Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

UDSM YAKANA KUWANYANYASA WATUMISHI WAKE.

$
0
0
Na. Aron Msigwa - MAELEZO.
6/3/2016. Dar es salaam.

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) umekanusha  tuhuma zilizotolewa na baadhi ya wafanyakazi waendeshaji wa chuo hicho kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa unaendesha vitendo vya dhuluma, uonevu na upendeleleo katika ulipaji wa mishahara na kuwasahau watumishi hao  jambo linalokwamisha ufanisi wa chuo hicho.

Taarifa ya kanusho dhidi ya tuhuma hizo iliyotolewa na Ofisi ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Utawala na kusainiwa  na Prof.Preksedis Marco Ndomba leo jijini Dar es salaam imeeleza kuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Utumishi Umma nchini na kamwe hakina mamlaka ya  kumwonea, kumdhulumu wala kutoa upendeleo kwa mtumishi yeyote kwa kuwa suala hilo liko nje ya misingi iliyoanzisha chuo hicho.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kama ilivyo kwa vyuo vingine vya umma suala la maslahi hasa nyongeza za mishahara na marupurupu mengine ya watumishi wa vyuo hususan Chuo Kikuu cha Dar es salaam linapangwa na kuidhinishwa na Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina na siyo uongozi wa chuo hicho.

Aidha, mishahara ya watumishi wa chuo hicho hupangwa kulingana na kanuni na taratibu za Serikali na kuongeza kuwa wanataaluma wa Chuo hicho hupewa mishahara yao kutokana na Muundo wa Pamoja wa Utumishi wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu vya Umma wa mwaka 2014 na Sheria ya Kazi na mahusiano kazini ya mwaka 2004 na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009.

Kuhusu tuhuma za kuwepo kwa tofauti ya mishahara miongoni mwa watumishi wa Chuo hicho imeeleza kuwa hilo inatokana na tofauti ya vyeo waliyonayo watumishi hao na kuongeza kuwa wao kama viongozi wa chuo hicho hawana mamlaka ya kuwapangia mishahara watumishi wala kutengeneza nyaraka za mishahara.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam hupokea nyaraka za mishahara kwa watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina na kuzitekeleza na kuwataka watumishi hao kutambua kuwa tofauti ya vyeo waliyo nayo inawafanya walipwe mishahara tofauti.

Kupitia taarifa hiyo uongozi wa chuo hicho umeeleza kuwa hakuna upendeleo katika nafasi  za uongozi chuoni hapo kwa kuwa nafasi zote hujazwa kwa kufuata hati idhini ya chuo, pia hupatikana  kwa kushindanishwa kwa waombaji kwa sifa zao na inapotokea mtumishi katika nafasi ya Mkurugenzi uendeshaji anastaafu kazi  Menejimenti ya chuo humwomba mwanataaluma kutoka chuoni hapo kukaimu nafasi hiyo wakati taratibu za kuitangaza nafasi hiyo ili kumpata mkurugenzi mpya zikiwa zinaendelea.

Kwa upande wa tuhuma ya kuwepo kwa matumizi mabaya ya mali za chuo hasa magari kwa safari zisizohusiana na chuo hicho imefafanua kuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kina Sera, Kanuni na miongozo mbalimbali inayodhibiti matumizi ya magari na mali za umma ikiwemo ujazaji wa vitabu maalum vya makabidhiano ya magari " Log Book".

Taarifa imebainisha kuwa UDSM hudhibiti matumizi ya magari yake  kwa  kuyawekea maandishi ubavuni na kwamba magari  hutakiwa kuegesha chuoni baada ya matumizi saa 12 jioni na wafanyakazi wanaoyatumia kinyume na miongozo iliyowekwa wanachukuliwa hatua za kinidhamu.

Aidha, ili kuboresha maslahi ya watumishi wa chuo hicho hasa upandishwaji wa vyeo ndani ya chuo muundo wa Utumishi wa wafanyakazi waendeshaji hutumika pia maboresho hufanyika kupitia vikao rasmi vya ajira kulingana na matakwa ya sheria ya kazi.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Menejimenti ya chuo hicho baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa muundo wa Utumishi wa Waendeshaji iliamua kuuhuisha na kuuwasilisha kwa Msajili wa Hazina ili ufanyiwe kazi.

Pia kikao cha Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam kilichofanyika Februari 12, 2016 pamoja na mambo mengine kilielekeza Chama cha Wafanyakazi UDSM kwa kushirikiana na Uongozi wa chuo kuandika muhtasari unaoaininisha changamoto za watumishi zilizopo ili ziwasilishwe katika Ofisi ya Msajili wa Hazina.


Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Mhe Jaffary Michael atembelea masoko

$
0
0
 Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Mhe. Jafary Michael akisalimiana na wafanyabiashara wa soko la Pasua alipofanya ziara ya kutembelea masoko yaliyopo katika mji wa Moshi kusikiliza kero za wafanyabiashara hao.
 Mbunge wa jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akiongozana na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya wakitembelea soko la Majengo  kusikiliza kero mbalimbali pamoja na kuona namna bora ya kuboresha masoko hayo.
 Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Mhe. Jafary Michael akiongozana na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi Mhe. Raymond Mboya wakitembelea soko la Mbuyuni kusikiliza kero mbalimbali pamoja na kuona namna bora ya kuboresha masoko hayo.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Mhe. Jafary Michael akimsikiliza kiongozi wa soko la Mbuyuni aliyefahamika kwa jina la Lameck ,wakati Mbunge huyo alipofanya ziara ya kutembelea masoko ya mjini Moshi akiongozana na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi,Raymond Mboya.

 Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Mhe. Jafary Michael akiongozana na Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya wakitembelea soko la Mbuyuni kusikiliza kero mbalimbali pamoja na kuona namna bora ya kuboresha masoko hayo.

