Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 828 | 829 | (Page 830) | 831 | 832 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akikagua matengenezo ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi leo tarehe 25 Aprili 2016 jijini Dar es Salaam
  Mkuu wa wilaya Kinondoni Ally Salum Hapi wa kwanza kulia akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa barabara ya Ali Hassani Mwinyi Halipo tembelea leo kuona maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo.
  Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akiwa na wafanyakazi wa MS ESTIM CONSTRUCTION CO.LTD
  Mkuu wa wilaya Mhe.Ally Hapi akiongea na msimamizi wa ujenzi.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi kushoto akiwa na meneja wa Tanroad katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi leo tarehe 25 Aprili 2016. 

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Salum Hapi leo ametembelea ujenzi unaoendelea wa upanuzi wa barabara ya Mwenge-Morocco kuona maendeleo yake. Barabara hiyo ambayo ilikua na kero kubwa ya foleni iliamriwa kupanuliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli katika hatua yake ya kubana matumizi na kupeleka fedha katika shughuli za maendeleo. 

  Katika ziara yake hiyo Mh. Hapi alitembea umbali wa mita 500 kwa miguu kukagua pia usafi wa mazingira ya kando ya barabara ambapo alipofika katila kituo cha mafuta cha Total, aliagiza uongozi wa kituo kufanya usafi wa mazingira yaliyo mbele ya kituo chao.

  Aidha Mh. Mkuu wa Wilaya pia alizungumza na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam, Mkandarasi na wataalam wengine wa ujenzi na kujua maendeleo yao.

  Meneja wa TANROADS na Mkandarasi walimueleza Mkuu wa wilaya kuwa tayari kazi imekamilika kwa asilimia 90 na kwa mbali wanatarajia kukabidhi mwezi June mwaka huu.

  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Hospitali ya wilaya ya Tengeru (Patandi) inakabiriwa na ukosefu wa vitanda ,hali inayopelekea baadhi ya wagonjwa kulala zaidi ya mmoja katika kitanda kimoja.

  Wakizungumza na mwandishi wa habari hii,Wagonjwa hao mara baada ya kupokea msaada wa vyandarua kutoka kwa wafanyakazi wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) tawi la Arusha, walisema kuwa wao kama wagonjwa wa hospitali hiyo wamekuwa wakipata tabu sana haswa wakati wakiandikiwa kulazwa,kwani wamekuwa wakibanana sana na wakati mwingine wamekuwa wakikosa kabisa vitanda.

  Mmoja wa wagonjwa hao ambaye alijitambulisha kwa jina la Anna Akyoo alisema kuwa wamekuwa wakilala wagonjwa wawili hadi watatu hali ambayo imekuwa ikiwafanya wajisikie vibaya kwani wana banana sana katika vitanda hivyo vichache.
  picha ikionyesha wafanyakazi wa NSSF pamoja na Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Tengeru katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada wa vyandarua
  wafanyakazi wa NSSF wakiwa wanabadilishana mawazo nje ya hospitali hiyo 
  mmoja ya wagonjwa akiwa amekaa kitanda kimoja na watoto wawili wakiwa kila mmoja ana mama yake.
   

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Dkt. Lu alifika Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya  kuzungumza masuala mbalimbali ya kimaendeleo na Rais Dkt. Magufuli. 
   Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing akimkabidhi Rais Dkt. John Pombe Magufuli ujumbe wa barua ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kutoka kwa Rais wa China Xi Jinping Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing wanne kutoka kushoto, Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa wapili kutoka kulia pamoja na maafisa wengine kutoka nchini na Ubalozi wa China.
  Picha na IKULU.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

  CHINA imekubali kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya kati yenye urefu wa kilometa 2,561 kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge" ambao zabuni za ujenzi zinatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

  Balozi wa China hapa nchini Mheshimiwa Dkt. Lu Youqing ametoa kauli hiyo leo tarehe 25 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambapo pia amemkabidhi barua yenye ujumbe kutoka kwa Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping.

  Katika Mazungumzo hayo Rais Magufuli amemweleza Balozi Lu kuwa Tanzania imedhamiria kuanza ujenzi wa Reli ya kati haraka iwezekanavyo na tayari imetenga fedha kiasi cha shilingi Trilioni 1 katika bajeti yake ijayo kwa ajili ya kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi huo.

  "Tuna imani kuwa mradi huu utasaidia kuleta mapinduzi makubwa ya uchumi katika nchi yetu na katika nchi nyingine za Afrika Mashariki na kati zikiwemo Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ndio maana hatutaki kupoteza muda kwa mazungumzo marefu, tunataka kazi ianze na watu waanze kunufaika" Amesisitiza Rais Magufuli.

  Kwa upande wake Balozi China hapa nchini Dkt. Lu Youqing amempongeza Rais Magufuli na serikali yake kwa kujiandaa kwa fedha, vifaa na rasilimali watu kwa ajili ya kutekeleza mradi huu mkubwa na kwamba Serikali ya China, Taasisi za fedha za China na Makampuni mbalimbali yatatoa ushirikiano wote katika utekelezaji wa mradi huu.

  "Kama ambavyo Prof. Mbarawa amefanya mazungumzo na Serikali ya China, Taasisi za fedha za China na Makampuni, naahidi kuwa tutaanza kazi kama ambavyo taratibu na viwango vya ujenzi vimewekwa, tutafanya kazi kwa kujali muda, ubora na gharama nafuu" Amesema Balozi Lu.

  Mradi mzima wa ujenzi wa reli ya kati unatarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani bilioni 6.8 na umepangwa kutekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa kilometa 1,216 za kutoka Dar es salaam - Tabora - Isaka - Mwanza na itajengwa kwa ushirikiano wa Tanzania na China.

  Tayari Rais Magufuli amemtuma Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa Mnyaa kwenda nchini China kukamilisha mazungumzo juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ukiwemo wa ujenzi wa reli ya kati, ambapo Prof. Mbarawa anasema hatua inayofuata sasa ni kutangaza zabuni ya ujenzi wa reli hiyo kwa uwazi, ili makampuni mbalimbali ya ujenzi yaombe na hatimaye kupata washindi watakaoanza kazi mara moja.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  25 Aprili, 2016.

