Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

Kivuko cha Mv Dar es Salaam kuanza kazi hivi karibuni

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Kivuko cha Mv Dar es Salaam maarufu kama kivuko cha Rais Magufuli kipo katika matengenezo ya kawaida na kinatarajiwa kuanza kutoa huduma kama kawaida siku za hivi karibuni.

Akitoa ufafanuzi juu ya madai ya kutelekezwa kwa kivuko cha Mv Dar es Salaam katika maegesho yaliyopo kigamboni Jijini Dar es Salaam ,Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Manase Le-Kujan amesema sio kweli kwamba kivuko hicho cha Mv Dar es Salaam kimetelekezwa bali kimepumzishwa kutokana na matengenezo yaliyohitajika kufanywa katika kivuko hicho ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wasafiri.

“Sio kweli kwamba Kivuko cha Mv Dar es Salaam kimetelekezwa katika maegesho ya Kigamboni bali kimepumzishwa kwa muda kwa ajili ya matengenezo yake ya kawaida, hii ikiwa ni juhudi ya kukiwezesha Kivuko hiki kuwa katika ubora unaotakiwa katika kutoa hudumazake”“Mbali na matengenezo pia kuwepo kwa upepo mkali katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea imetufanya tukipumzishe kwa muda kivuko hicho” Alisema Mhandisi Manase.

Akifafanua zaidi,Mhandisi Manase amesema kuwa wapo katika mchakato wa kukipeleka kivuko hicho kwa ajili ya matengenezo makubwa Mjini Mombasa ili kukiongezea mwendo kasi na uhimili wake ili kiweze kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika usafirishaji kwa kutumia vivuko na kuhuimili mabadiliko ya hali ya hewa.

Aidha amesema hakuna mvutano wa watendaji wakuu TEMESA wala madai yoyote ya kukisimamisha kwa makusudi kivuko hicho bali ni mpango wa TEMESA katika kukiboresha ili kiweze kuhudumia wananch iipasavyo.

Kivuko cha Mv Dar es Salaam hufanya safari zake za kusafirisha abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Bagamoyo ikiwa ni juhudi za serikali za kupunguza tatizo la usafiri wa majini na kwa sasa kimesimama kwa muda kwa ajili ya matengenezoambayo yakikamilika kitaendelea kutoa huduma kama kawaida.


Ufanisi wa kivuko hiki utapunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa Bagamoyo, Mbweni, Ununio, Boko,Bunju, Kunduchi na  Msasani wanaofanya safari zao kwenda Posta nakurudi sehemu wanakotokea. Na pia kitapunguza msongamano wa magari katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kwani baadhi ya watu wataacha kutumia magari yao binafsi na kupanda kivuko hicho.

Jamii yatakiwa kuripoti Uhalifu unaofanywa kwa njia ya laini za simu na mitandao.

$
0
0

Na. Benedict Liwenga-Maelezo.

JESHI la Polisi limewataka wananchi kuwa makini ili kuepukana kutapeliwa fedha na watu wasio waaminifu wanaojipatia fedha hizo kwa njia ya simu na mitandao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Mrakibu Mwandamizi (SSP), Advera Bulimba wakati akiongea na Mwandishi wa Idara ya Habari kwa njia ya simu ambapo amesema kuwa jamii hainabudi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwaibua watu wanaojihusisha na uhalifu kwa njia ya laini za simu pamoja na njia ya mtandao kwa kutoa taarifa mapema katika vituo vya Polisi.

Ameongeza kuwa, watu wanatakiwa kuwa makini kabla ya kutuma pesa kwa watu wanaodaiwa kuhitaji kutumiwa pesa ili kujiridhisha nao na kuepuka kutapeliwa.

‘’Jeshi la Polisi limekuwa likifanyia kazi taarifa zinazotolewa na walalamikaji kwa kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani ambapo mpaka hivi sasa tayari kuna baadhi tumewafikisha mahakamani na baadhi wanatumikia vifungo vyao,’’alisema Bulimba.

Aidha, pamoja na juhudi za Jeshi la Polisi katika kjutoa elimu kwa umma kuhusiana na wizi wa mtandao, amevitaka vyombo vya Habari pamoja na wadau wengine kutoa elimu hiyo pia kwa jamii kuhusiana na wizi wa aina hiyo.‘’Zoezi hili la kuwabaini wahalifu kwa njia ya mtandao ni endelevu ili kupunguza ama kuondoa kabisa uhalifu wa aina hii’’, alisisitiza Bulimba.

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy amesema kuwa wizi kwa njia ya simu na mitandao ni makosa ya kiuhalifu ambayo yanapaswa kuripotiwa Polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Amesisitiza kuwa watu wasithubutu kutuma fedha kwa watu bila kujiridhisha kwani kuna baadhi ya watu hutumia vitambulisho bandia katika kusajili laini zao za simu na hivyo hutumia kufanyia uhalifu kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa watu kwa lengo la kuomba pesa.

‘’Sisi kama TCRA tunatoa elimu kwa umma ili wananchi waepuke kutapeliwa na pia tunawashauri kuripoti mara moja matukio ya uhalifu kwa njia za simu na mitandao katika vituo vya Polisi kwa uchunguzi na hatua stahiki,’’ alisema Mungy.

Hivi karibuni matukio ya wizi kwa njia ya simu na mitandao yamekuwa yakijitokeza ambapo baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maneno na kuomba pesa kwa ndugu na jamaa ili kujipatia fedha kwa njia ya utapeli.

NMB Yatoa Mafunzo Ya Kijasiriamali Kwa Wafanyabiashara Wakubwa Na Wadogo Nchini

$
0
0
   Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo wa NMB - Abdulmajid Nsekela akiongea na wafanyabiashara kwenye hafla ya wajasiliamali ambao ni wateja wa NMB wa wilaya ya Kinondoni.
  Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni  Mh. Paul Makonda akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa hafla ya Business Club iliyofanyika Sinza jijini Dar es Salaam
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam - Vicky  Bishubo akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni 
NMB imekuwa ikuwakutanisha wafanyabiashara wakubwa na wadogo walio kwenye mtandao wa NMB Business Club kwaajili ya kuongea nao na kupokea maoni yao na mrejesho wa jinsi gani benki inaweza kuboresha huduma kwa wateja zaidi ya wajasiliamali 300 walihudhuria katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni – Mh Paul Makonda.
NMB Yatoa Mafunzo Ya Kijasiriamali Kwa Wafanyabiashara Wakubwa Na Wadogo Nchini .Benki ya NMB PLC imetoa mafunzo ya kijasiriamali kwa zaidi ya wafanyabiashara 300 jijini Dar es Salaaam. NMB ina jumla ya vilabu vya biashara 34 nchi nzima vyenye wanachama zaidi ya 10,000. NMB

Business Clubs zina malengo ya kuwafikia jamii ya wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa ambao wanajumuisha wafanyabiashara zaidi ya 50,000 ambao ni wateja wa NMB nchi nzima.

Benki ya NMB PLC imekuwa kipaumbele kuhamasisha wanafanyabiashara nchini kujikimu kimaisha kwa kufungua vituo vya biashara nchini kimoja ambacho kipo kwenye wilaya ya Kinondoni- Sinza Business

Centre. Vituo hivi sio sehemu tuu ya kuchukulia mikopo bali pia ni sehemu ya wafanyabiashara kupata ushauri kuhusu mikopo na biashara kutoka kwa wa wataalamu wetu. Kaimu Afisa wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB PLC alisisitiza kwamba lengo kuu la vilabu hivi vya

biashara vimeundwa kuhakikisha wafanyabiashara nchini wanakuza mitaji yao, kuajiri watanzania wengi zaidi na pia kuchangia uchumi wa taifa hili kupitia ulipaji kodi.

Akiongea na wafanyabiashara nchini Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni Paul Makonda ameipongeza benki ya NMB kwa kuonyesha shauku ya kufanya mapinduzi ya kiuchumi kupitia vilabu vya biashara ambavyo vinawapa wananachi elimu ya kijasiriamali na hivyo kupiga hatua ya kuiuchumi kimaisha.

Kongamano la Moyo wa Wanawake lafana

$
0
0

Mwishoni mwa wikiendi ilipopita kumemalizika tukio kubwa kuelekea siku ya mwanamke Duniani, kulikuwa na Kongamano la Moyo wa Mwanamke Katika kanisa la Living Water Centre kawe,Kongamano hilo lilikuwa na lengo la kuwakutanisha wanawake wa kila dini,rika,rangi na wengine ikiwa ni kwa lengo la kuwakumbusha nafasi yao katika ufalme wa Mungu.

