Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 822 | 823 | (Page 824) | 825 | 826 | .... | 1897 | newer

  0 0


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaambia watendaji na wadau wa mradi Mabasi Yaendayo Haraka wa jijini Dar es Salaam (BRT) kuwa hawana muda wa kulala wa kupumzika na akawataka wakamilisha haraka vipengele vichache vilivyobakia ili mradi huo uweze kuanza kazi mapema iwezekanavyo. 

  Ametoa agizo hilo jana usiku (Ijumaa, Aprili 15, 2016) wakati akizungumza na wakuu wa taaasisi, watendaji wakuu na wadau wa mradi huo kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam. 

  “Watu wa DART, UDA-RT hakuna muda wa kulala tena. Nanyi wa eGA, MAXCOM, POLISI NA SUMATRA inabidi mfanye kazi kama timu moja na wenzenu ili maeneo yaliyobakia yaweze kukamilika katika muda mfupi na kikubwa ni kuhakikisha mnatoa elimu ya kutosha,” alisisitiza. 

  Akielezea utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Bw. Ronald Rwakatare amesema miundombinu ya mradi huo imekamilika na utoaji huduma unatarajiwa kuanza hivi karibuni kwani hivi sasa wanamalizia ufungaji wa mfumo wa ukusanyaji nauli na uendeshaji wa mabasi hayo. Pia aliwatka wananchi kutunza miundombinu ya mradi huo na kuwa makini na matumizi ya barabara wakati mradi huo ukiwa kwenye majaribio na hatimaye kuanza kazi rasmi. 

  Alisema watakuwa na karakana itakayotumika kwa ajili ya hayo mabasi ambayo itakuwepo eneo la Jangwani na kwamba ofisi za mradi pia zitakuwa eneo hilo. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UDA Rapid Transit (UDA-RT), Bw. Robert Kisena amesema mpango wa kuanza kwa mradi huo umekamilila na tayari mabasi yote yamelipiwa kodi pamoja na bima. UDA-RT ni kampuni ya muunganiko wa UDA na wamiliki wa daladala ya kutoa huduma ya usafiri katika miundombinu ya mabasi yaendayo haraka. 

  Bw. Kisena amesema kesho wataanza majaribio ya mradi huo kwa kutumia mabasi 10 na watakuwa wanaongeza mabasi 10 kila siku hadi yafikie 50 hivyo amewataka wananchi kuondoa shaka juu ya mradi huo. Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom Africa, Bw. Juma Rajab amesema mabasi hayo yatakuwa yanatumia kadi za kielektroniki zitakazokuwa zinalipiwa kwa kutumia mitandao mbalimbali ya simu za mkononi. 

  Bw. Rajab amesema Tanzania inakuwa nchi ya kwanza kuanza kutumia mfumo huo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba fedha za mteja zitakuwa salama na hata kama atakapopoteza kadi yake. “Mtu akinunua kadi yake anapaswa atunze namba ya usajili iliyoko kwenye kadi hiyo kwani itatumika kurudishia fedha zake kupitia namba yake ya simu ya mkononi,” alisema. 

  Amesema Maxcom Africa ndio wakusanyaji wa nauli kwa kushirikiana na UDA-RT ambapo watatumia mawakala wa MaxMalipo hivyo kila mwananchi atapata fursa ya kununua kadi yake kwa urahisi. Alisema taarifa za kila mtumiaji zitaunganishwa na simu yake ya mkononi ambapo mhusika ataweza kujua kwa urahisi salio la fedha lililomo kwenye kadi yake. 


  IMETOLEWA NA: 
  OFISI YA WAZIRI MKUU 
  2 MTAA WA MAGOGONI, 
  S. L. P. 3021, 
  11410 DAR ES SALAAM 
  JUMAMOSI, APRILI 16, 2016.

  0 0

  ZIKIWA zimebaki siku chache kabla ya mradi wa mabasi yaendayo kasi kuanza, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa taasisi zinazohusika na utekelezaji wa mradi huo kuhakikisha wanatoa elimu kwa umma ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.

  “Katika kipindi hiki cha majaribio, ambacho madereva wameanza kutumia barabara za BRT, hakikisheni mnatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu namna ya kuvuka barabara, kuzuia wenye bodaboda kutumia barabara hizo kuelezea na matumizi ya taa za barabarani kwa madereva wote,” amesema.

  Ametoa agizo hilo jana usiku (Ijumaa, Aprili 15, 2016) wakati akizungumza na wakuu wa taaasisi, watendaji wakuu na wadau wa mradi huo kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mkuu aliwataka watendaji wa wakuu wa taasisi wahakikishe wanapanua wigo na kutumia vyombo vya habari vingi kadri iwezekanavyo pamoja na mitandao ya kijamii katika kuelimisha raia juu ya zoezi hilo.

  Akifafanua kuhusu hatua zilizofikiwa kwenye mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale alisema miundombinu kwa ajili ya mradi huo imekamilika na usafiri huo utaanza hivi karibuni.

  Mhandisi huyo ametumia fursa huyo kutoa wito kwa wananchi kutunza miundombinu ya barabara hizo kwa sababu imeigharimu Serikali fedha nyingi.

