Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 795 | 796 | (Page 797) | 798 | 799 | .... | 1903 | newer

  0 0
 • 03/15/16--05:26: Article 16
 • amani kipepelushi


  0 0

  ummm

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Masuala ya Wanawake, Wazee na Watoto wa Tanzania, Mh. Ummy Mwalimu akiwasilisha mada kuu ambapo aliwakilisha kundi la Afrika katika mkutano huo mkubwa unaoendelea nchini Marekani.

  Bara la Afrika na hasa wanawake ndio wanaobeba mzigo zaidi wa madhara ya mabadiliko ya tabianchi, huku wakinyimwa fursa ya kushiriki katika kutafuta suluhu kwa tatizo hilo, ameeleza leo Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Masuala ya wanawake, wazee na watoto wa Tanzania.

  Bi Mwalimu amesema hayo akihutubia kikao cha 60 cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake, CSW60 kwa niaba ya kundi la nchi za Afrika, akisisitiza umuhimu wa kushirikisha zaidi wanawake katika uongozi wa kimataifa kuhusu suala la mabadiliko ya tabianchi.

  "Wanawake wanapaswa kuweza kuongoza katika ngazi za kitaifa na serikali za mitaa. Ubunifu wao, ujuzi wa kiasili, matarajio yao yanaweza kusaidia katika kubuni na kushawishi suluhu kuhusu mabadiliko ya tabianchi.Aidha amezungumzia suala la kilimo ambacho hushughulisha wanawake zaidi, akisema la msingi ni kusaidia sekta binafsi ili kukuza ukuaji wa uchumi katika sekta hiyo na hivyo kuwezesha wanawake.
  ummBaadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanawake unaofanyika nchini Marekani ulioanza jana Machi 14-24, wakiwa nje ya jengo la Umoja wa Mataifa unapofanyika mkutano huo
  unwomen
  Baadhi ya washiriki wakifuatilia mkutano huo wa #CSW60
  ummy

  0 0  Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha wameanza kurudisha kadi za chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mara tu baada ya uteuzi wa Katibu Mkuu mpya wa Chama.

  Viongozi hao wa CHADEMA Arusha wametoa madai kadhaa ambayo yamewafanya kufikia uamuzi huo kwa nyakati tofauti.

  Mwenyekiti wa Mtaa wa Olumuriaki Ndugu Godfrey Kitomari na wanachama wanachama wa chadema 97 wa Kata ya Sombetini wamerudi CCM kwa sababu zifuatazo;-

  1. Kuridhishwa na kasi ya Mhe Dkt Magufuli.

  2. Kuchukizwa na Mbowe kukiuza chama na kuiacha agenda ya kukemea ufisadi kama ilivyokuwa mwanzo na badala yake kuwatetea.

  3. Uteuzi wa Katibu Mkuu asiye na uwezo lakini mwenye rekodi mbaya kwenye jamii.
  Pichani: Ndugu Kitomari akiveshwa Kofia ya CCM kwenye Mkutano wa hadhara wa kukaribishwa CCM.

  Wananchi wa Kata ya Sombetini wakishuhudia tukio la Mwenyekiti huyo wa Mtaa kujiunga na CCM.

  WanaCCM wakimlaki Ndugu Kitomari mara baada ya kujiunga na Chama hicho.

  Katika tukio jingine;
  Mwenyekiti wa BAVICHA Kata ya Mjini Kati Ndugu Ally Kaole (pichani) naye amejiuzulu nafasi yake hiyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi - CCM.

  Kaole ametoa sababu za uamuzi wake huo kuwa ni;-
  1. Uteuzi wa Katibu asiyekijua Chama lakini asiyejua falsafa za Uongozi na Utawala, amesema uteuzi huo unalenga kuua Chama hicho. Ndugu Ally amedai kuwa Katibu Mkuu mpya wa CHADEMA na yule aliyestaafu hawafanani hata chembe, ni sawa na kufananisha Kifo na Usingizi.

