Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 785 | 786 | (Page 787) | 788 | 789 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Meneja Mkuu Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk alipokuwa akizungumza na wandishi wa Habari kuhusu uvumi ulionea kwamba litasitisha  huduma ya kuuza umeme kwa siku kadhaa katika Mkutano uliofanyika Ofisi za ZECO ziliopo Bulioni Mjini Zanzibar.

  Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar .
  Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) limekanusha uvumi ulionea kwamba litasitisha  huduma ya kuuza umeme kwa siku kadhaa na kusababisha ghofu kwa wateja  na kupelekea msongamano katika vituo vya kununulia umeme vya Shirika hilo katika siku za karibuni.

  Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Makadara, Meneja Mkuu wa ZECO ndugu Hassan Ali Mbarouk amesema kuongezeka kwa wateja katika vituo vya kuuzia umeme vya Shirika hilo kumesababishwa kukosekana huduma hiyo kwa kutumia simu za mkononi za Zantel kwa Easy pesa.

  Ndugu Mbarouk amesema huduma ya kununua umeme katika vituo vyote vya ZECO itaendelea kama kawaida kwa siku zote na hakutakuwa na kuzimika wala kusita kuuza umeme katika vituo hivyo.

  Hata hivyo amesema huduma ya kununua umeme  kwa kutumia  simu za mkononi kwa njia ya easy pesa itaendelea kukosekana  na amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati huu ambapo ZECO na Zantel  wanaendelea kulitafutia ufumbuzi tatizo lililojitokeza.

  Amesema kukosekana  huduma hiyo  kwa njia ya easy pesa imesababishwa na mfumo  huo  kupata matatizo kuanzia tarehe 20 mwezi uliopita.
  Amewahakikisha watumiaji wa umeme kwamba tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi katika kipindi kifupi kijacho kwani mkataba wa mwanzo wa miaka miwili wa ZECO na Zantel utakapo malizika  mkataba mpya utatoa fursa kwa mashirika mengine ya simu kuingia mkataba wa kuuza umeme.

  Akizungumzia zoezi linaloendelea la kubadilisha mita za zamani na kuweka mita za Tukuza, Menaja Mkuu amesema  Shirika limepanga itakapofika  mwishoni mwa mwaka 2017  wateja wote wa umeme watakuwa wanatumia mita za  Tukuza.

  Amesema pamoja na mafanikio makubwa waliyopata ya kubadilisha mita za zamani wanawasi wasi kwa baadhi ya wateja wasiowaaminifu kuzihujumu mita za Tukuza na kulikosesha fedha shirika kwani mita hizo zinachukua muda mkubwa kukaguliwa baada ya kuwekwa tafauti na mita za zamani ambazo hukaguliwa kila mwezi.

  Meneja Biashara wa Shirika la umeme Zanzibar ndugu Thabit Salum Khamis amewaeleza waandishi wa habari kuwa usambazaji umeme katika visiwa vya Unguja na Pemba umefikia asilimia 86 lakini watumiaji umeme ni chini ya asilima 50.

  Ndugu Thabit amewataka wananchi kubadili mfumo wa maisha kwa kutumia  zaidi  umeme kwani ni rahisi  kwa matumizi ya nyumbani ikilinganishwa na nishati ya kuni na mkaa.       
          

  0 0

  Meneja Mkuu Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) Hassan Ali Mbarouk alipokuwa akizungumza na wandishi wa Habari kuhusu uvumi ulionea kwamba litasitisha huduma ya kuuza umeme kwa siku kadhaa katika Mkutano uliofanyika Ofisi za ZECO ziliopo Bulioni Mjini Zanzibar.


  Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar 

  Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) limekanusha uvumi ulionea kwamba litasitisha huduma ya kuuza umeme kwa siku kadhaa na kusababisha ghofu kwa wateja na kupelekea msongamano katika vituo vya kununulia umeme vya Shirika hilo katika siku za karibuni.

  Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Makadara, Meneja Mkuu wa ZECO ndugu Hassan Ali Mbarouk amesema kuongezeka kwa wateja katika vituo vya kuuzia umeme vya Shirika hilo kumesababishwa kukosekana huduma hiyo kwa kutumia simu za mkononi za Zantel kwa Easy pesa.

  Ndugu Mbarouk amesema huduma ya kununua umeme katika vituo vyote vya ZECO itaendelea kama kawaida kwa siku zote na hakutakuwa na kuzimika wala kusita kuuza umeme katika vituo hivyo.

  Hata hivyo amesema huduma ya kununua umeme kwa kutumia simu za mkononi kwa njia ya easy pesa itaendelea kukosekana na amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati huu ambapo ZECO na Zantel wanaendelea kulitafutia ufumbuzi tatizo lililojitokeza.Amesema kukosekana huduma hiyo kwa njia ya easy pesa imesababishwa na mfumo huo kupata matatizo kuanzia tarehe 20 mwezi uliopita.

  Amewahakikisha watumiaji wa umeme kwamba tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi katika kipindi kifupi kijacho kwani mkataba wa mwanzo wa miaka miwili wa ZECO na Zantel utakapo malizika mkataba mpya utatoa fursa kwa mashirika mengine ya simu kuingia mkataba wa kuuza umeme.

  Akizungumzia zoezi linaloendelea la kubadilisha mita za zamani na kuweka mita za Tukuza, Menaja Mkuu amesema Shirika limepanga itakapofika mwishoni mwa mwaka 2017 wateja wote wa umeme watakuwa wanatumia mita za Tukuza.

  Amesema pamoja na mafanikio makubwa waliyopata ya kubadilisha mita za zamani wanawasi wasi kwa baadhi ya wateja wasiowaaminifu kuzihujumu mita za Tukuza na kulikosesha fedha shirika kwani mita hizo zinachukua muda mkubwa kukaguliwa baada ya kuwekwa tafauti na mita za zamani ambazo hukaguliwa kila mwezi.

  Meneja Biashara wa Shirika la umeme Zanzibar ndugu Thabit Salum Khamis amewaeleza waandishi wa habari kuwa usambazaji umeme katika visiwa vya Unguja na Pemba umefikia asilimia 86 lakini watumiaji umeme ni chini ya asilima 50.

