Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

ZIARA YA KAMATI NDOGO YA BUNGE YA SHERIA KATIKA IDARA YA MPIGACHAPA MKUU WA SERIKALI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa Kuandaa na Kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za Bunge Mhe. William Ngeleja (katikati) akiwa katika ziara yake katika Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Machi, 15, 2016. 
 Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa Kuandaa na Kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za Bunge Mhe. William Ngeleja akielezea umuhimu wa kuhifadhi nyaraka za serikali wakati wa ziara yake katika Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Machi 15, 2016 wa kwanza kulia ni Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo. 
 Mbunge wa Manyoni Mashariki Mhe.Daniel Mtuka akiangalia moja ya kitabu kilichochapishwa na Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa ziara ya Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa kuandaa na kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za bunge, wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uchapishaji Bi.Joyce Benjamin. 
 Katibu Mkuu Sera na Uratibu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Hamis Mwinyimvua (wa sita kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa kuandaa na kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za Bunge pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu, mara baada ya ziara ya kamati hiyo Machi 15, 2016. 
 Mjumbe wa Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa Kuandaa na Kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za bunge Mhe. Halima Mdee (mb) akichangia hoja wakati wa kikao cha kamati hiyo katika Ukumbi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Machi 15, 2016.
Katibu Mkuu Sera na Uratibu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Hamis Mwinyimvua (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa Kuandaa na Kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za bunge Mhe. William Ngeleja wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Machi 15, 2016.
 Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa Kuandaa na Kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za Bunge Mhe. William Ngeleja (kushoto) akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo (hawapo pichani) wakati wa ziara yake katika Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Machi, 15, 2016 wa kwanza kulia ni Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo. 

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI BAADA YA KUWAAPISHA WAKUU WA MIKOA IKULU JIJINI DAR LEO

BAADHI YA VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO

TCRA YAADHIMISHA SIKU ZA HAKI YA WATUMIAJI WA HUDUMA ULIMWENGUNI JIJINI DAR

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Ally Simba akihutubia washiriki wa semina hawapo pichani wakati akifunga semina, siku ya watumiaji wa huduma Ulimwenguni.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, akihutubia kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika ufunguzi wa semina ya siku ya haki za watumiaji wa huduma Ulimwenguni.
 Baadhi ya washiriki wa semina wakimsikiliza mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo hayupo pichani siku ya watumiaji wa huduma Ulimwenguni  inayoadhimishwa tarehe 15 Machi, ya kila Mwaka.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Ally Simba (kushoto) siku ya watumiaji wa huduma Ulimwenguni.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA

$
0
0
 aziri Mkuu, Kassim Majliwa kizungumza na wakimbizi wa Burundi walioko katika kambi ya  Lumasi  iliyopo wilayni Ngara. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15 2016.
 Baadhi ya wakimbizi wa Burundi walioko kwenye kambi ya Lumasi iliyopo wilayani Ngara wakimsikilza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2916.
 Waziri Mkuu, Kassim  Majliwa akiagana na viongozi kambi ya wakimbizi wa Burundi ya Lumasi iliyoko Ngara  viongozi wa wilaya na UNHCR baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na waumishi wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO baada ya kuwasili kwenye eneo unapowekwa mtambo mpya wa kufua umeme mjini Ngara ambao aliweka jiwe la msingi la ujenzi wake Machi 15, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiweka jiwe la msingi la usimikaji mtambo mpya wa kufua umeme wa Ngara akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2016. Kushoto ni Naibu Waziriwa Nishati na Madini Dkt. Kalemani.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiweka jiwe la msingi la usimikaji mtambo mpya wa kufua umeme wa Ngara akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2016. Kushoto ni Naibu Waziriwa Nishati na Madini Dkt. Kalemani.
 Moja ya mabango ambayo yalibebwa na wananchi wa Ngara katika mkutano uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Ngara Machi 15, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Wananchi wa Ngara baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Mtambo Mpya wa Umeme mjini Ngara Machi 15, 2016.
  Waziri Mkuu Kassim Majliwa akizungumza na Watumishi na Viongozi wa Mkoa wa Kagera kuhitimisha ziara yake mkoani humo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilay ya Ngara Machi 15, 2916. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu)

KATIBU MKUU NISHATI ATOA MAAGIZO EWURA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi (aliyesimama), akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Mamlaka hiyo wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa alipofanya ziara ya siku moja Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na Viongozi Waandamizi wa Mamlaka hiyo, wakiwa katika kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani), alipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
 Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati  na Maji (EWURA), Omary Bendera (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa Vitabu mbalimbali vyenye maelezo kuhusu Mamlaka hiyo, wakati alipotembelea Makao
Makuu ya EWURA hivi karibuni.
 Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Omary Bendera (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa Vitabu mbalimbali vyenye maelezo kuhusu Mamlaka hiyo, wakati alipotembelea Makao Makuu ya EWURA hivi karibuni.
Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Omary Bendera (kulia) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo Vitabu mbalimbali vyenye maelezo kuhusu Mamlaka hiyo, wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Justin Ntalikwa Makao Makuu ya EWURA hivi karibuni.

