Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

MAMIA WAUAGA MWILI WA MAMA MZAZI WA MWANAHABARI ABSALOM KIBANDA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mamia ya waombolezaji, wengi wao wakiwa wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, leo wamejitokeza kuuaga mwili wa mama mzazi wa Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Bw. Absalom Kibanda, leo  asubuhi  huko Masaki jijini Dar es Salaam.
Mama yake mzazi Kibanda, alifariki juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ambako alikuwa akitibiwa ugonjwa wa kiharusi. Mwili wa marehemu Marehemu Mama Gwaseko Kapyela (76)  baada ya kuagwa u mesafiriskwa kwa ndege kuelekea Tukuyu, wilayani Rungwe,  mkoani Mbeya kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi.
 Wanahabari nguli Neville Meena na Peter Nyanje wakiandaa shada la maua na msalaba kabla ya safari ya kwenda Tukuyu kuanza
 Safari ikianza
Waombolezaji wakipeleka jeneza lenye mwili wa mama mzazi wa  Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, baad ya hafla ya  kuaga mwili wa mama yao mzazi marehemu Marehemu Gwaseko Kapyela Masaki jijini Dar es salaam.
Waombolezaji wakimpa pole Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, na kaka yake wakati wa kuaga mwili wa mama yao mzazi marehemu Marehemu Gwaseko Kapyela Masaki jijini Dar es salaam 
Waombolezaji wakimpa pole Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, na kaka yake wakati wa kuaga mwili wa mama yao mzazi marehemu Marehemu Gwaseko Kapyela Masaki jijini Dar es salaam 
Kwa picha zaidi ya hafla hii BOFYA HAPA


WAZIRI WA ARDHI AKUTANA NA WAMILIKI WA MABENKI NCHINI

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akutana na Wamiliki wa Mabenki Nchini ili kuzitambua Hati Miliki za Ardhi za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali leo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwasisitiza Wamiliki wa Mabenki Nchini kuzitambua Hati Miliki za Ardhi za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali, kushoto ni Bibi Medelina Kiwayo Meneja Usimamizi wa Taasisi za Fedha-Benki Kuu na Tuse Joune Kaimu Mkurugenzi Mkuu Chama cha Wenye Mabenki Tanzania (TBA).
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwasisitiza Wamiliki wa Mabenki Nchini kuzitambua Hati Miliki za Ardhi za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali alipo kutana nao leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwasisitiza Wamiliki wa Mabenki Nchini kuzitambua Hati Miliki za Ardhi za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali alipo kutana nao leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa katika kikao na Wamiliki wa Mabenki Nchini ili kuzitambua Hati Miliki za Ardhi za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali, kulia ni Bibi Medelina Kiwayo Meneja Usimamizi wa Taasisi za Fedha-Benki Kuu na Tuse Joune Kaimu Mkurugenzi Mkuu Chama cha Wenye Mabenki Tanzania (TBA), kushoto ni David Shambwe Mkurugenzi wa Hazina na Maendeleo ya Biashara-NHC na Mary Makondo Kaimu Kamishna wa Ardhi.
Baadhi ya Wamiliki wa Mabenki Nchini wakiwa katika kikao hicho.

MAKABIDHIANO YA OFISI KATIBA NA SHERIA ZANZIBAR

$
0
0
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini akikabidhiana Ofisi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishiwa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman leo katika ukumbi wa Jengo la Wizara ya Utumishi wa Umma Shangani Mji Mkongwe wa Zanzibar,baada ya uteuzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheun,[Picha na Ikulu.]
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini akitoa shukurani kwa wafanyakazi wa Wizara ya Katiba,Sheria,Utumishiwa Umma na Utawala Bora wakati wa makabidhiano ya Ofisi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishiwa Umma na Utawala Bora Mhe Haroun Ali Suleiman leo katika ukumbi wa Jengo la Wizara ya Utumishi wa Umma Shangani Mji Mkongwe wa Zanzibar, baada ya uteuzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheun,[Picha na Ikulu.]

BALOZI WA IRELAND NCHINI TANZANIA MHE. FIONNUALA GILSENAN AMTEMBELEA WAZIRI MH. ANGELLAH KAIRUKI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angellah Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na Balozi wa Ireland nchini Tanzania Mhe. Fionnuala Gilsenan alipotembelea ofisini kwake mapema leo.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA AFYA DUNIANI KWA KUTOA ELIMU YA MARADHI YASIYOAMBUKIZA SKULI MBALI MBALI.

