Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 827 | 828 | (Page 829) | 830 | 831 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Na Woinde Shizza,Arusha

  Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na michezo nchini,Nape Nnauye ametaja
  mambo manne ambayo ni vikwazo ndani ya sekta ya sanaa ya filamu nchini
  na kuyaita kwamba ni majipu huku akisisistiza kwamba serikali
  itakwenda kutunga sera ya sekta hiyo katika mwaka wa fedha 2016/17.

  Nape,aliyataja mambo hayo na kuyafananisha na majipu kuwa ni uporaji
  wa kazi za wasanii nchini,ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za
  wasanii nchini,usimamizi mbovu wa bodi ya filamu nchini sanjari na
  tatizo la mfumo mbovu wa usambazaji wa kazi za wasanii nchini.

  Akizindua tamasha la filamu la Tanzanite International Film
  Festival(TIFF) jijini Arusha juzi ambao ulihudhuriwa na wasanii
  maarufu wa filamu nchini waziri huyo alisema kwamba jipu la kwanza
  ambalo atakwenda kulitumbua ni uporaji wa kazi za wasanii nchini.
  “Jipu la kwanza tutalitumbua kwenye bajeti yetu ya mwaka 2016/17 ni
  uporaji wa kazi za wasanii nchini wengi wananyonywa jasho lao”alisema
  Nape

  Hatahivyo,alisema kwamba jipu la pili ni ujenzi duni wa miundombinu ya
  kazi za wasanii za filamu nchini na kudai kwamba chini ya uongozi wake
  atahakikisha anaimarisha miundombinu bora kwa lengo la kuwasaidia
  wasanii hao pamoja na kulinda haki zao.

  Alisema ya kwamba mfumo wa kazi za usambazaji wa kazi za wasanii
  nchini pamoja na hakimiliki ni wa kinyonyaji huku akitolea mfano wa
  kazi za msanii maarufu wa sanaa hiyo nchini marehemu Stephen Kanumba
  na kusema kwamba familia yake hainufaiki na matunda ya kazi zake hadi
  sasa kutokana na mfumo mbovu wa usimamizi wa kazi za wasanii nchini.

  Alitaja takwimu kwamba mwaka 2011/12 jumla ya filamu 218
  zilitengenezwa nchini na mwaka 2014/15 kazi hizo ziliongezeka hadi
  kufikia 14,00 huku akidai hilo linadhihirisha kwamba sekta hiyo inakua
  kwa kasi nchini na kuongeza ajira .

  Hatahivyo,Rais wa shirikisho la wasanii wa filamu nchini(TAFF),Simon
  Mwakifamba aliwataka wasanii wa filamu nchini kujiandaa kisaikolojia
  kukabiliana na soko la ushindani wa filamu duniani kwa kuwa wabunifu.

  “Serikali tunaiomba iandae sera itakayoandaa mazingira mazuri kwa
  wasanii nchini kuhusu usalama wa kazi zao”alisema Mwakifamba

  Naye, muaandaji wa tamasha hilo,Said Sassi alisema kwamba tatizo la
  uharamia wa kazi za wasanii nchini limetanda na kuwaomba
  wafanyabiashara na makampuni kujitokeza kudhamini vipindi mbalimbali
  vya luninga kwa lengo la kuinua sekta hiyo.

  Mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya vito ya Tanzanite One
  Mining Ltd ambao ni miongoni mwa wafadhili wa tamasha hilo,Feisal
  Shabhai alisema lengo la kampuni yao kujitosa kufadhili tamasha hilo
  ni kutoa mchango wao katika kusaidia jamii kupitia faida wanayoipata
  ili kuinua sekta ya ajira nchini.

  0 0

  WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, amemuomba Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama, kupeleka huduma hiyo katika mikoa ya Kusini kwa sababu wanakosa huduma ya neno la Mungu.

  Kampuni ya Msama huandaa Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba mwaka huu na Pasaka linalotarajia kufanyika mwakani hapa nchini.

  Majaliwa alisema kwa sasa tamasha hilo limekuwa na nguvu kubwa ya kuhakikisha inahamasisha jamii katika mambo mbalimbali hivyo ni wakati wa mikoa ya kusini kufaidika.

  Alisema kuwa serikali yake imejipanga kuhakikisha kuwa kila Mtanzania ana haki ya kuona serikali yake inawajali na kuwapenda hivyo taasisi kama Msama Promotions, sasa inahitaji kujitanua na kufika mikoa mingi ya Tanzania.

  Waziri Mkuu alisema kuwa amekuwa akifuatilia namna Tamasha la Pasaka linavyojitahidi katika kuelimisha na kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia hasa wajane na yatima hivyo na mikoa kama Lindi na Mtwara nayo inahitaji huduma hiyo.

  “Nimefarijika sana na namna kampuni ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake, Alex Msama namna inavyofanyakazi zake katika kutoa burudani na kuelimisha jamii kwa maana hivyo ningependa kuwaunga mkono katika hilo,” alisema Majaliwa.

  Alisema mikoa mingi ikiwamo Lindi na Mtwara nayo inachangamoto nyingi hivyo wanahitaji ujumbe kama unatolewa katika Tamasha la Pasaka kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

  “Kutoa misaada kwa yatima sio kitu kidogo lakini kubwa ni namna kampuni ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, inavyofanyakazi zake kwa kufuata sheria katika hili nawapongeza lakini kubwa ni kukumbuka mikoa ya Kusini nayo inahitaji huduma hiyo.

  Alisema kuwa kuna waimbaji wengi wakubwa ambao kwa sasa wamekuwa wakifanya kazi kwa ushirikiano na Msama lakini bado hawajawahi kufika katika mikoa ya kusini hivyo ni wakati wake kuhakikisha nao wananufaika na tamasha hilo.

  Majaliwa amemtaka Msama kuendelea na huduma hiyo kwani serikali iko tayari kutoa msaada wa hali na mali.

  Aidha Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama amemshukuru Waziri Mkuu Majaliwa na kusema kuwa atajitahidi kuboresha na kuhakikisha wananchi wote wa Tanzania wananufaika na huduma hiyo.

