Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 793 | 794 | (Page 795) | 796 | 797 | .... | 1903 | newer

  0 0
  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akitoa taarifa kuhusiana na dhima ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang nchini Tanzania na manufaa yake kwa pande zote mbili, leo 11 Machi, 2016 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Nguyen Bal Son akieleza makubaliano waliyofikia ya ushirikiano baina ya Tanzania na Vietnam ikiwa ni sehemu ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang nchini Tanzania na manufaa yake kwa pande zote mbili, leo 11 Machi, 2016 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Nguyen Bal Son akieleza makubaliano waliyofikia ya ushirikiano baina ya Tanzania na Vietnam ikiwa ni sehemu ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang nchini Tanzania na manufaa yake kwa pande zote mbili, leo 11 Machi, 2016 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Wizara toka pande mbili za Tanzania na Vietnam pamoja na Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Nguyen Bal Son leo 11 Machi, 2016 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Wizara toka pande mbili za Tanzania na Vietnam pamoja na Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Nguyen Bal Son leo 11 Machi, 2016 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)

  0 0

  Immaculate Makilika - MAELEZO
   
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,  Balozi Augustine Mahiga amesema Tanzania na Vietnam zimeahidi kuendeleza  ushirikiano  katika nyanja mbalimbali kufutia makubaliano yaliyofanyika wakati wa ziara ya Rais wa Vietnam nchini.

  Waziri Mahiga ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa habari wakati wa majumuisho ya ziara ya siku nne ya Rais wa Vietnam nchini Mheshimiwa Truong Tan Sang.

  Akiwa ameongozana  na Waziri Habari na Mawasiliano wa Vietnman Nguyen Bal Son  ameyataja maeneo ambayo Tanzania na Vietnam zimekubaliana kushirikiana  kuwa ni uwekezaji wa  kilimo cha mpunga, uvuvi wa samaki wa ziwani na baharini na uanzishwaji wa viwanda vya kusindika mazao ya biashara.

  “Tumekubaliana kushirikiana katika maeneo kadhaa ikiwemo kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kuongezeka kwa uwekezaji kutoka Vietnam kwani kwa sasa biashara inayofanyika kati ya Vietnam na Tanzania ni dola milioni 300 kwa mwaka, tumekubaliana ifikie dola bilioni 900  ifikapo mwaka 2020”

  Aidha, maeneo mengine ya ushirikiano ni pamoja na kufungua mahusiano ya mawasiliano na elimu, ambapo kutakua na fursa kwa wanafunzi wa Kitanzania kwenda kusoma nchini Vietnam, na wataalamu wa Vietnam kuja kufanya kazi pamoja na watanzania na kusema kuwa kampuni ya simu ya Halotel imefungua mlango kwa Vietnam kuwekeza nchini na kuongeza kuwa lengo la ushirikiano huu ni kuwa na uhusiano ulio sawa na kila mmoja anufaike na mahusiano hayo.

  Hata hivyo, Mahiga amesema kuwa pamoja na maeneo  kadhaa waliyokubaliana jambo la msingi ni namna  ambavyo nchi hizo zitatekeleza makubaliano hayo kwa kuwa na mawasiliano ya karibu  na kukutana  mara kwa mara baina ya watendaji wa Serikali hizo mbili.

  Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang, aliwasili nchini machi 8 mwaka huu, ambapo alikutana na Rais Mhe. John Magufuli na kufanya mazungumzo Ikulu na kutia saini mkataba wa kibiashara baina ya Tanzania na Vietnam.Aidha, Rais Truong na ujumbe katika ziara yake ya siku nne nchini alikutana na Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete, alizungumza na jukwaa la wafanyabiashara na viongozi wao, na  pia  alitembelea eneo la viwanda (EPZA) Ubungo jijini Dar es salaam.

  Vilevile, alifanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein ambapo walikubaliana kuwa na mahusiano ya karibu na visiwa vya Zanzibar kwa ajili ya uwekezaji katika utalii na uvuvi wa samaki.

  Kwa upande wake, Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Vietnam Mhe. Nguyen Bal Son amesema nchi yake ina historia nzuri ya ushirikiano na mahusiano ya kidiplomasia ya muda mrefu yaliyo asisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na hivyo wataendeleza uhusiano huo na Tanzania pamoja na kushirikiana ili kukuza uchumi wa nchi hizo.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona akiwa anakata utepe ikiwa ni ishara ya kufunguliwa rasmi kwa maonyesho hayo ya vito na madini
   Wafanya biashara wakubwa ambao ni  wa pili kulia ni mkurugenzi wa  kampuni ya Jacaranda Holding  DR,Antony Haj Frisby akiwa na mwenzake wanachagua madini ya vito kwa ajili ya kuyanunua ambapo alisema kuwa maonyesho haya ni mazuri sana ila aliomba  wachimbaji wadogo wajitokeze kwawingi kuleta bidhaa zao.
   Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona wa tatu kulia akiwa anaonyeshwa moja ya madini ya vifo yalioletwa katika maonyesho ya wafanyabiashara wa ndani wa madini hayo yaliyofanyika ndani ya mji mdogo wa mirerani mkoani Manyara
   Mmoja kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Saniniu Laizer akiwa anaonyesha jiwe la Tanzanite ambalo lipo tayari kuuzwa.
   Idha benki ya NMB ilimefungua rasmi tawi katika mji huu ndogo wa mererani hapa meneja wa mji mdogo wa benki hiyo akiwa anamueleza mkuu wa wialaya pamoja na wananchi waliouthuria semina hiyo huduma ambazo wanazitoa benki hiyo ndani ya mji mdogo wa mirerani
   habari picha na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog,Mererani
  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewaagiza wote waliovamia na kujikatia viwanja au kujenga kwenye eneo huru la usafirishaji bidhaa nje (EPZA) waondoke na kubomoa kabla hawajaondolewa kwa nguvu. 

  Inadaiwa kuwa vigogo watatu wa mji mdogo wa Mirerani, wamejenga nyumba za kuishi kwenye eneo hilo na watu wengine zaidi ya 11 wamejimegea viwanja kiubabe na kujiandaa kujenga ili hali mradi huo unatarajia kuanza kujengwa.
   

  Akizungumza juzi wakati akifungua maonyesho ya madini ya vito ya siku
  mbili yaliyofanyika mji mdogo wa Mirerani, Kambona alisema mchakato wa
  kuwalipa fidia waliokuwa wanamiliki eneo hilo upo tayari hivyo wavamizi hao waondoke. 


  Alisema baada ya kuwalipa waliokuwa wamiliki wa eneo la EPZA, mchakato wa ujenzi utaanza mara moja kwani kutajengwa kituo kikubwa cha biashara za kuuza nje ikiwemo soko la madini ya Tanzanite litakalojengwa sehemu hiyo. 


