Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

MABORESHO YA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA NDIO MKOMBOZI WA SIASA NCHINI- MHE. JENISTER MHAGAMA

$
0
0
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja za wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam.
Mhe. Dkt Abdallah Possi, Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu) Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu akiteta jambo na Msajili wa vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi akitoa ufafanuzi wa hoja za wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti yam waka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Manaibu waziri ,Mhe Antony P. Mavunde na Mhe. Dkt Abdallah Possi
Mjumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe Richard Ndassa akiwasilisha hoja kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam. Kulia ni wajumbe wa kamati.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja za wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam. Kulia ni Mhe. Dkt Abdallah Possi, Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu .
Angelina Sanga, Katibu kiongozi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria akiwapitisha wajumbe (hawapo pichani) kwenye vifungu vya bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam.
Waadhi ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia kwa makini mawasilisho ya bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe. Jaji francis S. K Mutungi pamoja na Maaafisa Wandamizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiwa nje ya ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam Leo kabla ya kuanza kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Sheria wamepewa rai ya kushikamana na Serikali katika kuhakikisha kuwa maboresho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka1992 na Sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 yanafanyika ili kuondoa utata na migongano ya utekelezaji wa masuala ya siasa nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati akijibu swali kutoka kwa wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam ambao walihoji uhalisia wa utekelezaji wa sheria zililizopo sasa.

Wajumbe hao walihoji utitiri wa vyama vingi nchini ambavyo miaka nenda rudi havina madiwani wala wabunge na vingine kutoshiriki katika chaguzi . Wajumbe pia walihoji gharama ndogo za usajili wa vyama vya siasa ukilinganisha na hali ya maisha iliyopo kwa sasa.

Jambo lingine ambalo wajumbe wamehoji ni nafasi ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika kushughulikia migogoro ya kisiasa ndani na nje ya Vyama vya Siasa na ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi ndani ya vyama vya siasa.

Akijibu hoja hizo Mhe Mhagama amesisitiza kuwa maboresho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za uchaguzi ndio njia pekee itakayompa meno Msajili wa Vyama vya Siasa nchini katika kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

“Sheria tulizonayo ndio inatoa mwanya wa haya yote haya na ndio maana Serikali kwa sasa inaendelea na taratibu za kuboresha sheria hizi, tayari Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ameshawasilisha mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Vyama vya Sasa na Sheria ya gharama za uchaguzi na sisi tumeridhia , tunasubiri tu bunge kujadili ili ziweze kutumika”alisisitiza mhe Mhagama.

Imeandaliwa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

Rais Magufuli atuma salamu za Rambirambi kifo cha Askofu Mathias Issuja

$
0
0
ASKOFU AFARIKI: Askofu msaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mathias Issuja amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mt. Gaspar, Itigi, Dodoma.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Baraza la Askofu Tanzania (TEC) Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mhashamu Mathias Issuja Joseph, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 13 Aprili, 2016 Mkoani Singida.


Baba Askofu Mstaafu Mathias Issuja aliyekuwa na umri wa miaka 87, amekutwa na mauti katika Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Gaspar iliyopo Itigi, wilaya ya Manyoni Mkoani Singida alikokuwa akipatiwa matibabu.


Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema Askofu Mstaafu Mathias Issuja alikuwa Mzalendo wa kweli, kipenzi cha watu, aliyefanya kazi kubwa ya kuwajenga watu kiroho na kimwili, na kamwe mchango wake katika maendeleo ya Elimu, Afya na malezi ya watoto yatima hautasahaulika.


"Nimepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha Baba Askofu Mathias Issuja. Kazi kubwa aliyoifanya duniani kuwahudumia watu kiroho na kimwili ni vigumu kuipima, nitamkumbuka daima" Amesema Rais Magufuli.


Dkt. Magufuli amemuomba Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa, kufikisha pole nyingi kwa baraza la Maaskofu, Waumini wa Kanisa Katoliki na wote walioguswa na msiba huo na amemuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Amina.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

13 Aprili, 2016

Miss Tabata 2016 kuanza mazoezi Jumanne

$
0
0
Miss Tabata 2014 Ambasia Mallya
MAANDALIZI ya kumsaka mrembo wa kitongoji cha Tabata mwaka huu ‘Miss Tabata 2016’ yanatarajiwa kufanyika kuanzia Jumanne Aprili 19 kwenye Ukumbi wa Da West Park, Tabata jijini Dar es Salaam.
 
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana kuwa warembo wote waliojiandikisha wanatakiwa kufika mazoezini na bado fomu za kushiriki shindano hilo zinaendelea kutolewa.
 
Kapinga alisema kwamba Keen Arts ambayo ni kampuni tanzu ya Bob Entertainment ndiyo imepewa kibali cha kuendesha shindano hilo na waratibu wa taifa Lino Agency iliyoko chini ya mkurugenzi wake Hashim Lundenga.Mratibu huyo alisema uzinduzi rasmi wa shindano hilo utafanyika mwishoni mwa mwezi huu.
 
“Baada ya uzinduzi washiriki watatembelea hifadhi ya Mikumi na Dar es Salaam Zoo ikiwa ni njia mojawapo ya kutangaza utalii wa ndani,” Kapinga alisema.Aliwataka warembo wenye sifa za kushiriki shindano hilo kujitokeza na kusema fomu hizo pia zinapatikana kwenye ukumbi wa Da West Park na ofisi za Miss Tanzania zilizoko Mikocheni.
 
Miss Tabata ni miongoni mwa vituo vitatu vilizoko kanda ya Ilala huku vingine vikiwa ni Ukonga na Dar City Centre.Washiriki watano kutoka kila kituo watashiriki kwenye shindano la Miss Ilala na hatimaye Miss Tanzania baadaye mwaka huu.
 
