Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 825 | 826 | (Page 827) | 828 | 829 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na watumishi hewa waliopo katika Manispaa za Mkoa wa  Dar es Salaam. Amesema kuwa mchakato wa kuwatafuta watumishi hewa wengine unaendelea katika manispaa za mkoa wake.
  Picha na Avila Kakingo.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kazi ya kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jiji la Dar es Salaam bado linaendelea baada kubaini njia chafu wanazotumia watumishi hewa hao.

  Akizungumza leo na waandishi habari ,Makonda amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kioo kwa nchi hivyo jitihada zinaendelea ya kutafuta na kazi hiyo itafanywa sekta kwa sekta.

  Amesema kuwa Wakuu wa Wilaya katika jiji la Dar es Salaam hakuna kufanya kazi yeyote mpaka wamelize kutafuta watumishi hewa kwa kutumia malipo ya watumishi kutoka taasisi za fedha
  (Pay Row).

  Makonda amesema idadi ya watumishi hewa 71 aliowasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –Tamisemi, Georgre Simbachawene  ni ndogo katika  jiji la Dar es Salaam hivyo kazi lazima iwe endelevu.

  Amesema kuwa watumishi Hewa hawawezi wakawa wanalipwa mshahara huku wanaofanya kazi kwa moyo mmoja wanajisikia  vibaya hivyo ni lazima watafutwe na wachukuliwe hatua na vyombo vya dola.

  Mkuu Mkoa amesema kuwa kati ya watumishi hewa 71 ni watumishi 34 hewa wamefunguliwa mashitaka katika mahakama mbalimbali kutokana kuchukua fedha wasioifanyia kazi.

  0 0  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  SERIKALI imesema kuanzisha kambi za kufanya oparesheni kwa watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa itasaidia kuokoa maisha ya  watoto hao kutokana na wazazi wao kushindwa kumudu gharama za oparesheni hizo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati makababidhiano ya magari kwa ajili ya kambi hizo, Mwakilishi wa Waziri wa Afya na Maendeleo jamii jinsia, Watoto , Mkuu  wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa Mfuko wa GSM wametambua matatizo ya watoto hao na kuamua kutoa sehemu yao katika kuhakikisha watoto hao wanafanyiwa oparesheni.

  Makonda amesema kambi hizo wazazi watapeleka watoto tu ambayo ndio gharama yab kufanya watoto wao wafanyiwe oparesheni ya matatizo yao.
  Amesema kuwa watu walikuwa wanafikiria ndani ya bajeti tu bila kuangalia wadau wana uwezo gani na kusababisha mambo kurudi nyuma kwa GMS wameonyesha  njia katika kufanya ufadhili wa oparesheni hiyo.

  ‘’Naamini watoto hao watakuwa kuwa watumishi wenye maadili kutokana na matatizo waliopata na watu wengine wakahangaikia hivyo hawawezi kuwa mafisadi kwa kujua atachochukua kuna watu wanahitaji’’amesema Makonda.

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk.Othman Kiloloma amesema kuwa daktari wenye utaalamu huo ni daktari tisa tu kati ya hao nane  ni Hospitali ya Taifa Muhimbili na mmoja Hospitali ya Bungando.

  Dk.Kiloloma amesema kufanya operesheni ya mtoto mmoja ni sh. Laki saba hadi milioni moja ambapo baadhi wanashindwa kumudu hivyo ufadhili wa GSM utafanya kuweka kambi na kutoa huduma hiyo bure kwa watoto pamoja na kutoa elimu kwa baadhi ya daktari juu ya oparesheni ya watoto wenye migongo wazi na vichwa vikubwa.

  Afisa  Mawasiliano wa GSM , AKhalfan Kiwamba amesema kuwa wanatambua matatizo ya watoto hao na kuamua kufanya ufadhili ili waweze kufanyiwa oparesheni  hiyo.

  Amesema kambi hizo awamu ya kwanza itakuwa Mkoa wa Mwanza Aprili 27 hadi 30, Shinyanga  Mei 2 hadi 4,  Singida Mei 6 hadi 8, Dodoma  10  hadi 13, Morogoro Mei 15  hadi 17 .
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata na utepe kuzindua magari ambayo yametolewa na Mfuko wa GSM kwaajili ya kusidia kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa pamoja na watoto wenye migongo wazi katika kambi itakayofanyika katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa kambi ya upasuaji ya watoto wa wenye vichwa vikubwa na watoto wenye matatizo ya mgongo wazi ambapo Mfuko wa GMS kushirikiana na Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili wataanza kambi hiyo katika mikoa ya Mwanza Aprili 27 mpaka Aprili 30, Shinyanga Mei 2 mpaka 4, Singida Mei 6 mpaka Mei 8, Dodoma Mei 10 mpaka 13 na Morogoro 15 mpaka 17. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma na Mkurugenzi wa tiba MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Samwel Swai.
   Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kambi ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na watoto wenye Migongo wazi. Kulia ni kuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.
  Afisa Uhusiano wa Mfuko wa GSM, Khalfan Kiwamba akizumgumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na GSM kutoa mchango wake kwa kusaidia watoto wenye matatizo ya Mgongo wazi na watoto wenye vichwa vikubwa. Kusoto ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa GSM, Shannon Kiwamba.

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimpa ufunguo za magari,Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Taasisi ya tiba na upasuaji ya Mhimbili, Othman Kiloloma leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mfuko wa GSM leo katika hospitali ya Muhimbili kwenye kitengo cha MOI jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Askofu Mkuu wa Jimbo la Dodoma , Beatus Kinyaiya katika mazishi ya Askofu Mstaafu wa Dodoma Mathias Isuja yaliyofanyika kwenye kanisa kuu la Mtakatifu Paul wa Msalaba Mjini Dodoma Aprili 20, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Askofu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mathias Isuja katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa   Kuu la Mtakatifu Paul wa Msalaba Aprili 20, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mathias Isuja  katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa  Kuu la Mtakatifu Paul wa Msalaba,  Aprili  20, 2016.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya waumini na wakazi wa mkoa wa Dodoma katika mazishi ya Mhashamu Askofu Mstaafu, Mathias Isuja wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.

