Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Spika wa Bunge la EALA aziasa nchi wanachama kutumia Kiswahili katika kufanya kazi ndani ya Jumuiya.

$
0
0

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mhe. Daniel Kidega (kulia) akitoa taarifa ya Jumuiya hiyo mbele ya ya Wabunge wa Mabunge ya Afrika Mashariki leo Jijini Dar es Salaam kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu Jumuiya hiyo. Kushoto ni Mbunge wa Bungo hilo Mhe. Makongoro Nyerere.
Baadhi ya Wabunge wa Mabunge ya Afrika Mashariki pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wakati akisoma taarifa yake leo Jijini Dar es Salaam kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu Jumuiya hiyo.
(Picha zote na Benedict Liwenga)

Na. Benedict Liwenga.

NCHI wanachama wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wameaswa kuenzi lugha ya Kiswahili na kuifanya kuwa lugha ya kufanyia kazi katika Jumuiya hiyo.


Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Daniel Kidega alipofanya Mkutano uliowahusishwa Wabunge wa Mabunge ya Afrika Mashariki (EALA) lengo likiwa kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Jumuiya hiyo.


Mhe. Kidega ameeleza kuwa, lugha ya Kiswahili ina umuhimu mkubwa kwa Jumuiya hiyo ambapo ameshauri kuwa kuna haja ya kupitia katika Sheria ya Bunge hilo ili kuhakikisha kuwa Kiswahili na Kiingereza vinatumika ama kuzungumzwa kila mahali katika Afrika Mashariki.


‘’Tupate muda wa kutumia Kiswahili na kuhakikisha kuwa Kiswahili kinazungumzwa katika nchi zote za Afrika Mashariki kwani ni lugha ya Afrika na sisi ni Waafrika, hivyo tutafute namna ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya kufanya kazi kwa Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki,’’ alisema Kidega.


Aidha, Spika Kidega amegusia suala la watu wenye ualibino ambapo ameeleza kuwa, nchi wanachama hazinabudi kupiga vita masuala ya ukatili kwa watu wenye ualbino ambapo amezitaka Serikali wanachama wa Jumuiya hiyo kuhakikisha kuwa Albino wanaheshimika kama binadamu wengine na kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika wanaojihusisha na ukatili dhidi ya watu hao, kwani kwa kufanya hivyo kwa pamoja kutapunguza ama kuondosa changamoto zinazowakabili watu wenye ualbino.


Mhe. Kidega hakusita kuwapongeza Wabunge wanachama wa EALA waliohudhuria Semina ya Siku mbili (3 Machi- 4, 2016) iliyolenga kujadili masuala ya changamoto za uchaguzi kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo waliweza kujadili kwa undani baadhi ya changamoto za uchaguzi na madhimio mbalimbali yenye kuleta maendeleo katika Jumuiya hiyo.


Kwa upande mwingine, Mhe. Kidega amewaasa Wazanzibar ambao hivi karibuni wanaenda kupiga kura na kuwataka kufanya uchaguzi huo kwa uhuru na haki ikiwemo kudumisha amani ya Kisiwani humo pamoja na Tanzania kwa ujumla.


‘’Niwaombe Wazanzibar ambao mda si mrefu mnaenda kurudia uchaguzi wenu, tiini sheria za nchi, jitokezeni kupiga kura kwa wingi na hakikisheni kuwa mnafanya uchaguzi wenu kwa uhuru na haki ili kudumisha amani ya Tanzania, alisema Kidega.


Mhe. Kidega pia amewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya ambayo inabadilisha sura ya Tanzania pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kujituma kwao katika kuwatumikia watanzania wote.

Katibu Bodi ya Filamu awapokea washindi wa tuzo za filamu Bora Africa(AMVCA)

$
0
0
Katibu  Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi.Joyce Fissoo (kulia) akiwa na Ivone ‘Monalisa’ Cherry ambaye ameshiriki kucheza filamu iliyoshinda tuzo ya Filamu Bora yaLugha ya Kiswahili Afrika inayoitwa Kitendawili.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi.Joyce Fissoo (kushoto) akiwa pamoja na mshindi wa tuzo ya Filamu Bora ya Lugha ya Kiswahili AfrikaBw.Single “Richie”Mtambalike baada ya kuwapokea leo jijini Dar esSalaam.Richie amepata tuzo hiyo kupitia filamu ya Kitendawili ambayo amecheza naYvone“Monalisa”Cherry.

WANATABORA WAISHIO DAR WAPATA MWENYEKITI

$
0
0
Ndugu Imani Matabula akila kiapo mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja huo mbele ya Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huo Rukia Thabit.


Umoja wa wana Tabora waishio Dar es Salaam kupitia jumuiya ya Tabora Kwanza  jana tarehe 6 Machi wamefanya uchaguzi wa kwanza rasmi tangu jumuiya hii kusajiliwa na kumchagua Ndugu Imani Matabula kuwa Mwenyekiti wao kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa katiba. Jumuiya hii inajumuisha wilaya zote za Mkoa wa Tabora yaani Tabora Manispaa,Uyui,Sikonge,Urambo,Kaliua,Nzega na Igunga.


Wajumbe waliohudhuria  kilichofanyika kwenye hotel ya Lamada jijini Dar es salaam walikuwa 27 kati ya 32. Inahusisha waliozaliwa,kusomea,kuishi au kufanya kazi katika Mkoa wa Tabora na wale wenye mapenzi mema na Mkoa wetu wa Tabora. Karibuni tushirikiane. Umoja huo pia ulimchagua Jannat Mzee kuwa Makamu M wenyekiti na Idrisa Mangapi kuwa Mweka Hazina.
 Ndugu Imani Matabula akiomba kura kwa wajumbe
 Ndugu Imani Matabula akipiga kura yake wakati wa uchaguzi huo.

