Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

MONGELLA AZINDUA MRADI WA UZINDUZI WA MRADI WA UIMARISHAJI WA MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA KATIKA MKOA WA MWANZA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akitoa ufafanuzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma,Mh.Mongella alisema kuwa mradi huo utafanyika katika mikoa 13, ambayo itaanza na mradi huo Mwanza ni mmoja wapo.
Mkurugenzi wa TAMISEMI Bibi Betrece Kimoleta, alipokuwa akitoa maelezo kuhusu jukumu la TAMISEMI katika uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Mwanza, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma.

Dr. Peter Kilima, akitoa maelezo jinsi mradi utakavyo fanya kazi na afua zitakazo zingatiwa katika kutekeleza mradi huo.
Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza wakiwa katika majadiliano ya Pamoja wakati wa Uzinduzi huo.( Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza)

MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI MSAAFU AZINDUA RIPOTI YA MPANGO WA UHAMASISHAJI UWAZI KATIKA MAPATO YA MADINI, GESI ASILIA NA MAFUTA (TEITI)

$
0
0
Mwenyekiti wa mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI), Mark Bomani akimkaribisha Aliyekuwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh ili aweze kuzindua ripoti ya mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI) jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh akizungumza wakati wa uzinduzia  ripoti mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI)  jijini Dar es Salaam leo.
 Aliyekuwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ripoti mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI) jijini Dar es Salaam leo akiwa na Mwenyekiti wa mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI), Mark Bomani na wengine ni wajumbe wa mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI) wakiwa katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick akionyesha ripoti mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI)  jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzindua ripoti hiyo.
Mkurugenzi wa Utawala wa Kampuni ya BDO Afrika Mashariki, Juvinal Betambila akifafanua jinsi ripoti mpango wa Uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi asilia na Mafuta (TEITI) jijininDar es Salaam leo wakati wa kuzindua repoti hiyo.

MATUKIO BUNGENI LEO.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 28, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mahonda, Bahati Ali Abeid kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 28, 2016. Kushoto ni Mbenge wa Kwahani na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi (kulia) wakati alipomuuliza swali katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu, bungeni Mjini Dodoma Aprili 28, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma Aprili 28, 2016.

  Mbunge wa Welezo, Saada  Salum Mkuya akichangia Bungeni Mjini Dodoma Aprili 28, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kwahani na  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi  (kushoto) kwenye viwanja vya Bunge  mjini Dodoma Aprili 28, 2016. Katikati ni Mbunge wa Mahonda, Bahati Ali Abeid
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Bariadi na Mwenyekiti wa Bunge Mtemi Andrew Chenge kwenye viwanja vya Bunge mjini  Dodoma Aprili 28, 2016. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BOSTON CITY CAMPUS TANZANIA, BRANCH NOW OPEN

$
0
0
Boston City Campus and Business College carries a legacy of over 20 years in South Africa. It currently has 44 branches with over 25000 students studying every year. In Tanzania, Boston has opened its first branch outside South Africa, 45thBranchin total this year.


Boston offers Professional Courses and Short Learning Programs with plans to introduce tertiary education in the future. These are further learning programs which will enhance one’s skills and assist to get better jobs. They have extended their wide range of courses which they offer in South Africa in various fields to Tanzania. 

Students can choose from multiple course under various categories such as Accounting, ICT, Business Management, Business Communications, Marketing and many more. There are professional courses offered at their college such as ACCA and CompTIA certified A+, N+ and many more.


The teaching methodology Boston is bringing to Tanzania is quite different from the conventional way of classroom teaching. At Boston, a student would study on a computer assigned to him or her, for a scheduled time slot. All the teachings are imparted in the form of video tutorials which the student views on his computer screen and listens to through earphones. This enables the student to learn on a one to one basis.


This type of teaching method gives multiple benefits to the student: The student will be able to study at his own pace without having to worry about keeping pace with other students. The student will have a prescheduled flexible timetable to study at the college, unlike going to a classroom where he has to adjust his schedule to the class’s timings.


While a student can be studying one subject on a computer, the student sitting next to him can be studying an entirely different subject at the same time. There is a flexibility for the student to enroll whenever he wants, all round the year. Also, as the student is studying, he can view the videos multiple times, till he understands the concepts, by forwarding or rewinding the video.


The exams too are taken at their own ease, once they are done studying a module. Most of these exams are computer based and will be assessed at their headquarters in South Africa. While the learning is computer based, Boston also provides course books to the students, price of which is already included in the fee.


In the case that the student is having difficulty in understanding the tutorial, there are Training Advisors to help the students clear their doubts and move forward. The training advisor will be able to tutor the student on a one to one basis. 

If the student still does not understand, they have the option to contact experts in South Africa who are qualified for each subject that is being taught here. This will be done from the college itself.


Further, for benefit of the students, refresher sessions are conducted in their workshop room on weekly basis where a student can participate if he is having any difficulty understanding any concepts and get clarifications.


Access to the computers and video tutorials is only from the college. It is mandatory for the student to be present at the college for the tutorials, as Boston wants the students to study under a controlled environment. This way the progress of each student can be monitored. However, the student is provided with study material and books which are kept by them, to be used to revise and prepare for the next class.


More information on Boston City Campus & Business College is available at www.boston.co.tz  0765 008827 or 0685 626366.

MKAKATI WA UTOZAJI WA FAINI KWA WAMILIKI WA ARDHI.

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Rehema Kilonzi (Kushoto) akielezea mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusu hatua ya kazi ya mkakati wa utozaji wa faini kwa Wamiliki wa ardhi waliokiuka masharti ya uendelezaji na ulipaji kodi ya pango la ardhi leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Uliopo jijini Dar es Salaam.Picha na Benedict Liwenga-MAELEZO.

MKAKATI WA UTOZAJI WA FAINI KWA WAMILIKI WA ARDHI.

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Kodi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Rehema Kilonzi (Kushoto) akielezea mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusu hatua ya kazi ya mkakati wa utozaji wa faini kwa Wamiliki wa ardhi waliokiuka masharti ya uendelezaji na ulipaji kodi ya pango la ardhi leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Uliopo jijini Dar es Salaam.Picha na Benedict Liwenga-MAELEZO.

-MWANZILISHI WA TAASISI YA MAN AT WORK YAKUTANA NA WADAU WAKE JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanaume Man at Work Maxwell Stansalaus akizungumza na Wanaume jana jijini Arusha katika mkutano Mkuu wa Wanaume uliofanyika jana na kuhudhuriwa na zaidi ya wanaume 700 ambao lengo lake ni kuwakumbusha wanaume wajibu walionao kwa familia,jamii na Taifa. Picha na woinde shizza, arusha.


Na Woinde ShizzaArusha 

Taasisi isiyo ya  kiserikali ya Wanaume Kazini maarufu kama Man at Work imelaani vikali vitendo vya ushoga vinavyoshusha hadhi na thamani ya wanaume hivyo wameitaka serikali kupiga vite vitendo hivyo ambavyo ni kunyume cha Maadili ya Tanzania na Afrika kwa Ujumla.