  Amesema kifo hicho ni pigo kwa watu wote na si kwa kanisa pekee kwa sababu walimtegemea kulisaidia Taifa kiroho na kimaendeleo.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 20, 2016) wakati akizungumza na waumini na wakazi wa mkoa huo na mikoa jirani kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiaskofu la Mtume Paulo wa Msalaba mjini Dodoma.

  Askofu Isuja ambaye alizaliwa Agosti 14, 1929 alikuwa Askofu wa kwanza mzalendo katika Jimbo la Kanisa Katoliki la Dodoma. Alistaafu kazi ya uaskofu mwaka 2004 kwa mujibu wa sheria ya kanisa. Alifariki Aprili 13, mwaka huu.

  Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kumuenzi Askofu Isuja kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati wa uhai wake na kuyaendeleza yote aliyoyaanzisha kwenye maeneo aliyowahi kuyatumikia.

  “Tumepoteza mtu makini, sisi ni mashahidi wa mchango mkubwa wa marehemu siyo tu katika kutoa huduma za kiroho, bali pia huduma za kijamii zilizolenga kuleta maendeleo kwa wananchi katika jimbo hili la Dodoma na katika taifa kwa ujumla,” amesema.

  Mapema, akitoa mahubiri wakati wa ibada hiyo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Judathadeus Ruwa’ichi alisema waumini wa kanisa hilo wa mkoa wa Dodoma na Tanzania nzima wanapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha marefu aliyomjalia Askofu Isuja.

  “Tunapaswa kumshukuru kwa maisha marefu ambayo Mungu alimzawadia baba yetu Isuja. Katika Zaburi ya 90 tunasoma kuwa mwanadamu ana miaka ya matazamio ambayo ni 70, lakini yeye alipewa miaka ya matazamio 70 na akazawadiwa nyongeza ya miaka 10 na kisha miaka mingine sita na nusu,” alisema.

  Alisema zawadi nyigine ambayo Mungu aliwapatia waumini hao ni ya imani ambayo Baba Askofu Isuja aliipokea, aliifundisha na aliishi na akawataka waendelee kumshukuru Mungu kwa hilo. “Miaka 56 ya utumishi wake kama padre na askofu ni zawadi kwa Dodoma na Tanzania na siyo kwake yeye binafsi,” alisema.

  Ibada hiyo ya mazishi ilihudhuriwa na Maaskofu Wakuu na Maaskofu wa kawaida 28 kutoka majimbo ya Dodoma, Mwanza, Mbeya, Njombe, Mpanda, Iringa, Songea, Tabora, Morogoro na Mahenge. Mengine ni Musoma, Rulenge, Mbinga, Moshi, Same, Kahama, Sumbawanga, Shinyanga, Mtwara na Lindi. Majimbo mengine ni Bukoba, Tanga, Singida, Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha, Kondoa na Kayanga.
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980.
  DODOMA.

  JUMATANO, APRILI 20, 2016.

  0 0

  KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanziba, kesho (Aprili 23, 2016) inatarajia kukutana chini ya Mwenyekiti wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

  Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Itikadi na Uenezi Mama Waride Bakari Jabu imesema kikao hicho kitafanyika Afisi Kuu ya CCM, iliyopo mtaa wa Kisiwandui, Mjini Unguja.

  Taarifa imesema kikao hicho kawaida cha siku moja, pamoja na mambo mengine kitapokea na kujadili taarifa kadhaa kutoka Idara na Vitengo mbali mbali vya Chama hicho, ikiwemo taarifa ya hali ya kisiasa ya Zanzibar, kabla na baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Marudio wa Zanzibar.

  Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, kilichofanyika April 20, mwaka huu, chini ya M/kiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai, kwa ajili ya kuandaa ajenda za kikao hicho.

  Taarifa imesema kikao hicho kinafanyika kwa mujibu wa Ibara ya 114 (b) ya Katiba ya CCM, Toleo la mwaka 2012 na kwamba maandalizi yote yamekamilika.

  Sgd.

  (Waride B. Jabu),
  Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,
  Idara ya Itikadi na Uenezi - CCM,
  ZANZIBAR.
  22/04/2016.

  0 0

  JAJIMkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli za Mahakama katika Kanda ya Mbeya.

  Ziara ya Mhe. Jaji Mkuu katika kanda hii imelenga kujionea hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha Watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuboresha huduma ya utoaji haki nchini. 

  Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Maafisa na Watendaji kadhaa wa Mahakama kutoka Makao makuu ili kujionea hali ya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kubainisha na kufanyia kazi changamoto ambazo watumishi wanakumbana nazo katika utendaji kazi wa kila siku. 
   Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, (katikati) akipata taarifa fupi ya utendaji kazi wa Mahakama Kanda ya Mbeya kutoka kwa Mhe. Noel. P. Chocha, Jaji Mfawidhi Kanda ya Mbeya (aliyesimama), mara baada ya kuwasili katika kikao kilichohusisha Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya.

  Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye alipata nafasi ya kukagua na kuongea na Watumishi wa ngazi mbalimbali za Mahakama katika mkoa huo.

  Katika kikao alichofanya na Watumishi wa Mahakama mkoani humo ikiwa ni pamoja na Wahe. Majaji na Mahakimu, Mhe. Jaji Mkuu alisisitiza mara zote juu ya utendaji kazi kwa kujituma ili kubadili taswira ya Mahakama kwa wananchi ambao ndio wadau muhimu wa Mahakama.
  Akiongea na Watumishi wa Mahakama wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Jaji Mkuu alieleza kufurahishwa na kasi ya usikilizaji na umalizwaji wa mashauri katika Mahakama za Mwanzo mkoani humo.
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman akizungumza na  Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya alipokutana nao na kuwaasa kuendelea kutenda Haki kwa wakati ili kuweza kupunguza na kumaliza mashauri yanayowasilishwa mahakamani.

  Awali; katika taarifa yake kwa Mhe. Jaji Mkuu, Mhe. Noel Chocha, Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, alimtaarifu Mhe. Jaji Mkuu juu ya mkakati waliojiwekea wa kumaliza mashauri ya aina yoyote kwa kipindi kisichozidi miezi sita. 

