Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

WAZIRI NAPE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU NDANDA KOSOVO JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Sanduku lenye Mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo ukiwasili mapema leo mchana katika  nyumba ya Ubalozi wa Congo,iliopo Hananasifu-Kinondoni jijini Dar,kwa ajili ya kuagwa na hatimae mazishi yake kufanyika jioni ya leo katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
 Waziri Nape Nnauye akisalimiana na Waombolezaji waliofika kwenye msiba wa Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini, Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo ambaye  anatarajiwa kuzikwa jioni ya leo Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
  Waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na Michezo.Mh Nape Nnauye akisalimiana na Waombolezaji waliofika kwenye msiba wa Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini,Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo ambaye  anatarajiwa kuzikwa jioni ya leo Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
  Waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akitoa salamu za rambirambi kwa Waombolezaji, wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo,katika nyumba ya Ubalozi wa Congo,iliopo Hananasifu-Kinondoni jijini Dar ,Ndanda Kosovo anatarajiwa kuzikwa jioni ya leo Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
  Baadhi ya Marafiki ndugu jamaa na wanamuziki wenzake wakiwa wamekusanyika nje ya nyumba ya Ubalozi wa Congo,iliopo Hananasifu-Kinondoni jijini Dar ,wakisubiri kuwasili kwa mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo kwa ajili ya kuagwa na hatimae mazishi yake kufanyika leo alasiri katika makaburi ya Kinondoni.
  Mwanamuziki Lady Jay Dee akiwasili kwenye kuaga mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo mapema leo mchana.
 Sanduku lenye mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo likiwa mbele ya Waombolezaji tayari kwa kuanza kumuaga.

 Baadhi ya Marafiki,Ndugu na Jamaa wakiwemo Wanamuziki wenzake wakiwa wamejipanga nje ya nyumba ya Ubalozi wa Congo,iliopo Hananasifu-Kinondoni jijini Dar, wakisubiri kuupokea mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo kwa ajili ya kuagwa na hatimae mazishi yake kufanyika leo alasiri katika makaburi ya Kinondoni,jijini Dar.
  Waombolezaji wakiwa katika hali ya huzuni.
 Baadhi ya Marafiki ndugu jamaa na wanamuziki wenzake wakiwa wamekusanyika nje ya nyumba ya Ubalozi wa Congo, iliopo Hananasifu-Kinondoni jijini Dar, wakisubiri kuwasili kwa mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo kwa ajili ya kuagwa na hatimae mazishi yake kufanyika leo alasiri katika makaburi ya Kinondoni.
 Mama wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo akilia kwa uchungu mara baada ya kuwasili mwili wa Marehemu mwanae kwenye nyumba ya ubalozi wa Congo,Hananasifu-Kinondoni jijini Dar mchana huu.

  Baadhi ya waombolezaji wakilia kwa uchungu.
 Baadhi ya Wanamuziki na Ndugu Jamaa na marafiki wakiwa kwenye msiba huo.

WAZIRI MHAGAMA AAGIZA IDARA YA MAAFA KUFANYA TATHIMINI YA MAAFA BAHI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwasilisha bajeti ya ofisi yake wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Kupitisha Bajeti uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam Aprili 12, 2016
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya kupitisha bajeti wakifuatilia bajeti ya ofisi hiyo walipokutana kuijadili na kuipitisha bajeti hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam Aprili 12, 2016.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Issa Nchansi akifafanua jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya kupitisha bajeti kilichofanyika tarehe 12 Aprili, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Kupitisha Bajeti Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye ni mbunge wa Rufiji (katikati) akieleza jambo wakati wa kikao hicho walipokutana kujadili Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 12, 2016 katikaUkumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen Mbazi Msuya (katikati) akifuatilia bajeti ya Idara yake pamoja na wataalamu wake kushoto kwake ni Charles Msangi na kulia ni Daniel Alfei wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Kupitisha Bajeti Aprili 12, 2016.(Picha Zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ameiagiza Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kufanya tathimini ya hali halisi za athari zilizosababishwa na ndege aina ya kwerea kwerea katika mashamba ya mtama na uwele yaliyopo Mkoani Dodoma katika Wilaya Bahi.

Waziri Mhagama aliyasema hayo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha Kupitisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kilichofanyika jana katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kiliibua hoja za wajumbe ikiwemo hoja iliyo bainisha athari za maafa kwa wakazi wa Wilaya ya Bahi kuhusu ukosefu wa chakula baada ya mashamba yao kuvamiwa na ndege waharibifu aina ya Kwerea kwerea.

Hoja hiyo iliibuliwa na Mbunge wa Bahi Bw. Omar Badwel alisema wananchi wake wapo katika wakati mgumu hivyo wanahitaji msaada kutoka serikalini kwa kuwa mazao yao yamevamiwa na ndege hao.

“Kwerea kwerea wamekuwa ni changamoto kwa wakazi wa wilaya yangu hususani maeneo ya Manyoni ninaomba serikali kupitia Idara ya Maafa isaidie kwa kuwapa chakula na mbegu Wananchi ili waweze kujikimu na kuitatua changamoto hiyo”Alisema Badwel.

“Mazao yaliyoshambuliwa na kuharibiwa na ndege aina ya kwerea kwerea ni mazao ya mtama na uwele, Alisisitiza”.

Waziri Mhagama alisema anatafuta uwezekano wa kuona umuhimu wa kushirikisha Wizara ya kilimo na Mifugo kwa kuangalia namna zinavyoweza kushirikiana kuondoa wadudu waharibifu wa mazao mkoani Dodoma.

“Serikali itafanya tathmini kwa waathirika hao wa maafa Wilayani Bahi, ni vizuri Idara ya Maafa ifanye hivyo haraka ili kusaidia kunusuru hali ya wakazi wa Dodoma”Alisisitiza Mhagama.

Waziri Mhagama alimpongeza Mhe.Badwel kwa kuwajali wananchi wa Bahi kwa kuibua jambo muhimu hivyo aliahidi kulitafutia ufumbuzi wa haraka.