  Naye Mrakibu wa Polisi (SP), John Shawa kutoka Makao Mkuu ya Trafiki alisema kuanzia kesho zoezi la majaribio kwa mabasi yaendayo haraka litaanza hivyo amewaomba wananchi kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

  "Kuanzia kesho linapoanza zoezi la majaribio kwa mabasi yaendayo haraka ni vema watu wakatumia vizuri barabara hasa madereva wa bodaboda na madereva wengine watambue kuwa hawaruhusiwi kupita katika barabara hizo," alisema.  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMAMOSI, APRILI 16, 2016.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) na Makamu wa Rais wa Shirika la Koica la nchini Korea Kusini, Taemyon Kwon, wakiweka tofali kwa pamoja kuashiria uweka wa jiwe la msingi la Hospitali ya Chanika iliyopo Manispaa ya Ilala, inayojengwa kwa ufadhili wa nchi hiyo Dar es Salaam jana. Ujenzi huo hadi kukamilika utagharimu sh. bilioni 8.8 za kitanzania.
  .
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mr Isaya (kulia), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Victriana Ludovic na Meneja wa Mradi wa ujenzi wa Hospitali hiyo Mr Kim wakiweka jiwe la msingi la Hospitali hiyo.
  Meneja wa Mradi huo, Mr Kim akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na ujumbe wake ramani ya majengo ya Hospitali hiyo.Na Dotto Mwaibale
  Hutuba na taarifa ya mradi huo zilisomwa.
  Balozi wa Korea nchini Geum-young Song (katikati), akizungumza katika hafla hiyo.

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na balozi wa Korea nchini Geum-young Song wameweka jiwe la msingi la Hospitali ya Chanika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam ambapo itakapo kamilika itakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi 4000.

  Akizungumza katika hafla ya kuweka jiwe hilo la msingi Chanika jijini Dar es Salaam jana, Makonda aliishukuru serikali ya Korea kwa msaada wa ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo itawasaidia wananchi wa Chanika na kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Amana.

  "Tunawashukuru hawa ndugu zetu wa Korea Kusini kwa msaada wa kutujengea Hospitali hii nawaombeni wananchi kuitunza ili kila mtakapokuwa mnafika kutibiwa tuwakumbuke wakorea" alisema Makonda.

  Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Victorina Ludovic alisema ujenzi wa Hospitali hiyo utasaidia kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi wapatao 398,882 kutoka maeneo ya Chanika, Msongola, Zingiziwa na Majohe hivyo kupunguza muda na gharama ambazo wananchi wamekuwa wakitumia kufuata huduma hizo umbali wa kilometa 30 kwenda hospitali ya Amana ya Rufaa.

  Ludovic alisema ujenzi wa mradi huo hadi utakapokamilika utagharimu dola la milioni 4 sawa na sh.bilioni 8.8 za kitanzania.Balozi wa Korea nchini , Geum-young Song amesema wakorea hawafurahishwi wanapoona mama na mtoto wanapoteza maisha wakati wa kujifungua nchini Tanzania.

  "Nchi yetu kupitia shirika la Koica imeamua kujitolea kujenga hospitali hii ili kuwasaidia wananchi wa Tanzania kupata huduma bora ya afya ya mama na mtoto wakati wa kujifungua kwani hatupendi kuona wanapoteza maisha wakati wa kujifungua" alisema Young Song.

  Balozi huyo aliipongeza serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na nchi ya Korea katika shughuli mbalimbali jambo linaloimarisha uhusiano baina ya wananchi wa nchi hizo.
  Wananchi wa Chanika wakiwa kwenye hafla hiyo ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali yao.
  Diwani wa Kata ya Chanika, Mr Massaburi akitoa neno la Shukurani kwa RC Makonda, Serikali pamoja na Serikali ya Korea kwa ujenzi wa Hospitali hiyo
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chanika wakiwa kwenye hafla hiyo.
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chanika wakitoa burudani katika hafla hiyo.


  Wasanii wakitoa burudani katika hafla hiyo.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Manispaa ya Ilala na Korea Kusini.Na Dotto Mwaibale

  0 0

  DSC_1352Mama Samia akipata picha ya pamoja na familia ya Millen Magese

  DSC_1347Mama Samia Suluhu akiwa na Millen Magese na rafiki zake wakati wa tukio hilo..
  DSC_1364Mustafa akiwa pamoja na Mama Samia na Millen
  DSC_1371
  Baadhi ya Madaktari ambao ni wataalam wa kushughulikia tatizo la Endometriosis akiwemo Dkr. Kiiruki wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Samia na Millen Magese
  DSC_1400DSC_1367
  Kaka wa Millen Magese akiwa akipata picha pamoja na Mama Samia na marafiki wengine wakiweo kutoka
  DSC_1376Baadhi ya waandishi wa Habari wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Samia pamoja na Millen wakati wa tukio hilo
  DSC_1387Baadhi ya wanahabari wa kiume wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Samia pamoja na Millen wakati wa tukio hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam katika makazi Makamu wa Rais. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).  DSC_1274Mwandada Millen akiwa pamoja na Mama Samia wakati wa tuki hulo. Kushoto ni Katibu wa Makamu wa Rais.DSC_1282Millen akimuonyesha Mama Samia eneo linalomsumbua katika tatizo lake hilo
  DSC_1323Mama Samia akieleza namna walivyopokea tatizo hilo la Millen ambapo amemweleza kuwa Serikali itaendelea kupambana nalo tatizo hilo hivyo kumuakikishia Millen na taasisi yake kumuunga mkono.
  DSC_1326Mama Samia akimfuta machozi Millen ambapo alimwelezea kuwa kwa sasa asiie tena kwani Serikali itahakikisha inapambana na ugonjwa huo ilikusaidia wanawake wengi hapa nchini.
  nightofhope17Mama Samia akiangalia moja ya tuzo hiyo..
  DSC_1337Millen Magese akimkabidhi tuzo yake hiyo Mama Samia wakati wa tukio hilo
  DSC_1361Mama Samia akiwa katika picha pamoja na rafiki wa Magese na wageni wengine waliojumuika katika tukio hilo..