  Msama amesema kuwa amesikia kilio cha Waziri Mkuu nakusema kuwa kamati yake iko makini na inajipanga kuhakikisha ombi hilo linafanyiwa kazi.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati akiwapokea waliokuwa viongozi wa Chama cha UDP, waliokihama chama ambao ni Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara na Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu na Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na aliyekuwa Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho , Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga CCK jijini Dar es Salaam leo asubuhi mbele ya waandishi wa habari.
  Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma (kulia), akizungumza wakati wa kuwapokea viongozi hao. Kushoto Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara aliye hamia CCK. 
  Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam, Joachim Mwakitiga aliyejiunga na chama hicho na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya aliyehamia chama hicho.
  …………………………………………………………………
  Na Dotto Mwaibale
  CHAMA cha United Democratic Party (UDP) kinachoongozwa na Mwenyekiti wake wa Taifa, John Momose Cheyo, kimepata pigo baada ya wenyeviti wawili wa mikoa ya Mtwara na Dar es 
  Salaam kukihama na kujiunga na Chama Cha Kijamii (CCK).
  Viongozi waliokihama chama hicho ni Salum Makunganya ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho na Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Halmshauri Kuu, Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga CCK leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa 
  habari.
  Wenyeviti hao baada ya kujitoa walikabidhi kadi zao za UDP kwa Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi ambaye naye aliwakabidi kadi ya CCK na kuwatangaza rasmi kuwa wanachama wa chama hicho.
  Makunganya alikabidi kadi yake ya UDP yenye namba 4544 na kukabidhiwa ya CCK namba 1597 huku Mwakitiga akibidhi kadi yake ya UDP namba 2852 na kukabidhi ya CCK yenye namba 01599 katika tukio lililofanyika ofisi za CCK.
  Wakizungumzia sababu zilizowafanya wajitoe UDP walisema ni kutokana na chama hicho kutokuwa na mwelekeo wa kimaendeleo ambacho kwa zaidi ya miaka sita viongozi wake wa kitaifa hawajaitisha mikutano ukiwamo wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu.
  Walisema sababu nyingine ni kwamba viongozi wa kitaifa wa UDP wamekigeuza chama hicho kama kampuni binafsi ambapo wamekuwa wakitoa maamuzi mbalimbali ambayo hayajaamuliwa na wanachama kwenye vikao .
  “Nyie waandishi si mnaishi Dar es Salaam tangu lini mlishaona Mwenyekiti wa Taifa wa UDP, John Cheyo akiitisha hata mkutano wa hadhara hapa Dar es Salaam kuzungumzia mambo mbalimbali ya chama na taifa kwa ujumla kama vinavyofanya vyama vingine…jibu ni hakuna, UDP inabuka tu wakati wa uchaguzi na tena kwenye eneo moja tu,”alisema Mwakitiga.
  Muabhi akizungumza baadhi baada ya kuwakabidhi kadi wenyeviti hao alisema CCK inawapokea kwa mikono miwili viongozi hao na kwamba wakiwa ndani ya chama hicho wataona utofauti na vyama vingine kwa kuwa chama kimejiwekea misingi ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
  Muabhi aliitaka serikali kulitazama upya suala la vikao vya Bunge kutotangazwa kwenye vyombo vya habari kwa kuwa kufanya hivyo kunawanyima haki wananchi ya kupata habari na hivyo kushindwa kujua nini kinaendelea Bungeni.
  “Serikali ijitathimini, wananchi wasipojua nini kinaendelea Bungeni kuna haja gani kwa wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi kwenda Bungeni, wananchi watajuaje kama wawakilishi wao wamezifikisha kero zao serikalini,”alisema.
  Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma, alisema ujio wa wanachama hao wapya ambao ni wakongwe katika siasa na hivyo CCK itajifunza mambo mengi kutoka kwao.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro iliyokuwa na kaulimbiu “ Weka Mlima Safi, Tunza Mazingira Yakutunze” katika lango la Marangu mwishoni mwa wiki. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kati) na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita Loibooki.
  Wakurugenzi kutoka TANAPA wakifuatilia uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Mtango Mtahiko, Mkurugenzi Utumishi na Utawala Bi. Witness Shoo, Mkurugenzi wa Mipango Dk. Ezekiel Dembe, Mkurugenzi wa Fedha Nassoro Mndeme na nyuma yake Mkurugenzi wa Utalii na Masoko Ibrahim Mussa.
  Wanafunzi kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi Mwanza nao walishiriki katika kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
  Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita Loibooki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usafi Mlima Kilimanjaro.
  Baadhi ya wadau walioshiriki kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa TANAPA pamoja na wadau kutoka Kampuni mbalimbali za mawakala wa utalii kutoka Kilimanjaro na Arusha wanaoshiriki Kampeni maalum ya usafi Mlima Kilimanjaro.
  Idadi kubwa ya wadau wa sekta ya utalii walishirikiana vema na TANAPA kusafisha Mlima Kilimanjaro.
  Wageni waalikwa wakivaa ‘gloves’ kabla ya kuanza zoezi la usafi.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
  Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
  Mazingira safi yataendelea kuufanya Mlima Kilimanjaro kutiririsha maji kwa wingi zaidi.Na Dixon Busagaga waGlobu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0


  Mtangazaji wa kipindi cha wanawake live kulia Bi. Joyce Kiria kushoto akionyesha kitambilisho  chake cha uchangiaji wa hiari kutoka kwa Meneja  wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa  mfuko wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe kushoto wakati wa mafunzo kwa wajasiriamali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
  Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa  mfuko wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe kushoto akimkabidhi  Mtangazaji wa kipindi cha wanawake live kulia Bi. Joyce Kiria kitambulisho cha uchangiaji wa hiari katika mafunzo kwa  wajasiriamali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

  0 0

  Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
  jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya 
  Baadhi ya wajumbe waliouzuria mkutano huo.

  Na Woinde Shizza,Arusha.
  BARAZA la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya
  Arumeru umelaani kitendo cha UVCCM mkoani hapa kumsimamisha kamanda wa
  umoja wa Vijana wa UVCCM wilaya ya Arumeru Mathias Manga kutokana na 
  kuisaliti CCM katika uchaguzi mkuu wa mwa Oktaba 25 mwaka jana.

  Aida baraza hilo limelaani tamko lililotolewa wiki iliyopita na
  Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Lengai Sabaya na kumtaka ajitathmini 
  na kujipima kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa,kama ataona 
  hawezi ajing'oe mwenyewe.

  Akizungumza na waandishi mara baada ya baraza hilo kukutana
  jana,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arumeru, Boniface Mungaya,aliesema kuwa 
  wanamtambua Manga ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa 
  (NEC),kama Kamanda wao wa vijana.

