuchumi.

"Shaka nimekuwa nikikusikiasikia tu na kukusoma katika vyombo vya habari,wewe bado kijana mdogo, ila unatosha kubeba hata dhamana kubwa, endelea Mungu atakusaidia uthibitishwe kuwa Katibu mkuu "alisema mbisha.

Awali Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Raibu Juma aliisifu wilaya ya mwanga kwa kuendelea kuwatoa mchanga wa macho kwa kuilinda jimbo hilo lisichukuliwe na upinzani.Raibu alisema heshima ya wana mwanga kwa ccm itaendelea kuenziwa na kukumbukwa kila wakati kwa sababu ni watu jasiri wenye msimamo thabiti.

"Unapokuwa vitani halafu wapiganaji wako wakakataa katakata kupokea hongo toka kwa maadui, wakasema hatutaki na hatufaiki chochote , hao ni wazalendo"alisema Juma

Hata hivyo Mwenywkiti huyo wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro alimpongeza Kaimu katibu mkuu shaka kwa uthubutu wake wa kupania kurudisha heshima na hadhi ya UVCCM iliyokuwa inapotea.Shaka anaendelea na ziara yake katika wilaya ya Same ambako atahitimisha katika mkoa kilimanjaro kabla ya kuanza mkoani Tanga kwa siku sita baadae Mikao ya Manyara,Kilimanjaro na Arusha itafanya majumuisho ya pamoja mkoani mkoani hapa.

MBATIA AMUONGOZA MKURUGENZI WA IDARA YA MAAFA NCHINI KUTEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA KWA MAFURIKO

$
0
0
Madereva wa bodaboda wakijaribu kupita katika eneo hilo kwa umakini mkubwa. 
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika kwa mafuriko.
 Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akizungumza jambo na Mkurugenzi wa idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya wakati wakitembelea kijiji cha Mandaka Mnono kujionea athari ya mafuriko,katikati ni Mbunge wa viti Maalum (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro Lucy Owenya. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya akimweleza jambo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila (wa tatu kutoka kushoto) wengine ni Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia,Diwani wa kata ya Mabogini Emanuel Mzava . 

 Baadhi ya wananchi katika kjiji cha Mandaka mnono ambao mashamba yao yameathirika kwa mafuriko. 


 Sehemu ya barabara inayounganisha vijiji vya Miwaleni na Mandaka Mnono ikiwa imeharibika vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko. 
 Usafiri wa pikipiki pekee ndio unatumika kuvusha watu kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine. 
 Hivi ndivyo hali inavyoonekana. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu,Mbazi Msuya akizungumza na wananchi katika eneo hilo lililoharibika vibaya. 
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

DAWA NA VIFAA TIBA KUWA NJIANI MIAKA MINNE BOHARI YA DAWA (MSD) YATOA UFAFANUZI

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akionesha moja ya nyaraka inayoonesha upelekaji wa dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu dawa za shilingi bilioni mbili kuwa njiani kutoka MSD Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwaka 2012.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Victoria Elangwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Sako Mwakalobo. 
 Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kulia), akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa MSD (kushoto), kuzungumza na wanahabari.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Terry Edward.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imetoa ufafanuzi kuhusu dawa za sh.bilioni mbili kuwa njiani kutoka Bohari ya Dawa ya Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwaka 2012.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema hakuna dawa ambazo ziko njiani tangu mwaka 2012 kutoka Bohari ya Dawa kwenda Muhimbili kama ilivyodaiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bungeni.

Bwanakunu alisema kuwa ripoti ya CAG ilionesha dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya sh.bilioni 2.03 havikuwa vimefika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu Mei 2012 licha ya kuonekana kwenye ankara 23 na Bohari ya Dawa.

"Tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa ankara hizo sio kwamba dawa hazikufika hospitalini hapo, bali hazikuonekana kwenye vitabu vya kupokelea mali vya Hospitali ya Muhimbili" alisema Bwanakunu.

