Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

SPIKA NDUGAI AFANYA MABADILIKO YA BAADHI YA WAJUMBE WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE.

$
0
0
Na Benedict Liwenga-Maelezo.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge ili kuzingatia mahitaji mapya na changamoto zilizojitokeza baada ya kuunda Kamati hizo mwezi Januari 2016.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Ofisi ya Bunge Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ambapo imeelezwa kuwa, mabadiliko hayo, yamefanywa chini ya Kanuni ya 116(3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge inayompa Spika Mamlaka ya kuteua Wabunge kuunda Kamati Mbalimbali za Bunge.
 
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, kufuatia mabadiliko hayo ambayo baadhi yake yamehusu Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au wote wawili, Kamati za Kudumu za Bunge zilizoathirika na mabadiliko haya zitawajibika kufanya Uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa kanuni ya 116 (10).

Baadhi ya Kamati ambazo zimeathirika na mabadiliko hayo na ambazo zitawajibika kufanya uchaguzi kwa viongozi ni zikiwemo; Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii ambayo itahitaji kupata Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wapya, Kamati ya Nishati na Madini ambayo itahitaji kupata Mwenyekiti mpya, Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma itahitaji kupata Mwenyekiti mpya, Kamati ya LAAC ambayo pia itahitaji kupata Makamu Mwenyekiti mpya na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambayo itahitaji kupata Makamu Mwenyekiti mpya.  
 
Aidha, taarifa hiyo imeeleza pia mabadiliko hayo kwenye kamati zote yanaanza mara moja ambapo orodha ya wajumbe waliobadilishwa imeshatolewa na Ofisi hiyo na kusambazwa katika vyombo vya habari.

Wizara ya Habari yapokea Ipad kwa Ajili ya Maafisa Habari wa Mikoa 13.

Jiji la Dar es salaam lapata Meya Mpya.

$
0
0
Na Anitha Jonas – MAELEZO

Kaimu Mkurugenzi Jiji la Dar es Salaam Bi. Sara Yohana amemtanganza Mhe. Isaya Chacha Diwani wa Kata ya Vijibweni (CHADEMA) kutoka Manispaa ya Temeke kuwa Meya Mpya wa Jiji hilo.
 
Kaimu Mkurugenzi huyo alimtangaza Isaya kuwa mshindi mara baada ya uchaguzi huo kufanyika leo  jijini Dar es Salaam ambapo mshindi alipata kwa kura 84 dhidi ya mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw.Yenga Yusuph ambaye alipata kura 67 wakati kura 7 ziliharibika katika uchaguzi huo.

 “Tunawashuruku wapiga kura wote mlioshiriki zoezi hili la upigaji kura kwa utulivu bila vurugu na kuweza kufanikisha mpaka kumpata Meya wa Jiji hili” alisema Bi Yohana.
 
Kwa upande wa mshindi wa Kiti cha Meya wa Jiji Mhe. Chacha aliwashukuru wapiga kura wake wa kata ya Vijibweni kwa kumchagua kuwa Diwani pamoja uongozi wa chama chake kukubali kumpa nafasi ya kugombea kiti hicho.
 
“Nimejipanga kuleta maendeleo katika sekta ya elimu pamoja na kupambana na kero ya foleni katika jiji letu na nitahakikisha wananchi wote maskini wanafaidika  na mapato ya jiji hili ikiwemo kuendeleza miundombinu mbalimbali ,”alisema Chacha.
 
Aidha, Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Bw.Freeman Mbowe alisema idadi ya wapiga kura tu inaonyesha wazi kuwa ushindi wa kiti hicho cha Meya ni lazima uchukuliwe na  CHADEMA sababu  madiwani wengi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanatoka katika chama hicho.

BENKI YA BARLAYS YAMZAWADIA MSHINDI WA KAMPENI YA 'BARCLAYS PREMIER LEGUE'

$
0
0
Wapili kutoka kulia ni Mkuu wa kitengo cha bidhaa kwa wateja wa rejareja wa benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa akizungumza na waandishi wa habarijijini Dar es Salaam leo na kuwapa zawadi zawadi wateja mbalimbali na mmoja kumpa hundi ya shilingi milioni sita na laki tisa kwa kujishindia safari ya kwenda uingereza kuungalia mpira wa ligi ya uingereza. Kulia ni Mkurugenzi wa wateja wa rejareja wa benki ya Bacclays, Kurmaran Pather kutoka kushoto ni Mkuu wa Matawi ya Barclays Tanzania, Emmanuel Katuma na Mshindi wa milioni sita na laki tisa kutoka Morogoro, Hamadi Chambo.
Mkurugenzi wa wateja wa rejareja wa benki ya Bacclays, Kurmaran Pather akimkabidhi hundi ya shilingi milioni sita na laki tisa mshindi ambaye alitakiwa kwenda Uingereza kuangalia ligi ya uingereza lakini kwa sababu zilizo chini ya uwezo wa wadhamini hao kushindwa kumpeleka huko na kumkabidhi fedha hizo mshindi huyo, Hamadi Chambo kushoto. wengine ni  Mkuu wa kitengo cha bidhaa kwa wateja wa rejareja wa benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa na kuu wa Matawi ya Barclays Tanzania, Emmanuel Katuma.
Washindi wengine wa zawadi kutoka benki ya Barclays wakiwa katika picha ya pamoja na kuu wa Matawi ya Barclays Tanzania, Emmanuel Katuma, Mkurugenzi wa wateja wa rejareja wa benki ya Bacclays, Kurmaran Pather na Mkuu wa kitengo cha bidhaa kwa wateja wa rejareja wa benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa.Washindi hao wamechagua kuzawadiwa mipira ambayo ni Origino kutoka uingereza.

Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA AMTEMBELEA SPIKA

$
0
0
   Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson kizungumza na Wajumbe wa  Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati Kamati hiyo ilipokutana na  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa. 
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Meneja Mahusiano wa EWURA Bw Titus Kaguo wakati walipomtemblea Ofisini kwake kati kati ni Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA Bw. Felix Mgamlagosi (Picha na Ofisi ya Bunge)
     Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akifuatilia Mjadala kati ya  Wajumbe wa  Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa alipoitembelea kamati hiyo. Anayezungumza  kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Balozi Adadi Rajabu  na (kulia mwenye tai yekundu) ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Charles Kitwaga.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA Bw. Felix Mgamlagosi aliyemtembelea leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

WAZIRI WA VIWANDA,BIASHARA NA UWEKEZAJI ATEMBELEA KIWANDA CHA KAMAL.

$
0
0
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kiwanda cha Nondo cha Kamal Steels Ltd. kilichopo Chang'ombe, DSM, pembeni yake ni Gagan Gupta ambaye ni Mwenyekiti na Mtendaji wa Kiwanda hicho.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akiangalia makopo yanayotumiwa na Kiwanda cha Kamal kama nalighafi za kiwanda akiwa na uongozi wa kiwanda.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akimuangalia fundi wa kusawazisha chuma kwa kutumia Shaper Mashine.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akipanda Mti wa kumbukumbu mara baada ya kukitembelea Kiwanda cha Kamal.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Kamal wakishuhudia ziara ya Waziri kiwandani hapo.    