“Suala hili ni muhimu kwa kuwa linagusa maisha ya Wananchi moja kwa moja sisi kama serikali tumelichukua kwa uzito na tutahakikisha Idara ya maafa inatembelea maeneo husika kwa ajili ya kufanya tathimini za haraka kwa waathirika waliopoteza mazao yao ili kujua namna tunavyoweza kutoa msaada wa haraka katika maeneo husika ” alisema Mhagama.

Awali; kikao hicho kililenga kupitia na kujadili bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu yenye fungu namba 25 (Ofisi Binafsi ya Mhe.Waziri Mkuu), 37(Sera, Uratibu a Bunge), 15 na 65 (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) na fungu 27 na 61 (Tume ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume ya Uchaguzi.

HEART MARATHON KUFANYIKA APRILI 26 MWAKA HUU

$
0
0
Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary Chillo (katikati) akiongea na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya mbio maalum za kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza zijulikanazo kama Heart Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es salaam, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon Dkt. Chaka Halfani na kulia kwake ni Kaimu Katibu Chama cha Riadha Tanzania Bi.Ombeni Zavala.
Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary Chillo (wa kwanza kulia) akiongea na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya mbio maalum za kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza zijulikanazo kama Heart Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es salaam, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon Dkt. Chaka Halfani na Mratibu Msaidizi Heart Marathon Bi.Catherine ikangaa.
4 Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon Dkt. Chaka Halfani akionyesha kwa waandishi wa habari namba watakazopewa washiriki wa mbio maalum za kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza zijulikanazo kama Heart Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es salaam,kulia kwake ni.Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary Chillo na Kaimu Katibu Chama cha Riadha Tanzania Bi.Ombeni Zavala .
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Heart Marathon Dkt. Chaka Halfani akionyesha kwa waandishi wa habari fulana watakazovaa washiriki wa mbio maalum za kupambana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza zijulikanazo kama Heart Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26 mwaka huu jijini Dar es salaam,kulia kwake ni.Mratibu wa Heart Marathon Dkt. Omary Chillo.(Picha na Lorietha Laurence-Maelezo).

NA Beatrice Lyimo-MAELEZO
Taasisi ya Tanzania Health Summit imeandaa mbio maalumu za kupambana na ongezeko la magonjwa yasioambukiza yajulikanayo kama Heart Marathon zitakazofanyika Aprili 26, 2016 katika viwanjwa vya michezo vya Chuo Kikuu jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Mratibu Kamati ya Maandalizi ya Mbio hizo Dkt. Omary Chillo ambapo amesema kuwa lengo lake ni kusaidia juhudi za Serikali na wadau wa Sekta ya Afya kupunguza tatizo linalokuwa kwa kasi la magonjwa yasioambukizwa hapa nchini.

“Watanzania wote kwa ujumla tunawaalika kushiriki katika mbio za Heart Marathon zitakazoambatana na upimaji wa magonjwa yasiyoambukizwa na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa ugonjwa wa Kisukari, Shinikizo la Damu, Uwiano wa urefu na uzito, wingi wa mafuta mwilini pamoja na Saratani ya matiti” alisema Dkt. Chillo.

Amesema mbio hizo zinatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 2,000 kutoka taasisi, makampuni, mashirika, familia na jamii kwa ujumla, rika tofauti ikiwemo watoto, vijana na wazee, makundi ya walemavu na watu wenye magonjwa yasioambukiza watashiriki.

Aidha, Dkt. Chillo ameongeza kuwa mbio hizo zimegawanywa kwa umbali tofauti ambazo ni mbio ndefu za Kilometa 21.1 kwa ajili ya wakimbiaji wazoefu, kilometa 10 kwa wakimbiaji wa kati, Kilometa 5 wakimbiaji wa kawaida, kifamilia na kampuni pamoja na mbio za watoto chini ya miaka 12 watakimbia umbali wa mita 700.

Kauli mbiu kwa mwaka huu katika mbio maalumu za kupambana na ongezeko la magonjwa hayo ni “Epuka magonjwa yasioambukiza”.Viingilio katika mbio hizo maalumu zitakuwa kuanzia elfu tano kwa watoto wa chini ya umri wa mika 13 hadi Shilingi 10,000 kwa mtu mmoja ambapo watu wenye ulemavu hawatalipia kiingilio.

MAJALIWA:VIJIJI 42 RUANGWA KUPATIWA UMEME

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiteta na wapiga kura kijijini kwake Namdagala wilayani Ruangwa Aprili 11, 2016., Alikuwa katika ziara ya siku tatu jimboni Ruangwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amesema vijiji 42 vya wilaya ya Ruangwa vitaunganishiwa umeme katika Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA) awamu ya tatu.

Amesema hadi sasa tayari vijiji 48 vya wilaya hiyo vimeunganishiwa umeme na kwamba lengo lake ni kuhakikisha vijiji vyote 90 vinapata huduma hiyo, hivyo amewaomba wananchi kuendelea kuwa na subira.Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Michenga, Chinongwe, Makanjiro na Chinokole katika mikutano ya hadhara aliyoifanya wilayani Ruangwa.

“Niliwaahidi kuwatumikia, kuwahudumia na kuwasemea ndani na nje ya nchi, nawahakikishia kuwa sitowaangusha hivyo endeleeni kuwa na subira, nitafanya mambo mengi ya maendeleo kama isemavyo kauli mbiu yangu, Ruangwa kwa maendeleo inawezekana.” amesema.

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO mkoa wa Lindi, Sotco Nombo amesema tarehe 15 mwezi huu wataanza kusambaza vifaa katika kijiji cha Chinongwe na kwamba hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu umeme utakuwa umewaka katika kijiji hicho.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, Majaliwa amewasisitiza wananchi kuanza kulima kwa wingi zao la muhogo kwa sababu kuna soko la uhahika la zao hilo baada ya kujitokeza kwa wafanyabiashara kutoka China na Marekani wanaotaka kununua zao mihogo nchini.