  0 0  0 0

  Watoto wa marehemu kwa umoja wao wakiweka shada la Maua kwenye kaburi la Baba yao.

  Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Joachim Liyumba (68), aliyefariki Aprili 18 na umezikwa mwishoni mwa wiki kijijini kwao, Kwiro, Mahenge Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.Mwili ailaze roho ya Marehemu Mahali pema Peponi-Amin
  Mazishi yalifanyika huku mvua kubwa ikinyesha
  Pamoja na Mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha kijijini hapo,lakini Watu mbalimbali walishiriki kuupumzisha mwili wa Marehemu Liyumba katika nyumba yake milele
   Watoto wa Marehemu Liyumba wakiangua vilio wakati kaburi la Mpendwa baba yao likifukiwa.
  Mwili wa marehemu wa Liyumba ukiwasili katika makaburi yaliyopo nje ya kanisani la Katoriki parokia ya Kwiro jimbo la Mahenge,tayari kwa kupumzishhwa kwenye nyumba yake ya milele.PICHA KWA HISANI YA http://shekidele.blogspot.com/

  0 0

  Na Lorietha Laurence-Maelezo

  Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wametakiwa kuachana na mfumo wa zamani wa kutumia makaratasi katika kuhifadhi taarifa zao muhimu na badala yake kuanza kutumia mfumo wa kisasa wa kieletroniki.

  Hayo yalisemwa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Pof. Makame Mbarawa leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na wafanyakazi hao na kueleza kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza matumizi ya fedha za kununulia karatasi.

  “Katika ofisi zenu nimeona kila mtu anakomputa ni jambo zuri hivyo zitumieni katika kuhifadhi taarifa muhimu za taasisi yenu kwa mfumo wa kieletroniki” alisema Mhe.Prof.Mbarawa.Aliongeza kwa kusema kuwa serikali imetumia fedha nyingi katika kujenga mkongo wa taifa wa kuhifadhi taarifa muhimu hususani za serikali pamoja na Taasisi zake hivyo ni budi waanze kuutumia mkongo huo kwa kuhifadhia taarifa zao.

  Pia amewataka watumishi kuwa waadilifu,wachapaka kazi ,wabunifu na kuwa na uwazi baina ya watendaji wa juu na watumishi wa ngazi ya chini kwa kushirikiana na wafanyakazi wa mikoani . 

  “Watanzania wanamatarajio mengi kutoka kwetu katika kukuza uchumi wa nchi hivyo ni wajibu wetu kutimiza matarajio yao kwa kuwapatia mahitaji muhimu ikiwemo miundo mbinu imara ya barabara, bandari ,shirika la ndege la kisasa na utabiri wa hali ya hewa wenye uhakika ” alisema Mhe.Prof.Mbarawa.

  Prof.Mbarawa alitoa wito kwa kuwataka watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano kila mmmoja kujituma katika eneo lake la kazi ili kuleta matokeo yaliyobora na hivyo kukuza uchumi wa nchi kwa kufikia uchumi wa kati.

  0 0


  0 0

  Mgeni rasmi katika mahafali ya 31 ya kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru ,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania ,Joel Raulent akitoa hotuba yake wakati wa mahafali hayo.
  Mgeni rasmi katika mahafali hayo,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,Joel Raulent akitunuku vyeti kwa wahitimu 390 wa kidato cha sita katika shule hiyo.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
  Wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru wakiimba wakati wakielekea ukumbini kwa ajili ya kuanza rasmi kwa sherehe ya kuwaaga.
  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru Rosemery Tarimo akimuongoza mgeni rasmi katika mahafali ya 31 ya kidato cha sita ,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania ,Joel Raulant (kulia) wakati wakielekea ukumbini kwa ajili ya sherehe za mahafali hayo.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Kongamano la kila mwaka la waTanzania waishio Marekani (DICOTA) litafanyika mwishoni mwa juma hili jijini Dallas Texas.

  Katika kipindi cha Jukwaa Langu jumatatu hii, tulipata fursa ya kuzungumza na viongozi waandamizi wa DICOTA, Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini Lunda Asmani na Mwenyekiti wa DICOTA Dr Ndaga Mwakabuta.Pia wachangiaji mbalimbali
  KARIBU


  0 0

  Wauguzi wa zahanati ya kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakiwaongoza waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliofika kuwatembelea wazee wanaoishi katika kituo hicho kujua jinsi wanavyoishi na kuwa kutambua suala la uzazi wa mpango. Ziara hiyo ya waandishi wa habari iliyofanyika wiki iliyopita iliratibiwa na taasisi inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango (TCDAA) wakishirikiana na Marie Stopes Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. 
  Moja ya nyumba wanayoishi wazee hao.
  Waaandishi wakiendelea kufanya mahojiano na Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi.
  Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakiendelea na kazi za mikono. 
  Mmiliki wa Blog ya Kajunason akimsaidia kusuka kikapu mmoja ya wazee anayelelewa katika kituo hicho. 
  Ofisa Mfawizi wa Makao ya wazee wasiojiweza, Michael Bundala akifanya mahojiano na waandishi wa habari ambapo katika mahojiano hayo alielezea kuwa kuna changamoto nyingi za kuishi na wazee hawa kama kiongozi kwa vile wazee wamekuwa wakorofi mno na kuona siwatendei haki katika maamuzi ambayo nimekuwa nikiyatoa ikiwemo katika ugawaji wa vyakula. 

  --- Na Cathbert Kajuna - Mwanza. 

  Wazee wanaoishi katika kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wanaiomba Serikali kuwapatia huduma za afya katika Zahanati ya kituo chao. Wazee hao wanaeleza kwamba changamoto hizo katika ziara ya waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliounganishwa pamoja na kuratibiwa na taasisi inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango (TCDAA) na Marie Stopes Tanzania. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wazee hao wanasema katika zahanati hiyo hakuna dawa na wanapoumwa wanalazimika kununua dawa.

