Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

MAHAKAMA YA TANZANIA YAKUTANA NA WADAU JIJINI DAR ES SALAAM, YASISITIZA UTOAJI WA HAKI KWA WAKATI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU

$
0
0
  Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein Katanga (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi  Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja,  jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mtendaji Mkuu Mahakama Kuu, Solanus Nyimbi na Kulia ni Msajili wa Mahakama ya Rufaa,  John Lugalema Kahyoza
  Mmoja wa washiriki wa kikao hicho akichangia.
 Msajili wa Mahakama ya Rufaa,  John Lugalema Kahyoza akizungumza na Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi Februari 1 hadi 3, 2016  katika viwanja vya Mnazi mmoja,  jijini Dar es salaam.
 Washiriki wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi  Februari 1 hadi 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja, wakifuatilia kikao hicho leo jijini Dar es salaam.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

Mahakama ya Tanzania imesema kuwa inaendelea na mkakati wa kufanya maboresho ya miundombinu yake ili kurahisisha  utoaji wa huduma ya mahakama kwa wadau na wananchi kwa wakati.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania Bw. Hussein Katanga wakati wa kikao cha Mrejesho wa Wadau walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya Sheria kwa wananchi Februari 1 hadi 3 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi mmoja,  jijini Dar es salaam.

Bw. Katanga amewaambia wadau hao kuwa Mahakama ya Tanzania inaendelea kufanya mabadiliko ya huduma zake kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka Serikalini pia kutoka kwa wadau wa Haki wanaoiwezesha Mahakama kufanya maboresho hayo kwa lengo la kukuza Utoaji wa Haki nchini.

Amesema ili kusogeza huduma karibu na wananchi  Mahakama itatekeleza Mpango mkakati wa miaka 5 wa kuiwezesha kushirikiana kwa karibu zaidi na wadau na Taasisi za utoaji Haki katika masuala yanayohusu shughuli za kila siku za utendaji wa Mahakama nchini.

“ Mahakama tutaanzisha mpango wa miaka 5 ambao utaanzisha mfumo wa wa kushirikiana na wadau wetu kwa karibu katika mambo yanayohusu shughuli zetu ili kuwaondolea wananchi usumbufu na upotevu wa muda pindi wanapofuatilia huduma” Amesema.

Amefafanua kuwa Mahakama imeshaanza kujenga majengo mapya ya kisasa ya Mahakama za Mwanzo katika maeneo mbalimbali  nchini ikiwemo Mahakama ya mwanzo Kigamboni jijini na Kawe zote za jijini Dar es salaam, Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga  na Kibaha mkoani Pwani ili kurahisisha utoaji wa Haki.

“ Mahakama sasa tuko katika mwelekeo mzuri wa kufanya mabadiliko, kwa kushirikiana na wataalam wetu wa ndani wakiwemo Chuo Kikuu Ardhi , tunaendelea kujenga majengo mapya ya Mahakama katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mahakama ya Mwanzo Kigamboni, Mkuranga, Kibaha na Kawe ambayo yatakamilika ifikapo Juni mwaka huu” Amesisitiza.

Bw. Katanga ameongeza kuwa mpango uliopo ni kuhakikisha kuwa majengo yaliyopo yanakarabatiwa sanjali na ujenzi wa majengo mapya katika Mahakama zote 133 nchi nzima.

Aidha, amebainisha kuwa Mahakama inaendelea kujenga mazingira wezeshi kwa watumishi wake ikiwemo ununuzi wa mabasi ya kusafirishia watumishi, magari madogo na Pikipiki ili kuwawesha watumishi wa Mahakama kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Solanus Nyimbi akizungumza na wadau hao amewataka wafanye kazi kwa kushirikiana katika kuwahudumia wananchi ili kuongeza imani yao kwa Mahakama.