  "Tunalaani tamko lililotolewa na Mkoa na hatumtambui kamanda
  mwingine,Kamanda wetu hajatendewa haki,wajumbe wa baraza la tumetathmini 
  tamko la Lengai tunaona ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni,amepoka madaraka 
  yasiyo yake,kitendo ambacho ni kurudisha chama nyuma badala ya  
  kukijenga"alisema na kuongeza.

  "Sabaya ajitathmini,ajipime kama anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti wa mkoa 
  kwani tunaona akiendelea hivi kukiuka kanuni atakiua chama,ni bora ajing'oe 
  mwenyewe kama anaona hawezi,tunampa siku saba akanushe madai aliyoyatoa 
  dhidi ya kamanda wetu"

  Alisema kuwa tamko hilo ni batili na hawalitambui na kumtaka Manga
  asivunjike moyo aendelee na haratkati za kukijenga chama hivyo asirudishwe 
  nyuma na changamoto anazokabiliana nazo.

  Akizungumzia yeye kuwepo kwenye baraza hilo alidai kuwa siku ya kikao
  alikuwepo ila alikataa kupiga kura ya kumkataa Kamanda wake na kuamua
  kutoka nje.

  Naye Anjelina Lukumay ambaye ni mjumbe wa baraza hilo kutoka Kata ya
  Oldonyosambu,alimuomba Mwenyekiti wa CCM mkoani hapa,Lekule Laizer
  kuliangalia suala hilo na kulitafutia ufumbuzi kwani Sabaya amekiuka kanuni 
  za chama.

  "Mwenyekiti wa wilaya ametumia kanuni ipi kumkataa kamanda wetu bila
  kutushirikisha?hatutakubali kuvurugwa wilaya ya Arumeru,tumepokea kwa
  mfadhaiko kauli hiyo kwani Sabaya kachaguliwa hata miezi miwili hana ila
  inakuwaje anataka kumtoa Manga tena bila kutushirikisha?alihoji Anjelina
  Wiki iliyopita uamuzi wa kumsimamisha Manga ulifikiwa katika kikao cha
  baraza la UVCCM mkoa wa Arusha kilichozinduliwa na kaimu katibu mkuu Shaka 
  Hamdu Shaka,ambapo kikao hicho kilikuwa na wajumbe 34 huku 33 kati yao 
  wakipiga kura za ndiyo.

  Pia kikao hicho kilitoa onyo kali kwa kamanda wa UVCCM wilaya ya Arusha
  Mjini,Longido na Monduli na kuwataka wajipime na kujitathimini kama
  wanatosha kuwa makamanda wa UVCCM na wakiona hawatoshi tunaomba wakae 
  pembeni kabla baraza halijawachukulia hatua.

  Uamuzi wa kumsimamisha Manga ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya 
  taifa (NEC)wilaya ya Arumeru ulifikiwa katika Manga
  Akisoma tamko lilitolewa na Kikao hicho cha baraza kikao hicho cha
  baraza Katibu wa Hamasa wa (UVCCM) Mkoa wa Arusha, Lucas Nsomi alisema 
  Manga kuanzia wakati huo si kamanda wa Vijana Wilaya ya Arumeru tena kwani 
  amepoteza sifa baada ya kudhibitika kukisaliti chama kwenye uchaguzi Mkuu 
  wa mwaka 2015,kwani wakati wa uchaguzi huo alionekana akifanya vikao 
  vyakufanikisha ushindi kwa UKAWA.

  “Kikubwa alichofanikiwa Manga ni kuwagawa vijana wa Arumeru hali
  inayopelekea kushindwa kuijenga jumuiya hiyo na kuanzia sasa sio kamanda wa 
  vijana tena wa wialaya hiyo na sipo tayari kufanya naye kazi yoyote ile 
  ndani ya CCM”.


  Sabaya alidai kuwa vijana waliompitisha kuwa kamanda lilikuwa ni genge
  la wahuni ambao walikuwa wakiendesha vikao vya vijana wenye njaa na kuwa 
  hayupo tayari kuwa Mwenyekiti wa magenge ya vijana wenye njaa na wasaliti 
  ndani ya CCM.

  0 0

   Hivi juzi tumeshuhudia ufunguzi wa daraja la Kigamboni ambalo Mh. Rais Dr. John Pombe Mgufuli alilipa jina la daraja la Nyerere. Daraja hili ni matunda ya uwekezaji wenye tija unaofanywa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii la NSSF.

  Shirika hilo kwa kushirikiana na serikali limeweza kujenga daraja lenye urefu wa mita 680 likiwa na barabara sita; tatu zikielekea Kigamboni na tatu zikitokea Kigamboni.  Daraja hili lina njia ya watembea kwa miguu yenye upana wa mita 2.5 kila upande.

  Daraja hilo limejengwa kisasa na kampuni ya  China Railway Construction Engineering Group iliyotekeleza mradi huo kwa kushirikiana na kampuni ya China Railway Major Bridge Group kutoka nchini China.

   Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili, kumejumuisha barabara za kufika katika daraja hili zenye jumla ya urefu wa kilomita 2.5. Katika ujenzi wa daraja hili, Shirika la NSSF limetoa asilimia 60 ya gharama za Ujenzi na Serikali asilimia 40 ya gharama hizo.

   Akizungumza na waandishi wa habari waliotembela daraja hilo hivi karibuni, Meneja wa Mradi huo kutoka NSSF, Muhandisi Karim Mattaka alisema daraja la Kigamboni limejengwa ili kuondoa kero ya siku nyingi ya usafiri kwa wakazi wa Kigamboni na wakazi wa Dar es Salaam kwa ujumla, kuimarisha hali ya uchumi wa Mkoa huu wa Dar es Salaam, mikoa ya jirani na nchi kwa ujumla pamoja na kuimarisha hali ya uchumi wa shirika, kuliwezesha shirika kuboresha na kulipa mafao kwa kutunza thamani ya fedha kupitia kitega uchumi hiki.

  Faida zitokanazo na uwekezaji huo kwa mujibu wa Muhandisi Mattaka ni faida ya moja kwa moja kwa wanachama kwani huingizwa katika akaunti zao pindi wanapochukua mafao yao pamoja na kulipia matibabu yatolewayo bure kwa wanachama.