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Watumishi wa Serikali pamoja na Wadau walio chini ya wizara yake wa mkoa wa Tabora ambapo aliwaambia kuwa atawaondoa wala rushwa na matapeli katika michezo nchini.
  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akizungumza na viongozi wa CCM mkoa wa Tabora mara baada ya kumaliza kutia saini kitabu cha wageni na kuwataka wana CCM wote kuisoma kwa umakini ilani ya uchaguzi ya CCM 2015-2020 kwani ndio inayotekelezwa na serikali ya awamu ya 5.
  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo ya mitambo ya kurusha matangazo ya TBC mkoani Tabora kuroka kwa Mkuu wa kituo cha TBC Tabora Ndugu AMani Ganally Kalelesi.

  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na watumishi wa serikali waliochini ya wizara yake pamoja na washika dau wa habari, utamaduni sanaa na michezo wa mkoa wa Tabora ikiwa sehemu ya ziara yake yenye lengo la kuifanya wizara yake kumfikia kila mtu nchini na si kuishia Dar es Salaam tu.
  Katibu wa CHANETA mkoa wa Tabora Mwalimu Mwajuwa Yusufu akisoma taarifa ya chama chao pamoja na changamoto zinazowakabili kwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
  Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu mkoa wa Tabora Ndugu Lawrence Safari akichangia maoni mbali mbali ya kuboresha michezo nchini kwenye mkutano na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye.
  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za CCM mkoa wa Tabora ambapo aliwataka Mawaziri wanaofanya ziara kwenye mikoa mbali mbali wajenge utamaduni wa kupitia kwenye ofisi za chama na kusaini kitabu cha wageni kwani chama ndicho kimetengeneza ilani inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano.

  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (mwenye kaunda suti nyeusi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wa kwaya kutoka kikosi cha 823 KJ Msange JKT mkoani Tabora.

  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na watumishi na wadau walio chini ya wizara yake wa mkoa wa Singida ambapo alisisitiza kuwa kila manispaa inatakiwa kuwa na afisa habari ambaye anapata nafasi ya kuingia kwenye vikao vya maamuzi.


  0 0

  Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akikagua kwaride rasmin aliloandaliwa na Jeshi la Polisi alipofika kufunga mafunzo ya ungozi mdogo katika chuo cha Polisi Ziwani Zanzibar.
  Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akimvisha cheo mmoja waaskari waliofanya vizuri zaidi G.944 Makuza Azekiel Shuka kwa niaba ya wenzake katika sherehe ya kumaliza mafunzo ya uongozi mdogo kwa ngazi ya Koplo, Sajenti na Stafu Sajenti yaliyofanyika Chuo cha Polisi Ziwani Zanzibar.
  Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akipokea salamu ya heshima kwa Maafisa na wahitimu wa mafunzo ya uongozi mdogo katika chuo cha Polisi Ziwani Zanzibar.
  Maafisa na wahitimu wa uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi wakitoa saluti kwa mgeni rasmini Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali.
  Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi katika viwanja vya Jeshi hilo Ziwani Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga-Habari Maelezo Zanzibar.

  Na Khadija Khamis /Maryam Kidiko –Maelezo Zanzibar

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwataka wahitimu wa mafunzo ya uongozi mdogo kutumia mafunzo waliyoyapata ili kuleta mageuzi makubwa ya utendaji katika sehemu zao za kazi.

  Balozi Seif ameeleza hayo leo katika sherehe za ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la Polisi ngazi ya koplo, sajenti na staff sajenti yaliyofanyika katika viwanja nya Polisi Ziwani mjini Zanzibar.

  Amesema kuyatumia mafunzo hayo vizuri katika utendaji wa kazi itapelekea kupunguza uhalifu na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi.

  “Nategemea mtabadilika na kuwa watendaji wazuri wanaochukia rushwa, kesi zitaendeshwa kwa haraka , haki itatendeka katika kutekeleza majukumu na haki za binaadam zitazingatiwa kwa lengo la kujenga heshima ya Serikali na kuleta uhusiano wa karibu baina yenu na Wananchi “Alisema Balozi.

  Aidha alilitaka Jeshi la polisi kutopuuza uhalifu mdogo mdogo kwani uhalifu huo hatimae hupelekea uhalifu mkubwa na kusababisha uvunjifu wa amani katika nchi.

  Nae Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame amewakumbusha wahitimu hao kuwa wanawajibu mkubwa wa kuwalinda raia na mali zao pamoja na kulinda sheria za nchi.

  Hata hivyo amewataka kufanya kazi kwa kutumia elimu waliyoipata chuoni kwa vitendo, kuwaelimisha na kuwaongoza kwa uweledi askari huko vituoni mwao.

  Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa chuo cha Polisi Zanzibar Deusdedit Kaizilege Nsimeki amesema Jeshi la polisi litaendelea kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi ili kuwajengea uwezo na uwelewa wa umuhimu wa utii wa sheria bila ya kushurutishwa.

