Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live

Mkuu wa Mkoa, Makonda atembelea timu ndani ya EFM redio leo.

$
0
0
 Mkurungenzi wa EFM redio Francis Siza katika picha ya pamoja  na  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo alipotembelea kituo hicho cha Redio cha EFM ziara  hiyo ilikuwa kuangalia utendaji kazi wa redio hiyo pamoja na kujadiliana mambo kadha wa kadha yahusianayo na jamii kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na baadhi ya ya watangazaji wa kipindi cha UHONDO ambao ni Dina Marios, Swebe Santana pamoja  na Sofia Amani.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika kitengo cha mauzo na masoko cha EFM redio akizungumza na maafisa masoko wa kituo hicho. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa chumba cha uzalishaji (Production) cha EFM redio akiwa katika kitengo cha utafiti, mawasiliano na ubunifu.

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM (BARA) AWATAKA WATUMISHI WA CCM KWENDANA NA KASI YA MABADILIKO YA SASA

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akisalimia baadhi ya viongozi wa CCM, baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi hiyo, akiwa katika ziara ya kikazi leo. Anayemsalimia ni Katibu wa CCM wilaya ya Mbarali Abdallah Mpokwa.  Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo Mwangi Kundya
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhwavi akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya leo. Kulia ni Katibu ambaye hajapangiwa kituo, Mariam Yusuf
 Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Mwangi Kundya akimsindikiza Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Rajab Luhwavi kwenda ukumbini kuzungumza na watumishi wa Ofisi ya CCM mkoa huo leo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhwavi akiingia ukumbini kuzungumza na wafanyakazi katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya leo. Kulia kwake ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Mwangi Kundya

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rajabu Luhwavi akiwasili ukumbini
 Katibu wa UVCCM mkoa wa Mbeya Adiya Mamu akihamasisha watumishi wa Chama, kumkaribisha ukumbini Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Rajabu Luhwavi leo
 Watumishi wa CCM Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya wakiwa ukumbini
 Katibu wa CCM, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Lobe Zongo akimkaribisha Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu Bara kuzungumza na wafanyakazi hao wa Chama mkoa wa Mbeya
 Watumishi wa Chama mkoa wa Mbeya wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara alipozungumza nao
 Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Mwangi Kundya akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhwavi kuzungumza na watumishi wa Chama mkoa huo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akizungumza na watumishi wa Chama mkoa wa Mbeya
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akizungumza na watumishi wa Chama mkoa wa Mbeya. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO


Na Bashir Nkoromo, Mbeya

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ( Bara) Rajab Luhwavi, amewataka watumishi wa chama kubadilika kwa vitendo ili kwendana na hali ya mazingira yaliyopo sasa na kuonya kuwa asiyetaka kwendana na mabadiliko hayo ataachwa kupisha wengine waendelee.


Amesema, mabadiliko ndani ya CCM, siyo dhana iliiyoanzishwa wakati wa uchaguzi mkuu, kama vilivyojinadi baadhi ya vyama wakati huo, bali ni dhana ambavyo Chama kiliiazimia kuitekeleza wakati wa mkutano wake mkuu uliopita.



Luhwavi alisema hayo, leo mjini Mbeya wakati wa kikao chake na wafanyakazi wa Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake katika mkoa huo, kikao ambacho pia alikitumia kuwapa fursa watumishi wa kada mbalimbali kuelezea kero au changamoto zote zinazowakabili kama wafanyakazi wa chama.



Luhwavi alisema ni lazima kila mtumishi wa chaa kuwa mstari wa mbele kwa kufayakazi kulingana na wakati uliopo ili ifikapo mwaka 2020 wananchi waikubali CCM kutokana na kile kilichofanyika.



Alisema, watumishi wa CCM, ndiyo nguzo muhimu ya Chama katika kila jambo, akifafanua kwamba watumishi wa Chama ni tofauti na viongozi wa chama kwa kuwa viongozi wao si watendaji bali ni watekelezaji wa yale anayokuwa wameandaliwa na watumishi.



"Ninyi ndio mnaosababisha picha halisi ya Chama ionekane vipi, siyo viongozi, maana ninyi ndio ambao huandaa hata mikutano ya viongozi, na ili mikutano hiyo ionekane imefaa ninyi nndiyo chachu, kwa hiyo watumishi ndiyo nguzo kubwa ya Chama katika ufanisi wake", alisema Luhwavi.



Mapema, Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Alhaji Mwangi Kundya alimpongeza Naibu Katibu Mkuu kwa hatua yake ya kuamua kuzungumza na watumishi wa chama, na kwamba katika utumishi wake ndani ya Chama hiyo ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kuhudhuria kikao ambacho Naibu Katibu Mkuu anazungumza na wafanyakazi.