  Ndugu Thabit amewataka wananchi kubadili mfumo wa maisha kwa kutumia zaidi umeme kwani ni rahisi kwa matumizi ya nyumbani ikilinganishwa na nishati ya kuni na mkaa. 

  0 0

   Mbunge wa viti maalum, Faharia Khamis Shomari  akizungumza na Wajumbe wa Umoja wa WanawakeTanzania (UWT) katika ukumbi wa CCM Mkoa pichani hawapo kwenye sherehe ya makabiziano ya magari hayo yalio fanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa Amani Zanzibar.
   Mhe: Faharia  Shomari Khamis akimkabidhi funguo Mgeni Rasmi katika sherehe za Makabidhiano Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai kwaajili ya kuwakabidhi wahusika.
   Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akitoa shukurani  kwa Mhe Faharia  na kuwataka wanawake wengine kuiga mfano wake wa kujitolea ndani ya chama,hafla ya Makabidhiano hayo ilifanyika katika ukumbi wa  CCM Mkoa Amani Zanzibar.
   Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akimkabidhi funguo za Gari Mwakilishi wa Umoja wa Wanawake UWT Tanzania Asha Mzee ambazo zimetolewa na Mhe. Faharia Shomari Khamis.

   Mwakilishi kutoka Umoja wa Wanawake UWT Tanzania, Asha Mzee akilifungua gari walilokabidhiwa na Mhe. Faharia  Shomar Khamis.
  Magari aina ya Noha waliokabidhiwa Umoja wa Wanawake UWT Tanzania.(PICHA NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR).

  0 0


  Aliyekuwa Mwenyekiti wa vyama vya wafanyakazi JUWATA, Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Pwani na baadaye balozi wa Tanzania nchini Zambia halafu akawa Waziri wa viwanda na Biashara, na baadaye waziri wa Kazi na mwisho Waziri wa mambo ya nchi za nje, Ndugu Joseph Clemence Rwegasira amefariki dunia leo saa kumi alfajiri.Mzee Rwegasira alizaliwa tarehe 21/03/1935.

  0 0

  Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kwenye gari kushoto) na Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela wakitoa heshima katika hafla ya kuagwa iliyofanyika Viwanja vya Twalipo Mgulani Dar es Salaam leo mchana. Maofisa Majenerali 16 waliostaafu Utumishi Jeshini waliagwa.

  Mkuu wa Majeshi, Jenerali, Davis Mwamunyange (kushoto), akisalimiana na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi hilo mstaafu, Luteni Jenerali, Samuel Ndomba.

  Mkuu wa Majeshi, Jenerali, Davis Mwamunyange (kushoto), akisalimiana na kumpongeza Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela katika hafla hiyo.
  Brigedia Jenerali mstaafu, Msangi (kulia mbele), akikagua gwaride maalumu waliloandaliwa maofisa hao wastafu wakati wakiagwa rasmi baada ya kumaliza utumishi wao jeshini.
  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), mstaafu Meja Jenerali, Raphael Muhuga, akikagua gwaride hilo.


  Gwaride likipita mbele ya jukwaa kuu kutoa heshima.


  Gwaride likipita mbele ya jukwaa kuu kutoa heshima.
  Wanafamilia wa wastaafu hao wakiwa kwenye hafla hiyo ya kuagwa jamaa zao.
  Ukaguaji gwaride rasmi ukiendelea.
  Maofisa hao wastaafu wakiwa jukwaa kuu.
  Hapa maofisa hao wakiwa wamesimama wakati gwaride likipita jukwaa kuu na kutoa heshima.
  Askari wa JWTZ wakifuatia matukio mbalimbali kwenye 
  hafla hiyo.
  Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba, akikagua gwaride hilo maalumu kwa ajili ya kuagwa.
  Wapiga picha wa magazeti wakiwa kazini kuchukua matukio mbalimbali.
  Taswira ya jukwaa kuu katika hafla hiyo.
  Wastaafu hao wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa majeshi.
  Mkuu wa majeshi, Davis Mwamunyange (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa majeshi wastaafu. Kushoto Robert Mboma na George Waitara (kulia).
  Mkuu wa majeshi akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali, Samuel Ndomba.
  Hapa ni furaha tupu kwa kustaafu utumishi ndani ya jeshi.
  Askari wa JWTZ wakiwa imara wakati wa kuwaaga maofisa hao.
  Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kwenye gari kushoto) na Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela wakitoa heshima katika hafla ya kuagwa iliyofanyika Viwanja vya Twalipo Mgulani Dar es Salaam.
  Hapa ni saluti wakati wakiwaaga wapiganaji wenzao.

  Na Dotto Mwaibale

  JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limewaaga Mameja generali, Luteni na Brigedia Generali 16, akiwemo, aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Luteni Generali Samwel Ndomba.

  Tukio la kuwaaga majenerali hao ambao wamestaafu  utumisho wao jeshini limefanyika jijini Dar es Salaam leo katika viwanja Twalipo Mgulani saa tatu hadi saa tatu asubuhi ambapo liliambatana na gwaride maalumu la vikosi mbalimbali vya Anga, nchini kavu, majini pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

  Hafla hiyo ya kuwaaga Magenerali hao iliongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Davis Mwamunyange ambapo waaga hao ni wa vyeo mbalimbali vya Brigedia Generali waliokuwa nane, Meja Jenerali sita na Luteni wawili na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali na wastaafu wa jeshi hilo.

  Majenerali hao kila mmoja alipata fursa ya kukagua gwaride kila alipowasili viwanjani hapo ambapo kati yao ni Luteni Generali walipata heshima ya pekee na kufanyiwa gwaride lililokuwa tofauti na wengine.

  Majenerali hao ni Mnadhim Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama JWTZ, Luteni Jenerali Samwel Ndomba ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mkuu wa Utumishi katika jeshi hilo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

  Wengine ni Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi jeshini, Luteni Jeneral Paul Ignas ambaye pia aliwahi kuwa ni Mkuu wa Mjeshi ya kulinda amani Darfur nchini Sudani.

  Kwa upande wa Mameja Jenerali ambao walipewa heshima na kukagua vikosi hivyo ni Mkuu wa Jeshi la Nchi kavu, Meja Jenerali Salum Kijuu, Mkuu wa Utumishi Jeshini, Meja Jenerali Vicent Mlitaba, Mkuu wa Jeshi la Anga, Meja Jenerali Joseph Kapwani, Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu kilichopo Duruti mkoani Arusha Meja Jenerali Ezekiel Kiunga.

