Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 782 | 783 | (Page 784) | 785 | 786 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


  BAADHI   ya wazazi wa wanafaunzi waliokuwa wakisoma Chuo Kikuu cha St Joseph katika  matawi ya Arusha na Songea wametupa lawama kwa Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) kwa hatua yake ya kufuta vibali vya kuanzisha matawi hayo na kwamba hali hiyo imewathiri watoto wao.


  February 26 mwaka huu ,tume ya vyuo vikuu ilitangaza kufuta kibali cha chuo kikuu cha St Joseph (SJUIT) tawi la Arusha ikiwa ni wiki moja imepita tangu kuchukuliwa kwa hatua kama hiyo kwa Chuo kikuu cha St Joseph tawi la Songea,vyuo vilivyoko chini ya shirika la kitawa la Dada wa Maria Imakulata (DMI).


  Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti baadhi ya wazazi wameeleza kusikitishwa na hatua hiyo huku wakidai kuwaathili kisaikolijia watoto wao ambao wengine walikuwa katika maandalizi ya mitihani.


  “Nadhani ingekuwa ni jambo la busara  kwa TCU kukaa meza ya mazungumzo na uongozi wa chuo badala ya kuchukua hatua ya kukifutia vibali….Chuo hiki kimekuwa kikitoa mchango mkubwa katika kuzalisha wataalumu mbali mbali.”alisema Mrisho Sume.


  Nchi yetu ina wataalamu wachache  katika sekta ya Sayansi na Teknalojia ,chuo hiki kilikuwa ni kimojawapo kinachotoa wataalamu hao hivyo mchango wake unapaswa kuheshimika na kusaidiwa pale inapobidi,” aliongeza Sume ambaye mwanaye alikuwa akisoma katika chuo cha Sayansi ya kilimo katika chuo hicho tawi la Songea.


  Mzazi mwingine alijitambulisha kama Mariam Ali alisema taarifa alizokuwa nazo ni kuwa uamuzi wa kufunga baadhi ya matawi hayo ulifikiwa bila ya kukipa taarifa chuo hicho juu ya mapungufu yaliyopo ikiwa ni pamoja na kukipa muda wa kuyafanyia kazi.


  “Binti yangu alikuwa akisoma tawi la Arusha na nimepata taarifa kuwa  timu ya ukaguzi kutoka tume ilifika chuoni hapo   kwa ajili ya ukaguzi lakini cha kushangaza ni kuwa chuo hakikupewa taarifa ya mapungufu yaliyoonekana ili yafanyiwe kazi na badala yake kililetewa barua za kufutiwa vibali.”alisema Mariam.


  Uamuzi ulifanywa ni wazi haukuzingatia haki na unatuumiza sisi wazazi pamoja na watoto wetu, tulitegemea TCU kukipatia chuo  ripoti ya mapungufu waliyoyagundua na kupewa muda wa kuyafanyia kazi  na endapo kingeshindwa kuyafanyia kazi katika muda ambao kimepewa tume ingekuwa na haki ya kutoa adhabu,” aliongeza Mariam.


  Naye John Budigle alisema tangazo lilitolewa na TCU kuhusu kufunga vyuo hivyo lilisema moja ya matatizo yaliyopelekea kufungwa ni migomo ya wanafunzi huku akiongeza kuwa migomo yote  ilitokana na kucheleweshewa mikopo na siyo matatizo ya chuo .

  “Mimi kwa mtizamo wangu naona kama TCU imetumia nguvu kubwa kwenye suala hili, kama chuo kilifanya makosa kilipaswa kupewa maelekezo ya kushughulukia kasoro au mapungufu kwani hakuna chuo kisichokuwa na mapungufu hata hivyo vya umma. “alisema Budigle.


  “Hatua hii inawavunja moyo wawekezaji katika sekta ya elimu. Hawa ni wadau katika elimu na ni vizuri TCU wakatuchukuliwa hivyo. Wao ni wasimamizi ambao wanatakiwa kuwaongoza na kuwarekebisha pale wanapokosea. Kitendo cha kukifutia vibali bila kufuata haki kinawavunja moyo wadau wa elimu pamoja na wanafunzi pia,” aliongeza Budigle.


  Akitangaza hatua hiyo hivi karibuni  Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya, alizitaja sababu za kufikia uamuzi huo kuwa ni matukio ya migogoro ya muda mrefu baina ya uongozi wa chuo hicho na wanafunzi na ukiukwaji wa sheria za uendeshaji wake kama ulivyobainishwa na Sheria ya Vyuo Vikuu.

  0 0
 • 03/01/16--23:17: DONDOO ZA HABARI MAGAZETINI.

 • 0 0

   Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amefanya mazungumzo na watendaji wa mgodi wa chumvi wa Nyanza uliopo mkoani Kigoma ambao walifika Wizara ya Nishati na Madini ili kuzungumza masuala mbalimbali yanayohusu mgodi huo.
  Mkurugenzi wa Mgodi wa chumvi wa Nyanza (kulia), Mukesh Mamlani wa mgodi huo,  Bonny Mwaipopo (kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati  alipokutana nao hivi karibuni katika ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Katikati), Dkt. Medard Kalemani,  akizungumza  na  watendaji wa Mgodi wa Nyanza, Bonny Mwaipopo ( wa kwanza kushoto) na Mukesh Mamlani (wa pili kushoto) katika kikao kilichofanyika  hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini. Kulia ni Mjiolojia Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Aloyce Tesha.