  2. Amesikitishwa na Mwenyekiti wa Chama kutetea majipu tena hadharani, akisema hatua hiyo imeondoa uhalali wa yeye kuwepo katika chama hicho ambacho aliamini kuwa kinachukizwa na majipu na kwamba kilikuwa kinaomba ridhaa ili kuyashughulikia.

  Pichani: Ndugu Ally Kaole (aliyekuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Arusha.

  0 0  0 0

   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu namna Wizara ya Katiba na Sheria ilivyojipanga katika kutatua changamoto za utoaji haki nchini . Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva (wa pili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju (kulia).
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akizungumza  kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu namna alivyoishauri Wizara ya Katiba na Sheria  inavyoweza kutatua changamoto za utoaji haki nchini bila kuharibu kanuni zilizopo.

  0 0

  Msanifu wa Majengo na mbunifu wa Mchoro wa Uwanja wa Taifa Aloyce Peter Mushi akifafanua jambo wakati wa kikao cha ukaguzi wamaendeleo ya ujenzi wa uwanja huo jana jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Bibi. Cecilia Kasongo, Mhandisi wa Uwanja wa Taifa Yusuf,Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge, Muhandisi wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa Uhuru E. Mwamakunga na Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.
  Meneja wa Ujenzi wa Kampuni ya BCEG inayojenga uwanja wa Uhuru Zhang Jiawei akifafanua jambo wakati wa kikao cha ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo jana jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge,Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio, Msanifu wa Majengo na mbunifu wa Mchoro wa Uwanja wa Taifa Aloyce Peter Mushi Muhandisi wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa Uhuru E. Mwamakunga.
  Wajumbe wa kikao cha kukagua na kutathmini maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Uhuru wakikagua miunndombinu ya majitaka inayoendelea kujengwa katika uwanja wa Uhuru jana jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio(mwenye suti nyeusi) akielezea jambo wakati wa kikao cha ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Uhuru jana jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija.
  Muonekano wa nje wa Uwanja wa Uhuru.
  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge akielekeza jambo kuhusu wavu uliowekwa kwa ajili ya kuzuia mashabiki wasirukie na kuharibu miundombinu katika maeneo ya vyoo vya uwanja wa Uhuru jana wakati wa kikao cha ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.

  0 0

  Ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Machi 14, 2016) wakati akizungumza na uongozi wa kiwanda cha sukari cha Kagera pamoja na uongozi wa mkoa wa Kagera alipotembelea kiwanda hicho ambapo alisema wamezuia sukari kutoka nje ili kuhakikisha sukari inaisha katika maghala yao.

  Akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Kagera, Waziri Mkuu ameviagiza viwanda kuzalisha sukari nchini vizalishe sukari ya kutosha ili kukidhi mahitaji ya soko.

  Alisema mahitaji halisi ya sukari hapa nchini ni tani 420,000 huku uwezo wa viwanda vya ndani ni kuzalisha tani 300,000 hivyo alitoa wito kwa viwanda hivyo kuongeza uzalishaji.

  "Tunahitaji viwanda vya ndani vizalishe sukari ya kutosha na mahitaji yawe yamefikiwa kama tulivyokubaliana, lengo ni kuzuia uagizaji wa sukari kutoka nje ambao ukiendelea utavivuruga viwanda vya ndani," alisema.

  Pia alivitaka viwanda hivyo viwe vimefikia malengo ya kuzalisha sukari ya kutosha katika kipindi cha kuanzia miaka mitatu hadi minne kama walivyokubaliana katika kikao cha wadau wa sukari nchini kilichofanyika hivi karibuni.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika mashamba ya miwa, ununuzi wa mitambo pamoja na kuajiri idadi kubwa ya watumishi ambao ni Watanzania.

  Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Ash Rana alisema kwa sasa wanazalisha tani 60,000 za sukari na kwamba wana lengo la kuzalisha tani 120,000 katika kipindi cha miaka minne ijayo.

  Alisema uzalishaji wa sukari kiwandani hapo umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo mwaka wa fedha wa 2011/2012 walizalisha tani 35,362 na mwaka 2015/2016 wamezalisha tani 60,000.

  Ofisa huyo aliiomba Serikali ipunguze riba ya mikopo ya kwenye uwekezaji wa sekta ya kilimo ambapo kwa sasa wanatozwa asilimia 20 kiwango ambacho alisema ni kikubwa sana.

  Alisema wana mipango ya kukiboresha na kukipanua zaidi kiwanda hicho na hivi sasa wako katika hatua za mwisho za kupata mkopo wa Dola za Marekani milioni 68 ambao kati ya hizo, dola milioni 10 zitapelewa katika uboreshaji wa umwagiliaji na zilizobaki katika kuimarisha miundombinu ya kiwanda hicho.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, MACHI 15, 2016.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa kahawa iliyoyokaangwa maarufukwa jina la akamwani ikiwa ni mapokezi ya kimila ya Wahaya wakati alipokwenda nyumbani kwa Waziri wa Zamani wa Ardhi, Profesa Tibaijuka mjini Muleba kutoa pole kufuatia msiba wa mama yake mzazi, Aulelia Kajumulo Machi 15, 2016.
  Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kiwasalimia wnanchi wa eneo la Benaco wilayani Ngara akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi, 2016.

   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Alphayo Kidata kuwa  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

  Na Raymond Mushumbusi- MAELEZO
  15/3/2016. Dar es salaam.

  Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya takribani Sh. billioni 12 kutoka kwa wafanyabiashara ambao walikwepa kodi na kupewa muda wa siku 14 na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.  John Pombe Magufuli kulipa kodi hizo kwenye mamlaka hiyo.

  Akitoa takwimu hizo mara baada ya kuapishwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata amesema, kila Mtanzania ana jukumu la kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na sio kukwepa na amehaidi kulisimamia vizuri suala la ukusanyaji wa mapato katika sehemu mbalimbali ili kuongeza mapato ambayo yatasaidia kufanikisha maendeleo katika sekta mbalimbali.

  “Tutajitahidi kwa kila namna kuwaelimisha wananchi wetu ili wafahamu wajibu wao na umuhimu katika kulipa kodi na sio kukwepa kulipa kodi na tunawaomba wananchi kila waendapo kupata huduma yoyote ile iwe katika sekta binafsi au Serikalini  basi anatakiwa aombe stakabadhi za manunuzi au huduma ili tuweze kudhibiti upotevu wa kodi” alisema Kidata.

  Kamishna  aliongeza kwamba Kidata mamlaka hiyo ipo kwa ajili ya  kuwahudumia wananchi na kama kuna suala lolote au tatizo kuhusu kodi kuna ofisi katika mikoa yote ikiwa ni hatua ya kutatua shida zao na kama kuna mtumishi yoyote wa mamlaka hiyo atashindwa kumuhudumia mwanachi inavyotakiwa basi taarifa zitolewa mara moja kupitia namba zao zilizoko kwenye tovuti ya mamlaka hiyo, ambayo ni www.tra.go.tz ili kuimarisha huduma zetu kwa wateja.

  Aidha Kamishna Mkuu huyo amesema kuwa watawachukulia hatua wale wote ambao hawatalipa au hawajalipa kodi zao kwa kuwapeleka mahakamani kwa kukaidi kulipa kodi halali kwa mujibu wa Sheria.

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria na ina mamlaka ya usimamizi wa makusanyo ya Mapato Tanzania na kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na ukwepaji wa kodi uliotokana na sakata la upotevu wa makontena katika Bandari ya Dar es Salaam hivyo kuikosesha mapato Serikali lakini jitihada thabiti zimefanywa na mamlaka hiyo kukusanya madeni kutoka kwa wakwepa kodi na kuwafikisha mahakamani ambao wamekaidi kulipa.

