Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU WATAKIWA KUWA WABUNIFU KATIKA SEHEMU ZAO ZA KAZI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akitoa ufafanuzi wa masuala ya wafanyakazi wa Ofisi hiyo wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 9, 20 katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hoja za Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani)) wakati wa mkutano wa baraza hilo tarehe 9 Aprili, 2016 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamis Mwinyimvua akizungumza wakati wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aprili 9, 2016 Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi hiyo mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo Aprili 9, 2016.(Picha Zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wametakiwa kuwa wabunifu katika sehemu zao za kazi ili kuongeza ufanisi katika majukumu yao ya kila siku.

Akitoa wito huo wakati akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge, Ajira,Kazi na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema watumishi wanatakiwa kutumia rasilimali walizonazo kuonesha ubunifu wao katika idara na vitengo walivyopo ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.

“Ofisi ya Waziri Mkuu ni mratibu na msimamizi wa shughuli za kila siku za Serikali hivyo basi naomba tuwe wabunifu katika sehemu zetu za kazi ili tumsaidie Mhe. Waziri Mkuu kutelekeza majukumu haya kwa kasi na ufanisi unaotakiwa.” Alisema Mhe. Jenista.

Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa wakuu wa Idara na Vitengo kushirikiana na watumishi katika ofisi zao ili kuongeza ufanisi wa kazi za kila siku katika idara na Vitengo mbalimbali.

Akizungumza mara baada ya kikao Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu Dkt Hamis Mwinyimvua amesema kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi ni fursa muhimu kwa wafanyakazi kukutana na kujadili masuala mbalimbali ili kupata mbinu za kupambana na changamoto zinazokabili Idara na vitengo mbalimbali.

Kwa mujibu wa Waraka wa Rais Namba 1 wa Mwaka 1970, moja ya madhumuni ya kuanzishwa kwa Mabaraza ya Wafanyakazi ni kuongeza ufanisi na tija katika sehemu za kazi na kupitia Mabaraza haya, wafanyakazi pamoja na waajiri hupata fursa ya kubadilishana mawazo na kubuni mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto katika sehemu zao za kazi.

KIPINDUPINDU HAKIENEZWI KWA KUROGWA-WAZIRI UMMY MWALIMU

$
0
0
Na.catherine Sungura,Kyela 

Wananchi wa wilaya ya kyela wametakiwa kuachana na mila potofu na kupelekea kufanya mauaji ya watu kwa kuhusisha ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa unaoletwa kwa imani ya kishirikina

Hayo yamesemwa leo na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu,wakati alipofanya ziara katika wilaya hii na kuongea na watendaji wa halmashauri.

Mh.Ummy alisema ameshangazwa na baadhi ya wananchi katika kijiji cha unyakyusa kujichukulia sheria mkononi na kuwauwa wanawake watatu kwa madai ndio wanaoneza ugonjwa huo.

Naye mkuu wa wilaya ya kyela dkt. Thea Ntara alisema kamati yake ya ulinzi na usalama imeshawakamata watuhumiwa wawili wa tukio hilo na kuwafikisha mahakamani ingawa bado mtuhumiwa mmoja aliyekimbilia nchi jirani ya malawi anatafutwa.

Matukio hayo yametokea mwezi februari na machi mwaka huu.
Wilaya ya kyela ilipokea mgonjwa wa kipindupindu novemba 2015 na hadi kufikia machi 2016 jumla ya wagonjwa 405 waliugua ambapo vifo vilikua 8. Kwa sasa wilaya hii haina mgonjwa wa kipindupindu

Hali ya kipindupindu nchini imekua ni tatizo kubwa nchini,takribani mikoa yote tanzania bara imekubwa na ugonjwa huu tangu ulipotiwe mwezi agosti mwaka jana,isipokuwa kwa mkoa wa Ruvuma na Njombe ambapo hawajaripoti mgonjwa wowote hadi Sasa

Ripoti ya wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto ya tarehe 4 machi mwaka huu inaonesha jumla ya wagonjwa 20,294 wametolewa taarifa na kati ya hao 320 wamepoteza maisha.Kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka,mwenendo wa kipindupindu unaashiria idadi ya wagonjwa nchini inaongezeka

MTANANGE WA YANGA AFRICANS DHIDI YA AL AHLY YA MISRI UWANJA WA TAIFA

WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA KAKA YAKE

$
0
0
 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  akiweka udongo kwenye kaburi la kaka yake, Selemani Selemani katika mazishi yaliyofanyika  kwenye kijiji cha Narungombe wilayani Ruangwa Aprili 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LA ZANZIBAR HILI HAPA

$
0
0
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.