  “Daraja hili linadhihirisha uwezo wa shirika katika nyanja za uwekezaje na kuwapa wanachama uhakika kuwa pesa zao ziko salama,’’.
   “Ni dhahiri kuwa daraja litaondoa usumbufu mkubwa ambao wananchi walikuwa wanaupata na hata wakati mwingine kupoteza maisha, kwani vivuko vya Kigamboni vikiwa vimeharibika wananchi walikuwa wanatumia mitumbwi ambayo wakati mwingine sio salama,.’’ Alisema  

  > Kukamilika kwa daraja hilo kunaelezwa kuwa kutachangia sana katika kusukuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Kigamboni, Jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

   Inaelezwa kuwa daraja hilo sasa limefungua fursa  kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kukamilisha utaratibu wa kujenga mji wa kisasa (Kigamboni Elite City) utakaokuwa na nyumba za kisasa,   kuongeza  ufanisi katika utalii kwa kujenga mahoteli ya kitalii katika fukwe zilizopo eneo la Kigamboni, kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoa ya kusini mwa nchi yetu na hata nchi jirani zetu, kupanua kilimo cha matunda, mboga na mazao mengineyo yanayozalishwa  katika eneo hili.

   “Wakulima sasa wataweza kufikisha bidhaa zao sokoni kwa urahisi zaidi na hivyo kuongeza kipato chao,’’ aliongeza.


   Kwa mujibu wa Muhandisi Mattaka daraja hilo vilevile  litarahisisha uwezekano wa upanuzi wa bandari upande wa Kigamboni.

   “Kwa ujumla Daraja la Kigamboni litaboresha sana usafiri ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa magari unaolikabili Jiji la Dar es Salaam hasa baada ya ujenzi wa barabara ya Dar es Salaam – Chalinze kwa kiwango cha “Expressway” ambayo itaunganishwa na Bandari ya Dar es Salaam kupitia Daraja la Kigamboni.,’’ alisema

   Muhandisi Mattaka alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wadau wa shirika hilo kuhusu usalama wa fedha zao na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa kiwango cha kimataifa.

   Kwa upande Muhandisi wa Mradi huo kutoka kampuni ya  China Railway Construction Engineering Group iliyotekeleza mradi huo kwa kushirikiana na kampuni ya China Railway Major Bridge Group kutoka nchini China, Muhandisi Jamal Mruma alitumia fursa hiyo kuwatoa hofu watumiaji wa daraja hilo kwa kuwa limetengenezwa katika ubora na teknolojia ya hali juu kabisa.

   “Ni aina ya mradi bora kabisa kuwezeshwa na NSSF pamoja serikali na hatimaye kutekelezwa kampuni bora katika masuala ya ujenzi kutoka China.Niwatoe hofu watumiaji wa daraja pamoja na wanachama wa NSSF kuwa wajivunie mradi huu unafaida kubwa sana kwao na taifa kwa ujumla...waulinde na wajivunie haya ni matunda ya pesa zao,’’ alisema.

   Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa daraja, Naibu waziri wa kazi, ajira, vijana na walemavu aliwaasa waajiri wasiopeleka michango yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii kutekeleza sheria kwa kuchangia kwa wakati ili kuepuka usumbufu wakati wanachama watakapokua wanahitaji mafao yao.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bw. Anthony Mavunde, akimkabidhi, Nahodha wa NSSF, Pili Mogola, kombe la mshindi wa kwanza wa Netiboli, wakati wa Bonanza la Usalama na Afya mahali pa kazi, lililofanyika Dar es Salaam juzi na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaam juzi.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bw. Anthony Mavunde (kulia) na Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Dk. Akwilina Kayumba, wakishiriki kufanya mazoezi na wakati wa maadhimisho ya Bonzanza la usalama na Afya mahali pa kazi lililodhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dar es Salaam juzi. 
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bw. Anthony Mavunde (aliyesimama katikati), akizungumza na wachezaji wa timu za Netiboli za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), wakati wa Bonanza la usalama na Afya hahali pa kazi lililofanyika Dar es Salaam juzi kwa udhamini wa NSSF.
   Wachezaji wa timu ya Netiboli ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakishangilia baada ya kutwaa kombe wakati wa bonanza la Usalama na Afya mahali pa kazi, lililofanyika Dar es Salaam juzi na kudhaminiwa na NSSF.
  Mshambuliaji wa timu ya soka ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ali Chuo (kushoto), akimiliki mpira mbele ya mlinzi wa timu ya Wizara ya Kazi, Abdallah Sanga, wakati wa Bonaza la Usalama na Afya mahali pa kazi lililofanyika Dar es Salaam juzi kwa udhamini na NSSF.

  0 0


   Mkurugenzi wa Halotel tawi la Dar, Bwana Alex Thiem akizungumza na wanafunzi wakati wa Bonanza la Halotel lilifanyika viwanja vya Mabibo Hostel.
   Msanii Ruby akiburudisha wakati wa tamasha la Halotel lililofanyika Mabibo Hostel.
   Wanafunzi wakichuana katika mchezo wa netball wakati wa bonanza la Halotel lililofanyika katika viwanja vya Mabibo Hostel.
   Wanafunzi wa Chuo kikuu Dar es Salaam wakipambana na wanafunzi wa chuo cha ualimu (DUCE) wakati wa bonanza la Halotel lililofanyika Mabibo Hostel.
   Msanii Msami akitoa burudani wakati wa tamasha la Halotel lililofanyika Mabibo.
   Stamina akiburudisha wanafunzi wakati wa tamasha la Halotel lililofanyika Mabibo Hostel.
  Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria tamasha la Halotel katika viwanja vya Mabibo Hostel.

  KAMPUNI ya simu Halotel juzi ilizikonga nyoyo za wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia tamasha lake la ‘Back to University’ lililofanyika katika Viwanja vya Hostel ya Mabibo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maelfu ya wanafunzi.

  Tamasha hilo lilipambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Msami, Ruby na Stamina pia lilitawaliwa na michezo ya aina mbalimbali kama vile Netiboli, soka na mingineo.

  Akizungumzia kuhusiana na tamasha hilo Mkurugenzi wa Halotel tawi la Dar es Salaam, Bwana Alex Thiem alisema tamasha hilo lina lengo la kuimarisha uhusiano baina ya Halotel na wanafunzi wa vyuo vikuu.

  ‘Toka mtandao wetu umeanza hapa nchini tumejikita katika kuhakikisha tunaboresha huduma za simu nchini, lakini kwa upekee kabisa tumekuwa tunawapa wanafunzi huduma bora na nafuu zaidi’ alisema bwana Thiem.

  Kwa upande wa burudani Msami alipopanda jukwaani alitumia takribani dakika 45 kuzikonga nyoyo za mashabiki wake hao ambapo aliimba nao na kucheza pia hasa akionesha umahiri wake wa kucheza dansi.