  0 0

  Ben Pol
  With ‘NINGEFANYAJE’ (What was I supposed to do?) video topping the Top 10 East and Africa Rox Countdown charts on SoundCity and making a splash on MTV Base Africa, it was only a matter of time before Ben Pol put a twist on his hit song to bring us the official...REMIX!

  This New release(NINGEFANYAJE REMIX)brings togetherTanzania'sundisputed King of R&B Ben Pol,one ofNaija'sfinest multi -talented artiste and media personalityVJ Adams,and Tanzanian extraordinaire rapper G-Nakoof the WEUSI Hip Hop group.

  The song is now available on Tanzania's Music Selling platform MKITO and will soon be available itunes, Amazon, Spotify, Deezer and on all key music distribution channels.

  Consume without moderation!
  Be the first one to listen 'Press Play' and enjoy!

  0 0

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mbele ya Waku wa Mikoa mara baada ya kuwaapisha leo Ikulu jijini Dar.Rais Dkt Magufuli amewapa siku 15 Wakuu wa Mikoa kuwaondoa watumishi hewa walio katika orodha ya malipo ya mishahara ya watumishi wa umma katika Mikoa yao.Picha na Michuzi Jr-MMG

  Na Jacquiline Mrisho- Dar es salaam.     

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewapa siku 15 Wakuu wa Mikoa kuwaondoa watumishi hewa walio katika orodha ya malipo ya mishahara ya watumishi wa umma katika Mikoa yao.

  Rais Dkt. Magufuli amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa aliowateua Machi 13 mwaka huu ambapo amewaagiza washirikiane na Wakurugenzi wa Halmashauri kuwaondoa watumishi hewa.

  “Nimewapa siku 15 kuanzia leo mkashirikiane na Wakurugenzi wa Halmashauri zenu kuwatoa wafanyakazi hewa, nikigundua kuwa bado kuna wafanyakazi hewa, Mkurugenzi husika atafukuzwa kazi na atapelekwa mahakamani”,

  Na kusisitiza “Nimeamua kuwachagua nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika Mikoa yenu, nawaomba mkatimize majukumu yenu bila kuogopa” alisema Dkt. Magufuli.

  Aidha, Mhe.  Dkt. Magufuli amesikitishwa na utafiti wa watumishi uliofanywa katika Mikoa ya Singida na Dodoma ambapo imegundulika watumishi 202 wanalipwa mishahara hewa.

  Wakati wa utafiti huo, zaidi  ya watumishi 26,900 walioko katika Halmashauri 14 za Mikoa hiyo, watumishi 3,320 hawakuwepo kazini kwa sababu mbalimbali.Kwa mantiki hiyo, ukichukua utafiti huo wa Mikoa miwili ni dhahiri Serikali inapoteza mapato mengi kwa kulipa mishahara ya watumishi hewa nchi nzima.

  Vivyo hivyo, Mhe. Dkt. Magufuli amewasisitiza Wakuu wote wa Mikoa wakasimamie ilani ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwakuwa waliahidi kutatua kero za wananchi na wahakikishe wanazitatua ili wananchi waishi vizuri kwa amani ndani ya nchi yao.


  Naye Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Majiji na Halmashauri zote nchini wajiandae kupokea na kuzipangia matumizi shilingi milioni 50 za kila Kijiji zilizoahidiwa wakati wa kampeni kwa lengo la kuboresha na kuimarisha shughuli za maendeleo.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aende Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kufanya upya tathmini na kukagua ugawaji wa viwanja 843 kwenye
  manispaa hiyo.

