Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

DKT. SHEIN AWAONGOZA VIONGOZI MBALIMBALI KATIKA DUA YA KUMUOMBEA MAREHEMU MZEE KARUME

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka shada la mauwa katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume baada ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli,kuweka Shada la mauwa katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume baada  ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli,(wa pili kulia) pamoja na Viongozi mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa.
Viongozi mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanawema Shein (kushoto) Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume,Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume,Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi pamoja wake wa Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa.


MCHEZAJI KANU WA NIGERIA AZINDUA DUKA JIPYA LA STARTIMES KESHO KWENDA KUTEMBELEA SHULE YA MSINGI MAJIMATITU MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (kulia),akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la Kampuni ya StarTimes lililopo jengo la Mkuki Mall Barabara ya Nyerere Dar es Salaam leo mchana. Mchezaji huyo yupo nchini kwa ziara ya siku tano. Kulia kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao.
 Ofisa Mauzo wa StarTimes Tanzania na mshereheshaji wa uzinduzi huo, Tang Jing Yu 'Juma Shorabaro wa Kichina' (kulia), akiendelea na majukumu yake.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Mr.Canter, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao (wa pili kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

 Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaamleo mchana, baada ya kuzindua duka la Kampuni ya StarTimes lililopo jengo la Mkuki Mall wakati wa ziara yake aliyoianza jana  nchini. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Mr.Canter, Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao, Katibu wa mchezaji huyo, Kingstey Obiekwe na Makamu wa Rais wa StarTimes, Zuhura Hanif.
  Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (katikati), akitia saini yake katika jezi.
 Kanu akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa StarTimes na wa jengo la Mkuki Mall baada ya kuzindua duka hilo.
Mmiliki wa Blog ya Full Shangwe, John Bukuku akichukua picha na mchezaji huyo.

Na Dotto Mwaibale


Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Naijeria (Super Eagles) na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu ameshiriki katika uzinduzi wa duka jipya la kampuni ya StarTimes Tanzania lililopo katika jengo la Mkuki Mall Barabara ya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mchezaji Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika ambapo inafanya shughuli zake katika nchi zaidi ya 10 amesema kuwa anajisikia mwenye furaha kuwepo nchini na atashiriki shughuli mbalimbali za kampuni pamoja na za kijamii.

“Ni mara ya kwanza mimi kuwepo nchini Tanzania, nashukuru nimefika salama na kupokelewa kwa ukarimu mkubwa, kwa kweli sikutarajia. Uwepo wangu hapa ninaiwakalisha kampuni ya StarTimes barani Afrika kama balozi wao na kama balozi ninao wajibu wa kufika kila nchi ambayo kampuni hii ipo. Kwa namna nilivyopokelewa ninaamini kuwa kweli StarTimes ni kampuni kubwa, inapendwa na kujulikana miongoni mwa watanzania wote.” Alielezea Bw. Kanu

“StarTimes wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanafurahia huduma za matangazo ya dijitali kwa ubora wa hali ya juu na gharama nafuu. Na hii ni kutokana na falsafa iliyojiwekea kampuni ya kutaka kuhakikisha kuwa kila nyumba ya muafrika inafikiwa na matangazo hayo. Changamoto ni nyingi katika uendeshaji na utoaji huduma za kidijitali lakini kampuni imejizatiti kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika uboreshaji wa vipindi na chaneli zake. Kwa mfano kwa sasa kama mnavyoweza kushuhudia kuwa ligi kubwa barani Ulaya za Bundesliga na Serie A za nchini Ujerumani na Italia zinaonyeshwa moja kwa moja kupitia StarTimes Pekee.” Aliongezea Kanu

“Michezo na burudani ni maudhui muhimu sana ambayo lazima yawekewe mkazo kwani ndivyo vitu vinavyopendwa na kuwavutia wateja wengi hivyo haina budi kuweka mkazo. Ninaamini kuwa uwepo wangu nchini Tanzania utasaidia kwa kukaa chini na uongozi wa kampuni nchini na kuweza kuona wanawaongezea na kuwapatia nini wateja wao. Ninatumaini ninacho cha kuongezea kwa nilichojifunza kutoka nchi kama za Uganda na Kenya ambazo nimetokea huko pia,” alisema na kumalizia Kanu kuwa, “Nashukuru kuwepo Tanzania na ninaamini nitajifunza na kushirikiana kwa mengi kwa kipindi nitakachokuwepo mpaka kuondoka kwangu.”