Ambasia Mallya ndiye mrembo anayeshikilia taji la kitongoji hicho ambacho kimetoa wawakilishi waliofanya vizuri katika ngazi ya taifa.Wadhamini ambao wameshathibitisha kudhamini shindano hilo ni pamoja na CXC Africa, Fredito Entertainment, Saluti5 na Bob Entertainment.

OLE SENDEKA AWASILI KILIMANJARO LEO

$
0
0
Msemaji wa CCM, Cheristopher Ole Sendeka akizungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wilaya za mkoa wa Kilimanjaro baada ya kuwasili akiwa katika ziara ya kikazi leo.
Msemaji wa CCM, Cheristopher Ole Sendeka akizungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wilaya za mkoa wa Kilimanjaro baada ya kuwasili akiwa katika ziara ya kikazi leo. Picha na Bashir Nkoromo).
Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka akiiingia ukumbini kuzungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM kutoka wilaya za mkoa wa Kilimanjaro, leo.
Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM kutoka wilaya za mkoa wa Kilimanjaro wakimpokea Ole Sendeka alipoingia ukumbini
Ole Sendeka baada ya kuingia ukumbini
Msemaji Mkuu wa CCM, Ole Sendeka akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ukumbini kuzungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM kutoka wilaya za mkoa wa Kilimanjaro leo.
 

TMAA yang’ara katika sekta ya madini

$
0
0
Mtendaji Mkuu  wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini  Tanzania (TMAA), Dominic Rwekaza (pichani) akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya wakala huo kwa mwaka wa  fedha 2015/2015 mbele ya Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na watendaji wa Wizara  ya Nishati na Madini (hawapo pichani)
Mtendaji Mkuu  wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini  Tanzania (TMAA), Dominic Rwekaza (mbele) akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya wakala huo kwa mwaka wa  fedha 2015/2015 mbele ya Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na watendaji wa Wizara  ya Nishati na Madini.
Sehemu ya wajumbe  wa  Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na watendaji wa Wizara  ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini  taarifa utekelezaji wa majukumu ya  Chuo cha Madini Dodoma (MRI) kwa mwaka wa fedha 2015/2016, iliyokuwa inawasilishwa na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Musa Magufuli (hayupo pichani)
Sehemu ya maofisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini na  Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) wakifuatilia kwa makini  taarifa mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Profesa Abdulkarim Mruma akisisitiza jambo katika kikao hicho.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) na Kaimu Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Ally Samaje (kulia) wakifuatilia kwa makini taarifa mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kikao hicho.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI) Musa Magufuli (pichani) akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya chuo hicho kwa mwaka wa fedha 2015/2016, mbele ya  wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na watendaji wa Wizara  ya Nishati na Madini (hawapo pichani).
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akifafanua jambo katika kikao hicho.


TMAA yang’ara katika sekta ya madini
Kamati ya Bunge yaipongeza
Yatakiwa kuongezewa fedha zaidi

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam 

Kamati ya  Kudumu ya Bunge  ya Nishati na Madini  hivi karibuni iliupongeza Wakala wa  Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA)  kwa  kazi nzuri ya kudhibiti madini yanayotoroshwa  nje ya nchini

 Wakizungumza kwa nyakati tofauti wajumbe wa kamati hiyo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya wakala huo kwa kipindi cha  mwaka wa fedha 2015/2016, walisema kuwa wakala umechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la mapato katika sekta ya madini na kuitaka serikali kuuwezesha zaidi ili uweze kuzalisha zaidi na hivyo kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kupitia sekta ya madini.

Mjumbe wa kamati hiyo, Suzan Kiwanga alisema kuwa TMAA ina uwezo mkubwa wa kufanya kazi ya kudhibiti madini yanayotoroshwa nje ya nchi  kupitia  wataalam wake walioko migodini na  viwanja  vya ndege, hivyo ni vyema wakawezeshwa ili kufanya kazi hiyo  kwa bidii na uaminifu mkubwa.

“Kulingana na  ripoti yao, TMAA imefanya kazi kubwa ya kuokoa mabilioni ya shilingi  kupitia ukamataji wa madini yaliyokuwa yanatoroshwa nje ya nchi, kazi  waliyoifanya ni kubwa yenye kuhitaji  uaminifu mkubwa,  hivyo wakiwezeshwa zaidi wana uwezo wa kufanya vizuri zaidi,” alisema Kiwanga

Naye mjumbe  mwingine wa kamati hiyo, Ikupa Alex aliongeza kuwa  wahalifu wanaokamatwa na TMAA wanatakiwa kufikishwa katika vyombo  vya sheria  na kutozwa faini kubwa  ili iwe  fundisho wa watoroshaji wengine.

“ Huu  wakala ndio unaowezesha  Mamlaka  ya Mapato  Tanzania (TRA) kubaini kodi inayostahili kulipwa na makampuni yanayojishughulisha na utafutaji na uchimbaji wa madini nchini, rai yangu ni wakala huu kuwezeshwa zaidi katika nyanja zote ikiwamo  rasilimali fedha na  rasilimali watu ili uweze kufanya   kwa ufanisi zaidi,” alisema Alex.

Awali  akielezea  mafanikio  ya  TMAA  tangu kuanzishwa kwake Mtendaji Mkuu  wa wakala huo, Dominic Rwekaza alisema  kwa kipindi cha  mwaka 2009 hadi Januari 2016, kampuni mbalimbali zimelipa jumla ya Shilingi bilioni 680.5 kama kodi ya mapato.


Aliongeza kuwa mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na kuongezeka kwa malipo ya mrabaha kutokana na madini ya ujenzi na viwandani baada ya kufanyika kwa ukaguzi  ambao umewezesha  kiasi cha Shilingi bilioni 14 kulipwa kama mrabaha katika kipindi cha Juni 2011 hadi Januari 2016.