Kundya alimuomba Naibu Katibu Mkuu kuwapangia vituo vya kazi makatibu watatu, ambao wapo kwenye Ofisi ya CCM ya 



mkoa huo huku wakiwa hawana kazi maalum.



"Mheshimiwa Naibu Katibu Mkuu, tunao Makatibu watatu hapa, lakini hawajapangiwa vituo, sasa tutakuwa tunaendelea kuwalipa huku hakuna kazi wanazofanya, mwisho tutaonekana na sisi ni majipu, maana kazi zilizopo hapa si nyingi kiasi cha kuhitaji makatibu hao wa nyongeza", alisema  Kundya.



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Luhwavi yupo katika ziara ya kukagua uhai wa Chama ndani ya Chama katika mkoa huu wa Mbeya, kabla ya kwenda Njombe.



MABONDIA WANNE WAPIGWA PINI.

$
0
0
MABONDIA WANNE WAPIGWA PINI AKIWEMO THOMAS MASHALI, FRANSIC MIYEYUSHO, NASSIB RAMADHANI NA RAMADHANI SHAULI KUCHEZA NA MABONDIA KUTOKA NJE MEI 14 DAR ES SALAAM.
Bondia THomasi Mashali katikati akisaini mkataba mbele ya katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa PST Anton Ruta kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa wa Dunia na muirani Sajjad Mehrabi utakaofanyika mei 14 katika uwanja wa ndani wa taifa kushoto ni bondia Fransic Miyeyusho.
Bondia Ramadhani Shauli kushoto akisaini mkataba wa kuzipiga Mei 14 na bondia Salim Salim kutoka Malawi katikati ni katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa PST Anton Ruta na kocha wa bondia huyo Cristopher Mzazi.
Bondia Nassibu Ramadhani akisaini mkataba wa kuzipiga na bondia kutoka nje ya nchi mbele ya katibu mkuu wa chama cha gumi za kulipwa PST Anton Ruta kulia na kocha wa bondia huyo Cristopher Mzazi.
Bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' kushoto akisaini mkataba wa kuzipiga na bondia kutoka nje siku ya mei 14 katika uwanja wa ndani wa tasifa kushoto ni kulia ni katibu mkuu wa PST Anton Ruta katikati ni bondia Thomas Mashali .

Picha na SUPER D BOXING NEWS

SERIKALI YAWASILISHA MAPENDEKEZO YA KIWANGO NA UKOMO WA BAJETI KWA MWAKA 2016/17

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza kabla ya Waziri wa Fedha na Mipango hajawasilisha Mapendekezo ya kiwango na ukomo wa Bajeti ya serikali kwa mwaka 2016/2017 wakati wa mkutano wa Wabunge wote uliofanyika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mpiango Dkt Philip Mipango akiwasilisha Mapendekezo ya kiwango na ukomo wa bajeti kwa mwaka 2016/17 wakati wa mkutano wa Wabunge wote uliofanyika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim akiongoza kikao cha Wabunge wote wakati Serikali ilipowasilisha mapendekezo ya kiwango na ukomo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2016/17. Kulia kwake ni Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai na kushoto ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson.(Picha na Ofisi ya Bunge).

EFM REDIO YAJA TENA NA SHINDANO LA SHIKA NDINGA

$
0
0
EFM redio kwa mara nyingine tena inakuja na shindano la shika ndinga, litakalo washindanisha wakazi kutoka (Dar es salaam na Pwani). Likianza na wakazi wa wilaya ya Temeke, wiki hii siku ya jumamosi pale uwanja wa Zakhiem Mbagala kuanzia saa 3:00 Asubuhi hadi saa 10:00 Jioni.
Mwaka huu Efm inalisongesha kwakutoa zawadi ya magari mawili aina ya Suzuki Carry pamoja na Piki Piki aina ya boxer. Endelea kusikiliza Efm redio kila siku.Baadhi ya picha za shikandinga mwaka jana 2015


RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA LIBYA

$
0
0
 Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika (AU) katika mgogoro wa Libya, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete leo amekutana na Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Italy Dk. Mario Giro, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo maalum.


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo, Msaidizi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Suleyman Mwenda alisema, Dk. Kikwete amekuwa na mahusiano ya kirafiki ya muda mrefu na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italy Dk. Mario Giro, Hivyo Naibu Waziri huyo amefanya ziara hiyo ikiwa ni sehemu ya kumjulia hali kama rafiki yake wa muda mrefu.

"Pamoja na kuja kumsalimia kama rafiki wa siku nyingi, lakini lengo hasa la Naibu waziri huyo ni kutaka maelezo juu ya suala la Libya'' alisema Mwenda na kuongeza "Kama mnavyofahamu kuwa Dk. Kikwete ameteuliwa na Jumuiya ya Afrika (AU) kuwa mwakilishi katika kutafuta suluhu ya mgogoro wa Libya.

