Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 790 | 791 | (Page 792) | 793 | 794 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe wakiwapungia mkono viongozi mbalimbali waliokuja kumpokea mara alipowasili katika Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe wakishuka kutoka kwenye ndege mara walipowasili katika Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akimkaribisha Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (katikati) mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere akiongozana na mkewe 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuja kumpokea mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa 
  Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa tatu kulia) akiwasalimia baadhi ya Watanzania na Wavietnam waliokuja kumpokea mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. 
  Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akiangalia vikundi vya ngoma vikivyotumbuiza uwanjani mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. 
  Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang akiwapungia mkono wacheza ngoma na matarumbeta waliokuja kumpokea mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo)

  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki wakati wa kumpokea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 08 Maachi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda wakiteta jambo wakati wa kumpokea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 08 Maachi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Halotel wakiwa tayari kumpokea Rais wao wa Vietnam Mhe. Truong Tan Sang akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara yake ya siku tatu.

  Vikundi vya burudani ya matarumbeta na ngoma vikitumbuiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam wakati wa kumpokea Rais wa Vietnam aliyewasili nchini kwa ajili ya ziara ya siku tatu akiwa amefuatana na ujumbe wake.

  Ndege iliyombeba Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

  Ndege iliyombeba Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang ikiwa imewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Serikali ya Vietnam na Tanzania wakiwa tayari kumpokea Rais wao Mhe. Truong Tan Sang akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (wa pili kulia) akielekea kumpokea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Augustine Philip Mahiga. 

  0 0

  Mgeni Rasmi ,Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk .Ashatu Kijaji akitoa hotuba yake katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili iliyopita .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia.
  Mwenyekiti wa Tanzania Women of Achievement , Sadaka Gandi akiongea na washiriki wa kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili.Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia. 
  Rais wa Tanzania Women of Achievement Irene Kiwia akitoa hotuba ya ufunguzi katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili.Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia. 
  Waziri wa fedha mstaafu Mama Zakhia Meghji akichangia katika ya uwiano sawa katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili iliyopita .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) kukiwa na kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia 
  Mhadhiri kutoka Centre of Foreign Relations and International Affairs Prof.Ruth Meena akifafanua jambo wakati mjadala kuhusu uwiano sawa wa kijinsia katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili iliyopita .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) kukiwa na kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia. 
  Mmoja wa wazungumzaji wakuu Prof Slyvia Kaaya akichangia mada katika mjadala wa uwiano sawa wa kijinsia pembeni yake ni Bi Mary Rusimbi aliyekuwa mkurungezi mtendaji wa BOT ,na kulia kwake ni Mwenyekiti wa TAWLA Aisha Bade ,anayefuatia ni Mtendaji Mkuu wa WOMEN FUND TANZANIA Mary Rusimbi katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili iliyopita .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) kukiwa na kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia .
  Mwandishi wa habari Mkongwe Bi Edda Sanga akichnagia mada ya Usawa wa Kijinsia katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili iliyopita .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) kukiwa na kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia .

  Mwongoza Mada Modesta Mbughunia kifurahia jambo katika mjadala wa Uwiano sawa wa kijinsia uliofanyika katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili iliyopita .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia. 
  Mfanyabiashara na blogger Monica Joseph akichangia mada katika mjadala wa usawa wa kijinsia katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili iliyopita .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) kukiwa na kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia 
  MC Taji Liundi akiongoza utaratibu katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili iliyopita .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) kukiwa na kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia 
  Mwanafalsafa Dk Elie Waminian akitoa mada katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili iliyopita .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) kukiwa na kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia
  Mmoja wa wasichana waliopata usimamizi (Mentorship ) kutokaTaasisi ya TWA Dalini Kilemba akitoa ushuhuda kwa washiriki jinsi TWA walivyoweza kubadilisha maisha yake katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi yaliyofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili.Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia
  Mtendaji Mkuu wa WOMEN FUND TANZANIA Mary Rusimbi ambaye alikuwa mmoja wa wazungumzaji wakuu katika mazungumzo yaliyofanyika katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi akitoa neno la shukrami kwa washiriki .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsi 
  Mwanamzuki CHi akitumbuiza katika katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili iliyopita .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) kukiwa na kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia 
  Washiriki mbalimbali wa kongamano wakiweka saini zao katika ubao maalum katika namna ya kutoa ahadi ya Uwiano sahihi wa kijinsia katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili iliyopita .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) kukiwa na kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia .

  0 0

   Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali kifungua semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kuandika na kutoa habari za sekta za uchumi, biashara na fedha maendeleo yenye tija kwa taifa.
    Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Victoria Msina akimkaribisha Mkurugenzi wa BoT, Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali wakati wa ufunguzi wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika na kutoa habari za za uchumi, biashara na fedha maendeleo yenye tija kwa taifa.
   Baadhi ya washiriki wa semina wakimskiliza Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali wakati wa ufunguzi wa semina inayofanyika mjini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika na kutoa habari za za uchumi, biashara na fedha maendeleo yenye tija kwa taifa.
  Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa semina inayofanyika mjini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi hao kuandika na kutoa habari za za uchumi, biashara na fedha maendeleo yenye tija kwa taifa.


  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
  Wanahabari nchini wameaswa kutumia taaluma yao vema katika kuhabarisha umma kuhusu masuala ya uchumi, biashara na fedha kwa lugha ambayo wananchi wa ngazi mbalimbali wataweza kuelewa kirahisi ili waweze kuchangia katika maendeleo yenye tija kwa taifa.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali alipokuwa akifungua semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kuandika na kutoa habari za sekta ya uchumi na fedha.

  “Benki Kuu ya Tanzania inatambua na inathamini sana mchango mkubwa unaofanywa na magazeti, vituo vya televisheni na radio kwa kutenga nafasi maalum kwa ajili ya habari za fedha na uchumi na hasa zinatolewa na Benki Kuu” alisema Bw. Richard.

  Katika kuhakikisha vyombo vya habari vinatoa elimu katika masuala ya fedha na uchumi, Bw. Richard amesema kuwa BoT imechukua jukumu la kuwajengea uwezo wanahabari kila mwaka ili kuwaongezea uelewa wao kuhusu majukumu na kazi za Benki hiyo na mchango wake katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

  Malengo mengine ya semina hiyo ni kuchochea na kukuza ari ya wanahabari katika kuandika habari za uchumi  na fedha, kutafsiri   na kuchambua taarifa mbalimbali za uchumi na fedha zinazotolewa na taasisi mbalimbali, kuwafahamisha wanahabari   masuala yanayoendelea katika uchumi wa Tanzania na wa dunia, mwelekeo wa uchumi na masuala ya fedha katika siku zijazo na kuimarisha uhusiano mzuri wa kikazi uliopo baina ya vyombo vya habari,  wanahabari na Benki Kuu.