Naye kwa upande wake akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya ambalo litakuwa ni la saba kwa mkoa wa Dar es Salaam pekee, Mkurugenzi wa Uendeshaji (Operesheni) wa StarTimes Tanzania, Bw. Carter amebainisha kuwa duka hilo jipya litawarahishia wateja wote wanao kama maeneo ya jirani kama vile Tandika, Mbagala, Temeke, Kurasini, Yombo, Kiwalani, Vingunguti na kwengineko kujipatia huduma na bidhaa kwa urahisi zaidi.

“Leo tunayo furaha kubwa kufungua duka hili jipya ambalo katika kumbukumbu litakuwa limezinduliwa na balozi wetu barani Afrika, Nwanko Kanu. Duka hili litakuwa msaada mkubwa kwa wateja walio maeneo ya jirani na kwingineko na ningependa kuwatoa wasiwasi kuwa litakuwa linatoa huduma zenye ubora sawa na maduka yetu yote hivyo wasiwe na wasiwasi. Ninawaomba wateja wetu watembelee hapa kujipatia huduma kama vile kununua visimbuzi, antena na kebo, vocha za malipo ya mwezi pamoja na huduma kwa wateja.” Alimalizia Bw. Carter.


Rais Magufuli ashiriki kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari Mjini Kigali

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wameungana na wananchi wa Rwanda kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 22 ya tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu takribani milioni 1.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika eneo la Gisozi Mjini Kigali, yalipo makumbusho ya mauaji ya Kimbari ambapo Rais Magufuli na Mkewe wakiwa na mwenyeji wao Rais Paul Kagame wa Rwanda na Mkewe Mama Janeth Kagame wameweka shada la mauaji katika eneo walipouawa idadi kubwa ya wananchi wa Rwanda na pia wakawasha mwenge wa matumaini kwa walionusurika katika mauaji hayo na kwa Taifa zima la Rwanda.


Pamoja na kupata historia ya mauaji hayo ya kimbari, Rais Magufuli akiongozwa na mwenyeji wake Rais Kagame ametembelea jumba maalum lililohifadhi kumbukumbu ya watu waliopoteza maisha, ambapo amepata maelezo kutoka kwa wahifadhi wa makumbusho hiyo, na pia kujioonea picha na mabaki ya mifupa na mafuvu ya binadamu waliouawa.


Akizungumza mara baada ya kutembelea jumba hilo la makumbusho Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na mauaji hayo na kusema tukio hilo halipaswi kurudia."Haitatokea tena, hatuwezi kubadilisha yaliyopita lakini tunaweza kubadilisha mambo ya sasa na yajayo, mauaji haya hayapaswi kutokea tena"Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ambaye aliingia nchini Rwanda jana tarehe 06 April, 2016 ikiwa ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu aingie Madarakani Tarehe 05 Novemba, 2015 ameondoka Mjini Kigali jioni hii na kurejea Jijini Dar es salaam.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Kigali


07 April, 2016

SIMBACHAWENE AKUTANA NA WAFANYABIASHARA NA KUAHIDI USHIRIKIANO

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene akiongea na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene (kulia) akiteta jambo na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Bw. Johnsen Estomih Minja mara baada ya kikao chao leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………….

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene amekutana na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania na kupata nafasi ya kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili na kuahidi kushirikiana nao katika kutatua kero hizo.

Akizungumza na wafanyabiashara hao waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Tamisemi wamejadiliana masuala mbalimbali ya kibiashara ili yaweze kunufaisha jamii na taifa.

“Nimesikia mapendekezo yenu nitayafanyia kazi, nitawaita ili tujadiliane katika kujenga mazingira bora na rafiki ya biashara yatakuwa na manufaa kwenu taifa kwa ujumla” alisema Mhe. Simbachawene.

Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kushirikiana na wafanyabiashara nchini na kulihakikishia taifa kuwa uchumi imara kulingana na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025. 

Katika kikao hicho wafanyabiashara walipata nafasi ya kumueleza Mhe. Waziri kero mbalimbali zinazowakabili zikiwepo utitiri wa kodi, ugumu katika upatikanaji wa leseni na kukosekana kwa uwiano wa tozo za leseni kati ya sehemu moja na nyingine ambapo Mhe. Waziri aliahidi kufanyia kazi kero na mapendekezo mbalimbali ya kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara waliyowasilisha kwake.

Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Bw. Johnsen Estomih Minja alisema wafanyabiashara wanapenda kuona Tanzania ikikua kiuchumi na wao kama wafanyabiashara wangependa kuwa wadau wa kuisaidia nchi kukua kiuchumi, hivyo wanaomba serikali iweze kuwashirikisha katika masuala mbalimbali yanayohusiana na masuala ya kibiashara ili waweze kutoa mchango wao wa mawazo na kuondoa ugomvi kati ya wafanyabiashara na Serikali yao.

Miongoni mwa masuala ambayo Jumuia ya Wafanyabishara Tanzania imependekeza yaangaliwe kwa undani kuwa ni pamoja na serikali kuangalia upanuzi wa wigo wa ulipaji wa kodi,kuunganishwa kwa kodi na tozo mbalimbali katika ulipaji na kurahisishwa kwa utaratibu wa ulipaji wa leseni.

MIUNDOMBINU INAYOLETA MAJI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM YAENDELEA KUJENGWA.

$
0
0
Msimamizi wa ujenzi wa Mradi wa bomba jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 40 ambalo liko katika hatua za mwisho za ujenzi kutoka DAWASA Mhandisi Christian Gava akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiufundi kuhusu mradi huo. Kushoto ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Jamii wa DAWASA Neli Msuya.
Msimamizi wa ujenzi wa Mradi wa bomba jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 40 ambalo liko katika hatua za mwisho za ujenzi kutoka DAWASA Mhandisi Christian Gava akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiufundi kuhusu mradi huo.
Ujenzi wa Mradi wa bomba jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 40 ambalo liko katika hatua za mwisho.

TANZIA: Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Mh. Christina Lissu Mughwai afariki dunia

$
0
0
Taarifa iliyotufikia hivi punde, inaeleza kuwa, Mbunge wetu wa Viti Maalum na Dada wa Mh. Tundu Lissu, Mh. Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Kansa tangu mwaka jana. 

Mungu aiweke roho Marehemu Mahala pema peponi 

Amin.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE KUMBUKUMBU YA KARUME

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijiandaa kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muasisi ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar, ambapo Makamu wa Rais amemusakilisha Rais John Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa pili kulia, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kulia na Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Dua ya pamoja mbele ya Kaburi la Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muasisi ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar,Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Amani Abeid Karume mara baada ya Dua kufanyika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa pili kulia Mama Mwanamwema Shein kulia Mama Asha Ali Iddi wa pili kushoto na Mama Zakia Bilal kushoto, wakiwa katika Dua ya pamoja kwa ajili ya kumuombea Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muasisi ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar, Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli.

RAIS MAGUFULI AREJEA NYUMBANI KUTOKA RWANDA KATIKA SAFARI YAKE YA KWANZA NJE YA NCHI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange huku Inspekta jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu akisubiri zamu yake  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Msajili wa vyama vya Siasa Mhe Jaji Francis Mutungi mara baada ya kutua  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongozana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 

MCHEZAJI NWANKO KANU ATEMBELEA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE MUHIMBILI

$
0
0
Mmoja wa wagonjwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ya hospitali ya taifa ya Muhimbili mtoto Mariam Omary akifurahi baada ya kupata fursa ya kutembelewa na kujuliwa hali na aliyekuwa mchezaji nyota wa nigeria, Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika.
Fatuma Shaban akipokea zawadi kutoka kwa aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Nigeria na kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika Nwankwo Kanu kwa niaba ya mtoto wake, Ramadhan Shaban ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo kwenye taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya Taifa ya Nigeria Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika akizungumza jambo na madaktari katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) alipotembelea taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ya hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika akiwasili katika Jengo la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako amewatembelea wagonjwa wa moyo leo. Kanu atakiwepo nchini kwa muda wa siku tano kushiriki shughuli mbalimbali za kampuni na kijamii.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo, Dk Peter Kisenge katika taasisi hiyo akimkaribisha Nwankwo Kanu Ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika. Kanu atakuwepo nchini kwa muda wa siku tano kushiriki shughuli mbalimbali za kampuni na kijamii.

Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika akimsikiliza Daktari bingwa katika Taasiai ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk Peter Kisenge wakati akitoa taarifa fupi ya taasisi hiyo
Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Nigeria, Nwanko Kanu akifafanua jambo kwa madaktari wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo hospitali ya taifa ya Muhimbili wakati alipotembelea hapo.
Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Nigeria, Nwanko Kanu akimsikiliza mmoja wa madaktari wakati alipotembelea katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo huku madaktari wa hospitali hiyo wakifuatilia mazungumzo hayo.

