Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 791 | 792 | (Page 793) | 794 | 795 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma
  Watanzania wameaswa kujenga tabia ya kujiwekea akiba kupitia mabenki kwa manufaa yao na taifa kwa kwa ujumla ikiwa ni mchango wao katika kutekeleza kaulimbiu ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kufikia malengo waliojiwekea katika kujiletea maendeleo endelevu.

  Hayo yamesemwa na Meneja wa Fedha na Utawala kutoka Bodi ya Bima na Amana (DIB) iliyo chini ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Richard Malisa wakati akitoa mada juu ya bodi hiyo katika semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi hao katika kuandika, kutoa na kusambaza habari za sekta ya uchumi biashara na fedha.

  “Pesa zinapowekwa na kuwa benki hutumika kuchangia kuinua na kuimarisha usalama wa akiba ya mtu binafsi na kwa upande wa nchi zinatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuinua sekta ya elimu, afya, maji,  ujenzi wa barabara na kilimo” alisema Malisa.

  Katika kuonesha umuhimu wa bodi hiyo nchini, Malisa alisema kuwa taasisi ama mtu binafsi anapoweka pesa zake benki, hiyo ni amana kubwa na muhimu kwa kuwa tabia hiyo ya uwekaji pesa ina tija na inaongeza usalama wa pesa ambayo ni njia salama ikilinganishwa na kutumia njia za zamani za watu kuweka pesa kwenye godoro ambayo sio salama.

  Faida nyingine za mtu binafsi ama taasisi kuweka pesa zao benki ni kuongeza mtaji wake kwa kupata riba kulingana na muda pesa hizo zinapokuwa benki na mteja anauhakika pesa yake ipo salama kwa kuwa ipo mikononi mwa Bodi ya Bima na Amana endapo litatokea tatizo lolote kwenye benki alipoweka pesa zake.

  Katika kufanikisha na kutekeleza majukumu yake, DIB inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uelewa mdogo wa mtu mmoja mmoja katika masuala ya kibenki na fedha kwa undani wake ili aweze kufanya maamuzi yatakayomfanya awe bora zaidi kiuchumi ikilinganishwa na hapo awali kabla ya kufahamu masuala ya kibenki na fedha ikiwemo kuongeza nidhamu ya matumizi.

  Akitolea mfano Malisa amewaasa Watanzania wawe makini wanapochukua mikopo ambapo alisema kuwa watu wasikope kwa kufuata mkumbo ama kwa shinikizo fulani, bali wakepo kwa lengo la kuwekeza ili kuinua hali zao za kiuchumi katika maisha.

  Hadi kufikia Juni 30, 2015 Bodi ya Bima na Amana ina akiba ya jumla ya kiasi cha Sh. biloni 220.5 ikilinganishwa na wakati ilipokuwa inaanzishwa na Serikali mwaka 1994 ambapo kianzio kilikuwa kiasi cha Sh. bilioni 1.5.

  Aidha, katika semina hiyo Bw. Bernard Dadi kutoka Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa alisema kuwa BoT itaendelea kuboresha mifumo ya malipo ya hundi, kielektroniki ili kuongeza ufanisi kwenye mifumo hiyo, kuongeza usalama, kuongeza njia mbalimbali za malipo ili kupunguza malipo kwa fedha taslimu na kuongeza kasi ya malipo yaweze kuwa ya wakati kwa wateja popote walipo ndani na nje ya nchi.

  Ili kuendana na wakati BoT kupitia Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa katika kuwahudumia wananchi katika masuala ya fedha na mabenki,imeanza kutumia mfumo wa TACH unaohusisha malipo ya hundi na malipo madogo ya kielektroniki (EFT) ambao umeanza kutumika tarehe 30 Aprili 2015 nchini.

  Mfumo wa TACH unatumika na mabenki kutuma na kupokea hundi za wateja wao ikiwemo kulipa malipo madogo madogo yaliyojumishwa pamoja, mishahara, pension na hata malipo ya mtu mmoja mmoja.Kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa TACH nchini, awali hundi zilikua  na muda tofauti wa siku za kuhakiki  kulingana na kanda hali iliyopelekea muda wa siku za kuhakiki  za hundi ulikua ni siku 3, 7 na 14 kutegemeana na kanda.

  Baada ya kuanzishwa mfumo wa TACH hali imekuwa tofauti ambapo kwa mfumo  huo sasa, hundi zote za Tanzania popote zitakapowasilishwa zitakuwa zinafanyiwa kazi ndani ya siku moja ya kuzihakiki hundi  hizo (T+1) mpaka hapo itakapolipwa.Hatua hiyo imewapunguzia muda wateja ili waweze watapata hela zao mapema na hivyo kuzitumia kwenye shughuli zao za kiuchumi.

  Aidha, Bw. Dadi aliongeza kuwa nchi washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zenyewe zinatumia unaojulikana kama EAPS ikiwa ni jitihada za kuunda umoja  wa kiuchumi miongoni mwa nchi hizo.Mfumo huo wa malipo umeunganisha mifumo ya malipo (RTGS) ya nchi washiriki wa Afrika Mashariki ili kurahisisha malipo kati ya nchi washirika.

  Kwa maana hiyo mabenki ya kibiashara ya nchi husika zina uwezo wa kutumiana na kupokea pesa za wateja wao kwa kutumia sarafu za nchi wanachama kufanya muamala.
  Hadi sasa, mfumo huo umeunganishwa kwa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, wakati Burundi na Sudan ya Kusini wako mbioni kujiunga. 

  0 0

  Bango Sangho
  Mwenyekiti wa Umoja wa Jamii ya watu kutoka India, Bengali waliopo Tanzania (Bango Sangho), Kunal Banerjee akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inayotayotaraji kufanyika katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mmoja wa madaktari watakaoendesha zoezi la upimaji afya kwa watoto hao Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki ya Al Hilal ya jijini Dar es Salaam.

  Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) unataraji kutoa huduma ya upimaji wa afya bure kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano, upimaji utakaofanyika Jumapili ya Machi, 13 katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam.

  Akizungumzia huduma hiyo, Mwenyekiti wa Bango Sangho, Kunal Banerjee amesema huduma hiyo itawawezesha wazazi kutambua magonjwa yanayowakabili watoto wao bila kulipa malipo yoyote kwa kutambua umuhimu wa afya ya watoto kwa maendeleo ya taifa.Alisema kupitia huduma hiyo madaktari watawapima watoto walio na umri chini ya miaka mitano afya ya kinywa, uzito, ukaguzi na ushauri wa lishe hivyo kuwataka wazazi kuwapeleka watoto wao ili waweze kupata huduma bure.
  Ali Mzige
  Mmoja wa madaktari watakaoendesha zoezi la upimaji afya kwa watoto hao Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki ya Al Hilal ya jijini Dar es Salaam akifafanua jambo kuhusiana na umuhimu wa kupima afya za watoto katika mkutano na waandishi wa habari.“Tunataka kusaidia marafiki zetu wa Tanzania na katika kuendelea hilo tutatoa huduma ya bure kwa watoto kupima afya zao na tunataka wazazi wawalete watoto ili wapime afya,” alisema Banerjee.