Alisema kwamba baada ya kupitia nyaraka zake, Bohari ya Dawa mpaka sasa imefanikiwa kupata uthibitisho wa hati za kupelekea mali za dawa na vifaa tiba vyote vilivyopokelewa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambavyo ni pamoja na dawa za figo na moyo ambazo zilikwishapelekwa Muhimbili.

Aliongeza kuwa pamoja na juhudi za MSD imewasiliana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuainisha taarifa za kwenye ankara na shehena ya dawa na vifaa tiba vilivyopelekwa hospitalini hapo kwani utaratibu wa kupeleka na kukabidhi dawa hospitalini unamlazimu mpokeaji kusaini ankara ya kupeleka mali ambazo zote zipo MSD.

Akitolea ufafanuzi kuhusu picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii za gari aina ya lori lenye herufi "MSD" na kutoa maelezo kuwa ni gari la MSD amesema nembo inayoonekana kwenye gari hilo siyo ya Bohari ya Dawa.


Katika ripoti ya CAG ilionesha kwamba madawa na vifaa tiba ambavyo havikupokelewa kwa muda mrefu kutoka MSD vilikuwa vyenye thamani ya sh.bilioni 2.03 ambapo katika hali ya haikutajiwa kuchukua zaidi ya wiki moja kufikishwa sehemu husika ukizingatia ofisi zao ziko Dar es Salaam.

KUSANYIKO LA KUMUENZI MAREHEMU ANDREW NICKY SANGA KUFANYIKA KESHO 30.04.2016, TRIPLE 7 KAWE

$
0
0
Ndugu zetu pamoja na Marafiki zetu, wakati huu tukiendelea kuomboleza msiba wa mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga, tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa ushiriki wenu wa hali na mali katika kuandaa safari yake ya mwisho.

Katika kumuenzi na kukumbuka urafiki wake wa kipekee, Kamati ya Maandalizi ya Dar es Salaam inawaalika na kuwakaribisha katika kusanyiko la kumuenzi jioni ya tarehe 30 April 2016 kuanzia saa 11 jioni pale Triple 7 (@777). Kusanyiko hili ni mahsusi kwa mambo mawili makubwa, moja likiwa ni kukumbuka na kuenzi maisha yake katikati yetu na pili kupashana habari za kuhitimisha maandalizi ya Safari ya kumuweka katika nyumba yake ya Milele.

Naomba tujumuike wote na tunaamini hata huko aliko atafurahi tunapomkumbuka.


Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe


Imetolewa na Dr. George Longopa

KNY Kamati ya Maandalizi ya Dar ES SALAAM
Simu 0754 870969.

UCHUKUZI SC VINARA MEI MOSI WATWAA VIKOMBE 11

$
0
0
Mwanaisha Athuman wa Uchukuzi SC akipokea kombe la ubingwa wa netiboli kutoka kwa mgeni rasmi Mwenyekiti TRAWU, Mussa Kalala, katika mashindano ya Mei Mosi.Wachezaji wa Uchukuzi SC wakiwa wamevipanga vikombe 11 walivyotwaa kwenye michezo mbalimbali ya Mei Mosi, iliyomalizika juzi mkoani Dodoma.Bingwa wa baiskeli Chaptele Muhumba wa Uchukuzi SC akiwa amekumbatia kombe alilotwaa kwenye mashindano ya Mei Mosi.Wachezaji na viongozi wa Uchukuzi SC wakishangilia baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya Mei Mosi yaliyomalizika juzi mkoani Dodoma. 

TIMU ya Uchukuzi SC iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, imeibuka kinara kwenye mashindano ya Mei Mosi baada ya kutwaa vikombe 11 vya michezo mbalimbali.

