Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 792 | 793 | (Page 794) | 795 | 796 | .... | 1896 | newer

  0 0

   Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Wakili Bahame Nyanduga akimuelezea Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe juu ya utendaji kazi waTume hiyo na changamoto mbalimbali wanazozikabili . Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri leo  jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na watendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, yaliyofanyika ofisini kwake leo jijini Dar Es Salaam.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mapango wa ukusanyaji kodi nchini kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji.

  SERIKALI ya Kifalme ya Norway imetoa kiasi cha Dola za kimarekani shilingi Milioni 5 kwa Serikali ya Tanzania kwa kuwaunga mkono Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Serikali ya awamu ya tano katika jitihada zake katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini.

  Makubaliano hayo ya ufunguzi wa kuchangia mapato yamefanyika leo jijini Dar es salaam kati ya Naibu Waziri wa mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji.

  Akizungumza katika ufunguzi huo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen amesema kuwa lengo la mpango huo ni kuimarisha na kuongeza kodi ya mapato ya ndani kwa  kuhakikisha kwamba mianya ya wakwepaji kodi inazuiwa.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amesema kuwa Serikali imeendelea kuimarisha na kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa ulipaji kodi bila kushurutishwa ili kuondokana bajeti  tegemezi kutoka nje.

  “Lengo la kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa  ulipaji kodi bila kushurutishwa na kuzuia mianya yote ya ukwepaji kulipa kodi  ni kuondokana na utegemezi wa bajeti na kuanza kujitegemea hivyo hatuwezi kufika huko bila kuimarisha ukusanyaji wa  mapato nchini” alisisitiza Naibu Waziri huyo.

  Naye Kaimu Kamishna Mkuu TRA Bw. Alphayo Kidata ameishukuru Serikali ya Kifalme ya Norway kwa kuimarisha uwezo wa wataalamu nchini kwa kuwawezesha mbinu mbalimbali za kukagua mahesabu katika makampuni makubwa nchini.
   
  Awali Serikali ya Kifalme ya Norway ilitoa zaidi ya Dola za kimarekani million 3 katika mpango huo wa kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Naibu Gavana wa BOT Dkt. Natu Mwamba akiwasili makao makuu ya Benki Kuu ya Tanzania alikofanya ziara ya kushtukiza leo Machi 10, 2016 .

  0 0

   Balozi Mdogo wa Uingereza, Matt Sutherland  akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na Uingereza na Tanzania kufanya kazi kwa pamoja katika mafunzo haya. Historia yenye kufanana katika sheria na taasisi zetu za kisheria inatoa fursa pana kwa nchi hizi kuweza kufanya kazi na kujifunza baina ya kila mmoja. Mafunzo haya yatawezesha kutoa ujuzi wenye thamani kwa wale watendaji wa mstari wa mbele katika kupambana na makosa makubwa nchini Tanzania.leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Shaban Lila.
   Jaji Kiongozi kutoka mahakama kuu ya Tanzania Shaban Lila akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mahakimu watatumia  ujuzi  na elimu walioipata katika kutatua changamoto ya ucheleweshwaji wa kesi na mashauri mbalimbali, leo jijini Dar es Salaam.
   Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Shaban Lila akimpa cheti chamafunzo ya namna ya kushughulikia makosa makubwa Joachim Tiganga katika hoteli ya White Sands, Mbezi Beach, Dar es Salaam.
  Balozi Mdogo wa Uingereza, Matt Sutherland na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Shaban Lila wakiwakatika picha ya pamoja na Mahakimu wafawidhi 14 toka mahakama mbalimbali Tanzania ikiwemo; Kisutu, Kigoma, Arusha, Moshi, Mwanza, Sumbawanga, Temeke, Dodoma, Kinondoni na Mbeya wamehudhuria mafunzo hayo.leo jiji Dar es Salaam.
  (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

  Na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
  MAHAKIMU nchini wametakiwa kuhakikisha wanatumia vyema mafunzo wanayoyapata katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufasaha hasa katika kuamua kesi kubwa kama za ugaidi, madawa ya  kulevya ,ufisadi na utakatishaji wa fedha haramu  ili kuiendeleza nchi.

  Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Jaji Kiongozi Mahakama kuu ya Tanzania, Shaban Lila  wakati akifunga mafunzo maalumu kwa ajili ya kuongeza ujuzi wa kijaji wa kuhukumu makosa makubwa ya kialifu.

  Mafunzo yalioandaliwa na serikali ya uingereza  kwa kushirikiana na mahakama  kuu ya uingereza ambapo amesema  mafunzo hayo yatakuwa na msaada zaidi endapo wahusika ambao ni mahakimu watatumia  ujuzi  na elimu walioipata katika kutatua changamoto ya ucheleweshwaji wa kesi na mashauri mbalimbali.