WAJASIRIAMALI WA DAR NA PWANI WAKUTANA KUPANGA MIKAKATI YA KUJIKWAMUA KIMAENDELEO

$
0
0
Mgeni rasmi Mh. Devota Likokola akizungumza na wamama wa vikundi mbalimbali vya ujasiliamali juu ya wanawake inabidi wajitambue, wawe na uthubutu na kusaidiana katika kuelimishana ili kuweza kuinua kipato cha cha Familia.
Mtangazaji wa kipindi cha uhondo wa Efm Dina Marious akimkalibisha mgeni rasmi katika tafrija ya wajasiriamali kutoka Dar es salaam na Pwani katika ukumbi wa Litostar Park Mbezi Salala, leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mh. Devota Likokola akikata keki katika tafrija ya wajasiriamali kutoka Dar es salaam na Pwani katika ukumbi wa Litostar Park Mbezi Salala, leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mh. Devota Likokola akimlisha keki msanii mkongwe kwenye gemu la filamu Bongo Suzan Natasha Humba katika tafrija ya wajasiriamali kutoka Dar es salaam na Pwani katika ukumbi wa Litostar Park Mbezi Salala, leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mh. Devota Likokola akikabiziwa tuzo ya mwanamke wa shoka na Mtangazaji wa kipindi cha uhondo wa Efm, Dina Marious katika tafrija ya wajasiriamali kutoka Dar es salaam na Pwani katika ukumbi wa Litostar Park Mbezi Salala, leo jijini Dar es Salaam. 
Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu,Mzee Yusuph akiwaburudisha wajasiriamali kutoka Dar es salaam na Pwani katika ukumbi wa Litostar Park Mbezi Salala, leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa Efm Denis Ssebo akiwakaribisha wajasiriamali kutoka Dar es salaam na Pwani katika ukumbi wa Litostar Park Mbezi Salala, leo jijini Dar es Salaam.
Sehem ya wajasiriamali kutoka Dar es salaam na Pwani katika ukumbi wa Litostar Park Mbezi Salala, leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

Sizonje – Mrisho Mpoto ft Banana Zorro (Official Video)

MWIGULU NCHEMBA AJIPANGA KUBORESHA UZALISHAJI SHAMBA LA KITULO.

$
0
0

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Makete Mh.Noramn Sigalla wakati alipowasili kwenye shamba la Kitulo ambalo ni moja ya Mashamba makubwa ya kufuga Ng’ombe wa kisasa aina ya Mitamba.
Huwa ni mfano wa Ng’ombe wa kisasa aina ya Mitamba wanaopatikana shamba la kitulo wenye uwezo wa kutoa maziwa lita 15 hadi 20 wanapokamuliwa mara moja kwa kila mmoja.
Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo kutoka kwa meneja wa shamba la kitulo kuhusiana na uzalishaji wa Ng’ombe aina ya mitamba.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya . Makete Ndg Mh.Mwigulu Nchemba akiwa kwenye shamba la kitulo akipewa maelezo mbalimbali yanayohusiana na kuyumba kwa ufugaji wa ng’ombe kwenye shamba hilo.
Moja ya Farasi ambaye anafugwa kwenye shamba la Kitulo,Idadi ya Farasi wanaofugwa imepungua kutokana na wengi kuuzwa kwa wananchi.
Moja ya Dume la Ng’ombe la kisasa ambalo limezalishwa Shamba la kitulo.
Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia namna ukamuaji wa maziwa unavyofanyika kwenye shamba la kitulo.
Akiwa njiani kutokea shamba la Kitulo,Mh.Mwigulu Nchemba alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa kata ya kikondo ambao walikuwa na malalamiko ya kulipwa fidia baada ya kuhamishwa kutoka hifadhi ya Kitulo,Madai yao ya fidia ni fedha ya Tanzania Bilion 1.8,Mwigulu amewaahidi kuwasaidia wananchi hao kwa kuzungumza na waziri wa Mali asili na Utalii aweze kuprocess malipo hayo.
Mbunge wa Makete,Dr.Norman Sigalla akiomba kwa Waziri wa kilimo,Mifugo na Uvuvi kufanikisha zoezi la kuboresha shamba la kitulo ili uchumi wa wananchi wake wa Makete na wanaozunguka shamba hilo uimarike.

Shamba la Kitulo la Ufugaji wa Ng’ombe aina ya Mitamba lilianzishwa mwaka 1963 na Mwl.Nyerere kama eneo la kuzalisha maziwa ya kusambaza nchi nzima,Ng’ombe aina ya Mitamba wanaopatikana kwenye shamba hilo waliingizwa nchini kutokea Marekani na nchi za Ulaya Mashariki ambazo hali yake ya hewa inaendana na ile ya kitulo ambayo kuna wakati ni 0 centgrade,na hali ya juu zaidi inaweza kuwa 19 Centgrade.

Kuanzia miaka hiyo ,Shamba la kitulo ambalo linauwezo wa kulisha ng’ombe elfu nne (4000),Shamba hilo kwa sasa lina ng”ombe mia saba tu(700).

Mbali zaidi,nyenzo za kutunzia ndama na kukamua maziwa haziridhishi na ukuziaji wa nyasi zilizopandwa kwaajili ya malisho haulidhishi.

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba,baada ya kusikiliza na kuona changamoto zinazolikabili shamba la kitulo kwa ufugaji wa ng’ombe,Ameahidi kuhakikisha analiboresha na kusaidia upatikanaji wa ng’ombe wa kutosha,huduma za kutosha ili eneo la kitulo liwe ni shamba darasa hata kwa mashamba mengine ndani na nje ya nchi yetu.

Picha/Maelezo na Festo Sanga Jr.

SERIKALI IPO KWENYE HATUA ZA MWISHO ZA KUANZA UJENZI WA BARABARA YA TANGA,PANGANI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akionyeshwa eneo la uwanja wa ndege itakakopita barabara ya Mchepuko itakayotoka Horohoro kuunga na inayokwenda Pangani kupitia Utofu, Majani Mapana hadi Duga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua eneo ambalo barabara ya Mchepuko itakayotoka Horohoro kuunga na inayokwenda Pangani kupitia Utofu, Majani Mapana hadi Duga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawaakitoa maelekezo kwa meneja wa Tanroads Mkoa wa Tanga, Alfred Ndumbaro kuhusu ujenzi wa barabara ya mchepuko.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawaakitoa maelekezo kwa meneja wa Tanroads Mkoa wa Tanga, Alfred Ndumbaro kuhusu ujenzi wa barabara ya mchepuko.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo katika makutano ya barabara ya mchepuko eneo la Duga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitazama ramani ya gati ya Bandari ya pangani ambayo inajengwa kwa gharama ya sh. bilioni 2.3.
Muonekano wa gati inayojengwa katika bandari ya Pangani iliyogharimu kiasi cha sh. bilioni 2.3.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitazama ramani ya daraja la Mto Pangani ambalo upembuzi yakinifu wa ujenzi wake umekamilika na litaanza kujengwa hivi karibuni.