Alisema malipo hayo yametokana na uzalishaji wa jumla ya tani milioni 33.6 za madini ya ujenzi na viwandani yenye thamani ya Shilingi bilioni 465.7 kulingana na uhakiki uliofanywa na Wakala.

Aliendelea kueleza kuwa wakala  ulichangia kwa uongezeko  la malipo ya mrabaha kutokana na shughuli za uchenjuaji wa marudio kwa kutumia teknolojia ya vat leaching ambapo kiasi cha shilingi  bilioni 7.5 kililipwa kama mrabaha katika kipindi cha Julai 2012 hadi Januari 2016.

Alifafanua kuwa malipo hayo yalitokana na uzalishaji na mauzo ya dhahabu kutoka kwa wazalishaji wanaotumia teknolojia ya “vat leaching” katika mikoa ya Mwanza, Geita na Mbeya ambapo kulikuwa na jumla ya kilo 3,046 za dhahabu zenye thamani ya Shilingi bilioni 179.8 kulingana na uhakiki uliofanywa na Wakala.

Alisisitiza kuwa  wakala uliwezesha  serikali  kupata mrabaha na takwimu sahihi za madini yaliyozalishwa na migodi mikubwa nchinikupitia  ukaguzi na uhakiki madini yaliyozalishwa na kuuzwa na migodi mikubwa ya Biharamulo, Bulyanhulu, Buzwagi, Geita, New Luika, North Mara, TanzaniteOne, Mwadui na Ngaka, ambapo ukaguzi huo ulisaidia kujua kiasi na thamani halisi ya madini yaliyozalishwa na kuuzwa.

“Ukaguzi huo umewezesha kukusanywa kwa jumla ya Dola za Marekani milioni 430 kama mrabaha kutoka kwenye migodi hiyo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2009 hadi 2015,” alisema  Rwekaza.

Akielezea udhibiti  wa utoroshwaji  wa madini kupitia  viwanja vya kimataifa vya ndege hapa nchini, Rwekaza alifafanua kuwa wakala  ulianzisha ukaguzi maalum wa kukagua madini yanayosafirishwa nje ya nchi kupitia Viwanja vya Ndege vya Julius Nyerere - Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza na kuwakamata watu wasio waaminifu wanaojaribu kusafirisha madini nje ya nchi kinyume cha sheria.

Alisema kupitia  ukaguzi huo  jumla ya matukio 89 ya utoroshaji wa madini yaliripotiwa hadi Desemba 2015 ambapo madini hayo yalikuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 10.8 na Shilingi bilioni 1.1. na kuongeza kuwa wahusika wamechukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.

Aliongeza kuwa  wakala  umekuwa ukifanya ukaguzi wa mara kwa mara wa shughuli za ukarabati na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya migodi mikubwa, ya kati na midogo ambapo wahusika wamekuwa wakipewa maelekezo yenye lengo la kuboresha hali ya mazingira kwenye maeneo yao.
 

ISMAIL ADEN RAGE AJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF, AHIMIZA WANAMICHEZO KUJIUNGA NAMPANGO HUO

$
0
0
RAIS wa zamani wa Klabuya Simba ya Dar es Salaam, Alhaj Ismail Aden Rage, (kushoto), akipokea kadi yake ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, kutoka kwa Meneja Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa PSPF, Bi.Costantina Martin, makao makuu ya PSPF, katikati ya jiji la Dar es Salaam, Aprili 14, 2016. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Alhaj Rage akionyesha kadi hiyo

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

RAIS wa zamani wa Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Alhaj Ismael Aden Rage, amejiunga na mpangowa uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Aprili 14, 2016.

Rage ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Tabora mjini, kufuatia kujiunga huko, amefaidika kuingizwa kwenye fao la huduma ya afya litolewalo na Mfuko huo kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF ambao una ushirikiano wa kutoa huduma za afya kwa wanachama wa PSPF wanaotaka kufaidikana huduma hiyo.

“Nitoe wito kwa wanamichezo wakiwemo wa mpira wa miguu, kuchangamkia fursa hiyo kwani mambo sasa yamebadilia kujiunga na PSPF kupitia mpango huu wa hiari ambao unamruhusu mtu binafsi au vikundi kujiunga na uanachama, lakini pia kutokana na kupanda kwa huduma za afya, ukiwa mwanachama wa PSPF unaweza kupata huduma ya afya wewe na familia yako, hii ni faida kubwa.” Alisema Rage wakati akikabidhiwa kadi yake ya uanachama na Meneja Masoko, Mawasiliano na Uenezi wa PSPF, Bi. Costantina Martn.

Rage alisema, yeye kama mwanamichezo atahamasisha wanamichezo hususan wacheza mpira kujiunga na mpango huu kwani maisha ya sasa yanahitaji kwenda kisasa, na jambo muhimu ni kuwa na afya bora, na afya bora utaipata kama unapata huduma bora, nimeambiwa kupitia mpango huu ninaweza kupata matibabu kwenye hospitali yoyote nchini na wakati wowote, Alisema.