SHUGHULI YA MAWLID YA KUMSIFU MTUME WETU MUHAMMAD (S.A.W) JUMAMOSI SEGEREA MWISHO

$
0
0
ASSALAAM ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATU
Al Madrasat Rahman iliyopo Segerea mwisho,Dar-es-Salaam
.
INAWAALIKA KATIKA SHUGHULI YA MAWLID YA KUMSIFU
MTUME WETU MUHAMMAD (S.A.W) siku ya jumamosi 19/03/2016 Jitokezi kwa wingi!

Ndugu zetu watukufu wa kiislam Uongozi wa Al Masjid Qubbah na  Madrasat Rahman ya Tabata Segerea Mwisho,Dar-es-salam inawaalika waislamu wote waume kwa wanawake,Masheikh,na Madrasat mbalimbali kuwa siku ya jumamosi ya tarehe 19/3/2016 kutakua na Maulid ya kumsifu bwana Mtume Muhammad (S.A.W) katika viwanja vya madrasat Rahman segerea mwisho. 

Kama ilivyoada kuanzia saa nne asubuhi kutakua na maulid ya kina mama mpaka saa kumi alasiri, na baada ya swalatul inshai kutakua na maulid ya jumuiya waume kwa wanawake.Jitokezeni kwa wingi katika shughuli hii,tuuzaje uwanja wa shughuli hii ,kushiriki kwenu ndio mafanikio na baraka ya shughuli hii ya Maulid ya Mtume Muhammad(S.W.A)
 Karibuni sana.INSHAALLAH

WABILLAH TAUFIQIH mawasiliano Simu 0777 000036, au 0712 840 960

“Mwanamke wa Afrika bado anakabiliwa na changamoto” - Waziri Ummy Mwalimu

$
0
0

9222e2ae-9627-4a09-abd3-72692b57d550Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu akiwa katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Tanzania wa Kudumu Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manong.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu ( Mb) ametoa hutuba kwa niaba ya Kundi la Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Mkutano huu wa wiki mbili .

unawakusanya wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na Asasi za Kiraia ambapo hujadiliana na kubalishana uzoefu na kuelimishana kuhusu hatua mbalimbali ambazo serikali zao zinachukua katika kuboresha maisha ya mwanamke na mtoto wa kike.

Wakati mamia ya wanawake kutoka serikalini na Asasi za Kiraia wakiwa wanakutana hapa Umoja wa Mataifa kwa mkutano wao unaojadili hali yao katika maeneo mbalimbali. Mamia mengine ya wanawake hususani wale wa Afrika wanaendelea kukumbana na changamoto lukuki zinazowarudisha nyuma kimaendeleo.

Ni wanawake hao wanaoishi katika nchi zenye migogoro, vita visivyokwisha, wenye kukabiliwa na uhaba na ukosefu mkubwa wa chakula, maji safi na salama, matatizo yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, ndio ambao Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu(Mb) ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya ushirikiano ili malengo mapya ya maendeleo endelevu (Agenda 2030) yaweze kuwafikia.

Waziri Mwalimu ametoa wito huo jana jumatatu, wakati alipotoa hutuba kwa niaba ya nchi za Afrika katika siku ya kwanza ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya wanawake (CSW) ambao umeanza hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

08b03dc1-8077-433f-a8db-425449efcc49Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu akitoa hotuba katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). 

Changamoto hizo pamoja na nyinginezo nyingi zikiwamo kutopata fursa ya huduma za afya ya uzazi salama, elimu na usawa wa kijinsia zinamfanya mwanamke wa Afrika ashindwe kushindana na wanawake wenzie hususani wale walioko katika mataifa yaliyoendelea. 

Waziri Mwalimu ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu wa wiki mbili, alitoa hotuba hiyo kwa niaba ya nchi za Afrika kutokana na kwamba Tanzania kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ni Mwenyekiti wa Kundi la Nchi za Afrika kwa mwezi huu wa March.

Amewaeleza washiriki wa mkutano huo waliofurika katika Ukumbi Mkuu wa Mikutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwamba ingawa pamekuwapo na makubaliano na mapendekezo mengi kuanzia yale yaliyofikiwa huko Beijing, bado mwanamke anayeishi katika nchi zenye migogoro na vita barani Afrika ataendelea kuachwa nyuma na hivyo kukosa fursa ya kushinda na wenzie.

“ Ingawa vita, ukame wa kutisha, ukosefu wa chakula, ukosefu wa maji safi, ukichanganya na ukosefu wa fursa za kiuchumi, kijamii na kisiasa ni matatizo yanayowakabili watu maskini lakini mwanamke ndiye anayeathirika zaidi,” alieleza Waziri Mwalimu.
Na kuongeza kwamba Afrika inaendelea kutilia mkazo hoja ya kuwashirikisha wanawake katika majadiliano na utoaji wa maamuzi katika masuala yanayowagusa yakiwamo masuala yanayohusu mabadiliano ya tabia nchi na usuluhishi wa migogoro. 