  Aidha Mhe. Jaji Mkuu alitumia ziara hiyo ya kikazi kuwaeleza Watumishi juu ya mikakati ambayo Mahakama imejiwekea katika kuhakikisha kuwa huduma ya utoaji haki inaboreshwa nchini. 

  “Kwa hivi sasa Mahakama ya Tanzania imejiwekea mikakati/vipaumbele ambavyo vinalenga kuboresha huduma ya utoaji haki nchini, na malengo haya inabidi yafanyiwe kazi na kila mmoja wetu kwa maana ya kila Mtumishi na mdau wa Mahakama awajibike katika kufikia malengo yetu ya kuboresha huduma ya utoaji haki nchini.” Alisema, Mhe. Jaji Mkuu.

  Uimarishaji wa ukusanyaji wa takwimu; hili pia ni eneo ambalo limewekwa kama kipaumbele katika maboresho Mahakamani, Mhe. Jaji Mkuu alisema Mahakama pia imejipanga vyema kuhakikisha inakuwa na takwimu sahihi za kesi mbalimbali zilizopo katika Mahakama mbalimbali nchini ili kuangalia ni sehemu ipi inayohitaji nguvu zaidi katika kushughulikia mashauri/kesi za muda mrefu. 

  Uboreshaji wa Miundombinu: miundombinu hii ni pamoja na majengo ya Mahakama, vitendea kazi n.k, Mhe. Jaji Mkuu alisema pia katika kuboresha huduma zake Mahakama imejipanga katika kuboresha miundombinu yake ikiwa ni pamoja na kujenga majengo ya Mahakama na kukarabati majengo yaliyochakaa. 

  “Tatizo kubwa ambalo Mahakama inakabiliana nalo ni uchakavu wa miundombinu yake, kwa hili tuko mbioni kuhakikisha Mahakama inakuwa na miundombinu bora zaidi, tumejipanga kuboresha ikiwa ni pamoja na kujenga Mahakama Kuu katika mikoa yote ambao haina majengo, taratibu zinaendelea na kwa mwaka huu tumepanga kuanza ujenzi wa Mahakama Kuu katika mikoa ya Kigoma na Musoma/Mara.

  Uboreshaji wa hali ya Wafanyakazi wa Mahakama; Hili pia ni moja kati ya eneo ambalo limepewa kipaumbele katika maboresho yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama; Mhe. Jaji Mkuu aliwaeleza Watumishi wa Mahakama Mbeya kuwa uboreshaji huu unaangalia upatikanaji wa stahili za Watumishi kwa wakati ikiwa ni pamoja na nauli za likizo, madeni mbalimbali, uboreshaji wa mishahara ya watumishi suala ambalo linaendelea kufanyiwa kazi. 

  Aidha Mhe. Jaji Mkuu aliongeza kuwa suala Maadili na nidhamu pia limewekewa kipaumbele, alisema kuwa kuna baadhi ya Watumishi wa Mahakama hawana nidhamu na maadili katika utendaji kazi, hali hii imesababisha kuwa Mahakama nzima kutupiwa lawana juu ya utendaji kazi wake. 

  “kuna baadhi ya Watumishi ya watumishi wa Mahakama hawana maadili na nidhamu hali hii inachafua taswira nzima ya Mahakama, lazima tuongeze uadilifu, Watanzania wanataka Watumishi wanaotoa haki, wanaoaminika ili kila mwananchi aridhike,” alisema.
  Naibu Msajili, Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya waliokutana na kuzungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania kuhusu utendaji kazi Mahakama kwa Kanda ya Mbeya.
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman  akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.

  0 0

  Na Magreth Kinabo- Maelezo.

   Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) umetoa ufafanuzi kuhusu  matibabu ya wagonjwa wa Selimundu(Sickle cell) ambapo umesema kwamba  hudumma hiyo haijasitishwa kama ilivyoelezwa  na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

   Ufafanuzi huo, umetolewa leo na   Mkuu wa   Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Aminiel  Eligaesha  kuupitia taarifa kwa vyombo vya habari ,ambapo amesema uongozi wa  hospitali hiyo haina mpango wa kusitisha huduma hiyo.

  “Watu wanaoeneza uvumi huo kuwa  huduma hii imesitishwa  wana maslahi yao binafsi kuhusu tiba ya wagonjwa hawa,”   alisema Eligaisha.

   Aliongeza kwamba ni kweli huduma hiyo imekuwa ikitolewa  kwa kipindi cha miaka kumi, hivyo kulikuwa na mradi uliokuwa ukifadhili matibabu  ya pamoja na utafiti wagonjwa wa Selimundu, ambao muda wake umeisha 31 Machi,  mwaka huu  kwa sababu ya utafiti ulihitaji wagonjwa wote kuja muhimbili kwa ajili ya utafiti na tiba.

   Mkuu huyo alisema  hivyo basi  hali hii ilisababisha wanaohitaji  huduma ya selimundu kufuata matibabu hospitalini hapo, licha ya kwamba  mahitahi yao hayakuhitaji wataalamu wa MNH.

  “ Tunaomba jamii ikumbuke kabla ya mradi huo, hospitali hiyo  ilikuwa inatibu wagnjwa  hao waliokuwa  wanapata rufaa, hivyo baada ya mradi huo kuisha hospitali hiyo  imewaagiza wagonjwa hao kufuata mfumo wa kawaida kama ilivyo kwa wagonjwa wengine. Hii ina maana kwamba wagonjwa hao wasiohitaji  wataalamu   wetu wattaendelea  na huduma  katika hospitali  zilizo karibu nao na watakao onwa na  Muhimbili  ni wale watakaopata rufaa kutokana na matatizo yao,” alisisitiza.

   Aidha Eligaesha  alisema wagonjwa hao  wanaohitaji huduma yao watapata huduma za matibabu kwa mujibu wa taratibu  na kanuni zilizopo bila ya ubaguzi.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Mwigulu Nchemba, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 20, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Feza  ambao Aprili 22, 2016  walikwenda Bungeni mjini Dodoma kwa ziara ya mafunzo.
   Watendaji wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasilisha bungeni  Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi  ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2016/2017.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasilisha  bungeni   Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi  ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2016/2017.