 

TFF YAPIGA MARUFUKU KUCHEZA MCHEZO WA KUBAHATISHA(BETTING)

$
0
0
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inapenda kuwakumbusha wanafamilia wa mpira wa miguu kuto kushiriki katika michezo ya kubahatisha (Betting)juu ya ibara ya 59 kifungu kidogo cha 11 kinachotamka:
TFF Family members shall at all times comply with the following ethical principles "To not take part in betting connected with football and do not tolerate any form of manipulation or unlawful influencing of match results".

Hivyo wanafamilia ya mpira wa miguu Tanzania wanakumbushwa kuheshimu Katiba ya TFF Kwa kutoshiriki katika michezo ya kubahatisha (betting).

Wanafamilia ya TFF ni pamoja na viongozi wa mpira wa ngazi, zote, wachezaji, makocha, waamuzi, makamisaa, waajiriwa wa TFF, wajumbe wa kamati mbali mbali za TFF na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine wanajihusisha na mpira wa miguu

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MILIONI 255 KWA AJILI YA KUSAIDIA UJENZI WA KITUO CHA KISASA CHA MAWASILIANO YA JESHI LA POLISI.

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu (katikati), akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shs. milioni 255 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kituo cha mawasilianio ya Jeshi la Polisi. Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Siro, Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi, Omary Issa (wa pili kulia) na kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka.
(Picha na Francis Dande)
 Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP, Irnest Mangu (katikati) akionyesha furaha yake baada ya kupokea mafano wa hundi yenye thamani ya shs. Milioni 55.
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
 Baadhi ya wageni waalikwa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza kabla ya kukabidhi hundi ya Shs. Milioni 255 kwa Jeshi la Polisi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mfano wa hundi yenye thamani ya shs. milioni 255 kutoka Benki ya CRDB kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kituo cha mawasilianio ya Jeshi la Polisi.
 Meza Kuu.
 Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB.
Na Glory Chacky.
BENKI ya CRDB imekabidhi msaada wa sh.Milioni 255 kwa Jeshi la polisi kwa ajili ya  ujenzi wa kituo cha mawasiliano.

Akizungumza jana jijini Dar es salaam wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei amesema kuwa wanatambua kuwa jeshi la polisi ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi linahitaji mfumo bora wa mawasiliano kati yake na raia.

Alisema wameamua kuelekeza msada huo kwa jeshi la polisi kwa kutambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na jeshi hilo ya kuhakusha kwamba kuna usalama na amani kwa raia.

Kimei alisema juhudi za wanachi katika kujikwamua  katika umaskini  hazitafanikiwa kama kutakuwa na ukosefu wa usalama wa raia na  mali zao kwa ujumla.

Naye mkuu wa Jeshi la polisi IGP, Ernest Mangu alisema  kuwa wanashukuru kwa msaada huo kwani itasaudia kupunguza matukio ya kiualifu.

“ Kituo  hiki kitasaidia kulisogeza jeshi la polisi karibu zaidi na wananchi na kushirikiana nao katika kutaarifiana juu ya maswala ya kiualifu pindi yanapojitokeza”alisema Mangu.

MBUNGE WA JIMBO LA MLALO ATOA MSAADA WA MABATI KATIKA SHULE YA MKUNKI.

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi akikabidhi msaada wa mabati katika shule ya awali ya Kisirui kata ya Rangwi jimbo la Mlalo mkoani Tanga.
Mbunge wa jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi akizungumza na  wakazi wa  Kisirui kata ya Rangwi jimbo la Mlalo mkoani Tanga, mwishoni wa wiki alipotoa msaada wa Mabati katika shule ya awali Mkunki mwishoni mwa wiki.

SALIM ASAS AJITOLEA KUMUUNGA MKONO RAIS DR MAGUFULI JUU YA VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA ,ASAIDIA KUHUDUMIA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Mlezi wa kituo hicho cha Iringa Sober Hous Bw Godwin Msillu kushoto akiwa na baadhi ya vijana waliokuwa watumiaji wa dawa za kulevya ambao wanaishi kituoni hapo .
Shadrack John ambae ni anaishi kituo cha Iringa Sober House aliyetoka mkoa wa Arusha akijisomea Biblia baada ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya .

Na MatukiodaimaBlog.

KAMANDA wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Bw Salim Asas ameunga mkono kwa vitendo mapambano ya vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini yaliyoanzishwa na Rais Dr John Magufuli kwa kusaidia uanzishwaji wa kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya mkoani hapa.

Bw Asas ambae wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu alipata kuweka bayana mkakati wake wa kusaidia vijana walioathiriwa na matumizi ya madawa ya kulevya ameungana na kituo cha Iringa Sober House kilichopo Semtema katika Manispaa ya Iringa kuwasaidia vijana hao ambao afya zao zimeathiriwa na madawa ya kulevya kwa kuwakusana na kuwapatia tiba.

Akizungumza na mtandao wa matukiodaima leo Dr Alli Ngalla ambae ni Mkurugenzi wa NGOs ya Foundation for ellevition of drug eddiction anda sufferings (FADAS) wameanzisha kituo cha kutoa huduma kwa waathirika wa madawa ya kulevya cha Iringa Sober House ambacho kimeanza kufanya kazi chini ya ufadhili mkubwa wa Bw Asas .

Alisema kuwa kituo kituo hicho toka kimefunguliwa kina zaidi ya mwezi mmoja ambapo jumla ya wategemezi 7 ambao wanahudumiwa katika kituo hicho pamoja na wasimamizi watatu ambao pia walikuwa ni watumiaji wa dawa za kulevya ambao kwa sasa waliacha .

" Kwa kweli kuendelea kwa kituo hiki kumechangiwa kwa karibu na Salim Asas ambae amekuwa bega kwa bega kuona vijana walioathirika na madawa ya kulevya wanasaidiwa na anachofanya salim pia ni kumuunga mkono Rais Dr Magufuli ambae ametangaza vita dhidi ya madawa ya kulevya ......hivyo bado tunaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia mapambano haya ya kunusuru afya za vijana wetu "alisema Dr Ngalla 

Kuwa lengo la kituo kuweza kuwahudumia waathirika wa madawa ya kulevya kutoka mikoa mbali mbali nchini hasa wamelenga kuwafikia vijana wa mkoa wa Mbeya, Njombe , Ruvuma na Iringa japo tafiti zinaonyesha mkoa wa Mbeya ndio unaongoza kwa matumizi ya madawa ya kulevya .Msimamizi wa kituo hicho Bw Godwin Msillu alisema kuwa mkakati wa kuanzisha kituo hicho ulitokana na mkakati wa NGOS ya FADAS ambao walikuja na mpango wa kuanzisha kituo hicho .