EFM RADIO WAITIKISA TEMEKE NA SHINDANO LAO LA SHIKA NDINGA,WATANGAZAJI GERALD HANDO,PAUL JAMES NA ABEL ONESHO WAWA KIVUTIO

$
0
0
Kituo cha EFM redio kwa mara nyingine tena kimeibuka na shindano lake la shika ndinga kwa mashabiki wake wa jiji la Dar na Pwani. Pamoja na kufanyika kwa shindano hilo lililozua msisimko mkubwa miongoni mwa wilaya ya Temeke,EFM Radiao pia waliwatangaza watangazaji wao Wapya watatu waliokuwa Clouds FM,Watangazaji hao ni Abel Onesmo,Paul James na Gerald Hando.Shindano hilo Kwa mwaka huu ,limezinduliwa rasmi jana April 9/2016 kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke  jijini Dar.

Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Sebo alisema kuwa shindano hilo litaendelea pia kwa wilaya ya Ilala, Kinondoni, Bagamoyo, na Kibaha na hatimae kilele chake kufanyika katika uwanja wa Sinza TP.


Sebo alisema kuwa Shindano hilo litaanza na washiriki 60 kwenye kila wilaya na washiriki 10 kati yao wanawake watano na wanaume watano ambao wataingia kwenye fainali ya kujinyakulia gari ambao wamepata nafasi ya kushiriki kwa njia ya kupiga simu na kujibu kiufasaha swali husika ili kupata nafasi ya kushiriki shindano la shika ndinga.
Alisema kuwa shindano hilo mwaka huu limeboreshwa zaidi kwa kutoa zawadi za pikipiki kwenye ngazi ya wilaya na magari kwenye ngazi ya fainali.Lengo ni kuwawezesha wasikilizaji wake kwa namna moja ama nyingine katika kuongeza na kukuza kipato kitakacho changia kuimarisha maisha yao kupitia zawadi watakazoibuka nazo.
Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, DenisSebo akiwatambulisha watangazaji wapya wa kituo cha redio cha Efm,Abel Onesmo,Paul James na Gerald Hando kwa wananchi jana katika shindano la shika ndinga kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam.
Watangazani wapya Paul James na Gerald Hando na ,Abel Onesmo akielekea jukwaani kutangazwa rasmi kwa wakazi wa Temeke,jijini Dar.
Watu wa huduma ya kwanza wakiwahudumia washiriki wa Shindano hilo waliokuwa wamezimia kutokana na mshtuko alioupata kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam.
Mshindi wa shindano la shika ndinga alieshinda pikipiki Salehe Maga akizungumza na waandi wa habari (hawapo picha) juu ya kuushukuru uongozi wa Efm kwa kuanzaisha shindano hilo.
Mshindi wa shindano la shika ndinga alieshinda pikipiki Philipina Mshanga akizungumza na waandi wa habari (hawapo picha) juu ya kuushukuru uongozi wa Efm kwa kuanzaisha shindano hilo , na kuwaomba wakina wanawake wajitokeze kwa wingi kwenye mashindano hayo.
Ndinga na pikipiki zikiwa juu ya jukwaa kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam.
 

DIAMOND PLATNUMZ KUWASHA MOTO WASHINGTON DC MAREKANI MAY 29 -MEMORIAL WEEKEND

UVCCM KIGOMA WAMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI,WAMTAKA MKUU WA MKOA KWENDA NA KASI YAKE ILI KUIKOMBOA KIGOMA NA UMASKINI

$
0
0
Mwenyekiti wa umoja wa vijana(UVCCM) Mkoa wa Kigoma peter Msanjilla akiongea na mwandishi wa habari hii ofisini kwake(hayupo pichani) baada ya kikao cha kamati ya  utekelezaji umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Kigoma

Na Editha Karlo wa blog ya jamii Kigoma. 

