Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

Lolensia Bukwimba:Tamasha la Pasaka ni furaha iliyoje

0
0
MBUNGE wa Busanda (CCM) LOLENSIA BUKWIMBA ameeleza furaha yake kwa kamati maandalizi ya Tamasha hilo ambalo halikuwahi kufanyika mkoani humo na imekuwa faraja kwake kama mwakilishi wa wananchi  wa mkoa huo  unaokabiliwa na mauaji kwa walemavu wa ngozi.

Alisema amefurahishwa  kufanyika kwa tamasha hilo mkoani Geita na mikoa mgine kwani ana imani wakazi wa mkoa huo watahamasika  kuacha mauaji ya Watanzania wasio na hatia ambao ni walemavu wa ngozi na vikongwe ambayo yanaendelea. Mbunge huyo anaelezea furaha yake, ana imani wananchi wa mkoa wa Geita watafurahi kwa sababu mkoa huo umesuswa kwa kuwapelekea matamasha ya namna hiyo na kusikia yanafanyika katika mikoa mingine kama Dar es Salaam na Mwanza.

“Nimefurahi sana Msama kulileta Tamasha hili litakalopiga vita mauaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi, nina imani wananchi wataweza kuelimika kwa njia moja au nyingine, baada ya hapo inawezekana kabisa likaweza kubadilisha fikra na mtizamo juu ya suala hili na kupunguza kabisa mauaji haya,” anasema Lolensia.

Alieleza kuwa limekuwa jambo la bahati kwa mkoa huo kufikiwa na tamasha hilo ambalo lina mafanikio makubwa katika kutimiza malengo yanayokusudiwa hivyo anaamini kilichokusudiwa kwa Geita kitafanikiwa kwa kiasi kikubwa. “Tunawakaribisha sana na nichukue nafasi ya pekee kumpongeza Msama kwa uamuzi wake wa kutuletea tamasha hili tunatarajia kupata mambo makubwa pia nina imani wanageita watafurahia mno kwasababu wanapenda mambo hayo ya muziki hasa huu wa Injili,” alisema Lolensia.

Aidha alifafanua kuwa ana uhakika wananchi watalifurahia na watafika kwa wingi na hata wale wa pembezoni mwa mji huo kwani kote huko wameathirika na mauaji. Lolensia alisema kuwa Msama sio kampuni ngeni masikioni mwake anaifahamu muda mrefu huku akisisitiza kuwa amewahi kuiandikia barua ya kuomba sapoti  kwa ajili ya watu wake wa jimbo, hivyo anafurahi kuwa Msama ameamua kwenda mwenyewe.


Kama kampuni ya Msama imeamua kuja Geita tunafurahi maana ataweza kutoa sapoti kwa njia hii maana wahitaji wako wengi ukizingatia eneo lenyewe linashughuli nyingi za kiuchumi” alisema.

Alizitaja baadhi ya shughuli hizo ni  pamoja na uchimbaji wa madini na kwamba watu wengi wanaingia na kutoka hivyo inasababisha wingi na watoto wanazaliwa kwa wingi ambako wazazi wao wanajishughulisha na shughuli za kiuchimbaji katika maeneo ya mbali na karibu.

Hivyo watoto hao wanakosa matunzo ya wazazi wao na kupelekea kuwa wa mitaani na wengine kujiingiza katika vitendo viovu . Alisema kwa mtazamo aliokuja nao Mwenyekiti wa Kamati Alex Msama ambaye pia  Mkurugenzi wa Msama Promotions  wa kusaidia jamii ya Geita anamuunga mkono ili aweze kuwafikia watu wengi zaidi.

Mbunge huyo wa CCM, alisema pengine kufanyika kila mwaka kwa tamasha hilo huenda huo ujumbe utaisaidia jamii kubwa hasa ile ilioingiwa na imani potofu ya kuuwa walemavu wa ngozi  pamoja na vikongwe. 

“Tunaomba kama Msama Promotions wameanza safari hii, basi isiwe mwisho iwe ni mwanzo kwa nia ya kuendeleza jitihada za kuelimisha jamii kadri tunavyopeleka ujumbe ndivyo itakavyowafikia wengi ukizingatia mkoa wetu unachangamoto nyingi.” alisema

TRA WAFUNGA MRADI WA MAFUNZO KATI YA TANZANIA NA JICA.

0
0
MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA(TRA) yafunga mradi wa miaka minne kati ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Shirika la  maendeleo la Japani (JICA) la Serikali ya Japani  mara baada ya  mradi huo kumaliza muda wake.

 Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurgenzi wa Rasilimali watu Mamlaka ya Matapo Tanzania(TRA), Victor Kimaro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa  Mradi huo umewanoa wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania pamoja na wanafunzi 608 na umeghalimu kiasi cha dola za kimarekani milioni3.5.

Pia amesema mradi huo wa Shirika la  Maendeleo la Japani (JICA) wa Serikali ya Japani umesaidia kuboresha mafunzo kwa  wafanyakazi na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).

Mwisho wa Mradi huo ni mwamzo wa kuanzisha mradi mwingine wa mafunzo na kuboresha ukusanyaji wa mapato hapa nchini.

Mradi uliokuwa unaitwa  'PROJECT FOR ENHANCEMENT OF TAXATION TRAINING IN TANZANIA.'
 Kaimu Mkurgenzi wa Rasilimali watu Mamlaka ya Matapo Tanzania(TRA), Victor Kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusina na kufunga mkataba wa miaka minne kati ya Tanzania na Japani mkataba ambao ulikua unatoa mafunzo ya kukusanya Kodi hapa nchini kwa wanafunzi wa chuo cha kodi (TRA) pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA). Kushoto ni  Msimamizi wa Mradi wa Shirika la  maendeleo la Japani (JICA), Toshio Nagase.
Msimamizi wa Mradi wa Shirika la  maendeleo la Japani (JICA), Toshio Nagase akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. kulia ni Kaimu Mkurgenzi wa Rasilimali watu Mamlaka ya Matapo Tanzania(TRA), Victor Kimaro.
 Mkuu wa Chuo cha Kodi (TRA), Isaya Jairo(Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kufunga mkataba wa mradi wa miaka minne ambao ulikuwa unatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na wanafunzi wa chuo cha kodi. Kulia ni Kaimu Mkurgenzi wa Rasilimali watu Mamlaka ya Matapo Tanzania(TRA), Victor Kimaro.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

MAKABIDHIANO YA UONGOZI WA MKOA WA DODOMA

0
0

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akitoa salamu zake wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa wa Dodoma baina yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe Mhe. Chiku Gallawa (hayupo pichani) Machi 22,2016.
 Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akitoa salamu zake wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa wa Dodoma baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (hayupo pichani) Machi 22,2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa huo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Chiku Gallawa (wa tatu kushoto) Machi 22,2016
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (wa kwanza kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa huo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Chiku Gallawa (wa tatu kushoto) Machi 22,2016.

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (wa kwanza kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa huo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Chiku Gallawa (wa tatu kushoto) Machi 22,2016.