Alisema, Italy inalipa umuhimu wa kipekee suala la Libya kutokana na kwamba ni nchi jirani hivyo inayo maslahi mapana na ya karibu juu ya suala la amani ya Libya, Dk. Giro ameiwakilisha nchi yake katika kujua hatua ya usuluhishi na hatma ya mgogoro wa Libya.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri huyo aliambatana na Balozi wa Italy hapa nchini, Luigi Scotto pamoja na Dk. Raffaele De Lutio,Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa wa Italy


RAIS DKT MAGUFULI PAMOJA NA RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME WAZINDUA RASMI DARAJA LA KIMATAIFA LA RUSUMO NA KITUO CHA HUDUMA

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakifurahia mara baada ya kuzindua rasmi daraja hilo la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa daraja la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.

Ujenzi wa Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma Pamoja Mpakani Rusumo ni moja ya miradi inayotekelezwa kwa msaada kutoka Serikali ya Japan kwa Nchi za Tanzania na Rwanda kupitia shirika lake la maendeleo la JICA. Mradi huu kwa upande wa Tanzania umegharimu takribani kiasi cha TShs. 33,206,508,072.07 hadi kukamilika. Miradi mingine inayotekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia JICA ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Arusha – Namanga, Iringa – Dodoma, Namtumbo – Kilimasera – Matemanga – Tunduru pamoja na barabara ya Masasi - Mangaka. 

 Muonekano wa sehemu ya Daraja hilo la Rusumo
 Jiwe la msingi lililowekwa baada ya uzinduzi wa  daraja hilo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakipita kwenye Daraja hilo la Rusumo mara baada ya uzinduzi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.

 Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa huo 

MWENYEKITI WA CCM, RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI VYA CCM,

$
0
0
Kaimu Mhariri Mtendaji wa Uhuru ublications Limited, Wachapishaji wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Ramadhani Mkoma, akimweleza jambo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaa Kikwete alipotembelea Ofisi za Kampuni hiyo, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Uhuru Publicatiions Ltd alipotebelea kampuni hiyo leo. Pamoja naye ni Msemaji wa CCM, Cliristopher Ole Sendeka na Mwenyekiti wa Bodi ya Uhuru Media, Adam Kimbisa.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni alipoingia katika Ofisi za Uhuru FM leo. Wengini ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka, Adam Kimbisa na Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali
Baadhi ya wayanyakazi wa UHURU FM wakiwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipoingia studio wa Uhru FM.KWA PICHA KIBAO ZA UPL NA UHURU FM>BOFYA HAPA

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI ZA RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME NA RAIS WA TANZANIA DKT JOHN POMBE MAGUFULI ALIPOKARIBISHWA KIGALI NCHINI RWANDA

TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WALIMU KUSHONEWA SARE INAYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

$
0
0
         JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 
 
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI


TAARIFA KWA UMMA


YAH: TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WALIMU KUSHONEWA SARE INAYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII


Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari “NDALICHAKO NA WALIMU TZ”.

Taarifa hiyo inadai kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare watakazo vaa wakati wa kazi. 

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa Taarifa hizi si za kweli. Aidha, Wizara inawataka watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza. Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu.

IMETOLEWA NA


KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

07/04/2016




TAARIFA YA MAZISHI YA MAREHEMU BARAKA KOMBE

$
0
0
Asalaam - Salaam - Aleykum. Kwa niaba ya familia ya marehemu Tunapenda kuwajulisha kuwa mazishi ya Ndugu yetu  Marehemu Baraka Kombe pichani hapo juu  yatakuwa siku ya Jumamosi tarehe 9/4/2016.

Maiti itasaliwa Masjid Alnoor Cultural & Education Trust 
170 Gascoigne Rd, Barking, Essex IG11 7LH
Baada ya Salah Zuhur 12:30

Msikitini kutakuwa mchanganyiko wanawake na wanaume.

Makaburini: Wanaume tu

Baadae kumsalia maiti tunaelekea makaburini ya Woodgrange Park Cemetery 
(Near Woodgrange Park Station, Close to Manor Park Station)
540 Romford Road, 
Manor Park 
London
E7 8AF

Bus Route: 25 to Ilford

TUNAOMBA KANA INAWEZEKANA ALIYEGUSWA NA MSIBA HUU ATOE MCHANGO WAKE KWA: 

MS SARA A TEMU ( Mke wa Marehemu)
SANTNDER
ACCOUNT NUMBER 46132094
SORT CODE 09 01 28

KWA TAARIFA ZAIDI NAOMBA MUWASILIANE NA :
JESTINA GEORGE   +447557304940
MARIAM MBILINYI   +447913978572
SARA. A. TEMU        +447769711918
EMELIA MAKYAO     +447983901141

Tunatanguliza Shukrani kwanza Mwenyezi Mungu awabariki kwa Misaada yenu ya hali na mali.