UMOJA wa vijana wa chama cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Kigoma wamempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kazi yake nzuri anayofanya ya kuwatumikia wananchi tangu alipoingia madarakani. 

Mwenyekiti wa umoja huo wa UVCCM Mkoa wa Kigoma Peter Msanjilla, alimwambia mwandishi wa blog hii ofisini kuwa kamati ya utekelezaji ya vijana Mkoa wametoa pongezi hizo katika kikao kilichofanyika leo (jana) kwenye ofisi za CCM mkoa. 

Alisema kuwa wameamua kumpongeza Rais kwa sababu ya kasi yake anayofanya ya kudhibiti uchumi na kutaka nchi ijiendeshe kwa kutumia fedha za ndani. Msanjilla alisema kuwa pia katika kikao hicho wamemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga kufanya kazi kwa kuendana na kasi ya Rais kwa kusimamia vyanzo vya mapato vilivyopo katika Mkoa akishirikiana na mamlaka ya mapato nchini(TRA). 

"Hapa Mkoani kwetu kuna mahotel mengi tu na sheli za mafuta nyingi, lakini huwa hawatumii mashine za EFD kutoa risiti wao wanaandika kwa mkono hii haikubaliki ni sawa na luhujumu uchumi wa nchi"alisema Msanjille.

Pia umoja huo umempongeza mwenyekiti wa wazazi Taifa Alhaji Bulembokwa kuadhimisha wiki ya wazazi katika jumuiya hiyo ambapo Kitaifa inafanyika Mkoani Morogoro. 

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO

MKURUGENZI WA HALMASHAURI ATAKAESHINDWA KUTENGA ASILIMIA KUMI KWA AJILI YA WANAWAKE NA VIJANA ATAONDOLEWA-WAZIRI MKUU

$
0
0
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amesema Mkurugezi yeyote wa Halmashauri nchini atakayeshindwa kutenga asilimia 10 ya mapato kwa ajili ya wanawake na vijana ataondolewa.

Amesema suala la kila Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi ni la lazima na si hiari.Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo leo (10 Aprili, 2016) alipokuwa anazungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Kitandi, Mtimbo, Likunja, Nkowe na Namahema ambako lifanya mikutano ya hadhara.

“Halmashauri ambayo itashindwa kutenga asilimia 10 kwa maana asilimia tano kwa ajili ya vijana na tano kwa ajili ya akinamama Mkurugenzi wake atakuwa anatafuta safariiri,” amesema Waziri Mkuu, Majaliwa.

Waziri Mkuu, Majaliwa yupo wilayani Ruangwa, Lindi kwa ajili ya ziara ya kikazi inayolenga kukagua shughuli za maendeleo, ambapo amewasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutimiza wajibu wao na serikali haitamvumilia yeyote atakayeshindwa.

Pia Waziri Mkuu, Majaliwa amewataka wananchi hao kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili zitakapofika sh milioni 50 za kila kijiji zilizoahidiwa na Rais, Dk. John Magufuli waweze kunufaika.Amesema fedha hizo ambazo zitatolewa kuanzia mwezi Julai mwaka huu zitagawiwa katika vikundi mbalimbali vilivyosajiliwa na si kwa mtu mmoja mmoja hivyo amewataka watendaji wa kata na vijiji kuwahamasisha wananchi kujiunga katika vikundi.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu, Majaliwa amesema serikali imefuta tozo tano kati ya tisa za zao la korosho zilizokuwa kero ya muda mrefu na kufanya wakulima wachukie mfumo wa Stakabadhi ghalani.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu

Barabara ya Nanganga-Ruangwa kuwekwa lami

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwendesha pikipiki maarufu na hodari, Zaina Amour wa kijiji cha Nandagara wilayani Ruangwa Aprili 10, 2016.

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema serikali inatarajia kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Nanganga, Ruangwa hadi Nachingwea.

