Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

WANANCHI WA ITOBO, ITIRIMA - SIMIYU WAASWA KUZAA KWA KUFUATA UZAZI WA MPANGO Inbox x

$
0
0
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu mapema wiki iliyopita. Elimu hiyo ya uzazi wa mpango iliendana na huduma ya upimaji wa afya ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya uzazi wa mpango. Picha/Video na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango.
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima.  --- Na Cathbert Kajuna - Itirima, Simiyu. 

 Wananchi wa Kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wameaswa kuachana na mila za kuzaa watoto wasio kuwa na idadi ili kuepusha taifa lenye wategemezi wengi. Akizungumza katika mafunzo ya Uzazi wa Mpango yaliyotolewa wiki iliyopita na Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena alisema kuwa kuna haja ya wazazi hasa waishio vijinini kuacha dhana ya kuzaa ovyo kama wanyama bila mpangilio jambo linalowafanya kuendea kuwa maskini.

 "Nawaasa wananchi wa Kijiji cha Mitobo kuache mila potofu za kuzaa kila mwaka mimba kila mwaka mtoto maana mtakosa kuwa na maendeleo, nnakuta mtu anawatoto 10 - 15 jambo linalopelekea kuwa omba omba kwa vile atashindwa kuwahudumia," alisema Meena. Bi. Meena aliwashukuru wananchi wa Kijiji cha Mitobo kwa kuweza kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya uzazi wa mpango. 

 Akiongea mara baada ya kumaliza mafunzo hayo Bi. Ester Meena alisema kuwa muitikio wa wananchi katika kupata elimu ya uzazi wa mpango umekuwa mkubwa jambo linaloleta faraja kwa vile linaweza kupunguza idadi ya watu.

TAHA watakiwa kufuata Sheria za Usajili.

$
0
0
Na: Shamimu Nyaki WHUSM.

Chama cha mpira wa mikono Tanzania (TAHA) kimetakiwa kufuata sheria na taratibu za usajili wa Katiba wanayoitaka kama walivyoagizwa na Msajili wa Vyama vya michezo nchini.


Hayo yamesemwa na Afisa Michezo Mkuu Kitengo cha Usajili wa Vyama vya Michezo Bw. Allen Allex kufuatia malalamiko ya Chama hicho kwa vyombo vya habari kuwa wamenyimwa usajili wa katiba mpya ya chama chao.


Amesema kuwa Chama hicho wakati kinawasilisha barua ya kuomba kusajili Katiba yao aliwapa utaratibu wa kufuata katika usajili ambao kwanza ni kurudisha Cheti cha mwanzo cha Katiba ya zamani, pamoja na Orodha ya mabadiliko wanayotaka kuyafanya (Schedule of Ammendment).

“Lazima waonyeshe mabadiliko wanayotaka kuyafanya yaliopo katika katiba ya zamani na kuonyesha wanayotaka kuyaweka katika  katiba mpya”.Alisema Bw. Allen.


Aidha chama hicho kinatakiwa kufanya mkutano mkuu wa mabadiliko ya Katiba chini ya sheria ya Usajili wa Vyama vya Michezo ya  Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambayo inaeleza kuwa ni lazima mkutano kuwa na wajumbe wa  vyama vya michezo  kutoka mikoa  isiyopungua  13 ya Tanzania Bara.


Kutokana na masharti hayo chama hicho hakikuweza kutimiza na badala yake wakafanya mkutano na wajumbe ambao sio sahihi kisheria.Chama hicho Tarehe 17/12/2015   kiliwasilisha barua ya kuomba usajili wa Katiba mpya ambayo ilikuwa inataka kubadilisha jina la chama hicho kutoka Tanzania Ameteur Handball Association (TAHA) na kujulikana kama Shirikisho la la Mpira wa Mikono la Tanzania (THI).

WANANCHI JIJINI MBEYA WAJITOKEZA KUPATIWA DAWA ZA KINGA TIBA KWA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa akitoa Dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa wananchi wa Jiji la Mbeya katika eneo la kituo cha Mabasi madogo(Daladala)Kabwe April 29 -2015 mara baada ya kuzindua rasmi . 
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa akiongoza zoezi la ugawaji wa Dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ,Magonjwa hayo ni Minyoo ya Tumbo,Matende ,Ngirimaji na Usubi, ambapo dawa hizo zinatolewa kwa wananchi wote kuanzia miaka Mitano (5)na kuendelea . 
Wananchi eneo la kwabwe jijini Mbeya stendi wakisubiri kwa hamu kupatiwa dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuanza rasmi mei 2 hadi 5 mwaka huu .Picha EmanuelMadafa,Jamiimojablog-Mbeya . 

MICHUZI BLOG YATOWA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA M.P FC JIJINI MBEYA.