  Hata hivyo, alipongeza Wizara ya Nishati na Madini kufanya maonyesho hayo kwa mara ya kwanza kwenye mji mdogo wa Mirerani, sehemu yanapopatikana madini ya Tanzanite, kwani itasaidia kuboresha soko la madini katika eneo hilo.
   

  “Ni heshima kubwa tumepatiwa watu wa Simanjiro hususan mji mdogo wa
  Mirerani, hivyo tutumie fursa hii kwa wachimbaji kuleta madini yetu kwenye
  maonyesho haya ili kuboresha uchumi wetu,” alisema Kambona. 


  Mmoja kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Saniniu Laizer alisema
  maonyesho kama hayo yanachangia kutangaza madini hayo, kwani kuna baadhi ya watu wana dhana potofu kuwa yanachimbwa nchi ya jirani.
   

  “Kupitia maonyesho haya tunaiomba serikali iboreshe zaidi sekta ya madini
  ya vito kwa kuwapa kipaumbele wachimbaji wadogo kwani wana changamoto nyingi zinazowakabili,” alisema Laizer.  


  Kwa upande wake, kaimu kamishna wa madini kanda ya kaskazini Elias
  Kayandabila alisema maonyesho hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza mji mdogo wa Mirerani na yanatarajia kufanyika tena mwakani kwenye eneo hilo.
   

  Kayandabila alisema kupitia maonyesho hayo wafanyabiashara wadogo kwa wakubwa wa madini ya vito ikiwemo Tanzanite, Tomarine ya kijani, Garnet ya kijani, Roadlite na mengineno, watanufaika nayo kwa kuboresha masoko yao.
   

  Maonyesho hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Nishati na Madini kanda ya ya kaskazini na vyama vya wachimbaji madini (Remas), chama cha madalali wa madini (Tasgedo) na chama cha wauzaji wa madini (Tamida).

  0 0

  Wakazi wa mji wa Sumbawanga watakiwa kuchukua taadhari juu wa ugonjwa wa mlipuko wa Kipindupindu ili kuepukana na madhara ya ugonjwa huo.

   Watu zaidi ya Sita wanaripotiwa kuwa na ugonjwa huo na wamefikishwa katika hospitali ya mkoa wa Sumbawanga kwajili ya matibabu.

   Serikali ya mji huo wa Sumbawanga imewataka wakazi wote wa mji huo kuchukuwa taadhari juu ya ugonjwa huo kwa Kunawa mikono yao kabla ya kula chakula na baada ya kula na 
   kufanya usafi wa mazingira.

  Pia wameaswa kuwakataza watoto wao kucheza katika mitaro ambayo haitiririshi maji machafu (inayotuamisha maji) na tahadhari zinginezo kujikinga na Ugonjwa huo uliopo hivi sasa Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona wa tatu kulia akiwa anaonyeshwa moja ya madini ya vifo yalioletwa katika maonyesho ya wafanyabiashara wa ndani wa madini hayo yaliyofanyika ndani ya mji mdogo wa mirerani mkoani Manyara
  Mmoja kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Saniniu Laizer akiwa anaonyesha jiwe la Tanzanite ambalo lipo tayari kuuzwa 
  Idha benki ya NMB ilimefungua rasmi tawi katika mji huu ndogo wa mererani hapa meneja wa mji mdogo wa benki hiyo akiwa anamueleza mkuu wa wialaya pamoja na wananchi waliouthuria semina hiyo huduma ambazo wanazitoa benki hiyo ndani ya mji mdogo wa mirerani
  Mkuu wa wilaya akiwa anakata utepe hii ikiwa ni ishara ya kufunguliwa rasmi kwa maonyesho hayo ya vito na madini 
  Wafanya biashara wakubwa ambao ni wa pili kulia ni mkurugenzi wa kampuni ya Jacaranda Holding DR,Antony Haj Frisby akiwa na mwenzake wanachagua madini ya vito kwa ajili ya kuyanunua ambapo alisema kuwa maonyesho haya ni mazuri sana ila aliomba wachimbaji wadogo wajitokeze kwawingi kuleta bidhaa zao.
  Habari picha na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog,Mererani

  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewaagiza wote waliovamia na kujikatia viwanja au kujenga kwenye eneo huru la usafirishaji bidhaa nje (EPZA) waondoke na kubomoa kabla hawajaondolewa kwa nguvu. 


  Inadaiwa kuwa vigogo watatu wa mji mdogo wa Mirerani, wamejenga nyumba za 
  kuishi kwenye eneo hilo na watu wengine zaidi ya 11 wamejimegea viwanja 
  kiubabe na kujiandaa kujenga ili hali mradi huo unatarajia kuanza kujengwa. 

  Akizungumza juzi wakati akifungua maonyesho ya madini ya vito ya siku
  mbili yaliyofanyika mji mdogo wa Mirerani, Kambona alisema mchakato wa
  kuwalipa fidia waliokuwa wanamiliki eneo hilo upo tayari hivyo wavamizi hao 
  waondoke. 

  Alisema baada ya kuwalipa waliokuwa wamiliki wa eneo la EPZA, mchakato wa 
  ujenzi utaanza mara moja kwani kutajengwa kituo kikubwa cha biashara za 
  kuuza nje ikiwemo soko la madini ya Tanzanite litakalojengwa sehemu hiyo. 

  Hata hivyo, alipongeza Wizara ya Nishati na Madini kufanya maonyesho hayo 
  kwa mara ya kwanza kwenye mji mdogo wa Mirerani, sehemu yanapopatikana 
  madini ya Tanzanite, kwani itasaidia kuboresha soko la madini katika eneo 
  hilo. 

  “Ni heshima kubwa tumepatiwa watu wa Simanjiro hususan mji mdogo wa
  Mirerani, hivyo tutumie fursa hii kwa wachimbaji kuleta madini yetu kwenye
  maonyesho haya ili kuboresha uchumi wetu,” alisema Kambona. 

  Mmoja kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Saniniu Laizer alisema
  maonyesho kama hayo yanachangia kutangaza madini hayo, kwani kuna baadhi ya 
  watu wana dhana potofu kuwa yanachimbwa nchi ya jirani. 

  “Kupitia maonyesho haya tunaiomba serikali iboreshe zaidi sekta ya madini
  ya vito kwa kuwapa kipaumbele wachimbaji wadogo kwani wana changamoto 
  nyingi zinazowakabili,” alisema Laizer. 

  Kwa upande wake, kaimu kamishna wa madini kanda ya kaskazini Elias
  Kayandabila alisema maonyesho hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza mji mdogo 
  wa Mirerani na yanatarajia kufanyika tena mwakani kwenye eneo hilo. 