WADAU WAKUTANA

$
0
0
Sunday Shomari alipokutana na madam Rita Paulsen  hivi karibuni kwenye studio za BSS Mikocheni Daresalaam.

MFANYABIASHARA WA UTALII ARUSHA ATOA MISAADA YA KIJAMII HOSPITALI MKOA WA ARUSHA LEO.

$
0
0
Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet .c.Mfuko akizima mshumaa alipokuwa akiazimisha siku yake ya kuzaliwa iliyofanyikia katika hospitali ya mt.Meru jijini Arusha jana
Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet .C.Mfuko akikata keki alipokuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa iliyo fanyika katika hospitali ya mt.Meru iliyoko jijini Arusha jana.
Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet Mfuko akimlisha keki mkurugenzi mwenzake, ambae ni (mme wake) ndugu Kim Godwin Fute,alipokuwa akiazimisha siku yake ya kuzaliwa iliyo fanyika katika hospitali ya mt.Meru iliyoko jijini Arusha jana.
Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet Mfuko akimkabidhi shuka mganga mkuu mfawidhi wa hospital ya mt.Meru dr.Jackline Urio alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana.
Picha ya pamoja ya marafiki wa Violet ilipigwa.
Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Viola,Violet Mfuko akimuombea mgonjwa Frida Shayo alipotembelea hospitali ya mt.Meru alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana. 
Mkurugenzi Viola Mfuko anamlisha keki Habibya Fadhili alipotembelea hospital ya mt.Meru alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa jana.
********************
Katika kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani machi nane baadhi ya wanawake jijini Arusha wanaadhimisha siku hiyo kwa matukio mbalimbali ambapo mwanamke mjasiriamali wa jijini humo Violet Mfuko amejitolea kujenga sehemu ya kusubiria na kufanyia ibada katika mochwari ya hospitali ya mkoa wa Arusha ya mountmeru pamoja na mashimo nane ya vyoo katika sehemu hiyo.

Akiwa ameongozana na wakina mama wengine walianzia kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika wodi ya wanawake na watoto ambapo Viola anasema baada ya kutembelea sehemu ya mochwari katika hospitali hiyo aligundua changamoto hiyo ambayo ilimgusa na kuamua kujitolea kuanza ujenzi wa jengo hilo kuanzia jumatatu machi 7 ambalo litagharimu kiasi cha shilingi milioni 50.

Alisema ameamua kujikita katika kusaidia jamii badala ya kutumia fedha zake katika mambo ambayo hayana faida kwa jamii na kysisitiza kuwa baada ya kupewa ramani na uongozi wa hospitali ataanza ujenzi jumatatu machi 7 mwaka huu.

Alisema baada ya kujionea adha wsnayoipata wafiwa kukosa sehemu ya kusubiria miili ya marehemu na vyoo vinavyotumika kuwa ndani ya mochwari aliguswa na suala hilo na kuamua kujenga vyo na sehemu hiyo.

“Tayari nimeshapokea ramani nitaanza ujenzi jumatatu nawaomba wana Arusha mnipe ushirikiano tuweze kumsaidia rais magufuli yeye alianza na muhimbili sisi tumeamua kumsaidia hospitali yetu ya mkoa”alisema Violet.

Viola ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Viola car hire yenye makao makuu yake jijini Arusha anatumia siku yake ya kuzaliwa kutoa msaada katika hospitali hiyo na kutoa wito kwa wakazi wa mji wa Arusha kuanza kuisadia serikali kuboresha sekta ya afya kwa kuwa sekta hiyo inachangamoto nyingi.

“Mimi nikiwa ni mwanamke ninajua changamoto nyingi zinazotukaabili kina mama na watoto ambapo naamini ukimsaidia mama na mtoto umegusa jamii nzima”alisema Violet

Hata hivyo baadhi ya wajasiriamali wengine wa jijini humo wanaunga mkono jitihada za mwanamama huyo ambapo daktari Edmund Matafu anajitolea mashine mbili za hewa safi kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya muda yaani njiti.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa ya mountmeru Jackline Uriyo amemshukuru Violet na Dakta Matafu kwa msaada wao ambao amesema umefika wakati mwafaka.

“Kwa niaba ya uongozi wa hospitali ya mountmeru tunatoa shukrani za dhati kwa Viola na dakta Matafu tunawaomba waendelee na moyo huo lakini tunatoa wito kwa watu wengine wenye mapenzi mema kuisaidia hospitali ya mkoa kwani inalabiliw na changamoto nyingi”alisema Uriyo

Mbali na msaada huo Viola pia ametoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo mashuka mia mbili,sabuni,mchele,juisi soda mablanketi vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni kumi.

PROFESA MAKAME MBARAWA MGENI RASMI TAMASHA LA PASAKA KAHAMA

$
0
0
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 28 kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama Profesa Mbarawa amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo linashirikisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili.

Msama alisema Profesa Mbarawa kukubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ni ishara kwamba tamasha hilo halijaegemea upande mmoja wa dini kama inavyodhaniwa na baadhi ya wadau wa muziki huo.

“Tunampongeza Profesa Mbarawa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka, kwani huwa halijali dini, jinsia wala kabila katika utekelezaji wake,” alisema Msama.