$
0
0
Muwakilishi wa Globu ya Jamii Bwana Fadhiri Atick a.k.a Mr.Pengo ambae pia ndiye Msimamizi Mkuu wa Timu ya Vijana wenye Umri wa Chini ya Miaka 18 akikabidhi Jezi kwa Vijana wa timu ya M.P FC (Mr.Pengo Football Club) Waliopo Jijini Mbeya wenye Vipaji vya kucheza Mpira wa Miguu.
Kutoka Kulia ni Fadhili Atick a.k.a Mr.Pengo akiwa na Kijana wake Dominick katika Picha ya pamoja mara baada ya Kuwakusanya Vijana wenye Vipaji vya Kucheza Mpira wa Miguu na kuunda Timu kwa Vijana wenye Umri chini ya Miaka 18 kwa Lengo la Kuwaandaa na  kuwaepusha Vijana kutofikiri au Kutenda Mambo Mbalimbali yasiyo faa katika Jamii kama kuvuta Bangi, Kucheza Kamali, Wizi na Udokozi, kuwaweka vijana kuwa Ngangari na pia kuendeleza Vipaji kwa Vijana hao.
Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Mr.Pengo Football Club (M.P FC) wakiwa katika Pozz

Kongamano la Uwekezaji Tanzania na Urusi lililofanyika jijini Dar

$
0
0
Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akifungua kongamano la kujadili Fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililofanyika jana jijini Dar es salaam ambalo limewakutanisha wafanyabiashara mbalimbali wa Mataifa hayo mawili. 
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akifafanua kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu faida za ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Urusi utakaochangia maendeleo katika sekta za Kilimo, Usafirishaji na Nishati hapa nchini.
Waziri wa Viwanda na Biashara wa Urusi Mhe. Denis Manturov akizungumza kwenye kongamano la kujadili fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililofanyika jana Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la kujadili fursa za Uwekezaji kati ya Tanzania na urusi wakifuatilia mada wakati wa kongamano hilo jana Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Bw. Reginald Mengi jana  Jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (wanne kutoka kushoto) akiwa na Wawakilishi wa Serikali ya Urusi, anayefuata ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage akifuatiwa na Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amina Salum Ali.Picha zote na (Fatma Salum- MAELEZO)

HALMASHAURI ZA MASASI, NANYAMBA KUANZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO SEKTA ZA UMMA AWAMU YA KWANZA MKOANI MTWARA

$
0
0
MKUU wa Wilaya ya Newala, mkoani Mtwara, Christopher Magala akizungumza wakati wa kuhitisha mafunzo ya utekelezaji wa Mradi wa Usimamizi wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) yanayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Misaada la Marekani (USAID) na kutekelezwa katika Halmashauri 97 katika mikoa 13 nchini. Uzinduzi wa mradi wa PS3 ngazi ya mkloa wa Mtwara ilifanyika juzi mjini humo.

Mkoani Mtwara mradi huo utatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itahusisha Halamshauri ya Nanyamba na Halmashauri ya Wilaya Masasi.

Awamu ya pili ambayo itatekelezwa mkoani mtwara kwa halamashauri saba zilizobaki utafanyika mwezi Februari na Oktoba mwaka 2017 na utahusisha Halmashauri za Mjiwa Newala, Wilayaya Newala, Mji wa Masasi, Wilaya ya Nanyumbu, Manispaa ya Mtwara, Wilaya ya Mtwara na Wilaya yaTandahimba.
 Baadhi ya Maofisa wa Mradi wa PS3 pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya Mkoani Mtwara wakifuatilia ufungaji wa mafunzo hayo.
 Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika mafunzo hayo.
 Mshauri wa Mradi katika Masuala ya Rasilimali Fedha, Dk Daniel Ngowi akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
 Mshauri wa Mradi katika Masuala ya Elimu, Dk Rest Laswai akifafanua jambo juu ya uimarishaji mifumo ya sekta za Umma katika nyanja ya elimu.
 Washiriki akifuatilia mada katika mafunzo hayo.
Wakuu wa Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mtwara wakifuatilia mada katika mafunzo hayo. 
  
  Maafisa wa Mradi wa PS3  Godfrey Nyombi (kulia) na Rahma Musoke  wakifuatilia kwa makini mawasilisho ya vikundi.
 Mtaalam wa Fedha wa Mradi wa PS3, Abdul Kitula akifafanua jambo katika moja ya vikundi vilivyokuwa katika majadiliano.
 Dk Rest Laswai (kushoto) akisimamia majadiliano ya moja ya vikundi.
 
Makundi mbalimbali yakishiriki katika majadiliano na baade kuwasilisha taarifa za mijadala yao.

Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo.

Chama cha Wakunga Tanzania(TAMA) watoa mafunzo kwa wanahabari Nchini

$
0
0
Chama cha Wakunga Tanzania (Tanzania Midwives Association-TAMA) imefanya mkutano maalum wa kuhamasisha waandishi wa Habari kuhusu kazi za wakunga katika kuelekea siku ya Wakunga Dunia ifikapo hapo Mei 5 mwaka huu.

Katika mkutano huo uliofanyika jana Aprili 28, TAMA ilibainisha kuwa, wanahabari wengi wamekuwa wakichanganya habari za wakunga wataalam ambao wapo chini ya Chama hicho na wale wakunga wa jadi ambao hawana taalum pamoja na kiapo cha kufanya kazi hiyo kitu ambacho kinaleta usumbufu mkubwa kwa jamii.

Mratibu wa TAMA, Bi. Martha Rimoy katika mkutano huo, ameeleza kuwa, shughuli za Wakunga wataalam ni wale tu ambao wamesomea taaluma hiyo pamoja na kula kiapo katika kumsaidia Mama na Mtoto na na huyo ndiyo anaitwa Mkunga na si wale ambao hawajapata mafunzo wala kula kiapo.

Aidha, aliomba wanahabari na vyombo vya habari kuzipatia nafasi/Kipaumbele habari za Wakunga kwani zitaondoa woga kwa jamii iliyojenga Imani potofu kwa wakunga.“Jamii imekuwa ikijenga Imani potofu namna ya Wakunga buka kujua mkunga huyo ni yupi. Tunaomba ifahamike Mkunga ni yule aliyepata mafunzo yake kitaalam na pia kula kiapo pamoja na kusajiliwa na taasisi husika kama ilivyo taratibu za Nchi.