Muasisi wa Taasisi hiyo  yenye makao yake jijini Arusha Maxwell  Stanslaus  amesema kuwa Wanaume kazini wanapinga vikali vitendo vya ushoga kwa zaidi ya Asilimia 100% na kuwataka wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha Mara moja.

Maxwell alisema hayo jana katika mkutano Mkuu wa Wanaume kazini uliofanyika jijini hapa huku akisema kuwa taasisi hiyo imelenga kuhimiza wanaume kote nchini kutimiza wajibu wao na kutenda majukumu yao kama wanaume katinga ngazi ya familia,jamii na taifa ili kuchochea maendeleo.

“Kwa sasa tunaona nidhamu ya serikali imerudi kutokana na Mwanaume mmoja tu Rais John Pombe Magufuli kuamua kutimiza wajibu yake hivyo Basi  Wanaume zaidi ya Milioni  walioko Tanzania wakiamua kutimiza majukumu yao na wajibu Tanzania itanyooka” Alisema Maxwell

Moja kati ya Wanaume waliohudhuria ni Joseph Mayagila alisema kuwa matatizo ya ushoga yanatokana na baadhi ya wanaume kujisahau na kujaribu kuwa wanawake ,jukwaa hili la wanaume ni muhimu kuwakumbusha wanaume juu ya uanaume wao na kutimiza yale yanayowapasa kama wanaume.

Dokta Emmanuel Buganga  ameeleza kuwa vuguvugu la wanawake kudai haki zao linatokana na baadhi ya wanaume kutotimiza wajibu wao kama wanaume wameacha majukumu yao ya kutunza familia zao na kuwa walezi na walinzi wa familia . 

Mhamasishaji wa Masuala ya kijamii Samuel Sasali amesema kuwa wanaume wengi wamejisahau sana katika masuala ya malezi ya familia kwani usimpolea mtoto katika njia impasayo atakuja kukuaibisha ukubwani.

Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanaume Man at Work Maxwell Stansalaus akizungumza na Wanaume jana jijini Arusha katika mkutano Mkuu wa Wanaume uliofanyika jana na kuhudhuriwa na zaidi ya wanaume 700 ambao lengo lake ni kuwakumbusha wanaume wajibu walionao kwa familia,jamii na taifa.

WADAU WA KAMPENI YA OKOA TEMBO WA TANZANIA WAMWANGUKIA RAIS MAGUFULI.

$
0
0

Mwenyekiti wa Kampeni ya Okoa Tembo Bw. Shubert Mwarabu (katikati) akielezea kuhus Kampeni yao ya kuokoa Tembo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Kampeni hiyo Bw. Lameck Mkuburo pamoja na Bw. Arafat Mtui (wa kwanza kulia).(PICHA NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO).

Na Anitha Jonas – MAELEZO

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Okoa Tembo Tanzania imemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kuteketeza ghala la meno ya tembo liliopo nchini kufuatia Tanzania kusaini mpango wa kuwalinda Tembo mwaka 2014 unaozuia uuzaji wa meno ya Tembo kwa muda wa miaka 10.

Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar s Salaam na Mwenyekiti wa Kampeni ya Okoa Tembo Tanzania Bw.Shubert Mwarabu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Barua ya Wazi waliyomwandikia Mheshimiwa Rais.

Amesema Tanzania inafungwa na mkataba wa kimataifa wa biashara juu ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka (Convetion on International Trade in Endangered Species-CITES) ambao unabainisha kuwa Tanzania kwa sasa haiwezi kuuza ghala lake la meno ya Tembo.

Amesema uhifadhi wa meno hayo unaigharimu serikali fedha nyingi na kufafanua kuwa kwa sasa Tanzania ina hifadhi kubwa ya meno ya Tembo yaliyokamamwa kutokana na ujangili.

“Tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kasi yake ya utendaji tangu kuchaguliwa kwake,tunamuomba atekeleze lengo la tatu la kampeni yetu ya Okoa Tembo wa Tanzania kwa kuliteketeza hadharani ghala la meno ya tembo,tunaona hakuna haja ya kuendelea kuwa na ghala hili” amesema Bw.Mwarabu.

Amesisitiza kuwa ombi lao kwa Rais kutaka ghala la meno ya Tembo liteketezwe kutasidia kutuma ujumbe mzito kwa majangili na wafanyabiashara kuwa meno ya Tembo hayana thamani ya pesa kiasi cha serikali kuona wepesi kuteketeza hazina hiyo.

“ Tunataka ieleweke kwamba kuharibu ghala la meno ya Tembo kunatuma ujumbe mzito kwa majangili na wafanyabiashara kuwa meno ya Tembo hayana thamani ya pesa na kuwa ujangili ni kosa la jinai lisilokubalika” Amesisitiza.

Amesema ipo haya ya Tanzania kuunga mkono mpango wao wa kuteketeza ghala la meno ya Tembo kama inavyotarajiwa katika nchi ya Kenya ambayo inatarajia kuteketeza ghala lake la meno ya Tembo hadharani Aprili 30 mwaka huu.Amezitaja nchi ambazo zina mpango wa kuchukua hatua kama ya Kenya kuwa ni Ethiopia,Chad,Gabon, Mozambique na Congo.

Naye mmoja wa wajumbe wa Kampeni ya Okoa Tembo wa Tanzania Bw.Arafat Mtui akizungumza katika mkutano huo amesisitiza kuwa kuendelea kuwepo kwa ghala hilo nchini Tanzania kunawapa moyo wafanyabiashara haramu wa meno hayo kuona kuwa ipo siku biashara hiyo itaendelea tena.

Amesema Kampeni yao ya Okoa Tembo wa Tanzania inaendelea kusisitiza kuwa kuwa hatma ya Tembo wa Tanzania iko mikononi mwa watanzania, hivyo ni vema Serikali ikashirikiana na wadau mbalimbali kuchukua hatua madhubuti kuokoa viumbe hao walio hatarini kutoweka kwa ajili ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

WANAFUNZI WA SHULE YA KIMATAIFA YA TANGANYIKA WATEMBELEA UN.

$
0
0
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao mara baada ya ziara yao ya mafunzo kutembelea Ofisi za UN Tanzania.Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao mara baada ya ziara yao ya mafunzo kutembelea Ofisi za UN Tanzania.Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) wakijibu maswali mara baada ya kuelezwa namna ofisi ya Umoja wa Mataifa, UN zinavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto.Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) wakijibu maswali mara baada ya kuelezwa namna ofisi ya Umoja wa Mataifa, UN zinavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto.
Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai.Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai.Mmoja wa wafanyakazi wa UN nchini Tanzania (kulia), akitoa somo kwa Wanafunzi wa 'International School of Tanganyika-IST' waliotembelea ofisi hiyo nchini Tanzania kujifunza shughuli mbalimbali za msingi zinazofanywa na UN.Mmoja wa wafanyakazi wa UN nchini Tanzania (kulia), akitoa somo kwa Wanafunzi wa 'International School of Tanganyika-IST' waliotembelea ofisi hiyo nchini Tanzania kujifunza shughuli mbalimbali za msingi zinazofanywa na UN.Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) wakifuatilia maelezo toka UN ya namna ofisi hizo za Umoja wa Mataifa zinavyofanya kazi hasa kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto. Nyuma ni baadhi ya walimu wa IST walioambatana na wanafunzi hao.Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) wakifuatilia maelezo toka UN ya namna ofisi hizo za Umoja wa Mataifa zinavyofanya kazi hasa kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto. Nyuma ni baadhi ya walimu wa IST walioambatana na wanafunzi hao.
Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai.Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai.Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama mbele), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai.Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama mbele), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai.Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama kulia), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai.Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama kulia), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai.