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenhye Ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) na Naibu wake, Dktt.  Abdallah Posi wakiteta bungeni mjini Dodoma Aprili 22, 2016. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Afisa Habari wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Hamis Dambaya (katikati) na  Mhadhiri Msaidizi  wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam , Egbert Mkoko kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 22, 2016. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana nchini kimepungua kwa asilimia 2.5 na kwamba Serikali itaendeleza juhudi za kuvutia uwekezaji ili kupunguza zaidi kiwango hicho.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Aprili 22, 2016) wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma.

  “Utafiti wa hali ya ajira nchini wa mwaka 2014 umeonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kimepungua kutoka asilimia 11.7 mwaka 2006 hadi asilimia 10.3 mwaka 2014. Aidha, ukosefu wa ajira  kwa vijana umepungua kutoka asilimia 14.2 mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 mwaka 2014,” amesema. 

  Waziri Mkuu amesema moja ya changamoto zinazosababisha ukosefu wa ajira ni vijana kutojengewa maarifa na ujuzi wa kuajiriwa na kuajirika. Hivyo, Serikali itaendelea kutekeleza Programu ya Miaka Mitano ya Kukuza Ujuzi Nchini (2015/2016 – 2019/2020).

  “Programu hiyo inalenga kuongeza idadi ya watu wenye kiwango cha juu cha ujuzi kutoka asilimia tatu ya sasa hadi asilimia 12 inayotakiwa kuendesha uchumi wa viwanda. Vilevile, kupunguza idadi ya watu wenye kiwango cha ujuzi wa chini kutoka asilimia 75 ya sasa hadi asilimia 54,” amesema.

  Amewaagiza watendaji wakuu wa wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, taasisi za umma, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha kuwa ukuzaji wa ajira  unakuwa ni agenda ya msingi ya kudumu katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.

  Akizungumzia kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu hususan watu wenye ualbino, Waziri Mkuu amesema Serikali inafanya jitihada kubwa kukomesha vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwakamata wote wanaojihusisha na vitendo hivyo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

  “Ukatili huo umesababisha watu wenye ualbino kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu. Hali hiyo haikubaliki na haivumiliki katika jamii ya Watanzania. Napenda kusisitiza watu wenye ulemavu wana haki ya kuthaminiwa utu wao na kulindwa dhidi ya ukatili na aina yoyote ya ubaguzi,” amesema.
  Waziri Mkuu amesema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itaviboresha Vyuo vya Ufundi na Marekebisho (Vocational and Rehabilitation Training Centres) vya watu wenye ulemavu nchini ili kutoa ujuzi unaoendana na mahitaji yao katika soko la ajira ikiwa ni pamoja na kuandaa walimu wa elimu maalum na kutoa vifaa saidizi kwa walimu na wanafunzi wenye ulemavu mashuleni.

  Akitoa maelezo kuhusu juhudi za Serikali kuwawezesha wananchi kiuchumi, Waziri Mkuu amesema Serikali imesaidia uanzishwaji wa taasisi mwavuli ya kusimamia VICOBA inayoitwa VICOBA FETA ambayo imeanza kuonyesha matunda mazuri.

  “Takwimu zilizotolewa mwezi Februari 2016 na taasisi hiyo zinaonesha kuwa kuna vikundi 100,000 vya VICOBA vyenye wanachama milioni 2.2 na mtaji wa shilingi trilioni 1.2. Ni jambo la kujivunia kwamba asilimia 79 ya wanachama wa VICOBA ni wanawake,” amesema.

  Amezitaka Halmashauri zote nchini ziweke orodha sahihi ya vyama vya ushirika wa kuweka na kukopa vilivyosajiliwa kwa kila kijiji na kuchukua hatua za kuwezesha uanzishaji na usajili wa SACCOs zinazokidhi vigezo kulingana na shughuli za uzalishaji katika Halmashauri husika.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  IJUMAA, APRILI 22, 2016.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana nchini kimepungua kwa asilimia 2.5 na kwamba Serikali itaendeleza juhudi za kuvutia uwekezaji ili kupunguza zaidi kiwango hicho.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Aprili 22, 2016) wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapatona matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma.

  “Utafiti wa hali ya ajira nchini wa mwaka 2014 umeonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kimepungua kutoka asilimia 11.7 mwaka 2006 hadi asilimia 10.3 mwaka 2014. Aidha, ukosefu wa ajira  kwa vijana umepungua kutoka asilimia 14.2 mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 mwaka 2014,” amesema. 

  Waziri Mkuu amesema moja ya changamoto zinazosababisha ukosefu wa ajira ni vijana kutojengewa maarifa na ujuzi wa kuajiriwa na kuajirika. Hivyo, Serikali itaendelea kutekeleza Programu ya Miaka Mitano ya Kukuza Ujuzi Nchini (2015/2016 – 2019/2020).

  “Programu hiyo inalenga kuongeza idadi ya watu wenye kiwango cha juu cha ujuzi kutoka asilimia tatu ya sasa hadi asilimia 12 inayotakiwa kuendesha uchumi wa viwanda. Vilevile, kupunguza idadi ya watu wenye kiwango cha ujuzi wa chini kutoka asilimia 75 ya sasa hadi asilimia 54,” amesema.

  Amewaagiza watendaji wakuu wa wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, taasisi za umma, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha kuwa ukuzaji wa ajira  unakuwa ni agenda ya msingi ya kudumu katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.

  Akizungumzia kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu hususan watu wenye ualbino, Waziri Mkuu amesema Serikali inafanya jitihada kubwa kukomesha vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwakamata wote wanaojihusisha na vitendo hivyo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

  “Ukatili huo umesababisha watu wenye ualbino kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu. Hali hiyo haikubaliki na haivumiliki katika jamii ya Watanzania. Napenda kusisitiza watu wenye ulemavu wana haki ya kuthaminiwa utu wao na kulindwa dhidi ya ukatili na aina yoyote ya ubaguzi,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itaviboresha Vyuo vya Ufundi na Marekebisho (Vocational and Rehabilitation Training Centres) vya watu wenye ulemavu nchini ili kutoa ujuzi unaoendana na mahitaji yao katika soko la ajira ikiwa ni pamoja na kuandaa walimu wa elimu maalum na kutoa vifaa saidizi kwa walimu na wanafunzi wenye ulemavu mashuleni.