Kongamano hilo liliandaliwa na huduma ya Wamama kanisani hapo ikiongozwa na mmbeba maono Mwalimu Lilian Ndegi kwa msaada wa mme wake Apostle Onesmo Ndegi kiongozio wa huduma ya Living Water Centre Ministry.

Kongamano hilo huwa linalofanyika mara moja kila mwaka kanisani hapo kwa kusudi la kuwajenga Wanawake kuwa na uwezo katika kumtumika Mungu na kujua nafasi yao ya kutumika nafasi aliyowapa katika ufalme Mungu.

Kongamano hilo limefanyika baraka na msaada kwa wakina mama wengi Kuombewa na kwa kufundishwa kukabiliana na mazingira magumu na changamoto mbalimbali katika maisha kwa kujua nafasi yao Mungu aliyowapa na uwezo aliowapa kukabiliana na majukumu katika ngazi ya Familia,Huduma,Jamii na Taifa kwa ujumla.

Kongamano hilo lilikuwa na wazungumzaji kuoka baadhi ya nchi za Afrika Mch. Salome Mushi kutoka Botswana,Askofu Angela Acha Morfow kutoka Cameroom,Mch. Jael Tengu kutoka Nairobi Kenya na Mwenyeji Mwl.Lilian Ndegi.Waimbaji mbalimbali walikuwepo Women of The Kingdom,Living Waters,More than Enough Band na wengine wengi.
Mwenyeji Mwl.Lilian Ndegi

Askofu Angela Acha Morfow kutoka Cameroom
Mch. Jael Tengu kutoka Nairobi Kenya
Mch. Salome Mushi kutoka Botswana
Mch. Naomi Mhamba wa Living Water Center Tanzania
Wanaume wachungaji walikuwepo kuhudhulia Kongamano hilo





Wanenaji wa Kongamano la Mwanamke 2016 katika picha ya pamoja wa kwanza kushoto ni mwenyeji Mwl. Lilian Ndegi,Angela Morfaw kutoka Cameroon,Apostle Onesmo Ndegi mwenyeji,Jael Tengu kutoka Kenya na Salome Mushi Botswana.
Maombi na Maombezi kwa wenye magonjwa na uhitaji yalikuwepo .

Maombi na Maombezi kwa wenye magonjwa na uhitaji yalikuwepo .

Maombi na Maombezi kwa wenye magonjwa na uhitaji yalikuwepo

Wizara ya habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kuendelea kushirikiana na kampuni ya UK sport

$
0
0
 Waziri wa Habari, tamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye (kulia) akizungumza na mshauri wa maendeleo ya kimataifa wa kampuni ya Uk sport Bi.ClareBarell juu ya miradi mbalimbali ya maendeleo ya michezo na kumuomba mwakilishi huyo kuwekeza kupitia kampuni yao katika miundombinu ya michezo hapa nchini
 KatibuMkuuWizarayaHabari, Utamaduni,SanaanaMichezoProf.Elisante Ole Gabriel akizungumza jambo na mshauri wa maendeleo ya kimataifa wa kampuni ya Uk sport Bi.ClareBarell.Kampuni hiyo nimshirika wa Tanzania katika maendeleo ya Michezo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa katika picha ya pamoja namshauri wamaendeleo ya kimataifa wa kampuni ya Uk sport Bi.ClareBarell (wa pili kushoto) alipomtembelea ofisini kwake.Wengine pichani ni Kaimu mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bw.Alex Nkenyenge (wa pili kulia).

Waziri Mahiga afungua Mkutano wa Pili wa Vyama vya Kijamii vya ICGLR

$
0
0


Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Masahriki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (Mb.) akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Jukwaa la vyama visivyo vya Kiserikali (Vyama vya Kijamii), kutoka Nchi za Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) uliofanyika mapema leo katika Hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam. Katika ufunguzi huo Waziri Mahiga aliwashukuru wajumbe kwa kuchagua kuufanyia mkutano wao hapa nchini vilevile kuwa na ushirikiano katika masuala ya kijamii ambayo yatapelekea kuondoa machafuko ya wenyewe kwa wenyewe katika nchi wanachama.
Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza kwa makini Balozi Mahiga (hayupo pichani) alipokuwa akifungua Mkutano huo.
Sehemu nyingine ya wajumbe kutoka Sudan Kusini nao wakifuatilia kwa makini ufunguzi huo.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN eneo la Maziwa Makuu Balozi Said Djinnit naye alipata fursa ya kuzungumza katika ufunguzi wa mkutano huo.
Sehemu ya Watumishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa nao wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani), wa kwanza kulia ni Katibu wa Waziri Mahiga, Bw. Adolf Mchemwa, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kushoto) na katikati ni Afisa Mambo ya Nje, Bw. Ally Ubwa
Mwenyekiti wa Kikanda wa Jukwaa la Vyama visivyo vya Kiserikalikutoka nchi za Maziwa Makuu, Bw. Joseph Butiku naye akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano huo.
Mwakilishi wa Umoja wa Afrika eneo la Maziwa Makuu Bi. Altine Traore naye akizungumza
Meza kuu wakimsikilza Bi. Traore (hayupo pichani) alipo kuwa akitoa hotuba yake.
Waziri Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari.
Picha ya Pamoja.Picha na Reginald Philip

POLISI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA MTEJA.

$
0
0

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro (SACP) Ulrich Matei, akitoa neno mbele ya washiriki wa mkutano mkuu wa URA SACCOS (hawapo pichani) wakati akifungua mkutano huo wa siku mbili wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na mikopo, unaofanyika mkoani Morogoro.
 Washiriki wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na mikopo URA SACCOS Wakiimba wimbo wa maadili  kabla ya ufunguzi wa mkutano mkuu  wa siku mbili unaofanyika mkoani Morogoro.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro (SACP) Ulrich Matei, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa Chama cha Ushirika cha Kuweka Akiba na Mikopo (URA SACCOS) mara baada ya kufungua rasmi mkutano huo wa siku mbili unaofanyika mkoani morogoro huku ukiwashirikisha askari polisi kutoka mikoa yote Tanzania bara na visiwani.(Picha na Demetrius Njimbwi wa Jeshi la Polisi)

TANZANIA NA JAPAN KUANZISHA USHIRIKIANO KATIKA MATUMIZI YA TEHAMA.

$
0
0
Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (kushoto).

Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase (kulia) akizungumza na baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo upande wa Mawasiliano wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akisisitiza jambo alipokutana na  Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase. Bw. Toshio Nagase amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhusu namna Japan na Tanzania zinavyoweza kushirikiana katika masula ya TEHAMA.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO

Na. Aron Msigwa –MAELEZO
TANZANIA na Japan zinatarajia kuanzisha ushirikiano katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa kuwaunganisha wafanyabishara na vijana wanaojihusisha na masuala ya TEHAMA ili waweze kunufaika na fursa zilizopo katika nchi hizo.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase ambaye alimtembelea ofisini kwake kueleza nia ya Shirika lake na nchi ya Japan kutaka kuwekeza kwenye Sekta ya TEHAMA nchini Tanzania.

Amesema mara baada ya kukamilika kwa taratibu zote za ushirikiano katika sekta ya TEHAMA vijana na wafanyabishara wa Tanzania wataweza kushirikiana na vijana na wafanyabiashara kutoka Japan katika kubadilishana uzoefu na ujuzi katika masuala ya TEHAMA na kuwawezesha kujiajiri wenyewe au kuajiriwa ndani na nje ya nchi.

Prof. Kamuzora amesema  kuwa Tanzania na Japan kwa muda mrefu zimekuwa zikishirikiana katika masuala mbalimbali ya maendeleo kupitia miradi ya ushirikiano  hususan ujenzi wa miundombinu na masuala ya Ufundi.

Aidha, amesema kuwa Tanzania imekuwa ni nchi ya kuigwa duniani na kupigiwa mfano kwa kuwawezesha wananchi kupata huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia simu za mkononi na kufanya malipo mbalimbali.

“sisi kama Serikali tunawakaribisha wenzetu wa Japan kuja Tanzania kushirikiana nasi kuendeleza Sekta ya Mawasiliano na kuwekeza nchini kwetu ili wananchi wetu wanufaike na maendeleo ya Sekta hii kama ambavyo wenzetu wamepiga hatua kwa kuwa na kampuni za vifaa vya TEHAMA kama vile kampuni ya Sony”. Amesema Prof. Kamuzora.

Amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli imeweka msisitizo katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda kwa lengo la kukuza ajira miongoni mwa watanzania na kuongeza kuwa mkakati uliopo ni kuanzisha viwanda vya kuzalisha vifaa mbalimbali vya TEHAMA kwa kuwa Soko bidhaa hizo lipo.

Ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na JICA imejipanga kuwekeza katika Elimu,Ujuzi na Stadi kwa vijana ili waweze  kutengeneza Program za TEHAMA ambazo zinahitajika ndani na nje ya nchi hivyo kukuza uchumi miongoni mwa vijana hao.

Kuhusu kuwekeza katika Elimu katika masuala ya TEHAMA Prof. Kamuzora amesisitiza kuwa hakuna nchi iliyowahi kuendelea duniani bila kuwa na wabunifu wake wa ndani na kuongeza kuwa Tanzania sasa inao vijana wenye uwezo wanaofanya vizuri katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

“Dhana ya kutengeneza viwanda lazima ihusishe ubunifu wa kutengeneza Programu, hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa na wabunifu wa ndani tunachohitaji sasa ni uwepo wa vijana ambao wakao tayari ” Amesisitiza Prof. Kamuzora.

Prof. Kamuzora amesema Tanzania inazo fursa nyingi za kuwawezesha vijana ikiwemo uanzishaji wa viwanda vidogo na vya kati vya kutengeneza programu za TEHAMA hivyo ushirikiano ulioonyeshwa na JICA utawezesha  viwanda vya kutengeneza vifaa mbalimbali kuanzishwa kupitia wabunifu waliopo.
 “ Tanzania tunao vijana wabunifu wenye uwezo, kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) wameweza kubuni na kutengeneza teknolojia mbalimbali  kusaidia shughuli za Kilimo na uhifadhi wa Maliasili hapa nchini” Amesema.

Aidha, amesema Wizara kwa kushirikiana na JICA inafanya mpango wa kuwakutanisha wafanyabiashara; wawekezaji; kampuni; sekta binafsi na wadau mbalimbali wa Sekta ya Mawasiliano wa Tanzania na Japan ili kubadilishana uzoefu na kuainisha fursa na maeneo ya kushirikiana kwa lengo la kuendeleza sekta hiyo na ushirikiano wa nchi hizo mbili kwenye Nyanja ya TEHAMA.

Kwa upande wake mwakilishi Mkuu wa JICA nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase akizungumza mara baada ya kufanyika kwa mazungumzo hayo amesema kuwa Tanzania na Japan kwa miaka mingi zimekuwa na ushirikiano wa karibu katika masuala mbalimbali.

Ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua na kufanya vizuri katika matumizi ya TEHAMA kwenye huduma za fedha kwa njia ya Simu na kubainisha kuwa Japan inayo mengi ya kujifunza kupitia mafanikio haya.

Amesma JICA imejipanga kusaidia awamu ya pili ya program zao nchini Tanzania hususan kwenye Miundombinu, uwekezaji kwenye TEHAMA na masuala ya kiufundi katika maeneo mbalimbali ambayo miradi ya ushirikiano inatekelezwa.
Nagase ameeleza kuwa Japan imejipanga kushirikiana kikamilifu katika masuala ya TEHAMA hususan kuwawezesha vijana na wafanyabiashara wa Tanzania na Japan kubadilishana uzoefu, ujuzi, ufundi katika masuala ya TEHAMA.

Amebainisha kuwa Japan iko tayari kushirikiana na Sekta binafsi nchini Tanzania kupitia biashara na uwekezaji kwenye makampuni yanayojishughulisha na TEHAMA.

SPIKA AKUTANA NA KATIBU KUTOKA UMOJA WA MABUNGE KANDA YA MAZIWA MAKUU NA UJUMBE KUTOKA KOREA YA KUSINI

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai  akisalimiana na  Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe kutoka Korea Kusini ambaye pia ni Makamu wa Rais wa cha Chuo Kikuu cha Yeugnam cha Korea Kusini Prof. Choioe Choo aliyemtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo tarehe 8 Machi, 2016.

 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Ujumbe kutoka Korea Kusini akiwemo Kiongozi wa Msafara huo ambaye pia ni Makamu wa Rais wa cha Chuo Kikuu cha Yeugnam cha Korea Kusini Prof. Choioe Choo mwenye tai nyekundu. Ujumbe wa wageni hao ambao waliambatana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula.

 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Ujumbe kutoka Korea Kusini akiwemo Kiongozi wa Msafara huo ambaye pia ni Makamu wa Rais wa cha Chuo Kikuu cha Yeugnam cha Korea Kusini Prof. Choioe Choo mwenye tai nyekundu. Ujumbe wa wageni hao ambao waliambatana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akipokea zawadi kutoka kwa Kiongozi wa Ujumbe kutoka Korea Kusini ambaye pia ni Makamu wa Rais wa cha Chuo Kikuu cha Yeugnam cha Korea Kusini Prof. Choioe Choo mara baada ya kuzungumza nao ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiagana na Kiongozi wa Ujumbe kutoka Korea Kusini ambaye pia ni Makamu wa Rais wa cha Chuo Kikuu cha Yeugnam cha Korea Kusini Prof. Choioe Choo mara baada ya kuzungumza nao ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

 Spika wa Bunge akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Korea Kusini akiwemo Kiongozi wa Msafara huo ambaye pia ni Makamu wa Rais wa cha Chuo Kikuu cha Yeugnam cha Korea Kusini Prof. Choioe Choo mwenye tai nyekundu. Ujumbe wa wageni hao ambao waliambatana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Katibu wa Jukwaa la Umoja wa  Mabunge ya Ukanda wa Maziwa Makuu Mhe.Prosper Higiro aliyemtembelea  ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Spika wa Bunge Mhe Dkt Tulia Ackson akisalimiana na Katibu wa Katibu wa Jukwaa la Umoja wa  Mabunge ya Ukanda wa Maziwa Makuu Mhe.Prosper Higiro aliyemtembelea  Spika ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai  na Naibu Spika wa Bunge Mhe Dkt Tulia Ackson wakimskiliza  Katibu wa Jukwaa la Umoja wa  Mabunge ya Ukanda wa Maziwa Makuu Mhe. Prosper Higiro aliyemtembelea  Spika ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

 Spika wa Bunge akipokea zawadi kutoka kwa Katibu wa Jukwaa la Umoja wa  Mabunge ya Ukanda wa Maziwa Makuu Mhe. Prosper Higiro aliyemtembelea  Spika ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia pembeni ni Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson.
  1. Spika wa Bunge akipokea zawadi kutoka kwa Katibu wa Jukwaa la Umoja wa  Mabunge ya Ukanda wa Maziwa Makuu Mhe. Prosper Higiro aliyemtembelea  Spika ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Bunge)

TANZANIA NA JAPAN KUANZISHA USHIRIKIANO KATIKA MATUMIZI YA TEHAMA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase kuhusu Japan na Tanzania kushirikiana katika masula ya TEHAMA . Bw. Toshio Nagase amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora leo jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akisisitiza jambo alipokutana na  Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase. Bw. Toshio Nagase amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuhusu namna Japan na Tanzania zinavyoweza kushirikiana katika masula ya TEHAMA.

Na. Aron Msigwa - Dar es salaam. 

Tanzania na Japan zinatarajia kuanzisha ushirikiano katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa kuwaunganisha wafanyabishara na vijana wanaojihusisha na masuala ya TEHAMA ili waweze kunufaika na fursa zilizopo katika nchi hizo.


Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase ambaye alimtembelea ofisini kwake kueleza nia ya Shirika lake na nchi ya Japan kutaka kuwekeza kwenye Sekta ya TEHAMA nchini Tanzania.


Amesema mara baada ya kukamilika kwa taratibu zote za ushirikiano katika sekta ya TEHAMA vijana na wafanyabishara wa Tanzania wataweza kushirikiana na vijana na wafanyabiashara kutoka Japan katika kubadilishana uzoefu na ujuzi katika masuala ya TEHAMA na kuwawezesha kujiajiri wenyewe au kuajiriwa ndani na nje ya nchi.