  Zaidi ya hayo, Bw. Richard ameongeza kuwa Benki Kuu kama taasisi, inajukumu la kujifunza namna vyombo vya habari vinavyofanya kazi na mahitaji yao katika kuandaa na kuwasilisha taarifa na habari za uchumi na fedha.

  Aidha, Bw. Richard amesema kuwa ukuaji wa uchumi nchini unaoendelea sasa unatokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali na BoT katika kutekeleza sera za uchumi na fedha pamoja na usimamizi wa uhakika wa sera hizo.

  “Kadiri uchumi unavyokua na kadiri mazingira ya biashara yanavyoendelea kuvutia wawekezaji, mahitaji ya taarifa na habari sahihi na kwa wakati kuhusu uchumi wa nchi yetu ikiwa ni pamoja na masoko ya fedha, uchumi wa kanda na dunia kwa ujumla yanaongezeka sambamba na umuhimu wake” alisisitiza Bw. Richard.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa semina hiyo kwa niaba ya wanahabari hao Ezekiel Kimwaga kutoka gazeti la Raia Mwema ameupongeza uongozi wa BoT kwa kufikisha miaka 50 na kuishukuru benki hiyo kuthamini na kutoa fursa ya semina hiyo kwa wanahabari kila mwaka ambayo inawaongezea uelewa katika masuala ya uchumi na fedha.

  Semina hiyo ya siku nne inajumuisha mada mbalimbali zinazowasilishwa na wataalam kutoka BoT ni pamoja na kuzijua kurugenzi ambazo zinazohusika na masuala ya uchumi, biashara na fedha ambazo ni Utafiti na Sera za Uchumi, Masoko ya Fedha, Usimamizi wa Mabenki, Bodi ya Bima na Amana, Mifumo ya Malipo ya Taifa na Huduma za Kibenki.

  Mada nyingine katka semina hiyo ni kuzijua alama za usalama zilizopo katika fedha, dawati la malalamiko ya wateja wa mabenki pamoja na kuzijua kazi za matawi ya Benki Kuu ya Tanzania.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akitoa Hotuba yake kwa wakazi wa Mtwara na Kuzindua Rasmi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2016 linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la  OXFAM Tanzania .
   Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh. Fatma Ally akizungumza na wakazi wa Mtwara,wageni mbalimbali na wadau pia kufungua rasmi sherehe hizo wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani na Uzinduzi wa Shindano la Mama wa Chakula kwa Mwaka 2016
   Meneja wa Programu ya Uwazi na Utawala Bora kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Bi. Betty Mlaki akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika Hilo Jane Foster wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani na uzinduzi rasmi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2016.

  Mamia ya wakazi wa Mtwara wakiwa katika Sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani na uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kwa mwaka 2016, katika Uwanja wa Mashujaa.
   Kamanda Mkuu wa Polisi Mkoa wa Lindi Renatha Mzinga akizungumzia nafasi ya Mwanamke katika kujenga Taifa wakati wa siku ya Maadhimisho ya Sikukuu ya wanawake Duniani.
   Kamishna Msaidizi wa Polisi Tatu Abdallah Mfaume ambaye ni Mkuu wa Dawati la Jinsia na Ulinzi wa Mtoto kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar es salaam, akizungumzia juu ya Dawati la Jinsia linavyofanya kazi
   Mshereheshaji akiendelea na kutoa Utaratibu 
  Mwanamuziki wa Muziki wa Kizazi Kipya Mwasiti akitumbuiza wakati wa Sherehe za Siku  ya Mwanamke Duniani
   Bi. Jovitha Mlay Kutoka Shirika la Kimatafa la OXFAM Tanzania akizungumza na wakazi wa Mtwara juu ya wanawake na uziduaji
   Bw.  Mohammed Mapalala kutoka Morogoro anayehusika na Maswala ya Ardhi akizungumzia juu ya Haki ya Ardhi kwa wanawake
   Meneja wa Utetezi Kutoka Shirika la OXFAM Tanzania Bi. Eluka Kibona akitoa Maelezo ya  kina kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambapo Msimu huu wa Tano linatarajiwa kuanzi mwezi Septemba na kurushwa katika Runinga ya ITV 
  Mwanamuziki Vitaris Maembe akitoa Burudani ya Nguvu wakati wa Sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani na Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akitembelea katika Mabanda mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani a Uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kwa Mwaka 2016
  Mwanamuziki matata wa Miondoko ya Taarabu Jike la Simba Bi. Aisha Mashauzi akitoa Bonge la Burudani wakati wa kilele cha Siku ya wanawake Duniani
  Burudani ikiendelea
  Mamia ya wakazi wa Mtwara wakiwa katika Sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani na uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kwa mwaka 2016, katika Uwanja wa Mashujaa.

  Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika la kimataifa la OXFAM  limezinduliwa rasmi  na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mh Halima Dendegu na kuwataka washiriki kuuletea ushindi katika Mkoa wao wa Mtwara. 

  Mh Halima Dendegu alitoa hamasa  hiyo katika uzinduzi huo uliokwenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huku akiwataka washiriki ambao ni wanawake wajitahidi kadiri wawezavyo mshindi wa shindano hilo atokee mkoani mtwara.

  Katika uzinduzi huo uliohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali, Taasisi za Umma, Mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na wakazi wa Mkoa wa Mtwara pia Mh. Halima Dendegu alipata nafasi ya kugawa fomu za ushiriki kwa wakina mama watatu wa shindano hilo na kupata nafasi ya kuwaandikisha katika fomu hizo.

  Pia katika hatua hiyo mkuu wa mkoa huyo amewaomba wakina mama wajasiriamali kujiokeza kwa wingi katika ushiriki wa shindano hilo ili kuongeza muamko wa shindano hilo na kujiongezea uwezo wa kushindana kuwataka wanawake wajasiriamali kujaza fomu za ushiriki kwa wingi na bila ya kuogopa.