  Akitoa maelezo kuhusu juhudi za Serikali kuwawezesha wananchi kiuchumi, Waziri Mkuu amesema Serikali imesaidia uanzishwaji wa taasisi mwavuli ya kusimamia VICOBA inayoitwa VICOBA FETA ambayo imeanza kuonyesha matunda mazuri.

  “Takwimu zilizotolewa mwezi Februari 2016 na taasisi hiyo zinaonesha kuwa kuna vikundi 100,000 vya VICOBA vyenye wanachama milioni 2.2 na mtaji wa shilingi trilioni 1.2. Ni jambo la kujivunia kwamba asilimia 79 ya wanachama wa VICOBA ni wanawake,” amesema.

  Amezitaka Halmashauri zote nchini ziweke orodha sahihi ya vyama vya ushirika wa kuweka na kukopa vilivyosajiliwa kwa kila kijiji na kuchukua hatua za kuwezesha uanzishaji na usajili wa SACCOs zinazokidhi vigezo kulingana na shughuli za uzalishaji katika Halmashauri husika.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  IJUMAA, APRILI 22, 2016.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake nchini Francisco Montecillo
   ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Vatican hapa nchini anayemaliza muda wake Francisco Montecillo  Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Balozi wa Algeria hapa nchini Belabed Saada akikabidhi ujumbe uliotoka kwa Rais wa Algeria kuja kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.


    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Canada hapa nchini Alexandre Leveque Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi huyo wa Canada alifika Ikulu na ujumbe wake  kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Balozi wa Canada hapa nchini Alexandre Leveque wapili kutoka kulia pamoja na waakilishi wengine wa Serikali pamoja na Ubalozi wa Canada.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana na Balozi wa Canada hapa nchini Alexandre Leveque mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  PICHA NA IKULU

  0 0

   Muogeleaji nyota wa kiume wa Tanzania, Hilal Hilal (wa kwanza kulia) akiwa kwenye jukwaa mara baada ya kupokea medali yake ya Shaba katika mashindano ya Kanda ya Nne ya Cana. 
  Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kinanchoshiriki katika mashindano ya Cana Kanda  ya nne. kutoka kulia ni Amani Doggart, Catherine Mason, Hilal Hilal na Smriti Gokarn.

  Na Mwandishi wetu
  Muogeleaji wa Tanzania, Hilal Hilal ametwaa medali ya Shaba katika mashindano ya kuogea ya Cana Kanda ya Nne yanayoendelea nchini Mauritius.

  Hilal ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa katika mchezo huo, amemaliza katika nafasi ya tatu katika staili ya butterfly kwa kutumia muda wa sekunde 26.70 katika mashindano hayo magumu yaliyoshirikisha nchi za Uganda, Kenya, Rwanda Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Somalia, Sudani Kusini na Sudan.

  0 0

  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa Korea Kusini nchini Song Geum aliyemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Balozi wa Korea Kusini nchini Song Geum akimuonesha jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisikiliza kwa makini Balozi wa Korea Kusini nchini Song Geum aliyemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma. Kulia ni Mke wa Balozi huyo.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Chirau Ali aliyemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza kwa makini Balozi wa Kenya nchini Chirau Ali aliyemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (mwenye tai nyekundu katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa shule ya msingi Feza iliyopo Dar es Salaaam. Wanafunzi hao walikuja kutembelea Bunge.(Picha na Ofisi ya Bunge)

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasilisha bungeni Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2016/2017.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenhye Ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) na Naibu wake, Dktt. Abdallah Posi wakiteta bungeni mjini Dodoma Aprili 22, 2016.
  Watendaji wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasilisha bungeni Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2016/2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Mwigulu Nchemba, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 20, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Fedha ambao Aprili 22, 2016 walikwenda Bungeni mjini Dodoma kwa ziara ya mafunzo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Afisa Habari wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Hamis Dambaya (katikati) na Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam , Egbert Mkoko kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana nchini kimepungua kwa asilimia 2.5 na kwamba Serikali itaendeleza juhudi za kuvutia uwekezaji ili kupunguza zaidi kiwango hicho.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Aprili 22, 2016) wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma.

  “Utafiti wa hali ya ajira nchini wa mwaka 2014 umeonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kimepungua kutoka asilimia 11.7 mwaka 2006 hadi asilimia 10.3 mwaka 2014. Aidha, ukosefu wa ajira kwa vijana umepungua kutoka asilimia 14.2 mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 mwaka 2014,” amesema. 

  Waziri Mkuu amesema moja ya changamoto zinazosababisha ukosefu wa ajira ni vijana kutojengewa maarifa na ujuzi wa kuajiriwa na kuajirika. Hivyo, Serikali itaendelea kutekeleza Programu ya Miaka Mitano ya Kukuza Ujuzi Nchini (2015/2016 – 2019/2020).

  “Programu hiyo inalenga kuongeza idadi ya watu wenye kiwango cha juu cha ujuzi kutoka asilimia tatu ya sasa hadi asilimia 12 inayotakiwa kuendesha uchumi wa viwanda. Vilevile, kupunguza idadi ya watu wenye kiwango cha ujuzi wa chini kutoka asilimia 75 ya sasa hadi asilimia 54,” amesema.

  Amewaagiza watendaji wakuu wa wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, taasisi za umma, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha kuwa ukuzaji wa ajira unakuwa ni agenda ya msingi ya kudumu katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.

