Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

KATIKA KUHAKIKISHA JIJI LA DAR ES SALAAM KUWA SAFI

$
0
0
Katika kuhakikisha kuwa Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi, Manispaa ya Ilala imethubutu kwa kuanza kukata miti ambayo imekuwa ikihatarisha usalama wa wananchi wakiwemo wapita njia na magari, kama picha inavyoonyesha usafi ukifanyika katika moja ya mitaa wa Samora 23 Aprili, Jijini Dar es Salaam.Picha na Benedict Liwenga-MAELEZO

MPANGO WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI (PSSN) WABADILISHA MAISHA YA WANANCHI VIKUGE, KIBAHA

$
0
0
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Natalia Kanem (kulia) akifanya manunuzi ya bidhaa zinazotengenezwa na wanakijiji wa Vikuge ambao wamewezeshwa na mpango wa PSSN wa TASAF. (Picha na Modewjiblog).

Washirika wa maendeleo nchini wametembelea vijiji viwili Vikuge na Mwanabwito vilivyopo Wilayani Kibaha kwa ajili ya kutazama miradi ya kusaidia kaya masikini ambayo imeanzishwa kwa msaada wa fedha ambazo zinatolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambapo washirika hao wamekuwa wakitoa fedha ili kusaidia miradi hiyo.

Washirika hao wa maendeleo kutoka UN Tanzania, Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (DFID), Irish Aid, USAID na Shirika la Kimataifa la Misaada la Sweden (SIDA) ambao wamekuwa wakishirikiana na TASAF katika Mpango wa Kusaidia Kaya Masikini (PSSN).

Wakitoa taarifa mbele ya washirika wa maendeleo, wanavikundi kutoka Kijiji cha Vikuge wamesema kuwa kupitia mpango huo wameweza kuboresha maisha yao tofauti na jinsi ilivyokuwa awali.Walisema kuwa maisha yao ya awali yalikuwa magumu lakini kutokana na msaada walioupata kutoka TASAF wameweza kuanzisha vikundi ambavyo vinawasaidia kuboresha maisha kwa kufanya biashara za mazao, nguo na chakula.

“Kuna mafanikio tumeyapata darasani mahudhurio yameongezeka, klini wamama wanakwenda na hata utapiamlo haupo tena kwa watoto kwa sababu ya TASAF kutusaidia,” alisema mwakilishi wa wanavikundi kutoka Vikuge.
Mratibu TASAF Kibaha, Goodson Hare, akitoa neno la ukaribisho kwa ujumbe wa washirika wa maendeleo nchini waliotembelea vijiji viwili Vikuge na Mwanabwito vilivyopo Wilayani Kibaha kwa ajili ya kutazama miradi ya kusaidia kaya masikini ambayo imeanzishwa kwa msaada wa fedha ambazo zinatolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Akizungumzia ziara hiyo, Mratibu Mkazi wa Umoja wa MATAIFA NCHINI, Alvaro Rodriguez alisema wamefanya ziara hiyo ili kuona ni hatua gani imefikiwa na wanufaikaji na kuona ni changamoto gani bado zinawakabili.“Tunaangalia changamoto zilizopo ili kuona ni jisni gani tunaweza kuwasaidia kama Mpango wa Kusaidia Kaya masikini ulivyo nab ado kuna wahitaji zaidi licha ya kuwa tumeshasaidia kaya Milioni1.1 kwa nchi nzima,“Mpango huu ni mzuri na kawa wasaidiwa wakiwa kama wajasiliamali na kutengeneza kipato inaweza kusaidia Tanzania kuondokana na umasikini kuelekea katika uchumi wa kati kama jinsi ilivyojiwekea malengo,” alisema Rodriguez.
Kiongozi wa msafara wa washirika wa maendeleo nchini, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumzia madhumuni ya ziara yao kwa wanakijiji.
Mkurugenzi wa Programu Jamii wa TASAF, Amadeus Kamagenge akizungumza jambo wakati wa utambulisho wa ujumbe huo.
Wanufaikaji wa mpango wa PSSN wakisoma risala kwa wageni.
Mmoja wa wanufaikaji wa mpango wa PSSN akitoa maoni wakati wa mkutano na washirika wa maendeleo waliotembelea kijiji chao.
Mwenyekiti kijiji cha Vikuge, Vitus Mchami akitoa salamu kwa niaba ya wanakijiji kwa ugeni huo.
Baadhi ya wanakijiji cha Vikuge wanaonufaika na mradi wa PSSN waliohudhuria mkutano huo.
Zoe Glorious (kulia) kutoka ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini akifanya mahojiano na Mnufaikaji wa kijiji cha Vikuge, Bi. Halima ambaye aliwezeshwa na mpango wa PSSN na kuanzisha biashara ya kufuga bata ambayo imemuwezesha kuendesha maisha yake na kumuingizia kipato.
Bi Halima akiwa katika picha ya pamoja na mtoto wake wakati wa ziara ya washirika wa maendeleo nchini walipomtembelea nyumbani kwake.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Finland nchini, Milma Kettunen (kulia) akinunua moja ya bidhaa iliyotengenezwa na ukili kutoka kwa wakinamama wa kijiji cha Vikuge walionufaika na mpango wa PSSN na kujikwamua kiuchumi.
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Natalia Kanem (kulia) akifanya manunuzi ya bidhaa zinazotengenezwa na wanakijiji wa Vikuge ambao wamewezeshwa na mpango wa PSSN wa TASAF.
Mwakilishi wa USAID, Daniel Moore akinunua kitamba cha Batiki kutoka kwa wanufaikaji wa mpango wa PSSN unaoendeshwa na TASAF wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya TASAF mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Eric Beaume wakimsikiliza mmoja wa wanakijiji cha Vikuge aliwezeshwa na mpango wa PSSN na kufanya biashara ya kilimo cha matunda na mazao mbalimbali. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Vikuge,Vitus Mchami, anayefatia Mratibu TASAF Kibaha, Goodson Hare
Baadhi ya Biashara za wananchi wa Vikuge walionufaika na mpanngo wa PSSN wa TASAF.