Hatua hiyo itawezesha kutatuliwa kwa kero ya changamoto ya miundombinu ya barabara inayowakabili wananchi wa wilaya za Ruangwa na Nachingwea kwa muda mrefu.Waziri Mkuu, Majaliwa amesema barabara hiyo ambayo kwa sasa haipo katika hali nzuri itajengwa kwa kiwango cha lami, ambapo serikali inatarajia kuanza kuifanyia upembuzi yakinifu katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Hayo yamesemwa jana jioni (10 Aprili, 2016) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Likunja, Nkowe na Namahema katika mikutano ya hadhara aliyoifanya wilayani Ruangwa wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi.

Amesema serikali imejipanga katika kuboresha miundombinu ya barabara kwenye maeneo mbalimbali nchini na kwamba mara baada ya kumalizika kwa upembuzi yakinifu ujenzi wa barabara hiyo utaanza, hivyo amewataka wananchi kuwa na subira.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, Majaliwa amewataka wananchi wa vijiji hivyo kushirikiana katika shughuli za maendeleo na kuweka kando itikadi zao za kisiasa kwa sababu uchaguzi ulishamalizika tangu Oktoba 25 mwaka jana.

“Mimi nitaendelea kuwaheshimu, kuwasikiliza na kuwahudumia, nawaomba tushirikiane na tuweke kando masuala ya itikadi za vyama, sasa ni wakati wa kazi, hivyo ni bora tukashirikiana kufanya kazi kwa maendeleo ya Ruangwa jambo ambalo linawezekana.

Hata kama wewe ambaye najua ulinichukia mimi nimekusamehe kutoka moyoni, wewe ni wangu hata kama hukunichagua nitakuhudumia na kukutumikia kwa sababu mimi ndiye mbunge wako hivyo naomba tushirikiane,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Rashid Nakumbya aliomba wakazi wa wilaya hiyo kushirikiana kwa pamoja kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya wilaya yao na hatimaye iweze kupiga hatua.

--- Article Removed ---

$
0
0
***
***
*** RSSing Note: Article removed by member request. ***
***

Watuhumiwa dawa za kulevya wazidi kubanwa

$
0
0
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa Magereza mkoa wa Lindi, kuhakikisha hakuna mtuhumiwa wa dawa za kulevya atakayetoweka katika gereza la mkoa huo.

Amesema kuna watuhumiwa wa dawa za kulevya ambao wanahifadhiwa katika gereza la mkoa wa Lindi hivyo ni vema akajiridhisha kama ulinzi na usalama wa watuhumiwa hao umeimarishwa.Hata hivyo, Waziri Mkuu, Majaliwa amemtaka mkuu wa gereza hilo kuwa makini na baadhi ya zabuni wanazozitoa kutoka nje na kuhakikisha ulinzi unaimarisha wakati wote gerezani hapo.

Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo jana (10 Aprili, 2016) wilayani Ruangwa wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Lindi iliyowasilishwa kwake na Mkuu wa mkoa huo, Godfrey Zambi.“Mkuu wa Magereza wa mkoa atembee gereza ambalo wanashikiliwa watuhumiwa wa dawa za kulevya na aangalie mradi unaolenga kupeleka maji gerezani hapo kama ni kweli au njia…,” amesema Waziri Mkuu, Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu, Majaliwa amemtaka mkuu huyo wa Magereza kujiridhisha kama ulinzi na usalama wao umeimarishwa na kuhakikisha hakuna mtuhumiwa anayetoweka.Awali akisoma taarifa kwa Waziri Mkuu, mkuu wa mkoa wa Lindi, Zambi amesema matumizi ya dawa za kulevya hususan kwa vijana ni miongoni mwa changamoto zinazoukabili mkoa huu ambapo wilaya ya Kilwa inaongoza kwa kuwa na waathirika wengi.

