Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 821 | 822 | (Page 823) | 824 | 825 | .... | 1896 | newer

  0 0  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Biashara wa Oman, Dkt. Ally Mohamed Al Sunaidy Ofisini kwake jijini Dar es salaam, Aprili 14, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Biashara wa Oman, Dkt. Ally Mohamed Al Sunaidy (wapili kushoto) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 14, 2016.Wapili kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri wa Biashara wa Oman, Dkt Ally Mohamed Al Sunaidy baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 14, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Magufuli akisaini makubaliano ya kuikaribisha Sudan kusini katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Rais wa Jamhuri ya Sudan kusini Mhe. Salva Kiir akisaini hati za makubaliano ya kuikaribisha rasmi Sudan kusini kuwa Mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Magufuli akizungumza wakati wa kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Sudan kusini Mhe. Salva Kiir Salaam katika ziara yake ya kikazi lenye dhumuni la kujiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Rais wa Jamhuri ya Sudan kusini Mhe. Salva kiir akiagana na Jaji Mkuu wa Tanzania jaji O5thman Chabde mara baada ya kumaliza kutia saini ya makubaliano ya nchi yake kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Magufuli akiaga viongozi mbalimbali wa ikiatifa na kimataifa mara baada ya kumaliza kutia saini ya makubaliano ya nchi ya Sudan Kusini kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Na. Immaculate Makilika – MAELEZO

  Rais wa Jamhuri ya Sudani ya Kusini Salva Kiiri ametia saini makubaliano ya mkataba wa kujiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza baada ya kutia saini mkataba huo, Rais Salva Kiiri amesema uamuzi wa nchi yake kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki si tu kuwa kunaimarisha ujirani ulipo kati ya nchi hizo, lakini pia kunaimarisha ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki pamoja na watu wake ikiwa ni pamoja na kuendelea kukuza utamaduni wa Afrika.

  “Naishukuru Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa kukubali Sudani ya Kusini kuwa mwanachama wa Jumuiya, na sasa Sudani ya Kusini imepata sehemu sahihi kwa kujiunga na Jumuiya hii ambayo inalenga kuleta maendeleo kwa wananchi wake” amesema Rais Kiir.

  Rais Kiir amesema “tunajua malengo makubwa ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ni kuleta maendeleo kwa wananchi wake, na tunashuhudia kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mfani bora Afrika na duniani kwa ujumla”.

  Ameongeza kuwa Sudani ya Kusini imeona fursa zilizopo katika Jumuiya hii ikiwa ni pamoja na soko la pamoja (Common markert). Tayari tumetengeneza mifumo itakayosaidia ushiriki wetu katika Jumuiya ikiwemo kuanzishwa kwa Wizara itakayoshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, ikiwa ni pamoja na kutunga sheria mbalimbali zitakazowezesha kupatikana kwa Amani ya kudumu nchini humo.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amepongeza juhudi zilizofanywa na Sudani ya Kusini na hatimaye kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ikiwa ni muda mfupi tu tangu nchi hiyo ipate uhuru wake mnamo Julai 20, 2012.

  Rais Magufuli amesema kuwa siku zote Sudani ya Kusini imekuwa sehemu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa uchumi wake, utamaduni wake, lugha pamoja na historia yake na inaunganishwa na nchi za Jumiya hii kwa barabara pamoja na mto Nile.

  Aidha, Rais Magufuli “amesema malengo ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji, kutoa bure huduma na uhuru wa wananchi kwenda popote ndani ya Jumuiya. Hata hivyo, Jumuiya hii inakumbwa na machafuko ya mara kwa mara na kuwa kikwazo kwa maendeleo ya uchumi wake”.

  Amesema Sudani ya Kusini imekubaliwa kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa kuwa imetimiza makubalino yaliyowekwa na Jumuiya ikiwemo kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

  Naye, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi, Dkt. Augustine Mahiga, amesema kuwa Sudani ya Kusini inakuwa mwanachama wa sita wa Jumuiya hiyo, na kuwa ushirikiano wa kiuchumi uliopo katika nchi hizi utakuwa mfano wa kuigwa kwa nchi zinazoendelea.

  Sudani ya Kusini iliomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki mnamo Novemba 10, 2012, ikiwa ni chini ya miezi minne tangu nchi hiyo ipate uhuru wake.

  0 0


  Mount Kilimanjaro, the highest mountain in Africa, and the highest free-standing mountain in the world, was declared Africa’s leading tourist attraction in 2016 during the World Travel Awards Africa and Indian Ocean Gala Ceremony in Zanzibar. The red carpet event attended by hundreds of tourism industry leaders was hosted by Diamonds La Gemma Dell’est,Nungwi the northern tip of Zanzibar, Tanzania on 9th April 2016.