  Mafunzo haya ni ya pili kutolewa kwa Mahakama ikiwa ni kufatiwa kwa mafunzo yaliyokwisha kutolewa mnamo Novemba, 2015 kwa Majaji wa Mahakama Kuu.

  Ukanda wa Bahari ya India unakabiliwa na ongezeko kubwa la wasafirishaji wa madawa ya kulevya ambao husafirisha viwango vikubwa vya madawa haramu ya kulevya kuyaleta Afrika Mashariki toka nchi za Afghanistan na Pakistani. 

  Tangu mwaka 2012 Majeshi ya Kimataisha ya Wanamaji katika ukanda huu yamemudu kudhibiti zaidi ya vyombo vya baharini 44 na kukamata zaidi ya tani 8 za madawa aina ya heroini na tani 30 za madawa aina ya “hashish”.

  Ushirikiano katika kazi baina ya Uingereza na Tanzania umefanikisha kukamatwa na kuchukuliwa hatua kwa wasafirishaji wakubwa wa kimataifa wa madawa ya kulevya kote Tanzania na Uingereza Matt Sutherland alieleza na kufafanua kwanini Uingereza inafadhili kazi hizi Tanzania na Uingereza ina mtizamo unaoshabihiana katika kukabiliana na makosa makubwa. 

  Tunaona kuongezeka kwa wahalifu wa kimataifa wakitumia mitandao ya kimataifa kusafirisha madawa ya kulevya, mazao haramu ya wanyamapori au kuficha wahalifu. Ni kwa kufanya kazi kwa ushirikiano tu ndipo kunaweza tukahakikisha wahalifu hawana mahala pakujificha.

  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) akizungumza na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Vietnam Bw.  Nguyen Bac Son (kushoto) kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Vietnam na (kulia) ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwini Ngonyani.

  Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Vietnam Bw.  Nguyen Bac Son (kulia) akimuaga mwenyeji wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa wa pili (kushoto) baada ya kufanya mazungumzo ya ushirikiano katika sekta ya Mawasiliano, (kushoto) ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwini Ngonyani.


   

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
  VIETNAM KUPANUA WIGO WA UWEKEZAJI KWENYE SEKTA YA MAWASILIANO TANZANIA.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Mb) amekutana na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa nchi ya Vietnam Bwana Nguyen Bac Son ofisini kwake kwa lengo la kupanua wigo wa uwekezaji kwenye Sekta ya Mawasiliano nchini Tanzania na kushirikiana kwa pamoja kuendeleza Sekta hizo baina ya Tanzania na Vietnman. Kikao hicho ni muendelezo wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang na ujumbe wake nchini Tanzania.


  Prof. Mbarawa alisema kuwa Tanzania imekuwa na ushirikiano na Vietnam kupitia Kampuni ya Viettel kwa kuwekeza kwenye miundombinu ya kufikisha huduma za mawasiliano vijiini kwa kutiliana saini Mkataba. 

  Mkataba huo ni wa miaka mitatu kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2014 hadi Novemba, 2017 ikijumuisha ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wenye urefu wa kilomita 20,000 kwenye wilaya zote nchini; kujenga miundombinu ya mawasiliano kwenye vijiji  4,000; kuunganisha Ofisi za Wakuu wa Wilaya; hospitali za Wilaya; Ofisi zote za Posta  za Wilaya; na kupeleka na kutoa huduma za intaneti bila malipo kwenye shule 3 za Sekondari za Serikali katika kila Wilaya nchini kwa kipindi cha miaka mitatu.


  Aidha, Prof. Mbarawa aliongeza kuwa tangu Kampuni ya Viettel yenye jina la biashara la Halotel ilipoanza kufanya kazi rasmi mwezi Oktoba mwaka 2015, imeweza kupeleka huduma ya mawasiliano maeneo ya vijijini na hadi hivi sasa ina watumiaji wa simu za mkononi wapatao milioni 1.2 na wananchi walio wengi wanafurahia huduma hiyo tofauti na hali ilivyo kuwa hapo awali kipindi cha miezi sita iliyopita na ikizingatiwa kuwa sehemu nyingine za vijijini hapakuwa na mawasiliano. Pia alisema kuwa, “Serikali ya Tanzania itaendelea kujenga na kuwekeza kwenye Sekta ya Mawasiliano ili kuwavutia wawekezaji na kampuni za simu za mkononi ambapo Serikali ya Tanzania ilitoa ruzuku kiasi cha dola za marekani milioni 30 ili kuziwezesha kampuni hizo kupeleka mawasiliano vijijini na maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara”. Hadi kufikia mwezi Machi, 2016 Halotel imejenga Mkongo wenye urefu wa kilomita 18,000 kati ya kilimota 20,000; na kujenga miundombinu ya mawasiliano kwenye vijijini 1,605 kati ya vijiji 4,000 visivyokuwa na mawasiliano.