Awali Rage alijaza fomu za kujiunga na uanachama ambapo alipokewa na Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, PSS, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe. Ambaye alimshukuru Rage kwa kuwa mwanachama wa Mfuko huo.
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, (kushoto), akipokea fomu za kujiunga na uanachama kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Klabu ya soka ya Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, makao makuu ya PSPF, katikati ya jiji la Dar es Salaam, Aprili 14, 2016
Alhaj Rage, (kushoto), akiweka dole gumba kwenye fomu yake ya uanachama huku akisaidiwa na Bi. Mwanjaa Sembe, (kulia) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw.Abdul Njaidi
Alhaj Rage akijaza fomu, kuliani Bi. Mwanjaa Sembe
Alhaj Rage, akikabidhi fomu kwa Bi. Mwanjaa Sembe, huku Njaidi akishuhudia
Rage akizungumza baada ya kukabidhi fomu kwa Bi. Mwanjaa Sembe (kushoto)
Meneja wa Mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, akiwa mwenye furaha baada ya kupokea mwanachama mpya, Alhaj Ismail Aden Rage
Alhaj Rage akipokewa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Njaidi alipowasili kujiunga na Mfuko huo
Alhaj Rage, akibadilishana mawazo na Bi. Costantina Martin, na Njaidi baada ya kuwa mawanachama wa Mfuko huo

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI KUWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BARABARA YA JUU (FLYOVER) YA TAZARA NA KUFUNGUA DARAJA LA KIGAMBONI JIJINI DARA ES SALAAM

$
0
0
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya juu(Flyover) katika makutano ya TAZARA na ufunguzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Siku ya Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais ataweka jiwe na msingi la ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya barabara Nyerere na Mandela (Flyover ya TAZARA).

Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais atafungua rasmi Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5. Ujenzi huu umefanywa na Kampuni ya China Railway 15 Group ilishirikiana na Kampuni ya China Bridge Engineering Group.

Aidha wakati tunasubiri uzinduzi rasmi, Wananchi na magari yenye uzito usiozidi tani 10 yataruhusiwa kutumia Daraja la Kigamboni kuanzia Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 ili kuwawezesha kuelewa vizuri miundombinu na matumizi ya daraja.

Utekelezaji wa miradi hii ni mojawapo ya jitihada za Serikali za kuboresha miundomninu na kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.

Imetolewa na;

Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

14 Aprili, 2016

RAIS SHEIN AKUTANA MAKAMO WA RAIS WA KOICA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini "KOICA GLOBAL" Bw.Kwon  Taemyon akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo pamoja na mwenyeji wa Ujumbe huo Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed(hayupo pichani)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  akizungumza na  Makamo wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini "KOICA GLOBAL" Bw.Kwon  Taemyon akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo pamoja na mwenyeji wa Ujumbe huo Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed(hayupo pichani)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)  akizungumza na  Makamo wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini "KOICA GLOBAL" Bw.Kwon  Taemyon (wa pili kushoto) akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo pamoja na mwenyeji wa Ujumbe huo Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed(wa pili kulia) akiwepo Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  akiagana na   Makamo wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini "KOICA GLOBAL" Bw.Kwon  Taemyon baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ukumbi wa  Ikulu Mjini Zanzibar leo (katikati) Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed,[Picha na Ikulu.]

TAMISEMI MKOANI MWANZA YADAIWA KUONGOZA KWA RUSHWA

$
0
0
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha Mkoani Mwanza (Pichani) Mhandisi Ernest Makale, leo ametoa taarifa ya Utendaji kazi wa taasisi hiyo mbele ya Wanahabari katika kipindi cha robo mwaka (Januari hadi Machi) mwaka huu.

Katika taarifa hiyo, Mhandisi Makale amebainisha kuwa Takukuru imepokea jumla ya malalamiko 45 yanayohusiana na vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi ambapo katika malalamiko hayo, 27 yameelekezwa kwa watumishi wa idara za Serikali za Mitaa TAMISEMI hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 60. Kati ya malalamiko hayo 27, malalamiko 13 yameelekezwa katika idara ya ardhi.

Zaidi Bonyeza HAPA

TAKUKURU MKOANI PWANI YAZITAJA TAASISI NA IDARA 11 ZINAZOONGOZA KWA MALALAMIKO YA VITENDO VYA RUSHWA

$
0
0
Kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Rymond akiwaonyesha waandishi wa habari ofisini kwake hawapo pichani orodha ya majina ya taasisi na idara ambazo zimeongoza kwa malalamiko ya vitendo vya rushwa (Picha na Victor Masangu)
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo wa Takukuru.

NA VICTOR MASANGU, PWANI

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani Pwani imezitaja taasisi na idara zipatazo 11 ambazo zimelalamikiwa kuhusika katika matukio mbali mbali ya vitendo vya kupokea rushwa kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi januari hadi machi mwaka huu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Rymond alisema kuwa wale waliohusika watapeekwa katika vyombo vya sheria.

Susan alisema kwamba kwa sasa wamepokea jumla ya malalamiko 49 yanayohusina na vitendo vya rushwa baada ya kufanya uchunguzi waa wa wameweza kubaini idara inayoongoza kwa malalaamiko hayo kwa Mkoa mzima wa Pwani ni serikali za mitaa ambayo ina jumla ya malalamiko 18.

Kamanda huyo alifafafnua kuwa idara nyingine iliyoshika nafasi ya pili ilikuwa ni afya ambayo ilipata malalamiko 8,polisi 4,mahakama 3 ardhi 3 sekta binafsi 3 elimu 2 tanesco 2 fedha 1 vipimo 1 pamoja na maji 1.

“Ndugu zangu waandishi wa habari leo tumewaita ili kuwapa taarifa ua utekelezaji wa majukumu yetu kwa kipindi cha kuanzia mwezi januari hadi kufikia mwezi machi, na katika miezi hiyo tumepata malalamiko mengi yanayohusina na vitendo vya rushwa katika mkoa wetu wa Pwani.

Aidha Kamanda huyo alisema malalamiko ambayo wameshayapokea katika ofisi yaa ni 64 ambapo kati yao 49 ndio yanahusina na malalamiko ya vitendo vya upokeajiwa rushwa katika idara za serikali pamoja na taasisi mbali mbali.