Alieleza kwamba, nchi zinazoendelea na zilizoendelea zinapashwa kuongeza kasi ya ushirikiano na ubia baina yao ili kufanikisha utekelezaji wa Agenda 2030), Makubaliano juu Mabadiliko ya Tabia nchi yaliyofikiwa huko Paris Ufaransa mwaka jana na makubaliano yaliyofikiwa na waafrika wenye kupitia Ajenda 2063 , ili katika umoja wake dunia basi iweze kumwondoa mwanamke na jamii nzima kutoka hapa ilipo na kufikia hali bora zaidi ya maisha.

Kama hiyo haitoshi Waziri alisema, Afrika inaamini pia katika uwezeshwaji wa Sekta binafsi, kupanua wigo wa ujasiliamali kama njia mojawapo ya kukuza uchumi endelevu , usawa wa kijamii, usawa wa jinsia, ulinzi wa mazingira na uwezeshaji wa mwanamke.
Mada kuu ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake, ni “Uwezeshaji wa Wanawake na uhusiano wake na Ajenda 2030.

Awali akizungumza mwanzoni mwa mkutano huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amasema tangu alipoingia madarakani mwaka 2006 amejjitadi kuongeza nafasi za viongozi wanawake katika Idara za Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.


Akitilia msisitizo hoja na haja ya kupanua wigo wa wanawake kushika nafasi katika ngazi za juu za maamumizi, Ban Ki Moon amesema, ingawa nchi nyingi zimejitahidi sana kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za juu za uongozi bado kuna Nchi Tano ambazo hazina wanawake katika Mabunge yao ili hali Nchi nyingine 7 hazina mawaziri wanawake katika serikali zao.

Naye Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa Bw Monges Lykketoft, akizungumza wakati wa mkutano huo, pamoja na kusisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Agenda 2030 ambayo ameitaja kuwa ni jumuishi ameendelea kupigia chapuo la kutaka Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa awe Mwanamke.

Na Mwandishi Maalum, New York

DARAJA LA KIGAMBONI KUFUNGULIWA RASMI APRILI.

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema daraja la Kigamboni litafunguliwa rasmi Aprili, 16 mwaka huu.
Amesema kazi inayoendelea sasa hivi ni kupitisha magari maalum kwa ajili ya kupima ubora wa daraja hilo ili kujiridhisha kabla ya kukabidhiwa rasmi Serikalini.
Amewataka watumiaji wa daraja hilo kuwa waangalifu, kulinda miundombinu na kuepuka vitendo vya hujuma  ili lidumu kwa muda mrefu.“Daraja hili lina urefu wa mita 640, barabara sita, tatu zinapanda na tatu zinashuka, hivyo tunawaomba wananchi watakaovuka kuzingatia usafi na ustaarabu”, amesema Profesa Mbarawa.
Amebainisha kuwa Serikali itaweka sheria kali kwa wote watakaokiuka matumizi sahihi ya daraja hilo na kusisitiza umuhimu wa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani wanapovuka katika daraja hilo.
Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja hilo Eng. Karim Mattaka amesema wataalam wanaendelea na taratibu za kulipima daraja hilo ili kujiridhisha kama linamudu kupitisha uzito uliokusudiwa kabla ya kulikabidhi kwa Serikali mapema mwezi ujao.
Amesema awamu ya kwanza ya kulipima daraja hilo imekamilika na sasa wanaendelea na awamu ya pili hadi watakapomaliza awamu nne ili kujiridhisha kabla ya kuanza kutumika.
Takribani shilingi bilioni 216 zimetumika katika ujenzi wa daraja hilo linalotazamiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa abiria na magari katika kivuko cha Magogoni na Kigamboni.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni Eng. Karim Mattaka alipokagua daraja hilo leo jijini Dar es salaam.
 Mwonekano wa daraja la Kigamboni ambalo litafunguliwa rasmi mwezi ujao.
Barabara za maingilio (inter change) ya Daraja la Kigamboni upande wa Kurasini.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja miradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Eng. John Msemo wakati alipotembelea daraja la Kigamboni kuangalia ujenzi wa daraja la Kigamboni leo jijini Dar es salaam.

DONDOO ZA MAGAZETI LEO

MWIGULU NCHEMBA AANZA SAFARI YA KUHAKIKISHA WAFUGAJI WANAACHA KUFUGA KIHOLELA,WAFUGE KWA VITARU.

$
0
0
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba akimuangalia mmoja wadume la ng’ombe anayetumika kuzalisha Mitamba kwenye kitaru namba 9 shamba la kitengule-Karagwe.
Baadhi ya ng’ombe waliopo kitaru namba 9 shamba la kitengule ambapo kwenye block hii moja kuna Ng’ombe zaidi ya 800 wanaolishwa na kuhudumiwa vizuri na mmiliki wa kitaru hiki
.Ng’ombe wakitoka kuogeshwa kwaajili ya kuua baadhi ya wadudu kama kupe wanaopendelea kukaa kwenye mwili wa ng’ombe.Hili ni moja ya josho la kisasa ndani ya kitaru namba 9.

