Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

Rais kumwapisha Balozi Mteule Mheshimiwa Chikawe kesho asubuhi

$
0
0


Itakumbukwa kuwa leo asubuhi tarehe 18 Aprili, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.


Tunapenda kuwataarifu kuwa Balozi Mteule Mathias Meinrad Chikawe ataapishwa kesho tarehe 19 Aprili, 2016 saa 3:00 Asubuhi, Ikulu Jijini Dar es salaam.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam


18 Aprili, 2016


UFAFANUZI JUU YA UVUMI KUHUSU HALI YA MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA JAMII (NSSF)

$
0
0
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zisizo rasmi kuhusu hali na mwenendo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Baadhi ya taarifa hizo zimekuwa zikieleza kwamba mali za Mfuko huo zimetumiwa vibaya na hivyo kuathiri mafao kwa wanachama.

Taarifa hizi zimesababisha hofu na taharuki miongoni mwa wanachama wa NSSF na wadau wa Sekta ya Hifadhi ya jamii kwa ujumla kwa kuhofia usalama wa wa fedha na mafao yao.

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) inapenda kuwaondoa hofu wanachama wote wa Mfuko wa NSSF na Wananchi kwa ujumla na kuwahakikishi kwamba Mfuko wa NSSF upo katika hali nzuri kifedha na unaendelea kulipa mafao ya wanachama kama kawaida.

Kama mnavyofahamu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko alikwishateuliwa na anaendelea na majukumu ya kusimamia shughuli zote za Mfuko.

Vilevile, taratibu za kupata Bodi mpya ya Wadhamini ya Mfuko huo zipo katika hatua za mwisho.

Aidha, SSRA kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania kwa mamlaka waliyopewa chini ya Kifungu cha 6(2) (c) cha Sheria Na.8 ya mwaka 2008 ikisomwa pamoja na kifungu cha 40 na cha 48 wanaendelea kufanya kaguzi za Mifuko yote ukiwemo Mfuko wa NSSF kwa lengo la kuhakikisha kwamba muda wote Mifuko yote inakuwa katika hali nzuri kwa maslahi ya wanachama na taifa kwa ujumla.

Mwisho, Mamlaka inapenda kuwaondoa wasiwasi wanachama walioathirika na taarifa hizi pamoja na wanachama wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuwahakikishia kwamba fedha na mafao yao yapo salama na Mamlaka inazifanyia kazi kero zao kwa bidii kubwa.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz
Dar es Salaam

MKUU WA MKOA WA MWANZA AAGIZA ALIYEDHULUMIWA KIWANJA AREJESHEWE

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ameuagiza uongozi wa Jiji la Mwanza kuhakikisha linakabidhi kiwanja namba 28-A kilichopo katika eneo la Bugando ifikapo Aprili 25, 2016 kwa mmiliki halali wa kiwanja hicho bwana Justine Eminoga ambacho amekuwa akikidai kutoka kwa mfanyabiashara wa Jijini humo kwa zaidi ya miaka sita sasa.

Mongella amefikia hatua hiyo mara baada yakupokea malalamiko kutoka kwa bwana Justine ambaye alifika katika Jiji la Mwanza kwa ajili kufatilia suala lake ambalo limedumu kwa zaidi ya miaka sita sasa. Akitoa malalamiko yake mbele ya mkuu huyo wa mkoa, bwana Justine alidai kuzulumiwa kiwanja hicho na mfanyabiashara aliye mtaja kwa jina Shanif Mansour ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwimba.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ametoa siku saba kwa halmashauri za mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanakamilisha zoezi la kuhakiki watumishi, ili kubaini endapo kuna watumishi hewa waliosalia katika zoezi la awali, zoezi la sasa ambalo linasimamiwa na Ofisi ya katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza kwa kamati maalumu zilizo undwa na mkuu wa Mkoa huo, 

Akiwa katika ziara hiyo mkuu huyo wa mkoa aliagiza kukamatwa kwa Afisa Utumishi msaidizi wa jiji la Mwanza Henry Sedetale, ambaye alisaidia watumishi hewa watano kuchukua mikopo ya zaidi ya Mil.90 kutoka katika benki tofauti tofauti, hata hivyo taarifa kutoka Taasisi yakupambana na kuzuia rushwa mkoani Mwanza iliyotolewa wakati wa kikao hicho na mkuu wa Takukuru mkoani humo, ilisema mtuhumiwa huyo tayari alikuwa ametiwa nguvuni na taasisi hiyo kwa mahojiano zaidi.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza yupo katika ziara kujitambulisha katika mkoa huo na hii ikiwa ni Wilaya yake ya tatu mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi na Magu hapo awali.

Imetolewa na
Atley J. Kuni
AFISA HABARI NA MAHUSIANO –RS MWANZA. 18 Aprili, 2016

DARAJA LA KIGAMBONI, WATANZANIA WAFARIJIKA, MAMIA WAENDA KULISHANGAA NA KUPIGA SELFIE

$
0
0
 Daraja la kiasa la Kigamboni linalounganisha eneo la Kigambonina upande wa Kurasini likikatisha bahari ya Hindi. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kulizindua rasmi daraja hilo Jumanne Aprili 19, 2016. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)


NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, Kurasini
ZAMANI kwa mgeni aingiae jiji la Dar es Salaam, ataambiwa “Kashangae Ferry” lakini mgeni atakayeingia leo jijini, ataambiwa Kashangae Kurasini-daraja la Kigamboni.