Pia Suzan alisema kwamba kwa sasa katika kuhakikisha wanakomesha vitendo vya kupokea na kutoa rushwa wataendelea kufanya uchunguzi wa kina katika maeneo mbali mbali ili pindi watakapowabaini wahusika waweze kuwachukulia kali na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Kamanda huyo alisema hadi sasa tayari kuna jumla ya kesi 22 zinazohusiana na vitendo vya rushwa ambazo zimeshafikishwa mahakamani,na pia bado kuna baadhi ya kesi nyingine bado zinafanyiwa uchunguzi zaidi.

Katika hatua nyingine Kamanda huyu aliwaomba wananchi wote wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanatoa taarifa katika vyombo vinavyohusika endapo wakibaini kuna daily zoozte za mtu kutoa au kupokea rushwa ili sheria iweze kufuata mkondo wake wa kuwakamata wahusika ambao wamekuwa na tabia kama hiyo.

Ziara ya Mhe. Salva Kiir, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Tarehe 15 Aprili 2016

$
0
0


Ziara ya Mhe. Salva Kiir, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Tarehe 15 Aprili 2016.
Mhe. Salva Kiir Mayardit, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini atafanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Tanzania tarehe 15 Aprili 2016. Rais Kiir anakuja nchini kusaini Mkataba wa kuwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo tangazo la kukubaliwa kuwa Mwanachama wa EAC lilitangazwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC uliofanyika jijini Arusha mwezi Machi 2016.
Rais Kiir atawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 3:00 asubuhi na baadaye ataelekea Ikulu na kupokelewa na Mwenyeji wake, Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli. Baada ya hapo, Viongozi hao watashiriki hafla ya uwekaji saini ya Mkataba huo iliyopangwa kuanza saa 5:00 asubuhi na kisha watapata fursa ya kutoa hotuba na kusaini Communique.
Rais wa Sudan Kusini atashiriki hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa heshima yake na Mwenyeji wake kabla ya kuondoka nchini baada ya hafla hiyo.
Sudan Kusini ni nchi ya sita kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo inaongeza fursa nyingi za kiuchumi ambazo zinaweza kuzifaidisha Nchi Wanachama ikiwemo Tanzania, endapo mipango madhubuti itawekwa kuzichangamkia. Fursa hizo ni pamoja na za kibiashara kwa kuwa bidhaa nyingi zinazotumika Sudan Kusini zinaagizwa kutoka Nje ya nchi. Hivyo, jamii ya wafanyabiashara wa Tanzania wanahimizwa kuchangamkia fursa zinazopatikana nchini humo na ndani ya Jumuiya kwa ujumla.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Dar es Salaam, 14 Aprili, 2016

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS-TAMISEMI, GEORGE SIMBACHAWENE AVUNJA BODI YA MACHINGA COMPELEX

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, George Simbachawene akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda  nyaraka za jengo la Machinga Complex baada ya kuvunja bodi  ya jengo hilo mapema leo, na kutangaza kuwa amelikabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Mkoa  leo jijini Dar es Salaam.

NEWZ ALERT:RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MHARIRI MTENDAJI WA MAGAZETI YA SERIKALI (TSN) GABRIEL NDERUMAKI.

Wafanyakazi wa Airtel katika Mikoa mbalimbali waitambulisha huduma ya Airtel Jipimie yatosha yako Sokoni

$
0
0
Wafanyakazi wa Airtel katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya na Morogoro leo wameingia katika mitaa mbalimbali katika mikoa yao kuitambulisha huduma mpya ya Airtel Jipimie Yatosha yako kwa wateja na kutoa elimu jinsi ya kufurahia uhuru wa kutengeneza vifurushi vinavyokidhi mahitaji yao

Zoezi hili limefanyika jana katika mkoa wa Dar es salaam ambapo wafanyakazi wa Airtel Makao makuu waliweza kutembelia maeneo mbalimbali na kutoa elimu hiyo, halikadhalika timu ya Airtel imefikia wateja wake kupitia vyombo vya habari mbalimbali ikiwemo radio, Tv na mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwahabarisha wateja na watanzania kwa ujumla juu ya huduma hiii ya kipekee, kibunifu na ya kwanza nchini Tanzania inayomuwezesha wateja kununua kifurushi cha muda wa maongezi tu, au kuchanganya kifurushi cha muda wa maongezi na MB za intaneti au Muda wa Maongezi na SMS lakini pia bado wanaweza kupata vifurushi vyote yaani muda wa maongezi zaidi, SMS zaidi na MB zaidi. Vifurushi hivi vinapatikana kwa siku, wiki au mwezi

Ili kujiunga na kufurushi cha Airtel jipimie yatosha yako mteja anatakiwa kupiga *149*99# kisha kufata maelekezo.
Wafanyakazi wa Airtel Mkoani Mwanza wakitoa elimu kwa wakazi Mwanza mjini na wafanyabiasharaa waendesha Bodaboda kuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake. 
Wafanyakazi wa Airtel Mkoani Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuingia mtaani kukutana na wateja na kuitambulisha huduma mpya ya kibunifu ya Airtel jipimie yatosha yako itakayowawezesha wateja kujitengenezea vifurushi vya yatosha wanavyovitaka
Wafanyakazi wa Airtel Mkoani Morogoro wakishuka kutoka kwenye basi kwenda kukutana na wateja katika maeneo yao ya kazi ili kutambulisha huduma mpya ya kibunifu ya Airtel jipimie yatosha yako itakayowawezesha wateja kutengeneza vifurushi vya yatosha wanavyovitaka
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akifanya mahojiano na Jembe radio mkoani Mwanza na kutoa elimu kwa wasikilizaji wa vipindi vyake juu ya huduma mpya ya kibunifu ya Airtel jipimie yatosha yako itakayowawezesha wateja kutengeneza vifurushi vya yatosha wanavyovitaka
Wafanyakazi wa Airtel mkoani Arusha wakiongea na wateja sokoni na kutoa elimu jkuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.
 