 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (kulia) akisalimiana na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa huo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Chiku Gallawa (hayupo pichani) Machi 22,2016.
 Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma wakifuatilia hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa wa Dodoma baina ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Jordan Rugimbana na Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (hawapo pichani) Machi 22,2016.
 Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma wakifuatilia hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa wa Dodoma baina ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Jordan Rugimbana na Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (hawapo pichani) Machi 22,2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (kulia) na Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) wakitilianan saini hati za makabidhiano ya Uongozi wa Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla fupi iliyofanyika Machi 22,2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (kulia) na Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) wakibadilishana hati za makabidhiano ya Uongozi wa Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla fupi iliyofanyika Machi 22,2016.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akionesha juu hati za makabidhiano ya uongozi wa Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya makabidhiano baina yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe Mhe. Chiku Gallawa (hayupo pichani) Machi 22, 2016.

TASAF yatoa Milioni 137.8 kwa kaya masikini 57 Serengeti

0
0
   Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
 
MPANGO wa Kunusuru Kaya Masikini Tanzania  (TASAF III) umetoa zaidi ya shilingi Milioni 137.8 kwa kaya masikini 3627 katika vijiji 57 wilayani Serengeti mkoani Mara.
 
Hayo yamesemwa na Mratibu wa TASAF Wilaya ya Serengeti Bi Nancy Nzota alipokuwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Gesarya, Kata ya Rung’abure  kuhusu malipo ya kaya hizo kuwa yamefikia awamu ya tano.
 
Alisema malipo ya fedha hizo yameyotolewa katika kipindi cha utekelezaji wa mpango huo kwa mwezi Machi hadi Aprili 2016.
 
“Fedha hizi mnazopewa ni mbegu na mnapaswa kuzitumia kukidhi mahitaji muhimu yakiwemo ya elimu, afya na kuanzisha shughuli za uzalishaji” alisema Bi Nancy.
 
Bi Nancy aliongeza kuwa, watendaji wa vijiji wanatakiwa kubaini kaya zinazotumia fedha hizo kinyume na matakwa ya mpango huo ambapo amewataka watendaji watakaogunduliwa waondolewe katika uwakilishi wa kaya na mchakato wa kubadili wasimamizi/wawakilishi wapya wa kaya zao ufanyike kwa utaratibu maalumu.
 
Aliwaonya wanufaika wa mpango huo kutokutumia fedha hizo kwa shughuli zinazokinzana na mpango huo kwani kufanya hivyo hakutawatoa wananchi katika hali ya umasikini.
 
Alisema kuwa elimu hasa ya ujasiriamali ilishatolewa kwa wanufaika katika kila kijiji juu ya kuanzisha shughuli za ufugaji, kilimo na biashara ndogo ndogo.
 
Aliongeza kuwa pia elimu hiyo huendelea kutolewa mara kwa kwa mara na wawezeshaji wa mpango wa TASAF ambao hutoa elimu hiyo kwa wananchi katika kila awamu ya malipo.
 
Mpango huu ulizinduliwa mkoani Dodoma, Agosti 2012 na Rais mstaafu, Dk Jakaya Kikwete, ambapo kwa Wilaya ya Serengeti malipo kwa kaya masikini lilianza rasmi Julai 2015 na limeonesha kuanza kuzinufaisha kaya hizo.

KAMATI YA BUNGE YAIWEKA ‘KIPORO’ UDA

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
 
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) imesema suala la Shirika la Usafiri Mkoa  Dar es Salaam (UDA) wameliweka pembeni kutokana na baadhi ya wajumbe kubadilishwa katika kamati hiyo ikiwa ni pamoja na unyeti wa suala hilo kwa masilahi mapana ya wananchi wa jiji la Dar es Salaam.
 
Akizungumza leo Kaimu Makamu Mwenyekiti wa LAAC , Abdallah Chikota amesema kuwa wajumbe wapya lazima wasome taarifa  ya shirika hilo , ili waje na ushauri ambao utasaidia kumaliza suala hilo.
 
Amesema kuwa kamati itafanya kila jitihada za kukutana na jiji katika kuweza kushughulikia masuala mawili ambayo  ni UDA pamoja na Kiwanda cha Nyama yamekuwa yakileta matatizo kwa wananchi ya sitofahamu.
 
Aidha amesema kuwa suala hilo kuwa suala la wa UDA linatakiwa kila taarifa kutoka wadau mbalimbali ziweze kupitiwa katika kuweza kuepuka kufunguliwa kesi zisizo kuwa msingi.
 
Chikota ametaka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam irudishe ardhi ya kiwanda cha Nyama (Tanganyika Packers) katika mamlaka yake huku huku wakisubiri hatima ya kiwanda hicho.
 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amesema kuwa wanakubaliana na kamati kutokana na unyeti   wa  suala la Uda  kwa masilahi mapana kwa wananchi.
 
Simbachawene amesema wamechoshwa na suala la uda na Kiwanda cha nyama na kuahidi akipata muda atakutana na wadau ili kuondokana mlolongo wa kesi zitakazotokana na ufumbuzi wa UDA  na ufumkwa minajili ya kulinda masilahi ya wananchi wa jiji la Dar es Salaam.
 
Nae, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema kuwa yeye ni mgeni hivyo anahitaji kupata muda wa kusoma taarifa mbalimbali juu ya hoja ya UDA pamoja na suala la kiwanda cha Nyama.

SERIKALI KUIPIGANIA SHERIA YA WAZEE.

0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(Kulia) akionesha kitabu cha sera ya wazee ambayo inatarajiwa kuandikiwa mswaada wa kuwa sheria na kupelekwa Bungeni kushoto ni Katibu Mkuu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Sihaba Nkinga.
 2 Mwenyekiti wa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Hemed Mkali akizungumza katika kikao cha wazee wa mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy mwalimu(Kushoto).

Baadhi ya wazee wa mkoa wa Dar es Salaam wakifatilia kikao chao na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kilichofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.


Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
SERIKALI imejipanga kuipa nguvu Sera ya wazee nchini kuwa Sheria itakayowasaidia wazee kujikwamua katika changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa sasa.

Waziri Ummy amesema wazee wanakumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao ya kila siku nakusema kuwa azma ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wazee wanapata mahitaji yao muhimu ambayo ni huduma ya afya,haki ya kuwezeshwa kiuchumi na uwakilishi katika vyombo vya maamuzi.

“Mimi mwenyewe nalichukua jukumu hili la kufanikisha kuandikwa kwa mswaada wa Sheria ya wazee nchini na kuipeleka katika Bungeni mwezi Septemba ili tuwe na Sheria itakayowezesha kuwabana watu ambao watakaidi kutekeleza masuala yahusio wazee” Alisema Mhe.Ummy.

Naye mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Mzee Hemed Mkali akiwasilisha mada katika kikao hicho amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwajali na kuwapa kipaumbele wazee kwa kuwapa wizara ambayo itawasaidia kutatua changamoto zinazowakabili na wanaimani na Waziri husika na watashirikiana naye ili kufanya wazee wa Tanzania waishi katika maisha mazuri.