Baadhi ya wanakijiji wa Mwanabwito, Kibaha mkoa wa Pwani waliohudhuria mkutano wa washirika wa maendeleo.


Mratibu TASAF wa wilaya ya Kibaha, Goodson Hare akizungumza jambo wakati wa kutizama biashara zinazofanywa na wajasiriamali walionufaika na mpango wa PSSN wa TASAF kutoka kijiji cha Vikuge, Kibaha.


Ujumbe wa washirika wa maendeleo nchini akiwemo Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia) wakiwasili kwenye kijiji cha Mwanabwito.


Ujumbe wa washirika wa maendeleo nchini na viongozi wa TASAF katika picha ya pamoja walipotembelea shamba la miti katika kijiji cha Mwanabwito mkoani Pwani.


Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama (katikati) akifafanua jambo kwa baadhi ya wajumbe wa msafara wa washirika wa maendeleo nchini wakati wa ziara hiyo.

WIKI YA CHANJO AFRIKA

$
0
0
 MRATIBU wa chanjo kutoka Kituo cha Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Nd. Yussuf Haji Makame, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari na maofisa wa afya kutoka wilaya mbalimbali za Unguja juu ya wiki ya chanjo barani Afrika,  inayoanza leo Aprili 23, 2016.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI  JUU YA WIKI YA CHANJO AFRIKA,KAULI MBIU YA MWAKA HUU NI “KAMILISHA RATIBA YA CHANJO, EPUKA UGONJWA WA POLIO.”
 MWANDISHI wa habari mwandamizi kutoka Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC),  na Mwenyekiti wa mkutano  Sheikh  Said Suleiman, akizungumza katika semina  juu ya umuhimu wa chanjo  ya polio kwa washiriki (hawapo pichani), katika hospitali ya Kidongo Chekundu.
 WAANDISHI  wa habari wa vyombo mbalimbali na maofisa wa afya wa wilaya za Unguja waliohudhuria katika mkutano huo. (Picha zote na Abdalla Omar-MAELEZO ZANZIBAR).

WIZARA YA UJENZI ,UCHUKUZI NA MAWASILIANO YAENDELEA NA MCHAKATO WA UKUSANYAJI MAONI JUU YA UBORESHAJI SERA YA TAIFA YA (TEHAMA)MKOANI MBEYA

$
0
0
Mhandisi Enock Mpenzwa Idara Mawasiliano toka Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Forest jijini Mbeya waliofika kwa ajili ya zoezi la utoaji maoni na ushauri juu ya uboreshaji wa sera mpya ya Taifa ya TEHAMA katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu TIA jijini Mbeya April 22, 2015. 
Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Simu katika Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Ndugu John Mwera akizungumza na wanahabari katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu jijini Mbeya( TIA ) juu ya zoezi la uchukuaji maoni na ushauri kwa wadau katika kuboresha sera ya Taifa ya Habari ,Teknologia na Mawasiliano (TEHAMA). 
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Forest jijini Mbeya wakiwa katika foleni ya kujiandikisha ili kutoa maoni yao na ushauri juu ya uboreshaji wa sera ya Taifa ya TEHAMA,zoezi ambalo limefanyika katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu Mbeya (TIA) April 22 ,2015.



Mwanafunzi shule ya sekondari Forest jijini Mbeya Mariam Jordan akijiandikisha kwa ajili ya kutoa maoni yake katika zoezi la uboreshaji wa sera ya Taifa ya TEHAMA zoezi ambalo limeratibiwa na Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ,katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu Jijini Mbeya (TIA).

BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI

Waziri Mhe. Kairuki afungua Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kufungua mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi uliofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Dkt.  Ndumbaro ni Mwenyekiti wa Baraza hilo.
 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati akifungua mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi uliofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifungua  mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi uliofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi katika Ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Mstari wa mbele katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe  wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Utumishi uliofanyika katika Ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. 
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akifunga mkutano maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma uliofanyika katika  Ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Mwakilishi Tunguu atoa msaada wa mabati

$
0
0
MWAKILISHI wa jimbo la Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said, akikabidhi msaada wa mabati 24 kwa familia ya mzee Ali Nyau (kushoto) na mkewe Bi. Tamasina Thomas (wa tatu kutoka kushoto), baada ya nyumba yao iliyoko Kibele Kwa Bohora kuanguka kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha nchini. (Picha na Martin Kabemba).


Na Salum Vuai, MAELEZO

VIONGOZI wa majimbo pamoja na watu wengine wenye uwezo, wamehimizwa kuendelea kuwasaidia wananchi walioathirika na mvua za masika zinazoendelea kunyesha kote nchini.

Mwakilishi wa jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said, amesema maafa yaliyowakumba wananchi mbalimbali, yanahitaji msaada wa kila mwenye uwezo bila kuangalia tofauti za kisiasa, kidini au maeneo waliko.

Said alisema hayo huko Kibele Kwa Bohora, jimbo la Tunguu baada ya kukabidhi mabati 24 yenye thamani ya shilingi laki tatu kwa familia ya mzee Ali Nyau Mavangu na Bi. Tamasina Thomas, ambao nyumba yao ilianguka kutokana na mvua zinazoendelea.

Mwakilishi huyo alisema, kipindi hichi ambacho wananchi wengi wameathiriwa na mvua, ndicho muafaka kwa viongozi wa majimbo walioshinda uchaguzi, kufanya mrejesho kwa wapiga kura wao.Hata hivyo, alisema jambo la kutoa msaada halipaswi kufanywa na viongozi hao wa majimbo pekee, bali ni wajibu wa kila mmoja kwa uwezo alionao.

Alifahamisha kuwa baada ya kupata taarifa za familia hiyo yenye watoto kadhaa kuangukiwa na nyumba yao usiku wa Aprili 16, mwaka huu, yeye na mbunge wa jimbo hilo Khalifa Salum pamoja na madiwani, wameamua kutoa mabati hayo kuifuta machozi familia hiyo.