Hiyo ndiyo hali halisi ilivyokwa sasa ambapo mamia ya wakazi wa jiji wamekuwa wakienda kwenye Daraja la kisasa la Kigamboni mosi kushangaa maajabu ya daraja lenyewe ambalo ni refu kuliko madaraja yote hapa nchini pengine Afrika Mashariki, lakini pili kupiga picha za kisasa “Selfie”.

Daraja hilo lenye urefu wa mita 680 likiunganisha eneo la Kigamboni na Kurasini wilayani temeke jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa za wakandarasi wa mradi huo, Daraja hilo litakuwa na barabara sita, tatu kila upande, na pia njia za waenda kwa miguu (Pedestrians).

Hali pametengwa milango kwa ajili ya matumizi ya magari aina tofauti.
Geti namba 1 ni kwa wale wenye vibali maalum, geti namba 2 geti namba 3 na geti namba 4 ni wenye magari madogo binafsi, geti namba 5 ni mini bus (daladala) na Geti namba 6 nimaalum kwa malori.Daraja hilo ambalo ujenzi wake umeanza Februari 1, 2012 ni mradi wa ubia kati ya Serikali yenye asilimia 40 naMfuko wa Hifadhi ya Jamii, NSSF yenye asilimia 60.

Daraja hilolinaongeza vivutio vikuu viwili ambavyo wilayaya Temeke jijini Dar es Salaam inavyo, daraja lenyewe la Kigamboni lakini pia uwanja wa kisasa wa taifa.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kulizindua rasmi daraja hilo umanne Aprili 19, 2016 na tayari maandalizi ya hafla hiyo yanaendelea ambapo K-VIAS MEDIA, imezuru eneo hilo leo Aprili 18, 2016 na kujionea wajkandarasi namaafisa wa serikali wakiweka mambo sawa tayari kwa shughuli hiyo muhimu katika historia ya nchi hii.

Lakini pia ukitaka kuona mfano wa “Flyover” basi pitia hapo Kurasini uone jinsi barabar zilivyobebana kuelekea eneo la daraja na zile zinazoungana na barabara ya Mandela.

 Akina mama hawa na watoto wao walikuwa ni miongoni mwa wakazi wa jiji la Dar es Salaamwanaofika kulishangaa daraja hilo la kisasa
Barabara inayoelekea kwenye daraja hilo

SYMBION POWER-TANZANIA REACTS OVER DUBAI BASED FIRM, RENTAL SERVICES AND SOLUTION ON TAX CLAIMED

$
0
0
 Paul Hinks, President Symbion Power Limited
K-VIS MEDIA/Reporter

Symbion Power, today brushed off what it described as fraudulent and grossly exaggerated claims by a Dubai based firm, Rental Services and Solutions and it’s associated sub suppliers.

Speaking from Washington DC, Symbion Senior Vice President of Communications and Public Affairs Adi Raval said “  This is actually a tax matter. This company and it’s sub suppliers were working as a subcontractor to Symbion for 3 years from 2011 to 2014. During that time none of them paid the Tanzania government a single dollar of tax,  as they are required to by law”.

He continued “ This company maintained a presence in Tanzania and they had expatriate and local staff based in Arusha, Dodoma and Dar es Salaam.  The law requires that they pay taxes and they have not done that. We have withheld tax from payments to them and we have paid that money to the Tanzania Revenue Authority. When they produce a certificate that shows they have paid their taxes to the TRA we will release further payment to them”.

RAIS DKT MAGUFULI AMTEUA HAMPHREY POLEPOLE KUWA MKUU WA WILAYA YA MUSOMA

$
0
0
Hamphrey Polepole 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Hamphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara.

Bw. Hamphrey Polepole anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Musoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (Mstaafu) Zelothe Steven ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Uteuzi wa Bw. Hamphrey Polepole umeanza leo tarehe 18 Aprili, 2016

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
18 Aprili, 2016

VICHAKA HATARISHI KATIKA KITUO CHA AFYA BUZURUGA JIJINI MWANZA VYAFYEKWA.

$
0
0
Hali ya Usalama katika Kituo cha Afya cha Kata ya Buzuruga kilichopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza imeimarika, baada ya Wakazi wa Kata hiyo wanaounda Kikundi cha Kijamii cha “Ulipo Tupo” kufyeka vichaka vilivyokuwa katika kituo hicho ambavyo vilikuwa vikitumiwa na wahalifu kama maficho yao.

Baada ya kufyeka vichaka hivyo jumamosi iliyopita, Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Ndaisaba Aron alisema kuwa vichaka hivyo vilikuwa hatarishi kwa wananchi, wagonjwa pamoja na wahudumu wa Afya katika Kituo hicho, kutokana na kupata malalamiko kwamba vibaka walikuwa wakikimbilia katika vichaka hivyo baada ya kufanya uhalifu.

Hidaya Bashiru ambae ni mwanachama wa kikundi hicho pamoja na Sixtus Ijugo ambae ni Katibu, waliwasihi wananchi wengine kuwa na desturi ya kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo katika maeneo mbalimbali kama hospitali, shule na kwingineko kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe.

Diwani wa Kata ya Buzuruga, Richard Machemba, alijumuika na Kikundi hicho kwa ajili ya kufanya usafi katika Kituo hicho ambapo alipongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na wakazi pamoja na vikundi mbalimbali vya maendeleo katika Kata yake ambapo amewasihi wananchi kuendelea kujitoa kwa ajili ya kushiriki shughuli za maendeleo.