  Katika mazungumzo hayo ya kuendeleza sekta ya Mawasiliano Tanzania, Prof. Mbarawa aliwaalika wawekezaji kutoka Vietnam wa Sekta ya Mawasiliano na kampuni ya Halotel kujiandaa na kuja Tanzania kushiriki mnada wa kununua masafa ya 700MHz ambayo yamepatikana baada ya kuhama kutoka Teknolojia ya Utangazaji ya Analojia na kuhamia Teknolojia ya Utangazaji ya Dijitali.  Pia alisema kuwa Kampuni za Vietnam zinakaribishwa kuanzisha na kuendeleza huduma za mawasiliano za mfumo wa kumpatia mteja huduma tatu kwa pamoja ya sauti; intaneti; na kuangalia televisheni ikijulikana kwa jina la triple player ili Tanzania iweze kwenda sambamba na kasi ya ukuaji wan a maendeleo ya TEHAMA yanayotokea dunia nzima.


  Katika kikao hicho, Prof. Mbarawa alimweleza Mhe. Ngoyen Bac Son kuwa Tanzania iko tayari kusaini Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano na Serikali ya Vietnam wa kubadilishana wataalamu kwenye Sekta ya Mawasiliano na kuwapatia mafunzo ili kujenga uwezo wa wataalamu wetu wa Tanzania; na kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo vidogo vya TEHAMA (ICT Small Scale Factories) nchini Tanzania ambapo viwanda hivyo vitazalisha ajira; kurahisisha upatikanaji wa vifaa na huduma za TEHAMA kuendana na mahitaji na mazingira yetu; kuongeza mapato; na kuwahudumia wateja wa nchi za jirani na Tanzania.


  Mhe. Ngoyen Bac Son alisema kuwa Serikali ya Vietnam iko tayari kuendeleza ushirikiano baina ya Serikali yao na ya Tanzania ya kuendeleza Sekta ya Mawasiliano;  na sekta ya kukuza Uchumi na Maendeleo ya Tanzania kama alivyozungumza Rais wa Vietnam. Pia aliongeza kuwa, “Serikali ya Vietnam iko tayari kuleta kampuni za kuwekeza Tanzania kwa kuanzisha Kiwanda cha vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya kuwapatia watanzania huduma za mawasliano na ni matarajio yetu kuhakikisha kuwa ni kiwanda kikubwa ambacho kitahudumia na wateja wa nchi za jirani na Tanzania”. Aidha, Mhe. Ngoyen Bac Son aliongeza kuwa Serikali ya Vietnam inaridhia kusaini Mktaba wa Ushirikiano baina ya nchi hizo na amewakaribisha wafanyabiashara na kampuni za Tanzania kwenda kuwekeza nchini Vietnam.


  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  KATIBU Mkuu Kiongozi, Mhadisi  Balozi  John Kijazi(Pichani) amesema makatibu wakuu na manaibu wafanye kazi kwa mujibu sheria na waishi kama viongozi wa umma katika maisha.

  Katibu Mkuu Kijazi ameyasema hayo leo wakati wa mafunzo maadili ya viongozi wa Umma kwa Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam,amesema kuwa kama sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma ina matatizo ya utekelezaji wa kisheria kwa viongozi wa umma serikali iko tayari kuyarekebisha.

  Amesema mafunzo kwa viongozi wa umma ni muhimu katika kupunguza masuala ya rushwa pamoja na ubadhirifu wa mali za umma.
  Aidha amesema kuwa makatibu wakuu na manaibu wafanye kazi kwa kutenda haki kwa waliochini yao  kutokana na maadili ya utumishi  wa umma.

  Nae Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada zinazofanyika hivi sasa za kukuza na kuinua kiwango cha uwajibikaji na maadili katika utumishi wa Umma kutokana na maadili ya taifa ni moja ya tunu taifa muhimu inayotambulisha Taifa.

  Angellah amesema mafunzo waliopata yawe ni chachu ya kasi ya kujenga na kukuza maadili katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

  Amesema watendaji wakuu wanatakiwa kuwa mfano bora  na wa kuigwa kwani serikali imechukua hatua mbalimbali ili  kuongeza  mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na ukosefu wa maadili hususani miongoni mwa viongozi wa umma. 