  Sanjali na hatua hiyo mkuu wa mkoa amesema kuwa licha ya kuwepo na harakati za wanawake kujikwamua kiuchumi ambao wengi wao wanaotegemea kilimo kama njia ya kujipatia mazao lakini bado kumekuwepo na changamoto kubwa kwa mwanamke ya kumiliki Ardhi ambapo ametaja kama moja ya changamoto ya ukandamizaji wa kijinsia na kuwataka wanawake kusimama kidete katika kutetea haki hiyo kama moja wapo ya msingi.

  Naye Meneja wa Utetezi wa Shirika la Kimataifa la OXFAM, Eluka Kibona alieleza kuwa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kwa mwaka huu 2016 linatarajiwa kuanza Septemba na litakuwa linaoneshwa kupitia kituo cha runinga cha ITV.

  Meneja wa mradi kutokea shirika la OXFAM, Bi. Jovitha Mlay amewatoa hofu washiriki watakaoshiriki katika shindano hilo kwa kuwataka kujitokeza kwa wingi na hasa ikiwa kama bahati kwa shindano hilo la Mama shujaa wa chakula kuzinduliwa mkoani mtwara na hivyo kuwataka wakina mama wajasiriamali wakubwa na wadogo kujitokeza kwa kuchukua fomu za ushiriki kwa wingi.

  Aidha baadhi ya wanawake wadau wa OXFAM kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wametumia nafasi hiyo zaidi kwa kuwataka wajasiriamali wakina mama wa Mtwara kutumia fursa mbalimbali ili kuongeza kipato chao na kuacha suala la utegemezi kotoka kwa waume zao.

  Uzinduzi wa Mama shujaa wa chakula ulihudhuriwa na wasanii mbalimbali waliotoa burudani kwa wakazi waliofika katika uzinduzi wa shindano hilo; alikuwepo Valis Maembe, Mwasiti na Isha Mashauzi.

  Shindano la mama shujaa wa chakula lililoanzishwa na Shirika lisilo la kiserikali la Oxfam lililoanzishwa hapa nchini mnamo mwaka 2011 lenye lengo zaidi ya kumsaidia mwanamke kujitambua zaidi katika haki zake mbalimbali na kujitambua kama mwanamke na kumuinua kiuchumi.
  0 0


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akionesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mfumo wa ufatiliaji wa kielektroniki katika jengo la kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) kitakachoanza kazi rasmi mwezi Aprili mwaka huu jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitizama kwa karibu mtambo wa kuratibu usalama katika kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) jijini Dar es Salaam. Kituo hicho cha kwanza kujengwa nchini kitatunza taarifa za Serikali na sekta binafsi.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda wakati akikagua kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) kitakachoanza kazi rasmi mwezi Aprili jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda wakati akikagua kituo hicho cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) kitakachoanza kazi rasmi mwezi Aprili jijini Dar es Salaam.

  ……………………………………………
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amezitaka taasisi za Serikali na binafsi kukitumia kituo cha kisasa cha kuhifadhi taarifa (data centre) kutunza taarifa zao ili kuzihakikishia usalama na uhakika wa kuzitumia wakati wote.

  Akizungumza baada ya kukagua kituo hicho kinachosimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sekta ya Mawasiliano amesema asilimia 75 imetengwa kwa ajili ya kutunza taarifa kutoka sekta binafsi na asilimia 25 itatunza taarifa za Serikali.

  Waziri Mbarawa amezitaka taasisi za Benki, Simu, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala wa Serikali Mtandao (e-GA) kutembelea kituo hicho kujifunza mifumo ya uhifadhi taarifa na kujiunga ili kunufaika na huduma za kituo hicho.

  Amesema huduma ya mtandao katika kituo hicho imeimarishwa kutokana na kuunganishwa na mkongo wa taifa na hivyo itawarahisishia wateja wake kuweka na kuchukua taarifa kwa haraka.

  Kituo hicho ambacho ni cha kwanza kujengwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ni fursa mpya kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali wenye taarifa nyingi kuzihifadhi na kuzitumia wanapozihitaji kinalimikiwa na Serikali.

  0 0


  0 0

   Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige akimueleza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), tarehe 08 Machi, 2016, Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimueleza jambo Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige (hsyupo pichani), tarehe 08 Machi, 2016, Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).
   Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige (wa kwanza kulia) akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), (hayupo pichani) alipokutana naye Ofisini kwake, tarehe 08 Machi, 2016, Jijini Dar es Salaam.
   Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa  Idara ya uratibu wa shughuli za serikali Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery (kushoto) alipotembelea ofisi hiyo, tarehe 08 Machi, 2016, Jijini Dar es Salaam.

  Tanzania na Uingereza zinatarajia kuendelelea kushirikiana katika masuala ya Uchumi kupitia Mpango wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Tanzania na Uingereza “UK partnership in Prosperity” ambao unajikita katika maeneo makubwa ya ushirikiano ya Mafuta na Gesi, Nishati Jadidifu; Kilimo; na Uboreshaji Mazingira ya Biashara.
  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa kufanya mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige, leo jioni, terehe 08 Machi, 2016, Jijini Dar es salaam.
  Tunatarajia mpango huu ukishafanyiwa maboresho utaimarisha uchumi wa nchi zote mbili, tunatarajia baada ya maboresho hayo makampuni mengi kutoka uingereza kuja kufanya biashara nchini kuwekeza .Tunaelewa nia ya serikali ya Uingereza kuwekeza  katika miundo mbinu iliyopo vijijini hasa katika sekta ya maji na kilimo hii itasaidia kuinua maisha ya wananchi wanaoishi vijijini hasa wanawake , hii ni kutokana na kuwa asilimia 80 ya wananchi nchini wanaishi vijijini na wengi wao ni wananawake na leo ukizingatia ni siku ya wanawake Duniani” Alisema Mhagama.

  Aliongeza kuwa mpango huo umekuja muda muafaka wakati serikali inaendelea na juhudi za kuishirikisha sekta binafsi katika kukuza uchumi nchini kwa kuwa serikali inatambua sekta binafsi ndio chachu ya maendeleo nchini.

  “Tunahitaji ushirikiano wenu ili muweze kutujengea uwezo wa kuwavutia wawekezaji wa ndani na wa kimataifa kwa msingi wa kuendeleza viwanda nchini na hatimaye tunaweza kufanya kwa ubora  biashara kimataifa ” alisistiza.

  Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige ali fika ofisini hapo kwa lengo la kuonana na Waziri Mkuu kwa ajili ya kumueleza ushirikiano wao watakaoendelea kuutoa kwa serikali ya awamu ya tano katika masuala ya Dawa za kulevya na biashara haramu ya pembe za ndovu nchini pamoja na uboreshaji wa Mpango wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Tanzania na Uingereza “UK partnership in Prosperity”  .

  Mpango huo wa Ushirikiano wa Ushirikiano Kati ya Tanzania na Uingereza ulizinduliwa rasmi Novemba 2015 na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda.

  Imetolewa na
  KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  O8 MACHI 2016


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara ndogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara. Kulia kwake ni Meneja wa Mradi Huo wa Habari, Celestine Mkama. Picha na Cathbert Angelo Kajuna.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara ndogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara. Kulia kwake ni Meneja wa Mradi Huo wa Habari, Celestine Mkama.

  TAASISI ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imebuni mfumo maalum wa taarifa kupitia mtandao wa intaneti na simu za mkononi utakaotumiwa na wafanyabishara ndogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara. Mfumo huu utazinduliwa wiki ijayo jijini Dar es Salaam.


  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amewambia waandishi wa habari kwamba ikiwa ni muendelezo wa jitihada za serikali ya awamu ya tano kuziwezesha biashara ndogo ndogo, kushawishi wananchi kuanzisha biashara na vilevile kurasimisha biashara hizo, mfumo huu utazisaidia biashara ndogo ndogo kutimiza malengo yake.

   Alisisitiza kwamba mfumo huo wa habari ni wa aina ya kipekee kwani unawaruhusu watumiaji wa intaneti kupitia kompyta na simu kutumia na vilevile watumiaji wa simu zisizo na intaneti wataweza kutumia mfumo huu hususani katika kuboresha uelewa wa masuala ya fedha na ujuzi katika ujasiriamali huku ukiwawezesha wajasiriamali kujua namna ya kupata huduma sahihi za kifedha.

   Mfumo huu wa habari umetengenezwa mahususi ili kuwa kituo cha taarifa zote muhimu ambazo biashara ndogo inahitaji kuweza kukua. “Mfumo huu ni rafiki kwa mtumiaji, unapatikana kirahisi, na utawafikia walio na huduma ya intaneti na wasio na intaneti na umelenga katika kuwajengea uwezo wafanyabiashara kupitia taarifa mbalimbali muhimu kibiashara.” 

   Simbeye alisema kuwa mfumo huo wa habari utapunguza vizingiti vya uelewa ambavyo vimekuwa vikifanya biashara ndogo zishindwe kupata huduma na bidhaa za kifedha zitolewazo na taasisi mbalimbali, na vilevile mfumo huu utawapatia wafanyabiashara ndogo jukwaa la kutoa maoni na kujadiliana masuala mbalimbali. 

  Hii itasaidia katika kutengeneza sera ambazo zinakidhi mahitaji yao huku mfumo huo ukitoa mafunzo mbalimbali na nyenzo za kufanya biashara. Vilevile mfumo huu wa habari utasaidia kuanzishwa n kuendelezwa kwa mawazo mapya ya biashara na fursa mbalimbali, utaleta fursa kwa watoa huduma za fedha kupata taarifa za soko bure hususani kuhusu mahitaji ya wateja wao. 

   “Uboreshaji elimu kuhusu fedha na ujasiriamali kwa wafanyabiashara wadogo na wadau katika sekta ya ya fedha utasaidia kuleta tabaka la watumiaji huduma waelevu ambao watahitaji kupewa bidhaa na huduma zinazoendana na mahitaji yao ya muda mfupi na muda mrefu, wakati huo huo taasisi za kifedha zikishindana kubuni bidhaa na huduma zinazoendana na mahitaji ya wateja. Vilevile taasisi zinazosimamia huduma hizi na watunga sera wataweka mazingira mazuri kwa kila mdau kunufaika kutokana na huduma za mwenzake. 

  Hii ni hali ambayo itampa faida kila mmoja ambapo waombaji mikopo wataweza kuchagua mikopo ipi inafaa kwa biashara zao jambo ambalo litapunguza uwezekano wa kushindwa kurudisha mikopo huku taasisi za kifedha zikiweza kutoa mikopo zaidi na kupata faida zaidi,” alisema. Meneja Mradi wa Mfumo huo wa Habari, Celestine Mkama alisema kwamba baadhi ya huduma muhimu zitakazotolewa na mfumo huo ni pamoja na muongozo kamili juu a kupata huduma za kifedha, kuanzisha biashara, kuendesha na kukuza biashara, msaada wa kitaalamu katika maeneo mbalimbali, majukwaa ya majadiliano, taarifa za masoko na uwezeshaji wafanyabiashara kuyafikia masoko hayo, taarifa za fursa mbalimbali pamoja na mafunzo mbalimbali kupitia mtandao ikiwa ni pamoja na utoaji habari za biashara kupitia machapisho na majarida mbalimbali.

   Mfumo huu wa habari pia utatoa muongozo wa mchakato wa kufanya biashara na sheria husika, taarifa za fedha za nje na utatoa mfano wa nyaraka za kuendesha biashara. 

   Mkama pia alitaja baadhi ya huduma nyingine muhimu zitakazosaidia biashara kukua kuwa ni pamoja na mafunzo juu ya ujasiriamali kupitia mtandao, miundombinu ya kuwawezesha wafanyabiashara kufanya biashara kupitia mtandao ambapo wataweza kuuza bidhaa na huduma, na huduma ya mawasiliano ambapo wafanyabiashara wataweza kupatiwa majibu na wahusika kupitia mtandao.

   Vilevile Taasisi ya Sekta Binafsi itafanya vipindi vya redio na warsha za mafunzo zikiwahusisha zikiwahusisha wajasiriamali na wadau mbalimbali nchi nzima ili kuongeza uelewa kuhusu mfumo huu wa habari na kuwashauri wajasiriamali namna ya kuanzisha na kukuza biashara kufata misingi sahihi ya biashara.