  Nae Dkt. Ali Mzige kutoka Kliniki Al Hilal alisema Bango Sangho kimekuwa chama ambacho kikisaidia jamii ya Tanzania katika sekta ya afya na wamekuwa wakitoa huduma ya kupima watoto bure walio na umri chini ya miaka mitano kwa mwaka wa tatu mfululizo.

  Alisema ripoti ya afya Tanzania inaonyesha kuwa kuna watoto 81 wamekuwa wakipoteza maisha kati ya watoto 1,000 walio na umri chini ya miaka mitano kutokana na sababu mbalimbali ambapo wamekuwa hawapati huduma na kupitia huduma hiyo ya kuwapima bure watoto walio na magonjwa wataweza kutambulika.

  “Tutafanya huduma ya kupima bure watoto walio chini ya miaka mitano na tutakaobaini wanamatatizo maalum ya kiafya tutawapa rufaa ili wakapate huduma ya matibabu,” alisema Dkt. Mzige.

  Huduma hiyo ya kupima watoto walio na umri chini ya miaka mitano ilifanyika pia mwaka jana na watoto 289 walipimwa afya zao huku baadhi walikutwa na matatizo ikiwemo maambukizi ya mfumo wa njia ya mkojo UTI, Utapiamlo, kukatwa vimeo na wengine wakionekana kuwa na afya duni.
  Husna Abdallah
  Mtaalamu wa afya ya uzazi kutoka Kliniki ya Al Hilal, Bi. Husna Abdallah akitoa msisitizo kwa akina mama kuzingatia kanuni za afya ya uzazi wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
  Zawadi Chogongwe


  Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Zawadi Chogongwe (kulia) akiuliza swali kwa wataalamu wa afya wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inayotayotaraji kufanyika katika Shule ya Msingi Kibugumu iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York
  Jumuiya  ya Kimataifa  imezitaka pande zinazopinga  Nchi  Burundi, kumpatia ushirikiano wa  kutosha ,Rais  Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ameteuliwa na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuratibu   majadiliano ya kutafuta  ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa   unaoendelea nchi humo.
  Pamoja na  pande zinazopingana kutakiwa kufanya hivyo kwa moyo mmoja,  pia     Taasisi za Kimataifa na Kikanda  ukiwamo Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, pamoja na wadau wengine wametakiwa pia kumuunga mkono na kutoa ushirikiano kwa Rais Mstaafu  Benjamin Mkapa.
  Wito huo umetolewa siku ya Jumatano, hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  wakati  Wajumbe wa    Burundi Configuration walipokutana katika kikao chao  na kujadili hali ya kisiasa na kiusalama inavyoendelea nchi Burundi kufuatia ziara  iliyofanywa na  Mwakilisji wa Kidumu wa……  Balozi Jurg Lauber ambaye ni   Mwenyekiti wa   Burundi  Configuration.
  “Tunakaribia  uteuzi wa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa kuwa  mratibu wa mazungumzo  ya  kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi. Tunatoa wito kwa pande zinazopingana nchi  humo, serikali na  vyama vya kiasa kumpatia ushirikiano bila ya mashari yoyote” akasema Mwakilishi wa Marekani.
  Naye Mwakilishi  wa Kudumu wa  Ubeligiji, Balozi Benedicte Frankinet. Pamoja na kueleza kwamba   ujumbe wake   unawasiwasi kuhusu  taarifa za kuendelea kwa matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu na mbinyo kwa vyombo vya habari na uhuru wa watu  kutembea.
  Amesema .“ Rais Mstaafu wa Tanzania , Benjamin Mkapa, anauzoefu mkubwa na wa hali ya juu katika   uratibu na  utafutaji ufumbuzi wa  migogoro ya kisiasa, ujumbe wangu unakaribisha uteuzi wake, hapana shaka ataratibu  na kusimamia  majadiliano jumuishi  yatakayohusisha wadau wote wanaopingana  nchini Burundi wakiwamo pia wajumbe wa asasi zisizo za kiserikali”.
  Kwa upande wake, Mwakilishi wa  Kudumu wa  Netherland,  Balozi Karel Van Oosterom,  amesema ujumbe wake pia  unakaribisha uteuzi wa  Rais Mkapa, na kwamba pande zinazopinga nchini Burundi zinatakiwa kuitumia  fursa ya  uteuzi wa Mkapa kurejea katika  meza  ya majadiliano  ambayo  yatakuwa  jumuishi na  huku akizisihi pande hizo kutotoa masharti ya aina yoyote ile.
  Naye   Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda,  pamoja na  kukaribisha  uteuzi wa Rais Mstaafu Mkapa ambaye amesema ana uzoefu mkubwa na wanaimani naye,  alimshukuru pia, Rais  John Pombe  Magufuli  kwa  kumteua Mkapa.
  Karibu wajumbe wote waliochangia majadiliano kuhusu  hali ya  Burundi walikaribisha na kupongeza uteuzi wa Mkapa  huku, Mjumbe wa Nigeria pamoja  naye kuunga mkono uteuzi wa Mkapa.  Alisisitiza pia kwamba Majadiliano jumuishi ya kutafuta ufumbuzi wa  kudumu nchini  Burundi  yanapashwa kumilikiwa na Warundi wenyewe.
  Akatahadharisha kwa kusema kwamba,   mashinikizo kutoka nje ya Burundi  hayana nafasi  katika  mchakato huo na kwamba hali  hiyo ikiruhusiwa inaweza  siyo tu kuathiri majadiliano hayo lakini pia  itakuwa ni kuwaingilia wananchi wa Burundi.
  Mwakilishi wa  Kudumu wa Tanzania,  Balozi Tuvako Manongi akichangia  majadiliano hayo, yeye ametaka ushughulikiaji wa  hali tete ya kisiasa na kiusalama uende sambamba na  uondoajji wa vikwazo  vya kiuchumi   kwa Serikali ya Burundi.
  “  Hakuna  matinki ya kutia msisitizo wa  kuitaka serikali ya  Burundi kutekeleza mambo kadha wa kadhaa yakiwamo ya  ukiukwaji wa haki za binadamu, pasi kuzungumzia hali  mbaya  ya uchumi na kijamii  inayoikabili Burundi na watu  wake. Akasema Balozi
  Nakusisitiza . “Tunapojadili hali ya  usalama tujadili  basi na uondoaji wa  vikwazo vya  kiuchumi kwa sababu mambo haya yanakwenda kwa  pamoja.  Njia sahihi ya kusaidia mchakato  wa  kutafuta amani ya  kudumu nchini Burundi ni kwa   sisi sote   tulio katika meza hii  kufanya kazi  kwa  pamoja  na  katika  namna  inayoeleweka”.
  Vile vile Balozi Manongi ambaye Tanzania ni  mjumbe wa Burundi Configuration ambayo ni sehemu ya Kamisheni ya Ujenzi wa Amani ( Peace Building Commission)  amesisisiza  wananchi wa Burundi kumiliki   mchakato wa majadiliano kuhusu mustakabali wa nchi yao.
  Hoja ya  kuondolewa kwa vikwazo vya  kiuchumi, Warundi kumiliki majadiliano yao, pia  imeungwa mkono  na  mjumbe wa China ambaye  amesema Haki za binadamu  zinahusu pia haki ya kupata maendeleo na kwamba Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kuisadia Burundi kiuchumi ili wananchi wapate  maendeleo ambayo ni haki yao.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya Maafa Zanzibar ndugu Ali Juma Hamad akifungua mafunzo ya waandishi wa habari juu ya kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu katika Ukumbi wa gereji ya Wizara ya Afya Mombasa Mjini Zanzibar, (kulia) daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt Fadhili Mohd na (kushoto) Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza kwa makini Daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt. Fadhili Mohamed alipokuwa akielezea njia za kukabiliana na kipindupindu katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika Ukumbi wa Gereji ya Wizara ya Afya Mombasa Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Rafii Haji Mkame akiwasilisha mada ya wajibu wa waandishi wa habari katika kukabiliana na maradhi ya miripuko katika mafunzo yaliyofanyika Ukumbi wa Gereji ya Wizara ya Afya Mombasa Mjini Zanzibar.
  Katibu wa Jumuiya ya Maafisa wa Afya Zanzibar Ahmed Suleiman Said akitoa elimu ya kupambana na maradhi ya kipindupindu kwa wananchi wa shehia ya Shaurimoyo Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  Baadhi ya wananchi wa shehia ya Shaurimoyo Mjini Zanzibar wakifuatilia juu ya elimu ya ugonjwa wa Kipindupindu iliyotolewa na Jumuiya ya Maafisa wa Afya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  Mwashungi Tahir – Maelezo Zanzibar.