“Mnataka hela, mnataka hela? ila lazima mfanye kazi…mimi nimewatafutia hela nawaomba mlime mihogo kwa wingi maana kuna wafanyabiashara wanataka kununua mihogo, hela ndiyo hiyo ambayo ni soko la uhakika la mihogo. Nawasihi mchangamkie dili hili,” amesema.

Amesema wafanyabiashara hao wanataka kununua mihogo kutoka wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale kwa ajili ya kusaga unga na kutengeneza vyakula vingine vitokanavyo na zao hilo, hivyo amewaomba wananchi hao kuchangamkia fursa hiyo na kulima mashamba makubwa ya mihogo.

POLISI JAMII WA MTAA WA OYSTERBAY, AWAPEWA PIKIPIKI KWAAJILI YA ULIZI WA MTAA HUO.

$
0
0
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva ni mfano wa kuigwa na jamii kwani ni kiongozi wa mtaa ambaye amesaidia jamii yake kwa kadiri ya uwezo wake.

Mwenyekiti huyo ambaye ameweza kusaidia vijana katika mtaa wake leo amewakabidhi pikipiki aina ya boxer vijana  wa kikundi cha Polisi jamii katika mtaa huo jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva amesema kuwa katika kutekeleza maagizo ya Serikali kuu ya kuimalisha ulinzi na usalama wa mitaa kupitia vikundi vya Polisi jamii.

Ameyasema hayo mara baada ya kuwakabidhi Pikipiki aina ya Boxer  wanakikundi cha Polisi jamii cha mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuimarisha ulinzi wa maeneo yote ya mtaa huo.

Lubuva ameishukuru serikali kwa kumuunga mkono katika kutekeleza majukumu yake kama kiongozi wa Serikali za Mtaa.

Pia Lubuva amewaomba wananchi wa maeneo hayo pamoja na makampuni mbalimbali taasisi  mbalimbali za eneo hilo kuweza kusaidia vijana wa polisi jamii ili nao waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva akimkabidhi Kamanda wa Kikosi cha Polisi jamii cha Guard, Moksin Mwalimu pikipiki ya wanakikundi cha Polisi jamii kwaajili ya kuwasaidia katika kazi yao ya ulizi hasa wakati wa usiku.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva akizunumza mara baada ya kukabidhi Pikipiki aina ya Boxer kwa wanakikundi cha polisi jamii cha mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.

Amesema kuwa pikipiki hiyo ni ya mwanzo kwaajili ya kuwasaidia vijana wanaojitolea kulinda usalama wa mtaa huo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva akimkabidhi ufunguo wa pikipiki ambayo ni msaada mkubwa kwao kwaajili ya ulizi wa mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Kikosi cha Polisi jamii cha Guard, Moksin Mwalimu akipanda pikipiki kwaajili ya kuijaribu mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, Zefrin Lubuva jijini Dar es Salaam leo.

SHIRIKA la Ndege la Etihad limepokea tuzo ya uzinduzi bora katika sekta ya usafiri wa ndege

$
0
0
 SHIRIKA la Ndege la Etihad  SHIRIKA la Ndege la Etihad limepokea tuzo  ya  uzinduzi bora katika sekta ya usafiri wa ndegelimepokea tuzo  ya  uzinduzi bora katika sekta ya usafiri wa ndege kwa mwaka 2016 kutoka kwenye jarida la kimataifa linaloongoza kwa makala za usafiri wa anga. Sherehe za tuzo hizo zilifanyika katika maonyesho ya ndege yaliyofanyika jijini Hamburg, nchini Ujerumani.

Shirika lilijinyakulia tuzo hiyo kwa kuzingatia viwango vya juu vya teknolojia na maendeleo ya burudani inayotolewa ndani ya ndege (E-BOX) pamoja na mtandao wa mawasiliano (IFEC) zinazopatikana kwenye safari zake za kimataifa. Tuzo hii ni muedelezo wa tuzo ambazo shirika limekuwa linajinyakulia kwa mwaka uliopitia kupitia huduma zake bora za ndani ya ndege zikiwemo, tuzo ya shirika bora la ndege mwaka 2015 kutoka jarida la Inflight, tuzo ya uzinduzi bora mpya kwa shirika la ndege mwaka 2016 kutoka jarida la kimataifa la PAX kwa kanda ya mashariki ya kati, pamoja na tuzo ya shirika lenye huduma bora za burudani ndani ya ndege kutoka jarida la World Travel.

Shane O'Hare, Makamu wa Rais kitengo cha Masoko wa Shirika la ndege Etihad, alisema: " Tuzo hii, iliyopigiwa kura na wasomaji wa jarida la kimataifa la PAX kwa kipindi cha miezi sita, ni utambuzi tosha juu ya dhamira ya shirika la ndege Etihad  kuhakikisha wageni wetu wanaendelea kufurahia burudani bora ndani ya ndege pamoja na mtandao thabiti wa mawasiliano ndani ya ndege zetu.”
 
Shirika la ndege Ethihad linamiliki idadi kubwa ya ndege aina ya Airbus za kisasa pamoja na Boeing kubwa za kubeba abiria/mizigo kwa wingi na ndogo ze abiria/mizigo kidogo.

Huduma ya Tv zenye kurusha matangazo na vipindi moja kwa moja  hupatikana kwenye ndege kubwa za Shirika la ndege, hii ni kuleta vipindi bora kutoka vituo saba ikiwa ni pamoja na BBC World News, Sport 24 na CNN, zikiwa zinaongoza kwa utazamajia, na CNBC, euronews , Japan NHK World Premium na Sky News Arabia.

Shirika limetambulisha huduma mpya ya burudani ndani ya ndege ya E-BOX kwa ajili ya burudani binafsi kwa kutumia mfumo wa Panasonic eX3, na ndio shirika la kwanza kufunga huduma hiyo kwenye ndege aina ya Airbus A380. Ndege zote aina ya Airbus A380s na Boeing 787s  zitakuwa zimeunganishwa na mfumo huo wa burudani na vifaa vya Panasonic eX3. Mfumo huu hutoa mamia ya masaa ya burudani ya kutazamwa yenye muonekano mzuri, kwenye TV zenye ukubwa wa kuanzia inchi 11.1 kwa daraja la Uchumi, Inchi 18 kwa daraja la Biashara, Inchi 24 kwa daraja la Kwanza na Inci 32 kwa wanaotumia huduma ya “Makazi”.