   Mwenyekiti wa kambi hiyo, Helen Emmanuel anasema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za huduma ya afya pamoja na wenzao wasiojiweza kufukuzwa kambini. "Tunapofika katika zahanati hii daktari anatupima vizuri lakini hakuna dawa hivyo anatuandikia kwenye karatasi anatuambia tukanunue. "Kwakweli hii ni changamoto kubwa sana kwetu kwasababu wakati mwingine tunapoandikiwa dawa hela ya kununulia tunakosa hali inayosababisha tunaendelea kuumia kutokana na kwamba afya zetu ndio hizi na hatuna sehemu ya kujipatia kipato" alisema Heleni. Pia alisema kwa sasa wapo wazee 78 katika kambi hiyo lakini wapo walemavu wenzao saba ambao wameambiwa wahame kambini waende vijijini wakati hawana uwezo. 

   "Kwakweli inaumiza sana kwasababu hawana uwezo wa kujitafutia pia mimi sina uwezo wa kuwasaidia kwasababu mimi mwenyewe ni mlemavu ,"alisema. Ofisa Mfawizi wa Makao ya wazee wasiojiweza,Michael Bundala alisema hapa kambini tuna watoto 17 ambao wazazi wao wako humu kambini na wengine waliotimiza miaka 18 tuliwapunguza na kuwatengea eneo kwa ajili ya makazi na tusingefanya hivyo tungekuwa zaidi ya 800 kwasababu wengine wanapeana mimba wenyewe kwa wenyewe. Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Kigongo Kata ya Idetemya,

   Sebastian Kisumu alisema ipo changamoto ya vijana wa nje kuwapa mimba wasichana wa kambi hiyo. Alisema wapo wataalamu mbalimbali mambo wanafika katika kambi hiyo kutoa elimu ya uzazi wa mpango lakini wengi wao hawaipokei hali inayosababisha kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao hawana baba.

  Waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliotembelea Wazee wa kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi wakifanya mahojiano ili kujua changamoto mbali mbali zinazowakabili ambapo wazee hao walisema jambo kubwa linalowaumiza kicha ni upatikanaji wa matibabu katika zahanati yao jambo linalowafanya wengine kuishi na maradhi kwa muda mrefu. 

  0 0

  Mwalimu Julius Nyerere (kushoto) na Sheikh Abeid Amani Karume (kulia) wakibadilishana Hati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili, 1964.

  Na Emmanuel J. Shilatu.
  Ni miaka 52 imetimia tangu jahazi lililowabeba Watanganyika na Wazanzibar liweke historia ya kung’oa nanga mara baada ya Jamhuri Muungano wa Tanzania kuzaliwa rasmi mnamo April 26,1964. Hii ilitokana na ujasiri, ushupavu na nia ya dhati waliyokuwa nayo waasisi wa Muungano huu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanganyika) na Abeid Aman Karume (Zanzibar).

  Hatua hiyo ilifikiwa kutokana na mtiririko wa kimazingira na mahusiano ambayo yalishabihiana kama sio kufanana kabisa kwa pande zote mbili (Tanganyika na Zanzibar). Zipo sababu za kijiografia, kisayansi, kitamaduni na kihistoria zilizochangia huu muungano wetu.

  Kutokana na sababu za kijiografia na kisayansi inaaminika kabisa kwamba Visiwa vya Zanzibar (Pemba na Unguja) vilikuwa vimeungana na hata kushikamana kwa pamoja pembezoni mwa pwani ya ardhi ya Tanganyika. Hivyo tangu awali tulikuwa ni kitu kimoja, tulio katika ardhi moja na ya pamoja.

  Pia kuna historia (isiyo na shaka) ya muingiliano wa kiutamaduni baina ya Wakazi wa Tanganyika na Zanzibar ambapo hali nzima ya kuoa ama kuolewa ilizidi kushamiri baina yao.

  Halikadhalika harakati za kudai ukombozi wa uhuru wetu ili tuweze kujitawala wenyewe kutoka kwa dudu la wakoloni nazo zilichangia kutuunganisha. Inaaminika (na ndiyo ilivyo) ya kuwa asilimia kubwa ya Wazanzibar walishiriki kwenye harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Mwingereza ambapo kutokana na nia, ushupavu na nguvu ya pamoja walifanikiwa kupata Uhuru wa Tanganyika mnamo Desemba 9, 1961.

  Lakini pia licha ya asilimia kubwa ya Wazanzibar kushiriki katika mchakato wa Mapinduzi ya Zanzibar lakini pia kulikuwepo na asilimia kubwa ya mchango wa ushiriki kutoka kwa Watanganyika. Hatimaye matunda yake yalionekana ya mapinduzi matukufu yaliyofikia kilele katika uwanja wa Gombani Pemba yaliyofanyika Jamhuri 12, 1964, baada ya kuchoshwa na hila na ghiliba za Waarabu uliotamalaki visiwani humo kwa zaidi ya karne mbili na hatimaye waliwaacha wazalendo watwana katika ardhi yao.

  Pia tusisahau lengo na nia ya dhati aliyokuwa nayo Mwalimu Nyerere ya kutaka kuiunganisha Afrika mzima kwa hatua lakini jitihada zake zilianza kuzaa matunda ambayo hayatakaa yatokee tena Afrika kwa kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar.

  Mnamo April 22, 1964, Maraisi wa nchi hizi mbili ambazo sasa zinaunda Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (wa Jamhuri ya Tanganyika) na Abeid Amani Karume (wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar ) walitia sahihi Mkataba wa kimataifa wa kuunganisha nchi zao, unaojulikana kama “Hati ya Muungano” (Articles of union) na hivyo kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ama United Republic of Tanganyika and Zanzibar (URTZ) ambao ni muungano sahihi kabisa kisheria na unaotambulika Kikatiba.

  Siku ya Jumatatu ya tarehe 26 Aprili, 1964 viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee kwa nia ama lengo moja tu la kubadilishana “Hati za Muungano”.