…………………………………………………
SERIKALI ipo kwenye hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa Barabara ya Tanga,Pangani ,Saadani mpaka Bagamoyo yenye urefu wa kilometa 242 kwa kiwango cha lami ambapo mpaka sasa tayari kazi iliyobaki ni kupata mzabuni wa kuendesha mradi huo.

Waziri wa ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa alisema kuwa ujenzi wa Barabara hiyo utaanza rasmi kutekelezwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 na kwamba serikali ipo kwenye mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB)ambayo imeonesha nia ya kufadhili mradi huo.

Mradi huo utaenda sambamba na ujenzi wa Daraja katika Mto Pangani lenye urefu wa mita 550 ambalo linategemewa kuwa kiunganishi cha mawasiliano ya kuimarisha shughuli za utalii katika ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi.

Kwa mujibu wa Prof.Mbarawa ni kwamba wakati wa utekelezaji wa mchakato huo serikali itawalipa fidia wananchi ambao wanastahili na wameshafanyiwa tathimini kwa mujibu wa sheria ya Barabara ya mwaka 2007 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009.

“Nasisitiza kwamba kama sheria inavyotamka kwamba nani anastahili kulipwa basai kila mwenye haki na anayestahili kulipwa atalipwa na kama hastahili hatalipwa na hii itakuwa ni kulingana na tathmini iliyokwishafanyika……”,alisema Waziri huyo.

Alisema kuwa serikali inatambua umuhimu wa ujenzi wa Barabara hiyo kwamba ndiyo kiini na moyo wa uchumi wa wilaya ya Pangani hasa kwa kutambua namna ambavyo ina vivutio vingi vya kitalii hatua itakayolenga kuwaongezea fursa za kibiashara wananchi na kukuza Pato lao.

“Daraja hili litakuwa na uwezo wa kupitisha magari na watembea kwa miguu kwa wakati mmoja na hivyo ni mkombozi wa wananchi hasa kwa kuzingatia kuwa walikuwa wakitegemea kuvuka ng’ambo ya pili ya mto kwa kutumia kivuko tu ambacho wakati mwingine kinakumbwa na hitilafu”,alifafanua Prof.Mbarawa ambaye yupo mkoani Tanga katika ziara ya kikazi.

Akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara yake baada ya kukagua Kivuko cha Mto Pangani,Barabara ya Tanga,Saadani mpaka Bagamoyo na eneo linalotakiwa kujengwa Daraja,Prof.Mbarawa aliuagiza Uongozi wa Wakala wa ufundi na Umeme(Temesa)kuhakikisha wanaweka kumbukumbu za utendaji wa kivuko kwa kila siku.

Aliwaagiza kutumia mfumo wa malipo kwa njia ya elektroniki ili kuepusha vitendo vya ubadhirifu wa fedha wakati serikali ikiwa kwenye mpango wa ukusanyaji wa fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

“Suala la kutumia mashine za kieletroniki halina mjadala habari ya kutumia vitabu vya risiti ili muongeze sifuri mbele hatuzitaki….hapa kuna shida kuna siku I naandikwa imeingia shilingi milioni moja lakini Benki zimeenda laki nane na hamsini hii laki moja na hamsini zinaishia wapi hili ni tatizo”,alisema.

Hata hivyo alisema ipo haja kwa Temesa kuajiri manahodha wa vivuko ambao wanafanya kazi kwa viwango vya kitaaluma ambavyo vinakubalika badala ya kutumia Wazee ambao wanafanya kazi kwa mazoea.

Wakulima Musoma Vijijini watakiwa kulima kisasa

$
0
0
 Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya wazee wa jimbo la Musoma Vijijini mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa jimbo.
 Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi hawapo pichani wakati wa mkutano wake na wananchi wa jimboni mwake.
Baadhi ya wananchi wa Musoma Vijijini waliohudhuria mkutano wa Mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani)


Wananchi wa Musoma vijijini wametakiwa kuondokana na kilimo cha kizamani ili kujiongezea kipato.

Wito huo umetolewa hivi karibuni katika kijiji cha Murangi Mkoani Mara, na Mbunge wa jimbo hilo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika mkutano wake na wananchi wa jimbo hilo.


Profesa Muhongo alisema kuwa tayari mbegu za zao la alizeti zipatazo kilogramu 2,025 zimegawiwa kwa wakulima jimboni humo na huku zingine kilogramu 2,000 zitagawiwa ndani ya wiki hii. “Tumegundua kilimo cha pamba hakifanyi vizuri hapa kwetu, sasa tunajaribu kilimo cha alizeti na tena alizeti inachukua muda mfupi baada ya miezi mitatu unavuna.”Alimuagiza Afisa Kilimo kusimamia upandaji wa mbegu hizo ili kuwe na tija na vilevile kushirikiana na wakulima mara kwa mara.

Vilevile Profesa Muhongo alisema kilimo kinachotarajiwa jimboni humo ni kilimo cha kisasa na pia kitakuwa cha umwagiliaji wa kitaalamu ambao hautokuwa na athari.Alisema alikwisha agiza wasaidizi wake jimboni humo kufanya tathmini ili kubaini vijiji vingapi vinahitaji visima ili kuanza kwa shughuli hiyo na kuongeza kwamba kilimo cha kisasa ndiyo ajira ya sasa na hivyo atahakikisha wakulima jimboni humo wanafaidika na kilimo husika.

Mbali na hilo, Profesa Muhongo alibainisha kwamba amemkaribisha Profesa wa Kilimo kutoka Dakawa ili kufanya utafiti zaidi ya kuwa na kilimo chenye tija na vilevile kutoa mafunzo kwa wataalamu wa kilimo pamoja na wakulima jimboni humo.Alisisitiza umuhimu wa uundaji wa vikundi ili iwe rahisi kusaidiwa kuwa na kilimo chenye tija ikiwa ni pamoja na kupatiwa vifaa maalum vya umwagiliaji. “Ninataka jimbo hili liwe ni jimbo la mfano; wengine waige kwetu,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ambaye ni Diwani wa Kata ya Mgango, Charles Magoma akizungumza wakati wa mkutano huo, alipongeza juhudi zilizoonyeshwa na Profesa Muhongo katika kuliletea maendeleo jimbo hilo.Alisema amejifunza kutoka kwa Profesa Muhongo kwamba kuwa na uhusiano mzuri na watu ni jambo jema. “Nimejifunza kwa mbunge, kumbe kuwa na mahusiano mazuri ni jambo jema kama tuonavyo hapa namna ambayo ameweza kufanya mambo makubwa katika kipindi kifupi.”