SIO KILA HOMA NI MALARIA, NENDA UKAPIME

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipima afya yake kujua kama ana vimelea vya ugonjwa wa malaria baada ya kutoa tamko la maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani mjini Dododma Aprili 25 mwaka huu.

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.

La mgambo likialia kuna jambo, safari ya kujenga taifa bora na imara katika sekta ya afya ni jukumu la watu wa taifa husika kuanzaia na mtu mmoja mmoja.Katika kuhakikisha watu wanajenga afya njema itakayowawezesha kuwa uchumi imara, ni jukumu la taifa hilo na kila mtu kutumia nguvu zake katika kujenga uchumi imara wenye kusimamiwa na afya bora ambayo ni ni msingi maendeleo.Katika hali ya kawaida, mtu anayefanya kazi za mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisaiasa ni lazima awe na afya bora na njema, kwa maneno mengine ni lazima awe mzima.  

Siku ya Malaria Duniani inayoadhimishwa kila mwaka Aprili 25, ni moja ya siku adhimu inayopaswa kuzingatiwa na kutiliwa maanani.Maadhimisho hayo yalianza kuadhimishwa tangu mwaka 2001 inatoa nafasi kwa Wataalamu wa Afya na Wananchi kwa jumla kuchambua kwa kina utekelezaji wa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria kwa kila mwaka.Siku hiyo inatoa nafasi ya kuangalia tulikotoka, tulipo na tunakokwenda katika suala zima la kufanikisha mapambano dhidi ya malaria.

Jitihada hizo hufanywa ulimwenguni kote kutokana na kutambua kuwa Malaria haina mipaka hivyo mikakati ya kupambana na ugonjwa huo inahitaji ushiriki wa Wadau wote si tu katika Bara la Afrika peke yake, bali Ulimwenguni kote.Kila mpenda maendeleo anatambua namna Ugonjwa wa Malaria unavyoendelea kuwa tishio kwa maisha ya Watanzania kwa miaka mingi sasa.

Taarifa za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto zinaonyesha kuwa, Ugonjwa wa Malaria unaongoza kuwa na wagonjwa wengi wa Nje (OPD) katika hospitali nyingi hapa nchini pamoja na wagonjwa wa malaria wanaolazwa katika Hospitali katika hospitali mbalimbali. Pia ugonjwa wa malaria unaongoza kwa vifo vyote vinavyotokea katika Vituo vya Tiba.


Mwanga bora wa kutatua tatizo hili nchini umeanza kuonekana ambao ni dalili njema ya kulitoa taifa kwenye janga na hatari za ugonjwa wa malaria hatua ambayo itasaidia kupungua kwa kiasi kikubwa ugonjwa huo nchini.Kutokana na Ripoti ya Utafiti wa viashiria vya VVU/UKIMWI na malaria inaonekana kupungua kwa asilimia 50 kutoka asilimia 18 kwa mwaka 2007/2008 hadi asilimia 10 mwaka 2011/2012.


Pamoja na kupungua kwa maambukizi ya malaria, takwimu zinaonesha kuwa ugonjwa huo bado ni tatizo kubwa katika vijijini ikilinganishwa na maeneo ya mjini ambapo maambukizi ya maeneo ya vijijini ni asilimia 10.7 na mjini ni aslimia 3.4

Kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa malaria nchini, Watanzania wana kila sababu ya kujipongeza na kumshukuru kila mdau aliyeyechangia kwa namna moja au nyingine katika jitihada za kutokomeza ugonjwa huo.


Juhudi hizo zinatoa msukumo kwa Watanzania kutambua kuwa bado kuna kazi ya kufanya ambapo lengo la taifa ni kuhakikisha maambukizi ya ugonjwa wa malaria yanapungua  hadi asilimia 5 mwaka 2016 na asilimia 1 ifikapo mwaka 2020.

Hatua hiyo inawezekana kufikiwa na taifa ikiwa kila mtu anawajibika kwa nafasi yake kushiriki katika kupambana na vita dhidi ya malaria.


Ukiona vya elea ujue vimeundwa, hatua ambazo zimesababisha kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo zinatokana na juhudi mbalimbali zinazosimamiwa vema na viongozi wenye dhamira ya dhati ya kupambana na adui wa taifa ambaye maradhi.Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa uongozi wake na hata baadha ya muda wake wa uongozi amekuwa msari wa mbele katika kupambana na adui wa taifa ambaye miongoni wao ni ugonjwa malaria.

Jitihada zake za kupambana na malaria ndani na nje ya nchi zimeonesha tija na zimezaa matunda na kupelekea kutunukiwa tuzo iliyotukuka ya “White House Summit Award” mapema Aprili mwa huu ndio maana waswahili husema “Chanda chema huvikwa pete”.


Je? Mimi na wewe, tumejifunza nini katika kupambana na ugonjwa wa malaria? Tambua zama zimebadilika, si kila homa ni malaria, chukua hatua nenda kituo cha afya kilicho karibu nawe uweze kupima afya yako badala ya kuanza kutumia dawa bila kufanya vipimo.

Vipimo ndio iwe mwalimu na mwongozo wa kujua mtu anasumbuliwa na ugongwa gani ndipo aweze kutumia dawa sahihi za kupambana na adui anayemsumbua.


Hadi sasa nchini, Serikali inapaswa kupongezwa kwa kuanzisha utaratibu kabambe wa kupambana na ugonjwa wa malaria ambapo watu watakaoenda kupima ugonjwa huo katika zahanati, vituo vya afya na hospitali mbalimbali za umma wanakiwa kupima bure na mara baada ya wakigundulika kuwa wana ugonjwa wa malaria wanapswa kupewa dawa za kutibu ya ugonjwa huo bure.


Hatua hiyo njema ni na ya kupongezwa na kila mpenda na mthamini uhai,   Waziri mwenye dhamana ya afya nchini chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alipokuwa akitoa tamko la maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani mjini Dododma amesisitiza kuwa huduma ya vipimo na matibabu ya ugonjwa wa malaria itakuwa intolewa bure isipokuwa malipo ya kumuona daktari ndio yanapaswa kulipwa.


Kwa hatua hiyo itaifikisha Tanzania kujiridhisha na usemi wa “Tanzania bila malaria inawezekana” maana wananchi sasa wamepunguziwa mzigo mkubwa uliokuwa ukiwasumbua kwa muda mrefu na kuwafanya watu wengi kupoteza maisha kabla hata ya kufikishwa vituo vya afya kutokana na kukosa fedha za kupata matibabu.Hatua hiyo ya taifa ya kupambana na malaria ni njia na mwanga bora kwa kuwa na watu wenye afya njema ambao watakuwa mstari wa mbele katika kujenga na kuhakikisha nchi inafikia uchumi wa kati ifikapo 2025.