  Wengine ni Mkuu wa Shirika la Mzinga mkoani Morogoro, Meja Jenerali Chalres Mzanila, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Mhunga.

  Na wengine ambao ni Mabrigedia ni Mkuu wa Chuo cha Kijeshi cha Sayansi ya Tiba Lugalo, Brigedia Jenerali Dk.Luhindi Msangi , Mkuu Tawi la Ukaguzi jeshini ambaye pia aliwahi kuwa mkaguzi wa majeshi ya SADC, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga.

  Wengine ni Mkuu wa Tawi la Akiba, Brigedia Jenerali Agustino Gailanga ambaye pia aliwahi kuwa mpambe wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Mratibu wa Miradi ya Maendeleo Jeshini, Brigedia Jenerali Mrisho Abdallah , Mkuu wa Kikosi cha Ndege cha usafirishaji, Brigedia  Jenerali Ezra Ndimugwango.

  Na wengine ni Kamanda wa Brigedi ya Tembo mkoani Songea, Brigedia Jenerali John Chacha, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa jeshini, Brigedia Jenerali Martini Mwankanye na Mkuu wa Shule ya 'Eflantria' mkoani Arusha, Brigedia Harodi Mzirai.

  Akizungumza mara baada ya hafla hiyo Luteni Jenerali mstaafu Ndumba alifurahia hatua hiyoa na kubainisha kuwa kwa sasa wanaenda kuanza maisha mapya.


  0 0

  Mwenyekiti wa Tamasha Upendo Gospel International, Amarido Charle's akizungumza na waandishi wa habarin (hawapo pichani) juu ya tamasha la pasaka litakalofanyika Machi 27 katika viwanja vya leadar's jijini Dar es Salaam,katika ni Maneja Uendeshaji, Shaweji Steven, Kushoto ni Meneja wa Gospel, Emmanuel Mweta.
  02.Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tamasha Upendo Gospel International, Amarido Charle's wakati akitangaza tamasha la pasaka la Machi 27 mwaka huu leo jijini Dar es Salaam
  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya jamii)

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  UPENDO Music Festival imeandaa tamasha la Injili litakalofanyika  Machi 27 mwaka huu katika viwanja vya Leader,s jijini Dar es Salaam .
  Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tamasha Upendo Gospel International, Amarido Charle's amesema  kuwa tamasha hilo litakuwa  na ubora kutokana na walivyoliandaa kwa miaka mingi na sasa imetimia waumini mbalimbali kuungana kuikaribisha pasaka.

  Charle's amesema kuwa tamasha litakuwa na vionjo mbalimbali kutoka kwa wasanii wa injili katika wa vikundi mbalimbali bila kujali kanisa analotaka.

  Amesema wamekuja katika tamasha kwa muonekano tofauti kwa wasanii kutumia majukwa tamasha hilo kujitangaza na sio kupigiwa simu hali hiyo ndio imesaidia nchi zilizoendelea kuwa na wasanii nyota kutokana na kujitoa katika matamasha.

  Tamasha hilo litakuwa na viingilio ikiwa kama sehemu ya uendeshaji wa uwanja na sio kwa ajili ya kujinufaisha kwa kuwa na kiingilio kwa mkubwa sh.5,000 na viti maalum kwa sh.10,000.

  Charle's amesema kuwa kuanzia majira saa nne kutakuwa na michezo mbalimbali katika viwanja hivyo nia ikiwa na kutambua na vipaji vingine vya michezo.

  0 0

  Diwani wa Kata ya Tabata, Patric Assenga akizungumza na wananchi wa Segerea ambao walifika katika Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi kusikiliza ombi la kibali cha kufungua kesi ya kupinga ubomoaji wa nyumba za wananchi wa segerea leo jijini Dar es Salaam,kulia ni Naibu Meya wa Ilala, Omary Kumbilamoto.kesi hiyo imearishwa na Jaji Fredrica Mgaya kutokana na wakili wa serikali kupatwa msiba na itasikilizwa tena Machi 8 mwaka huu katika mahakama hiyo.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na waandishi hawapo pichani mara baada ya kutoka Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi kusikiliza ombi la kibali cha kufungua kesi ya kupinga ubomoaji wa nyumba za wananchi wa segerea leo jijini Dar es Salaam, ,kesi hiyo imearishwa na Jaji Fredrica Mgaya kutokana na wakili serikali kupatwa msiba na itasikilizwa tena Machi 8 mwaka huu katika mahakama hiyo.
  Wananchi wa segerea wakiwasilikiliza viongozi wao Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi waliofika kusikiliza ombi la kibali cha kufungua kesi ya kupinga ubomoaji wa nyumba za wananchi wa segerea leo jijini Dar es Salaam,.kesi hiyo imearishwa na Jaji Fredrica Mgaya kutokana na wakili serikali kupatwa msiba na itasikilizwa tena Machi 8 mwaka huu katika mahakama hiyo. 

  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya jamii)

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence M. Melo (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufungua kesi Mahakama Kuu Dar es Salaam kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinavunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao ya kijamii. Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence M. Melo (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufungua kesi Mahakama Kuu Dar es Salaam kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinavunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao ya kijamii.Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao. Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao.]Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao. Baadhi ya wanasheria wa Jamii Media wakieleza kwa wanahabari dhumuni la kufungua kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao.

    KAMPUNI ya Jamii Media, waendeshaji wa mitandao ya JamiiForums.com na FikraPevu.com wametinga Mahakamani kufungua kesi ya kikatiba wakipinga baadhi ya vifungu vya sheria ya makosa ya mtandao kwa kile kuingilia Uhuru wa Maoni na Kujieleza wa wananchi. Jamii Media imefungua kesi hiyo Mahakama Kuu leo jijini Dar es Salaam, kesi namba 9 ya mwaka 2016 kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinasababisha kuvunjwa kwa haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao ili kulinda maslahi ya umma kwa kuzingatia vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

   Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence M. Melo mara baada ya kesi hiyo kufunguliwa mahakamani, alisema kampuni hiyo imelazimika kufungua kesi hiyo baada ya kushinikizwa mara kadhaa na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za baadhi ya wateja wao.