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un

Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria "Super Eagles", Nwankwo Kanu awasili Dar es salaam kwa ziara ya siku tano

$
0
0
 
 Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria "Super Eagles", Nwankwo Kanu akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo kwa mwaliko wa siku tano wa Kampuni ya Vizimbuzi ya StarTimes.
 Hapa Kanu akihojiwa na wanahabari. Kushoto na kulia ni Mabaunsa waliokuwa wakimlinda baada ya kufika Uwanja wa Ndege kabla ya kuelekea Hoteli ya Serena.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Be Lanfang Liao (kulia), akimuelekeza jambo mchezaji huyo wakati wakielekea kupanda gari kuelekea Hoteli ya Serena. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa StarTimes Tanzania,  William Masy.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


KAMPUNI YA MAFUTA YA TOTAL YAWAKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA SHINDANO LA "START UPPER OF THE YEAR BY TOTAL CHALLENGE"

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya TOTAL Tanzania, Tarik Moufaddal akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la wajasialiamali hapa nchini ambapo washindi watatu bora wajasiliamali walikabidhiwa zawadi zao na kampuni ya TOTAL katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Mradi wa Kampuni ya Mafuta ya TOTAL, Marsha Msuya akiwakaribisa wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la wajasialiamali la Kampuni ya TOTAL katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa shindano la Kijasiliamali ya Kampuni ya TOTAL Tanzania wakiwa kwenye hafla hiyo kabla ya kukabidhiwa zawadi zao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki(Kutoka kushoto wa pili) akiwa na viongozi wa Kampuni ya TOTAL Tanzania katika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya TOTAL hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Honorary Patron of the 2016 edition of Start uper Challenge ,Erric Mutta akizungumza katik hafla ya kuwakabidhi zawadi za washindi wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mwanamziki wa Bongo Freva, Elias Barnabas (Barnaba) akitumbuiza katika katik hafla ya kuwakabidhi zawadi za washindi wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa tatu wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya TOTAL, Krantz Mwantepele ambaye ameshinda shilingi milioni kumi na tano(15,000,000katika shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa pili wa shindano la wajasiliama, Mercy Kitomari akifafanua bidhaa ya Ice cream ya ladha za matunda mbalimbali ya hapahapa nchini ambapo shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL  Na ni Mshindi wa shilingi milioni ishirini(20,000,000)akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Kwanza, Iddi Kalembo ambaye ni mshindi wa shilingi milioni thelathini na tano(35,000,000)akifafanua huduma anayoitoa ambayo yeye anafanya biashara ya kupiga picha na kuzisafisha kwa wakati huohuo katika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi na tano Mshindi wa tatu wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya TOTAL, Krantz Mwantepele (wa pili kutoka kulia) katika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni ishirini Mshindi wa pili wa shindano la wajasiliama, Mercy Kitomari (wa pili kutoka kulia)katika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni thelathini na tano Mshindi wa Kwanza, Iddi Kalembowa pili kutoka kuliakatika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya TOTAL Tanzania na washindi wa shindano la wajasiliamali mara baada ya wajasiliamali hao kukabidhiwa zawadi zao katika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

MKUU WA WILAYA YA BABATI AIFUNGA SHULE KUFUATIA KUHARIBIKA KWA VYOO.

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela
Na Woinde Shizza,Manyara

Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela ameifunga shule ya msingi Matufa kwa muda usiojulikana baada ya kutitia kwa matundu ya vyoo vya wanafunzi na walimu kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazonyesha.

Akizungumza baada ya kuitembelea shule hiyo, Meela alisema kutokana na matundu  24 ya vyoo vya shule hiyo kuharibika inabidi shule hiyo ifungwe kwani hakuna vyoo vingine vya kutumiwa kwa wanafunzi na walimu. Hata hivyo, kaya 64 zilizokuwa zinaishi kwenye shule hiyo ya Matufa kwa kukosa makazi baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha siku mbili hivi sasa wamepatiwa hifadhi kwa kuwekwa kambini.

Alisema kutokana na maafa hayo hana budi kuifunga shule hiyo kwa muda usiojulikana na anatarajia watahakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi kwa muda mfupi kupitia ushirikiano wa viongozi wa wilaya na mkoa huo. “Namuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati vijijini Dominick Kweka, kuhakikisha shule hiyo inajengewa vyoo mara baada ya wiki moja kupita ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao,” alisema Meela.