Tuondoe Imani zingine kwa Wakunga pia tunawaomba wanahabari kuweza kutoa elumu ya kutosha kuhusiana na mambo ya Wakunga hasa wakunga wataalam ambao wamepatiwa mafunzo yote ya kuhakikisha wanamuokoa Mama na mtoto wakati wa uzazi” alieleza Bi. Martha Rimoy.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, ameeleza kuwa, Wakunga wataalam wanao wajibu wa kumsaidia Mwanamke na mtoto katika kukabiliana na vifo vitokanavyo na Masuala ya Uzazi vinavyozidi kuwatesa akina mama wengi, hasa inapokuja wakati wa tendo la kujifungua.
Aidha, Dkt. Sebalda amebainisha kuwa, pamoja na Changamoto mbalimbali, vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5, imepungua kwa asilimia 81, huku akitaka muendelezo wa elimu utolewe kwa Jamii.

Kwa upande wake, Afisa Mipango wa Afya ya Mama na Uzazi wa Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA)nchini, Bi. Felista Bwana ameelezea kuwa, upo umuhimu wa Mkunga mtalaam katika kuokoa Uhai wa Mama na mtoto kwani bila wao Dunia ingekuwa kwenye matatizo makubwa.

Siku ya Ukunga Duniani Inatarajiwa kuadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam, Mei 5 mwaka huu huku ikibeba ujumbe wa kauli mbinu ya “Wanawake na Watoto wachanga ni muhimili wa Ukunga”.

Aidha, mkutano huo ulieza changamoto wanazokabiliana nazo wakunga ni nyingi hivyo wameimba Serikali kuangalia namna ya kukabiliana nayo ili kila Mkunga kufanya kazi yake kwa uhuru na haki kwa dhama za sasa huku wakiomba jamii kuondoa dhana potofu dhidi yao pindi wawaonapo katika vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali zote.

Mkutano huo maalum wa TAMA, ulihusisha wanahabari mbalimbali kutoka katika vyombo vya Habari nchini ikiemo, Magazeti, Radio, Televisheni na magazeti ya mtandaoni.
DSC_2376Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari (kushoto) akieleza jambo kwa wanahabari na watu mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo kwa waandishi wa habari juu ya kufahamishwa shughuli za Wakunga. Kulia ni Bi. Felister Bwana kutoka UNPFA, Nchini Tanzania.
DSC_2381Mkutano huo ukiendelea...
DSC_2383DSC_2389Baadhi ya maafisa kutoka taasisi za Wakunga na mambo ya Afya wakifuatilia mkutano huo.

DSC_2391Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari akito mada katika mkutano huo..
DSC_2397DSC_2402Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo
DSC_2408Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huoDSC_2409Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari akitoa mada katika mkutano huo kwa wanahabari..
DSC_2436Mratibu wa TAMA, Bi. Martha Rimoy akitoa mada maalum kwa waandishi wa habari namna kazi na shughuli za Wakunga wanazofanya hapa nchini
DSC_2432
Afisa Mipango wa UNFPA, hapa nchini, Bi.Felista Bwana akitoa maelezo mafupi juu ya wakunga hapa nchini
DSC_2448Mratibu wa TAMA, Bi. Martha Rimoy akitoa mafunzo hayo katika mkutano huo kwa wanahabari
DSC_2464Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo
DSC_2479Bi. Felista Bwana akitoa mada katika mkutano huo
DSC_2467Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari akifafanua maswali kwa wanahabari wakati mkutano huo..
DSC_2481
DSC_2426Picha ya pamoja baadhi ya wanahabari na wandaaji wa mkutano huo maaalum kwa wanahabari kuelekea siku ya Wakunga Duniani ambayo kilele chake ni hapo Mei 5 mwaka huu huku kwa Tanzania ikitarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

NDUGAI AKABIDHI UENYEKITI WA JUKWAA LA MASPIKA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimkabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega baada ya Tanzania kumaliza muda wake. Alimkabidhi Uenyekiti huo wakati wa Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha leo tarehe 29 Aprili, 2016. Kulia ni Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Bunge la Seniti la Burundi Mhe Reverien Ndikuriyo wakati wa Mkutano wa Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha.
Spika wa Bunge Job Ndugai akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mhe Jeanne Uwimanimpaye wakati wa Mkutano huo.Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (wa kwanza kulia) akifurahia jambo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega (katikati) na Spika wa Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi wakati wa Mkutano wa Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha.

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amemkabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega baada ya Tanzania kumaliza muda wake.

Spika Ndugai alimkabidhi Uenyekiti huo wakati wa Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha leo tarehe 29 Aprili, 2016.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Spika wa Bunge la Seneti la Kenya, Spika wa Bunge la Kenya, Rais wa Bunge la Seniti la Burundi, Naibu Spika wa Bunge la Burundi, Naibu Spika wa Bunge la Rwanda, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki pamoja na Makatibu wa Mabunge ya nchi wanachama wa Afrika Mashariki.

Akiukabidhi Uenyekiti huo Spika Ndugai aliwashukuru Maspika wenzake kwa ushirikiano walimuonesha katika kipindi chote cha Uongozi wake na kumtakia kila la kheri Mwenyekiti mpya wa jukwaa hilo.

Maspika wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hushika Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo Tanzania ilichukua Uenyekiti wa Jumuiya hiyo mwaka jana.

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe Kidega atashiki Uenyekiti wa Jukwaa hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kuukabidhi kwa Spika mwingine katika mkutano ujao unaotarajiwa kufanyika nchini Kenya.