  0 0

  KATIKA kusherekea siku ya Wanawake duniani Benki ya CRDB tawi la Mlimani City washerekea siku hiyo na wanawake wenye kaunti za MALKIA katika tawi hilo siku hiyo ya wanawake hufanyika Machi 8 kila mwaka.
   Keki na vinjwaji mbalimbali ambayo imeandaliwa na wafanyakazi wanawake wa benki ya CRDB  tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika  Machi 8 kila mwaka.
    Mgeni rasmi Anna Jeremiah Kaaya akikata keki pamoja na wateja mbalimbali wa benki ya CRDB  tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam kwaajili ya kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.
  Wateja wa Akaunti ya MALKIA katika benki ya CRDB  tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wakifungua shampeini katika hafla iliyofanyika katika tawi hilo leo.
  Meneja huduma kwa wateja wa benki ya  CRDB tawi la Mlimani City, Catherine Momburi akikabidhi zawadi kwa wateja wanawake wenye akaunti ya MALKIA katika tawi hilo.
  Mgeni rasmi Anna Jeremiah Kaaya akimlisha keki meneja uhisiano wa mikopo Martha Ngowi wakati wa kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi kila mwaka.
  Wafanyakazi wa Crdb tawi la Mlimani City, Fatma Tinna na Dorice Temu wakijiandaa kugawa zawadi kwa wateja wenye akaunti za MALKIA kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
  Wafanyakazi wanawake wa benki ya  CRDB tawi  Mliman City wakiwa katika picha ya pamoja katika maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani.


  Wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pampoja mara baada ya kudhimishi siku ya wanawake dunia katika tawi lao jijini Dar es Salaam.
   
  Selfiiiiiiiiiiiiiiiiii

  0 0

  Mbunifu wa mavazi, msanii wa filamu na mrembo maarufu nchini, Jokate Mwegelo akikabidhi moja ya msaada wake kwa mmoja wa mama aliyejifungua mtoto wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika hospitali ya Palestina jijini.
    Mmoja wa mofisa wa kampuni ya Suining Zerong Commercial Trading, Shuxia B akizungumza kwa niaba ya kampuni hiyo. Kampuni hiyo inafanya kazi pamoja na kampuni ya Kidoti.
   Jokate Mwegelo ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya na mmoja wa maofisa wa kampuni ya Suining Zerong Commercial Trading, Shuaijie Duan wakikabidhi cheti cha shukrani kwa daktari mkuu wa hosptiali ya Palestina, Dk  Kariamel Wandi.
  Mbunifu wa mavazi, msanii wa filamu na mrembo maarufu nchini, Jokate Mwegelo akimbeba mtoto aliyezaliwa siku ya wanawake duniani katika hospitali ya Palestina jijini. Jokate alitembelea wodi hiyo na kutoa msaada.
  Mrembo wa Tanzania namba mbili wa 2006, mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu za kibongo, Jokate Mwegelo  amewaomba wasanii wenzake na wadau wengine  kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha huduma ya afya ya wazazi na watoto.
  Akizungumza mara baada ya kutembelea wodi ya wazazi ya hospitali ya Palestina na kutoa misaada mbalimbali kwa wanawake waliojifungua wakati wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake duniani, Jokate alisema kuwa sekta hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi na kutokana na umuhimu wake, wadau wanatakiwa kusaidia serikali.
  Jokate alisema kuwa serikali inafanya kitihada kubwa ya kuboresha sekta  hiyo na kumpongeza Rais Dk John Magufuli kwa kuelekeza nguvu  na kufanikiwa kutatua  tatizo sugu lililokuwa linaisumbua la  hospitali ya Taifa ya Muhimbili T-scan matatizo kadhaa sugu katika.
  “Kila mmoja wetu anajua nini maana ya afya, huwezi kufanya jambo lolote kama huna afya bora, hivyo matibabu bora ni muhimu, serikali inafanya vitu vingi katika kuondoa kero za wananchi wake ikiwemo suala la afya, nimeguswa na kuamua kuunga mkono kupitia kampuni yangu ya Kidoti ambayo inazalisha viatu na nyewe,” alisema Jokate.Alisema kuwa amefuraishwa na huduma ya wodi ya wazazi ya hospitali ya Palestina na ushirikiano waliopata kuanzia mganga mkuu wa manispaa ya Kinondoni na uongozi wa hospitali hiyo kwa ujumla.

  “Kama unavyojua, misaada mingu uelekezwa kwenye hospitali kubwa kubwa tu, kuna hospitali na zahanati nyingi ambazo zinahitaji kusaidia, hivyo wasanii wenzagu, hii ni fursa kwenu kurudisha faida kwa jamii, si lazima utoe fedha, hata kuwaona wagonjwa na kuwafariji,” alisema.
  Alisema kuwa mikakati yake ni kuona anatembelea na kutoa alichonacho kwa hospitali na vituo vya afya mbalimbali nchini.
  Mmoja wa maofisa wa kampuni ya Kidoti, Shuxia Bi kutoka China alisema kuwa ni vizuri jamii hasa wasanii wa muziki, filamu, warembo  na wanamitindo kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua matatizo kwa jamii yenye mahitaji maalum. Shuxia alisema kuwa kupitia chapa ya Kidoti wanaamini watafikia wadau wengi jijini nan je ya mkoa.
    Dakitari Mkuu wa hospitali ya Palestina, Kariamel Wandi aliimpongeza Jokate na kampuni yake kusaidia wodi ya wazazi. “Tumefarijika sana, umeonyesha kuwa unajali, wengi wameshindwa kufanya kama unavyofanya pamoja na kuwa na nafasi hiyo, naomba uwe na moyo huo huo,” alisema Wandi.
  Wandi alisema kuwa  Jokate amewasaidia wakati muafaka kwani hadi anakamilisha kutoa misaada mbalimbali, jumla ya watoto  26 walizaliwa katika hospitali hiyo. Kati ya hao, 18 ni wasichana na nane ni wavulana.

  0 0

  Ajali mbaya iliyohusisha Magari matatu likiwemo Daraladal ya abiria linalofanya safari zake kati ya Gongo la Mboto kwenda Ubungo, imetokea mapema leo asubuhi katika barabara ya Mandela eneo la Tabara Matumbi, Jijini Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 16 kujeruhuwa vibaya sana na kukimbizwa hospitali ya Amana, Ilala kwa Matibabu.

  Inaelezwa kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma, hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugonga na Lori lingine lililokuwa limepakia Ng'ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu Mnadani.

  Jitihada za kuyatoa magari hayo zinafanyika sasa. Kama unaweza kutoitumia barabara hiyo asubuhi hii ni vema kuepuka msongamano
  Muonekano wa Daladala hilo baada ya kugongana uso kwa uso la Lori lililokuwa limepakia Ng'ombe, eneo la Tabata Matumbi, Jijini Dar es salaam leo.
  Askari wa Usalama Barabarani na baadhi ya mashuhuda wakiwa eneo la tukio.
  Baadhi ya Ng'ombe walikuwemo kwenye Lori hilo, wakiwa wamewekwa kando baada ya kuokolewa.
  Kichwa cha Lori hilo, kikiwa Chini baada ya Ajali.

