Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LIMEFANIKIWA KUWAKAMATA WATU 63 WANAOZANIWA KUWA MAJAMBAZI.

$
0
0
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro kizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limekamata majambazi sitini na tatu (63) wa matukio ya unyang'anyi wa kutumia silaha katika oparesheni maalum iliyoendeshwa kwa wiki nzima na Jumla ya silaha sita, (6) ikiwemo SMG 1, SHORTGUN PUMP ACTION 3 na RIFLE 2. 
 Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro akionesha silaha huizo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimsiliza Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata watu 63 wanaozaniwa kuwa  majambazi wa kutumia silaha katika operesheni endelevu ya kuwasaka majambazi wanaofanya matukio mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi kanda maalumu Simon Sirro aamesema, miongoni mwa majambazi waliokamatwa ni Ibrahim Juma(31) mkazi wa Kiwalani Kigilagila, Samweli Mbonea (40) Fundi gereji Mkazi wa Kiwalani pamoja na Anthony Kanywenywe (60) Mwindaji na mkazi wa Kiwalani.

Amesema majambazi hao walikutwa na taa kubwa nne za magari, pawa windo moja na nati za magari na watuhumiwa sita  kati ya waliokamatwa wamekiri kushiriki katika matukio ya unyanganyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali likiwemo la Riki Hill Hotel katikati ya jiji na Lake oil Buguruni.

Katika tukio jingine  kikosi maalumu cha kupambana na majambazi kimefanikiwa kukamata silaha sita  aina ya SMG  moja ,Short gun pump action tatu na Rifle mbili katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

amesema silaha aina ya SMG iliyokatwa kitako ilipatikana baada ya askari kuwafyatulia risasi majambazi hao waliokuwa eneo la vingunguti ndipo walipoitupa silaha hiyo ikiwa kwenye mfuko mweusi wa plastiki na wao kukimbia katika bonde la Mto Msimbazi.

“Tunaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao na upelelezi unaendelea ili kubaini mmiliki halali wa silaha hiyo hatupotayari kuendelea kuona maovu yakiendelea kufanya jeshi lipo imara na tutapambana nao,” alisema Sirro.

Ameongeza kuwa jeshi hilo pia lilifanikiwa kukamata silaha Rifle mbili katika eneo la Masaki ambazo zilikuwa zimeficha na kufunikwa kwa taulo zikiwa na maandishi ya Collessium Fitness Club  moja ikiwa na namba A 6777013 iliyosajiliwa nchini kwa namba TZCAR 58596, na nyingine ikiwa na namba L 691848176 iliyosajiliwa kwa namba TZCAR 75062.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Kanda maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata jumla ya risasi 15 za silaha ndogo aina ya bastola zikiwa kwenye magazine, Risasi hizo alikutwa nazo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mamboleo Willium (41) Mfanyabiashara mkazi wa Mikocheni.
Katika mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kuwa na risasi hizo kinyume na sheria na kushindwa kueleza mahali alipozipata, mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa  na uchunguzi unaendelea kufanyika 

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MKUTNO WA ALAT.

$
0
0
 Waziri mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Edwin  Rutageruka wakati alipotembelea abanda la maonyesho  la TANTRADE kabla ya kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala  za Mitaa (ALAT) kwetuo cha Mikutano cha Dodoma  Aprili  8, 2016.
 Wasanii wa kikundi cha Nyota cha Dodoma  wakitumbuiza katika Mkutano Mkuu Malum wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma  mjini Dodoma Aprili  8,2016. 
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jafo kizungumza kabla ya kumakribisha Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kufungua Mkutano Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Dodoma Aprili 8, 2016. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Akizungumza wkati alipofungua mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania  (ALAT) kwenye  Kituo cha Mikutano cha Dodoma Aprili 8, 2016.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa  Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma Aprili 8, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT), Gulam Mkadam Taarifa ya Utafiti  kuhusu Sekta ya Umma na Binafsi kwenye serikali za Mitaa wakati alipoizindua baada ya kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi wa Jumuiya ya Tawla za Mitaa Tanzania (ALAT) kwenye Kituo cha  Mikutano cha Kimataifa cha  Dodoma  Aprili 8, 2016. Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawla za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WIZARA YA ARDHI YAWASILISHA HOTUBA YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2015/16

$
0
0
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb), akitoa hotuba ya utekelezaji wa bajeti ya wizara kwa mwaka 2015/16 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2016/17 kwenye Kamati ya kudumu ya Bunge ya ardhi, Maliasili na Utalii.
 Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, wakifuatilia Hotuba ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2015/16 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2016/17 iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe. Lukuvi.  
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbalimbali wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifuatilia Hotuba ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2015/16 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2016/17 iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe. Lukuvi.  

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA DUKA LA DAWA LA MSD KANDA YA MBEYA.

$
0
0
Na Rabi Hume.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefanya uzinduzi wa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa Kanda ya Mbeya.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mwalimu amesema uzinduzi wa duka hilo ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na serikali ya Rais Magufuli kuwatia wananchi huduma bora na kwa gharama nafuu.