DK. KIGWANGALLA AKUTANA NA AFISA MIRADI KUTOKA SHIRIKALA LA KIMATAIFA LA NGUVU ZA ATOMIKI (IAEA)

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla (wa pili kushoto) akisikiliza kwa makini mazungumzo na Afisa miradi anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika kutoka wakala wa Kimataifa wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon Haile (wa kwanza kulia). Wengine ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba anayeshughulikia magonjwa yasiyo ambukiza, Profesa Ayoub Magimba (katikati), akifutiwa na Mkurugenzi taasisi ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaisalage na kushoto Mratibu wa Magonjwa ya Saratani Kitaifa pamoja na magonjwa yasiyoambukiza kwa watu wazima, Dk. Sara Maongezi. (Picha na mpiga picha wetu).

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla amekutana na Afisa miradi anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika kutoka wakala wa Kimataifa wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon Haile katika mazungumzo yaliyofanyika leo asubuhi Aprili 14.2016, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Dk. Kigwangalla ameomba Tanzania ipatiwe kibali cha kununua mashine mpya ya kutibu saratani (LINAC) Sambamba na sehemu ya msaada iliyoahidiwa na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Bw.Yukiko Amano mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Mizengo Kayanda Pinda miaka mitatu iliyopita.

Tanzania tayari imetenga kiasi cha Euro 1.65 Milioni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya mchango wake kwa asilimia 50 kama mradi ulivyokuwa awali.Mh. Kigwangalla alisema: “Bahati mbaya sana kutokana na ucheleweshwaji, Bajeti ya msaada huo kutoka IAEA ilipitwa na wakati na kusababisha Tanzania kukosa fursa hiyo. Malengo ya Tanzania ni kununua mashine hizo mbili kwa ajili ya kuboresha huduma za tiba ya Mionzi nchini”.

Ujenzi wa jengo kwa ajili ya kufunga mashine hizo mbili umesha kamilika na mashine moja itakamilika mwaka huu na ya pili mwakani ili kuboresha huduma za Saratani nchini.

Katika mazungumzo hayo, Maafisa waandamizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Woto walishiriki, akiwemo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba anayeshughulikia magonjwa yasiyo ambukiza, Profesa Ayoub Magimba, Mratibu wa Magonjwa ya Saratani Kitaifa pamoja na magonjwa yasiyoambukiza kwa watu wazima, Dk. Sara Maongezi pamoja na Kaimu Mkurugenzi taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage.

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BARAZA LA USAJILI LA MAZINGIRA

$
0
0
Waziri afya ,maendeleo ya jamii,jinsia ,wazee na watoto Ummy Mwalimu akiongea na wajumbe wa baraza jipya la usajili wa wataalam wa afya ya mazingira nchini(hawapo pichani) kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof: Bakari Mohammad
Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo pamoja na maofisa mazingira wakifuatilia hotuba ya Mh. Waziri Ummy Mwalimu
Mwenyekiti mpya wa baraza la usajili wa wataalam wa afya ya mazingira nchini Bartholomayo Ngaeje(katikati) akitoa neon la shukrani kwa waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto(hayupo pichani) mara baada ya kuzinduliwa kwa baraza hilo,kulia ni msajili wa baraza hilo Iddy Hoyange na kulia ni njumbe wa baraza hilo toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa wizara hiyo
Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akimkabidi cheti cha Uongozi kwa kuthamini mchango wake kwa baraza hilo aliyekuwa mwenyekiti wa awamu ya pili Bi.Mary Swai

FILAMU ZA BI KIDUDE KUONESHWA KATIKA KUMBUKUMBU YA KIFO CHAKE

$
0
0
Kushoto ni mmiliki wa ukumbi wa ZANCINEMA Mohammed Bajbeir, akiwa pamoja na Andy Jones, raia wa Uingereza, mtengenezaji wa filamu za ‘As Old sa My Tongue’ na ‘I shot Bi. Kidude’, zinazoonesha historia ya maisha hadi kufa kwa msanii mkongwe marehemu Fatma Baraka ‘Bi. Kidude’, wakizungumza na waandishi wa habari juu ya kumbukumbu ya msanii huyo aliyefariki dunia Aprili 17, 2013. (Picha na Yussuf Simai-MAELEZO, ZANZIBAR.

Na Salum Vuai, MAELEZO

KATIKA kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa tatu tangu kufariki kwa msanii mkongwe aliyeitangaza sana Zanzibar duniani Fatma Baraka ‘Bi. Kidude’, filamu mbili zinazohusu maisha na kifo chake zitaoneshwa mjini Zanzibar.

Mohammed Bajbeir, mmiliki na Mkurugenzi wa ukumbi wa sinema uliopo mjini Zanzibar, ZANCINEMA, amewaambia waandishi wa habari jana, kwamba maonesho ya filamu hizo yanalenga kuwapa fursa Wazanzibari na wageni, kumjua kwa undani nyakanga huyo wa sanaa ya uimbaji na unyago.

Marehemu Bi. Kidude, alifariki dunia Aprili 17, 2013 baada ya kuugua maradhi ya kisukari yaliyochangiwa na umri mkubwa, na kuzikwa kijijini kwao Kwambani katika mazishi yaliyoweka rekodi miongoni mwa wasanii kwa kuhudhuriwa na watu wengi wakiwemo viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

Bajbeir amezitaja filamu hizo kuwa ni ‘As old as my tongue’ inayoelezea kwa urefu maisha ya msanii huyo katika tasnia ya muziki, pamoja na ‘I shot Bi. Kidude’ (Kifo cha Bi. Kidude), ambayo inaelezea kuumwa kwake hadi pumzi zake za mwisho.