Kufuatia ziara ya waziri mkuu,Mh:Kassim Majaliwa ndani ya mkoa wa Kagera akiwa ameambatana na waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani,Ziara hiyo imekuja na maagizo kadhaa ikiwamo wamiliki wote wa vitaru kwenye ranchi za Taifa ambao hawajaziendeleza waziachie mara moja na maeneo hayo yagawiwe upya,Waziri Mkuu ameagiza pia kwa wamiliki wa vitaaru ambao sio watanzania wajisalimishe au waondoke kwenye vitaru hivyo kabla hatua kali hazijaanza kuchukuliwa.

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba akiwa na timu yake ya wataalamu wameshaanza kupitia vitaru vyote “blocks” na wamiliki wake ikiwepo pia idadinya mifugo kwa kila block,Hii leo Mwigulu Nchemba amekutana na wamiliki wa vitaru kwenye shamba la Kitangile-Karagwe na kuagiza wamiliki wote ambao hawajaendeleza maeneo wanayoyamiliki yanachukuliwa na serikali kwaajili ya kuwapatia watanzania wenye uwezo wa kuziendesha.

Mwigulu Nchemba ameagiza pia wamiliki wa vitaru kuacha mchezo wa kukodisha na kuingiza mifugo kutoka kwa wafugaji haramu wa nchi jirani,kitendo hicho ni kosa na yeyote atakayebainika anakwenda jela na adhabu kali itafuta. Mbali na vitaru hivyo,Waziri Mkuu akishirikiana na waziri wa kilimo wameagiza ofisi ya mkuu wa mkoa wa kagera kuondoa wavamizi wote kwenye pori tengefu ya serikali kabla hatua zingine zinazofuata kuanza kutekelezwa.
Kupitia uwekezaji mzuri kwenye kitaru namba 9 cha shamba la Kitengule,Mwigulu Nchemba ametoa rai kwa wafugaji wote nchini kuanza kujipanga kufuga kwa mfumo wa vitaru ili kuachana na ufugaji holela unaopelekea migogoro mbalimbali na wakulima.
Picha/Maelezo na Festo Sanga Jr.

Airtel yazindua duka jipya ndani ya Mwanza Mall

$
0
0
Kamanda wa Polisi Wilaya ya ilemala , Sweetbert Kisha akikata utembe kuzindua duka jipya la Airtel Airtel lililopo ndani ya Rockcity shopping Mall jijini Mwanza, akishuhudia Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel, Adriana Lyamba.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya ilemala , Sweetbert Kisha na Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel, Adriana Lyamba wakikata keki kwa pamoja wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel lililopo ndani ya Rockcity shopping Mall jijini Mwanza, akishuhudia (kuli) ni wakala Mkuu wa Airtel Money Mwanza, Mohamed Gichani.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel, Adriana Lyamba akitoa maelezo kwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya ilemala , Sweetbert Kisha kuhusu huduma ya Airtel Money inayotelewa katika duka jipya la Airtel wakati uzinduzi wa duka jipya la Airtel lililopo ndani ya Rockcity shopping Mall jijini Mwanza.

WAZIRI MWAKYEMBE ATOA RAI KWA TAASISI MBALIMBALI NA WADAU KUIPITIA RIPOTI YA UCHAGUZI MKUU ULIOPITA ILI KUBORESHA CHAGUZI ZINAZOKUJA

$
0
0
Mgeni rasmi,Waziri wa sheria na Katiba Dkt Harrison Mwakyembe akifafanua jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na Ripoti ya maoni ya jumla  kuhusu uchaguzi Mkuu uliopita,aliyoipokea kutoka kwa Waandaaji  CEMOT (umoja wa taasisi za waangalizi wa ndani wa uchaguzi inayohusisha Kamati ya Uangalizi wa Uchaguzi (Temco) na Muungano wa taasisi zisizo za kiraia za kusimamia uchaguzi (Tacceo) ),kwenye semina iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Hyatt Hotel jijini Dar na kuwakutanisha Wadau mbalimbali wakiwemo Tume ya Uchaguzi (NEC),Polisi,PCCB pamoja na Nchi Wahisani .Pichani kushoto ni Mjumbe wa kamati ya CEMOT Bwa.Ezekiel Massanja

Katika mahojiano mafupi na Waandishi wa habari mara baada ya kuipokea ripoti hiyo,Dkt Mwakyembe alisema kuwa Ripoti hiyo iliangalia mapungufu yaliyokuwepo na namna ya kuyaboresha,Dkt Mwakyembe ametoa rai kwa Serikali,taasisi mbalimbali na wadau wengine waweze kuipitia ripoti hiyo na kujadiliana ili kuboresha chaguzi nyingine zinazokuja.
 Wa pili kulia ni Mgeni rasmi,Waziri wa sheria na Katiba Dkt Harisson Mwakyembe akiandika jambo wakati ripoti ya maoni ya jumla  kuhusu uchaguzi Mkuu uliopita,aliyoipokea kutoka kwa Waandaaji  CEMOT  ikisomwa.
 Mkuu wa Waandaaji wa Ripoti ya maoni ya jumla  kuhusu uchaguzi Mkuu uliopita (CEMOT),Dkt.Alexander Makulilo akisoma ripoti hiyo mbele ya Wadau na walioshiriki kuiandaa ripoti hiyo.
  Baadhi ya Wadau walioshiriki kundaa Ripoti ya maoni ya jumla  kuhusu uchaguzi Mkuu uliopita,wakifuatilia kwa makini wakati ripoti hiyo ikisomwa. 