“Neema hii imekuja kwa kipindi cha Rais Magufuli, sasa amekidhi matakwa na shauku ya wananchi wa Mbeya kwa kuwapa duka la dawa.

“Sera ya huduma ya afya inataka wananchi wachangie isipokuwa wazee, watoto na wajawazito na kupitia duka hili wananchi wataweza kupata dawa kwa gharama nafuu,” amesema Mhe. Mwalimu.

Duka hilo la dawa la Kanda ya Mbeya limetumia Shilingi Milioni 13 kwa ukarabati wa jingo na vifaa vyake.
Ummy Mwalimu akionesha moja ya dawa inayouzwa dukani hapo kwa shilingi 7,000 ambapo kwenye maduka binafsi inauzwa shilingi 25,000,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurine Bwanakunu na kulia ni Mfamasia wa duka hilo, Cornel Mkeng'e
Mfamasia wa Duka la Dawa, Cornel Mkeng'e akitoa maelezo kwa Ummy Mwalimu mara baada ya kuzindua duka hilo
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu akiangalia jinsi ya ufungashaji wa dawa kwenye ghala jipya la Kanda ya Mbeya.ghala hilo limelozinduliwa leo jijini Mbeya.
Duka la Dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Kanda ya Mbeya ambalo litahudumia mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipata maelezo jinsi ya utunzaji dawa kwenye ghala hilo.

SENDEKA: LOWASSA ANADANGANYA WATANZANIA KUTAFUTA MASLAHI KISIASA

$
0
0

Ole Sendeka akizungumza leo, Ofisi Ndogo ya makao
makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam.
Picha na Bashir Nkoromo
NA BASHIR NKOROMO
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, Rais Dk. John Magufuli hatafuti umaarufu, isipokuwa anachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania.


Hayo yamesemwa na Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa tuhuma za ufuisadi, Edward Lowassa, kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa ikiwemo hali ya kisiasa nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali na kile alichokiita tatizo la mfumo wa nchini, aliyosema katika mazungumzo yake na wanazuoni kutoka vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi, Aprili 7, 2016.



"Alichokifanya Ndugu Lowassa ni kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala yasiyo sahihi kwa maslahi ya kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi Rais John Magufuli hatafuti umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake wanachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania kwa jumla" alisema Sendeka na kuoneza;



"Pili, kuhusu suala la mfumo, Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani iliyopo ambayo iliwekwa na waasisi wa taifa hilo, Hayati Mwalimu Nyerere na Abeid Aman Karume ni imara na imekuwa ikiboreshwa kulingana na majitaji". 


KUSOMA TAARIFA RASMI > BOFYA HAPA

MAAFISA HABARI MKOA WA MWANZA WANUFAIKA NA VITENDEA KAZI KUTOKA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (aliyesimama) akizungumza na wadau wa sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Mhe. Nape Nnauye kukutana na wadau hao jana Jijini Mwanza pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo jijini hapo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga na kulia ni katibu wa CCM Mwanza Ndg. Miraji Mtaturu
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella (wapili kulia) akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye alipowasili ofisini kwake wakati wa ziara yake jana Jijini Mwanza kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa na kutembelea viwanja vya Michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo Jijini Mwanza. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga na kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Ndaro Kulwijira.
Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza Ndg. Atley Kuni akitoa taarifa ya sekta ya habari kwa mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Mhe. Nape Nnauye kukutana na wadau wa sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jana Jijini Mwanza pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo jijini hapo.
Msanii kutoka jiji la Mwanza Ndg. Feizal Saul (aliyesimama) akichangia wakati wa ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji jana Jijini Mwanza
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimkabidhi iPad afisa habari kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Bw. Stephen Msengi wakati wa ziara ya yake kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia jana Jijini Mwanza pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo jijini hapo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akimsikiliza Meneja wa Star times kanda ya ziwa Bw. Bakari Hassani (kushoto) alipotembelea ofisi hizo wakati wa ziara yake kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia jana Jijini Mwanza pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo jijini hapo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na watendaji wa TBC pamoja na Star Times nje ya ofisi za TBC zilizopo jijini Mwanza jana wakati wa ziara yake kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo jijini hapo. Wapili kushoto ni Meneja wa Star times kanda ya ziwa Bw. Bakari Hassani na watatu kulia ni Kaimu Mkuu wa Kanda ya ziwa TBC Bibi. Rachel Mwasha.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza alipowasili katika uwanja vya CCM Kirumba kupata taarifa ya uwanja huo wakati wa ziara yake kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa huo na kutembelea viwanja vya michezo na vituo vya utangazaji vilivyopo Jijini Mwanza. Kushoto ni Katibu wa CCM Mwanza Ndg. Miraj Mtaturu.

Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Mwanza

HOSPITALI YAKABILIWA NA UHABA WA VYUMBA VYA KUHUDUMIA WAGONJWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda akizungumza na Wagonjwa katika Hospitali ya Ngarenaro iliyoko jijini Arusha ,hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa pamoja na gari la wagonjwa

Na Woinde Shizza,Arusha.