Mbali na mabati hayo, pia ameahidi kutoa msaada mwengine wa madirisha na kifusi kwa wananchi hao ambao sasa wanapata usumbufu wa pahala pa kulala kwa amani kutokana na mvua zinazonyesha.Wakitoa shukurani zao, baba wa familia hiyo mzee Ali Nyau na mkewe Tamasina Thomas, walisema msaada huo umewapa faraja kwani utawawezesha kupata sehemu nzuri ya kujistiri.

Walieleza kufurahishwa sana na viongozi wao kwa hatua ya haraka waliyochukua kuwasaidia, mara baada ya kupata taarifa za maafa yaliyowapata.“Hatuna neno linaloweza kutosha kuelezea shukurani zetu, lakini kubwa ni kuwaombea dua viongozi wetu hawa Mwenyezi Mungu awazidishie moyo wa imani na waendelee kuwa pamoja nasi katika shida na raha,” walisema.Aidha, walisema kufuatia kupata msaada huo, wametambua kwamba kura zao hazikupotea na zimekwenda kwa watu sahihi

WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI, EALA, WAWAFAGILIA SAID SALIM BAKHRESA NA DKT. MENGI

$
0
0
Mhandisi mitambo wa Azam TV, (kushoto), akiwapatia maelezo ya juu ya chumba cha uthibiti matangazo, (control room), wabunge wa EALA-Tanzania walipotembelea studio za Televisheni hiyo, Tabata jijini Dar es Salaam, Aprili 22, 2016.

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

WABUNGE wa bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania, wamewafagilia wafanyabiashara wakubwa hapa nchini, Dkt. Reginald Mengi na Mzee Said Salim Bakhresa, kwa uthubutu wao wa kutambua na kuzitumia fursa zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwahimiza watanzania wengi kuiga mfano huo.

Pongezi hizo walizitoa Aprili 22, 2016 wakati walipotembelea studio za Azam Media, mwishoni mwa ziara yao ya kuvitembelea vyombo vya habari kwa lengo la kuhamasisha umma wa Watanzania kuchangamkia fursa kwenye Jumuiya hiyo ambayo mwenyekiti wa wabunge hao Mh. Charles Makongoro Nyerere ameiita kuwa ni jumuiya ya watu wa Afrika Mashariki na sio ya viongozi.

“Napenda kumpongeza sana mzee Said Salim Bakhresa kwa kutambua fursa zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo Azam TV inaonekana kwenye nchi kadhaa wanachama wa Jumuiya lakini pia bidhaa za Azam zimesambaa karibu Afrika Mashariki na Kati, na Mzee Mengi pia anastahili pongezi kwa utambuzi wao wa fursa zilizopo kwenye Jumuiya.” Alisema Mh. Shy-Rose Bhanji, ambaye alikuwa miongoni mwa wabunge hao.

Kuna haja ya watanzania kuondokana na dhana ya kujiona wanyonge kwenye Jumuiya hii kwani wanatakiwa kuchangamkia kila fursa iliopo, mfano mimi ni mwalimu wa hisabati, ukijumlisha na Kiswahili, unaweza kupata kazi huko Sudani Kusini na maeneo mengine ya Afrika Mashariki, kwani walimu wa Kiswahili wanahitajika sana, unachopaswa ni kujiongeza tu, unakuwa na kitu kingine cha ziada.” Alisema Mh. Nderaikindo Kessy.

Kwa upande wake, Mh. Abdulla Mwinyi, alisema, wabunge wa EALA kutoka Tanzania, wamefanya jitihada hizo za kutembelea vyombo vya habari kwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na waandishi wa habari katika kuhabarisha umma na vyombo vya habari vinao mchango mkubwa wa kutangaza kwa kina fursa za kiuchumi kwenye Jumuiya.

Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa kituo cha televisheni cha Azam TV, Mkurugenzi wa uendeshaji vipindi wa Azam TV, Yahya Mohammed alisema, malengo ya Azam TV ni kufika kufanya kazi zake kwenye nchi zote za Afrika Mashariki, na Kati, ambapo kwa sasa wana soko zuri tu DRC, Rwanda, Uganda. Kenya na Burundi zinajikongoja lakini matumaini makubwa ya kulishika soko la nchi hizo yapo.
Mh. Shy-Rose Bhanji, (kulia), na Mkurugenzi wa TV, Bi. Jane Shirima
Mkurugenzi wa uendeshaji vipindi wa Azam TV, Yahaya Mohammed, (wapili kushoto), akizungumza wakati akitoa taarifa yake kwa wabuneg hao
Mkurugenzi wa uendeshaji vipindi wa Azam TV, Yahaya Mohammed, (wapili kushoto), akizungumza wakati akitoa taarifa yake kwa wabuneg hao. Wanne kulia ni Mkurugenzi wa TV, Jane Shirima
Mkuu wa chumba cha habari Azam TV, Bw. Hassan Mhelela, akizungumza wakati wabunge hao (hawapo pichani), walipotembelea chumba cha habari
Bw. Mhelela akimpokea Mh. Shy-Rose Bhanji
Mh. Nderaikindo Kessy
Mh. Shy-Rose Bhanji
Mh. Abdulla Mwinyi
Mh. Nderaikindo Kessy
Mh. Shy-Rose Bhanji, akipokewa na Bi. Jane Shirima
Mh. Shy-Rose Bhanji
Picha ya pamoja, wabunge na uongozi wa Azam TV

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda, (wapili kushoto), Mh. Makongoro Nyerere, (wakwanza kushoto) Mh. Shy-Rose Bhanji (wakwanza kulia) na msanii nguli, Mrisho Mpoto, (mjomba), wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye chumba cha wageni Azam TV, waheshimiwa hawa walikutana. wakati Mh Mkuu wa mkoa na "mjomba" walifika kwenye mahojiano maalum kuhusu kampeni ya usafi, wabunge walifika kwa ziara ya kikazi
Wabunge wa EALA-Tanzania, kutoka kushoto, Mh. Kessy, Mh. Mwinyi, Mh. Bhanji, Mh.Makongoro

Wahandisi Temesa watunukiwa vyeti

$
0
0
Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan akikabidhi cheti kwa Mhandisi Amani Mwanga baada ya kuhitimu mafunzo ya teknolojia ya umeme wa jua (Solar Photovoltaic Technology)
Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan akikabidhi cheti kwa Mhandisi Sara Moses baada ya kuhitimu Mafunzo ya teknolojia ya umeme wa jua (Solar Photovoltaic Technology).
Dr. Brenda Kazimili kutoka kitengo cha Fizikia Chuo kikuu cha Dar es Salaam, akielezea umuhimu wa mafunzo ya teknolojia ya Umeme wa Jua(Solar Photovoltaic Technology) yaliyotolewa kwa Watumishi wa TEMESA wa tatu kulia ni Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan.
Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase OleKujan ( wa sita kulia waliosimama) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa Mafunzo ya teknolojia ya umeme wa jua (Solar Photovoltaic Technology) kutoka TEMESA.(Picha Zote na Theresia Mwami wa TEMESA).

