Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

SPIKA WA BUNGE ATUMA SALAMU ZA POLE KWA MAJERUHI WA AJALI ILIYOTOKEA LEO BAGAMOYO


RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATEKELEZA AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA LA KUHAKIKI SILAHA.

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kwa makini zoezi la uhakiki wa silaha zake lililokuwa likifanywa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Laizer Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe. Rais amekuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi Silaha aina ya Bastola Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi silaha aina ya shortgun Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiiweka silaha yake vizuri mara baada ya kuhakikiwa Ikulu jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa mtu kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam la kuhakiki silaha, ambapo bunduki zake mbili aina ya Shortgun na Pistol zimehakikiwa nyumbani kwake Ikulu Jijini Dar es salaam.

Uhakiki huo umefanywa na maafisa wa Jeshi la Polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro.


Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Rais Magufuli amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Jeshi la Polisi kwa kuendesha zoezi la uhakiki wa Silaha, na ametoa wito kwa watu wote wanaomiliki silaha nchi nzima kuhakikisha zinahakikiwa.Dkt. Magufuli pia amelitaka Jeshi la Polisi kuongeza juhudi za kukabiliana na watu wanaojihusisha na vitendo vya uharifu ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo.

"Ni aibu kumuona askari polisi mwenye silaha ananyang'anywa silaha, ni aibu, na nasema hiyo ni aibu, mpaka jambazi akunyang'anye silaha na wewe una silaha?"Amehoji Rais Magufuli.Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro, amemshukuru Rais Magufuli kwa kuunga mkono zoezi hilo na amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa mafanikio.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ametaka pande zinazogombea kiti cha Umeya katika Jiji la Dar es salaam, kukamilisha mchakato wa kumpata Meya katika uchaguzi uliopangwa kufanyika kesho tarehe 22 Machi, 2016 badala ya kuendelea kurumbana.


Dkt. Magufuli amesema upande wowote uwe tayari kupokea matokeo ya uchaguzi huo, ili Meya apatikane na Jiji liweze kuendelea na mipango yake ya kuwahudumia wananchi bila vikwazo.


"Mahali tunapostahili kushinda kama tumeshinda tushinde kweli, lakini mahali tunaposhindwa napo tukubali kushindwa, na hiyo ndio demokrasia ya kweli"ameongeza Rais Magufuli


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam


21 Machi, 2016


Vyama vya ushirika Hufa kutokana na madeni makubwa

WAZIRI NNAUYE AZUNGUMZA NA WAKONGWE WA MUZIKI WA DANSI JIJINI DAR LEO.

$
0
0
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezungumza na wadau wa mziki wa Dansi leo jijini Dar es Salaam na kusikiliza changamoto mbalimbali za wadau hao wa muziki huo wa Dance.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na wanamziki wa Dansi leo alipokutana nao katika ukumbi wa vijana Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey Mungereza akizungumza na wakongwe wa muziki wa Dansi leo katika ukumbi wa Vijana Kinondoni jijini Dar es Salaam.  Kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
 Mkurugenzi wa bendi ya Muziki wa Dance nchini African Starz (Twanga Pepeta), Asha Baraka akizungumza katika mkutano wa wanamziki wa Dansi  na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye 
 Mwanamziki wa Mziki wa Dansi, Duncan Nnjirima akichangia maada katika mkutano huo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
 Wakongwe wa mziki wa Dansi wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Nape Nnauye leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Al-Hassan Michuzi.











NAIBU SPIKA WA BUNGE AHUDHURIA VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE KATIKA KUMBI ZA BENKI KUU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
  Naibu Spika wa Bunge, Tulia Mwansasu (kushoto) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo alipohudhuria kikao cha kamati hiyo kilichoketi katika Kumbi za Benki Kuu (BoT Dar es Salaam leo.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa  kamati hiyo, William Ngeleja.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo, William Ngeleja (kulia), akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo wakati akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge, Tulia Mwansasu (kushoto), katika kikao cha kamati hiyo kilichoketi Dar es Salaam leo. Naibu Spika jana alihudhuria baadhi ya vikao vya Kamati za Bunge.
 Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba, Joseph Mhagama (kulia), akizungumza na wajumbe wa kamti hiyo (hawapo pichani), wakati akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge kwenye kikao hicho.
 Mjumbe wa kamati hiyo, Omary Badwel akichangia jambo kwenye kikao hicho mbele ya Naibu Spika. Kushoto ni Mjumbe Anna Joram Kidarya.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo wakiwa kwenye kikao hicho.

Kipindi cha redio cha Shuga charudi kwa kishindo

$
0
0
Mratibu wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Njombe – TACAIDS Abubakari Magege akiongea na washiriki wa kipindi cha redio cha shuga katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini. 
Mwakilishi wa UNICEF Alice Ijumba akijibu maswali ya washiriki wa wa kipindi cha redio cha shuga katika uzinduzi rasmi wa msimu wa pili wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini.
washiriki wa kipindi cha redio cha shuga wakifuatilia mada kutoka kwa Mwakilishi wa UNICEF Alice Ijumba katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini Alice Ijumba toka UNICEF .
Waratibu wa Shuga Radio drama series msimu wa pili - Pendo Laizer na David Sevuri wakichanganua ushiriki wa watangazaji na vikundi vya wasikilizaji .
Mshiriki akichangia mada katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini;
Mratibu wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Iringa - TACAIDS,Fadhila Mturi akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa semina elekezi .