Timu hiyo imetwaa ubingwa katika michezo ya netiboli, baiskeli na bao (wanaume), kamba (wanawake na wanaume); huku vikombe vya ushindi wa pili ni vya michezo ya bao (wanawake) na draft (wanaume); wakati vya ushindi wa ni katika soka, karata (wanaume), riadha (wanawake na wanaume).

Hatahivyo, kutokana na uwingi wa vikombe timu hiyo inatarajia kutangazwa mshindi wa  jumla kesho kwenye sherehe za Mei Mosi na kukabidhiwa kombe na Mh. Rais John Magufuli.Timu nyingine na idadi ya vikombe zilizopata ni Tamisemi saba kikiwemo cha ubingwa wa soka baada ya kuwafunga GGM katika fainali kwa magoli 2-0, huku TPDC wakiwa na vikombe vitano sawa na Tanesco.

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wamejikusanyia vikombe vinne, Ujenzi vikombe viwili, na Mawasiliano, Ukaguzi na Halmashauri ya Nyasa kila mmoja wana kikombe kimoja kila mmoja.Awali katika michezo iliyochezwa jana timu ya Uchukuzi SC iliwafunga Tamisemi kwa magoli 18-15 katika mchezo wa netiboli, ambapo wafungaji wake Tatu Kitula na Matalena Mhagama waliwapeleka puta wapinzani wao na hadi mapumziko walikuwa mbele kwa magoli 11-7.

Washindi wote walikabidhiwa kombe na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU), Mussa Kalala, ambaye katika hotuba yake aliwashutumu viongozi walioshindwa kupeleka timu zao kwenye mashindano hayo na kusema michezo mahala pa kazi husaidia kuijenga miili ya wafanyakazi kuendelea kuwa mikakamavu na kuwa na afya bora, ambapo hutoa huduma bora iliyotukuka na kuzalisha  tija zaidi.

Naye Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya Mei Mosi, Joyce Benjamin alisema wamesikitishwa na ushiriki wa timu chache mwaka huu, ambazo ni 11 pekee ukilinganisha na mwaka jana zilikuwa 28.

“Pamoja na kamati yetu kusikitika kwa uchache wa timu zilizoshiriki katika michezo ya mwaka huu, hata mkuu wa mkoa katika hotuba yake ya uzinduzi wa michezo hii naye alisikitika ambapo wote kwa pamoja tumesikitishwa sana na viongozi wengi kutoleta timu zao hatujii kwa sababu ya kumuogopa Mh. Rais pengine kwanza labda amekataza michezo, au wana sababu zingine tu zao binafsi,” alisema Benjamin.

SHAKA ITAKA MIKOA YA KASKAZINI KUKATAA SIASA ZA UKANDA NA UZAWA

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu uvccm Taifa SHAKA HAMDU SHAKA akikabidhi kadi kwa wanachama wapya wilaya ya Mwanga

Kaimu katibu mkuu UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akifungua shina la wakereketwa wa CCM katika kijiji cha Mtalang'a
kikundi cha ngoma kutoka katika kabila la kichaga kikitumbuiza wakati wa kaimu katibu mkuu wa UVCCM akiwasili wilayani Mwanga 
 
Na Woinde Shizza, Mwanga

Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umewataka wananchi wa mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania kukataa na kuzikwepa siasa za uzawa na ukanda kwasababu ubaguzi ni dhambi isiyosamehewa na mungu.

Wametakiwa kutambua kuwa ubaguzi ni zaidi ya laana ambayo ikiemea na kujengeka katika jamii kuiondosha kwake ni kazi ngumu na kwamba kafara yake lazima maisha ya watu yapotee au damu imwagike.

Hayo yameelezwa leo na Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu shaka wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika kijiji cha Mtalang'a kata ya Mwanga mkoani hapa.

Shaka alisema ni aibu binadamu aliyestaarabika, kupata elimu akawa anaishi, kupigania madaraka., vyeo au utawala kwa kutumia maneno au sera za ubaguzi wa dini, ukabila, uzawa au ukanda.