Pamoja na mambo mengine mkutano huo wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulijadili maswala mbalimbali yanayohusiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki lilianzishwa mwaka 2008.

TANZANIA COMMENDED FOR ENHANCING GIRLS EDUCATION IN ICT.

$
0
0
The Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia H.E. Naimi Hamza Aziz(centre) poses for a picture with four student girls from Tanzania who participated in the Girls in ICT Day Celebrations in Addis Ababa under the auspices of International Telecommunication Union ITU held at AU Headquarters yesterday.

From left, Elida Alex Paul from Msalato Girls Secondary school, Dorice Mhanga from Kleruu Secondary School in Iringa, Khudhaima Bedran Sultan from Chasasa Secondary school in Pemba and Elician Yohana Kapi from Nyankumbu Secondary school in Geita .(photo courtesy of Tanzanian Embassy in Addis Ababa Ethiopia).


Tanzania has been commended for its efforts in enhancing girl’s education in the country including rural areas with the aim of achieving gender balance by availing opportunities for girls to acquire skills in science and technical subjects including Information and Communication Technology (ICT).

The compliments were given yesterday (April,28,2016) by the International Telecommunication Union (ITU) Regional Director for Africa Mr. Andrew Rugege when officiating at the opening ceremony of the International Girls in ICT Day Celebration held at the African Union Headquarters in Addis Ababa, Ethiopia.

“ Your Excellency Tanzanian Ambassador Naimi Aziz, I would like you to convey my regards to your government for its efforts in promoting ICT education for girls as witnessed by four girls who travelled all the way from Tanzania to join us in this auspicious occasion. The girls, excelled in ICT competition organized by ITU,” he said praising the girls for successful creating useful IT applications that could be used for provision of social services.

The four girl students from Tanzania who were invited for the occasion in the Ethiopian capital, Addis Ababa include, Khudhaima Bedran Sultan from Chasasa Secondary school in Pemba Zanzibar, Elician Yohana Kapi from Nyankumbu Secondary school in Geita, Dorice Mhanga from Kleruu Secondary school in Iringa and Elida Alex Paul from Msalato Girls Secondary school in Dodoma.

Mr. Rugege said ITU estimates a skills shortfall of over two million jobs in the Information and communication technology (ICT) sector within the next five years adding that, Girls and young women who learn coding, apps development and computer science will not only be well-placed for a successful career in the ICT sector, but ICT skills are rapidly becoming a strong advantage for students in just about any other field they might choose to pursue.

“ Girls in ICT Day reminds us that ICTs help to improve the lives of people everywhere and especially in Africa – through better health care, better environmental management, better communications, and better educational systems that transform the way children and adults learn,” he said adding that the technology has been instrumental in creating job opportunities to African youths.

The girls participating in the school workshops were invited to the African Union in Addis Ababa HQ for a half day celebration where they had the opportunity to present their work and what they learned during the workshops to the ITU officials, the diplomatic community, AU Staff and ITU Delegates.

Six girls from various secondary schools in Tanzania who excelled in ICT competition coordinated by the ITU were invited for the ADDIS Girls in ICT Day celebration having emerged winners from zonal and eventually national ICT contests. Two of them could not travel to Addis Ababa to join their colleague due to delay in visa application.

The Four Girls are scheduled to return home on Saturday.

ITU’s Girls in ICT Day, is a global initiative aimed at raising awareness among girls and young women about the importance of digital skills for a successful professional career in all sectors and encouraging them to consider studies and careers in Information and Communication Technologies (ICT).

.ITU is the United Nations specialized agency for information and communication technologies – ICTs.

An organization based on public-private partnership since its inception, ITU currently has a membership of 193 countries and almost 800 private-sector entities and academic institutions. ITU is headquartered in Geneva, Switzerland, and has twelve regional and area offices around the world.

ITU membership represents a cross-section of the global ICT sector, from the world’s largest manufacturers and telecoms carriers to small, innovative players working with new and emerging technologies, along with leading R&D institutions and academia.

Founded on the principle of international cooperation between governments (Member States) and the private sector (Sector Members, Associates and Academia), ITU is the premier global forum through which parties work towards consensus on a wide range of issues affecting the future direction of the ICT industry.

From Freddy Maro,

Tanzania Embassy Addis Ababa Ethiopia

Bomba la mafuta kukamilika 2020

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na  Madini anayeshughulikia madini Profesa James Mdoe ( wa kwanza kushoto, waliokaa mbele); Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara  ya Nishati na Madini anayeshughulikia nishati Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa  pili kushoto waliokaa mbele)  pamoja na wataalam wengine  wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini  hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini   Uganda, Mhandisi  Irene  Muloni (hayupo pichani) katika mkutano  kati ya nchi ya  Tanzania na  Uganda lengo likiwa ni kujadili mpango  wa  ujenzi wa bomba la mafuta kutoka  Hoima, Uganda hadi katika bandari ya  Tanga nchini Tanzania.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akielezea uzoefu wa Tanzania kwenye ujenzi wa miradi  ya mabomba ya gesi na mafuta katika mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini   Uganda, Mhandisi  Irene  Muloni na kulia ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.
Wataalam kutoka Wizara, taasisi na makampuni ya mafuta kutoka Tanzania na Uganda wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inawasilishwa na mwakilishi kutoka kampuni ya Total katika mkutano huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini  Uganda, Dk. Fred Kaliisa (kushoto) akifafanua  jambo katika kikao hicho. Kulia ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini   Uganda, Mhandisi Irene Muloni.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu  utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika bandari ya  Tanga nchini  Tanzania. Kulia ni Waziri wa Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini   Uganda, Mhandisi  Irene  Muloni.