  0 0

  Mwanamuziki wa bendi ya muziki ya COCODO, Remi Tone ameachia video ya wimbo wake alioupa jina la Kosa Lake. Kuwa wa kwanza kuitazama hapa

  0 0

  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akipongezana na Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse (kushoto) baada ya Airtel na Fastjet kuingia ubia wa kibiashara utakaowawezesha Wateja wa Fastjet kununua tiketi za usafiri kupitia Airtel Money. akishuhudia ni Meneja wa Airtel Money, Asupya Naligingwa (kati) hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika jana katika ofisi za Airtel makao makuu Morocco jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya kununua tiketi za ndege za Fastjet kupitia Airtel Money. (kushoto) Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse (kulia) ni Meneja wa Airtel Money, Asupya Naligingwa.
  Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse (kulia) akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Fastjet na Airtel utakaowawezesha Wateja wa Fastjet kununua tiketi za usafiri kupitia Airtel Money. katikati Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akifatiwa na Meneja wa Airtel Money, Asupya Naligingwa.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akimpongeza mmoja wa waandishi wa habari wa clouds TV James Lyatuu mara baada ya kuibuka mshindi wa tiketi ya bure ya fastjet wakati wa uzinduzi wa ubia wa kampuni ya Airtel na Fastjet utakaowawezesha wateja kulipia tiketi zao za ndege kupitia huduma ya Airtel Money. 


  0 0

  WASANII wa muziki mbalimbali hapa nchini, Jumamosi hii wanatarajiwa kukinukisha vilivyo katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam, katika tamasha la Amsha Mama Festival.

  Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake, Balozi wa tamasha hilo  Khalid Ramadhani ‘Tundaman’, ambaye amepewa Ubalozi  huo kupitia waandaaji wa tamasha la (AFWAB)  AMSHA MAMA Festival 2016, lililo chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa lebo ya Candy na Candy   Records Joe Kariuki, alisema tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Machi 5 mwaka huu katika uwanja wa Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.

  Tundaman na Muandaaji wa tamasha hilo Kariuki, wamesema kwamba maandalizi ya shoo hiyo tayari yameshakamilika kwa kiasi kikubwa hivyo angependa kutumia fursa hii kuwaalika wakazi wote wa jiji la Dar, kujumuika siku hiyo kushuhudia burudani mbalimbali zitakazotolewa na wasanii kibao ambao tayari wemedhibitisha kufanya makamuzi siku hiyo.

  “Tunapenda kuwaalika Watanzania wote kwa ujumla siku ya jumamosi hii ya Machi 5, mwaka huu waje kwa wingi katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar  Salaam, ili tujumuike kwa pamoja katika tamasha la kuhamasisha wanawake kujikwamua katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.

  Tamasha hili litakuwa ni la wazi kwa maana kwamba watu wote watapata burudani kibao bila malipo yaani bure kabisa hivyo waje kuwashuhudia wasanii kama, Khadija Kopa, Mr Blue, Snura, Msaga Sumu, Ali Chocky na Tunda Man wakitoa burudani ya hali ya juu kwani  ulinzi na usalama siku hiyo ni wa uhakika,” alisema Tunda Man.

  Kwa upande wake,  Joe Kariuki ambaye ni mratibu mkuu wa tamasha hilo ametumia muda huu kuongea na baadhi ya akinamama wanaojishughulisha na biashara za vitu mbalimbali hususani mama ntilie, wauza matunda na wauzaji wa mitumba ili nao wajitokeze kwa wingi kuja kunadi bidhaa zao  siku hiyo kwani hiyo ndiyo fursa yao ya kipekee ya kujitangaza bure.

  0 0

  DSC_5118
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Kongamano la pili la Kimataifa linayojadili kuhusu Bayoanuwai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Kongamano hilo limefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.

  Maimuna Tarishi
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la pili la Kimataifa linayojadili kuhusu Bayoanuai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Kongamano hilo limefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
  IMG_4589
  Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Afrika, Firmin Matoko kuhutubia kwenye kongamano hilo.
  Firmin Matoko
  Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UNESCO, Irina Bokova wakati wa ufunguzi wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
  Song Geum-Young
  Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song ambao ni wafadhili wa mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda bayoanui akisoma taarifa yake baada ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kufungua Kongamano hilo la pili la Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuai katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
  DSC_5078
  Pichani juu na chini washiriki wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda Bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.

  IMG_4562
  IMG_4616
  IMG_4549
  Samia Suluhu Hassan
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima wa Uyoga (DMGA), Bi Judith Simon Muro, kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda bayoanui.
  IMG_4733
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti Mhifadhi wa Hifadhi ya Mazingira asili Amani (Amani Forest Nature Reserve - ANR), Bi. Mwanaidi Kijazi, kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda Bayoanui. Wanaoshuhudia tukio hilo kulia Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko, Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar (wa kwanza kushoto).
  DSC_5150
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti Amiri Saidi Sheghembe wa mradi wa Vipepeo Amani kwa kutambua mchango na ushiriki wao kwenye kutekeleza mradi wa uchumi wa kijani kwa kulinda Bayoanui.
  Mary Kawar
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan , akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar.
  Samia Suluhu Hassan
  Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na washiriki kutoka nje ya Tanzania wanaohudhuria Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
  IMG_4817
  Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort.
  Samia Suluhu Hassan
  Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa UNESCO walioshiriki kwenye maandalizi ya kongamano hilo.
  Samia Suluhu Hassan
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Afisa Tathimini na Logistki wa UNESCO Ofisi ya Dar es Salaam, Rahma Islem (kulia) mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.
  Firmin Matoko, UNESCO
  Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko (kushoto) akisalimiana na mmoja wadau wa maendeleo Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mh. Geum-Young Song .
  IMG_4886
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi katika picha ya kumbukumbu na Mwanafunzi wa kidato cha pili ambaye pia ni Katibu Klabu ya Safe Space inayojihusisha na utunzaji wa Mazingira, Lilian Tadei wa Shule ya Sekondari Potwe, Muheza.
  Zulmira Rodrigues
  Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Ngosi Mwihava.
  Zulmira Rodrigues
  Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (katikati) akifurahi jambo na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdula Lutavi (aliyeipa mgongo kamera) wakati wakisubiri kumpokea mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) kwa ajili ya kufungua Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara linaloendelea katika hoteli ya Tanga Beach Resort, Mkoani Tanga. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

  Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda Bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara (GEBR) limefanyika mkoani Tanga.Wenyeji wa kongamano hilo walikuwa ni Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, sayansi na Utamaduni (UNESCO) ofisi ya Dar es salaam.
  Akifungua kongamano hilo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Korea kusini kupitia shirika lake la maendeleo na ushirikiano la kimataifa (KOICA) kuongeza muda wa mkataba wa mradi wa GEBR ambao unafikia ukomo mwishoni mwa mwaka huu.

  Akizungumza na washiriki mbalimbali wapatao 40 kutokana ndani na nje ya nchi zikiwemo Ghana na Nigeria kutoka Afrika, alisema ombi hilo linatokana na ukweli kuwa walengwa wamekuwa wakifaidika na mradi huo, kwa kuweza kubadilisha maisha yao na kuwa bora zaidi.Makamu wa Rais alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika na kutoweka kwa uotoasili unaotoa fursa ya uoto wa mimea zaidi ya 10,000, jamii 6,000 ya wadudu, jamii ipatayo 1000 ya ndege warukao.

  Aidha Samia katika hotuba yake alirejea msimamo wa serikali wa kutaka kuhifadhi mazingira, pamoja na kuziweka rasmi chini ya uangalizi halali jumla ya hekta milioni 33.5 za misitu asili, huku akitanabaisha kuwa serikali pia ina mapori ya akiba yapatayo 800 pamoja na misitu mingine.Aliwakumbusha washikadau pamoja na nchi wafadhili kwamba Tanzania inakabiliwa na ukuaji mkubwa wa idadi ya watu wake wanaotegemea raslimali kwa matumizi yao ya kila siku pamoja na mahitaji ya nishati.“Tunaelewa kwamba kuna shughuli nyingi za uharibifu wa mazingira zinazopelekea uharibifu wa misitu na mazingira”, alisema Samia na kuongeza kwamba kuna kupokonyana kwa ardhi na maji.

  Katika warsha hiyo wafaidika wakubwa katika mradi huo, ambao walitekeleza kwa vitendo elimu iliyopatikana kutokana na mradi huo, walikabidhiwa vyeti ya ushiriki kwa vitendo na kwa ufanisi mkubwa walioonyesha.
  Washiriki hao wengi walitoka katika miradi midogo midogo inayotekelezwa Amani, Muheza ambayo ni pamoja na ufugaji nyuki, samaki, vipepeo na uyoga.
  Zulmira Rodrigues
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) alipowasili kwenye hoteli ya Tanga Beach Resort jana kufungua Kongamano la pili la kimataifa la uchumi endelevu unaozingatia uhai wa mazingira kama njia ya kupunguza umaskini, kulinda bayoanui na maendeleo endelevu Kusini mwa Jangwa la Sahara lililoandaliwa na UNESCO. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Ngosi Mwihava.

  Awali, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza aliwataka wakazi wa Tanga na Tanzania kwa ujumla kutumia vyema nafasi adhimu kwenye miradi ya maendeleo inayogharimiwa na wafadhili na kuwasihi wawe makini kwani mafanikio yao huwa ni kivutio kwa wafadhili kuweza kuendelea kutoa ufadhili kwa misaada.Mradi wa GEBR ambao uko katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wake, unafadhiliwa na serikali ya Korea kupitia Shirika lake la Kimataifa la misaada Korea International Cooperation Agency (KOICA).

  Mradi huo wa Unesco wa binadamu na bayosfia (MAB) unatekelezwa nchini Ghana, Nigeria na Tanzania kwenye milima ya Usambara.Katika hotuba yake Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika, Firmin Matoko alimpongeza Makamu wa rais kwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya juu katika utawala tangu historia ya kuundwa kwa Tanzania.Alisema amefurahishwa sana na wanawake kuchukua nafasi kwa kuwa Unesco wameweka kipaumbele wanawake katika maendeleo.
  Samia Suluhu Hassan
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano hoteli ya Tanga Beach Resort akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika, Firmin Matoko.

  Akizungumzia mradi wa GEBR alisema umelenga kutekelezwa katia msingi wa wazo la UNESCO la binadamu na bayosfia.Alisema kwamba mradi huo umelenga kutumia elimu ya asili, elimu ya sayansi na utamaduni ili kuboresha maisha ya biandamu huku wakihifadhi mazingira.Aidha alitaka kuwapo ushirikiano katika utekelezaji wa ajenda za maendeleo na hifadhi ya bayosfia kwa lengo la kuwezesha maendeleo endelevu.Washiriki wa mradi huo pia walipata nafasi ya kutembelea eneo la hifadhi ya Usambara mashariki.Naye Balozi wa Jamhuri ya Korea, Bw Geum-Young Song alisema kwamba wataendelea kushiriki katika mradi huo ambao umejikita katika kuwezesha maendeleo endelevu huku mazingira yakihifadhiwa.