   Alisema takribani miezi mitatu iliyopita, Jeshi la Polisi limekuwa likiushinikiza mtandao huo kwa njia ya barua kutoa taarifa za baadhi ya wateja wake wanaoonekana kutoa taarifa zile ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaibua ufisadi mkubwa na ukwepaji wa kodi. 

   Aliongeza kuwa JamiiForums katika kuhakikisha inasimamia usiri (privacy) wa wateja wao, wamekuwa wakihoji mashinikizo hayo yanazingatia sheria gani na kutaka kujua ni vifungu gani vya sheria ambavyo wadau wa mtandao huo wamevivunja lakini wamekuwa hawapewi maelezo yanayoridhisha zaidi ya kuelezwa kuwa hatua zaidi zitachukuliwa kama hautatolewa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi. 

   "...Baada ya kupata mashinikizo takribani manne yanayoashiria kuwa haki ya watanzania watumiao mtandao wa intaneti na hasa watumiaji wa mtandao wa JamiiForums, Jamii Media imeshauriana na Wanasheria wake na kuona ni wakati sasa wa Kuilinda haki ya wananchi kupata taarifa na kulindwa kwa Uhuru wao wa Maoni na Kujieleza inayolindwa kwa mujibu wa Katiba ya Nchi ibaraya 18 ambapo imefungua Shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Kesi namba 9 ya mwaka 2016); kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinapelekea kuvunjwa kwa haki za msingi za watanzania watumiao mitandao ili kulinda maslahi ya umma kwa kuzingatia vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano," alisema Melo. Alibahinisha kuwa mtandao wa JamiiForums utaendelea na shughuli zake kama kawaida na utaendelea kuwahakikishia watumiaji wake kuwa mahala salama pa kutolea madukuduku yao na hata kuisaidia Serikali kuonyesha nyufa zilipo kwa maslahi mapana ya Taifa (wakizingatia mwongozo wa ushiriki wa mijadala anuai). 

   Alisema JamiiForums itaendelea kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli katika jitihada zake za kupambana na ufisadi kwa kutoa uwanja/fursa salama na rahisi kwa wananchi kuweza kuyaainisha yale wanayoyabaini kuwa yanachelewesha maendeleo ya Taifa lao. 

   Mtandao wa JamiiForums ni mtandao mkubwa wa Kiswahili kwa Afrika Mashariki na Duniani ukiwa na wasomaji wasiopungua Milioni 4 kwa mwezi ambapo kwa mwaka 2016, mtandao huu unatimiza rasmi miaka 10 tangu uanzishwe. Mtandao huu unasifika kwa kutoa fursa ya kipekee kwa watumiaji wake kutoa yaliyo mioyoni mwao huku wengine wakijifunza mbinu kadha wa kadha za kijasiriamali, afya, elimu na hata kuibuka wanasiasa wapya waliofundwa na wana JamiiForums. "Pamoja na kuendelea kutoa huduma hata katika nyakati ngumu, mtandao wa JamiiForums unakumbana mara kwa mara na changamotonyingi zinazopelekea waanzilishi na waendeshaji wake kuwa katika misukosuko mara kwa mara." Anasema Melo.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Bwa. Ammish Owusu Amoah akitowa maelezo kwa Washiriki wa Warasha ya Siku Mbili ya Kuwajengea Uwezo Wafanyabiashara kuibua Mipango ya Biashara iliowashirikisha Wadau mbalimbali katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
  Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Ammishi Owusu-Amoah akisisitiza jambo wakati wa ufungaji wa Warsha hiyo ya Siku mbili ilioandaliwa na Bank Of Africa kwa ajili ya wafanyabiashara na wadau kuweza kuweza kufanya Mpango wa Biashara. 
  Mtaalam wa Banking Tanzania Bwa,Michael Alcorn akitowa maelezo wakati wa Warsha hiyo ya Siku mbili kwa Wafanyabiashara wa Zanzibar ilioandaliwa na Bank Of Africa Tanzania iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.

  Washiriki wa Warsha hiyo wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mafunzo hayo.
  Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
  Meneja SME Banking Albert Nsato akizungumzia jinsi ya Bank yao inavyowajali wateja wao katika kuwapatia Mikopo kwa Wafanyabiashara Wakubwa na Wajasiriamali. 
  Meneja Bank of Africa Tawi la Zanzibar Ndg. Juma Burhan akizungumza wakati wa Warshac hiyo huduma zinazopatikana katika Bank yao kwa Wateja wao.
  Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika makundi kujifunza jinsi ya kupanga Mpango wa Biashara Zao ili kujenga na Kuboresha Uwezo wa Biashara. 
  Washiriki wakiwa katika makundi kujifunza kuboresha na kujenga Uwezo wa Biashara zao wakati wa Warsha hiyo ilioandaliwa na Bank Of Africa kwa Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Zanzibar. 
  Washiriki wakiwa katika makundi kujifunza kuboresha na kujenga Uwezo wa Biashara zao wakati wa Warsha hiyo ilioandaliwa na Bank Of Africa kwa Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Zanzibar. 
  Washiriki wakiwa katika makundi kujifunza kuboresha na kujenga Uwezo wa Biashara zao wakati wa Warsha hiyo ilioandaliwa na Bank Of Africa kwa Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa Zanzibar. 