Huduma nyingine za burudani ni pamoja na kuimarishwa kwa ubora wa video, kuimarishwa kwa kioo cha kugusa cha TV, uwezo wa kufanya manunuzi kwenye TV pamoja na michezo ya video, huduma ya ramani na Graphical User Interface (GUI) kwa ajili ya abiria wenye umri mdogo.

Shirika la ndege Etihad linaendelea kuleta bidhaa mpya zenye ubunifu ili kufikia malengo yake ya kubadilisha sekta ya usafiri wa anga. Tayari shirika linatoa huduma ya “Makazi” kwenye ndege zake aina ya Airbus A380, ina wahudumu binafsi waliobobea na kupata mafunzo kutoka hoteli ya Savoy yenye sifa kubwa Jijini London, wapishi wakuu kwenye daraja la Kwanza, mameneja wa vyakula na vinywaji kwenye daraja la Biashara, na wahudumu wa watoto waliohitimu kutoka chuo cha mfunzo cha Norland. Mkusanyika wa kumbi za mapumziko zinapatikana dunia nzima zikitoa huduma na vyakula kama vinavyopatikana kwenye hoteli kubwa duniani. Uwekezaji wa shirika la ndege Etihad kwenye burudani na mtandao wa mawasiliano kwenye ndege ni sehemu kubwa ya mipango yao katika kufikia mainduzi katika sekta ya usafiri wa anga.

FILAMU YA MAISHA YA BIKIDUDE NAMBA MBILI YAONYESHWA ZANZIBAR

$
0
0
Marehemu Bikidude Binti Baraka katika Uhai wake akiimba katika sehemu mbalimbali ambazo alipata mualiko.hii ni sehemu ya Filamu ya maisha ya Bikidude namba mbili ilionyeshwa katika holi la Rumaisa Bwawani Mjini Zanzibar. 
Marehemu Bikidude binti Baraka akiwa katika picha ya pamoja na Mtayarishaji wa Filamu ya Bikidude namba mbili ilioonyeshwa katika Ukumbi wa Rumaisa Bwawani Mjini Zanzibar.
Meneja wa Baraza la Habari Tanzania (MCT)Suleiman Seif akiuliza maswali kwa mtayarishaji wa Filamu ya Bikidude namba mbili Andy Jones ilioonyeshwa katika Ukumbi wa Rumaisa Bwawani Mjini Zanzibar.
Mtayarishaji wa Filamu ya Bikidude namba mbili Andy Jones (kulia)akijibu maswali kwa waandishi wa Habari waliofika katika kuiangalia Filamu hio ilioonyeshwa katika Ukumbi wa Rumaisa Bwawani Mjini Zanzibar.mwengine ni mmiliki wa Ukumbi wa Rumaisa Mohd Bajbeir.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA MWENDESHA MASHTAKA WA KIMATAIFA LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa Bw. Serge Prammertz wakati Bw. Serge alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 13,2016 kwa ajili ya kujitambulisha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa Bw. Serge Prammertz wakati Bw. Serge alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 13,2016 kwa ajili ya kujitambulisha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa Bw. Serge Prammertz wakati Bw. Serge alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 13,2016 kwa ajili ya kujitambulisha. (Picha na OMR)   . 


NEC YAPONGEZWA KWA KUENDESHA UCHAGUZI MKUU KWA AMANI

$
0
0
Na Elias Malima , NEC

Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala imeipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kufanikisha kuendesha Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015 vizuri na kuiacha nchi ikiwa na Amani, utulivu na Usalama.

Hayo yalisemwa jijini Dar ess Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Najma Murtaza Giga walipokutana na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere convention Center katika kikao mahsusi cha Kupitia Bajeti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Aidha, pongezi hizo kwa NEC zilitolewa na wajumbe wa pande zote mbili yaani wa Chama tawala na wale wa upinzani wa kamati hiyo kwa nyakati tofauti. Baadhi ya wabunge hao ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mheshimiwa Najma Murtaza Giga(CCM), Twahir Awesu Mohammed (CUF) na Nassor Suleiman Omar (CUF).

Alisema ni jambo la heri sana pale ambapo taasisi ama mtu anafanya kazi ya kutukuka kupewa sifa yake na kupewa moyo ili aendelee na moyo wa kufanya kazi kwa bidii na hatimaye kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi si tu kwa manufaa ya taasisi yake bali hata kwa Taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhan aliiambia kamati hiyo kwamba haikuwa kazi rahisi kuendesha na kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na Nchi ikaendelea kuwa na amani na utulivu kwani ushindani wa kisiasa ulikuwa mkubwa kiasi cha kutishia maisha ya watanzania.

“Tulijitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kufuata Sheria Kanuni na taratibu za kusimamia Uchaguzi pamoja na kwamba Bajeti ilikua haitoshi hasa wakati tunaanza zoezi la Uandikishaji wa Wapiga Kura kwa kutumia Teknolojia ya BVR ambapo tulilazimika kuandikisha wapiga Kura kwa kuhamahama” Alisema Kailima.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge Jenista Mhagama aliwashukuru wabunge kwa niaba ya Serikali kwa jinsi walivyothamini na kutambua Kazi kubwa iliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuahidi kufikisha Serikalini mawazo ya kuitafutia Tume fedha kwaajili ya Tume kuzipatia Asasi za Kiraia zinazotoa Elimu ya Mpiga Kura kwani lilijitokeza suala la Ukosefu wa Fedha za Kuendeshea Elimu hiyo.

Bajeti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 ni jumla ya Tsh4,830,537.167/= ikiwa ni fedha za matumizi ya kawaida OC Miradi ya Maendeleo pamoja na Mishahara ya watumishi.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ulifanyika tarehe 25 Oktoba ambapo aliyekua Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh.Dkt John Pombe Magufuli aliibuka Mshindi.