Akitoa tamko katika kilele cha maadhimisho ya siku ya malaria duniani mjini Dodoma, Waziri Ummy alisema kuwa Watanzania ni lazima kutambua maadhimisho hayo ya Malaria nchini yapaswa kuwa chachu ya wananchi kupima na kuthibitisha kama wana vimelea vya malaria kabla ya kuanza kutumia dawa.


Waziri Ummy aliongeza kuwa pale mtu anapogundulika kuwa ana malaria, anapaswa kuhakikisha anatumia dawa na kumaliza kozi nzima kulingana na maelekezo ya daktari.

Katika kuhakikisha taifa linapambana na ugojwa wa malaria, Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa Mbu Waenezo Malaria Charles Damas anabainisha umuhimu wa jamii kushiriki kikamilifu katika kuharibu mazalia ya mbu kwa kufukia madimbwi ya maji, kusafisha mifereji na kuweka mazingira safi ili kuondoa maji yanayotuama hatua ambayo itachangia kupunguza maambukizi ya malaria.

Ni dhahiri Tanzania sio kisiwa, imeendele kuwa na mahusiano mazuri na mataifa rafiki pamoja na wadau wengine wa maendeleo katika kupambana na ugonjwa wa malaria nchini.


Wadau ambao wapo mtari wa mbele katika mapambano ya malaria ni pamoja na Mfuko wa Dunia wa kushughulikia ugonjwa wa UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria, Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kushughulikia Malaria (PMI), Shirika la Misaada la Uingereza (DFID), Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC), Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika la UNITAID,Taasisi zisizo za Kiserikali, Sekta Binafsi kupitia Mpango wa malaria Safe na Taasisi za Utafiti za NIMRI na Ifakara.


Katika kupambana na adui maradhi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, alitoa mwongozo wa Serikali yake kupitia hotuba yake ya kufungua rasmi Bunge jipya la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,mjini Dodoma Novemba 20, 2015 ambapo alibainisha dhamira ya dhati katika masuala ya afya.

Rais Dkt. Magufuli anasema “Dhamira ya kujenga uchumi wa kisasa na suala la kupambana na umasikini linakwenda sambamba na kuwa na wananchi wenye afya bora. Kwa kutambua ukweli huu na mahitaji ya huduma bora za wananchi wetu Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha kwamba wananchi wanapata huduma bora za afya”.

Dhamira hiyo ya Serikali ni kuimarisha huduma za afya sehemu ambapo huduma hizo zipo na kuanzisha pale ambapo hazipo ikiwa na lengo la kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na Zahanati, kila Kata inakuwa na Kituo cha Afya, kila wilaya inakuwa na Hospitali, na kila Mkoa unakuwa na hospitali ya Rufaa.

Ni dhahiri nia ya Serikali ya kuboresha huduma za afya nchini itasaidia kuongeza utaalamu katika sekta ya afya kwa kuwapatia mafunzo watumishi wake ndani na nje ya nchi, kuzipatia vifaa bora na vya kisasa hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizopo nchini.

Lengo hilo la Serikali kuchukua hatua hizo itasaidia kuwezesha upatikanaji wa huduma mahsusi hapa nchini na hivyo kutolazimika kupeleka wagonjwa kutibiwa nchi za nje.

Ili kufanikisha hayo, Rais alisema kuwa Serikali yake itaendelea kuongeza bajeti ya dawa na kuboresha mfumo wa upatikanaji wa dawa hizo ili kuhakikisha zinapatikana katika hospitali, vituo vya afya na zahanati na kuhamasisha wananchi wajiunge na Bima ya Afya ili kuwa na uhakika wa kupata huduma za afya mahali popote nchini na wakati wowote.

Alipokuwa akitoa tamko hilo siku ya maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani, Waziri Ummy aliongoza kupimwa kujua kama ana vimelea vya malaria ambapo waaandishi wa habari ambao walihudhuria wakati tamko hilo kutolea mjini Dododma waliungana naye kujua hali ya afya zao.

Ili kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini, kila mtu anapaswa kuzingatia kupima ili kujua uwepo wa vimelea vya malaria kabla ya kutumia dawa, kumaliza kozi ya dawa kulingana na maelekezo ya daktari na mtoa huduma, kutumia vyandarua vyenye viaatilifu kila siku wakati wa kulala pamoja na kuzingatia usafi wa mazingira kuzuia mazalia ya mbu katika maeneo yanayozunguka nyumba zao.

Jukumu la kupambana na malaria sio la mtu moja, halmashauri  zao zinapaswa kuboresha takwimu zao ili kujua ukubwa wa tatizo la malaria katika halmashauri zao na kuweka bajeti kwenye mipango yao ya halmashauri (CCHP) kwa ajili ya udhibiti wa mbu.

Majukumu mengine ya halmashauri ni kuhakikisha miongozo ya uchunguzi na tiba ya malaria inazingatiwa katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya umma na vya sekta binafsi pamoja na kufanya ufuatiliaji katika vituo vya kutolea huduma vya umma na vya sekta binafsi ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.

Juhudi hizo kupambana na ugonjwa wa malaria sio za kuachiwa Serikali tu, kila mtu awajibike na atambue kuwa zama zimebadilika, “Sio kila homa ni malaria, nenda ukapime” na “lala kwenye chandarua kila siku” kujikinga na malaria. 

WAZIRI NAPE APANIA KUIBORESHA TASNIA YA HABARI

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akikabidhi Ipad tano kwa mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Jackson Msome kwa ajili ya matumizi ya maafisa habari wa mkoa wa Kagera. Bwana Msome alikuwa akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa kijuu.


Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
 
Sekta ya habari ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya wananchi na serikali yao. Ndiyo maana wanazuoni hupenda kusema kuwa habari ni muhimili wa nne wa dola. Kwa kuzingatia umuhimu huo, katika kuchekecha huku na huko, Mhe. Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akamteua mtu mahiri kuongoza sekta hii, Mhe. Nape Moses Nnauye.

Kwa uteuzi huu ninadiriki kusema hatimaye Wizara imepata mtu sahihi na mchapakazi anayeweza kwenda na kasi ya Mheshimiwa Rais Magufuli na ni dhahiri kabisa kuwa kumpa Mhe. Nape ni kuthibitisha usemi wa wahenga usemao upele umepata mkunaji.

Kwa jinsi hii tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, Muumba wa Mbingu na Nchi kwa kutujalia kupata kiongozi wa nchi ambaye ni mchapakazi na aliyejaliwa kipawa cha kuona mbali kwa kuwaweka viongozi wa chini yake katika nafasi za uongozi wanazostahili.