WAZIRI MKUU AAGIZA KUFUTWA UMILIKI WA MASHAMBA MAKUBWA 11 WILAYANI NGARA

$
0
0
·         Yana ukubwa ekari 7,700 katika vijiji viwili tu
·         Aagiza Afisa Ardhi arudishwe kutoka Rorya kusaidia uchunguzi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kufutwa mara moja umiliki wa mashamba makubwa 11 yenye ukubwa wa ekari 7,700  kwenye  vijiji vya Kasharazi na Rwakalemera wilayani Ngara Kagera, ambayo hayana hati na yametelekezwa.

Ametoa agizo hilo leo asubuhi  (Jumatano, Machi 16, 2016) wakati akizungumza na wakazi wa vijiji vya Kasulo na Rwakalemera katika kata ya Kasulo wilayani Ngara akiwa njiani kuelekea mkoa wa Geita.

Waziri Mkuu alilazimika kufanya mkutano huo mapema asubuhi baada ya kuamua kuitisha uongozi wa wilaya ya Ngara ufike kwenye mkutano huo ili kujibu kero za wananchi waliosimamisha msafara wake jana wakati akielekea Ngara mjini.

Uamuzi huo unafuatia hatua ya Waziri Mkuu kumwita kwenye mkutano huo Afisa Ardhi na Maliasili wa Wilaya, Bi. Betty Munuo ili aeleze chanzo cha mgogoro wa ardhi katika vijiji hivyo.

Bi. Munuo ambaye amehamishiwa wilaya hiyo Agosti, mwaka jana,  alisema aliyakuta malalamiko hayo na amefanya uchambuzi wa majina ya wamiliki wote wa mashamba na walikuwa wanapanga kuwapatia notisi ili wajieleze.

Katika orodha yake, Bi. Munuo alitaja wamiliki 18 wa mashamba makubwa lakini kati yao ni wamiliki saba tu ambao mashamba yao yana hati lakini matatu ndiyo yameendelezwa na manne hayajaendelezwa.

Mashamba yaliyoendelezwa yanatumika kwa kilimo,  ufugaji na shule. Nayo yanamilikiwa na Dayosisi ya Rulenge (shamba na. 606 lenye ekari 161 liko Mbuba); Dario Zakaria (shamba na. 639 lenye ekari 282 liko Nyakariba) na Masista wa Mt. Fransisco (shamba na. 234 lenye ekari 759 liko Kasulo).

Mashamba manne yenye hati lakini yametelekezwa ambayo yote yako kijiji cha Rwakalemera ni ya Abdallah Sadala na. 235 lenye ekari 521; Mahsen Saidi shamba na. 333 lenye ekari 458; Mshengezi Nyambele shamba na. 746 lenye ekari 388 na  Mushengezi Nyambele shamba na. 745 lenye ekari 497.


Akitangaza uamuzi wake, Waziri Mkuu aliwataja wamiliki wa mashamba yasiyo na hati kuwa ni Bw. Joseph Rugumyamheto mwenye shamba na. 527 (ekari 505 liko Rwakalemera); Bw. Nicolaus Kidenke shamba halina namba na ukubwa wake haujulikani; Bw. Gwasa Angas Sababili shamba na. 714 (ekari 236 liko Kasharazi);  na Bw. Makumi Adili Rufyega (ekari 500 liko Rwakalemera).

Wamiliki wengine ambao mashamba yao yapo kijiji cha Rwakalemera ni Paulo Shikiri ekari 250; Frank Mukama Derila ekari 750; Godfrey Kitanga ekari 800; Philemon Mpanju ekari 200; Issa Sama ekari 500; Hekizayo Mtalitinya ekari 225 na Joel Nkinga ekari 1,250.

Waziri Mkuu aliagiza ifanyike sensa ili kubaini kama wamiliki wa mashamba hayo yote ni Watanzania au la. "Haya yenye hati nataka yafanyike mapitio ya hati zao na kubainisha ni namna gani walipatiwa hati hizo. Nataka taarifa inifikie ofisini kwangu Dar es Salaam ifikapo tarehe 20 Machi, 2016," alisema.

Ili kukamilisha kazi hiyo, Waziri Mkuu ameagiza kurejeshwa mara moja kwa aliyekuwa Afisa Ardhi wa Wilaya hiyo, Bw. Enock Mponzi ambaye amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ili aje asaidie uchunguzi wa ugawaji wa maeneo hayo.

