Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 786 | 787 | (Page 788) | 789 | 790 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akimkabidhi nyaraka za gari la wagonjwa la Kituo cha Afya cha Murangi, Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Dkt. Naomi Nyanchara.
  Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akifungua mlango wa gari la wagonjwa kabla ya kulikabidhi rasmi.
  Daktari Bingwa wa huduma za dharura na Majanga, Dkt. Christopher Mnzava (kulia) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi gari la wagonjwa la Kituo cha Afya cha Murangi. Kushoto ni Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo


  0 0

  KUELEKEA siku ya wanawake duniani  wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la Water front jijini Dar es Salaam leo wametoa msaada wa vitu mbalimbali pamoja na fedha katika taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwasaidia baadhi ya wagonjwa waliopo katika hospitali hiyo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufika katika Taasisi ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road  jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya kutoa masaada wa vitu mbalimbali.
  Baadhi ya vitu vilivyotolewa na wafanyazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam. 
   Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam.


  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam wakitoa vitu kwenye gari kwaajili ya kutoa msaada katika Taasisi ya magonjwa ya Saratani  Ocean Road jijini Dar es Salaam leo.
  ......................................
  Hata hivyo wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam wametoa elimu kwa wafanyakazi na wanakikundi cha  'The Great Ten'wa Kampuni ya Busines Times jijini Dar es Salaam kuhusiana na kufungua Akaunti ya MALKIA katika benki hiyo kwa kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo kilele cha maadhimisho ya siku hiyo ni Machi 8 kwa kila mwaka.
  Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam, Adam Akaro (kulia) akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya Business Times wanaounda kikundi cha 'The Great Ten', kuhusiana na huduma wanaozitoa benki hiyo kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo kilele chake ni Machi 8 kwa kila mwaka.  
   Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam, Adam Akaro (kulia) na Meneja wa huduma kwa mteja wa benki ya CRDB tawi la water Front jijini Dar es Salaam wakiwa katika kikao na wafanyakazi wa wafanyakazi wa kampuni ya Business Times wanaounda kikundi cha 'The Great Ten'.
  Mwanachama wa kikundi cha 'The Great Ten', Sebastian Sungi akifafanua jambo katika kikao kilichofanyika katika ofisi za  kampuni ya Business Times wanaounda kikundi cha 'The Great Ten'. Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam, Adam Akaro (kulia) na Meneja wa huduma kwa mteja wa benki ya CRDB tawi la water Front jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa kikundi cha 'The Great Ten', Grace Ndossa akichangia maada katika kikao kilichofanyika katika ofisi za kampuni ya Business Times na wanakikundi cha 'The Great Ten' walipokuwa wanazungumza na  Meneja wa huduma kwa mteja wa benki ya CRDB tawi la water Front jijini Dar es Salaam wakiwa katika kikao na wafanyakazi wa wafanyakazi wa kampuni ya Business Times wanaounda kikundi cha 'The Great Ten'.
  Baadhi ya wafanyakazi wa wafanyakazi wa kampuni ya Business Times wanaounda kikundi cha 'The Great Ten'.wakimsikiliza 
   Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam, Adam Akaro jijini Dar es Salaam leo.