  Tanzania Tourist Board is honoured to see that Mt. Kilimanjaro has been voted as the leading tourist destination in Africa. This nomination will definitely contribute towards our efforts in promoting Destination Tanzania, especially in making the world know that Tanzania is home to Mt. Kilimanjaro; the pinnacle wonder of Africa, and as many know, it is affectionately known as the rooftop of Africa.

  Mount Kilimanjaro is the world’s most accessible high snow–capped summit, a beacon for visitors from around the world and is also a UNESCO World Heritage Site.

  In addition to Mt. Kilimanjaro, the following Tanzanian tourism companies also won different awards in various categories. http://www.worldtravelawards.com/about

  Tanzania Tourist Board congratulates all companies nominated at the World Travel Awards Africa & Indian Ocean Gala Ceremony and is confident that their victory is a very strong tool in the marketing and promotion of destination Tanzania. Likewise, Tanzania Tourist Board thanks all tourism stakeholders for voting for Mount Kilimanjaro and other Tanzania tourism facilities and making them become winners.

  ——————-
  World Travel Awards™ was established in 1993 to acknowledge, reward and celebrate excellence across all key sectors of the travel, tourism and hospitality industry. Today, the World Travel Awards™ brand is recognized globally as the ultimate hallmark of quality, with winners setting the benchmark to which all others aspire.

  Each year World Travel Awards™ covers the globe with a series of regional gala ceremonies staged to recognize and celebrate individual and collective successes within each geographical region. 

  Issued by 

  TANZANIA TOURIST BOARD

  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia Watu Wenye Usonji Tanzania (NAPAT) Dkt.Stella Rwezaula(wa tatu kulia) akiongea na waandishi wahabari kuhusu matembezi ya hiyari kuadhimisha siku ya usonji Aprilli 16, kushoto ni Katibu wa Chama cha Kuhudumia Watu Wenye Usonji (NAPAT) Bi. Ella Mgalla na wengine ni wajumbe.(Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)


  Na Lorietha Laurence-Maelezo

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dk.Abdalla Possi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika matembezi ya hiyari ya kuazimisha siku ya watoto wenye usonji Aprili 16 mwaka huu.

  Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama cha Kuhudumia Watu Wenye Usonji Tanzania (NAPAT) Dkt.Stella Rwezaula ameeleza kuwa lengo la matembezi hayo ni kutoa elimu kwa jamii kuhusu watu wenye matatizo ya Usonji.

  “Jamii imekuwa ikiwanyima uhuru watu wenye usonji kwa kuwafungia ndani na hivyo kuwanyima haki zao za msingi ikiwemo kupata elimu ” alisema Dkt.Rwezaula.

  Aliongeza kuwa watu wenye matatizo ya usonji wanapopatiwa msaada wa haraka na unaostahili ikiwemo huduma ya afya husaidia kuimarisha hali zao na baadaye kuwa msaada katika jamii yake.

  “Usonji ni tatizo linalotokana na hitilafu katika ukuuaji wa ubongo wa mtoto na kupelekea mtoto kuwa na matatizo katika mawasiliano na mahusiano ya kijamii na utambuzi lakini linapogundulika haraka inasaidia kuimarisha hali ya mtoto“ alisema Dkt.Rwezaula.

  Naye Katibu wa Chama cha Kuhudumia Watu Wenye Usonji (NAPAT) Bi. Ella Mgalla ametoa wito kwa wazazi kuwasaidia watoto wenye usonji kwa kuwapeleka katika shule maalum ili waweze kupata elimu.

  Pia ameeleza kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni ukosefu wa waalimu maluum wa kuwafundisha watoto wenye usonji pamoja na upungufu wa shule maalum ambapo mpaka sasa kuna shule 8 Tanzania nzima.

  “Ninaiomba serikali iweze kutusaidia kwa kutoa mafunzo maalum kwa waalimu ambao watakuwa wakiwahudumia watoto wenye matatizo ya usonji na kuongeza idadi ya shule ambapo kwa sasa ni mikoa minne tu inayotoa huduma hiyo ikiwemo Dar es Salaam shule mbili, Arusha shule nne, morogoro shule moja na Mwanza shule moja” alisema Bi.Mgalla

  Chama cha Kuhudumia Watu Wenye Usonji (NAPAT) kimeanzishwa mwaka 2012 kikiwa kinajumuisha wanachama 53 ambao ni wazazi, walezi na waalimu wa watoto wenye usonji.

  0 0

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imesikitishwa na kulani viakli matukio ya mauaji ya wazee kumi (10) yaliyotokea wilaya ya Nzega, mkoani Tabora kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi, 2016.

  Inaelezwa kuwa, miongoni mwa chanzo cha mauaji ya wazee ni imani za kishirikina, uchu wa kumiliki mashamba na visasi mambo ambayo Serikali imekuwa ikiyakemea vikali. Wizara inawataka wananchi kushirikiana na uongozi wa Wilaya ya Nzega, kuhakikisha kuwa watuhumiwa wa mauaji haya wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali ili kuwa fundisho kwa watu wengine. 