  0 0

  Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Evans Lyimo(kushoto)akimuuliza swali mtaalamu wa masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Chris Mauki(hayupo pichani)wakati alipokuwa akiongea na wafanyakazi wanaume wa kampuni hiyo kuhusiana na jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike katika kuazimisha siku ya wanawake duniani jana.
   Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Chris Mauki(kulia)akifafanua jambo wakati alipokuwa akitoa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi wanaume wa Vodacom Tanzania ya jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike katika kuazimisha siku ya wanawake duniani jana.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt. Chris Mauki(kulia)baada ya kutoa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi wanaume wa kampuni hiyo ya jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike ikiwa katika kuazimisha siku ya wanawake duniani jana.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakimsikiliza Mtaalamu wa Masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt. Chris Mauki(hayupo pichani)wakati wa kuelimishwa kwa baadhi ya wafanyakazi wanaume wa kampuni hiyo,Jinsi ya kuwekeza kwa mtoto wa kike ikiwa katika kuazimisha siku ya wanawake duniani jana.

  0 0

   Mhadhiri wa Idara ya Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Dk.William John akizungumza na waliokuwa waangalizi wa uchaguzi 2015 katika majimbo mbalimbali katika utoaji wa ripoti ya CEMOT  iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya waliokuwa waangalizi katika uchaguzi 2015 wakifuatilia mada katika utoaji wa ripoti ya CEMOT leo jijini Dar es Salaam.
   Meneja wa Mradi-CEMOT Bwa.Bernard Kindoli akizungumza na waliokuwa waangalizi wa uchaguzi majimbo mbalimbali katika utoaji wa ripoti iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Mjumbe wa Kamati Tendaji ya CEMOT,Bi.Harusi Miraji akizungumza na waliokuwa waangalizi wa uchaguzi 2015 katika majimbo mbalimbali wakati utoaji ripoti ya CEMOT leo jijini Dar es Salaam.
    Sehemu ya waangalizi wakifuatilia mada katika utoaji wa ripoti ya CEMOT leo jijini Dar es Salaam.


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  RIPOTI ya Muungano wa Asasi za Kitanzania zinazoangalia uchaguzi nchini kwa Kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (CEMOT)  imesema  kuwa, kuweza kupata uwiano wa 50 kwa 50 kati ya wanaume na wanawake  kwa upande wa wanawake itachukua miaka 150 kutokana na ushiriki wao kuwa mdogo katika nafasi za kugombea.

  Akizungumza na waangalizi wa uchaguzi wa mradi wa CEMOT, kutoka  Idara ya Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Dk.William John amesema kuwa ushiriki wanawake ni mdogo katika nafasi mbalimbali za kugombea na kufanya uwakilishi wa 50 kwa 50 kuchukua muda mrefu.

  Amesema kuwa wanawake waliogombea katika kiti cha urais kwa  kuchaguliwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikuwa saba lakini hawakuweza kuingia katika  nafasi ya kwanza ya kupeperusha bendera.

  Dkt.John amesema kuwa wanawake waliogombea katika nafasi ya ubunge kwa vyama vyote vilivyoshiriki  uchaguzi wa mwaka 2015 walikuwa 238 walioweza kuchaguliwa katika nafasi hiyo ni wabunge 24 tu .

  Amesema kuwa ushiriki wa uchaguzi kwa wanawake ongezeko kwa mwaka 2015 ilikuwa asilimia 2 ambayo ni kiwango kidogo katika kuweza kufikia asilimia 50 kwa 50.

  Ripoti hiyo  pia imesema kuwa wanawake katika nafasi ya urais ni mwanamke mmoja tu ndio aliweza kupeperusha bendera ya chama chake hali ambayo katika nafasi hiyo ni ndogo ya kufikia uwiano huo.


  0 0

  Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim, Bw. Selemani Ponda (katikati) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kutangaza kuingia kwa benki hiyo nchini Uganda na kuweka rekodi ya kuwa benki ya kwanza ya Kitanzania kuingia nchini humo. Wengine ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Bw. Abdulrahman Nkondo (kushoto) na Meneja Mwandamizi Huduma kwa Wateja, Bw. Frank Matoro.

  BENKI ya Exim Tanzania imezidi kajitanua nje ya mipaka ya nchi baada ya kufanikiwa kuingia rasmi nchini Uganda na kuweka rekodi ya kuwa benki ya kwanza ya Kitanzania kuingia nchini humo.

  Mafanikio hayo yamekuja baada ya benki hiyo kutwaa asilimia 58.60 ya hisa za iliyokuwa benki ya Imperial ya Uganda. Hatua hiyo inapelekea benki hiyo kutambulika kama ‘Exim Bank Uganda Ltd’ nchini humo huku ikihusisha wamiliki wenza wawili ambao ni kampuni ya Amazal Holdings (maarufu kama ‘Mukwano Group’) yenye hisa 36.7%  pamoja na kampuni ya Export Finance Ltd yenye hisa 4.9%.

  “Tunayo furaha kuwatangazia wana Afrika Mashariki kwamba Benki ya Exim imefanikiwa kuingia nchini Uganda ikiwa katika ushirikiano na makampuni makubwa na yanayoheshimika nchini Uganda,’’ alisema Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim, Bw Selemani Ponda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

  Aliongeza kuwa ushirikiano huo umekuja wakati muafaka ikiwa ni kipindi ambacho nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pia zimeongeza ushirikiano ili kuwa na nguvu ya pamoja.

  Akizungumzia uendeshwaji wa benki ya Exim Uganda Bw Ponda alisema kwa kuanzia benki hiyo itaanza na matawi matano jijini Kampala ikiwa na rasilimali (asset) yenye thamani ya takribani dola za kimarekani milioni 100.

  “Makao makuu ya benki yatakuwa barabara ya Hannington na kwa kuanzia tutakuwa na zaidi ya wafanyakazi 100 walio na ari ya kutimiza majukumu yao ambayo ni kuhudumia wateja wetu wakubwa na wadogo kwa kuwa benki hiyo itatoa huduma zote za kibenki,’’ alibainisha.