Aidha Waziri Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote nchini katika Hospitali zilizopo chini yao kuanzisha na kuboresha madirisha kwa ajili ya wazee na kuongeza kuwa huduma kwa wazee ni bure kuanzia kumwona Daktari, Vipimo mpaka madawa na kuhamasiha wazee kuungwa kwenye Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF) ambao unatoa huduma za afya katika maeneo mengi zaidi.

Kikao hiki cha wazee wa mkoa wa Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto dhumuni kubwa ni kwa wazee ni kuomba kukutana na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli  kujadili mshtakabali wa maendeleo ya wazee nchini.

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAONGEZA UFANISI WAKE NA USALAMA WA MATENGENEZO YA NDEGE ZAKE.

0
0
 Mhandisi wa Ndege akitumia mkebe wa vifaa uliokwisha unganishwa kwenye mfumo mpya mbele ya Ndege ya shirika la Etihad aina ya Airbus A330 ambayo ilikuwa inapitia marekebisho ya kawaida.
Wakisimama pembeni ya mikebe ya vifaa iliyounganishwa na mfumo mpya kwenye karakana ni (kutoka kushoto) Isam fares, Meneja GSE, Vifaa na maduka, Michael Adams, Makamu Rais MRO Services, Reinhard Luksch, Mkuu wa Vifaa na Utendaji Kitengo cha uhandisi wa matengenezo ya ndege cha Shirika la Ndege la Etihad.

SHIRIKA la ndege la Etihad kupitia idara yake ya uhandisi limeimarisha uwezo wake wa matengenezo ya ndege na mfumo mpya wa kujiendesha wenyewe moja kwa moja (ATC), mfumo ambao unasaidia wahandisi katika upatikanaji, utunzaji na ufuatiliaji wa vifaa huku ukipunguza uwezekano hatarishi wa zana kupotea katika mifumo muhimu ya ndege wakati wa matengenezo.

Mfumo huo ukiwa umeunganishwa na kituo kikuu cha mawasiliano kupitia njia ya mtandao na hivyo kuuwezesha kukagua zaidi ya matengenezo 15,000 yaliyofanyika, mfumo huu utaweza kutambua vifaa vilivyo potea, kuvunjika au vilive ambavyo havijarudishwa.

Mkebe wa vifaa hautoweza kufunguliwa mpaka mhandisi aonyeshe kitambulisho chake mbele ya kifaa maalumu ha kuhakiki kilichopo mbele ya mkebe huo wa vifaa. Kitambulisho kitasaidia kuhakikisha mhandisi anamamlaka ya kutumia vifaa ndani ya mkebe husuika na hivyo mkebe kufunguka. Mkebe huu wa vifaa unakuja na sehemu ya mhandisi kujaza matengenezo anayotakiwa kufanya (Idadi/Aina) pamoja na eneo la kazi.

Mfumo huu mpya ulipitia majaribio yenye mafanikio katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Abu Dhabi mnamo mwezi Novemba mwaka 2015, na ulikwisha sambazwa katika vituo vyote vya shirika la ndege la Etihad vya matengenezo mwezi Januari.

Karibu wafanyakazi 350 wamepata mafunzo juu ya mfumo mpya, na zaidi ya matengenezo 50,000 yamekwisha fanyika bila upotevu wa kifaa chochote cha ufundi.

Jeff Wilkinson, Makamu wa Rais, Etihad Airways, Ufundi, alisema: "Udhibiti wa vifaa ni swala muhimu kwa ajili ya mafanikio hasa pale tunapolenga kuboresha shughuli ya matengenezo ili kupunguza michakato ya kazi, kuongeza ufanisi na kuimarisha usalama.

"Kupitia mfumo mpya, wahandisi wetu ni wataweza kumaliza matengenezo haraka na kwa ufanisi, bila ya kuchukua hatua za ziada kufuatilia, kujiandikisha au kuangalia walipoacha vifaa wanavyotumia na hivyo kuokoa kwa kiasi kikubwa muda.”  

"Hii pia huongeza usalama kwani kifaa kilichopotea mikononi mwa mhandisi sio tu usumbufu bali kinageuka kuwa kifaa hatarishi kwa usalama wa mtu mwingine” aliongeza

Mfumo huu unawezesha mikebe yenye vifaa hadi 1,000 mbalimbali ndani yake pamoja mikebe mingine yenye na vifaa maalumu kwa ajili ya matengenezo ya umeme na uhandisi wa ndani ya ndege, kupangiwa mhandisi mwenye mamlaka husika aliyepangiwa kazi maalumu kwenye dege.

Kitengo cha uhandisi wa matengenezo ya ndege cha Shirika la Ndege la Etihad hivi sasa kina mikebe 32 ya vifaa vya matengenezo vinavyotumia mfumo huu mpya ndani yake, kati yake mikebe isiyopungua 20 huwa inatumika kwa wakati mmoja.  Mifumo iliyobaki itaunganishwa na kituo kikuu na hivyo kuwezesha mifumo hiyo kama inavyotakiwa ili kukidhi mahitaji ya timu matengenezo kama ndege inakuja katika kwa ajili ya matengenezo.

BASI SUPER SAMI LAANGUKA WILAYANI IGUNGA MKOA WA TABORA.

0
0
Ajali imetokea Wilayani Igunga ikihusisha basi la Super Sami lililokulikitokea Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam.

Chanzo cha ajali hiyo ni Dereva alipokuwa akitaka kukwepa Ng'ombe na  gari likamshinda na kuanguka na kusabaisha ajali hiyo.

Watu wakielekea kwenye gari lililopata ajali leo Wilayani Igunga.

WITO WA KUFANYA USAFI KITAIFA KILA JUMAMOSI YA MWISHO WA MWEZI.

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA.

Watanzania Wenzangu mtakumbuka kwamba tulikubaliana tuwe tunafanya usafi wa mazingira yetu nchi nzima kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kuitikia wito wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliouanzisha tarehe 09 Desemba 2015.

Nachukua nafasi hii kuwasihi Watanzania wote kushiriki kikamilifu kufanya Usafi wa Mazingira kwenye Makazi yetu, Maeneo yetu ya Biashara, maeneo ya Taasisi za Umma na maeneo yenye mikusanyiko ya watu mbalimbali kama masokoni na minadani.

Mbali ya kwamba kufanya usafi kuna fanya mazingira yetu yapendeze na hivyo kuondoa magonjwa yanayo sababishwa na uchafu lakini pia zoezi la kufanya usafi kwa pamoja lina jenga Umoja na Mshikamano wa kitaifa, linaondoa matabaka ndani ya jamii yetu. Natoa wito kwa kila Mtanzania Kujitokeza kufanya usafi bila kujali uwezo wa mtu,hadhi yake,cheo chake, au nafasi yake katika jamii. Viongozi wa makundi yote katika jamii tuwe mfano katika jambo hili jema.

Nichukue fursa hii kusisitiza tuendelee kujitokeza
kufanya Usafi ili Utamaduni huu ujengeke kwa Kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

Watanzania wote wa Mijini na Vijijini tujenge desturi ya kuweka mazingira yetu katika hali ya usafi wakati wote na katika jambo hili kila mmoja wetu awe mlinzi wa kukemea watu wenye tabia za kutupa taka hovyo ili maeneo yetu yawe katika hali ya usafi na yakuvutia wakati wote. 