Sikiliza Sauti HAPA Au Bonyeza Play Hapa Chini

Tazama Picha HAPA

MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA IRINGA RITHA KABATI AAPISHWA HII LEO BUNGENI NA KUWA MBUNGE KAMILI.

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mch Petter Msigwa akimpongeza mbunge wa viti maalum Ritha Kabati mara baada ya kuapishwa sambamba na watu wengi walimpongeza mbunge huyo kama wanavyoonekana kwenye picha.
Mbunge wa jimbo la iringa mjini mch Petter Msigwa na mbunge wa jimbo la kilolo mkoani iringa Vennance Mwamoto wakimpongeza mbunge wa viti maalum Ritha Kabati mara baada ya kuapishwa.
watu mbalimbali walijitokeza kumpongeza mbunge rita kabati mara baada ya kuapishwa hii leo.
Mbunge wa jimbo la iringa mjini mch Petter Msigwa na mbunge wa jimbo la kilolo mkoani iringa Vennance Mwamoto wakimpongeza mbunge wa viti maalum rita kabati mara baada ya kuapishwa.


Na fredy mgunda iringa. 

mbunge wa viti maalumu mkoa wa iringa Ritha Kabati ameapishwa leo kuwa mbunge kamili hii imekutaja mara Baada ya kukamilika kwa Uchaguzi wa Majimbo hayo nane (8), Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF) ndivyo vilivyoendelea kupata angalau asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Ubunge, kwa maana hiyo, vyama hivyo ndivyo vitaendelea kuhusishwa kwenye Mchakato wa kugawanywa hivyo Viti 3 vilivyobaki.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliwatangaza ndugu Ritha Enespher Kabati na ndugu Oliver Daniel Semuguruka wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na ndugu .Lucy Fidelis Owenya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa Wabunge Wanawake wa viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ikumbukwe kuwa Tume katika Kikao chake cha tarehe 11/11/2015 ilifanya Uteuzi wa Wabunge Wanawake wa Viti Maalum 113 kwa mwaka 2015. Hata hivyo, Wabunge Wanawake wa Viti Maalum walioteuliwa jumla yake ilikuwa ni 110 kati ya 113 ambapo Viti vitatu (3) vilibakizwa kusubiri Uchaguzi wa Majimbo nane (8) ambayo Uchaguzi wake ulihairishwa kutokana na sababu mbalimbali.

Uteuzi wa awali ulihusisha Vyama vitatu vilivyofikisha asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Wabunge kama matakwa ya Katiba yanavyotaka.hata hivyo mbunge wa iringa mjini mchungaji petter saimoni msingwa na mbunge wa jimbo la kilolo vennance mwamoto ambaye nia ndugu na ritta kabati kwa pamoja walimpongeza kwa kuchaguliwa na kuapishwa kwake siku ya leo.

Zantel Yakabidhi Computer 21 Kwa Vyuo vya Walimu Zanzibar

$
0
0
Afisa Mtendaji wa Millcom Africa Bi Cynthia Gordon akimkabidhi Computer Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma, anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania Benoit Janin, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Zanzibar 
Afisa Mtendaji wa Millcom Africa Bi Cynthia Gordon akimkabidhi Computer Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma, anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania Benoit Janin, Afisa wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha na kushoto Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi Khadija Juma Bakari,hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Zanzibar 
Maofisa wa Zantel wakifuatilia hafla hiyo ya kukabidhi Computer Vyuo vya Walimu Zanzibar.
Maofisa wa Zantel wakifuatilia hafla hiyo ya kukabidhi Computer Vyuo vya Walimu Zanzibar.
Afisa wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha akitowa maelezo wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Computer Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa ajili ya matumizi ya Vyuo vya Ualimu Zanzibar.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel Tanzania Benoit Janin akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Computer kwa ajili ya Matumizi ya Vyuo vya Ualimu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Hyatt Shangani Zanzibar. Na kusema lengo la Zantel ni kushirikiana na Serikali kwa lengo la kukuza na kuboresha elimu ya teknolojia na mawasiliano kusaidia vyuo vya Ualimu vinavyotoa Mafunzo hayoili kuongeza ufanisi katika ufundishaji wao.
Afisa Mtendaji wa Millcom Africa, Bi Cynthia Gordon, akizungumza wakati wa hafla hiyo na kusema Walimu ndio msingi wa maendeleo kwenye Taifa na ndio maana Zantel imewapa kipaumbele katika miradi yake ya Kijamii. na Kusema Zantel Daima imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha tunaboresha sekta elimu kwa wazanzibari na kama tunavyojua elimu ya teknolojia na mawasiliano ni muhumu kwa dunia ya sasa. 

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Computer na Kampuni ya Simu ya Zantel kwa ajili ya Vyuo vya Ualimu Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hotel ya Hyatt Shangani Zanzibar, na kuipongeza kampuni hiyo kwa jitihada zake inayofanya kwa kushirikiana na serikali katika kukuza na kuboresha elimu visiwani Zanzibar.

'Ili kutoa elimu bora kwa walimu wa teknolojia ya mawasiliano wa ngazi zote ni muhimu kuhakikisha mafunzo ya komputa yanajumuishwa kwenye mtaala wa vyuo vya elimu ili kuwajengea uwezo walimu katika kufundisha wanafunzi' 










Maofisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya makabidhiano ya Computer kwa ajili ya matumizi ya Vyuo vya Walimu Zanzibar.