  Kuingia kwa Benki ya Exim nchini Uganda kunaifanya izidi kusimika mizizi yake kwenye ukanda wa Afrika mashariki na hivyo kuzidi kutoa mwanga wa kutimiza lengo lake la kuwa muhimili imara kwenye huduma za kibenki katika ukanda huo.
  Benki hiyo ambayo kwa sasa ina rasilimali ya Sh trilioni 1.259 (Dola za kimarekani milioni 580) inatarajiwa kutimiza miaka 19 ifikapo mwezi Agosti mwaka huu tangu kuanzishwa kwake hapa nchini huku kwa sasa ikiwa ina jumla ya matawi 30 nchini na matawi mengine 9 nchini Comoro na Djibout. Kuingia kwake nchini Uganda kunaongeza idadi ya matawi ya benki hiyo nje ya nchi

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Jordan Rugimbana akisoma hotuba ya ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Bodi ya Barabara kilichofanyika leo tarehe 9 Machi 2016 kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa ,wengine waliokaa kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye na Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Barabara ,Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mhe. Hamidu Bobali.
   Wajumbe wa kikao cha kwanza cha Bodi ya barabara mkoani Lindi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa Kikao Mhe. Jordan Rugimbana.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara mkoani Lindi.
   Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Barabara ,Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mhe. Hamidu Bobali akijitambulisha kwa wajumbe wa kikao.
   Wajumbe wa kikao cha kwanza cha Bodi ya barabara mkoani Lindi.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya Nawanda kabla ya kuanza kwa kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara mkoani humo.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye akitaniana na Mwandishi maarufu wa mkoa wa Lindi Abdul Aziz

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini Mhe. Seleman Said Bungara almaarufu Bwege muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara cha mkoa wa Lindi.  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kushoto) akimkaribisha mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.
   Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye koti la drafti) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam. Kulia niRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli
   Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa tatu kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (wa tatu kushoto) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam. Wa pili kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakipanda jukwaani kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za Taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakiwa katika jukwaa kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za Taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (mwenye tai nyekundu) akikagua gwaride la heshima katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi,
   2016.
   Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akipokea zawadi ya ua toka kwa mtoto mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 akiwa amefuatana na mmewe kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.

   
   Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe mamaMai Thi Hanh wakiwasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbalikati ya Tanzania na Vietnam.
  (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)

  0 0

   Meneja   wa biashara wa kampuni ya  simu za mkononi nchini  Airtel  kanda ya nyanda  za  juu  Bw Straton Mushi (kushoto) akimkabidhi  jana kaimu  mkuu  wa mkoa  wa Iringa Bw  Richard Kasesela msaada  wa saruji mifuko 100 na mabati  200 vyenye  thamani ya Tsh milioni  5  kwa ajili ya kusaidia waathirika  wa mafuriko Pawaga  na Idodi wilaya ya   Iringa.
   Kaimu  mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Bw Richard Kasesela (kulia ) akipokea  msaada wa bati 200 pamoja na  saruji  100  vyote  vikiwa na thamani ya  Tsh milioni 5 kutoka kwa meneja  wa biashara  wa Airtel kanda ya nyanda za juu Bw Straton  Mushi jana   msaaada   uliotolewa kwa ajili ya  waathirika  wa mafuriko Pawaga na Idodi  wilaya ya Iringa.
   Kaimu  mkuu  wa mkoa wa Iringa Bw  Richard Kasesela (kushoto mwenye suti)  akimpomngeza meneja  wa biashara  wa Airtel kanda ya nyanda za juu Bw Straton Mushi kwa niaba ya kampuni hiyo  simu  za mikononi kwa  kusaidia waathirika wa mafuriko Pawaga  na Idodi  Iringa.
  (Picha na mpiga picha  wetu )

  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imetembelea wahanga wa mfuriko ya mvua katika jimbo la Isimani, wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa na kuwapatia msaada wa mahitaji muhimu kwaajili ya ujenzi wa makazi baada ya makazi yao ya awali kuzoewa na mafuriko. Zaidi ya familia 220 zimepoteza makazi kufatia mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa Februari mwaka huu.

  Akiongea wakati wa makabithiano ya msaada huu, Meneja mauzo wa Airtel kanda ya Nyanda za juu kusini Bwana Straton Mushi alisema” Tunaungana kwa pamoja katika maafa haya na kutoa pole kwa familia zilizoathirika na mafuriko haya.

  Tunatambua pia mafuriko haya yamewaacha wakazi wengi bila makazi, huku mazao yao ya chakula na biashra kuharibiwa na mifugo yao kufa hivyo tunaungana kwa pamoja na wakazi wa Iringa vijijini ili kuwawezesha kujenga makazi yao upya. Leo kwa niaba ya Airtel kupitia ofisi yetu ya kanda ya juu kusini tunatoa msaada wa mabati 200 na saruji mifuko 100 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 5 na kuwaomba watanzania kuungana nasi kuwasaidia ndugu zetu wa Isimani ili kuepuka milipuko ya magonjwa isitokee. Pia huu ni wakati muhimu wa kushirikiana  kuwawezesha wenzetu kurudi na kukaa na familia zao ili kufanya shughuli zao za kawaida mapema iwezekanavyo.

  Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa Isimani, Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela Alisema “Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu umekuja wakati tunauhitaji zaidi, napenda kuwaomba watanzania kushiriki kwa kuchangia na kwa makampuni mengine kujitolea na kutusaidia katika hali ngumu ambayo imetuweka kwenye hatari kupata milipuko ya magojwa na zaidi tumekosa makazi na shughuli zetu za kiuchumi zimeteketea. Tunawashukuru waliojitolea mpaka sasa na tunaomba muendelea na moyo huo wa kujitolea.

  0 0


  Kushoto ni msaidizi wa Mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa (CCM), Tumaini Ambakisye Mwakatika, akimkabidhi mashuka 40 na magodoro 20, mkuu wa wilaya ya Mbeya, Nyerembe Mnasa Sabi (wa pili kutoka kushoto), kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Iyunga Technical school ya Jijini Mbeya, waliounguliwa juzi bweni la shule hiyo na vitu vyao.
  DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA
  Kushoto ni msaidizi wa Mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa (CCM), Tumaini Ambakisye Mwakatika, akizungumza jambo na wanafunzi wa shule ya sekondari Iyunga ya Jijini Mbeya, alipoenda kukabidhi msaada wa mashuka 40 na magodoro 20, kwa niaba ya Mbunge Dkt. Mwanjelwa leo, kufuatia wanafunzi hao kuunguliwa na bweni moja juzi.
  Kushoto ni msaidizi wa Mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa (CCM), Tumaini Ambakisye Mwakatika, akimkabidhi mashuka 40 na magodoro 20, mkuu wa wilaya ya Mbeya, Nyerembe Mnasa Sabi (wa pili kutoka kushoto), kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Iyunga Technical school ya Jijini Mbeya, waliounguliwa juzi bweni la shule hiyo na vitu vyao.