Msama alisema hivi sasa kamati yake ya maandalizi inaendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha hilo ambalo litaanzia mkoani Geita Machi 26, Mwanza Machi 27 na kumalizia Kahama Machi 28.

Msama anataja viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na shilingi 2000 kwa watoto ambako kupitia tamasha hilo amepanga kugawa baiskeli za walemavu 100 kwa wakazi wa mikoa hiyo na kwingineko.

Waimbaji waliothibitisha kushiriki tamasha hilo ni Rose Muhando, Upendo Nkone, Joshua Mlelwa, Jesica BM, Christopher Mwahangila, Christopher Mwabuka, Jenipher Mgendi, Bonny Mwaitege, Goodluck Gozbert, Kwaya za Wakorintho Wapili ya Mafinga na AIC Makongoro Vijana ya jijini Mwanza na wengineo wengi.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MWAKILISHI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI UNHCR ANAYEMALIZA MUDA WAKE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR anayemaliza muda wake Bi. Joyce Mends-Cole Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR anayemaliza muda wake Bi. Joyce Mends-Cole Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU. 

Kampuni ya Chicco yatakiwa kukamilisha miradi ya umeme vijijini kwa wakati.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt.Medard Kalemani (mwenye suti nyeusi),  Mbunge wa jimbo la Magu Mhe. Desidery Kiswaga (kulia kwa Naibu Waziri) na watendaji wengine kutoka wilaya ya Magu wakitoka kukagua kituo cha Afya cha Kabila wilayani Magu ili kujionea endapo miundombinu ya umeme imefika ambapo Naibu Waziri aliagiza kituo hicho kiunganishiwe umeme ifikapo Jumanne ya wiki hii.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (mwenye suti nyeusi) akikabidhi kifaa kijulikanacho kama readyboard kwa Mbunge wa Magu, Desidery Kiswaga (katikati) ambacho hufungwa ndani ya nyumba na kuwasha umeme bila kusuka nyaya za umeme ndani ya nyumba.
Mbunge wa Magu, Mhe. Desidery Kiswaga (katikati) akiwaonesha wananchi wa kijiji cha Kikangama wilayani Magu, kifaa kijulikanacho kama readyboard mara baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (kushoto) kukabidhi kifaa hicho kinachowasha umeme bila kuhitaji kusuka nyaya za umeme ndani ya nyumba.

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MHE. BALOZI ENG. JOHN WILLIAM KIJAZI KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Eng. John William Herbert Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Kijazi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi wakwanza kushoto na Wamwisho kulia ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue pamoja na viongozi Wakuu wa Ulinzi na Usalama nchini.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha  na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. 
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha  na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU. 

kampuni mpya ya huduma za tiketi za ndege pamoja na Utalii ya SkyPalm Travel yazinduliwa

$
0
0
BALOZI wa Uturuki nchini Yesemin Eralp amezindua kampuni mpya ya huduma za tiketi za ndege pamoja na Utalii ya SkyPalm Travel and Tour Ltd.

Tukio hilo lilitokea jumamosi hii hapa jijini ambapo balozi huyo alitoa wito kwa wawekezaji zaidi kujitokeza kuwekeza kwenye sekta hiyo.

Alisema kuwa Tanzania imekuwa ikifanya vema kwenye sekta ya utalii huku ikiwa na vivutio vingi vya utalii vinavyovutia zaidi na kuwavutia watalii kutokea nchi mbalimbali. Aliongeza kuwa wageni kutokea nchi mbalimbali duniani wanahitaji huduma kutokea kwa kampuni bora zaidi itakayowahudumia kwa ufanisi na umakini.

Kwa upande wake Mkuu wa Biashara wa kampuni hiyo Meysun Buyuksarac alisema kuwa kampuni hiyo imelenga kuimarisha utoaji bora wa huduma za usafiri wa ndege pamoja na utalii nchini.

Alisema kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za utalii ambapo zimekuwa zikipelekea wageni wengi kujitokeza kuja nchini kutalii, na hivyo kupekekea wageni kutokea nje ya kuja kwa wingi na wao kama kampuni wamejipanga kutoa huduma bora zaidi ili kukidhi uhitaji.
sky palms launch-153
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Yesemin Eralp akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi kampuni mpya ya huduma za tiketi za ndege pamoja na Utalii ya SkyPalm Travel and Tour Ltd.
sky palms launch-146
Mkuu wa Biashara wa kampuni mpya ya huduma za tiketi za ndege pamoja na Utalii ya SkyPalm Travel and Tour Ltd, Meysun Buyuksarac akizungumza katika hafla hiyo.
sky palms launch-51
sky palms launch-147
Baadhi ya Wageni waalikwa.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, WAKUU WA WILAYA YA ILALA NA TEMEKE WATEMBELEA SHULE ZA MSINGI.

$
0
0
 Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha wamiliki wa Maroli Tanzania(TATOA) na Menejimenti leo iliungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Wakuu wa Wilaya wa Ilala na Temeke kutembelea shule za Msingi za Majimatitu, Mbande na kisongola ili kujionea hali halisi ya shule hizo na kujua changamoto mbalimbali wanazopitia.

 Hii ni katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa watoto wote wanapewa elimu ya msingi bure. Wanachama wataendelea kupatiwa utaratibu wa namna ya kushiriki kuchangia juhudi hizi.


Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha wamiliki wa Maroli Tanzania(TATOA) na Menejimenti leo iliungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick na Wakuu wa Wilaya wa Ilala, Raimond Mushi na Mkuu wa Wilaya ya Temeke walipotembelea shule za Msingi za Majimatitu, Mbande na kisongola ili kujionea hali halisi ya shule hizo na kujua changamoto mbalimbali wanazopitia.

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA MABALOZI OFISINI KWAKE.

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ufaransa Nchini Bi. Malika Berak aliyemtembelea Ofisini kwake kuzungumzia masuala ya mazingira na mashirikiano ya Nchi hizo mbili.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Balozi wa Ufaransa Nchini Bi. Malika Berak alimpomtembelea Ofisini kwake mtaa wa Luthuli. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu pamoja na Afisa toka ubalozi wa Ufaransa.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akichanganua jambo wakati akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida alimpomtembelea Waziri Ofisini kwake kuzungumzia na kushauriana juu ya programu ya kuteketeza taka hapa Nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwasikiliza kwa makini Wageni kutoka The Giants Club Keith Roberts (wa kwanza kulia) na mwingine kutoka Michael Foundation Jean du Plessis (katikati). Ujumbe huo ulimtembelea Waziri Makamba Ofisini kwake kujadili masuala ya mazingira.

WAFAMASIA WA BODI YA CHAKULA DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR WAPATIWA MAFUNZO JUU YA UDHIBITI WA DAWA.

$
0
0
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa Zanzibar Zaharani Ali Hamad akifungua mafunzo ya siku tano ya udhibiti wa Dawa kwa wafamasia wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar katika Ukumbi wa Ofisi za Malaria Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
Mrajis wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar ambae pia alikuwa mwenyekiti katika mafunzo hayo Dk. Burhani Othman Simai akiongoza mafunzo hayo.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya udhibiti wa Dawa Nasir Salum Buheti akiuliza swali na kutoa mchango wake katika mafunzo ya udhibiti wa Dawa.
Mkufunzi wa Usajili wa Dawa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) David Robert Matle akitoa mada kusu njia bora za Uagiziaji na udhibiti wa Dawa katika mafunzo yaliyoandaliwa na Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar.
Picha ya pamoja ya washiriki wa Mafunzo ya siku tano ya udhibiti wa Dawa, yaliyoandaliwa na Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

………………………………

Na Fatma Kassim

BODI ya Chakula Dawa na Vipodozi inajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa Dawa zinazoingia nchini ni salama na zinafaa kwa matumizi ya mwanadamu.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa Zahran Ali Hamad wakati akifungua mkutano wa siku tano wa udhibiti wa dawa kwa wafamasia wa hapa nchini. Amesema ni vyema wafamasia hao kutumia taaluma walinayo ili kuhakikisha wanadhibiti uingiaji wa dawa zisizo na viwango kwa lengo la kumkinga watumiaji na maradhi mbali mabali yanayotokana na dawa.

Amewataka wafamasia hao kuongeza jitihada katika suala zima la udhibiti wa dawa wakati zinapoingia nchini kwa kuwezesha kuepuka matatizo ya afya za wanaadamu.Alisema hivi sasa Tanzania ni miongoni mwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni vyema kuongeza ushindani wa utoaji wa huduma bora kwa jamii na kuhakikisha kuwa Zanzibar haiingizi dawa bandia.

Mrajis wa Bodi ya Chakula Dawa na vipodozi Dk Burhan Othman Simai amesema kuwa katika mpango mkakati wao ni kuwapatia mafunzo wafanyakazi wake ili kuweza kukabilina na mabadiliko yanayotokea ulimwenguni.Amefahamisha kuwa katika kukabilina na hali iliyopo hivi sasa ni vyema Serikali kuongeza wafanyakazi wa kada ya ufamasia ili kuweza kufanyakazi kwa ufanisi katika sehemu tofauti.

Alisema wataendeleza mafunzo kwa wafanyakazi wake ili kwenda sambamba na haja iliyopo na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.Mapema mkufunzi wa usajili wa Dawa kutoka Mamlaka ya Chakula Tanzania David Robert Matle amesema ni vyema dawa kuifanyia usajili kwa kutimiza vigezo vya ubora, usalama wa dawa hizo.

Amesema lengo la usajili wa dawa ni kuwalinda wanaadamu wasipate madhara yanayotokana na dawa.