  Wizara inasisitiza kwamba wazee ni binadamu, na wanayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yao kwa mujibu wa Sheria za nchi. Vitendo vya mauaji ya kikatili wanavyofanyiwa wazee vinasababisha hofu kubwa kwa wananchi. Mauaji hayo yanawakosesha amani na vinadhohofisha ari ya kufanya shughuli za za maendeleo ya familia na taifa kwa ujumla. 

  Familia inayoishi na mzee anayewindwa, itatumia muda mwingi kutekeleza jukumu la ulinzi na hivyo kupunuza tija na uzalishaji wa mwananchi mmoja na familia kawa ujumla. Kwa kutambua hili Wizara inahimiza wadau wote kuunga mkono jitihada za Serikali katika ulinzi wa wazee na kuboresha huduma zao ili kuelekeza nguvukazi katika uzalishaji. 

  Wizara inapenda kutoa pole kwa familia ambazo zimeguswa na mauaji ya wazee waliopoteza maisha kwa kuuawa kinyama. Wizara inaitaka jamii itambue kuwa wazee wana haki ya kuthaminiwa utu wao, kupata huduma stahiki, na kushiriki haki zote za msingi bila ubaguzi wowote ambao unaweza kuhatarisha maisha yao ikiwemo haki yao ya kuishi. 

  Aidha, Jamii ihakikishe kuwa wazee na wananchi wote, wanaishi katika hali ya usalama, amani na utulivu kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Taifa letu.

  Erasto T. Ching’oro (Msemaji)

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

  15/4/2016

  0 0

  Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (Eala) wameomba ushirikiano kutoka kwa wabunge wenzao wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusaidia kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kuhusu fursa za mtangamano (integration) wa Jumuiya.

  Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania katika EALA, Makongoro Nyerere, aliwaambia wabunge wa kamati za Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na ile ya Viwanda, Biashara na Mazingira katika kikao cha pamoja jana jijini Dar es Salaam kuwa miongoni mwa fursa zitokanazo na mtengamano wa Afrika Mashariki ni pamoja na zile za biashara na masoko.

  Akizungumza kwa niaba ya wabunge wenzake tisa wa EAlA, Makongoro alizitaja fursa nyingine kuwa ni za elimu, uwekezaji, ajira na kujiajiri, kwenda popote katika Jumuiya, uhuru wa kuishi popote katika nchi wanachama kwa wale wenye shughuli maalum, kuboreshwa kwa miundombinu, maonesho ya wajasiriamali na maonesho ya utamaduni na fursa zinazotolewa kwa familia (Dependants).

  Alisema Watanzania wanapaswa kuelewa kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inajengwa katika mfumo wa ushindani wa soko na kwamba kila fursa iliyopo katika Jumuiya inapatikana kwa ushindani miongoni miongoni mwa wananchi wa nchi wanachama.

  "Hivyo, Watanzania kama raia wa nchi zingine wanachama ni lazima wachangamkie fursa na kuzitumia. Ili kushindana, Watanzania wanatakiwa kujiamini na kuacha kujiona wanyonge ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani akili tunazi, uwezo tunao na nguvu tunazo," alifafanua.

  Akichangia katika mkutano huo, Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Allan Kiula, alisema ni vema elimu kuhusu mtangamano wa Afrika Mashariki, hususan kuhusiana na fursa za kibiashara, ikatolewa pia kwa wafanyakazi wa taasisi zinazofanya kazi kwenye maeneo ya mipakani, kama vile Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa kikwazo kwa wafanyabiashara kutokana na utendaji wao usioridhisha.

  Alisema watumishi katika vituo vya mipakani wamekuwa wakiwakatisha tamaa wananchi wanaofanya biashara kiasi cha kuwafanya waendelee kutumia njia za panya.

  Naye mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (Chadema) alisema Tanzania bado ina kazi kubwa katika ushindani ndani ya Jumuiya akitolea mfano wa Kenya ambayo imefikia uchumi wa kati kwa kuwa na viwanda vya kutosha wakati nchi yetu ndio inafikiria kufufua na kuanzisha viwanda.

  Alisema kuna hatari ya Tanzania kubakia kuwa soko wakati nchi kama Kenya zinapambana kufanya uzalishaji mkubwa wa viwandani na kuimarisha ubora wa bidhaa zake.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Adadi Rajabu aliwataka Watanzania kutafuta mbinu za kuwa wabunifu zaidi katika ushindani ndani ya Jumuiya ili kuweza kufanikiwa kukamata fursa za mtangamano.