WAZIRI, MAKAMBA AFUNGUA WARSHA YA MAZINGIRA LEO.

$
0
0

  Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Washirika wa Maendeleo wanaojihusisha na Mazingira hapa Nchini  Mh. Egon Kochanke akiongea wakati wa warsha hiyo.
  Sehemu ya Wahudhuriaji wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba(hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha hiyo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, January Makamba akifungua warsha ya wadau wa Mazingira wa ndani na nje ya Nchi iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais juu ya kujadili jinsi Wafadhili wanavyoweza kusaidia Ofisi katika kuimarisha mambo mbalimbali ya mazingira.

MWIGULU,SENDEKA WASHIRIKI MAZISHI YA CHRISTINA LISSU MKOANI SINGIDA

$
0
0
 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akitoa heshima zake za mwisho mapema leo kabla ya mazishi, kwa aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lisu,Wilayani Ikungi mkoani Singida.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida,Bi Martha Mlata akitoaa heshima zake za mwisho mapema leo kabla ya mazishi, kwa aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lissu,Wilayani Ikungi mkoani Singida. 
Msemaji wa chama cha CCM,Ole Sendeka, Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba wakimpa pole Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA),Mh Tundu Lissu,ambao waliwasili wilayani Ikungi mkoani Singida kushiriki Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lissu.
 Msemaji wa chama cha CCM,Ole Sendeka akimpa pole Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA),Mh Tundu Lissu kwa kufiwa na dada yake
 Msemaji wa chama cha CCM,Ole Sendeka akitoa neno la pole kwa Wafiwa,ndugu,jamaa na marafiki kabla ya kufanya maziko, kwa aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lissu,Wilayani Ikungi mkoani Singida. 

WABUNGE WA AFRIKAMASHARIKI KUTOKA TANZANIA WATEMBELEA THE GUARDIAN NA KUTOA WITO KWA VYOMBO VYA HABARI KUWAELEZA WANANCHI FURSA ZILIZOPO KWENYE JUMUIYA HIYO

$
0
0

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Wabunge wa bunge la Arika Mashariki, (EALA), kutokaTanzania, wameendelea na ziara yao ya kutembelea vyombovya habari hapa nchini, ikiwa ni mkakati wa Jumuiya hiyo, kushirikisha vyombo vya habari ili kuwafahamishawananchi wa nchi hizo manufaa ya jumuiya hiyo kwao. 

LeoAprili 13, 2016, wabunge hao wakiongiozwa na Mwenyekiti wao Mh. Makongoro Nyerere, wametembelea kampuni ya The Guardian, wachapishaji wa magazeti  ya The Guardian, Nipashe na Lete Raha, na kupata fursa ya kuelezwa shughuli zifanywazo na waandishi wa habarikwenye kampuni hiyo ambapo walitembelea kitengo cha habari mtandao, (E-NEWS), kitengo cha usanifu gazeti na kumalizia kwa mkutano wa kubadilishana mawazobaina ya wabunge hao na uongozi wa chumba cha habari cha The Guardian. 

Pichani, msanifu wa gazeti la The Guardian, Ben Mgana (aliyekaa), akiwaonyesha jinsi gazeti hilo linavyoandaliwa kabla ya kuchapishwa. Wakwanza kushoto ni Mhari Mtendaji wa gazeti hilo, Wallace Maugo, Mkuu wa chumba cha Habari cha The Guardian, Jesse Kwayu, (wapili kushoto) na wabunge wa hilo wakiongozwa na wmenyekiti wao Mh. Makongoro Nyerere (watatu kulia)
 MhaririMtendaji wa The Guardian, Wallace Mauggo, (watatu kushoto) na Mhariri Mkuu wa Chumba cha Habari cha The Guardian Limited, Bw. Jesse Kwayu) wakiwaonyesha wabunge hao baadhi ya magazeti yanayochapishwa na kampuni hiyo
 Mwenyekiti wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, 9wapili kulia), akisalimianana Mkuu wa kitengo cha habari mtandao (E-NEWS), cha The Guardian Limited, Mashaka Mgeta, wakati wabunge hao walipotembelea chumba cha Habari cha The Guardian Mikocheni jijini Dar es Salaam
 Mashaka(kushoto) akisalimiana na Mbunge Mh. Nderakindo Kessy
 Mauggo (kushoto), akitoa maelezo kwa wabunge hao
"Sisi The Guardian, tukotayari kushirikiana na wabunge wa EALA, katika kuujulisha umma kuhusu manufaa ya jumuiya na nitoe wito kwa mbunge mmoja mmoja au kwa kupitia kundi lenu, mpatabo jambo muhimu mnalotaka jamii ilifahamu msisite kutujulisha nasi tutashirikiana nanyi" Jesse Kwayu (kushoto). Anayemsikiliza ni Mwenyekiti wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere.
"Tuko tayari kuweka column maalum kwa ajili ya shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki, miongoni mwenu mnaweza kuchangia kwa kuandika" Wallace Mauggo 
 "Lazima tukienzi Kiswahili ninampongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuonyesha njia" Mh. Nderaikindo Kessy
 "Waambieni Watanzania waondokane na uoga ni wakati muafaka sasa kwa wananchi wa Jumiya ya Afrika Mashariki kushiriki katika fursa za kiuchumi katika mfumo wa soko la pamoja, ili wmananchi wa Kigoma aweze kuvuka mpaka na kuingia Bunjumbura kuuza mihogo yake" Mh. Makongoro Nyerere
 "Tunaomba ushirikiano zaidi wa vyombo vya habari katika kutangaza fursa za kiuchumi zilizoko kwenye Jumuiya lakini pia ninaomba tuungane pamoja katika kuhakikisha Kiswahili inakuwa lugha rasmi ndani ya bunge la Afrika Mashariki." Shy-Rose Bhanji
 Jesse akisikiliza kwa makini
 Mh. Bernard Murunya (kulia), akimuonyesha kitu Mashaka Mgeta
 Picha ya pamoja, kutoka kushoto), Mh. Nderaikindo Kessy (Mb), Mh. Bernard Murunya (Mb.), Bw. Wallace Mauggo (Mhariri Mtendaji The Guardian), Mh Twaha Taslima (Mb), Bw. Jesse Kwayu, (Mkuu wa chumba cha Habari The Guardian Ltd), Mh. Makongoro Nyerere (Mwenyekiti wa wabunge wa EALA-Tanzania), Mh.Maryam Mohammed (Mb),Mh. Shy-Rose Bhanji (Mb) na Bw.Asheri Michael
 Jesse (kushoto), Mh. Makongoro Nyerere, na Bw. Wallace Mauggo
 Mh. Nderaikindo Kessy
 Mh. Bernard Murunya (kushoto) na Mh. Maryam Mohammed
 Mh. Maryam Mohammed
 Mh. Twaha Mussa Taslima, (kushoto) na Mh. Shy-Rose Bhanji
Wabunge kutoka kulia, Mh. Shy-Rose Bhanji, Mh. Twaha Mussa Taslima, Mh. Makongoro Nyerere, Mh. Maryam Mohammed, Bw.Asheri Michael wakimsikiliza MhaririMkuu wa chumba cha Habari cha The Guardian Limited, Bw. Jesse Kwayu