Vipindi vya redio vya Shuga vitaanza kuunguruma tena kupitia redio mbalimbali nchini kuanzia wiki ya pili ya mwezi wa nne mwaka huu. Vipindi hivyo vinalenga kuwaelimisha vijana kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, usawa wa jinsia, kufanya maamuzi sahihi, matumizi sahihi ya kondomu na kuepukana na msongo rika.

Mfulilizo huu wa mchezo wa redio wa Shuga unawalenga zaidi vijana hususan wasichana, kwa kuangalia mtazamo wao, matarajio yao, changamoto wanazopitia ili kutimiza malengo yao na jinsi wanavyopambana na maisha yao ya kila siku. 

Mchezo wa redio wa Shuga ulianzishwa mnamo mwaka 2014 kwa ushirikiano kati ya MTV, HIV and AIDS Free Generation, Shirika la TACAIDS pamoja na UNICEF. Baada ya mafanikio makubwa msimu wa kwanza, TACAIDS na UNICEF pamoja na wadau wengine waliamua kupanua wigo wa program hii kwa kuandaa vipindi zaidi ili kuimarisha tabia chanya zilizojengwa katika msimu wa kwanza wa vipindi vya Shuga.

Katika kuboresha utoaji elimu kuhusiana na mahudhui ya vipindi, mashirika ya UNICEF pamoja na TACAIDS kwa kushirikiana na kampuni ya True Vision Production wanaendesha mafunzo elekezi kwa vituo vya radio za jamii, mameneja wa radio shiriki, watangazaji na waandishi wa habari pamoja na kwa waratibu wa UKIMWI ngazi za Halmashauri na Mkoa, ambapo warsha hii inafanyika mkoani Iringa.

Radio zitakazoshiriki katika urushaji wa vipindi vya Shuga msimu wa pili ni Clouds FM, Nuru FM – Iringa, Kitulo FM – Makete, Kyela FM – Kyela pamoja na Furaha FM, Hope FM, Qibla Ten FM za Iringa

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kifo cha DC Sara Dumba

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi, kufuatia kifo cha ghafla cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba, Kilichotokea jana jioni tarehe 21 Machi, 2016.


Bi. Sara Dumba aliugua ghafla kuanzia jana mchana na baadaye kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Njombe (Kibena), ambako wakati akipatiwa matibabu alifariki dunia majira ya saa moja za jioni.


Katika salamu hizo Rais Magufuli ameelezea kushitushwa na kifo cha ghafla cha Bi. Sara Dumba, ambaye amesema alimfahamu kwa uchapakazi wake, uaminifu na uadilifu katika utumishi wa umma na katika uongozi."Nimeshitushwa sana na kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba, kwa mara nyingine Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye mchango wake ulikuwa bado unahitajika"amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amebainisha kuwa Marehemu Sara dumba atakumbukwa kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuhimiza maendeleo ya wananchi, hususani katika kilimo na ufugaji, kuhimiza nidhamu ya utumishi serikalini na kuwatetea wananchi wa hali ya chini wakati wote wa majukumu yake ya ukuu wa wilaya.


Rais Magufuli amesema anaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu mkubwa, katika kipindi hiki kigumu na pia amewataka wote kuwa na subira na uvumilivu.

Amemuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam


22 Machi, 2016

MBUNGE VITI MAALUMU ASAIDIA AKINA MAMA WAJASILIAMALI.

$
0
0

 Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve akiwa na baadhi ya wananchama wa chama ch mapinduzi.
Na Sebastian Emmanuel jr. Mafinga.


Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve ameendelea kukutana na makundi mbalimbali katika mkoa huo, mwishoni mwa wiki hili amekutana na wajasiliamali wanawake katika makundi mawili tofauti. Kundi la kwanza alilokutana nalo ni lile la umoja wa wanawake wa ccm Iringa mjini, waliounda vicoba kwa ajili ya kukopeshana na kuendeleza miradi kadhaa ya kijasiliamali.


Aidha wanawake hao wakati wakisoma risala kwa mbunge huyo wamesema kuwa wanakabiliana na changamoto kadhaa hasa ukosefu wa mtaji utakao wafanya waendeleze vicoba hivyo ambavyo imekuwa kimbilio la makundi mbalimbali mijini na vijijini.


Pia wanawake wao wamemwomba mbunge huyo kuhakikisha kuwa wanawake wa mkoa wa Iringa wanakuwa mfano wa kuigwa katika kuanzisha, kukilinda na kukitetea chama chao hicho cha vicoba kwa kuwa vinaonesha nia ya kuwasaidia kujikimu kimaisha, mpaka sasa wameanza kutafuta wataalamu wa kufundisha namna ya kufuga kuku ili wapate elimu sahihi na kasha kuanza kutekeleza mladi huo.


Kwa upande wake mbunge huyo kijana ametoa milioni moja taslimu kama mkopo usiokuwa na riba ili uweze kuwasaidia kuendeleza mtaji wao pia akatumia fursa hiyo kuwaomba mkopo huo wauzungushe katika miradi mbalimbali kama ya ufugaji kuku n.k. pia ameonesha nia ya kuwasaidia wanawake hao na kuwaahidi kuwa wakiwa na uaminifu wa kulinda mtaji wao hata kama ni mdogo atahakikisha kuwa vicoba hiyo inakuwa ya mfano wa kuigwa mkoani Iringa. 