Alisema kuwa kati ya waathirika wa dawa za kulevya ambao wapo kituoni hapo baadhi yao ni kutoka mkoa wa Arusha na kuwa kumekuwepo na mafanikio makubwa kwa walengwa hao afya zao kuanza kuimarika na hivyo kuwataka vijana wengine walioathirika na dawa za kulevya kutosita kufika kituoni hapo ili kusaidiwa zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake walioathirika na madawa ya kulevya Bw Shadrack John alisema kuwa amepata kufika mkoani Arusha kuja kupatiwa huduma hiyo na kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri zaidi.

Huku kijana Ibrahim Abdu alisema kuwa amekuwa akitumia madawa hayo kwa zaidi ya miaka 10 sasa kabla ya kuamua kuacha na kujiunga na kituo hicho hivyo kupongeza jitihada za Asas kuunga mkono kituo hicho huku akiwataka vijana wenzake kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya .

Msaada wa Matibabu ya Mtoto EBENEZA PEMBE anasumbuliwa na Kansa ya Ngozi

$
0
0
Mama ROIDA MUHAMA mkazi wa Mkimbizi mjini Iringa, anamuuguza mwanaye aitwaye EBENEZA PEMBE anayesumbuliwa na saratani ya ngozi kwa miaka sita sasa.

Anaomba msaada wa hali na mali ili aendelee kumtibia mwanaye, Anahitaji kiasi cha fedha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuendelea na matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Kwayeyote atakayeguswa tuma mchango wako kwa njia ya M-pesa 0767834377 au Tigo pesa 0717353529 kwa SILVANUS KIGOMBA au 0762 174 573 ROIDA MUHAMA (Mama wa Ebeneza).
Mtoto EBENEZA PEMBE anayesumbuliwa na Kansa ya Ngozi kwa zaidi ya Miaka 6 anahitaji Msaada wa fedha zitakazo muwezesha kwenda kupatiwa Matibabu katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Mtoto EBENEZA PEMBE aliyevaa shati la Bluu akiwa amebebwa na Mama yake Mzazi Bi ROIDA MUHAMA mkazi wa eneo la  MKIMBIZI manispaa ya Iringa, kushoto ni mtoto mwingine wa Bi ROIDA wakiwa katika Picha ya Pamoja.
...................

Nimeguswa na maumivu na mateso anayoyapata mtoto Ebeneza kwa zaidi ya miaka 6 nimejitolea kusaidia kusambaza taarifa za Ugonjwa wake ili kukusanya michango kwaajili ya matibabu yake. 

                     Naomba ushirikiano wenu rafiki zangu na Mungu awabariki sana.

MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU CHINI YA UNESCO YAZINDULIWA CHUO KIKUU HURIA, DAR

$
0
0
Faith Shayo - Unesco, Tanzania
Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda (hayupo pichani) kufungua rasmi mafunzo ya Tehama kwa walimu nchini.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

MAFUNZO kwa walimu watakaotumia teknolojia ya mawasiliano na habari (Tehama) kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu yamefunguliwa katika maabara za Chuo Kikuu Huria jijini Dar es salaam.

Mafunzo hayo yanayohusisha walimu kutoka Vyuo vya Monduli, Tabora na Morogoro yamelenga kuoanisha ufundishaji na matumizi ya Tehama katika program ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya kuboresha elimu Tanzania kupitia ufadhili wa taifa la China.

Programu hiyo inayotoa ushirikiano mpya kati ya China na shirika hilo la Umoja wa Mataifa inafanyakazi katika mataifa manane ya kusini mwa jangwa la sahara inatekelezwa kwa lengo la kuwezesha mafanikio kwa malengo ya 2030.Nchi zinaozhusika na mpango huo ni Tanzania Kongo ya Kinshasa (DRC), Congo, Liberia, Uganda, Côte d’Ivoire, Ethiopia na Namibia.
Mpango huo ambao kwa ujumla wake , awamu ya kwanza na ya pili unachukua miaka minne umelenga kuwezesha vyuo vya walimu kutoa walimu wa kufunza wenzao kwenye stadi za kufundisha kwa kutumia Tehama.

Mradi huo unaojulikana kama UNESCO-China Funds-in-Trust (CFIT) wenye lengo la kuziba pengo la ubora wa elimu wa kuwawezesha walimu kufundisha kwa kutumia Tehama ulizinduliwa Novemba 22,2012 kwa nchi tatu za kwanza na baadae kuongezwa nchi nyingine tano kufikia nane mwaka 2013.Mpango huo ni wa dola za Marekani milioni 8 kutoka China mahususi kwa mataifa ya Afrika kuboresha elimu kupitia Unesco.
Prof. Elifas Bisanda
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa walimu watakaotumia teknolojia ya mawasiliano na habari (Tehama) kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu yanayoendelea katika maabara za Chuo Kikuu Huria (out) jijini Dar es salaam

Walioketi kutoka kushoto ni Basiliana Caroli Mrimi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo pamoja na Kiongozi wa kitaifa wa timu ya mradi wa CFIT kit, Prof. Ralph Masenge.


Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku 10 katika Chuo Kikuu Huria, Mtaalamu wa program za elimu kutoka makao makuu ya Shirika la Unesco mjini Paris, Ufaransa, Gabriel El Khili alisema kwamba program hiyo imelenga kutatua chnagamoto zinazokabili elimu ili elimu iwe ileinayotakiwa kuwezesha maendeleo ya kasi katika sayansi.
Alisema ni lengo la Unesco kupitia ufadhili huo kuhakikisha kwamba kunapatikana walimu bora watakaowezesha matumizi ya Tehama katika kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu ili kutengeneza wataalamu wa baadae katika taifa hili.

Alisema kuna pengo kubwa kuhusiana na ubora wa elimu na kwamba baada ya kumaliza program ya elimu kwa wote mwaka jana nguvu sasa inastahili kuelekezwa katika ubora wa elimu ili kufikia malengo ya 2030. Alisema changamoto kubwa ni kuleta karibu matumizi ya digitali kwa kuzingatia ukweli wa sasa kwamba matumizi yake ni madogo ukizingatia na haja kubwa inayoambatana na haja ya kuwa na elimu bora.Alisema ni vyema kuiga mfano wa China kwamba kuna tatizo la kidunia la kielimu lakini linalohitaji suluhu ya eneo la husika kwa kuzingatia rasilimali zilizopo eneo hilo.
Gabriel El Khili - Unesco, Paris
Mtaalamu wa program za elimu kutoka makao makuu ya Shirika la Unesco mjini Paris, Ufaransa, Gabriel El Khili (kulia) akizungumzia madhumuni ya programu hiyo inayoratibiwa na UNESCO wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya wiki mbili kwa walimu yanayoendelea katika maabara ya Tehama Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.