Waziri wa Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini   Uganda, Mhandisi  Irene  Muloni (kulia)  akifafanua jambo alipokuwa  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa mkutano huo.  Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

Balozi wa Uganda Nchini Tanzania, Dorothy Hyuha akifafanua jambo katika mkutano huo.





Na Greyson Mwase, Dar es Salaam.


Bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika bandari  ya Tanga nchini Tanzania linatarajiwa kukamilika  mwezi Juni mwaka  2020.

Hayo yalielezwa na  Waziri wa Nishati na Madini,  Profesa Sospeter Muhongo alipokuwa   akizungumza na waandishi wa habari  mara baada ya kufanyika kwa mkutano kati yake na Waziri wa Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini   Uganda, Mhandisi  Irene  Muloni  aliyeambatana na ujumbe wake katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kujadili mpango wa  mradi wa ujenzi wa bomba la  mafuta kutoka Hoima nchini  Uganda hadi katika  bandari ya  Tanga  nchini Tanzania ambapo ulikutanisha wataalam kutoka nchi zote mbili, ambao ni  wa  ardhi, miundombinu, maji, ujenzi, uchumi,, maji barabara pamoja na makampuni ya  mafuta.


Profesa Muhongo alisema  kuwa mara baada ya marais wa Tanzania na  Uganda kukubaliana kuanza kwa ujenzi wa bomba la mafuta,  kinachofuatia ni utekelezaji wa kasi  ya ajabu ambapo  tayari wameanza kukutana na kuunda kamati  ndogo ndogo  zitakazokuwa na wataalam mbalimbali kwa ajili ya kuanza mara moja kwa utekelezaji  wa mradi huo.


 Profesa Muhongo alisema kuwa  serikali  za nchi zote mbili zimejipanga katika kuhakikisha kuwa  ujenzi huo unakwenda kwa kasi  kubwa, ikiwezekana ujenzi ukamilike mwishoni mwa mwaka   2019.


Aliongeza kuwa serikali ya  Uganda inatarajia kujenga kiwanda kwa ajili  ya kusafisha mafuta ghafi Hoima ambapo  wametoa hisa  40 zenye  thamani  ya Dola za Marekani  bilioni 4.7 kwa nchi  zilizomo ndani ya Jumuiya ya  Afrika Mashariki ambapo kila nchi itaweza kununua asilimia nane ya hisa hizo na kusisitiza kuwa  Tanzania ipo  tayari kununua hisa  nane kwa thamani ya  Dola za Marekani  milioni 150.4


Aliendelea kusema kuwa hisa zitanunuliwa na serikali pamoja na wawekezaji binafsi watakaoonesha nia ya kununua hisa ili waweze kunufaika na mradi huo.

Hata hivyo aliongeza kuwa nchi ya  Uganda pamoja na nchi nyingine zilizomo ndani ya  Jumuiya ya  Afrika Mashariki wameomba  kununua  gesi kutoka nchini  Tanzania  na kusema kuwa kwa kuanzia  serikali inatarajia  kujenga bomba la  gesi hadi nchini Uganda   ili waweze kunufaika na  gesi hiyo.


Alisema kuwa bomba la gesi litasambazwa katika mikoa ya kaskazini na mingineyo ili  uchumi wa nchi uweze kukua kwa kasi na  Tanzania kuwa nchi  yenye  kipato cha kati  ifikapo mwaka  2025 kama   Dira  ya Maendeleo  ya Taifa inavyofafanua.


“ Kila sehemu  yenye  gesi ya kutosha, lazima  tuhakikishe  tunaweka bomba la  gesi ambalo  ni  mkombozi wa uchumi wa nchi,” alisisitiza Profesa Muhongo.

Wakati huo huo Waziri wa Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini   Uganda, Mhandisi  Irene  Muloni, aliishukuru serikali ya  Tanzania kwa kuwa tayari  kushirikiana na Uganda kwa ajili ya mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta.


Alisema kupitia  uzoefu  wa Tanzania  katika ujenzi wa mabomba ya  gesi na mafuta pamoja na wataalam  waliobobea anaamini kuwa mradi huu  utakwenda kwa kasi  kubwa na kukamilika kwa wakati.


Aliiomba  nchi ya   Tanzania pamoja na  wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na  makampuni ya mafuta, jamii itakayopitiwa na miundombinu  ya  bomba la mafuta kutoa ushirikiano ili mradi uweze kukamilika kwa wakati kama ilivyopangwa.



Alisema kuwa   mkutano  wa pili unatarajiwa kufanyika  Hoima nchini  Uganda tarehe  27 Mei, mwaka huu na kuendelea kufanyika katika  maeneo mbalimbali  yatakayopitiwa na bomba la  mafuta.

MATUKIO KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Ilala Azzan Mussa Zungu, bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, Angeline Mabula bungeni mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Butiama , Nimrod Mkono kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na wabunge Ahmed Shabiby wa Gairo (kushoto) na Suleiman Ahmed Saddiq wa Mvomero, kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Aprili 29, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Rais Magufuli afungua Kikao kazi cha makamanda Polisi na waendesha mashitaka awapa neno

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi nchini na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu wao huku wakitanguliza maslahi ya taifa.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 29 Aprili, 2016 wakati akifungua kikao cha kazi cha Makamanda wa polisi wa mikoa, Mawakili wafawidhi wa serikali  wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi, kinachofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Dodoma uliopo katika eneo la Tambukareli Mjini Dodoma.