Aidha aliongeza kuwa baada ya miaka 52 ya uhuru na Muungamo wa mataifa ya Tanganyika na zanzibar, anapotokea kiongozi au chama cha siasa kinachofanya shughuli za kisiasa kwa kueneza sumu ya uzawa na watu kupiga kura kwa ukanda ni hatari mpya mbele ya watanzania.

"Ndugu zangu wananchi wa mikoa ya Kaskazini kuna hatari inawanyemelea, msipoitahadhari na kukwepa, ikiwaingia kutoka kwake ni mbinde, ili ifanyike kafara ya kuondoa laana hiyo si ajabu damu ikanwagika "alisema Shaka.
 

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO APRIL 30

Kwaheri Mpendwa wetu Consolata Haika Venance Kimario.

$
0
0
Tungependa leo kusoma risala na kusema jinsi ambavyo umekuwa ukituletea furaha kila wakati lakini wapi leo tarehe 30 April 2016 tukiwa na moyo wa majonzi twashiriki na ndugu, marafiki pamoja na mwanao mpendwa Beno kusema kwaheri ya kuonana.

Kweli ni huzuni kubwa na ni ngumu kuamini kuwa hatutaona tena tabasamu lako na ucheshi wako.

Tulikupenda sana, ila Mwenyezi Mungu amekupenda Zaidi. Bwana ametoa bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe

wana KIFUNGILO.

TANZANIA SISI NYUMBANI - TSN YAFUNGUA HYPERMARKET JIJINI MWANZA

$
0
0
Ufunguzi wa Hypermarket kubwa kuliko Mwanza unaendelea hivi sasa katika Mall ya Rock City Mwanza.

Hypermarket hii ambayo ni tawi jingine jipya la TSN linatazamiwa kuwahudumia wakazi wa Mwanza waliokuwa wakikosa uhondo wa bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu zikiwemo mbogamboga fresh kutoka hapa hapa nyumbani.

Akizungumza katika ufunguzi huo masaa machache yaliyopita Mkurugenzi wa TSN alisema,Tanzania Sisi Nyumbani  TSN itatoa zawadi kwa watu 100 wa mwanzo kufika katika uzinduzi huo. 

"Hii ni hatua nyingine kubwa ya kuhakikisha Watanzania wanapata vitu fresh.. kutoka nyumbani tena kwa bei nafuu.Tanzania Sisi Nyumbani tunahakikisha Watanzania wanafurahia mazao yao wenyewe...tena kwa bei ya gengeni katika Hypermarket hii.. Wateja wetu ni majirani zetu... karibuni sana TSN Hypermarket Mwanza." alisema.
 Sehemu ya mpnagilio wa bidhaa kwa ndani kama zinavyoonekana. 
 Sehemu ya malipo kwa ndani kama inavyoonekana
 Bidhaa ain ya mboga mboga fresh kabisa 
 Bidhaaa mbalimbali zikiwa ndani ya TSN,tayari kwa wateja kuanza 
Watu na wateja mbalimbali wamefika kujionea Hypermarket hiyo ya kisasa kabisa ndani ya jiji la Mwanza.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA 

MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA AZINDUA KAMPENI YA USAFI JIJI LA DAR

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda (wa pili kushoto),akiwa sambamba na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa za Wilaya ya Kinondoni,Ilala pamoja na Temeke wakishiriki kwa pamoja kufagia ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono Mh Paul Makonda kuzindua kampeni ya Usafi wa jiji la Dar Es Salaam,uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika mapema leo asubuhi Katika viwanja vya .Lidaz Club,Kinondoni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali serikali,dini na makundi mengine yakiwemo makundi ya michezo na waendesha boda boda.Mkuu wa Mkoa alizindua kampeni hiyo ya Usafi kwa kuwakabidhi Wenyeviti hao kila mmoja ufagio wa ajili ya kwenda kuwahamasisha wananchi wao katika mitaa yao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda akiwahutubia Wananchi mbalimbali mapema leo asubuhi katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar mara baada ya kumaliza kufanya usafi na hatimae kukusanyika kwenye viwanja hivyo,ambapo Mh.Paul Makonda alizindua kampeni ya Usafi kwa jiji la Dar.

Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda akimkabidhi ufagio Mwenyeki wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Temeke ndugu Bakari Makere,kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa Paul Makonda katika uzinduzi wa Kampeni hiyo ya Usafi kwa jiji hilo.

Mkuu wa Mkoa Mh.Paul Makonda akimkabidhi ufagio Mwenyeki wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Kinondoni Ndugu Juma Mgendwa
Sehemu ya meza kuu ikifuatilia yaliokuwa yakijiri uwanjani hapo


Wananchi wakishangilia jambo


Wananchi weakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo

Yamoto Band wakitumbuiza jukwaani.
Wasanii wa muziki wa kizazi wa kundi la Yamoto Band wakitumbuiza jukwaani na wimbo wao wa kuwahamasisha wananchi suala la usafi katika jiji la Dar na kwingineko

Baadhi ya Wananchi wakiwa wamekusanyika katika viwanja vya Leaders Club,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo mara baada ya kumaliza kufanya usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiongoza maelfu ya Wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika matembezi maalum ya kampeni ya kuhamashisha usafi katika jiji hili #Dar es salaam Ya Makonda, Usijifanye Mstaarabu kuwa Mstaarabu. Matembezi hayo yalimeanzia katika Uwanja wa Karume, Ilala na kuishia katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Sehemu ya wananchi wa Jiji la Dar es salaam wakishiriki Matembezi ya maalum ya kampeni ya kuhamashisha usafi, kuunga mkono kauli ya Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda aliyeongoza matembezi hayo. #Dar es salaam Ya Makonda, Usijifanye Mstaarabu kuwa Mstaarabu.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

MKUU wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza siku ya Jumamosi ya wiki ni siku ya usafi kuanzia saa moja hadi saa tatu na ndipo shughuli zikingine zitaanza ikiwa ni lengo la kufanya jiji la Dar es Salaam kuwa kitovu cha usafi na wengine waanze kuiga mfano huo.

Makonda ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya usafi wa jiji la Dar es Salaam uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya na Mkoa pamoja na wasanii waliojitolea kuhamasisha wananchi kufanya usafi kwa kutumia muziki, Makonda amesema kuwa haiwezekani kila siku watu wawe wanasifia nchi ya Rwanda kufanya usafi, sasa kazi hiyo itafanywa jijini Dar es Salaam na wenyewe wajifunze kwetu katika kupata mabadiliko ya usafi kwa muda mfupi.

Mkuu wa Mkoa amesema vyombo vya usafiri hususani Daladala zitaanza kufanya kazi saa tatu na biashara zote zitafunguliwa muda huo ili kuwapa watu wote kutumia muda wa asubuhi kufanya usafi katika maeneo yao.

Makonda ameagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dar es Salaam kufanya ukaguzi wa Daladala zote kuhakikisha vyombo hivyo vinakuwa na vifaa vya kuhifadhia taka (Dust Been) na wasiofanya hivyo hatua za kisheria kuchukuliwa.

Amesema kuwa kila mtu katika jiji la Dar es Salaam kufanya usafi bila kusimamiwa na watu watakaochafua mazingira kwa makusudi au kwa ustaarabu watachukuliwa hatua .Aidha ameagiza watumushi wote katika manispaa tatu kuhakikisha hawajihusishi na kampuni za kufanya usafi kutokana na kudorola kwa usafi wa jiji kwa kipindi kirefu ikiwa ni pamoja na kupitia zabuni zote za usafi na watu ambao watakuwa hawana vigezo vya kufanya usafi waondolewe.