  Naye msanii Ruby anayetamba na kibao chake kipya cha Forever, alitoa burudani kali kwa maelfu ya wanafunzi waliojitokeza katika hosteli hizo.

  Ilipofika majira ya saa 12 jioni akapanda jukwaani msanii Stamina ambae ameandika historia ya kipekee kwa wanafunzi hasa kwa aina yake ya uimbaji wa mashairi yaliyokuwa yakishangiliwa mara kwa mara.

  Tamasha hilo lilianza majira ya saa nne asubuhi kwa michezo ya aina mbalimbali kama vile Netiboli pamoja na soka ambapo katika mchezo wa Netiboli timu ya wanafunzi wanaume iliibuka na ushindi wa mabao 11 - 10 dhidi ya timu ya wanawake.

  Kwa upande wa mchezo wa soka zilicheza timu mbili ambapo ilianza timu ya Baraza la Mawaziri la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyoibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya Idara ya Mazoezi ya Viungo.

  Katika mechi nyingine, timu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ikaifunga timu ya Chuo Kikuu cha Ualimu (DUCE) 1-0.

  Michezo hiyo kwa ujumla ilizokonga nyoyo za wanafunzi wengi ambapo pia walipata wasaa wa kujiunga na huduma za mtandao huo wa simu kama vile kununua laini, kujiunga vifurushi na mengineo.

  Kwa upande wake waziri wa michezo wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, bwana Jackson Mayunga aliishukuru kampuni ya Halotel kwa kufanikisha tamasha hilo.
  ‘Tunawashukuru sana Halotel kwa kufanikisha tamasha hili, na kama unavyoona wanafunzi wamepata nafasi ya kuburudika lakini pia kubadilishana mawazo’ alisema Mayunga.

  0 0

  Na Lorietha Laurence-Maelezo

  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa amekagua mradi wa upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco yenye kilomita 4.3 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 95.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara hiyo Prof.Mbarawa ameeleza kuwa tayari njia tano zimeanza kutumika kuanzia eneo la Mwenge hadi Kijitonyama zenye urefu wa kilomita 2 huku kilomita nyingine 2.3 zikiwa katika harakati za mwisho za kukamilishwa.

  “Serikali imedhamiria katika kuhakikisha kuwa inatatua kero ya msongamano wa magari kwa kufanya upanuzi wa njia muhimu ili kurahisisha hali ya usafiri jijini Dar es Salaam ” alisema Prof.Mbarawa.

  Aliongeza kwa kusema hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli alizindua mradi wa daraja la Kigamboni linalounganisha kurasini na Kigamboni pamoja na kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa flyover katika eneo la Tazara .

  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi.Patrick Mfugale ameeleza kuwa mradi huo umekabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo uhamishaji wa mabomba ya maji safi na maji taka katika eneo la Makumbusho na Mwenge ili kuendelea na ujenzi.

  Novemba 30 mwaka jana Rais John Magufuli aliagiza kiasi cha shilingi bilioni nne kilichopangwa kutumika katika shamrashamra za siku ya Uhuru kitumike katika kazi ya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 ili kuiunganisha barabara hiyo na ile ya Mwenge – Tegeta yenye urefu wa KM 12 .

  0 0

  Bi.Yasmin Razak, akiwa amembeba mtoto anayeugua maradhi ya Selimundu (Sickle cell), wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mama huyu ambaye mwanaye pia anaugua ugonjwa huo, lakini matibabu yake anapatanchini Uingereza, ameamua kusimama kidete kutetea wagonjwa wa selimundu kuendelea kuhudumiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na kumuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuingilia kati mpango wa kuwaondoa wagonjwa 6,000 hospitalini hapo na kuwapeleka kwenye hospitali wanakotoka.
  NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, MNH

  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili, MNH, na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, wametoa msimamo kuhusu sintofahamu iliyowakumba wagonjwa wa sickle cell (Selimundu), waliokuwa wakipatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo kubwa kabisa hapa nchini.

  Kauli ya MNH kuhusu tiba ya Selimundu

  “Tunapenda umma uelewe kuwa huduma hii haijasitishwa na wala Hospitali haitasitisha utoaji wa huduma hiyo.” Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence M. Museru, amewaambia waandishi wa habari leo Aprili 25, 2016.

  Hofu ya wagonjwa

  Awali baadhi ya wazazi wa watoto wenye kuugua maradhi ya Selimundu, wakiongozwa na Bi.Yasmin Razak, wameonyesha hofu ya maisha ya watoto wao kufuatia taarifa kuwa jumla ya wagonjwa 6,000 waliokuwa wakipatiwa matibabu ya Selimundu hospitalini hapo chini ya mradi wa utafiti wa ugonjwa huo, “Welcome Trust.” Watarudishwa kwenye utaratibu wa matibabu chini ya muongozo wa Wizara ya Afya kwenye hospitali walikotoka, kwa vile mradi huo wa utafiti umemaliza kazi yake Machi 31, 2016.

  Gharama za matibabu ya Selimundu

  Ni kweli kwamba takribani miaka kumi kulikuwa na mradi uliokuwa ukifadhili matibabu pamoja na utafiti wa wagonjwa wa selimundu, Mradi huu kwa sababu ya utafiti ulihitaji wagonjwa wote wa selimundu kuja Muhimbili kwa ajili ya utafiti na tiba. Hivyo basi hali hii ilisababisha wagonjwa wengi wanaohitaji huduma ya selimundu kuja Hospitalini hapa licha ya kwamba mahitaji yao hayakuhitaji utalaamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,

  Amesema Profesa Mseru. 

  Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Dkt.Doroth Gwajima, amewaondoa hofu wagonjwa kuhusu gharama za matibabu hayo ambapo alisema, muongozo wa serikali uko wazi, wazee na watoto watapatiwa matibabubure na wengine wanachangia kupitia bima ya afya na fedha taslim, hata hivyokwa wale ambao hawatakuwa na uwezo utaratibu wa kuwapatia matibabu upo.

  Hofu ya wagonjwa

  Kutokana na mazoea ya muda mrefu ya kupatiwa matibabu bure ya ugonjwa huo wa selimundu, na hasa ikizingatiwa hakuna tiba ya kuuponya kabisa ugonjwa huo, wagonjwa wamehoji watawezaje kumudu kulipia gharama hizo?
  Wazazi wa watoto wanaougua ugonjwa huo, wametmuomba Rais John Magufuli, kuingilia kati suala hilo ili kuokoa maisha ya wagonjwa hao ambao kwa asili ya ugonjwa wenyewe, mgonjwa hupata maumivumakali mwilini, mabadilikoya viungo, na wakati mwingine kupungukiwa damu mara kwa mara.