Mbunge huyo amewaomba wanawake wote wa mkoa wa Iringa wasikate tamaa badala yake wapende kujifunza na kutaka kupata nafasi ambayo itawapeleka kwenye mwanga wa  mafanikio. Amesema kuwa hata yeye amekuwa akithubutu kujituma kwa bidii ili aweze kufikia lengo la kuwasaidia wanawake wote bila kujali itikadi, kabila wala dini zao.


Aidha kundi jingine la pili ni lilela wanawake wanaoishi na ulevu Mjini Iringa, wametumia fursa hiyo kuongea na mbunge huyo na kumweleza changamoto wanazokumbana nazo, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mtu wa kuwasaidia kwa mda mrefu kulingana na changamoto zinazo wakabili na kuonesha imani kwa mbunge huyo kuwa sasa wanamatumaini mapya kuwa wamepata mtu muafaka wa kuwasaidia.


Wanawake hao wanaoishi na ulemavu wameomba pia kupatiwa mtaji ili uweze kuwasaidia katika umoja wao wa kazi za mikono ikiwa ni ususi wa shanga za kimasai, mikoba ya kimasai na mikoba ya kisasa kwa kutumia shanga mbalimbali za asili, ambapo mbunge huyo licha ya kuwapa kiasi cha pesa kwa ajili ya kuendeleza mtaji wao pia amewaomba waanzishe mladi wa utengenezaji wa batiki utakao wanufaisha kwa kiwango kikubwa kwani unaonesha kuwa na soko la uhakika..

VIDEO MPYA YA MSANII AMINI-HAWAJUI

machi 24 mwisho wa kuhakiki watumishi Ilala

$
0
0
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala wamepewa mpaka tarehe 24 Machi mwaka huu wawe wamekwenda kuhakikiwa katika ofisi za utawala za Halmashauri hiyo katika kutekeleza agizo la Mhe.Rais Dkt John Pombe Magufuli la kuhakiki watumishi wote wa umma.

Akizungumza kwa njia ya simu ofisini kwake msemaji wa Halmashauri ya Ilala Bi. Tabu Shahibu amesema tangazo limeshatoka na watumishi wote wanatakiwa kufika kuhakikiwa katika ofisi za utawala ambapo wanatakiwa kwenda na nyaraka mbalimbali muhimu zizohusu ajira zao.

Bi Tabu Shahibu amezitaja nyaraka hizo ambazo mtumishi anatakiwa kuambatanisha wakati wa uhakiki wake kuwa ni vyeti halisi vya taaluma,barua ya kuajiriwa na kudhibitishwa kazini, salary slip na picha ndogo za hivi karibuni.

“Zoezi la uhakiki linaendelea vizuri na watumishi wengi wamejitokeza kwa wingi na tunategemea kumaliza zoezi hili March 24 mwaka huu ili kuandaa taarifa rasmi ya kujua watumishi halali na wale watumishi  hewa” Alisema Bi Tabu.

Aidha Bi Tabu Shaibu amesema kumekuwa na changamoto ya watumishi wengi kutokuwepo kwenye vituo vya kazi ikiwa wengine wapo masomoni na likizo ila wameshatoa taarifa ya kuwaita ili kufanyiwa uhakiki mara moja ili kuendana na muda uliotolewa na Mhe Rais Magufuli wa siku 15.

Zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma katika limekuja mara baada ya uchunguzi uliofanywa katika mikoa ya Singida na Dodoma katika Halmashauri 14 na kugunduwa wafanyakazi hewa 202 wanaolipwa mishahara na hivyo Mhe. Rais Magufuli kutoa agizo la kuhakiki watumishi wote katika Wizara,mikoa,Wilaya,Idara,Taasisi na Wakala za Serikali ndani ya siku 15.

MWISHO

Watumishi wa Halmashauri ya Wiyala ya Temeke walioko masomoni na likizo watakiwa kurudi vituo vyao vya kazi kuhakikiwa

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO.

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke walioko masomoni na likizo wametakiwa kurudi mara moja katika vituo vyao vya kazi ili kuhakikiwa.

Agizo hilo limetolewa hivi karibuni na uongozi wa Halmashauri hiyo ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli la kuhakiki watumishi wote wa umma waliopo kwenye orodha ya malipo ya watumishi wa umma ndani ya siku 15 ili kubaini watumishi hewa wanaoendelea kulipwa mishahara.

Akizungumza kwa njia ya simu msemaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke Bi Joyce Nsumba amesema zoezi hilo ni muhimu sana kwa watumishi hivyo basi  watumishi wote wa Halmasahuri hiyo waliopo likizo na masomoni wanatakiwa kurudi katika vituo vyao vya kazi ili kuhakikiwa.

“ Taarifa imeshatoka kwa watumishi wote kuwa wanatakiwa kuhakikiwa na kwa wale waliopo likizo na kwenye masomo wanatakiwa kurudi ili wahakikiwe na kuendelea na likizo na masomo yao kwani mara baada ya uhakiki huu kukamili majina ambayo yatakuwa hayajahakikiwa yatafutwa kwenye orodha ya  watumishi” Alisema Bi Joyce.