Na Theresia Mwami TEMESA

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Mhandisi Manase Ole Kujan, wamewatunuku baadhi ya waandisi na mafundi wakati akifunga mafunzo ya umeme wa jua (Solar Photovoltaic Technology) kwa watumishi wa TEMESA.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa wiki mbili, yametolewa kwa kushirikia na chuo kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha Fizikia, kwa watumishi 20 wa TEMESA kupata mafunzo ya nadharia na vitendo.

Katika hotuba yake Mhandisi Manase aliushukuru uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuendesha mafunzo hayo kwa wataalamu wa TEMESA, kwani yatawapa uwezo wahandisi na mafundi wa kuendana na mabadiliko ya sayansi na tekenolojia.

“Nishati ya umeme wa jua imeshika kasi kwa sasa na inatumiwa sana katika maeneo ambayo umeme wa kawaida haujafika hivyo basi kwa mafunzo haya wahandisi na mafundi wetu wataweza kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuandaa na kutekeleza miradi itakayosaidia kuondokana na tatizo la umeme nchini.” Alisema Mhandisi Manase.

Aidha, TEMESA inasimamia miradi mbali mbali ya teknolojia ya umeme wa jua nchini ikiwemo mfumo wa teknolojia ya umeme wa jua kwa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Songea, mfumo wa teknolojia ya umeme wa jua katika ofisi ya Rais Utumishi, kusimamia na kuhakiki mifumo ya teknolojia ya umeme wa jua inayofungwa vijijini katika mikoa ya Geita, Kigoma Ruvuma na Tabora iliyo chini ya REA, kusimamia matengenezo ya mifumo ya teknolojia ya umeme wa jua katika ofisi zote za TRA pamoja na miradi mbali mbali ya taa za kuongozea magari barabarani zinazotumia teknolojia ya umeme wa jua.

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI,APRIL 24

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA CHUO CHA KILIMO FAFU CHINA

$
0
0
Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete akiwa pamoja na uongozi na wanafunzi wa Tanzania wanaosoma chuo cha Kilimo na Misitu FAFU.
Dkt Kikwete akiwa katika chuo cha Kilimo FAFU ambapo alialikwa kutembea leo hii.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete jana Aprili 23, 2016 alitembelea Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha jimbo la Fujian (Fujian Agriculture and Forest University-FAFU) kilichopo katika mji mkuu wake Fu Zhou.

Mwenyekiti alikaribishwa chuoni hapo kuonyeshwa hatua ambazo jimbo hilo imepiga katika kuendeleza kilimo cha kisasa, teknolojia ya kuzalisha mbegu na teknolojia ya kupambana na magonjwa na wadudu waharibio mazao. Akiwa chuoni hapo, alikutana pia na wanafunzi wa kitanzania wanaosomea shahada za uzamivu kwa ufadhili wa serikali ya China.

Katika mazungumzo yake na Mkuu wa Chuo hicho Profesa Lan Siren, Mhe Kikwete amependekeza kuanzishwa kwa mahusiano na ushirikiano baina ya Chuo Cha Kilimo SUA na Chuo hiko. Pia amependekeza wanafunzi na wakufunzi wa chuoni hapo kuja Tanzania kufanya mafunzo ya vitendo na tafiti zao.

Kufuatia pendekezo hilo, Rais wa Chuo hicho ameelezea utayari wa Chuo hicho kushirikiana na SUA. Aidha, ameelezea kulipokea ombi la Mwenyekiti la kuongeza nafasi za masomo kwa vijana wa Tanzania na kuahidi kulifanyia  kazi ombi hilo.

Chuo Kikuu cha FUFA kina takribani wanafunzi elfu arobaini (40,000) ambapo wanafunzi kutoka Afrika ni takribani 120 kati yao watatu tu (3) wanatoka nchini Tanzania.

Mhe Kikwete yuko nchini China kwa ziara ya kichama iliyotokana na mualiko rasmi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China Mhe Xi Jinping.

NAPE AZINDUA TAMASHA LA KIMATAIFA LA FILAMU MJINI ARUSHA

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifunua pazia kuashiria uzinduzi wa Tamasha la kimataifa la filamu la Tanzanite mjini Arusha.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (mwenye kaunda suti ya kijivu) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Ntibenda kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na wadhamini kwenye uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mkoani Arusha .

Waziri Nape aliwaambia wadau na waigizaji wa Filamu waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha hilo kuwa hii ni moja ya hatua kubwa kwenye historia ya filamu nchini na kuahidi Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha haki za wasanii hazipotei wala haziliwi na wajanja.
Mkurugenzi wa Tanzanite One ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha, Ndugu Faisal Juma akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mjini Arusha kwenye hotel ya Mt. Meru.
Viongozi wa Arusha wakiwa .
Baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Tanzanite.
Yvonne Cherry 'Monalisa' pamoja na mama yake, Suzan Lewis 'Natasha' (katikati) wakifuatilia sherehe uzinduzi wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Tanzanite kwenye hotel ya Mt. Meru

Uganda imetangaza rasmi kutumia Bandari ya Tanga nchini Tanzania kusafirishia mafuta ghafi yake.

$
0
0

Hatimaye Serikali ya Jamhuri ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia Bandari ya Tanga nchini Tanzania kusafirishia mafuta ghafi yake. 
Uamuzi huo umetangazwa na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika Jijini Kampala Uganda. 