Usafi kwenye nyumba na mazingira yako,Usafi kwenye sehemu ya Shughuli zako na mazingira yake ndio usafi wa Taifa. Tujitokeze,Tuungane tukafanye Usafi kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi kuanzia saa 12 Asubuhi
Asanteni.
Imetolewa na:
George B. Simbachawene (Mb)
WAZIRI WA NCHI
OFISI YA RAIS - TAMISEMI

ACT WAZALENDO WAMTAKA SPIKA WA BUNGE KUSHUGHULIKIA SUALA LA RUSHWA KWA WABUNGE WALIOTUHUMIWA.

0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa, wa ACT Wazalendo, Yeremia Maganja akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Chama cha ACT Wazalendo wakimtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda mara moja kamati ya uchunguzi kwa kamati zote zilizotuhumiwa ili ukweli ubainike na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mawasiliano wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu.
 Katibu Mawasiliano wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu akisisitiza jambo katika mkutano  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa wa ACT Wazalendo, Yeremia Maganja.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa wa ACT Wazalendo, Yeremia Maganja leo  Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
CHAMA cha ACT Wazalendo kimepokea kwa masikitiko uamuzi uliofanywa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, kwa kuhamisha kamati, Wenyeviti, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa baadhi ya Kamati za Kudumu za Bunge uliofanywa jana.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa ACT Wazalendo, Yeremia Maganja,
amesema uamuzi huu wa spika unafuatia kashfa nzito ya viongozi na wajumbe wa kamati mbalimbali za Bunge kupokea rushwa kutoka mashirika tofauti ya umma kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari

Amesema bunge ni mhimili wenye jukumu la kuisimamia serikali , hivyo baadhi ya wabunge akiwemo Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) walimwandikia barua za kujiuzulu Spika wa Bunge, Job Ndugai ili kupisha uchunguzi ufanyike na wataobainika kupokea rushwa kuchukuliwa hatua za kisheria.

Maganja amesema ACT Wazalendo imempongeza Mbunge wao na Wabunge wengine waliochukua hatua ya kujiuzulu ujumbe kwenye kamati zao ili kupisha uchunguzi.

Aidha amesema kuwa uamuzi huo wa mbunge wao unakwenda sambamba na misingi ya Chama cha ACT Wazalendo ya uadilifu na uwajibikaji.

Amesema mabunge yaliyopita, kamati za Bunge zimekuwa zikituhumiwa mara kadhaa kujihusha na vitendo vya kupokea rushwa kutoka kwa Mashirika ya Umma, Makampuni na watu binafsi.


Maganja amesema rai zimekuwa zikitolewa mara kwa mara huko nyuma ya kuitishwa kwa uchunguzi ili kulinda hadhi na heshima ya Bunge ilipuuzwa na matokeo yake, kashfa hizi zimeliondolea heshima Bunge na Wabunge.

Amesema kwa mujibu wa Ibara ya 63(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bunge ndiyo chombo kikuu chenye madaraka kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri serikali na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake. Kinapotuhumiwa kupokea rushwa, kinawezaje chenyewe kuisimamia serikali na kuongoza mapambano dhidi ya rushwa?

Maganja amesema uamuzi wa kuwahamisha Kamati viongozi na wajumbe wa Kamati zilizotuhumiwa kupokea rushwa ni sawa na kuufunika uozo na kuendeleza utamaduni mbovu wa siku nyingi hapa nchini wa kuwahamisha au “kuwapangia kazi nyingine” viongozi na watumishi wa umma wanaotuhumiwa kupokea rushwa au kukosa ufanisi. Kimsingi Utamaduni huu unafifisha mapambano dhidi ya rushwa na uwajibikaji.

Mwenyekiti huyo amemtaka Spika kuonyesha kwa vitendo jinsi ofisi yake inavyochukizwa na vitendo vya rushwa nchini kwa kuitisha uchunguzi utaovishirikisha vyombo vya dola ili ukweli ujulikane.

BAYPORT YAKABIDHI HATI ZA VIWANJA VYA VIKURUTI.

0
0
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo imekabidhi hati za viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa baadhi ya wateja waliomaliza kulipa mikopo yao tangu walipochukua mikopo hiyo yaa viwanja mapema mwaka jana. 

Baadhi ya wateja waliokabidhiwa hati hizo ni pamoja na Desidery Didas Kalimwenjuma wa Temeke na James Moses Lubinza wa Kimara jijini Dar es Salaam, huku hati za wateja wengine zikiwa zimekaamilika kwa ajili ya kukabidhiwa wateja hao ambao walikuwa miongoni mwa Watanzania waliochangamkia fursa ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti, vilivyokuwa vinauzwa na Bayport kwa kushirikiana na Kampuni ya Property International Ltd.
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed (kushoto), akishuhudia bwana James Moses Lubinza akitia sahihi katika tukio la upewaji wa hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani leo mchana, jijini Dar es Salaam. Lubinza alikuwa miongoni mwa Watanzania waliochangamkia fursa ya mikopo ya viwanja vya Bayport. Huduma hizo za viwanja mwaka huu zinaendelea kwa kuanzishwa miradi ya Bagamoyo, Kigaamboni, Chalinze, Kibaha na Kilwa vikuhusisha watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali. Picha kwa hisani ya Bayport Financial Services.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services Ngula Cheyo katikati akikabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti kwa mteja wao James Moses Lubinza leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Sheria wa Bayport, Mrisho Mohamed.
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services Mrisho Mohamed kushoto akiangalia mteja wao Desidery Didas Kalimwenjuma wakati anatia sahihi katika makabidhiano ya kupewa hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services Mrisho Mohamed kushoto akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti mteja wao Desidery Didas Kalimwenjuma.
Mwanasheria wa Bayport Financial Services Mrisho Mohamed kushoto akipiga picha ya pamoja na mteja wao Desidery Didas Kalimwenjuma baada ya kumkabidhi hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha mkoani Pwani leo mchana.

Akizungumza leo mchana katika makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo, alisema ni furaha yao kubwa kuanza kutoa hati ya viwanja vilivyouzwa kwa baadhi ya Watanzania walioamua kuchangamkia fursa za viwanja vyao. Alisema hatua hiyo ni sehemu muafaka ya kuhakikisha kwamba viwanja hivyo vilivyopimwa na vyenye hati vinakuwa sehemu ya kuendeleza na kusaidia wananchi ambao kwa kupitia viwanja hivyo wanaweza kuvitumia katika fursa mbalimbali kama vile mikopo, kujenga nyumba za biashara na makazi ya kuishi wao na familia zao.

“Hii ni hatua muhimu kwetu Batyport kuona viwanja vya Vikuruti vimeanza kutoka kwa hati zao na kuona kila aliyepata kiwanja basi hatakuwa na usumbufu wowote wa kupewa hati yake, iwe kwenye mradi wa Vikuruti au maeneo mengine ya Tanzania tunayoendelea na biashara ya kuuza viwanja kwa njia ya fedha taslimu na mkopo.