  Kayandabila alisema kupitia maonyesho hayo wafanyabiashara wadogokwa
  wakubwa wa madini ya vito ikiwemo Tanzanite, Tomarine ya kijani, Garnet ya
  kijani, Roadlite na mengineno, watanufaika nayo kwa kuboresha masoko yao. 

  Maonyesho hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Nishati na Madini 
  kanda ya ya kaskazini na vyama vya wachimbaji madini (Remas), chama cha 
  madalali wa madini (Tasgedo) na chama cha wauzaji wa madini (Tamida).

  0 0


  Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Chemba amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bi. Fionnuala Gilsenan ofisini kwake katika jitihada zake za kuinua sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.  

  Waziri Nchemba alimweleza Balozi huyo kuhusu hali ya sekta ya kilimo na mikakati ya serikali katika kukabiliana na changamoto zinazokikumba kilimo chetu hapa nchini ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa mbegu, ambapo vituo vya utafiti vya serikali na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) vimejikita katika kutafiti mbegu mbali mbali. “Serikali imejipanga kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa mbegu bora kwa wakulima wetu” alieleza Mhe. Chemba.

  Pia alisema kuwa uzalishaji wa mbegu bora na hasa za viazi utasukumwa kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji ili ziweza kupatikana kwa wakati kwa wakulima wetu. Upatikanaji wa uhakika na kwa wakati wa mbolea kwa wakulima ni moja ya mikakati ya Serikali katika kuboresha na kuinua kilimo.

  Mikakati mingine kwa mujibu wa Waziri Nchemba ni kwa upande sekta ya mifugo ambapo kuna changamoto ya kuwabadilisha wafugaji kutoka ufugaji wa kiasili na kuingia katika ufugaji wa kisasa.

  Jitihada nyingine ni kuwaingiza vijana katika ufugaji wa kisasa wa samaki kwa kuwawezesha kupata zana bora za uvuvi, alibainisha Mhe Nchemba.Balozi Bi. Gilsenan alimfahamisha Waziri Nchemba kuwa nchi yake imedhamiria kusaidia kuinua tija kwa kuboresha mnyororo wa thamani ya mazao.Sehemu nyingine muhimu kwa mujibu wa Bi. Gilsenan ni pamoja na huduma za ugani, hifadhi na matumizi bora ya ardhi yanayolenga kupunguza migogoro, na kuchochea upatikanaji wa masoko kwa mazao yanayozalishwa. 

  Naye Mratibu wa Kitengo cha Mahusiano na Misaada ya Kimataifa kwa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Bi. Margareth Ndaba ameainisha maeneo ambayo Ireland inaweza kusaidia kuwa ni pamoja na lishe, Kilimo cha mboga mboga, zana za kilimo, utafiti na viwanda vya maziwa ili kusaidia kuondoa umaskini kwa Watanzania.

  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara ya Mifugo , Tanzania Dkt. Furaha Mramba alianisha changamoto ambazo Ireland inaweza kusaidia katika kuendeleza mifugo kuwa ni mabadiliko ya tabianchi ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa katika kuibua magonjwa mapya ya mifugo.

  “Tunaomba Ireland kusaidia katika chanjo za mifugo ili kupambambana na magonjwa yanayoambatana na mabadiliko ya tabianchi” , alisisitiza Dkt Mramba.Wakati huo huo Waziri Nchemba alikutana na wadau wa kilimo cha viazi kutoka Finland wakiongozwa na Naibu Balozi wa Finland nchini, Bwana Simo – Pekka Parviainen ambapo walimweleza nia ya kutaka kujikita katika kuboresha kilimo cha viazi mviringo. 

  Naye Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Peruna Mestant Bwana Aero Pisila alimfahamisha Waziri kuwa tayari wametembelea Mkoa wa Mbeya, Njombe na Arusha ili kuona fursa ya kuinua kilimo cha viazi mviringo na hasa kwa vijana wa Tanzania. 

  Aidha, Mratibu wa Mradi wa Kuendeleza kilimo cha Viazi Mviringo hapa nchini Bi. Matilda Byanda alifamweleza Waziri kuwa tayari wamefanya ziara za kujitambulisha katika Mikoa husika na kuonana na viongozi wa serikali na watalaam wa kilimo katika ngazi za halmashauri na kanda husika.

  Waziri Nchemba aliwataka kubainisha maeneo ambayo serikali itachangia katika kutimiza lengo hilo la kuboresha kilimo cha viazi mviringo.

  0 0

  MKUU wa Wilaya ya Geita Manzie Mangochie anasema Tamasha la Pasaka ni jambo kubwa sana kwao kwa sababu linafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.

  Mangochie anasema ukubwa na umuhimu wa tamasha hilo ni kutajwa kwa neno la Mungu na waimbaji sambamba na viongozi mbalimbali wa dini wanaofika katika tamasha hilo.Mangochie anasema Mkoa wa Geita una matatizo mengi ambayo yalikuwa yanahitaji kukemewa, lakini mwaka huu Mungu amesikia matakwa ya wakazi wengi wa mikoa hiyo ambayo ilitawaliwa na matukio ya mauaji yakiwemo ya vikongwe na walemavu wa ngozi ‘Albino’.

  “Mikoa hii ya Kanda ya ziwa iligubikwa na shetani ambaye ni mauaji ya Maalbino na Wakongwe ambao walikuwa wakitendewa unyama ambao Mungu alikuwa akichukizwa nao, hivyo kupitia Tamasha la Pasaka neno la Mungu litasaidia kuondosha madhila hayo,” alisema Mangochie.

  Mangochie anasema kupitia Tamasha la Pasaka waandaaji watasaidia wakazi wa mikoa hiyo kuachana na kusahau matukio ya kumchukiza Mungu.Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yanaendelea vilivyo kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.

  Msama alisema tamasha hilo linatarajia kuanza Machi 26 kwenye ukumbi wa Desire ulioko mkoani Geita, Machi 27 litafanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na Machi 28 litafanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.

  Msama alisema viingilio kwa wakubwa ni shilingi 5000 na watoto shilingi 2000 ambako alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.