  0 0


  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba akiangalia baadhi ya sampuli za mifuko isiyoharibu mazingira ambayo inatengenezwa na Umoja wa Watengeneza mifuko isiyoharibika Tanzania (UWAMITA) Kulia  ni Mwenyekiti wa kikundi hiko Jumanne Mgude.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba, akiongea na Wanakikundi wa Umoja wa Watengeneza Mifuko isiyoharibika Tanzania (UWAMITA) walipomtembelea Ofisini kwake mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Mwalimu wa Chuo cha Zenith Learning Center Ali Mussa Mohammed, akizungumza kabla ya kuaza Mahafali ya Nne ya Chuo hicho yaliofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho Majestik Zanzibar jengo la Zanlink,Jumla ya Wahitimu 28 wametunikiwa Vyeti vyao na Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib.
  Mkuu wa Mafunzo wa Chuo cha Zenith Learning Center Mundhir Nassor akitowa maelezo ya Kozi zinazotolewa na Chuo hicho kwa mgeni Rasmin kabla ya kuzungumza na wahitimu na kuwakabidhi vyeti vyao, Chuo hicho kinatowa Kozi ya Kimataifa ya Ukataji wa Tiketi za Ndege kwa Njia ya Kielectoniki
   (GALILEO  RESERVATION SYSTEM) 
  Wahitimu wa Mafunzo hayo wakiwa ukumbi wa Mahafali hayo ya yaliofanyika katikav Ukumbi wa Chuo hicho Majestik Zanzibar jengo la Zanlink 
  Mgeni Rasmin wa Hafla hiyo ya Mahafali ya Nne ya Chuo cha Zenith Learning Centr akiwa na Viongozi wa Chuo hicho wakati wa Mahafali hayo yaliofanyika katika Chuo hicho Zanzibar. 
  Mwakilishi wa Travelport Zanzibar Ndg Rashid Ntalaluka akizungumza wakati wa mahafali hayo ya Nne ya Chuo hicho kwa Wahitimu wa Kozi ya Kimataifa ya kutowa huduma ya Ukataji wa Teketi kwa Njia ya Kieletroniki (Galileo Reservation System) na kuwaasa Vijana hao kutumia mafunzo hayo kwa utaalamu wa hali ya juu. 
  Mkurugenzi wa Zenith Tours& Travel Ndg Salim M Suleiman, akitowa nasaha zake kwa wahitimu hao wakati wa mahafali hayo ya Nne ya Chuo hicho yaliofanyika katika ukumbu wa chuo hicho jengo la Zanlink Zanzibar.
  Wahitimu wa Mafunzo hayo wakiwa ukumbi wa Mahafali hayo ya yaliofanyika katikav Ukumbi wa Chuo hicho Majestik Zanzibar jengo la Zanlink 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wahitimu hao wa Mafunzo ya Ukataji Tiketi kwa Njia ya Kielectoniki(Galileo Reservation System) kuyatumia mafunzo hayo kwa ukamilifu wakati wa kutowa huduma kwa wataja wao wanapofika kupata huduma hiyo. , 
  Wageni waalikwa katika Mahafali hayo wakiwa katika ukumbi wa hafla hiyo.
  Wahitimu wakiwa katika ukumbi wa hafla hiyo ya mahafali ya Nne ya Chuo hicho.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akimkabidhi mmoja wa Wahitimu hao Cheti chake baada ya kumaliza Kozi ya Ukataji wa Tiketi kwa Njia ya Kieletroniki, kulia Mkurugenzi Mkuu wa Zenith Tour & Travel Ndg Salim M Suleiman, na kushoto Mkuu wa Chuo hicho Ndg Mundhir Nassor.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akimkabidhi mmoja wa Wahitimu hao Cheti chake baada ya kumaliza Kozi ya Ukataji wa Tiketi kwa Njia ya Kieletroniki, kulia Mkurugenzi Mkuu wa Zenith Tour & Travel Ndg Salim M Suleiman.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akimkabidhi mmoja wa Wahitimu hao Cheti chake baada ya kumaliza Kozi ya Ukataji wa Tiketi kwa Njia ya Kieletroniki, 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akimkabidhi mmoja wa Wahitimu hao Cheti chake baada ya kumaliza Kozi ya Ukataji wa Tiketi kwa Njia ya Kieletroniki, kulia Mkurugenzi Mkuu wa Zenith Tour & Travel Ndg Salim M Suleiman.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akimkabidhi mmoja wa Wahitimu hao Cheti chake baada ya kumaliza Kozi ya Ukataji wa Tiketi kwa Njia ya Kieletroniki, kulia Mkurugenzi Mkuu wa Zenith Tour & Travel Ndg Salim M Suleiman.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akimkabidhi mmoja wa Wahitimu hao Cheti chake baada ya kumaliza Kozi ya Ukataji wa Tiketi kwa Njia ya Kieletroniki, kulia Mkurugenzi Mkuu wa Zenith Tour & Travel Ndg Salim M Suleiman.
  Mhitimu akiwa na furaha baada ya kukabidhi Cheti chake cha Huduma ya Kukatisha Tikeki ya Ndege kwa Njia ya Kieletroniki.
  Mhitimu akiwa na furaha baada ya kukabidhi Cheti chake cha Huduma ya Kukatisha Tikeki ya Ndege kwa Njia ya Kieletroniki.

  Mgeni Rasmin Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib na Ungozi wa Chuo hicho wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao baada ya kuwakabidhi Vyeti vyao.
   Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.com
  Zanzinews.com 

  0 0

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA Dkt.Agness Kijazi (Katikati) akitoa taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016. Kushoto ni Samwel Mbuya ambae ni Meneja Kitengo Kikuu cha Habari TMA Dar es salaam na Kulia ni Dkt.Hamza Kabelwa ambae ni Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA.

  Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
  Mamla ka ya Hali ya Hewa nchini TMA imewatahadharisha Wananchi pamoja na Taasisi mbalimbali ikiwemo za Uokoaji, kujiandaa juu ya namna ya kukabiriana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za masika ambazo tayari zimeanza kunyesha hapa nchini.


  Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Dkt.Agness Kijazi alitoa tahadhari hiyo juzi Jijini Mwanza, wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa Mvua za Masika kwa Kipindi cha kuanzia mwezi Machi hadi mwezi Mei Mwaka huu.


  Dkt.Kijazi alisema kuwa mvua za Masika zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza nay a pili ya mwezi machi mwaka huu, katika maeneo ya Ukanda wa Ziwa na kusambaa katika maeneo mengine yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.


  Alisema Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi nchini, na kwamba zinaweza kusababisha athari mbalimbali ikiwemo mafuriko hivyo ni vema wananchi pamoja na mamlaka za uokozi zikajiandaa kikamilifu ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.
  Mkutano baina ya Wanahabari pamoja na TMA uliofanyika Jijini Mwanza, ambapo TMA ilikuwa ikitoa taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
  Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
  Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.

  Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
  Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
  Bonyeza HAPA Kutazama Semina Kwa Wanahabari.

  0 0  0 0


  *Ni wa Ardhi, Maliasili na TAMISEMI

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atawatuma mawaziri watatu waje mkoa wa Simiyu ili wakae na uongozi wa kila wilaya pamoja na wananchi ili kubaini tatizo la mipaka baina ya wilaya hizo na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa vijiji vya Mwakaluba na Mwandoya akiwa kwenye siku ya tano ya ziara yake mkoani Simiyu.