WAZIRI MKUU AMPA ZAWADI YA LAPTOP MWANAFUNZI WA SHULE YA KATA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema shule za sekondari za kata zina fursa ya kufanya vizuri kama zilivyo shule nyingine licha ya kuwa watu wengi wamekuwa wakizidharau.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Machi 7, 2016) wakati akikabidhi zawadi ya kompyuta mpakato (laptop) kwa mwanafunzi aliyeshinda shindano la kuandika insha katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC ). Kompyuta hiyo ina thamani ya sh. 1,992,000/-.
Mwanafunzi huyo, Jabir Mandando (20),  amehitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Mbekenyera iliyoko wilayani Ruangwa mkoani Lindi. Amepata ufaulu wa daraja la pili na sasa anasubiri matokeo ya kujiunga na kidato cha tano. Lakini aliandika insha hiyo mwaka jana wakati akiwa kidato cha nne.
“Huyu ni mtoto wa kijijini tu. Anatoka kijiji cha Namilema wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi. Shule ya Mbekenyera aliyosoma ni shule ya kata. Ameweza kushinda tuzo na kushika nafasi ya tatu katika shindano lililoshirikisha shule nyingi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.”
“Jabir ameweza kuchomoza kitaifa kwa kushiriki shindano la kimataifa. Nimeamua kumpa zawadi yalaptop pamoja na begi lake ili aweze kujisomea  zaidi na kupata elimu ya masuala mbalimbali kwa kutumia kompyuta hii. Pia nataka iwe ni chachu kwa vijana wengine kushiriki mashindano kama haya,” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu pia alikabidhi Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Shanael Nchimbi fedha taslimu sh. 500,000/- zikiwa ni zawadi kwa ajili ya shule hiyo. mwalimu Nchimbi alimsindikiza mwanafunzi huyo Arusha kupokea zawadi hizo kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliomalizika Arusha wiki iliyopita.
Kwa upande wake, kijana Jabir alisema anashukuru sana kwa zawadi aliyopewa na kuahidi kuwa atajitahidi kusoma kwa bidii masomo ya kidato cha tano na sita ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa daktari.
Alipoulizwa alipataje taarifa ya uwepo wa shindano hilo, Jabir alisema: “Walimu walipata taarifa wakazileta darasani na kutuambia tushiriki kuandika. Walizikusanya na kuchagua tatu bora, ndipo yangu ikashinda.”
Amesema insha aliyoiandika ilihusu: “The importance of political stability in the East African Integration.”
Alimwonyesha Waziri Mkuu cheti na dola za Marekani 200 ambavyo alipewa zawadi kutokana na ushindi huo. Shule ya Mbekenyera ambayo alikuwa akisoma, pia ilizawadiwa laptop na printerkutokana na ushindi wa kijana Jabir.
Mshindi wa kwanza katika shindano hilo ametoka shule ya Sekondari Mzumbe, mshindi wa pili  alitoka Kenya na wa tatu alitoka shule ya Mbekenyera.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
  1. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
JUMATATU, MACHI 7, 2016.

NIDA YASITISHA MIKATABA YOTE YA WAFANYAKAZI WA MKATABA WALIOKO KATIKA OFISI ZAKE ZOTE


SERIKALI YAZISHAURI TAASISI ZA KIBENKI NCHINI KUWA NA VILABU VYA MICHEZO NA MASHINDANO

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imezishauri Taasisi za Kibenki zilizopo nchini kuanzisha timu na vilabu vya michezo ili kukuza michezo pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa vijana walio wengi ambao wana vipaji lakini hawana timu za kuwaendeleza.

Hayo yamebainishwa kupitia kwa Waziri mwenye dhamana, Mh. Nape Nnauye mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali ikiwemo tuzo za wachezaji bora walioshinda katika michezo maalum ya BRAZUKA KIBENKI iliyoandaliwa na benki ya Barclays na wadau wengine.

Waziri Nape amebainisha kuwa, Nia ya Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inakuza michezo na kuwa na fursa za kiuchumi kupitia michezo hivyo taasisi hizo zinazo fursa ya kuongeza ajira na ustawi mzuri wa michezo endapo zitaanzisha timu za michezo na kimashindano kwani zinaweza na zinao wajibu huo.

Kwa mujibu wa Mratibu wa michuano hiyo, Nasikiwa Berya alieleza kuwa, jumla ya timu 16 zilishiriki huku ikianza 28 Novemba 2015 na kufikia tamati 20 Februari 2016 ilikuwa ni ya aina yake na kutoa mwangaza wa kimaendeleo wa kimichezo ambapo pia imesaidia kuimarisha afya, ushikamano na undugu kwa baina ya wachezaji na washangiliaji ambao wengi wao walitoka katika mabenki shiriki 15 ikiwemo matawi yao ya Tanzania Bara na Visiwani.