Alisema mapinduzi ya kitamaduni ya China baada ya kujikomboa yalizingatia elimu na kwa kutumia rasilimali za nyumbani waliweza kusonga mbele na nia yao ya sasa ni kufikiri shida ya elimu na maendeleo kimataifa lakini kupata suluhu ya tatizo hilo kwa nchi husika kwa kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatumika kuboresha elimu.

Anasema mafunzo kwa Tehama maana yake kusambaza elimu bora kwa kutumia nyenzo za Tehama zilizopo kuanzia redio televisheni, CD na kadhalika.Alisema ni matumzi ya Unesco kwamba mafunzo yanayotolewa yatasaidia kuboresha elimu ya walimu na wanafunzi wao kwa kutumia Tehama, matumizi yake yaliyotukuka ambayo yatasaidia kuimarisha na kutoa ubora wa elimu pamoja na kuwa na walimu wachache.

Naye Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akifungua mafunzo hayo aliwataka walimu hao kutambua umuhimu wao katika kusukuma mbele lengo la mafunzo hayo na wala si kujipatia cheti cha mahudhurio.
Prof. Ralph Masenge
Kiongozi wa kitaifa wa timu ya mradi wa CFIT kit, Prof. Ralph Masenge akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo katika hafla fupi ya ufunguzi.

Alisema ulimwengu wa sasa ni wa walimu kutoa mwongozo wa namna ya kujifunza kwa kumuelekeza mwanafunzi kwa kuwa ulimwengu wa digitali umerahisisha mambo mengi.
Alisema wasishangae wakigundua kwamba wanafunzi wao ni weledi zaidi kuliko wao ila wasaidie kuhakikisha kwamba Tehama inatoa nafasi ya wanafunzi wengi kujifunza na kupata elimu wanayohitaji katika kubadili maisha na uchumi katika jamii.

Alisema kwamba ni matumaini yake kwamba kwa mafunzo hayo elimu ya Tanzania itapaa hasa kutokana na ukweli kuwa China imesema wazi kuwa haitapenda Tanzania kushindwa katika mradi huu wa kuleta maboresho makubwa katika elimu ya Tanzania ili iweze kutumika kutengeneza maarifa.

Profesa Bisanda alisema kwamba kwa sasa Tanzania ina shida kubwa katika masomo ya sayansi (bayolijia,kemia na fizikia ) pamoja na hesabu na kwamba uwapo wa program hiyo kutasaidia kufikisha mafunzo kwa wanafunzi kwa namna bora na yenye uhakika zaidi hata kama walimu wapo wachache.
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
Pichani juu na chini walimu kutoka Vyuo vya Monduli, Tabora na Morogoro wakishiriki mafunzo ya matumizi ya Tehama kwa vitendo katika program ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ya kuboresha elimu Tanzania kupitia ufadhili wa taifa la China.

Alisema ni vyema walimu wakajifunza namna ya kufanya na kutafuta majawabu ya matatizo kwa kutumia tehama na kuambukiza mwenendo huo kwa wenzao na kwa wanafunzi.
Alisema ni kweli kuwa Tanzania ipo gizani katika ICT kutokana na matumizi yake madogo na hivyo walimu wakielewa na kuwafunza wengine taifa hili litaondoka katika giza hilo na kupata mapinduzi makubwa ya fikira na elimu.Aidha alisema kwa kutumia ICT wanaweza kupunguza gharama za uendeshaji na uzalishaji hasa katika masomo na mafunzo.
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
Alitolea mfano kwamba kama wakipata softwea ya mitihani ambayo ipo wanaweza kuokoa zaidi ya shilingi milioni 700 wanazotumia kwa ajili ya mitihani na michakato yake.
“Fikiria unaweka program ambayo mwanafunzi anafanya mitihani moja kwa moja na hii inawezekana, utafanya nini na fedha hizo ambazo unazitumia sasa kwa ajili ya uandazi wa mitihani kuifanya na kuisahihisha” aliuliza na kusema kwamba zingelisaidia vitu vingine.
Alisema kihistoria walikuwa wanakazi kubwa ya kuandaa mitihani na kusambaza lakini mwanzo wa kuwafanya wanafunzi wajieleze kama wanataka kufanya mitihani kwa kutumia Tehama sasa wanatengeneza mitihani kwa kadiri ya maombi na kupunguza gharama.
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
UNESCO-China Funds in Trust (CFIT)
Picha ya pamoja ya wakufunzi na washiriki.
Faith Shayo - Unesco, Dar es Salaam
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda (kushoto), Mtaalamu wa program za elimu kutoka makao makuu ya Shirika la Unesco mjini Paris, Ufaransa, Gabriel El Khili (katikati) pamoja na Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo (kulia) mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.

Mahafari ya 12th ya Life Transforming School yalivyofana

$
0
0
Siku ya Jumapili ilifanyika mahafari ya 12th ya Life Transforming School ambayo huwa inaandaliwa na Kanisa la Living Water Centre Kawe mara moja kwa mwaka,kozi hiyo huwa ni kwa lengo la kufundisha watu mafundisho ya utumishi na kukua katika maisha ya wokovu na kupitia mafunzo mbalimbali kwa muda wa mwezi mmoja na siku kadhaa na kwenda kambi ya maombi na masomo mbalimbali.

Katika mahafari kulikuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa mahitimu ikiwepo ushahiri,dance,igizo,risala,shuhuda, na uimbaji kwa wahitimu wote,Wahitimu walikuwa na risala yao kwa Kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Ministry Apostle Onesmo Ndegi ilipendekeza kwa mwaka huu darasa hilo lifanyike mara mbili tofauti na miaka mingine,maombi hayo yamekuja baada ya wahitimu kuona jinsi darasa hilo lilivyo na umuhimu kwa maisha ya mkristo hata kama umeokoka au uko kwenye wokovu muda mrefu maana kuna vitu unahitaji kukumbushwa na watumishi wa Mungu. 

Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Ndegi alilidhia maombi ya wahitimu hao kupendekeza darasa hilo kufanyika mara mbili kwa mwaka kwa jinsi lilivyo na umuhimu kuanzia mwaka huu liwe linafanyika mara mbili ili kuondoa muda mrefu wa kusubiri darasa hilo mpaka mwakani,waliongeza kwa kusema maana yao ya kutaka kwa mwaka lifanyike mara mbili ni ili kuona watu wengi wanajitokeza kusoma darasa hili ili kuboresha maisha yao ya ushirika wao na Mungu zaidi.

Darasa hilo limewahi kuwa msaada kwa watu mbalimbali nchini wengine wameshakuwa wachungaji na huduma zao na wengine viongozi wakubwa serikalini mfano Mheshimiwa Mkuu wa Mmkoa Dar es salaam Paul Makonda,Watangazaji Hudson Kamoga, na Samuel Sasali hao ni baadhi na wengine wengi,Hivyo kama na wewe unataka kusoma darasa hilo jitahi usipitwe na darasa hili mwezi wa saba litakapo kwenda kuanza tena kisha mwakani mwezi wa kwanza,wasiliana nao kwa namba 0712116647.
picha ya pamoja kati ya wahitimu na waalimu wao pia mkuu wa shule.