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye akizungumza katika uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa kumi na sita (16) wa Taasisi hiyo na uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na mwenyekiti mtendaji wa IPP LTD Dkt. Reginald Mengi akizungumza katika uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa kumi na sita (16) wa Taasisi hiyo na uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), wakifuatilia uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa Taasisi hiyo na uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza katika uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa Taasisi hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza mara baada ya kuzindua mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara ulioendana na mkutano mkuu wa Taasisi hiyo na uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Furaha mara baada ya uzinduzi huo. Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), wakiwa katika nyuso za furaha mara baada ya kupewa vyeti vya shukrani. 

  0 0

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang leo mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kushoto) akiongea na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muunhgano wa Tanzania (hayupo pichani) mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiongea na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (hayupo pichani) leo mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni Naibu Spika wa Bunge hilo, Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
  Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kushoto) akiongea na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (hayupo pichani) mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kushoto) na ujumbe wake akiongea na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kulia ) na ujumbe wake mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya ujumbe alifuatana nao Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakifuatilia mazungumzo yao leo mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam. .
  Baadhi ya ujumbe alifuatana nao Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai wakifuatilia mazungumzo yao leo mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni Naibu Spika wa Bunge hilo, Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiongea na baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge hilo, Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akiongea na baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya mkutano uliofanyika kati ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar esSalaam.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (katikati) na Naibu Spika wa Bunge Mhe Dkt Tulia Ackson wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo yaliyohusishwa na baadhi ya ujumbe toka nchi ya Vietnam na Tanzania leo mara walipokutana kwa ajili ya mazungumzo katika Hoteli ya Kilimanjaro 10 Machi, Jijini Dar es Salaam.
  (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)

  0 0


  Na Anitha Jonas – MAELEZO

  Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewahakikishia wawekezaji kutoka Vietnam kuwepo kwa fursa za uwekezaji nchini.

  Majaliwa ameyasema hayo jana katika kongamano la ujumbe wa Rais wa Vietnam Mheshimiwa Troung Tan Sang pamoja na wadau wa uwekezaji kutoka nchini humo ambapo wanatarajia kufanya ziara ya siku nne nchini wakitazamia fursa za uwekezaji nchini.

  “Nchi yetu inamazingira mazuri ya uwekezaji, usalama wakutosha na pia kuna uhahika wa soko kwani ipo mikataba ya kikanda ya kukuza masoko katika nchi wanachama kama EAC na SADC kwani katika nchi hizo kuna watu zaidi ya milioni 300”, alisema Majaliwa.

  Akiendelea kuzungumza na wawekezaji hao Waziri Mkuu alisema serikali ya Tanzania imekuwa ikiboresha Mazingira ya uwekezaji nchini na hiyo imechangia ongezeko la wawekezaji.

  Mbali na hayo Majaliwa alisema serikali imekuwa ikiboresha sheria na kuimarisha ushirikishwaji wa wadau wa sekta binafsi lengo likiwa ni kuchochea mazingiraya uwekezaji ikiwa ni kuimarisha uchumi wa taifa pamoja na kukuza kipato cha kila mtanzania.

  Hata hivyo Waziri Mkuu aliipongeza Kampuni ya VIETTEL Tanzania Ltd kutoka Vietnam ambayo imewekeza katika Sekta ya Mawasiliano kwani imewasaidia watanzania wengi wa vijijini kupata mawasiliano.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kushitukiza katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ambapo pamoja na mambo mengine ameiagiza Benki hiyo kusitisha mara moja ulipaji wa malimbikizo ya malipo ambayo tayari yalishaidhinishwa (Ex-Chequer) na badala yake yarejeshwe Wizara ya fedha na Mipango kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki.

  Mpaka Rais Magufuli anatoa agizo hilo, Benki Kuu ya Tanzania ilikuwa katika mchakato wa kufanya malipo ya shilingi Bilioni 925.6, ambazo Wizara ya Fedha ilitoa idhini ya kufanyika malipo.

  Akizungumza na watendaji wakuu wa Benki Kuu ya Tanzania waliojumuisha Gavana, Naibu Magavana, Wakurugenzi na Mameneja, Rais Magufuli ametaka Wizara ya Fedha ifanye upya uhakiki wa malipo hayo, ili kubaini kama walengwa walioidhinishwa kulipwa wanastahili kulipwa ama vinginevyo.

  Aidha, Dkt. Magufuli ameagiza Kitengo cha madeni ya nje ambacho awali kilikuwa chini ya Benki Kuu na baadaye kikahamishiwa Wizara ya Fedha, kirejeshwe Benki Kuu mara moja ili kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa madeni.

  Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Beno Ndulu kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa Benki hiyo, na kuwaondoa mara moja wale wote ambao hawana ulazima wa kuwa wafanyakazi katika benki hiyo.

  "Haiwezekani tukawa na kundi kubwa la wafanyakazi, wanalipwa mishahara wakati hata kazi wanazofanya hazijulikani" Amesema Dkt. Magufuli.

  Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati ambapo Benki Kuu ya Tanzania ina wafanyakazi 1391.


  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  10 Machi, 2016.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mapango wa ukusanyaji kodi nchini kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji.
  ………………
  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  Serikali ya Kifalme ya Norway imetoa kiasi cha Dolla za kimarekani shilingi Milion 5 kwa Serikali ya Tanzania kwa kuwaunga mko no Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Serikali ya awamu ya tano katika jitihada zake katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini.

  Makubaliano hayo ya ufunguzi wa kuchangia mapato yamefanyika leo jijini Dar es salaam kati ya Naibu Waziri wa mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji.

  Akizungumza katika ufunguzi huo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen amesema kuwa lengo la mpango huo ni kuimarisha na kuongeza kodi ya mapato ya ndani kwa kuhakikisha kwamba mianya ya wakwepaji kodi inazuiwa.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amesema kuwa Serikali imeendelea kuimarisha na kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa ulipaji kodi bila kushurutishwa ili kuondokana bajeti tegemezi kutoka nje.

  “Lengo la kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa ulipaji kodi bila kushurutishwa na kuzuia mianya yote ya ukwepaji kulipa kodi ni kuondokana na utegemezi wa bajeti na kuanza kujitegemea hivyo hatuwezi kufika huko bila kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini” alisisitiza Naibu Waziri huyo.

  Naye Kaimu Kamishna Mkuu TRA Bw. Alphayo Kidata ameishukuru Serikali ya Kifalme ya Norway kwa kuimarisha uwezo wa wataalamu nchini kwa kuwawezesha mbinu mbalimbali za kukagua mahesabu katika makampuni makubwa nchini.

  Awali Serikali ya Kifalme ya Norway ilitoa zaidi ya Dola za kimarekani million 3 katika mpango huo wa kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini.

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza – CGP John Casmir Minja akisalimiana na Mkuu wa Gereza Kuu Butimba, Mwanza Kamishna Msaidizi wa Magereza, Jaili Mwamugunda alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera ambapo leo Machi 10, 2016 ametembelea eneo kunakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato lililopo Mkoani Geita pamoja na Gereza la Wilaya ya Biharamulo(wengine) ni Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Ofisi ya Magereza Mkoani Mwanza.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akifurahia jambo pamoja na Luteni Jenerali Mstaafu Samuel Ndomba walipokutana katika Kivuko cha Busisi kabla ya kuendelea na safari kuekelea Mkoani Kagera(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Mwanza, Goleha Masunzu.
  Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Shaban Ntarambe(kushoto) akiwa na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya wakielekea eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato mara baada ya Kamishna Jenerali wa Magereza kuwasili Wilayani Chato kabla ya kuelekea Mkoani Kagera
  Mkuu wa Magereza Mkoani Kagera, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Omar Mtiga(wa pili kushoto) akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa tatu kulia) nyumba mbili za Askari wa Jeshi la Magereza ambazo tayari zimekamilika katika eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Biharamulo(wa pili kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Shaaban Ntarambe.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(suti nyeusi) akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Chato wakiaangalia moja ya Bweni la kulala Wafungwa/Mahabusu ambalo tayari limekamilika katika eneo linakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato Mkoani Geita. Kukamilika kwa Gereza hilo kutasaidia kutatua tatizo la Msongamano wa Wafungwa na Mahabusu katika Magereza ya Biharamulo na Gereza Muleba.
  Kamishna Jenerali wa Magereza John Casmir Minja akisaini katika kitabu cha Wageni alipotembelea Gereza la Wilaya ya Biharamulo katika ziara yake ya kikazi leo Machi 10, 2016.
  Mkuu wa Gereza la Biharamulo, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Gidion Kakulu akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza maeneo mbalimbali ya Gereza hilo katika ziara yake ya Kikazi leo Machi 10, 2016. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo ambao wameambatana na Kamishna Jenerali wa Magereza katika ziara yake ya kikazi.