Ujumbe wa Tanzania ulio kamilisha mazungumzo hayo na hatimaye kushuhudia utangazwaji wa hatua hiyo uliongozwa na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa .

Jopo la wataalamu kutoka Tanzania lililoongozwa na Mhe. Prof. Sospeter Muhongo bado wako jijini Kampala kukamilisha mpango huo wa Bomba la Mafuta Ghafi ambapo pia nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati zinatarajia kunufaika.

 

 
Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,

Dar es Salaam

23 Aprili, 2015



MONGELLA ATOA SAA 24 KOMPYUTA ILIYO IBWA IPATIKANE.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa MWANZA John Mongella ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Ally Mkaripa,kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata kompyuta iliyo ibwa usiku wa kuamkia April 22,2016 kwenye chumba kinacho tumika na mifumo ya ukusanyaji mapato na uaandaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR)

Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kilicho fanyika katika ukumbi wa halmashauri,ambapo taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri.

“OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana,amesema Mongella na kuongeza ,sisi tunajua Nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo komputa hiyo.

Akizungumza kando ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri,kaimu mhazini wa halmashauri hiyo Baraka Munuo,alidai kupokea taarifa za kupotea kwa Komputa hiyo kutoka kwa afisa TEHAMA wa halmashauri ya Ukerewe akimuelezea upotevu huo.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa MWANZA, amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ukerewe,, kupitia mafaili na kubaini watumishi waliofanya kazi katika kituo hicho kwa muda mrefu, jambo ambalo mkuu wa mkoa amedai linachangiawatumishi kufanyakazi kwa mazoea,”Mkurugenzi nakuagiza pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote waliokaa katika kituo hiki kwa muda mrefu, haiwezekani mtu amekaa hapa miaka ishirini na moja halafu uniambie kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana, alisema Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili yao na kama kuna mtumishi aliye kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo kingine.

Awali akisoma taarifa ya wilaya hiyo, mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti,alimwambia mkuu wa mkoa kuwa hali ya ulinzi na usalama ni shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo huku akisema wilaya imefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu kilicho kuwa kimepiga kambi katika Wilaya hiyo kwa zaidi ya miezi 6.

Mkuu wa mkoa wa yupo katika ziara yakujitambulisha na hii ikiwa ni wilaya yake ya saba,Mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi, Magu, Nyamagana, Ilemela na Kwimba na hii ya Ukerewe inakuwa wilaya ya saba huku akiwa amebakiza wilaya moja ya Sengerema yenye halmashauri za Buchosa na Sengerema yenyewe.

NEWZ ALERT;MWANAMUZIKI NGULI WA CONGO PAPA WEMBA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Mwanamuziki Papa Wemba enzi za Uhai wake.

Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo.

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu Papa Wemba amefia hospitali alikokimbizwa mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akiwa katika onesho jukwaani.

Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa na kujizolea mashabiki wengi.
 Papa Wemba akiwa jukwaani kwa mara ya mwisho jijini Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia
 Papa Wemba aanguka na kupoteza fahamu katikati ya onesho
Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wamepanda jukwaani. Hali ilizidi kuwa mbaya wakamkibiza hospitali ambako alikata roho

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI KATIKA VIWANJA VYA MAISARA.

$
0
0
Vikundi vya mazoezi vikiwa katika matembezi ya hiari ya kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika kuanzia Mazizini Wilaya ya Magharibi B na kumalizikia Maisara Mjini Unguja.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi (katikati) akiongoza Matembezi ya hiari ya kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika kuanzia mazizini na kumalizikia maisara mjini Unguja.kulia yake ni Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na kushoto yake ni katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Juma Malik Akili.

Vikundi mbalimbali vya Mazoezi vikifanya mazoezi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Maisara katika maadhimisho ya Siku ya malaria Duniani ambayo yamefanyika Mjini Unguja.
Vikundi mbalimbali vya Mazoezi vikifanya mazoezi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Maisara katika maadhimisho ya Siku ya malaria Duniani ambayo yamefanyika Mjini Unguja.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (wa mwanzo ) akishiriki katika mchezo wa kuvuta kamba kwenye maadhimisho hayo ambapo timu ya Baraza la Wawakilishi ilipambana na Wizara ya Afya ambapo Afya ilipata ushindi. 
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimkaribisha Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika Maisara Mjini Unguja.kulia yake ni Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na Kushoto yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Juma Malik Akili.

PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka wananchi wa wanaosafiri mara kwa mara kwa ajili ya harakati zao za maisha kuchukua vyandarua na kuvitumia wanapokuwa safarini ili kujikinga na maradhi ya Malaria.

Akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani katika viwanja vya Maisara, Mjini Zanzibar, Balozi Seif alisema licha ya Zanzibar kuwa na kiwango cha chini ya asilimia moja cha Malaria, utafiti unaonyesha watu wanaogunduliwa kuugua maradhi hayo hivi sasa ni wale wenye utaratibu wa kusafiri nje ya Zanzibar.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kwa dhati kuimarisha afya za wananchi na itaendelea kuboresha huduma za afya sehemu zote na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi hizo.

Hata hivyo alisema wakati Zanzibar inajivunia mafanikio katika vita dhidi ya Malaria bado maradhi ya Kipindupindu yanaendelea kuwa tishio kwa wananchi na kuwataka kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya.

Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Afya Juma Malik Akili alisema katika kumaliza Malaria kuanzia tarehe 25 mwezi huu watatoa vyandarua 760,000 vilivyotiwa dawa bure kwa wananchi katika Wilaya zote za Zanzibar.

Amewashauri wananchi kuvitumia vyandarua hivyo kikamilifu kwani inaonekana kuwa ndio njia kubwa inayosaidia kukinga Malaria.

Katika maadhimisho hayo, wananchi na vikundi vya mazoezi wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais walifanya matembezi ya hiari yaliyoanza Mazizini, Wilaya ya Magharibi B na kumalizia viwanja vya Maisara, Mjini Zanzibar.

