Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

JESHI LA POLISI MKOA WA KILIMANJARO LANASA BHANGI MISOKOTO 4500,BASTOLA PAMOJA NA ZANA NYINGINE

$
0
0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,kamishna msaidizi ,Wilbroad Mutafungwa akionesha misokoto ya Bhangi iliyokamatwa baada ya wahusika kufanikiwa kuwakimbia askari Polisi.
Kamnad wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,kamishna msaidizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa akionesha misokoto 4500 pamoja na kilogramu 10 za bhangi ambayo haijasokotwa iliyokamatwa wilaya ya Siha baada ya wahusika kuitelekeza.
Sehemu ya Bhangi iliyokamatwa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa akionesha vifaa mbalimbali yakiwemo mapanga na mashoka yaliyokuwa yakitumika katika utekaji wa magari wilayani Mwanga.
Baadhi ya vitu mbalimbali walivyokamtwa navyo watuhumiwa wa ujambazi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa akionesha bastola ambayo inadaiwa kutumika katika kufanyia uharifu.
Kamanda wa Polisi akiwaonesha watuhumiwa wa usafirishaji wa Mirungi namna ambavyo wamebuni mbinu mpya ya kusafirisha dawa hizo za kulevya.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa za kamanda Mutafungwa.
Baadhi ya askari Polisi pia walikuwepo kuimarisha usalama katika chumba cha mikutano katika ofisi ya kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini

DK.SHEIN AHUDHURIA MAZISHI YA MAREHEMU ABDALLA MOHAMD MSHINDO(M\KITI CCM)

$
0
0
Maelfu ya wananchi na waislamu waliobeba jeneza la Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo katika mazishi yake yaliyofanyika leo kijiji cha Kihinani Wilaya ya Magharibi ‘A’Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzipia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto)akitia udongo katika kaburi la Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba katika mazishi yaliyofanyika leo Kihinani Wilaya ya Magharibi ‘A’,Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi (Gavu) akitia udongo katika kaburi la Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba katika mazishi yaliyofanyika leo Kihinani Wilaya ya Magharibi ‘A’ Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,[
Mwenyekiti wa CCM MKoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Haji Juma Haji akitia udongo katika kaburi la Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba katika mazishi yaliyofanyika leo Kihinani Wilaya ya Magharibi ‘A’ Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzipia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Sif Ali Iddi(katikati)pamoja na wananchi na wanaCCM wakiitkiia dua iliyoombwa baada ya mazishi ya Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo aliyekuwa wenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba yaliyofanyika leo Kihinani Wilaya ya Magharibi ‘A’ Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzipia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akiwapa pole familia ya Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba kabla ya mazishi yake yaliyofanyika leo Kihinani Wilaya ya Magharibi’A’ Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzipia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Sif Ali Iddi(katikati)pamoja na wananchi na wanaCCM wakiswali katika baada ya mazishi ya Marehemu Abdalla Mohamed Mshindo aliyekuwa wenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba yaliyofanyika leo Kihinani Wilaya ya Magharibi ‘A’ Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,[Picha na Ikulu.]

RC RUGIMBANA AONGOZA KONGAMANO LA MIAKA 52 YA MUUNGANO UDOM

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Lugimbana akizungumza na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM -UDOMASA), wakati wa mdahalo wa miaka 52 ya Muungano uliofanyika katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo UDOM leo. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Professa Idrissa Kikula. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mwenyekiti wa Jmuiya ya Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA), Mhadhiri Msaidizi, Edson Baradyana akitoa shukurani kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Lukimbana kwa kukubali kufungua kongamano hilo.
Baadhi ya wanachuo na wanataaluma wakishiriki kwenye kongamano hilo la miaka 52 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Jopo la wawezeshaji wa kongamano hilo












RC Rugimbana akizungumza jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha UDOM, Kikula kabla ya kuondoka. Kushoto ni Mwenyekiti wa Udomasa, Paradyana.
Rugimbana akiagana na wahadhiri wa Udom
Rugimbana akiteta jambo na Profesa Kikula
Wakiwa katika picha ya kumbukumbu
Mhadhili wa UDOM, Profesa Davis Mwanfupe akitoa mhadharakuhusu umuhimu wa wanataaluma kuuenzi Muungano