Amezitaka Taasisi na wadau wanaohusika na utoaji wa Haki kujikita katika kushughulikia matatizo ya wananchi ili kufanikisha dhana ya Utoaji Haki kwa Wakati ili kwenda na mpango uliowekwa na Mahakama wa kuondoa mrundikano wa mashauri mahakamani na ule wa kuzifuta kesi zilizokaa muda mrefu.

Naye Msajili wa Mahakama ya Rufaa,  John Lugalema Kahyoza ametoa wito kwa Taasisi za Utoaji wa Haki kukutana mara kwa mara ili kujdili na kutatua changamoto zinazoukabili Utoaji wa Haki nchini.

DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUFUNGWA CHUMBA CHA UPASUAJI CHA HOSPITALI YA SANITAS YA MIKOCHENI

$
0
0
Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji cha hospitali ya Sanitas ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake kimefungwa kwa kutokidhi vigezo vya kimataifa vya namna chumba hicho kinavyotakiwa kuwa.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo mapema jana Februari 29.2016, alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo majira ya saa nane na nusu mchana ambapo baada ya kutembelea hospitali nzima na kushuhudia namna ya utolewaji wa huduma, hakuridhishwa na hali aliyokutana nayo kwenye chumba hicho na kutoa maagizo kwa Msajili wa Hospitali Binafsi, Dkt. Pamela Sawa kufunga chumba hicho mpaka uongozi wa hospitali hiyo utakapofanya marekebisho ya mapungufu yaliyopo.

“Chumba cha upasuaji hakiko sawa, siwezi kuvumilia kuacha chumba hiki kiko chini ya kiwango cha kimataifa. Rekebisheni chumba hiki kwa kutumia mfumo wa ramani wa wizara,” alieleza Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo kwa mmoja wa Ofisa wa Hospitali hiyo.

Aidha uongozi wa hospitali hiyo umepewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo ya kutowalipa mishahara kwa kipindi cha miezi minne watumishi wake pamoja na jinsi wanavyoteketeza taka hatarishi za hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alipata malalamiko kutoka kwa watumishi hao ambao wamelalamikia kukatwa kwa makato ya mafao pasipo kupelekwa mahali husika kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu.

Dkt. Kigwangalla alivitaja viwango vya chumba cha upasuaji kuwa kinatakiwa chumba cha kubadilishia mavazi,kunawa mikono,sehemu ya alama maalum zenye rangi nyekundu, meza ya upasuaji, ukanda wa usafi, chumba cha mapunziko baada ya kutoka kwenye upasuaji na chumba cha kusafishia vifaa vya upasuaji na kuna mashine maalum kwa kuwa kila upasuaji una idadi ya vifaa vinavyotumika.

Aliongeza kuwa viwango hivi vinawekwa ili kuepuka maambukizi.
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral alisema watarekebisha mapungufu yaliyobainika pamoja na kufanya yale yote waliyoagiziwa baada ya tukio hilo.
Tazama MO tv, kuangalia tukio hilo hapa:
Imeandaliwa na Magreth Kinabo, (MAELEZO), Andrew Chale, Modewjiblog/MO tv)
dk kigwa
Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo machache kutoka kwa Meneja uendeshaji wa Hospitali ya Sanitas, Bi. Gean Cabral wakati walipowasilia katika ziara hiyo..
dk hk 888Dk Kigwangalla akikagua baaadhi ya sehemu katika hospitali hiyo.
dk hk55Dk. Kigwangalla akizungumza na baadhi ya wagonjwa (hawapo pichani) namna Serikali ya Rais Magufuli inavyofanya kazi kwa kusimamia haki na usawa ikiwemo kufika katika maeneo yenye kero na kuchukua hatua ilikumuokoa Mwananchi katika kupata haki yake na huduma bora anayostahiki.
Kigwangalla akitoa maagizo
Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo kwa Meneja uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral
dk hkna
Dk. Kigwangalla akimuonesha moja ya 'karatasi' iliyoandikwa ujumbe mbalimbali dhidi ya madai kutoka kwa wafanyakazi wa Hospitali hiyo.
dk kigwa
Meneja Uendeshaji wa Hospitali hiyo Bi. Gean Cabral akifafanua jambo pamoja na Naibu Waziri wakati wa ziara hiyo..
dk hk iio
Dk Kigwangalla akiangalia namna hali ya Maabara ya Hospitali hiyo licha ya kuwa na vifaa vya kutosha, lakini imeshindwa kuweka mpangilio mzuri unaotakiwa kutumika katika mahabara. ikiwemo suala la usafi
dk hk67
Naibu Waziriwa Afya, Dk. Kigwangalla (kushoto), Msajili wa Hospitali Binafsi pamoja na maafisa wengine akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dk. Aziz (kulia) wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ya kushtukiza kuangalia namna ya uendeshaji katika huduma za Sekta za Afya, zikiwemo za Serikali na zile za watu binafsi. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv).