  Mafunzo ya uongozi mdogo wa vyeo vya Koplo, Sajenti na Staff sajenti yalifunguliwa rasmi tarehe 16/02/2016. Yakiwa na jumla ya wanafunzi 1532 kati ya hao kozi ya koplo 591, kozi ya Sajenti 706 na kozi ya Staff sajenti 235.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi na kuanza kwa ujenzi  wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifungua  jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akifungua ramani ya mradi wa barabara ya juu eneo la Tazara kuashiria ufunguzi rasmi na kuanza kwa ujenzi  wa mradi huo Tazara Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea maelekezo kuhusu mradi wa barabara za juu eneo la Tazara kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wakala wa barabara (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale katika ufunguzi rasmi wa mradi huo Jijini Dar es Salaam.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbaliwa kitaifa na kimataifa wakati wa ufunguzi rasmi na kuanz akwa ujenzi  wa mradi wa barabara ya juu Tazara Jijini Dar es Salaam. 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, eneo la Tazara Jijini Dar es salaam ambayo inatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018.

  Sherehe ya uzinduzi wa mradi huo imefanyika kando ya eneo la makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Mameya wa Jiji la Dar es salaam na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida.


  Barabara hiyo ya juu itakuwa ya kwanza kujengwa hapa nchini na ujenzi wake umepangwa kugharimu takribani shilingi Bilioni 100 ambapo kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3.


  Barabara ya juu itakayojengwa itakuwa na njia nne na urefu wa mita 300 kutokea maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, na inatarajiwa kupunguza kero ya msongamano wa magari yaendayo na yatokayo Uwanja wa ndege na Bandari ya Dar es salaam.


  Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema barabara hiyo inajengwa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya serikali yake ya kumaliza tatizo la msongamano wa magari Jijini Dar es salaam, ambao kwa mwaka 2013 pekee utafiti umeonesha ulisababisha upotevu wa shilingi Bilioni 411.55


  Rais Magufuli amebainisha juhudi nyingine za kukabiliana na msongamano wa magari Jijini Dar es salaam kuwa ni pamoja na kujenga barabara  ya njia sita ya Dar es salaam hadi Chalinze ambayo itakuwa na Flyover tano, ujenzi wa barabara nyingine za juu katika makutano ya barabara za Nelson Mandela, Morogoro na Sam Nojuma eneo la Ubungo na ujenzi wa daraja jipya la Salander lenye urefu wa kilometa 6.23 kuanzia Coco Beach hadi hospitali ya Agha Khan.


  Juhudi nyingine ni ujenzi wa awamu ya pili wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika barabara za Kilwa, Chang'ombe na Kawawa, na ujenzi wa awamu ya tatu wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika barabara za Nyerere - Gongo la Mboto na Uhuru - Azikiwe.


  Aidha, Rais Magufuli amezungumzia awamu ya kwanza ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, kuwa serikali yake imelazimika kusimamisha kuanza kwa huduma hiyo baada ya kubaini dosari katika mkataba wa mradi ambazo zingesababisha serikali kupoteza fedha nyingi na wananchi kutwishwa mzigo mzito wa viwango vikubwa vya nauli, na amewahakikishia wananchi wa Dar es salaam kuwa mabasi hayo yataanza kutoa huduma hivi karibuni baada ya kurekebisha kasoro zilizobainika.


  Dkt. Magufuli pia amezungumzia usafi wa Jiji la Dar es salaam kwa kuwataka viongozi wa Manispaa zote za Jiji, kuhakikisha wanatafuta namna ya kudhibiti utupaji hovyo wa takataka ikiwemo kutoza faini kubwa kwa watakaokamatwa wakitupa takataka hovyo.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es salaam

  16 Aprili, 2016

  0 0

  Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Mtibwa Sugar, Majaliwa Shaban katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijii Dar es Salaam. Yanga imeshinda 1-0 na kufikisha pointi 59 na kuongoza katika msimamo wa Ligi huku ikifuatiwa na Simba yenye Pointi 57. (Picha na Francis Dande)
  Mshambukiaji wa Yanga, Thaban Kamusoko akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Mtibwa Sugar.
  Kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
  Donald Ngoma akipiga kwa kisigino huku akizongwa na beki wa Mtibwa Sugar, Andrew Vicenti.
  Hapo je utaweza......
  Mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu (kulia) akitafuta mbinu za Henry Joseph katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Henry Joseph akichuana na mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe (kushoto).
  Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe akichuana na beki wa Mtibwa Sugar, Andrew Vicent
  Henry Joseph akipeana mkono na kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi.
  Kocha na wachezaji wa Yanga wakitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo.
  Harua Niyonzima akibadilishana mawazo na Simon Msuva baada ya mchezo kumalizika.
  Kocha wa Yanga, Mecky Maxime kulia akiwa na msaidizi wake Zuberi Katwila.
  Kikosi cha mtibwa Sugar kilichoanza leo
  Kikosi cha Yanga kilichoanza leo.  Deus Kaseke akiwatoka mabeki wa Mtibwa Sugar.  Simon Msuva akimtoka beki wa Mtibwa Sugar.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunziza amemtumia ujumbe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, akimhakikishia kuwa hali ya Burundi ni shwari na amemuomba awasihi wananchi wa Burundi waliokimbia nchi yao warejee nyumbani.

  Barua yenye ujumbe huo, imewasilishwa kwa Rais Magufuli leo tarehe 16 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam na Mjumbe Maalum wa Rais Nkurunziza ambaye ni Mnadhimu wa Jeshi la Burundi Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye.