  "Tangu niingie hapa mkoani malalamiko ya mipaka nimeyapokea kila mahali nilikopita. Nimeamua kuwatuma mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi; Waziri wa Maliasili ua Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Bw. George Simbachawene waje mkoa huu kutatua matatizo yenu," alisema.

  "...Nitawatuma waje na wapite kila wilaya, wakae na kuzungumza na wakulima na wafugaji ili kubaini ni chanzo cha tatizo la migogoro hii kwenye mipaka ya vijiji na hifadhi ya Serengeti. Pia Waziri wa TAMISEMI itabidi atoe ufafanuzi kuhusu agizo lao la kutofanya shughuli yoyote mita 60 kutoka kwenye mto Simiyu ili wananchi waelewe," alisema.

  Mapema, Mbunge wa Kisesa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi (OMR - Mazingira) alimweleza waziri Mkuu mbele ya wananchi hao kwamba limetolewa zuio linalowakata wakazi wa mkoa huo wasifanye shughuli zozote umbali wa mita 60 kutoka kwenye kingo za mto huo.

  "Limebandikwa tangazo linalokataza wananchi waishio kando ya mto Simiyu wasifanye chochote kuanzia Julai 30, 2016. Wananchi hawajashirikishwa wala kuelezwa chochote zaidi ya kuona bango la matangazo tu. Watu wananakatazwa wasichote maji wala kunywesha mifugo wakati hakuna mabwawa, itawezekanaje? Tunaomba kauli yako kuhusu jambo hili," alisema.

  Ili kumaliza tatizo la migogoro ya ardhi hapa nchini, Waziri Mkuu alisema Serikali ina mpango wa kuunda mabaraza ya ardhi 100 kwa nchi nzima ambayo yatakuwa na jukumu la kutatua migogoro ya ardhi kwa wakati.
    
  Akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Bw. Erasto Sima alisema wilaya hiyo iliyoanzishwa Julai mosi, 1987 ina ukubwa wa kilometa za mraba 8,835 ambapo asilimia 49 (sawa na kilometa za mraba 4,329) ya eneo lote la wilaya hiyo ni hifadhi za wanyamapori.

  Alilitaja eneo hilo kuwa ni pori la akiba la Maswa, sehemu ya hifadhi ya Serengeti, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na pori la hifadhi ya usimamizi wa wanyama (WMA) la Makao na kwamba asilimia 51 iliyobakia indiyo inayotumiwa kwa makazi ya watu, kilimo na malisho ya mifugo.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAMOSI, MACHI 5, 2016.

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mh. Hamisi Kigwangala akiongea na washiriki wa matembezi ya shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo . Matembezi hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia.
  Mwenyekiti wa Tanzania Women of Achievement , Sadaka Gandi akiongea na washiriki wa matembezi ya shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo . Matembezi hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mh. Hamisi Kigwangala akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washirikimatembezi ya shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo . Matembezi hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mh. Hamisi Kigwangala akijiandaa kuanza matembezi ya shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo . Matembezi hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mh. Hamisi Kigwangala akiwa sambamba na washiriki wa matembezi ya shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo . Matembezi hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akimvika kitambulisho Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina Dar es Salaam leo asubuhi, baada ya kuvizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wa kwenda kazini kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia walimu hao.
  DC Makonda akimfika kitambulisho Mwalimu Gideon Mwenenyi.
  DC Makonda akimvika kitambulisho, Mwalimu Ramadhani Korowelle.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wananchi na walimu wakati wa uzinduzi wa vitambulisho hivyo.
  Ofisa Elimu wa Sekondari wa wilaya ya Kinondoni, Rogers Shemwelekwa (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Turiani, Alpherio Nchimbi (kushoto), akizungumza kwenye uzinduzi huo.
  Walimu na viongozi wengine wakiwa kwenye hafla hiyo
  Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo.

  Wananchi na walimu wakiwa kwenye uzinduzi huo.
  Mwalimu Happyness Mailo (kushoto), akimshukuru DC Makonda kwa kuwawezesha mpango huo.
  Mwakilishi wa wananchi, Ahmed Muhonga akimshukuru DC Makonda.
  Mshairi, Msafiri Himba akitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Turiani, Beatrice Mhina akitoa neno la shukurani kwa DC Makonda.
  ………………………………………………………………………………….
  Na Dotto Mwaibale

  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amezindua vitambulisho vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wakitoka nyumbani kwenda kazini.

  Katika hatua nyingine Makonda ameziomba sekta mbalimbali nchini kushiriki katika kutoa mawazo yao ya maendeleo ili taifa lizonge mbele badala ya kuwa watizamaji.

  Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam jana mbele ya wazazi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Turiani wakati akizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu wa wilaya yake kupanda daladala bure kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia walimu hao.

  “Nawaomba watanzania na sekta mbalimbali kuwa na mawazo ya maendeleo ambayo yatawekwa mezani na kuyafanyia kazi jambo litakalo msaidia Rais wetu Dk.John Magufuli katika kuliinua taifa kiuchumi badala ya kumuachia kila kitu akifanye yeye” alisema Makonda.

  Makonda alitoa mwito kwa makondakta wa daladala kutoa ushirikiano kwa walimu hao kesho wakati watakapoanza kupanda magari yao huku wakijua walimu ndio waliowafundisha na kufikia hatua hiyo ya kazi walizonazo.