HALI YA UNYONYESHAJI WATOTO NCHINI SIO NZURI

$
0
0
DSC_0599Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman akitoa neno la ufunguzi katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.(Picha zote na Rabi Hume wa Modewjiblog)
DSC_0630Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF akielezea hali ya unyonyeshaji kwa watoto ilivyo nchini.
DSC_0622Baadhi ya wadau wa sekta ya afya waliohudhuria katia warsha hiyo wakifatilia kwa makini ripoti zilizokuwa zikitolewa.
DSC_0654Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akielezea kuhusu makala za The Lancet juu ya uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama jinsi kunavyoweza kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.
DSC_0655Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin akiwaonyesha wahudhuriaji wa warsha hiyo ripoti ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet linalohusika na kuandika habari za afya.
DSC_0661Viongozi wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakifatilia ripoti ya utafiti uliofanywa na jarida la The Lancet. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman.
DSC_0665Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery Nkya akielezea hatua ambazo serikali imechukua ili kupunguza idadi ya kina mama ambao hawanyonyeshi watoto.
DSC_0674Viongozi wa Taasisi mbalimbali waliofika katika warsha hiyo wakisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wadau wa sekta ya afya na waandishi wa habari. Wa kwanza kulia ni Mshauri Mwandamizi wa maswala ya watoto wadogo na unyonyeshaji kutoka Makao Makuu ya UNICEF, New York, Dr. France Begin, Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Vicent Assey, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu,Obey Assery Nkya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda na Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman.
DSC_0696Mkuu wa kitengo cha fedha na malipo nchini kutoka Benki ya Dunia, Douglas Pearce akiuliza swali katika warsha hiyo.
DSC_0711Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman akitoa neno la shukrani kuashiria kumalizika kwa warsha hiyo.
Imeelezwa kuwa wastani wa unyonyeshaji kwa watoto walio chini ya miezi sita nchini sio mzuri na hivyo kuwa na uwezekano wa watoto kudhoofika kwa kukosa maziwa ya mama ambayo yanakuwa na virutibisho muhimu kwa ukuaji ya mtoto.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe, Dkt. Joyceline Kaganda katika warsha iliyoandaliwa na UNICEF ili kujadili jinsi uwekezaji mkubwa zaidi katika kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kusaidia maendeleo kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto nchini.
Dkt. Kaganda amesema wastani wa unyonyeshaji kwa watoto walio chini ya miezi sita ni asilimia 42 na wastani huo ni mdogo hivyo kuashiria kuwa hali sio njema kwa watoto ambao hawapati maziwa ya mama.
Amesema kiafya inatakiwa mtoto aanze kunyonya nusu saa baada ya kuzaliwa na mtoto anyonye maziwa ya mama yake kwa kipindi kisichopungua miezi sita na baada ya hapo anaweza kuanza kuwa anachanganya na vyakula vingine kama uji na maji.
“Hali sio nzuri ukiangalia wastani wa wamama ambao wanawapa watoto wao maziwa ya kunyonya ni wachache na labda inawezekana wengi wakawa hawatambui matatizo yanayoweza kutokea kama hawatawanyonyesha watoto wao,” amesema Dkt. Kaganda.
Aidha Dkt. Kaganda amesema kazi zinachangia kina mama wengi kushindwa kuwanyonyesha watoto wao lakini wanaweza kuweka utaratibu wa kuwa wanakamua maziwa yao na kuyahifadhi sehemu nzuri ili hata kama wanapokuwa mbali na watoto wao, msimamizi anayemuangalia mtoto aweze kumpa mtoto ili kumfanya apate virutubisho muhimu kutoka kwenye maziwa ya mama yake.
Nae Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman amesema katika kusaidia Tanzania kuongeza wastani wa watoto ambao wananyonya wamekuwa wakitoa elimu kwa kina mama wanaonyonyesha pamoja na familia zao ili wajue umuhimu wa mtoto kunyonya maziwa ya mama.
Alisema watoto wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa matatizo ambayo yanatokana na kukosa maziwa ya mama zao na hivyo ili kuzidi kushughulikia tatizo hilo wanataraji kuanza kutoa elimu kwa watumishi wa afya katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe na wanataraji kutembelea zaidi maeneo ya vijijini kutokana maeneo hayo kuonekana kutokuwa na elimu hiyo zaidi.
“Watoto wamekuwa wakipata matatizo na kupoteza maisha na hiyo inachangiwa na kutokunyonya kwa mama … tumeshirikiana na serikali tunataraji kutoa elimu katika vijiji zaidi ya 15,000 kwenye mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya na tutafundisha pia mama na familia umuhimu wa mtoto kunyonya,” alisema Bi. Zaman.
Alisema baada ya kumalizika kwa mikoa hiyo wataendeleza utoaji wa elimu nchi nzima ili jamii ya Tanzania itambue umuhimu wa watoto kunyonya maziwa ya mama na pia kuwaomba waandishi wa habari kutumia nafasi yao katika jamii ili kuwaelimisha watanzania kuhusu tatizo hilo.
Katika makala zilizoandikwa katika jarida la habari za afya la The Lancet linaonyesha kuwa uboreshaji wa kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kuokoa maisha zaidi ya watoto 820,000 kila mwaka duniani na Dola za Kimarekani Bilioni 302 kila mwaka.
Imendaliwa na Rabi Hume wa Modewjiblog