Amesema matumizi ya dawa hizo yanasababisha kupunguza kwa nguvu kazi kwani watumiaji wengi ni vijana, hivyo alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na serikali katika kupiga vita matumizi ya dawa hizo kwa kuwafichua wauzaji na watumiaji.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA TAASISI YA BASILA MWANUKUZI JIJINI DAR LEO

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Basila Mwanukuzi (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation) yenye lengo la kusaidia wanawake kuinua uwezo wao wa kibunifu ili kujiinua kiuchumi  hasa Mama Lishe kwa kushirikiana na wadau mbali mbali. Uzinduzi huo umefakika leo Aprili 11, 2016 kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Basila Mwanukuzi (kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia, Timoth Mgonja pamoja na Mwakilishi wa Mama Lishe, Bi. Grace Foya.PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu, akitoa hotuba yake wakati wa Uzinduzi wa Taasisi ya Basila Mwanukuzi (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation), uliofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2016.
 Mwanzilishi wa Taasisi ya Basila Mwanukuzi (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation), Basila Manukuzi, akizungumza machache wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi yake hiyo yenye lengo la kusaidia wanawake kuinua uwezo wao wa kibunifu ili kujiinua kiuchumi  hasa Mama Lishe uliofakika leo Aprili 11, 2016 kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja na baadhi wa Wageni wa waalikwa pamoja na Kina Mama Lishe.

STATOIL YATAJA VIJANA WATANO WALIOINGIA TANO BORA YA SHINDANO LA MASHUJAA WA KESHO

$
0
0
Kampuni ya Statoil Tanzania ina furaha kutangaza majina ya vijana watano waliongia fainali za shindano la biashara la mashujaa wa kesho ambalo lina dhumuni la kuhamasisha ujasiriamali kwa mikoa ya kusini mwa Tanzania yaani Mtwara na Lindi.

Akitoa taarifa hii meneja wa shindano hilo kutoka Statoil, Erick Mchome amewataja washindi hao kuwa ni Razaki Kaondo, Edward Timamu and Sifael Nkiliye (walioshiriki kama timu moja), Saleh Rashid Kisunga, Azizi Doa, na Yunus Mtopa.

Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi kuwasilisha mawazo yao ya biashara ambayo baadae yalibadilishwa na kuwekwa kwenye andiko la biashara.

Mwaka huu shindano hili lilivutia vijana zaidi ya 400 ambao waliwasilisha mawazo ya biashara zao zinazolenga sekta mbalimbali za uchumi kama kilimo, ufugaji, mawasiliano, na biashara nyingine ndogondogo. Vijana waliruhusiwa kushiriki mmoja mmoja au hata kuunda vikundi vya watu wawili mpaka watatu.
Mwazo bora yaliyopatikana kati ya 400 yalikuwa 60 na wamiliki wa mawazo hayo ambao ni zaidi ya vijana 80 kutoka Lindi na Mtwara walipewa mafunzo maalum ya kuandaa andiko la biashara ambapo yalishindanishwa tena na kupatikana vijana kumi bora waliopelekwa mbele ya majaji ambao wiki hii walichagua maandiko matano bora kati ya kumi waliyopokea.

“Vijana hawa watano watawasili jijini Dar es Salaam wiki ijayo ili kuja kutetea maandiko yao ya biashara mbele ya jopo la majaji ambao mwisho wake wataamua nani anafaa kuwa mshindi wa shindano letu,” alisema Bwana Mchome.

Mshindi wa shindano hili atatangazwa siku ya Ijumaa tarehe 15 Aprili jijini Dar es Salaam katika hafla maalum iliyoandaliwa na Statoil ili kumpongeza mshindi huyo na wenzake wanne ambao wamefanikiwa kuingia fainali. Mshindi huyo atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani 5,000 wakati washindi wanne waliobakia watapata dola 1,500 kila mmoja. Washindi wengine watano waliofanikiwa kuingia kumi bora watapata dola 1,000.

“Statoil inaamini katika kuwawezesha vijana wenye vipaji katika maeneo yote ambayo tunafanya shughuli zetu na kwa kufanya hivi tunachochea maendeleo katika maeneo hayo ambayo nasi ni sehemu yake kwani tunafanya shughuli zetu za uendelezaji wa nishati kama gesi na mafuta.,” amesema Meneja Mkazi wa Statoil Tanzania, Øystein Michelsen.