Prof. Kamuzora amesema  kuwa Tanzania na Japan kwa muda mrefu zimekuwa zikishirikiana katika masuala mbalimbali ya maendeleo kupitia miradi ya ushirikiano  hususan ujenzi wa miundombinu na masuala ya Ufundi.Aidha, amesema kuwa Tanzania imekuwa ni nchi ya kuigwa duniani na kupigiwa mfano kwa kuwawezesha wananchi kupata huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia simu za mkononi na kufanya malipo mbalimbali.

“sisi kama Serikali tunawakaribisha wenzetu wa Japan kuja Tanzania kushirikiana nasi kuendeleza Sekta ya Mawasiliano na kuwekeza nchini kwetu ili wananchi wetu wanufaike na maendeleo ya Sekta hii kama ambavyo wenzetu wamepiga hatua kwa kuwa na kampuni za vifaa vya TEHAMA kama vile kampuni ya Sony”. Amesema Prof. Kamuzora.


Amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli imeweka msisitizo katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda kwa lengo la kukuza ajira miongoni mwa watanzania na kuongeza kuwa mkakati uliopo ni kuanzisha viwanda vya kuzalisha vifaa mbalimbali vya TEHAMA kwa kuwa Soko bidhaa hizo lipo.


Ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na JICA imejipanga kuwekeza katika Elimu,Ujuzi na Stadi kwa vijana ili waweze  kutengeneza Program za TEHAMA ambazo zinahitajika ndani na nje ya nchi hivyo kukuza uchumi miongoni mwa vijana hao.


Kuhusu kuwekeza katika Elimu katika masuala ya TEHAMA Prof. Kamuzora amesisitiza kuwa hakuna nchi iliyowahi kuendelea duniani bila kuwa na wabunifu wake wa ndani na kuongeza kuwa Tanzania sasa inao vijana wenye uwezo wanaofanya vizuri katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.


“Dhana ya kutengeneza viwanda lazima ihusishe ubunifu wa kutengeneza Programu, hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa na wabunifu wa ndani tunachohitaji sasa ni uwepo wa vijana ambao wakao tayari ” Amesisitiza Prof. Kamuzora.


Prof. Kamuzora amesema Tanzania inazo fursa nyingi za kuwawezesha vijana ikiwemo uanzishaji wa viwanda vidogo na vya kati vya kutengeneza programu za TEHAMA hivyo ushirikiano ulioonyeshwa na JICA utawezesha  viwanda vya kutengeneza vifaa mbalimbali kuanzishwa kupitia wabunifu waliopo.


 “ Tanzania tunao vijana wabunifu wenye uwezo, kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) wameweza kubuni na kutengeneza teknolojia mbalimbali  kusaidia shughuli za Kilimo na uhifadhi wa Maliasili hapa nchini” Amesema.


Aidha, amesema Wizara kwa kushirikiana na JICA inafanya mpango wa kuwakutanishawafanyabiashara; wawekezaji; kampuni; sekta binafsi na wadau mbalimbali wa Sekta ya Mawasiliano wa Tanzania na Japan ili kubadilishana uzoefu na kuainisha fursa na maeneo ya kushirikiana kwa lengo la kuendeleza sekta hiyo na ushirikiano wa nchi hizo mbili kwenye Nyanja ya TEHAMA.


Kwa upande wake mwakilishi Mkuu wa JICA nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase akizungumza mara baada ya kufanyika kwa mazungumzo hayo amesema kuwa Tanzania na Japan kwa miaka mingi zimekuwa na ushirikiano wa karibu katika masuala mbalimbali.


Ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua na kufanya vizuri katika matumizi ya TEHAMA kwenye huduma za fedha kwa njia ya Simu na kubainisha kuwa Japan inayo mengi ya kujifunza kupitia mafanikio haya.


Amesma JICA imejipanga kusaidia awamu ya pili ya program zao nchini Tanzania hususan kwenye Miundombinu, uwekezaji kwenye TEHAMA na masuala ya kiufundi katika maeneo mbalimbali ambayo miradi ya ushirikiano inatekelezwa.


Nagase ameeleza kuwa Japan imejipanga kushirikiana kikamilifu katika masuala ya TEHAMA hususan kuwawezesha vijana na wafanyabiashara wa Tanzania na Japan kubadilishana uzoefu, ujuzi, ufundi katika masuala ya TEHAMA.



Amebainisha kuwa Japan iko tayari kushirikiana na Sekta binafsi nchini Tanzania kupitia biashara na uwekezaji kwenye makampuni yanayojishughulisha na TEHAMA.


TANZANIA NA UGANDA KUJENGA BOMBA LA MAFUTA.

$
0
0
MKURUGENZI Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam amesema mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga utaanza mara baada ya hatua mbalimbali za mazungumzo kukamilika. 

Alisema ujenzi wa bomba hilo utagharimu dola za Marekani bilioni 4 na bomba litakuwa na urefu wa Km. 1,403 huku uwekezaji huo ukitarajiwa kutoa fursa za ajira zaidi ya watu 10,000 wakati wa ujenzi na watu wapatao 1,000 hadi 5,000 wakati wa kuendesha mradi. 

Alizitaja faida za mradi huo ni pamoja na fursa mbalimbali zikiwemo kuongeza wigo wa uwekezaji kwa TPDC na ajira kwa Watanzania pamoja na ushiriki wa kampuni za Kitanzania katika mradi huo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio akionesha katika ramani njia inayotarajiwa kujengwa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio akizungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu makubaliano ya Serikali ya Tanzania na Uganda kujenga bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania, kushoto ni Meneja Mawasiliano wa TPDC, Marie Msellemu.

WAANDISHI wa habari wanawake Mkoa wa Kigoma watoa msaada wa vitu mbali mbali wodi ya wazazi hospitali ya mkoa Kigoma.

$
0
0
Na Editha Karlo, wa blog ya jamii Kigoma.

WAANDISHI wa habari wanawake wa Mkoa wa Kigoma wametoa msaada wa vitu mbalimbali katika wodi ya wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani. 

Akiongea na mtandao huu kabla ya kukabidhi msaada huo Mratibu wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Kigoma Diana Rubanguka alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuungana na wanawake wote duniani katika kusherekea siku hii muhimu kwa kuwafariji wagonjwa hasa wazazi na watoto. 

Amewataka wanawake kujitambua, kujithamini na kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kujikwamua kiuchumi ili ifikapo mwaka 2030 ili waweze kufikia malengo ya kaulimbiu ya mwaka huu inayosema"KUFIKIA MALENGO YA 50 KWA 50 MWAKA 2030"

Naye Mganga mfawidhi wa hispital ya Mkoa wa Kigoma Dkt Fadhil Kibaya amewapongeza waandishi wa habari wa Kigoma wanawake kwa kitendo walichofanya cha kuwafariji wanawake waliopo hospital katika siku yao. 

"Mmefanya jambo zuri sana leo kuwa kumbuka akina mama wenzenu kuna wengine walikuwa hawajui kama leo ni siku ya wanawake Dunia"Alisema Dkt Fadhil.
Mwandishi wa blog ya michuzi Editha Karlo akimpatia zawadi mama aliyejifungua katika wodi ya wazazi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma baada ya kutoa msaada kwa wazazi katika hospital ya mkoa wa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Baadhi ya Waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma wakimtia moyo mmoja wa wazazi baada ya kutoa msaada kwa wazazi katika hospital ya mkoa wa Kigoma,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Baadhi ya Waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa msaada kwa wazazi katika hospital ya mkoa wa Kigoma,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Serikali ya Tanzania na afrika kusini zakubaliana kubadilishana uzoefu katika sekta ya Filamu.

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akifurahi jambo na Balozi wa Afrika kusini nchini Tanzania Bw.Thamsanga Mseleku alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Katika maongezi yao wamekubaliana kushirikiana katika masuala ya sekta ya filamu na hasa katika kubadilishana uzoefu katika mambo ya haki miliki na Sera.
Balozi wa Afrika kusini nchini Tanzania Bw.Thamsanga Mseleku akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na wizara ya habari,Utamaduni,Sanaa na michezo leo jijini Dar es Salaam.

…………………………………………

Na Daudi Manongi.

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo zimekubaliana kubadilishana uzoefu na mafunzo katika masuala ya filamu, haki miliki na Sera.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye alipokuwa akiongea na balozi wa afrika kusini nchini ofisini kwake jijini dar es Salaam.