  Wabunge wa Afrika Mashariki ambao wapo katika shughuli za kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu fursa za mtangamano wa Afrika Mashariki wamesema siku za usoni wanatarajia kufanya mkutano na wabunge wote ili kubadilishana nao uzoefu kuhusiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, (EALA), Makongoro Nyerere akifafanua jambo wakati wabunge kutoka EALA walipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ulinzi na Usalama pamoja na Kamati ya Viwanda Biashara  na Mazingira jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kadumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Adadi Rajabu na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Dk. Dalali Kafumu. (Picha na Francis Dande)
   Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Twaha Taslima akifafanua jambo mbele ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama pamoja na Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Mmoja wa wataalamu wa kizalendo walioshiriki kwenye ujenzi wa Daraja la Kigamboni Muhandisi Jamal Mruma (kushoto) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) namna mradi huo ulivyowajengea uwezo kiutendaji wafanyakazi wazalendo. Kulia ni Meneja wa Mradi huo huo Bw. Zhang Bang Xu.

  SIKU chache kabla ya uzinduzi wa daraja la kisasa la Kigamboni, wafanyakazi na wataalamu wazawa walioshiriki kwenye ujenzi wa daraja hilo wamesema kupitia mradi huo wamepata fursa ya kuongeza ujuzi unaowapa mwongozo katika kutekeleza kwa ufanisi miradi mikubwa inayofanana na huo.

  Mradi huo uliogharimu Dola za Kimarekani milioni 135 umetekelezwa na kampuni ya China Railway Construction Engineering Group kwa ushirikiano na kampuni ya China Railway Major Bridge Group ya nchini China.

  Wakizungumza kwenye eneo la ujenzi wa daraja hilo jijini Dar es Salaam jana baadhi wa wataalamu na wafanyakazi hao walisema kupitia mradi huo wameweza kujifunza mbinu na teknolojia za kisasa zaidi hatua inayowapa mwanga kuhusiana na utekelezaji wa miradi mikubwa na inayohusisha teknolojia ya kisasa kama huo.

  “Mafunzo ambayo tungeweza kwenda kusomea nje ya nchi kwa gharama kubwa tumeweza kuyapata kupitia mradi huu tena kwa vitendo zaidi kwa kuwa tulikuwa tukishirikiana na wenzetu kutoka China bega kwa bega,’’ alibainisha mmoja wa wataalamu hao, Muhandisi Jamal Mruma.

  Alitoa wito kwa Serikali na taasisi za elimu ya mafunzo ya ufundi stadi hapa nchini kuhakikisha wanaweka utaratibu wa kutumia miradi mikubwa kama hiyo kuwajengea uwezo wanafunzi na wataalamu kutoka vyuo hivyo kupata mafunzo kwa vitendo.

  “Tulipokea baadhi ya wanafunzi kutoka baadhi ya vyuo hapa nchini ikwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na vyuo vingine waliotembelea kuona mradi na mafunzo mafupi… nahisi tulitakiwa tungechamkia zaidi hii fursa ili waje wengi zaidi,’’ aliongezea

  Nae Francis Mambo ambaye ni mkadiliaji ardhi kwenye mradi huo pamoja na kushukuru kwa ushirikiano walioupata kutoka kwa wenzao kutoka China, alitoa wito kwa serikali na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanawekeza nguvu nyingi kwenye kujifunza lugha ya kichina kutokana muingiliano wa kijamii na kiuchumi unaozidi kukua kila siku.

  Kwa upande wake Meneja mradi kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group ambao wametekeleza mradi huo kwa ushirikiano na kampuni ya China Railway Major Bridge Group Bw. Zhang Bang Xu alisema mradi huo umehusisha ajira zaidi ya 5000 wakiwemo wataalamu na wafanyakazi huku akionyesha kuridhishwa na uwezo mkubwa wa kiutendaji ulioonyeshwa na wafanyakazi hao.

  “Mbali na daraja hili la kisasa walipatata pia fursa ya kujifunza kutengeneza daraja la awali ambalo lilihusisha teknolojia ya kati ambalo ndio lilitumika katika ujenzi wa daraja hili kubwa,’’ alisema.

  Alisema kuchelewa kukamilika kwa mradi huo kwa kiasi kikubwa kulisababishwa na changamoto zisizotarajiwa ambazo ziliukumba mradi ikiwemo kugundulika uwepo wa pango- hewa chini ya bahari na hivyo kusababisha wao kutumia zaidi miezi sita kujaza pango-hewa hilo.

  “Pamoja na changamoto kadhaa tunashukuru tumekamilisha salama mradi huku kwa kiasi kikubwa tukiwa tumefanikiwa kutunza mazingira ikiwemo bahari yenyewe, uoto jirani na bahari pamoja na kubadili hali ya kiuchumi ya wafanyakazi na majirani wanaoishi jirani na mradi,’’ alishukuru.

  Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake leo (JUMAMOSI) wanatapa fursa ya kulitumia kwa mara ya kwanza Daraja hilo ili kutoa fursa kwa mkandarasi kuhakiki uwezo na ubora wa daraja hilo kabla halijazinduliwa na Rais Magufuli siku Jumanne.