  Ofisa Elimu wa Sekondari wa Wilaya hiyo, Rogers Shemwelekwa aliwaomba wananchi hao na walimu kuendelea kuunga mkono jitihada za Makonda za kuwaletea maendeleo na kumuombea kwa mungu badala ya kumbeza kwani kazi hizo anazozifanya ni kwa ajili ya wananchi.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Balozi Joseph Rwegasira, aliyefariki dunia jana tarehe 04 Machi, 2016 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.Balozi Joseph Rwegasira amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.

  Wakati wa uhai wake, Balozi Rwegasira amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini zikiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Balozi wa Tanzania nchini Zambia.


  Katika salamu zake kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Rais Magufuli amesema Taifa litaukumbuka mchango mkubwa uliotolewa na Marehemu Balozi Rwegasira katika harakati za kukuza diplomasia na kuleta amani katika nchini majirani.


  Rais Magufuli ameongeza kuwa Marehemu Balozi Rwegasira alikuwa mchapakazi, muadilifu na mzalendo wake kweli kwa nchi yake.


  "Tungependa kuendelea kumuona Marehemu Balozi Rwegasira akiwa hai, lakini siku zote kazi ya Mungu haina makosa, namuombea kwa Mwenyezi Mungu apumzishwe mahali pema peponi, Amina" Amesema Rais Magufuli.

  Dkt. Magufuli amewataka familia, ndugu, jamaa na marafiki wote kuwa wavumilivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu na kwamba anaunga nao katika kumuombea marehemu.

  Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es salaam

  05 Machi, 2016. 

  0 0

  Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akifungua jengo la Maabara la Shule ya Sekondari ya Mwakaluba katika jimbo la Kisesa akiwa aktika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu , Dkt Titus Kamani na Wazpili kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, J. Mpina. 

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maabara ya Shule ya Sekondari ya Mwakalubi katika jimbo la Kisesa akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016.
  Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akikagua shamba la pamba la mfano la mkulima Gamuga Kimali kqtika kijiji cha Nandoya wilayani Meatu akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongeza Mama Anastazia Petro kwa kujifungua salam motto wa kiume aliyepewa jina la Majaliwa wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Mwandoya akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akiteta na Waganga na wauguzi wa Kituo cha Afya cha Mwandoya wilayani Meatu akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Madaktari na Wauguzi wa Kituo cha Afya cha Nandoya wilayani Meatu baada ya kuzindua jengo la upasuaji na kusalimia wagonjwa akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiinadi video ya Sizonje kwa wadau mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi huo.Nape aisema video hiyo inawakilisha serikali ya awamu ya tano na utumbuaji wa majipu.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye Nape Nnauye akizindua rasmi video ya Sizonje,Kushoto kwake ni Mrisho Mpoto
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Msichana Butogwa Charles Shija aliyeongoza kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Congcong Wang aliyeshika nafasi ya pili kitaifa katika mtihani wakidato cha nne.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha ushujaa kwa kijana Salmin Selemani ambae alifanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne lakini hakukata tamaa na kujitokeza hadharani ili asaidiwe,Waziri Nape amejitolea kumwendeleza kijana uyu.Picha na Daudi Manongi.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipiga ngoma alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa Golden Jubelee Towers alipokuja kushiriki katika uzinduzi wa Video mpya ya Mshairi Mrisho Mpoto inayoitwa Sizonje .Wengine Pichani ni Mrisho Mpoto,Dr Mwaka na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sanaa Bi leah Kihimbi..

  …………………………………………
  Na Daudi Manongi-WHUSM

  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye amewataka watanzania kutumia utamaduni wetu kujenga nchi yetu.

  Waziri nape ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa video ya mshairi Mrisho Mpoto mbele ya wadau mbalimbali wa sanaa kutoka kila kona ya jiji la Dar es Salaam waliofurika kuangalia uzinduzi huo ulioendana sambamba na mada kubwa mbili za utamaduni na lugha na kauli mbiu ya Kufeli elimu sio mwisho wa maisha.

  “Serikali ya awamu ya Tano imejipanga vyema katika kutumia utamaduni wa nchi yetu kushape vijana wetu wawe na morali,wajitambue ili wafike mbali,tutatumia utamaduni huu kujenga nchi yetu kikamilifu kwani ni silaha tosha kuvutia hata nchi nyingine.Maisha sio rahisi,ni kuvumilia,kutokata tamaa na kuweka malengo.Safari tumeianza na tutafika mbali”Alisema Nape.

  Pia Waziri uyo aliwataka watanzania kumuunga mkono Mrisho mpoto na kutomkatisha tamaa kwani anamsaidia rais wa awamu ya Tano Mhe.John Pombe Magufuli katika kutumbua majipu.Mbali na hilo alimshauri Mrisho mpoto kwenda mikoani kwani hata uko kina Sizonje wapo wengi muwaonyeshe kwamba iko njia kwa watu waliokata tamaa.

  Kwa upande wake Mrisho mpoto aliwasii watanzania kujenga taifa letu na pia tujenge Kiswahili na kukitumia kama ajira kwani ni lugha ya sita kwa sasa duniani.

  “Lazima tujue kwamba Kiswahili ni lugha ya kibiashara,tuangalie fursa zilizopo kupitia Kiswahili kujipatia ajira kwani nchi kama Namibia,Zimbabwe wamepokea Kiswahili na wanaitaji kufundishwa zaidi na kwa namna hii izi zote ni fursa kwani lugha imekuwa bidhaa sasa”Alisema Mpoto.