Hospitali ya Ngarenaro inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa pamoja na kukosekana kwa miundombinu imara ya maji katika chumba cha upasuaji hivyo kuhitaji upanuzi pamoja na ukarabati wa hospitali hiyo ambayo inahudumia zaidi ya Wakazi 74000 wa kata ya Ngarenaro jijini Arusha.

Akizungumzia changamoto hizo Daktari Mfawidhi wa Hospitali hiyo Josephat Kivuyo katika taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Kivuyo amesema kuwa hospitali hiyo inahitaji upanuzi na ukarabati ili kuweza kuboresha huduma za afya ambazo zinahitajika na wananchi wengi.

Daktari huyo Mfawidhi alisema kuwa changamoto nyingine ni uhaba wa magari ya wagonjwa maarufu kama Ambulance kwani gari lililopo ni la zamani na haliwezi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kama inavyotarajiwa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amewataka wananchi na wadau mbalimbali kuunganisha nguvu katika kuboresha huduma kwa kufanya ukarabati ambao tayari umeshaanza ili kuboresha mazingira bora kwa wananchi na wahudumu wa afya.

Pia Amewataka Wahudumu wa Afya kuepuka kutoa lugha mbaya kwa wagonjwa na kuwahudumia vizuri ili kupunguza malalamiko katika sekta ya afya ambayo inahudumia watanzania wengi.Alisema Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ngarenaro unaendelea na tayari hivyo nguvu ya serikali n wadau wa maendeleo inahitajika katika kuhakikisha kuwa vituo hivi vinakuwa katika mazingira rafiki ya utoaji huduma za afya.

VITUO VYA POLISI VYAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UCHAKAVU

$
0
0

Na Woinde Shizza,Arusha.

Vituo vingi vya polisi hasa vile vilivyopo pembezoni mwa miji vimekua vikikabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo,uhaba wa majengo pamoja na vitendea kazi suala ambalo linapunguza kasi ya jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha aliyemaliza muda wake Liberatus Sabas amesema kuwa uhaba wa majengo na vituo katika maeneo ya vijiji umekua ukipunguza ufanisi wa kazi ya polisi katika kulinda raia na mali zao hivyo ameitaka serikali kukarabati vituo hivyo pamoja na kuweka vitendea kazi vya kutosha.

Akizungumza katika uzinduzi wa kituo kipya cha polisi cha Tengeru kilichozinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amesema kuwa hatua ya kuboresha vituo vya polisi itasaidia kutatua kero za kiusalama zinazokabili maeneo mengi mkoani Arusha.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru amelitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua baadhi ya polisi ambao huwabambikia wananchi na kujihusisha na vitendo vya rushwa ambavyo huwaumiza wananchi wengi

Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyezindua kituo hicho amewataka Wananchi wa kushirikiana vyema na jeshi la polisi katika kutoa taarifa za uhalifu ili kutokomeza vitendo vya uhalifu vinavyojitokeza kila mara

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA WATAFITI TOKA WASHINGTON DC-MAREKANI.

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na Bwana Tye Ferrell kutoka Shirika la Utafiti la Tetra Technology lililopo nchini Washington DC Marekani, pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mkandala (katikati) wakati walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam 08 Aprili, 2016.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimweleza jambo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mkandala (katikati) wakati wa mazungumzo katika ofisi ya Mhe. Spika jijini Dar es Salaam leo 08 Aprili, 2016.
Mtafiti toka Shirika la Utafiti la Tetra Technology lililopo nchini Washington DC Marekani Bwana Tye Ferrell akimweleza jambo Mhe. Spika Job Ndugai (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo katika ofisi ya Mhe. Spika jijini Dar es Salaam leo 08 Aprili, 2016.
Watafiti kutoka Shirika la Utafiti lililopo Washington DC-Marekani Bwana Patrick McGoven (kushoto) pamoja na Bwana Tye Ferrell wakimsikiliza Mhe. Spika Job Ndugai (hayupo pichani) wakati akiongea, wakati walipomtembelea ofisini kwake leo 08 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)

MCHEZAJI KANU WA NIGERIA ATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WA SHULE YA MSINGI YA MAJI MATITU MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Hapa Kanu akimkabidhi msaada wa sabuni ya unga Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi.
Kanu akitoa msaada wa magodoro.

Kanu akitoa msaada wa vyombo vya jikoni kwa wanafunzi hao.
Hapa Kanu akikabidhi unga wanafunzi hao. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha watoto hao, Rehema Lemway na kulia kwake ni Mlezi wa watoto hao, Somoe Said Omary.
Kanu akiwakabidhi wanafunzi hao Luninga.

Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wazazi wa watoto wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Kanu akiwa katika picha ya pamoja na watoto hao.
Kanu akishiriki kucheza na watoto hao wakati wakitoa burudani.