WABUNGE WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUHAMASISHA JAMII JUU YA FURSA ZA KIBIASHARA ZINAZOPATIKANA AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0
WABUNGE wa Jumuiya la Afrika Mashariki kuanza kuhamasisha jamii ili kujua fursa za Kibiashara zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ameyasema hayo leo Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa wataanza kuhamasisha jamii katika soko la Kariakoo na Soko la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam pamoja na vyombo vya habari mbalimbali.

Makongo amesema kusudi la kuelimisha jamii ili wafanyabishara waweze kufanya biashara katika nchi za Afrika Mashari kama Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashari Makongoro Nyerere akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na wabunge wa bunge la Afrika Mashariki kuanza kuhamasisha jamii kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Banji, Miriam Yahaya Usi, Ndarakilo Kessy na Dk.Twaha Tasilima wakiwa katika mkutano huo leo.


Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Mwinyi (Katikati)akifafanua jambo katika mkutano wa waandishi wa habari na wabunge wa bunge la Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.
Mbune wa Bunge la Afrika Mashariki, Nderakilo Kessy (aliyesimama )akizungumza na waandhishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na wabunge hao kuanza kuhamasisha jamii juu ya Fursa zilizopo katika jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Banji akizungumza kuhusiana na Fursa zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashari.

Amesema kuwa frusa zilizopo kwa waalimu wa Lugha ya Kiswahili wanaweza kwenda kufundisha Kiswahili kwenye Nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni Kenya Uganda, Rwanda, Burundi na Afrika ya kati ipo mbioni kujiunga na Umoja huo.

Amesema Lugha ya Kiswahili kwa sasa imeanza kushika karibu nchi zote za Afrika Mashariki na hii ndio fursa Kubwa tuliyo nayo.

Picha na Avila Kakingo.

KIJIJI CHA OLBILI CHAKABILIWA NA NJAA.

$
0
0
Wananchi wa Kijiji cha Olbili kilichopo kitongoji cha Tilili,kata ya Shambarai wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakibeba mabango kupinga kunyang`anywa ardhi ya waliyokua wakiitumia kwa kilimo na kubadilishwa kuwa ya malisho ya mifugo,kijiji hicho kinakabiliwa na tatizo la ukosefuchakula cha miongoni mwa familia nyingi hali inayochangia kuzorota kwa hali ya lishe na shughuli za kijamii pamoja na za kiuchumi.

Na Woinde Shizza,Simanjiro.
KIJIJI cha Olbili kilichopo kitongoji cha Tilili,kata ya Shambarai wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kinakabiliwa na tatizo la ukosefuchakula cha miongoni mwa familia nyingi hali inayochangia kuzorota kwa hali ya lishe na shughuli za kijamii pamoja na za kiuchumi.

Wananchi wa kijiji hicho Zuhura Salim na Anna Lazaro wamesema kuwa uhaba huo wa chakula unatokana na kunyang`anywa maeneo waliyokua wanatumia kwa kilimo na kutumika kama ardhi ya malisho.

Wananchi hao waliandamana na mabango yao kuzunguka eneo la shamba hilo 
wameiomba serikali kupitia wizara ya ardhi na wizara ya kilimo kuingilia kati mgogoro huo baina yao na wafugaji wanaogombea eneo hilo ambalo kwa zaidi ya miaka 24 tangu mwaka 1992 hadi mwaka 2013 ambapo walizuiwa kutumia maeneo hayo ambayo walikua wakiyatumia kwa shughuli za kilimo cha kujikimu.

Eliud Jackson ni Mwanakijiji wa Olbili amesema kuwa licha ya kunyimwa
maeneo ya kulima pia mwaka huu hawakupata chakula cha msaada kama kata 
nyingine zilizopata mgao huo hivyo kuteseka na njaa wao na watoto wao 
,wamemuomba Rais Magufuli kutazama suala hilo na kulipatia ufumbuzi.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Tilili Kingi Lomayani Laizer amesema kuwa 
baada ya kuzuiliwa kulima na Mtendaji wa Kata na Diwani aliyekua 
madarakani walifika katika ngazi za wilaya bila mafanikio hivyo 
 wanamuomba Mkuu wa Mkoa wa Manyara afike kutatua mgogoro huo ili 
kuwanusuru na baa la njaa.