Kwa upande wake, mbunge wa jimbo la Babati vijijini Vrajlal Jitu Soni aliwapa pole wakazi wa vijiji vya Magugu na Matufa vilivyopo kwenye tarafa ya Mbugwe ambao wameathirika kutokana na mafuriko hayo. Jitu Soni alisema hivi sasa wanafanya tathmini ya mafuriko hayo ili kamati ya maafa kupitia ofisi ya Waziri Mkuu waweze kuwapatia msaada wananchi hao ambao nyumba na mazao yao yamechukuliwa na mafuriko hayo.

TPDC yachangia madawati 500 Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

$
0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara imepokea jumla ya madawati  500 kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Akiongea wakati wa kupokea madawati hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego alisema msaada huu unamaliza kabisa tatizo la madawati kwa kata zote za kijiji cha Madimba na Msimbati. Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alisema kwamba TPDC itaendelea kutoa misaada katika maeneo ambayo inafanya shughuli zake lengo likiwa ni kuboresha maisha wa wananchi wa maeneo hayo na kufaidika na shughuli za utafiti na uendelezaji wa gesi na mafuta.  
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio akikabidhi rasmi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego na Mbunge wa Mtwara Vijijini. Mhe. Hawa Ghasia wakifurahia kwa pamoja baada ya TPDC kukabidhi madawati kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Madimba wakiwa wamekaa katika madawati waliyopokea kutoka TPDC.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio akionesha moja ya jezi ambayo TPDC ilitoa msaada kwa timu ya Wazawa FC iliyopo kijiji cha Mngoji, na Tagesh Academy zote za Mtwara.

 Wachezaji wa timu ya Wazawa FC wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, Mbunge wa Mtwara Vijijini. Mhe. Hawa Ghasia, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi. Fatma Ally  na viongozi wengine baada ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Tshs. 5,000,000/=

UMOJA WA ULAYA(EU) WAZINDUA PROGRAMU WA KUZISAIDIA ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI HAPA NCHINI.

$
0
0
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer kizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa programu ya kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali iliyofanyika jana. Picha na Geofrey Adroph
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya(EU) kutoka Brussels, Bi Rosario Bento Pais akizungumzia masuala ya kuzisaidia asasi zisizo za kiserikali ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa maana hizo zinawalenga watu katika jamii husika.
Mwakilishi wa asasi za kiraia, Bw. Francis Kiwanga akizungumza juu ya ushirikiano wa Umoja wa Ulaya(EU) ulivyoamua kuzisaidia asasi zisizo za kiserikali za Tanzania Bara pamoja na Zanzibar. Maeneo ambayo Umoja wa Ulaya inajikita nayo katika asasi zisizo za kiserikari ni tatu amabazo ni kuweka mazingira bora kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kufanya kazi katika mazingira bora hapa nchini, pili ni kuyajengea uwezo mashirika hayo na mwisho nikufanya kazi katika Sere pamoja na sheria ili kuwa na sheria bora na nzuri kwa maendelea ya nchi yetu.
Baadhi ya mabalozi kutoka Umoja wa Ulaya(EU) pamoja na wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa programu ya kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali iliyofanyika jana
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya(EU) kutoka Brussels, Bi Rosario Bento Pais(kulia) akisaini kuashiria uzinduzi rasmi wa programu ya kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali kushoto ni Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Bw. Roeland Van De Geer.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Bw. Roeland Van De Geer(kushoto) pamoja na Mwakilishi wa asasi za kiraia, Bw. Francis Kiwanga wakisaini kuashiria uzinduzi rasmi wa programu ya kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali za Tanzania Bara na Zanzibar. Katikati ni Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya(EU) kutoka Brussels, Bi Rosario Bento Pais
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya(EU) kutoka Brussels, Bi Rosario Bento Pais(kushoto), Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Bw. Roeland Van De Geer(katikati) pamoja na Mwakilishi wa asasi za kiraia, Bw. Francis Kiwanga wakizindua rasmi programu ya kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali za Tanzania Bara na Zanzibar.

Picha ya Pamoja.

Kamati ya PIC Yaitaka Serikali Kuisaidia TTCL Ijiendeshe Kibiashara.

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini (TTCL) leo jijini Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini (TTCL) leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (hayupo pichani) katika mkutano na wanahabari leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (hayupo pichani) katika mkutano na wanahabari leo jijini Dar es Salaam.Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akipitia nakala ya taarifa ya Kampuni ya Simu nchini (TTCL) jujiridhisha na takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akipitia nakala ya taarifa ya Kampuni ya Simu nchini (TTCL) jujiridhisha na takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.

KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imeitaka Serikali kutekeleza kwa vitendo ahadi zake za kuiwezesha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kujiendesha kibiashara. Akitoa maazimio ya Kamati ya PIC leo Dar es Salaam baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini TTCL, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya PIC, Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) alisema, ili TTCL iweze kutekeleza jukumu lake kwa Taifa, Serikali iharakishe utekelezaji wa ahadi zake kwa Kampuni hiyo Kongwe ya Mawasiliano nchini. "Serikali ikamilishe kwa haraka mchakato wa kuondoka kwa Kampuni ya Bharti Airtel ndani ya TTCL, mchakato huu umechukua muda mrefu sana, ni vyema sasa ukatekelezwa sambamba na kuisaidia TTCL kupata malipo yake inayodai kutoka kwa Wateja wake zikiwemo taasisi za Serikali," alisema Bi. Bukwimba.

 Aidha Mhe Bukwimba aliongeza kuwa, Kamati ya PIC inaiagiza Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuharakisha mchakato wa kukabidhi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa TTCL ili utumike kibiashara na kwa ufanisi zaidi kuliko hivi sasa ambapo umiliki wake haupo bayana.Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini (TTCL) leo jijini Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini (TTCL) leo jijini Dar es Salaam.[/caption] Alisema kwa kipindi cha miaka 15 hivi sasa Serikali haijafanya uwekezaji wa aina yoyote ndani ya TTCL hivyo kuitaka kuwekeza ili kampuni iweze kusonga mbele kibiashara. "...Kwasababu huwezi kutegemea kupata mapato mazuri bila kuwekeza uwekezaji wa aina yoyote...miaka kumi na tano ni mingi mi nauhakika wakiwekeza fedha wataweza kuisaidia kampuni kuiuwisha na kuweza kufanya shughuli zake vizuri kama taasisi zingine.

." Agizo jingine la PIC kwa Serikali ni kuiongezea TTCL wigo wa kutumia rasilimali zake kama dhamana ili kupata mitaji kutoka taasisi za fedha na kufanikisha mpango wa kampuni hiyo wa kufanya mageuzi ya kibiashara. Awali, Wabunge waliochangia hoja katika kikao hicho, waliitaka Bodi na Menejimenti ya TTCL kusimamia kikamilifu mipango mizuri ya kibiashara iliyowasilishwa mbele ya Kamati. Wabunge Esther Matiko (Tarime Mjini), Steven Ngonyani (Korogwe) Riziki Lulida (Viti Maalum), Sabrina Sungura (Viti Maalum), na Frank Mwakajoka (Tunduma) wamesema, Seriki inao wajibu mkubwa wa kuisaidia TTCL ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa ikipitia kipindi kigumu hasa kutokana na uwekezaji usio na tija uliofanywa ndani ya Kampuni hiyo.

MIUNDOMBINU YA KULETA MAJI JIJINI DAR ES SALAAM YAENDELEA KUJENGWA.

$
0
0
 Msimamizi wa ujenzi wa Mradi wa bomba jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 40 ambalo liko katika hatua  za mwisho  za ujenzi kutoka DAWASA Mhandisi Christian Gava akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiufundi kuhusu mradi huo. Kushoto ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Jamii wa DAWASA Neli Msuya.
 Wataalam wa ujenzi kutoka DAWASA na kampuni ya Megha Engineering & International Ltd inayojenga bomba jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es salaam India wakiangalia moja ya matoleo 12 yanayopita chini ya barabara kuu ya Morogoro eneo la kimara.
 Moja ya daraja linapopitisha bomba hilo kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 40 linavyoonekana mara baada ya kukamilika eneo la Kibamba. 
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.

Na.Aron Msigwa - MAELEZO.
MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam ( DAWASA) imesema kuwa wakazi zaidi wa jiji la Dar es salaam na Kibaha mkoani Pwani wanatarajia  kunufaika na huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama ifikapo Juni mwaka huu kufuatia mradi wa ujenzi wa bomba jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi, Kibaha hadi jijini Dar es salaam kuwa katika hatua  za mwisho za ujenzi.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Jamii wa DAWASA Neli Msuya ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea eneo Kimara na Kibamba ambako mafundi wa Kampuni inayojenga mradi huo ya Megha Engineering & International Ltd kutoka India wanaendelea na kazi ya ujenzi wa madaraja na matoleo ambayo bomba hilo linapitia katika barabara ya Morogoro.

Amesema hadi kukamilika kwake mradi huo utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani milioni 59.3 na utawezesha kiasi cha Lita milioni 196 za maji kusafirishwa kwa siku ambazo zitaongezwa kwenye lita milioni 270 zinazozalishwa kwa siku na Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini ulioko Bagamoyo mkoani Pwani.

Ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaondoa kabisa tatizo la uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ambayo yameunganishwa na mtandao wa mabomba ya DAWASCO ambayo yalikua hayapati maji kwa muda mrefu au kupata kwa mgawo kufikia mwezi Juni, 2016. 