HOSPITALI YA NGARENARO YAKABILIWA NA UHABA WA VIFAA TIBA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
Ruth Mtoi Simba akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Muuguzi Mkuu wa
Hospitali ya Ngarenaro Hosea Naaman ,msaada uliotolewa na Umoja wa
Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama (WATJAM)jana jijini Arusha.
kuu wa Kitengo cha Rasilimali watu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
Ruth Mtoi Simba akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Muuguzi Mkuu wa
Hospitali ya Ngarenaro Hosea Naaman ,msaada uliotolewa na Umoja wa
Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama
(WATJAM)jana jijini Arusha.


Na Woinde shizza,Arusha.

Hospitali ya Ngarenaro iliyoko wilaya ya Arusha mjini mkoa wa Arusha inakabiliwa na uhaba wa vifaa tiba pamoja na ukosefu wa miundombinu ya  maji katika wodi ya wazazi jambo ambalo linapunguza ufanisi wa upatikanaji wa huduma za afya kwa wagonjwa.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo Hosea Naaman amesema kuwa uchache wa vifaa tiba umekua ukiathiri ari ya wauguzi katika kuwahudumia wagonjwa licha ya juhudi zinazofanywa na serikali bado hospitali hiyo ina mahitaji ya vifaa tiba hasa katika wodi ya wajawazito.

Kufuatia Changamoto hizo Umoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama (WATJAM) wameitikia wito na kujibu changamoto hizo kwa kutoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali ikiwemo gloves,mashuka,ambavyo vitawezesha upatikanaji wa huduma bora kwa mama na mtoto.

Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu Ruth Mtoi Simba amesema kuwa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya wameamua kuchangia huduma za kijamii ili kuwasaidia watanzania wenye kipato cha chini kupata huduma bora za afya.Mwanachama wa Umoja huo Fadhili Mganya na Katibu wake Costantini Mashauri wamesema kuwa umoja huo umelenga kuwasaidia watanzania kutatua changamoto mbalimbali za afya ,kijamii na kiuchumi kwa kushiriki katika kutatua changamoto hizo

Umoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika jumuiya ya Afrika Mashariki leo wamesheherekea sikukuu ya Muungano kwa kutembelea hospitali ya Ngarenaro na kutoa msaada wa vifaa tiba ili kusaidia kuboresha huduma za afya .

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kifo cha Lucy Kibaki

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kufuatia kifo cha Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mama Lucy Kibaki aliyefariki dunia leo tarehe 26 Aprili, 2016.


Mama Lucy Kibaki ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki amefariki dunia Jijini London nchini Uingereza, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.


Katika salamu hizo Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na kifo hicho na kuongeza kuwa Kenya imempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yake.


“Kupitia kwako Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta napenda kumpa pole nyingi Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki, Familia yake, Ndugu, Jamaa na Marafiki wote walioguswa na msiba huu mkubwa”Amesema Rais Magufuli.


Dkt. John Pombe Magufuli pia amemuombea marehemu Lucy Kibaki apumzishwe mahali pema peponi, Amina.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam


26 Aprili, 2016

Maadhimisho ya Siku ya YWCA Duniani Yalivyofanyika Kanda ya Ziwa Mjini Shinyanga

$
0
0
Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako leo Aprili 26,2016 kumefanyika maadhimisho ya Siku ya Chama Cha Wanawake na Wasichana( Young Women's Christian Association- YWCA) duniani ambayo kwa kanda ya Ziwa Victoria yamefanyika mkoani Shinyanga na kukutanisha wadau kutoka mikoa ya Mara,Mwanza na Shinyanga. 

Mgeni rasmi alikuwa kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga. Maadhimisho hayo yameanza kwa maandamano kupitia maeneo mbalimbali mjini Shinyanga kisha kumalizika kwa mkutano katika viwanja vya Shycom. 

YWCA ni shirika lisilo la kiserikali linatoa huduma kwa wanachama na wasio wanachama bila kujali utaifa,jinsia au imani ya mtu. Lengo la shirika hilo ni kuunganisha uongozi na sauti za wanawake na wasichana ili kujenga usawa wa kijinsia,kiuchumi,kudumisha amani na uhuru sambamba na kutunza mazingira ya ustawi wa jamii yote. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kidunia ni "Kuunda Ulimwengu Unaojumuisha Wote" huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo kanda ya ziwa ikiwa ni "Kwa Pamoja Tuzuie Ndoa na Mimba za Utotoni,Tutaleta Mabadiliko Kielimu". 