  0 0  ORODHA YA MAJINA WATEULE   0 0

  Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba akikabidhi msaada wa Mabati 64 kwa ajli ya Ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari ya Bazo iliyopo kata ya Vuga Wilayani Lushoto mkoa wa Tanga.
  Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba akizungumza na Wananchi wa Kata Mponde katika Mkutano hadhara, ambapo Mbunge huyo ameeleza Mikakati mbalimbali ya kuwasaidia wananchi wa Kata hiyo ambao wengi wao hujishughulisha na masuala ya Kilimo.
  Gari ikiwa imebeba Rola 70 za Mabomba ya kusafirishia Maji, ambayo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba kwa wananchi wa Kata ua Usambara ili kupunguza Kero ya muda mrefu ya wananchi hao katika Suala la Upatikanaji wa maji safi na salama.( Picha na Imani Nsamila ).  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) Antony Mavunde ametaka kuondolewa kwa changamoto maeneo ya kazi ili kazi isaidie maendeleo ya binadamu badala ya kujikimu.Naibu Waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua ripoti ya maendeleo ya binadamu ya mwaka 2015 inayoelezea kazi kwa maendeleo ya binadamu.

  Alisema kwa sasa kuna figisu kubwa katika kazi nchini hasa kutokana na waajiri wengi kugeuza kazi kama sehemu ya kujikimu kwa wafanyakazi wao kwa kutowapa stahiki husika ikiwamo mikataba ya ajira.

  Alisema kazi inapokuwa ni ya kujikimu kunakuwa na migogoro mingi na kuvurugika kwa uzalishaji na kutishia maendeleo ya taasisi husika na maendeleo ya mtu binafsi.Alisema Tanzania imefurahishwa na yaliyomo katika ripoti hiyo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kutokana na kuzungumzia jinsi kazi zinavyoweza kusaidia upatikanaji wa maendeleo.
  UNDP HUMAN DEVELOPMENT REPORT 2015 LAUNCH
  Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) akizindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Machi 11, 2016.
  Anthony Mavunde
  Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde akionyesha ripoti hiyo kwa wageni waalikwa na waandishi wa habari (hawapo pichani).
  IMG_6200
  Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo kwa pamoja wakiwa wameshikilia ripoti hiyo.
  Alisema wakati Tanzania inaelekea kujipanga kwa uchumi wa kati, Ripoti inaonyesha ni jinsi gani kazi inaweza kuboresha maisha ya Mtanzanzania kwa kuondoa kazi na kuwapatia wananchi kazi zenye staha na zinazoweza kuwasaidia wao binafsi na hivyo kukuza uchumi na ustawi wa jamii.

  Alisema amekuwa akizungumza katika maeneo mengi ya kazi na kukutana na changamoto nyingi zikiwemo za kukosekana kwa mikataba, mazingira mabaya ya kufanyakazi, ujira usiokidhi na kutaka waajiri kufuata sheria za kazi kwa kuwapatia mikataba ya kazi na pia kuhakikisha kazi zinakuwa na staha.

  Awali akizungumza na wageni waalikwa katika hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dar es Salaam, alisema kwamba uzinduzi wa kitaifa ambao unafuatia uzinduzi wa kimataifa uliofanyika mwaka jana mjini Addis Ababa, Ethiopia ni faraja kubwa kwa wadau wa maendeleo nchini.Alisema uzinduzi huo unaweka ripoti hiyo karibu zaidi na wananchi na kuahidi serikali kuifanyia kazi kutokana na umuhimu wake hasa wa kuhakikisha kazi inasaidia maendeleo ya watu.

  Anthony Mavunde
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (kushoto) akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kulia) kabla ya kuelekea kwenye uzinduzi rasmi wa ripoti ya maendeleo ya watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) uliofanyika Machi 11, 2016 jijini Dar es Salaam na kuratibiwa na ESRF.

  Anasema ripoti hiyo inaonesha namna ambavyo kazi inaweza kuchangia maendeleo na ustawi wa jamii.Alisema wakati Tanzania inaelekea kuwa taifa ambalo limejengeka katika msingi wa maendeleo ya watu kama ilivyokusudiwa tangu kupatikana kwa Uhuru wake 1961, Ripoti hiyo ni chanzo kizuri cha maarifa katika kufanikisha mabadiliko yanayotakiwa kufanikisha maendeleo ya watu.

  Alisema kazi ni msingi wa maendeleo kwa hiyo ni vyema kuboresha mazingira ya kazi na wafanyakazi ili kuleta maendeleo kusudiwa kwa kuwa na kazi zenye staha.Alipongeza UNDP na wadau wengine kwa kufanikisha uzinduzi huo ambao alisema umeenda sanjari na dhima ya serikali ya kutumia maarifa yote yaliyopo kusaidia maendeleo ya watu.Ripoti hiyo ya UNDP imetazama kwa undani kuhusu kazi, mahusiano ya kazi na maendeleo ya binadamu.
  George Mulamula
  Mshehereshaji wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) akisherehesha uzinduzi huo uliofanyika Machi 11, 2016 jijini Dar es Salaam na kuratibiwa na ESRF.
  Aidha imeangalia masuala ya usalama wa kazi na mahitaji ya utaalamu; masuala ya kulipwa na kutolipwa kazini, uangalizi, kujitolea ubunifu na kazi endelevu.
  Pia ripoti hiyo inatoa majumuisha yanayostahili kufanywa bali mapendekezo ya utengenezaji wa sera unaotanua uzalishaji kwa kutoa fursa na kulinda wafanyakazi, ubora wa kazi, ujira stahiki, kazi yenye staha na kazi endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

  Kimsingi Ripoti hiyo inapendekeza kuongeza faida za maendeleo ya binadamu, kupitia utendaji kazi, kwa kupendekeza mikakati ya kujenga fursa za ajira, ili kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi, na kuendeleza maeneo yaliyolengwa, ambayo yatabadilisha hali halisi ya sasa.

  Aidha ainaangalia Sera zilizopendekezwa, kuhakikisha utendaji kazi bora, utendaji kazi endelevu, ambayo inachangia usawa, badala ya kujenga ukosefu wa usawa, na kazi ambayo inaheshimu haki za wafanyakazi, na kuhakikisha usalama wao.
  Human Development Report 2015, Tanzania
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisoma taarifa kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) uliofanyika jijini Dar es Salaam Machi 11, 2016 na kuratibiwa na ESRF.
  Kwa mujibu wa ripoti hiyo kuna hatua njema kwenye maendeleo ya watu katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania ikiwamo lakini ipo haja ya kuangalia pengo kubwa lililopo katika fursa mbalilmbali zikiwamo za kazi.

  Imeelezwa ndani ya ripoti hiyo kwamba toka mwaka 2000 nchi ziloizo kusini mwa Jangwa la Sahara zimekuwa na ukuaji wa maendeleo ya binadamu( Human Development Index -HDI) wa kazi wa kiwango cha asilimia 1.7 kati ya mwaka 2000 na 2010 : asilimia 0.9 kwa mwaka 2010 na 2014.HDI ni kipimo kinachotathmini maendeleo ya muda mrefu ya afya na maisha marefu, elimu na maisha yenye staha.