Waziri nape amemwomba balozi uyo nafasi hiyo kwa sababu afrika kusini ipo vizuri zaidi na mbali katika sekta ya filamu na kwayo itakuwa nafasi nzuri kwa nchi izi mbili kukaa pamoja ili wabadilishane uzoefu na hasa suala la haki miliki na sera,kwani serikali yetu iko mbioni kutengeneza sera madhubuti ili sekta hii ya filamu iwe rasmi.

Alieleza kuwa ili tusonge mbele hatuna budi kuangalia kwa wenzetu wanafanyaje ili litatuongezea ujuzi na maarifa wakati tunajipanga na mengine kwani wageni sasa wameanza kuingia Tanzania kwa kuwa inafanya vizuri katika sekta hii ya filamu na ivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunatengeneza sera na mazingira madhubuti ili wakija wasiondoke.

Kwa upande wake Balozi wa Afrika kusini nchini Tanzania Bw. Thamsanga Mseleku ameishukuru serikali yake kuendelea kuimarisha mahusiano baina yao na amehaidi kufanikisha makubaliano ya kukutanisha wasanii kutoka afrika kusini na wa Tanzania ili wabadilishane uzoefu ili watoe kazi zenye viwango bora Zaidi ili kazi zao zifike mbali.

Makubaliano haya yamekuja baada ya wasanii wa filamu Single Mtambalike na Elizabeth Michael kushinda Tuzo katika Africa magic Viewer’s choice Awards na walipomtembelea ofisini kwake walimwomba waziri uyo mwenye dhamana kuwasaidia kutengeneza Sera madhubuti ili sekta hii iwe rasmi na wanufaike na jasho lao.

Ninawatakia wanawake wenzangu‎ Ulimwenguni kote, Heri ya Siku ya Mwanamke

$
0
0
Monica Joseph
 Mmiliki wa  Kampuni ya Monfinance Investment
 Group na Muwakilishi  wa Philips Tanzania.
"Wanawake Tunapashwa Kuona Jinsia yetu kama rasilimali na sio Dhima". ( Women should view their gender as a resource rather than a liability) - MJ.

Ningependa kutumia fursa hii kama Dada, Mke, Mama, mfanyakazi, Mwanaharakati na mjasiliamali kuwapongeza wanawake wote kwa kuadhimisha siku hii muhimu ya kuwaenzi wanawake wote ulimwenguni. 

Historia ya Maisha yangu, ni kielelezo cha maisha ya wanawake wengi ulimwenguni wanaopitia changamoto mbalimbali.‎ Nililelewa katika mazingira kandamizi ya Jinsia ya kike-kwenye jamii ambayo mtoto wa kiume alipewa nafasi ya kipekee katika masuala mbalimbali dhidi ya mtoto wa kike.Kwa mfano kipaumbele cha kupata elimu walipewa watoto wa kiume wakati watoto wa kike wakitarajiwa kushughulika na kazi za nyumbani, kupika,kuchota maji na kusaidia shughuli za kilimo na hatimaye kuolewa. 

Bibi yangu (Apumzike kwa Amani) alikuwa mhanga wa mfumo huo kandamizi. Kwa taabu alizopita Bibi yangu alijiwekea nadhiri kwamba Mjuu wake, hatopitia shida alizopitia yeye...na hivyo siku zote alikuwa akiniasa kwamba "Niyu (jina langu la nyumbani),Unaweza kila kitu kinachofanywa na mtoto wa Kiume". Aliniimarisha kifikra na kiakili. 

Na siku zote alikuwa na msemo wake "Niyu Kasome, Ukasome umshinde Babu yako, Usije kuwa unanyanyasika kama sisi"- ushauri wake ndio ulikuwa dira yangu ya maisha ambapo nilisoma kwa bidii na kufanikiwa kuhitimu shahada ya uzamili katika masuala ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Uingereza. 

Hadi hivi leo, sauti ya Bibi haijakoma masikioni mwangu, sijaacha kutafuta elimu na maarifa ya masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo katika jamii...ni kwa sababu hiyo nilipata mafunzo ya muda mfupi ya uongozi na majadiliano kutoka Chuo kikuu cha Harvard cha nchini Marekani. Nitaendelea kuitafuta Elimu na pia kusaidia wenzangu, sababu naamini moja ya njia ya Mwanamke kujikomboa katika ukandamizaji wa kijinsia ni kuongeza kiwango cha elimu kwake mwenyewe na kwa wanawake wenzake. 

 Waswahili wana msemo usemao maisha ni shule.....msemo huu nimeuishi katika maisha yangu ya baada ya masomo. Nimefanya kazi katika mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali na sekta binafsi. nimefanya kazi na taasisi ya ISHI iliyokuwa inashughulikia masuala ya Ukimwi, baada ya hapo nimefanya pia katika kampuni‎ ya Philips Medical Systems ya Uholanzi na baadaye nimefanya kazi kampuni ya mawasiliano ya Maktech. Kwote nilipopita nimekumbana na changamoto mbalimbali zilizohusiana na jinsia yangu.

 Utekelezaji wa majukumu yangu ulinilazimu kuwa na mikutano na watu mbalimbali Serikalini na kwenye taasisi za fedha ambapo watu niliokuwa nakutana nao ni wanaume ambao baadhi yao wamekuwa na mawazo ya mfumo dume yaliyojaa dharau na manyanyaso. Wengine kwenye fikra zao wanadhani mwanamke yeyote mwenye mafanikio, iwe kwenye biashara, siasa, ajira, lazima anabebwa na wanaume.‎ Wakiona mwanamke amefanikiwa tu, utasikia..huyu 'hawala wa fulani'. hii ni dhana potofu na inayolenga kumdhalilisha na kumnyanyasa mwanamke. Mimi binafsi sikukubali kuyumbishwa na watu wenye mawazo ya aina hiyo. 

Kila nilipokumbana na changamoto za aina hiyo nilipata hamasa ya kufanya kazi kwa bidii zaidi na kuwadhihirishia kwamba NINAWEZA, ilee sauti ya bibi ndioa ilikuwa ikinitia hamasa zaidi na zaidi na hatimaye kuniwezesha kufanya vizuri hadi kufikia kuaminiwa kupewa majukumu makubwa zaidi kama vile Mkurugenzi Mkuu katika kampuni ya Mokasi Medical Systems ambayo ni wakala wa kampuni ya Philips ya Uholanzi. Hasama hiyo iliniwezesha pia kuanzisha kampuni yangu inayotoa Huduma za kifedha - Monfinance Investment Group Ltd. 

Mbali na shughuli hizo nimeweza pia kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya FINCA Microfinance Tanzania. Kwa ujumla siku zote za maisha yangu nimejihusisha na harakati za kupigania haki za wenye shida na mahitaji katika jamii kutokana na msingi niliojengewa na bibi yangu wa kukataa unyonge na kusaidia wanyonge. Hurka hiyo ndio ilipelekea ajira yangu ya kwanza kuwa kwenye taasisi ya uhamasishaji wa masuala ya ukimwi ya ISHI. Niliguswa kujihusisha na kampeni hizo kwasababu binafsi nimepoteza ndugu, jamaa na marafiki kutokana na ugonjwa huo. Mbali na ISHI,nimekuwa nikijihusisha na kampeni ya kuzuia mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) iitwayo IMETOSHA.

 Ni jambo la udhalilishaji uliopitiliza kuwakata binadamu wenzetu viongo vyao kwa imani za kishirikina. Pia nimeshiriki kwenye uhamasishaji wa magonjwa yasiyojulikana (Rare diseases).‎ Tunaposherehekea siku ya Mwanamke duniani rai yangu kwa wanawake wenzangu, tushirikiane, tusaidiane, tupeane moyo na tuwezeshana ili tufikie lengo letu la usawa 50/50 kufikia mwaka 2030. Kila mwanamke atimize wajibu wake kwa kujitambua na kuhakikisha haki yake hainyongwi. ‎‎

Mimi nimejitambua, ninasimamia haki yangu, na wala siipiganii, ni yangu, Jinsia yangu hainitofautishi kiutendaji na jinsia ya kiume. Ninachoangalia ni Mchango wangu katika maendeleo ya Uchumi, jamii na familia na sio Jinsia yangu. Ninachotambua katika jinsia yangu ni kuwa mimi ni Dada, Mama, rafiki, na Mke. Mengine yote,nipo sawa na wote, wanaume na wanawake.‎ Happy Women's Day 2016.
a7caeb96fbdcd21385508290de4f359f"Wanawake Tunapashwa Kuona Jinsia yetu kama rasilimali na sio Dhima".  Women should view their gender as a resource rather than a liability) - MJ. 


CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE (TAWLA) CHAZUNGUMZA NA WANAHABARI NA KUELEZEA CHANGAMOTO ZINAZOKABILI WANAWAKE

$
0
0
1
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA Aisha Bade akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za shirika hilo zilizoko Ilala kuhusu kuadhiisha siku ya wanawake duniani pamoja na changamoto mbalimbali ambazo shirika hilo limepambana nazo katika kutetea haki za wanawake hapa nchini, kutoka kulia ni Tike Mwambipile Mkurugenzi wa TAWLA na katikati ni Amaria Marenji Mjumbe wa Kamati ya Uongozi TAWLA.
2
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA Aisha Bade akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za shirika hilo zilizoko Ilala kuhusu kuadhiisha siku ya wanawake duniani pamoja na changamoto mbalimbali ambazo shirika hilo limepambana nazo katika kutetea haki za wanawake hapa nchini, kutoka kushoto ni Nasieku Kisambu Mkurugenzi wa Miradi TAWLA na kulia ni Amaria Marenji Mjumbe wa Kamati ya Uongozi TAWLA.
4
Baadhi ya wakuu wa vitengo na maofisa wa TAWLA wakiwa katika mkutano huo.
5
Tike Mwambipile Mkurugenzi wa TAWLA akielezea jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.

...........................................
Kwanza kabisa, hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema na fadhila, kwa kutujalia uhai na afya njema na kutuwezesha kujumuika hapa leo kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Awali ya yote napenda kuwashukuru waandishi wa habari kwa kutenga muda wenu na kuwa nasi mbali na kuwa na shughuli nyingi. 

Natambua vyombo vya habari ni njia nzuri ya kufikisha ujumbe kwa haraka, lakini pia nyenzo muhimu katika kuhamasisha na kutetea upatikanaji wa haki za wanawake na watoto nchini.Napenda pia kushukuru wanachama, uongozi wa TAWLA pamoja na wafanyakazi mliopo hapa.

Ndugu waandishi wa habari, Siku ya Wanawake ilianza kuadhimishwa mwanzoni mwa miaka ya 1900 kwa kupitia wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani walioandamana kupinga mazingira duni ya kazi zao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira. Kutokana na hali hiyo, nchi ya Marekani ilikubali kuwa na siku ya maadhimisho ya kitaifa ili kutafakari masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wa wanawake. 

Baadaye Umoja wa Mataifa ulipaoanzishwa mwaka 1945 uliridhia siku ya tarehe 8 Machi iwe Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani. Uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa ulitokana na kukubali kwake kwamba masuala ya haki, maendeleo na usawa wa wanawake yalihitaji msukumo maalumu na wa pekee. Tanzania ilianza kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka 1996, maadhimisho yamekuwa yakiandaliwa Kitaifa na katika ngazi ya mkoa.

Katika kuadhimisha siku ya wanawake leo tarehe 8 March, 2016, TAWLA imeona ni vyema kushirikiana na vyombo vya habari kwa lengo la kuikumbusha jamii juu ya umuhimu wa usawa wa kijinsia. Kauli mbiu ya mwaka huu 2016, ni 50-50 ifikapo 2030, Tuongeze jitihada (Planet 50-50 by 2030: Step It Up for Gender Equality). Kauli mbiu hii inalenga katika kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali za Kimataifa/ kikanda na kitaifa zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia na wanawake katika kuhakikisha ushiriki wa wanawake kiuchumi, kijamii, na kisiasa unatambuliwa na kuheshimiwa na jamii kwa ujumla.

Ndugu waandishi, wanawake wanamchango mkubwa katika kuleta maendeleo has pale mazingira yanapowaruhusu. Ni kwa misingi hio basi, TAWLA inasisitiza kwamba kila Mtanzania anajukumu la kuweka mazingira ya usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana kushiriki katika masuala ya kiuchumi, elimu, ajira, siasa na sheria ifikapo mwaka 2030. Ni kutokana na misingi hio chama kinatoa ahadi zifuatazo.
TAWLA INAAHIDI:
  1. Kusaidia wanawake kufikia malengo
TAWLA inaahidi kudumisha uendelevu wa huduma za msaada wa kisheria kwa makundi maalumu. Hili linafanyika kwa wanachama kutumia taaluma yao ya sheria pamoja na sheria za nchi katika kuhakikisha haki inatendeka na hasa kusisitiza kutekelezwa kwa mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania imeridhiai. Katika hili tutaendelea kufanya ushawishi wa kurasimisha sheria zenye uwiano na usawa wa kijinsia.
  1. Kuondoa ubaguzi wa wazi na uliojificha.
TAWLA imegundua kwamba kuna changamoto kubwa katika ubaguzi na ukatili kwa wanawake na suala hili limekua ni tatizo hapa nchini. Ubaguzi na ukatili vimechangia sana katika kuwakwamisha wanawake kufikia ndoto na malengo yao. Ili kufanikisha hili Chama kinaahidi kuendelea kutoa elimu kwa jamii na kuendesha mikutano ya kubadili mitazamo kwa jamii dhidi ya wanawake.
  1. Wito kwa uongozi wa kijinsia na uwiano
Chama kinatambua uwezo wa mwanamke katika ngazi mbalimbali za uongozi kutoka kwenye kaya mpaka ngazi ya kitaifa. Ushiriki wa wanawake katika uongozi unawapa fursa ya kushiriki katika ngazi za maamuzi ambayo yanamanufaa kwa wanawake na wanaume kwenye jamii. Kwa misingi hio, chama kimeanzisha programu ya kuwakutanisha pamoja wanawake walioshika ngazi mbalimbali za uongozi nchini na ambao wanatarajia au ni wapya katika ngazi za uongozi kwa lengo la kuhakikisha kwamba wanakuwa viongozi wazuri, bora na wa kutegemewa lakini pia wenye kuleta mabadiliko katika jamii. Programu hii inalenga kuwashawishi wanawake mbalimbali kugombea ngazi za uongozi ili kuhakikisha kwamba masuala ya wanawake yanapewa kipaumbele.
  1. Kuthamini Usawa wa kijinsia kwa jamii.
Tutaendelea kuhamasisha jamaii kuhusu kuelewa kwamba usawa wa kijinsia sio suala la wanawake peke yao bali ni jukumu la kila mwanajamii na linahitaji ushirikiano kutoka kwa wanaume na wanawake pamoja na jamii kwa ujumla. “kwa kuongezea usawa wa kijinsia kutachangia kuboresha maisha ya wanawake na wasichana, familia, jamii na taifa kwa ujumla. Endapo vitendo vya ubaguzi wa kijinsia vitapigwa vita ina maana idadi ya watoto wa kike watakaokuwa wanaenda shule itaongezeka, familia zitakuwa na afya bora, uzalishaji katika kilimo utaongezeka na hivyo kipato kitaongezeka.
  1. Kujenga utamaduni chanya
TAWLA inatambua kwamba katika jamii zipo mila na desturi mbalimbali ambazo hutofautiana kutokana na mazingira. Aidha baadhi ya tamaduni hizo zimekuwa kikwazo kwa wanawake na wasichana kwa karne nyingi. Ili kujenga utamaduni chanya chama kimekua kikifanya uchechemuzi juu mabadiliko ya sheria kandamizi na kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kubadili mitazamo na tamaduni hasi ambazo ni kandamizi. Kwa kuisadia jamii kujenga mitazamo chanya Chama kimekuwa kikifanya mazungumzo na jamii katika mada mbalimbali kama vile madhara ya ndoa za utotoni, ukeketaji na ukatili wa kijinsia.
Chama katika kuadhimisha siku ya mwanamke dunia, itafanya shughuli zifuatazo;
  1. Itafanya mazungumzo na waandishi wa habari leo tarehe 8/3/2016.
  2. Kutoa msaada wa kisheria katika wilaya zote za Dar es salaam na katika ofisi zake za mikoani kwanzia tarehe 7/3/2016 mpaka 10/3/2016.
  3. Kufanya midahalo/ mazungumzo katika jamii.
  4. Kampeni ya kutumia mitandao ya kijamii kuhamasisha na kutoa elimu ya usawa wa kijinsia kwa mwezi mzima wa March.
Chama pia kitashirikiana na taasisi ya Wanawake wenye mafanikio (TWA), kwa kuhamasisha wanachama wake kushirikia katika shughuli zifuatazo;.
  1. Kushiriki katika matembezi ya kilomita sita ambayo yataanzia kwenye “Uwanja wa Mbio za Mbuzi”, Masaki, Dar es Salaam Jumamosi Machi 5, 2016
  2. Kushiriki katika Kongamano la Siku ya Kimataifa ya Wanawake litakaofanyika kwenye Hoteli ya Regency Kilimanjaro, Jumapili, Machi 6.2016.
Taarifa kwa wahariri:
TAWLA inatoa huduma zifuatazo
  1. Kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto, huduma hizo hutolewa Jumatatu na Jumatano kwa Dar es salaam na kila siku katika ofisi zetu mikoani – Tanga, Arusha, Dodoma, na Mwanza . Pia kupitia toll free number: 0800110017/ 0800751010