  0 0  Wasichana wa Shule ya Sekondari Luchelele wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji toka DidaVitengeWear Foundation mara baada ya kupokea taulo za usafi (Pedi) na Elimu ya Usafi wa mwili na uzazi chini ya mradi wa Binti Box unaotekelezwa katika shule za Sekondari na Msingi kanda ya Ziwa.
  Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa DidaVitengeWear Foundation ambae pia ni Mratibu wa Mradi wa Binti Box akijadiliana jambo na Mbunge wa Viti Maalum Vijana mkoa wa Mwanza kupitia CCM, Mh. Maria Kangoye Ndila (Katikati) pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Wanawake mkoa wa Mwanza Mh. Zawadi Kiteto (Kushoto), wakati wa utekelezaji wa mradi wa kugawa taulo za usafi kwa Mabinti wa Shule ya Msingi Igombe.
  Mkufunzi wa Afya ya Uzazi ambae pia ni muuguzi msaidizi kutoka kituo cha Afya cha Makongoro akitoa elimu ya usafi wa mwili na kuepuka mimba za utoto kwa wanafunzi wa kike wa shule ya msingi Igombe chini ya mradi wa Binti Box ulioandaliwa na DidaVitengeWear Foundation kwa kushirikiana na wadau mbalimbali jijini Mwanza
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Igombe wakiwa katika picha ya pamoja huku wakiwa na nyuso za furaha baada ya kupewa vifaa vya usafi vitakavyowasaidia katika mzunguko wao wa kila mwezi na kuepuka magonjwa mbalimbali yanayotokana na kutumia vifaa visivyo salama.
  Kushoto ni Bi. Khadija Liganga Mkurugenzi wa taasisi ya kusaidia wanawake na maendeleo ya wasichana yenye makao makuu jijini Mwanza, DidaVitengeWear Foundation akihimiza jambo juu matumizi mazuri ya vifaa vya usafi kwa wasichana wa shule ya sekondari ya Bujora (hawapo pichani), Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Vijana mkoa wa Mwanza, Bi. Maria Kangoye Ndila ambae aliungana katika mradi huo kuwasaidia mabinti walio shuleni.
  Mabinti wa shule ya sekondari ya Bujora iliyopo Wilayani Magu mkoani Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa taulo za usafi toka taasisi ya DidaVitengeWear Foundation.

  Katika kusheherekea siku ya Wanawake Duniani Machi 08,2016, taasisi ya kusaidia wanawake na wasichana yenye makao makuu jijini Mwanza, DidaVitengeWear Foundation, Imefanikisha kugawa taulo za usafi zaidi ya 2,000 kwa wasichana zaidi ya 600 wa shule ya msingi Igombe na Shule ya Sekondari ya Luchelele zote za Jijini Mwanza kupitia mradi wa kuwasaidia Mabinti kufikia malengo yao, ujulikanao kama ‘Binti Box’. 

  Hatua hiyo pia imefikiwa kwa ushirikiano wa karibu baina ya taasisi hiyo pamoja na Mtandao wa Wanawake jijini Mwanza wa ‘Women Roundtable’, na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM) Mh.Stanslaus Mabula, Mbunge Viti Maalum Wanawake Mkoani Mwanza Zawadi Kiteto na Mbunge wa Viti Maalum Vijana Mkoani Mwanza Mh.Maria Kangoye Ndila 

  Binti Box ni mradi ulioanzishwa kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike waliopevuka kubaki shule na kuimarisha mahudhuria ya wasichana shuleni kwa kuwapatia vifaa vya usafi vitakavyowasaidia wakati wa siku zao za hedhi. Wasichana wengi hasa wa vijijini hukosa kwenda shule kwa siku 5 mpaka 7 kwa mwezi kwa sababu ya kukosa vifaa vya usafi wakati wa mzunguko wa hedhi, hivyo mradi huu kwa upande wa kanda ya ziwa ni mkombozi kwa mabinti wengi kuhudhuria shule na kuinua kiwango cha ufaulu katika masomo yao.

  Akiongea wakati wa kugawa taulo hizo za usafi mashuleni, Bi. Khadija Liganga, Mratibu wa Mradi na Mkurugenzi wa DidaVitengeWear Foundation, alieleza kwamba, elimu ya wasichana ni jambo la msingi katika jitihada za kuleta maendeleo kwa nchi masikini kwa sababu mafaniko ya wanawake hasa katika elimu inamaanika kuwa na faida ya muda mrefu na huenda mbali Zaidi katika kuinua uchumi wa jamii na nchi.

  “Kuna sababu nyingi zinazochangia kudumaa kwa ustawi wa elimu ya mtoto wa kike hasa wale wa vijijini, tatizo la ukosefu wa vifaa vya usafi kwa mabinti wakati wa hedhi kwa kila mwezi nayo imeibuka kuwa ni tatizo sugu linalofumbiwa macho na wadau wengi wa maendeleo katika nchi zinazoendelea na Tanzania ikiwemo. Wasichana hawa hujawa na uwoga na kuhofia kupoteza thamani yao na utu wao wawapo shuleni au mbele za watu na kuwafanya wasihudhurie darasani au kutokwenda shule na matokeo yake wengi huacha shule,” amesema Bi. Khadija Liganga 