Washiriki wa maadhimisho hayo walisisitiza umuhimuwa jamii kuungana kwa pamoja ili kupiga vita mimba na ndoa za utotoni kwani janga kubwa sana katika kanda ya ziwa na hasa katika mkoa wa Shinyanga ambao unaongoza kitaifa kwa asilimia 59 ukifuatiwa na mkoa wa Tabora na Mara. 

Akizungumza katika maadhimisho hayo mgeni rasmi ambaye ni kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro alikemea tabia ya wazazi na walezi kuwapa "Samba" Watoto wa Kike "Dawa ya kusafisha nyota watoto wa kike ili wapendwe na wanaume" hali inayochangia watoto kupewa mimba wangali wadogo matokeo yake kubaki wanalalamika wakati wao ndiyo chanzo cha matatizo. Matiro aliagiza waganga wa jadi na wazazi wanaowapa "Samba" watoto wao wakamatwe kwani wanaharibu watoto na kusababisha tatizo la mimba na ndoa za utotoni kuendelea kuwepo katika jamii. Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio ametuletea picha zifuatazo Katibu wa YWCA mkoa wa Shinyanga Maryciana Makundi akizungumza wakati wa maadhimisho hayo katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambapo alisema YWCA Tanzania ilianzishwamwaka 1959 ikiwa ni miongoni mwa nchi 125 duniani zinazounganishwa na World YWCA ambayo makao yake makuu yapo Geneva Uswis.Alisema maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka mwezi Aprili yakiwa na lengo la kujenga jamii yenye kuheshimu utu wa binadamu,kutetea na kulindaa haki,usawa na amani kwa wote AKC kwaya kutoka Kanisa la Kambarage wakitoa burudani AKC Kwaya wakitoa burudani Kulia ni Katibu mkuu wa YWCA Tanzania Louisa Bulemela akitoa historia ya shirika hilo na jinsi linavyofanya kazi zake nchini.Alisema shirika hilo lina matawi 21 katika mikoa 11 nchini Tanzania,likiwa na wanachama zaidi ya 2000 wengi wao wakiwa ni akina mama na vijana Wanachama wa YWCA wakiwa eneo la tukio Tunafuatilia kinachoendelea hapa.... Maadhimisho yanaendelea Mwenyekiti wa YWCA mkoa wa Shinyanga Neema Adam akizungumza katika maadhimisho hayo Maadhimisho yakiendelea Wanachama wa YWCA wakifurahia jambo Mgeni rasmi ambaye ni kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika maadhimisho hayo aliwataka wazazi na walezi kukaa na watoto wao na kuwapa elimu kuhusu afya uzazi badala ya kuona aibu Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro alipiga marufuku tabia ya wazazi kupeleka watoto wao wa kike kufanyiwa dawa za mvuto/nyota kwani vinachangia kwa kiasi kikubwa watoto hao kuanza kufanya mapenzi katika umri mdogo matokeo yake wanapata mimba mimba za utotoni Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro alisema ni jukumu la kila mtu katika jamii kuwalinda watoto dhidi ya mimba za utotoni Kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Josephine Matiro pia alikemea vitendo vya kunyanyasa wajane katika jamii hasa pale wanapofiwa na waume zao kwani wamekuwa wakinyimwa haki zao ikiwemo kumiliki mali Tunamsikiliza mgeni rasmi Mwenyekiti wa dawati la Jinsia wilaya ya Shinyanga Pili Misungwi ambaye ni mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Shinyanga akiwahamasisha akina mama,vijana na jamii kwa ujumla kutoa taarifa kwenye dawati hilo pale wanapoona watoto wanafanyia ukatili ikiwemo kupewa mimba katika umri mdogo Misungwi alisema hivi sasa wanaendelea na zoezi la kuwakamata wasichana wanaofanya biashara ya kuuza miili yao ili kuwaepusha watoto katika jamii kuiga tabia za wanawake wanaojiuza Mc Mama Sabuni ambye ni Muuguzi akizungumza katika maadhimisho hayo ambapo alisema siku ya Jumapili wiki hii atakutana na wasichana kutoka shule mbalimbali katika ukumbi wa Ibanza Hotel Mjini kuzungumza nao kuhusu mambo ya afya uzazi Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea eneo la tukio Mc Mama Sabuni akifanya yake Mwinjilisti Esther Emmanuel akitoa neno katika maadhimisho hayo Mwinjilisti Esther Emmanuel akiwasisitiza watoto wa kike kuacha tamaa zinazosababisha wapate mimba wangali wadogo Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