Katika uzinduzi huo Makonda amezindua mashindano ya usafi kwa wenyeviti wa serikali za mitaa 50,kushindana katika usafi kwa vigezo katika mitaa iliyopangwa pamoja na isiyopangwa na mshindi atapata zawadi ya sh.milioni 50.

MAPENDEKEZO YA SHERIA YA WAZEE KUWASILISHWA BUNGENI

$
0
0
NAIBU WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali imekamilisha mapendekezo ya uundwaji wa Sheria ya Wazee ambayo yatawasilishwa katika mkutano wa Bunge wa Septemba.

Dk. Kigwangalla aliyasema hayo jana (Ijumaa, Aprili 29, 2016) wakati akitoa ufafanuzi kwa Viongozi wa Mtandao wa Wazee waliomtembelea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake mjini Dodoma.

Dk. Kigwangalla alisema kuwepo kwa Sheria ya Wazee kutawezesha mambo mbalimbali yanayohusu wazee kutekelezwa kwa mujibu wa sheria hiyo likiwemo suala la pensheni.“Mimi pamoja na Waziri wangu, Ummy Mwalimu baada ya kupewa jukumu la kuongoza wizara tuliunda kikundi cha wazee kwa ajili ya kuamua mambo makubwa mawili ambayo tutayatekeleza likiwemo la pensheni kwa wazee wote,” alisema.

Naibu Waziri huyo alisema suala jingine ambalo wamepanga kulitekeleza ni utoaji wa huduma ya bure kwa wazee, ambapo watawapatia bima ya afya ili wasiendelee kusumbuka.Kwa upande wake Waziri Mkuu aliwahakikishia wazee hao kwamba Serikali inawatambua na ndiyo sababu ya waliamua wawe na sehemu ya kufikishia malalamiko yao ambayo ni Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .

Kuhusu ombi la wazee hao kwa Rais Dk. John Magufuli la kuwa na uwakilishi Bungeni kwa kupitia nafasi zake 10 za uteuzi, Waziri Mkuu alisema amelipokea na atalifikisha kwa Mhe. Rais.Pia amewataka wapanue taasisi yao na kuimarisha mtandao uweze kujulikana na wazee wengi zaidi, wawe na viongozi kuanzia ngazi za vijiji ambapo Serikali ipo tayari kushirikiana nao kwa karibu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema amefurahishwa na utoaji wa huduma za afya kwa wazee katika hospitali mbalimbali alizotembelea na kukuta yameanzishwa madirisha maalumu ya kuhudumia.Akizungumzia kuhusu suala la wazee kupewa elimu ya mapambano dhidi ya UKIMWI aliwataka waandaaji wa matamasha na semina za mafunzo hayo kujumuisha watu wote wakiwemo wazee.

Naye Mwenyekiti wa mtandao huo , Bw. Sebastian Bulegi alisema lengo la kumtembelea Waziri Mkuu ni kumuomba awafikishie shukurani zao kwa Rais Dk Magufuli kwa kuwapatia wizara maalumu inayoshughulikia masuala yao.“Vile vile shukurani hizi tufikishie kwa mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli kwa kufanya wazee kuwa agenda yake ya kwanza na tayari ameshatembelea makazi ya Nunge Kigamboni (Dar es Salaam) na Bukumbi (Mwanza),”alisema.

Mwenyekiti huyo ambaye aliambatana na wajumbe wanane wa mtandao huo unaoundwa na Asasi 26 za wazee katika ngazi za wilaya na mkoa kutoka mikoa ya Kigoma, Tanga, Arusha, Mwanza, Lindi na Dodoma, aliiomba Serikali isimamie kutokomeza mauaji ya wazee.Ombi jingine alilolitoa kwa Serikali ni utekelezwaji wa Sera ya Wazee ya mwaka 2003, Sera ya Matibabu bure kwa wazee, mafunzo ya kupambana na UKIMWI pamoja na uwakilishi katika ngazi za kutoa maamuzi.