  Kwa Tanzania kumekuwepo na ongezeko la HDI la asilimia 1.18% kati ya mwaka 1985 na 2014, ikiongezeka kutoka 0.371 hadi 0.521, ikiwa ni ongezeko la asilimia 40.5 juu ya ongezeko la nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara la 0.518.
  Human Development Report 2015, Tanzania
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (hayupo pichani) kuhutubia wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) uliofanyika jijini Dar es Salaam Machi 11, 2016 na kuratibiwa na ESRF.

  Mratibu wa Umoja wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza katika uzinduzi huo alisema kwamba ongezeko hilo si haba.

  Hata hivyo aliwaambia wadau waliokuwepo kushuhudia uzinduzi huo kwamba Taifa bado linakabiliwa na changamoto nyingi zikkiwemo umaskini uliokithiri, kutanuka kwa pengo la usawa na kushindwa kuhimili matukio ya mabadiliko ya tabianchi na uchumi.

  Aidha alisema kwamba :”Ripoti ya maendeleo ya binadamu ya mwaka 2015, inaonyesha kuwa, kuimarisha maendeleo ya binadamu, kupitia utendaji kazi, inahitaji sera na mikakati katika maeneo makuu matatu: kujenga fursa za ajira, kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi na kuendeleza maeneo yaliyolengwa. Hii inaongeza kasi ya kutengeneza ajira nchini Tanzania.”
  Tanzania ikiwa na zaidi ya watu milioni 12 wakiishi katika umaskini na wengi wao uliokithiri changamoto kubwa kwa Tanzania, ni kutafsiri uwezo huu katika miundombinu inayoonekana, kwa kujenga mazingira mazuri, na kuongeza ujuzi wa watu wake kama ilivoainishwa katika Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu mwaka elfu mbili na kumi na tano.
  Human Development Report 2015, Tanzania
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde akisoma hotuba ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) kwa niaba ya Waziri Jenista Mhagama, uliofanyika jijini Dar es Salaam Machi 11, 2016 na kuratibiwa na ESRF.

  Alisema changamoto zote hizo ni za kweli na zenye uhusiano na maendeleo ya binadamu na ni vyema ilivyowekwa katika Muono wa maendeleo ya Tanzania kufikia 2025 na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).

  Katika hotuba yake ya shukurani Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo, alisema kwamba taasisi yake ipo tayari kusaidia Tanzania na nchi nyingine kuwezesha kutambua uhusiano kati ya kazi na maendeleo ya binadamu katika utekelezaji wa Maendeleo endelevu (SDGs).
  Human Development Report 2015, Tanzania
  Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) na meza kuu wakijiandaa kuzindua ripoti hiyo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo.
  Human Development Report 2015
  Muonekano wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015). Kwa picha zaidi bofya link hii
  IMG_6050
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) akiwasili kwenye uzinduzi wa ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) huku akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kulia) uliofanyika Machi 11, 2016 jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael akiwa ameongozana na Mkuu wa usalama wa uwanja huo Macmilan Matili kuangalia maeneo mbalimbali ya uwanja huo. 
  Meneja wa uwanja mdogo wa ndege Moshi,Fredrick Kimaro akimuonesha Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael eneo la maegesho ya ndege katika uwanja huo. 
  Mbunge Jafary Michael na ujumbe wake wakiongozwa kupita katika eneo la kutua ndege uwanjani hapo. 
  Meneja wa uwanja wa ndege wa Moshi ,Fredrick Kimaro akimsikiliza kwa makini Mbunge Jafary Michael wakatia akishauri jambo baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uwanja huo. 
  Eneo la kukimbilia ndege katika uwanja mdogo wa ndege Moshi likionekana katika hali hii.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
   Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael (katikati) akiwa na Diwani wa kata ya Korongoni Ally Mwamba (kushoto) walipotembelea uwanja wa ndege mdogo wa Moshi . 
   Meneja wa Uwanja mdogo wa ndege wa Moshi,Fredrick Kimaro akisoma taarifa ya uwanja huo kwa Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafary Michael alipotembelea uwanja huo. 
   Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini ,Jafry Michael akizungumza jambo alipotembelea uwanja huo kuona namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo. 
   Meneja wa Uwanja huo Fredrick Kimaro akisisitiza jambo wakati akitoa maelezo kwa Mbunge wa jimbo la Moshi mjini alipotembelea uwanjani hapo. 

  0 0  Mariamu Hussein akihudhuria harambe ya kumchangia iliyofanyika siku ya Jumamosi Silver Spring, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na WanaDMV na marafiki zao. Mariam Hussein nasumbuliwa na ugonjwa wa saratani.
  Vitu mbalimbali vilivyoletwa na WanaDMV kwa ajili ya kuvipiga mnada kwenye harambee iliyofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, Maryland nchini Marekani.
  WanaDMV na marafiki zao waliohudhuria harambee ya Mariam Hussein (wanne toka kushoto) iliyofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, Maryland nchini Marekani.
  Baadhi ya WanDMV wakiendelea kupata mapochopocho kwenye harambee ya kumchangia Mariam Hussein (hayupo pichani) iliyofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, Maryland nchini Marekani.
  Mariam Hussein (kati) akiwa na familia yake kwenye harambee ya kumchangia fedha za matibabu ya saratani iliyofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016
  Mnada ukiendelea
  Vitu mbalimbali vilivyoletwa katika mnada wa harambee ya Mariam Hussein uliofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, maryland nchini Marekani.
  Mariam Hussein (kati) akifuatilia Harambee ya mnada wa kuwezesha kupatikana kwa fedha za matibabu ya Saratani siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, maryland nchini Marekani.
  Picha ya pamoja
  Picha ya pamoja

  Picha ya pamoja. kwa picha zaidi bofya hapa

  0 0

  Bango Sangho - Kibugumo
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (katikati) akimpima uzito mtoto Shafii Haji (mwaka mmoja na nusu) mkazi wa Kibugumo Darajani, kama ishara ya kuzindua kambi ya huduma za upimaji afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa kambi hiyo kutoka Kliniki ya Al Hilal, Dk. Ali Mzige, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile (wa kwanza kulia) pamoja na Muuguzi wa Zahanati ya Kibugumo, Agnes Mokiwa (wa pili kulia) wakishuhudia tukio hilo.
  Bango Sangho - Kibugumo Primary Schoo.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (katikati) akiwa amembeba mtoto Shafii Haji (mwaka mmoja na nusu) mkazi wa Kibugumo Darajani, baada zoezi la kumpima uzito wakati akizindua kambi ya huduma za upimaji afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam.
  Bango Sangho - Kibungumo Primary School
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akikagua kadi ya kliniki ya maendeleo ya mtoto Shafii Haji (mwaka mmoja na nusu) mkazi wa Kibugumo Darajani (hayupo pichani) mara baada ya kuzindua kambi ya upimaji afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa kambi hiyo kutoka Kliniki ya Al Hilal, Dk.Ali Mzige na Kulia ni Muuguzi wa Zahanati ya Kibugumo, Agnes Mokiwa.
  Bango Sangho-Kibugumo
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakigaiwa madaftari yaliyotolewa kama zawadi na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho).
  Bango Sangho-Kibugumo Primary School
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akielekea kuzindua moja ya madarasa yaliyokaribatiwa na kuwekewa umeme na Bango Sangho.