  Kauli ya Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam

  “Hospitali zote za Manispaa ya jiji la Dar es Salaam, na hata zile zilizopo mikoani na wilayani, zina uwezo wa kutoa huduma za ugonjwa wa Selimundu, na hata ikionekana kuwa mgonjwa anahitaji matibabu zaidi, rufaa huandaliwa na mgonjwa hupelekwa kwenye hospitali kubwa zaidi ili kupatiwa matibabu yanayofaa.” Dkt.Grace Magembe, Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam.
  Bi.Getrude Thadeo kutoka Tabora, akiwa na mtoto wake wa miaka 13, Angela Romwadi, ambaye anaugua Selimundu
  Bi.Mkami Titus wa Temeke jijini Dar es Salaam akiwa na mtoto wake Shedrack Yahaya(4), anayeugua selimundu
  Bi.Walivyo Mohamed kutoka Rufiji mkoani Pwani, akiwa na mtoto wake wa miaka 4, Siraji Majid
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitaliya Taifa Muhimbili, (MNH), Profesa Lawrence Museru, (kulia), akiwa na Mkuu wa Idara ya Magonjwa na Afya ya Watoto ya MNH, Dkt. Mary B. Charles, akizungumza na waansdishi wa habari wakati akitoa taarifa yake mapema leo Aprili 25, 2016
  Profesa Museru
  Dkt.Doroth Gwajima, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia Wazee na Watoto
  Profesa Museru natimu yake wakati akiongea na waandishi wa habari
  Dkt.Grace Magembe, Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam
  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Elineema Meda. Dkt. Meda ni mmoja wa walioshiriki kwenye utafiti wa ugonjwa huo wa Selimundu chini ya mradi wa Welcome Trust
  Bi. Yasmin wakati wa mkutanona waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
  Baadhiya akina mama wakiwa na watoto wao wanaosumbuliwa na maradhi ya Selimundu. Hapa wakihudhuria mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na Bi. Yasmin ambaye ameamua kuwasimamia na kuwasemea wagonjwa wa Selimundu
  Bi. Yasmin (katikati), akiwa na Bi.Walivyo Mohammed na mtoto wake Siraji (kushoto) na Bi. Getrude Thadeona mtoto wake Angela

  0 0

  Paulina Mgeni ndio Miss Utalii Mkoa wa Iringa mwaka 2013 mpaka sasa kabla mashindano hayo hayaja simamishwa; ila kwasasa anafanya kazi za mitindo akiwa kama Mwanamitindo (Model), lakini anahitaji meneja wa kusimamia kazi zake hizo za Urembo (Modeling).

  Paulina Mgeni ni Mwanamitindo (Model) anaefanya kazi za urembo na maonesho ya mitindo kwa kujitegemea yeye mwenyewe hayupo chini ya kampuni yoyote wala chini ya lebo ya mtu yeyete, japokua amekuwa akifanya shoo nyingi kwa kushirikiana na baadhi ya makampuni na wabuni mbalili, kwasasa anatafuta Meneja wa kuwa anamsimamia kazi zake.

  Mwaka 2013 Paulina alikuwa Miss Utalii mkoa wa Iringa, akafanikiwa kuingia ngazi ya Taifa na kupata tuzo ya the Best Model of Tanzania, pamoja na kuwa Balozi wa models Tanzania; amefanikiwakufanya maonesho (shows) mbali mbali hapa Tanzania na nje ya Tanzania.
  Mwanamitindo Paulina Mgeni akiwa katika pozi.

  Paulina amefanya kazi na wabunifu mbali mbali (designers) kama vile Asia Idalus, Kurwa Mkwandule, Adam Zanzibar house, Wolta Di Maria n.k. Maonesho (shows) makubwa ambayo amefanya ni Zanzibar fashion house mwaka 2014 na yale East Africa Fashion Week jijini Nairobi –Kenya akiwa na makeke internasional, maonesho hayo yalifanyika mwezi 3 tarehe 29 mwaka 2016. Hivyo kwa yeyote atakaehitaji kuwa meneja wa mrembo huyu kwa ajili ya kusimamia kazi zake unaweza kuwasiliana nae kwa namba +255 716 66 66 96 au kwa barua pepe mgenipaulina3@gmail.com 
  Paulina Leonard akiwa katika maonesho Zanzibar, Fashion House.  Paulina Mgeni (wa kwanza kulia) akiwa katika maonesho ya East AfricaFashion Week jijini Nairobi mwezi 3 mwaka 2016


  Paulina akiwa katika show ya Lady in RED jijini Dar es Salaam.  Mwanamitindo Paulina Mgeni katika photo shoot.

  0 0

  Ummy Mwalimu

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwaonesha waandishi wa habari kipimo cha haraka cha kupima malaria(mRDT) wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani leo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa Mbu waenezao Malaria Charles Dismas kutoka mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria.

  Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amewataka watanzania kwa pamoja kuungana kupambana na ugonjwa wa Malaria ili kusaidiana na serikali kutokomeza ugonjwa huo ambao husababisha vifo vya watu wengi nchini.

  Waziri Ummy ameyesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku ya Maralia Duniani ambapo huadhimishwa Aprili, 25 ya kila mwaka na kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu ili kutokomeza ugonjwa huo.

  “Msisitizo mkubwa wa Wizara yangu ni kwa wananchi na wadau wote kuona umuhimu na kutoa kipaumbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria kwa kuhakikisha matumizi sahihi ya mikakati iliyopo katika kuuthibiti ugonjwa huu,“Iwapo mikakati hiyo itatekelezwa ipasavyo ni dhahiri kuwa maambukizi yataendelea kupungua kwa kiasi kikubwa na hatimaye kumaliza kabisa tatizo hili,” alisema Waziri Ummy.
  Waziri Ummy Mwalimu
  Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Dkt.Renata Mandike (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusiana na utekelezaji wa udhibiti wa Malaria nchini wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu.
  Malaria
  Baadhi ya wataalam wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri Ummy Mwalimu.
  mwalimu
  Fundi sanifu maabara, Habiba Malima akimchukua damu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu kwa kipimo cha malaria Rapid Diagnosist Test(mRDT), kipimo hicho ni cha haraka na huchukua dakika ishirini kugundua kama una Malaria, kipimo hiki kilianza kutumika nchini mwaka 2009.
  Richard Mwaikenda
  Mwandishi wa habari na mmiliki wa globu ya mzee wa matukio, Richard Mwaikenda akichukuliwa kipimo cha malaria na fundi sanifu maabara Habiba Malima ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria duniani katika ukumbi wa viwanja vya Bunge.