  Wakichangia katika mjadala uliopewa jina “kufeli elimu sio kufeli maisha” Bw.Ruge Mutahaba alisema kufeli darasani kusikuzwe na kuwataka vijana kutengeneza maono mapema kwani yatakuwa ndio mwongozo wa maisha yao yote na yatawafanya vijana kutokata tama mapema.

  “Vijana Mjifunze kuwasiliana,muwe wabunifu,mjifunze kuwa na utaratibu wa kujifunza kitu kipya kila siku,pia mtengeneze jamii ya watu ambao ni watatua matatizo na sio watumikaji tu kwani kwenye matatizo ndo kwenye fursa zote,msiiachie serikali pekee kushughulikia huduma za jamii bali tumieni mwanya huo kuanzisha za kwenu”Alisema Ruge.

  Naye mwakilishi kutoka TBL Bw George Kavishe aliwataka vijana kujua mihimili yao pamoja na uwezo wao na kwa kufanya ivyo watakuwa wamejua wapi wanacho na nini kinafaa kufanya ili kuboresha maisha yao.

  Mjadala huo pamoja na uzinduzi wa video ya sizonje uliambatana na waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na michezo Mhe.Nape kuwapa vyeti vya pongezi na ushujaa vilivyoandaliwa na Mrisho Mpoto wanafunzi waliofanya vizuri na wale waliofanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (watatu kulia) akiongoza wanawake kufanya mazoezi wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga(Picha na: Beatrice Lyimo na Genofeva Matemu)
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (katikati) akifanya mazoezi ya kukimbia wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Michezo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bibi. Zainabu Mbussi.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiongea na wanawake (hawapo pichani) walioudhuria tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akirusha mpira kuashiria ufunguzi wa mchezo wa mpira wa pete wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam. Anayezuia mpira ni Mjumbe wa Baraza la Michezo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bibi. Zainabu Mbussi.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (wapili kushoto) akipata maelekezo kuhusu michezo mbalimbali iliyoandaliwa kutoka kwa Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja (wapili kulia) wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
  Wanamichezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya kushiriki michezo mbalimbali wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
  Wanamichezo kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), wakijiandaa kushiriki mchezo wa kuvuta kamba ambapo walishindana na Wanamichezo kutoka Wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
  Wanamichezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwavuta wapinzani wao kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) mbalimbali wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikagua timu ya mpira wa miguu kutoka Shule ya Sekondari Makongo ambao walishiriki tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipokea fomu ya kujiunga kwa hiari katika Mfuko wa Hiara wa PSPF kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
  Mgeni rasmi (katikati mstari wa mbele) Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja washiriki na wadau waliondaa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi wa wanafunzi wakifuatilia michezo mbalimbali iliyokua ikiendelea wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam.
  Matukio ya michezo mbalimbali wakati wa tamasha la maadhimisho kuelekea kilele cha siku ya wanawake katika viwanja vya Uhuru leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba akiangalia baadhi ya sampuli za mifuko isiyoharibu mazingira ambayo inatengenezwa na Umoja wa Watengeneza mifuko isiyoharibika Tanzania (UWAMITA) Kulia ni Mwenyekiti wa kikundi hiko Jumanne Mgude.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba, akiongea na Wanakikundi wa Umoja wa Watengeneza Mifuko isiyoharibika Tanzania (UWAMITA) walipomtembelea Ofisini kwake mtaa wa Luthuli.

  0 0

   Mwalimu wa mazingira wa shule ya sekondari Mgutwa iliyopo Kata ya Shambarai, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Godlove Issa (kushoto) akiwaonyesha wageni walioitembelea shule hiyo, baadhi ya miche inayotarajiwa kupandwa ili kutunza mazingira.
   Wageni mbalimbali wakiwemo Megan Allen wa Marekani na Juliane Friedrich wa Ujerumani, walioitembelea shule ya sekondari Mgutwa iliyopo Kata ya Shambarai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiangalia baadhi ya miche ambayo itapandwa kwenye shule hiyo.
  Mwalimu wa mazingira wa shule ya sekondari Mgutwa iliyopo Kata ya Shambarai, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Godlove Issa na raia wa Marekani Megan Allen, wakipanda mti kwenye shule hiyo ili kutunza mazingira.


  ILI kukabiliana na ukame, kupiga vita jangwa na kutunzaji wa mazingira, shule ya sekondari Mgutwa iliyopo Kata ya Shambarai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ina mpango wa kupanda zaidi ya miti 1,500 kwenye eneo hilo.

  Akizungumza na wageni waliotembelea shule hiyo Megan Allen kutoka Marekani na Juliane Friedrich wa Ujerumani, meneja wa shule hiyo Monica Mlemeta, alisema wao ni wana mazingira, hivyo wataendelea kupanda miti mingi zaidi japo eneo hilo waliloligeuza kuwa la kijani tofauti na awali.

  Mlemeta alisema shule hiyo ina wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne, ina lengo la kuanzisha kidato cha tano hadi cha sita, ili kuboresha elimu ya eneo hilo la Simanjiro pamoja na kuzidi kutunza mazingira kwa kupanda miti mingi. 

  Alisema japokuwa wanatumia gharama kubwa kupanda miti katika eneo hilo kutokana na jiografia iliyopo ikiwemo kutoa udongo sehemu nyingine, watahakikisha wanabadili mandhari ya eneo kwa kuotesha miti zaidi.