  Wanafunzi wa shule ya sekondari Iyunga Technical ya Jijini Mbeya, wakibeba magodoro 20 na mashuka 40, kwenda kuyahifadhi baada ya kukabidhiwa na mwakilishi wa Mbunge wa viti maalim mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa leo.
  Kushoto ni msaidizi wa Mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa (CCM), Tumaini Ambakisye Mwakatika, akimkabidhi mashuka 40 na magodoro 20, mkuu wa shule ya Iyunga Technical ya Jijini Mbeya, Edward Mwantimwa, kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo, waliounguliwa juzi bweni la shule hiyo na vitu vyao.
  Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Nyerembe Mnasa Sabi (katikati), akimshukuru Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya, (hayupo pichani) Dkt. Mary Mwanjelwa, kwa msaada wake alioutoa kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Iyunga Technical school ya Jijini Mbeya, waliounguliwa juzi bweni la shule hiyo na vitu vyao.
  Kulia ni msaidizi wa Mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya, Dkt. Mary Mwanjelwa (CCM), Tumaini Ambakisye Mwakatika, akiwakabidhi mashuka 40 na magodoro 20, wanafunzi wa shule ya sekondari Iyunga Technical school ya Jijini Mbeya, waliounguliwa juzi bweni la shule hiyo na vitu vyao.


  Na, Gordon Kalulunga, Mbeya


  MWENYEKITI wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mary Mwanjelwa, ambaye ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya (CCM), amewapa pole wanafunzi wa shule ya ufundi Iyunga Technical School, kufuatia kuungua kwa bweni la shule hiyo juzi, iliyopo Jijini Mbeya.

  Akizungumza kwa niaba yake shuleni hapo leo, msaidizi wa Mbunge huyo, Tumaini Ambakisye Mwakatika, alisema Dkt. Mwanjelwa ameguswa na kusikitishwa na tukio hilo na kwamba ameamua kutoa msaada wa magodoro na mashuka kwa wanafunzi walioathirika.

  “Mhe. Dkt. Mwanjelwa kama kiongozi mwanamke, amesikitishwa na tukio la moto katika bweni la wanafunzi lililotokea siku ya Jumatatu na ametumia siku ya maazimisho ya wanawake kuja kuwaona kwa kutoa magodoro 20 na mashuka 40 na akitoka Dar es Salaam ameahidi kufika hapa shuleni kwa ajili ya kuja kuwaona” alisema Tumaini.

  Akizungumza kwa njia ya simu na www.kalulunga.blogspot.com Dkt. Mwanjelwa alisema maandiko matakatifu yanasema kuwa lieni na wanaolia, hivyo licha ya kuwa mbali, ameona atangulize msaada huo.“Mimi ni mama, nimeumizwa sana na tukio hili la kuungua bweni la shule ya Iyunga ambayo ni moja ya shule za kihistoria katika mkoa wetu wa Mbeya, nashukuru Mungu nimepokea taarifa kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Mbeya ndugu Nyerembe Sabi Mnasa, kuwa hakuna mwanafunzi ambaye ameathirika na moto huo” alisema mbunge huyo.


  Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Nyerembe Sabi Mnasa, alimwambia msaidizi wa mbunge huyo kuwa, msaada huo ni mkubwa na Dkt. Mwanjelwa anapaswa kupewa sifa katika kujitoa kwake hasa kwa wahitaji na tayari tume imeundwa kuchunguza tukio hilo ambalo lina sentensi za utete ikiwemo kuwa wiki moja lilipoungua bweni la kwanza hakukuwa na umeme shuleni hapo.

  Akipokea msaada wa magodoro 20 na mashuka 40 yaliyotolewa na Dkt. Mary Mwanjelwa shuleni hapo, mkuu wa shule hiyo, Edward Mwantimwa, huku akionekana ni mtu ambaye hayupo kwenye hali yake ya kawaida, alishukuru na kwamba kwa sasa wapo katika kipindi kigumu sana.

  “Namshukuru sana mbunge Mwanjelwa kwa moyo huu wa utoaji na kwa kuwaza kwa ajili yetu” alisema Mwalimu Mwantimwa.Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Dkt. Stephen Mwakajumilo ameumbia mtandao huo wa kalulunga blog kuwa “Sisi kama bodi ni kupokea msaada wa aina yeyote kote duniani, tunawashukuru waliojitokeza kutoka CCM na Chadema. Tunaomba Dkt. Mwanjelwa atusaidie kuwashawishi wengine na viongozi tutafakari pamoja kuhusu shule zote za zamani nchini hasa miundombinu ya shule hizo. Alisema.

  0 0

   Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiambatana na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Ikulu na Utawalabora Mheshimiwa Dkt. Mwinyihaji Makame, amemtembelea kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar  Maalim Seif Shariff Hamad ambaye yuko hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko baada ya kutolewa hospitali. Amesema afya yake inazidi kuimarika siku hadi siku. Dkt. Shein alifika hotelini hapo mnamo majira ya saa mbili usiku. (Picha na Salmin Said, OMKR)
   Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akimjulia  hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar  Maalim Seif Shariff Hamad hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
  Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akimjulia  hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar  Maalim Seif Shariff Hamad hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Picha na OMKR

  0 0

  Rais wa Vietinam, Trung Tan Sang akihutubia mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Vietinam, Trung Tan Sang kuhutubia mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam uliofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
  Rais wa Vietinam, Trung Tan Sang akimpongeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alizungumza na kumkaribisha Rais huyo kuhutubia mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016.
  Rais wa VietinamTrung Tan Sang (kuliakwa Waziri Mkuu) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja badhi ya viongozi na wafanyabiashara wa Tanzania na Vietinam baada ya mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016.
  Rais wa Vietinam, Trung Tan Sang akiongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoka katika mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam uliofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  Rais wa Vietinam, Trung Tan Sang akizungumza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kabla ya kuanza kwa mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  Rais wa Vietinam, Trung Tan Sang akiteta na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietinam kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Machi 9, 2016. 

older | 1 | .... | 790 | 791 | (Page 792) | 793 | 794 | .... | 1897 | newer