Bi Joyce Nsumba ameongeza kuwa mpaka sasa uhakiki unaendelea  kwa makundi mbalimbali wakiwemo watumishi kutoka Idara ya Afya, Elimu, Fedha na Biashara, Kilimo,Mifugo,Ujenzi,na Maendeleo ya Jamii na mpaka  sasa wameshahakiki zaidi ya watumishi  8,000.

Zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma nchini limekuja mara baada ya uchunguzi uliofanywa katika mikoa ya Singida na Dodoma katika Halmashauri 14 na kugundulika kwa watumishi hewa 202 wanaolipwa mishahara  na hivyo Mhe. Rais Magufuli kutoa agizo la kuhakiki watumishi wote katika Wizara,mikoa,Wilaya,Idara,Taasisi na Wakala za Serikali ndani ya siku 15.

SPIKA WA BUNGE MH.NDUGAI AFANYA MABADILIKO YA BAADHI YA WAJUMBE WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE

UNFPA yakabidhi vifaa tiba vyuo na taasisi za afya nchini.

$
0
0
 Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Natalia Kanem (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya kutumia simu kwa ajili ya kufundisha wakunga na wauguzi njia ya uzazi salama, waliokaa kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali) Dkt. Otilia Gowele, Msajili wa Baraza la Uuguzi Lena Mfalila na Geeta Lal kutoka makao makuu ya UNFPA.
Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle akipokea simu ya kufundishia uzazi salama kutoka kwa Mwakilishi wa Shirika la UNFPA Natalia Kanem (katikati) huku wakishuhudiwa na Geeta Lal kutoka makao makuu ya UNFPA.
Mwalimu wa Uuguzi Asha Ally Khamis (wa pili kulia) kutoka Chuo cha Afya Mbweni Zanzibar akipokea simu ya kufundishia uzazi salama kutoka kwa Natalia Kanem, wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini na Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Otilia Gowelle, kulia ni Nayanesh Bhandutia kutoka makao makuu ya UNFPA. 
Mkuu wa Chuo cha Uuguzi Newala Tecla Ungele (wa kwanza kulia) akipokea seti ya simu ya kufundishia uzazi salama kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Otilia Gowelle , wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Natalia Kanem
 Wawakilishi kutoka Vyuo vya Afya na Taasisi zinazojihusisha na uzazi salama nchini  wakifuatilia mafunzo ya uzazi salama kwa kutumia teknolojia mpya ya simu. 

 Geeta Lal kutoka Makao Makuu ya UNFPA akitoa maelekezo kwa washiriki (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya uzazi salama ambayo yanapatikana ndani ya simu hiyo.
 Mkuu wa Chuo cha Uuguzi Newala Tecla Ungele (wa kwanza kulia) akipokea seti ya simu ya kufundishia uzazi salama kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Otilia Gowelle , wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Natalia Kanem
 Wawakilishi kutoka Vyuo vya Afya na Taasisi zinazojihusisha na uzazi salama nchini  wakifuatilia mafunzo ya uzazi salama kwa kutumia teknolojia mpya ya simu.

Na Lilian Lundo-MAELEZO

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNFPA) limekabidhi simu za kufundishia huduma ya uzazi salama kwa vyuo vya Afya pamoja na taasisi zinajihusisha na masuala ya afya ya mama na mtoto ili kuboresha huduma kwa akina mama wajawazito na watoto wanaozaliwa.

Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam Machi 21, 2016 baina ya shirika la UNFPA na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Akikabidhi vifaa hivyo Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini Natalia Kanem alisema wanashirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukuza na kuboresha elimu juu ya uzazi salama na kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

“Dhumuni la matumizi ya simu za kufundishia uzazi salama ni kutoa elimu kwa wauguzi na wakunga walioko vijijini na maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi ili kuwasaidia kupata elimu ya uzazi salama na kupunguza vifo vya mama na mtoto,” alisema Natalia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowele ambaye alimwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali alisema kuwa simu hizo zitarahisisha ufundishaji kwa wauguzi na wakunga kwani zitawawezesha kujifunza masuala yote yanayohusu uzazi salama bila kuondoka kwenye vituo vyao vya kazi.

Dkt. Gowele aliongeza kwa kusema kuwa, simu hizo zitakuwa na mafunzo ya uuguzi ambayo yako katika mitaala ya vyuo vya uuguzi na mtumiaji wa simu hiyo anaweza kuuliza swali lolote linalohusu uzazi salama akapata majibu kwa njia ya sauti, picha na maandishi.

Aidha, simu hizo zinachajiwa kwa kutumia umeme wa mwanga jua, umeme wa wakawaida na inatumia betri pia, hivyo inaweza kutumika hata maeneo ambayo bado hayajafikiwa na umeme.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Afya ya Mama na Mtoto wa UNFPA Felister Bwana alisema kuwa, simu hizo zimegawiwa kama majaribio kwa baadhi ya vyuo vya Afya na na taasisi zinazojihusisha na uzazi salama, endapo teknolojia hiyo italeta mafanikio yanayotarajiwa simu hizo zitagawanywa kwa vyuo vyote vya uuguzi na hospitali nchini.

Vyuo na taasisi ambavyo vimepokea vifaa hivyo ni pamoja na Chuo cha Afya Kilosa, Bugando, Newala, Nachingwea, Bagamoyo, Geita, Kahama, Maswa, Sengerema, KCMC, Zanzibar, Ifakara pamoja na taasisi ya TAMA na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Kwa mujibu ya sensa ya mwaka 2010, jumla ya vifo 454 vimekuwa vikitokea  katika kila vizazi hai 100,000 kwa mwaka, idadi hiyo imepungua na kufikia vifo 432 kwa kila vizazi hai 100,000 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.