Kanu akiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa watoto hao.
Hapa Kanu akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule hiyo.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu (wa pili kushoto), akitoka kusaini kitabu cha wageni katika Shule ya Msingi ya Majimatitu baada ya kufika shuleni hapo leo asubuhi kutoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu wanao soma kwenye shule hiyo. Kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi. Wengine ni walinzi wake.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi, akimkaribisha mchezaji huyo shuleni hapo. Kutoka kulia ni Mwalimu Shabani Msabaha wa shule hiyo, Mchezaji Kanu na Makamu Rais wa Kampuni ya StarTimes, Zuhura Hanif.
Mchezaji Kanu akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kukabidhi msaada huo.

ITUMIENI MICHEZO KUJENGA UZALENDO NDANI YA JESHI LETU - WAZIRI NNAUYE

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimvisha medali bondia wa jeshi kama moja ya ishara ya ufunguzi wa ulingo wa ngumi waliopewa na wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ili kuimarisha mchezo wa ngumi jeshini na nchini kwa ujumla kwani ulingo huo utatumiwa na baraza la Michezo ya majeshi kujiimarisha katika mchezo huo.Wengine pichani ni Mkuu wa Mafunzo na Operesheni JWTZ Meja Jenerali Issa S. Nassoro(wa kwanza kushoto).
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi Mkuu wa Mafunzo na Operesheni JWTZ Meja Jenerali Issa S. Nassoro ulingo wa Ngumi wa kisasa ambao wizara ilipewa na Serikali ya China kwa ajili ya maendeleo ya ngumi nchini.Wizara imeamua kuwapa jeshi kwakuwa ni sehemu salama na watakuwa na nidhamu ya kuutunza na pia ulingo huo utaimarisha Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania(BAMMATA). Wengine pichani ni Brigedia Jenerali Martin Busungu ambaye ni mkurugenzi wa michezo jeshini (wa kwanza kushoto) na Kaimu mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Alex Nkenyenge(wa kwanza kulia).
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(wa pili kushoto) akiwa na Mkuu wa Mafunzo na Operesheni jeshi la wananchi Tanzania Meja Jenerali Issa S. Nassoro(wa kwanza kushoto) wakati wa makabidhiano ya Ulingo wa Ngumi uliotelewa na Wizara hiyo kwa jeshi la wananchi Tanzania(JWTZ).Wengine pichani ni Brigedia Jenerali Martin Busungu ambaye ni mkurugenzi wa michezo jeshini (wa pili kulia) na Kaimu mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Alex Nkenyenge.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipiga gitaa pamoja na bendi ya jeshi la wananchi Tanzania(JWTZ) wakati wa makabidhiano ya Ulingo wa Ngumi uliotelewa na Wizara hiyo kwa jeshi hilo leo jijini Dar es Salaam.Picha na Daudi Manongi-(WHUSM).


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amelihasa jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) kujenga uzalendo ndani ya jeshi letu kupitia michezo mbalimbali ya ndani.

Waziri Nape ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya Ulingo wa Kisasa wa Ngumi kwa Jeshi hilo ili wautumie kwa ajili ya maandalizi mbalimbali ya mchezo wa ngumi kwani Serikali imeona ni sehemu salama Zaidi na nidhamu ya kuutunza ipo na hata pale utapoitajika kutumika kwingine uchukuliwe na kurudishwa jeshini hapo kwani jeshi hilo limeleta heshima kubwa ya michezo nchini na kulifanya baraza la michezo ya majeshi (BAMMATA) kuimarika zaidi.

“Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa na mchango mkubwa sana katika michezo hapa nchini na limetuletea sifa kubwa sana kwetu na hivyo hatukuwa na shaka tulipoletewa ombi la ulingo huu.Ulingo huu utumike vyema na ulete heshima hapa nchini”Alisema Nape.

Aidha Waziri nape alitoa rai kwa jeshi hilo kurudisha michezo jeshini kwani inajenga uzalendo na kuimarisha umoja,undugu na urafiki.

Waziri huyo pia alikazia kuwa wizara yake itaendelea Kwa upande wake Meja Jenerali Issa Nassor ambaye ni mkuu wa mafunzo na Operesheni Jeshini alimshukuru Waziri Nape na Wizara yake kwa kuwapa ulingo huo na kuwa utawasaidia “Ulingo huo utatumika kwa mabondia wote Tanzania kwani utajenga Umoja na Kufahamiana na kukuza michezo na pia tutashirikisha askari wote kwani michezo ni sehemu ya kazi pia”.

Alisema Aidha alisema kuwa Msaada wa Ulingo huo ni chachu ya mazoezi na itawajengea wana mchezo huo chachu ya ushindi na kuwataka wadau mbalimbali wa michezo kuunga mkono jitihada za Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo imetoa ulingo huo kwa jeshi hilo baada ya kupewa msaada na serikali ya watu wa china mwaka jana ikiwa ni jitihada za kuboresha jeshi hilo.

kushirikiana na jeshi hilo katika michezo mbalimbali nchini. sana katika suala la mazoezi na hata mashindano mbalimbali. Meja Jenerali Issa. jeshi hilo kwani wana nia ya wazi ya kuwa kituo cha ubora. michezo nchini.

MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA TRA YAENDELEZA ZOEZI LA KUBOMOA MTANDAO WA WAFANYA BIASHARA YA MAGENDO UKANDA WA KUSINI MWA PWANI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu-Kilwa.