Aliyekuwa mchezaji nguli wa timu ya taifa ya Nigeria au Super Eagles, Nwankwo Kanu ambaye pia kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika leo ametembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa lengo la kujua ni jinsi gani taasisi hiyo inafanya kazi pamoja na kuwajulia hali wagonjwa wa moyo waliolazwa katika Taasisi hiyo. pia

Akizungumza baada ya kuwasili katika Taasisi hiyo Kanu ameelezea kuguswa na tatizo la ugonjwa wa moyo hasa kwa watoto wadogo ambao amewatembelea na kuahidi kubadilishana uzoefu kuhusu huduma za matibabu zinazotolewa na wataalamu wa tasisi hiyo.

“Tatizo la moyo ni kubwa sana kwa sasa na limekuwa likiongezeka kwa kasi lakini cha kusikitisha ni kuwa sio kila mtu anaweza kumudu gharama za matibabu yake. Hivyo basi kuna umuhimu mkubwa sana kwa serikali na wadau wengine kuanzisha vituo maalumu kama hivi ili kuwasaidia wasiojiweza.” Alisema Kanu

Katika mazungumzo yake mchezaji huyo wa nyota wa zamani ambaye aliwahi kuwika na vilabu kama vile vya Arsenal, Ajax na Inter Milan, amesema kuwa pamoja na kuja kwa shughuli mbalimbali kama balozi wa kampuni ya StarTimes lakini pia ana nia ya kushirikiana na watalaamu wa Taasisi hiyo ya Moyo. Alielezea kuwa lengo ni kuwasaidia matibabu watoto wenye matatizo ya Moyo ambao wazazi wao hawana uwezo na kwamba watazungumzia suala hilo.

“Nimefarijika sana kuona serikali ya watu wa Tanzania inachukua hatua stahiki katika kuwasaidia wananchi wake. Pia ningependa kuchukua fursa hii kuwataka watanzania hasa wanamichezo kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara kwani ukijua tatizo mapema ni rahisi kupata matibabu na kupona. Tumeona mifano michache ya wachezaji maarufu mbalimbali barani Afrika na kwingineko duniani wakifariki au kunusurika kufa wakiwa katika ya mchezo kutokana na kutoweka wazi mustakabali wa afya zao.” Alihitimisha balozi huyo wa StarTimes barani Afrika

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dkt. Godwin Godfrey amelezea kuwa tangu Julai mwaka jana mpaka sasa tasisi hiyo kwa kushirikiana na wataalam kutoka nje ya nchi wamewafanyia upasuaji watoto zaidi ya 200.

Nwankwo Kanu mbali na kujizolea umaarufu na heshima kubwa katika medani za soka barani Afrika na Ulaya yeye pia alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka 1996 na ndipo alipoamua kufungua taasisi yake ya moyo inayoitwa “The Kanu Heart Foundation.”

Taasisi yake hiyo iliyoko nchini Nigeria ambako ndiko alipozaliwa aliianzisha kwa madhumuni makubwa ya kusaidia wenye matatizo kama yake na ameahidi taasisi hiyo kushirikiana na taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika masuala mbalimbali.

UJUMBE MWANANA KUTOKA KWA NATHAN MPANGALA

DELILAH - Brand new release by Mad Ice

TUNAWEZA KUIMALIZA MALARIA - RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, New York

Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amesema, anaimani kubwa kwamba  ushirikiano  uliopo  baina ya serikali mbalimbali barani Afrika,  mashirika ya kimataifa, makampuni binafsi  na kila mtu katika nafasi yake, hapana shaka ugonjwa wa malaria unaweza  kumalizwa kabisa.

Mhe. Kikwete ameonyesha matumaini hayo   jana( alhamisi) wakati wa hafla  ya kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa jitihada za  kuutokomeza   ugonjwa wa malaria ( Malaria No More) zilizoanzishwa na  Bw. Ray Chambers akishirikiana na  Bw. Peter Chernin.

Katika  hafla hiyo na ambayo  mshereheshaji alikuwa Bw. Wolf Blitzer mtangazaji maarufu wa Televisheni ya Kimataifa  ya CNN kupitia kipindi chake cha situation Room, Rais  mstaafu alitunukiwa tuzo ijulikanayo  kama  White House Summit Awards ikiwa ni kutambua uongozi wake,   kujitoa kwake na  kubwa zaidi kusimamia  uanzishwaji wa muungano wa viongozi wa Afrika dhidi ya Malaria ( ALMA) muungano ambao   hadi sasa una viongozi 49.Wengine waliotunukiwa tuzo hiyo ni  Bw. Ray Chambers na Sumitomo Chemical.