Katika tukio hilo, washindi mbalimbali walipatiwa vyeti vya shukrani hii ni pamoja na wadhamini wa mashindano hayo ikiwemo kutoka mabenki, kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) na makampuni mengine walipewa vyeti vya shukrani katika kufanikisha michuano hiyo.
Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv)Nao
Mwakilishi kutoka MeTL Group, Bw.Zainul Mzige (kulia) akikabidhi cheti cha ushindi kwa Mchezaji Nuhu Mkuchu kutoka benki ya NMB.
nape bora
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akikabidhi tuzo ya golikipa bora, Gabriel Bernard.
Nape boraa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akikabidhi tuzo ya mfungaji bora mchezaji kutoka benki ya NMB, Ahmed Nassoro.
nape ddfBaadhi ya washiriki na wageni mbalimbali walifika katika tukio hilo...
nape ff
Mratibu wa michuano hiyo Brazuka Kibenki, Bi. Nasikiwa Berya akikabidhi cheti kwa mmoja wa washindi wa michuano hiyo..
nape fg
Mratibu wa michuano hiyo, Nasikiwa Berya akikabidhi cheti kwa mshindi..
nape h
Waratibu wa mashindano ya Brazuka Kibenki, Bi.Nasikiwa Berya akiwa na Raymond Bunyinyiga wakifurahia jambo kutoka kwa Waziri wa Habari, Nape Nnauye. (Hayupo pichani).
Nape mchezji
Waziri Nape akimkabidhi tuzo ya mchezaji Bora, Ahmed Nassoro.
nape na maliz
Rais wa shirikisho la Soka nchini, (TFF), Jamal Malinzi akikabidhi cheti cha ushind kwa moja ya washiriki wa michuano ya Brazuka Kibenki.
nape oo
Mratibu wa michuano hiyo, Nasikiwa Berya akikabidhi cheti kwa mshiriki..
nape rr
Baadhi ya washiriki..
nape vbc
zoezi likiendelea..
nape vbv
Utoaji wa vyeti ukiendelea..
Nape yu
Waziri Nape akimkabidho tuzo, Kocha Bora, Bw. Mohamed Hussen 'Machinga' ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa timu za Taifa na klabu kubwa za Tanzania ikiwemo Simba.
NAPE ZANI
Mwakilishi kutoka MeTL Group, Zainul Mzige akikabidhi cheti kwa mmoja wa washindi wa michuano ya Brazuka Kibenki. Zainul alikabidhi cheti hicho akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji 'MO'.
nape zx
Waziri Nape akimkabidhi cheti Rais wa TFF, Jamali Malinzi, ambapo cheti hicho ni maalum kwa TFF kuongeza mchango wao kaatika kukuza michezo nchini..
Nape4rt
Waziri Nape akitoa tuzo hizo..
Nape112
Waziri Nape akitoa tuzo hizo..
Nape112
Waziri Nape akitoa tuzo hizo..
Napecheti
Rais wa TFF akikabidhi tuzo hizo
naper tyu
Utoaji wa tuzo hizo ukiendelea..
napess
Waziri Nape akitoa tuzo hizo..
NAPESSS
wageni waalikwa na washiriki kutoka mabenki mbalimbali..
Napeww
Waziri Nape akitoa tuzo hizo..
Npaae
Mwakilishi kutoka MeTL Group, Zainul Mzige akitoa vyeti kwa washiriki
Npe2
Baadhi ya washindi walifanikiwa kutwaa tuzo hizo za Brazuka Kibenki kutoka benki ya NMB.
Npe222
Wachezaji bora 11, wakipata picha ya pamoja..
npe44
Waziri Nape Nnauye akitoa nasaha fupi katika tukio hilo..
Nape22
Mwandishi Mwandamizi wa habari wa mtandao wa Modewjiblog, Bw. Andrew Chale akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi kutoka MeTL Group, Zainul Mzige.
Npe33
Baadhi wa washriki na washindi wa Brazuka Kibenki..
Nape2
Hapa ilikuwa ni furaha kwa washiriki katika tukio hilo la Brazuka Kibenki..
Nape
Ilikuwa ni mwendo wa kucheza na kufurahia Kibrazuka..
Nape
Waziri Nape akipeana mkono naMwakilishi wa MeTL Group, Zainul Mzige katika meza kuu ya wageni waalikwa. Zainul Mzige alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa MeTL Group, Mohammed Dewji 'MO'.
Nape222
Baadhi ya washiriki wakipata picha za ukumbusho katika tukio hilo.

MSAADA KWA NDUGU YETU AHMED ALBAITY UNAHITAJIKA

$
0
0
albety
Ukiwa ndugu, jamaa na rafiki, bado mchango wako wa hali na mali unahitajika kwa ajili ya ndugu na mpendwa wetu, Ahmed Albaity (pichani) ilikuweza kuendelea na hali yake ya matibabu. Waweza kuhabarika zaidi kupitia taarifa hii ya video hapa chini. Karibuni sana.

UNDP WAFANYA KONGAMANO LA VIJANA, LENGO NI KUWASAIDIA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI

$
0
0
Hawa Dabo

Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la vijana na maendeleo, kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).


Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam limefanya kongamano la vijana na maendeleo kujadili jinsi vijana wanavyoweza kutumika kusaidia kuleta maendeleo nchini na kubadili mfumo wa vijana katika kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Akizungumzia kongamano hilo limelofanyika siku ambayo UNDP imetiza miaka 50 tangu kuanzishwa, Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP nchini, Amon Manyama alisema kuwa vijana wana nafasi kubwa katika jamii na kama wakitumika vizuri wanaweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo na hivyo kupitia kongamano hilo wanataraji kuwapa mbinu mpya.

Alisema mbali ya kuangala jinsi wanavyoweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo pia wanajadili kwa pamoja ili kuona jinsi gani wanaweza kubadili mfumo wa vijana wa kufanya maamuzi ambao wengi wao wamekuwa wakifanya maamuzi ambayo baadae yanaonekana kutokuwa sahihi.

“Tunafanya kongamano hili na vijana kutoka vyuo mbalimbali ili kuona mustakabali wa vijana wa Tanzania, kuona jinsi gani wanaweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo Tanzania na hata kubadili mfumo wao wa kufanya maamuzi,” alisema Manyama.
Youth and Development Symposium UNDP, Tanzania
IMG_5271
Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP nchini na mshereheshaji wa kongamano hilo, Amon Manyama akizungumza katika kongamano la vijana na maendeleo.

Nae Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo alisema vijana wana nafasi kubwa kusaidia uapatikanaji wa maendeleo nchini na wao kama UNDP wamekuwa wakisaidia na serikali ili kuwasaidia vijana kwa kuwapa mbinu ambazo wanaweza kutumia ili kufikia malengo waliyonayo.

Alisema licha ya kuwepo changamoto zilizopo katika sera ya vijana lakini pia vijana wamepoteza udhubutu wa kufanya maamuzi na hivyo kongamano hilo wanaweza kukuza uwezo wao wa kujiamini na kufanya maamuzi ambayo yanakuwa ni sahihi.