  Sophia Mjema
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akikata utepe kuzindua moja kati ya madarasa yaliyokarabatiwa na Bango Sangho huku Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile wakishuhudia tukio hilo.
  Bango Sangho - Kibugumo Primary School
  Muonekano wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kibugumo baada ya kupakwa rangi na kuwekwa umeme na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho).
  Bango Sangho - Kibugumo
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akikagua moja ya darasa lililokarabatiwa na Bango Sangho
  Bango Sangho- kibugumo Primary School
  Meza kuu kwenye uzinduzi wa kambi ya upimaji afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mratibu wa kambi hiyo ya upimaji kutoka Kliniki ya Al Hilal, Dk.Ali Mzige, Mwenyekiti wa Umoja wa Jamii ya watu kutoka India, Bengali waliopo Tanzania (Bango Sangho), Kunal Banerjee, Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Kibugumo, Mzamilo Ally, Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

  Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi nchini (Bango Sangho) umetoa msaada wa kompyuta, printa, tanki la maji la lita 5000, umeme, madarasa saba yaliyofanyiwa ukarabati, madaftari na kalamu katika Shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni ulio na thamani ya shilingi Milioni 20 pamoja na huduma ya kupima afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano.

  Akizungumzia msaada huo, Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee alisema wameamua kutoa msaada huo kwa shule ya Msingi Kibugumo na huduma ya kupima bure kwa kutambua umuhimu wa afya na elimu bora kwa maendeleo ya sasa na baadae kwa taifa.

  Alisema wamekuwa wakitoa misaada katika shule hiyo kwa mwaka wa tatu mfululizo na mwaka huu waliamua kuwaletea tena na huduma ya upimaji afya bure kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano ili wazazi wapate fursa ya kutambua hali ya afya za watoto wao lakini pia kuwajengea utaratibu wa kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya ili kujua hali zao za kiafya,

  “Sisi tunapenda kuona hali nzuri ya elimu na tumeshasaidia kwa muda shule hii tumeshatoa madawati 100 na tulijenga madarasa mawili na leo tumeleta msaada mwingine na pia awamu hii tena tumeleta huduma ya afya ili watoto  wapimwe afya zao,” alisema Banerjee.

  Bango Sangho
  Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee akisoma risala ya Umoja huo mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile.

  Nae mgeni rasmi katika halfa hiyo ya kupokea msaada kutoka Bango Sangho, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bi. Sophia Mjema aliwashukuru Bango Sangho kwa msaada huo ambao wameotoa katika shule hiyo na huduma ya kupima afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano na kuwaomba kama ikiwezekana wawapelekee huduma hiyo ya kupima afya kila baada ya miezi mitatu.

  Alisema wilaya yake bado ina changamoto nyingi katika sekta ya elimu na kupitia msaada huo utaweza kusaidia kuboresha elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo na kuwaomba kuendelea kuwasaidia.“Wilaya yetu bado ina changamoto nyingi na kwa msaada huuu naomba niwashukuru sana na ninaomba muendelee kuwa na moyo huo,” alisema Bi. Mjema.

  Aidha Bi. Mjema aliwataka wananchi wa wilaya yake ya Temeke kuwa na utaratibu wa kupima afya zao angalau mara moja kwa mwaka ili waweze kutambua magonjwa waliyonayo kabla hayajaanza kuwasumbua na hata wengine kupelekea kupoteza maisha kutokana na kutokuwa na utaratibu wa kupima hadi wanapoanza kusumbuliwa.

  Nae Mratibu wa kambi ya upimaji, Dkt. Ali Mzige alisema kupitia huduma hiyo ya upimaji wa afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano wanataraji kupima watoto sio chini ya 400 na huduma zitakazotolewa ni kupima uzito, wingi wa damu, ushauri kuhusu lishe, afya ya kinywa na watoto watakaobainuka kuwa na matatizo watapewa rufaa kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Temeke.

  Alisema kupitia huduma hiyo wataweza kutambua magonjwa waliyonayo watoto lakini pia kuwapa elimu wazazi jinsi ya kuwalea watoto katika mfumo bora wa kiafya.
  “Tunafanya huduma hii kwa watoto sababu asilimia 32 ya watoto nchini walio na umri chini ya miaka mitano wamedumaa na pia tutaweza kuwapa vipeperushi wazazi ili wajue jinsi ya kulea watoto na wanapougua wajue nini cha kufanya,” alisema Dkt. Mzige.

  Nae mwalimu wa afya katka shule ya Kibugumo, Tatu Mhina aliwashukuru Bango Sangho kwa misaada ambayo wamekuwa wakiwapatia tangu mwaka 2014 mpaka sasa na kuwaomba kuendelea na moyo huo wa kusaidia elimu katika shule hiyo na kuzidi kuwapelekea huduma za kiafya katika jamii inayozunguka shule hiyo ili wanafunzi waweze kuwa na afya njema.
  Bango Sangho Kibugumo
  Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema kutoa nasaha katika ufunguzi wa kambi hiyo.
  Bango Sangho - Kibugumo
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akitoa neno la ufunguzi wa kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam.

  0 0

  mssoga

  Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiongozwa na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Msoga, Dk. Juliet Lema wakati wa ukaguzi huo. Kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Dkt. Beatrice Jane Byalugaba.(Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipa hadhi ya kuwa Hospitali Wilaya iliyokuwa Zahanati ya Msoga ambayo tayari imekamilisha jengo lake jipya la Hospitali hiyo inayotarajia kuanza kuanzia Mwezi Aprili mwaka huu.

  Akitoa maagizo hayo baada ya ukaguzi wa timu ya wataalam kutoka Wizara hiyo ya Afya pamoja na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla waliofanya hivi karibuni katika Hospitali hiyo, ameeleza kuwa kuanzia Mwezi Aprili ianze kazi kwa kuanza na huduma za wagonjwa wa nje na baada ya miezi mitatu itaendeshwa na huduma zote muhimu ikiwemo kulaza wagonjwa.