Sekta ya habari ni sekta nyeti na muhimu sana katika dunia hii kwa kua bila kupashana habari na kujua kinachoendelea daima hakutakua na maendeleo kwa hiyo, ni sekta inayohitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu ili kuhakikisha kwamba inachukuliwa uzito na inapewa kipaumbele kwa kupewa vifaa na elimu ya kutosha ili kuepusha upotoshaji na kukosekana kwa habari muhimu hasa za Serikali zinazotakiwa kuwafikia wananchi kwa muda husika.

Tukiangalia katika sekta ya habari, Mhe.Rais hakukosea kabisa kumuweka Waziri Mhe. Nape kwa kuwa ameanza kuitumikia Wizara kwa kasi nzuri na ameonyesha nia ya kuiboresha Wizara hasa kwa tasnia ya habari kwa kuanzia kwenye wizara yake hadi katika ofisi za umma zilizoko mikoani ili kuhakikisha wanahabari wote nchini wanatambua thamani ya kazi yao. 

Kwa maneno yake aliyoyatoa Jijini Mbeya alipokua akigawa vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya mawasiliano yaani ipad kwa maafisa mawasiliano wa mkoa huo alikaririwa akisema,"Nataka Wizara ihamie mikoani" hii haimaanishi kuwa Wizara ihamie mikoani kama alivyosema bali alimaanisha kiutendaji zaidi kuwa yale yote anayoyafanya katika Wizara yake atahakikisha na maafisa wa mikoani pia wanafanyiwa hivyo ikiwemo kugawiwa vitendea kazi pamoja na mambo mengine. 

Katika kuhakikisha hilo, kwa upande wa sekta ya habari, Waziri Nape ameanza kwa kugawa ipad kwa maafisa mawasiliano walioko mikoa ya pembezoni ambao wana upungufu mkubwa wa vitendea kazi na kwa muda mrefu wameshindwa kuifanya kazi yao kwa ufanisi kwa sababu ya uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi hiyo.

Ipad hizo zilizotolewa kama msaada kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kampuni ya Startimes ambayo imeahidi kuwa bega kwa bega na Wizara hii katika kuisaidia ili kuongeza ufanisi hasa katika sekta hii nyeti ya habari maana kwa maneno mengine tunaweza kusema sekta ya habari ndio daraja linalounganisha serikali na wananchi.

Siku aliyokabidhiwa ipad hizo Mhe. Nape alikaririwa akisema "Nawashukuru sana Startimes kwa kutujali,ipad hizi tutaanza kuzigawa kwa maafisa habari wa mikoa ya pembezoni kwa kuwa ndiko kuna uhaba mkubwa sana wa vifaa kwa maafisa hao"alisema Mhe Nape.

Maneno haya ya Mhe.Nape yanaungana na usemi wake wa kuifanya Wizara kuhamia mikoani kwa maana ya kuwapa kipaumbele katika kuwapatia vitendea kazi ili nao wasijione kuwa wametengwa au kutokuthaminiwa kama maafisa mawasiliano wengine hasa walioko Dar es salaam na mikoa mingine iiliyoendelea. Maana anaamini kuwa mikoani ndiko kuna wadau na ndiko ziliko shughuli nyingi kwa kuwa watu wengi wenye uwezo wa kuzikuza tasnia anazozifuatilia wapo mikoani.

Ni mengi sana Mhe.Nape ameyaongea hasa kwenye ziara zake alizozifanya kwenye baadhi ya mikoa kama Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Geita, Simiyu,Dodoma, Kagera pamoja na Mwanza ambako alipita kugawa ipad na kuangalia jinsi maafisa habari wanavyofanya kazi katika vituo vyao vya kazi. Ziara hiyo pia inalenga katika kujua changamoto wanazokumbana nazo ili kuweza kufanya kila kinachowezekana kuzitatua ili kufanya sekta hii kufanya kazi ya kupeleka taarifa kwa wananchi kama inavyopaswa kufanyika ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Jemedari Mkuu Mhe. Rais John Pombe Magufuli.

Kiongozi huyu ameongelea kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ambao ulishirikisha wadau mbali mbali hasa wahariri pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari kutoa maoni yao ambayo kwa asilimia 99 maoni hayo yamewekwa katika muswada huo.

"Muswada huo umeshakamilika, uko tayari kufikishwa bungeni, pia nataka niwathibitishie kuwa muswada huo utalinda maslahi ya waandishi wa habari kuanzia mishahara yao, mikataba ya kazi zao pamoja na bima ya matatizo wanayoyapata kwenye kazi zao lakini muswada huo utakua na sheria zitakazobana ufundishwaji wa masomo ya habari ili tupate waandishi ambao wamebobea katika fani hiyo" alisema Mhe. Nape.

Ndoto ya changamoto zinazoikabili tasnia ya habari mikoani zinakaribia kuwa historia kwa kuwa Waziri Nape amepanga kuleta teknolojia mpya na kuzitoa zile zilizopitwa na wakati ili kuharakisha ufanisi wa utoaji wa taarifa, kuweka busta kwa baadhi ya maeneo ili televisheni ya taifa (TBC) iwe bora zaidi na kuongeza urefu wa minara ili matangazo yafike mbali zaidi.

Waziri Nape ameamua kuboresha urefu wa minara ili matangazo yafike mbali kwani mikoa mingi ya pembezoni imepakana na nchi ambazo teknolojia zao za mawasiliano ni kubwa kiasi kwamba wananchi wengi wa mipakani wanasikiliza redio za nchi jirani na kuacha kusikiliza redio za hapa nyumbani Tanzania.


Katika harakati za kuboresha tasnia ya habari, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla ameelezea changamoto na jinsi alivyopanga mikakati ya kusaidia na kuiboresha tasnia hii mkoani kwake ambapo alikaririwa akisema "Mkoa wangu unaomba kibali cha kuajiri maafisa habari ili kila Halmashauri iwe na afisa habari wake pia naahidi kuendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kununua vitendea kazi vya maafisa hao".

Wakati huo huo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa wito kwa wananchi kuanzisha vituo vya utangazaji 19 katika Wilaya na Halmashauri mbalimbali na wamewaomba wadau kutuma maombi kabla ya Aprili 29 mwaka huu.

Akiongea katika mkutano wa Mhe.Nape na wadau wake, Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Nyanda za Juu Kusini, Mhandisi Lilian Mwangoka alisema, "Mamlaka ya Mawasiliano ipo tayari kushirikiana na wananchi kuongeza vituo vya utangazaji ili kuongeza idadi ya vituo na kuongeza fursa katika ukusanyaji wa kodi".

Aidha, Waziri Nape amesisitiza suala la maafisa habari kupewa ruhusa ya kushiriki katika vikao vya maamuzi ili wajue mambo yanayoendelea katika ofisi zao kwani kufanya hivi kutasaidia maafisa habari kuacha kuwakimbia waandishi wa habari na badala yake kuwapa taarifa kamili ili wakawajulishe wananchi taarifa sahihi kuhusu Serikali yao.


Akiongea kwa kujiamini Waziri Nape amehakikisha kuwa yote yatawezekana maana fedha za kutatua kero hizo zitapatikana kwa kuwa Mhe.Rais tayari alifanya maamuzi ya kuziamuru taasisi zote za Serikali zilizopewa huduma ya kutoa matangazo yao kupitia Televisheni ya Taifa bila kulipa waanze kulipa madeni yao mara moja kwa hiyo fedha hizo ndizo hasa zitatumika katika kuboresha tasnia hii.