UVCCM WAPONGEZA USHINDI WA DKT.SHEIN.

$
0
0
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM )umesema ushindi alioupata mgombea wa CCM Rais Dk Ali Mohamed Shein kwamba ni kielelezo cha kuimarika kwa msingi ya demokrasia Zanzibar na kukubalika kwa mgombea huyo kwa wapiga kura na wananchi wa Zanzibar . 


Umesema ushindi huo sasa umehitimisha mvutano na maneno yaliyokuwepo ambayo yalikuwa yakienezwa kwa makusudi ,  kupotoshwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani visiwani humu. 


Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ameeleza hayo Afisi kuu ya UVCCM Kikwajuni wakati akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kumaliza kwa maandano makubwa yaliyoandaliwa na UVCCM kusherehekea ushindi wa CCM uliotangazwa  na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar  Jecha Salim Jecha kulitangaza jina la Dk shein mshindi wa uchaguzi huo. 


Alisema ushindi alioupata Dk shein kwa kupata jumla ya kura  299982sawa na asilimia 91.4 kumeidhihirisha dunia jinsi ya kukubalika kwa kiongozi huyo katika aina ya utawala na uongozi wake.  "Ameonyesha umahiri, upeo na uwezo mkubwa  katika kuongoza serikali ya umoja wa kitaifa kwa miaka mitano iliopita; amekuwa mstahamilivu na nguzo muhimu ili jamii isiendelee kugawanyika "alisema shaka 


Kaimu Katibu Mkuu alisema aina ya uongozi wa Rais Dk Shein ni wa kipekee na kwamba kama angekuwa si mtawala mwenye maarifa mapana na uvumilivu wa kisiasa serikali hiyo anaamini ingevunjika mapema.  Shaka alisema serikai za mseto za Zimbabwe na Kenya ziliweza kuyumba  na kwamba hazikudumu kutokana na baadhi ya viongozi wake kukosa kuaminiana, kuvumiliana na kustahamiiiana .


"Ushindi huu ni pigo jipya kwa chama cha CUF ambacho kimesusia uchaguzi wa marudio bila sababu za msingi, ushindi wa Dk shein  naamini utaleta mageuzi makubwa ya kiuchumi  na kuishangaza dunia katika maendeleo ya demokrasia "alisems Shaka .Aidha alisema anatarajia serikali mpya ijayo haitakuwa na viongozi wababaishaji na badala yake watateuliwa wazalendo, wachapa kazi na watu wenye uchungu wa kiyatetea Mapinduzi bila kushiriki usaliti. 


Hata hivyo Shaka alisema anaamini kuwa chini ya uongozi wa kipindi cha pili cha utawala Dk Shein na sera makini za ccm ,ataendelea kusimamia uadilifu serikalini,  kujenga umoja wa kitaifa nchini  pamoja na kuwatumikia wananchi ipasavyo na kudumisha huduma za jamii . "UVCCM tuna matumaini makubwa na na Dk shein katika awamu mpya ya ushindi wake; ataunda baraza la mawaziri makini, na hatutosita kumpongeza kila atakapofanya vizuri  pia hatutakaa kimya pale tutakapoona mambo  hayaendi ipasavyo "alisema .


Shaka anewahimiza vijana mahali popote walipo kumuunga mkono Dk shein na kuisaidia serikali yake ili iweze kupiga hatua za kimaendeleo na kwamba hatawaangusha katika uongozi wake.


"Tunahitaji kutoka mahali tulipo na kufika tunakotarajia, tungependa kuona uwajibikaji mpya,utendaji wenye kubeba dhamira na utekelezaji wa malengo na sera hivyo ni wazi kuwa   wapatikane watu wenye uwezo na upeo ya kukwamua nchi mahali ilipo sasa" 

TWAWEZA, IBM NA BITES & BYTES WAANDAA MKUTANO WA KITEKNOLOJIA MACHI 29 NA 30 MWAKA HUU.

$
0
0

TWAWEZA, IBM NA BITES & BYTES WAANDAA MKUTANO WA KITEKNOLOJIA MACHI 29 NA 30 MWAKA HUU.

Mwanzilishi wa Bites& Bytes, Lilian Madeje (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na shindano la kiteknologia litakalofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam Machi 29 na 30 mwaka huu. Kulia ni Mkuu wa Utafiti Twaweza, Elivis Mushi.
NBV wa benki ya CBA Group, Eric Luyangi(Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kutoka kushoto ni Risha Chande, mwanzilishi wa Bites &Bytes, Lilian Madeje na wamwisho kulia ni
Mkuu wa Utafiti Twaweza, Elivis Mushi.

ASASI isiyo ya kiraia ya Twaweza na Kampuni ya IBM ikishirikiana na Bites &Bytes imeandaa mkutano mkubwa wa Kiteknolojia na uvumbuzi unaoitwa Bites &Bytes ambao utafanyika Machi 29 na 30 mwaka huu katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na mwanzilishi wa Bites &Bytes, Lilian Madeje wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Liliani amesema kuwa lengo mkutano huo ni kuhamasisha uendelezaji wa mawazo mpya pamoja na uvumbuzi wa mawazo mapya ya kibiashara ili aanzishaji wapya wa mawazo waweze kuwapa mwanya wa kubadilishana mawazo na wadau wengine ili waweze kushirikiana kwa pamoja.