“Nimefuatilia suala hili kwa Mwenyekiti,Mtendaji wa kata na Diwani
aliyemaliza muda wake bila mafanikio kwani wao ndio walitoa zuio la
 kutuzuia kulima katika maeneo haya ,inaonekana jambo hili linashikiliwa na wafugaji wenye fedha wanatumia fedha zao kuwanyanyasa wakulima” Alisema Laizer

Aliiomba serikali kupitia wizara ya kilimo,ardhi kufika katika kijiji
hicho na kutatua kero hiyo ya muda mrefu kwani wamekua wakishindwa 

kuendesha familia zao kutokana na kutegemea kilimo kama shughuli ya 
kuwapatia chakula na kipato.

BREAKING NYUZZZZZ...WAFANYAKAZI HEWA WAMPONZA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA,MAMA ANNA KILANGO, RAIS DKT. MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WAKE

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, mchana huu ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mama Anna Kilango Malecella, kwa kubaini kuwa alimwambia uwongo kuwa Mkoa wake hauna wafanyakazi hewa wakati kumbe wapo wengi tu.

Rais Magufuli amesema kwamba hakuamini kwamba kuna mkoa ambao hauna wafanyakazi hewa, hivyo akatuma kikosi kazi ambacho hadi usiku wa kuamkia leo kimebaini kuwepo na wafanyakazi hewa 45 mkoani Shinyanya.

Rais Magufuli, ambaye alikuwa anaongea baada ya kupokea Ripoti ya TAKUKURU  toka kwa Mkurugenzi wake Mkuu  Valentino Mlowola,  amesema kasikitishwa sana na kauli ya Mama Malecela ambaye bila shaka alikuwa amepata ushauri mbaya toka kwa watendaji wake. 

Amesema idadi hiyo ya wafanyakazi hewa mkoani Shinyanga huenda ikaongezeka zaidi kwani wilaya mbili zilikuwa bado zinaendela kuhakikiwa.
Rais Magufuli amesema pia kwamba hadi jana jumla ya wafanyakazi hewa zaidi ya 5, 507 wamebainika nchi nzima, wengi wao wakitoka katika halmashauri.

Hivyo Rais pia ametengua uteuzi wa  Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Abdul R. Dachi kwa kumshauri vibaya Mkuu wa Mkoa.Mama Anna Kilango Malecela, ambaye katika awamu ya nne alikuwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi na Mbunge wa Same Mashairiki, anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza kuachishwa kazi. Wakuu wa mikoa waliapishwa mwezi uliopita.


Katika siku hiyo Rais aliwapa wakurugenzi wa halmashauri siku 15 wawatoe katika Orodha ya Malipo ya Mshahara (Pay Roll) wafanyakazi hewa wote katika halmashauri zote nchini, na kuwataka wakuu wa Mikoa hao wasimamie zoezi hilo kwa ukamilifu.

Vile vile Rais Magufuli alionya kuwa halmashauri yoyote baada ya muda huo itakayokuwa na mfanyakazi hewa, mkurugenzi wake atakuwa amejifuta kazi mwenyewe.Vilevile Rais amewaagiza mawaziri wote kuwaeleza watendaji wao wawaondoe wafanyakazi hewa wote ndani ya kipindi hicho cha siku 15 na kubainisha kuwa watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo watafukuzwa kazi kwani sheria ni msumeno.

KUKOSEKANA KWA UWAJIBIKAJI KUNAFANYA MFUMO MAISHA YA WANANCHI KUHARIBIKA –DK.MPANGO.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA), Ludovick Utouh akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la  Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la  Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA), Ludovick Utouh  wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kongamano la  Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango akikabidhiwa kibao maalumu mara baada ya kuzindua Kongamano la  Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA), Ludovick Utouh jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja  katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo. 
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango amesema kukosekana kwa uwajibikaji na utawala bora  kunafanya mfumo wa maisha ya wananchi kuharibika.

Dk.Mpango ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa Kongamano la  Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) ,amesema katika kuweza kufikia uchumi wakati lazima lipewe kipaumbele katika uwekezaji wa Gesi na Mafuta.