  Alisema ni lengo la taifa lake la kuwezesha hifadhi endelevu kwa maendeleo endelevu.
  Aidha alitaka kuwepo na fikra za mradi kuwa endelevu baada ya wafadhili kuondoka.
  Viongozi waliohudhuria siku ya ufunguzi ni pamoja na Makamu wa Rais Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika, Bw. Firmin Matoko, Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania, Mh. Geum -Young Song, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Unesco nchini Tanzania, Zulmira Rodrigues, Wawakilishi wa KOICA nchini Ghana, Nigeria na Tanzania; mwakilishi wa KOICA nchini Korea, Seoul; na kamati za MAB kutoka nchi zinazotekeleza mradi huo.

  0 0
  0 0


  Meneja utetezi wa Oxfam Tanzania, Eluka Kibona amesema uelewa wa wanawake katika kumiliki ardhi na kufuatilia haki zao za ardhi unaongezeka siku hadi siku nchini na kuondoa ile dhana kwamba wanawake wako nyuma katika shughuli za maendeleo.  Bi Eluka ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Blogs za Mikoa kuhusu namna taasisi binafsi zinavyotetea harakati za wanawake katika kumiliki ardhi hapa nchini na kujiendeleza kiuchumi ambapo amesema kwa kulinganisha miaka 10 iliyopita na sasa, wanawake kwa sasa wamekuwa na muamko zaidi wa kupambana na changamoto za umiliki wa ardhi wanazokutana nazo.  ''Sisi tunaunga mkono harakati na jitihada za kuleta usawa kati ya wanaume na wanawake mjini na vijijini na hii ni baada ya kutambua kuwa matatizo ya umiliki wa ardhi kwa wanawake wa mjini na vijijini yako sawa kutokana na mfumo ulivyo katika jamii.''Ameeleza Bi Eluka.


  Mmoja wa wanawake (Kulia) akipokea hati yake ya kumiliki ardhi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster katika kijiji cha Gongoni wilayani Kilosa.


  ''Kuna madai ya ardhi ambayo wanawake wanakumbana nayo katika jamii kwa kudhulumiwa na wengine kwa kunyimwa haki zao za msingi hivyo tunawasaidia katika kuwawezesha kutambua namna ya kupigania haki zao.''Amesisitiza Bi Eluka.  Kuhusu siku ya wanawake duniani ambayo huazimishwa kila Machi 8 kila mwaka, Bi Eluka amesema Oxfam Tanzania imejipanga kufanya maadhimisho katika mkoa wa Mtwara ili kuunga mkono jitihada za wanawake katika kujikwamua na mifumo kandamizi hapa nchini na kujiendeleza kiuchumi.

  Mmoja wa wanawake akiwakatika kilimo
   

  Kwa mujibu wa Bi Eluka, Oxfam imewezesha wanawake wengi kuweza kupata haki zao katika mikoa mbalimbali nchini na baadhi ya mikoa hiyo ni Shinyanga, Arusha, Tanga Morogoro.  Aidha kwa mujibu wa sheria ya ardhi inatamka bayana kuwa mwanamke ana haki sawa na mwanaume katika kupata, kumiliki, kutumia na kugawa ardhi. (Kifungu 3(2) cha sheria ya ardhi na sheria ya ardhi ya vijiji za 1999).  Hata hivyo ni muhimu kila mmiliki wa ardhi awe na hati/ cheti halisi cha hakimiliki kuthibithisha haki yake ya kumiliki ardhi kisheria.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano nchini (TCRA), Dk.Ally Simba akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) juu hatua mbalimbali walizochukua kwa kampuni za simu za mikononi leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu watendaji wa TCRA na waandishi habari wakisikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii).


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  KAMPUNI za Mawasiliano ya Simu za Mkononi zimepigwaa faini ya Sh.Milioni 90 kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya kanuni za ubora wa huduma.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jijini leo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA), Dk.Ally Simba amesema kuwa kampuni hizo zimepigwa faini tofauti kutokana na makosa mbalimbali ya utoaji huduma ya mawasiliano kwa wananchi.

  Dk.Simba amesema kampuni ziliitwa na mamlaka ambapo zilikiri kufanya hivyo na kukubali na kosa na maamuzi yaliyofikiwa kuwapiga faini kwa mujibu wa sharia za nchi.Mkurugenzi Mkuu huyo alizitaja kampuni hizo na faini zake kuwa ni Aitel sh.milioni 22.5 ,Smart sh.milioni 12.5, Tigo sh.milioni 25,Vodacom sh.milioni 27.5 pamoja na Zantel sh.milioni 25.

  Amesema kuwa kutokana kampuni hizo kushindwa kutimiza masharti TCRA itaendelea na utekelezaji wa sheria na maamuzi mengine kwao kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.Amesema baadhi ya makosa ni simu iliyopiga kudai kuwa inatumika wakati sivyo, wakati mwingine simu unapiga mwito wake unadai simu hiyo haipatikani wakati simu hiyo iko hewani.


  Aidha amesema kuwa watoa huduma wote wa simu za mkononi kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa na kuzingatia vigezo vilivyoanishwa.Dk.Simba amesema kuwa kampuni za simu za mikononi zimejikita katika kujitangaza kwa njia mbalimbali katika kuweza kupata wateja wapya lakini hazifanyi uwekezaji wa huduma bora kwa wananchi wanaotangazia.

  Hata hivyo TCRA imeipiga faini kampuni ya Azam Marine Sh.Milioni Tano kutokana na kufanya usafirishaji wa vifurushi kutoka Dar es Salaam na Zanzibar bila kuwa na leseni ya utoaji wa huduma hiyo.Amesema kuwa ni kosa kwa Azam Marine kufanya huduma ya posta bila kuwa leseni huku wakikri kufanya biashara ya kusafirisha vifurushi.