Sasa ni wakati wa maafisa habari pamoja na waandishi wa habari wote nchini kuunga mkono jitihada za waziri wetu kwa kufanya kazi za kukusanya na kutawanya taarifa kwa ufanisi na usahihi wa hali ya juu ili kuifanya jamii ielewe umuhimu wetu pamoja na kukuza uchumi wa nchi kupitia taarifa tunazozitoa kwenye vyombo vya habari.

Wahenga wanasema Taifa lisilo na taarifa haliwezi kukua kiuchumi, litadumaa. Hivyo tumuunge mkono Mzalendo huyu ili kukuza na kuinua Tasnia ya Habari na ionekane kweli kuwa muhimili wanne wa dola ambao unachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta maendeleo.

RAIS DKT MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA TIC

MAJALIWA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA NSSF.

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria wananchi waliobadili matumizi ya Ardhi ya makazi na kuyageuza kuwa maeneo ya biashara

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Kodi toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Bi.Rehema  Kilonzi   akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu  mapato yaliyokusanywa kutokana na kodi ya pango la ardhi kwa mwaka  fedha 2015/2016 ambapo Serikali imekusanya zaidi ya Bilioni 60 kati ya bilioni 70 zilizopangwa.kulia kwake ni mwanasheria toka Wizara hiyo Bw.Seif Hiza na mwisho ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Bi Mboza Lwandiko.

 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu mkakati wa Serikali  kuwachukulia hatua  za kisheria wananchi waliobadili matumizi ya Ardhi ya makazi na kuyageuza kuwa maeneo ya biashara na kuisababishia Serikali kukosa mapato yanayostahili.(Picha na Fatma Salum-Maelezo)

Frank Mvungi-Maelezo

Serikali imesema itawachukulia hatua kali za kisheria wananchi waliobadili matumizi ya Ardhi ya makazi na kuyageuza kuwa maeneo ya biashara na kuisababishia Serikali kukosa mapato  ya kodi ya Ardhi.


Hayo yamebainishwa  leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Kodi toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Bi.Rehema  Kilonzi wakati  akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu  mapato yaliyokusanywa kutokana na kodi ya pango la ardhi kwa mwaka  fedha 2015/2016.


Amesema kuwa  baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali nchini wameyageuza maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya makazi ya watu kuwa nyumba za kulala wageni,hosteli, maeneo ya biashara kinyume cha Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 chini ya fungu la 33.


“Rai yetu kwa wananchi waliopata fursa ya kumiliki maeneo yaliyopangwa na kumilikishwa kisheria,tunawaomba walipe kodi ya Pango la ardhi kwa wakati kuepuka usumbufu wa kufikishwa Mahakamani .”alisisitiza  Kilonzi.


Amesema katika kipindi cha mwaka wa 2015/2016 Serikali imefanikiwa kukusanya kiasi cha Bilioni 60 kutokana na kodi ya Pango la Ardhi ambazo ni sawa na asilimia 85 ya lengo lililowekwa la kukusanya shilingi bilioni 70.


Amesema  mkakati wa wizara  hiyo ni kuhakikisha kuwa inafikia lengo la kukusanya Kodi  hiyo na kuongeza kuwa hiyo imesambaza maafisa wake katika Ofisi zote za Kanda ili kuhakikisha kuwa Halmashauri na Manispaa zinasambaza hati za madai ya Kodi ya pango la Ardhi na kuwafikia wadaiwa wote kwa wakati muafaka.


Amesema wizara hiyo inaendelea na mkakati wa kufungua mashauri ili kupata kibali cha mahakama cha kukamata mali za wadaiwa sugu na  kuwapokonya hati milki katika maeneo mbalimbali nchini.


Akizungumzia hatua hiyo amesema kuwa katika  jiji la Dar es salaam mashauri yataanza kusikilizwa katika Baraza ya Nyumba na Ardhi La Wilaya ya Kinondoni kuanzia mwezi Mei 2016,  kisha zoezi hilo litaendelea kwa Mikoa na Wilaya zote Jijini hilo.


Akitoa ufafanuzi kuhusu Kodi ya Ardhi inayotozwa na wizara hiyo amesema kuwa  inatozwa kwa kuzingatia Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 chini ya fungu la 33.


Amesema kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu ( kuanzia Februari 2016) Wizara imewafikia  wamiliki wa Ardhi 679 katika Maeneo ya Sinza na Kijitonyama Jijini Dar es salaam na kufanya uthamini wa maendelezo kwa kwa wale waliokiuka masharti ya matumizi yaliyopangwa ambapo ilibainika kuwa kuna ukiukwaji wa masharti ya Uendelezaji kwa kubadili matumizi yaliyoainishwa katika milki zao.



Aidha, amesema kutokana na uthamini uliofanyika mwezi Februari Serikali inatarajia kukusanya jumla ya milioni mia nane kama faini kutokana na ubadilishaji wa matumizi ya maeneo usiozingatia Sheria za Ardhi katika maeneo ya Sinza na Kijitonyama.

GSM FOUNDATION NA MOI WAANZA KAMBI ZA UPASUAJI BUGANDO.

$
0
0
Jumla ya watoto 120 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza, kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa nalo chini ya udhamini wa taasisi ya GSM ambayo imedhamini zoezi hilo litakalofanyika katika mikoa mitano ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne zinazotarajiwa kufanyika tanzania nzima. 

Akiongea na waandishi wa habari katika uzinduzi wa zoezi hilo linalojumuisha madaktari Bingwa 10 kutoka Taasisi ya mifupa na Upasuaji MOI, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta aliishukuru taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.

Dk Kien aliwaambia wanahabari kwamba jumla ya watoto 2000 huzaliwa na vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu ambapo pia kwa Tanzania nzima, wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa wako tisa tu.

Cha kusikitisha ni kwamba kati ya hao, ni wachache sana hurudi kwa ajili ya matibabu bali wengi wao hufariki kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha kwa imani za kishirikina ama kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za matibabu.

PICHANI JUU: Mkuu wa Hospitali ya Bugando, Profesa Kien Mteta(kushoto) akiongea na wanahabari huku akisikilizwa kwa umakini na Halfan Kiwamba(kulia) na Mkurugenzi wa taasisi ya Mifupa na upasuaji Dk Othman Kiloloma(katikati)

 Mtaalamu wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya Fahamu, Dk Gerald Mayaya akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusiana na kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa katika Hospitali ya Bugando
 Meneja Mkuu wa taasisi ya GSM, Shannon Kiwamba (katikati) akiongea na wanahabari kuhusiana na sera yao mpya ya kusaidia watanzania katika masuala ya elimu na Afya, kulia kwake ni Mkuu wa Hospitali ya Bingando, Prof Kien Mtena na kushoto kwake ni Mkuu wa mawasiliano wa Taasisi ya GSM, Halfan Kiwamba
 maelezo ya ufafanuzi yakiendelea kutolewa na Halfan Kiwamba(Wa pili kutoka kushoto) kutoka GSM Foundation.
 Mkuu wa kitenngo cha Upasuaji na Mifupa ambaye ndio mratibu wa kambi ya tiba ya watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi akifafanua jambo kwa wanahabari(hawapo pichani)
 Baadhi ya wahudumu wanaoshiriki kambi ya watoto wenye vichwa vikubwa wakisikiliza viongozi wao wakatiwakiongea na wanahabari
 Wanahabari kazini

 Ufafanuzi ukiendelea...
 Picha ya pamoja ya wawezeshaji wa zoezi la kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi 
 Mkuu wa Hospitali ya Bingando, Prof Kien Mtena (kulia) katika picha ya pamoja na mwanahabari wa Jembe Fm Mwanza G. Sengo.
Taarifa kwa umma kupitia mabango ya Hospitali ya Rufaa Bugando. 