  0 0


  0 0
 • 04/15/16--12:03: TAARIFA KUTOKA TEMESA
 • Napenda kukutaarifu kuwa; kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Wakala, kikao kilichopangwa kufanyike tarehe 19/04/2016 kati ya Mtendaji Mkuu wa TEMESA na Maafisa Usafirishaji (Transport Officers) wa Wizara, Idara, Taasisi na Wakala wa Serikali katika ukumbi wa KARIMJEE (main hall), ili kujadili utaratibu mzuri wa kutunza magari ya Serikali, hali ya madeni pamoja na taarifa za matengenezo ya magari ya Serikali,kimeahirishwa hadi tarehe 25/04/2016 saa nne kamili (4.00) asubuhi, kwenye Ukumbi ule ule wa KARIMJEE (Main Hall).

  Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

  Imetolewa na Ofisi ya Mtendaji Mkuu
  TEMESA

  0 0

   Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akiingia ukumbini kuzungumza na Makatibu na Wajumbe wa Kamati ya Siasa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro leo
   Katibu wa CCM wilaya ya Hai akimkaribisha Ole sendeka
   Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanajro akizungumza maneno ya utangulizi kabla ya Ole Sendeka kuzungumza katika kikao hicho
   Wajumbe wakiwa ukumbini katika kikao hicho

   Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akiteta jambo na Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Gratius Ruta wakati wa kikao hicho
   Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Hai, Dk Amini Uronu akimkaribisha Ole Sendeka kuzungmza katika kikao hicho
   Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Hai, Dk Amini Uronu akimkaribisha Ole Sendeka kuzungmza katika kikao hicho

  Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akizungumza na Makatibu na Wajumbe wa Kamati ya Siasa  wa wilaya ya Hai mkoani Kiimanjaro leo.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
   Msemaji wa CCM, Chrisopher Ole Sendeka akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Hai, Dk Amini Uronu, baada ya kuwasili Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mkoani Kilimanjaro leo. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Deogratius Ruta
   Msemaji wa CCM, Chrisopher Ole Sendeka akisalimiana na Katibu wa CCM wilaya ya Hai, Katibu Allan Kingazi, baada ya kuwasili Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mkoani Kilimanjaro leo. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Deogratius Ruta
   Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili Ofisi ya CCM wilaya ya Hai, leo
   Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ofisi ya CCM wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Hai, Dk Amini Uronu
   Mjumbe wa NEC na Ofisa Mwandamizi katika Idara ya Itikadi na Uenezi, Kilumbe Ng'enda akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Deogratius Ruta, kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Hai
   Msemaji wa CCM Oe Sendeka akizungumza na wajumbe wa Sekretatieti ya CCM wilaya ya Hai
   Madereva Yahaya Chillumba na Maoud Fundikira wakiwa imara baada ya kuwasili na msafara wa Msemaji wa CCM Ole Sendeka katika Ofisi ya CCM wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro leo

  0 0

  Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akipokea maua kutoka kwa mtoto Sharon Innocencia Shiyo mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli.
  Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu kwa ajili ya Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akiwa amesimama na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.


  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na washika dau wa Habari, Utamaduni Sanaa na michezo wa mkoa wa Mara ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukutana na wadau hao wakiwemo watumishi wa serikali .

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye leo ameendelea na ziara yake katika mkoa wa Mara na Shinyanga ambapo alikutana na Watumishi na wadau walio chini ya Wizara yake.

  Waziri Nape alipokea taarifa zaSerikali pamoja na maoni ya wadau mbali mbali ambapo aliwapongeza kwa kuwa na maoni mazuri na kusisitiza Wizara yake itakuwa karibu nao na kufanya ziara za mara kwa mara katika kuhakikisha mambo waliyopanga yanafanikiwa.

  Waziri Nape aligusia mambo mbali mbali ya msingi wakati akiongea na washika dau waliokuwa chini ya wizara yake na kusisitiza kuwa Madiwani wanaoshiriki katika mipango mji wanatakiwa kuzingatia kutenga viwanja vya michezo kwa watoto wa eneo husika pia alishauri mikoa kuanzisha vituo vya utamaduni wa mkoa ambavyo vitakuwa vyanzo vya kutunza utamaduni lakini pia sehemu ya kuvutia utalii akitolea mfano kituo cha Bujora mkoani Mwanza. 

  Mhe. Nape pia aliwataka Makatibu Tawala za Mikoa wajenge utamaduni wa kukutana na vyama vya michezo kwani wao ni walezi muhimu wa vyama hivyo. 
  Sehemu ya washika dau waliohudhuria kikao cha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa Mara.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mara.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Mhe. Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa CCM katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mara.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Mhe. Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa CCM katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mara ambapo aliwataka viongozi hao kutembea kifua mbele kwani ilani waliyoiandaa inatekelezwa vyema.
  Sehemu ya uwanja wa mpira wa Kambarage mkoani Shinyanga.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifafanua jambo kwenye uwanja wa mpira wa Kambarage mkoani Shinyanga.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na wadau kwenye uwanja wa mpira wa Kambarage mkoani Shinyanga.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mitambo ya kurusha matangazo ya TBC mkoani Shinyanga.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na watumishi wa serikali pamoja na wadau wa sekta ya habari, utamaduni, sanaa na michezo wa mkoa wa Shinyanga .