Alimuahidi Profesa Muhongo ushirikiano wa kutosha pamoja na kuhakikisha yote aliyoagiza yanatekelezwa. Vilevile aliwasisitiza wananchi waliohudhuria mkutano huo kumuombea Mungu Profesa Muhongo ili azidi kuliletea jimbo hilo maendeleo endelevu.

SERIKALI YAANZISHA MFUMO WA MALIPO KWA WATUMISHI WA UMMA

$
0
0
SERIKALI imeanzisha mfumo wa Kielektroniki wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao unalenga kuondoa tatizo la madai ya malimbikizo ya stahili zao.


Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana (Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa sekta mbalimbali  katika wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu.


Waziri Mkuu alisema mfumo huo ujulikanao kama LAWSON, unatumika kwenye ajira za watumishi wote nchini, wa Serikali Kuu na wale wa Serikali za Mitaa  .Waziri Mkuu alisema mfumo huo unasaidia kutunza, kutuma na kuhuisha  taarifa za watumishi kwa wakati na kwa ufanisi tangu mtu anapoajiriwa hadi inapofikia wakati wa kupandishwa madaraja na hadi anapostaafu.


Kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo, maafisa utumishi walipaswa kukusanya taarifa za watumishi wote walioajiriwa na kuzipeleka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili zikathibitishwe kabla ya kuzipeleka HAZINA kwa maandalizi ya mishahara. 


Akitolea mfano wa kada ya ualimu, Waziri Mkuu alisema ajira za walimu zilikuwa zinaanzia Idara ya Utumishi wa Walimu  (TSD)  lakini anapaswa aende kuripoti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  (DED) ambaye ni mwajiri wake chini ya TAMISEMI. "Hii ilileta ugumu wa malipo ya kupanda madaraja, uhamisho ama likizo kwa sababu mwajiri anakuwa hajatenga hizo fedha."

"Sasa hivi tuna Tume ya Utumishi wa Walimu  (TSC) ambayo iko chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. Kwa hiyo ni rahisi wao kukaa pamoja na kuamua tuwapandishe daraja walimu 10 na wote hao wakalipwa bula bila kuchelewa," alisema.


Alisema mfumo huo umeanza kutumika tangu mwaka 2012 na ulianza kwa ajira mpya za wakimu na hadi sasa umethibitisha kuwa inawezekana kumlipa mtumishi mshahara wake hata kama ameajiriwa ndani ya mwezi huohuo.
"Kama mtumishi anaripoti kwenye kituo kipya hata iwe wilaya ya wapi ili mradi amefika na barua zake zote na ziko sahihi mtu huyu ataingiziwa taarifa zake na wakati huohuo taarifa zitaonekanaOfisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na pia zitapokelewa kwa maafisa wanaoshughikia mishahara kule HAZINA."


Alisema changamoto pekee waliyokutana nayo wakati mfumo huo umeanza ilikuwa ni kutoingizwa taarifa za wale ambao wameripoti baada ya tarehe 10 ya mwezi husika. "Hii ni kwa sababu matayarisho ya mishahara yanakuwa yameshaanza. Kwa hiyo wengi walishauriwa kuripoti kati ya tarehe 25 hadi tarehe 9 ya mwezi uliofuata na wote hawa hawakupata matatizo ya kucheleweshewa mshahara," alisema.

Akifafanua kuhusu upandishaji madaraja ya watumishi, Waziri Mkuu alisema  Serikali imeondoa utaratibu wa mtumishi kulazimika kuandika barua ya kukiri kupandishwa daraja/cheo ndipo aanze kupata stahili zake mpya. "Hii imeondoa ucheleweshaji wa kufanyika marekebisho ya mshahara  na pili imeondoa tofauti za mishahara kwa watumishi wenye ngazi moja (sifa sawa za kitaaluma, tarehe moja ya kuajiriwa) ambao walikuwa wakilipwa tofauti kwa sababu mmoja aliwahi kuandika barua ya kukiri na mwingine alichelewa kuandika barua hiyo hiyo " alisema.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amelazimika kukatisha ziara ya mkoa wa Simiyu ambayo ilikuwa imalizike kesho kutokana na msiba wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambayo alipangiwa kuitembelea leo.


Mkurugenzi huyo Bw. Traceas Kagenzi alifariki dunia usiku wa kuamkia jana kutokana na shinikizo la damu. Atasafirishwa kwenda Muleba  kwa mazishi.Akitoa salamu za rambirambi kwenye ibada ya kumuombea marehemu Kagenzi iliyofanyika nyumbani kwake Maswa mjini, Waziri Mkuu alisema ameshtushwa na msiba huo uliotokea ghafla na kwamba Taifa limempoteza mtumishi mahiri ambaye bado Taifa lilikuwa likimtegemea.



"Nimeshtushwa sana na taarifa za msiba huu. Nimeambiwa hadi juzi usiku alikuwa akishirikiana na Mkuu wa Wilaya hii kuandika taarifa ya ziara ya wilaya hii. Kwa niaba ya Serikali, ninawapa pole sana wafiwa na Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi," alisema.



"Nimelazimika kukatisha ziara ya mkoa huu kwa sababu huyu ni mtumishi mwenzetu.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, MACHI 6, 2016.

WAZIRI LUKUVI APOKEA MSAADA KWA WAHANGA WA MAFURIKO IRINGA.

$
0
0
Mhe. William Lukuvi akipokea msaada wa Wahanga wa mafuriko Isimani Iringa kutoka kwa Bibi Sawidath Mohamed Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) tawi la Dar es salaam akiwa na Bibi Rose Majuva Kamishna wa Makao Makuu ya Taasisi hiyo (wa pili kulia) na Grace Shaba Naibu Katibu Mkuu TGGA.
Bibi Sawidath Mohamed Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) tawi la Dar es salaam akimkabidhi Mhe. William Lukuvi msaada wa Wahanga wa mafuriko Isimani Iringa.
Baadhi ya vitu alivyopokea Mhe. Lukuvi kwa ajili ya wahanga hao vikiwa katika gari ambavyo ni Chakula, Nguo , viatu na Madaftari.
Mhe. William Lukuvi akiwa na viongozi wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) ofisini kwake.
…………………………………………………

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi apokea Msaada kwa Wahanga wa mafuriko Iringa. Msaada huo ni kutoka Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) ambayo imemkabidhi Mhe. Lukuvi Unga kilo 155, Nguo na viatu balo 2, Sukari kilo 25 na Madftari Boksi 2 kwa ajili ya wahanga wa mafuriko jimboni kwake Isimaani.