Amesema jamii inayoamini uwajibikaji na utawala bora inafanya jamii hiyo kuwajibika kwa pamoja katika maendeleo ya kiuchumi.

Dk.Mpango amesema akiwa Waziri mwenye dhamana ni kuangalia uwajibikaji kwa raia katika nchi na bila kuangalia uwajibikaji na utawala bora  mfumo wa maisha ya wananchi unaharibika.

Amesema taasisi ya wajibu ni moja ya taasisi ambayo itasaidia juu ya kutafsiri wa uwajibikaji kwa wananchi kwa lugha inayofahamika na kueleweka.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA), Ludovick Utouh amesema nia ya kongamano hilo ni kutafuta mawazo ya watu wengine katika uwajibikaji wa katika sekta ya Gesi na Mafuta.

Utouh amesema kuwa kutokana na rasilimali hiyo kugundulika wameona kuna umuhimu wa kushirikisha watu wengine ambao walipata rasilimali hiyo lakini hakuweza kuwasaidia ambapo hata Tanzania tunaweza kuangukia huko.

Mkutano huo umeshirikisha watu waliobobea katika sekta ya Gesi na Mafuta katika kutoa mawazo yao juu ya Tanzania inavyoweza kufanya  katika sekta hiyo.

UPANDISHWAJI WA MADARAJA KWA WALIMU WAZUA SITOFAHAMU ARUSHA

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

Baadhi ya walimu wa jiji la Arusha wamelalamikia utaratibu uliotumika wa upandishwaji wa madaraja na kusema kuwa utaratibu huo ni ujawatendea haki walimu waliofanya kazi kwa kipindi kirefu pamoja na wale ambao wamestaafu
.

Walimu hao walisema kuwa utaratibu uliotumika wa kuwachanganya walimu waliofanya kazi kwa kipindi cha mda mrefu zaidi ya miaka 20 pamoja na walimu wageni ambao wengine hawana mda mrefu kazini kwani wamefanya kwa zaidi ya mwaka mmoja hadi miaka mitatu ni mbovu na unawakatisha tama ya kufanya kazi kwa umakini.

Mmoja wa walimu hao aliyejitambulisha kwa jina la Mark Mbwabwo alisema kuwa mfumo huo wa upandishwaji wa madaraja haukuwatendea haki kabisa walimu ambao wamefanya kazi kwa kipindi cha mda mrefu kwani katika swala la ulipwaji mshahara mnakuta mwalimu aliefanya kazi kwa kipindi cha miaka 20 analipwa sawa na mwalimu ambaye amefanya kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja au mitatu.

Gazeti hili lilitembelea ofisi ya chama cha walimu (CWT) mkoa wa Arusha ili kujua kama wamepata malamiko hayo ambayo yalitolewa na baadhi ya walimu ambao wamepandishwa madaraja na kukutana na katibu wa chama cha walimu Halmashauri ya jiji la Arusha Magreth Hovokela ambapo alitolea ufafanuzi tuhuma hizo na hatua ambazo wao kama chama cha walimu wamezifikia.

Katika ufafanuzi wake alisema kuwa swala la upandishwaji wa madaraja kwa walimu waliogota ni la mda mrefu kwani wao kama CWT walipeleka pendekezo hilo tangu December 17 mwa ka 2014 na serekali ikakubali kupandisha walimu waliogota kwa kipind cha muda mrefu , serekali ilisema kuwa walimu hao wanaopandishwa madaraja wapandishwe kutokana na muundo wa zamani ambapo ilipitishwa walimu wapandishwe kuanzia mapema July 1 ,2015 lakini swala hilo halikutekelezeka.

Aidha aliongeza kuwa swala hilo alikutekelezwa kwa kipindi hicho na lilianza kutekelezwa rasmi January 1 hadi machi mwaka huu na kila halmashauri imeshaanza kutekeleza swala hilo kutokana na ilivyojipanga pamoja na bajeti yake na katika barua ambazo walimu wamepewa za kupandishwa madaraja zinaainisha kuwa walimu hao wamepanda madaraja kuanzia January 1 mwaka huu badala ya July 7,2015 kama vile waraka unavyoelekeza.


HABARI ZAIDI  BOFYA HAPA
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images