  Akizungumzia kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu hususan watu wenye ualbino, Waziri Mkuu amesema Serikali inafanya jitihada kubwa kukomesha vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwakamata wote wanaojihusisha na vitendo hivyo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

  “Ukatili huo umesababisha watu wenye ualbino kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu. Hali hiyo haikubaliki na haivumiliki katika jamii ya Watanzania. Napenda kusisitiza watu wenye ulemavu wana haki ya kuthaminiwa utu wao na kulindwa dhidi ya ukatili na aina yoyote ya ubaguzi,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itaviboresha Vyuo vya Ufundi na Marekebisho (Vocational and Rehabilitation Training Centres) vya watu wenye ulemavu nchini ili kutoa ujuzi unaoendana na mahitaji yao katika soko la ajira ikiwa ni pamoja na kuandaa walimu wa elimu maalum na kutoa vifaa saidizi kwa walimu na wanafunzi wenye ulemavu mashuleni.

  Akitoa maelezo kuhusu juhudi za Serikali kuwawezesha wananchi kiuchumi, Waziri Mkuu amesema Serikali imesaidia uanzishwaji wa taasisi mwavuli ya kusimamia VICOBA inayoitwa VICOBA FETA ambayo imeanza kuonyesha matunda mazuri.

  “Takwimu zilizotolewa mwezi Februari 2016 na taasisi hiyo zinaonesha kuwa kuna vikundi 100,000 vya VICOBA vyenye wanachama milioni 2.2 na mtaji wa shilingi trilioni 1.2. Ni jambo la kujivunia kwamba asilimia 79 ya wanachama wa VICOBA ni wanawake,” amesema.

  Amezitaka Halmashauri zote nchini ziweke orodha sahihi ya vyama vya ushirika wa kuweka na kukopa vilivyosajiliwa kwa kila kijiji na kuchukua hatua za kuwezesha uanzishaji na usajili wa SACCOs zinazokidhi vigezo kulingana na shughuli za uzalishaji katika Halmashauri husika.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  L. P. 980,
  DODOMA.
  IJUMAA, APRILI 22, 2016.

  0 0

  Mkuu wa shule ya Bwawani Sekondari, ACP. Emmanuel Lwinga akitoa maelezo mafupi ya maendeleo ya shule kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kutoa hotuba yake.Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga akiwasalimu wahitimu na wazazi kabla ya kutoa hotuba fupi kwa wahitimu wa kidato cha sita Bwawani Sekondari(hawapo pichani).
  Mgeni rasmi Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga akitoa cheti kwa mwanafunzi mhitimu wa kidato cha sita katika mahafali ya kwanza ya kidato cha sita Bwawani Sekondari, yaliyofanyika leo Aprili 22, 2016.
  Wanafunzi wahitimu wa Kidato cha sita Bwawani Sekondari wakiimba wimbo wa shule kwenye mahafali hayo yaliyofanyika leo Aprili 22, 2016, Mkoani Pwani.
  Wazazi wa wahitimu wa kidato cha sita shule ya Bwawani Sekondari wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi.
  Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika shule ya Bwawani Sekondari ukiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi kama inavyoonekana katika picha.
  Mgeni rasmi Kamishna wa Sheria na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wahitimu kidato cha sita Bwawani Sekondari(waliosimama mstari wa nyuma)mahafali hayo yamefanyika leo Aprili 22, 2016(Picha zote na lucas mboje wa Jeshi la Magereza).

  Na Lucas Mboje, Pwani.

  WAHITIMU wa Kidato cha sita nchini wameaswa kuwa waadilifu na wazalendo ili hatimaye taifa liweze kupata viongozi bora na raia wema katika jamii.

  Rai hiyo imetolewa na Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza Gaston Sanga akiongea kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini katika mahafali ya kwanza ya Kidato cha sita ya Shule ya Bwawani Sekondari iliyopo Mkoani Pwani.

  “Nadhani wote ni mashahidi kwa namna Serikali ya Awamu ya Tano inavyowahudumia wananchi kwa kasi na kiwango cha kuridhisha. Hivyo mkipata kazi nawasihi mkawajibike kwa kasi, uadilifu na mkawe wazalendo kwa taifa”. Alisema Kamishna Sanga.

  Kamishna Sanga ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wameunga mkono kwa vitendo juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

  Aidha, Afande Sanga ameahidi kuwa Uongozi wa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Bodi ya shule hiyo utaendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazozikabili shule hiyo kadri uwezo wa kifedha unavyopatikana.

  Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Bwawani, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga alipokuwa akitoa taarifa fupi kwa mgeni rasmi katika mahafali hayo amesema kuwa shule yake ni miongoni mwa shule bora nchini ambazo zinafanya vizuri kitaaluma na masuala mengineyo yasiyoyakitaaluma.

  Aliongeza kuwa katika mitihani mbalimbali waliyofanya wanafunzi hao wa kidato cha sita wamekuwa na matokeo mazuri kutokana na mazingira mazuri ya kujisomea, ushirikiano mzuri wa walimu pamoja na kuimarishwa kwa miundombinu muhimu ya kujifunzia.

  “Afande mgeni rasmi wanafunzi wahitimu 13 wa leo tuna hakika kuwa watatuletea matunda mazuri kutokana na mwelekeo waliouonesha katika mitihani ya ndani na nje ya shule waliyoifanya”. Alisema Mkuu wa Shule Lwinga.

  Shule ya Sekondari Bwawani inamilikiwa na Jeshi la Magereza, ilianzishwa Mwaka 1978 kwa lengo la kutoa elimu ya Sekondari kwa Watumishi wa Magereza ambapo hivi sasa shule hiyo inatoa elimu kwa vijana wa kike na kiume kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini kuanzia kidato cha kwanza hadi cha Sita.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema ambaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa Michuano ya Shule za Sekondari Nchini (UMESETA), akipiga dana dana wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam leo.
  Wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye uzinduzi huo.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto), akikabidhi vifaa vya michezo kwa Shule ya Sekondari ya Azania vilivyotolewa na Kampuni ya Coca Cola. Kulia Ofisa kutoka kampuni ya Coca Cola wadhamini wakubwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2016.
  DC Mjema akisalimiana na mwamuzi wa mchezo kati ya timu ya Sekondari ya Tirav ya Yombo na Makongo uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Makongo ilishinda mabao 2-1.
  DC Mjema akiwasalimia wachezaji wa timu ya Tirav.
  DC Mjema akisalimiana na wachezaji wa timu ya Makongo Sekondari.
  Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema (kulia), akitoa nasaha zake kwa wachezaji hao kabla ya kuanza kucheza.
  DC Mjema hapa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya sekondari ya Tirav na viongozi mbalimbali.
  DC Mjema hapa akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya sekondari ya Makongo na viongozi mbalimbali.
  Hapa akiwa katika picha ya pamoja na waamuzi wa mchezo huo na viongozi mbalimbali.
  Hapa mtanange ukiendelea.
  Golikipa wa timu ya Tirav, Abdul Badi akiokoa moja ya hatari katika lango lake.
  Wachezaji wa timu ya Makongo wakishangilia baada ya kupata bao lao la kwanza.  Na Dotto Mwaibale

  MKUU wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema amezindua michuano ya Shule za Sekondari Nchini (UMESETA) katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku akisisitiza kuwa yataendelea kuwaibua wachezaji wengi chipukizi.