Alimtaka Mwenyekiti wa kijiji cha Rwakalemera, Bw. Brighton Kemikimba aitishe mkutano wa kijiji kabla ya tarehe 31 Machi 2016 na abainishe mashamba yote makubwa ambayo yanazidi ekari 50. Pia afuatilie kama yana kibali cha Baraza la Madiwani.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu ameagiza kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Bw. Colnel Ngudungi na kutaka arejeshwe wilayani humo kujibu tuhuma za kuhusika na upotevu wa fedha za mauzo ya mbao kutoka kwenye msitu wa Rumasi, wilayani humo.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera,  Bw. Adam Swai ameagizwa kumwandikia  barua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga ili atekeleze maagizo hayo na Bw. Ngudungi arejeshwe Ngara kujibu tuhuma hizo. Bw. Ngudungi alihamishwa  kwenda Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga,  Agosti 2015.

Akiwa njiani kuelekea Ngara jana mchana (Machi 15, 2016), waziri Mkuu alisimamishwa katika kijiji cha Rwakalemera na wananchi wenye mabango wakiomba kurejeshewa ardhi ya kijiji huku baadhi yao wakidai wanatishiwa na bunduki pindi wakisogelea mashamba hayo makubwa.

Pia walidai kuuzwa kwa msitu wa Rumasi na mapato kutojulikana yalipokwenda huku wakidai kuwa kijiji chao hakipati mapato yoyote kutokana na minada ya ng’ombe inayofayika kijijini hapo wakati sharia inataka asilimia 20 ya mapato ibakizwe kijijini.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, MACHI 16, 2016.

WAZIRI KITWANGA ATUA ZANZIBAR, AKUTANA NA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akikagua gadi maalumu iliyoandaliwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi Zanzibar alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, mjini Magharibi Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar, Makamanda wa Polisi, Wakuu wa Upelelezi pamoja na Maafisa Wanadhimu wa mikoa mitatu ya Unguja. Kulia meza kuu ni Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akipewa maelezo na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame (kulia) wakati wa kikao chake na Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar, Makamanda wa Polisi, Wakuu wa Upelelezi na Maafisa Wanadhimu wa mikoa mitatu ya Unguja.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimuuliza jambo Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ajili ya ziara ya kikazi Zanzibar. Kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimsalimia Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame, mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ajili ya ziara ya kikazi Zanzibar. Kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NDEGE MPYA YA MIZIGO YAWASILI ABUDHABI KIJIUNGA NA KITENGO CHA MIZIGO CHA ETIHAD

$
0
0
KITENGO cha mizigo cha Etihad kimepokea ndege mpya aina ya Boeing 777 ambayo itawezesha kitengo cha mizigo cha shirika la ndege la Etihad kundelea kutanua mipango yake kwa mwaka 2016. Ndege hiyo imekua ya 11 katika kitengo hicho ambapo tayari imeshaanza kazi rasmi Machi 01 mwaka huu.

Kitengo cha mizigo cha Etihad kilitangaza kuwa kingepokea ndege zingine mbili katika maonyesho ya ndege ya Dubai mwaka jana, na kutumia sehemu ya dola bilioni 67 za kimarekani kwa oda iliyotolewa mwaka 2013 kwa ajili ya ndege 199. Ndege hizo mbili zilizoongezwa zina thamani ya dola milioni 637 za kimarekeni na ndege ya pili imewasili Abu Dhabi mwezi huu.

Ndege hizo mpya zitakua na siti tisa ambazo zitaruhusu kitengo hicho cha mizigo cha Etihad kubeba na watu wengine kama sehemu ya mpango wa kubeba farasi wasafirishwao kwa anga, ambayo inasaidia kwa wanyama hao wenye thamani kubwa. Zitakua ndege za kwanza katika kitengo cha mizigo cha Etihad kuwa katika muundo huu. 

Wanyama wasafirishwao kwa anga husimamiwa na mameneja ambao pia husaidiwa na timu ya watunzaji wakiwa angani na pia ardhini, ambapo farasi hao watasafirishwa kwenda sehemu tofauti katika mabara ya Ulaya, Asia, Amerika, Afrika na Australia.

Kevin Knight, Afisa Mkuu wa mipango na mikakati wa shirika la ndge la Etihad alisema, “Ndege iliyoongezwa inatupa fursa ya kutanua kitengo chetu cha mizigo na kukuza soko letu pia. Mwaka uliopita, tuliweza kujitanua katika mabara ya Amerika ya Kusini, Afrika na Asia na ndege hii mpya itaongeza uwezo na kutuwezesha kukua zaidi kwa kupitia mtandao wetu, lakini la muhimu ni pia kuongeza fursa za kukuza mikataba yetu sehemu mbali mbali duniani”.

Mwaka 2015, kitengo cha mizigo cha Etihad kilikuza upatikanaji wake ulimwenguni kwa kutoa huduma katika vituo vipya 6 vya shirika la ndege la Etihad ikiwa ni pamoja na Edinburgh, Madrid na Kolkatta. Etihad sasa inafanya kazi za huduma ya mizigo kwa ratiba maalum katika vituo vya mizigo pekee ambavyo ni; Hahn, San Juan, Bogota, Guangzhou, Dakar, Douala, Eldoret, Hanoi, Houston, Nouakchott, Sharjah na Tbilisi.