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha maradhi yasiyoambukiza (NCD) Omar Mwalimu Omar akitoa elimu kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki juu ya njia bora za kujikinga na maradhi yasiyoambukiza ikiwa ni maadhimisho ya siku ya afya Duniani. 
Muuguzi kutoka kliniki ya wagonjwa wa kisukari Hospitali ya Mnazimmoja Bi. Mwanaharusi Shaaban akitoa elimu ya ugonjwa wa kisukari kwa wanafunzi wa Skuli ya Mwanakwerekwe C katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afya Duniani zinazoadhimishwa kila ifikapo tarehe 7 April. Zanzibar imeadhimisha siku hiyo April 13 kwa kutoa elimu skuli za serikali na binafsi.
Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya Mwanakwerekwe C wakimskiliza kwa makini mtoa elimu ya maradhi yasiyo ambukiza Bi. Mwanaharusi Shaaban (hayupo pichani) wakati wa sherehe za siku ya Afya Duniani zinazoadhimishwa kila ikifika tarehe 7 kila mwaka.
Mwanafunzi Shadia Issa Juma akiuliza swali kwa Muuguzi kitengo cha wagonjwa wa kisukari Bi. Mwanaharusi Shaaban.
Mkufunzi kutoka kitengo cha maradhi yasiyoambukiza (NCD) cha Wizara ya Afya Rabia Ali Makame akifundisha wanafunzi wa Skuli ya SOS kuhusiana na visababishi vinavyopelekea maradhi yasiyo ya kuambukiza katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afya Duniani.
Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya Mwanakwerekwe C wakimskiliza kwa makini mtoa elimu ya maradhi yasiyo ambukiza Bi. Mwanaharusi Shaaban (hayupo pichani) wakati wa sherehe za siku ya Afya Duniani zinazoadhimishwa kila ikifika tarehe 7 kila mwaka.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

MWAKILISHI WHO ATEMBELEA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR KUPATA TARIFA ZA KIPINDUPINDU

$
0
0
Waziri wa Afya Mhe, Mahmoud Thabit Kombo kulia akisalimiana na Muakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO alioko Zanizbar Dk, Ghirmay Andemichael mara baada ya kuwasili Ofisini kwake Mnazi mmoja Mjini Zanzibar, kupata taarifa ya maradhi ya kipindupindu yalioanza mwezi Septemba mwaka jana hapa Zanzibar.
Waziri wa Afya Mhe, Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na muakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO nchini Tanzania Dk, Rufaro Chatora kushoto yake pamoja na ujumbe aliofuatana nao Ofisini kwake Mnazi mmoja Mjini Zanzibar. Muakilishi huyo alifika kuangalia hali ya maradhi ya kipindupindu Zanzibar.
Muakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO Dk, Rufaro Chatora katikati akizungumza na Wakuu wa sekta mbalimbali katika Wizara ya Afya Zanzibar kuhusiana na Maradhi ya Kipindupindu Zanzibar. Kushoto yake ni Muakilishi wa WHO aliopo Zanzibar Dk, Ghirmay Andemichael na kulia yake ni Katibu Mkuu wizara ya Afya Zanzibar Mohd Saleh Jidawi.

NA RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR 

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzaia Dkt. Rufaro Chatora amezishauri taasisi za Serikali, taasisi za kiraia na watu binafsi kila mmoja kutekeleza wajibu wake katika kukabiliana na maradhi ya kipindupindu nchini.

Amesema maradhi ya kipindupindu yanapotokea katika nchi moja yanagusa nchi nyingi duniani kutokana na watu kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyengine katika harakati zao za maisha.

Dkt. Chatora ameeleza hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano na watendaji wakuu wa Wizara ya Afya na waandishi wa Habari katika ziara yake ya kuangalia hali ya maradhi ya kipindupindu Zanzibar tokea yalipoanza mwezi Septemba mwaka jana hadi hivi sasa ambapo watu 2703 wamepata ugonjwa huo.

Amesema maradhi ya kipindupindu ni rahisi kutibika iwapo kila mtu atatimiza wajibu wake na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya ikiwa ni pamoja na kuacha kutumia maji yasiyo salama ambayo ni moja ya chanzo kikubwa cha kupata maradhi hayo.

Mwakilishi huyo wa WHO amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na mashirika mengine ya Kimataifa litaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukabiliana na maradhi hayo ili kuhakikisha yanamalizika.

Akieleza hali ya kipindupindu ilivyo hivi sasa Zanzibar katika mkutano huo uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Mkurugenzi Kinga na ELimu ya Afya Dkt. Mohd Dahoma amesema hali bado sio nzuri na wanaendelea kupokea wagonjwa wengi katika kambi ya Chumbuni.