  Daktari dhamana kanda ya Unguja Dkt. Fadhil Mohammed Abdallah amewataka wananchi kuchukua tahadhari kuhusu maradhi ya kipindupindu ambayo kwa sasa ni tishio kubwa Zanzibar.

  Hayo ameyasema katika Ukumbi wa Gereji ya Wizara ya Afya Mombasa kwenye mafunzo ya waandishi wa habari juu ya kujikinga na ugonjwa huo ambao bado unaendelea katika sehemu mbali mbali Zanzibar.

  Amesisitiza kuchukuliwa tahadhari zaidi kupambana na maradhi ya kipindu pindu ikiwemo kuweka mazingira safi, kufuata masharti ya afya, kuchemsha maji ya kunywa ama kutumia maji yaliyotiwa dawa ya kuulia bektiria wanaosababisha maradhi hayo..

  Dkt. Fadhil amewataka wananchi kuacha tabia ya kula ovyo njiani, kukosha matunda na mboga mboga kabla ya kula na kuchukua tahadhari kubwa wakati wa kumshughulikia maiti ya maradhi ya kipindu pindu kwani ni miongoni mwa njia za maambukizi ya maradhi hayo.

  Amewataka waandishi wa habari kutekeleza majuku yao ya kutoa elimu kwa wananchi ili wapate uelewa mkubwa zaidi kukabiliana na maradhi hayo.

  Amesema maradhi ya kipindu pindu ingawa ni tishio kwa maisha ya wananchi lakini ni rahisi zaidi kuyadhibiti kuliko maradhi mengine iwapo wananchi watafuata masharti ya afya.

  “Waandishi wa habari mnao mchango mkubwa wa kutoa elimu kwa jamii katika kukabiliana na maradhi ya kipindupindu hivyo tunategemea mashirikiano makubwa kutoka kwenu,” alisisitiza Dkt. Fadhili

  Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya Maafa Zanzibar ndugu Ali Juma Hamad amesema juhudi za pamoja zinahitajika katika kukabiliana na kipindupindu na mchango wa kila mtu na taasisi unahitajika.

  Amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika kukabiliana na maradhi hayo tokea yalipogundulika mwezi Septemba mwaka jana ikiwa ni kipindi cha jua kali, kuchukua muda mrefu na kusambaa sehemu mbali mbali za Unguja na Pemba kinyume na watu walivyozoea vipindi vya nyuma.

  Akiwasilisha mada ya majukumu ya vyombo vya Habari katika kudhibiti miripuko ya maradhi ya kuambukiza, Mkurugenzi wa Idara y Habari Maelezo Zanzibar Rafii Haji Makame amesema vyombo hiyo vinajukumu la lazima katika kusaidia umma kudhibiti vifo na athari nyengine za kiuchumi na kijamii zinazosababishwa na miripuko ya maradhi .

  Katika kufanikisha majukumu hayo Mkurugenzi Rafii ametaka kuongezwa ushirikiano kati ya vyombo vya habari na sekta ya afya ili kupata taarifa sahihi kwa wakati katika kufikisha ujumbe kwa umma.

  Aidha amesema utoaji wa elimu ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza kupitia vyombo vya habari liwe suala endelevu ili jamii iweze kupata uwelewa na kubadilika kitabia.

  Jumla ya kambi 18 zilifunguliwa na kuhudumia wagonjwa 1066 Unguja na Pemba na kati yao wagonjwa 22 walifariki. Hivi sasa kuna kambi nne tu zinazoendelea kupokea wagonjwa katika kisiwa cha Unguja.

  Wakati huo huo Katibu wa Jumuiya ya maafisa wa afya Zanzibar Ahmed Suleiman Saidi amewashauri wananchi wa shehia ya Shaurimoyo kubadili tabia na kuweka mazingira wanayoishi katika hali ya usafi ili kujikinga na kipindupindu.