  Akizungumza katika uzinduzi huo Mjema aliishukuru kampuni ya Cocacola kwa kudhamini mashindano hayo huku akiyaomba makampuni na wadau wengine kujitokeza kudhamini michezo mbalimbali.

  Mashindano hayo yatashirikisha timu zaidi ya 40 katika mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana wa Shule za Sekondari kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini huku ikishirikiana na waandaaji wa michuano ya michezo ya Shule za Sekondari UMISETA katika kuhakikisha wanapata wachezaji wenye elimu kutoka mikoa yote hapa nchini.

  Akizungumzia mashindano hayo Meneja wa Biashara wa Coca Cola Maurice Njowoka alisema wameamua kuongeza mchezo ili kupanua wigo wa mashindano hayo hapa nchini.Aidha alisema lengo la kuungana na waandaaji hao, badala ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) pekee ni kutaka kupata wachezaji sahihi, kutoka mikoa yote, na ambao wako katika mashule ya Sekondari.

  "Hii itatusaidia kupata wachezaji sahihi wenye elimu na ambao kweli wanasoma shule za sekondari,"alisema Njowoka.Alisema tofauti na mwaka jana, tuliwatumia TFF pekee jambo ambalo tulipata wachezaji lakini katika mazingira magumu zaidi.

  Alisema michuano ya mwaka huu wanaimani watapata wachezaji kiurahisi kwa sababu UMISETA ina rekodi ya wanafuzni wanaosoma katika shule za sekondari.Njowoka alisema kwa kuanzia jijini Dar es Salaam, wametoa jezi na vifaa kwa shule za Sekondari zilizohudhuria katika mashindano hayo.

  Alisema baada ya Dar es Salaam, wanaelekea Mwanza, Mbeya, Arusha na Moshi kwa ajili ya kuzindua rasmi michezo hiyo ambayo shule zinaanza kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa.Alisema katika udhamini wao watatumia kinywaji cha Coca Cola kwa upande wa soka, wakati Kikapu watatumia Sprite, lengo ni kufanikisha michuano hiyo safari hii kutokana na kuongeza idadi ya mchezo.

  0 0

   Wabunge wa bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania, na wafanyakazi wa Clouds Media Group, akiwemo mchekeshaji maarufu Bishanga Bashaija, wakiwa kwenye moja ya studio za Clouds Media Group, wakati wa kipindi maarufu cha Leo Tena, Aprili 22, 2016.

  NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

  WABUNGE wa bunge la Afrika Mashariki (EALA), kutoka Tanzania, wametembelea Clouds Media Group,Mikocheni jijini Dar es Salaam  Aprili 22, 2016  ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya takriban siku 20 kutembelea vyombo vya habari kwa nia ya kuvishirikisha vyombo hivyo kutoa elimu kwa wananchi kuchangamkia fursa zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.


  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, inayomiliki kituo cha radio, Clouds FM, Clouds TV, Bw. Ruge Mutahaba, amewaeleza wabunge hao walioongozwa na mwenyekiti wao Mh. Chrles Makongoro Nyerere kuwa, Tanzania inakabiliwa na tatizo kubwa la kutogeuza vipaji kuwa biashara na hivyo kujiingizia kipato.


  Ruge amewahimiza wabunge hao kushawishi serikali ya Tanzania kurekebisha sera zake za kuwawezesha wananchi na kuwajengea uwezo wa kuvitumia vipaji walivyojaaliwa na Mwenyezimungu ili kujiingizia kipato.


  Akielezea nia ya ziara hiyo, Mwenyekii Mh. Makongoro Nyerere alisema, wabunge kutoka nchi wanachama walipewa jukumu la kuwatembelea wananchi wa nchi watokako ili kwahimiza kuchangamkia fursa zilizopo kwenye Jumuiya hiyo ambayo kwa sasa ina jumla ya wanachama sita, Tanzania, Kenya Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.


  “Jumuiya ya Afrika Mashariki ina soko la kutosha na wananchi wa Jumuiya hii wanyo fursa ya kwenda kufanya shughuli za kiuchumi bila kizuizi chochote ikiwemo biashara na kufanya kazi hivyo ni wakati wa watanzania kuacha kulalamika na kuchangamkia fursa hiyo.” Alisema Mh. Makongoro.


  Pamoja na Mh. Makongoro, wabunge wengine ni pamoja na Mh. Shy-Rose Bhanji, na Mh. Nderaikindo Kessy.