“Tunapokea wagonjwa kati ya 10 hadi 15 kwa siku katika kambi ya Chumbuni, kwa bahati mbaya jana tulipokea wagonjwa 20 na kambi moja mpya imefunguliwa katika kisiwa cha Tumbatu,’’ alisema Dkt. Dahoma.

Amesema jumla ya Kambi 17 za wagonjwa wa kipindupindu zimefunguliwa katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba na kumi kati yao zimefungwa baada ya kukosa mgonjwa wa maradhi hayo.

Ameongeza kuwa kati ya wagonjwa 2703 waliogunduliwa na maradhi hayo 34 wamefariki ikiwa ni sawa na asilimia 1.3 na vijana wenye umri kuanzia miaka 17 ndio walioathirika zaidi.

Dkt. Dahoma amesema kisiwa cha Unguja kimekuwa na wagonjwa wengi zaidi wa kipindupindu asilimia 52.3 na Pemba ni asilimia 47.3 huku Mkoa Mjini Magharibi ukiongoza ukifuatiwa na Mkoa Kaskazini Pemba.

Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya amewashauri wananchi kuwawahisha mapema vituo vya afya watu wanaobainika na dalili za maradhi ya kipindupindu kwa vile imeonekana wagonjwa wengi wanapopelekwa vituoni afya zao zinakuwa mbaya na matibabu yanakuwa magumu.

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA ARUSHA AWATAADHARISHA WANACHAMA WASIO NA MSIMAMO

$
0
0
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Lekule Laizer akiwa anaongea na wananchi wa tawi la chama cha mapinduzi Simba lililopo ndani ya kata ya Mbulumbulu
Katibu wa itikadi na uenezi wa mkoa wa Arusha Shabani Mdoe akiwa anaongea na wananchi wa kata ya mbulumbulu wakati wa ziara ya viongozi wa mkoa wa chama cha mapinduzi.
Katibu wa ccm wialaya ya karatu Loth Olelemeiruti akiwa anaongea na wananchi
mmoja wa wananchi wa kata ya mbulumbulu akiwa anamueleza mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha matatizo yanayowakabili katika kata yao ikiwemo ukosefu wa barabara
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Lekule Laizer akiwa na baadhi ya viongozi wa matawi wa ccm wa kata ya mbulumbulu wilayani karatu mkoani Arusha.

Na Woinde Shizza,Karatu

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Lekule Laizer amewaagiza viongozi wa matawi wa kata ya mbulumbulu na wilaya ya karatu kwa ujumla kufanya tadhimini ya uchaguzi uliopita haraka iwezekanavyo na kupeleka majibu kwa katibu wa chama cha hicho wilaya ya karatu Loth Olelemeiruti ili kuweza kujua ni watu gani ambao waliweza kuhujumu chama na kuchukuliwa hatua kali.

Hayo aliyasema jana wakati alipokuwa akiongea na wanachama wa chama cha mapinduzi ndani ya kijiji cha Losteti kilichopo ndani ya kata ya mbulumbulu wilayani Karatu Mkoani Arusha .Alisema kuwa katika uchaguziwa uliopita baadhi ya viongozi pamoja na wananchama waliweza kusaliti chama kwa kutoa siri za chama pamoja na kuwapa ushirikiano viongozi wa upinzani hali ambayo ilichangia kwa kiasi kikubwa kupoteza baadhi ya kata.

“napenda kuwaambia viongozi wote wa matawi wafanye tadhimini haraka iwezekanavyo baada ya hapo wapeleke majibu kwa katibu wa wilaya ya karatu ili aweze kuyafikisha mkoani na sisi tuweze kuyatumbua majipu yote ambayo walikisaliti chama wakati wa kampeni”alisema Laizer

Aidha aliongeza kuwa sasa ivi viongozi wa chama wanatakiwa kufanya kazi kama kwa nguvu zao zote pamoja na akili zao zote ili kuhakikisha chama kinarudi katika mstaari wake na sio hivyo tu iwapo viongozi watafanya kazi kwa nguvu zao zote itasaidia pia kumpa nguvu rais wa nchi ambaye ametoka katika chama cha mapinduzi.