  Alitoa ushauri huo alipokuwa akizungumza na wananchi wa shehia hiyo katika skuli ya Shaurimoyo walipowatembelea kutoa taaluma juu yamaradhi hayo kwa vile shehia hiyo ni miongozi kati ya shehia zilizoathirika na kipindupindu.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akipofika kwa mazungumzo na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wake (kushoto) wakiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Rais wa Vietnam Truong Tan Sang jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akiwa nchini kwa ziara ya Kikazi
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akifuatana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(katikati) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(kulia) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Augustin Mahiga.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akiagana na mgeni wake Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(katikati) mawair mbali mbali wa Vietnum walioungana na Rais Truong


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali toka Tanzania na Vietnam kwenye halfa ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang akizungumza na viongozi mbalimbali toka Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akigonga glass na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang ikiwa ni ishara ya ushirikiano kati ya Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   ais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang akigonga glass na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang (Kulia) akiwa amenyanyua glass juu pamoja na  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa ikiwa ni ishara ya kutakia heri kati ya Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang wakitoa heshima kwa nyimbo za mataifa hayo mawili.
   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Generali Aldof Davis Mwamunyange (Wa pili kulia) akifatilia hotuba za Rais wa Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspecta Generali Ernest Mangu, wa pili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali  Casmir Minja, katikati ni Mkuu wa Usalama Rashid Othman na kushoto ni Kamanda wa Kanda maaalum Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro.
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (katikati) akifatilia halfa ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kushoto ni Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la wananchi la Tanzania Luteni Generali Abdulrahman Shimbo.Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Waajiri (ATE), Zuhura Muro akizungumza katika hafla ya Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam juzi. Hafla hiyo iliandaliwa na ATE kwa ushirikiano na kampuni ya Kazi Services Ltd jijini Dar es Salaam.
  Mratibu wa Mradi wa Program ya Mwanamke wa Wakati Ujao  ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Lilian Machera (kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Masako na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Neema Rose Singo katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na ATE kwa ushirikiano na kampuni ya Kazi Services Ltd jijini Dar es Salaam juzi. 
   Mratibu wa miradi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Joyce Nangai (wa pili kushoto), akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Joyce Mhaville katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na ATE kwa ushirikiano na kampuni ya Kazi Services Ltd jijini Dar es Salaam juzi.
   Mratibu wa Mradi wa Program ya Mwanamke wa Wakati Ujao  ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Lilian Machera (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Masako na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Neema Rose Singo katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoandaliwa na ATE kwa ushirikiano na kampuni ya Kazi Services Ltd jijini Dar es Salaam juzi.

   Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
    Baadhi ya watumishi wa ATE wakipozi kwa picha katika hafla hiyo.  0 0

  Rais John Magufuli akiteta na Rais Mstaafu Ali Hasan Mwinyi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika chakula cha jioni alichomwandalia Rais wa Vietinam, Truong Tang Sang, Ikulu jijini Dar es salaam Machi 9,2016. 
  Rais John Magufuli akizungumza na Marais Wstaafu Ali Hasan Mwinyi na Jakaya Kikwete Waziri Mkuu katika chakula cha jioni alichomwandalia Rais wa Vietinam, Truong Tang Sang, Ikulu jijini Dar es salaam Machi 9,2016. Kulia ni Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha UDP,John Cheyo chakula cha jioni ambacho Rais John Magufuli alimwandalia Rais wa Vietinam, Truong Tang Sang, Ikulu jijini Dar es salaam Machi 9,2016. Kulia ni Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Mkewa Rais Mama Janeth Magufuli alimwongoza Mke wa Rais wa Vietinam, Mai Ti Hahn (kushoto) kwenda kwenye chakula cha jioni alichoandaa Rais John Magufuli ikulu jijini Dar es salaam Machi 9, 2016 kwa heshima ya Rais wa Vietinam, Truong Tang Sang. Wapili kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa na kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mkewe Salma wakiingia kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam kushiriki chakula cha jioni alichoandaa Rais John Magufuli ikulu jijini Dar es salaam Machi 9, 2016 kwa heshima ya Rais wa Vietinam, Truong Tang Sang. 
  Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi Celestine Mushy wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashari, Kikanda na Kimataifa katika chakula cha jioni alichoandaa Rais John Magufuli ikulu jijini Dar es salaam Machi 9, 2016 kwa heshima ya Rais wa Vietinam, Truong Tang Sang. 

  0 0
 • 03/10/16--02:15: BIDHAA FEKI


 • 0 0

  Siku ya Figo Duniani huadhimishwa duniani kote kila AlhamisI ya pili ya mwezi Machi tangu mwaka 2006. Mwaka huu itaadhimishwa leo tarehe 10/3/2016.

  Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Figo mwaka 2016 ni“Chukua Hatua Mapema Kuepuka Magonjwa ya Figo kwa Watoto”. Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha jamii juu ya matatizo ya figo yanayoikabili jamii yetu hususani watoto.

  Tanzania kama zilivyo nchi nyingine duniani inaadhimisha siku hii.Wizara Kwa kushirikiana na Chama cha Watalaam wa Magonjwa ya Figo Tanzania kutoa elimu ya kujikinga na madhara ya magonjwa ya figo kwa kuzingatia kanuni za afya na kupima mapema ili kutambua na kupata matibabu kwa wakati

  Magonjwa ya figo huathiri utendaji wa viungo hivi muhimu katika mwili wa binadamu, miongoni mwa kazi za figo mwilini ni kutengeneza kemikali inayochochea utengenezaji wa chembe nyekundu za damu, kusaidia upatikanaji wa madini yanayoimarisha mifupa, kusaidia upatikanaji wa vitamin D mwilini, kurekebisha shinikizo la damu na kuondoa maji, uchafu utokanao na utendaji wa mwili na sumu mwilini. Magonjwa ya figo huathiri watu mbalimbali katika jamii bila kujali umri, kuanzia watoto wachanga mpaka wazee.

  Magonjwa ya figo hutokana na sababu mbalimbali kulingana na umri wa waathirika. Magonjwa haya kwa watoto husababishwa na magonjwa mengine yakiwemo malaria, kichocho, homa ya manjano, kuhara, ugonjwa wa kisukari kwa watoto na maambukizi ya bakteria ya koo na ngozi. 

  Pia yapo magonjwa yanayotokana na matatizo ya mfumo wa mkojo ambayo watoto huzaliwa nayo. Zipo sumu na dawa za mbalimbali zinazoathiri figo ikiwa ni pamoja na dawa za maumivu kama diclofenac hasa zinapotumika kiholela. Matumizi ya mitishamba yameripotiwa kuathiri utendaji wa figo.

  Kwa watu wazima chanzo kikubwa cha magonjwa ya figo ni ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu. Pia utumiaji wa dawa, mitishamba na magonjwa ya kuambukiza kama ilivyo kwa watoto yanaweza kuathiri figo kwa watu wazima. Yapo pia magonjwa mengi ambayo huathiri figo moja kwa moja mfano mawe ya figo na njia ya mkojo.