Mkuu wa Vyo vya Ualimu Zanzibar Maulid Omar Hamad akitowa neno la shukrani kwa Uongozi wa Zantel Tanzania kwa msaada wao wa Computer 21 kwa ajili ya matumizi ya Vyo hivyo katika kutowa mafunzo kwa Walimu hao.



Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma Afisa wMtendaji Mkuu wa Zantel Benoit Janin.wakifuatilia hafla hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Vyuo vya Walimu akitowa shukrani.


Viongozi wa meza kuu wakimsikiliza Mkuu wa Vyuo vya Walimu Zanzibar Maulid Omar Hamad, akitowa shukrani kwa niaba ya Vyuo hivyo wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Computer na Kampuni ya Simu za Mkoni Zantel hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Zanzibar. 



Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma, Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania Benoit Janin Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Zanzibar Bi Khadija Juma Bakari kushoto Afisa Mtendaji wa Millcom Bi Cynthia Gordon na Afisa wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Zantel na Wizara ya Elimu Zanzibar.



Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amaali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akibadilisha mawazo na Mtendaji Mkuu wa Zantel Benoit Janin na Mtendaji wa Millicom Bi. Cynthia Gordon, baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi Computer kwa ajili ya Matumizi ya Vyuo vya Walimu Zanzibar.



Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akitowa shukrani kwa Kampuni ya Zantel kwa msaada wao wa Computer kusaidia matumizi katika Vyuo vya Walimu Zanzibar. wakati akizungumza na waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Zanzibar. 



Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya hafla ya kukabidhi Computer 21 kwa ajili ya matumizi ya Vyuo vya Ualimu Zanzibar.

SERIKALI KUCHUNGUZA MKATABA WA JENGO LA MACHINGA COMPLEX

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda (kulia), akikagua vizimba katika Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana, baada ya kufanyika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kilichoketi jana kujadili uendeshaji wa biashara wa katika jengo hilo pamoja na kamati ya mkoa iliyoundwa kuchunguza mkataba wa jengo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda akizungumza na wafanyabiashara katika Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana, kuhusu uendeshaji wa jengo hilo.
Makonda akiwasili katika viwanja vya Jengo la Machinga Complex kuzungumza na wafanyabiashara na wadau wengine. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wengine ni viongozi wa jengo hilo.
Makonda akiangalia Uwanja wa Karume akiwa jengo la Machinga Complex.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro akimuaga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kufanyika kwa uchunguzi katika ujenzi wa jengo la Machinga Ciomplex ili kubaini uhalali wa mkataba uliotumika kujenga jengo hilo.Aidha, amebainisha kuwa jengo la Machinga Complex kwa sasa linadaiwa zaidi ya Sh bilioni 36 kiasi ambacho ni mara tatu ya thamani halisi ya jengo hilo ambayo ni Sh 12 ambazo zinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara wa jengo hilo.

Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati alipotembelea jengo hilo lililopo Manispaa ya Ilala ili kujionea mazingira ya kufanyia biashara. Alisema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa itaanza kufanya uchambuzi wa mikataba ili kupata uhalali wa gharama na kujua kiwango kinachostahili kulipwa na wafanyabiashara hao.

Alisema kamati hiyo ya ulinzi na usalama imekubali kutengeza kamati ndogo itakayoanza kazi leo ya kuchambua na kuanza mikataba.“Ingekuwa vyema tungekuwa na mkutano wa kuwasikilizeni na kujua kero zenu, lakini tunayo sababu moja ya msingi ya kutowasikiliza , kwanza tunatafuta uhalali na utaratibu wa jengo hili lilivyojengwa.

Katika maelezo ya awali tuliyoyapata jengo hili uko mkanganyiko mkubwa, inawezekana ni miongoni mwa mradi mkubwa uliofanyiwa ufisadi Tanzania, sasa hatuwezi kukaa kusikiliza habari ya kizimba change, kwanza tupate uhalali wa mkataba uliopelekea kujenga jengo hili,” alisema Makonda.

Alisema kamati ya wafanyabiashara wa soko hilo itakayoundwa chini ya usimamizi wake itaanza kazi ya kuchunguza ili kubaini uhalali wa mkataba na kujua kama waliongia mikataba hiyo walikuwa sahihi.Makonda alitoa rai kwa wafanyabiashara kuwa rai ya Rais Magufuli ni kuwapigania wanyonge na kuhakikish awanatoka sehemu moja kwenda nyingine, hivyo wasaidiza wake kwa kupenda au kutokupenda wana jukumu la kuhakikisha wanafanikisha hilo.

Hivi karibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene aliifuta bodi inayosimamia jengo hilo na kumsimamisha kazi meneja anayesimamia jengo hilo na kumtaka kwenda katika ofisi za jiji kwa ajili ya kumpangia kazi nyingine.

Katika hatua nyingine, Simbachawene alilikabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuwaingiza wafanyabiashara bila masharti huku ukiangaliwa utaratibu mpya kwa wafanyabiashara hao.Katika mkutano wake na Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Simbachawene alisema, jengo hilo limekuwa likitumiwa kinyume na lengo ambalo walitakiwa wafanyabiashara kulitumia kwa gharama kidogo lakini limekuwa likitumiwa na watu wengine tofauti na wafanyabiashara jambo ambalo limesababisha kushindwa kulipa deni linalodaiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Airtel yazindua Duka la kwanza katika Wilaya ya Kahama

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bwana Vita Kawawa akikata utepe wakati wa kuzindua duka jipya la kwanza na la kisasa la Airtel litakalowawezesha wakazi wa Kahama kupata huduma bora za mawasiliano, akishuhudia (kulia) ni Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Airtel bi Adriana Lyamba , (kushoto) ni Meneja Mauzo wa Mkoa wa Shinyanga Bwana Ezekieli Nungwi.
Mfanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja Bwana Diliwish Tully akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bwana Vita Kawawa ( wa kwanza kushoto) juu ya vifaa na simu mbalimbali za smartphone zinazopatikana katika duka jipya la Airtel Kahama wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya na la kwanza wilayani hapo. Akishuhudia (katikati) Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Airtel bi Adriana Lyamba.
Wakazi wa wilaya ya kahama wakiangalia simu ya smartphone ya Bravo Z 10 inayopatikana katika duka jipya la Airtel Kahama wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya na la kwanza wilayani hapo litakalowawezesha wakazi hao kupata huduma bora za mawasiliano. 


Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel Tanzania imeendelea na mikakati yake ya kusogeza huduma bora kwa wateja wake kwa kufungua duka lake la kwanza katika wilaya ya Kahama Mkoani, Shinyanga

Duka hilo la kisasa ni moja ya ahadi ya Airtel kujali wateja wake Tanzania nzima na kuwapa huduma iliyobora na ya kiwango cha juu popote pale walipo.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel, Adriana Lyamba alisema, “ Airtel imefanikiwa kuwafikia wateja kwa kufungua milango mjini Kahama na kuwahakikishia tunaendelea kuwa wabunifu kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora za kisasa zenye gharama nafuu kwa watumiaji wa simu za mkononi nchi

Duka hili ni la kwanza hapa mjini kahama, hivyo tunajisikia furaha sana kuleta huduma zetu karibu na wateja wetu na kuwapatia fursa ya kutumia huduma zetu kama vile Airtel Money kujiongezea kipato. 

Natoa wito kwa wakazi wa Kahama kupata nafasi ya kutembelea duka hili na kupata huduma pamoja na bidhaa mbalimbali ikiwemo modemu ya maajabu ya Airtel Wingle pamoja na simu orijino za smartphone kwa bei nafuu. Aliongeza Lyamba

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Vita Kawawa alisema “Kahama ni moja ya miji inayokuwa kwa kasi kubwa hivyo kufunguliwa kwa duka hilo kutaongeza ufanisi wa huduma za mitandano. 

Tunawashukuru sana Airtel kwa kuona ni vyema kutuletea huduma hii hapa mkoani na kutuhakikishia mawasiliano bora wakati wote na kuondoa changamoto zilizoko hapo awali. Kwa wakazi wa kahama huu ni wakati muafaka kutumia duka hili vyema ili kupata bidhaa zitakazotusaidia katika kuendesha shughuli zetu za uchumi na kijamii

Mpango huu wa Airtel kufungua maduka zaidi nchini, unalenga kuboresha maduka ya kampuni hiyo, ili yawe ya kisasa kama ilivyo katika mikoa ya mwanza, Arusha,Kilimanjaro na Mlimani City Dar es Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MATHIAS MEINRAD CHIKAWE KUWA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI JAPAN

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Magufuli akimpongeza Mathias Meinrad Chikawe mara baada ya kumuapisha kuwa  Balozi Mpya wa Tanzania nchini Japani.
Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuamuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi Ikulu jijini Dar es Salaam. 
PICHA NA IKULU.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe ameapishwa leo tarehe 19 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Batilda Salha Burian ambaye Mkataba wake  umemalizika.Akizungumza mara baada ya kuapishwa, Mheshimiwa Chikawe ameahidi utumishi uliotukuka na kuiunganisha vyema Tanzania na Japan hususani katika masuala ya kiuchumi.

Mheshimiwa Chikawe ametoa wito kwa watanzania wote hasa waishio Japan na nchi nyingine zinazotumia Ofisi ya Ubalozi huo wa Tanzania, kuutumia vizuri ubalozi huo ili kunufaika na fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji.


Ubalozi wa Tanzania nchini Japan, pia unatoa huduma za kibalozi katika nchi za Korea Kusini, New Zealand, Papua New Guinea na Australia.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

19 Aprili, 2016.


MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF), WATOA ELIMU KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NCHINI

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafnyakazi, WCF, Masha Mshomba, akizungumza wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, na kufanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam Aprili 19, 2016. Lengo la semina hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kwa viongozi hao juu ya shughuli za Mfuko na faida ya wafanyakazi kupatiwa fidia endapo patatokea madhara awapo kazini. Wengine pichani ni mgeni rasmi, Pendo Z.Berege, (Mwakilishi wa Msajili wa vyama vya afanyakazi na waajiri, na Peter J. Mbelwa kutoka Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii, (SSRA).

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, umeendesha semina ya siku moja kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kuwalipia michango ya mwezi.

Semina hiyo iliyofanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Aprili 19, 2016, ilifunguliwa na mwakilishi wa Msajili wa vyama vya wafanyakazi na waajiri, Bi.Pendo Z.Berege.Katika hotuba yake, Bi. Berege alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatwapo na majanga wakiwa kazini.

Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi ni taasisi ya serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi No. 20 ya mwaka 2008.Akiwakaribisha wana semina kwenye semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Msomba alisema, Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa wafanyakazi na kwa kutambua kuwa viongozi wa wafanyakazi ndio wadau wakuu wa Mfuko huo, semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.