“Tunawahakikishia usalama na huduma bora kabisa kutoka kwetu Bayport, tukiamini kwamba viwanja vyenye hati tunavyotoa ni maeneo mazuri na yanayoweza kujibu maswali rahisi ya Watanzania wote kuweza kumiliki ardhi kwa utaratibu rahisi na mzuri,” alisema Cheyo.
Akizungumza baada ya kupewa hati yake, Kalimwenjuma alisema anashukuru kwa kupata hati yake haraka bila usumbufu wowote, hali inayoonyesha umakini mkubwa uliokuwapo kwenye huduma hiyo ya mikopo ya viwanja vya Bayport. “Nashukuru kwa sababu nilikuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza kununua viwanja vya Bayport na leo nimepigiwa simu kwa ajili ya kukabidhiwa hati yangu huku nikiwa na furaha kubwa pamoja nja kuwapongeza mno kwa huduma bora,” Alisema.

Naye Lubinza alisema hajawahi kukutana na huduma bora za viwanja kama vya Bayport kwa sababu havina longolongo wala usumbufu wowote, jambo linaloonyesha utulivu na umakini uliozalisha kupewa hati yake haraka bila tatizo. “Ni maendeleo makubwa kwa kuwekeza fedha zangu kwa kununua viwanja vya Vikuruti nikiamini kuwa ardhi ni kitu kinachopanda thamani siku hadi siku, huku nikifurahia zaidi kwa sababu ni miongoni mwa Watanzania waliopewa hati na Bayport,” Alisema.

Maeneo mengine ya Tanzania ambayo Bayport inatoa mikopo ya viwanja ni pamoja na Bagamoyo (Kimara Ng’ombe), Kibaha (Boko Timiza), Kilwa (Msakasa), Kigamboni (Tundi Songani) na Chalinze katika maeneo ya (Kibiki na Mpera), ambayo Watanzania wote wakiwamo watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali wanaweza kupata fursa ya kukopeshwa viwanja hivyo vilivyopimwa na vyenye hati na kuidhinishwa na mamlaka zote za Serikali kupitia kwa wabia wao wa kibiashara.

Kwa viwanja vinavyoendelea kukopeshwa, wilayani Kilwa eneo la Msakasa kilomita moja ya mraba inauzwa kwa Sh 2000, Chalinze ni Sh 4500, Bagamoyo Sh 10,000, Kigamboni Sh 10,000 na Kibaha mkoani Pwani mita ya mraba itapatikana kwa Sh 9000.

MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI KWA MWEZI MACHI NI ZAIDI YA TILIONI 1.4.

0
0
 Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Philip Mpango akizungumza na waandishi wa habari mda mfupi uliopita katika ukumbi wa mikutano wa wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwezi Machi mwaka huu, ambapo Mapato ya Kodi (TRA) shilingi 1,283,274,000,000. Mapato yasiyo ya kodi ni shilingi 77,504,000,000. Mapato yatokanayo na vyanzo vya halmashauri ni shilingi 43,490,000,000 Jumla ikiwa ni 1,404,268,000,000. Pia amesema kuwa Serikali inatarajia kupata mikopo na misaada ya mifuko ya Basket na Miradi ya maendeleo kutoka kwa washirika wa maendeleo shilingi 71,200,000,000.
 Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Philip Mpango akizungumza na waandishi wa habari mda mfupi uliopita jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ashantu Kijaji akiwa katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

UFAFANUZI WA
MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI KWA MWEZI MACHI, 2016


A:  MAPATO 
(i)                 Mapato ya kodi (TRA) shilingi 1,283,274,000,000

(ii)                Mapato yasiyo ya kodi shilingi 77,504,000,000

(iii)              Mapato yatokanayo na vyanzo vya Halmashauri shilingi 43,490,000,000

Jumla shilingi 1,404,268,000,000

(iv)              Tunatarajia pia kupata mikopo na misaada ya mifuko ya Basket na miradi ya maendeleo kutoka kwa washirika wa maendeleo shilingi 71,200,000,000


B: MATUMIZI


1.  Mishahara
(a)        Watumishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa shilingi 484,057,177,680 ikijumuisha malimbikizo ya shilingi 9,479,389,384 na hasa kwa walimu katika Halmashauri 154


(b)        Watumishi wa Taasisi na Wakala za Serikali shilingi 97,985,822,320 ikijumuisha malimbikizo ya shilingi 518,822,320 kwa Taasisi na Wakala 24 na hasa sehemu kubwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Jumla ya mishahara ni shilingi 582,043,000,000

  
2.           Posho ya chakula kwa ajili ya vyombo vya ulinzi na usalama shilingi 43,556,500,000.
3.         Ruzuku ya Vyama vya Siasa shilingi 1,433,583,000
4.         Posho ya Madaktari wanafunzi 1608 shilingi 1,721,000,000.
5.         Wizara ya Afya Ununuzi wa madawa na vifaa tiba shilingi 2,597,961,000
6.         Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa semista ya tatu shilingi 57,040,000,000
7.         Kutekeleza mpango wa Elimu bure shilingi 18,777,000,000
8.         Mapato ya ndani kwa Halmashauri kwa ajili ya miradi na uendeshaji wa ofisi shilingi 43,490,000,000
9.         Madeni ya watumishi wasio walimu katika Halmashauri  shilingi 3,618,900,612
10.      Miradi ya umeme shilingi 73,252,000,000
-            Wakala wa Umeme Vijijini shilingi 24,020,000,000

-            Mradi wa Umeme Kinyerezi I shilingi 43,800,000,000


-            Mradi wa kufua umeme makambako – Songea shilingi 5,482,000,000


11.      Malimbikizo ya madeni ya Makandarasi wa barabara shilingi 166,905,919,730
12.      Miradi ya Maji shilingi 10,951,000,000
13.      Mfuko wa Reli shilingi 2,651,000,000
14.      Fidia kwa wananchi kupisha mradi wa Kurasini Trade and Logistic Hub shilingi 3,048,904,930
15.      Mradi wa Ununuzi wa dawa na vifaa Tiba (ORIO) shilingi 2,106,657,644

16.      Mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo shilingi 5,124,997,500

PROFESA MUHONGO APOKEA RIPOTI YA NYAMONGO

0
0
Mwenyeki wa kamati John Nayopa akimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo,Taarifa ya kamati ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa Nyamongo na Kampuni ya mgodi wa dhahabu ya Acacia North Mara.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo,akionesha taarifa aliyokabidhiwa na Kamati hiyo ambapo ameahidi kuisoma na kuitolea majibu yanayostahili ndani ya kipindi cha wiki tatu tangu Machi 23,2016 alipokabidhiwa taarifa hiyo.
Sehemu ya wajumbe kutoka Serikali za vijiji wakisikiliza taarifa ya kamati ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa North Mara katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara na Mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia wa North Mara, kutoka Serikali ya kijiji.
Sehemu ya ya wanakamati wakisikiliza taarifa ya utekelezaji kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa North Mara katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara na Mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia wa North Mara.
Sehemu ya ya wanakamati wakisikiliza taarifa ya utekelezaji kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa North Mara katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara na Mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia wa North Mara.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, akizungumza jambo mara baada ya kupokea Taarifa ya utekelezaji kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa North Mara katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara na Mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia wa North Mara.
Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Nyamongo na Kampuni ya mgodi wa dhahabu ya Acacia North Mara, John Nayopa, akisoma taarifa ya utekelezaji wa kamati hiyo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini( hayupo pichani)
Meza kuu ikimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati( hayupo) akitoa taarifa ya utekelezaji ya Kamati ya kushughulikia mgogoro kati ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa North Mara katika eneo la Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara na Mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia wa North Mara, kutoka kushoto waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga, Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche.