  Wananchi wa Tanzania walipiga kura kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa kwanza kabisa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo mwaka 1965.

  Kama nilivyodokeza kwamba Muungano wa Tanzania ulifikiwa kwa kutiwa sahihi mkataba unaoitwa Hati ya Muungano (Articles of the Union) na wakuu wa nchi hizi mbili, Mwalimu Nyerere (Tanganyika) na Abeid Karume (Zanzibar) Aprili 22,1964 na kuridhiwa na mabunge ya nchi hizo Aprili 25, 1964 na hatimaye kuwa sheria ya Muungano ya (Acts of Union) ya mwaka 1964.

  Kimsingi sheria ya Muungano ndiyo iliyoanzisha na ndiyo iliyopewa haki ya chombo cha kikatiba kinachodhibiti katiba zote mbili za Serikali ya Muungano.

  Mwanzoni kabisa Hati ya Muungano (Articles of Union) iliyomo ndani ya sheria ya Muungano iliorodhesha na hata kudadavua mambo 11 ya Muungano. Mambo hayo ni kama vile:- Mambo ya nchi za nje, Ulinzi na usalama (lakini si usalama wa Taifa); Polisi, Uraia, uhamiaji, mikopo na biashara za nchi za nje, utumishi katika serikali ya Muungano, kodi ya mapato, usimamizi wa fedha, Bandari, Usafiri wa anga, Posta na simu.

  Kwa nia safi na malengo mazuri yanayojitokeza Hati ya Muungano imekuwa ikiboreshwa zaidi kwa kadri siku zinavyozidi kusonga mbele kwa malengo kusudi ya kuleta umoja, mshikamano, amani na utulivu wetu ule ule tulioanza nao awali na halikadhalika maridhiko yanayoendelea kuufanya Muungano huu uendelee kudumu hadi hii kesho.

  Ndio maana mtu timamu hatoshangaa sana kuona Hati ya Muungano ikiendelea kuboreshwa kila siku (na itaendelea hivyo) ambapo ilianzia na mambo 11 ambapo hii leo yamefikia takribani 23.

  Mengineyo ama baadhi ya yale yalioongezeka ni kama vile;- Noti; Elimu ya juu,; Maliasili na mafuta (mafuta) yasiyochujwa, bidhaa za mafuta na gesi asilia , ya mwaka 1968; Baraza la Mitihani ya Taifa; utafiti; utabiri wa hali ya hewa; Takwimu,; Mahakama ya Rufaa ya juu ya mwaka 1979; pamoja na uandikishwaji wa vyama vya kisiasa .


  Tusisahau mwaka 1965 iliundwa katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (The Interim Constitution of The United Republic of Tanzania) mpaka kufikia mwaka 1977 ndipo ilipoundwa katiba ya kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndiyo inaendesha nchi hadi sasa.

  Mwaka huo huo wa 1977 (yaani miaka 13 baada ya Muungano kutokea) kulikuwa na muungano wa vyama vikubwa viwili kuungana kutoka pande zote mbili (Bara na Visiwani). Vyama hivyo ni TANU (Tanganyika African National Union) pamoja na ASP (Afro Shiraz Party) cha Zanzibar kuungana na kuunda Chama cha Mapinduzi (CCM) .

  Hatua ama vitendo na mafanikio hayo si tu kwamba yalidumisha bali hata yaliendeleza kukuza Muungano wetu ambao Jahazi lake liligubikwa na misukosuko ya mawimbi makubwa baharini uliojaa uzito wa mambo mbalimbali uliokuja kwa sera ya kero zilizoleta chokochoko mbalimbali katika Muungano wetu., ambao hatutakiwi kamwe kuusahau maishani mwetu. 

  Tusisahau mchezo mchafu uliojaa rafu za kutisha uliotaka kufanywa na Bunge miaka ya 1990 na 1992 ya kutaka kuyakubali madai yaliyotolewa na kundi la G55 ambalo lilitaka kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika , hali hii ingetuvuruga kwani ilihitaji uwepo na serikali tatu yaani Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hakika yatupasa tuzishukuru hekima na busara za Mwalimu Nyerere kwa kutuokoa na chokochoko ya kero hii.

  Pia tusiisahau kero ama chokochoko nyingine ya Muungano wetu iliyoibuka Decemba 1, 1992, ambayo Zanzibar ilitaka kujiunga na umoja wa Nchi za Kiislam Duniani (OIC) kama nchi nje ya Muungano.

  Tuendelee kukumbuka ni kwa jinsi gani Zanzibar iliyokuwa inasaka ukuu nje ya Muungano kwa kuibua madai ya Bendera ya Taifa lake (Zanzibar), wimbo wa Taifa, na nembo yao ya Taifa.

  Kwa nyakati tofauti tofauti tumekuwa tukisikia baadhi ya Wazanzibari walio wachache wakiilalamikia hali nzima ya ongezeko la mambo kwenye Hati Muungano (Articles of Union) kutoka mambo 11 hadi kufikia 23 ambalo ni sawa na ongezeko la mambo 12 ambao kwa baadhi yao hawaoni umuhimu wa wa uwepo wake na hata kutishia kujitoa. Ila asilimia kubwa ya Wazanzibari wanayaunga mkono, hali iliyo sababisha hoja ya wachache kuzidiwa nguvu.

  Pia tumekwisha sikia jinsi gani Wazanzibari wanavyotaka jambo la maliasili ya mafuta pamoja na mafuta yasiyochujwa na aina nyingine za mafuta au bidhaa na gesi asilia iondolewe katika masuala ya Muungano ili Zanzibar ipate kunufaika zaidi na maliasili zake. 

  Kukuru kakara za Wazanzibari zinatookana na madai yao ya kuwa Tanganyika(Bara) imeimeza Zanzibar (Visiwani) katika masuala mazima yahusuyo Muungano. Ikumbukwe Ubaguzi wa dhana ya Tanganyika umeimeza Zanzibar si ya kweli na hii imebainishwa katika katiba ya Muungano kuwa kuna Serikali ya Jamhuri ya Muungano na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Haya ni mapenzi ya dhati waliyoonyesha kwa Wazanzibari kwa kuwaruhusu wawe na serikali yao ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ikumbukwe Serikali ya Muungano inaongozwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaongozwa na Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar na chombo chao cha kutunga sheria kinaitwa Baraza la Wawakilishi.