  Kampuni ya Lifalo imepigwa faini sh.10 kutokana na kufanya masafa ya ujumbe mfupi bila kuwa na kibali cha TCRA na lifalo ilikiri kufanya hivyo.Dk.Simba amesema kuwa walipewa namba mara ya kwanza kwa muda na baada ya kuisha hawakuweza kuendelea huku wakiendelea kutoa huduma ya ujumbe mfupi.

  0 0

  In this photo taken Wednesday March 2, 2016 at Tanzania’s Dar es Salaam Port, Handler from Tanzania Police Force leads the trained canine from the U.S Customs and Border Protection (CBE), as the Canine sniffs illegal items from one of these boxes during the handing over ceremony of four canines trained at CBE’s world class facility in El Paso Texas in the U.S. The U.S Government through it’s Embassy in Dar es Salaam has equipped police working at Julius Nyerere International Airport and the Port of Dar es Salaam with capability to detect a variety of illegally trafficked items, including wildlife products and drugs. U.S Embassy Deputy Chief of Mission, Virginia Blaser has Said. (PHOTOS; K-VIS MEDIA/Khalfan Said).
  The bravery canine snatch a suspected illegal item
  Canines line-up with their handlers, during the parade
  U.S deputy chief of mission in Tanzania, Virginia Blaser, makes her remarks during the event .

  BY K-VIS MEDIA/Khalfan Said

  THE U.S Government through it’s Embassy in Dar es Salaam has equipped police working at Julius Nyerere International Airport and the Port of Dar es Salaam with capability to detect a variety of illegally trafficked items, including wildlife products and drugs.

  Presenting four canines at a ceremony held at Dar es Salaam Port, Wednesday March 2, 2016. U.S Embassy Deputy Chief of Mission, Virginia Blaser, said, Wildlife and narcotics trafficking are serious crimes with devastating consequences for Tanzania’s natural resource, economy, and security, these are the rezones led to the U.S Government to support Tanzania Government to curb the vice.

  Four Police Officers, from Tanzania Police’s Dog and Horse Unit, who were specially selected for the canine detection program Tanzania, by the Office of the Inspector General of Police were trained together with their canines and certified in 2015 at CBE’s world class facility in El Paso, Texas in the U.S, said Blasser.

  In February 2016, CBE trainers arrived in the country to conduct on-the-job training at the Airport and Port.
  The Canine Detection Program is a model of what can be achieved when partners work together, stopping the poaching crisis and illicit narcotics trafficking requires everyone to contribute, she said.

  In his part. The Minister for Tourism and Natural Resources, Professor Jumanne Maghembe, who received the canines on behalf of the government, thanks the U.S Government for their endeavor support.

  He warned that, the country is facing serious threats on poaching and other crimes, “This support came timely and we promised to use this expertise to confront the hardcore criminals.
  Professor Jumanne Maghembe
  Eng. Hamad Yusuf Masaunui, deputy Minister for Home Affais
  Representative of TPA's acting Director General, the act. deputy director general, Johnson Noni, speaks during the event.
  Deputy Inspector General of Police, (DIGP), Kaniki, (L), exchanges ideas with the Senior Public Relations Officer with Tanzania Airports Authority (TAA), Godfrey Luitego
  From left, Head of Police Dog and Horse Unit, Senior Superintendent of Police (SSP), Egyn Emmanuel, Police Spokeswoman, Senior Supretendant of Police, (SSP), Advera Bulimba and TPA official, attend the event
  The audience
  High table from left to right, deputy minister fro home affairs, Eng. Hamad Masauni, minister for tourism and natural resources, Professor Jumanne Maghembe, U.S embassy deputy chief of mission, Virginia Blaser, deputy inspector general of police, Abdulrahman Kaniki, and MichaleS. Lata, from the U.S department of homeland security and border control attached in the U.S embassy in Nairobi, Kenya
  Ms.Virginia and DIGP, Kaniki 
  Eng. Masauni, and Prof. Maghembe share a ligh moment
  Eng. Masauni and Virginia shakes hands
  Deputy Inspector General of Police, Abdulrahman Kaniki, briefs themedia
  Deputy Minister for Home Affairs, Eng. Masauni, briefs the media
  TAA's Senior Public Relations Officer, Godfrey Lutego, chats with the U.S embassy official from the Public Affairs Department

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari akiongea na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam leo, wakati alipofanya nao mkutano kwa mara ya kwanza tanga ateuliwe kushika wadhifa huo. Kushoto ni Mwanasheria wa TCAA, Patrice  Chegani.
   Baadhi ya wafanyaakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA, wakimsikilaza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka hiyo , Hamza Johari hayupo pichani, wakati alipokutana nao kwa mazungumuo ya utendaji kazi leo jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw.Hamza Johari, amewataka wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kujiangalia pale wanapoona waliteleza na kubadilika kwa kufanya mabadiliko na kuachana na  tamaduni walizoziea hapo awali.

  Mkurugenzi Johari aliyasema hayo leo alipokuwa katika kikao chake cha kwanza kilichafanyikia TCAA Makao Makuu na kuhusisha  wafanyakazi wa TCAA wa Makao makuu, kituo cha uwanja wa ndege wa JNIA, chuo cha usafiri wa Anga (CATC) na Karakana ya TCAA Chang’ombe baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni, na kuongeza kuwa kila mtu au kila jamii ina utamaduni fulani, tatizo ni tafsiri au namna tamaduni hiyo ilivyo inaweza kuwa nzuri ama mbaya.

  Bw. Johari ameongeza pia kuwa yeye anawaona wafanyakazi wote wa TCAA kama timu moja ya ushindi na anaamini kwa kufanya kazi kwa kushirikiana basi TCAA itapiga hatua  na ikitokea kinyume chake TCAA Itakwama .