Na Zuena Msuya

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amepokea ripoti maalumu ya kumaliza mgogoro wa wananchi wa Nyamongo na mgodi wa wa dhahabu wa Kampuni ya Acacia North Mara uliodumu kwa miaka 6 sasa.
Akizungumza mjini Tarime Mkoani Mara baada ya kupokea ripoti hiyo Prof. Muhongo ameshauri wananchi wa Tarime kuwa watulivu wakati akiendelea kuisoma ripoti hiyo na kutolea majibu mambo yalioyo andikwa katika riporti hiyo.
Profesa Muhongo alisema anaimani mambo yote yalioandikwa katika ripoti hiyo ni mawazo ya wananchi waliohojiwa na atashangaa endapo kuna mtu atajitokeza kuikataa.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya Tarime,Glorious Luoga alisema ripoti hiyo itatoa majibu stahiki kwa wanaohitaji kulipwa na hata wasiostahili hivyo wananchi wakae tayari kupokea utekelezaji wa ripoti baada ya kusoma na kupitishwa na Waziri.

Naye Mbunge wa Tarime vijijini John Heche alisema kuwa anaimani na ripoti hiyo kuwa itatenda haki kwa wananchi wake wa Nyamongo ili kutimiza ahadi ya Rais aliyoitoa wakati akiomba kura kuwa hatamaliza kabisa tatizo la Nyamongo lililodumu kwa muda mrefu.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhandisi John Nayopa alisema kamati hiyo imepokea malalamiko zaidi ya 4400 ya wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi,malalamiko ambayo yalilenga masuala ya fidia ya ardhi,athari za shughuli za mgodi hasa upande wa mazingira,uvamizi wa mgodi,sakata la tegesha na Askari kutuhumiwa na kunyanyasa na kutesa wananchi.

Kamati hiyo iliundwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mwezi mmoja uliopita ina wajumbe 27,19 wataaalamu wa Serikali, na Wenyeviti wa vitongoji 80.

MAJALIWA AKUTANA NA WAWEKEZAJI WA SUKARI KUTOKA INDIA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na ujumbe wa Wawekezaji kutoka India wanaokusudia kuwekeza katika kilimo cha miwa na kiwanda cha sukari hapa nchini, Ofisini kwake jijini Dar es salaam machi 23, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Kilimo, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na ujumbe wa Wawekezaji kutoka India wanaokusudia kuwekeza katika kilimo cha miwa na kiwanda cha sukari hapa nchini, Ofisini kwake jijini Dar es salaam machi 23, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Kilimo, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

TCRA YAWATAKA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO SEHEMU HUSIKA.

0
0
Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka wananchi wenye malalamiko yanayohusu huduma zitolew azz na makampuni ya simu kutosita kupeleka malalamiko yao kwenye makampuni husika.

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam katika mahojiano maalumu alipokua akijibu swali kuhusu malalamiko ya wananchi juu ya huduma zinazotolewa na makampuni mbalimbali ya simu hapa nchini.

Amesema mteja ana wajibu wa kujua matumizi na gharama za huduma za mitandao anazotumia pia ana haki ya kutoa malalamiko kwa kampuni husika ili aweze kupatiwa majibu na endapo hatasikilizwa anaruhusiwa kuwasiliana malalamiko yake Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

Bw. Mungy ameongeza kuwa,wananchi wanaweza kufikisha malalamiko yao TCRA kwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0784558270 au barua pepe;malalamiko@tcra.go.tz na malalamiko hayo yatafanyiwa kazi haraka.

Aidha, amefafanua kwamba,TCRA haipangi bei elekezi kwa makampuni hayo hivyo gharama za mawasiliano ziko kwenye mifumo mbalimbali kutegemeana na gharama za uendeshaji wa huduma kwenye kampuni husika. “Mwananchi halazimishwi kutumia huduma ya mtandao mmoja wa simu ana uhuru wa kuchagua na kutumia mtandao wowote wenye unafuu kwake” Amesisitiza.

Amewaomba wananchi waelewe kwamba soko la makampuni ya simu limekuwa na ushindani mkubwa jambo linaloyalazimisha makampuni yanayotoa huduma kubuni ofa mbalimbali kwa lengo la kuvutia wateja. “ Sasa hivi soko la makampuni ya simu limekuwa na ushindani mkubwa nchini, jambo linalofanywa na makampuni hayo ni kuweka ofa mbalimbali ambazo hizo huwasaidia wananchi kupunguza gharama za matumizi ya simu”

TRL KUSAFIRISHA SARUJI YA TANGA KWA NJIA YA RELI

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (kushoto) wakisaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza. Huku Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakishuhudia.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (kulia) kabla ya kusaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo baada ya kusaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart na (Kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akisaidiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa pili kulia) wakipakia mfuko wa saruji kwenye kontena kabla ya kuanza kusafirishwa kwa njia ya reli kutoka katika kiwanda cha Simba Cement kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela akitoa taarifa ya hali ya miundombinu katika mkoa wa Tanga kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ofisini kwake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa pili kulia) akimwonesha moja ya nyaraka Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (wa pili kushoto) kabla ya kusaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa tatu kulia) pembeni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa.

……………………………………….

Kiwanda cha Saruji Tanga (Simba Cement), kimeingia makubaliano na Shirika la Reli Tanzania (TRL), kusafirisha shehena ya saruji kwa njia ya reli kutoka mkoani Tanga kwenda mikoa ya Mwanza na Kigoma.

Chini ya Makubaliano hayo zaidi ya tani laki nne na nusu zitasafirishwa kwa mwaka na hivyo kupunguza gharama ya bei ya Saruji katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Magharibi kutokana na usafirishaji wa reli kuwa wa bei nafuu.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema katika mkataba huo TRL litapata zaidi ya shilingi Bilioni 40 na hivyo kufufua huduma ya usafirishaji wa mizigo katika reli ya kati na kuongeza mapato kwa nchi.

Prof. Mbarawa amewataka wafanyabiashara nchini kuanza kutumia reli kusafirisha bidhaa zao, kwani usafiri huo ni salama na nafuu na unachukua shehena kubwa kwa wakati mmoja.

“Asilimia 95 ya mizigo hapa nchini inasafirishwa kwa barabara hivyo mkakati wa Serikali wa kufufua viwanda utafanikiwa kwa haraka endapo wasafirishaji watatumia njia ya reli “, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, amefafanua kuwa usafirishaji wa reli ukiimarika utapunguza ajali za barabarani zinazosababishwa na malori na kupunguza kasi ya uharibifu wa barabara unaotokea sasa kutokana na maroli kuzidisha uzito.