Pia Liliani amesema kuwa washiriki 16 wa mechanguliwa kushiriki katika shindano hilo la ubunifu wa biashara ambapo washiriki hao watashindania kuwania kitika cha shilingi milioni tano(5,000,000).

Nae NBV wa benki ya CBA Group, Eric Luyangi amesema kuwa katika shindano hilo la Software Developers wanalenga kuleta suluhisho la kuwezesha kufikisha takwimu na tafiti mbalimbali za Twaweza kwa kutumia mitandao tofauti tofauti.

ISAYA CHACHA (CHADEMA) ACHAGULIWA KUWA MEYA WA JIJINI LA DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Chacha (katikati)akizungumza na wananchi juu ya kuwashukuru sana wapiga kura wake wa kata ya Vijibweni kwa kumchagua kuwa Diwani pamoja uongozi wa chama chake kwa kukubali kumpa nafasi ya kugombea kiti hicho, Jiji la Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Bw.Freeman Mbowe akizungumza na wananchi  baada ya   ushindi wa kiti hicho cha meya wa Jiji la Dar es Salaam.
 Wafuasi wa chadema wakingombania bendera mara baada ya uchaguzi huo Jijini Dar es Salaam leo.
 Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Chacha akisindikizwa na wananchi wa  kuelekea Makao Mkuu ya Chama hicho,leo Jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wafuasi wa Chadema  waliojitokeza katika uchaguzi huo, leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

KAIMU Mkurugenzi  Jiji  la Dar es Salaam Bi. Sara Yohana amemtanganza Isaya Chacha Diwani wa  Kata ya Vijibweni  (CHADEMA) kutoka Wilaya ya Temeke kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam mara baada ya Uchaguzi.

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema hayo mara baada ya uchaguzi uliyofanyika leo  jijini Dar es Salaam ambapo mshindi alipata kwa kura 84 dhidi ya mgombea mweza kupitia chama cha CCM Bw.Yenga Yusuph ambaye alipata kura 67,na katika uchaguzi huo kura 7 ziliharibika.


 “Tunawashuruku wapiga kura wote mlioshiriki zoezi hili la upigaji kura kwa utulivu bila vurugu na kuweza kulifanikisha mpaka kumpata Meya wa Jiji hili”,alisema Bi Yohana.


Kwa upande wa mshindi wa Kiti cha Meya wa  Jiji Mhe. Chacha alisema anawashukuru sana wapiga kura wake wa kata ya Vijibweni kwa kumchagua kuwa Diwani pamoja uongozi wa chama chake kwa kukubali kumpa nafasi ya kugombea kiti hicho.


“Nimejipanga kuleta maendeleo katika sekta ya elimu pamoja na kupambana na kero ya foleni katika jiji pia hakikisha wananchi wote maskini wanafaidika  na mapato ya jiji hili katika kuendeleza miundombinu mbalimbali ,”alisema Chacha.


Mbali na hayo naye Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Bw.Freeman Mbowe alisema idadi ya wapiga kura tu inaonyesha wazi kuwa ushindi wa kiti hicho cha meya ni lazima uchukuliwe na  CHADEMA sababu  madiwani wengi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanatoka katika chama hicho.

‘MABASI YAENDAYO KASI KUANZA NDANI YA WIKI HII’

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mabasi yaendayo kasi (DART) yataanza kufanyiwa majaribio ndani wiki moja kuanzia sasa ili madereva waanze kuzoea njia na taa za kuongozea magari.

“Wataanza na mabasi kati ya 30 – 50 ambayo yatapita kwenye njia zote za mradi huo. Zoezi hilo litafanyika ili watumiaji wengine wakiwemo waendesha daladala, bodaboda na watembea kwa miguu waweze kutambua kuwa njia ya mabasi yaendayo kasi si ya kwao, hivyo waanze kuzoea,” alisema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Machi 22, 2016) wakati alipofanya ziara ya ghafla katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri iliyokuwa na lengo la kuangalia mfumo wa majiko ya gesi sokoni hapo na kukagua ujenzi wa ukuta unaotenganisha soko hilo na mabasi yaendayo kasi.

Waziri Mkuu ambaye ametembelea soko hilo kuanzia saa 5:10 hadi saa 5:54, alitoa jibu hilo wakati akijibu maombi ya mfanyabiashara mmoja, Bw. Sharifu Ramadhani ambaye alisema wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya usafiri kwa vile mabasi mengi yanaishia Mnazi Mmoja. “Mabasi yanaishia Mnazi Mmoja na huku ni mbali kwa hiyo tunalazimika kutembea kwa miguu kwa sababu kukodi taxi ni gharama kubwa,” alisema.

Akifafanua kuhusu hatua iliyofikiwa kwenye utekelezaji wa mradi huo, Waziri Mkuu alisema: “Hivi sasa wanakamilisha ufungaji wa mitambo ya kukatia tiketi ambapo abiria atakuwa na kadi kama za benki ambayo anaijaza fedha halafu anapita kwenye mashine, kiasi cha nauli kinakatwa halafu anaingia kwenye basi, hakutakuwa na muda wa kukata tiketi.”