  Mratibu wa asasi ya Community Education resources foundation, Godfrey Lema walioipatia shule ya Mgutwa miti hiyo 1,500 alisema lengo lao ni kuhakikisha wanatunza mazingira na kuondokana na ukame uliopo katika eneo hilo.

  Alisema  kwa kushirikiana na asasi za Nick’s Eco safaris na Moivaro Jitegemee Family wamefanikisha hilo, japo ardhi ya eneo hilo ina mwamba na magadi, uongozi wa shule umelibadili kuwa la kijani, kwa kuendeleza utunzaji mazingira na kuwa mfano wa kuigwa.

  “Wageni wetu Megan Allen kutoka Marekani na Juliane Friedrich wa Ujerumani, wamefurahia ukijani uliopo hapa na tutahakikisha tunaendelea kuiunga mkono shule hii, kwani imekuwa mfano bora wa utunzaji mazingira,” alisema Lema.

  Alisema elimu ya mazingira inatakiwa kutolewa kwa sehemu kubwa ya jamii ya wananchi wa wilaya ya simanjiro, ili kuhakisha wanapanda miti kwa wingi kwani ndiyo vyanzo vya mvua na kupata kivuli, matunda na hewa safi.

  0 0

  Mwalimu wa Chuo cha Zenith Learning Center Ali Mussa Mohammed, akizungumza kabla ya kuaza Mahafali ya Nne ya Chuo hicho yaliofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho Majestik Zanzibar jengo la Zanlink,Jumla ya Wahitimu 28 wametunikiwa Vyeti vyao na Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib.
  Mkuu wa Mafunzo wa Chuo cha Zenith Learning Center Mundhir Nassor akitowa maelezo ya Kozi zinazotolewa na Chuo hicho kwa mgeni Rasmin kabla ya kuzungumza na wahitimu na kuwakabidhi vyeti vyao, Chuo hicho kinatowa Kozi ya Kimataifa ya Ukataji wa Tiketi za Ndege kwa Njia ya Kielectoniki
   (GALILEO  RESERVATION SYSTEM) 
  Wahitimu wa Mafunzo hayo wakiwa ukumbi wa Mahafali hayo ya yaliofanyika katikav Ukumbi wa Chuo hicho Majestik Zanzibar jengo la Zanlink 
  Mgeni Rasmin wa Hafla hiyo ya Mahafali ya Nne ya Chuo cha Zenith Learning Centr akiwa na Viongozi wa Chuo hicho wakati wa Mahafali hayo yaliofanyika katika Chuo hicho Zanzibar.
   
  Mwakilishi wa Travelport Zanzibar Ndg Rashid Ntalaluka akizungumza wakati wa mahafali hayo ya Nne ya Chuo hicho kwa Wahitimu wa Kozi ya Kimataifa ya kutowa huduma ya Ukataji wa Teketi kwa Njia ya Kieletroniki (Galileo Reservation System) na kuwaasa Vijana hao kutumia mafunzo hayo kwa utaalamu wa hali ya juu. 
  Mkurugenzi wa Zenith Tours& Travel Ndg Salim M Suleiman, akitowa nasaha zake kwa wahitimu hao wakati wa mahafali hayo ya Nne ya Chuo hicho yaliofanyika katika ukumbu wa chuo hicho jengo la Zanlink Zanzibar.
  Wahitimu wa Mafunzo hayo wakiwa ukumbi wa Mahafali hayo ya yaliofanyika katikav Ukumbi wa Chuo hicho Majestik Zanzibar jengo la Zanlink 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wahitimu hao wa Mafunzo ya Ukataji Tiketi kwa Njia ya Kielectoniki(Galileo Reservation System) kuyatumia mafunzo hayo kwa ukamilifu wakati wa kutowa huduma kwa wataja wao wanapofika kupata huduma hiyo. , 
  Wageni waalikwa katika Mahafali hayo wakiwa katika ukumbi wa hafla hiyo.
  Wahitimu wakiwa katika ukumbi wa hafla hiyo ya mahafali ya Nne ya Chuo hicho.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akimkabidhi mmoja wa Wahitimu hao Cheti chake baada ya kumaliza Kozi ya Ukataji wa Tiketi kwa Njia ya Kieletroniki, kulia Mkurugenzi Mkuu wa Zenith Tour & Travel Ndg Salim M Suleiman, na kushoto Mkuu wa Chuo hicho Ndg Mundhir Nassor.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akimkabidhi mmoja wa Wahitimu hao Cheti chake baada ya kumaliza Kozi ya Ukataji wa Tiketi kwa Njia ya Kieletroniki, kulia Mkurugenzi Mkuu wa Zenith Tour & Travel Ndg Salim M Suleiman.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akimkabidhi mmoja wa Wahitimu hao Cheti chake baada ya kumaliza Kozi ya Ukataji wa Tiketi kwa Njia ya Kieletroniki, 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akimkabidhi mmoja wa Wahitimu hao Cheti chake baada ya kumaliza Kozi ya Ukataji wa Tiketi kwa Njia ya Kieletroniki, kulia Mkurugenzi Mkuu wa Zenith Tour & Travel Ndg Salim M Suleiman.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akimkabidhi mmoja wa Wahitimu hao Cheti chake baada ya kumaliza Kozi ya Ukataji wa Tiketi kwa Njia ya Kieletroniki, kulia Mkurugenzi Mkuu wa Zenith Tour & Travel Ndg Salim M Suleiman.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib akimkabidhi mmoja wa Wahitimu hao Cheti chake baada ya kumaliza Kozi ya Ukataji wa Tiketi kwa Njia ya Kieletroniki, kulia Mkurugenzi Mkuu wa Zenith Tour & Travel Ndg Salim M Suleiman.
  Mhitimu akiwa na furaha baada ya kukabidhi Cheti chake cha Huduma ya Kukatisha Tikeki ya Ndege kwa Njia ya Kieletroniki.
  Mhitimu akiwa na furaha baada ya kukabidhi Cheti chake cha Huduma ya Kukatisha Tikeki ya Ndege kwa Njia ya Kieletroniki.