Akijibu swali la nini anadhani kumechangia katika kupunguza idadi  ya  vifo vitokanavyo  na   ugonjwa wa malaria. Rais  mstaafu  amesema, zipo sababu kadhaa, lakini  kubwa ni  utashi wa kisiasa wa kusimamia na kuongoza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Akawaeleza wageni zaidi ya 250 walioalikwa wakiwa ni wawakilishi wa makapuni na mashirika mbalimbali  yanayochongia juhudi za kuukabili ugonjwa wa malaria. Kwamba, Upatikanaji  na usambazani wa dawa sahihi za kutibu ugonjwa wa  malaria,  utengenezaji,  usambazaji na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu na unyunyiziaji wa dawa za kuuwa mazalia ya mbu ni mambo ya msingi ambayo  yamechangia katika  kupunguza  vifi vya watoto chini ya miaka mitano.

“mchanganyiko wa mambo hayo matatu umesaidia sana kupunguza idadi ya  watoto wanaofariki kwa malaria, lakini pia matumizi ya  vyandarua vyenye viatilifu ambapo zaidi ya vyandarua  milioni 24.2 vimesambazwa,  kumechangia wanafunzi kuendelea na masomo yao bila kukatishwa mara kwa mara sababu ya malaria, halikadhalia nguvu kazi imeimarika”. akasisitiza Rais Kikwete na kushangiliwa na  wageni waalikwa.
 Mwanzilishi wa  Malaria no More, Bw Peter Chernin akimkabidhi Mhe. Rais Mstaafu, Kikwete  tuzo ya White House Summit Awards ikiwa ni kutambua na kuthamin mchango na uongozi wake katika jitihada za kuukabili  ugonjwa wa malaria, wengine waliopewa tuzo hiyo ni Bw. Ray Chambers na Kampuni ya  Sumitomo Chemical  ambayo imejenga kiwanda cha vyandarua cha A-Z Arusha Tanzania.
  Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akielezea  juhudi zilizofanywa na  serikali ya Tanzania katika kuukabili ugonjwa wa malaria, ilikuwa wakati wa hafla ya miaka 10 ya Malaria no More iliyofayika jana alhamis New York Marekani, Mhe. Kikwete amealikwa katika hafla hiyo   kutokana na mchango wake mkubwa katika pamoja na  mengin kuwahamasisha viongozi wa Afrika kuongeza juhudi za kisera, kimkakati na bajeti  hali ambayo imechangia sana katika  kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano. pamoja naye ni  Bw. Peter Chernin, Bw. Ray Chambers na mwezeshaji,  Bw. Wolft Blitzer wa CNN.
  Mhe. Rais Mstaafu katika mkutano na Bodi mpya ya Malaria no More muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya miaka 10 ya Malaria No More.
  Sehemu  ya Wageni zaidi ya 250 kutoka masharika na makampuni mbalimbali  ambako ni sehemu ya wadau wa kubwa wanaochangia juhudi za kutokomeza na kudhibiti ugonjwa wa malaria.
Burudani pia ilikuwapo.


AIRTEL YADHAMINI MASHINDANO YA ICT KWA WASICHANA HAPA NCHINI

$
0
0
  Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati) akipiga picha ya pamoja na washindi wa mashindano   ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF ( Universal  Communications Services Access Funds ) na kushirikisha  wasichana 240 hapa nchini, na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu, Airtel  ni mdhamini wa mashindano hayo . Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam
  Mwanafunzi  Elisia Yohana (kulia) wa shule ya sekondari Nyankumbu iliyopo Geita akielezea jinsi program ya kikundi chao jinsi itakavyokuwa inafanyakazi katika mashindano  ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF ( Universal  Communications Services Access Funds ) na kushirikisha  wasichana 240 hapa nchini na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu, Airtel  ni mdhamini wa mashindano hayo. Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam
 Afisa Mtendaji mkuu wa mfuko wa Mawasiliano kwa wote (Universal  Communications Services Access Funds) UCAF, Eng. Peter Ulanga (aliyesimama) akiongea na wanafunzi  katika  mashindano ya  ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF na kudhaminiwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel na kushirikisha  wasichana 240 hapa nchini na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu. Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam
 Mkurugenzi  wa Sayansi na Teknolojia wizara ya elimu, sayansi, teknolojia na ufundi, Prof. Evelyne Mbede (kushoto) akiongea  na wanafunzi wa kidato cha tatu katika mashindano ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF ( Universal  Communications Services Access Funds ) na kushirikisha  wasichana 240 hapa nchini na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu, Airtel  ni mdhamini wa mashindano hayo . Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam
Mkurugenzi wa Elimu ya sekondari, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali- Zanzibar bi Asya Iddi (kushoto) akikabidi cheti kwa Aines Mtani (wa tatu kulia) kama mmoja wa washiriki katika mashindano ya ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF ( Universal  Communications Services Access Funds ) na kushirikisha  wasichana 240 hapa nchini na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu, Airtel  ni mdhamini wa mashindano hayo . Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam

BEI YA MADAFU LEO.