SERIKALI YAITAKA GAZETI LA DIRA MTANZANIA KUKANUSHA NA KUMUOMBA RADHI BALOZI OMBENI SEFUE

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

IDARA YA HABARI - MAELEZO

                          
                    P.O. Box 8031, Dar es Salaam, Tel:  2110585, 2122771/3, Fax: 2113814, e-mail: maelezo@habari.go.tzTarehe: 01/03/2016

Gazeti la Dira ya Mtanzania, Toleo Na.404 la Februari, 29 – Machi 6, 2016 liliandika taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho “Uchafu wa Ombeni Sefue Ikulu”.  Taarifa hiyo, ambayo ni muendelezo wa makala nyingine kwenye toleo la gazeti hilo la wiki iliyopita, ilimtuhumu Katibu Mkuu Kiongozi kushawishi juu ya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD pamoja na Kampuni za “CRJE” na “UGG” kupewa tenda ya kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma, Daraja la Kigamboni na Reli ya Dar es Salaam - Kigali. Taarifa zote hizi ni za uongo na za kupotosha wananchi.  

Kuhusu uteuzi wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD,

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, hakuhusika kwa namna yoyote kushawishi uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD. Uteuzi huo ulitekelezwa kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa. Nafasi hiyo ilitangazwa na Bodi tarehe 20 Novemba, 2013. Usaili ulifanywa na kampuni huru iliyopewa jukumu hilo na Bodi. Mapendekezo ya majina matatu yalipelekwa kwa Mhe. Rais na Waziri wa Afya, kwa ajili ya uteuzi. Balozi Sefue alikuwa hamjui aliyeteuliwa na wala hakuwahi kuwa na uhusiano naye. 