“tunajua watu wengi walichukuliwa na mafuriko sasa napenda kusema yale mafuriko yameisha sasaivi ni kazi tu ,na pia napenda kutumia fursa hii kuwaambia wananchi yeyote ambaye anataka kuwa mwana chama wa ccm achukuwe kadi mapema kwani itafikia mahali chama akitatoa kadi tena na sio kuchukuwa kadi tu bali kulipia ada maaana mwanachama ambaye ajalipa ada ya uanachama basi yeye sio mwananchama hai kwakua ajalipa ada ni bei ndogo sana kwa iyo kila mwanachama anatakiwa alipe ada ili awe mwanachama hai”alisema Laizer.

Alibainisha kuwa kwa sasa amana kiongozi ambaye atachaguliwa kwa kutegemea rushwa hivyo ,kama kunamwananchi au mwanachama ambaye anategemea aje achukuwe fomu katika chaguzi zijazo kwa kutoa rushwa au anategemea atatumia pesa zake kushinda katika uchaguzi asahau kabisa maana sasa ivi ndani ya ccm awataki watu ambao wanatumia fedha kupat a nafasi za uongozi wamepotea kwani aita kubalika kabisa.

Hata hivyo mwenyekiti huyo amejinasibu kuwa aliyekuwa mgombea wa urais kupitia umoja wa vyama vinavyounda ukawa Edwad lowasa kamwe atakaa aje kuwa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kulingana na mazambi yake aliyoyafanya kwani amefanya nae kazi kwa muda mrefu na anafahamu vizuri.

Kw aupande wake katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Arusha Shabani Mdoe amesema kuwa wao kama viongozi wa chama wamejitoa sadaka kwa ajili ya kuimarisha chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha na watafanya kila jitiada kuhakikisha chama kina simama imara na iwapo kunamtu ndani ya chama anaejijua kuwa ni jipu aanze kujitumbua mapema kabla ajatumbuliwa .

KASESELA AFUNGUA WARSHA YA KUWAWEZESHA WANAFUNZI KUTUMIA KOMPYUTA NA WAVUTI MKOANI IRINGA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya Iringa Richard Kasesela amefungua warsha ya kuwawezesha wanafunzi kutumia kompyuta na wavuti (Bring Computer literacy to children in Tanzania), mradi huu wa Global Out reach ulibuniwa na Bwana Mussle ambaye alitembelea Tanzania akimtembelea binti yake aliye kuja kijitlea Iringa (hawa ni raia wa marekani). Mradi huu unafadhiriwa na;

 BENKI KUU YA TANZANIA, ROTARY  INTERNATIONAL, ROMAN CATHOLIC CHURCH IRINGA, ST THOMAS MORE PARISH KICHANGANI, SUNRISE ROTARY USA, BRADENTON ROTARY USA, ST STEPHENS, TTCL

Mradi huu unashirkisha shule 12 Iringa (POMELINI, MAWELEWELE,LUGALO, IRINGA GIRLS, IFUNDA TECH, NYERERE HIGH SCH, BOMALANG'OMBE,IMAGE, MAFINGA, ST JOSEPH, ST MICHAEL na CAGLIERO). Kila shule imepata kompyuta na wamepewa mafunzo, pia wametoa vifaa kwa ajili ya kituo chenye maktaba kilichotolewa kwa hisani ya baba askofu wa Roman Catholic Iringa.
 
Mkuu wa wilaya aliwaasa waalimu wote wa shule za sekondari kuanza kufikiria uwezekano wa kuwa na maktaba ya kompyuta. baada ya zoezi la maabara kwisha na madawati kuptakina shule zote kitakacho fuatia ni kuhakikisha shule zote zinakuwa computarized.
 


TAASISI YA BENJAMIN MKAPA YAFANYA HARAMBEE, YAKUSANYA BIL.1.17

$
0
0
Mwanzilishi wa Taasisi ya Mkapa (Mkapa Foundation), Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa (kushoto), mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Mkapa Foundation, Balozi Charles Sanga wakiwasili katika sherehe za miaka 10 ya Mkapa Foundation zilioambatana na harambe ya kutunisha mfuko wa taasisi hiyo zilizofanyika kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha iliyoandaliwa na wafanyakazi pamoja na bodi ya Mkapa Foundation, Mwanzilishi wa taasisi ya Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa wakati wa sherehe za miaka 10 ya taasisi hiyo zilizoambatana na harambee ya kutunisha mfuko wa taasisi hiyo ambapo jumla ya shilingi bilioni moja na milioni mia moja sabini zilichangishwa.
Mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji (kushoto) akimkabidhi tuzo Mwanzilishi wa taasisi ya Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa ya kutambua mchango wake wa kuleta matumaini kwa watu wenye mahitaji na kuthamini maono na muongozo kama mwanzilishi wa taasisi ya hiyo iliyoanzishwa mwaka 2006 kwenye sherehe za miaka 10 ya taasisi hiyo iiliyoambatana na hafla ya harambee kwa ajili ya kuchangia taasisi hiyo.
Mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji na Mwanzilishi wa taasisi ya Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa kwa pamoja wakizundua jina jipya ambalo ni Mkapa Foundation -"Bringing HOPE to the Underserved".

Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ameuchangia mfuko wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa (Mkapa Foundation), Milioni 210 ili kuiwezesha kuzidi kutoa huduma bora kwa jamii.

Mohammed Dewji ametoa kiasi hicho cha pesa akiwa kama mgeni rasmi katika sherehe za kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Benjamini Mkapa (Mkapa Foundation) ambapo Milioni 200 imetolewa na Taasisi ya Mohammed Dewji (Mo Dewji Foundation) na Milioni 10 imetolewa na MeTL Group.

Akitoa hotuba katika sherehe hiyo, Mohammed Dewji amesema kuwa ametoa msaada huo ili kuiongezea nguvu Taasisi ya Benjamin Mkapa (Mkapa Foundation) katika kutoa huduma mbalimbali kwa jamii ya Watanzania.

Alisema kuna changamoto nyingi nchini ambazo zimekuwa zikijitokeza na ili kukabiliana nazo zinahitajika taasisi kama ya Benjamin Mkapa ili ziweze kusaidiana na Serikali na ili waweze kutatua changamoto hizo zinahitajika sekta binafsi kusaidiana nao kukabili changamoto hizo.Nimekuwa mstari wa mbele kusaidia sehemu ambazo zinaonekana kuwa na mahitaji na changamoto nchini zipo nyingi haina jinsi inabidi kushirikiana ili kupambana na changamoto hizo,” alisema Dewji.

Aidha Rais na Mkurugenzi Mkuu huyo wa MeTL Group aliyataka mashirika binafsi mengine kuungana kwa pamoja na kusaidia kumaliza changamoto zilizopo nchini kwani anaamini kuwa wana nafasi kubwa kukabiliana na matatizo hayo na kuweza kuyamaliza.
Nae mwanzilishi wa Taasisi ya Mkapa (Mkapa Foundation), Rais Mstaafu wa  awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa alimshukuru Mohammed Dewji kwa msaada ambao amewapatia na anaamini ni mmoja wa watu wa kuigwa nchini kutokana na misaada ambayo amekuwa akiitoa nchini kwa kupitia taasisi yake ya Mohammed Dewji (Mo Dewji Foundation).

“Mohammed Dewji ni mfano wa kuigwa nchini na ameweza kuboresha biashara ya Tanzania kimataifa, ninaamini utadumu kwa kipindi kirefu zaidi na kuwa balozi mzuri wa Tanzania,” alisema Mkapa.Katika sherehe hizo za kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Benjamin William Mkapa, kulifanyika harambee ambapo jumla ya Bilioni moja na Milioni mia moja na sabini zilichangishwa.


SERIKALI YAOMBWA KUWEKEZA ZAIDI KATIKA VIJANA

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRIL 15

MLATA: SERIKALI NJOENI NA MKAKATI WA UZAZI WA MPANGO

MBUNGE WA JIMBO LA MKURANGA MH.ABDALLAH ULEGA APOKEA MRADI WA MAJI MKAMBA NA KUKABIDHI KWA WANANCHI

$
0
0
ul14
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah ulega akifungua bomba la maji huku baadhi ya wananchi wakishuhudia katika kata ya Mkamba kijiji cha Tungi katika hafla fupi ya kukabidhi kisima cha Maji kilichochimbwa kwa ufadhiri wa Taasisi ya kimarekani ya African Reflections Foundatioan wiki hii, katika picha mwenye kofia anayeshuhudia ni Mama Maryborne Pool Mtekelezaji wa mradi kutoka taaisi ya Marekani kutoka African Reflections Foundatioan na kushoto ni Diwani Kata ya Mkamba Bw.Dunga Hassan (Picha zote na Raphael Malekela)
ul1
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah ulega akizungumza na baadhi ya wananchi wa kata ya Mkamba kijiji cha Tungi katia hafla fupi ya kukabidhi kisima cha Maji kilichochimbwa kwa ufadhiri wa Taasisi ya kimarekani ya African Reflectins Foundatioan, kulia ni Mama Caren kutoka Taasisi ya African Reflectins Foundatioan na kushoto ni Mama Maryborne Pool Mtekelezaji wa mradi huo.
ul4
Mama Maryborne Pool Mtekelezaji wa mradi kutoka taaisi ya Marekani kutoka African Reflections Foundatioan akizungumza jambo huku Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akifurahia wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji katika kijiji cha Tungi wilaya ya Mkuranga.
ul8
Mama Maryborne Pool Mtekelezaji wa mradi kutoka taaisi ya Marekani kutoka African Reflections Foundatioan na mama Caren kutoka taasisi hiyo pia wakikabidhi madawa ya majikwa mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega.