Siku ya tarehe 6/4/2016 maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kikosi cha (FAST)  wakiwa na maofisa wa Polisi walifanya upekuzi kwa lengo la kutafuta magendo kwenye nyumba ya mfanyabiashara Yusuf Barkat Sareh.

Upekuzi huo ulifanyika baada ya kupata taarifa za kiintelijensia zilizofanyiwa kazi muda mrefu.

Bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi zilikamatwa kama zifuatazo
Sukari ya India kilo 50 jumla mifuko762Sukari ya nje iliyokamatwa kwenye mifuko ya viwanda vya hapa nchini kilo 25 jumla mifuko 135,Mafuta ya kula lita ishirini (20) aina mbalimbali kutoka nje jumla madumu 49,Betri aina ya tigger katoni 223,Amira katoni 135,Sabuni za kufulia katoni 48

Vitu mbalimbali vilivyokamatwa kama ushahidi wa biashara haramu ya magendo ya sukari.Mashine mbili (2) za kushonea kwenye mifuko ya iliyowekwa sukari inatoka nje ya nchi na kuwekwa kwenye mifuko ya viwanda vya nchini nya sukari vya Kilombero,TPC na Mtibwa Sugar.
Mifuko mitupu mipya ya sukari kilo 25 toka India  2000
Mifuko iliyotumika ya kilo 50 mitupu ya sukari36,000
mifuko ya sukari iliyotumika ya Viwanda vya Tanzania ya kilo25 kiasi cha 1150
Madumu mafuta ya nje mchanganyiko ya kula lita 20 kiasi cha 609
Madumu matupu ya lita 10 ya nje kiasi cha 310.
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayomboakionesha ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta.
Sukari na viroba vya kuweka kwa matayarisho ya kuingizwa sokoni.
Hii ni Sukari iliyomwangwa chini kabla ya kuwekwa kwenye viroba
Askari wakisimamia zoezi la kuvunja mlango

Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi.
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA akionesha sukari.
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA 
Aina ya mafuta kutoka nje ya nchi tayari kuwekwa kwenye ndoo kwa kupeleka Sokoni
Polisi akilinda viroba vyenye sukari kutoka nje ya nchi.
Madumu yaliyokua na mafuta ya kula na ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta

Nyumba ya mtuhumiwa Yusuf Sareh iliyopo Somanga Njia nne Kikanda.

Nyumba hii ndiyo Ofisi ya Bosi ambayo hutumika kuweka bidhaa kabla ya kusambazwa sokoni iliyopo Somanga njia nne eneo la Kikanda Wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi.
sehemu ya kuweka sukari na kupima.

Nyumba inayotumika kuweka sukari

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO APRIL 9

Waziri Ummy Mwalimu atembelea Hospitali za Mkoa wa Mbeya

$
0
0
8e796dee-b674-43f7-97f8-3bad1046087d
Na Catherine Sungura, Mbeya

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara katika hospitali zilizopo Mbeya na kuzitaka hospitali zinazotumia mfumo wa ukusanyaji mapato wa kieletroniki wasibweteke na mapato wanayoyakusanya kila siku.Rai hiyo imetolewa na aziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea hospitali ya rufaa ya kanda ya mjini Mbeya.

Ummy alisema ukusanyaji wa mapato kwa mfumo huu unasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwemo ununuzi wa dawa, vifaa na vifaa tiba pamoja na utoaji wa motisha kwa watumishi."Bado tunatambua hali ya uhaba wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kuanzia ngazi zote, tukiweza kusimamia vizuri hili tutafanikiwa," alisema.

Aidha alisema wanatarajia katika serikali ya awamu hii bajeti ya dawa itaongezeka zaidi ya mara tatu kulinganisha na bajeti za nyuma, hivyo wameishauri Bohari Kuu ya Dawa (MSD) wanunue dawa toka kwa wawekezaji wa hapa nchini ambapo itakua na bei nafuu na itaongeza tija na upatikanaji wa dawa kwa haraka.

Waziri Ummy Mwalimu aliutaka Mkoa kufuatilia, kuwafichua na kuwachukulia hatua wale wote watakaojihusisha na wizi wa dawa."Tunao watumishi wachache wa afya ambao wanahujumu na kuiba dawa na kuzipeleka kwenye maduka ya dawa binafsi, hao hatutowafumbia macho na kuwapeleka mahakamani"

Kuhusu upungufu wa watumishi wa kada ya afya nchini, Waziri wa afya alisema, nchi ina upungufu wa asilimia 52, hivyo serikali inatarajia kuajiri watumishi takribani elfu kumi hivi karibuni ambao watatawanywa nchi nzima ikiwemo mikoa iliyo pembezoni.

Katika hospitali ya uzazi ya Meta, waziri huyo ameguswa na ufinyu wa wodi za wazazi na kupelekea mama wajawazito na waliojifungua kulala chini na wawili wawili kwenye kitanda kimoja na hivyo kuwataka kufanya haraka ujenzi wa jengo jipya litakaloondoa mrundikano wa mama wajawazito na watoto njiti.

Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya inakusanya kwa mwezi kiasi cha shilingi Milioni mia tano na pia inahudumia mikoa saba nchini na kuhudumia zaidi ya watu milioni mbili.
46e02c3a-bc41-4fed-9ff6-a180f42fa264
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisalimia na watumishi mara alipofika kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mbeya.
afc64d2e-46a1-49a8-be9b-59340b6d8a8a
Waziri Ummy akimsalimia mtoto Jenifer Joel (9) mkazi wa Chunya aliyelazwa hospitalini hapo.
5f7ab771-5109-4c0c-95e6-83931c8ec108
Waziri wa afya akimjulia hali mtoto Baraka Jekonia (1) mkazi wa Chunya aliyelazwa wodi ya watoto, Waziri Ummy ameitaka hospitali hiyo kuwachaji pesa wagonjwa wote wanaofika hospitali ya rufaa moja kwa moja bila kupatiwa rufaa kutoka vituo vya afya vilivyopo jirani na wananchi ili kupunguza msongamano kwenye hospitali za rufaa nchini.
8e796dee-b674-43f7-97f8-3bad1046087d
Katika hospitali ya uzazi ya Meta, Waziri Ummy Mwalimu alimsalimia Binti Kanisia Komba aliyejifungua mtoto wa kike katika hospitali hiyo mama wajawazito wote wanatibiwa kwa kadi ya bima ya afya inayodhaminiwa mpango wa kusaidia akina mama wajawazito wa KFW toka Banki ya Ujerumani.
9518e21d-3e1e-43ad-a96a-c9b85ce91018
Hospitali ya Meta tayari imetekeleza maagizo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ya kutoa kipaumbele kwa wazee wote nchini wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma.
974627cc-137b-436b-996a-f364952f7580
Waziri Ummy akiwasalimia wazazi waliolazwa kwenye moja ya wodi Hospitali ya Meta kutokana na ufinyu wa wodi inawalazimu akinamama wengine kulala chini hospitali hiyo inatarajia kuanza ujenzi wa jengo jipya ambalo litaondoa msongamano wa wazazi hospitalini hapo.

5b44d003-a727-495c-bde5-dea332ef407f
Waziri wa Afya akiwasalimia wagonjwa waliofika Hospitali ya Uzazi ya Meta kupata matibabu.

BREAKING NEWZZZ:MWANAMUZIKI NDANDA KOSOVO AFARIKI DUNIA

$
0
0
Globu ya jamii imepokea taarifa za Mwanamuziki mkongwe aliyewahi kujizolea sifa kem kem katika miondoko ya dansi hapa  nchini wakati akiwa na bendi ya FM miaka ya nyuma kabla ya kujiengua na kuunda kundi lake lililojulikana kwa jina la Stono Musica a.k.a Wajela Jela Gwaa, Ndanda Cosovo ‘Kichaa’ amefariki Dunia leo asubuhi,baada ya kuugua kwa siku chache

Taarifa kutoka kwa mtu wake wa Karibu ambaye pia ni Mwanamuziki wa dansi,Kardinal Gento amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na ameongeza kuwa Ndanda Kosovo amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa tangu juzi kutokana na matatizo ya tumbo.
*Tutazidi kupeana taarifa zaidi hapa hapa kadiri zitakavyokuwa zikiingia*
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-AMIN. 

Waziri Mkuu Majaliwa atemblea hospitali ya Benjamini Mkapa

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua mashine ya MRI katika hospitali ya Benjamin Mkapa kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma wakati alipoitembela Aprili 9, 2016. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, , Dkt. Hamis Kigwangala.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Khamis Kigwangala wakikagua mashine ya Mobile Digital xray wakati walipotembelea hospitali ya Benjamin Mkapa kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma Aprili 9, 2016.Kulia ni Kaimu Mkuu wa Hospitali hiyo ProfesaGesai. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA PALM VILLEGE MSASANI BEACH WATERFONT LEO

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Kampuni ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront akikabidhi Mfano wa hundi yenye jumla ya Tshs. 10,000,000. Kwa Uongozi wa Shule Msingi Mbuyuni kwa ajili ya kuendeleza Shule hiyo. Leo April 09,2016. Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wapili kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Geoge Simbachawene, na Waziri Biasha na Uwekezaji Mhe. Chales Mwinjage.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront Leo April 09,2016. Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wa tatu kushoto Mwenyekiti wa Kampuni Uwekezaji ya Group 6 Jonson Huang wa pili kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Geoge Simbachawene, na Waziri Biasha na Uwekezaji Mhe. Chales Mwinjage.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Pazia kuzindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront Leo April 09,2016. Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wa tatu kushoto Mwenyekiti wa Kampuni Uwekezaji ya Group 6 Jonson Huang.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront, Leo Aapril 09,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Afisa Muandamizi wa Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wakati wa ghafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Villege unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Gropu 6 ya China zinazojengwa Msasani Beach Waterfront. 
 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China. Mradi huo unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront unategemewa kutoa ajira jumla ya watu 2000 utakapokamilika. Kuli Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Jonson Huang, Leo Aapril 2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China. Mradi huo unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront unategemewa kutoa ajira jumla ya watu 2000 utakapokamilika. Leo Aapril 09,2016.