MBUNGE WA MONDULI JULIUS KALANGA AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MORINGE

$
0
0
Mbunge wa Monduli Julius Kalanga akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari Moringe iliyoko wilayani huko jana wakati wa mahafali ya kidato cha sita.
wanafunzi wahitimu wakiwa wanasikiliza amgeni rasmi kwa makini.
mgeni rasmi ambaye ni mbunge Monduli Julius Kalangaakiwa anagawa cheti kwa mmoja wa mwanafunzi aliyemaliza (picha na woinde shizza,Monduli).

POSSI: SERIKALI KUBORESHA MAKAZI YA WATU WENYE ULEMAVU NA WENYE MAHITAJI MAALUM.

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe Dkt. Abdallah Possi akiwasilisha hoja za masuala ya Watu wenye Ulemavu wakati wa Mkutano wa Bunge wa kujadili Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/17 kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde tarehe 25 Aprili, 2016.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akiwasilisha hoja zinazohusu masuala ya Kazi na Ajira wakati wa mkutano wa Bunge wa Kujadili Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/17 Bungeni Dodoma tarehe 25 Aprili, 2016.

Serikali imeahidi kuboresha Makazi ya watu wenye ulemavu na wenye mahitaji maalum ili kutatua changamoto wanazokabiliana nazo katika maisha yao ya kila siku.Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt Abdallah Possi wakati akichangia hoja katika Mkutano wa Bunge wa kujadili Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/17 Bungeni mjini Dodoma.

Naibu Waziri aliwaeleza Wabunge umuhimu wa Serikali kuboresha makazi ya Watu wenye Ulemavu na wenye mahitaji maalum kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya watu wenye Ulemavu namba 9 ya mwaka 2010 inayoeleza haki za watu wenye Ulemavu kuboreshewa maeneo muhimu ikiwemo elimu, ajira, fursa sawa na miundombinu.

“Dhamira ya Serikali ni kuhakikiasha Watu wenye Ulemavu wanashiriki katika shughuli mbalimbali kwa kuwawekea mazingira rafiki yanayowasiaida kutekeleza majukumu yao kulingana na hali zao” Alisema Mhe.Possi.

Aidha, Serikali imefanya jitihada za awali kwa kuyatembelea makazi ya watu wenye ulemavu yakiwemo makazi ya Nunge yaliyopo wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es salaam, Sarame Mkoani Manyara, Kituo cha Wagonjwa wa Ukoma cha Msufini mkoani Tanga pamoja na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na kubaini umuhimu wa kuyaangalia maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto za uvamizi wa makazi ya watu wenye mahitaji maalum.

“Makazi ya watu wenye ulemavu na wale mahitaji maalum yana changamoto nyingi ikiwemo uchakavu wa majengo, kukosa vifaa, uhaba wa wahudumu, changamoto za kifedha na uvamizi wa mara kwa mara” Alisema Naibu Waziri.

Naibu Waziri Possi alisisitiza kuwa hadi sasa Wizara hiyo imeshakubaliana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuangalia hatua za kuzuia uvamizi katika Makazi ya Watu wenye Ulemavu na wenye Mahitaji maalum ili kuimarisha usalama wao.

Msingi wa hoja iliyojibiwa na Naibu Waziri imetokana na michango iliyotolewa na wabunge kuhusu masuala ya Watu wenye Ulemavu kuitaka Serikali kuhakikisha inaboresha mazingira ya watu wenye ulemavu.