ul13
Mama Caren kutoka taaisi ya Marekani kutoka African Reflections Foundatioan akizungumza katika makabidhiano hayo huku Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega na kushoto na Mama Maryborne Pool Mtekelezaji wa mradi kutoka taaisi ya Marekani kutoka African Reflections Foundatioan
ul9
Mbunge wa mkutanga Mh. Abdallah Uleha na Mama Maryborne Pool Mtekelezaji wa mradi kutoka taaisi ya Marekani kutoka African Reflections Foundatioan wakiimba pamoja na akina mama wakati wa makabidhiano hayo.
ul10
Mbunge wa jimbo la Mkuranga akisalimiana na wanakikiji ambao ni wapiga kura wake wakati alipowasili katika kijiji cha Tungi Mkuranga.
ul11
Mbunge wa jimbo la Mkuranga akizungumza na akina mama wakati alipowasili kijijini hapo.
ul12
Akina mama mbalimbali wakiwa katika makabidhiano ya mradi huo.

Waziri Nape afanya Ziara mkoani Kagera

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisalimiana na uongozi wa mkoa wa Kagera baada ya kuwasili mkoani hapo akiwa kwenye ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara, kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mkoa huo.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili mkoani Kagera kwa ajili ya kufanya ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara, kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mkoa huo.Wengine pichani ni Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw,Jackson Msome na Kaimu katibu tawala mkoa wa kagera Bw.Adam Mohamed Swai.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akikabidhi Tablet tano kwa mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Jackson Msome kwa ajili ya matumizi ya maafisa habari wa mkoa wa kagera.Bwana Msome alikuwa akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa kijuu.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Jackson Msome ambaye anamwakilisha Mkuu wa mkoa wa kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa kijuu akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wakati wa ziara ya waziri huyo katika mkoa wa kagera.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza jambo na waandishi wa habari wakati alipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Kaitaba.Uwanja huo umeshawekwa nyasi za bandia na maboresho mengine yanaendelea. 

Wakazi Dar ‘kuonja’ daraja la Kigamboni bure kesho

$
0
0
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake kesho  wanatapa fursa ya kulitumia kwa mara ya kwanza Daraja la Kigamboni linalotarijiwa kufunguliwa rasmi na Rais John Pombe Magufuli siku ya Jumanne ya wiki ijayo ili ‘kuonja’ na kujionea ubora wa daraja hilo kisasa.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam jana, Meneja mradi kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group ambao wametekeleza mradi huo kwa ushirikiano na kampuni ya China Railway Major Bridge Group Bw.Zhang Bangxu,  alisema  siku ya kesho, wataruhusu wakazi hao na magari kupita katika daraja hilo lililogarimu Dola za Kimarekani milioni 135 kujengwa.

“Kama wajenzi kesho tutaruhusu magari kupita kwenda upande wa Kurasini na upande wa Kigamboni siku ya Jumamosi tu kama ikiwa ni sehemu ya majaribio yetu kitaalamu ikiwa ni pamoja na kutumia fursa hiyo kufanya majaribio ya mitambo na mashine zote ambazo zitatumika katika kufanya tozo mbali mbali baada ya kuanza rasmi kwa mradi," alifafanua.

Kwa mujibu wa Bw. Bangxu, daraja la Kigamboni ndiyo daraja refu kuliko yote katika ukanda wa Afrika Mashariki lililotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya matumizi ya kamba (cable) kubeba uzito wa daraja, ambayo itaunganisha jiji la kibiashara la Dar es Salaam na eneo la Kigamboni na Kurasini. Ujenzi ulianza mnamo Tarehe moja Februari mwaka 2012.