(Picha na OMR).

HOSPTALI YA RUFAA IRINGA YAPEWA MWEZI MOJA KUTAFUTA UFUMBUZI WA UTEKETEZAJI WA TAKA HATARISHI

$
0
0
Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, Mh luhaga Mpina , kushoto Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesera Kulia Naibu Meya wa mji wa Iringa Bw. Joseph Liata ambae pia ni diwani (Chadema) kwa pamoja wakifanya usafi katika soko la mji wa Iringa.
Kushoto Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesera kulia Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina wakimwaga maji wakati wakifanya usafi sokoni Mkoani Iringa Leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, Akiuandaa mche wa mti kabla kuupanda katika eneo la chanzo cha maji cha chemchem cha Kitwiru, Leo Mkoani Iringa.
Kulia Mganga Mkuu mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Iringa dkt Robert Salim, akitoa maelezo ya uteketezaji wa taka katika hospatali ya Rufaa kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina na Ujumbe wake walipokagua mazingira ya hosptali hiyo leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina Akimwagilia maji mara baada ya kupanda mti , katika eneo la chanzo cha maji cha Kitwiru Mkoani Iringa.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa, Mkoani Iringa Kulitaftia ufumbuzi suala la uteketezaji wa taka ngumu katika hospitali hiyo.

Mh. Mpina ametoa maagizo hayo leo alipotembelea Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa katika ziara yake ya kukagua usafi wa mazingira na utekelezaji wa sheria ya usimamizi wa maziringa katika viwanda vya mkoa wa Iringa.

Imeelezwa kuwa uteketezaji wa tanga hatarishi katika hosptali hiyo ya mkoa umekumbana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa kifaa cha kuteketeza taka hospitalini hapo kwa muda mrefu bila matengezo yeyote uliosababishwa na taratibu za utekelezaji manunuzi serikalini.

Kwa Upande wake mganga mkuu mfawidhi wa hospital hiyo dkt Robert Salim Amemueleza Naibu waziri Mpina kuwa taka zizalishwazo katika hosptali hiyo zimekuwa zikitupwa katika Dampo la mkoani hapo na hata hivyo..hosptali imekuwa na wakati mgumu sana katika kuteketeza taka hatarishi kama vile za sindano, gloves, nyembe na bandeji mana haziozi ardhini kirahisi.

Akitolea ufafanunuzi sualala za uteketezaji wa taka hatarishi hospitalini hapo, mratibu wa kanda ya nyanda za juu kusini wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) bw. Godlove Mwamsojo..ameleeza kuwa baraza limewahi kushauri uongozi wa hosptali hiyo kuteketeza taka hizo kwa kusaidiwa na kiwanda cha mbao cha Sao hill kilichopo wilayani Mufindi kwa kuwa kiwanda hicho kina vifaa vya kutosha, bila mafanikio kutokana na sababu kwamba hospital hiyo huzalisha taka nyingi kuzidi uwezo wa kiwanda cha Sao Hill kusaidia kuziharibu.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Mpina alikagua mazingira ya soko la Mjini Iringa na kushiriki katika usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti, ambapo Mh. Mpina,alipanda mti katika kata ya Kitwivu na kuwaasa wakazi wa Iringa kuwa walinzi wa misitu na kutoa taarifa za wizi na uhujumu wa magogo ili sheria ichukue mkondo wake na kuwaasa watunze vyanzo vya maji kama walivyotunza vizuri chanzo cha maji ya chemchem cha Kitwivu.

“Taifa lazima lipande miti ili kuhepukana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi tunazokumbana nazo.” Alisisitiza. Aidha Mh Mpina aliiongeza Wilaya ya Mufindi kwa kupitiliza lengo la kupanda miti milioni moja na laki tano kila mwaka katika kila wilaya na kupanda miti milioni thelathini na tano kwa mwaka.

WAZIRI JENISTA ATOA UBANI KWA WAFIWA MAAFA YA KAWE

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagamaakitoa ubani kwa Gaudensia Deogratius aliyefiwa na watoto wawili na mume baada ya kufunikwa na kifusi Kawe Ukwamani Dar Es Salaam Aprili 9, 2016
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa mkono wa pole kwa mama wa marehemu Ephrahim Mangule (aliyefariki kwa kuangukiwa na kifusi Kawe) wakati wa msiba huo Kinondoni Dar es Salaam tarehe 9 Aprili, 2016
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagamaakitoa salamu za pole kwa wafiwa waliopotelewa na ndugu 3 baada ya mvua zilizonyesha Aprili 7, 2016 na kuangukiwa na nyumba Kawe Dar es Salaam kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Raymond Mushi
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Raymond Mushi akizungumza na moja ya familia ya wafiwa walioangukiwa na kifusi Kawe Dar es Salaam wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipowatembelea tarehe 9, Aprili, 2016
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia chumba kilichoangukiwa na kifusi baada ya mvua kubwa zilizonyesha Aprili 7, 2016 na kuua watu 5 wa familia moja Kawe Dar es Salaam.

Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Uratibu,Ajira,kazi na watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama amewatembelea wananchi waliopatwa na majanga ya kuangukiwa na kifusi eneo la Kawe na kuwapa mkono wa pole.

Akiongea na moja ya familia zilizopatwa na maafa hayo Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya tukio hilo na kwa vifo vilivyojitokeza na kuahidi kutoa ushirikiano kwa familia ya wafiwa na waathirika wa tukio hilo.

“Ndugu zangu tumekuja kushirikiana nayi kwenye msiba huu mzito, ambao wenzetu wamepoteza karibu familia nzima kutokana na haya maafa, poleni sana kwa msiba na Serikali ipo pamoja nayi katika kipindi hiki kigumu.” Alisema Mhe Jenista.
`
Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wakati Serikali inapokuja kwa ajili ya kujadili jinsi ya kutatua mambo yanayowezesha kuhatarisha maisha yao hasa, tatizo la makazi yaliyopo mabondeni kwa ajili ya usalama wao na familia zao katika kuzingatia suala la mipango miji ili kuepukana na majanga kama haya.

Aidha kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Raymond Mushi amesema kwa upande wake amesikitishwa na tukio hilo na kuongeza kuwa Wilaya imejipanga kwa kushirikiana na kamati ya maafa ya Wilaya na Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuendelea kuangalia ni kwa namna gani wataweza kuwasaidia wananchi waliobaki katika maeneo hayo.

Akitoa shukrani kwa niaba ya familia ya wafiwa Bi Gaudencia Deogratius ambaye amepoteza mume na watoto wawili ameishukuru Serikali kwa faraja aliyopata kutoka kwa Waziri na hakutegemea kupata ugeni huo na ameiomba Serikali kuwasaidia wale waliopo mabondeni ili kuepusha majanga mengine zaidi kutokea.

Tukio la hili la nyumba kuangiwa na kifusi katika eneo la kawe Jijini Dar es Salaam lilitokea April 7 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja.

WAZIRI MBARAWA ARIDHISHWA NA UJENZI WA FLOW METER.

$
0
0
Meneja wa mradi wa Ujenzi wa Flow Meter ya Kigamboni Eng. Mary Mhayaya akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi huo.
Muonekano wa Flow Meter mpya ya Kigamboni katika hatua za mwisho za ujenzi wake.
Muonekano wa Daraja la Kigamboni mara baada ya ujenzi wake kukamilika.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kivuko cha Magogoni (kushoto) na Nahodha wa kivuko hicho (kulia) wakati alipokikagua.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelekezo kwa Mkurugenzi Msaidizi Barabara za Mijini Eng. Hussein Mativila (kushoto) alipokagua Daraja la Kigamboni.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema mtambo mpya wa kisasa wa kupima mafuta yanayoingia nchini flow meter unaojengwa Kigamboni jijini Dar es salaam uko katika hatua za mwisho za kukamilika kwake na utaanza kazi rasmi mapema mwezi ujao.

Prof. Mbarawa amesema hayo wakati alipokagua mtambo huo unaosimamiwa na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) na kuhimiza waendeshaji wa mtambo huo wawe watu wenye uadilifu wa hali ya juu na elimu ya kutosha ili kuulinda na kuwezesha kufanyakazi inavyostahili.

“Hakikisheni mnawasiliana na Wakala wa Vipimo nchini (WMA), ili wahakikishe mtambo huu unaviwango vinavyotakiwa vitakavyowawezesha wafanyabiashara wa mafuta kuridhika na ufanyakazi wa mtambo huu ili kuondoa malalamiko”, amesema Prof. Mbarawa.

Zaidi ya shilingi bilioni 12 zimetumika katika ujenzi wa mtambo huo ambao utawezesha Serikali kupata mapato stahiki na wafanyabishara kupata mafuta sahihi kwa mujibu wa mahitaji yao.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni na kuwataka wananchi kuhakikisha wanalitumia daraja hilo kwa usahihi na kuepuka vitendo vyote vya hujuma.

Amesema daraja hilo lililojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 214 linatarajiwa kufunguliwa rasmi Aprili 16 na litakuwa na njia sita za magari na mbili za watembea kwa miguu.

“Nawataka wananchi na watumiaji wote wa daraja hili kuhakikisha kuwa miundombinu ya daraja haihujumiwi na watu wenye nia mbaya kwani vitendo vya aina hiyo licha ya kuharibu daraja vitahatarisha usalama wa watumiaji”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Naye Msimamizi wa Daraja hilo kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eng. Karim Mataka amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa Daraja la Kigamboni umekamilika katika hatua zote na kinachosubitriwa na ufunguzi na kuanza kutumika.

Amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya daraja hilo kwa madereva na watembea kwa miguu ili kuepuka usumbufu siku za mwanzoni.

Daraja hilo litakalofunguliwa rasmi Aprili 16 litapunguza msongamano wa usafiri kwa wakazi wa kigamboni na maeneo ya katikati ya jiji la Dar es salaam
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images