  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Bw. Ruge Mutahaba, (kulia), akitoa maelezo ya uendeshaji wa kampuni hiyo, wakati wabunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA-Tanzania), walipotembelea studio za Clouds radio/TV Mikocheni jijini Dar es Salaam Aprili 22, 2016. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa wabunge hao Mh. Charles Makongoro Nyerere, Mh. Nderaikindo Kessy, na Mh. Shy-Rose Bhanji.
  Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena, Gea Habib
   Mwenyekiti Mh. Charles Makongozo Nyerere (kulia) akizungumza kwenye kipindi cha Leo tena
   Mh. Shy-Rose Bhanji mkutanoni
   Mh. Nderaikindo Kessy akiwa mkutanoni
   Mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena Husna Abdul  "DAHUU"
   Mchekeshaji maarufu Bishanga Bashaija, (kulia), akiwa katika kipindi cha Leo Tena aprili 22, 2016

   Dahuu
  Bi. Gea
   Mwenyekiti Mh. Charles Mkongoro Nyerere akizungumza kwenye kikao cha kubadilishana mawazo na uongozi wa Clouds Media Group
   Mh. Shy-Rose Bhanji, akizungumza kwenye kikao hicho
   Mwenyekiti akizungumza na uongozi wa Clouds Media Group, chini ya Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji, Bw. Ruge Mutahaba, (watatu kulia), Mkurugenzi wa Biashara na Maendeleo, wa Clouds Media Group, Bi. Sheba Kusaga, na Afisa Uhusiano wa Clouds Media Group, Bw. Simon Simalenga  0 0

  IMG_0724

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (pichani) amewasimamisha kazi kupisha uchunguzi kwa watendaji Wakuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ubadhirifu wa fedha za mfuko huo kwa Mkoa wa Mara.
  New Doc 1_1 (1)New Doc 1_2

  0 0  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Maxmalipo Juma Rajabu akifafanua jambo kwa wakurungezi wa serikali za mitaa kutoka Uganda , Kulia ni Mkuu wa Uendeshaji Kanda Group COO – Maxcom Africa Jamson Kassati , Kushoto Mwanzo Mr. Moses Kimaro Kutoka ALAT (jumuiya ya serikali za MItaa Tanzania) na pembeni yake katikati ni Mwenyekiti wa wakurugenzi wa Serikali za Mitaa Kutoka Uganda Dunstan Balaba ambapo Jumuiya hiyo ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda leo wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi Gani kampuni hii imeweza kugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji na majiji Nchini Tanzania. 
  Mkuu wa Kitengo cha Biashara Kutoka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari Akifafanua Jambo kwa Wakurugenzi hawa kutoka Uganda, Akielezea Jinsi mfumo wa Ukusanyaji Kodi na tozo mbalimbali ulivyorahisisha upatikanaji wa mapato katika halmashauri mbalimbali na Taasisi za Serikali kwa Ujumla na kuzuia mianya ya upoteaji wa mapato katika vyanzo mbalimbali vya halmashauri. 
  Mwenyekiti na Msemaji wa Umoja wa wakurugenzi kutoka Uganda Bwana Dunstan Balaba Akieleza Jambo kwa Hadhara na Kukiri kushangazwa na watanzania Kuweza Kugundua Teknolojia kama hii. Pia Kumwomba Mkurugenzi wa Maxmalipo Afungue Ofisi Uganda Mapema iwezekanavyo. 
  Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa Kutoka UGANDA wakifuatilia Mada Kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Kampuni ya Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Maxmalipo Juma Rajabu anasema; Safari ya kuuaminisha Umma na Serikali kwamba wazawa wanaweza kubuni mbinu mbalimbali za kusaidia kuboresha makusanyo, inaenda sambamba na ufanisi mzuri uliothibitika katika kazi mbalimbali ambazo kampuni Imekua ikizifanya, Juma Rajabu ameongeza kwa kuelezea jinsi ambavyo teknolojia imerahisisha ulipajji wa bili mbalimbali Ikiwamo Luku, Kodi za TRA, Ving’amuzi na hata ukusanyaji wa mapato kwenye vivuko. 
  Mmoja Wa wakurugenzi kutoka Uganda Bibi Lilian Akiuliza Swali kwa Maxmalipo wakati Jumuiya hiyo ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda leo wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi Gani kampuni hii Imeweza kuugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji na majiji Nchini Tanzania. 
  Jumuiya ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya MAXCOM Africa mapema leo walipokuwa wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi Gani kampuni hii Imeweza kugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji na majiji Nchini Tanzania. 

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti B. Sillo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)juu ya vipodozi vyenye madhara kwa watumiaji na ambavyo vimeshapigwa marufuku na Serikali, jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti B. Sillo akitowa maelekezo kwa maofisa wa (TFDA.
  Mafundi wa (TFDA) wakiendelea na kazi.
  Afisa wa (TFDA) akiwa amebeba kiroba chenye vipodozi vyenye madhara kwa watumiaji na ambavyo vimeshapigwa marufuku na Serikali, jijini Dar es Salaam.
  Maofisa wa (TFDA) wakipakia kwenye gari vipodozi vyenye madhara kwa watumiaji na ambavyo vimeshapigwa marufuku na Serikali, jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais na Jeshi la Polisi, imefanyaukaguzi maalum na kufanikiwa kukamata shehena kubwa ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na Serikali katika baadhi ya majengo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na thamani yake haijajulikana mara moja haditathmini ikakapokamilika.

  Akiongea na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti B. Sillo ambaye alikuwa nimiongoni mwa washiriki wa zoezi hilo kwa masikitiko makubwa, alisema “ Kiasi cha vipodozi hivihatarishi vyenye madhara kwa watumiaji na ambavyo vimeshapigwa marufuku na Serikali, ni kikubwakatika historia ya ukaguzi hapa nchini na wafanyabiashara wote wanaohusika na biashara hii haramu ni lazima wachukuliwe hatua stahiki za kisheria”.

  Mkurugenzi Mkuu huyo, aliendelea kusema kwamba kwa vile vipodozi hivi huingizwa kwa njia yamagendo, ukaguzi huo ni endelevu na wahusika hawataweza kukwepa mkono mrefu wa Serikali mahalipopote na wakati wowote.

  Alitoa rai kwa wafanyabiashara kuacha mara moja kuvunja Sheria za nchi na wasalimishe kwa hiyari yao vipodozi vyote vilivyopigwa marufuku TFFDA badala ya kusubiri Taasisi hiyo iwafuate.Katika hatuanyingine, Mkurugenzi Mkuu huyo aliwaasa wananchi kufanya maamuzi sahihi ya kutumia vipodozisalama vilivyosajiliwa na Mamlaka na kuachana na vile vilivyopigwa marufuku ili kulinda afya zao.Zoezihili limefanyika kuanzia tarehe 21/4/2016 na haikuelezwa mara moja kwamba litaisha lini

  0 0


older | 1 | .... | 825 | 826 | (Page 827) | 828 | 829 | .... | 1897 | newer