Awali kabla ya kutoa hotuba yake Rais Magufuli aliwapa nafasi Makamanda na Mawakili Wafawidhi hao kutoa maoni yao juu ya changamoto zinazowakabili katika kutekeleza wajibu wa kufanya upepelezi na kuendesha mashitaka, hususani kujua sababu za kuchelewesha kesi za makosa ya jinai, ambapo wamedai ufinyu wa bajeti ndio sababu kubwa ya kucheleweshwa kwa kesi za hizo.

Kufuatia kutajwa kwa changamoto hiyo Rais Magufuli ameahidi kuhakikisha anawatafutia fedha kwa ajili ya kukabiliana nazo, lakini ametaka fedha zitakazotafutwa zitumike vizuri kwa kuwa taarifa zinaonesha Jeshi la Polisi limekuwa likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha hali inayoongeza ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa kazi.


Ametolea mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya kununulia vifaa na sare za askari, ama mikataba yenye mashaka inayotiwa saini kati ya Polisi na wawekezaji kuwa ni baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya utendaji kazi kwa jeshi hilo.


"Oysterbay pale ni eneo ambalo ni very prime, kila mmoja anajua, mmeingia kwenye mikataba mnayoijua nyinyi, akapewa mtu anawajengea pale, sifahamu kama majengo hayo yanafaa. Palikuwa na ubaya gani eneo la Oysterbay likawa na hati, mkaitumia hiyo hati kwenda kukopa benki na kujenga nyumba hata za ghorofa 20 pale, mkaweka investment  na Polisi wenu wakakaa pale. Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi, nisiposema kwa uwazi nitajisikia vibaya nikimaliza mkutano huu, nataka muelewe na muelewe ukweli direction  ninayoitaka mimi" Amesema Rais Magufuli.


Aidha, Rais Magufuli ameitaka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujipanga kufanya kazi kwa ufanisi na ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo vya serikali kushindwa katika kesi nyingi mahakamani licha ya kuwa na wanasheria mahiri.


"Niwaombe mawakili na polisi wanaohusika na upelelezi mtangulize maslai ya nchi mbele, kwa sababu kumekuwa na usemi kwa baadhi ya wapelelezi na mawakili wachache, nasema wachache, panapokuwa na kesi inayohusiana na pesa pesa, wana misemo yao wanasema dili limepatikana, na saa nyingine kesi inapopelekwa mahakamani wana-collude Mawakili wa serikali na mawakili wanaomtetea  mhalifu, na wanapo-collude siku zote serikali inashindwa. Unapoona hali hiyo ya kila siku serikali inashindwa, halafu siku hiyo unataka serikali ikuwezeshe, kwa vyovyote serikali inapata kigugumizi" amesisitiza Rais Magufuli.


Dkt. Magufuli pia amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na kashfa ambazo zimekuwa zikisemwa dhidi yake, ikiwemo maafisa wa Polisi kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kuazimisha silaha kwa wahalifu wa ujambazi.Hata hivyo Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa  Mashitaka kwa kazi kubwa wanayoifanya na ametaka apelekewe mpango wa mahitaji yao ili atafute namna ya kuimarisha vyombo hivyo.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dodoma


29 Aprili, 2016 

TANAPA YAKABIDHI MABATI 2800 KUSAIDIA UJENZI WA MAABARA NA ZAHANATI WILAYANI SERENGETI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mhe. Marwa Ryoba (kushoto) akipokea msaada wa mabati kutoka kwa Meneja Ujirani Mwema wa TANAPA Bw. Ahmed Mbugi wilayani Serengeti.

Na Jacquiline Mrisho – Dar es Salaam

Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limekabidhi jumla ya mabati 2800 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kusaidia ujenzi wa maabara 15 za shule za sekondari na zahanati zilizo katika Kata mbalimbali za wilaya hiyo.Akikabidhi msaada huo Meneja ujirani mwema wa Tanapa, Ahmed Mbugi amesema TANAPA imetoa msaada huo kusaidia Maendeleo ya Elimu na Afya katika wilaya hiyo.“Mabati haya ni msaada ambao tumeutoa kwa Wilaya ya Serengeti ikiwa ni muendelezo wa misaada tunayoitoa kwa jamii hii ili kusaidia shughuli za maendeleo wilayani hapa” alisema Mbugi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Naomi Nnko aliongeza kuwa ujenzi wa maabara hizo kutawawezesha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo, na hivyo kuongeza ufaulu katika shule za sekondari wilayani humo.Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Juma Keya alishukuru kwa msaada huo toka TANAPA na kuomba mashirika mengine ndani na nje ya Wilaya ya Serengeti kushirikiana na Halmashauri hiyo kuleta maendeleo katika jamii.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Maftah Mohammed aliliomba shirika hilo kuchangia upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na sekondari zilizopo wilayani humo.Mpaka sasa TANAPA imeisaidia Halmashauri hiyo kwenye ujenzi wa maabara katika Kata ya Natta, uchimbaji wa marambo na ujenzi wa mabweni katika shule za Sekondari.

MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI AGAWA MAENO YA BIASHARA KWA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO

$
0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob akizungumzana wa wafanyabiashara ndogo ndogo waeneo la Ubungo Stendi ya Mkoa kuhama katika eneo hilo na kuhamia katika kituo cha mabasi Simu 2000, leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara ndogo ndogo waeneo la Ubungo Stendi ya Mkoa wakijibapanga kwenye maeneo yao waliypewa bure na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara ndogo ndogo waeneo la Ubungo Stendi ya Mkoa wakimsikiliza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob leo amefanya ziara katika eneo la ubungo na kuongea na wafanyabiashara ikiwemo kuwaonyesha eneo la kufanya biashara zao.