  “Naagiza ndani ya mwezi mmoja ianze kazi na huduma za kawaida. Baada ya miezi mitatu itaendelea na huduma muhimu zote katika Hospitali hii mpya ya Wilaya” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa hitimisho lake kwa wasimamizi wa Zahanati hiyo ya Msoga.
  Dk. Kigwangalla na timu yake waliweza kukagua majengo ya Hospitali hiyo mpya ambapo na kuona inakidhi vigezo ya kuwa Hospitali ya Wilaya.

  Majengo ya Hospitali hiyo yapo katika Kituo cha afya cha Msoga, kata ya Msoga, Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani, Ni miongoni mwa Hospitali itakayokuwa ya kisasa na kubwa.Aidha, kutokana na matukio mengi ikiwemo ya ajali nyingi zinazotokea mara kwa mara katika barabara ya Chalinze-Segera, Hospitali hiyo ya Wilaya itakuwa msaada na itawezesha kupunguza mzigo wa vituo vya afya vya vya jirani ikiwemo Lugoba, Chalinze na vinginevyo ndani ya Halmashauri hiyo yaa mji mdogo wa Chalinze.
  msoga
  Jengo hilo la Hospitali ya Wilaya inavyoonekana kwa nje
  msoga 55
  Waziri Dk. Kigwangalla akiwa na timu yake wakikagua eneo hilo la Hospitali ya Wilaya. Jengo linaloonekana nyuma awali lilipangiwa kuwa sehemu ya kuhifadhia maiti (Mochwari) hata hivyo wamebadilisha matumizi yake na Mochwari itajengwa mbali kidogo na hapo ilikutoa naafasi kubwa kwa kujengwa mochwari ya kisasa.
  msoga 22
  Dk. Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni katika Zahanati ya Msoga mara baada ya kufanya ukaguzi na kuagizia majengo mapya ya Hospitali hiyo kuanzia mwezi ujao wa Aprili yaanze kutumika kama Hospitali ya Wilaya ambapo Madawa na vifaa vinatarajiwa kupelekwa muda wowote kuanzia sasa. 

  0 0

  Ni Katibu wa TSD Mkoa wa Singida,Bwana Samweli Ole Saitabau(aliyesimama) akitoa ufafanuzi juu ya upatikanaji wa haki za walimu wa wilaya ya Manyoni ambao bado haapandishwa madaraja yao.

  Ni Baadhi ya wanachama wa CWT Wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Katibu Muu wa CWT,Bwana Ezekiah Oluoch  .
  WALIMU 447 wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida hawajapandishwa madaraja yao mbalimbali kutoka mwaka 2014/2015 mpaka sasa hali ambayo imepunguza ari ya utendaji wao wa kazi za kila siku.
  Katibu wa Chama Cha Walimu (CWT) Wilaya ya Manyoni, Nelea Nyang’uye aliyasema hayo kwenye taarifa ya kamati ya utendaji ya chama hicho aliyotoa kwa Naibu katibu mkuu CWT,Ezekiah Oluoch aliyekuwa na ziara ya siku moja wilayani Manyoni iliyolenga kusikiliza kero pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
  Aidha Nelea alifafanua kwamba kati ya walimu hao,walimu 390 ni walimu wa shule za msingi na kwamba walimu 276 licha ya kuwa na sifa za kupandishwa madaraja lakini mpaka wamefikia hatua ya kugota na bila kupandishwa na walimu 114 wanastahili kupandishwa kwa utaratibu wa kawaida.
  Kwa mujibu wa katibu huyo wa CWT,kwa upande wa idara ya elimu sekondari kuna walimu 9 waliogota na walimu 50 wanastahili kupandishwa kwa utaratibu wa kawaida lakini mamlaka zinazohusika zimeshindwa kushughulikia wilayani hapa.
  Kuhusu malipo ya fedha za likizo,Nyang’uye aliweka bayana kuwa kwa kipindi cha mwezi disemba,mwaka jana Halmashauri ya wilaya ya Manyoni ilitarajia kupokea shilingi milioni 30 lakini fedha walizopokea ni shilingi milioni 21 na hivyo kuwa na upungufu wa shilingi milioni saba.
  Hata hivyo msemaji huyo wa chama alisisitiza kwamba fedha hizo za nauli ya likizo hupelekwa kidogo sana na kibaya zaidi fedha hizo hupelekwa wakati likizo ikiwa imeshaanza au inakaribia kwisha,jambo ambalo linapelekea walimu wwenye haki ya kulipwa kuanza kukopa.
  “Nauli za likizo kuletwa kidogo mno na zinaletwa wakati likizo ikiwa imeanza au inakaribia kwisha,jambo ambalo linapelekea walimu wenye haki ya kulipwa kuanza kukopa,kwa mfano nauli ya mwezi disemba,mwaka jana iliyoletwa kwa idara ya elimu ya msingi ni shilingi 23,000,000/= na idara ya elimu sekondari ni shilingi milioni saba”alisisitiza katibu huyo wa CWT.
  Nyang’uye hata hivyo alionyesha masikitiko yake kutokana na Tume ya Utumishi wa Walimu(TSD) wilaya ya Manyoni kushindwa kushughulikia mashauri ya kinidhamu kwa wakati na hivyo kuchukua muda mrefu sana na kutoa mfano wa shauri moja la walimu wawili waliosimamishwa kazi tangu mwaka 2013 mpaka sasa hawajuia hatma yao.

  0 0

  mada wote
  Baadhi ya wadau wakitoa zawadi na vitu mbalimbali kwa Madam Sophy ambavyo vitagawiwa kwa wanafunzi wa shule hiyo ya Jeshi la Wokovu na wale wa Makumbusho Sekondari.
  madae
  Wanafunzi wenye ulemavu wa viungo na ngozi wakiwa katika tukio hilo.
  madass
  Wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wakitoa burudani kwa mgeni rasmi (hayupo pichani).
  Taasisi mpya ya Kijamii ijulikanayo Madam Sophy Charity Events yenye malengo ya kusaidia jamii hasa ile yenye uhitaji maalum ikiwemo watu wasiojiweza imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam sambamba na kutoa misaada mbalimbali kwa watu na watoto wenye uhitaji huo maalum.

  Tukio hilo la kipekee lililoandaliwa na kuratibiwa na Mwanadada, Sophia Mbeyela pia lilijumuisha wadau na marafiki mbalimbali walioungana na Madam Sophy katika kufanikisha tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jeshi la Wokovu ambayo ilishirikisha watoto wanafunzi wa kituo cha Matumaini wenye Ulemavu wa viungo na ngozi.