DC HAPI ATEMBELEA WANANCHI BUNJU, MBWENI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Hapi leo amewatembelea wananchi maeneo ya Bunju na Mbweni waliokuwa na kero mbalimbali.

Katika eneo la Bunju Kilungule, baadhi ya wananchi nyumba zao zimezungukwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Mkuu wa Wilaya akiambatana na Katibu tawala wa Mkoa wa Dar es salaam na mainjinia wa manispaa alitembelea eneo hilo na kuona adha inayowapata wananchi.

Akipokea maelezo ya Mwenyekiti wa serikali ya mtaa na baadae kuzungumza na wananchi wa eneo hilo, mkuu wa wilaya aliambiwa na baadhi ya wakazi wa asili wa eneo hilo kuwa sehemu hiyo ilikua ni bwawa la maji miaka yote.

Wakazi hao ambao nyumba zao zimezungukwa na maji walimuomba Mkuu wa wilaya kusaidiwa pampu kubwa ili maji hayo yavutwe na kupelekwa kwenye mitaro upande wa pili wa barabara.

Akijibu maombi hayo Mh. Hapi aliwaagiza mainjinia wa manispaa kuhakikisha kuwa wanafanya utaratibu wa kupata pampu kubwa ya kuvuta maji hayo. Aidha, Mkuu huyo wa wilaya ya Kinondoni aliwaambia wananchi kuwa wale wote waliojenga  katika eneo hilo ambalo ramani inaonesha kuwa ni eneo la wazi wajiandae kuondoka.

"Serikali itawasaidia kutoa haya maji kama hatua ya dharura. Lakini suluhu ya kudumu ni kuwa waliojenga hapa wote wamejenga eneo la wazi tena ni bwawa. Hivyo lazima wajiandae kuhama.
Serikali kazi yake ni kuwaambia wananchi ukweli, hata kama ukweli huo utakua na maumivu. Hivyo ukweli wa jambo hili ni kuwa waliojenga hapa wahame."

Akitoa rai kwa viongozi wa serikali ya mtaa ambao wameshiriki katika kuuza eneo hilo kinyume na taratibu mh. Mkuu wa Wilaya aliagiza na kusema

" kila Mwananchi aliyejenga hapa aende ofisi ya mtaa kujisajili akiwa na vielelezo vyote vya kumiliki eneo hili na alikonunua. Kisha nipewe taarifa na uhakiki utafanyika. Kama kuna viongozi wa serikali ya mtaa walishiriki kuuzia watu viwanja hapa kinyume na ramani ambayo wao wana nakala yao basi wajiandae kuwajibishwa."

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya alitembelea eneo la Mbweni ambako Mwananchi asiyefahamika amejenga ukuta kuzunguka eneo la wazi. Hapi alifika eneo hilo na kujionea ukuta huo kisha akaagiza mtendaji wa mtaa pamoja na anayejenga ukuta huo kufika ofisini kwake kesho Ijumaa mchana wakiwa na vielelezo vyote na vibali vya ujenzi kama wanavyo.

Ziara ya mkuu wa wilaya inaendelea muda huu katika maeneo ya barabara za Sinza ambazo wakandarasi walipewa kujenga.


WADAU MBALIMBALI WAOMBWA KUJITOKEZA KUWASAIDIA WALEMAVU

$
0
0
Katibu Mkuu akiwa anatoa msaada katika shule ya watoto wenye ulemavu wa akili  na viungo katika shule ya msingi mreyai iliyoko ndani ya wilaya ya rombo.
 Shaka akiwa anapanda MTI katika shule ya watoto wenye ulemavu mreyai rombo
Shaka akiwa na baadhi ya wanafunzi

Na Woinde Shizza, Rombo
Viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara, viongozi wa kiserikali na wafanyajazi wametakiwa kuwajali na kuwathamini sana watoto wenye ulemavu na wanaoishi kwenye mazingira magumu kwani wao pia ni binadamu wanao sitahili kupata haki na mahitajj muhimu ya kibinadsmu

Hayo yamebainishwa  leo na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wakati alipotembelea shule ya msingi Mreyai iliyopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro yenye  huduma ya watoto wenye ulemavu wa viungo na Mtindio wa akili.

Alisema kuwa ni muhimu kuwajali sana watoto wenye ulemavu kwani wakitengenezwa vizuri na kuandaliwa vizuri kwa kupewa elimu watakuwa viongozi wazuri wa baadae. 

Aidha alivitaka vyama Vya siasa vijielekeze kutatua changamoto na ma tatizo ya watoto ambao ni Walemavu na sio kuendeleza Kufanya siasa hata sehemu ambayo haitakiwi siasa.

"Napenda kuviambia vyama vingine vya siasa, sasa hivi uchaguzi umeisha, ni kipindi cha kufanya kazi na kuachana na  mambo ya siasa, sasa hivi ni kipindi cha kufanya kazi na kutatua matatizo ya wananchi " alisema Shaka.

Kwa upande wa Mkuu wa shule ya msingi Mreyai, Nuruel Laizer alisema kuwa shule hiyo inahudumia wanafunzi wenye Mtindio wa akili na wanafunzi ambao ni walemavu wa viungo,amesema kuwa shule hiyo inakabiriwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa chakula cha wanafunzi, ukosefu wa vitanda na mgodoro ya kulalia Wanafunzi ambao ni walemavu ,baiskeli kwa ajili ya watoto ambao ni walemavu wa miguu.

Alisema kuwa Wanafunzi hao wanakaa katika mabweni hapo shuleni, lakini wanaupungufu mkubwa wa vitanda na mgodoro,  kwani vitanda ambavyo wana vitumia wameviazima kutoka kwa watu na mda wowote wenyewe wanaweza kuja kuvichukuwa.

Aliomba serekali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia ili watoto hao waweze kuishi kwa amani na furaha kama watoto wengine."watoto hawa wana wazazi lakini wazazi hao hawana uwezo na ndio maana wamewaleta hapa ili wapate elimu, hivyo tunaomba sana serekali na wadau mbalimbali wajitokeze kutusaidia"alisema laizer

Shule hii ya msingi Mreyai imepata msaada wa chakula, maharage, malindi, sabuni, mafuta, miswaki na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka aliaidi kusaidia shule hii vitanda Nane na mgodoro kwa ajili ya wanafunzi hawa wenye ulemavu wa viungo pamoja na Mtindio wa ubongo.

WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI WAUWAWA MKOANI MBEYA

$
0
0
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya (Hawapo pichani)katika kuzngumzia tukio la kuuwawa kwa majambazi watatu wakati wakijaribu kufanya uhalifu katika duka la kuuzia vinywaji mji mdogo wa Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silaha aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine ambayo ilikuwa ikitumika na majambazi hao katika tukio la kutaka kufanya uhalifu kwenye duka la vinywaji mali ya Hamisi mji mdogo wa Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya April 27 mwaka huu.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silahaaina ya panga ambalo linadaiwa kutumiwa na majambazi hao .
Baadhi ya askari polisi wakifuatilia kwa makini mkutano wa kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa mbeya Butusyo Mwambelo wakati akizungumza na waandsihi wa habari kufuatia tukio la kuuwawa kwa majambazi watatu waliotaka kufanya uhalifu katika duka la vinywaji vya jumla linalomilikiwa na ndugu Hamisi Mkazi wa Matundasi Chunya Mkoani Mbeya .
Silaha mbalimbali zilizo kamatwa katika tukio la kuuwawa kwa majambazi wilayani Chnua mkoani mbeya April27 mwaka huu. 

Na EmanuelMadafa,(Jamiimojablogu-Mbeya).

JESHI la Polisi mkoani Mbeya limewauwa watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wa kurushiana rasasi.Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo amesema tukio hilo limetokea April 27 mwaka huu saa 2 usiku , huko katika kijiji cha Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .

Amesema watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na bunduki moja ya aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine , walifika kijijini hapo kwa lengo la kufanya uhalifu kwenye duka la jumla la kuuzia vinywaji mali ya Ndugu Hamis Mkazi wa eneo hilo la Matundasi Chunya..

Kamanda Mwambelo , amesema watu hao ambao miili yao imehifadhi kwenye chumba cha mochwari katika hospitali ya wilaya ya Chunya , majina na makazi yao bado hayajajulikana.Akifafanua, amesema taarifa za siri kutoka kwa raia wema zilifikia jeshi la polisi na ndipo askari polisi walipofika kwenye eneo la tukio.

“Baada ya polisi kufika katika eneo la tukio watu hao walistuka kuwa wanafuatilwa na askari polisi na hivyo kuanza kukimbia kuelekea kijiji cha Matondo kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili MC 761. AFS aina ya Sanlag yenye rangi nyeusi”,amesema Mwambelo .Amesema walipoona Polisi wanawakaribia walianza kurusha risasi hovyo hewani ambapo jambazi mmoja alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi mguuni na tumboni na kufariki dunia ambapo majambazi wanne walifanikiwa kutoroka .

Amesema kutokana na hali hiyo jeshi hilo la polisi lilianzisha msako usiku huo na kufanikiwa kuwaua majambazi wengine wawili ambao huku wengine wakitoroka ambapo msako mkali unaendelea ili kuwakamata wahalifu hao.Amesema katika eneo la tukio, ilipatikana bunduki moja aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 ikiwa na risasi 27 kwenye magazine. Pia pikipiki iliyokuwa iantumiwa na majambazi hayo, iliwezea kupatikana pamoja na panga .

Mwambelo alitoa wito kwamba wananchi waendelee na moyo huo huo wa kuwafichua watu wanaowatilia shaka ili waweze kudhibitiwa mapema kabla ya kufanya uhalifu sanjali na kufika katika hospital ya wilaya ya Chunya kwa lengo la kufanya utambuzi wa miili ya majambazi hao kwani majina yao bado hayajatambulika.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA KWA RAIS VLADMIR PUTIN WA URUSI NA KUFUNGUA MKUTANO WA MAMBO YA FEDHA KWA WANAWAKE LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia unga unaotokana na matunda ya mashelisheli pamoja na bidhaa mbalimbali za matumizi ya Nyumbani zinazofanywa na wajasiriamali wadogowadogo alipotembelea maonesho baada ya kufungua mkutano unaojadili kuhusu  mambo ya kifedha unaoangalia jinsi Mwanamke atakavyoweza kuingia kwenye mifumo yote ya kiuchumi hasa katika upatikanaji wa mikopo na mitaji kwa Mwanamke utakaorahisisha kufanya kazi zao kwa ufanisi. Mkutano huo umefunguliwa leo April 28,2016 katika Ukumbi wa BOT Dar es salaam.(Picha na OMR) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katikati akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam leo April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam leo April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam leo April 28, 2016. Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi.
 picha ya pamoja
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki kikanda na Kimataifa Mhe. Augustine Mahiga akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Urusi Mhe. Denis Manturov aliyeongoza ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Urusi Mhe. Vladmir Putin wakati ujumbe huo ulipofia Ikulu Dar es salaam leo April 28, 2016. Kwa ajili ya kuonana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo kwenye mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia kuhusu kuendelea kuzidisha ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo baina ya Tanzania na Urusi. Katikati Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

RC.MAKONDA AWATAKA WAMILIKI WA KUMBI ZA STAREHE PAMOJA NA WAMILIKI WA BENDI KUPELELEKA MAPENDEKEZO MAPYA SHERIA YA KUFANYA BIASHARA HIYO.

$
0
0
Sehemu ya wamiliki wa Kumbi za Starehe,Bendi na Wanamuziki wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka ,Globu ya Jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiingia katika ukumbi wa Vijana leo kuwasilikiliza juu ya kilio wamiliki wa Kumbi za Starehe,Bendi na Wanamuziki juu ya agizo la kufunga kumbi hizo saa sita leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

WADAU wa Muziki na wamiliki wa bendi wamekutana kwa ajili kuangalia jinsi ya kuweza kuendesha shughuli zao kutokana na sheria ya muziki kufungwa saa sita.

Akizungumza na Wamiliki wa Bendi na Wanamuziki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka watu hao kuunda kamati ya kuona jinsi watavyoweza kubadili sheria kutokana na mazingira ya sasa.Makonda amesema kuwa Watu wenye bendi wanamchango mkubwa katika pato la taifa kutokana na vinywaji kunywewa katika kumbi hizo wakati bendi hizo zikifanya kazi.

Aidha amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa watu wafuate sheria na amri zikitolewa watu wakubali na sio kila mtu kuamuka kufanya yake pamoja na kuangalia haki ya mtu mmoja inayoadhiri watu wengine

Amesema katika watu wanaofanya biashara hiyo wanatakiwa kuangalia katika vipengele moja ni ya muda gani wa kufanya biashara ,wamiliki wa baa ni muda gani wanaweza kuanza , wapi watu bendi wanaweza kufanya muziki.

Makonda amesema kuna vitu vya kuangalia katika kufanya biashara hiyo kuwa ni sehemu gani watapiga na mazingira je kuna hospitali,shule ,kanisa, msikiti.Amesema kamati lazima iwe na majibu ya vitu ambavyo ni vya msingi katika kuendesha shughuli zao bila kuathiri watu wengine.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images