TAMASHA LA SABA LA BIASHARA ZA UBUNIFU LAFANYIKA JIJINI DAR.

$
0
0
Mratibu wa tamasha la Pop Up Bongo, Natasha Stambuli (kulia) akinunua bidhaa za duka la Chasing Faboulous wakati wa tamasha hilo, anaemuuzia ni Groria Mwakasole na wa katikati ni Victoria Martin wamiliki wa duka hilo.
Mmiliki wa duka beauty heaven Tanzania Winfrida Mgongolwa (kulia) akiwaonesha wateja waliotembelea eneop la duka lake katika tanmasha la biashara la Pop Up Bongo lililofanyika Masaki juzi katika mgahawa wa Tuk Tuk Thai.
 Bidhaa kama hizi zilizotengenezwa kwa mbao zilikuwapo pia 

Na Mwandishi Wetu 
MAMIA ya vijana walijitokeza juzi katika tamasha la biashara lililohusisha burudani ya muziki la Pop Up Bongo na kununua bidhaa mbalimbali.


Tamasha hilo la saba kufanyika kwa mwaka huu limefanyikia katika mgahawa wa Tuk Tuk Thai uliopo Masaki na kupambwa na burudani kutoka kwa Dj D Ommy.

Akizungumzia tamasha hilo, mratibu wake, Natasha Stambuli alisema kuwa wabunifu wa ndani wengi wamejitokesha kushiriki tamasha hilo.



Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa na hamasa ya kubuni bidhaa zao wenyewe na kuziuza hasa wakihusisha zaidi nakshi za kiasili katika kupendezesha bidhaa hizo.

Alisema kuwa kutokana na mwamko huo tamasha hilo limewakutanisha wajasiriamali hao pamoja na wanunuzi kwa maana ya wateja ili wawaunge mkono.

Alisema kuwa bidhaa kama vile nguo, viatu vidani na bidha nyingine vimeuzwa katika tamasha hilo.
Alisema “kwa awamu hii ambayo ni ya saba tukiwa bado na mdhamini wetu kinywaji cha Smirnoff watu wengi wamejitokeza na kupata huduma kadhaa ambapo wamekuwa wakinunua bidhaa huku wakipata burudani ya muziki”.

Kwa upande wake Meneja wa vinywaji vikali kutokea, Serengeti Breweries Limited (SBL) Shomari Shija alisema kuwa kampuni hiyo kupitia kinywaji chake cha Smirnoff imeamua kudhamini tamasha hilo kwa kuwa inatambua mchango wa ujasiriamali katika maendeoleo.

Mmoja kati ya wajasiliamali walioshiriki katika tamasha hilo, Sackry Papillon wa huduma ya mwili, The Ryb Spa iliyopo Kijitonyama alisema kuwa tanmasha hilo limemkutanisha na wadau mbalimbali hasa vijana wanaopenda huduma hiyo.

PROFESA MUHONGO ASISITIZA MAPINDUZI YA KIUCHUMI KATIKA SEKTA YA NISHATI NA MADINI.

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhungo akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini na kufungua baraza la wafanyakazi wa wizara yake katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Baraza la wafanyazaki wa wizara ya Nishati na Madini, Selina Msumbushi akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini na kusoma mapendekezo ya wafanyakazi hao leo katika mkutano wa kufungua baraza la wafanyakazi uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa wizara ya Nishati na Madini wakiimba wimbo wa Solidarity leo katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa wizara ya Nishati na Madini wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo wakati wa ufungunzi wa Baraza la wafanyakazi jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Mhe. Sospeter Muhongo amelishauri Baraza la Wafanyakazi wa Nishati na Madini kujikita katika kujadili mwelekeo wa mapinduzi ya kiuchumi kwa kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye viwanda.

Mhe. Muhongo ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, ambapo baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni masuala ya usafiri kwa wafanyakazi wa wizara hiyo, upandishwaji vyeo kwa wafanyakazi, mafunzo pamoja na uhaba wa nafasi wa ofisi kwa wafanyakazi.