  Waziri Mkuu Majaliwa alitoa agizo hilo jana (Jumapili, Machi 14, 2016) wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadharauliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mayunga mjini Bukoba.Alifikia hatua hiyo baada ya wananchi kubeba bango lenye ujumbe kuelezea kutopewa viwanja hivyo vilivyopimwa na Manispaa ya Bukoba. Viwanja hivyo vilipimwa na kugawiwa kwa wananchi ambao baadhi yao baada ya kulipa fedha, hawajapewa viwanja hivyo ikiwa ni takriban miaka zaidi ya 10.

  Akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Kagera, Waziri Mkuu alilazimika kumpandisha jukwaani Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Bw. Wallace Karia ili atoe maelezo ya nini kimekwamisha wananchi kupewa viwanja hivyo. Katika maelezo yake, Bw. Karia alisema mwaka 2003, vilitengwa viwanja 843, kati ya hivyo 352 vilikuwa eneo la Kyabitembe, 137 Ihungo na
  Rwome na vingine 132.

  Bw. Karia ambaye hana muda mrefu tangu ahamishiwe katika manispaa hiyo, alisema kumbukumbu za ofisi zinaonesha kuwa viwanja 182 ndio wahusika hawajapewa, na viwanja vingine 85 vilikuwa havijapimwa eneo la Kilimahewa na Kashai, huku kukiwa na vingine 5,000 vya mradi.

  Aliongeza kuwa walitarajiwa kuwalipa wananchi hao katika mwaka wa fedha 2016/17; kauli ambayo ilisababisha kelele kutoka kwa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa Waziri Mkuu. Kutokana na hilo, Waziri Mkuu aliingilia kati na kumueleza Mkurugenzi huyo kuwa kelele hizo zinaashiria kuwa watu hao hawajaridhishwa na majibu yake.

  Alisema anafahamu kuwa mkurugenzi huyo na meya ni wapya, lakini akawaagiza ndani ya mwezi mmoja, kufanya mapitio ya viwanja hivyo 843, na hasa watu 182 ambao hawajapatiwa viwanja wahakikishe wanawapatia kwa sababu viwanja vipo.

  “Rais mstaafu alikuja hapa na kupewa kilio cha kupunjwa fedha. Najua wakati huo mtasema ninyi hamkuwepo. Wewe (MD) na Meya wako mkae na kupitia mikataba na mafaili. Nyie na mkoa mkae pamoja na kujua vile viwanja vilivyochukuliwa na JWTZ. Nitamleta CAG hapa, ndani ya mwezi mmoja afanye mapitio ya viwanja tu,” alieleza Waziri Mkuu na kushangiliwa na maelfu ya wananchi.

  Katika mkutano huo, Waziri Mkuu pia aliwahakikishia wakazi wa Manispaa ya Bukoba kuwa watalipwa fidia zao baada ya kukubali kupisha ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh. bilioni 31. Waziri Mkuu aliendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa
  kutembelea wilaya za Misenyi na Karagwe na leo atakuwa wilayani Ngara.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, MACHI 15, 2016.


  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya akifuatilia hoja za wajumbe wa  Kikao cha Wataalam kutoka Wizara, Idara na Taasisi za serikali (hawapo pichani), walipokutana kwa ajili ya maandalizi ya kikao cha Kamati ya Taifa ya Uratibu wa maafa nchini (TANDREC),   tarehe 15 Machi, 2016Jijini Dar es Salaam.

   Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen, Mbazi Msuya akiwaongoza wajumbe kupitia makabrasha ya Kikao cha Wataalam kutoka Wizara, Idara na Taasisi za serikali walipokutana kwa ajili ya maandalizi ya kikao cha Kamati ya Taifa ya Uratibu wa maafa nchini (TANDREC),  tarehe 15 Machi, 2016, Jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ambaye pia niKamishna wa Operesheni, Rogatius Kipali akipitia makabrasha ya Kikao cha Wataalam kutoka Wizara, Idara na Taasisi za serikali walipokutana kwa ajili ya maandalizi ya kikao cha Kamati ya Taifa ya Uratibu wa maafa nchini (TANDREC), tarehe 15 Machi, 2016, Jijini Dar es Salaam..
   Baadhi ya Wataalam kutoka Wizara, Idara na Taasisi za serikali wakipitia makabrasha ya kikao walipokutana kwa ajili ya maandalizi ya kikao cha Kamati ya Taifa ya Uratibu wa maafa nchini (TANDREC), Jijini Dar es Salaam, tarehe 15 Machi, 2016.