Akitoa mada juu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa fidia kwa wafanyakazi waumiapo kazini.
Naye Bi.Amina Likungwala kutoka WCF, amesema katika mada yake ya Wajibu wa Vyama vya Wafanyakazi ambapo alisema, ni wajibu wa vyama kutoa elimu kwa wanachama wao ambao ni wafanyakazi lakini pia kuwaeleza waajiri umuhimu wa kutoa michango kwa wakati 

Mshiriki akisoma kijitabu chenye maelezo ya kina kinachofafanua majibu ya maswali ya mara kwa mara ambayo wadau wanataka kujua kuhusu WCF.
Bi. Pendo Berege, akifungua semina hiyo 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, SSRA, Bi.Irene Isaka, akitoa hotuba ya kufunga semina hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, SSRA, Bi.Irene Isaka, akitoa hotuba ya kufunga semina hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba.
Mzee Mchafu Chakoma, mwakilishi wa viongozi wa wafanyakazi akitoa neno la shukrani
Bw. Chakoma (kushoto), akibadilihana mawazo na Bi. Pendo Berege
Bi Amina Likungwala kutoka WCF, akitoa mada kuhusu wajibu wa vyama vya wafanyakazi
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence, akitoa mada "Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
Bi. Pendo Z.Berege, (kushoto) na Mkuu wa kitengo cha Ukauzi wa ndani cha Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii, (SSRA).Peter J. Mbelwa, wakiteta jambo.
Majadiliano yakiendelea
Mmoja wa washiriki wa semina akizungumza kwenye kipindi cha majadiliano cha semina hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa WCF wakichykua taarifa muhimu.
Mshiriki akifuatilia kwa makini

MultiChoice Tanzania yawatangaza washindi wa “JISHINDIE NA DSTV”

$
0
0
Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akizungumza kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) juu ya droo hiyo pamoja na ofa mbalimbali zinazoendelea kutolewa kwa wateja wa DSTV 
Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo akichanganya droo hiyo kwa njia ya kielektoniki kupitia kompyuta. wengine wanaoshuhudia ni maafisa wa MultiChoice Tanzania. Kulia ni mwakilishi kutoka Bahati Nasibu ya Kubahatisha, Bw. Mrisho Millao.
Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akihakiki moja ya majina ambayo yameingia kwenye droo ya ushindi kwa wateja wa DSTV .
Droo hiyo ikiendelea.
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionyesha majina ya washindi kwenye 'sreen' kubwa (Haipo pichani) wakati wa tukio hilo.
Droo hiyo ya JISHINDIE NA DSTV ikienndelea huku maafisa wa MultiChoice Tanzania na Mwakilishi wa Mchezo wa kubahatisha Tanzania pamoja na wanahabari wakishuhudia tukio hilo mapema leo Aprili 19.2016, Makao makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Kampuni ya MultiChoice Tanzania inayosambaza vifaa vya ving’amuzi vya DSTV hapa nchini mapema leo Aprili 19.2016 imechezesha droo maalum na kuwapata washindi wa “JISHINDIE NA DSTV” katika tukio lililofanyika Makao makuu ya kampuni hiyo Oysterbay, barabara ya Ali Hasan Mwinyi, Jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini.

Awali katika droo hiyo, Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo alieleza kuwa, droo hiyo ilianza tokea mwezi wa kwanza ambapo wateja walitakiwa kuwa na malipo kwenye ving’amuzi vyao vya DSTV bila kukatika kuanzia hiyo Januari hadi mwezi Machi.

Wateja ambao hawajakatiwa ving’amuzi vyao katika promosheni hiyo ya JISHINDIE NA DSTV, waliotangazwa leo ambaoo ni wateja waliojiunga mwezi wa kwanza na kuweza kulipia DSTV zao bila kukatiwa matangazo kwa muda wa miezi mitatu wameweza kujishindia zawadi ya safari ya kwenda Zanzibar wakiwa wao na familia zao.

“Washindi wawili ambao kila mmoja atapata nafasi ya kupelekwa Zanzibar na kukaa huko kwa siku mbili katika hoteli huku akilipiwa kila kitu kuanzia usafiri, malazi, chakula yeye na familia yake ikiwemo baba, mama na watoto wawili. Washini hao ni Mwelly Nyakusaima ambaye ni mkazi wa Igoma-Mwanza na mshindi mwingine ni Evarist Ndambo mkazi wa Tabataa Jijini Dar es Salaam.” Alisema Bi. Hilda Nakajumo.

Aidha, alibainisha kuwa, washindi wengine waliojishindia droo hiyo ambao ni wa kipengele cha pili ni wale wateja ambao tayari walishajiunga na DSTV huku wakitakiwa wasikatiwe malipo yao kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa tatu.

Ambapo wateja 50 wamejishindia DSTV EXPLORA Decoders huku wateja 90 wao wakibahatika kupata kuunganishwa malipo ya bure ya mwezi ikiwemo ya mwezi mmoja, miezi mitatu, miezi sita na miezi 12 bure.

Aidha, washindi hao wote walioshinda MultiChoice ilibainisha kuwa, watapigiwa simu na kuelekezwa namna ya kuchukua zawadi zao hizo kuanzia sasa kwa muda hadi June mwaka huu.

Kwa upande wake, Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu aliwakumbusha wateja wa DSTV kuendelea kulipia malipo ya ving’amuzi vyao huku wakitoa ofa mbalimbali sambamba na vipindi vizuri ikiwemo vya uhondo wa soka la kimataifa, filamu na muziki..