Alichofanya Balozi Sefue ni kutangaza tu uteuzi baada ya Rais kuteua. Gazeti hilo pia limeandika uwongo kuwa MSD haijawahi kuongozwa na Mkurugenzi Mkuu asiye Mfamasia.  Tangu MSD ianzishwe mwaka 1993 hadi sasa, ni Mkurugenzi Mkuu mmoja tu, Rino Meyers (1996-1999), ndiye  alikuwa Mfamasia. Wakurugenzi wengine kama  Peter Mellon (1993-1995), Jay Drosin (2001-2004) na Joseph Mgaya (2004-2013) hawakuwa Wafamasia.



Kuhusu Kampuni ya CRJE kuhusishwa na Balozi Ombeni Y. Sefue

Suala la kumhusisha Katibu Mkuu Kiongozi na kampuni hii nalo ni uzushi na uongo wa kupindukia. Wakati kampuni hii ikipewa tenda ya kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma mwezi Oktoba 2007, Balozi Ombeni Y. Sefue hakuwa Katibu Mkuu Kiongozi; alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani. Kadhalika mchakato wa kumpata mkandarasi wa daraja la Kigamboni, ulipoanza mwezi Machi, 2011, Balozi Sefuehakuwa Katibu Mkuu Kiongozi; alikuwa Balozi wa Tanzania, Umoja wa Mataifa, New York. Hata mkataba wa ujenzi wa Daraja hilo uliposainiwa tarehe 9 Januari, 2012, Balozi Sefue alikuwa na wiki moja tu ya kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kufuatia kuteuliwa tarehe 30 Disemba, 2011. Aidha, Kampuni iliyoshinda tenda hiyo wala siyo CRJE kama ilivyoandikwa na gazeti hilo bali ni China Major Bridges Engineering Company (BCEC) kwa kushirikiana na Kampuni ya China Railway Construction (CRCEG).


Kuhusu tuhuma kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Chapuo Kampuni ya UGG:

Katibu Mkuu Kiongozi hajawahi kuipigia chapuo kampuni yoyote ile pahala popote. Isitoshe, hakuna kampuni yenye jina la “UGG” iliyowahi kuonesha nia ya kujenga reli ya kati. Hii ni moja ya uthibitisho kwamba  gazeti hili linatoa taarifa za kuokoteza zisizo na ukweli kama vile walivyopotosha kuhusu jina la Katibu Mkuu Kiongozi kwenye makala yao ya pili kwenye ukurasa wa tisa wa gazeti hilo yenye kichwa cha habari “Magufuli anaishi na jipu Ikulu” ambapo walimpachika Katibu Mkuu Kiongozi jina la Sifuni, jina ambalo hajawahi kuwa nalo.  Balozi Sefue hajahusika, hahusiki na wala hatahusika katika kuchagua wa kupewa tenda hiyo kwa sababu yeye si sehemu ya wenye mamlaka ya kutoa tenda.


Kuhusu Eliachim Maswi:

Gazeti la Dira ya Mtanzania limeandika kuwa moja ya “madudu” aliyofanya Balozi Sefue ni walichoita kumsafisha Bwana Eliachim Maswi.  Wanadai hivyo wakati wamekiri kuwa alichofanya Balozi Sefue ni kusoma matokeo ya uchunguzi, ambao hakuufanya yeye.  Waliomsafisha Maswi ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali; Sekretarieti ya Maadili ya Umma; na hatimaye kamati ya uchunguzi iliyoongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu.   Kwa hiyo, kwa maoni ya gazeti hili, Balozi Sefue asingepaswa kusoma matokeo ya uchunguzi uliofanywa na vyombo hivyo huru.  Kwa maoni yao kusoma taarifa ya uchunguzi ni “madudu”.


Habari hizo hazina chembe yoyote ya ukweli, na wao wenyewe ndani ya gazeti wamekiri hawana ushahidi,  ni wazi kuwa habari hizo ni za kubuni na zimetungwa.