  Ndugu zangu hali ya kupuuzia na hata kuuchezea Muungano wetu ni hatari sana tena ni dhambi iliyotukuka. Mathalani Wazanzibari wakiamua kujiengua kwenye huu Muungano ili wawe kivyao vyao,hawatabaki salama. Mwalimu Nyerere alishawahi kusema ya kuwa “wakifika kwenye hatua hiyo watagundua kuwa ndani yao kuna Wazanzibari na Wazanzibara”. Nao wataamua kuwafukuza wale wa Wazanzibara, lakini hiyo haitakuwa mwisho. Punde si punde watajigundua kuwa nao (Wazanzibari) wamegawanyika kwani kuna Wapemba na Waunguja, na wakifikia hapo pia hawatakuwa salama ni lazima machafuko yatatokea.

  Daima Wazanzibari watambue ya kuwa dhambi ya kutokutamalaki kwa dhana ya Unguja na Pemba unatoka na kufunikwa na kivuli cha mwamvuli cha Muungano. Hivyo umoja, mshikamano, amani na utulivu wao unategemea sana uwepo wa nguzo hii imara ya Muungano huu tulionao.

  Vivyo hivyo kwa watu wa Bara (Tanganyika) ni rahisi kwao kutafunwa na dhambi ile ile ya ubaguzi watakayo ianzisha nje ya uwepo wa Muungano ni rahisi sana kwa ukabila, udini, ukanda na hata U-rangi kutamalaki ndani ya jamii wakishafikia hapo, hawatabaki salama kwani watachafuana tu.

  Muungano huu tulionao unawafanya wale wageni, mataifa ya nje na watu wote wenye hila, donge, roho ya korosho kuogopa kutugusa na kutuvuruga kutokana na kuwepo kwa nguvu kubwa ya umoja, ushirikiano na mshikamano baina yetu. 

  Muungano huu wetu unatupatia fursa kubwa ya uhuru wa kusafiri kwa pande zote iwe ni bara ama ni visiwani. Leo hii ni rahisi sana kwa mtu wa bara kwenda Visiwani na hata wale wa Visiwani kuja Bara kwa uhuru zaidi kwani Uhuru huo wa uwepo wa nafasi hiyo umeshalipiwa na huu Muungano wetu tulionao. 

  Kutokana na uwepo wa uhuru wa kusafiri usio na mipaka baina yetu, pia Muungano wetu tulionao unazidi kutuongezea fursa na nafasi zaidi ya uwanja mpana wa ufanyaji biashara. Hali hii imesababisha uwepo wa mzunguko mkubwa wa pesa ndani yetu kwani si jambo la ajabu kuona pesa zikitoka Visiwani (Zanzibar) kuja Bara (Tanganyika) kupitia mabadilishano ya bidhaa kama vile nafaka, kahawa, matunda, vipuri vya magari na kadhalika. 

  Pia si jambo geni tena kwa sasa kuona pesa zikivuka Bahari na kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya ufanyaji ama ununuzi wa biashara kama vile Magari, nazi, Karafuu, Tende na kadhalika.

  Muungano huu unatuzidishia fursa ya mianya ya uwanja mpana tena usio na kikomo wa ufanyaji biashara, Muungano huu hautubagui ama kutojulisha au kuwa na upendeleo wa upatikanaji wa Elimu bora, huduma za kijamii bora, Muungano hautugawi wala kuwa na upendeleo bali umejaa uwiano sahihi wa upatikanaji wa mabo yote ya msingi yaliyomo ndani ya “Hati ya Muungano” (Articles of union). Muungano huu ni nguzo imara katika muktadha mzima wa nyanja za kimaisha yetu. 

  Ni ukweli uliodhahiri kuwa haitakaa itokee Muungano kama huu (wa Tanganyika na Zanzibar) hapa Barani Afrika umoja ushirikiano, ushikamano, amani na utulivu ni sehemu mojawapo ya manufaa ya Muungano huu. 

  Njia mojawapo ya kuwaenzi vyema waasisi wetu ni kwa kuudumisha Muungano wetu ambao ni urithi wa aina yake waliotuachia. Watanzania yatupasa tuenzi Muungano wetu kwa kuulinda na kuudumisha kwa vitendo kwani ni nguzo na fahari ya kipekee na ya aina yake Barani Afrika.

  Endapo itatokea kiongozi yeyote Yule ama utawala wowote ule utakaokuwa na malengo ya kuubomoa ama kuuvunja Muungano huu, basi ajue dhambi hii itamtafuna yeye na kizazi chake milele.

  Mungu atuepushe na mawazo ya kuuvunja Muungano huu vichwani mwa viongozi/watawala wetu, atuepushe na balaa hili lisijitokeze kwenye Katiba Mpya ijayo. Kheri ya Miaka 52 ya maadhimisho ya Muungano!!
  Tuwasiliane 0717 488622 www.ndgshilatu.blogspot.com

  0 0

  Mgogoro uliokuwa unaashiria kuvunja amani kati ya vijiji viwili Ilore (wilaya ya Kilolo) na Ilambilore (wilaya ya Iringa),ulitulizwa na wakuu wa wilaya ya Kilolo Mh Selemani Mzee na  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela ambao walipofika kwenye eneo la tukio na kukutana na wananchi wa vijiji vyote viwili ambao walikuwa na hasira huku kila mmoja akidai mwenzie kaingilia eneo la mwenzake. 

  Katika mgogoro huo eneo la kijiji cha kitongoji cha Igominyi kwenye gazeti la serikali linaonyesha kipo Kijiji cha Ilore (Kilolo) lakini kwenye ramani ya mpaka wa wilaya kinaonyesha kipo Ilambilore (Iringa). wakuu hao waliahidi ndani ya siku 30 wataleta jibu.