“Pamoja na kujengwa katika ubora wa hali ya juu, daraja hili lina jumla ya njia sita yaani njia tatu kwa kila upande, pamoja na njia mahususi kwa ajili ya waenda kwa miguu na waendesha baiskeli ambayo ina upana wa mita 2 na nusu (2.5 meters) katika kila pande. Daraja hilo litaruhusu magari yenye uzito usiozidi tani 30 kupita.,’’ aliongeza
 
 Bw. Bangxu alisema kwamba kaskazini mwa daraja hilo, litaungana na barabara lenye urefu wa kilometa  moja ambayo inakatiza reli ya TAZARA kisha kuungana na barabara ya Mandela. Kwa upande wa Kigamboni, daraja litaungana na barabara lenye urefu wa Kilometa 1.5 ambayo inaungana na barabara ya Kigamboni Ferry - Kibada.

Aliongeza kwamba kukamilika kwa daraja hili ni ya maendeleo kwani inatarajiwa kuchochea kasi ya maendeleo ya mji wa kisasa wa Kigamboni (Kigambani satellite city), kutengeneza fursa za ajira katika sekta ya ujenzi wa maeneo ya makazi pamoja na sekta za huduma ambazo  zitastahimili ongezeko kubwa wa idadi ya wakazi wapya katika mji huo mpya.

Kukamilika kwa daraja hilo kunatajwa kuwa kutawapafusra wakazi wa Kigamboni na viunga vyake ikiwa ni kutoa njia mbadala ya kufikia makazi yao, biashara zao au shuguli zao za ujenzi wa taifa kwa njia ya barabara.
 
Maeneo ya Kigamboni na Kurasini kwa sasa hufikika kwa kutumia vivuko viwili vya MV Magogoni na MV Kigamboni ambazo kwa pamoja zinaumezo wa kubebe abiria 1000 na magari 78 kwa kila safari.

Mradi huo umedhaminiwa kwa kwa ubia kati ya Shirika la Hifadhi ya Jamii ya Taifa (NSSF) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

RAIS WA SUDANI KUSINI, MHE. JENERALI SALVA KIIR MAYARDIT AWASILI LEO NCHINI

$
0
0

Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (wa tatu kulia) akisalimiana na Kamanda Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Siro mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye kofia nyeusi) akishuka katika ndege ya Shirika la Kenya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (wa tatu kushoto) akiwa tayari kumpokea Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuja kumpokea mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akipita katikati ya gwaride la Jeshi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (kushoto) akisalimiana na Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.

MAKAMPUNI BINAFSI HAYAHUSIKI ULINZI WA NDANI OFISI ZA BANDARI.

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imesema kuwa makampuni binafsi ya ulinzi yanayofanya kazi bandarini hayahusiki na ulinzi wa sehemu nyeti za za Mamlaka hiyo.

Akitoa ufafanuzi huo leo jijini Dar es salaam, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Janeth Ruzangi amekiri kuwepo kwa makampuni yanayofanya kazi ya ulinzi bandarini na amefafanua kuwa hayahusiki kwa namna yoyote ile kulinda sehemu za ndani za ofisi zilizoko bandarini.

“Ninapenda kuwafahamisha wananchi kuwa Bandari inalindwa na walinzi wa aina tatu ; Jeshi la polisi, Polisi wasaidizi walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (Auxilliary Police) pamoja na walinzi wa Makampuni binafsi”

Ameongeza kuwa makampuni hayo yanalinda maeneo ya nje ya bandari yakiwemo maegesho ya magari ya watumishi wa mamlaka kama ilivyo kwenye ofisi nyingine.

Aidha,amefafanua kuwa Polisi wa bandari walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania wako kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na Bunge na wamepata baadhi ya mafunzo ya kipolisi.

Ikumbukwe kuwa agizo la kuwandoa walinzi wa makampuni binafsi kwenye maeneo nyeti ya bandari lilitolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mwezi Februari mwaka huu alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo.

WABUNGE WAPONGEZA KUANZISHWA KWA TADB

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka (Kulia) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Dkt. Anaclet Kashuriza (Aliyesimama) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakifurahia jambo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi (Kulia) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.

WAZEE WA ZANZIBAR WAANZA KUPOKEA PENSHENI

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed akisalimiana na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na watu wenye ulemavu wa Tanzania Bara Dk. Abdallah Possi alipofika katika uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa Skuli ya sekondari ya Kiembe samaki nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na watoto Moudline Castico akielezea mikakati yao yakuwasaidia wazee katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa Wazee wa Zanzibar (kulia) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed akimkabidhi pencheni ya Sh/= elfu 20 Mzee. Kombo Moh’d Kombo itakayokuwa ikitolewa kila mwezi, katika uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa Skuli ya sekondari ya Kiembe samaki nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Khalid Salim Mohammed akimkabidhi pencheni Bi. Erestina Filex katika uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa leo April 15/2016.
Baadhi ya Wazee waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango wa pencheni kwa wazee wa Zanzibar uliozinduliwa Skuli ya sekondari ya Kiembe samaki nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.