  Tafiti za ugonjwa wa figo zinaonyesha kuwa kati ya mwezi Agosti 2014 na Februari 2015 kati ya watoto 513 waliopimwa magonjwa ya figo katika Hospitali za Bugando na Sekou Toure asilimia 16.2% walikuwa na matatizo ya figo. Katika utafiti huo ilionekana watoto waliokuwa na magonjwa ya figo walikuwa na malaria, ugonjwa wa seli mundu (sickle cell anaemia) maambukizi ya bakteria kwenye koo na ngozi na kutumia mitishamba kabla ya kufika Hospitali. Utafiti huu unaonyesha wazi uwepo wa matatizo ya figo kwa watoto.

  Utafiti mwingine uliofanyika Mkoani Kilimanjaro kati ya mwezi Januari na Juni 2014, uliohusisha watu 481 kutoka katika kaya 146, asilimia 7% walionekana kuwa na matatizo ya figo. Utafiti huu ulionyesha uhusiano wa karibu kati ya uwepo wa tatizo la figo na ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu na matumizi ya mitishamba.

  Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya figo duniani kwa mwaka 2016, inalenga kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu kinga dhidi ya ugonjwa wa figo kwa watoto. Jamii inawahamasishwa kuchukua hatua kuwahi Hospitali pale tunapohisi mtoto anaweza kuwa na ugonjwa unaoweza kusababisha matatizo ya figo. Pia ni muhimu kwa wananchi wote kuchukua hatua ya kupima ili kujua kama wana matatizo ya figo. Pia ni muhimu kwa wananchi wote kuchukua hatua ya kupima ili kujua kama wana matatizo ya figo hasa wale wenye matatizo yanayosababisha matatizo ya figo hususani kisukari na shinikizo la damu. Wizara inatoa wito kwa watoa huduma za afya kuhakikisha wanawapima matatizo ya figo mara kwa mara wale wote wanaosumbuliwa na magonjwa yanayoathiri figo yakiwemo kisukari na shinikizo la damu.

  Pamoja na magonjwa yaliyoripotiwa kusababisha matatizo ya figo, yapo mambo yanayochochea uwezekano wa kupata magonjwa ya figo yakiwemo ulaji usiofaa hasa matumizi ya chumvi kwa wingi, mafuta na sukari, uzito uliozidi, unene uliokithiri, kutofanya mazoezi, uvutaji wa sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku, unywaji pombe kupita kiasi na msongo wa mawazo.

  Ili kuzuia magonjwa ya figo na maradhi mengine yasiyo ya kuambukiza ni muhimu kufuata kanuni za afya ambazo ni ulaji bora, na mtindo bora wa maisha ambao ukifuatwa vyema huweza kwa kiasi kikubwa kuzuia mtu kupata magonjwa yanayosababisha matatizo ya figo, na kwa wagonjwa ambao wana magonjwa yanayoathiri figo kama kisukari na shinikizo la damu ni vizuri wakazingatia ushauri wa wataalamu ama kutumia dawa kama wanavyoelekezwa ili kuzuia uwezekano wa kupata matatizo ya figo.

  Serikali inaendelea na utekelezaji wa Sera ya Afya (2007) ambayo inalenga kutoa huduma kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo matatizo ya figo. Aidha, Serikali, Sekta Binafsi, Mashirika ya Kimataifa na Taasisi zinazotoa huduma bila faida zinaendelea kuandaa na kurekebisha Sheria, Kanuni na Taratibu zinazoimarisha uzuiaji na udhibiti wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kutumia maadhimisho haya kuwa sehemu ya uhamasishaji kwa jamii kama ilivyo kwenye nchi zote duniani. 

  Serikali inaendelea kuandaa miongozo na mikakati ya kisera kwa kushirikisha jamii katika kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza, ikiwemo magonjwa ya figo, kisukari na shinikizo la damu. Serikali imeimarisha ushiriki wa wadau mbalimbali na inaendelea kuhimiza Taasisi za Umma na za Binafsi kuweka mkazo ili kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

  Kwa kutambua gharama za kutibu ugonjwa wa figo, Serikali imekuwa ikigharimia matibabu ya wagonjwa wenye matatizo ya figo ikiwemo upandikizaji wa figo kwa wale wagonjwa ambao figo zao zimeshindwa kufanya kazi kabisa. Pia Serikali imejitahidi kusogeza huduma za figo kwa wananchi kwa kuanzisha huduma za figo kwa Hospitali za Rufaa baada ya kupeleka wataalamu wa magonjwa ya figo.

   Hospitali zenye wataalamu wa magonjwa ya figo ni Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya KCMC, Hospitali ya Rufaa Mbeya, Hospitali ya Bugando na Hospitali ya Benjamin William Mkapa iliyopo Dodoma. Mpaka sasa wagonjwa 190 wakiwemo watoto wawili wamepata huduma ya kupandikizwa figo na wanapata huduma katika kitengo cha figo Muhimbili na katika Hospitali nyingine za rufaa.

  Pia Serikali imeweka mkakati wa kuhakikisha huduma za upandikizaji wa figo zinapatikana hapa nchini haraka iwezekanavyo ili kupunguza gharama za kupelekwa wagonjwa nje ya nchi na kutoa huduma kwa watanzania wengi zaidi. Miongoni mwa mikakati iliyopo ni kuimarisha huduma za figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kupelekwa wataalamu nje ya nchi kwa mafunzo ili kufanikisha upatikanaji wa hizo huduma hapa Tanzania.

  Tanzania inaungana na Mataifa mengine duniani kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 2011 la kuwa na mpango kabambe wa kuthibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Lengo ni kuhakikisha Mataifa yote duniani yanapunguza magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025. Ili kufikia lengo hili ni muhimu kushirikisha wadau wengi zaidi na kufanya kazi kwa ushirikiano.

  Wengi wetu wanaweza kuwa na matatizo ya figo bila kujitambua hasa wale wenye magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu. Magonjwa ya figo yanaweza kuwa na dalili kadhaa zikiwemo kuvimba mwili kunakoanzia usoni, kupungua au kukosa mkojo kabisa, kukojoa mkojo wenye damu au rangi ya kahawia, kuwa na shinikizo la damu, kuchoka mwili na kupungukiwa na damu. 

  Dalili hizi hujitokeza baada ya figo kupata athari kubwa, hivyo inawezekana kabisa mtu kuwa na tatizo la figo bila kuwa na dalili. Mara unapoona una dalili nilizozitaja hapo juu ni vizuri ukaenda Hospitali ili upimwe na wataalamu na kupata matibabu au ushauri.

  Matatizo ya figo yakigundulika mapema inawezekana kupata matibabu ambayo yatazuia uharibifu wa figo na kumuwezesha mgonjwa kuishi bila kuhitaji matibabu makubwa ambayo ni ya gharama kubwa ikiwemo kupandikizwa figo.