   Afisa   Maafa wa Jeshi la Wananchi, Kanali Mohamed Mwakalikene akipitia makabrasha ya Kikao cha Wataalam kutoka Wizara, Idara na Taasisi za serikali walipokutana kwa ajili ya maandalizi ya kikao cha Kamati ya Taifa ya Uratibu wa maafa nchini (TANDREC), tarehe 15 Machi, 2016, Jijini Dar es Salaam. 


  Baadhi ya Wataalam kutoka Wizara, Idara na Taasisi za serikali wakipitia makabrasha ya kikao walipokutana kwa ajili ya maandalizi ya kikao cha Kamati ya Taifa ya Uratibu wa maafa nchini (TANDREC), Jijini Dar es Salaam, tarehe 15 Machi, 2016.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Baadhi ya waandishi wa kigoma wakimsikiliza ofisa wa TMF Dustan Kamanzi(hayupo pichani) wakati akilezea Tanzania Media Foundation mpya na jinsi ya kuomba ruzuku
  Ofisa Wa TMF  wa ruzuku  za vijijini  Dustan Kamanzi akiwaelezea waandishi wa Kigoma juu ya TMF mpya na jinsi ya kuomba ruzuku za vijijini kwa mwandishi mmoja mmoja.
  Ofisa wa TMF Razia Mawanga akiwaeleza waandishi wa Kigoma juu ya TMF mpya na jinsi ya kuomba ruzuku za mashirika

  Editha Karlo, wa blog ya jamii, Kigoma

  TANZANIA Media Fund(TMF) wameitambulisha TMF mpya kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma na kuwataka waandishi kuomba ruzuku zinazotolewa sasa kwa mfumo mpya. Akiilezea TMF mpya ofisa wa ruzuku za vijijini TMF Dustan Kamanzi alisema kuwa sasa hivi utaratibu umebadilika na umeboreshwa kwa waandishi na mashirika watakayoomba ruzuku. 

  Alisema waandishi watakaoenda kufanya kazi za vijijini watapewa ruzuku ya shilingi milioni 4 ambayo wataifanyia kazi kwa kipindi cha miezi mitatu kwa kuandika makala nne au vipindi vya radio na television.

  Kamanzi alisema kuwa kwa upande waandishi mmoja mmoja watakaomba ruzuku lazima ya vijijini au mjini na habari hizo lazima zilenge watu waliosahaulika au kutengwa na jamii. Alisema ruzuku hizo zinalenga kuongeza ubora wingi na anuwai za sauti na masuala ya watu wa kawaida katika vyombo vya habari. 

  Alisema ruzuku hizo zitawapa kipaumbele waandishi wanawake, waandishi chipukizi, waandishi wa kati na wenye hari ya kuandika habari za vijijini pia wenye uhakika wa wa kupata vyombo vya kutolea habari zao. 

  Naye Razia Mawanga alizungumzia ruzuku za taasisi kuwa zinalengo la kuviwezesha vyombo vya habari na taasisi za habari kutengeneza maudhui maalum yatakayovutia jamii. 

  0 0


  *Ni za matumizi ya sh. milioni 120 za Hospitali ya Mkoa

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera na kumpa siku tano Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Adam Swai amletee taarifa juu matumizi ya sh. Milioni 80 ambazo ni fedha za UKIMWI.