Amewataka wafanyabiashara hao kesho wasiwepo maeneo hayo na kuwataka kuhamishia biashara zao katika eneo la soko la Mawasiliano (Sinza), kwani wasipofanya hivyo Kamati ya Ulinzi na Usalama Manispaa ya Kinondoni imeshakaa na imepanga kuwaondoa.

Meya alieleza kuwa isingekuwa busara kuwaondoa bila kuwaeleza watakwenda wapi, Meya amewakabidhi wafanyabiashara hao kadi ambazo watazionyesha ili wasisumbuliwe,pia amewataka wasilipe pesa yeyote endapo watatakiwa walipie maeneo ya biashara waliyopewa.

Pia amesema kuhusu ushuru hawatalipa kwa muda wa mwezi mmoja baada ya hapo watalipia,Meya huyo amewahakikishia wafanyabiashara hao kuwa hakuna atakayekosa eneo la kufanya biashara.

Afisa biashara wa Manispaa ya Kinondoni amewataka wafanyabiashara hao kutokaidi agizo hilo la Meya,hivyo kuanzia kesho wataondolewa kwa nguvu.

Meya amesema kuna maeneo wamepewa madiwani akiwemo yeye na hayafanyiwi biashara, hivyo sio sawa maeneo hayo wapewe wafanyabiashara.

WAZIRI JENISTA ATEMBELEA BANDA LA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, KWENYE MAONYESHO YA USALAMA MAHALA PA KAZI

$
0
0
WAZIRI wa NCHI ofisini ya WAZIRI Mkuu, Jenista Mhagama(wakwanza kulia), na naibu wake, Dkt. Abdallah Possi.(wapili kulia), walipotembelea banda la WCF, kwenye maonyesho ya Siku ya Usalama na afya mahala pa kazi mjini Dodoma Aprili 28, 2016.Kushoto ni afisa uhusiano mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence.WCF inashiriki maonyesho hayo yaliyoratibiwa na OSHA kwa ushirikiano na TUCTA, ikiwa ni sehemu ya maadhimishi ya Siku ya wafanyakazi Duniani(Mei Mosi).
Afisa uhusiano mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence, akizungumza kwenye maonyesho hayo ya OSHA.
Wananchi wakipatiwa MAELEZO kuhusu mafao ya fidia kwa wafanyakazi kutoka kwa maafisa wa WCF(kushoto).


MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI KATIKA NCHI ZA UKANDA WA MASHARIKI NA KUSUNI MWA AFRIKA LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua mkutano kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkutano huo umeandaliwa na Jopo la Ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon aliloliteuwa Mwanzoni mwa huu, kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi ifikapo 2030. Umefanyika Leo April 29,2016 Hyatt Hotel Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Jopo la ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kuwezesha wanawake kiuchumi Baada ya kufungua mkutano kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkutano huo unazungumzia kuhusu kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi ifikapo 2030. Umefanyika Leo April 29,2016. (Picha na OMR)

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA TANESCO LAZINDUA ''TANESCO HUDUMA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba (kulia) akizungumza na Waandishi,viongozi wa Tanesco Dar es Salaam jana wakati wa Uzinduzi wa 'Tanesco Huduma' zilizoboreshwa kwa wananchi ,wateja wanaotumia simu za mkononi za kisasa katika mfumo uliotengenezwa COSTECH. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba (katikati) akizungumza.Wengine kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH),Hassan Mshinda na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTBi,George Mulamula.
kiongozi wa Tanesco akizungumza.
Wataalamu wa COSTECH wakipangalia mtandao.
Maofisa wa Tanesco wakijadiliana jambo.
Mtaalamu wa Mtandao COSTECH,Godfrey Magila akizungumza na kufafanua. 
Wataalamu wa Mtandao wa COSTECH
Viongozi wa Tanesco na Tume ya sayansi na Teknolojia COSTECH wakifurahia jambo.


Kwa Ufupi. 

Tanesco imezindua 'Tanesco Huduma' Itakayoboresha huduma kwa wananchi, kuwasilisha Taarifa kwa kutumia simu za mkononi za kisasa kwa mtu binafsi au kundi katika mitaa wanayohishi.Kutakuwa na mfumo utakaokujulisha mambo mbalimbali ya Shirika hilo,Katika majaribio yameanza kwenye mkoa wa tanesco wa Kinondoni.

DAWASCO YATOA MKONO WA POLE KWA DADA ASHA CHANDE ALIYEPATA ULEMAVU WA MGUU WAKATI WA KUTAFUTA MAJI

$
0
0
Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka (Dawasco), Bernadetha Mkandya akiwakatika picha ya pomoja na wafanyakazi wa(Dawasco), leo,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka (Dawasco), Bernadetha Mkandya akimkabidhi hundi ya sh mil 2.5 Dada Asha Chande Ramadhani ikiwa ni sehemu ya kumpa pole kufuatia kupata ulemavu wa mguu wakati wa harakati ya kutafuta maji .Dawasco imetoa mkono wa pole, Mchele Maharage Unga wa Mahindi na Sukari pamoja na hundi ya Sh. Milioni 2.5.
Asha Chande Ramadhani akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada wa kutoka Dawasco leo,jijini Dar es Salaam.