  0 0  0 0

   .Oh "Kumbe kinafanya kazi hivi" ndivyo anavyoelekea kusema Rais Obama mara baada ya kuweza kukiendesha kifaa hicho kwa kutumia simu, aliyechuchuma ni Stephen Mwingira ambaye pamoja na Wendy Ni na Armon Halwan walipata fursa ya kuonyesha ubunifu wao katika onyesho la mwisho  lililoandaliwa na Rais  Barack Obana na kufanyika White House  April 13. 2016.
   .Mwanafunzi  Armo Halwan akimuelekeza Rais  wa  Marekani,Barack Obama anavyoweza kutumia simu  kuendesha   cha  kufanyia usafi ( Vacuum Cleaner) kilichobuniwa na wanafunzi wa Baruch Collage Campus High School ya Jijini New York kupitia timu yao ya  ufumbuzi (Invent Teams)katikati ni Wendy Ni na anayefuatia ni  Stephen Mwingira ( mtanzania) anaonyesha  namna gani  kifaa hicho kinavyofanya usafi kwenye njia za treni za ardhini ( Subways).
   Stephen  Mwingira na Wendy Ni, wakiangalia kwa makini  jinsi Rais Obama anavyoelekezwa namna ya kutumia simu  kuendesha  mashine hiyo katika Onyesho la ubunifu wa kisayansi ambalo lilifadhiliwa na Rais Barack Obama katika Ikulu ya  Rais ( White House Science Fair 2016)
    Rais Barack Obama akipeana  mkono na Stephen  Mwingira na timu yake baada ya kumaliza kutoa maelezo yao kifaa walichokibuni. Kwa miaka sita Rais Barack Obama amekuwa akifadhili  maonyesho ya ubunifu wa   vifaa mbalimbali   vilivyobuniwa na wanafunzi kuanzia wale wa shule za wali  hadi  sekondari ikiwa ni jitihada zake za kuwahamasisha wanafunzi  kupenda masomo  ya sayansi, teknolojia na hesabu tangu wakiwa wadogo na hivyo kuibua vipaji vyao. katika onyesho hilo la mwisho wa utawala wa Barack Obama jumla ya wanafunzi 130 kutoka states mbalimbali walishiriki.

  Stephen Mwingira akiendelea kutoa maelezo zaidi  kwa Rais Obama namna kifanya cha kufanyia  usafi  kwenye njia za reli ambacho ni cha gharama nafuu kinavyofanya kazi.


   April 13, 2016,  Rais wa Marekani, Barack Obama, alifadhili  onyesho  la mwisho  katika utawala wake,  onyesho lililohusu ubunifu katika Nyanja za  sayansi ambalo  limewahusisha wanafunzi  kuanzia shule za  awali,msingi hadi za sekondari  kutoka  States  mbalimbali za  Marekani.

  Kwa miaka sita tangu mwaka 2010, Kiongozi huyo wa Marekani amekuwa akifadhili onyesho hilo  lijulikanalo  kama White House Science Fair  ambalo limekuwa  likifanyia  katika  Ikulu yake  (White House) lengo likiwa ni  kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi,  hisabati ,teknolojia  na  ufundi ( STEM)na hivyo   kuibua  vipaji  vya  ubunifu   mwiongoni  mwa wanafunzi ( young inventors) . 

  Katika onyesho hilo la  Aprili 13  jumla ya wanafunzi 130  walishiriki baada ya kukidhi vigezo vya kuingia katika  onyesho hilo. Miongoni mwa wanafunzi  waliopata fursa hiyo adhimu ya  kushiriki  baada ya kukidhi vigezo ya  ubunifu wao ni    mwanafunzi mtanzania  Stephen Wilfred Mwingira ambaye pamoja na wenzake wawili Armo Halwah na Wendy Ni  wanaosoma  Baruch College  Campus High School ya jijini New York,  wamebuni kifaa cha gharama nafuu ( vacuum  cleaner)   kinachoweza kutumika katika  kusafisha   njia za reli   za chini ya ardhi ( Subways). 

  Stephen Mwingira na timu yake,  walipata fursa ya  kuelezea  na  kuonyesha mbele ya Rais Obama namna gani kifaa walichobuni  ( Vacuum Cleaner) kinavyoweza kufanya usafi kwa kufungwa kwenye treni  na  hivyo kusaidia  katika  kuzifanya njia za treni ( subways) kuwa katika    mazingira ya usafi  na hivyo kupunguza gharama za usafishaji.