Maeneo yanayoboreshwa na kutekelezwa ni pamoja na kuwaboreshea namna ya wanavyotakiwa kupata elimu bora, kukomesha mauaji ya wenye ualbino, suala la kodi na Makazi ya watu wenye ulemavu na wenye mahitaji maalum wakati wa kuchangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/17.

JK AREJEA NCHINI AKITOKEA CHINA

$
0
0
Mwenyekiti a CCM, Rais Mstaafu jakaya Kikwete akiwa na Katibu wake, Suleiman Mwenda baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, leo akitokea chini China alikokuwa akiwa katika ziara ya kikazi kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akilakiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
Mwenyekiti wa CC,M Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na Madabida
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungmza na baadhi ya viongozi 
Jk akiingia ukumbini kuzungumza na waandishi
Jk akiwa tayari kuzungumza na waandishi wa Habari
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari leo baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam, akitoa nchini China alikokuwa katika ziara ya kikazi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam. Ramadhani Madabida. (Picha zote na Bashir Nkoromo).

KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATI YA WATANZANIA NA WARUSI 28 APRILI 2016, JNICC, DAR ES SALAAM

$
0
0
Tunayo furaha kubwa kuwakaribisha kwenye Kongamano la Uwekezaji kati ya Watanzania na Warusi litakalofanyika siku ya Ijumaa tarehe 28 Aprili 2016 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Kongamano hili limeandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kikishirikiana na Russian Export Club, Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi na Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania; kwa usimamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania, Wizara ya Biashara na Viwanda ya Urusi na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi 2016 linatarajia kuwaleta pamoja kundi la wawakilishi wa Serikali ya Urusi, wenye viwanda na wafanyabiashara wakubwa kwa lengo kushirikiana na kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji baina ya nchi hizi mbili. Kupitia mahusiano haya ya ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Urusi kutaongeza zaidi ushiriki wa makampuni ya Kirusi katika kufanya biashara na uwekezaji hapa nchini.

Ujumbe wa wafanyabiashara wa Kirusi unatarajiwa kufikia watu 60 ukiongozwa na Mheshimiwa Denis Manturov, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Serikali ya Shirikisho ya Urusi. Ujumbe huu pia utajumuisha viongozi wengine wa serikali, Wakuu wa makampuni na wawakilishi wa vyombo vya habari kutoka Urusi. Kongamano hili litajikita zaidi katika ushirikiano wa kiuchumi katika sekta za nishati, usafirishaji, miundombinu, mafuta & gesi, madini, huduma za fedha, kilimo na viwanda.

Wakati wa Kongamano hili, yatafanyika majadiliano ya moja kwa moja na mikutano ya Biashara-kwa-Bisahara (B2B), mikutano ya Serikali na Wafanyabiashara (B2G) na Serikali na Serikali (G2G). Wafanyabiashara wa kutoka Urusi watapata pia fursa ya kutembelea maeneo ya viwanda ya EPZA ili kujionea uzoefu wa moja kwa moja kuhusu sekta ya viwanda hapa nchini.

Ushirikiano baina ya Tanzania na Urusi katika nyanja za Uwekezaji na Biashara unaonesha kuwa mzuri kwa miaka ya hivi karibuni ingawa bado ni mdogo ukilinganisha na fursa zilizopo. Hivyo basi, kwa kupitia Kongamano hili, tutatoa nafasi ya kufungua na kujionea fursa lukuki zilizopo za kiuwekezaji na kibiashara baina ya nchi hizi mbili, pamoja na kukuza utalii.


Tunawakaribisha sana Wafanyabisahara wa Tanzania!
Imetolewa na: Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
Tarehe: 26 Aprili 2016.

NEWZ ALERT:RAIS DKT.MAGUFULI AVUNJA BODI YA TCRA NA KUMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI MKUU.