MASHINDANO YA UBINGWA WA MCHEZO WA CHESS AFRIKA KANDA YA 4.2 YAANZA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Chess Tanzania (TCA) Bw. Geofrey Mwanyika akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Ubingwa wa Afrika, Kanda ya 4.2 ya Mchezo huo jana jijini Dar es Salaam. Kanda ya 4.2 inahusisha Timu kutoka nchi za Misri, Ethiopia, Eritria, Sudan, Sudani Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia,Djibouti na wenyeji Tanzania.
Rais wa Chama cha Mchezo wa Chess Malawi, ambaye pia ni ni Mbunge mstaafu wa wa Bunge La nchi hiyo Mhe. Kezzie Msukwa akizungumza namna Mhcezo huo Mchezo huo ulivyopiga hatua nchini Tanzania ukilinganisha na kwao jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Ubingwa wa Afrika, Kanda ya 4.2 ya Mchezo huo jana jijini Dar es Salaam. Kanda ya 4.2 inahusisha Timu kutoka nchi za Misri, Ethiopia, Eritria, Sudan, Sudani Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia,Djibouti na wenyeji Tanzania. Mbunge huyo wa zamani wa Malawi yupo nchini kama Mwamuzi katika mashindano hayo.
Mwenyekiti wa Mfuko wa mchezo wa Chess Tanzania (TCF) Bw. Vinay Choudary akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Ubingwa wa Afrika, Kanda ya 4.2 ya mchezo huo jana jijini Dar es Salaam. Kanda ya 4.2 inahusisha nTimu kutoka nchi za Misri, Ethiopia, Eritria, Sudan, Sudani Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia,Djibouti na wenyeji Tanzania.Mashindano hayo yameanza jana tarehe 23 April hadi April 31ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya Ubingwa wa Chess Afrika, Kanda ya 4.2 kimchezo huo wakiendelea kuchuana jana jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yanendelea katika Ukumbu uliopo Hotel ya Peackok ambapo mshindi katika mashindano hayo atajinyakulia kitika cha Euro 3000.
Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya Ubingwa wa Chess Afrika, Kanda ya 4.2 kimchezo huo wakiendelea kuchuana jana jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yanendelea katika Ukumbu uliopo Hotel ya Peackok ambapo mshindi katika mashindano hayo atajinyakulia kitika cha Euro 3000.

WAZIRI MUHONGO AWASILI JIJINI DAR JIONI HII AKITOKEA NCHINI UGANDA KUKAMILISHA DILI LA BOMBA LA MAFUTA

$
0
0


 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kati) akiwasili jijini Dar es salaam jioni hii, akitokea Jijini Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, alioongozana nao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akionyesha kwa wanahabari, mpango wa ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda mpaka Jijini Tanga, mara tu baada ya kuwasili nchini akitokea jijini Kampala. Mbali na kunufaika kwa Watanzania kupitia Mpango huo, pia utazinufaisha nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio walipokuwa wakimsubiria Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alierejea jijini Dar es salaam leo akitokea Jijini Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga. 

CLOUDS MEDIA GROUP YATEMBELEA NYUMBANI KWA BALOZI MANONGI, NEW YORKCLOUDS MEDIA GROUP YATEMBELEA NYUMBANI KWA BALOZI MANONGI, NEW YORK

$
0
0
Mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Tovako Manongi akimkaribisha Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga nyumbani kwake siku ya Jumamosi April 23, 2016.Mkurugenzi huyo alitembelea nyumbani kwa Balozi jijini New York akiongozana na baadhi ya wafanyakzi wake ambao walikuja nchini Marekani kwa ajili ya tamasha la Radio lililofanyika jijini Las Vegas. Picha na Vijimambo New York.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi akiwatambulisha maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa kwa Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bwn, Joseph Kusaga (hayupo pichani) siku ya Jumamosi April 23, 2016.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Bwn. Joseph Kusaga akitambulisha timu yake kwa Mhe. Balozi Tuvako Manongi.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi, mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bwn. Joseph Kusaga.
Mkurugenzi wa Clouds Medea Group, Bwn. Joseph Kusaga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Tuvako Manongi na mkewe.
Timu nzima ya Clouds Media Group iliyohudhuria Tamasha la Radio nchini Marekani ikiwa katika picha ya pamoja na Balozi Tuvako Manongi na mkewe.Kutoka kushoto ni Saleh Mohammed, Daudu Lembuya, Dj Venture, Mhe. Balozi Tuvako Manongi, Mkurugenzi Joseph Kusaga, Mama Manongi, Dj Peter Moe na Jackson Joseph.

Kushoto ni Brightus Titus, Getrude Clement na NY Ebra wakiwa katika picha ya pamoja.

Siku hiyo pia lilifanyika kusanyiko la maDJ mbalimbali wa zamani waishio nchini Marekani ambao walikutana kwa nyama choma na kubadilishana mawazo. MaDj hawa ni wachache miongoni mwa wengi wanaounda kundi la Tanzania Djs Worldwide ambalo limeanza miezi mitatu iliyopita, na mpaka sasa lina wanachama wapatao 70. Kusanyiko lao la kwanza lilifanyika Escape One March 24 (lirejee hapa)



JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA LATOA TAMKO KUHUSU MWENENDO WA BUNGE LA BAJETI

$
0
0
LASIKITIKA WABUNGE WA BAADHI YA VYAMA VYA UPINZANI KUTOKA UKUMBINI, LAPONGEZA VIKAO KUTOKUWA LIVE, LAIOMBA SERIKALI NAYO KUACHA KUONYESHA LIVE SHUGHULI ZAKE ZAIDI YA ZILE ZINAZOHUSIANA NA SIKU ZA MAPUMZIKO
Katibu wa Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania, Mtela Mwampamba akizungumza na waandishi wa habari leo, Ubungo mjini Dar es Salaam, kuhusu mwenendo wa Bunge la Bajeti na hatua ya Wabunge wa baadhi ya Vyama Vya upinzani kutoka nje ya ukumbi na kutotoa bajeti mbadala ya Kambi ya Upinzani. Kulia ni Mwanachama wa Jukwaa hilo, Simon Simalenga (Picha na Bashir Nkoromo).
 TAARIFA KAMILI NI IFUATAYO KAMA ILIVYOTOLEWA NA MWAMPAMBA

JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA (JUHWATA)

TAMKO JUU YA MWENENDO WA SHUGHULI ZA BUNGE

Ndugu wanahabari poleni na majukumu ya kulihabarisha Taifa, ndugu wanahabari tulio mbele yenu ni wajumbe wa jukwaa huru la Wazalendo Tanzania ( JuhwaTa). Kama mnavyojua jukwaa huru la WAzalendo ni taasisi huru inashughulikia mambo mbalimbali ya kitaifa ikiwepo, Mijadala, Makongamano,Matamko na Elimu kwa umma kuhusiana na mambo mbalimbali ya kijamii,kisiasa na kiuchumi kwa maslahi mapana ya Taifa.