  Washiriki wakiwasilisha kazi za makundi yao baada ya kutengeneza Mpango wa Biashara wakati wa mafunzo hayo yaliowashirikisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali ili kuwajengea Uwezo wa kutengeneza Mpango wa Kuboresha na Kujenga Biashara zao ili kuzikuza.  Washiriki wakiwasilisha kazi za makundi yao baada ya kutengeneza Mpango wa Biashara wakati wa mafunzo hayo yaliowashirikisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali ili kuwajengea Uwezo wa kutengeneza Mpango wa Kuboresha na Kujenga Biashara zao ili kuzikuza.  Washiriki wakiwasilisha kazi za makundi yao baada ya kutengeneza Mpango wa Biashara wakati wa mafunzo hayo yaliowashirikisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali ili kuwajengea Uwezo wa kutengeneza Mpango wa Kuboresha na Kujenga Biashara zao ili kuzikuza.  Washiriki wakiwasilisha kazi za makundi yao baada ya kutengeneza Mpango wa Biashara wakati wa mafunzo hayo yaliowashirikisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali ili kuwajengea Uwezo wa kutengeneza Mpango wa Kuboresha na Kujenga Biashara zao ili kuzikuza.  Washiriki wakiwasilisha kazi za makundi yao baada ya kutengeneza Mpango wa Biashara wakati wa mafunzo hayo yaliowashirikisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali ili kuwajengea Uwezo wa kutengeneza Mpango wa Kuboresha na Kujenga Biashara zao ili kuzikuza.  Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Tanzania Ndg. Ammish Owusu-Amoah akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo kulia Mshauri wa Banking Michael Alcorn, mafunzo hayo wa Siku Mbili yaliowashirikisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali na Wadau Zanzibar.   Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Tanzania Ndg. Ammish Owusu-Amoah akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo kulia Mshauri wa Banking Michael Alcorn, mafunzo hayo wa Siku Mbili yaliowashirikisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali na Wadau Zanzibar.   Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Tanzania Ndg. Ammish Owusu-Amoah akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo kulia Mshauri wa Banking Michael Alcorn, mafunzo hayo wa Siku Mbili yaliowashirikisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali na Wadau Zanzibar.   Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Tanzania Ndg. Ammish Owusu-Amoah akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo kulia Mshauri wa Banking Michael Alcorn, mafunzo hayo wa Siku Mbili yaliowashirikisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali na Wadau Zanzibar. 


  Imeandaliwa na OthmanMapara.Blogspot.com


  Zanzinews.com  0 0

   Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Bi. Angel Akilimali (kushoto)akiwa na mtoto wake pamoja na mumewe wakiweka udongo kwenye kaburi la mama yake marehemu Celina Akilimali.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Celina Akilimali mama mzazi wa Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Bi. Angel Akilimali.
   Mwenyekiti wa bodi ya Uhuru Alhaji Adam Kimbisa akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Celina Mfala Akilimali , mama mzazi wa Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM .
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwa kwenye ibada ya kumuombea marehemu Mama Celina Akilimali kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe .
    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho kwa  marehemu Mama Celina Mfala Akilimali ambaye ni mama wa Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Bi. Angel Akilimali kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe .
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya Uhuru Media Alhaji Adam Kimbisa kwenye makaburi ya kinondoni wakati wa mazishi ya Mama Celina Mfala Akilimali ambaye ni mama mzazi wa Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM B. Angela Akilimali.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na watangazaji wa radio Uhuru FM waliojitokeza kwenye mazishi ya mama Celina Akilimali, mama wa Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Angel Akilimali kwenye makaburi ya kinondoni jijini Dar es Salaam.


  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   
   Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad, amewasili Zanzibar alasiri YA LEO akitokea nchini India na Oman. Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege alilakiwa na viongozi kadhaa wa CUF na baadaye kuelekea kwenye makaazi yake, Mbweni.
    


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Maabara katika shule ya Sekondari ya Budalabugija wilayani Itilima akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 4, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Machi 4, 2016. (P:icha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua bwawa la umwagiliaji na maji ya kunywa la kijiji cha Mkoma na Mwalushu wilayani Itilima akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu, Machi 4, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwsalimia wananchi baada ya kukagua bwawa la maji ya kunywa na umwagiliaji la vijiji vya Mkomana Mwalushu wilayani Itilima Machi 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwsalimia wananchi baada ya kukagua bwawa la maji ya kunywa na umwagiliaji la vijiji vya Mkomana Mwalushu wilayani Itilima Machi 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Askofu wa Jimbo la Shinyanga, Liberatus Sangu wakati alipoitembelea shule ya Sekondari ya Mwamapalala wilayni Itirima akiwa katika zira ya mkoa wa Simiyu Machi 4, 2016. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)

  0 0


  0 0

  Kontena la Maskani ya kisonge Mjini Unguja laripiliwa kwa bomu na watu wasiojulikanwa usiku wa jana
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shei akipata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Maskani ya Kisonge John Mwakanjuki leo wakati alipotembelea maskani hiyo baada ya kupata hasara kubwa ya mripuko wa bomu na watu wasiojuilikanwa usiku wa jana
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akiangalia hasara iliyopatikana katika Maskani ya Kisonge iliyotokea jana kwa mripuko wa bomu uliosababishwa na watu wasiojuilikanwa, (wa pili kushoto) John Mwakanjuki alipotoa maelezo zaaidi kuhu tukio hilo leo wakati alipotembelea maskani hiyo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akizungumza na wanachama wa CCM na wapenda amani wakati alipofika katika Maskani ya Kisonge Mjini Unguja leo kuangalia hasara iliyopatikana kutokana na mripuko wa bomu uliosababishwa na watu wasiojuilikanwa jana usiku,

  0 0


  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffesa Makame Mbarawa kushoto akimsikilia Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika wakati  alipotembelea eneo la Mwambani kunapotarajiwa kujengwa Bandari ambapo alitembelea eneo hilo kujionea namna lilivyo.

  Wa pili kushoto ni Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffesa Makame Mbarawa akionyeshwa eneo litakalojengwa
  Bandari ya Mwambani na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika
  wakati alipotembelea eneo la Mwambani kunapotarajiwa kujengwa Bandari
  ambapo alitembelea eneo hilo kujionea namna lilivyo.

  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Proffesa Makame Mbarawa katikati akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya
  Tanga,Abdulla Lutavi wakati alipotembelea eneo ambalo kutajengwa
  bandari mpya ya Mwambani kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika.Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika kulia akisistiza jambo kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Proffesa Makame Mbarawa wakati alipofanya ziara ya kutembelea Bandari hiyo
  kulia ni PRO wa TPA Tanga,Moni Jarufu.Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry
  Arika wakati alipofanya ziara ya kutembelea leo kuangalia namna inayofanya kaz.
  WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameipa muda mpaka mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu,Kampuni ya mawasiliano ya Halotel iwe imekamilisha Kazi ya kufunga mkongo wa intaneti katika shule tatu za kila wilaya hapa nchini.