Pia wazee hao wamemhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamekubali ombi linalotolewa na viongozi wakuu wa nchi la kuwataka wawaombee ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo, baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA. 
JUMAMOSI, APRILI 30, 2016.

RAIS DK.SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI KATIKA TAASISI MBALI MBALI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Salmin Amour Abdalla kuwa Naibu Katibu wa Baraza la Mapinduzi katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Asaa Ahmada Rashid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw, Mzee Ali Haji kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi,Mwanahija Almasi Ali kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi,Raya Issa Msellem kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Washauri wa Rais wa Zanzibar ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa kwa Viongozi wa Taasisi mbali mbali Serikali ya Mapinduzi leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar. Baadhi ya Viongozi mbali mbali Serikali na wananchi waliohuria katika hafla ya kiapo kwa Watendaji wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,Baadhi ya Viongozi mbali mbali Serikali na Wananchi waliohuria katika hafla ya kiapo kwa Watendaji wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi walipoapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Alo MOhamed Shein,[Picha na Ikulu.]

TUME YA PAMOJA YA KUDUMU YA USHIRIKIANO BAINA YATANZANIA NA RWANDA YAFANYA KIKAO CHAKE GISENYI RWANDA

$
0
0
Gisenyi RWANDA

Kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda kilichofanyika kuanzia tarehe 29 – 30 Aprili, 2016,kimekamilika Mjini Gisenyi, Rwanda,ambapo wataalam wa sekta mbalimbali wameazimia kuharakisha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.

Kikao hicho cha 14 cha ushirikiano kimefanyika kufuatia maagizo ya Marais wa Tanzania na Rwanda wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. John PombeMagufuli nchini Rwanda mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.

Wakati wa ziara hiyo,wakuu hao walikubaliana kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano na kuibua maeneo mapya yanayolenga kuinua shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.

Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha wataalamu kiongozi wa ujumbe wa Tanzania Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Njeya Tanzania aliwakumbusha wajumbe wa pande zote mbili kuendesha mazungumzo na mjadala kwa kuzingatia maagizo ya viongozi hao na vilevile kuchangamkia fursa za ushirikiano wa shughuli za kiuchumi za wananchi wa pande zote mbili baada ya mindombinu ya kikanda kuimarika.

Kwau pande wake, Balozi Jeanine Kambanda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Njeya Rwanda na mwenyeji wa kikao hicho, alihimiza wajumbe kujiwekea malengo yanayotekelezeka na tarehe za ukomo kwenye maeneo yote watakayokubaliana ili kusukuma utekelezaji na kupata matokeo ya haraka.

Pamoja na mambo mengine, pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta muhimu kama vile miundombinu ya ushorobawakati (Central Corridor), kuharakisha ujenzi wa reli ya kati katika kiwango cha kimataifa (Standard Gauge), kukuza ushirikiano katika sekta ya anga hususan baina ya mashirika ya ndege ya Rwandair na ATCL, kuimarisha ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia, afya, kilimo na ufugaji, utalii, elimu, mawasiliano n.k.

Mkutano huo pia umekubaliana kuanzisha Kamati yaPamoja ya Utekelezaji (Joint Implementation Committee) kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu maeneo yote ya ushirikiano yaliyokubaliwa katika Kikao hicho cha 14. Kamati hiyo itakayoongozwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za nchi hizo mbili, itakutana kila robo mwaka.

Aidha, Serikaliya Rwanda imeonesha utayari wake wakuleta nchiniMaafisa na Watumishi waSerikali kwalengo la kupata uzoefu na mafunzo katika vyuo vya kitaalamu nchini kama vile Chuo cha Diplomasia (CFR), Chuo cha Taifa cha Utalii na Wanyamapori (Mweka) na Chuo cha Usafirishaji (NIT).

Kwa upande wa Tanzania, Serikali imedhamiria kuwakutanisha wataalamu wa mitaala ya elimu kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Rwanda kwenye upande wa kuandaa mitaala ya elimu ya tehama kwenye shule za awali, msingi na sekondari.