Filamu hizo zimeandaliwa na kutengenezwa na Andy Jones, raia wa Uingereza, ambaye alikuwa akimsoma na kumfuatilia marehemu Bi, Kidude kwa miaka kadhaa hadi akamudu kuandika filamu hizo zinazogusa mtima wa kila anayeziangalia.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa ZANCINEMA ulioko Funguni mjini Zanzibar kuelekea siku ya kumbukumbu ya Bi, Kidude, Jones alisema Wazanzibari wana kila sababu ya kumuenzi gwiji huyo wa sanaa ambaye amefanya kazi kubwa kuitangaza nchi yake ulimweguni, kisanii na kiutamaduni.

Aidha, alieleza kwamba, kwa namna Bi. Kidude alivyokuwa mtu wa watu wa kila rika, mcheshi, na mwenye imani asiyeangalia kipato, anastahili kukumbukwa kwa namna ya pekee. 

“Wapo watu wa mataifa ya nje ambao hawakuwa wakimfahamu, lakini waliposikia kazi zake, walisafiri hadi Zanzibar kwa ajili ya kumjua na kumshuhudia jukwaani akionesha uwezo wake,” alisema Muingereza huyo.

Alifahamisha kuwa tayari filamu hizo zimeshaoneshwa katika nchi mbalimbali duniani, lakini maonesho ya Zanzibar yatakuwa ya kipekee.

Aidha, alisema zimewahi kuoneshwa katika matamasha ya Zanzibar, Sauti za Busara na lile la filamu (ZIFF), ambapo watu wengi walivutiwa nazo.

Andy Jones, alifika Zanzibar kwa mara ya kwanza mwaka 2000, na kuendelea kuja kila mwaka hadi 2006 alipokamilisha filamu ya kwanza, ‘As old as my tongue’ kuhusu historia ya Bi. Kidude.

Alieleza kuwa, alitumia pauni 15,000 za Kiingereza (sawa n ash. 51,000,000 kwa thamani ya sasa), kutengeneza filamu ya ‘Kifo cha Bi. Kidude’ (I shot Bi, Kidude), iliyochukua miaka miwili na nusu hadi kukamilika.

Jones alisema, wakati wa uhai wake, marehemu Bi, Kidude alikuwa akilipwa asilimia kumi ya mauzo kila ilipouzwa, na sasa fedha hizo ameamua kuzigawa kwa Akademi ya Muziki wa Nchi za Jahazi (DCMA) ya Zanzibar kwa ajili ya kuwaendeleza wasanii wa kike wanaochipukia.

KAMATI YA MUDA NGUMI ZA KULIPWA YAUNDWA.

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa(BMT) Bw. Mohamed Kiganja wa kwanza kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani leo jijini Dar es salaam kuhusu viongozi waliochaguliwa wa kamati ya muda ya mchezo wa Ngumi za kulipwa , kulia ni Katibu Mkuu wa kamati hiyo Bw. Yassin Ustaadh.
Katibu Mkuu mpya wa Kamati ya Muda ya Mchezo wa Ngumi za kulipwa Bw. Yassin Ustaadh akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani baada ya kukabidhiwa kamati hiyo leo jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa(BMT) Bw. Mohamed Kiganja hayupo pichani alipotambulisha viongozi waliochaguliwa wa kamati ya muda ya mchezo wa Ngumi za kulipwa , kulia ni Katibu Mkuu wa kamati.
 

Baraza la Michezo Taifa(BMT) kwa kushirikiana na wadau wa ngumi za kulipwa wameunda kamati ya muda kwa ajili ya kuratibu na kusimamia maendeleo ya mchezo huo ndani na nje ya Nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja amesema kuwa wameamua kuunda kamati ya muda ya mchezo huo itakayoongozwa na Katibu Mkuu Yassin Ustaadh kutoka TPBO na Makamu katibu Mkuu Chaulembo Palasa kutoka Chama cha Ngumi za kulipwa Tanzania(TPBC) kwa sababu hakukuwa na chombo kimoja kinachoratibu Ngumi za kulipwa nchini.

“Tuliamua kukutana na wadau wa mchezo wa ngumi za kulipwa mapema mwezi huu wakiwamo TPBO, TPBC,TPBC Limited , PST na KBF ili tuweze kupata chombo kimoja imara cha kuratibu mchezo wa ngumi za kulipwa nchini” alisema Bw. Kiganja.

Aidha Bw. Kiganja ameongeza kuwa viongozi waliochaguliwa wafanye kazi kwa bidii na sio kuongea sana ikiwemo kuwasilisha katiba ya kamati hiyo ndani ya siku 90 ili kuweza kuufikisha mbali mchezo huo na kuiletea sifa na heshima Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

“ Natoa wito kwa viongozi wa kamati hii wasifanye mzaha katika suala hili ikiwa kama mwanakamati hawezi kufanya kazi aseme mapema ili achaguliwe mwengine kwa manufaa ya Taifa” aliongeza Bw. Kiganja.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa kamati hiyo Bw. Yassin Ustaadh amesema kuwa wapo tayari kufanya kazi na kuufikisha mchezo huo mbali katika Nyanja za kimataifa na kuwataka mashabiki wakae mkao wa kula.

Mbali na hayo Bw. Ustaadh amewataka waandaaji wa mapambano hayo ambao hawana sifa na vigezo kukaa mbali na shughuli hiyo kwani hawahitaji ubabaishaji katika tasnia hiyo vinginevyo watatumbuliwa.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WAZIRI WA BIASHARA WA OMAN

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuendeleza sekta ya viwanda kama mkakati wa kukuza uchumi ili nchi iweze kutoka kwene umaskini na kufikia uchumi wa kati.