TAARIFA YA TAHADHARI YA MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI

Rais Magufuli awaapisha Makatibu Tawala wapya wa Mikoa

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ,SAID MECKY SADICK AFANYA ZIARA YA UTAMBURISHO WILAYA YA HAI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadick akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadickyakitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Hai hii leo.
Mkuu mpya wa wilaya Hai , Gelasius Byakanwa (kushoto) akimuelekeza jambo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick alipotembelea ofisini kwake mapema hii leo.
Mkuu mpya wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akitoa taarifa ya wilaya hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadick alipotembelea ofisini kwake mapema hii leo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ,Said Mderu akiandaa taarifa kwa ajili ya kukabidhi kwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadick.
Mkuu wa Polisi wilaya ya Hai ,OCD Pancras Mdimi akifuatilia taarifa ya wilaya iliyokuwa ikitolewa kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick akisoma ubao wenye majina ya wakuu wa wilaya waliowahi kufanya kazi katika wilaya hiyo .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadick akiongozana na Mkuu mpya wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa wakati wakitoka katika ofisi ya mkuu huyo wa wilaya.
Na Dixon Busagaga wa Globua ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Mbio za Heart Marathon zafana jijini Dar es Salaam

$
0
0
Washiriki wa mbio za Heart Marathon kwa waendesha Baiskeli wakiwa katika mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.
Wanariadha washiriki wa Heart Marathon wakichuana katika mbio za urefu wa kilomita 21 jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge akizungumza na wadau wa riadha wakati wa ufungaji wa mbio za Heart Half Marathon zilizofanyika jana katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Kongamano la Afya Tanzania na Mratibu wa mbio hizo Dkt. Omary Chillo.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon Dkt. Chakao Khalfan akizungumza na waandishi wa Habarai mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo jana jijini Dar es Salaam. Heart Marathon hii imejumuisha mbio za urefu wa 21Km, 10Km, 5Km, mita 700 kwa ajili ya watoto, Baiskeli Kilomita 21 na Baiskeli walemavu.


Benki ya Exim yazindua mashine yake ya kwanza ya kuweka pesa kwenye akaunti.

$
0
0
Mkuu wa Huduma za matawi Benki ya Exim Tanzania, Bw Eugine Massawe (kulia) pamoja na Meneja Mkuu wa kampuni ya Pacific International Lines, PIL Bw. Kevin Stone wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mashine ya kuweka pesa (CDM) ya benki hiyo itakayowawezesha wateja wa kampuni ya PIL kuweka pesa kwenye akaunti zao moja kwa moja bila kulazimika kufika kwenye ofisi au kuhudumiwa na wafanyakazi wa benki hiyo.
BENKI ya Exim Tanzania imezindua mashine yake ya kwanza ya kuweka pesa (CDM) itakayowawezesha wateja wa kampuni ya Pacific International Lines, PIL kuweka pesa kwenye akaunti zao moja kwa moja bila kulazimika kufika kwenye ofisi au kuhudumiwa na wafanyakazi wa benki hiyo.

Ufunguzi wa mashine hiyo ulifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni ukihusisha mwakilishi wa benki hiyo ambaye ni Mkuu wa Huduma za matawi Bw Eugine Massawe pamoja na Meneja Mkuu wa kampuni ya PIL Bw. Kevin Stone.

Akizungumzia mashine hiyo iliyopo kwenye jengo la Maktaba (Makataba Square)lililopo katikati ya jiji, Bw Massawe alisema ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo katika kurahisisha huduma zaidi za kifedha kwa wateja wa benki hiyo.

“Mashine hii itawawezesha wateja wetu kuweka pesa moja kwa moja kwenye akaunti zao wao wenyewe. Huduma hii itapatikana kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 na nusu jioni kila siku na itatoa fursa kwa wateja wa PIL kupata msaada kutoka kwa wahudumu wetu waliopo jirani na mashine pale watakapohitaji,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Bw Massawe, kwa kuanzia mashine hiyo itaanza kupokea noti za Dola ya Kimarekani kwa kiasi chochote huku akitahadharisha; “Ifahamike kwamba mashine hii ina uwezo mkubwa wa kutambua pesa bandia au zile zisizofaa kwa kuwa imewekewa mfumo bora kabisa wa kiusalama,”Aliongeza kuwa mashine hiyo inamuwezesha mtumiaji kupata risiti ya muhamala atakaoufanya sambamba na kumuhakikishia mafanikio ya muhamala husika.
“Mteja atapokea ujumbe mfupi wa maneno kuhusiana na mwenendo ya muhamala alioufanya,’’ alisema Bw Massawe huku akisisitiza: “Benki ya Exim itabaki kuwa benki pekee yenye kubuni huduma zinazokidhi matakwa ya wateja kulingana na mabadiliko ya kimahitaji katika huduma za kibenki,’’