WANANCHI WATAKIWA KUWAOMBEA DUA VIONGOZI WA TAIFA ILI WAWEZE KUFANYA KAZI ZAO KIKAMILIFU

$
0
0
MKE wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa amewaomba wananchi wa wilaya ya Ruangwa kuwaombea dua viongozi wa taifa, Rais Dk. John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili waweze kufanya kazi zao kikamilifu.


Amesema kazi nzito inayofanywa na viongozi hao ya kuhakikisha nchi inakuwa salama na inasonga mbele kimaendeleo ni shughuli ngumu na inahitaji nguvu ya Mungu, hivyo ni vema wananchi wakawaombea dua ili kazi hiyo iweze kuwa na tija kwao na taifa kwa ujumla.


Mke wa Waziri Mkuu ameyasema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Chinongwe wilayani Ruangwa, ambapo amewaomba mwananchi hao wajitahidi kuwaombea dua viongozi hao ili malengo yao ya kuwaletea maendeleo yatimie.


Mary ambaye ameongozana na Waziri Mkuu Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa, katika ziara yake ya kuwashukuru wananchi waliomchagua kwa nafasi ya ubunge na kisha  Rais Dk Magufuli kumteua kuwa kushika wadhifa huo.


"Nawashukuru sana wananchi kwa kuwa kura zenu ndiyo zilizosababisha Mheshimiwa Majaliwa ambaye ni mbunge wetu kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, hivyo nawaahidi kuwa tutaendelea kushirikiana,” amesema mke wa Waziri Mkuu.


Amesema licha ya kuongezewa majukumu atahakikisha anaendelea kushirikiana na wanaruangwa ili waweze kuendeleza shughuli za maendeleo katika wilaya hiyo na kwamba wasiwe na wasiwasi kwani hata wasahau kwa kuwa anawapenda na kuwaheshimu.



Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

MWILI WA MAREHEMU WASHINGTON BENBELLA WAAGWA LEO HOSPITALI YA MUHIMBILI JIJINI DAR

$
0
0
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kanisani wakati wa kumwombea marehemu Washington Benbella pamoja kuagwa katika kanisa la Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Mustafa Hassanali akimzungumzia marehemu Washington Benbella alivyomjua pamoja na kufanya kazi naye kwenye kwenye kampuni ya Swahili Fashion

Mama mzazi wa Marehemu Washington Benbella akialia kwa uchungu wakati wa kuaga mwili wa mwaye katika kanisa la Hospitali ya Muhimbili.
Mustafa Hassanali akiaga mwili wa marehemu Washington Benbella wakati wa misa iliyofanyika katika kanisa la Hospitali ya Muhimbili
Yusuph rafiki mkubwa wa marehemu Washington Benbella akiaga kwa uzini mkubwa

Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wakiaga mwili wa marehemu Washington Benbella leo katika Hospitali ya Muhimbili
Mwili wa Marehemu Washington Benbella ukitolewa kanisani baada ya kufanyiwa maombi pamoja na kugwa kwa mili huo katika kanisa la Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam
Mwili wa Marehemu Washington Benbella ukipandishwa kwenye gari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho tarehe 14 mwezi wa Nne.
Baadhi ya waombolezaji washuhudia tukio la mwili wa Marehemu Washington Benbella ukipandishwa kwenye gari kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea wilaya ya Same kwa ajili ya mazishi.

WAZIRI NAPE AFUNGIA KIWANDA BUBU UWANJA WA TAIFA

$
0
0

Na Zawadi Msalla.a

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amekifunga mara moja kiwanda kilicho kuwa kikiendeshwa kwa njia zisizo halali na Wakandarasi wa Uwanja wa Taifa, Kampuni ya BFG kutoka nchini China.

Mhe. Nape amefanya zoezi hilo leo baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya Uwanja wa Uhuru na kubaini kuwepo kwa kiwanda hicho ambacho ni kinyume na taratibu na mkataba wa kisheria walio ingia baina ya Serikali na Kampuni yao ambao unahusu ujenzi wa miudombinu ya michezo pekee ikiwemo Uwanja wa Taifa na Uhuru.

Kabla ya kukifungia kiwanda hicho Waziri Nape aliomba maelezo ya kina juu ya uhalali wa uwepo wake na namna uendeshwaji wake unavyofanyika ili kujiridhisha ndipo alipofikia uamuzi huo wa kukifungia baada ya kujiridhisha kuwa kinaendeshwa kinyume na utaratibu.

“Ninataka kujua kwa undani zaidi uhalali wa kiwanda hiki cha useremala kama kipo ndani ya mkataba wa ujenzi wa Uwanja wa Taifa na eneo changamani la michezo”. Alisisitiza Nnauye

Uwepo wa kiwanja hicho kunapelekea ucheleweshwaji wa kukamilika kwa maboresho na ujenzi wa Uwanja wa Uhuru.