Ndege zilizopo kitengo cha mizigo cha Etihad kwa sasa zipo tatu aina ya Boeing 777Fs, Boeing 747s na Airbus A330s. Kitengo hicho cha mizigo cha nchi za umoja wa Kiarabu kwa sasa kinahudumia vituo 14 vya mizigo pekee duniani kote kutoka katika kituo chake kikuu cha Abu Dhabi na ina uwezo wa kubebwa juu ya meli ya shirika la ndege la Etihad yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 100.

“Toka iingie katika huduma miaka 7 iliyopita, ndege ya mizigo 777 imezidi kutambulika kama ndege bora ya mizigo kubwa na bora duniani yenye injini mbili pacha,” alisema Marty Bentrott
Makamu wa Rais wa Mauzo Etihad kwa Mashariki ya Mbali, Urusi, na Asia ya kati. “Tunajivunia kuwa na ndege ya mizigo 777 ikiwa na mchango muhimu katika kitengo cha mizigo cha Etihad wakati ikiendelea kuimarisha na kukuza kitengo hicho sehemu mbali mbali duniani”.

Kitengo hicho cha mizigo cha Etihad huingiza zaidi ya dola bilioni moja kama mapato yake kwa mwaka na kuripotiwa kukua kwa kasi kubwa kwa mwaka 2015 kikiwa na tani 592,090 za mizigo na barua pepe zilizosafirishwa kwa ujumla, ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 4 toka hesabu za mwaka 2014. Kitengo hicho pia ndicho kiini kwa asilimia 88 kwa kuingiza na kusafirisha mizigo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi.

Kikiwa kimeanzishwa mwaka 2004, kitengo cha mizigo cha Eihad ndicho kitengo kikuacho kwa kasi katika kampuni ya ndege ya Etihad. Toka katika kituo chake kikuu kilichopo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi, kitengo cha mizigo cha Etihad kinatoa huduma mbali mbali za mizigo kwa wateja wake kikihusisha na ukuaji wake kimataifa.

KARIMJEE JIVANJEE YASAIDIA MATIBABU YA WATOTO WENYE SARATANI.

$
0
0
Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kulia) akimkabidhi Dk. Rehema Laiti cheti cha shukrani kwa kumaliza shahada ya uzamili katika matibabu ya saratani ya watoto na kwa mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya watoto. Katikati ni Dk. Trish Scanlan, Mwanzilishi wa Asasi ya Tumaini la Maisha.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kulia) akimkabidhi Dk. Shakilu Jumanne cheti cha shukrani kwa kumaliza shahada ya uzamili katika matibabu ya saratani ya watoto kwa mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya watoto. Katikati ni Dk. Trish Scanlan, Mwanzilishi wa Asasi ya Tumaini la Maisha.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kulia) akimkabidhi Dk. Moses Karashani cheti cha shukrani kwa mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya watoto wenye saratani. Katikati ni Dk. Trish Scanlan, Mwanzilishi wa Asasi ya Tumaini la Maisha.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari Moses Karashani aliyepewa nafasi ya kusoma uzamili wa kutibu saratani kwa watoto (kushoto) na Dk. Rehema Laitu (wa pili kushoto) na Dk. Shakilu Jumanne ambao walipatiwa vyeti vya shukrani kutokana na ubobezi katika matibabu ya saratani ya watoto.
 (Picha: Mpiga Picha Wetu)

 TAASISI ya Karimjee Jivanjee imetoa nafasi za masomo kwa madaktari watatu wa Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango wake kuwajengea uwezo madaktari wa Tanzania ili waweze kuwa wabobezi katika matibabu ya saratani kwa watoto. 

Madaktari hao wamepewa fursa za kusomea shahada mpya ya uzamili katika matibabu ya saratani kwa watoto wadogo inayotolewa na Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili. Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, amesema jijini Dar es salam leo kwamba taasisi hiyo inataka kuweka mazingira endelevu katika ubora wa huduma za afya kwa kuwajengea uwezo madaktari kuweza kuwatibu watoto wadogo wenye ugonjwa wa saratani. 

“Ili kutimiza lengo hili ni lazima wapatikane madaktari wenye sifa nchi nzima,” alisema Karimjee wakati akiongea kwenye hafla ya kuwapongeza madaktari waliomaliza kozi hiyo mwaka 2015 na wanaoanza kozi ya 2016 chini ya udhamini wa Karimjee Jivanjee Foundation.

 “Mwaka 2014, Tanzania haikuwa hata na daktari mmoja wa mwenye sifa za kutibu saratani kwa watoto lakini baada ya Daktari Trish Scanlan pamoja na Taasisi ya Tumaini la Maisha kuanzisha kozi hiyo ya uzamili kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili, taasisi ya Karimjee iliona kwamba ni muda muafaka kutoa mafunzo kwa madaktari wa Kitanzania katika eneo hili na ndio maana tuliamua kusaidia program hii.” 