  Mkuu wa wilaya ya Kilolo alipiga marufuku wananchi kujichukulia madaraka na kuanza kufyeka msitu. Naye Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Kasesela aliagiza wafugaji wasivushe kabisa mifugo yao kwenda upande wa wenzao. Pia ni wakati mufaka wafuigaji wakaacha kuwa wachungaji bali wafugaji hii iwe ni pamoja na kubadili aina ya mifugo.

  Mfugaji maarufu aitwaye Selemani alilaumiwa kwa mifugo yake kuvuka na kula mazao katika mashamba ya watu. Mkuu wa wilaya ya Iringa alimuamuru Mfugaji huyo kulipa kiasi cha shilingi 90,000/ na debe 2 za mahindi. Pia kufanya tathmini ya shamba la mkulima mwingine ili nalo lilipwe fidia. kikao hicho kiliisha mnamo majira ya saa 10 jioni.
  Kikao hicho kikiendelea  kati ya wananchi wa kijiji cha  Ilore (wilaya ya Kilolo) na Ilambilore (wilaya ya Iringa),kufuati mgogoro wao wa mipaka kati ya kijiji na kijiji.
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela  akizungumza na baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo katika suala zima kuleta amani miongoni mwao.
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela  akipewa ufafanuzi kutoka kwa mmoja wa wananchi wa vijiji hivyo katika suala zima kuleta amani miongoni mwao.

  0 0  0 0


  Pichani ni Mwanamuziki wa Muziki wa Kizazi Kipya anae tamba kwa Nyimbo kadhaa kutoka WCB Harmonize anaetarajiwa kufanya Makamuzi ya Nguvu katika Kilele cha kumpata Mshindi wa Shindano la Miss Mbeya 2016 lililo andaliwa na Redio Dream FM 91.3 Mbeya kwa kushirikiana na Michuzi Blog, Pepsi, Ufunuo Clinic, Access Computer Limited, Viva Night Club, Milo Group Limited, New karim Hardware, City Pub, Paradise Inn Hotel, Club K-Mo, Ace Classic Wear, Ally Rich Sanaa Art, New Mama Land Pub, Beaco Resort na Manyanya Inn Hotel and Tours na wasanii wanaofanya vizuri Nyanda za juu Kusini nao pia wataangusha bonge la shoo si yakukosa hiii ni Tarehe ishirini ya Mwezi wa Tano 20-05-2016 na sio Tarehe Sita tena....
  Baadhi ya Washiriki wa Shindano la Miss Mbeya 2016 wakiwa katika Pozz la Pamoja wakipata Taswira Mwanana..
  Washiriki wa Shindano la Miss Mbeya 2016 wakiendelea kupata Taswira kutoka kwa Mpiga Picha Mahiri Nyanda za Juu Kusini Mr.Pengo hayupo Pichani..
  Washiriki wa Shindano la Miss Mbeya 2016 wakiendelea Kujinoa kuajiri ya Shindano la kumpata Miss Mbeya 2016 linalo letwa kwenu na Redio Dream FM 91.3 Mbeya kwa kushilikiana na Michuzi Blog, Pepsi, Ufunuo Clinic, Access Computer Limited, Viva Night Club, Milo Group Limited, New karim Hardware, City Pub, Paradise Inn Hotel, Club K-Mo, Ace Classic Wear, Ally Rich Sanaa Art, Mzee wa chimbo blog, New Mama Land Pub, Beaco Resort na Manyanya Inn Hotel and Tours .PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0  0 0

  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Lucas Mweri akisoma mapendekezo mbalimbali kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi (kushoto) ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jackson Sipitieck. 

  Na Woinde Shizza,Simanjiro

  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Mahmoud Kambona ametoa wiki moja kwa wajumbe 12 wa Serikali ya Kijiji cha Kambi ya Chokaa waliosusa kutumikia nafasi hiyo kurejea ofisini au uchaguzi mwingine ufanyike.

  Inadaiwa kuwa wajumbe hao walisusa kufanya kazi wakipinga kuchaguliwa Mwenyekiti Mbuki Mollel badala ya Joshua Kuney, hivyo shughuli za utawala kwenye kijiji hicho zinashindwa kufanyika kutokana na kutokuwepo uongozi. 

  Kambona alitoa agizo hilo juzi mbele ya baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo kwani michango na huduma za kijamii hazifanyiki na kiongozi aliyepo ni mtendaji wa kijiji pekee tangu mwaka juzi uchaguzi ulipofanyika.

  Alisema anawapa muda wa wiki moja viongozi hao warudi ofisini na endapo hawatakubaliana na hali hiyo uchaguzi ufanyike upya kujaza nafasi hizo il ishughuli za kiutawala wa kijiji hicho ziendelee kwa manufaa ya wananchi.

  Kwa upande wake, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Lucas Mweri alibainisha vyanzo vya mapato vinavyotarajiwa kukusanywa na halmashauri ambavyo awali vilikuwa vinakusanywa na vijiji.

  “Vyanzo vya ushuru wa mchanga, kuni kavu na samaki wakavu, ambavyo awali vilikuwa vinakusanywa na vijiji, hivi sasa vitakusanywa na halmashauri kisha itatoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya vijiji husika,” alisema Mweri.

  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Jackson Sipitieck, alisema makusanyo na ushuru unapaswa kufanywa na halmashauri, kisha inarudisha kwa jamii kutokana na kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

  “Huko vijijini ndipo kunaliwa fedha za ushuru na michango mbalimbali, hivyo halmashauri itakusanya na kurudisha kwa kujenga shule, barabara, zahanati na kuibua miradi mingine ya maendeleo kama inavyofanya,” alisema Sipitieck.

  0 0

  IMG_8603

  Mwanzilishi wa Taasisi ya Fazel, Dkt. Sajjad Fazel akisalimiana na Diwani wa Kigogo, Bw. Manyama wakati wa funguzi wa huduma ya upimaji wa afya bure kwa wakazi wa Kigogo. Katikati ni Imam wa Msikiti wa Al Ghadir, Sheikh Jalala.(Picha na habari na Modewjiblog).