Mkutano ujao wa kuminatano waTume ya Pamoja yaKudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda utafanyika mwaka 2018, nchini Tanzania.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
30 Aprili, 2016

Gisenyi RWANDA

MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA MTANDAO WA VYAMA VYA WAZEE TANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake jijini bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI KUTUMIA SHILINGI BILIONI 59.5 KUWEZESHA VIJIJI NCHI NZIMA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Philip Mpango, amesema kuwa serikali imepanga kutumia shilingi 59.5bn kwaajili ya kuviwezesha vijiji nchi nzima katika kipindi cha mwaka fedha 2016/2017

Dokta Mpango, aliwaambia wabunge mjini Dodoma, leo tarehe 30, Machi, 2016, kwamba fedha hizo ni kwajili ya kukiwezesha kila kijiji shilingi 50m kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali.

Alisema kuwa fedha hizo zimewekwa kwenye mfuko wa Hazina, ili kuwawezesha wadau na taasisi zitakazo husika kupanga utaratibu mzuri wa matumizi ya fedha hizo.

“Fedha hizi zitaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu” aliongeza Waziri Mpango

Akizungumza kuhusu mikopo ya wanawake na vijana, Dokta Mpango, alisema kuwa serikali, kupitia Ofisi hiyo ya Waziri Mkuu, imepanga kutumia shilingi 1bn kuendeleza ujuzi kwa vijana wasio na ajira na shilingi 1.955bn kuwainua wanawake kiuchumi

Alifafanua kuwa halmashauri za wilaya, miji na majiji zitaendelea na utaratibu wao wa kutenga asilimia 5 ya mapato yao ya ndani kutoa mikopo kwa vijana na asilimia nyingine 5 kwaajili ya kuwawezesha wanawake katika maeneo yao.

SERIKALI YAIAGIZA MAMLAKA YA BANDARI NA TRA KUBAINI CHANZO CHA KUPUNGUA KWA SHEHENA YA KONTENA ZINAZOINGIA NCHINI

$
0
0
SERIKALI imeziagiza Mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kufanya uchambuzi wa kina ili kubaini sababu za kupungua kwa shehena ya kontena zinazoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi jirani.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dokta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini Dodoma, jana tarehe 30, Machi, 2016 kwamba taarifa zilizopo zinaonesha kwamba uingiaji wa mizigo inayopelekwa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, Malawi na Zambia kupitia bandari hiyo, umeshuka.

Alisema katika kipindi cha mwezi Oktoba mwaka jana na Machi mwaka huu kontena zilizopelekwa nchini Congo zilishuka kutoka 5,529 hadi 4,092, wakati yale yaliyokuwa yakipelekwa nchini Malawi yalishuka kutoka kontena 337 hadi 265, huku yale ya Zambia yakishuka kutoka 6,859 hadi kufikia 4,448.


Hata hivyo, Dokta Mpango aliwahakikishia waheshimiwa wabunge kwamba kushuka kwa kiwango cha kontena ziendazo nchi jirani kupitia  Bandari ya Dar es salaam, hakujaathiri malengo ya ukusanyaji wa mapato ya serikali.Alisema sababu mojawapo ya kushuka kwa idadi ya kontena zinazopitia bandari ya Dar es slaam zinachangiwa na kuporomoka kwa uchumi wa China ambao umeathiri nchi mbalimbali duniani ikiwemo  Tanzania.

"lakini naziagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA na Mamlaka ya Mapato-TRA, zichambue mwenendo huo ikilinganishwa  na nchi nyingine" alisisitiza Dokta Mpango.Alilieleza Bunge pia kwamba, Tanzania haitozi kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kontena zinazosafirishwa kutoka bandari hiyo kwenda nchi jirani hivyo hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuzikwaza nchi jirani kutumia bandari ya Dar es salaam
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images