  Hivyo Wizara inatoa wito kwa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa anapima afya yake kwa kuwa ugonjwa huu unaweza usionyeshe dalili yoyote mapema. Ni vyema kila mmoja akapima afya yake mara kwa mara ili kutambua hali yake ya afya. Endapo mtu atatambuliwa kuwa ana ugonjwa wa figo anashauriwa kutumia huduma za afya kulingana na ushauri atakaopewa na wataalam wa afya.

  Kwa wale ambao wameshajitambua kuwa na matatizo ya figo, kisukari na shinikizo la damu lakini hawatumii huduma za afya ipasavyo, wanaaswa kutumia huduma za afya zilizopo kwa manufaa ya afya zao na kuepusha athari zinazotokana na magonjwa hayo.

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

  10 Machi, 2016

  0 0


   Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Jordan Rugimbana akisoma hotuba ya ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Ushauri mkoa.
   Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri mkoa wa Lindi.
   Wajumbe wa Kikao cha Ushauri cha mkoa wa Lindi.
   Mbunge wa Jimbo la Lindi mjini Mhe. Hassan Kaunje akichangia maoni yake kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri  ya mkoa wa Lindi.
  Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Meneja Mahusiano wa Benki ya CBA, Caroline Makatu  akikabidhi msaada wa vitanda na mashine kumsaidia mtoto anayezaliwa kabla ya muda katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
  Watatu kutoka kulia ni Doris Mollel akiwa katika picha ya pamoja wadau waliofanikisha msaada huo katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  TAASISI ya Doris Mollel Foundation (DMF) kwa kushirikiana na Benki ya  CBA wametoa msaada vitanda viwili na mashine tatu za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati vyenye wa vitu vyenye thamani ya Sh.milioni  mbili  katika Hospitali ya  Rufaa ya Mwananyamala  jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam  Mkurugenzi wa DMF,  Doris Mollel, alisema  kwa kutambua umuhimu kwa sababu wanawakumbuka  wanawake wanaojifungua kabla ya wakati na kutoa msaada huo ni kutaka  kuokoa uhai wa watoto hao .

  “Kutambua thamani ya watoto njiti tumeona katika kuokoa uhai na kuweza kufikia malengo tumeona ..mashine za kuwasaidia kufikia malengo yao kama walivyo watoto wengine…taasisi itaendelea kutoa mchango kwa jamii,” alisema Doris.

  Naye Meneja Mahusiano wa Benki ya CBA ,Caroline Makatu amesema  kuna changamoto nyingi  hospitali ikiwemo na uhaba wa vifaa kwa kutambua hilo wametoa msaada huo  ili kusaidia mama na mtoto.

  Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Delilah Moshi amesema wanashukuru kwa msaada huo uliotolewa na taasisi hizo kwa kutambua uwepo wa wanawake na kuziwezesha hospitali.

  Amesema kwa sasa shida kubwa iliyopo kwa sasa ni uhaba wa majengo kutokana na nafasi chache za kuhifadhia watoto njiti kwa sababu idadi ya watoto inaongezeka.

  “Kutokana na kuwapo kwa mashine za kuhifadhia watoto njiti idadi ya vifo vya watoto hao imepungua hivyo naiomba serikali kuongeza madaktari wa watoto kwani hadi sasa wapo wawili tu,” amesema Mushi.

  0 0

   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura (kushoto) akipokea Kamusi kuu ya Kiswahili kutoka kwa Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Dr. Selemani Sewange alipotembelea ofisi za BAKITA kufahamu mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam.

   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura (kushoto) akikabidhiwa kitabu kiitwacho Furahia Kiswahili kilichoandaliwa na BAKITA alipotembelea ofisi za BAKITA kufahamu mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam. Anayemkabidhi ni Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Dr. Seleman Sewange

   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura akipitia Kamusi kuu ya Kiswahili aliyopewa baada ya kutembelea ofisi za BAKITA kufahamu mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam.

   Mtaalamu kutoka Idara ya Istilahi na Kamusi Taasisi ya BAKITA Bw. Mayolwa John (kushoto) akimwelezea Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura (kulia) kazi zinazofanywa na Idara hiyo alipotembelea ofisi za BAKITA kufahamu mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Dr. Selemani Sewange

   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura (wapili kushoto) akiangalia mfumo wa mradi wa kukuza kiswahili katika kompyuta ulioandaliwa na BAKITA alipotembelea Taasisi hiyo kufahamu mambo mbalimbali wanayoyafanya jana jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa Dr. Selemani Sewange na kushoto ni Afisa Utamaduni Bw. Christopher Mhongole.

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura (wapili kulia) akiongea na wataalamu wa Lugha na Fasihi kutoka Taasisi ya BAKITA alipotembelea Taasisi hiyo kufahamu mambo mbalimbali wanayoyafanya jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Dr. Seleman Sewange


  Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura akizungumza na Katibu Mtendaji BAKITA (hayupo pichani) alipotembelea ofisi za Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) kufahamu mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam.  

   Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA) Dr. Selemani Sewange (katikati) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Anastazia James Wambura (kushoto) alipotembelea ofisi za BAKITA kufahamu mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni maafisa Utamaduni kutoka Wizara hiyo.

  0 0  0 0

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amekutana na baadhi ya Madaktari waliohitimu mafunzo kwa vitendo kipindi cha 2014/2015 waliofika katika Wizara hiyo kwa lengo la kujua hatima na mustakabali wa mambo mbalimbali ikiwemo suala la ajira.

  Madaktari hao walioweza kuonana na Dk. Kigwangalla ni baadhi tu ya wawakilishi wa Madaktari wengine ambapo kupitia viongozi wao wamebainisha kuwa, kuwa kama wazarendo wapo tayari kuisaidia Serikali katika suala la tiba nchini hasa kwendana na hali ya kauli mbiu ya hapa kazi hivyo kupitia mazungumzo yao hayo na Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla na jopo la viongozi wa Wizara hiyo, madai yao na masuala mengine wana Imani kubwa madai yao yatashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi.
  kigwangalla ioNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akifuatilia mkutano huo uliowakutanisha Madaktari waliohitimu mafunzo kwa vitendo 2014/2015 (waliokaa upande wa kushoto). Wengine waliokaa upande wa kulia ni viongozi watendaji wa ngazi za juu wa Wizara hiyo wakifuatilia mkutano huo. Madaktari hao walifanya mkutano huo kwa lengo la kutaka kufahamu masuala mbalimbali ikiwemo suala la ajira.
  Kigwangalla34Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi hao juu ya mipango ya Wizara hiyo na namna ilivyojipanga ikiwemo kushughulikia suala lao hilo ambalo ni la kiutawala zaidi.
  kigwangalla99Viongozi wa Wizara ya Afya wakiwemo Makatibu wakuu na wakuu wa vitengo wakifuatilia mkutano huo kwa makini
  kigwangalla qBaadhi ya Madaktari waliohitimu mafunzo kwa vitendo wa mwaka wa 2014/2015 wakitoa maoni yao pamoja na mambo mbalimbali waliyoyawakilisha kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla pamoja na viongozi wa kutoka Wizara hiyo (Hawapo pichani).
  kigwangalla cvBaadhi ya Madaktari hao waliohitimu mafunzo kwa vitendo mwaka 2014/15