Taasisi ya TGGA ni shirika lisilo la Kiserikali na ni chama cha kujitolea kinachojishughulisha na kuwaendeleza Wanawake pamoja na Watoto wa kike katika maswala ya kijamii na kiuchumi kwa kuwapa elimu na mafunzo

Blackfox yapata mwekezaji Kampuni ya mitindo yapata mwekezaji

$
0
0
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Blackfox Models Aj Mynah akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kumpata muwekezaji ambae atawezesha kufungua ofisi itakayokuwa na sehemu ya kupigia picha na kufungua ofisi kwenye nchi nyingine mwaka ujao,katika mkutano uliofanyika leo jijini Daer es Salaam kushoto ni mwekezaji huyo David Johansson.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Blackfox Models Aj Mynah na mwekezaji huyo David Johansson wakisani mkataba katika mkutano uliofanyika leo jijini Daer es Salaam.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Blackfox Models Aj Mynah akimkabidhi tishet mwekezaji huyo David Johansson leo jijini Daer es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Blackfox Models Aj Mynah na mwekezaji huyo David Johansson wakiwa katika picha ya pamoja na Models leo jijini Daer es Salaam.
KAMPUNI ya inayojishugulisha na masuala ya mitindo nchini Blackfox Modeling Agency imeahidi kuwaendeleza vijana zaidi katika fani hiyo baada ya kupata mwekezaji mpya kutokea nchini Uingereza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa utiaji wa saini wa mkataba wa makubaliano na mwekezaji huyo, mmiliki wa Blackfox Aj Mynah alisema kuwa hatua hiyo itafungua milango ya wanamitindo wa Tanzania nje ya nchi.Alisema kuwa mkataba huo unalenga kuiongezea nguvu zaidi kampuni ya BlackFox katika harakati zake za kuiendeleza fani ya mitindo nchini na kuifanya kuwa ya kimataifa zaidi.

“Kama inavyofahamika kuwa fani hii ya mitindo nchini sio kongwe sana ikilinganishwa na nchi nyingine hivyo basi makubaliano haya yanalenga kuifikisha kampuni ya Blackfox kuwa ya kimataifa zaidi inayoweza kusaidia mamilioni ya vijana sio tu hapa nchini bali hata nje ya Tanzania” alisema Aj.

Aliongeza kuwa kampuni hiyo inalenga kufungua milango nchi nyingine za Afrika Mashariki, Afrika na hata kwenda katika nchi za Ulaya na Amerika.Alisema kuwa kampuni hiyo imewandaa vijana wengi kuingia katika fani ya mitindo na kujiajili kama wanamitindo, matangazo na mengineo mengi.Alisema kuwa chini ya mkataba huo wanamitindo wa hapa nchini wataweza kwenda kufanya kazi katika nchi za Ulaya na kwengineko.

Kwa upande wake mwekezaji huyo David Johansson alisema kuwa ameamua kuingia mkataba na Balck fox kutokana na fursa zilizopo hapa nchini kupitia fani hiyo.Alisema kuwa Tanzania inao wadada na wakaka ambao wanaweza kutangaza matangazo mbalimbali ya kimataifa na hata kufanya kazi nyingine zinazoendana na fani hiyo.

TAASISI YA WIPA YAJA NA SULUHISHO UWAJIBIKAJI KATI KUPUNGUZA MIGOGORO KATI YA SERIKALI NA WANANCHI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wajibu,  Ludovick  Utouh akizungumza na wadishi wa habari jijini Dar ers Salaam jana.Kushoto ni Afisa mahusiano Hassan Kisena. 

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

SERIKALI imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa kutowajibika ipasavyo kwenye matatizo yao  kutokana na kutokuwepo kwa kiunganishi cha moja kwa moja kati ya wawakilishi na wanaowakilishwa.


Hayo amesema leo Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Fikra ya Uwajibikaji Nchini (WIPA), Ludovick Utouh wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kutokana na kiunganishi nchi nyingi zimeingia katika migogoro kati ya wananchi na serikali zao yanayosababishwa na maamuzi ambayo yanaathiri maisha yao.


Amesema kuwa kuwa taasisi hiyo imeanzishwa kwa ajili ya masuala ya uwajibikaji na utawala bora kwa kufungua mlango utakaochochea na kuongeza uelewa mpana wa dhana ya uwajibikaji na utawala bora nchini.


 “Kuwezesha Wananchi Kushiriki Kikamilifu Kwenye Masuala ya Uwajibikaji na Utawala Bora Katika Usimamizi wa Rasilimali za Umma” amesema Utouh. Amesema  uhamasishajRi wa wananchi kwenye ushiriki katika masuala ya uwajibikaji na utawala bora ni  jambo  la  msingi  katika  kuhakikisha  maendeleo  yaliyopatikana  katika  utekelezaji  wa dhana hii yanakuwa endelevu.

Aidha amesema  jitihada za kuimarisha uwajibikaji nchini zilitaachiwa Bunge na taasisi za usimamizi za serikali peke yao, uwezekano wa kufanikisha utekelezaji huu  utakuwa  ni  mdogo  kwa  sababu  suala  la  uwajibikaji  linahitaji  ushiriki  wa  wadau mbalimbali ili kuleta tija kwa taifa. 


Ludovick Utouh Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) – Mstaafu kwa kushirikiana  na  aliyekuwa  Mtendaji  Mkuu  wa  Shirika  la  Maendeleo  la  Mafuta  nchini ,(TPDC),Yonna Killagane waliona hitaji la kuanzisha Taasisi-Fikra ya Usimamizi isiyo ya  kiserikali  itakayomilikiwa  na  wananchi  wenyewe  ambayo  itahusika  na  uchambuzi  wa mfumo na masuala ya uwajibikaji na utawala bora nchini. 

Amesema wameandaa mkutano wa kwanza  wa kimataifa    utakaohusu  uwajibikaji  katika  sekta  ya  gesi  asilia  na  mafuta  kwa  kuzingatia  umuhimu wa sekta hii kwenye maendeleo ya nchi utakaofanyika kuanzia Aprili 11 hadi 12 Aprili 2016 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere


Amsema wazungumzaji katika mkutano huo ni nchi  ambao  ni  pamoja  na,  Al  Kassim  Mtaalam  wa  mafuta  na  gesi  kutoka  Norway, Prof.  Patrick  Lumumba  kutoka  Kenya,  Bw.  Lai  Yahya  kutoka  Nigeria;  kwa  upande  wa Tanzania  ni  pamoja  na  Mtendaji  Mkuu  wa  TWAWEZA,   Aidan  Eyakuze,  Dk  Abel Kinyondo kutoka REPOA na Prof. Honest Ngowi wa Chuo Kikuu Mzumbe. 