  Bw.Hamza pia amesisitiza juu ya kila mmoja kutimiza wajibu wake mahala pake pa kazi na yeye pia kama Mkurugenzi Mkuu atatimiza ya upande wake, lengo likiwa kuipigisha TCAA hatua.

  Ameongeza pia kuwa, katika kipindi hiki cha uongozi wake atahakikisha masuala mbali mbali ambayo ni changamoto kwa wafanyakazi wa TCAA yanaangaliwa upya na kuboreshwa, ili waweze kuongeza Ari ya kufanya kazi.

  Akitoa salamu ya shukran kwa niaba ya wafanyakazi wa TCAA, Katibu Mkuu wa TUGHE –TCAA Bw.Maotola Miti alimuakikishia Mkurugenzi Johari kwamba wafanyakazi wote wa TCAA wapo nyuma yake katika kufanikisha malengo ya TCAA kupiga hatua yanafanikiwa, na kuongeza kuwa wafanyakazi wa TCAA wana matumaini makubwa juu yake.  

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Museven baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC,(kulia) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC.
  Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki wakisimama wakati wimbo wa umoja wa nchi hizo ukipigwa katika mkutano wa 17 wa EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto mkoani Arusha.
  Miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania walioalikwa katika mkutano wa 17 wa Viongozi wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto Hotel Mkoani Arusha,(katikati) Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini,akiwa na Mawaaziri wa Nchi za Jumuiya hiyo,{Picha na Ikulu.]

  0 0

   Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Trumark Tanzania, Agnes Mgongo akizungumza na waandishi wa habari jijiniDar es Salaam leo kuhusiana na kufanyika kwa tamasha la pamoja tunafanikisha linanaloandaliwa na kampuni ya Trumark litakalo fanyika Machi 5, mwaka huu katika ukumbi wa Kingsolomon Namanga jijini Dar es Salaam. Agnes amesema kuwa kutakuwa na burudani zitakazotolewa na Barnaba na Classic Band, Bi. Patricia Hillary na mchekeshaji maarufu MC Pilipili, wakisindikizwa na wasanii chipukizi.
  Aidha TruMark inawashukuru wahamasishaji na wadhamini wa maadhimisho haya, ambao ni Vayle Springs, Mummy’s Exclusive Shop, Flexible Entertainment, Marie Stopes Tanzania, King Solomon Hall, King Solomon Events, Mono Accessories, CSI Tanzania, MagicFM na Channel Ten.  
  Mwanamziki wa zamani wa Taarabu, Patricia Hilary akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa katika tamasha la Pamoja tunafanikisha linaloandaliwa na Kampuni ya TruMark kuwa atatumbuiza kwa nyimbo zake za zamani za Taarabu kama wimbo wa ewe njiwa utaimbwa laivu na mwanamziki huyo. Kulia ni Mratibu wa Tamasha la pamoja tunafanikisha wa kampuni ya TruMark, Azavery Phares.
  Mchekeshaji na Mshereheshaji ,Emmanuel Matebe a.k.a MC Pilipili akizungumza na waandhishi wa wahabari jijini Dar es Salaam leo. Amewaomba watanzania wote kwa ujumla wajitokeze katka tamasha hiyo ikiwa yeye atatumbuiza na kuchekesha wote watakao hudhulia katika tamasha hilo ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake duniani. kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Trumark Tanzania, Agnes Mgongo  na kulia ni Mkurugenzi wa kampuni ya CSI, Stella Mpanda.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiwasikiliza wadau wa maendeleo ya wanawake jijini Dar es Salaam leo.


   
  KAMPUNI ya TruMark yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam imeandaa tamasha la kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani la Pamoja Tunafanikisha, litakalofanyika Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa King Solomon, Namanga, Machi5,2016ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ndiye atakayekuwa mgeni rasmi tamasha hiyo litawashirikisha wanaume na wanawake ili kufurahia mafanikio ya wanawake.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa TruMark, Agnes Mgongo, amesema kampuni yake imeandaa tamasha hilo kwa kuwa kumekuwa na matukio mengi ya mafanikio kwa wanawake nchini Tanzania, ambayo bado wanaume hawajashirikishwa ipasavyo kuyatambua na kuyafurahia mafanikio hayo kwa kiwango kinachoridhisha.

  “Ni kweli, wapo wanawake wengi wenye mafanikio hapa nchini, lakini bado kuna changamoto nyingi, mojawapo ikiwa uchache wa ushiriki wa wanaume katika, kwanza, kufanikisha mafanikio hayo na, pili, kufungua fursa nyingi zaidi ili wanawake wengi zaidi waweze kuwa sehemu ya mafanikio hayo, kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii, kama vile sekta za fedha, elimu, sayansi, teknolojia, kilimo, viwanda, taaluma na biashara,” amesema.

  Kwa kutambua hilo, Agnesy amesema yeye na timu yake kabambe ya TruMark wameamua kuandaa adhimisho la kusheherekea Siku ya Wanawake Duniani ambapo mwaka huu, adhimisho hilo linaambatana na kaulimbiu ya kimataifa linalotutaka watu wote, wanaume na wanaume, kushirikiana kuharakisha harakati za kumwezesha msichana na mwanamke kufikia malengo na mafanikio yake, linalosema "PamojaTunafanikisha".

  Mwaka huu, maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, chini ya mwamvuli wa 'PamojaTunafanikisha' kampuni ya TruMark inaona fahari kubwa kuandaa sherehe hii ambayo ni jukwaa muhimu kwa taifa letu, katika kuhakikisha wanawake wanakuwa sehemu mojawapo ya kuchangia pato la taifa na maendeleo ya nchi.