  kigwangalla 87Mkutano huo ukiendelea..
  kigwaNaibu Waziri Afya, Dk. kigwangalla akipeana mkono na baadhi ya viongozi wa Madaktari hao waliohitimu mafunzo kwa vitendo 2014/15, mara baada ya mkutano wao huo.
  kiganngwalla4Hapa Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla aliombwa kupata picha ya 'selfie' ya ukumbusho na Madaktari hao waliohitimu mafunzo kwa vitendo 2014/15
  kigwangalla3"Selfie na Naibu Waziri": Baadhi ya Madaktari waliohitimu mafunzo kwa vitendo 2014/15 walipata wasaha wa kupiga picha ya kumbukumbu na Naibu Waziri. Naibu Waziri ambaye naye ni Daktari, Madakatri hao walifurahia nafasia hiyo kwani ni kumbukumbu muhimu sana kwao kama walivyodai wakati wa picha hiyo.
  kigwangalla 2Baadhi ya viongozi wa Madaktari waliohitimu mafunzo kwa vitendo mwaka 2014/15 wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Afya Dk. Kkigwangalla.
  Kigwangalla9Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Wizara hiyo pamoja na uongozi wa Baadhi ya Madaktari waliohitimu Mafunzo kwa vitendo wa mwaka 2014/15 pamoja wahitimu hao katika picha ya pamoja nje ya Wizara hiyo. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

  0 0

  MWIMBAJI na Msanii mahiri wa Filamu Tanzania, Jennifer Mgendi  amelipania Tamasha la Pasaka linalotarajia kuanza Machi 26-28 katika mikoa ya Geita, Mwanza na Kahama.

  Kwa mujibu wa Mgendi hivi sasa analisubiri kwa amu tamasha hilo ambalo lina malengo ya kusifu na kuabudu kupitia nyimbo mbalimbali za Injili sambamba na viongozi wa dini mbalimbali.

  Mgendi alisema analisubiri kwa hamu Tamasha la Pasaka ambalo litafanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambako hivi sasa waimbaji wengine pia wanaendelea na mazoezi kuelekea tamasha hilo.Mgendi alitumia fursa hiyo kuwaomba mashabiki wake wa mikoa hiyo hasa wa nyimbo za Injili na Filamu  kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ili kupokea baraka za bwana kupitia uimbaji.

  Aidha Mgendi alisema katika tamasha hilo aakuwa na albamu nyingine mpya inayokwenda kwa jina lka Nyuma ya Mlima  ambako alisisitiza kuwaomba mashabiki wa muziki wa Injili kujitokeza kuipata albamu hiyo.
  Anazitaja nyimbo zilizoko kwenye albamu hiyo ni pamoja na Nyuma ya Mlima, Naomba Uzima, Bwana ni Ebenezer, Nawashukuru adui na Nitafika lini Remix.

  0 0

    Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akimkaribisha Mkurugenzi wa Radio France Internationale(RFI) Bi.Cecile Megie ofisini kwake alipomtembelea kwa ajili ya kufahamiana na kuboresha mahusiano yaliyopo kwa miaka saba sasa.
   Ujumbe kutoka Radio France International (RFI) wakifurahia jambo wakati wa kikao na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(Hayupo pichani).

  Mkurugenzi wa Radio France Internationale (RFI) Bi.Cecile Megie(kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura kuhusu msaada ambao wameipa shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) ili kusaidia katika kufikisha matangazo yake mbali Zaidi.
   Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Radio France Internationale(RFI) Bi.Cecile Megie ofisini kwake jijini Dar es salaam.

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(kulia) akimpa zawadi ya kahawa kutoka Tanzania Mkurugenzi wa Radio France Internationale(RFI) Bi.Cecile Megie(kushoto) baada ya mazungumzo mafupi ofisini kwa Naibu Waziri uyo kuhusu kuimarisha mahusiano baina ya nchi izi mbili katika masuala ya Habari kati ya TBC na RFI.

  0 0


   Balozi wa Korea nchini Tanzania Bw. Chung IL akibadilishana mawazo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria alipomtembelea leo (10/3/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.
   Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na Balozi wa Korea nchini Tanzania Bw. Chung IL alipomtembelea leo (10/3/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.
   


  0 0

  Kama Usipoona jina lako hapa, basi liko kwenye list ya October,2016 ambapo event hii itafanyika tena. 

  WAPI: Hyatt Regency,The Kilimanjaro Marquee
  MUDA: Saa Nane Mchana 
  MAVAZI: Business ( Jeans na T Shirt havitaruhusiwa)
  TIKETI: Kwenye Dawati la Kujiandikisha, Hyatt Regency,The Kilimanjaro
  Vyeti vitatolewa kwa washiriki wote.

  WAALIKWA KWENYE CELEBRITY CORPORATE CONFERENCE AND COCKTAIL, MARCH 2016                                                    WANAMUZIKI
  1.  Ali Kiba 
  2.     Fareed Kubanda 
  3.      Ben Pol 
  4.     Wakazi 
  5.     Sarah Kaisi (SHAA) 
  6.      Maua Sama
   7.      Lady JayDee 
  8.     Godzilla 
  9.     Joh Makini 
  10.   Feza Kessy 
  11.    Nikki wa Pili 
  12.     Nahreel 
  13.     Aika Navy Kenzo 
  14.       Juma Nature 
  15.        Dully Sykes 
  16.         Mrisho Mpoto 
  17.          Kayumba BSS 
  18.           Mayunga 
  19.            Linah Sanga 
  20.            Barnaba


   Bloggers  na Wanahabari
  61. Ahmed Michuzi
  62. Othman Michuzi
  63. Shamim Mwasha
  64. Krantz Mwantepele
  65. Sek David
  66. Khadija Kalili
  67. Joachim
  68. John Bukuku
  69. Bongo5 (1)
  70. Henry Mdimu
  71. Fred Njeje
  72. William Malecela
  73. Geofrey Pamoja
  74. Salim Shao
  75. Maimuna Kubegeya
  WAIGIZAJI 
  21. Vicent Kigosi
  22. JB
  23. Richie Richie
  24. Emmanuel Myamba
  25. Irene Paul
  26. Wema Sepetu
  27. Riyama
  28. Elizabeth Michael
  29.  Rose Ndauka