MAMA JANETH MAGUFULI AWATAKA WADAU KUJITOKEZA KUSAIDIA WAZEE NA WATU WASIOJIWEZA.

$
0
0
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei mara baada ya kumaliza kuongea na wazee
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akishiriki katika kukabidhi misaada mbalimbali iliyotolewa na wadau mbalimbali wakiwamo CRDB, PPF na Makampuni binafsi kwa ajili ya kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akishiriki katika kukabidhi misaada mbalimbali iliyotolewa na wadau mbalimbali wakiwamo CRDB, PPF na Makampuni binafsi kwa ajili ya kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wazee katika kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na watoto wakati wa hafla ya utoaji wa Misaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza Bukumbi Mkoani Mwanza
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa ndege Jijini Mwanza kushiriki zoezi la utoaji wa msaada wa vifaa mbalimbali kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Serikali, Chama pomaja na Wananchi walifika kumpokea alipowasili uwanja wa ndege Jijini Mwanza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Serikali, Chama pomaja na Wananchi walifika kumpokea alipowasili uwanja wa ndege Jijini Mwanza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiangalia burudani ya ngoma alipowasili uwanja wa ndege Jijini Mwanza.
Baadhi ya misaada iliyotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea shada la maua alipowasili kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitoa heshima na kuwasalimia wananchi walifika kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei.
Baadhi ya sehemu ya wazee wakiimba kwa furaha wakati hafla ya utoaji wa Msaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bi. Mwajuma Nyiruka akiongea na wananchi waliojitokeza katika hafla ya utoaji wa Msaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza na kumshuruku Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa kushiriki katika hafla hiyo.
Afisa Mfawidhi na Mlezi wa Kituo kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza kilicho chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii Bw. Michael Bundala akiongea na wananchi na kushukuru wadau waliotoa msaada katika kituo hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akiongea na wazee wa kituo kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza, wananchi waliohudhuria hafla ya utoaji wa Msaada katika kituo hicho na kumshukuru Mama Janeth Magufuli kwa kuwakumbusha juu ya utoaji msaada na kuwajali wazee na watu wasiojiweza na kumahidi kuandaa sera mpya ya kusaidia watu wenye mahitaji.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akicheza ngoma na wazee wa Kituo kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo akimkaribisha Mama Janeth Magufuli kuongea na Wazee na pia kuwahakikishia wazee kuwa serikali ya awamu ya tano itaendelea kusimamia katika ahadi zake hasa katika kuhakikisha wazee wanapata huduma bila usumbufu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea na wazee katika Kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Bukumbi Mkoani Mwanza wakati wa hafla ya kutoa msaada wa vifaa mbalimbali na kuyashukuru mashirika, Taasisi za serikali pamoja na sekta binafsi kwa kutoa misaada hiyo ikiwemo Mchele, Unga, Maharage, Mafuta ya kupikia, mashine za kufulia pamoja na solar panel pia akatoa rai kwa wadau wengine kujitolea kusaidia wazee na watu wasiojiweza.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei mara baada ya kumaliza kuongea na wazee

NEWZ ALERT:Rais Magufuli amteua Balozi Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi,OMBENI SEFUE KUPANGIWA KAZI NYINGINE

$
0
0




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Kabla ya Uteuzi huo, Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India.

Uteuzi wa huu unaanza Mara moja.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
06 Machi, 2016.



DONDOO ZA HABARI MAGAZETINI.

Airtel Fursa yawezesha vijana kwa milioni 15 Manyara.

$
0
0
Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki (wa kwanza kushoto) akitoa maelekezo  kwa  Kijana Frank Rowland ( katikati)  kabla ya kumkabidhi banda la kuku la kisasa na kuku  100 wa kienyeji  kutoka Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA wa kuwezesha vijana hapa nchini  katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao, wilaya ya Hanang, Manyara hapo jana. Wanaoshuhudia ni ndugu zake Frank na wafanyakazi wa Airtel waliojumuika katika hafla hiyo.
 Kijana Frank Rowland (wa pili kushoto) anayejishughulisha na ufugaji wa kuku , akitoa maelekezo  kwa Afisa uhusiano na matuki wa Airtel Dangio Kaniki ( wa pili kulia) na Meneja wa mauzo kanda ya Manyara Peter Kimaro (kushoto) jinsi anavyotunza kuku baada ya kukabidhiwa na Airtel Tanzania, msaada wa  banda la kuku la kisasa na kuku  100 wa kienyeji , kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao, wilaya ya Hanang, Manyara hapo jana. Akishuhudiwa na mama yake Doris Kombe (kulia)
 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel , Dangio Kaniki (wa pili kulia) akipiga makofi pamoja na mama yake na Kijana aliyewezeshwa na Airtel Fursa   Doris Kombe (kushoto) na wafanyakazi wengine wa Airtel  wakati  wa hafla ya kumkabidhi vifaa hivyo Kijana Charles Samuel (wa pili kushoto).
 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa pili kulia), akimkabidhi kijana Charles Samuel (wa pili kushoto), anayejishughulisha na ufundi wa umeme, kadi ya pikipiki kama baadhi ya misaada aliyopatiwa na Airtel kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao mtaa wa Nakwa, Babati mjini hapo jana. Wanaoshuhudia ni Afisa masoko Airtel mkoa wa Arusha Geoffrey Sayore ( kulia), afisa mauzo kanda ya Babati Johnson Zephania (katikati) na mama yake mzazi Charles Doris Kombe (kushoto)
 Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa pili kulia), akimkabidhi kijana Charles Samuel (kushoto), anayejishughulisha na ufundi wa umeme, msaada wa vifaa mbali mbali vya ufundi na pikipiki kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwao mtaa wa Nakwa, Babati mjini hapo jana. Wanaoshuhudia ni Afisa masoko Airtel mkoa wa Arusha Geoffrey Sayore ( kulia) na afisa mauzo kanda ya babati  Johnson Zephania  (wa pili kushoto).