  Pia amemtaka ifikapo Machi 20, nwaka huu awasilishe taarifa nyingine ya matumizi ya sh. Milioni 40 za ukarabati wa jengo la wagonjwa maalum  (Grade A)

  Ametoa agizo hilo leo asubuhi (Jumanne,  Machi 15, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo baada ya kutembelea maeneo kadhaa yakiwemo wodi ya watoto, wodi ya wazazi, chumba cha wagonjwa mahututi (ICU ) na chumba cha kuhifadhia maiti.

  "Kulikuwa na frsha za ukimwi sh. Milioni 80 ambapo kila mtumishi alipaswa kupata sh. 200,000/- lakini ninyi mmewapa sh. 80,000 /-. RAS fedha hizi zimeenda wapi?  Nataka uniletee taarifa ofisini kwangu Dar es Salaam ifikapo tarehe 20 mwezi huu," alisema huku akishangiliwa.

  "Kwa mujibu wa taarifa ya CAG pale grade A kuna mgogoro wa sh. milioni 40. Wewe taarifa unayo lakini hujaifanyia kazi yoyote.  Nataka tarehe 20 nayo hii pia niipate na nione umetoa mapendekezo gani."

  Kuhusu tatizo la madaktari katika hospitali hiyo, Waziri Mkuu alisema atawasiliana na Waziri wa Afya ili madaktari watano ambao wanasubiri ajira rasmi lakini wameanza kazi kwa mkataba hospitali hapo wapewe ajira rasmi. Pia alisema amebaini upungufu wa madaktari bingwa uliopo katika hospitali hiyo.

  Pia aliahidi kufuatilia maombi yao ya gari la wagonjwa hasa ikizingatiwa kuwa anayo maombi kama hayo kutoka hospitali za Mawenzi (Kilimanjaro), na Ligula (Mtwara).

  Katika hatua nyingine,  Waziri Mkuu aliwapongeza watumishi wa hospitali hiyo kwa huduma zao nzuri wanazotoa kwa wagonjwa.  "Nineridhishwa na kauli walizotoa wagonjwa juu yenu. Tofauti na hospitali nyingine nilizopita, wao wamesema hawajatozwa fedha ili wapatiwe dawa. Nimefarijika sana."

  "Endeleeni kuwa na huruma kwa wagonjwa. Endeleeni kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa. Hawa wagonjwa hawakuogopa kuelezea hisia zao. Wamesema kwa uwazi kabisa kwamba mnawajali," alisema.

  Mapema,  akisoma taarifa mbele ya Waziri Mkuu,  Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk.  Thomas Rutachunzibwa alisema hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madaktari bingwa pamoja na madaktari wa kawaida.

  "Tunao madaktari 10 lakini wanaohitajika ni 30. Tunao madaktari wasaidizi wanane lakini wanaohitajika ni 23 na madaktari bingwa waliopo ni watatu tu lakini wanaohitajika ni 24. Tunaomba tupatiwe watumishi hawa ili tuweze kutoa huduma kulingana na matarajio ya wananchi wetu," alisema.

  Akifafanua kuhusu mahitaji ya hospitali hiyo, Dk. Rutachunzibwa alisema wanahitaji sh. bilioni 1.8 kwa mwaka bila ya kuweka mishahara ili waweze kufanya kazi yao kwa umakini. "Tunahitaji sh. milioni 802 kwa ajili ya matumizi ya kawaida lakini tunachopokea hivi sasa ni sh. milioni 299 ambayo ni sawa na asilimia 30 ya mahitaji yetu."

  "Bajeti ya dawa tuliyotenga ni sh. milioni 960 lakini tunapokea sh. milioni 143 ambazo kiuhalisia zinatosha kwa matumizi ya miezi miwili tu. Tumelazimika kufanya marekebisho ya bei za dawa kwa ridhaa ya Bodi ya hospitali ili tuweze kumudu kutoa huduma kwa wananchi," alisema.