Prof. Mbarawa amewataka watumishi wa TRL na wananchi kulinda miundombinu ya reli na kutumia fursa ya usafiri huo kujiongezea mapato.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela amesema usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli utatoa fursa za ajira na kuwezesha bandari ya Tanga kupata shehena kubwa ya mizigo na hivyo kurudisha hadhi ya Mkoa wa Tanga.

“Tanga tuna reli, barabara na bandari hivyo tukio la kuanza kusafirisha mizigo kwa njia ya reli itaongeza shehena kubwa katika bandari ,itatengeneza ajira kwa wakazi wa Tanga na kukuza uchumi wa mkoa”, amesema Bw. Shigela.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRL) Bw. Masanja Kadogosa amesema kusainiwa kwa mkataba huo kutawezesha TRL kusafirisha tani elfu thelathini na tano za Saruji kati ya tani laki moja na elfu tano zinazozalishwa na kiwanda hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji Tanga Bw. Reinhart Swart, amesema usafirishaji wa Saruji kwa njia ya reli utaongeza kasi ya usafirishaji wa saruji na kuwezesha kuwafikia watumiaji kwa bei nafuu.

Kiwanda cha Saruji Tanga kinakuwa kiwanda cha kwanza kuingia mkataba na TRL kusafirisha shehena ya mizigo tangu Serikali kuanza mikakati yake ya kufufua reli na kupunguza usafirishaji wa shehena kubwa kwa njia ya barabara na hivyo kuzuia uharibifu wa barabara na kupunguza ajali.

UZINDUZI WA MRADI WA USAID WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA WAFANYIKA MKOANI DODOMA

0
0
RC wa Dodoma, Jordan Rugimbana, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3
RC wa Dodoma Jordan Rugibana akiteta na Mkuturenzi wa Mradi wa PS3, Dk. Emmanuel Malangalila, wakati wa uzinduzi
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Dodoma wakifuatilia mada wakati wa uzinduzi wa Mradi wa PS3 mkoani humo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia majadiliano wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Dodoma
Dk. Conrad Mbuya wa PS3 akitoa mada wakati wa uzinduzi wa mradi mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Mradi wa PS3, Dk. Emmanuel Malangalila, akitoa mada kwenye uzunduzi wa mradi wa PS3 mkoani Dodoma
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais (Utumishi) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3
Matiko Machonchoryo wa PS3 akitoa mada wakati wa uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Dodoma
***************
Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Dodoma siku ya Jumanne na Jumatano, Machi 22-23, 2016. 


Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 97 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.


PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji.  Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na  Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.

Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana, na uzinduzi ulihudhuriwa pia na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Dodoma ambaye amehamishiwa mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.  Watu takribani 180 walihudhuria.  Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Dodoma, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe  wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri. 

Mkoa wa Dodoma una Halmashauri  nane, ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, na Halmashauri ya Mji wa Kondoa.


PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID.  Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni:  Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute. 


Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.


PS3 itaimarisha mifumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri. Mradi utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania.  Mafanikio yanayotarajiwa ni pamoja na:


·   Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Raia: Uimarishaji wa utawala katika ngazi ya kitaifa na ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ili kuweza kutumia rasilimali kwa uwazi, kuwezesha ushiriki wa wananchi katika kupanga, kufuatilia, na kutoa matokeo katika kila sekta.


·   Rasilimali Watu: Kuongezeka kwa usawa katika mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji wa huduma bora kwenye maeneo yenye uhitaji zaidi.  Kuimarisha mfumo wa ajira pamoja na kudumu kwa watumishi katika ajira serikalini.


·   Fedha: Ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma, kuongeza ufanisi  katika matumizi ya fedha za umma, na pia kuongeza uwiano kati ya kiasi cha fedha kilichotumika na mali iliyonunuliwa.


·   Mifumo ya Mawasiliano: Kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa iliyopo nchini, pamoja na matumizi ya takwimu kwa wadau.


Utafiti Tendaji: Tafiti Tendaji muhimu zitakazosaidia mradi kujua changamoto na mikakati ya kuzishughulikia changamoto hizo. Tafiti hizi zitasaidia kugundua fursa zilizopo na kuzitumia kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa.  Pia tafiti hizo zitasaidia kuboresha maamuzi serikalini.                

MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KINONDONI AZINDUA RASMI UGAWAJI WA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE NA VIJANA

0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob leo amezindua rasmi ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 zinazotarajia kupata Tsh 200,000,000/= kila Kata ifikapo julai, 2016.

Hadi sasa Manispaa ya Kinondoni imepeleka katika Benki ya wananchi ya Dar es Salaam, (DCB) Jumla ya Tsh 855,003,614017 kwa ajili ya mikopo ya wanawake na vijana ambapo ifikapo julai 2016 ambao ni mwisho wa Mwaka wa fedha 2015/2016 zitafikia zaidi ya Tsh 4.5 billion ambayo ni sawa na asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Manispaa ya Kinondoni kwa mujibu ya magizo ya Bunge.

Benki ya wananchi wa Dar es salaam,Tawi la Magomeni imefungua vituo 36, vya kuratibu shughulii za Mikopo ya vikundi vya wanawake na vijana katika maeneo mablimbali ya Kata za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma za mikopo hiyo kwa karibu.

Vikundi vilivyonufaika katika uzinduzi wa leo na kiasi cha fedha kilichotolewa:-
Stopover tsh 8,750,000/= kwa ajili ya biashara ya sabuni za Maji na Miche
Makabe tsh 5,250,000/= kwa ajili ya biashara ya utengenezaji wa sabuni na uuzaji wa Mkaa.
Mbezi luis, Tsh 7,000,000/= kwa ajili ya Nursery School, Tigo pesa, Mpesa.

Kilungule tsh 2,000,000/= kwa ajili ya Biashara ya Mitumba, genge na Saloon.
Kigogo tsh 10,000,000/=kwa ajili ya biashara ya Mama lishe, Saloon ya Kike na Kiume.

Aidha Mstahiki Meya amewataka wanawake na Vijana kujitokeza kwa wingi ili wapatiwe mafunzo na kupewa Mikopo kwa fedha zilizopo Benki na zile zinazoendelea kupelekwa kwa lengo la kuwawezesha wanawake na vijana kupata mikopo kwa utaratibu wa kuwashirikisha viongozi na watendaji ngazi ya Mitaa na Kata.
Imetolewa na:-
MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA KINONDONI
23/03/2016.
meya wa KinondoniMstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akizindua rasmi ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 Manispaa hiyo ya Kinondoni mapema leo.
a34feb2b-c375-4d48-baa9-2eec5d83537dBaadhi ya washiriki wakiifuatilia uzinduzi huo wa ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 Manispaa hiyo ya Kinondoni mapema leo
f5e6ac68-e0d5-46dd-b161-678ed2a77369Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akikabidhi moja ya hundi hiyo zilizozinduliwa rasmi wa ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 Manispaa hiyo ya Kinondoni mapema leo
d14600e6-34f1-4307-9900-d932dc726655Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akikabidhi moja ya hundi hiyo
c298a1b3-54db-422f-8389-dd914fbba4d4Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akikabidhi moja ya hundi hiyo

MIONGOZO RAHISI YA USIMAMIZI SHIRIKISHI NA UVUNAJI MISITU KATIKA VIJIJI YAZINDULIWA RASMI

0
0
Kampeni ya Mama Misitu (MMC) kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii Machi 23, 2016 imezindua miongozo miwili rahisi ya usimamizi shirikishi wa misitu kwa pamoja na uvunaji katika misitu ya hifadhi ya jamii.