  Eleuteri Mangi
  Afisa habari wa idara ya habari Maelezo, Eleuteri Mangi akipima malaria kwa kipimo cha mRDT.
  Kijah Yunus
  Mwandishi wa habari kutoka Clouds media, Kijah Yunus akipima Malaria.

  0 0

  Timu ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania Bunge Sports Club inatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo mkali na wa aina yake ambao ni wa kwanza na timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

  Mapema leo Aprili 25.2016 timu hiyo ilishuka katika dimba hilo la Amani na kupasha misuli maalum kwa hiyo mchezo huo wa hiyo kesho ambapo kwa mujibu wa viongozi wa timu hiyo ya Bunge wametamba kuibuka na ushindi wa kishindo.

  Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamotto ametamba kwa timu yake kuibuka na ushindi mnono katika mchezo huo kwani wana mazoezi ya kutosha na pia wamejiandaa kuonyesha uwezo.“Tunawaomba wabunge wote kutuunga mkono katika mchezo huu kwani tmu imejindaa vya kutosha kuhakikisha tunashinda. 

  Mchezo huu ni maalum kwa ajiri ya kuimalisha Muungano wetu tukufu hivyo tutaendelea kuuenzi na kuukumbatia na sote kwa pamoja tuzidishe Amani” alieleza Mh. Mwamotto.

  Kwa upande wake Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani 'Maji Marefu' ambaye ni miongoni mwa viongozi wa msafara wa timu hiyo ya Bunge ametamba timu yake kuibuk na ushindi mnono kwani wamejiandaa kisaikolojia na mazoezi ya kimichezo.

  Naye Mbunge wa Nzega Vijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla viongozi wa timu hiyo ya Bunge amebainisha kuwa, mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya Saa 12 Jioni kesho Aprili 26.2016 katika uwanja huo wa Amani.

  “Mechi kati ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Utachezwa kesho ni siku ya Kuadhimisha Muungano wa Nchi ya Jamhuri ya Tanganyika Na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Tunawaomba watu kujitokeza kwa wingi kuuona mchezo huu ambao utakuwa wa aina yake kwa timu zote mbili.” Alieleza DK. Kigwangalla.

  Timu hiyo ya Bunge yenye wachezaji Zaidi ya 19 imejiandaa vya kutosha katika kuakikisha inapata ushindi mnono na ipo Visiwani hapa kwa maandalizi ya mchezo huo tokea jana na leo imeweza kufanya mazoezi ya awali asubuhi na mengine wakitarajia kufanya hapo jioni.
  DSC_1627Timu ya Bunge ikifanya mazoezi yake mapema leo Aprili 25 kuajiandaa na mchezo huo utakaochezwa keshi Jioni uwanja wa Amani.
  DSC_1741Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani 'Maji Marefu' akisimamia mazoeszi hayo kwa muda wakati wsa asubuhi ya leo
  DSC_1664mazoezi hayo yakiendelea.

  DSC_1627Mazoezi yakiendelea
  DSC_1742DSC_1679DSC_1684Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamotto (kati) akitoa maelezo ya mazoezi hayo
  DSC_1636DSC_1717Benchi la ufundi likiwa tayari katika mazoezi hayo
  DSC_1751DSC_1721Mbunge William Ngeleja akijaribu kutaka kuchukua mpira kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Hamisi Kigwangalla.
  DSC_1683Mazoezi moto moto yakiendelea..
  DSC_1687Mazoezi makali ya timu ya Wabunge yakiendelea katika uwanja wa Amaan, Unguja leo Aaprili 25.2016. Timu hiyo kesho Aprili 26 inatarajia kucheza mchezo wao dhidi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog, Zanzibar).

  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha.
  SERIKALI imeombwa kuendelea kutenga fedha za ukarabati kila mwaka kwa shule kongwe ya wanafunzi wenye vipaji maalum ya Ilboru ili walau kuzirudisha katika hali yake nzuri na kuzijengea mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundishia, ili zionekane tofauti na shule zingine hatimaye ziwafanye wanafunzi wajitume zaidi katika masomo.

  Hayo yalisemwa jana na mkuu wa shule kongwe ya Ilboru sekondari Julius
  Shulla alipokuwa akizungumza na wadau wa elimu na walezi katika mahafali ya 24 ya kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo.

  Alisema kuwa shule hiyo kongwe na ambayo imekuwa ikitoa wataalamu mbali mbali imekuwa ina uhitaji wa kukarabatiwa na hivyo ili kuondokana na hali hiyo serikali inapaswa kutenga fedha kila mwaka ili kuweza kuirejesha shule hiyo katika mazingira mazuri yatakayowavutia wanafunzi.

  Alileleza kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu mkubwa wa madarasa na nyumba za watumishi hali ambayo inasababisha mara nyingi wanafunzi kukosa mahala pazuri pa kujifunzia hivyo kuwakatisha tama kimasomo.

  “tunaiomba na kuishauri serikali yetu sikivu iendelee kutenga fedha za
  ukarabati kila mwaka kwa shule hizi kongwe ili kuzirudisha katika mazingira yake mazuri ikizingatiwa hii ni shule ya wanafunzi wenye vipaji maalum kiakili hali hii itawafnya wanafunzi wajitume zaidi katika masomo kwa kuwa na mazingi mazuri ya kujifunzia”aliongeza Shulla.

  Aidha Shulla alitaja changamoto zingine zinazoikabili shule hiyo kongwe
  kuwa ni pamoja na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi ambapo hali hiyo inatokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi ikilinganishwa na idadi ya walimu.

  Alifafanua kuwa tatizo hilo husababisha shule hiyo kutafuta walimu wa muda wa masomo ya Fizikia,kemia ,na hisabati ambao malipo yao ni makubwa sana kwa mwezi ambapo shule haina uwezo wa kumudu gharama hizo kila mwezi.

  Aliwataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata katika kutatua matatizo
  yao na matatizo ya jamii yote kwa kufuata sheria na taratibu za nchi huku
  wakijiepusha na uzembe ,ulevi,uvutaji bangi na matumiz ya madawa ya kulevya kwani hivyo vyote havina tija katika maendeleo.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Busanda, Lolesia Bukwimba kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Aprili 25, 2016. Katikati ni Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sere,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati na Mwanansheria Mkuu wa Serikali, George Masaju,bungeni Mjini Dodoma Aprili 25, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango, bungeni mjini Dodoma Aprili 25, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sere,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama (katikati na Mwanansheria Mkuu wa Serikali, George Masaju,bungeni Mjini Dodoma Aprili 25, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, bungeni Mjini Dodoma Aprili25, 2016. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akiteta na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt,. Hussein Mwinyi, bungeni Mjini Dodoma Aprili 25, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mwibara, Kange Lugola, bungeni Mjini Dodoma Aprili 25, 2016
  Mwenyekiti wa Bunge Dkt. Mary Mwanjelwa (kushoto) akiteta na Mbunge wa Viti Maalum Grace Kiwelu, bungeni mjini Dodoma Aprili 25, 2016. 

  0 0

  Naibu Waziri wa afya akizindua Rasmi wiki ya chanjo Afrika kwa kumpatia tone la chanjo mtoto Mudrik Ali Khamis mkaazi wa Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
  MKUU wa wilaya ya Kaskazini B Haji Makungu Mgongo akimkaribisha Naibu waziri wa afya Harusi Said Suleiman kuzindua wiki ya chanjo Afrika.
  NAIBU Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akiwahutubia wananchi mbalimbali wliohudhuria katika sherehe hizo zilizofanyika kituo cha afya Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
  KATIBU Tawala wilaya ya Kaskazini B Juma Abdalla Hamad akitoa maelezo namna wilaya ilivyojiandaa kufanikisha uzinduzi wa wiki ya chanjo Afrika katika sherehe ziliofanyika kituo cha afya Kitope.
  Wananchi mbali mbali waliojitokeza katika kuitikia wito wa siku ya chanjo Afrika katika uzinduzi uliofanyika kituo cha afya Kitope.
  KIKUNDI cha ngoma za asili cha Magereza kikitoa burudani katika sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo Afrika.Baadhi ya watoto waliojitokeza katika maadhimisho hayo wakisubiri huduma ya chanjo.(PICHA NA ABDALLA OMAR HABARI MAELEZO ZANZIBAR.)

  0 0

  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akionesha ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma juu ya ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
  Waandishi wa habari wakipokea ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO
  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad amekabidhi ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 bungeni leo ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.

  Katika ripoti yake, CAG ametoa mapendekezo kadhaa ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kuboresha matumizi ya fedha za Serikali kwa malengo yanayokusudiwa.

  Miongoni mwa maeneo ambayo CAG ametoa mapendeklezo ni Ofisi ya Masjili wa Vyama vya Siasa nchini ifuatilie suala la uwasilishaji wa taarifa za fedha kwa wakati kulingana na matakwa ya sheria.

  Hatua hiyo ya CAG inafuatia ukaguzi uliofanywa kwenye vyama vya siasa nchini vyenye usajili wa kudumu ambavyo jumla yao ni vyama 22.

  Prof. Assad alisema kuwa kati ya vyama hivyo vyenye usajili wa kudumu, ni chama kimoja ndicho kilichowasilisha hesabu zake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi Juni 2015 ambacho ni Chama cha Wananchi (CUF).

  Vyama vingine 21 havikuwasilisha vitabu vya hesabu kwa ajili ya ukaguzi kinyume cha kifungu Na. 14 cha Sheria ya vyama vya siasa Na. 5 ya mwaka 1992.

  0 0  0 0

  Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan akifungua kikao cha maafisa usafirishaji wa Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi Silivester Simfukwe na kulia ni Mhandisi Elirehema Mmari.
  Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi Silivester Simfukwe akizungumza na maafisa usafirishaji wa Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali katika kikao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan.
  Baadhi ya cha maafisa usafirishaji wa Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali wakifatilia kikao kati yao na Wakala wa Umeme na Ufundi(TEMESA) kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Theresia Mwami-TEMESA).

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Maafisa usafirishaji kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbali mbali za Serikali wameaswa kuwa wazalendo kwa kufuata kanuni na utaratibu wa matengenezo na shughuli za kiufundi Serikalini.

  Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan alipokuwa akifungua kikao cha maafisa usafirishaji kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbali mbali za Serikali kujadili changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zinazosimamia matengenezo ya magari na mitambo ya Serikali.

  Kaimu Mtendaji Mkuu huyo amesema kwa hali ilivyo sasa imebainika kuwa Sheria na Kanuni za matengenezo ya magari na mitambo ya Serikali imekuwa ikikiukwa kwa kiasi kikubwa na hivyo kuilazimu mamlaka husika kutafuta njia mbadala ili kukabiliana na changamoto hiyo.

  “Lengo letu ni kupata namna bora ya kutoa huduma ya matengenezo ya kiufundi ya vifaa vya Serikali pasipo kukiuka Sheria na Kanuni zilizowekwa hivyo basi tunaomba ushirikiano kutoka kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuleta magari na vifaa kwetu ili tutekeleze wajibu wetu” alisema Mhandisi Manase.

  Mhandisi Manase ameongeza kuwa pamoja na uchache wa Wizara , Idara na Taasisi za Serikali zinazotekeleza Sheria na Kanuni za matengenezo ya magari ya Serikali kwa kuleta magari TEMESA ila kumekuwa na changamoto katika ulipaji wa gharama za matengenezo hali inayosababisha Wakala usiweze kufanya kazi kwa ufanisi.

  Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo kutoka TEMESA Mhandisi Sylivester Simfukwe amesema Wizara , Idara na Taasisi za Serikali zinatakiwa kuzingatia Sheria na Kanuni zilizopo kwa kupeleka na kulipa gharama za matengenezo ya magari na vifaa vya Serikali kwani Wakala huu ndio mshauri mkuu wa Serikali katika masuala ya kiufundi na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kuongezeka kwa mapato ya Serikali.

  Naye Meneja Usafirishaji kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Jonathan Mhagama ameiomba Serikali kuiongezea uwezo TEMESA kwa kuwa na karakana za kisasa ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ambapo kwa sasa uwezo walionao wakala huo ni mdogo ukilinganisha na magari yaliyopo Serikalini.

  Mkutano kati ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na maafisa usafirishaji wa Wizara,Idara na Taasisi mbalimbali za serikali umekuja mara baada ya kauli kutoka kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa ya kuyataka magari yote ya Serikali kutekeleza Sheria na Kanuni za matengenzo ya vifaa vya Serikali.

older | 1 | .... | 827 | 828 | (Page 829) | 830 | 831 | .... | 1897 | newer