TPSF KUZINDUA MFUMO WA HABARI KWA AJILI YA WAFANYABIASHARA WADOGO

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara ndogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara. Kulia kwake ni Meneja wa Mradi Huo wa Habari, Celestine Mkama. Picha na Cathbert Angelo Kajuna.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa mfumo mpya wa habari uliobuniwa na taasisi hiyo kuwasaidia wafanyabishara ndogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara. Kulia kwake ni Meneja wa Mradi Huo wa Habari, Celestine Mkama. 

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imebuni mfumo maalum wa taarifa kupitia mtandao wa intaneti na simu za mkononi utakaotumiwa na wafanyabishara ndogo na wa kati kupata taarifa muhimu, ujuzi na huduma za maendeleo ya biashara. 

Mfumo huu utazinduliwa wiki ijayo jijini Dar es Salaam. Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amewambia waandishi wa habari kwamba ikiwa ni muendelezo wa jitihada za serikali ya awamu ya tano kuziwezesha biashara ndogo ndogo, kushawishi wananchi kuanzisha biashara na vilevile kurasimisha biashara hizo, mfumo huu utazisaidia biashara ndogo ndogo kutimiza malengo yake. 


 Alisisitiza kwamba mfumo huo wa habari ni wa aina ya kipekee kwani unawaruhusu watumiaji wa intaneti kupitia kompyta na simu kutumia na vilevile watumiaji wa simu zisizo na intaneti wataweza kutumia mfumo huu hususani katika kuboresha uelewa wa masuala ya fedha na ujuzi katika ujasiriamali huku ukiwawezesha wajasiriamali kujua namna ya kupata huduma sahihi za kifedha. Mfumo huu wa habari umetengenezwa mahususi ili kuwa kituo cha taarifa zote muhimu ambazo biashara ndogo inahitaji kuweza kukua. 

“Mfumo huu ni rafiki kwa mtumiaji, unapatikana kirahisi, na utawafikia walio na huduma ya intaneti na wasio na intaneti na umelenga katika kuwajengea uwezo wafanyabiashara kupitia taarifa mbalimbali muhimu kibiashara.” Simbeye alisema kuwa mfumo huo wa habari utapunguza vizingiti vya uelewa ambavyo vimekuwa vikifanya biashara ndogo zishindwe kupata huduma na bidhaa za kifedha zitolewazo na taasisi mbalimbali, na vilevile mfumo huu utawapatia wafanyabiashara ndogo jukwaa la kutoa maoni na kujadiliana masuala mbalimbali. Hii itasaidia katika kutengeneza sera ambazo zinakidhi mahitaji yao huku mfumo huo ukitoa mafunzo mbalimbali na nyenzo za kufanya biashara. Vilevile mfumo huu wa habari utasaidia kuanzishwa n kuendelezwa kwa mawazo mapya ya biashara na fursa mbalimbali, utaleta fursa kwa watoa huduma za fedha kupata taarifa za soko bure hususani kuhusu mahitaji ya wateja wao. 

 “Uboreshaji elimu kuhusu fedha na ujasiriamali kwa wafanyabiashara wadogo na wadau katika sekta ya ya fedha utasaidia kuleta tabaka la watumiaji huduma waelevu ambao watahitaji kupewa bidhaa na huduma zinazoendana na mahitaji yao ya muda mfupi na muda mrefu, wakati huo huo taasisi za kifedha zikishindana kubuni bidhaa na huduma zinazoendana na mahitaji ya wateja. Vilevile taasisi zinazosimamia huduma hizi na watunga sera wataweka mazingira mazuri kwa kila mdau kunufaika kutokana na huduma za mwenzake.

 Hii ni hali ambayo itampa faida kila mmoja ambapo waombaji mikopo wataweza kuchagua mikopo ipi inafaa kwa biashara zao jambo ambalo litapunguza uwezekano wa kushindwa kurudisha mikopo huku taasisi za kifedha zikiweza kutoa mikopo zaidi na kupata faida zaidi,” alisema. Meneja Mradi wa Mfumo huo wa Habari, Celestine Mkama alisema kwamba baadhi ya huduma muhimu zitakazotolewa na mfumo huo ni pamoja na muongozo kamili juu a kupata huduma za kifedha, kuanzisha biashara, kuendesha na kukuza biashara, msaada wa kitaalamu katika maeneo mbalimbali, majukwaa ya majadiliano, taarifa za masoko na uwezeshaji wafanyabiashara kuyafikia masoko hayo, taarifa za fursa mbalimbali pamoja na mafunzo mbalimbali kupitia mtandao ikiwa ni pamoja na utoaji habari za biashara kupitia machapisho na majarida mbalimbali. Mfumo huu wa habari pia utatoa muongozo wa mchakato wa kufanya biashara na sheria husika, taarifa za fedha za nje na utatoa mfano wa nyaraka za kuendesha biashara. Mkama pia alitaja baadhi ya huduma nyingine muhimu zitakazosaidia biashara kukua kuwa ni pamoja na mafunzo juu ya ujasiriamali kupitia mtandao, miundombinu ya kuwawezesha wafanyabiashara kufanya biashara kupitia mtandao ambapo wataweza kuuza bidhaa na huduma, na huduma ya mawasiliano ambapo wafanyabiashara wataweza kupatiwa majibu na wahusika kupitia mtandao. Vilevile Taasisi ya Sekta Binafsi itafanya vipindi vya redio na warsha za mafunzo zikiwahusisha zikiwahusisha wajasiriamali na wadau mbalimbali nchi nzima ili kuongeza uelewa kuhusu mfumo huu wa habari na kuwashauri wajasiriamali namna ya kuanzisha na kukuza biashara kufata misingi sahihi ya biashara.

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA TANO WA BUNGE LA AFRIKA YA MASHARIKI.

$
0
0
  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashriki, Kanda na Kimataifa, Balozi Augustino Mahiga akiapa kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki katika Mkutano wa Tano wa Bunge hilo uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim majliwa kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Machi 8, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akihutubia Mkutano wa  Tano wa Bunge la Afrika ya Mashariki kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Machi 8,2016
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge Job Ndugai wakiwa katika picha ya pamoja na Spikia wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Daniel Fredrick Kadega (katikati) baada ya kuhutubia Mkutano wa  Tano wa Bunge la Afrika ya Mashariki kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Machi 8,2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiteta na Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Daniel Fredrick Kadega baada ya kuhutubia Mkutano wa  Tano wa Bunge la Afrika ya Mashariki kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Machi 8,2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiteta na Mbunge  wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Shyrose Bhanji baada ya kuhutubia Mkutano wa  Tano wa Bunge la Afrika ya Mashariki kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Machi 8,2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WA MWEZI FEBRUARI, 2016 WAPUNGUA KWA ASILIMIA 5.6

$
0
0
 Mkurugenzi wa Takwimu za Sensa na Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Februari, 2016. Kulia ni Meneja Idara ya Ajira na Bei, Ruth Minja.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale.
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei katika Februari mwaka huu umepungua  mpaka kufikia asilimia 5.6  kutoka asilimia 6.5 ya  mwezi Januari.

Akizungumza  katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, Mkurugezi wa Sensa za Jamii, Ephraim Kwesigabo alisema kasi ya upunguaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka huu kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi za vyakula na bidhaa zisiyakula kwa kipindi kilichoishia  cha Februlia, 20 ikilinganishwa na bei za Februari mwaka 2015.


Alisema kuwa mfumuko wa bidhaa za vyakula na vinjwaji baridi kwa Februari mwaka huu umepungua kwa  asilimia 10.3, mafuta ya dezeli kwa asilimia 4.5  na matunda kwa asilimia 7.2.