Alisema huduma hiyo imewekwa jirani na makao makuu ya benki hiyo ili kuwawezesha watumiaji wa huduma hiyo kupata msaada kwa urahisi kutoka kwa wafanyakazi wa benki pale wanapohitaji.“Itakapofikia kipindi ambacho wateja wetu watakuwa tayari wamejenga uelewa wa kutosha kuhusiana na matumizi sahihi ya mashine hii tutakuwa tayari kuongeza mashine nyingine katika maeneo mbalimbali ili waweze kufurahia huduma hii zaidi,’’ aliahidi.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAKATIBU TAWALA WAPYA WA MIKOA 10 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Amantius Casmiri Msole kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Jumanne Abdallah Sagini kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Selestine Muhochi Gesimba kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu Tawala wapya kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016 na kuwapangia vituo vyao vya kazi.
Makatibu Tawala hao wameapishwa leo tarehe 27 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam na kisha wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi lililoendeshwa na Kamishna wa maadili Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Makatibu Tawala walioapishwa ni;
1.Arusha -Richard Kwitega
2.Geita - Selestine Muhochi Gesimba
3.Kagera - Armatus C. Msole
4.Kilimanjaro -Eng. Aisha Amour
5.Pwani - Zuberi Mhina Samataba
6.Shinyanga - Albert Gabriel Msovela
7.Singida -Dr. Angelina Mageni Lutambi
8.Simiyu -Jumanne Abdallah Sagini
9.Tabora -Dkt. Thea Medard Ntara
10.Tanga -Eng. Zena Said
Makatibu Tawala wengine wa Mikoa ambao hawakuapishwa leo, ni wale waliohamishwa vituo vya kazi na wale waliobaki katika vituo vya kazi walivyokuwep,o ambao tayari walishakula kiapo cha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
27 Aprili, 2016

mkuu wa wilaya ya kinondoni akagua miradi mbalimbali ya maendeleo manispaa ya Kinondoni

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Salum Hapi jana tarehe 26/4/2015 alifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoko manispaa ya Kinondoni. Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni, Mh. Hapi alikagua na kupokea taarifa ya miradi mbalimbali iliyokamilika na inayoendelea kukamilika. Miradi iliyotembelewa ni kama vile

-Mradi wa ujenzi wa soko la kisasa Mburahati utakaogharimu Bilioni 1.8,
-Mradi wa ujenzi wa barabara ya Arsenal Magoti uliogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 1,
-Mradi wa ujenzi wa wodi ya wazazi Ubungo uliogharimu shilingi milioni 50,
-Ujenzi wa hostel ya wasichana katika shule ya sekondari Mabwepande utakaogharimu shilingi 283,988,270,

-Ujenzi wa Kalavati Mabwepande utakaogharimu shilingi 320,880,400,-Ujenzi wa Kituo cha Kilimo Malolo Mabwepande utakaogharimu shilingi 96,412,200 na-Ujenzi wa kisima cha maji Makongo utakaogharimu shilingi 240,000,000.
 

Akiwa katika mradi wa Kilimo Mabwepande, Mh. Mkuu wa Wilaya alivutiwa na mradi huo ambao unalenga kuweka programu ya kuwafundisha wananchi kulima mbogamboga, kufuga kuku, samaki na ng'ombe. Mh. Hapi alitoa agizo kwa Mkurugenzi kuhakikisha fedha zilizosalia kulipwa mkandarasi kiasi cha shilingi milioni 30 zilipwe haraka ili kituo kikamilike, jambo ambalo lilikubaliwa palepale.

Miradi ya maendeleo iliyokaguliwa inatarajiwa kuzinduliwa na mwenge wa uhuru ambao unatarajiwa kuwa Kinondoni katikati ya mwezi ujao.




Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh . Ally Salum Hapi akielekezwa jambo alipokuwa akikagua moja ya mradi ndani ya wilaya hiyo.
 Mh. Hapi akikagua na kupokea taarifa ya miradi mbalimbali iliyokamilika na inayoendelea kukamilika.
Mh. Hapi akipata maeelezo mara baada ya kagua na kupokea taarifa ya miradi mbalimbali iliyokamilika na inayoendelea kukamilika.