  Meja Jenerali Ndayishimiye amemueleza Rais Magufuli kuwa Rais wa Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunziza amemtuma kuleta barua hiyo pamoja na shukrani za dhati kwa Tanzania ambayo ni rafiki, jirani na ndugu wa kweli wa Burundi kwa ushirikiano mzuri inaoupata kutoka Tanzania katika masuala mbalimbali.


  "Burundi na Tanzania ni ndugu wa kweli, na sisi Burundi tunaiona Tanzania na nchi yetu kama Baba na mtoto wake" amesema Meja Jenerali Ndayishimiye.


  Kwa upande wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemshukuru Rais Nkurunziza kwa kumtumia ujumbe huo na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kuwa rafiki na ndugu wa dhati wa Burundi kama ambavyo mahusiano ya nchi hizi mbili yamejengwa tangu zamani.


  Kuhusu hali ya Burundi Rais Magufuli amesema anaamini kuwa wasuluhishi mgogoro wa nchi hiyo ambao ni Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu wa Tanzania Mheshimiwa Benjamin William Mkapa watafanikiwa kusuluhisha mgogoro huo.


  "Naomba umwambie Rais Mheshimiwa Nkurunziza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Burundi, na tunawaombea mgogoro uishe ili muendelee kuijenga nchi yenu"Amesema Rais Magufuli.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es salaam


  16 Aprili, 2016


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongozana na Meneja Mkuu wa Uzalishaji katika kiwanda cha Ushoni wa Nguo za aina mbalimbali Mw. Ritesh Krishandev Beesony, wakati alipowasili katika kiwanda hicho leo April 16,2016 kwa ajili ya kutembelea na kuangalia utendaji kazi zinazofanywa kiwandani hapo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia nguo za aina mbalimbali zinazotengenezwa na kiwanda cha Ushoni cha Mazawa kiopo Msamvu Mkoani Morogoro wakati alipotembelea  kiwanda hicho leo April 16,2016 kwa ajili ya kuangalia utendajia kazi zinazofanywa kiwandani hapo. 
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia nguo za aina mbalimbali zinazotengenezwa na kiwanda cha Ushoni cha Mazawa kiopo Msamvu Mkoani Morogoro wakati alipotembelea  kiwanda hicho leo April 16,2016 kwa ajili ya kuangalia utendajia kazi zinazofanywa kiwandani hapo. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia nguo za aina mbalimbali zinazotengenezwa na kiwanda cha Ushoni cha Mazawa kiopo Msamvu Mkoani Morogoro wakati alipotembelea  kiwanda hicho leo April 16,2016 kwa ajili ya kuangalia utendajia kazi zinazofanywa kiwandani hapo. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongea na Viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha Ushoni wa Nguo cha Mazawa kiliopo Msamvu Mkoani Morogoro wakati wa  ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho leo April 16,2016. Picha na OMR

  0 0

   Madansa wa msanii wa muziki wa kizazi kipya bongo fleva, Diamond   Platinum’s wakifanya yao wakati wa bonanza la Vodacom fungua semester lililoandaliwa na Vodacom Tanzania lililoshirikisha vyuo vikuu vyote vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Mabibo hosteli hapo jana.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya bongo fleva, Diamond   Platinum’s akiwapagawisha mashabiki wake kwenye bonanza la Vodacom fungua semester lililoandaliwa na Vodacom Tanzania lililoshirikisha vyuo vikuu vyote vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Mabibo hosteli hapo jana.
   Diamond   Platinum’s akiwapagawisha mashabiki wake kwenye bonanza la Vodacom fungua semester lililoandaliwa na Vodacom Tanzania lililoshirikisha vyuo vikuu vyote vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Mabibo hosteli hapo jana.
   Nyomi ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya jijini Dar es salaam na mashabiki wa msanii wa muziki wa kizazi kipya bongo fleva, Diamond   Platinum’s(hayupo pichani)wakipagawa naye wakati wa bonanza la Vodacom fungua semester lililoandaliwa na Vodacom Tanzania lililoshirikisha vyuo vyote vikuu vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya  Mabibo hosteli hapo jana. 


  0 0

   Wananchi wakiwa wamesheheni uwanjani wakati wa sherehe hizo za kumpongeza Diwani wa Kata ya Engarenaibor 
   Msemaji wa CCM Ole Sendeka akiwa na wenyeji baada ya kuwasili Kata ya Engarenaibor wilayani Longido mkoani Arusha akiwa katika ziara ya kikazi jana.
   Mwinjilisti akiiimba wimbo maalum wa makaribisho, Msemaji wa CCM Ole sendeka alipowasili kwenye sherehe hizo,katika Kata ya Engarenaibor wilayani Longido mkoani arusha
   Dada wa Kimasai akilia kutekeleza moja ya mila za kupokea mgeni muhimu, Msemaji wa CCM Ole Sendeka alipofika katika Kata ya Engarenaibor wilayani Longido akiwa katika ziara ya kikazi
   Wenyeji wa Jamii ya Kimasai wakiwa wamejipanga kumpokea Ole Sendeka kwenye eneo la sherehe katika kata ya Engarenaibor
   Msemaji wa CCM, Ole sendeka akisalimiana na baadhi ya viongozi alipowasili kwenye uwanja wa sherehe, katika Kata ya Engarenaibor wilayani Longodo mkoani arusha
   Ole sendeka akimtia baraka kimila mwari wa Kimasai alipowasili kwenye uwanja wa sherehe katika Kata ya Engarenaibor wilayani Longido mkoani Arusha
   Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akiwasalimia wananchi alipowasili katika Kata ya Engarenaibor kushiriki sherehe za kumpongeza Diwani wa kata hiyo Peter Ndereko, jana
   Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akisaini kitabu chawageni baada ya kuwasili kwenye eneo la sherehe ua kumpongeza diwani wa Kata ya Engarenaibor Peter Ndereko (kushoto)
   Mjumbe wa NEC, ambaye pia ni Oisa mwandamizi katika Idara ya Itikadi na Uenezi Makao makuu ya CCM, Kilumbe Ng'enda akiwa na Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Sharusha Shaban Mdoe wakati wa sherehe ya kumpongeza Diwani wa Kata ya Engarenaibor wilayani Longido mkoani Arusha jana