  Katika miaka sita tangu Rais Obama ambaye yeye binafsi amejipambanua kama mpenzi na shabiki mkubwa wa   sayansi na ubunifu, onyesho hilo limekuwa motisha na kivutio kikubwa kwa walimu, wanafunzi, wafadhili na  wataalamu waliobeba katika masuala ya  sayansi, teknolojia na   hesabu.
  Kila mwaka  State dining room ya Ikulu hugeuzwa kuwa eneo la maeonyesho  ambapo  wanafunzi hujipanga na kuonesha vifaa walivyobuni au  kutoa maelezo ya kisayansi ya namna ya kutatua tatizo Fulani kwa kutumia teknolojia nafuu. 

  Katika kutambua mchango wa Rais  Barack Obama katika kuwahamasisha wanafunzi  kupenda masomo ya  sayansi,   Ikulu  ya White House  imetangaza kwamba Kampuni ya Oracle inayojihusisha na  masuala ya teknolojia ya  Komputa katika miezi kumi na nane ijayo  itawekeza  dola za kimarekani 200 milioni kwaajili ya  masomo ya   sayansi ya computa   kwa wanafunzi wa kimarekani.

  Katika maelezo yake kwa vyombo vya habari kabla na baada ya  kuhitikishwa kwa onyesho lake la mwisho, Rais Barack Obama amesema,  mara zote ambazo ameshiriki kujionea ubunifu wa vijana hao wadogo na wenye kiu na ari ya kuibua mambo mapya, amekuwa akijifunza kitu kipya na  mara zote amejiona  kama anayepungukiwa na kitu kutokana  kile anachojifunza kutoka  kwa wanafunzi hao.

  “Nimeweza kujionea ubunifu  wa hali ya juu, kiu, na hamu ya    watoto na vijana wetu  wataalamu wa kesho wa taifa letu  la marekani.  Ipo siku huko mbeleni  nitajivunia pale ambapo miongoni mwa vijana wetu hawa watakapoweza kubuni tiba ya kansa. Nitaangalia  nyuma kwa fahari kubwa kwamba niliwawezesha vijana hawa kuibua vipaji vyao ”. Akasema Rais Obama kwa furaha   huku akiwashukuru wale wote ambao kwa miaka sita mfululizo wamewezesha kwa namna moja ama nyingine kufanyika  kwa onyesho  hilo.  

  0 0

  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiongea na baadhi ya wakazi wa kahama waliofika hospitalini hapo kuangalia wagonjwa wao.Waziri.Ummy Mwalimu akitoa angalizo kwa wagonjwa waliofika kupata matibabu kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa.shinyanga.Mh.Ummy Mwalimu akiwaelekeza kamati ya afya ya wilaya ya kahama mahali linapotakiwa kuwekwa bango linaonesha huduma za wazee inapopatikana.Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh.Vita Kawawa(Katikati) akionesha kwa vitendo bango hilo linapotakiwa kuwekwa,kushoto ni Mh.Ummy Mwalimu na kulia ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji kahama Anderson Msumba.Mfamasia Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Luciano Lodrick akimpatia maelezo waziri ,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto jinsi ya utengenezaji wa maji tiba.
  Waziri Ummy Mwalimu akiangalia kifaa cha kutengenezea maji tiba kwenye.hospitali ya.rufaa ya mkoa wa shinyanga.Mh.Ummy Mwalimu akiangalia matangazo yaliyobandikwa kwenye ubao hospitanini hapo.Waziri Ummy ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kubandika gharama za matibabu pamoja na namba za simu kwa ajili ya kupokelea maoni na malalamiko toka kwa wananchi.

  Na.Catherine Sungura,kahama
  Mkurugenzi wa halmashauri wa mji kahama amepewa siku tisini awe amenunua mashine ya mionzi (x ray)kwa ajili ya hospitali ya mji kahama.Agizo hilo amepewa jana na Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy mwalimu wakati alipotembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa kada ya afya wa wmji huo.


  Waziri Ummy alisema ametoa agizo hili ili kuweza kurahisisha usumbufu wanaupata wananchi wa wilaya hiyo kwa kwenda kupata huduma nje ya hospitali ambapo wakati mwingine vipimo hivyo vinakuwa havisomeki vizuri kwa kukosa viwango vinavyostahili za mashine hizo.

  Hata hivyo waziri ummy alisema upatikanaji wa mashine hizo itapunguza malalamiko mengi toka kwa wananchi kwa ukosefu wa kifaa tiba hicho ili kwani hospitali hiyo hivi sasa inahudumia wananchi zaidi ya milioni moja hususan toka wilaya zote za wilaya hii.

  Aidha, alizitaka halmashauri zote mjini kuweza kuwekeza kwenye huduma za vifaa tiba ambavyo inarahisisha kugundua matatizo yanayowakabili wananchi wanaofika kwenye kupata huduma na hivyo kuwapatia matibabu stahili wagonjwa wanaofika kupata matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma nchini.