Bi. Neli amesema kuwa ili kuhakikisha mradi huo unakamilika katika kipindi kilichopangwa na kuanza kuwanufaisha wananchi, ujenzi wake unakwenda sambamba na umaliziaji wa tenki jipya la kuhifadhia maji lililoko eneo la Kibamba lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 10 ambalo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 98.

 Aidha, amesema kuwa kazi ya ukarabati wa matenki ya zamani yaliyoko eneo la Kimara jijini Dar es salaam inaendelea sambamba na ubadilishaji wa mifumo ya mabomba ya zamani ambayo sasa ni chakavu ili iweze kuhimili wingi wa maji uliopo.

" DAWASA tumeshaingia mkataba na Mkandarasi kwa ajili kulaza upya mabomba ya maji kwa wananchi wasiounganishwa na maji ili waweze kuingia kwenye mtandao wa mabomba yetu, kazi hii inaendelea katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kimara, Mlandizi,Kibaha, Kwembe, Segerea, Changanyikeni, Mbezi na Makuburi" Amesema.

Bi. Neli ameongeza kuwa baadhi ya maeneo yataanza kupata mabadiliko ya huduma ya maji kuanzia mwezi Mei kufuatia maji yatakayosukumwa kutoka Ruvu, Mlandizi kuanza kutoka katika kituo cha kwanza kwenye tenki la maji la Kibamba.

“Tunatarajia wananchi waliounganishwa na mtandao wataanza kuona mabadiliko kuanzia mwezi Mei, japo sasa kuna maeneo yana mgawo wa Dawasco,lakini baada ya maji haya kufika na kuanza kutoka kwenye kituo cha tenki la Kibamba wananchi watakua na maji ya kutosha" Amesisitiza.

Kwa upande wake Msimamizi wa ujenzi wa Mradi huo kutoka DAWASA Mhandisi Christian Gava akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiufundi kuhusu mradi huo amesema kuwa ili kukamilisha ujenzi wa mradi huo imewalazimu kujenga maungio 15 ambayo bomba hilo linavuka mito na matoleo 12 yanayopita chini ya barabara kuu ya Morogoro.

Amesema kazi ya wekaji wa miundombinu ya kulifanya bomba lipite juu ya mto kupitia madaraja yaliyojengwa imefanyika kwa umakini mkubwa ili kuepuka kuathiri uasili wa mito husika.

Aidha, amesema kuwa ili kulinda bomba hilo na athari za mafuriko katika mito hiyo ulifanyika utafiti maalum ukihusisha upimaji wa kimaabara wa udongo ili kubaini namna udongo huo unavyoweza kubeba nguzo kubwa zilizoshika bomba hilo.

Mhandisi Gava ameongeza kuwa ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 10 umekamilikia kwa 98 na kubainisha kuwa kilichobakia ni umaliziaji wa kazi ndogondogo.

“Ujenzi wa Tenki umekamilika, hatua inayofuata ni kukamilisha kazi ndogondogo kisha kulijaza maji kama sehemu ya uangalizi na taratibu za kiufundi, Tunatarajia wiki ijayo tutajaza maji" Amesisitiza Mhandisi Gava.

KITWANGA ATAKA MADAKTARI, WAUGUZI WANAOJIHUSISHA NA RUSHWA WACHUKULIWE HATUA KALI JIMBONI KWAKE.

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (aliyevaa koti) akicheza ngoma ya asili na wananchi wa Kata ya Sumbugu wilayani Misungwi mara baada ya kuwasili katika eneo hilo kwa ajili ya kufungua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi hao. Waziri Kitwanga amemaliza ziara jimboni kwake leo na kuwaonya madaktari na wauguzi wilayani humo kuacha tabia ya kuwaomba rushwa wananchi. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Sumbugu wilayani Misungwi. Katika hotuba yake, Kitwanga aliwataka wananchi wa jimbo lake washirikiane ili kuliletea maendeleo jimbo hilo na kuwaonya madaktari na wauguzi wilayani humo kuacha tabia ya kuwaomba rushwa wananchi. Kitwanga amemaliza ziara jimboni kwake leo.  
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (katikati meza kuu) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihelele wilayani Misungwi. Katika hotuba yake, Kitwanga aliwataka wananchi wa jimbo lake washirikiane ili kuliletea maendeleo jimbo hilo na aliwaonya madaktari na wauguzi wilayani humo kuacha tabia ya kuwaomba rushwa wananchi. Kitwanga amemaliza ziara jimboni kwake leo.  Picha zote na Felix Mwagara.
Picha na Felix Mwagara.

Na Felix Mwagara, Misungwi
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga amemtaka Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Misungwi kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwafukuza kazi wauguzi na madaktari watakaokuwa wanawaomba rushwa wananchi jimboni kwake.

Kitwanga alisema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wananchi kwa muda mrefu kuwa rushwa imekithiri katika hospitali ya Wilaya jimboni humo na kuwakatisha tamaa wananchi wanaoenda kupata huduma hospitalini hapo.