   Mchungaji akifanya maombi wakati wa sherehe za kumpongeza diwani wa Kata ya Engarenaibor wilayani Longido zilizohudhuriwa na Msemaji wa CCM Ole Sendeka jana
   Msemaji wa CCM Ole Sendeka akifanyiwa maombi maalum wakati wa sherehe za kumpongeza Diwani wa Kata ya Engarenaibor wilayani Longido mkoani Arusha jana. Pamoja naye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Lekule Laiza
   Msemaji wa CCM Ole Sendeka akifanyiwa maombi maalum wakati wa sherehe za kumpongeza Diwani wa Kata ya Engarenaibor wilayani Longido mkoani Arusha jana. Pamoja naye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Lekule Laiza
   Mkuu wa wilaya ya Longido mkoani Arusha Ernest Kahindi akizungumza wakati wa sherehe za kumpongeza Diwani wa Kata ya Engarenaibor  
   Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha Shabani Mdoe akitoa utambulisho wakati wa sherehe za kumpongeza Diwani wa Kata ya Engarenaibor, Peter Ndereko zilizofanyika jana katika kata hiyo

   Vijana wa Kimasai wakionyesha umahiri wao wakati wa sherehe za kumpongeza Diwani wa Kata ya Engarenaibor wilayani Longido mkoani Arusha zilzofanyika jana
   Mjumbe wa NEC ambaye pia ni Ofisa mwandamizi katika Idara ya Itikadi na Uenezi makao Makuu ya CCM akimtuza Naanyu Mollel baada ya kufurahishwa na uimbaji wake wakati wa sherehe za kumpongeza Diwani wa Kata ya Engarenaibor wilayani Longido mkoani Arusha
   Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akiwa na  Naanyu Mollel baada ya kufurahishwa na uimbaji wake wakati wa sherehe za kumpongeza Diwani wa Kata ya Engarenaibor wilayani Longido mkoani Arusha
   Msemaji wa CCM Ole Sendeka akimtawaza Diwani wa Kata ya Engarenaibor wilayani Longido mkoani Arusha, Peter Ndereko kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Kata hiyo, wakati wa sherehe za kumpongeza diwani huyo jana
   Diwani wa Kata ya Engarenaibor Peter Ndreko akionyesha zana alipokabidhiwa na Msemaji wa CCM Ole Sendeka baada ya kumtawaza kuwa Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Kata hiyo jana. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Lekule Laizer
  .


   Mzee wa Kimila  Ngaya Ole Sembekwan akimkabidhi mkuki Diwani wa Kata ya Engarenaibor Peter Ndereko, wakati wa sherehehe za kumpongeza diwani huyo. Katikati ni Msemaji wa CCM Ole Sendeka
   Msemaji wa CCM Ole Sendeka akivishwa shuka la kimila kuzawadiwa wakati wa sherehe za kumpongeza Diwani wa Kata ya Engarenaibor PeterNdereko zilizofanyika jana. 
   Msemaji wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisaini kitabu cha Wageni alipopita Ofisi ya CCM mkoa wa Arusha akiwanjiani kwnda wilayani Longido akiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo jana. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Lekule Laiza na kulia ni Katibu Mwenezi wa mkoa huo, Shabani Mdoe
   Katibu Mwenezi wa mkoa wa Arusha Shabani Mdoe akitambulisha wageni, Msemaji wa CCM na Mjumbe wa NEC, Ole Sendeka alipofika Ofisi ya CCm mkoa wa Arusha akiwa njiani kwenda wilayani Longido mkoani humo jana akiwa katika ziara ya kikazi
   Msemaji wa CCM Ole Sendeka akizungumza na viongozi wa CCM mkoa wa Arusha alipofika Ofisi ya CCM mkoani huni humo akiwa njiani kwenda wilayani Longido akiwa katika ziara ya kikazi
   Vijana wa bodaboda wakimsalimia Msemaji wa CCM, Ole Sendeka wakati wa mapokezi akiwa njiani kwenda wilayani Longido mkoani Arusha kikazi. Kushoto ni wenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Lekule Laiza
   Msafara wa Msemaji wa CCM Ole Sendeka ukienda wilayani Longido mkoani Arusha
   Hiyo Ndiyo Longido
   Vijana wa Bodaboda wakiongoza msafara wa Msemaji wa CCM, Ole Sendeka ulipokuwa njiani kwenda Kata ya Engarenaibor wilayani Longido mkoani Arusha 
   Msemaji wa CCM Ole Sendeka akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Longido Ernest Kahindi, alipofika Ofisi ya CCm ya wilaya hiyo akiwa njiani kwenda Kata ya Engarenaibor akiwa katika ziara ya kikazi
   Mwanannchi wa Longido
   Msemaji wa CCM Ole Sendeka akienda katika Ofisi ya CCM wilaya ya Longido mkoani Arusha
   Msemaji wa CCM, Ole sendeka akisaini kitabu cha wageni alipowasili Ofisi ya CCM wilaya ya Longido mkoani Arusha jana
   Swaga za vijana wa Longido
   Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akiwa na kinamama wa Longido mkoani Arusha kwenye Ofisi ya CCM ya Longido
   Msemaji wa CCM, Ole Sendeka akiwa na kinamama wa Longido mkoani Arusha kwenye Ofisi ya CCM ya Longido
   Vijana wa bodaboda wakiongoza msafara wa Msemaji wa CCM Ole Sendeka  kwenda Kata ya Engarenaibor
   Kina mama wakimfurahia Msemaji wa CCM Ole Sendeka wakati msafara wake ukipita mitaani ulipowasili Kata ya Engarenaibor wilayani simanjiro mkoani Arusha
   Mgambo akielekeza msafara wa Msemaji wa CCM Ole sendeka kwenda kunakohusika katika Kata ya engarenaibor, Longido mkoani Arusha
   Wakazi wa Kata ya Engarenaibor wakimpokea wa burudani Msemaji wa CCM Ole Sendeka alipowasili katika kata ya Engarenaibor akiwa katika ziara ya kikazi jana
  PICHA ZAIDI>BOFYA HAPA