  Bi.Khadija aliendelea kusema kwamba “Baada ya kutembelea baadhi ya shule zilizo pembezoni na miji tumegundua tatizo ni kubwa, tukapata uwelewa wa kutosha na tukaona ni vyema badala ya kuandaa makongamano ya wanawake wakati wa sherehe za Siku ya Wanawake Dunaini 2016, kwanini tusiguse eneo ambalo ndio chimbuko la ukandamizaji wa maendeleo ya Mwanamke, ambalo ni Elimu. Ndipo tukaja na huu mradi utakaokuwa endelevu wa ‘Binti Box’ kwa lengo la kutoa taulo za usafi kwa mabinti wa shule za msingi na sekondari pamoja na elimu ya usafi wakati wa siku za hedhi”

  “Tungependa kuwashukuru watu wote pamoja na taasisi mbalimbali kwa mchango wa o wa maboksi ya taulo za usafi. Huu ni mwanzo tu, huku mipango ikiwa ni kuongeza uwezo wa mradi kuweza kutoa huduma hii kwa shule za sekondari na msingi katika mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, tuko tayari kushirikiana na watu binafsi au taasisi yoyote katika kumkomboa mtoto wa kike” alisema Bi. Khadija Liganga

  Lengo la Mradi wa Binti Box ni kuwapatia elimu ya uzazi,afya,kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuwapatia taulo za usafi wasichana wa sekondari na shule za msingi waliopo katika umri wa kuvunja ungo katika mikoa ya Mwanza na Mara. Mradi unatekeleza mpango wa taifa kwa vitendo wa kuhakikisha watoto wa kike hawabaki nyuma bali wanapata fursa sawa na wenzao wa kiume na kuongeza ufaulu kwa watoto wa kike.

  0 0

  Rais Truong Tang San akizindua Sanamu ya kiongozi wa zamani wa Vietnam iliyopo kwenye Kampuni ya Simu ya Halotel. 
  Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tang San akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Simu za mikononi kutoka nchini Vietnam ya Halotel inayofanya kazi hapa nchini Tanzania. Kampuni hiyo inatoa huduma ya simu Vijijini kwa gharama nafuu. Rais Truong Tang San anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku nne hapo kesho na kuelekea nchini Msumbiji kwa ajili ya ziara nchini humo. 
  Viongozi mbalimbali walioambatana na Rais Truong Tang San, wakiwa pamoja na Balozi wa Vietnam, Mhe. Vothanh Nam (katikati) wakisikiliza kwa makini mazungumzo aliyokuwa yakiendelea kati ya Rais Tang San (hayupo pichani) na viongozi wa Kampuni ya simu ya Halotel 
  Viongozi wa Halotel na Viongozi walioambatana na Rais Tang San (hayupo pichani) wakishangilia wakati uzinduzi ukiendelea 
  Rais Truong Tang San akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya simu ya Halotel. 


  Picha na Reginald Philip 

  0 0

  Rais Dkt Magufuli akizungumza na Uongozi wa juuu wa Benki Kuu

  0 0  Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk Richard Masika(kushoto)akimwongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen kuwasilimia wafanyakazi wa taasisi hiyo katika ziara yake ,Norway ni moja ya nchi zinazosaidia sekta ya elimu ya ufundi nchini.

  Ujumbe uliongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen kutoka Norway na maafisa kutoka ubalozi wao nchini wakisalimiana na wafanyakazi wa Chuo cha Ufundi Arusha.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen (kulia)akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhil Nkurlu(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Richard Masika.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen na ujumbe wake wakipata maelezo ya mfano wa kuzalisha umeme unaotokana na chanzo kidogo cha maji.
  Mmoja wa wanafunzi anayesoma katika Chuo hicho akimpa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen maelezo kuhusiana na kozi yake.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway,Tone Skogen akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo.Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com  0 0


  Serikali ya Marekani imeamua kutaifisha mali za mfanyabiashara wa dawa zilizopigwa marufuku za kulevya kutoka Tanzania, Ali Khatib Haji Hassan, maarufu kwa jina la “Shikuba” na mtandao wake na kupiga marufuku kampuni za nchi hiyo kujihusisha na biashara zake.
  Shikuba, ambaye amekuwa akihusishwa na biashara kubwa ya usafirishaji dawa za kulevya kati ya Afrika Mashariki, Asia, Ulaya na Marekani, alikamatwa mwaka 2014 nchini Tanzania akihusishwa na shehena ya kilo 210 za heroin zilizokamatwa mkoani Lindi mwaka 2012.
  Taarifa iliyotolewa juzi na kitengo cha udhibiti wa mali za nje cha Wizara ya Fedha ya Marekani imeeleza kuwa serikali imemtambua Shikuba kama kinara wa usafirishaji wa dawa za kulevya kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi wa Vinara wa Dawa za Kulevya wa Nje (Foreign Narcotics Kingpin Designation Act) ya Marekani