Miongozo hiyo ambayo imetokana na miongozo ya Kiingereza ambayo awali ilichapishwa na Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2013, inalenga kurahisisha kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya uhifadhi na uvunaji wa rasilimali za misitu kuanzia ngazi za taifa hadi kwa wananchi wenyewe.

Meneja wa kampeni hiyo Gwamaka Mwakyanjala anasema iliwalazimu kuiweka miiongozo hiyo katika lugha rahisi ya Kiswahili ili kuwezesha wananchi kuelewa na kuchukua hatua. “Miongozo ya awali ilikuwa katika lugha ya kingereza na hivyo kukwaza zoezi la uelimishaji kwa wananchi, tunaamini kwa kutumia miongozi hii iliyo kwenye lugha ya Kiswahili ujumbe utafika kwa walengwa na kampeni yetu itafanikiwa pia” anasema Gwamaka.

Uzindui huo ambao ulifanywa chini ya Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) ulihudhuria na wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, viongozi mbalimbali kutoka taasisi za serikali na mashirika binafsi.
Meneja wa kampeni ya Mama Misitu, Gwamaka Mwakyanjala (katikati) akionyesha miongozo hiyo kwa waandishi wa habari, kulia kwake ni Mratibu wa Ukaguzi na Tathmin wa Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), Wilbard Mkama na kushoto kwake ni Mratibu Kikundi Kazi Misitu Tanzania, Cassian Sianga.
Balozi wa Kampeni ya Mama Misitu, Asha Salimu alizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa miongozo hio
Mkurugenzi wa Shirikisho la Viwanda vya Misitu Tanzania na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF),  Ben Mfungo Sulus akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa miongozo hiyo

 Wadau wa Misitu wakifuatilia mkutano huo
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), John Chikomo akizungumza juu ya umuhimu wa wanahabari katika kutoa elimu ya mazingira
 Picha ya pamoja

WAOMBA SEREKALI KUANGALIA KWA UNDANI MAHABUSU YA WATOTO ARUSHA

0
0
kutoka Kulia Phidesia Mwakitalima,  katibu wa Jumuiya ya wazazi   ccm wilaya Arusha  Rehema mohamed , Augustino Masawe wawakilishi kamati ya utekelezaji wazazi wilaya ya Arusha wakiwa na Afisa ustawi wa jamii jiji la  Arusha  Mussa mkamate katika mazungumzo juu ya Mahabusu ya watoto Arusha.
picha ikionyesha uchakavu wa vyoo vya mahabusu ya watoto Arusha pamoja na pakti za viroba ambavyo wanakunywa kisiri  siri na kuletewa kinyemela na vijana wa mtaani kutokana na kukosa ulinzi  kwa mahabusu hayo pia kukosekana kwa uzio katika magereza hiyo ya watoto , na imeonekana pia kuna matundu ya mapaa  ya mabati ambayo ayapo pichani Matundu ambayo yamechakaa yanatumika na watoto hao kama  njia ya kutorokea nje ambapo  mara kadhaa  hukamatwa wakiwa wanatoroka na kurudishwa ndani



Na Woinde Shizza,Arusha


Kamati ya utekelezaji Jumuia ya wazazi wilaya ya Arusha  inatarajia kutembelea  mahabusu ya watoto Arusha  katika kuazimisha sherehe ya wiki ya wazazi Tanzania inayofanyika kila april 2 kila mwaka .


Katika maazimisho hayo pia kamati hiyo imejipanga kukarabati baadhi ya miundo mbinu ya kituo cha mahabusu ya watoto iliyopo jijini hapa .

Akizungumzia maadhimisho hayo katibu wa jumuiya ya wazazi  CCM wilaya ya Arusha  Rehema Mohamed alisema  wao kama wazazi wamegundua kuna changamoto nyingi katika mahabusu ya watoto mkoani Arusha ambazo wazazi kama walezi wameona ni vyema kutembelea mahabusu ya watoto kuwaona    na kuwapelekea chochote kinachopatikana .



Alisema kuwa wanajaribu pia  kutatua changamoto nyingi wanazokabiliana nazo ili kuweza kuwasaidia watoto hao nao waishi kama watoto wengine walioko majumbani .



 “kwa kweli natoa wito kwa wazazi wote watakaoguswa Arusha kujumuika nasi tar 2 mwezi wa nne kuanzia saa 3kamili asubuhi  kwani watoto wengine wazazi wao wamewatelekeza kabisa na wengine hawana wazazi kabisa”alisema  Rehema   Kwa upande wake  mjumbe wa Kamati hiyo  Phidesia  Mwakitalima alisema kuwa Watoto hawa wengine wazazi wao hawaji kuwaona wengine hawana wazazi wanakabiliana na changamoto nyingi sana ikiwemo pia kesi zao kwenda taratibu.




Mwakitalima alisema   kwa sababu watoto waliopo katika mahabusu hiyo  ni watoto wenye  haki ya kupata elimu  hivyo pia aliomba serekali ijaribu kuwafikiria watoto hawa ambao wapo mahabusu . Ameongeza kuwa endapo watoto hao watapatiwa elimu wakiwemo mahabusu  itawasaida kwani hata wakiondoka hapo hawataondoka bure  na pia atatoka na elimu ambayo itamsaidia ata akienda kuondoa ujinga mtaani na pia itamsaidia ata kutoweza kujiingiza katika makundi mabaya ya mtaani kwani atakuwa na elimu kidogo ambayo itamsaida katika maisha yake.



 Aidha aliomba serekali pia iangalie mahabusu hiyo kwani  watoto wengine kesi zao zinasikilizwa mda mrefu bila suluhu na makosa mengine kisheria likifikishwa mahakamani kesi inapaswa kuisha siku hiyo hiyo



“mfano hapa kuna kesi ya mauaji mtoto alimsaidia dada yake asichomwe kisu na shemeji yake akachukua kisu akamuwahi shemeji yake na amekubali kosa lakini mwaka wa pili mahakamani wanasema ushahidi haujakamilika hivyo jamani naomba serekali iangalie sana hawa watoto kwani mbali na yote wanateseka wasaidie angalau kesi zao zisikilizwe kwa wakati na watendewe haki jamani kiukweli inauma naomba  serekali iwaangalie awa watoto jamani “alisema Phidesia  



Aidha aliomba serekali kuangalia kwa makini sana mahabusu hii ya  watoto kwani mbali na hivi pia mahabusu hii watoto wakiumwa wanapelekwa hospital na pikipiki hakuna gari ya mahabusu saa nyingine dawa zinakosekana na maafisa kujikuta wakijipapasa mifukoni mwao kunusuru watoto umauti usiwakute.

Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images