 Mwaka 2014 tulitoa nafasi za masomo kwa madaktari wawili kusomea kozi hiyo mpya na pamoja na mafunzo ya miezi mitatu nchini Ireland ili kupata uzoefu wa kimataifa ambapo kozi nzima iligharimu shilingi milioni 70. Madaktari walionufaika na program hiyo ni Dokta Rehema Laiti na Dk. Shakilu Jumanne ambao wamemaliza masomo na mafunzo yao na sasa wameajiriwa na Hospitali ya Taif ya Muhimbili kwenye kitengo cha saratani kwa watoto.

 Katika hafla hiyo, taasisi za Karimjee na Tumaini la Maisha waliwapatia madaktari hao vyeti vya shukrani kwa kazi wanayofanya kuokoa maisha ya watoto. Madaktari hao pia walizawadiwa shilingi milioni 6.6 kila mmoja ili waweze kuhudhuria kongamano la kimataifa kuhusu watoto wenye kansa litakalofanyika Dublin nchini Ireland Oktoba mwaka huu 2016. Taasisi ya Karimjee Jivanjee pia ilimtangaza Dokta Moses Karashani kuwa daktari atakayenufaika na programu hii kwa mwaka 2016.

SIKU YA UTEPE MWEUPE WA UZAZI SALAMA YAADHIMISHWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu akizungumza wakati wa siku ya Utepe Mweupe ambapo na uzinduzi wa kampeni ya kuzuia vifo vya mama na mtoto katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Pia mama Samia amewasihi wanawake kujiunga na mfuko wa jamii wa bima ya afya ili kusaidia vituo vya afya. Pia amewataka wananchi kuachana na mila potofu hasa za ukeketaji kwani ni kumkosoa mwenyezi Mwenyezi Mungu. 
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Bakari Kambi akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya Upete Mweupo kwa niaba ya Waziri wa Afya maendeleo ya jamii, Jinsia, wazeee na watoto, Ummy Mwalimu leo katika uzinduzi wa kampeni ya kuzuia vifo vya mama na mtoto katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi wa UNICEF akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya Utepe mweupe  ambapo mama Samia amezindua wa kampeni ya kuzuia vifo vya mama na mtoto amesema atashirikiana vyema katika kuzuia vifo vya watoto wakati wa kuzaliwa.
 Mwakilishi wa mganga mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Benedict Msiba  akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuzuia vifo vya  mama na mtoto wakati wa kujifungua, ikiwa amesema kuwa katika mkoa wa Rukwa umejitahidi kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

 shuhuda, Efrazia Saidia ambaye amenusurika kifo cha chake na mwanae kutokana na kuumwa uchungu kwa muda mrefu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu akionyesha vitabu ambavyo vimezinduliwa leo ambayo ni mpango wa serikali kuendelea  kuchangia  kupunguza vifo vya mama na mtoto.
 

Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika siku ya Utepe mweupe jijini Dar es Salaam leo na uzinduzi wa mpango mkakati wa kuzuia vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi  wa siku ya Utepe Mweupe leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA JAJI WARIOBA.

$
0
0
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimsikiliza kwa makini Jaji Joseph Warioba alipomtembelea ofisini kwake leo (16/3/2016) kujadiliana kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya sheria ikiwemo uanzishwaji wa Mahakama maalum ya rushwa na ufisadi.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe (wa pili kulia)akiongea katika kikao na Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya sheria kilichofanyika leo (16/3/2016) jijini Dar Es Salaam. Wengine pichani ni Jaji Joseph Sinde Warioba (wa pili kushoto)aliyewahi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju.

RIPOTI NDANI YA MASAA 24 ZIPATIKANE OFISINI KWANGU –MKUU WA MKOA , MAKONDA.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akizungumza na watendaji wa halmshauri za jiji la Dar es Salaam,katikati Mkuu w Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, kulia Mkuu  Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Raymond Mushi akitoa neno la Shukrani kwa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda wakati wa Mkutano wa Kwanza na Mkuu wa Mkoa huyo kukutana na Watendaji, leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewagiza wakuu wa idara wa Halmashauri za jiji la Dar es Salaam kutoa ripoti za matatizo ya wananchi na jinsi walivyojipanga ndani ya masaa 24.

Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri hizo ikiwa ni siku ya kwanza kuingia katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa baada ya kuapishwa jana, Makonda amesema wananchi wa Dar es Salaam wanakabiliwa na changamoto za ulinzi,maji,biashara pamoja na elimu  hivyo lazima matatizo hayo yapate ufumbuzi katika kusaidia wananchi kuondokana na changamoto hizo.

Makonda amesema kuwa kwa muda alioutoa wa masaa 24 ni mkubwa hivyo lazima wafanye kazi hiyo jinsi walivyojipanga katika kutatua changamoto hizo.

Amesema wakati umefika katika kuwatumikia wananchi kuwaondolea  kero zao ambazo zinafanya kuwa na malalamiko yasioisha.

Makonda amesema amekutana na Kamanda wa Polis wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro kuzungumzanaye juu ya suala la ulinzi na usalama  kwa wananchi.

Aidha amesema kuwa kukutana huko sio mara ya kwanza ataendelea ikiwa ni lengo la kuwatumikia wananchi pamoja na kutatua kero zao.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images