  0 0
 • 03/10/16--23:57: TAARIFA YA KUMBUKUMBU


 • 0 0


  Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akizungumza jana katika Mkutano wa nane wa wadau wa LAPF unaoendelea jijini Arusha katika ukumbi wa AICC ambapo alikuwa mgeni rasmi mbali na mambo mengine,aliitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa mafao kwa wakati pindi wanachama wake wanapostaafu ili kuhakikisha kuwa wastaafu wanapata mafao yao, kwani wengi wao wanakabiliwa na msongo wa mawazo kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili baada ya kustaafu wanashindwa kujimudu kutokana na kukosa mafao yao(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha)

  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera ,Bunge ,Ajira na Walemavu Jenister Mhagama ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kuwekeza kwenye viwanda ili kuunga mkono msimamo wa serikali kuanzisha uchumi wa viwanda utakaotengeneza ajira na kuchochea maendeleo ya nchi

  Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa LAPF Eliudi Sanga akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kuwa Mifuko ya hifadhi ya jamii imekua chachu ya maendeleo ya taifa kutokana na uwekezaji unaofanywa na mifuko hiyo pamoja na mikopo mbalimbali inayotolewa kwa wanachama kujikwamua kimaisha

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha

  Afisa Masoko wa LPF James Mlowe akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kuwa tayari mfuko huo umeanzisha mkopo wa maisha popote na LAPF ambao unalenga kuwasaidia watumishi wa umma hususan wale walioajiriwa maeneo ya vijijini ili waweze kuanza maisha na kuwatumikia watanzania bila vikwazo vya kiuchumi.

  Makamu mwenyekiti wa bodi Husein Kamote alisema mfuko huo unakabiliwa na changamoto nyingi zinazokwamisha utekelezaji wa mipango yake ikiwemo deni inalolidai serikali ambalo halijalipwa kwa mda mrefu huku likizidi kuongezeka

  Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akiteta jambo na Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa LAPF Eliudi Sanga

  Wadau katika mkutano

  Mdau kutoka benki ya NMB akizungumza katika mkutano huo

  Mwandishi wa habari wa star tv Ramadhan Mvungi akifatilia mkutano kwa ukaribu

  Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akipokea zawadi ya saa aliyokabidhiwa na mfuko huo

  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera ,Bunge ,Ajira na Walemavu Jenister Mhagama akipokea zawadi ya saa aliyokabidhiwa na mfuko huo

  Waziri wa TAMISEMI George Simbachaweneakimkabidhi kaimu mkurugenzi Geita John Muta hundi ya shilingi milioni saba tu baada ya halmashauri hiyo kufanya vizuri na mfuko huo

  Wadau wakifatilia mkutano

  Wadau kutoka mifuko mingine pia walishiriki mkutano huo

  Mnufaika wa LAPF kupitia maisha popote Scolastika Francis kutoka Kilolo ambaye ni mwalimu akitoa ushuhuda jinsi mkopo huo ulivyoweza kubadili maisha yake ambapo sasa anamiliki nyumba pamoja na shamba mbali na ajira yake

  Mwalimu wa shule ya sekondari Rombo Njuguna Rombo akitoa ushuhuda jin si mfuko huo ulivyoweza kubadili maisha yake ambapo ameweza kununua

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  OFISI  YA RAIS
  TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
          

  TAARIFA KWA UMMA
  Kumekuwa na taarifa za upotoshaji zinasombazwa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kutolewa kwa ajira mpya ya walimu kwa shule za sekondari na msingi kwa mwaka 2015/2016.
  Taarifa hizo zinazosambazwa zinaeleza kwamba walimu wapatao 17,928 wa cheti (Daraja IIIA) , 5,416 wa Stashahada kwa sekondari na 12,677  kwa  shule za mazoezi za vyuo vya ualimu Tanzania Bara wamepangwa kwa ajili ya kuanza kazi.
  Katika taarifa hiyo inawataka walimu hao waliopangwa kuripoti kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kupangiwa vituo vya kazi na kuanza kazi tarehe 01/04/2016.
  Taarifa hizo pia zinaeleza kuwa walimu ambao hawataripoti ifikapo tarehe 10/04/2016 hawatapokelewa tena na watakuwa wamepoteza ajira zao.
  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inapenda kuchukua nafasi hii kukanusha taarifa hizo kuwa ni za upotoshaji. Wananchi wanapaswa kuzipuuzia kwani mpaka sasa bado Serikali haijatoa ajira za walimu kwa mwaka 2015/2016.
  Ajira mpya za ualimu zitakapokuwa tayari zitatangazwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari na katika tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz.
  Imetolewa na :
  Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
  Ofisi ya Rais
  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  11/03/2016

older | 1 | .... | 792 | 793 | (Page 794) | 795 | 796 | .... | 1896 | newer