Sherehe za miaka 5 ya kitchen party gala zafana!

$
0
0
Jumapili ya tarehe 24 April wanawake mbali mbali wa jiji la Dar es salaam walikutana pamoja kuadhimisha miaka mitano toka kuanzishwa kwa kitchen party gala."Kitchen party gala event imetokana na zile shughuli za kitchen party anazofanyiwa bi harusi mtarajiwa kufunzwa maisha ya ndoa.Lakini sisi tukasema kila mtu anahitaji mafunzo hayo kila inapobidi ikiwemo  Mahusiano,ndoa,ujanajike/uanamke,kujitambua,kujisimamia,kazi,familia,afya,ujasiriamali n.k.

Tamasha hilo lilifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Sheria,kilichopo karibu na kituo cha mawasiliano ,Ubungo nyuma ya jengo la Mawasiliano Tower,tamasha hilo lililokuwa limebeba ujumbe   "MWANAMKE......CHUKUA HATUA acha kulala na kuzubaa.Saa mbaya hizi kamata usukani wa maisha yako,lilionekana kuwavutia sana akina dada na akina mama kutokana na namna lilivyokuwa limeandaliwa. 

Mwanamke amezungukwa na mambo mengi sana ambayo kila wakati anahitaji kukumbushwa na kufundishwa ikibidi ndio tukaanza KITCHEN PARTY GALA 2011 mpaka Leo 2016 " Alisema Dina Marios moja ya waandaaji wa tukio hilo akishirikiana na Vida Mndolwa. "Tumelidesign Tamasha letu liwe la kuelimisha na kuburudisha pia ili kukufanya urelax na ufurahi na kila utakachosikia usikisahau." Aliongeza Dina Marios.
Mratibu wa Sherehe za miaka 5 ya kitchen party gala Dina Marios akitoa mwongozo mfupi wa shughuli nzima ukumbini.
Baadhi ya Washiriki wa kitchen party gala wakifurahia jambo huku wakibadilishana mawazo.
Mmoja wa wasemaji wa Hafla hiyo Dkt.Peter Mitimingi ambaye ni mtaalamu katika nyanja mbalimbali ikiwemo mambo ya uongozi,ushauri,biblia,saikolojia na pia ameandika vitabu vingi tu vya mafunzo na ushauri.
Pastor Debora Kaisi akitoa neno katika hafla hiyo ya Sherehe za miaka 5 ya kitchen party gala.
Baadhi ya Washiriki wa kitchen party gala wakiserebuka kwa pamoja huku wakibadilishana mawazo.
Akina mama waserebuka kwa raha zao.
Walipoguswa na mada yoyote hawakusita kuonesha hisia zao.
Akina Mama wakiserebuka kwa raha zao

NEWS ALERT: Harry Kitilya na wenzake wafutiwa shtaka moja, dhamana yagonga mwamba

$
0
0
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya (kushoto) akiwa na waliokuwa Wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania,  Sioi Sumari (katikati) na Shose Sinare, wakiwa Mahakam ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam.

Washitakiwa hao wanaokabiriwa na mastaka nane likiwemo la utakatishaji Fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 6, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic kwenda Serikalini, walifikishwa Mahakamani hapo leo kusikiliza keshi yao, na walifanikiwa kufutiwa Shitaka moja la kutakatisha Fedha kati ya nane yaliyokuwa yakiwakabili, ambapo Washitakiwa hao walisomewa kufutwa kwa shitaka hilo kwa madai ya kukosa Vidhibitisho.

Aidha mpaka mtandao huu unatoka Mahakamani hapo Mawakili walikuwa bado wakihangaikia kupata dhamana kufutiwa shitaka hilo lililokuwa na kikwazo kikubwa cha dhamana

Baada ya kufutiwa shitaka hilo, DPP aliwasilisha hati ya mapendekezo ya kukata rufaa ya kupinga uamuzi wa kufuta shitaka namba nane la utakatishaji Fedha linalowakabili watuhumiwa hao, ambapo zoezi la dhamana liligonga mwamba na Washitakiwa hao wamerudishwa rumande.

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images