Aidha Waziri Nape amemuagiza Meneja wa Uwanja wa Taifa Rishe Urio kutoa maelezo ya kina juu ya uwepo wa Kiwanda hicho katika eneo la ndani ya masaa 24 ni kwanini akutoa taarifa juu ya uwepo wa shughuli za Kiwanda hicho katika eneo hilo ila hali yeye ndiye msimamizi mkuu wa Uwanja huo.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya BFG Cheng Longhai amekiri kuwa Kiwand hicho kinaendeshwa kinyemela kwakuwa hakihusiani na mkataba wa kampuni hiyo.

Wakatihuohuo Nape ameuagiza uongozi wa Selcom Tz kuhakikisha inakimilisha mfumo wa Tiketi za Kielekroniki na kukabidhi kwa Serikali ndani ya siku 30 kuanzia sasa.

Agizo hilo ni muendelezo wa kutekeleza maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim wakati akiongea na wadau wa sekta ya michezo kwa mara ya kwanza toka kuteuliwa kwake kuwa Waziri Mkuu.

Watanzania watakiwa kutumia mobile banking kukuza uchumi wao

$
0
0
DSC_0032
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akitoa hotuba katika mkutano huo. (Picha zote na Rabi Hume, Modewjiblog).

Nae Mkurugenzi Mkuu wa NMB nchini, Ineke Bussemaker amesema kuwepo kwa huduma za kibenki kupitia mitandao ya simu kumewezesha wateja wao kupata huduma kirahisi tofauti na miaka ya nyuma kabla ya kuanza kwa huduma ya mobile banking.

Alisema kupitia huduma hiyo kwa sasa wateja wao wanauwezo wa kutoa fedha, kulipia huduma mbalimbali kama kodi, kununua umeme, tiketi za ndege na hata kuangalia salio lililo katika akaunti zao za benki na wanachokifanya kwa sasa ni kuangalia jinsi gani wanaboresha zaidi huduma hizo kwa wateja hasa walio maeneo ya vijijini.

“Miaka ya nyuma kama mteja yupo kijijini anatumia muda mwingi kwenda sehemu iliyo na huduma ya benki lakini kwa sasa huduma za kibenki katika mitandao ya simu imerahisisha hata wateja wetu walio vijijini kupata huduma zetu kiurahisi,” amesema Bi. Bussemaker.
DSC_0061
Na Rabi Hume, Modewjiblog.

Kutokana na kukua kwa huduma za kibenki kupitia simu za mkononi (mobile banking), Watanzania wametakiwa kutumia nafasi hiyo vizuri ili iweze kuwasaidia kukuza uchumi wao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa siku mbili unaozungumzia maendeleo ya sekta za fedha kwa kutumia mifumo ya huduma za kibenki kwa kutumia mitandao ya simu (Africa Digital Banking Summit), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema ni muda muafaka kwa Watanzania kutumia huduma hizo kwa ajili ya kujiongezea kipato.

Alisema kupitia huduma hizo, Watanzania wanaweza kutuma nakupokea pesa kutoka maeneo mbalimbali hata ambayo yapo mbali na matawi ya benki hivyo wanaweza kufanya shughuli mbalimbali ikiwepo kufanya biashara kwa kutumia huduma hizo.

“Serikali imeunganisha nchi nzima na mkongo wa taifa na hii inawapa fursa watanzania kutuma pesa sehemu yoyote hivyo niwasihi watanzania kutumia kikamilifu nafasi hiyo ili kuboresha uchumi wao,” amesema Dkt. Kijaji.
Mkurugenzi Mkuu wa NMB nchini, Ineke Bussemaker akizungumza katika mkutano huo.Nae Meneja wa Mifumo wa Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Dadi amesema huduma za kibenki kwa kutumia mitandao ya simu imekuwa ikizidi kukua siku baada ya siku tangu ilipoanza nchini mwaka 2008 na mpaka sasa kuna benki 30 ambazo zimejiunga katika mfumo huo ili kuwasogezea huduma wateja wake.
DSC_0043
Meneja Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Dadi akitoa taarifa kuhusu matumizi ya mobile banking nchini.

DSC_0015
Mwongozaji wa mkutano huo, Chris Mauki.
DSC_0026
Mwenyekiti wa mkutano wa Africa Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu akizungumza kuhusu mkutano huo.
DSC_0029
Baadhi ya washiriki walioshiriki mkutano huo unaofanyika kwa siku mbili.
DSC_0051
Pia Mkurugenzi Mkakati wa Jackson Group Ltd, Kelvin Twissa ni mmoja wa washirikia waliohudhuria mkutano huo (wa kwanza kulia).

KUBENEA HAUKUMIA KIFUNGO CHA NJE

$
0
0

Mhe. Said Kubenea– Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA).

Na. Raymond Mushumbusi– Dar es salaam.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saeed Kubenea kifungo cha nje cha miezi mitatu kutokana kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ambaye sasa ni Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam.

Akisoma hukumu hiyo leo Jijini Dar es Salaam Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Thomas Simba amesema kuwa mahakama imeamua kumpa mshitakiwa adhabu ya kifungo hicho kwa kuwa ndilo kosa lake la kwanza, hivyo Mshatakiwa anastahili kupata adhabu ya huruma.

Chini ya adhabu hiyo iliyotolewa chini ya kifungu no 89 kifungo kidogo cha kwanza Mhe. Kubenea hatakiwi kufanya kosa la aina yoyote ambalo litamsababisha arudishwe tena mahakamani na endapo itatokea akafanya hivyo mahakama itampa adhabu ya kifungo cha kwenda jela.

Awali kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo mshtakiwa Said Kubenea mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba alipewa nafasi ya kujitetea ni kwanini asipewe adhabu kali kwa kosa alilolitenda ambapo alieleza Mahakama hiyo kuwa hakuwa na nia mbaya ya kwenda kufanya fujo eneo la tukio ambapo kulikuwa na mgomo wa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha TOOKU cha jijini Dar es salaam bali alikwenda kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgomo huo akiwa kama mwakilishi wa wananchi wa
jimbo la Ubungo. 