  ?siku hizi lazima muwekeze kwenye kununua vifaa tiba ili kuweza kupata kutoa huduma nzuri ,pesa mnakusanya na kahama ni halmashauri tajiri,mkurugenzi nakupa siku tisini uwe umenunua mashine hiyo.

  Naye mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Vita kawawa amemuahidi waziri huyo kwamba amepokea maagizo yote aliyoyatoa na atayafuatilia ili kuweza kutatua malalamiko ya wananchi na yale ya watumishi wa kada ya afya

  0 0


  Wanamuziki wa bendi ya Inafrika toka Tanzania wakipata picha ya kumbukumbu Nashville jimbo la Tennessee ambapo wapo tangia March 18, 2016mpaka April 18, 2016 kwenye tamasha linaloandaliwa kila mwaka na Dolly Parton linalofanyika kwenye park iitwyo Dollywood iliyopo mjini humo. Tamasha hilo hushirikisha bendi mbalimbali kutoka mabara yote, Bara la Afrika liliwakilishwa na Inafrika Bendi kutoka Tanzania.

  Wanamuziki wa Inafrika Bendi wakiwa katika picha ya pamoja na Dolly Parton.
  Wanamuziki wa Inafrika wakipata picha ya kumbukumbu kwenye bango la Dollywood Park.

  Picha ya pamoja.

  0 0
 • 04/16/16--00:01: DONDOO ZA MAGAZETI

 • 0 0


  Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akifurahia jambo wakati alipokutana na kuzungumza na vijana watano waliongia katika hatua ya tano bora ya shindano la biashara la mashujaa wa kesho ambalo lina dhumuni la kuhamasisha ujasiriamali kwa mikoa ya kusini mwa Tanzania yaani Mtwara na Lindi, kwenye kambi yao iliyopo kwenye Jengo la Statoil ambao ndio wadhamini wa Shindano hilo, Masaki jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Genevieve Kasanga.

  Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi kuwasilisha mawazo yao ya biashara ambayo baadae yalibadilishwa na kuwekwa kwenye andiko la biashara.

  Mwaka huu shindano hili lilivutia vijana zaidi ya 400 ambao waliwasilisha mawazo ya biashara zao zinazolenga sekta mbalimbali za uchumi kama kilimo, ufugaji, mawasiliano, na biashara nyingine ndogondogo. Vijana waliruhusiwa kushiriki mmoja mmoja au hata kuunda vikundi vya watu wawili mpaka watatu.
  Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akisikiliza kwa makini maeneo ya namna shindano hilo lilivyoendeshwa kutoka kwa Afisa wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Eric Mchome.
  Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akipokea zawadi ya picha yenye mchoro wa wanyama aina ya Pundamilia, kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Genevieve Kasanga.
  Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa shindano hilo.
   Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akiwa katika picha ya pamoja na Sehemu ya Washiriki hao.

  0 0

  Na Woinde Shizza,Karatu

  Wananchi wa kata ya mbulumbulu walalamikia Mmalaka ya hifadhi ya Ngorongoro kushidwa kuzibiti wanyama pori kwani wanaharibu mazao yao.

  Hayo waliyasema juzi wakati wa ziara ya mwenyekiti wa CCM mkoa Arusha, Lekule Laizer wakati alipotembelea katika kijiji cah losteti ikiwa ni ziara yake ya kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho.

  Walisema kuwa mazao yao yamekuwa yakiaribiwa na wanyama wanaotoka katika hifadhi ya ngorongoro haswa nyakati za jioni na usiku na wametoa taarifa katika uongozi wa mamlaka hiyo lakini hamna hatua zozote ambazo wamezichukuwa.

  Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina Aron Saiteu alisema kuwa wanyama hao wamekuwa wanakuja katika mashamba yao ambayo wameotesha mahindi na maharage na kuingia na kula hali ambayo inawarudisha nyuma kimaendeleo na inawakosesha chakula.

  Alisema kuwa wamepeleka taarifa za malalamiko katika kituo kidogo ambacho kipo katika eneo hilo lakini hadi sasa hamna kiongozi ambaye amechukuwa hatua .

  “awali tulikuwa tunawafukuza wanyama hawa lakini mamlaka ikaja na kutunyima kufukuza wanyama lakini cha kushangaza mara baada ya kutuzuia kufukuza wakatuambia tukiona mnyama tupige simu tatizo lililokuja ukipiga simu unaambiwa na viongozi ambao wapo hapa katika kituo cha wanyama pori cha losteti wanasema hawana magari hivyo hawawezi kuja kufukuza wanyama na sisi wananchi tunashindwa tufanyaje unakuta tembo kaja au mbogo hivi unamfukuzaje jamani inabidi uache ale akitosheka aondoke “alisema Seuri lazier

  SOMA ZAIDI HAPA

older | 1 | .... | 821 | 822 | (Page 823) | 824 | 825 | .... | 1896 | newer