Kwa sababu hiyo, Serikali inalitaka Gazeti la Dira ya Mtanzania kukanusha uongo na uzushi wao na kumuomba radhi Balozi Ombeni Sefue, kuiomba radhi Serikali na kuwaomba radhi wote walioumizwa na uzushi huo   kwa uzito ule ule uliotumika kuchapisha taarifa hiyo. 


Vinginevyo iwapo gazeti la Dira ya Mtanzania lina ushahidi wa huo “uchafu” wa Katibu Mkuu Kiongozi,  waupeleke mara moja kwenye vyombo vinavyohusika ikiwamo Sekretarieti ya Maadili na TAKUKURU. Vinginevyo, hatua zikichukuliwa dhidi yao wasiseme Serikali inavibana vyombo vya habari.


Aidha Serikali inashauri wenye vyombo vya habari, wachapishaji, wahariri na waandishi wa habari wajikite kwenye weledi na ukweli, wafanye utafiti na kuandika mambo waliyo na uhakika nayo, na kamwe wasikubali kutumiwa kuendeleza agenda za watu wengine.



MWISHO.

BENKI YA BARCLAYS AFRIKA YAKUA KWA ASILIMIA 10.

$
0
0
 Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya Afisa mtendaji mkuu wa Benki ya Barclays Afrika , Maria Ramos na waandishi hao kwa njia ya simu ya mezani akiwaAfrika Kusini kuhusiana na benki hiyo kuongeza wateja wake wa bara la Afrika hasa katika nchi za Afrika Kusini, Botswana, Ghana na Zambia ikiwa benki hiyo inawateza zaidi ya 885,000 kwa bara la Afrika na kuongeza mapato yake kwa asilimia 10, Ikiwa kwa bara la Afrika  Maria amesema kuwa inakabiliwa na changamoto nyingi katika ufanyaji wa biashara hasa katika kutokupatawafanyakazi wachapakazi, umasikini na kutokua na usawa katika ufanyaji wa  biashara ya benki.
Kutoka kulia ni Afisa Masoko wa benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendela akisikiliza kwa ukaribu katika simu ya mezani ambayo ilitumika kuongea na Afisa mtendaji mkuu wa Benki ya Barclays Afrika, Maria Ramos akiwa afrika Kusini leo wakati wakiongea na waandishi wa habari wa jijini Dar es Salaam. Aidha Maria amesema kuwa Benki hiyo barani Afrika imeongeza mapato yake kwa asilimia 10 .
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

SADC YAJADILI UWEKEZAJI KATIKA SEKTA VIWANDA JIJINI DAR LEO.

$
0
0
 Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji (TIC), Julieth Kairuki akizungumza katika mkutano wa SADC uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wawakilishi wa nchi mwanachama wa SADC wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji (TIC), Julieth Kairuki akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika mkutano wa wadau wa SADC uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii
SERIKALI imesema itaendelea kuboresha miundombinu ili kuweza kuvutia uwekezaji wa viwanda ili nchi iweze kukua kiuchumi.

Hayo ameyasema leo Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji, Adolff Mkenda katika Mkutano wa w tano Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SADC),amesema kuwa katika kuhamasisha uwekezaji wa ndani nje serikali imejikita katika kujenga miundombinu ya barabara.

Amesema kuwa uchumi unakua kwa asilimia saba na nguvu kazi kubwa iko vijiji kwa theluthi mbili hivyo lazima kuweka mazingira uwekezaji katika nguvu kazi hiyo.

Mkenda amesema wakati inaanzishwa SADC ikiwa ni kujikomboa kisiasa lakini kwa sasa ni nchi kujikomboa katika uchumi katika sekta ya viwanda.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC),Julieth Kairuki amesema kuwa mkutano huo kufanyika nchini mafanikio ya kujifunza kwa nchi zingine zinavyofanya uwekezaji.


Amesema nchi 14 ziko nchini ambapo zitaweza kukubaliana ukuzaji wa uwekezaji wa viwanda katika mapinduzi ya kiuchumi kwa nchi zilizo katika jumuiya hiyo.