  Kwa kuhakikisha jamii inakuwa katika hali ya usalama wa kiafya, Taasii ya Fazel Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Afya na Madawa (TAHMEF) wametoa huduma ya upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi wa Kigogo, Dar es Salaam.

  Zoezi hilo lilifanyika Aprili, 23 katika Msikiti wa Al Ghadir uliopo Kigogo Post na jumla ya 352 wanawake wakiwa 150 na wanaumme 202 walipimwa Malaria, Kisukari, Shinikizo la Damu na Upungufu wa Damu mwilini.

  Kati ya watu hao, watu 38 wameonekana kuwa na Shinikizo la Damu, 36 Upungufu wa Damu, 8 Kisukari na mmoja Maralia ambapo walipata nafasi ya kupatiwa dawa na ushauri kutoka kwa madaktari mbalimbali.

  Aidha kwa mafanikio hayo, Fazel Foundation inawashukuru wote walioshiriki katika huduma hiyo akiwepo Dkt. Mohammed Alloo, Dkt. Sibtain Moledina, Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL Group), Salama Pharmaceuticals na Clinicheck Labs, Imam wa msikiti wa Al Ghadir Sheikh Jalala, Msikiti wa Al Ghadir, Diwani wa Kigogo, Bw. Manyama, Team ya Volunteers na Hawza ya Imam Sadiq kwa ushiriki wao katika zoezi hilo.
  IMG_8619
  Wakiwa katika picha ya pamoja, Wa kwanza kushoto ni Diwani wa Kigogo, Bw. Manyama, Imam wa Msikiti wa Al Ghadir, Sheikh Jalala, Mwanzilishi wa Taasisi ya Fazel, Dkt. Sajjad Fazel na Mwanzilishi wa Taasisi ya Elimu ya Afya na Madawa (TAHMEF), Juliana Busasi.
  IMG_8673
  Boniventure Pius akimpima Imam wa Msikiti wa Al Ghadir, Sheikh Jalala wakati wa uzinduzi wa upimaji afya bure kwa wakazi wa Kigogo. Aliyesimama kulia ni Mwanzilishi wa Fazel Foundation, Dkt. Sajjad Fazel.
  DSC_0006
  Mkisi Shamra akimuhudumia mmoja wa wananchi waliofika katika kituo kilichokuwa kikitumika kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo, Dar es Salaam.
  DSC_0009
  Mary Kalleku akimpima mmoja wa wananchi waliofika katika kituo kilichokuwa kikitumika kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo, Dar es Salaam.
  DSC_0014
  Victoria Msambichaka akimwambia jambo mmoja wa wananchi waliofika katika kituo kilichokuwa kikitumika kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo, Dar es Salaam.
  DSC_0017
  Baadhi ya wananchi waliofika kupimwa afya bure kutoka Fazel Foundation na TAHMEF.
  DSC_0021
  DSC_0019
  Eneo lililokuwa likitumika kupokea wananchi waliokwenda kupima bure afya zao.
  DSC_0024
  Dkt. Mohammed Alloo kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akimshauri jambo mmoja wa wananchi waliofika katika kituo kilichokuwa kikitumika kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo, Dar es Salaam.
  DSC_0025
  Alex Juma akimpa dawa mmoja wa wananchi aliyefika kupima afya bure baada ya kubainika kuwa na ugonjwa.
  DSC_0032
  Mwanzilishi wa Fazel Foundation, Dkt. Sajjad Fazel akizungumza jambo na Mwanzilishi wa Taasisi ya Elimu ya Afya na Madawa (TAHMEF), Juliana Busasi wakati wakati zoezi la kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo likiendelea.
  DSC_0034
  Kenneth Mananu akimsikiliza mmoja wa wananchi waliofika kituoni kupata vipimo vya afya bure. Anayefuatia ni Joshua Mnkeni akimpa ushauri mmoja wa wananchi aliyefika kupata huduma ya kupima afya bure.
  DSC_0035
  Eneo la kutolea huduma kwa wananchi wanaofika kupata huduma.
  DSC_0038
  Wagonjwa wakisubiri kumuona daktari.
  DSC_0039
  Hans Olomi akimpima mmoja wa watoto waliofika kupimwa afya zao bure, Anayefuatia ni Simon Nassary.
  DSC_0050
  Mwanzilishi wa Fazel Foundation, Dkt. Sajjad Fazel akimwambia jambo Kenneth Munanu wakati zozi la upimaji likiendeea.

  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha

  BARAZA la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya
  Arumeru umelaani kitendo cha UVCCM mkoani hapa kumsimamisha kamanda wa umoja wa Vijana wa UVCCM wilaya ya Arumeru Mathias Manga kutokana na kuisaliti CCM katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

  Aidda baraza hilo limelaani tamko lililotolewa wiki iliyopita na
  Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengai Sabaya na kumtaka ajitathmini na kujipima kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa,kama ataona hawezi ajing'oe mwenyewe.

  Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
  jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya,alisema kuwa wanamtambua Manga ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa (NEC),kama Kamanda wao wa vijana.

  "Tunalaani tamko lililotolewa na Mkoa na hatumtambui kamanda
  mwingine,Kamanda wetu hajatendewa haki,wajumbe wa baraza tumetathmini tamko la Lengai tunaona ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni,amepoka madaraka yasiyo yake,kitendo ambacho ni kurudisha chama nyuma badala ya kukijenga.

  Mungaya alisema kuwa "Sabaya ajitathmini,ajipime kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa kwani tunaona akiendelea hivi kukiuka kanuni atakiua chama,ni bora ajing'oe mwenyewe kama anaona hawezi,tunampa siku saba akanushe madai aliyoyatoa dhidi ya kamanda wetu".