  Madam Sophy na marafiki zake kwa pamoja waliweza kutoa misaada ya vitu  mbalimbali kwa watoto hao ambapo pia walipata wasaha wa kuzindua taasisi hiyo huku mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ambaye aliwakilishwa na Mbunge Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa ambaye aliahidi kufikisha kilio cha walemavu na watu wenye mahitaji maalum Serikalini paamoja na kwenda kuwasilisha Bungeni ilikuona utekelezaji wake kwa ukaribu.

  “Madam Sophy Charity. ni taasisi ambayo zaidi ni kuona wenzetu wenye uhitaji maalum hasa walemavu wanapata nafuu katika kuendana na majukumu ya nchi hii kwani sote tuna haki sawa kama wengine na ulemavu wetu usitutenganishe. Tunahitaji Serikali kuhakikisha inashusha bei vifaa vyote vya walemavu ikwemo viungo vya bandia ikiwemo mikono na miguu ambayo kwa kiungo mimoja pekee yake kinakaribia hadi milioni moja” alieleza Madam Sophy.

  Madam Sophy aliongeza kuwa, Serikali inayo wajibu wa kujenga shule nyingi zaidi za watu wenye ulemavu kwani zilizopo sasa bado ni chache na watu wenye ulemavu wamehamasika kujitokeza kusoma hivyo jukumu lililopo ni kuhakikisha wanaongeza shule za watu hao pamoja na kutengeneza miundombinu ambayo inakuwa rafiki kwa walemavu kuanzia mashuleni na hata maeneo muhimu.

  Aidha, Kwa upande wake, mgeni rasmi huyo aliweza kuchangia kiasi cha Sh Laki tano kwa ajili ya kuunga mkono juhudi na harakati za Madam Sophy ambapo alieleza kuwa, licha ya ulemvu wake ameweza kuonesha njia ya kujikwamua pamoja na kuwasaidia wenzake.

  Madam Sophy ambaye kitaaluma ni Mwalimu, ni miongoni mwa wanafunzi waliopata kusoma katika shule hiyo na kumaliza hapo darasa la saba mwaka 2002 ambapo pia aliendelea na shule mbalimbali ikiwemo Sekondari ya Jangwani na baadae chuo, ameomba wadau kujitokeza kuungana naye katika kuhakikisha wanasaidia watu na jamii yenye uhitaji maalum kwani kutoa ni moyo.


  0 0


  Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Mhe Nape Nnauye akifungua kikao chao cha kazi cha mwaka cha Maafisa habari na mawasiliano serikalini katika ukumbi wa VETA, Morogoro .
  Maafisa habari na Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo mhe Nape Nnauye wakati akifungua kikao chao cha kazi cha mwaka ukumbi wa VETA Morogoro.
  Maafisa habari na Mawasiliano Serikalini wakijitambulisha muda huu mbele ya Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo mhe Nape Nnauye ambae atafungua kikao chao cha kazi cha mwaka ukumbi wa VETA Morogoro.


  Maafisa habari na mawasiliano serikalini wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo,mara baada ya kujitambulisha mbele ya Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Mhe Nape Nnauye ambae amefungua kikao chao cha kazi cha mwaka ukumbi wa VETA Morogoro.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo BW. Assah Mwambene (wa pili kushoto) akiwa na wadau baada ya kumsindikiza Mhe. Nape Nnauye baada ya kufungua kikao cha kazi cha mwaka cha Maafisa habari na Mawasiliano Serikalini katika ukumbi wa VETA Morogoro.

  Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Mhe Nape Nnauye akifungua kikao cha kazi cha mwaka cha Maafisa habari na Mawasiliano Serikalini katika ukumbi wa VETA Morogoro.
  Maafisa habari na Mawasiliano Serikalini katika ukumbi wa VETA Morogoro.
  Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Mhe Nape Nnauye akiongea baada ya kufungua kikao cha kazi cha mwaka cha Maafisa habari na Mawasiliano Serikalini katika ukumbi wa VETA Morogoro.

  0 0

   Makatibu Wakuu kutoka Wizara tofauti wakihudhuria mafunzo ya ‘Warsha ya Usimamizi wa Vihatarishi na Udhibiti wa Ndani’ (Risk Management and Internal Control Systems Workshop) yaliyoandaliwa kwa ajili ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu na Taasisi ya UONGOZI tarehe 8 mpaka 9 Machi 2016 Dar Es Salaam.
     Mwezeshaji akiongoza kipindi cha maswali na majibu kwa Makatibu Wakuu baada ya kuwasilisha mada yake.
  Baadhi ya Makatibu Wakuu wakishiriki kwenye mijadala ya mafunzo hayo kwa kusikiliza kutoka kwa Wawezeshaji tofauti.

  0 0


  Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakiwa kwenye hali ya furaha wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na benki hiyo kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Ulimwenguni iliyofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  0 0

  WAKAZI wa Mji wa Kahama wamemkaribisha kwa mikono miwili, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kwenye Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 28 mjini humo.

  Wakazi hao ambao hawakujitambulisha majina yao walieleza kwamba Profesa Mbarawa ni Waziri ambaye walikuwa wanamhitaji wajumuike naye pamoja ili kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kama maandiko matakatifu ya Mungu yanavyoeleza kwamba wakutanapo wawili kwa jina langu, nipo katikati yao.

  “Tamasha la Pasaka si la kidini kinadharia kwa sababu, michango inayopatikana kupitia viingilio hayachagui, dini, jinsia wala kabila, hivyo wakijumuika naye itasaidia wakazi wa mikoa hiyo kupona kupitia maandiko matakatifu,” alisema mmoja wa wakazi wa mji huo maarufu kibiashara.

  Walisema watashukuru wakijumuika na Waziri Mbarawa kwa sababu italeta chachu ya ibada hiyo takatifu ambayo uwasilishaji wake unafanyika kupitia nyimbo za Injili na maombi kutoka viongozi wa dini.     

  “Kwanza tunashukuru kwa Kampuni ya Msama Promotions kutuletea Waziri Mbarawa kwenye Tamasha la Pasaka, kuja kwake kutasaidia kukemea machafu yaliyokuwa yakifanyika Kanda ya Ziwa kwa mauaji ya Vikongwe kwa imani za kishirikina na walemavu wa ngozi ‘Albino’,” alisema mmoja wa wakazi wa Kahama.

  Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema hivi sasa Kamati yake inaendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha hilo.Msama alisema waimbaji watakaopanda jukwaa la tamasha hilo wanaendelea kujifua vilivyo kwa lengo la kufanikisha kazi hiyo ya Mungu.Tamasha la Pasaka linatarajia kuanza Machi 26, mkoani Geita kwenye ukumbi wa Desire, Machi 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kumalizia Uwanja wa Taifa mjini Kahama.

older | 1 | .... | 793 | 794 | (Page 795) | 796 | 797 | .... | 1903 | newer