Ushahiri 
Dance mbele za Bwana
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe na Mgeni rasmi katika mahafari hayo
Lilian Ndegi Mkuu wa Shule ya Life Transforming 
Wahitimu wa Life Transforming School 2016
Wahitimu wakitoa shuhuda za kile Mungu amewatendea kipindi walichokuwa wanasoma darasa hilo la utumishi
Wahitimu wakitoa shuhuda za kile Mungu amewatendea kipindi walichokuwa wanasoma darasa hilo la utumishi
Viongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe na shule ya Life Transforming School wakisikiliza shuhuda
Wahitimu katika kuimba 
Ni mbele za Bwana


Keki ya iliyotolewa na wahitimu kwa ajilinya changizo la fedha kuandaa mazingira ya darasa linakuja


Wahitimu walitoa zawadi kwa watenda kazi walishiriki na kuhusika katika darasa hilo
Wahitimu walitoa zawadi kwa watenda kazi walishiriki na kuhusika katika darasa hilo
Ugawaji wa Vyeti kwa Wahitimu wa Life Transforming School
Ugawaji wa Vyeti kwa Wahitimu wa Life Transforming School
Ugawaji wa Vyeti kwa Wahitimu wa Life Transforming School
Zawadi ziligawiwa ikiwa ni katika kuponezana kwa kumaliza darasa hilo
Zawadi ziligawiwa ikiwa ni katika kuponezana kwa kumaliza darasa hilo
Ndugu jamaa na marafiki walikuwepo kupongezana


Imeandaliwa na Tunu Bashemela 
Gospelhabari.blogspot.com

Profesa Muhongo aikaribisha Canada kuwekeza nchini.

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mbele) na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (kushoto kwa Waziri) wakiwa katika kikao cha pamoja na Ubalozi wa Canada na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Taasisi zake.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mbele) akishuhudia Balozi wa Canada nchini Tanzania, Alexandre Leveque akitia saini kitabu cha Wageni mara alipofika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Kansela Siasa, Uchumi, Masuala ya umma kutoka Ubalozi wa Canada nchini,  Theressa de Haan.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati),  Balozi wa Canada nchini Tanzania, Alexandre Leveque (kulia kwa Waziri)  na Kansela Siasa, Uchumi, Masuala ya umma, Theressa de Haan wakiwa wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Alexandre Leveque katika picha ya pamoja ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  
Na Rhoda James
Serikali imesema inakaribisha kampuni mbalimbali kutoka nchini Canada ili kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini lengo likiwa ni kuongeza kiwango cha umeme.

Wito huo umetolewa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipokutana na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Alexandre Leveque. “Tunataka kiwango cha umeme nchini kiongezeke mara mbili ya kiwango kilichopo sasa,” alisema Profesa Muhongo.

Aliongeza kwamba bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam lina matoleo katika maeneo mbalimbali nchini ikiwamo wilayani Mkuranga ambapo linaweza kuzalisha si chini ya megawati 2000. “Tunahitaji mwekezaji makini ambaye ataweza kuwekeza kwenye eneo hilo,” alisema Profesa Muhongo.

Profesa Muhongo alisema kuwa tayari ameshafanya mazungumzo na makampuni mbalimbali duniani kwa ajili ya kuwekeza kwenye nishati ya umeme na kwamba bado anaendelea kutafuta makampuni makini ya ndani na nje ya nchi ili Tanzania iweze kuwa na nishati ya uhakika.

Kwa upande wa Sekta ya Madini Profesa Muhongo alisema kuwa Serikali itaendelea kuwawezesha wachimbaji wadogo katika masuala mbalimbali ikiwemo utoaji wa ruzuku na mafunzo ya uchimbaji bora wenye tija.

Alisisitiza kwamba lengo la Serikali ni kuwakomboa wachimbaji wadogo kuondokana na umasikini na alieleza kuwa wachimbaji hao wakiwezeshwa itachangia ongezeko la ajira.  

Pia Profesa Muhongo alimuomba Balozi huyo wa Canada kufuatilia suala la kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake ili kuleta ufanisi wenye tija katika sekta za Nishati na Madini.

Kwa upande wake Balozi Leveque, alisema Canada inavutiwa kuwekeza hasa katika nishati jadidifu ikiwemo umeme wa jua na kwamba atayakaribisha makampuni ya nchini Canada kuwekeza katika uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia.

Balozi Leveque pia aliishauri Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi na kutoa wito wa usimamizi madhubuti wa Sekta ya Madini ili kuepusha muingiliano wa maeneo ya wachimbaji madini wakubwa wa nje na ndani ya nchi.

Aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo mbili na kuahidi kuwa Serikali ya Canada itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa masuala mbalimbali yakiwemo kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara na Taasisi zake.


   

Naibu Waziri Dkt. Kolimba aeleza nia ya Wizara katika kuendeleza Chuo cha Diplomasia

$
0
0


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.) , akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Chuo cha Diplomasia wakati wa ziara yake Chuoni hapo. Chuo hicho ni moja ya Taasisi zilizo chini ya Wizara. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Dkt. Mohammed Maundi (katikati) na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Taaluma Chuoni hapo, Dkt. Wetengere Kitojo . Naibu Waziri akiangalia vitabu vilivyopo kwenye Maktaba ya Chuo hicho
Naibu Waziri akiwaeleza jambo uongozi wa chuo hicho.
Naibu Waziri akikagua Darasa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Chuo cha Diplomasia .

Dkt. Susan akisalimiana na Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia mara baada ya kuwasili Chuoni hapo. 

Dkt. Suzana Kolimba akizungumza na uongozi wa Chuo cha Diplomasia mara baada ya kumaliza kuzungukia eneo la Chuo cha Diplomasia.
Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia naye akizungumza wakati Naibu Waziri alipotembelea Chuo hicho .
Naye Mkurugenzi wa Taaluma, Dkt. Watengere Kitojo akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Naibu Waziri .
Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu Chuoni hapo Dkt. Charles Bekon akionesha Mpango Mkakati wa Chuo cha Diplomasia ikiwemo mfano wa michoro ya majengo ya Chuo.
Naibu Waziri Dkt. Susan Kolimba akitazama sampuli ya michoro ya majengo yanayotarajiwa kujengwa Chuoni hapo.
Naibu Wizara Dkt. Suzan Kolimba akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo cha Diplomasia, wa kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia Dkt. Mohammed Maundi, Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Dkt. Achiula (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi wa Taaluma wa Chuo cha Diplomasia Dkt. Watengere Kitojo (wa kwanza kulia) na Mhasibu Mkuu Dkt. Charles Bekon. Picha na Reginald Philip

Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa imejipanga kuhakikisha Chuo cha Diplomasia kinaboresha huduma zake za utoaji elimu na mafunzo ya masuala ya Diplomasia ili kukidhi mahitaji ya Watanzania katika taaluma hiyo.

Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba alipofanya ziara katika Chuo hicho kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam ambacho ni moja ya Taasisi zilizo chini ya Wizara.

Mhe.  Kolimba alisema kwamba Chuo cha Diplomasia ambacho kilianzishwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Msumbiji ni miongoni mwa vyuo vilivyojipatia sifa kubwa ndani na nje ya nchi kwa kutoa mafunzo katika masuala ya Diplomasia na hivyo Wizara haina budi kuhakikisha inaendelea kukiboresha ili kuhakikisha kinakidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.

Mhe. Dkt. Susan alisema kuwa, miongoni mwa masuala yanayotakiwa kufanyiwa kazi katika maboresho hayo ni pamoja na miundombinu ya Chuo kwa maana ya kuongeza majengo, vifaa vya kisasa vya kufundishia, maabara za kisasa za lugha, maktaba na kuongeza Wakufunzi.Aidha, Mhe. Kolimba aliueleza Uongozi wa Chuo hicho kuwa ni vema vipaumbele katika kukiletea chuo maendeleo vikaainishwa ikiwa ni pamoja na kuonyesha mikakati ya kila changamoto ili kupata suluhisho la haraka la changamoto hizo.

“Ninawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya na tunaahidi kuwa pamoja nanyi wakati wote ili kuhakikisha Chuo chetu kinafikia viwango vinavyostahili” alisema Mhe. Kolimba.Vilevile alieleza kuwa ni vema Chuo kikaimarisha ushirikiano na Vyuo vingine vya ndani na nje kwa kuainisha maeneo muhimu ya ushirikiano yenye faida kwa pande zote. Pia alikitaka Chuo kuwa na mikakati itakayokiwezesha Chuo hicho kuweza kujiendesha kibiashara kama vyuo vingine nchini na kuacha utegemezi mkubwa katika bajeti ya Serikali.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri Chuoni hapo, Mkurugenzi wa Chuo hicho, Balozi Mohammed Maundi alisema kuwa Chuo hicho kinaendelea kuboresha maeneo mbalimbali ya Chuo hicho ikiwemo kuanzishwa kwa Kozi ya Shahada mwaka 2015 na tayari chuo kimepata michoro ya majengo kwa Chuo kipya wanachotarajia kukijenga na sasa kinachohitajika ni fedha ili kukamilisha mpango huo ambao kwa kiasi kikubwa utamaliza changamoto zinazokikabili Chuo.

Chuo cha Diplomasia (CFR) ni chuo kilichoanzishwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Msumbiji mwaka 1978. Chuo kimekuwa kikitoa elimu katika ngazi ya Cheti, Diploma, Shahada na Shahada ya Juu.

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION KUENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA DODOMA

$
0
0
Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi  Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers  ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation utaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Dodoma kuanzia Jumatatu, tarehe 28 March 2016 kwenye ukumbi wa  LAPF House Mkoani  Dodoma. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30 kutoka mkoani Dodoma na mikoa ya jirani. 

Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Dodoma wanafikia malengo yao waliojiwekea. Wanawake wakazi wa Mkoa wa Dodoma waliotuma maombi na wanaopenda kunufaika na mradi huo  wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya Jumamosi tarehe 26 Machi 2016 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa  LAPF House Mkoani Dodoma.

Mafunzo yana lengo la  kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 

Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo bila riba ya bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa  Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 712 646 322  au +255 718 010 107

Zantel yakabidhi msaada kwa watoto wenye ulemavu wa macho wa shule ya msingi Kisiwandui Unguja.

$
0
0
 Mshauri wa Mahusiano ya Umma wa Zantel, Mohamed Mussa akizungumza wakati akikabidhi vifaa vya kusomea kwa watoto wenye ulemavu wa macho wa shule ya msingi Kisiwandui. kwa mwalimu mkuu wa shule Bi Taifa Ahmed pamoja na Mkurugenzi wa Elimu ya Shule ya Msingi, bwana Ahmed Abulmajid Shaaban. 
Mshauri wa Mahusiano ya Umma wa Zantel, Mohamed Mussa akikabidhi vifaa vya kusomea kwa watoto wenye ulemavu wa macho wa shule ya msingi Kisiwandui kwa Mkurugenzi wa Elimu ya Shule ya Msingi, bwana Ahmed Abulmajid Shaaban. Anayetazama katikati ni mwalimu mkuu wa shule Bi Taifa Ahmed. 
 Mshauri wa Mahusiano ya Umma wa Zantel, Mohamed Mussa akizungumza wakati akikabidhi vifaa vya kusomea kwa watoto wenye ulemavu wa macho wa shule ya msingi Kisiwandui. kwa mwalimu mkuu wa shule Bi Taifa Ahmed pamoja na Mkurugenzi wa Elimu ya Shule ya Msingi, bwana Ahmed Abulmajid Shaaban.


Kampuni ya simu ya Zantel leo imekabidhi vifaa vya kusomea kwa watoto wenye vifaa vya ulemavu wa macho wa shule ya msingi Kisiwandui Unguja vyenye thamani ya shilingi milioni 20. Vifaa hivyo ni mashine ya perkins brailler, index printer, braillon paper pamoja na salte na stylus.

Msaada huo umekabidhiwa na Mshauri wa Mahusiano ya Umma wa Zantel, Mohamed Mussa kwa mwalimu mkuu wa shule Bi Taifa Ahmed pamoja na Mkurugenzi wa Elimu ya Shule ya Msingi, bwana Ahmed Abulmajid Shaaban.Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mohamed Mussa alisema vifaa hivyo ni sehemu ya mkakati wa  kampuni ya Zantel katika  kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata elimu bora bila kujali tofauti zao.

‘Wajibu wetu kama wanajamii ni kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata msaada kama ilivyo kwa watu wengine na pia kuweza kuwaanda  kwa ajili ya kuweza kufikia malengo yao kama walivyo kusudia’ alisema Mussa.