  0 0

  Na Editha Karlo wa blog ya Jamii, Kigoma

  MBUNGE wa Jimbo la kigoma Kusini ,Hasna Mwilima amewakabidhi msaada wa shilingi milioni sita na laki tatu na tani kumi na saba za vyakula kwa wahanga wa mafuriko katika Kijiji cha Kirando kata ya Sunuka Wilayani Uvinza.

  Akizungumza na Wananchi wa kijiji hicho wakati akikabidhi misaada hiyo iliyo tolewa na Halmashauri ya Uvinza na Mkoa wa Kigoma na wadau mbalimbali alisema serikali kwa kuwathamini wananchi imeamua kutoa misaada ilikuweza kuwasaidia wahanga waliopoteza mali zao wakati wa mafuliko.

  Mwilima alisema anaupongeza uongozi wa Mkoa wa kigoma na halmashauri zote kwa kutoa msaada wa vyakula vitakazo wasaidia waathirika hao katika kipindi hika ambacho wanajipanga kurekebisha makazi yao.

  Pia aliishukuru Halmashauri ya Uvinza kwa kuthamini Wananchi wake na kutoa msaada wa shilingi milioni tano na Mwenyekiti wa Halmashauli hiyo kuongezea laki mbili wameonesha jinsigani serikali ya awamu ya tano inavyo wathamini wananchi.

  “mimi kama mbunge wenu nitatoa shilingi milioni moja nitaongezea katika mchango wa Viongozi wengine waliotoa tutahakikisha tunashirikiana katika wakati waraha, wakati washida na nyakati zote tupo pamoja nitawahudumia ipasavyo ndugu zangu “, alisema Hasna.

  Hata hivyo alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuchangia Chakula tani saba kupitia michango iliyotolewa na Halmashauri zote za Mkoa ilikuweza kuwasaidia Wanakijiji waliokumbwa na mafuriko.

  Rehema Hassani ni mmoja kati ya Wahanga wa mafuriko pia ni Mkazi wa Kirando alisema kwaniaba yawanakijiji wenzake wanaishukuru Serikali pamoja na Mbunge kwa kutoa misaada hiyo tunaimani itatusaidia na tutaweza kujipanga upya na kuziendesha familia zetu.

  Aliiomba Serikali kuwapatia maeneo mengine waweze kujenga na kuondoka kuishi mabondeni ambapo mvua kubwa ikinyesha maji hujaa mtoni na kuingia ndani kupelekea mafuriko hivyo serikali igawe maeneo mengine yakuweka makazi.

  Msaada uliotolewa ni maharage kilo218,mchere kilo1240, unga , mihogo,mahindi, mashuka kwaajili ya zahanati 218,na mafuta ya kupikia na chumvi na shilingi milioni sita na laki tatu watakazo gawiwa wahanga wa mafuriko hayo zilizo tolewa na serikali pamoja na wadau mbalimbali.

  Mafuriko hayo yalitokea tarehe 13 mwezi wa pili mwaka huu kufuatia mvua kubwa iliyonyesha uharibifu mkubwa wa mali na kaya zipatazo 49 kukosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kusombwa na maji.
  Mbunge wa jimbo la Kigoma kusini Husna Mwilima akimkabidhi fedha shilingi. Milioni sita na laki tatu mwenyekiti wa kijiji cha Kirando Athumani Chuma kwaajili ya wahanga wa mafuriko katika kijiji hicho.
  Mhe. Hasna Mwilima akimkabidhi Bi rehema Issa mfuko wa sembe mmoja wa wahanga wa mafuriko katika kijiji cha kirando.
  Mhe. Hasna akiteta jambo na muathirika wa mafuriko katika kijiji cha Kirando.
  Sehemu ya chakula tani kumi na saba zilizokabidhiwa na mbunge wa jimbo la kigoma kusini Hasna Mwilima kwa wahanga wa mafuriko katika kijiji cha Kirando.
  Baadhi ya makazi ya wanakijiji cha Kirando yaliyokumbwa na mafuriko