·        Wajasiliamali kupatiwa vitendea kazi vya milioni 20 kila wiki na Airtel FURSA.
 KMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA imeendelea kutoa msaada kwa vijana mkaoni Manyara wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 wakiwa na lengo la kutimiza dhamira yake ya kuwawesha vijana nchini kuweza kujipatia kipato na ajira.

Akizungumza Mkoani Manyara Meneja Mauzo wa Airtel Brighton Majwala amesema “Airtel FURSA baada ya kuendesha semina ya Ujasiliamali mwezi uliopita tulikutana na zaidi ya vijana 300 walijitokeza nakuzifahamu vyema FURSA zinazowazunguka ili kujitengenezea ajira. Leo hiii tumekuja kuwawezesha hawa walioonyesha bidi zaidi”

Kwa upande wake Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki ameeleza kuwa “Airtel tuko tayari kutumia zaidi ya milioni 20 kila wiki kuwawezesha vijana wanaojitokeza na kuonyesha wanania ya kujiendeleza hapa nchini’.

Nae kwa upande wake  kijana Frank Rowland kutoka wilaya ya Hanang aliyewezeshwa na Airtel Fursa alishukuru kwa kuwezeshwa na Airtel, sitakaa bure, ntahakikisha ninauendeleza mradi huu unisaidie kimaisha na kuwawezesha pia vijana wenzangu kupata ajira ntakazo wapa" alisema Frank.

Kijana mwingine aliyenufaika na Airtel Fursa ni fundi umeme, Charles Samuel, mkazi wa mtaa wa Nakwa, Babati mjini, ambaye amepewa msaada wa pikipiki na vitendea kazi vingine kwaajili ya kufanyia biashara ya kutembelea wateja watakaohitaji huduma yake ya ufundi.

Charles aliishukuru Airtel na kuongeza kuwa usafiri na zana alizozipata zitachochea mafanikio yake kimaisha na kuwataka vijana wenzake kuchangamkia fursa zinazotolewa na Airtel ili waweze kuondokana na umasikini

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji wa Katesh, wilaya ya Hanang, Michael Severine, ameishukuru kampuni ya simu ya Aitel kwa kutimiza ndoto za vijana kiuchumi kupitia mradi huo wa Airtel Fursa.

"Tulikuwa tunaambiwa  watu wanatoa hongo ili wapatiwe mitaji kwa njia ya upendeleo, na Airtel lakini kwa kumwezesha kijana mjasiriamali wa Hanang, tena kwenye kitongoji cha Katesh 'B", nimebaini kuwa ni uongo na uzushi" aliongeza mwenyekiti huyo.


BASATA YAWAPONGEZA WASANII LULU NA RICH RICH KUSHINDA TUZO ZA AMVCA 2016.

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini linapenda kutoa pongezi za dhati kwa Wasanii Singo Mtambalike (Rich Rich) na Elizabeth Michael (Lulu) kwa kushinda tuzo za African Magic Viewers’ Choice Awards (AMVCA2016) zilizotolewa mwishoni mwa wiki nchini Nigeria na kushuhudiwa na Dunia kupitia luninga na mitandao ya kijamii.

Katika tuzo hizo Msanii Singo Mtambalike ameshinda tuzo ya Filamu Bora ya Lugha ya Asili (Best Local Language - Swahili) kupitia filamu ya ‘Kitendawali’ huku Msanii Elizabeth Michael (Lulu) akishinda tuzo ya Filamu Bora ya Afrika Mashariki (Best Movie -Eastern Africa) kupitia filamu yake ya ‘Mapenzi’
Kuteuliwa na kushinda kwa Wasanii wa Tanzania katika tuzo hizi zilizoshirikisha wasanii na filamu nyingi za Afrika ni ishara kwamba wasanii wetu wanakubalika, kutambuliwa na kuthaminiwa ndani na nje ya Tanzania.

Aidha, ushindi huu unazidi kulipa heshima na kulitangaza taifa letu katika nyanja mbalimbali hivyo kuzidi kulifanya ling’ae na kuwa kinara katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.  

Baraza linatoa wito kwa wasanii na wadau wote kuzidisha ubunifu, bidii na weledi katika kazi wanazozifanya ili wasanii wengi zaidi waweze kuchomoza katika tuzo na majukwaa mbalimbali ya kimataifa kwa lengo la kulitangaza taifa na kukuza soko la kazi zao kimataifa.
Ni matumaini ya Baraza kwamba wasanii wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu za kutambuliwa na Serikali.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza
KAIMU KATIBU MTENDAJI

NIPE FAGIO YAUNGANA NA WAENDESHA BAJAJI KATIKA ZOEZI LA USAFI WA MTO MLALAKUWA JIJINI DAR.

$
0
0
Waendesha Bajaj kituo cha Survey kilichopo Mlalakua Dar es Salaam wakifanya usafi na baadhi ya wajumbe wa Taasisi ya Nipe Fagio kwenye eneo la pembezoni mwa mto Mlalakua baada ya taasisi hiyo kuwakabidhi vifaa mbalimbali vya usafi na programu ya usafi wa mto huo.
 Tania Hamilton, Mkurugenzi wa Taasisi ya Nipe Fagio inayoshughulikia uhifadhi mazingira akizungumza na Mwenyekiti wa Waendesha Bajaj wa Kituo Cha Survey, Aloyce Cassian wakati wa kufanya usafi katika eneo la Mto Mlalakuwa Dar es Salaam jana baada ya taasisi hiyo kuwakabidhi vifaa mbalimbali vya usafi na programu ya usafi wa mto huo. .
Tania Hamilton, Mkurugenzi wa Taasisi ya Nipe Fagio akizungumza na waendesha Bajaj wakati wa kufanya usafi katika eneo la Mwenge Dar es Salaam jana baada ya taasisi hiyo kuwakabidhi vifaa mbalimbali vya usafi na programu ya usafi wa mto huo.

BEI YA MADAFU HII LEO.

RAIS.DKT MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA FAMILIA YA BALOZI JOSEPH RWEGASIRA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Balozi Joseph Rwegasira, aliyefariki dunia jana tarehe 04 Machi, 2016 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.


Balozi Joseph Rwegasira amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.

Wakati wa uhai wake, Balozi Rwegasira amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini zikiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkuu wa Mkoa   wa Dar es Salaam na Balozi wa Tanzania nchini Zambia.


Katika salamu zake kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Rais Magufuli amesema Taifa litaukumbuka mchango mkubwa uliotolewa na Marehemu Balozi Rwegasira katika harakati za kukuza diplomasia na kuleta amani katika nchini majirani.