Waziri Mkuu amesema hayo leo (Alhamisi, Aprili 14, 2016) alipofanya mazungumzo na Waziri wa Biashara wa Oman, Dk. Ali Masoud Al Sunaidy ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam.

Amesema mbali na kuimarishwa kwa sekta ya viwanda, pia Serikali imelenga kuboresha sekta za nishati, uchukuzi na kilimo ambazo zitawezesha Taifa kufikia malengo yake ya kufikia uchumi wa kati.

“Sekta ya viwanda ni eneo ambalo tunataka kuliimarisha kwa sababu litatuwezesha kuongeza thamani ya mazao na bidhaa zinazozalishwa nchini jambo ambalo pia litakuza ajira kwa vijana. Hivyo nawakaribisha mje kuwekeza nchini,” amesema.

Pia Waziri Mkuu amemuhakikishia kuwa serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wa kutoka Oman kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake, Dk. Al Sunaidy amefurahishwa na mazingira mazuri ya uwekezaji nchini na kwamba wapo tayari kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo viwanda vya usindikaji, kilimo kinachotumia teknolojia ya kisasa, na mafuta, gesi, na ujenzi wa bandari.

Akitoa ufafanuzi, Waziri huyo alisema: “Oman ina bandari ya Salala ambayo ni moja kati ya bandari bora duniani yenye uwezo wa kupakua makontena 45 kwa saa. Lakini pia tunayo bandari ya Sohar maarufu kwa bidhaa za viwandani ambayo ina uwezo wa kupakua makontena 32 kwa saa,” amesema.

Dk. Al Sunaidy yuko nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu akiwa ameambatana na wafanyabiashara 80 wa Oman kwa mwaliko wa Kiserikali kwa ajili ya kukuza ushirikiano wa kiuchumi.

Naye Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amesema anatambua kuwa Oman imepiga hatua katika teknolojia ya gesi asili ya kimiminika (LNG) hivyo ana imani Tanzania itapata ujuzi kutoka kwao.

Amesema wafanyabiashara hao wana fursa ya kuwekeza kweye ujenzi ujenzi wa viwanda vya mbolea katika mikoa ya Lindi na Mtwara lakini pia wanaweza kuwekeza kwenye bandari za Tanga, Bagamoyo, Kilwa, Lindi na Mtwara ambazo Serikali imepanga kuboresha miundombinu yake.

ASILIMIA 71 YA WATANZANIA HAWATAKI KUFANYA KAZI

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista Mhagama,akizungumza katika katika uzinduzi wa matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014. Uzinduzi huo ulifanyika katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam, jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo na Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu nchini,Dk.Albina Chuwa.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista Mhagama,akizindua ripoti ya matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014 katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam, jana. Wengine wanaoshuhudia ni kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu nchini,Dk.Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo na Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani,Marry Kawar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista Mhagama,akionesha ripoti ya matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014 katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam, jana. Wengine wanaoshuhudia ni kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu nchini,Dk.Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo na Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani,Marry Kawar.

Na Raymond Mushumbusi – MAELEZO
14/4/2016.Dar es salaam.
Utafiti uliofanyika hivi karibuni na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) umebaini kwamba asilimia 71 ya watanzania wanatumia muda mwingi kufanya shughuli zisizokuwa za uzalishaji mali wala tija binafsi kwao na Taifa kwa ujumla.

Akizundua taarifa ya utafiti huo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  amesema kuwa idadi hiyo hufanya kazi zisizoleta tija kwao na taifa na muda mwingi huutumia kujihudumia binafsi kwa kulala na starehe nyingine.

Ameeleza kuwa takwimu hizo zinaonesha wazi ni kwa namna gani watanzania wanashindwa kujishughulisha katika kufanya kazi zenye kuwaingizia kipato na badala yake wanatumia muda wao mwingi kufanya shughuli zisizo za uzalishaji hasa kufanya starehe mbalimbali.

 “ Ndugu zangu watanzania unakuta mtu amekaa baa au anacheza “poll table” kuanzia asubuhi mpaka jioni na hujui anafanya kazi gani ya uzalishaji, ndugu zangu tuone aibu basi tujishugulishe tulijenge taifa letu ili kujiletea maendeleo yetu na nchi yetu.”

Aidha, matokeo hayo yamebainisha kuwa asilimia 18.5 ya wananchi wanafanya kazi za uzalishaji na asilimia 10.6 ni wale wanaofanya shughuli za nyumbani zisizo na malipo huku uchambuzi wa kijinsia ukionesha kuwa wanaume asilimia 23.8, wanatumia muda mwingi kwenye shughuli za kiuchumi ikilinganishwa na asilimia 13.5 ya wanawake.

Amefafanua kuwa wanawake ambao ni asilimia 16.5 katika utafiti huo wanatumia muda mwingi kufanya kazi za nyumbani zisizo na malipo ikilinganishwa na asilimia 4.4 ya wanaume.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisa ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa upatikanaji wa Takwimu hizo utaisaidia Serikali kupata mbinu sahihi za kuondokana na tatizo la ajira nchini kwa kuunganisha nguvu kutoka sekta isiyo rasmi ili kuleta changamoto katika soko la ajira nchini.

Amesema kuwa hii ni mara ya tano Tanzania inafanya utafiti huo na kubainisha kuwa ulianza  mwezi Januari hadi Desemba,  2015 ukitumia sampuli ya Sensa  ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyotumika kupata taarifa sahihi ya takwimu hizo.

Aidha, amebainisha kuwa ili kufanikisha utafiti huo NBS imeshirikiana na wadau mbalimbali ikwemo Wizara ya kazi na Ajira,Shirika la Kazi Duniani (ILO),Benki ya Dunia (WB),Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) na Asasi zisizo za Kiseikali.
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images