“Vijana wanatakiwa kuwa na malengo na kukuza uwezo wa kujiamini … vijana wanaweza kusaidia kupatikana maendeleo Tanzania na wana hamasa ya kusaidia kupatikana maendeleo hivyo wanatakiwa kupewa nafasi katika kufanya maamuzi,” alisema Bi. Dabo.
IMG_5296
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la vijana na maendeleo, kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
IMG_5323
Sehemu ya vijana kutoka vyuo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo wakati akitoa neno la ufunguzi wa kongamano hilo.

Kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Uchumi, Jehovaness Aikaeli alisema vijana wanaweza kutumiwa kama fursa hasa katika kipindi hiki ambacho kunakuwa na vijana wengi ambao wanatoka vijijini na kukimbilia mijini na hivyo kama wakishirikishwa wanaweza kusaidia kupatikana maendeleo.
IMG_5369
Mkuu wa Idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jehovaness Aikaeli akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano hilo.
Nae mmoja wa vijana aliyeshiriki katika kongamano hilo, Ncheye Revina alisema mifumo inayotumika sasa nchini inawabana vijana kusaidia kupatikana kwa maendeleo na kama watakuwa wanataka vijana wahusike kikamilifu basi wawatolee vikwazo vinavyowabana kushiriki akitolea mfano katika ajira kwa ajili wengi kutaka wafanyakazi walio na uzoefu mkubwa wa kazi jambo ambalo ni ngumu kupata vijana.
IMG_5571
Mmoja wa vijana aliyeshiriki katika kongamano hilo, Ncheye Revina.
IMG_5413
Benedict Kikove kutoka Ubalozi wa Japan nchini akiwaelezea vijana fursa zilizopo kwa vijana na changamoto wanazokumbana nazo wakati wa kongamano la vijana na maendeleo lililoandaliwa na UNDP.
IMG_5450
Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), Stella Karegyesa akifuatilia kwa makini kongamano la vijana na maendeleo.
Hawa Bayumi
Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) nae alikuwa ni miongoni mwa watoa mada katika kongamano hilo.
IMG_5666Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama (wa kwanza kulia) akifuatilia kilichokuwa kikiendelea katika kongamano hilo lililoandaliwa na UNDP.
IMG_5394Fatma Mohamed kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV) akizungumzia changamoto wanazokutana nazo vijana katika kutafuta mafanikio.
IMG_5507Mwakilishi wa Wizara ya Katiba na Sheria kutoka Zanzibar, Saleh Mubarak akielezea washiriki jinsi serikali inavyowasaidia vijana katika kongamano la vijana na maendeleo.
IMG_5390
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo ambao ni vijana na wadau kutoka mashirika na taasisi mbalimbali nchini lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Youth Symposium -UNDP Tanzania
Youth Symposium -UNDP Tanzania
IMG_5679
Afisa wa Utawala Bora kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Godfrey Mulisa akielezea jinsi washirika wa maendeleo wanavyotoa fursa kwa vijana na jinsi fursa hizo zinavyoweza kuwasaidia vijana wa Tanzania.
IMG_5687
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Natalia Kanem akizungumza wakati wa kongamano hilo.
IMG_5749
Pichani juu na chini ni vijana kutoka vyuo mbalimbali nchini wakishiriki kutoa maoni kwenye kongamano hilo.
Youth Symposium -UNDP Tanzania
IMG_5796
Makamu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Titus Osundina akitoa neno la hitimisho la kongamano la vijana na maendeleo.

Bagamoyo wapokea vizuri mradi wa viwanja vya Bayport

$
0
0
Meneja wa Bayport wilayani Bagamoyo, Francis Ndunguru, akizungumza na waandishi wa Habari walipotembelea mradi wa viwanja vya mikopo vinavyotolewa na taasisi yao, katika eneo la Kimara Ng'ombe, Bagamoyo, mkoani Pwani jana. Picha zote na Mpiga Picha Wetu, Bagamoyo.
Meneja wa Bayport Financial Services wilayani Bagamoyo Francis Ndunguru akionyesha alama za viwanja vilivyopimwa katika eneo la mradi wa Kimara Ng'ombe, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani. Viwanja hivyo vinauzwa kwa mkopo kwa watu wote wenye kuhitaji kumiliki ardhi.

Meneja akionyesha barabara zilivyochongwa kuonyesha ubora wa mradi huo wa Bagamoyo, mkoani Pwani.
Mwandishi wa habari Phillip Daud, akimhoji mwananchi wa Bagamoyo, Mwanaisha Khalfany juu ya ubora wa viwanja hivyo na uwezekano wa Watanzania hususan wakazi wa Bagamoyo kuvichangakia viwanja hivyo vilivyopimwa na vyenye hati.



WAKAZI na wananchi wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, wamepokea vizuri mradi wa viwanja vya mikopo vinavyotolewa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, wakisema kuwa mradi huo utachangia kwa kiasi kikubwa kuupanua na kuuweka mji wao katika kiwango cha juu kimaendeleo.


Kwa mjini Bagamoyo, mradi huo wa viwanja vya Bayport unapatikana Kimara NG’ombe, huku maeneo mengine ya nchi viwanja hivyo vikipatikana KIbaha, Chalinze, Morogoro, Kilwa na KIgamboni, vikihusisha watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali.


Akizungumza na mtandao huu, mkazi wa Bagamoyo, Said Juma, alisema kwamba huduma za viwanja vya Bayport vinavyopatikana kwa fedha taslimu na mikopo si vya kukosa, kwa sababu zitachangia kuuweka mji wa Bagamoyo kwenye kiwango cha juu pamoja na kujibu malalamiko ya wananchi kushindwa kumiliki viwanja kwa njia rahisi na isiyokuwa na gharama kubwa.