  Wachoraji/Wachongaji
  30.   Masoud Kipanya
  31 . Rams
  32 . Nafasi Art Space (1)
  33 . Cloud Chatanda
  34. Mwandale Mwanyekwa
  Wachekeshaji
  35. Dogo Pepe
  36. Joti
  37. Masanja
  38. Evan Bukuku
  39. MC Pilipili

  Wanamichezo
  40. Juma Kaseja
  41. Amisi Tambwe
  42. Danny Lyanga
  43. BBall Kitaa (1)
  44. John Bocco

  Wabunifu Mavazi
  45. Khadija Mwanamboka
  46. Ally Rehmtullah
  47. Zamda George
  48. Hameed Abdul
  49. Martin Kadinda
  50. The Speshoz
  51. Mtani Nyamakababi
  52. Kiki Zimba
  53. An Anisa
  54. Debora Dashki
  55. Bijoux Trendy
  Wanamitindo
  56. Maggie Vampire
  57. Lorraine Marriot
  58. Evans Athuman
  59. Lillian Kamazima
  60. Suma YM

  Watangazaji
  76. Dina Marios
  77. Barbara Hassan
  78. Seth
  79. Millard Ayo
  80. Perfect Crispin
  81. Hamis BDozen
  82. Rebecca Gyumi
  83.  Salama Jabeer
  84.  Hellen Kazimoto
  85. Mboni Masimba
  86. Fahad Fuad
  87. Zamaradi Mketema
  88. Betty Boniface
  89.Gea Habib
  90.  Zembwela
  91. Meena Ally
  92. Anna Peter
  93.  David Ramadhan
  94. Allan Lucky
  95.Sam Misago

  Urembo
  96. Rehema Samo
  97.  Manjano Dream Makers (5)  Wapiga Picha
  102.  Mx Carter
  103. Albert Manifester
  104. Akbar Thabeet
  105. Elle Emmanuel
  106. Maryam Lweno

  Special Invitations
  107.  Carol Ndosi
  108.  Jokate Mwegelo
  109.  Doris Mollel
  110. Idris Sultan
  111. Babu Tale
  112. Paul Makonda
  113. Issa Michuzi
  114. Maza Sinare
  115. Kelvin Twissa

  Celebrity Corporate Conference & Cocktail, March 2016 Inaletwa Kwako na Popular Links, Missie Popular, Heineken Tanzania, Coca Cola, Hyatt Regency, The Guardian, Nipashe, Jamii Media, NHC, Shear Illusions, COSOTA,BASATA, Ndovu Special Malt na Slide Visuals.

  Kwa maelezo zaidi, tutumie email kwa missiepopular@gmail.com au Facebook,Twitter na Instagram @MissiePopular 

  Kumbuka kuzingatia muda.

  xoxo
  Missie Popular
  0 0

  Na Avila Kakingo , Globu ya Jamii.
   KITABU cha HOW TANZANIA CAN MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  (Jinsi gani Tanzania kuweza kujikwamua na umasiki) kimezinduliwa jijini Dar es Salaam leo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi (akimwakilisha waziri mkuu Kassimu Majaliwa), Kitabu hicho kimetungwa na wahadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa hisani ya Ofisi ya waziri mkuu.

  akizungumza katika uzinduzi wa kitabu hicho Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi amesema kuwa
  kitabu hicho kicholenga kwenye mada  ya  "Tanzania Move from Poverty to Prosperity", hasa kwa kipindi hiki, ikizingatiwa kwamba Serikali ya awamu ya tano ipo katika vita ya kupambana na adui umaskini ili tuweze kufikia malengo ya millennia ya mwaka 2025. 

   "Chapisho hili la kitabu (How Can Tanzania Move from Poverty to Prosperity) limetolewa wakati sahihi kwa taifa letu Tanzaniani chapisho la aina yake toka Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam linaloonesha kiu ya wataalamu, wanataaluma na wale wanaotekeleza Sera  kutaka taifa letu lijikomboa kutoka kwenye dimbwi la umaskini na kufikia ustawi katika Nyanja za kiuchumi, kijamii, na kisiasa." Amesema Dkt. Possi.

  Kwa upande wa Mhadhir wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally amesema kuwa dhima ya kitabu cha (How Can Tanzania Move from Poverty to Prosperity) inalenga uchumi wa watu kwa watu wenyewe.

  Pia amesema kuwa kitabu hicho kimegusia suala la maliasili na umhimu wake kwenye mageuzi wa uchumi wa viwanda Tanzania, uvuvi, madini, misitu kilimo na nguvu kazi ya gharama nafuu pia kimetaja umhimu wa Diplomasia ya kiuchumi, mifumo ya kitaifa ya Sayansi na tecknologia, ubunifu usalama wa raia na mali zao. 
   
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi akizungumza katika uzinduzi wa kitabu cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  (Jinsi gani Tanzania kuweza kujikwamua na umasiki) kilichotungwa na wahadhili kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kitabu hicho kimezinduliwa katika ofisi za waziri mkuu jijini Dar es Salaam leo.
  Profesa Lasiun Sumbichako na mhariri Mkuu wa kitabu cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY (Jinsi gani Tanzania kuweza kujikwamua na umasiki) akizungumza katika uzinduzi wakitabu cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo katika ofisi ya waziri mkuu.
  Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Bashiru Ally  (Kushoto) akifafanua dhima nzima ya kitabu  cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  katika ofisi ya waziri mkuu jijini  Dar es Salaam leo.Katikati ni Mkuu wa Ndaki ya Sayansi ya jamii chuo kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Godius Kahyarara na kulia ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi wakiwa kwenye uzinduzi wa kitabu hicho.
  Mkuu wa Ndaki ya Sayansi ya jamii chuo kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Godius Kahyarara akifafanua jambo katika uzinduzi wa  kitabu  cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  katika ofisi ya waziri mkuu jijini  Dar es Salaam leo.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu  cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  katika ofisi ya waziri mkuu jijini  Dar es Salaam leo akiwa na wahadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi (katikati ) akionyesha kitabu kilichozinduliwa leo kitabu  cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY kitabu hicho kimezinduliwa katika ofisi ya waziri mkuu jijini  Dar es Salaam leo. Wengine ni wahadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam wakipiga makufi mara baada ya kuzindua kitabu hicho.

   Baadhi ya wahadhiri na waalikwa waliohudhulia katika uzinduzi wa kitabu kilichozinduliwa leo kitabu  cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  katika ofisi ya waziri mkuu jijini Dar es Salaam leo.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt. Abdallah Possi akiwa na baadhi ya wahadhiri, watunzi wa kitabu na waalikwa wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya uzinduzi wa kitabu  cha HOW CAN TANZANIA MOVE FROM POVERT TO PROSPERITY  katika ofisi ya waziri mkuu jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii. 

older | 1 | .... | 791 | 792 | (Page 793) | 794 | 795 | .... | 1898 | newer