Akizungumza huku akishangiliwa na mamia ya wananchi wa mjini Misungwi, Kitwanga alisema hali sasa imekuwa tete hivyo lazima tuchukue hatua kali kwa wale watumishi wachache ambao hawafuati sheria na kuweka mbele rushwa kwa wananchi.

“Ndugu wananchi madaktari na wauguzi ni watu muhimu sana katika jamii kwani wanatupa huduma nzuri kabisa, ila wataalamu hawa wanachafuliwa majina yao kwa watumishi wachache mno, sasa tunataka kuwaondoa wale wachache ili tubaki na wengi ambao wanaipenda kazi yao, nawaonya wale wachache wenye tabia hiyo waiache haraka iwezekanavyo,” alisema Kitwanga.

Alifafanua kuwa ni kosa kwa daktari au muuguzi kumuomba rushwa mgonjwa au ndugu wa mgonjwa, kufanya hivyo ni hatari ni sawa na kuua, hivyo lazima sheria ifuate mkondo wake ili kulimaliza tatizo hilo sugu ndani ya Hospitali ya Wilaya pamoja na Misungwi kiujumla.

“Ndugu wananchi msiwe na wasiwasi kabisa, nina aapa sitalivumilia tatizo hilo, na Mkurugenzi yupo hapa analisikia hili, hivyo lazima alifanyie kazi kwa kuwasimamisha kazi wauguzi au madaktari watakaotuhumiwa kuomba au kupokea rushwa,“ a;lisema Kitwanga huku akishangiliwa na wananchi jimboni humo.   

Wakati huohuo, Kitwanga aliwataka wananchi hao kuanzisha vikundi ili waweze kupewa mikopo kupitia fedha alizoziahidi Rais John Magufuli kuwa atatoa kwa kila kijiji shilingi milioni hamsini.
“Fedha zipo jirani kuja, hivyo anzisheni vikundi ili muweze kukopeshwa fedha hizo na muweze kufanya mambo ya maendeleo, fedha hizo ni kwa ajili ya mikopo hivyo tumieni fursa hiyo kwa kuanzisha vikundi vyenu ili muweze kuzipata fedha hizo kwa uharaka zaidi,” alisema Kitwanga.


Hata hivyo, Waziri Kitwanga aliwahakikishia wananchi wa jimbo hilo wawe watulivu na wasubiri maendeleo, na pia waendelea kuchangia maendeleo ya jimbo lao ikiwemo uchangiaji wa madawati katika shule zao. Kuhusu barabara Kitwanga alisema barabara zote ambazo hazipitiki zitatengenezwa hivi karibuni na tatizo la maji litakuwa historia kwani mipango ya upatikanaji wa maji hayo ilishakamilika.

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI SHUGHULI ZA KUMBUKUMBU YA MAUAJI YA KIMBARI (KWIBUKA) KIGALI NCHINI RWANDA.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisali mbele ya makaburi ya watu waliouwawa katika Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994. Kulia ni Rais wa Rwanda Paul Kagame pamoja na Mkewe Janeth Kagame na mtoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisali mbele ya makaburi ya watu waliouwawa katika Mauaji ya Kimbari nchini Rwanda mwaka 1994. Kulia ni Rais wa Rwanda Paul Kagame pamoja na Mkewe Janeth Kagame na mtoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakiwasha mwenge wa matumaini kuashiria kutotokea tena kwa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, mama Janeth Magufuli, Mama Janeth Kagame wakisikiliza historia ya jinsi mauaji ya kimbari yalivyotokea katika eneo la kumbukumbu ya mauji hayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, mama Janeth Magufuli, Mama Janeth Kagame waiwa wamesimama kutoa heshima kwa watu waliofariki katika mauaji hayo ya kimbari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiangalia kwa uchungu mafuvu ya watu waliopoteza maisha katika mauaji hayo ya kimbari.
Wageni mbalimbali waliofika kwenye kumbukumbu hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia picha za watoto waliouwawa kinyama katika eneo la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbaria Gishozi Kigali nchini Rwaanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu katika Jengo la makumbusho ya mauaji ya Kimbari Gishozi Kigali nchini Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea kitabu chenye maelezo mbalimbali kuhusu mauaji hayo ya kimbari.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akimpokea Rais Magufuli katika viwanja vya Gishozi kabla ya kwenda kuweka mashada ya maua kwenye makaburi ya watu waliouwawa katika mauaji ya Kimbari.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na Rais Magufuli pamoja na Mama Janeth Magufuli, Janeth Kagame wakielekea kwenye makaburi ya halaiki katika makumbusho ya mauaji ya Kimbari, Gishozi Kigali nchini Rwanda.
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live




Latest Images