  “Kila mtu mahali alipo kwa nafasi yake ni kiongozi wa kuleta chachu ya Maendeleo, hivyo basi, haina budi kila mtu, mahali popote, ashiriki vyema na kutimiza wajibu wake huo, huku tukisaidiana kwa pamoja kuanzia ngazi ya familia hadi taifa,” amesema.

  Bi. Mgongo amewashukuru Marie Stopes Tanzania ambao, kwa ushiriki wao, wameamua kutoa huduma ya bure ya upimaji na ushauri wa njia zote za uzazi wa mpango, upimaji wa saratani ya mlango wa uzazi kwa washiriki wote watakaofika kuhudhuria adhimisho hilo la Pamoja Tunafanikisha. Amewaomba wanaume kushiriki kwenye tamasha hili la Pamoja Tunafanikisha ili kwa pamoja jamii nzima iweze kufanikisha, sio tu mafanikio ya wanawake, lakini pia kuwawezesha kupata fursa zote za mafanikio, ikiwa ni pamoja na kutafuta fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.

  Adhimisho hilo, ambalo litafanyika kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga, Dar es Salaam, Jumamosi, tarehe 5 Machi 2016, litakuwa na burudani zitakazotolewa na Barnaba na Classic Band, Bi. Patricia Hillary na mchekeshaji maarufu MC Pilipili, wakisindikizwa na wasanii chipukizi.

  TruMark inawashukuru wahamasishaji na wadhamini wa maadhimisho haya, ambao ni Vayle Springs, Mummy’s Exclusive Shop, Flexible Entertainment, Marie Stopes Tanzania, King Solomon Hall, King Solomon Events, Mono Accessories, CSI Tanzania, MagicFM na Channel Ten.

  Imetolewa na TruMark Limited | +255-718-969 731 | +255-716-676 665 | info@trumark.co.tz

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi akiangalia maendeleo ya kazi ya ubomoaji wa jengo la ghorofa kumi na sita (16) ambapo ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ambapo kwa sasa zimebaki ghorofa sita (6) tu.
  Mafundi wakiendelea na Ubomoaji wa jengo la ghorofa kumi na sita (16) ambapo kwa sasa zimebaki ghorofa sita (6) tu.

  0 0

  Mhasibu wa Wizara ya Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Godfrey Osmund akimweleza Naibu waziri wa wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura jinsi atakavyozikatia risiti fedha ambazo wadau wa michezo wamezitoa kwa ajili ya kuichangia Timu ya Taifa ya wanawake ya Mpira wa miguu ya Twiga Stars.
  Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi leo Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund shilingi milioni mbili zilizotolewa na Mohammed Dewji kwaajili ya kuisaidia timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars. Hadi sasa wadau wa michezo wameshaichangia timu hiyo shilingi milioni 17.Picha na Anna Nkinda

  0 0

  RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Gianni Infantino kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) mwishoni mwa wiki nchini Uswisi.

  Katika barua hiyo, Malinzi amesema TFF ina imani na ahadi zake za kuendeleza mpira wa miguu, na kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ataendelea kushirikiana naye katika kila jambo katika nafasi yake hiyo na kumtakia kila la kheri na mafanikiko mema.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.PICHA NA IKULU.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kando ya Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Mkoani Arusha, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuimarisha mahusiano hususani katika masuala ya kiuchumi.

  Baadhi ya maeneo waliyokubaliana kutilia mkazo katika mahusiano hayo, ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo inayounganisha nchi mbili ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kukuza biashara na kuzalisha ajira kupitia viwanda.Rais Uhuru Kenyatta amesema amefurahishwa sana kuona Rais Magufuli yupo tayari kuhakikisha nchi ya Kenya na Tanzania zinakuwa karibu, na miradi ya maendeleo inaharakishwa.

  "Kwa sababu nia yetu sisi ni kuona maendeleo ambayo yatagusa mwananchi wa kawaida, tumalize umasikini, uchumi ukue, na hivyo hatuwezi kufanya tukiwa tumetengana" Amesisitiza Rais Kenyatta.

  Kwa upande wake Rais John Pombe Magufuli, amesema Tanzania na Kenya zina kila sababu ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara hasa katika ujenzi wa viwanda utakaozalisha ajira kwa kuwa watu wake ni wamoja.

  "Wazee wetu Mzee Kenyatta na Mzee Nyerere walijenga mazingira mazuri ya kuwa na nchi hizi mbili wakati wakipigania uhuru, sasa sisi vijana wao ni wakati wetu kwenda mbele kwa ajili ya maendeleo" amebainisha Rais Magufuli.Dkt. Magufuli amebainisha kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinajenga mahusiano na ushirikiano zinalenga kupata manufaa hayo ya kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wake.

  Ameutaja mradi mmojawapo kuwa ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tanzania kwenda nchini Kenya kupitia Namanga, na akaongeza kuwa Tanzania itakapoongeza uzalishaji wa umeme na kuanza kuvuna gesi, itaiuzia pia Kenya, halikadhalika Kenya nayo itauza bidhaa zake Tanzania.

  Kabla ya kukutana na Rais Kenyatta, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuzidisha mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda ambapo Rais Magufuli amemhakikishia kuwa serikali yake itakamilisha ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge" ili kurahisha usafirishaji wa bidhaa na watu.