Shule ya msingi Kisiwandui ilianzishwa mwaka 1991, na mpaka sasa wanafunzi 199 wamepitia shuleni hapo.


wahariri wa vyombo vya habari vya kidini watembelea kituo cha afya cha utoaji wa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU

$
0
0
Wahariri wa vyombo vya habari za kidini wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara ya kimafunzo mkoani Pwani, ziara hiyo imeandaliwa na TACAIDS .
Mhariri wa Habari kutoka Radio Maria Bi. Judidh Francis akiongea jambo katika ziara ya wahariri wa vyombo vya habari vya kidini katika kituo cha afya cha utoaji huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze,ziara hiyo imeandaliwa na TACAIDS 
Mhariri wa Habari kutoka Radio Sauti ya Quran Bw. Sadiki Faki akiongea jambo katika ziara ya wahariri wa vyombo vya habari vya kidini katika kituo cha afya cha utoaji huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze,ziara hiyo imeandaliwa na TACAIDS .
Mratibu wa TACAIDS mkoani Pwani Bw. Badru Abdunuru akiwafafanulia jambo wahariri wa vyombo vya kidini wakati wa ziara ya kujifunza iliyofanyika mkoani pwani katika Kituo cha utoaji wa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze .
Mratibu wa TACAIDS mkoani Pwani Bw. Badru Abdunuru akiwafafanulia jambo wahariri wa vyombo vya kidini wakati wa ziara ya kujifunza iliyofanyika mkoani pwani katika Kituo cha utoaji wa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze .
Mratibu wa TACAIDS mkoani Pwani Bw. Badru Abdunuru aliyesimama kulia akiwafafanulia jambo wahariri wa vyombo vya kidini wakati wa ziara ya kujifunza iliyofanyika mkoani pwani katika Kituo cha utoaji wa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze .
Msimamizi wa kituo cha Maarifa kwa ajili ya kutoa huduma za VVU kwa madereva wa masafa marefu wa kwanza kushoto aliyekaa mbele Bi. Amina Chandima akiwafafanulia jambo wahariri wa vyombo vya kidini wakati wa ziara ya kujifunza iliyofanyika mkoani pwani katika Kituo cha utoaji wa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze .
Wahariri wa vyombo vya habari za kidini walipotembelea kituo cha utoaji wa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU mkoani Pwani, Wilayani Kibaha .
Mhariri wa Tumaini Media Bw. Martin Kuhanga akiongea jambo wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari vya kidini wakati wa ziara ya kujifunza iliyofanyika katika Kituo cha utoaji wa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa watu wanaoishi na VVU kilichopo mkoani Pwani na mdaula Chalinze .
Msimamizi wa utoaji wa huduma za tiba na ushauri kwa watu wanaoishi na VVU kutoka Wilaya ya Kibaha Daktari Robert Mwakyusa akiongea jambo na wahariri wa vyombo vya habari za kidini wakati wa ziara ya kujifunza iliyofanyika mkoani pwani. 

DAWASA YATOA DARASA KWA VIONGOZI WA JUMUIYA 15 ZA WATUMIA MAJI DAR ES SALAAM, KIBAHA NA BAGAMOYO

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Bi.Neli Msuya akizungumza na viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji zilizojengwa chini ya mradi wa Maji Yetu uliofadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji uliogharimu shilingi Bilioni 14.5 alipokutana nao leo jijini Dar es salaam.
Mshauri wa Ufundi wa DAWASA BTC  Mhandisi Praygod Mawalla akitoa elimu kwa viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji katika jiji la Dar es salaam namna ya kuifanya miradi wanayoisimamia ijiendeshe na kuwa endelevu kwa manufaa ya wananchi.

Mshauri wa Ufundi wa DAWASA BTC  Manjolo Kambili akitoa akitoa ufafanuzi kuhusu Programu ya za utoaji wa mafunzo kwa watumiaji wa Maji katika maeneo yenye miradi hiyo wakati wa mkutano na viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji za jiji la Dar es salaam.


Viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji zilizojengwa chini ya mradi wa Maji Yetu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na watendaji wa DAWASA leo jijini Dar es salaam.


Afisa Uhusiano na Jamii  wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Bi. Mecktridis Mdaku Mtaalamu kutoka akiwasisitiza viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji katika jiji la Dar es salaam kupanda miti na kuiendesha miradi katika hali ya Usafi ili kulinda afya za watumiaji wa huduma za maji.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa DAWASA Bi. Mary Ntikula akipanda mtimara baada ya mkutano na viongozi wa Jumuiya ya Watumia Maji Dar es salaam kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Maji na Utunzaji wa Mazingira. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Bi.Neli Msuya
Baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji jijini Dar es salaam.


       Na. Aron Msigwa Dar es salaam.



Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) imewataka viongozi wa Jumuiya za watumia maji katika jiji la Dar es salaam na  baadhi ya maeneo ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani kusimamia kikamilifu mapato na matumizi ya miradi ya maji ili kuepuka migogoro inayosababishwa na matumizi mabaya ya fedha jambo linalochangia baadhi ya miradi kushindwa kujiendesha na kuwa kero kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka hiyo Bi.Neli Msuya wakati akitoa elimu kwa viongozi hao kuhusu uendelezaji wa miradi inayosimamiwa na Jumuiya 15 za Watumia Maji zilizojengwa chini ya mradi wa Maji Yetu kwa ufadhili wa Serikali ya Ubelgiji.

Amesema DAWASA imekukutana viongozi hao kuwakumbusha wajibu walio nao katika kuhakikisha miradi wanayoisimamia inakidhi matarajio ya wananchi kwa kutoa huduma bora na kujiendesha kwa faida kwa na kuwafikia wananchi wengi zaidi.


Kwa kuzingatia idadi ya watu zaidi ya Laki mbili (200,000)  wanaohudumiwa na mradi huu kwa kupata maji safi na salama na gharama kubwa iliyotumika kuanzisha mradi huu shilingi Bilioni 14.5 ,tumeona kuna umuhimu wa kuendelea kuweka msisitizo wa uangalizi kwa kuwa miradi hii ni muhimu na iko kwa wananchi Amesisitiza.


Amewaeleza viongozi hao kuwa majukumu ya DAWASA kama mmiliki wa miundombinu ya majisafi na majitaka ni kugharamia matengenezo makubwa na kufanya uwekezaji wa kupanua miundombinu ya majisafi na majitaka jijini Dar es Salaam na maeneo yaliyoainishwa chini ya Sheria ya DAWASA Namba.20 ya Mwaka 2001.


Bi. Neli amefafanua kuwa DAWASA iliingia mkataba wa uendeshaji na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) kutoa huduma ya uondoshaji wa majitaka katikA jiji la Dar es salaam, Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.


Aidha, amesema kupitia mkataba huo,  DAWASCO huuza maji kwa wateja, kutayarisha Ankara za maji, kukusanya maduhuli, kulipia gharama za uendeshaji na kufanya matengenezo ya mfumo mzima wa usambazaji maji na uondoshaji majitaka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam. 


“Kupitia elimu inayotolewa leo mtagundua kuwa ninyi ni muhimu katika kuwahudumia wananchi, mtaona kuwa ninyi ni DAWASCO ndogondogo kwenye maeneo yenu kwa kuwa mnauza maji kwa wateja, mnatayarisha Ankara za maji , mnakusanya fedha za malipo ya huduma mnafanya matengenezo ya mifumo ya maji kwa wateja wenu” Amesisitiza.