Tazama MO tv, kuona habari hiyo hapa: 

SERIKALI KUENDELEA KULINDA KAZI ZA WASANII NCHINI

$
0
0
Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipa kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo akionesha kwa waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam moja ya CD zilizokamatwa wakati wa msako wa kubaini wale wote wanaojihusisha na uuzaji na usambazaji wa kazi za wasanii bila kuwa na stempu za kodi katika bidhaa za filamu na muziki. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo na mwisho kulia ni Afisa Habari wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bi Mariam Mwayera.
Mkurugenzi wa Elimu kwa mlipa kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo (katikati) akitoa wito leo Jijini Dar es salaam kwa wasambazaji na wauzaji wa kazi za Filamu na muziki kuzingatia sheria na Kanuni zinazosimamia sekta hiyo kwa kuwa Serikali itawachukulia hatua kali wale wote watakaoenda kinyume cha sheria na taratibu zilizopo ikiwemo kutozwa faini isiyopungua milioni tano au kifungo kisichopungua miaka mitatu jela. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo,Kushoto ni Afisa Utamaduni wa Bodi ya filamu Bw. Wilhadi Tairo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mikakati ya Bodi hiyo kuhakiksha kuwa kazi za wasanii wa filamu zinaendana na maadili ya Taifa.kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Richard Kayombo.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Filamu Tanzania ukilenga kueleza Mikakati ya Serikali katika kulinda haki za wasanii wa filamu na Muziki zinalindwa.( Picha na Frank Mvungi- Maelezo)


Na Fatma Salum (MAELEZO)

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeahidi kuendeleza msako wa wafanyabiashara wote wanaouza kazi za filamu na muziki bila kubandikwa stempu halali za kodi ili kuzilinda kazi hizo kwa ajili ya kuwanufaisha wasanii na kuhakikisha Serikali inapata mapato yake.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma kwa Mlipa Kodi kutoka TRA Richard Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Kayombo amesema TRA kwa kushirikiana na wadau wa tasnia ya muziki na filamu imedhamiria kuhakikisha kuwa bidhaa za filamu na muziki zenye stempu za kodi ndizo zinazoingizwa sokoni ili kulinda kazi za wasanii wa taifa letu dhidi ya dhuluma zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiashara.

“Msako huu endelevu utahusisha kukamata bidhaa zote ambazo hazijabandikwa stempu za kodi na kuwachukulia hatua wahusika kwa mujibu wa sheria.” Alieleza Kayombo.

Aidha Kayombo amefafanua kuwa kwa kipindi cha mwezi Februari na Machi 2016, TRA kwa kushirikiana na Dalali wa Mahakama Yono Auction Mart & Company Limited ilifanya msako jijini Dar es Salaam na kukamata jumla ya CD na DVD zenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni 1.3 ambazo zilisambazwa bila kufuata sheria hivyo kukwepa kodi ya ushuru ipatayo shilingi Milioni 31.9 na gharama za stempu zaidi ya shilingi Milioni 11.1.

TRA inawatahadharisha wale wote wanaosambaza na kuuza kazi za filamu na muziki ambazo hazijabandikwa stempu kuacha mara moja na kufuata utaratibu wa kupata stempu hizo katika ofisi za TRA ili wawe na uhalali wa kuuza bidhaa hizo kinyume chake hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

WAZIRI MAJALIWA AKITETA JAMBO NA SPIKA NDUGAI NA MBUNGE LULIDA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) wakizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Riziki Lulida (kulia) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Katibu Mkuu Wizara ya Habari afungua mdahalo wa Vijana kujadili hatma ya ajira kwa vijana nchini

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda Bibi. Mary Kawar baada ya kufungua mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam.Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifungua mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda Bibi. Mary Kawar akizungumza na vijana (hawapo pichani) wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na shirikila hilo leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akitoa mada wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam
Mtaalam wa ajira kutoka ILO Bw. Jealous Chirore akichangia mada wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika hilo na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi kutoka YUNA – Chuo cha Bogamoyo akiuliza swali wakati wa mdahalo wa hatma ya ajira kwa vijana wa Tanzania ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) na kushirikisha vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dar es Salaam

MATUKIO YA BUNGENI LEO MJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongozwa na Mpambe wa Bunge kuingia kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kuongoza kikao cha kwanza cha mkutano wa tatu wa Bunge Aprili 19, 2016.
Ruth Owenya akiapa kuwa Mbunge kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Aprili 19, 2016.
Ritta Kabati akiapa kuwa Mbunge kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Aprili 19, 2016.
Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia) akimwapisha Ritta Kabati kuwa mbunge kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Aprili 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Spika wa Bunge, Job Ndugai akimwapisha Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Aprili 10, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza, Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mstaafu , Shamsi Vuai Nahodha baada ya kuapishwa kuwa Mbunge, Bungeni mjini Dodoma, Aprili 19, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Bumbuli na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, January Makamba, bungeni mjini Dodoma Aprili 19, 2016.

Rais Magufuli afungua daraja la Kigamboni na amsimamisha kazi Wilson Kabwe.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe huku viongozi wengine wakiushikilia kuashiria uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata picha ya kumbukumbu viongozi wengine baada ya  uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiteta jambo na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt Ramadhani Dau wakati wa  uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wengine wakitembea juu ya Daraja la Kigamboni baada ya kulizindua katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.PICHA NA IKULU.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Aprili, 2016 amefungua rasmi Daraja la Kigamboni linalounganisha usafiri wa barabara kati Kigamboni na Kurasini Jiji la Dar es salaam na amependekeza Daraja hilo liitwe Daraja la Nyerere (Nyerere Bridge).