Kwesigabo alisema pamoja na kupungua kwa  kasi  ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kuna baadhi ya bidhaa zinaonyesha  kuongezeka  katika hicho  ni pamoja na Sukari kwa asilimia 7.1, Mkaa asilimia 4.3, Mchele kwa asilimia 22.9 na viazi 16.3.



Aidha alisema hali ya mfumuko wa bei katika nchi za jilani unaelekea kufanana na nchi za afrika  mashariki ambapo Kenya umepungua hadi asilimia 6.84 kutoka  asilimi7.78 mwaka huu, Uganda umeongezeka kwa asilimia 7.7 kutoka  asilimia  7.6 kwa mwezi  Januari mwaka huu.

WAZIRI MKUU: RUSHWA YAPOTEZA DOLA BILIONI 150 AFRIKA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa Tano wa Bunge la Afrika ya Mashariki kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Machi 8,2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema tatizo la rushwa barani Afrika limesababisha bara hilo lipoteze dola za Marekani bilioni 150 kila mwaka.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Machi 8, 2016) wakati akihutubia wajumbe wa mkutano wa tano wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linaloendesha vikao vyake jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulioanza Machi 6, utamalizika Machi 18, mwaka huu.

Akizungumza kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema rushwa imechangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya Jumuiya hiyo. "Rushwa yaweza kuwa kwa njia kuhonga fedha, kupata fedha kwa kula njama, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, ama kwa njia za vitisho," alisema.

"Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Afrika (AU), rushwa na urasimu vimeainishwa kuwa ni vikwazo vikubwa vinavyochangia kuchelewesha ufanyaji wa biashara kwenye mipaka ya nchi za Jumuiya yetu," alisema.

Amesema sekta binafsi inachukuliwa kama injini ya maendeleo na ukuaji wa uchumi na akatumia fursa hiyo kuipongeza jumuiya ya wafanyabiashara wa Afrika Mashariki kwa kuandaa kanuni za kiutendaji  ambazo zimelenga kuhamasisha uadilifu kwenye ufanyaji biashara unaozingatia haki za binadamu, sheria za kazi, utunzaji mazingira na vita dhidi ya rushwa.

Akizungumzia kuhusu uondoaji wa vikwazo visivyohusisha kodi (non-tariff barriers) kama njia mojawapo ya kuimarisha biashara kwenye jumuiya hiyo, Waziri Mkuu alisema kwa upande wa Tanzania, vizuizi vya barabarani kwenye barabara kuu ya Kaskazini vimepunguzwa kutoka 50 hadi vitano.

Alivitaja vizuizi vitano vilivyobakia kuwa ni vile vilivyopo kwenye mizni ya Mikese (Morogoro), Nala (Dodoma), Njuki (Singida), Mwendakulima (Shinyanga) na Nyakahura (Kagera).

"Sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya uondoaji wa vikwazo visivyohusisha kodi ilipitishwa Machi 2015 na sasa hivi inaendelea kusainiwa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pamoja na mambo mengie, nia ya sheria hii ni kuondoa vikwazo vinavyosababisha uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, kurahisisha sheria za biashara ndani ya Jumuiya yetu," alisema.

Akizungumzia kuhusu miradi ya uwekezaji ya Jumuiya hiyo, Waziri Mkuu alisema miradi ya ujenzi wa barabara inahitaji kiasi cha dola za marekani bilioni 20; ukarabati na upanuzi wa njia za reli unahitaji dola za marekani bilioni 30; uendeshaji wa mashirika ya ndege na viwanja vya ndege unahitaji dola za marekani bilioni 15; uendelezaji bandari na usafiri wa majini unahitaji dola za marekani bilioni 10; utekelezaji wa miundombinu ya nishati inahitaji dola bilioni 5 ambavyo kwa pamoja vinahitaji dola marekani bilioni 80.

Alisema kuwepo kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi ndani ya jumuiya hiyo, kunaifanya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhesabika kuwa ni jumuiya yenye nguvu kubwa ya kiuchumi barani Afrika.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
JUMANNE, MACHI 8, 2016.

MGODI WA BULYANHULU WAALIKA WANAWAKE KUJIONEA UCHIMBAJI MADINI YA DHAHABU CHINI YA ARDHI

$
0
0
Mfanyakazi wa mgodi wa kuchimba dhahabu wa Bulyanhulu, unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, akiwa na baadhi ya akina mama sehemu ya uchimbaji chini ya ardhi (underground mining), wakati akina mama wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo na wafanyakazi wa kike walipotembelea ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake Duniani, leo Machi 8, 2016. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said) 


NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, Bulyanhulu

KATIKA kuadhimisha kilele cha siku ya Wanawake Duniani leo Machi 8, 2016, akina mama wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, unaomilikiwa na kampuni ya Acacia,huko wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, wao walitembelea na kuona shughuli za uchimbaji madini chini ya ardhi (Underground operations).

Akina mama hao kutka kada mbalimbali za vikundi vya wajasiriamali, wakulima, na viongozi wa dini, walifanya ziara ya kutembeela na kujionea shughuli za uchimbaji madini chini ya ardhi kiasi cha kilomita 2 kutoka uso wa ardhi, walieleza kufurahishwa kwao na kusema hata wao wanaweza.

Pamoja na maeneo waliyoyatembelea, walijionea mashine za kuchironga miamba, pamoja na karakana (gereji) ya kutengeneza magar na mashine zinazotumika kwenye eneo hilo. Ziara hiyo iliwachukua takriban masaa matatu (3), na bila kuchoka walikamilisha ziara hiyo na wote walikuwa katika hali nzur nay a furaha.

Katika tukio linguine, Mgodi huo ulimpatia kila mshiriki wa ziara hiyo, mche moja wa matunda ili wakapande kwenye maeneo wanayoishi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya mgodi kuhifadhi mazingira kwenye maeneo jirani na mgodi huo.

Siku ya wanawake Duniani, huadimishwa Machi 8 ya kila mwaka ili kuelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake na kutafuta majawabu yake.
Mama huyu ambaye ni sister wa kanisa Katoliki, alikuwa miongoni mwa wanawake waliotembelea mgodi huo chini ya ardhi
Ramadhani Chura, (kulia), mchimbaji wa madini chini ya ardhi, akiwapa maelezo akina mama hao umbali wa kilomita 2 kutoka uso wa ardhi
Mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu akimsaidia mama huyu kuvaa kibuyu cha gesi ya oxygen kabla ya kushuka chini ya ardhi
Mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu akimuwekea kibuyu cha gesi ya Oxygen mama huyu tayari kaunza safari chini ya ardhi.
Mkuu wa Uhusiano na mawasiliano wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, Mary Lupamba, (kulia), akimsaidia mama huyu kuweka sawa kibuyu chake cha gsi ya Oxygen ili kutembelea eneo la uchimbaji chini ya ardhi
Hapa akina mama wako chini ya ardhi umbali wa kilomita 2 kutoka uso wa ardhi, wakipatiwa maelezo ya namna miamba inavyochorongwa kuipata dhahabu
"Wanawake tunaweza". ndivyo inavyoonekana kwa mama huyu akidandia gari la oeperesheni za chini ya ardhi kwenye mgodi wa Bulyanhulu wakati akina mama wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo walipoadhimisha siku ya wanawake kwa kutembelea na kujionea kazi ya uchimbaji madini chini ya ardhi
Mwendesha mashine kubwa akiwa kwenye mashine yake
Mtaalamu wa kuchoronga miamba chini ya ardhi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, akiwapatia maelezo ya namna kazi hiyo inavyofanyika
Akina mama hao (kulia), wakiingia kwenye lango la kuelekea kupanda lifti ya kuwashusha chini ya ardhi
Hawa ndio akina mama shujaa waliomudu kutembelea mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu chini ya ardhi kujionea kazi ya uchimbaji madini inavyofanywa, wakiwa na baadhi ya wafanyakazi wanaohudumu kwenye eneo hilo.
Mary akiwaongoza akina maam hao katika hatuaya awali ya kuelekea kwenye ziara ya chini ya ardhi
Fundi mitambo akiwa kwenye karakana (gereji) ya magari na mashine zinazofanya kazi kwenye eneo hilo
Akina mama shujaa wakiwa katika picha ya pamoja
Baadhi ya akina mama wakiwa chini ya ardhi umbali wa kilomita 2 kuona kazi ya uchimbaji madini inavyofanywa
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images