Rais Magufuli ameongeza kuwa Marehemu Balozi Rwegasira alikuwa mchapakazi, muadilifu na mzalendo wake kweli kwa nchi yake.

"Tungependa kuendelea kumuona Marehemu Balozi Rwegasira akiwa hai, lakini siku zote kazi ya Mungu haina makosa, namuombea kwa Mwenyezi Mungu apumzishwe mahali pema peponi, Amina" Amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amewataka familia, ndugu, jamaa na marafiki wote kuwa wavumilivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu na kwamba anaunga nao katika kumuombea marehemu.


Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es Salaam

05 Machi, 2016.

Kongamano la Wanawake Serena Hoteli Lafana

$
0
0
Keki-ikikatwa-na-Emelda-Mwamanga-kutoka-Vital-Voices-Global-Partnership-kwa-kushirikiana-na-Shamim-Khan-kulia-na-Edna-Mdoe-wakisoma-hutuba-kutoka-Tazania-women-Interfaith-Network. 
Keki-ikikatwa-na-Emelda-Mwamanga-kutoka-Vital-Voices-Global-Partnership-kwa-kushirikiana-na-Shamim-Khan-kulia-na-Edna-Mdoe-kutoka-Tazania-women-Interfaith-Network.Baadhi ya wanawake walioshiriki katika kongamano la wanawake lililofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam jana wakifuatilia mada anuai. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Vital Voices Global Partnership limefanyika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8 Baadhi ya wanawake walioshiriki katika kongamano la wanawake lililofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam jana wakifuatilia mada anuai. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Vital Voices Global Partnership limefanyika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8.Mmoja wa watoa mada akitoa mada Mmoja wa watoa mada akitoa mada.Baadhi ya wanawake walioshiriki katika kongamano la wanawake lililofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam jana wakifuatilia mada anuai. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Vital Voices Global Partnership limefanyika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8 Baadhi ya wanawake walioshiriki katika kongamano la wanawake lililofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam jana wakifuatilia mada anuai. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Vital Voices Global Partnership limefanyika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8.Shamim Khan (kulia) na Edna Mdoe wakisoma hutuba kutoka-Tazania women Interfaith Network Shamim Khan (kulia) na Edna Mdoe wakisoma hutuba kutoka-Tazania women Interfaith Network.Wadau mbalimbali Wadau mbalimbali.Watoa mada  wakipata picha Watoa mada wakipata picha.
Meneja Masoko kutoka Jubilee Insurance, Francisca Mushi akizungumza Meneja Masoko kutoka Jubilee Insurance, Francisca Mushi akizungumza.Baadhi ya watoa mada wakibadilishana mawazo Baadhi ya watoa mada wakibadilishana mawazo.Baadhi ya wanawake waliohudhuria katika Kongamano hilo Baadhi ya wanawake waliohudhuria katika Kongamano hilo.Tauas Likokola akifuatilia mada Taus Likokola akifuatilia Mada.Modesta Mbughuni Mwenyekiti wa Malengo Women akitoa mada katika Kongamano hilo Modesta Mbughuni Mwenyekiti wa Malengo Women akitoa mada katika Kongamano hilo.Wadau wa kongamano wakifuatilia mada Wadau wa kongamano wakifuatilia mada.Wadau mbalimbali waliohudhuria katika Kongamano wakipata picha ya pamoja Wadau mbalimbali waliohudhuria katika Kongamano wakipata picha ya pamoja,mtoa mada-Gloria Shechambo katika kongamano lililofanyika Serena Dar es salaam mtoa mada-Gloria Shechambo katika kongamano lililofanyika Serena Hotel Dar es salaam.Belinda MlingoKatibu NGO ya TASOI 
Belinda Mlingo Katibu wa NGO ya TASOIDr Chris Mauki Kutoka chuo Kikuu cha Dar essalaam Dr Chris Mauki Kutoka chuo Kikuu cha Dar essalaam.Emelda Mwamanga kutoka Vital Voices Global Partnership  
Emelda Mwamanga kutoka Vital Voices Global Partnership.washiriki washiriki[/caption]   [caption id="attachment_68683" align="alignnone" width="782"]Bidhaa mbalimbali Bidhaa mbalimbali[/caption] [caption id="attachment_68684" align="alignnone" width="649"]Bidhaa mbalimbali za vipodozi Bidhaa mbalimbali za vipodozi[/caption] [caption id="attachment_68685" align="alignnone" width="800"]Bidhaa mbalimbali Bidhaa mbalimbali[/caption] [caption id="attachment_68686" align="alignnone" width="1000"]Burudani mbalimbali Burudani mbalimbali[/caption] [caption id="attachment_68687" align="alignnone" width="800"]Bidhaa mbalimbali Bidhaa mbalimbali[/caption] [caption id="attachment_68688" align="alignnone" width="800"]wakisalimiana wakisalimiana[/caption] [caption id="attachment_68689" align="alignnone" width="669"]Baadhi ya wanawake waliohudhuria katika Kongamano wakifurahia jambo Baadhi ya wanawake waliohudhuria katika Kongamano wakifurahia jambo[/caption] [caption id="attachment_68690" align="alignnone" width="800"]Baadhi ya wanawake walioshiriki katika kongamano la wanawake lililofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam jana wakifuatilia mada anuai. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Vital Voices Global Partnership limefanyika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8 Baadhi ya wanawake walioshiriki katika kongamano la wanawake lililofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam jana wakifuatilia mada anuai. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Vital Voices Global Partnership limefanyika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8[/caption] [caption id="attachment_68691" align="alignnone" width="785"]Baadhi ya wanawake walioshiriki katika kongamano la wanawake lililofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam jana wakifuatilia mada anuai. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Vital Voices Global Partnership limefanyika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8 Baadhi ya wanawake walioshiriki katika kongamano la wanawake lililofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam jana wakifuatilia mada anuai. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Vital Voices Global Partnership limefanyika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8[/caption] IMG_0075 [caption id="attachment_68696" align="aligncenter" width="485"]upande wa Kushoto ni Emelda Mwamanga kutoka Vital Voices Global Partnership na upande wa kulia Belinda Mlingo Katibu NGO ya TASOI upande wa Kushoto ni Emelda Mwamanga kutoka Vital Voices Global Partnership na upande wa kulia Belinda Mlingo Katibu NGO ya TASOI[/caption]
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images