“Uwezekano wa kumiliki viwanja Bagamoyo mjini ni mgumu kwa sababu vinauzwa bei ghari, hivyo kwa Bayport kuanzisha huduma hizi kwa watu wote bila kusahau sisi wajasiriamali, hakika ni jambo la kushukuru na kuwapongeza kwa mawazo yao mazuri yenye kutuendeleza sisi wananchi na wateja wao,” alisema Juma na kuwataka watu wa Bagamoyo na Watanzania wote kuchangamkia fursa hizo.

Mwananchi mwingine aliyekutwa kwenye mradi huo, Bi Mwanaisha Khalfany Sultan, alisema kwa kuanzisha mradi huo wa viwanja mji wao wa Bagamoyo utapanuka na kuongeza idadi ya watu wilayani humo.

“Tunafurahia kwa kiasi kikubwa mno kupata mradi huu wa mikopo ya viwanja vya Bayport tukiamini mji wetu utapiga hatua kubwa, hivyo tunawaomba kila mwenye uwezo wake na hitaji la kujenga achangamkie fursa hii muhimu kwa Watanzania wote, ukizingatia kuwa rasilimali ya ardhi ni muhimu na imekuwa ikiongezeka thamani kwa haraka nchini kote, huku katika eneo la mradi wa Kimara Ng’ombe mahitaji ya maji, umeme na barabara yakipatikana kwa urahisi,” alisema Mwanaisha.

Naye mwananchi Patrick Mwilongo, aligusia ubora wa mradi wa viwanja vya Kimara Ng’ombe akisema kuwa utakuwa umejibu swali na malalamiko ya wanasiasa waliokuwa hawataki Bagamoyo iingie kwenye Mamlaka ya Mji mdogo kwa madai kuwa mji utakuwa mdogo, ukizingatia kuwa endapo eneo hilo litajengwa mji huo utakuwa mkubwa na utapiga hatua kubwa kimaendeleo.

“Ni miongoni mwa wadau muhimu wa hapa Bagamoyo ambao hakika tumeendelea kuthamani mradi huu kwa sababu utakuwa na tija kwetu sote, hivyo ni wazi tunapaswa kujitokeza kupata viwanja hivi ili tujenge kwa sababu uwezo wa kununua kiwanja kwa fedha taslimu kwa baadhi yetu ni mgumu, ukizingatia kwa masharti nafuu unaweza kupata kiwanja kwa kukopeshwa na Bayport.



Naye Meneja wa Bayport wilayani Bagamoyo, Francis Ndunguru, alisema kwamba lengo ni kusudio lao kuu kuona mji wa Bagamoyo unakuwa na wananchi wanamiliki viwanja hivyo kwa utaratibu rahisi, hivyo ni budi kutembelea kwenye tawi lao la MJini Bagamoyo pamoja na matawi yote Tanzania ili kupata viwanja hivyo kwa ajili ya kuweka makazi ya kifamilia, kibiashara na mengineyo.

“Tunawaomba Watanzania wote popote walipo kutembelea ofisi zetu au mawakala wetu walionea nchi nzima ili wapate fursa ya kukopa viwanja hivi kwa mji wa Bagamoyo au vilivyopo kwenye maeneo mengine ya Tanzania, tukiamini Bayport imeendelea kuwa mkombozi wa watu wote kwa kumiliki kiwanja kwa utaratibu rahisi,” alisema Ndunguru, Meneja wa Bayport Bagamoyo.

Mita Moja ya mraba kwa viwanja vya Bagamoyo inapatikana kwa Sh 10,000, Kigamboni (Tundi Songani) Sh 10,000, Kibaha (Boko Timiza) Sh 9000, Kilwa (Msakasa) Sh 2000, Morogoro (Kiegea B) Sh 3500, Chalinze (Kibiki na Mpera) Sh 4500 tu, huku utaratibu wa kuweza kupata viwanja hivyo ukiwa rahisi kwa Watanzania wote, wakiwamo waaajiriwa wa serikali, waajiriwa binafsi na wajasiriamali.

Waziri Mahiga ashiriki ibada ya kumuaga Marehemu Balozi Rwegasira

$
0
0


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga akitoa pole kwa niaba ya Wizara kwa familia ya aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Marehemu Balozi Joseph Rwegasira wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Jijini Dar es Salaam.Balozi Mahiga alimwelezea Marehemu Balozi Rwegasira kuwa alikuwa kiongozi hodari wa kupigiwa mfano kutokana na moyo wake wa kufanya kazi kwa bidii na kujituma.
Ndugu na jamaa waliohudhuria ibada hiyo wakimsikiliza kwa makini Waziri Mahiga (hayupo pichani).
Sehemu nyingine ya watu waliohudhuria ibada hiyo .
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba naye alipata fursa ya kutoa neno la pole kwa familia ya Marehemu Balozi Rwegasira.
Mmoja wa wanafamilia ya Balozi Rwegasira akisoma utaratibu wa kutoa heshima za mwisho za kuuaga mwili wa Balozi Rwegasira .
Sehemu ya Viongozi wa Serikali na Vyama vya Kisiasa wakisikiliza utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Balozi Rwegasira.
Waziri Mahiga akimpa mkono wa pole Mama Rwegasira .
Waziri Mahiga pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Mlima wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Bolozi Rwegasira .
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakitoa mkono wa pole kwa familia ya Balozi Rwegasira .
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images