Kuhusu suala la upandishwaji vyeo, Mhe. Muhongo amesema kuwa tayari yeye kama Waziri alishafanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ili kuona namna gani wafanyakazi wanapandishwa vyeo kulingana na elimu pamoja uwezo wao kikazi ambapo alipendekeza kubadili mtindo wa upandishwaji vyeo uliopo sasa kwani ni wa zamani.

‘’Sifa za upandishaji vyeo kwa wafanyakzi ni vema ukabadilika pamoja na muda wa utoaji vyeo, hivyo napenda kuwasisitiza kuwaangalia vijana tulio nao kwani pale Wizarani tuna vijana wengi wazuri wenye uwezo mkubwa katika kufanya kazi. Katika kikao hiki ni vema mkajadili namna gani mnawapa kipaumbele vijana katika kuwapandisha vyeo vijana hawa,’’ alisema Muhongo.

Kuhusiana na uhaba wa nafasi za ofisi, Mhe. Muhongo alifafanua kuwa, ofisi nyingi za Serikali ziko katika mfumo wa zamani, hivyo amelishauri Baraza hilo kuona namna gani watabadilisha muundo wa ofisi ili watu wakae pamoja katika eneo moja lililo wazi na kufanya kazi kuliko kila mtu kuwa na sehemu yake ya kufanyia kazi hali inayosababisha ufinyu wa eneo na uvivu.

Aidha, Amewataka wajumbe wa Baraza hilo kujadili ni namna gani wanaweza kubadilisha hali ya kiuchumi toka asilimia 7% hadi kufikia asilimia 8% mpaka 10% ili kukuza uchumi wa nchi na kutokomeza umasikini.

‘’Jukumu kubwa la Wizara ya Nishati na Madini ni kuhakikisha kuwa tunakuza uchumi wa nchi kwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na umeme mwingi wa bei nafuu na wa uhakika, na kazi tuliyonayo hapa ni kuongeza uzalishaji wa umeme toka Megawati 1400 hadi kufikia Megawati 5,000 mpaka 10,000 na ikiwezekana hadi 15,000 baada ya miaka 10 ijayo’’, aliongeza Mhe. Mhongo.

Kuhusu suala la Mafunzo kwa wafanyakazi hao, Mhe. Muhongo amesisitiza kuwa hakuna mtu anayekatazwa kupatiwa mafunzo kwa maana ya kuongeza elimu juu ya jambo fulani, isipokuwa kuna utaratibu wa kwenda kusoma, ambapo panapotokea umuhimu wa wafanyakazi kwenda kusomea mambo muhimu yenye manufaa kwa umma nafasi hizo ni vema zikatolewa ili nchi iwe na wataalam mbalimbali katika nyanja mbalimbali.

‘’Hii Wizara inahitaji watu wasome na waelimike, hivyo tunahitaji watu wasome na wawe wataalam katika maeneo mbalimbali ya kazi lengo likiwa ni kuleta maendeleo ya nchi’’, Alisema Mhe. Muhongo.


Amegusia masuala ya Bajeti katika Wizara yake ambapo amefafanua kuwa zaidi ya asilimia 89.5/% ya bajeti itatumika katika kufanya shughuli za maendeleo ya nchi.

MFUMUKO WA BEI UMEPUNGUA MWEZI MACHI KWA ASILIMIA 5.4.

$
0
0

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kushuka kwa mfumuko wa bei kwa Machi mwaka huu. Kulia ni Meneja wa Ajira na Bei wa NBS, Ruth Minja.
Kulia ni Meneja wa Ajira na Bei wa NBS, Ruth Minja akiwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari na Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MFUMUKO wa Bei kwa Machi 2016 umepungua hadi asilimia 5.4 kutoka asilimia 5.6 ya Februari.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kuwa upandaji wa bei za bidhaa kwa mwaka ulioshia kwa Machi , 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioshia Februari mwaka huu.

Amesema Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 101.93 mwenzi Machi, 2016 kutoka 96.69 mwezi Machi 2015.

Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mweziMachi, 2016 umepungua hadi asilimia 8.5 kutoka 9.5 iliyokuwa kwa Februari, 2016.

Amesema kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Machi, 2016 kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Machi 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Machi 2015.

Kwesigabo amesema mwenendo wa bei za bidhaa zisizo za vyakula zinaonyeshwa kupungua kwa mwezi Machi 2016 ikilinganishwa na mwezi Machi 2015 bidhaa hizo ni Gesi asilimia 10, Diseli 5.8, Mafuta 1.0.