MSAJILI WA HAZINA ATOA UFAFANUZI KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UMILIKI WA HISA ZA SERIKALI KATIKA SHIRIKA LA USAFIRISHAJI DAR ES SALAAM (UDA)

$
0
0
Msajili wa Hazina Bw. Laurence Mafuru akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu umiliki wa hisa za Serikali katika Shirika la Usafirishaji Dar es salaam (UDA) na kubainisha kuwa Serikali inamiliki hisa 49% katika shirika hilo kinyume na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kuwa Serikali imeuza hisa zote kwa muwekezaji. Kulia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Gerald Chami.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Msajili wa Hazina leo jijini Dar es salaam uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu faida za Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika kuongeza uwajibikaji na tija kwenye utumishi wa umma hasa kwa kuzingatia mapendekezo ya ripoti ya mwaka 2014/2015.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI KIKAO KAZI CHA MAKAMANDA WA POLISI, WANASHERIA WA SERIKALI WAFAWIDHI WA MIKOA NA WAKUU WA UPELELEZI WA MIKOA NA VIKOSI.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali,  Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi kabla ya kufungua rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi katika Ukumbi wa Dodoma Convention Center. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na viongozi wengine wakati wimbo wa Jeshi la polisi ukipigwa. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola, Kushoto kwake ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harison Mwakyembe , Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad  Yusuph Masauni na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Ernest Mangu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convention Center kwa ajili ya ufunguzi wa rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi.
 Baadhi ya Makamanda wa polisi wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu kabla ya kufungua kikao kazi hicho.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kufungua kikao kazi hicho.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa mara baada ya kufungua kikao kazi chao katika ukumbi wa Dodoma Convention Center mjini Dodoma.
 Baadhi ya Makamanda wa polisi wa Mikoa mbalimbali wakiimba Wimbo wa Jeshi la Polisi kabla ya ufunguzi wa Kikao kazi hicho.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mohamed Mpinga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa mara baada ya kufungua kikao kazi cha Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa.
PICHA NA IKULU.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi nchini na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu wao huku wakitanguliza maslahi ya taifa. 

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 29 Aprili, 2016 wakati akifungua kikao cha kazi cha Makamanda wa polisi wa mikoa, Mawakili wafawidhi wa serikali  wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi, kinachofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Dodoma uliopo katika eneo la Tambukareli Mjini Dodoma.

Awali kabla ya kutoa hotuba yake Rais Magufuli aliwapa nafasi Makamanda na Mawakili Wafawidhi hao kutoa maoni yao juu ya changamoto zinazowakabili katika kutekeleza wajibu wa kufanya upepelezi na kuendesha mashitaka, hususani kujua sababu za kuchelewesha kesi za makosa ya jinai, ambapo wamedai ufinyu wa bajeti ndio sababu kubwa ya kucheleweshwa kwa kesi za hizo.

Kufuatia kutajwa kwa changamoto hiyo Rais Magufuli ameahidi kuhakikisha anawatafutia fedha kwa ajili ya kukabiliana nazo, lakini ametaka fedha zitakazotafutwa zitumike vizuri kwa kuwa taarifa zinaonesha Jeshi la Polisi limekuwa likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha hali inayoongeza ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa kazi.

Ametolea mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya kununulia vifaa na sare za askari, ama mikataba yenye mashaka inayotiwa saini kati ya Polisi na wawekezaji kuwa ni baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya utendaji kazi kwa jeshi hilo.

"Oysterbay pale ni eneo ambalo ni very prime, kila mmoja anajua, mmeingia kwenye mikataba mnayoijua nyinyi, akapewa mtu anawajengea pale, sifahamu kama majengo hayo yanafaa. Palikuwa na ubaya gani eneo la Oysterbay likawa na hati, mkaitumia hiyo hati kwenda kukopa benki na kujenga nyumba hata za ghorofa 20 pale, mkaweka investment  na Polisi wenu wakakaa pale. 

Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi, nisiposema kwa uwazi nitajisikia vibaya nikimaliza mkutano huu, nataka muelewe na muelewe ukweli direction  ninayoitaka mimi" Amesema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli ameitaka Ofisi ya mwendesha Mashitaka wa Serikali kujipanga kufanya kazi kwa ufanisi na ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo vya serikali kushindwa katika kesi nyingi mahakamani licha ya kuwa na wanasheria mahiri.

"Niwaombe mawakili na polisi wanaohusika na upelelezi mtangulize maslai ya nchi mbele, kwa sababu kumekuwa na usemi kwa baadhi ya wapelelezi na mawakili wachache, nasema wachache, panapokuwa na kesi inayohusiana na pesa pesa, wana misemo yao wanasema dili limepatikana, na saa nyingine kesi inapopelekwa mahakamani wana-collude Mawakili wa serikali na mawakili wanaomtetea  mhalifu, na wanapo-collude siku zote serikali inashindwa. Unapoona hali hiyo ya kila siku serikali inashindwa, halafu siku hiyo unataka serikali ikuwezeshe, kwa vyovyote serikali inapata kigugumizi" amesisitiza Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli pia amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na kashfa ambazo zimekuwa zikisemwa dhidi yake, ikiwemo maafisa wa Polisi kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kuazimisha silaha kwa wahalifu wa ujambazi.

Hata hivyo Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa  Mashitaka kwa kazi kubwa wanayoifanya na ametaka apelekewe mpango wa mahitaji yao ili atafute namna ya kuimarisha vyombo hivyo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma

29 Aprili, 2016 
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images