  Pia ameiagiza serikali mkoani Tanga kuifuatilia Kampuni ya mawasiliano ya Halotel kwa saababu imekuika taratibu za mkataba wake na serikali ambao alitakiwa kufunga mkongo wa mawasiliano ya intaneti kwenye shule tatu za sekondari kwa kila halmashauri ya wilaya lakini badala yake wamefunga Moderm ya 3G.

  Amesema moderm hizo za 3G haziendani na kasi ya teknolojia inayotumika kwa sasa na kwamba kitendo hicho ni ukiukwaji mkubwa wa mkataba huo na serikali ambao waliwekeana mwaka jana.Ametoa agizo hilo kwa kaimu mkuu wa mkoa wa Tanga, Abdulla Lutavi wakati alipokua akipokea taarifa ya mkoa ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo

  “Lengo la pamoja ni kuona maendeleo ya sekta ninazosimamia za miundombinu ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano zinaimarika na kuwawezesha watanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025”, amesema Prof. mbarawa.Amesisitza kuwa Serikali iliingia mkataba na Kampuni ya Halotel kwa makubaliano ya kufikisha huduma ya mawasiliano hasa vijijini na kuhakikisha inatoa huduma ya mtandao kwa ofisi za serikali wilayani na katika shule tatu katika kila wilaya jambo ambalo bado halijafanikiwa kwa kiasi kikubwa.

  “Tumepata taarifa kwamba hapa Tanga kuna shule za Old Tanga, Mikanjuni na Maweni wamefungiwia moderm tena za 3G tofauti na makubaliano sisi mkataba unaeleza kutumia mkongo sasa inakuaje”,alihoji Waziri Prof. Mbarawa.Katika hatua nyingine waziri Mbarawa ametembelea bandari ya Tanga na kuagiza kuanza kutumiwa kwa mfumo wa compyuta katika utendaji badala ya watu kutumia mfumo wa karatasi uliozoeleka ambao hauleti tija .

  Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha bandari inaongeza mapato kutoka takriban shilingi bilioni 600 mwaka uliopita hadi kufikia trilioni moja mwaka huu hivyo kusisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa kasi, weledi na kutumia mfumo wa kompyuta unaoleta uwazi.Amewataka wananchi wa eneo la Mwambani kutakakojengwa badari ya Tanga waondoke katika eneo hilo mara moja kwani wameshalipwa fidia na hatua iliyobaki ni serikali kuliendeleza eneo hilo.

  Ameiagiza Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kufanya upembuzi yakinifu haraka ili kuwezesha ujenzi wa bandari hiyo kuanza mara moja.“Bandari ndio moyo wa uchumi wa Tanzania hivyo fanyeni kazi kwa weleni,uadilifu,uwazi na kutumia mifumo ya kisasa ili matokeo makubwa ya uchumi yaonekane na Tanzania inufaike kwa fursa ilizonazo”, amesisitiza prof. Mbarawa.

  Katika ziara hiyo Prof. Mbarawa amekagua utendaji kazi na kutoa maelekezo kwa kampuni ya simu ya TTCL,Posta,Mamlaka ya Viwanja vya Ndege TAA, Mamlaka ya Anga TCAA na Mamlaka ya hali ya hewa TMA na kusisitiza kufanya kazi kwa weledi na kufikia malengo.
  IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.

  0 0


  Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mbunge wa Mlimba Bi.suzan Kiwanga(CHADEMA) mapema hii leo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mgeta-Mlimba.Pichana Festo Sanga
  Moja ya mashine za Umwagiliaji kwenye mashamba ya Mpunga ya KPL(Kilombero Plantation Limited) ikiwa tayari kwa kuanza kazi ya kumwagilia maji kwenye shamba hili la mpunga.
  Mh.Mwigulu akiangalia sehemu ya mpunga uliohalibiwa kwa kile kinachodhaniwa ni sumu iliyotokana na Umwagiliaji wa sumu aina ya Glyphosate iliyokuwa inatumiwa na wamiliki wa KPL kuchoma nyasi kwenye mashamba yao,Katika kikao cha pamoja cha wananchi,Uongozi wa serikali na uongozi wa KPL(Kilombero Plantation Limited),Mwigulu Nchemba amepokea hatua za awali za wataalamu na watafiti wa serikali waliobobea kubaini chanzo cha mimea kuharibika kwa kiasi kikubwa hivi,Wataalam hao wamemhakikishia Mh.Mwigulu Nchemba kuwa watatoa ripoti yao kamili ndani ya muda wa siku 21 ili kubaini aliyesababisha mimea ya mpunga kuungua.

  Mwigulu Nchemba amewahakikishia wananchi kuwa serikali ya Rais.Magufuli imejipanga kutetea haki za wananchi na itamuwajibisha yeyote anayehujumu kilimo na ustawi wa Taifa letu
  Vilevile Mh.Mwigulu Nchemba alifanikiwa kupitia shamba la Ruaha ambalo lipo chini ya muwekezaji kotaka nchini Marekani,hapa akipata maelekezo namna kilimo kinavyotakiwa kuendana na wakati.
  Utofauti wa Kilimo cha kisasa cha kuzingatia mbolea,Mbegu na wakati na kilimo cha kiholela ambacho hakizingatii mbegu na mbolea.
  Moja ya trekta la kisasa la muwekezaji wa “Ruaha Farm” ambalo linatumika kupanda mbegu,kuvuna na mwagilia dawa ya mimea.
  Waziri wa Kilimo akipewa maelezo kuhusu uhudumiaji wa mashamba ya Mahindi kuanzia uaandaji wa shamba,mbegu,mbolea na majira ya kupanda mahindi.Wakati wa ziara hiyo,Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya kilimo ameendelea kusisitiza kuwa kuna haja kama Taifa kuachana na kilimo cha jembe la mkono,lakini matumizi ya mbegu bora na mbolea bora ni muhimu yazingatiwe.

  Wizara inajipanga kuandaa mfumo mzuri wa kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa kupata pembejeo kwa wakati na upatikanaji wake uwe rahisi.
  Lakini,Mwigulu Nchemba pia amewasihi sana wawekezaji kwenye mashamba n.kuheshimu taratibu za uwekezaji,ili kuondoa mahusiano mabaya kati ya muwekezaji na wananchi.Mwisho,Mh.Mwigulu Nchemba anaendelea na ziara yake ya kukagua vituo vya utafiti,Mashamba ya mbeguna,Mifugo na uvuvi katika Mkoa wa mbeya kuanzia tar.5/03/2016.