Mfumko wa bei unafanana nchi za Afrika Mashariki , kwa mwezi Machi nchi ya Kenya Mfumuko umepungua hadi asilimia 6.45 kutoka asilimia 6.8 kwa Februari, Uganda mfumuko wa bei umepungua hadi asilimia 6.2 kwa Machi 2016 kutoka asilimia 7.0 kwa Februari 2016.

IDARA YA UHANDISI YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD MWENYEJI MKUTANO WA AE&M ABU DHABI.

$
0
0
IDARA ya Uhandisi ya Shirika la Ndege la Etihad itakuwa mwenyeji na mdhamini wa mkutano ujao wa uhandisi na ukarabati wa ndege wa mtandao wa MRO uliopo Mashariki ya Kati, Mkutano huo unaotazamiwa kufanyika mjini Abu Dhabi mwezi Aprili 26-27, 2016. Mjadala mkuu utakuwa juu ya ukuaji wa mtandao wa  MRO wenye historia isiyopungua miaka 20, wenye wadau katika sekta za – Ndege, MROs, OEMS na Wauzaji – kuwaleta pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya kimasoko.

Mada mbalimbali kama maendeleo katika masoko ya usafiri wa anga huko mashariki ya  Kati, sekta ya utabiri wa masoko ya MRO pamoja na jinsi mashirika ya ndege yanajenga mahusiano na wadau wengine wa MRO.

Miongoni mwa wazungumzaji sekta inayoongoza ni Jeff Wilkinson, Makamu wa Rais shirika la ndege la Etihad kwa upande wa Ufundi alisema: " Ni furaha yetu kuwa mwenyeji wa wajumbe wa uhandisi na ukarabati wa ndege hapa mjini Abu Dhabi – kitovu kipya cha masuala ya teknolojia ya anga na usafiri kanda ya mashariki ya Kati”

Ikiwa ni mwaka mmoja tangu kufanikisha maonyesho mengine kama haya, idara ya uhandisi ya Shirika la ndege la Etihad kwa mara nyingine tena itatoa ziara ya kituo chake kwa wajumbe baada ya kuhitimisha mkutano huo, hivyo kuwapa fursa wajumbe kukutana na timu ya uongozi ya idara ya uhandisi  pamoja na kutoa fursa ya kutembelea karakana  na warsha mbalimbali ndani ya kituo .


"Tumeandaa ziara ya kituo cha kisasa kabisa cha idara ya uhandisi ya shirika la ndege la Etihad, karakana zake  pamoja na warsha zitakazo fanyika katika kituo hicho kikubwa kuliko vyote katika mtandao wa MRO kanda ya mashariki ya kati. Hii ni pamoja na karakana sita (6) zenye uwezo wakuhifadhi hadi ndege kubwa tatu (3)  aina ya A380 kwa wakati mmoja. "

RAIS DKT.MAGUFULI AMEMTEUA GELASIUS GASPAR BYAKANWA KUWA MKUU WA WILAYA YA HAI, MKOANI KILIMANJARO.

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI WASHIRIKI KUTOA MADA KATIKA MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA (ALAT) UNAOFANYIKA DODOMA.

$
0
0
 Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw. Masha Mshomba, (Kushoto), baada ya kuridhishwa na maelezo ya kina kuhusu huduma na kazi zifanywazo na Mfuko huo katika kutoa mafao ya muda mfupi na fidia ya kudumu kwa Wanyakazi wa Sekta Binafsi na Umma watakaopata ajali na kuumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi wazifanyazo mwanzoni mwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa Tanzania (ALAT), ulioanza mjini Dodoma leo Aprili 8, 2016.
 Mkurugenzi Mkuu  wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, WCF,  Bw. Masha Mshomba, (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Juu ya Huduma na Mafao yatakayotolewa na Mfuko hususani fidia ya muda mfupi na fidia ya kudumu kwa Wanyakazi wa Sekta Binafsi na Umma watakaopata ajali na kuumia, kuugua ama kufariki kutoka na kazi. Awali Bw. Mshomba  alipata fursa ya kutoa mada kwa wajumbe wa ALAT, kutoka mikoa mbalimbali kuhusu huduma za Mfuko huo. Katikati ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI), Suleiman Jaffo.

 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba akiwasilisha mada
 Baadhi ya wajumbe wa ALAT na wageni waalikwa
 Baadhi ya wajumbe wa ALAT na wageni waalikwa
Mmoja wa wajumbe akizungumza kwenye mkutano huo.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images