  0 0


  Viongozi Shrika la Taifa Hifadhi ya Jamii NSSF wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakandarasi wa daraja la Kigamboni wakati lilipofunguliwa kwa ajili ya kupita magari kupita bure huku watembea kwa miguu na waendesha baiskeli wakipita bure. Daraja hilo litazinduliwa rasmi na Rais Dk. John Magufuli Jumanne tarehe 19.4.2016. 
  Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Karim Mataka akiwa katika eneo la daraja la Kigamboni mara baada ya kufunguliwa kwaajili ya kupita magari na waenda kwa miguu.
  Muonekano wa daraja la Kigamboni baada ya magari kuanza kupita.
  Eneo lililoandaliwa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi wakati wa uzinduzi rasmi.
  Pikipiki na magari yakipita darajani.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  Familia ya wanahabari kutoka media mbalimbali pamoja na baadhi ya wahariri walioshiriki mazishi ya mama wa mhariri mtendaji wa The New Habari Absalom Norman Kibanda aliyesimama katikati mwenye miwani mara baada ya maziko yaliyofanyika Rungwe mission wilayani Rungwe mkoani Mbeya jana mchana.
  Michuzi Media Group inakupa pole sana kwa msiba uliokupata mpiganaji Mwenzetu Absalom Kibanda,Tunaomba Mungu akupe uvumilivu wewe pamoja na ndugu wote katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wenu katika familia. Mungu alitoa na Mungu ametwaa jina la Bwana Lihimidiwe AMEN 

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe  wakati alipokwenda kumpa pole  kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha kaka yake   Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe   (kulia kwake) wakati alipokwenda kumpa pole  kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wanafamilia wakati alipokwenda  kumpa pole   Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe     kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwanasiasa mkongwe,Kingunge Ngombale- Mwiru  wakati alipokwenda  kumpa pole   Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe     kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu kushoto akimpatia maelezo Wazairi wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu a Mh. Jenista Mhagama maendeleo ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge unaotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu katikati, wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Steven Kebwe
  Baadhi ya wasanii wakiwa katika maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge unaotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu kesho.
  Maandalizi ya uzInduzi wa Mbio za Mwenge yakamilika mkoani Morogoro kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Mh. Steven Kebwe akiangali zoezi la matayarisho ya uzinduzi huo.
  Maandalizi ya uzunduzi wa Mbio za Mwenge yakamilika mkoani Morogoro kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Mh. Steven Kebwe akiangali zoezi la matayarisho ya uzinduzi huo na kushoto ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama.
  Baadhi ya watoto wa shule wakiwa katika maandalizi maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge unaotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu kushoto akimpatia maelezo Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu a Mh. Jenista Mhagama maendeleo ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge unaotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu

  0 0

   Wanandoa hao wakiwa katika pozi.
   Mchungaji Sostenes Langula wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God (EAGT) la Kiluvya Malango ya Mbinguni (kushoto), akifungisha ndoa hiyo.
   Bwana harusi Joseph Haule akimvika pete mke wake Delphina Mgesi wakati wa kufunga ndoa yao.
   Bibi Harusi Delphina Mgesi (kulia), akimvika pete ya ndoa mume wake Joseph Haule.
   Kaka yake Bwana harusi (mwenye suti katikati), akimtambulisha Joseph Haule kwa ndugu zake na mke wake
  .

   Mwanahabari Joseph Haule ambaye kwa sasa ni askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Joseph Haule akiwa katika ibada ya ndoa yake.

   Bibi Harusi, Delphina Joseph Haule Mgesi akiwa katika ibada ya ndoa yao na mume wake Joseph.
   Watoto watoa burudani katika harusi hiyo wakiwa kwenye ibada hiyo ya ndoa.
   Taswira katika ibada hiyo ya ndoa.
   Viongozi wa Kanisa hilo wakiwa kwenye ibada hiyo ya ndoa.
   Maharusi hao wakiwa na wapambe wao wakati wa ibada hiyo ya ndoa. Kushoto ni Mpambe wa Bwana Harusi Lameck Hussein na kulia ni Mpambe wa Bibi Harusi, Jacqualine Hussein.
   Taswira ndani ya kanisa hilo wakati wa ibada hiyo.
   Askofu Nicodemas Nyenye wa Kanisa hilo (wa pili kushoto), akiwafanyia maombi wanandoa hao baada ya kufunga ndoa akishirikiana na viongozi wenzake.
   Bwana harusi Joseph Haule akitia saini kwenye shahada yake ya ndoa. Anayeshuhudia kushoto ni mke wake kipenzi, Delphina Mgesi.
   Askofu  wa Kanisa hilo, Nicodemas Nyenye akiwapongeza wanandoa hao.
   Mwanahabari Joseph Haule na mke wake Delphina Mgesi, wakionesha shahada yao ya ndoa, baada ya kufunga pingu za maisha, Kanisa la Evangelist Assemblis of God Tanzania (EAGT) la Patimos Tungi, Kigamboni, Dar es Salaam jana. Bwana harusi ambaye hivi sasa ni askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), alikuwa mwandishi wa gazeti la Jambo Leo
   Waumini na wageni waalikwa wakiwa wamejipanga foleni wakati wakienda kuwapongeza wana ndoa hao.
  Kwaya ikitoa burudani.


older | 1 | .... | 822 | 823 | (Page 824) | 825 | 826 | .... | 1897 | newer