Na Miza Kona, Majda Kasim -Maelezo Zanzibar.

Wazee 21,750 wameanza kunufaika na mpango wa serikali wa utoaji fedha za kujikimu yaani pensheni kwa wazee wote wanaoanzia umri wa miaka 70 ili kuimarisha maisha yao.

Wazee 13,150 ni kutoka Unguja na 8,600 wanatoka Pemba, katika mpango huo, kila mzee atapewa shilingi elfu ishirini kila mwisho wa mwezi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo, katibu mkuu wizara ya uwezeshaji, wazee, vijana, wanawake na watoto Asha Ali Abdallah, amesema hatua hiyo ni muhimu kwani nchi nyingi duniani zinao utaratibu kama huo.

Amesema, mbali ya kuwa kufanya hivyo ni wajibu, lakini kunahitaji maamuzi ya kijasiri na utashi wa kisiasa, ambapo serikali ya Zanzibar imeweza kuonesha dhamira yake kuimarisha maisha ya wazee.

Amesema msingi wa pensheni kwa wazee wote wa Zanzibar, ni sera ya hifadhi ya jamii iliyopitishwa mwaka 2014, ukiwa mpango mkuu wa taifa wa dira ya 2020 unaolenga kukuza uchumi na kupunguza umasikini nchini.

sambamba na hilo alisema kuwa wataendelea kuwa na jukumu kubwa katika kuwasajili wazee wapya watakaokuwa wanaingia katika mpango huo.

Waziri wa fedha Dk Khalid Salum Mohammed, alisema kuwa ili serikali iweze kupata maendeleo ni lazima wafanyakazi na wananchi kuwa wawajibikaji katika utendaji wa kazi zao.

Alisema katika kutekeleza mpango huo watendaji wanapaswa kuwa waadilifu na waaminifu ili kuhakikisha wazee wanaostahi wanapata pencheni zao kama inavyopaswa.

“hali halisi na uzoefu unaonesha kuwa kumekuwa na tabia za udanganyifu na wizi katika masuala mengi yanayohusiana na malipo….lakini nachukua nafasii hii kuwatanabahisha watendaji wote watakaohusika na utekelezaji wa mpango huu katika ngazi zote yoyote atakaebanika kufanya udanganyifu hatua kali zinatuchukuliwa dhidi yake”alisema.

Aidha aliwataka watendaji wa mpango huo kuwa na hekima,busara,uvumilivu,upole na huruma ni lazima zichukue nafasi yake katika kuwahudumia wazee.

Nae waziri wa Kazi,uwezeshaji,wazee,vijana,wanawake na watoto Moudline Castico ameahidi kwamba mpango huo utasimamiwa kwa nguvu zote ili kuhakikisha wazee wote wanaostahiki wanapatiwa fedha zao kwa wakati na hakutakuwa na udanganyifu na upotevu wa fedha za serikali.

Mpango huo unatarajiwa kutumia shilingi miioni 435 kwa mwezi ambapo ni sawa na shilingi bilioni 5.220 kwa mwaka.

Zanzibar inakuwa nchi ya kwanza Afrika mashariki kuanzisha mpango huo, nay a sita kwa Afrika baada ya Mauritius, Afrika Kusini, Lesotho, Namibia na Botswana.

NAIBU WAZIRI DKT. KIGWANGALLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA LEO KATIKA VITUO VYA TIBA MBADALA.

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya nyaraka za kituo cha tiba Mbadala cha Korea Medical Clinic kilichopo Kariako0 Mtaa wa Livingstone na Mahiwa jijini Dar es Salaam akiwa katika ziara ya kushtukiza ambapo alifungia vituo viwili vya Korea Medical Clinic 
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili Bw. Edmund Kayombo akizungumza na waandishi wakati wa zoezi la Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla la kukagua vituo vya tiba mbadala ambavyo havijakidhi vigezo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa mmoja wa matabibu wa kituo cha Korea Medical Clinic kilichopo Kariako0 Mtaa wa Livingstone na Mahiwa jijini Dar es Salaam akiwa katika ziara ya kushtukiza ambapo alifungia vituo viwili vya Korea Medical Clinic 

: Baadhi ya vifaa vinavyotumiwa na vituo vya tiba mbadala ambavyo havijakidhi vigezo.
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images