  Mgeni Rasmin Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib na Ungozi wa Chuo hicho wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao baada ya kuwakabidhi Vyeti vyao.
   Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.com
  Zanzinews.com 

  0 0

  Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye kaburi la Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani. Mzee Selemani Kikwete alikuwa kaka mkubwa wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Rais wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi wakimsikiliza kwa Makini Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifafanua jambo huko Msoga Mkoani Pwani.
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimfafanulia jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya mazishi ya Kaka yake Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimfariji Mjane wa Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji Mjane wa Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete na wanafamilia, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016
  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Mama Salma Kikwete wakiwa msibani kwa kaka yake Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, MarehemuMzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016. Wengine kutoka kushoto ni Mama Asha Bilali, Mama Khadija Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi, Mama Asha Seif Ali Iddi, 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea hela ya utani toka kwa Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakati wa mazishi ya Baba yake Mkubwa Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016 wanaoshuhudia ni Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wastaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Benjamin Mkapa, Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe John Malecela. Katika utamaduni wa Kitanzania Wakwere na Wasukuma ni watani.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimkabidhi hela ya utani kwa mkaazi wa Chalinze ambaye ni Muskumu Bwana Luhende baada ya kuipokea toka kwa Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete wakati wa mazishi ya Baba yake Mkubwa Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016 wanaoshuhudia ni Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Rais wastaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Benjamin Mkapa, Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe John Malecela. Katika utamaduni wa Kitanzania Wakwere na Wasukuma ni watani.
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinayang Bw. Khamis Mgeja akiongea na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais MStaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa Mazishi ya Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete, kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016PICHA NA IKULU
  Mama Janeth Magufuli, mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufiwa na kaka yake, Mzee Selemani Mrisho Kikwete, wakati wa mazishi kijijini Msoga, Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Machi 5, 2016
  Kada wa Chadema Hamis Mgeja akimsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya mazishi ya Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba kabla ya mazishi ya Marehemu Mzee Selemani Mrisho Kikwete huko Msoga mkoani Pwani.PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Fatma Salum  (MAELEZO) .

  Wanawake nchini wamehimizwa kushiriki kwenye michezo mbalimbali kuanzia ngazi ya vijiji hadi taifa ili kuboresha afya zao na kujiongezea kipato.

  Hayo yamesemwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama leo jijini Dar es Salaam wakati akihutubia kwenye Tamasha la Michezo kwa wanawake lililoandaliwa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8 kila mwaka. 

  Akihutubia kwa niaba ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Jenista ameeleza kuwa Serikali ina mipango thabiti ya kuboresha sekta ya michezo hivyo ni wakati muafaka kwa wanawake wa rika zote kushiriki kwenye michezo kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla. 

  "Wanawake tunaweza tusisubiri kuwezeshwa tujitokeze kwenye michezo kuanzia kwenye maeneo tunayoishi kwani itatusaidia kuimarisha afya zetu na kuepuka majanga ikiwemo UKIMWI hasa kwa wasichana kwa kuwa wanaposhiriki kwenye michezo wanaepuka kujihusisha na vitendo viovu kama ulevi na uasherati vinavyopelekea maambukizi" alisema Mhe. Jenista.

  Aidha Mhe. Jenista amelitaka Baraza la Michezo Tanzania  (BMT) kuandaa program maalum za kuhamasisha makundi mbalimbali kushiriki kwenye michezo hasa wanawake, watoto na walemavu. 

  Pia Mhe. Jenista ametoa wito kwa wadau wa michezo ikiwemo Mifuko ya Hifadhi za Jamii kushirikiana na BMT kuandaa matamasha mengi ya michezo yatakayohusisha wanachama wa mifuko hiyo ili kuimarisha afya zao na kuepuka maradhi kama Shinikizo la Damu na Kisukari yanayosababisha mifuko hiyo kutumia gharama kubwa kuwatibia kupitia fao la matibabu.

  Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa BMT Mhe. Zainab Vullu  (Mb) ameiomba Serikali kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya michezo ikiwemo kupunguza kodi kwa vifaa vya michezo vinavyoingia nchini na kuboresha mitaala ya elimu ya michezo mashuleni. 

  Tamasha hilo la michezo kwa wanawake limefanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam likibeba kauli mbiu ya mwaka huu inayosema " 50 kwa 50 ifikapo 2030, Tuongeze Jitihada, Maendeleo ya Wanawake kupitia Michezo Inawezekana".