Leo tumewaita, Jukwaa likiwa na masikitiko makubwa kuhusu mwenendo wa shughuli za bunge, hususan bunge linaloendelea sasa pale Dodoma, bunge la bajeti, Kwa mujibu wa Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inalitaja bunge kuwa ndio chombo kikuu ambacho kitakuwa na madaraka , kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri serikali na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake

Kumekuwepo na tabia kwa baadhi ya wabunge kususia mijadala,vikao na shughuli nyingine za bunge kwahiyo wamekuwa wakivunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 63 (2) na kutupelekea wananchi kukosa fursa ya uwakilishi kutoka wa wale tuliwachagua huku wao wakiendela kupata stahiki zao kwa maslahi yao. Kwa mfano, Watanzania tunatambua kwamba kuna baadhi ya wabunge walisusia bunge maalum la katiba matokeo yake wananchi tukakosa mawazo mbadala kutoka kwao na walioumia ni wananchi wanyonge na sio wao.

Jukwaa linasikitika sana, Mnamo 22/04/2016, Kambi Rasmi ya Upinzani  Bungeni, ilishindwa kuwasilisha Mapendekezo Mbadala wa Bajeti Ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mujibu wa kanuni za bunge kwa visingizio vya kwamba serikali haina Mwongozo wa kuiongoza nchi, Serikali kubana sana Matumizi bila kuwashirikisha wao kama Wabunge na Hatua mbalimbali ambazo mh Rais John P Magufuli za  Kutumbua majibu hadharani bila kutoa mchakato  wa watumbuliwa wa ufisadi kujitetea kwanza. 

Wananchi tunaamini kabisa kuwa, Kambi Rasmi imeshindwa kuwasilisha na kutoka nje kwa sababu mosi, Mpango Uliowasilishwa Bungeni na serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mapendekezo ya Bajeti Ya Ofisi Ya Waziri Mkuu, umepokelewa vema na wananchi  na wasomi  huku wakiupongeza kwani Mpango umejikita katika, Ujenzi wa reli ya kati kwa standard gauge, Kuboresha Makusanyo ya Kodi, Vita Vya Ufisadi na Ubadhirifu, n.k. Pili Kambi Rasmi inawezekana kabisa hawakuwa na Hoja ya kupinga na njia pekee ni kutoka nje kuunga mkono Mapendekezo ya serikali.


Ndugu wanahabari ikumbukwe, Utaratibu, michakato na kuonea haya dhidi ya Mafisadi kimekuwa ni kilio cha wananchi wengi na tunashukuru mh Rais kusikia kilio chetu na kuweza kutufuta machozi yetu kwa vitendo. Pia ikumbukwe nchi hii imeliwa na Mafisadi kwa kuendekeza Michakato na Utaratibu, na sisi kama wananchi hatutakubali michakato na taratibu katika kushughulikia mafisadi wa Taifa iendelee. Na katika kumuunga mkono mh Rais, siku ya hotuba ya uzinduzi wa bunge la 11,Mh Rais alituomba Wananchi wazalendo tumuunge mkono katika vita aliyoianzisha ya kupambana na Mafisadi, Kubana matumizi, Kurudisha nidhamu ya Utumishi wa Umma, Uchapakazi na Uzalendo na sisi kama wananchi wanyonge tunauunga mkono jitihada hizo na tunamwambia na kumtia moyo kwamba tupo nyuma yake katika vita hii ijapokuwa wapo wachache wanaojaribu kuirudisha na kuhujumu jitahada zako kwa maslahi yao binafsi na Mafisadi wanaowatumia.


Ndugu wanahabari, sote tunajua mh Rais alipokuwa akiomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi alikuwa akitoa ahadi na viapombele mbalimbali na sasa mh rais amezidi kutekeleza ahadi zake kwa vitendo kwa wananchi aliowaahidi, mfano Kuwa na baraza dogo la Mawaziri, Elimu bure, Kubana Matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza fedha zitakazo okolewa kwenda kutatua kero sugu za wananchi wake, kupambana na Mafisadi nk. Sasa tunashangaa kuwekuwepo na baadhi ya watu wakiwemo wabunge kupinga na kuhujumu waziwazi juhudi na jitahada za utekelezaji wa ahadi za mh Rais. Kama vile Kubana matumizi ya fedha za bunge kwa wabunge kutosafiri kwenda nje ya nchi kwa kisingizio cha kwenda kukagua ujenzi wa balozi zetu ilihali tunajua wao sio mainjinia wa majengo na pesa hizo kuelekezwa katika kutengeneza madawati ya wanafunzi na kila mbunge wa jimbo atapewa madawati 600 kwa ajili ya jimbo lake. Hivyo tunaamini wabunge nao walitoa ahadi zao kwa wananchi wao kwahiyo tunaomba na tunawashauri wajikite katika kutekeleza ahadi walizowaahadi wananchi wao kuliko kufanya malumbano,hujuma dhidi ya jitihada za utekelezaji wa ahadi za mh Rais.