  Alisema ili kubana mianya ya upotevu wa mapato, wanahitaji kuwa na kompyuta 15 lakini hadi sasa wamefanikiwa kununua kompyuta mbili tu ambazo ziko Grade A na idara ya wagonjwa wa nje (OPD) ili kuimarisha utaratibu wa ukusanyaji mapato.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMANNE, MACHI 15, 2016.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga  kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga kuwa mkuu wa mkoa wa Geita,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Emmanuel Edward Maganga kuwa mkuu wa mkoa wa Kigoma,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Polisi,Zelote Steven Zelote kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mh.Anne Kilango Malecela kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Paul Christian Makonda kuwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.


  0 0


  0 0

  Mtoa mada kuhusu Huduma kwa mteja Bi. Joy Nyabongo akiwafunza maafisa habari na mawasiliano wa Serikali kuhusu jinsi gani ya kutoa huduma nzuri kwa wateja wao wanapokuwa katika vituo vyao vya kazi.
  Mtoa mada kuhusu Huduma kwa mteja Bi. Joy Nyabongo akigawa moja ya DVD kwa afisa habari wa TFDA Bi.Gaudensia Simwanza kwa ajili ya kumsaidia katika utendaji wa kazi yake.DVD izo zina mafunzo mbalimbali yanayousu kumhudumia vyema mteja.
  Mtaalamu wa masuala ya Itifaki Balozi Chilambo(aliyesimama) akitoa mada kuhusu itifaki kwa maafisa mawasiliano na habari wa serikali watakapokuwa katika majukumu ya kiserikali.
  Afisa Habari wa jiji la Mwanza Bw.Kaaya Elirehema Mosses akichangia jambo wakati wa kikao kazi cha maafisa habari wa serikali kinachofanyika jijini mkoani Morogoro.

  0 0

  indexMkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki,Dk.Asser Mchomvu .KAI1KAI2KAI3 

  Hospitali ya Kairuki (KH) inatimiza miaka 29 mwezi huu siku ya Alhamisi tangu ilipoanzishwa tarehe 17.03.1987.

  Akizungumzia maadhimisho hayo Dr Asser Mchomvu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki anasema kuwa uongozi wa KH unapenda kuwashukuru wadau wote walioshirikiana nao katika kuiwezesha KH kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa wote.

  Dr Mchomvu anaongeza kuwa katika kutambua mchango wa wadau mbalimbali kwa kufikisha miaka 29, KH itafanya maadhimisho yake kwa kutoa msaada kwa vituo vya afya pia kufanya upimaji wa kinywa na meno bure.

  “Madhimisho haya yataambatana na utoaji wa vifaa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha, ambapo KH itatoa msaada wa vitanda vya hospitali na magodoro siku ya Alhamis tarehe 17.03.2016,” alisema Dr MchomvuAlisisitiza kuwa pamoja na hilo, KH itatoa pia huduma ya upimaji na ushauri wa afya ya kinywa na meno kwa wananchi kwa siku mbili bure ( siku ya Jumatano na Alhamis tarehe 16 na 17, Machi 2016) kuanzia saa 2 asubuhi, pale pale Hospitali ya KAIRUKI, Mikocheni, Dar es Salaam.

  Dr Mchomvu anaeleza kuwa, kutakuwa na ghafla fupi ambapo Mkurugenzi atatoa salamu baada ya kukata keki na watoto waliozaliwa KH mwaka 1987. Watu wote wanakaribishwa katika ghafla hiyo itakayofanyika hapo KH siku hiyo ya Alhamisi tarehe 17.03.2016 saa 10 jioni.

  Kwa upande mwingine KH imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma zake huku ikizingatia ufanisi na ubora katika utowaji wa huduma zake kwani inatumia vifaa vya kisasa ambavyo vina ubora wa hali ya juu.

  0 0


older | 1 | .... | 795 | 796 | (Page 797) | 798 | 799 | .... | 1903 | newer