Sherehe za ufunguzi wa daraja hilo kubwa na la kipekee kwa Afrika Mashariki na Kati zimefanyika kando ya daraja hilo upande wa Kigamboni na kuhudhuriwa na viongozi na wageni mbalimbali wakiwemo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Edwin Ngonyani, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) Mheshimiwa Antony Mavunde, Wabunge na Mameya wa Jiji na Dar es salaam.


Ujenzi wa daraja hilo umehusisha nguzo mbili za pembezoni na mihimili miwili inayoshikilia nyaya 36, na daraja zima lina urefu wa meta 680, upana wa mita 32, njia sita za magari, njia mbili za watembea kwa miguu na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 2.5.



Daraja hilo limejengwa kwa fedha za ndani na kugharimu jumla ya shilingi Bilioni 254.12 ambapo kati ya fedha hizo asilimia 60 zimetolewa na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), na asilimia 40 zimetolewa na Serikali ya Tanzania.


Kujengwa kwa Daraja hili kutaondoa kero ya msongamano wa magari na usafiri kwa wakazi wa Kigamboni na wakazi wa katikati ya Jiji la Dar es salaam ambao walilazimika kutumia kivuko (Ferry) ili kukatiza eneo la mkondo wa bahari ya Hindi ama kutumia barabara ya kuzunguka kupitia Kongowe lenye urefu wa kilometa 52.


Daraja hilo limefanyiwa majaribio kwa kutumia Malori 44 yenye uzito wa tani 30 na limethibitika kuwa na uwezo wa kubeba jumla ya tani 1,320 na hivyo linatarajiwa kusaidia usafirishaji wa mizigo ya kutoka na kuingia katika bandari ya Dar es salaam.


Akizungumza katika sherehe hizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza vyombo husika vianze mchakato wa daraja hilo kupewa jina la "Daraja la Nyerere"(Nyerere Bridge) ikiwa ni kuuenzi mchango mkubwa wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefanya kazi kubwa ya kuijenga Tanzania.


Aidha, Rais Magufuli amewapongeza wadau wote waliohusika kufanikisha ujenzi wa Daraja hilo likiwemo Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi na wakandalasi kutoka China, na ametaka watanzania wajivunie daraja hilo kubwa na lililojenga heshima kubwa kwa nchi.


Pia Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa vyombo vya habari vya Tanzania kuitangaza vyema Tanzania na kuwa na uzalendo wa kweli kwa nchi yao badala ya kubeza kazi nzuri zinazofanywa ndani ya nchi kwa manufaa ya watanzania.


Katika hatua nyingine Rais Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Bw. Wilson Kabwe na kuagiza vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili za kusaini mikataba iliyosababisha serikali kupoteza mapato.


Dkt. Magufuli ametangaza uamuzi huo wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa daraja la Kigamboni, baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Paul Makonda kumueleza kuwa amebaini upotevu wa shilingi Bilioni 3 uliotokana na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Bw. Wilson Kabwe kusaini mikataba ya ukusanyaji mapato ya Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo kwa kutumia sheria iliyopitwa na wakati, na pia ukusanyaji wa tozo za uegeshaji wa magari ndani ya Jiji.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

19 Aprili, 2016



JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAMKAMATA MTU MMOJA ALIYEKUTWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU AINA YA CHARGER.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA. 
   
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA, MTU MMOJA MKAZI WA UYOLE JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MASHAKA RAMADHAN [21] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA KETE 12 ZA DAWA ZIDHANIWAZO ZA KULEVYA.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2016 MAJIRA YA SAA 10:20 ASUBUHI KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. UPELELEZI NA UCHUNGUZI ZAIDI UNAENDELEA ILI KUBAINI AINA YA DAWA HIZO.

KATIKA MSAKO WA PILI: JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA MATENKI – KASUMULU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA PETER CHANGWA [21] AKIWA NA POMBE HARAMU [GONGO] UJAZO WA LITA 20.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.04.2016 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO ENEO LA FORODHA –KASUMULU, KATA YA NGANA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUWA AKISAFIRISHA POMBE HIYO HARAMU KWENYE BAISKELI YAKE AKITOKEA MALAWI. 

KATIKA TUKIO LA TATU, MTU MMOJA MKAZI WA IGOGWE WILAYA YA RUNGWE MKOANI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LESSA JAPHET [45] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI CHUPA 24 AINA YA CHARGER. 

MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 19.04.2016 MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA HUKO ENEO LA MTAA WA IGOGWE, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA TUKUYU MJINI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. 

SERIKALI IMEPIGA MARUFUKU UINGIZAJI NA MATUMIZI YA POMBE HIZO KWANI NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. POMBE HIZO NI PAMOJA NA CHARGER, RIDDER, DOUBLE PUNCH, POWER NO.1 NA BWENZI AMBAZO UINGIZWA NCHINI KUTOKA NCHINI JIRANI YA MALAWI.

WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI EMANUEL G. LUKULA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE KALI NA POMBE HARAMU [GONGO] KWANI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UINGIZAJI WA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

KATIKA TUKIO LA NNE, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MHAMIAJI HARAMU RAIA WA NCHINI KONGO AITWAYE JEAN MWELA [21] KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

MHAMIAJI HUYO ALIKAMATWA NA ASKARI WALIOKUWA DORIA MNAMO TAREHE 19.04.2016 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO ENEO LA UZUNGUNI – ROMAN KATOLIKI, KATA NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.

Imesainiwa na:
[EMANUEL G.LUKULA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Namba ya Simu: 0658 376 006 – Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images