Alisema tatizo la usafiri kwa wafanyabiasha wa feri litakwisha hivi karibuni baada ya mabasi hayo kuanza.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MACHI 22, 2016.

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AWASILI TUNIS KUSHIRIKI MKUTANO WA 8 WA NCHI MAJIRANI WA LIBYA

$
0
0
Mwakilishi Maalum wa AU wa Mgogoro wa Libya akizungumza na Waziri wa Masuala ya Maghreb, Arab na Afrika Mheshimiwa Abdelkader Messahel.
Mwakilishi Maalum wa AU wa mgogoro wa Libya akiagana na Waziri Abdelkadir Messahel wa Algeria baada ya mazungumzo yao.

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika wa Usuluhishi wa Mgogoro wa Libya amewasili jana jijini Tunis nchini Tunisia kushiriki Mkutano wa 8 wa Nchi Jirani ya Libya. Mkutano huo ulioitishwa na Serikali ya Tunisia ni muendelezo wa jitihada za nchi jirani kusaidia kuleta hali ya amani na usalama nchini Libya. Rais Mstaafy amewasili Tunis akitokea Salalah nchini Oman aliposhiriki katika Mkutano wa Kamati ya Bunge la Kuandika Katiba ya Libya.

Akiwa jijini Tunis, Rais Mstaafu Kikwete amefanya mazungumzo jana na Waziri wa Masuala ya Maghreb, Arab na Afrika wa Algeria Mheshimiwa Abdelkader Messaleh aliyemtembelea hotelini kwake. Katika mazungumzo yao, Waziri Messaleh alimpongeza Rais Mstaafu Kikwete kwa kuteuliwa na Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika kusuluhisha mgogoro wa Libya. Alimuelezea hali ya usalama na kisisa ya Libya na mtizamo wa nchi yake juu ya namna bora ya utatuzi wa mgogoro huo.Alimhakikishia Rais Mstaafu ushirikiano wa Serikali ya Algeria katika jukumu lake alilokabidhiwa na Umoja wa Afrika.

Kwa upande wake, Rais Mstaafu Kikwete alimshukuru Waziri Abdelkader Messaleh kwa maelezo aliyompatia na ushirikiano aliomuahidi. Alimuelezea matumaini yake ya kupatikana kwa suluhu ya mgogoro huo madhali nchi jirani na Libya na Umoja wa Afrika zitashirikiana na wadau wote kuhakikisha mgogoro huo unatatulika. Alisisitiza kuwa hatimaye suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Libya uko mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe.

Katika ziara yake nchini Tunisia, mbali na kuhudhuria Mkutano wa 8 wa Nchi Jirani na Libya, Rais Mstaafu Kikwete anatarajiwa pia kukutana na Waziri Mkuu Mteule na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Libya (Presidency Council) Mheshimiwa Fayez Al-Sarraj, wadau wengine wa Libya pamoja na kutembelea Ofisi ya Ujumbe wa Umoja wa Afrika kwa Libya iliyoko jijini Tunis. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anatarajiwa kurejea nchini tarehe 25 Machi, 2016.

Startimes yakabidhi ipadi Wizara ya Habari.

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa Na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (wa pili kulia) akipokea moja ya Mini Pads 180 kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (wa kwanza kushoto), Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Wakishuhudia tukio hilo wa pili kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa. Elisante Ole Gabriel (kulia).
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa Na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akifurahia kupokea Mini Pads 180 kutoka kampuni ya StarTimes kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa, Elisante Ole Gabriel na wa pili kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing na muwakilishi kutoka ubalozini Bw. Mr Gao Wei. 
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili kushoto), akiteta jambo baada ya kupokea Mini Pads 180 kutoka kampuni ya StarTimes kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Pamoja naye kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dr. Lu Youqing.Picha na Dotto Mwaibale.


Na Shamimu Nyaki - WHUSM.

Kampuni ya ving’amuzi ya Startimes imekabidhi ipadi 180 kwa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ili kurahisisha utendaji kazi wa Maafisa Habari wa wizara hiyo.Ipad hizo zimekabidhiwa leo Jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu wa Startimes Bw.Lanfang Liao ambaye amehaidi kutoa misaada ya vitendea kazi zaidi kwa wizara ili kuongeza ufanisi katika sekta ya habari.

“Kampuni yetu na Wizara ya habari zina ushirikiano wa muda mrefu hivyo, tumeamua kuwakabidhi ipadi 180 zenye thamani ya shilingi milioni 90 ili ziweze kusaidia Wizara katika kazi zake”alisema Liao.

Bw Liao ameongeza kuwa, wataendelea kuongeza chaneli nyingi za Kiswahili zitakazokuwa na maudhui yatakayojikita katika nyanja za utamaduni na Sanaa za kitanzania.Naye Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye mbali na kuishukuru kampuni hiyo amesema kuwa Ipadi zitagaiwa kwa mikoa 15 ambayo maafisa wake wana uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo.

“Ni faraja kwamba wenzetu wa Startimes wametuelewa haraka na kukubali kutusaidia vifaa hivi vya mawasiliano (Ipadi) ,kwa hakika vitatusaidia sana kuboresha utendaji kwa maafisa wetu wa Wizara pia Maafisa Mawasiliano ambao ni wadau wa kutoa taarifa kwa Umma”alisema Nnauye.