  Alisema kuwa tamko hilo ni batili na hawalitambui na kumtaka Manga
  asivunjike moyo aendelee na haratkati za kukijenga chama hivyo asirudishwe nyuma na changamoto anazokabiliana nazo.Akizungumzia yeye kuwepo kwenye baraza hilo alidai kuwa siku ya kikao alikuwepo ila alikataa kupiga kura ya kumkataa Kamanda wake na kuamua
  kutoka nje.
  Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
  jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya 
  Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo
   

  0 0

  Timu ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania, Bunge Sports Club jioni ya leo kinatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo maalum na wa kwanza dhidi ya timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mchezoutakaochezwa uwanja wa Amaan, Unguja.

  Tayari asubuhi ya leo kikosi hicho cha timu ya Bunge kimefanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo huo wa jioni ambao unatarajia kuchezwa majira ya saa 12:45 Jioni katika uwanja wa Amaani. Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamotto amebainisha kuwa lengo la mchezo huo ni kiuimalisha Muungano ambapo pia michezo ni afya hivyo mchezo utakuwa ni wa ushindani na wa kuvutia kwa pande zote mbili.

  “Tunawaomba wabunge wote kutuunga mkono katika mchezo huu kwani tmu imejindaa vya kutosha kuhakikisha tunashinda wetu huu wa leo Aprili 26 katika uwanja wa Amaan karibuni watu wote kutushuhudia tutakavyoonyesha uwezo wa hali ya juu katika michezo” alieleza Mh. Mwamotto.

  Naye Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani ‘Maji Marefu’ ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi wa timu hiyo ya Bunge amewaomba wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanapiga hatua kwani timu ni nzuri na ina hali ya ushindi kwa pande zote hivyo anahakika na kuibuka na ushindi kwa mchezo wa leo.

  Kwa upande wake Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Bunge amewataka wabunge wote wanaounda timu hiyo kuzingatia maelekezo ya Kocha pamoja na kuzingatia taratibu za mchezo wa soka ilikuweza kupata ushindi mnono.

  Kwa upande wa Kapteni mpya wa timu hiyo, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, Mh. Sixtus Mapunda amesema kikosi cha timu yake kimejiandaa vya kutosha na kiko kamili kwa mchezo huo wa jioni ya leo huku akiahidi ushindi mkubwa.

  Mchezo huo wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ni maalum kwa ajili ya maadhimisho ya Muungano wa Nchi ya Jamhuri ya Tanganyika Na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambapo jioni ya leo viongozi mbalimbali watajumuika kushuhudia mchezo maalum.

  Kikosi cha Bunge chenye wachezaji zaidi ya 19 kimejiandaa vya kutosha katika kuakikisha inapata ushindi mnono ambapo kimepiga kambi visiwni hapa kwa siku kadhaa hivyo mchezo huo utakuwa ni wa ushindani kwa pande zote mbili licha ya timu ya Baraza la Wawakilishi ambayo imejaa vijana wengi yenyewe ikiwa imejificha katika kambi yao nje ya mji wa Unguja.

  Aidha, mbali na mchezo huo, pia kutakuwa na michezo mingine ikiwemo mchezo wa Ligi ya Zanzibar pamoja na mchezo maalum ambapo Wekundu wa Msimbazi Simba Sc ikitarajiwa kushuka dimbani kucheza na moja ya timu ya Visiwani hapa mchezo ambao ni wa kirafiki katika kunogesha Muungano huo.
  Kapteni mpya wa timu ya Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, Mh. Sixtus Mapunda akifanya mazoezi ya mwisho mwisho asubuhi ya leo katika uwanja wa Amaan, Unguja
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni akiwa katika mazoezi hayo leo uwanja wa Amaan
  Mbunge wa Mbulu Vijijini , Mh.Flatei Massay akifanya mazoezi katika kujiandaa na mchezo huo wa leo jioni
  Mbunge wa jimbo la Sengerema, William Ngeleja ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo akiwa katika mazoezi hayo

  Kikosi cha Bunge kikipata maelezo ya kina kutoka kwa kocha wao, Mh. Mwamotto


  Kocha wa Bunge Mh. Mwamotto akitoa maelekezo ya namna ya kumiliki mpira timu iwapo uwanjani


  Benchi la ufundi la timu ya Bunge likifuatilia mazoezi hayo ya mwisho leo asubuhi 

  Mbunge wa Nzega Vijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa timu hiyo ya Bunge (kushoto) akiwa katika mazoezi ya mwisho mwisho dhidi ya mchezo wa leo jioni.


  Mbunge wa Mbulu Vijijini , Mh.Flatei Massay akiwa katika mazoezi pamoja na Mbunge wa jimbo la Sengerema, William Ngeleja (juu) katika mazoezi hayo.

  kifanya mazoezi katika kujiandaa na mchezo huo wa leo jioni

  Kocha akitoa maelezo ya mwisho Waziri wa Kilimo, Mfugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba akionyesha umahiri wa kumiliki mpira wakati wa mazoezi hayo ya asubuhi ya leo tayari kujiandaa na mchezo wa hapo jioni  Timu ya Bunge ikitoka uwanjani mara baada ya kumaliza kwa mazoezi yao asubuhi hii

  Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akisalimiana na wachezaji wenzake wa timu ya Bunge wakati alipoungana nao. Mwigulu ni miongoni mwa wachezaji wa Bunge wa kutegemewa ambapo aliweza kuunhana na kikosi hicho na kuongeza hali ya mchezo kwa hapo jioni.

  Kikosi cha timu ya Bunge ambacho kitashuka dimbani jioni ya leo kimejiandaa vya kutosha kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo ambapo amebainisha kuwa, wachezaji wake wote wameshaandaliwa kisaikolojia na kimchezo hivyo wanatarajia ushindi wa kishindo. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog-Zanzibar).

  0 0

  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongoza kikao cha kazi na watendaji wa serikali wakiwemo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi, pamoja na ma-Katibu wakuu Wizara ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora, Katibu Mkuu Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, Naibu Katibu Mkuu Fedha na Mipango Mhe Dottoa James, Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Alphayo Kidata, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola pamoja na uongozzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na watendaji wengine. PICHA NA IKULU

older | 1 | .... | 828 | 829 | (Page 830) | 831 | 832 | .... | 1898 | newer