  0 0
 • 03/05/16--00:45: LEO JUMAMOSI MAGAZETINI
 •  
  Karibu katika magazeti ya leo jumamosi 05 March 2016. Tumekukusanyia habari kubwa za magazeti na kukuwekea kurasa za mbele na za nyuma.


  0 0

  uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Bank hiyo Mlandege Zanzibar. Na kuwataka Wafanyakazi na Uongozi wa BOA kutowa huduma bora na kuwafikia Wananchi wa Vijijini katika kutowa huduma zao.  

  Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf mwenye mkasi akijiandaa kukata utepe kuashiria kulizindua Tawi la Bank Of Africa Zanzibar lilioko katika barabara ya Mlandege.kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Balozi Mwanaidi Maajar. 
  Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bank Of Africa wakishiriki katika kukata utepe kulizindua rasmin Tawi la Bank Of Africa Zanzibar, uzinduzi huo umefanyika Zanzibar. 
  Wageni Waalikwa na Wajumbe wa Bodi na Maofisa wa Bank Of Africa wakishangilia Uzinduzi huo wa Tawi lao la Banki Zanzibar.
  Wageni Waalikwa na Wananchi wakihudhuria hafla hiyo.
  Maofisa wa Bank Of Africa wakifuatilia uzinduzi wa Bank yake Zanzibar uliofanywa na Waziri wa Fedha Mhe Omar Yussuf Mzee.

  Wajumbe wa Bank Of Africa wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Nchini Tanzania Bwa. Ammish Owusu-Amoah, katikati wakizungumza wakimsubiri Mgeni rasmin Waziri wa Fedha Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Bank Of Africa Tanzania Balozi Mwanaidi Maajar akisalimiana na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee alipowasili katika viwanja vya Bank hiyo hapo mlandege kwa ajili ya Uzinduzi wa Bank hiyo.
  Waziri wa Fedha Zanzibar akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Bank Of Africa alipowasili katika eneo hilo. akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya BOA, Balozi Mwanaidi Maajar. 
  Waalikwa Wakifuatilia uzinduzi wa Banki hiyo katika mtaa wa mlandege Zanzibar, wakimsikiliza Waziri wa Fedha.
  Waalikwa wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Fedha Zanzibar wakati wa Uzinduzi wa Bank Of Africa Zanzibar. 

  Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee, akimsikiliza Menaja wa Bank Of Africa Tawi la Zanzibar Juma Burhan, baada ya kulizindua Tawi hilo Katikati Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Bwa, Ammish Owusu-Amoah. 
  Meneja wa Bank Of Africa Tawi la Zanzibar Ndg Juma Burhan akitowa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bank Of Africa Balozi Mwanaidi Maajar. na Wajumbe wa Bodi hiyo wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.

  Wananchi wakipata vitafuwa katika tafrija hiyo. ya hafla ya Uzinduzi wa Tawi la Bank Of Africa Zanzibar.
  Kikundi cha Taarab cha Tausi kikitowa Burudani wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Bank Of Africa wakiongozwa na Mkongwe wa Muziki wa Taraab Zanzibar Mohammed Elys.
  Mshauri wa Masuala yac Kibenki Mr Micheal Alcorn, akizungumza na na kubadilisha mawazo na Mfanyabiasha wa Zanzibar wakati wa hafla hiyo.
  Meneja wa Bank Of Africa Ndg Juma Burhan akizungumza na Wateja wa Bank hiyo wakati wa tafrija hiyo ilioandaliwa wakati wa haflaWaziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Azinduzi wa Tawi la Bank Of Africa Mlandege Zanzibar. ya uzinduzi.
  Wajumbe wa Bodi ya Bank Of Africa wakibadilisha mawazo wakati wa tafrija ya uzinduzi iliofanyika katika jengo la bank hiyo mlandege Zanzibar. 
  Waalikwa wakipata msosi wakati wa uzinduzi huo wa Tawi la Bank Of Africa Zanzibar.Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.com
  Zanzinews.com 
  Tawi Jipya la Bank Of Africa lililofunguliwa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee likiwa Tawi la 22 Bank Of Afrika Nchini Tanzania, linalotowa huduma za Kibenki. 
  Afisa Bank Of Africa Kaishe Godwin, akitowa maelezo wakati wa Uzinduzi wa  Bank hiyo ilioko Mtaa wa Mlandege Zanzibar, wakati hafla hiyo.   
  Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee na Wajumbe wa Bodi ya Bank Of Africa wakimsikiliza Afisa wa BOA akitowa maelezo katika hafla hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Bwa. Ammish Owusu-Amoah, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Bank uliofanywa na Waziri wa Fedha Zanzibar kwa ajili ya kutowa huduma kwa Wananchi wa Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bank Of Africa Balozi Mwanaidi Maajar akitowa maelezo kuhusiana na maendeleo ya BOA katika jitihada zake kutowa huduma kwa wateja na kusema  Tawi hili ni la 22 kwa Bank Of Africa Nchini Tanzania. kutowa huduma kwa Wananchi wa aina mbalimbali.
  Wajumbe wa Bodi ya Bank Of Africa wakifuatilia hafla hiyo ya Uzinduzi wa Bank hiyo Tawi la Zanzibar katika eneo la Mlandege.