Amesema kwa sasa DAWASA imewekeza kwenye miradi mikubwa na kupanua chanzo cha Maji cha Ruvu chini ambacho huzalisha lita milioni 270 kwa siku, ujenzi wa Bomba kubwa lenye urefu wa Kilometa 56 kutoka Ruvu Chini hadi matenki yaliyopo chuo Kikuu Ardhi jijini Dar es salaam.


Aidha amesema kwa upande wa Ruvu juu maboresho makubwa yamefanyika kwa kupanua mitambo ya uzalishaji ambayo sasa itazalisha lita milioni 196 kutoka milioni 82 kwa siku.


Ameongeza kuwa upande wa maeneo ya kaskazini na kusini mwa jiji la Dar es salaam kuelekea wilaya ya Mkuranga DAWASA inaendelea kuwekeza katika uchimbaji wa visima virefu vya maji na kuweka mifumo ya usambazaji wa maji ili kuwawezesha wananchi kupata maji safi na salama kwa gharama nafuu.


Kwa upande wake Mshauri wa Miradi ya Maji kutoka DAWASA BTC Bw. Manjolo Kambili amewaeleza viongozi hao kuwa wao kama viongozi wa Jumuiya za watumia maji wanatakiwa kufuata sheria na taratibu za Serikali kwa kuwa miradi hiyo ni ya Serikali.


Ameeleza kuwa jukumu la kusimamia na miradi hiyo liko kisheria hivyo viongozi hao wanapaswa kutekeleza kikamilifu majukumu yao likiwemo la kuhakikisha kuwa miradi yote inaajiri wahasibu wenye taaluma kwa lengo la kuandika na kutunza kumbukumbu za kila siku zinazohusu mapato na matumizi yao.


Naomba nisisitize katika hili, nyie mmepewa jukumu la kusimamia miradi ya maji ya Serikali, lazima mlitambue hili miradi yenu itakaguliwa na wataalamu ndio maana tuliwaomba muajiri wahasibu kwa kuwa vitabu vyenu vitakaguliwa kujua mwenendo wa mapato na matumizi yenu Amesisitiza.

Amewataka viongozi hao kuhakikisha kuwa kila mradi wa jumuiya unakuwa na akaunti ya Benki pamoja na kusimamia suala la utoaji wa risiti halali zenye nembo za jumuiya husika ili kuweka uwazi na imani wa walipiaji Ankara za maji.


Naye Afisa Uhusiano na Jamii wa Mamlaka hiyo Bi. Mecktridis Mdaku amewasisitiza viongozi hao kusimamia suala la Usafi wa mazingira, upandaji wa miti na utunzaji wa  vituo vya miradi, majengo na miundombinu ya maji ili kuwakinga wananchi dhidi ya magonjwa ya milipuko  ikiwemo. 


Ninyi kama viongozi wa Kamati za miradi ya maji lazima msimamie suala la usafi wa mazingira ili maeneo ya miradi yavutie pia kuwakinga wateja wenu na ugonjwa wa kipindupindu Amesisitiza Bi. Mdaku.Ametoa wito kwa viongozi hao kuepuka kuyatumia majengo ya miradi ya maji ya wananchi kwa shughuli nyingine  nje ya maji ikiwemo kuhifadhi na kufanyia biashara ya mkaa.  
MWISHO.
 

WANANCHI WA KATA YA NGURUKA WAHAMASISHWA KUJIUNGA MFUKO WA JAMII (CHF)

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii, Kigoma. 

MKUU wa Wilaya ya Uvinza,Mrisho Gambo amewataka Wananchi wa Tarafa ya nguruka kuchangia Mfuko wa afya ya jamii (CHF) ili kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao.

Hayo ameyasema  katika Mkutano wa hadhara wa kuzindua kampeni ya uhamasishaji wa  kuchangia mfuko CHF katika kata ya Nguruka  uliofanyika leo kwenye viwanja vya shule ya msingi Nguruka.

Gambo alisema kuwa katika hospitali ya Nguruka kuna changamoto kubwa ya upungufu wa dawa kutokana na hali hiyo aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia mfuko huo iliwaweze kuwa na uhakika wa  kupata dawa na matibabu matibabu mengine katika hospital yao.

"Ninawaomba ndugu  zangu changieni CHF ili muwe na uhakika wa matibabu mnapo umwa tambueni ugonjwa unapokuja huwa hauna taarifa unaweza kuumwa na mfukoni huna pesa lakini kama umechangia CHF utakuwa na uhakika wa matibabu"alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Alisema uongozi wa Wilaya ya uvinza una mpango wa kukiboresha kituo cha afya cha Nguruka  kutokana na ahadi ya Muheshimiwa Rais wakati wa kampeni kukifanya kituo hicho kuwa Hospitali ya Wilaya na maandalizi yanaendelea.

Naye Mkurugenzi wa mifuko ya jamii(CHF) kutoka makao makuu ya bima ya afya (NHIF) Eugen Mikongoti aliwataka wananchi kuchangia mfuko huo kwa wingi kwakuwa serekali nayo uwachangia kiasi kile kile walichochangia wao ambayo huitwa tele kwa tele.

Mikongoti alisema endapo wananchi watachangia kwa wingi na hudumaza afya  zitaboreshwa zaidi kituoni hapo. "Nataka niwaambie hivi sisi wote ni wagonjwa watarajiwa, hakuna anayejua atagua lini tunachotakiwa ni kujiandaa kwa kujiunga na CHF ili tuwe na uhakika wa matibabu tutakapi ugua"alisema Mikongoti

Kwa upande wake Meneja wa bima ya afya Mkoa wa Kigoma Elias Odhiambo alisema kuwa hali ya uchangiaji wa mfuko wa afya ya jamii kwa kata ya nguruka hairidhishi hivyo kushindwa kufikia malengo ya huduma za afya.

Alisema kata ya Nguruka ina jumla ya kaya 6000 lakini kaya 756 ndiyo zimejiunga na kuchangia CHF.

"Kutokana na uhamasishaji wa kujiunga na CHF tuliofanya leo hapa jumla ya kaya 868 zimejiunga na mfuko huo hapa hapa, kwakweli ni jambo zuri sana tuendelee kujiunga kwaajili ya uhakika wa matibabu pale tunapougua.
Mkuu wa Wilaya ya uvinza Mrisho Gambo akiwahamasisha wananchi wa kata ya Nguruka kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF) kwenye uzinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Nguruka
Mkurugenzi wa mifuko ya jamii kutoka makao makuu ya bima ya afya Eugen Mikongoti akiwahamasisha wananchi wa Nguruka kujiunga na mfuko huo.
Mkurugenzi wa mifuko ya jamii Eugin Mikongoti(mwenye koti jeusi) akiteta jambo na Meneja wa mfuko wa bima ya afya wa Mkoa wa Kigoma Elias Odhiambo wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wananchi kujiunga na CHF kata ya Nguruka.
Baadhi ya umati wa wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kuhamasisha kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF kata ya Nguruka.

Viewing all 46401 articles
Browse latest View live


Latest Images