  0 0

  Makamu wa Pili wac Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokea mfano wa hundi ya shilingi miliono kumi na tano ikiwa mchango wa Benki ya Posta Tanzania kwa ajili ya kufanikisha Maonesho hayo ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kutoka Mkurugenzi Mkuu wa TPB. Ndg. Sabasaba Moshingi.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia Wanawake Wajasiriamali katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Kisonge, na kuyazindua rasmin maonesho hayo ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka 8, march. 
  Mwenyekiti wa Zanzibar Informal Sector Foundation Bi Nuru Mohammed Ahmeid akizungumza machache kuhusiana na maonesho hayo yalioandaliwa na Jumuiya hiyo kwa Wajasiriamali Wanawake wa Zanzibar kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani yaliofanyika katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezo Kisonge Zanzibar.na kuwashirikisha Wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Tanzania Informal Sector Foundation Ndg Masoud Maftah akitowa maelezo kuhusiana na maonesho hayo ya Wajasiriamali wa Zanzibar Wanawake katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. maonesho hayo yamefunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Kisonge leo.  

  Wanawake Wajasiriamali wakiwa katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Kisonge wakimsikiliza Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

  .
  Wanawake Wajasiriamali wakiwa katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Kisonge wakimsikiliza Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
  Wanawake Wajasiriamali wakiwa katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Kisonge wakimsikiliza Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
  Waziri wa Ustawi wa Jamii Vijana Uwezeshaji Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar akihutubia wakati wa hafla hiyo ya Maonesho ya Wajasiriamali Wanawake Zanzibar kuadhimishi Siku ya Wanawake Duniani, kabla ya kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuyafungua Maoesho hayo.  
  Wageni waalikwa wakiwa katika viwanja hivyo vya maonesho wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia 
  Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdalla Mwinyi Khamis Mwenyekiti wa Zanzibar Informal Sector Foundation Ndg Nuru Mohammed Ahmeid na Katibu wake Ali Mohammed,wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akihutubia wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya Wanawake Wajasiriamali Zanzibar. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akijiandaa kuyazindua Maonesho ya Wanawake Wajasiriamali Zanzibar ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kushoto Mwenyekiti wa Zanzibar Informal Sector waandalizi wa Maonesho hayo mwenye sati jeupe Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania Ndg Sabasaba Moshingi,  
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe katika Banda la Benki ya Posta Tanzania kuashiria kuyafungua maonesho hayo ya Wajasiriamali Wanawake Zanzibar.kulia Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania Ndg Sabasaba Moshingi.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimsikiliza Afisa wa Benki ya Posta Tanzania baada ya kuyafungua Maonesho hayo, katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Kisonge.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Maonesho hayo ya Wanawake Wajasiriamali Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Maonesho hayo ya Wanawake Wajasiriamali Zanzibar.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akitembelea Mabanda ya Wajasiriamali baada ya kuyafungua maonesho hayo katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Kisonge.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akitembelea Mabanda ya Wajasiriamali baada ya kuyafungua maonesho hayo katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Kisonge.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akitembelea Mabanda ya Wajasiriamali baada ya kuyafungua maonesho hayo katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Kisonge.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akitembelea Mabanda ya Wajasiriamali baada ya kuyafungua maonesho hayo katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Kisonge.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akitembelea Mabanda ya Wajasiriamali baada ya kuyafungua maonesho hayo katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Kisonge.
  Meneja Masoko wa Kampuni ya Tigo Ibrahm Atals akitowa maelezo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipotembelea banda hilo la Tigo.
  Makamu wa Pili wac Rais wa Zanzibar akitembelea mabanda ya maonesho hayo ya Wajasiriamali Zanzibar baada ya kuyafungua rasmin 
  Balozi Seif Akiangalia bidhaa za Wajasiriamali wakati wa maonesho hayo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimsikiliza Afisa wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichoko bububu Zanzibar akielezea jinsi ya kushiriki katika maonesho hayo kutowa fursa kwa Wajasiriamali kupata Elimu kupitia Chuo hicho kinatowa Kozi mbalimbali kwa Jamii.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi walioandaa maonesho hayo ya Wajasiriamali Wanawake kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
  Imeandaliwa na OthmanMapara.blogspot.com.
  Zanzinews.com.

  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Maonesho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge Zanzibar. katika Viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Zanzibar michezani Kisonge akiongozana na Mwenyekiti wa Tanzania Informal Sector Foundation Ndg Masaud Maftah, katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa Maonesho ya Wajasiriamali wa Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza na Mwenyekiti wa Tanzania Informal Sector Foundation Ndg Masaud Maftaha na  Mwenyekiti wa Zanzibar Informal Sector Foundali Bi Nuru Mohammed Ahmeid, wakati wa hafla hiyo ya Maonesho ya Biashara za Wajasiriamali Wanawake Zanzibar katika maonesho ya Siku ya Wanawake Duniani.
  Mkurugenzi Mkuu wac Banki ya Posta Tanzania Ndg Sabasaba Moshingi, akizungumza wakati wa maonesho hayo ya Wajasiriamali Wanawake kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani yaliofanyika katika viwanja vya Mnara wac Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Kisonge.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Banki ya Posta Tanzania Ndg Sabasaba Moshingi baada ya kusoma risara yake wa maonesho hayo na kukabidhi hundi kwa ajili ya kuchangia Maonesho hayo.  

older | 1 | .... | 786 | 787 | (Page 788) | 789 | 790 | .... | 1898 | newer