Mhe.Nnauye ameongeza kuwa,Wizara ya habari ina lengo la kuimarisha mawasiliano Serikalini kwa kuhakikisha maafisa habari ambao wanafanya kazi kwenye Halmashauri zote kupata vitendea kazi kwahiyo anatoa wito kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuboresha mawasiliano kwa Sekta ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.

Hivyo basi maafisa habari wanapaswa kuzitumia Ipadi hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta maendeleo katika sekta ya habari nchini.

SOKO LA FERI LATAKIWA KUTAFUTA GESI YA BEI NAFUU

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea kwenye soko la samaki la Feri akitokea ofisini kwake Magogoni jijini Dar es salaam kukagua hali ya soko hilo Machi 22, 2016. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la kukaangia samaki kwenye soko la samaki Feri la jijini Dar es salaam Machi 22, 2016, Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mama Lishe wakati alipotembelea soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam Machi 22, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia Mama Lishe wakati alipotembelea soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam Machi 22, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Bodi ya soko la Kimataifa la Samaki la Feri, kukutana na makampuni mbalimbali yanayouza gesi ili kupata kampuni inayouza kwa bei nafuu zaidi lengo likiwa ni kuwapunguzia gharama wakaangaji wa samaki sokoni hapo.

Pia Waziri Mkuu Majaliwa alimtaka Meneja wa soko hilo, Bw. Solomon Mushi kuhakikisha wanakuwa na kifaa maalumu cha kupimia ujazo wa mitungi ya gesi sokoni hapo ili kubaini kama ni sahihi.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumanne, Machi 22, 2016) wakati alipofanya ziara ya ghafla katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri iliyokuwa na lengo la kuangalia mfumo wa majiko ya gesi sokoni hapo ambapo aliridhishwa na unavyofanya kazi.

Waziri Mkuu ambaye ametumia dakika 44 kulitembea soko hilo, alitoa maagizo hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara ambao wamesema wamekuwa wakiuziwa gesi kwa bei kubwa ambayo imekuwa ikiongezeka mara kwa mara.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara hao, Bw. Ally Iddi amesema awali walikuwa wanauziwa mtungi wa gesi wenye ujazo wa kilo 32 kwa sh. 70,000 na sasa umeongezeka hadi sh. 98,000 kiasi ambacho ni kikubwa ukilinganisha na uzalishaji wao. “Nimeulizia kwenye baadhi ya maduka na kukuta mtungi wenye ujazo kama huo unauzwa sh. 75,000,” alisema.

Kijana mwingine ambaye ni mkaangaji wa samaki, Bw. Mwanya Selemeni alisema hivi sasa hali ya soko la feri ni nzuri tofauti na walivyokuwa wakitumia kuni kwa sababu hakuna moshi. Alimuomba Waziri Mkuu ahakikishe wanafikishiwa gesi ya kutoka Mtwara ili gharama ziweze kupungua.

Mfanyabiashara mwingine wa soko hilo, Bi. Mariam Samweli ambaye alikuwa akiuza kuni na sasa yeye na wenzake wanataka kufanya biashara nyingine lakini banda walilokuwa wakilitumia halina umeme licha ya kuwa wameomba mara nyingi. “Tunaomba kupatiwa umeme ili tuweke vipepeo tuweze kufanya biashara nyingine,” alisema.

Waziri Mkuu pia alitembelea eneo la mnada wa kuuza samaki sokoni hapo ambako alielezwa matatizo ya umeme na uzibaji wa mitaro ya maji machafu hali ambayo inatishia usalama wa afya zao.

“Kuna jipu la umeme hapa, tunachangishwa hela na kumpa mtu ambaye hatumjui lakini hatujawahi kuona risiti, wao wanaweka umeme juu kwa juu na umeme wenyewe wala haukai. Mita tunayo hapa lakini hata namba hatujapewa,” alisema Bw. Omari Masoud kwa niaba ya wenzake.

Kuhusu tatizo la uzibaji mitaro na kutiririsha majitaka, kiongozi wa mama lishe sokoni hapo, Bi. Fatma Ally aliomba watatuliwe tatizo hilo ambalo limedumu kwa zaidi miezi miwili.

Akijibu kero zao, Waziri Mkuu alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Raymond Mushi asimamie suala la kuweka umeme kwenye hilo banda pamoja ahakikishe mama lishe wa soko hilo upande wa mnadani waanze kutumia majiko ya gesi badala ya mkaa.

Kuhusu mitaro, alimwagiza meneja wa soko hilo, Bw. Solomon Mushi aimarishe uzibuaji wa mitaro katika soko hilo. “ Mwambie mkandarasi azibue mitaro kila siku jioni na watumiaji wa soko waache kutumia mifuko ya plastiki kwa sababu inapoingia kule inaziba na wala haiozi,” alisema.

Aliwataka wafanyabiashara waimarishe usafi kwa sababu ni sehemu ya chakula. “Lengo letu ni kufanya soko hili liwe kwenye viwango vya kimataiafa ili mteja anapokuja kununua samaki wabichi ama wa kukaanga awe na chaguo,” alisema.

Kwa upande wake, Meneja wa soko hilo, Bw. Mushi alisema bodi ya soko hilo ambayo imeundwa hivi karibuni itakutana kesho kwa mara ya kwanza na miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa ni maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu.

IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MACHI 22, 2016.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images