Sote tunajua kauli mbiu ya mh Rais ni “Hapa Kazi Tu”  anataka awamu ya tano watu wafanye kazi, lakini bunge  lilipokulinaoneshwa moja kwa moja kwenye television tulikuwa tukishuhudia mijadala isiyo na tija kwa taifa, na zaidi Bunge lilikuwa uwanja wa kampeni za kisiasa,Vijembe, Kejeli, Mipasho na Vitimbi mpaka kufikia wao wenyewe kuliita bunge, “ Silly Season” na wengine wakiliita Bunge Comedy hivyo bunge kukosa Tija kwa Taifa na kupoteza kabisa maadili na kusudio la wananchi kufuatilia mijadala ya bunge letu hadi wengine hususan vijana kuacha kufanya kazi na kutumia muda mwingi kuangalia bunge kujifunza yasiyokuwa na tija kwa Taifa letu. Sisi kama Jukwaa tunawashauri wabunge wasijikite kwenye bunge kuoneshwa live bali wapige kazi kwa mustakali wa maendeleo ya Watanzania, na Wananchi watajua tu. Imefikia hatua Wabunge wanagoma kuchangia hoja bungeni kwa sababu tu familia , marafiki, ndugu na jamaa zao hawatawaona live. Sababu nyingine ni kuwa serikali haina Mwongozo na inatumia inatumia mwongozo wa awamu ya nne, sheria sio vacuum ndio maana Mawaziri hata kama bado hawajapewa mwongozo bado wanaendelea kutumia instruments za mwongozo iliyopita na kupata mwongozo mpya na bora ni mpaka serikali ifanye utafiti.


Pia Ukawa wameendelea kuhujumu shughuli za bunge kwa kuwazuia wabunge wao wasiende kwenye kamati mbili za bunge za PAC na LAAT na kusabisha kamati hizo kukosa uongozi. Tunaishauri serikali nayo shughuli zake zote zitakazokuwa zinaenda moja kwa moja (live) zifanyike jioni au siku za mapumziko ya kitaifa.

Kwa kuhitimisha ndugu wana habari, tukirejea kauli ya Mh Mbowe na Ukawa wakijinadi kuwa mh Rais anatekeleza Ilani yao,sasa tunashangazwa na vitendo vyao vya ghafla vya kuanza kupinga na kujihujumu wao wenyewe kwa kutekelezwa kwa Ilani yao, tunapatwa na mashaka na nia yao katika Taifa hili na uenda wakawa wanatumika na Mafisadi na watu wasiokuwa na nia njema na taifa hili maana hata ile agenda ya ufisadi hatuisikii tena, Pia waache tabia ya kususa hata kama kasi ya Mh Rais ni kali ili tusiendelee kuwakosesha wananchi haki zao kama tulivyoona pale Zanzibar baada ya Chadema kuwashawishi Viongozi wa CUF kususia na  kuwazuia wana CUF  kushiriki uchaguzi  wa marudio na kuwapelekea kukosa uwakilishi ilihali wao wana wawakilishi ndani ya bunge.


Jukwaa tunaomba na tunatoa ushauri kwa Uongozi wa Bunge, kuchukua posho na ikiwezekana kukata mishahara ya wabunge wote wasioshiriki vikao na shughuli za bunge na fedha hizo zipelekwe kwenye matumizi mengine ya kutatua kero za wananchi ikiwemo upatikanaji wa chaki mashuleni.


Ndugu wana habari, Kuna baadhi ya watu pamoja na Wabunge wa Ukawa wakiongozwa na mh Mbowe, wamekuwa wakilalama kwamba Rais anakiuka katiba na sheria za kwa kubadili matumizi ya fedha. Sheria ya Usimamizi wa Bajeti {Appropriation Act ya 2015 (6)Waziri wa Fedha anapewa mamlaka ( Baada ya Maagizo au Mashauriano ya ndani ya serikali) Lakini pia Katiba inamruhusu Rais ndani ya miezi baada ya kuchaguliwa kuweza kubadili matumizi ya fedha . Bajeti ikishapitishwa inakuwa ya serikali na endapo itakuwa imezidi , fedha zile Waziri anaweza kuzipangia matumizi mengine au akasaini na Rais akatangaza maana ndiye anayewateua.


Jukwaa linaiomba serikali itusaidie maana wao wana mkono mrefu ili tujue dhamira zao ni nini? Ikiwa kama Mpango wa serikali ni Kutoa elimu bure, ikiwa Mpango ni kufufua Viwanda,Ikiwa Mpango ni Kubana Matumizi, Ikiwa Mpango ni Kupambambana na rushwa, ikiwa Mpango ni kujenga barabara, Ikiwa 41% ya Bajeti ni kwa ajili ya Maendeleo nk kama hawayataki haya kwa Watanzania, Je hawa wana Agenda gani nyuma?

Mwisho Mh Rais alitoa Rai, “Atakayejaribu kumkwamisha Atakwama Yeye


Imetolewa 24/04/2016 na :-

MTELA MWAMPAMBA 0755 17 89 27­, 0627 94 95 15

KATIBU JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA 

CHAMA CHA WAWEKEZAJI BINAFSI KATIKA SEKTA YA ELIMU CHAZINDULIWA

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Sekta ya Elimu Tanzania (TAPIE) ambaye pia ni Mmilikiwa Shule ya Tusiime Bw. Albert Katagira akizungumza wakati wa uzinduzi na mkutano wa kwanza wa chama hicho jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Chama hicho Bw.Kachwamba Ansar na wapili kulia ni Makamu Mwenyekiti Bw.Johson Ishengoma.
Mwanachama wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Sekta ya Elimu (TAPIE) ambaye pia ni mmiliki wa Shule ya Awali na Msingi ya Fortune iliyopo Tabata Kinyerezi Bw.Hope Kaiza akichangia hoja wakati wa uzinduzi na mkutano wa kwanza wa chama hicho jana jijini Dar es Salaam.
Mwanachama wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Sekta ya Elimu (TAPIE) Bw. Mahamoud Mringo (aliyesimama) akifafanua jambo wakati wa uzinduzi na mkutano wa kwanza wa chama hicho jana jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Albert Katagira na Makamu Mwenyekiti wake Bw. Johnson Ishengoma.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Wawekezaji BinafsiBaadhi ya wanachama wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Sekta ya Elimu (TAPIE) wakifuatilia mada wakati wa uzinduzi wa chama hicho jana jijini Dar es Salaam.Picha na: Frank Shija,WHUSM
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images