  0 0

  Hii  ni Ofisi ya afisa Mtendaji Kata ya Iwawa, Kituo cha wakulima

  Na Blogs za Mikoa Tanzania
  Mila potofu zinazokandamiza wanawake zimeripotiwa kuendelea kushamiri katika baadhi ya mambo baada ya kutembelea katika maeneo tofauti tofauti ya wilaya ya Makete mkoani Njombe na kuzungumza na wakazi wa wilaya hiyo

  Katika kijiji cha Iwawa wilaya ya Makete mkoani Njombe mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Jane Sanga amesema wanawake wengi wilayani hapo hawamiliki ardhi kutokana na mila potofu kuwa wamiliki wa ardhi ni wanaume pekee
  "Kwa hapa Makete wanawake unaowaona wanamiliki ardhi kwa kiasi kikubwa unakuta ni mjane anaimiliki baada ya kufiwa na mumewe au unakuta mwanamke huyo ana uwezo wa kifedha na ameamua kukunua kipande chake cha ardhi na anakimiliki mwenyewe, hapo hakuna anayemuingilia, na hata wale wajane bado utakuta wanasumbuliwa na ndugu wa marehemu mumewe, kwa hiyo bado hali ni ngumu" amesema Jane
  Hiki ni kipande kidogo sana ambacho analima Bi. Jane(Hayupo Pichani)


  Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Grace Mbilinyi ambaye amekutwa na mwandishi wetu akiandaa shamba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula katika msimu ujao, amesema anamiliki shamba aliloachiwa na marehemu mumewe, licha ya kuendelea kusumbuliwa na ndugu wa marehemu wakidai kuwa mwanamke hataweza kuendeleza ardhi aliyoachiwa na mumewe

  "Kwa kweli ni shida lakini Tutafanyaje sasa, mimi ni mama  wa nyumbani ambaye sana sana najishughulisha na ujasiriamali na kilimo kama hivi, kwa sasa ninamiliki hili shamba nililoachiwa na mume wangu kwa ajili ya kilimo, lakini vijimaneno vya ndugu vipo lakini bado sikati tamaa maana uwezo wa kumiliki ninao, na nitaiendeleza kwa kilimo" amesema Bi Grace

  James Sigala ni mkazi wa Makete ambaye amekiri kuwepo kwa mila hizo zinazokandamiza wanawake hasa katika umiliki wa ardhi na kusema ingawa elimu inaendelea kutolewa na wanaharakati lakini bado kuna haja ya kuendelea kuitoa ili jamii ibadilike na kuamini kuwa hata wanawake wanaweza kimilikishwa ardhi kama wanaume
  Afisa mtendaji kata ya Iwawa Bw. Festo Msigwa akiongea na mwandishi wa Blogs za Mikoa

  Blog za Mikoa kupitia Njombe yetu  haikuishia hapo imebisha hodi katika ofisi za kata ya Iwawa iliyoko katika mji mdogo wa Iwawa (Makete Mjini) na kukutana na afisa Mtendaji Bw. Festo Msigwa ambaye amekiri kuwa bado umilikishwaji au umiliki wa ardhi kwa wanawake ni mdogo kutokana na mila potofu 

  Amesema katika kata yake zipo kesi za ardhi zinazoletwa katika ofisi yake zikiwemo za wanawake wajane kupokonywa umiliki wa ardhi kutoka kwa ndugu wa mume wake kwa madai kuwa yeye kama mwanamke hawezi kumiliki wala kuiendeleza jambo ambalo limepingwa na kulaaniwa vikali na mtendaji huyo

  "Wanawake wanaweza kwanza katika shughuli za shambani wao ndio wachakarikaji kuliko sisi wanaume, fikiria kwa mfano hawa wajane wanaokuja kwenye kesi za ardhi katika baraza la ardhi hapa, unakuta wakati wa uhai wa waume zao wao ndio walikuwa walimaji wazuri na watunzaji wakubwa wa mashamba, sasa kama aliweza toka mwanzoni iweje sasa washindwe" amesema Msigwa

  Machi 8 mwaka huu ni kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kwa wilaya ya Makete maadhimisho yatafanyika katika kata ya Iwawa katika mji mdogo wa Iwawa

  0 0

  Shule ya Sekondari , J.K Nyerere iliyopo manispaa ya Moshi ni moja kati ya shule zitakazonufaika na msaada wa kujengewa majiko sanifu na Shirika la kimataifa la Mazingira (WWF-Tanzania) 
  Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akiongozana na wa wakuu wa idara katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi walipotembelea shule ya sekondari J.K Nyerere .
  Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako wakiwa katika jiko la shule hiyo kuangalia namna ambavyo wanaweza kupunguza matumizi ya kuni kupikia.
  Matumizi ya kuni ni makubwa katika shule za msingi ambazo zimekuwa zikitumika kupikia hali inayochangia ongezeko la uharibufu wa mazingira kwa kukata miti.
  Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akitia saini katika kitabu cha wageni katika shule hiyo ,katikati ni mkuu wa shule hiyo , Parfectius Mushi akimtizama na kulia ni afisa kutoka WWF .

  Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako (kulia) akiwa na kaimu mkuu wa shule ya msingi Langoni ,Mwl Hamad,alipotembelea kujionea namna gani wanavyoweza saidia katika ujenzi wa majiko sanifu. 
  Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akiwa ameongozana na wakuu wa idara za Halmashauri ya manispaa ya Moshi kutembelea jiko lilopo katika shule ya msingi Langoni mjini Moshi.
  Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akimueleza jambo Meneja Mradi wa ICLEI Africa Irina Velasco walipotembelea jiko la shule hiyo.
  Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akitia saini katika kitabu cha wageni katika shule ya msingi Msandaka alipotembelea shule hiyo.
  Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akiongozwa na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Danford Kamenya wakielekea kutizama jiko la shule hiyo.
  Jiko la shule ya msingi Msandaka.
  Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Msandaka katika manispaa ya Moshi.
  Baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo wakiwa katika chombo maalumu cha kuhifadhia nafaka shuleni hapo.
  Diwani wa kata ya Ng'ambo ,Genesis Kiwhelu akisalimiana na Irina Velasco wa ICLEI alipowapokea katika zahanati ya Msaranga ambapo ujumbe wa WWF ulifika kuangalia namna ya kuisadia zahanati hiyo vifaa vya Nishati ya Umeme unaotokana na jua.
  Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akitembelea katika zahanati hiyo.
  Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako akisikiliza maelezo kutoka kwa mganga kiongozi wa zahanati ya Msaranga Dkt Para.
  Mratibu wa Nishati wa Shirika la kimataifa la utunzaji Mazingira ,(WWF-Tanzania) Dkt Teresia Olemwako na ujumbe wake wakiwa katika eneo la kata ya Ngangamfumuni ambako WWF imepanga kuotesha miti.
  Afisa Habari wa manispaa ya Moshi,Ramadhan Hamisi akieleza jambo kwa ujumbe huo mara baada ya kutizama eneo litakalo oteshwa miti.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

older | 1 | .... | 785 | 786 | (Page 787) | 788 | 789 | .... | 1897 | newer