  Rais Kagame amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake bora uliolenga kuimarisha uchumi, ikiwemo kuimarisha bandari ya Dar es salaam ambayo Rwanda inaitegemea na ujenzi wa Reli ya Kati ambayo pia ni tegemeo kubwa kwa uchumi wa Rwanda.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiano, IKULU
  Arusha
  02 Machi, 2016

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliyofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.PICHA NA IKULU
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na badhi ya Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Museven baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC,(kulia) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC.
  Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki wakisimama wakati wimbo wa umoja wa nchi hizo ukipigwa katika mkutano wa 17 wa EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto mkoani Arusha,
  Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki akiwemo mwenyekiti wa mkutano wa 17 wa EAC Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kabla ya kuanza kwa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Ngrdoto Mkoani Arusha.
  Mwenyekiti wa Mkutano wa 17 wa Afrika ya Mashariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto) akiongoza mkutano huo uliofanyika leo ukumbi wa Ngrdoto Hotel mkoani Arusha,wengine ni Vionngozi mbali wa Jumuiya hiyokamawanavyoonekanwa,
  Baadhi ya waalikwa katika wakiwa katika ukumbi wa mkutano Ngurdoto Mkoani Arusha leo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Mkutano wa 17 wa Afrika ya Mashariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (kulia) akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa 17 wa Viongozi wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto Hotel Mkoani Arusha.
  Miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania walioalikwa katika mkutano wa 17 wa Viongozi wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto Hotel Mkoani Arusha,(katikati) Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini,akiwa na Mawaaziri wa Nchi za Jumuiya hiyo.

  0 0

  DIWANI wa kata ya Mangaka Halima Mchoma akikabidhi vitabu kwa mmoja wa walimu wakuu wa shule za msingi nne za kata ya Mangaka hii leo kwenye viwanja vya shule ya msingi Mangaka.

  ---------------------
  Na Clarence Chilumba, Masasi.

  DIWANI wa kata ya Mangaka jimbo la Nanyumbu mkoani Mtwara, Halima Mchoma amenunua vitabu 488 vya masomo ya sayansi na stadi za kazi vyenye thamani ya shilingi milioni 1,157,000/= kwa wanafunzi wa darasa la nne wa shule za msingi za kata hiyo.

  Shule zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na shule ya msingi Mangaka,Nahawara,Ndwika 2 naMtokora ambazo zote ni kutoka katika kata ya Mangaka Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara.

  Vitabu alivyovinunua diwani huyo ni pamoja na vitabu 388 vya somo la sayansi, vitabu 100 vya somo la stadi za kazi pamoja na boksi nne za peni zenye peni 400 ambazo watapewa walimu wa shule za msingi katani humo.

  Diwani huyo ameamua kununua vitabu hivyo pamoja na peni kwa walimu wote wa kata hiyo kwa fedha zake za mfukoni kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya kutoa elimu bila malipo.

  Akizungumza leo wakati wa kukabidhi msaada huo kwa walimu wakuu wa shule hizo katika viwanja vya shule ya msingi Mangaka alisema ameamua kununua vitabu vingi vya sayansi kutokana na ugunduzi wa gesi mkoani humo ambao wengi wa wataalamu wanaohitajika ni wale waliosoma masomo ya sayansi.

  Alisema kutokana na kero ya upungufu wa vitabu kwenye kata hiyo waliyokuwa wanailalamikia walimu ndicho kilichomsukuma kuamua kununua vitabu hivyo ambapo kwa sasa kila mtoto wa darasa la nne atatumia kitabu kimoja kama inavyotakiwa kitaalamu.

  Mchoma alisema kwa vitabu vya awamu ya kwanza alivyonunua vina thamani ya sh.1.2 milioni na kwamba lengo lake kwa sasa ni kutatua changamoto zilizopo kwenye shule hizo ikiwemo upungufu wa madawati,matundu ya vyoo,vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za walimu.

  “Nimeguswa na tatizo la wanafunzi wa kata yangu kutumia kitabu kimoja zaidi ya wanafunzi wawili…ndio maana nimeamua kununua vitabu hivi ambavyo kwa sasa naamini kila mwanafunzi anayesoma darasa la nne kwenye kata hii atatumia kitabu chake na nitafanya hivi kwa kipindi chote cha uongozi wangu ndani ya miaka mitano,”alisema Mchoma.

  Alisema pia amefanya uamuzi huo baada ya kuguswa na namna walimu wa kata hiyo wanavyojituma katika kufundisha kunakopelekea shule za kata hiyo kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani mbalimbali ikiwemo yale ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2015.

  Kwa upande wake ofisa elimu taaluma wa shule za msingi wilayani Nanyumbu Stephen Urassa alimpongeza diwani huyo kwa namna alivyoonesha njia na kwamba msaada huo umekuja wakati muafaka ambao wanafunzi wa darasa la nne wanajiandaa kufanya mitihani ya majaribio.
  “Nimekuwa Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu tangu mwaka 2008…lakini sijawahi kuona kiongozi yeyote wa kisiasa akitoa msaada wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za msingi hivyo hii inaonesha ni kwa namna gani wananchi wa kata ya Mangaka hawakufanya makosa kukuchagua”.alisema Urassa.

  Naye mratibu Elimu kata wa kata ya Mangaka Fidelis Hokororo alisema kata hiyo ina jumla ya wanafunzi 253 wa darasa la nne ambapo kutokana na msaada huo kwa sasa kila mwanafunzi wa darasa la nne atakuwa anatumia kitabu kimoja cha sayansi huku vitabu 135 vikiwa zidifu.

  Alisema kwa upande wa vitabu vya stadi za kazi ambavyo ni 100 kwa wastani kila wanafunzi watatu watakuwa wanatumia kitabu kimoja na kwamba watatumia baadhi ya vitabu vilivyopo kwenye shule hizo ili kufikia lengo la kila mwanafunzi kutumia kitabu kimoja.

older | 1 | .... | 782 | 783 | (Page 784) | 785 | 786 | .... | 1898 | newer