Ikumbukwe kuwa Jalada la kesi hiyo na 320 ya mwaka lilifunguliwa na Jamhuri dhidi ya Said Kubenea kwa kosa la kutumia lugha ya matusi kwa aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda, Aidha upande wa washtakiwa wameonyesha kutoridhishwa na
hukumu hiyo na wameomba kukata rufaa.

CHUO KIKUU ARDHI CHAWAPA MWONGOZO WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI ZA JIJI LA DAR NAMNA YA KUJIUNGA NA MASOMO YA ELIMU YA JUU KULINGANA NA UFAULU WAO.

$
0
0
Mtaalam wa Jiografia kutoka Chuo Kikuu Ardhi Dkt. Mlenge Fanuel Mgendi akiwahamasisha wanafunzi wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani kupenda kusoma na kuweka bidii katika masomo ambayo wanauwezo nayo ili yawasaidie kuendelea na Elimu ya Juu katika chuo Kikuu Ardhi leo jijini Dar es salaam. Chuo Kikuu Ardhi kinaendesha Programu ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa sekondari katika shule mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia kufanya uchaguzi sahihi wa kozi za masomo wanazotarajia kuendelea nazo pindi watakapohitimu masomo ya elimu ya Sekondari.
Mwanataaluma wa Chuo Kikuu Ardhi Bi. Latifa Litwe (kushoto) akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani namna ambavyo Chuo Kikuu Ardhi kinawajengea uwezo kielimu wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi na majanga mbalimbali pamoja na ushauri kuhusu sekta ya Ardhi kwa ujumla hapa nchini ikiwemo uhifadhi wa Ardhi na Sayansi ya Udongo.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani wakiangalia na kufurahishwa na moja ya Kazi ya Ubunifu wa Majengo na mitaa iliyofanywa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi mwaka wan nne leo jijini Dar es salaam.
Mwanataaluma wa Chuo Kikuu Ardhi Bw. Dennis Tesha akiwaeleke za wanafunzi wa shule ya wasichana ya Jangwani namna bora kuchagua masomo yao ya baadaye kulingana na sifa walizonazo watakapotaka kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini pamoja na kazi watakazofanya mara baada ya kuhitimu kulingana na masomo yao.
Moja ya kazi ya Ubunifu wa jengo la ghorofa lilobuniwa na mwanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani wakifurahia jambo mara baada ya kuangalia moja ya kazi ya ubunifu wa majengo iliyofanywa na wanafunzi wa mwaka wan ne wa Chuo Kikuu Ardhi walipokuwa wakizungumza na Afisa Uhusiano wa Chuo hicho Bi. Khadija leo jijini Dar es salaam.

VIJANA WA KITANZANIA WASHIRIKI MAFUNZO YA UWEZESHAJI KWA VIJANA JIJINI BEJA, NCHINI URENO

$
0
0
Vijana watano kutoka Tanzania ni miongoni mwa vijana 30 wanaoshiriki katika mafunzo ya wawezeshaji wa ujasiliamali unaozingatia mazingira yanayofanyika jijini Beja, nchini Ureno.

Mafunzo hao ambayo yanafanyika kwa muda wa siku saba yanalenga kuwajengea uwezo vijana hao kuendesha mafunzo kwa vijana wenzao katika nchi wanakotoka ili kusaidia kupunguza tatizo la ajira na uharibifu wa mazingira.

Nchi zinazoshiriki mafunzo hayo na majina ya taasisi zinazoshiriki kwenye mabano ni pamoja na wenyeji Ureno (Check In), Italia (Cesie), Argentina (Subiral Sur), Slovenia (Pina), Nepal (CNN) na Tanzania (TYCEN) ambapo kila nchini imewakilishwa na vijana watano chini ya mradi wa ujasiliamali wa kujali mazingira ‘Green Entrepreneurship’.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea kiwanda cha kuchakata taka cha Resialentejo, wakiongozwa na Injinia wa kiwanda hicho Pedro Sobral.
Wahsiriki wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea Halimashauri ya Manispaa ya Jiji la Beja ambao walipokelewa na Sonia Calvario Mshauri wa Meya wa Manispaa hiyo
Mkurugenzi wa TYCEN, Chris Ndalo kutoka Tanzania akitoa mada wakati mafunzo hayo
Mmoja wa wawezeshaji katika mafunzo hayo, Olga  Kuczynska

Rais wa taasisi ya Check In, Antonio Gomes akizungumza na washiriki katika mafunzo hayo

Picha ya pamoja ya washiriki

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO WA MABALOZI KUTOKA NCHI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Czech hapa nchini  Pavel Rezac, tukio hilo lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Ikulu jijini Dar es Salaam Balozi Mteule wa nchi ya  Jamhuri ya Czech hapa nchini  Pavel Rezac. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Czech hapa nchini  Pavel Rezac mara baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi mteule kutoka nchi ya  Jamhuri ya Sudani Kusini Mariano Deng Ngor aliyefika Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha hati yake za utambulisho.

 .  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Sudani Kusini Mariano Deng Ngor aliyefika Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha hati yake za utambulisho. 
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Brazil hapa nchini Carlos Alfonso Iglesias Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa Brazil hapa nchini Carlos Alfonso Iglesias Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa Tanzania nchini Kuwait Mahadhi  Juma Maalim Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Mahadhi alifika Ikulu kwa ajili ya kuagana na Mhe. Rais kwa ajili ya kwenda kuanza kazi yake hiyo rasmi nchini Kuwait. 
Kaimu Mnikulu Ngusa Samike kulia akimkaribisha Balozi Mteule wa Brazil Carlos Alfonso Iglesias Ikulu jijini Dar es Salaam katikati ni Kaimu Mkuu wa Itifaki James Mbwana kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kikanda na Kimataifa. PICHA NA IKULU

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images