Julieth amesema TIC imeweka mazingira ya mazuri kwa wawekezaji wa ndani na nje na sio kugawa maeneo ya vijiji kwa wawekezaji huku wakiwa na hekta 122000.

Benki ya NMB Yadhamini Mkutano wa Mwaka wa Wanasheria Tanzania.

$
0
0
Benki ya NMB imeendelea kuimarisha uhusiano wake na Chama Cha Wanasheria nchini (Tanganyika Law Society) kwa kuudhamini  mkutano wa mwaka kwa kiasi cha Tsh 10M kwaajili ya maandalizi na shughuli za mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
 Ofisa mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo Benki ya NMB PLC Abdulmajid Nsekela akiongea na wanasheria waliohudhuria Mkutano wa Mwaka wa Wanasheria uliyofanyika AICC mjini Arusha.


 Chama Cha Wanasheria nchini (Tanganyika Law Society) waliohudhuria Mkutano mkuu wa mwaka katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.

MKUTANO MKUU WA LAPF KUFANYIKA MACHI 10-11, 2016 UKUMBI WA AICC JIJINI ARUSHA.

$
0
0
 Viongozi meza kuu.

 Meneja Masoko na Mawasiliano Mfuko wa Pensheni wa LAPF  James Mlowe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,  kuhusu mkutano mkuu wa nane wa mfuko huo unaotarajiwa kufanyika machi 10 na 11 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti.
 Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale
MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kuwa na sh.trioni moja  na bilioni 87 za thamani ya uwekezaji kutoka mwezi juni mwaka jana.

Hayo yalibainishwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF James Mlowe wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mkutano mkuu wa nane wa mfuko huo unaotarajiwa kufanyika Machi 10 na 11 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.

Alisema LAPF imeendelea kupiga hatua kila mwaka ukilinganisha na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii hapa nchini.

" LAPF imeweza kutoa mikopo ya masomo kwa watu 800 katika maeneo mbalimbali nchini yenye thami ya sh.bilioni 1.2 jambo ambalo tunajivunia" alisema Mlowe.

Akizungumzia kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika  kwa wadau wa mfuko huo kupatiwa barua za mualiko.

Alisema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene na kuwa mawaziri wengine wakaoshiriki kwenye mkutano huo ni  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama na  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Jafo Selemani .

Alisema katika mkutano huo Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali atatoa taarifa ya hesabu za mfuko huo na pia kutakuwa na mada inayohusu afya kutoka kwa Daktari wa  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)

SHIDA YA MAJI JIJI LA DAR ES SALAAM KUWA HISTORIA

$
0
0
Mafundi wakiwa katika harakati za kulaza bomba litakalotumika kuleta maji kwenye tanki kubwa lililopo kibamba toka Ruvu chini na juu kwa ajili ya uhifadhi na usambazaji maji katika Jiji la Dar es salaam. 
Mafundi wakikarabati bomba kuu la kusambaza maji toka Ruvu juu katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani.
Mkuu wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Katikati) akisikiliza maelezo juu ya ufanyaji wa kazi wa mitambo inayotumika kusambaza maji toka Ruvu juu kutoka kwa Meneja Mradi toka kampuni ya WABAG Mr. Pintu Dutta wakati wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam ilipotembelea mitambo hiyo. 
Mkuu wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Kushoto) akisikiliza maelezo juu ya ramani inayoonesha usambazaji wa maji toka Ruvu Juu kwenda katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi Dawasa Romamus Mwang’ingo.
Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi Dawasa Mhandisi Romamus Mwang’ingo (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Kulia) juu ya ufanyaji kazi wa mitambo ya Ruvu chini.


Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Tatizo la ukosefu wa huduma ya maji katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam linatarajiwa kuwa historia mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa tanki kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita million 10 kwa siku lililopo Kibamba.

Hayo yamebainika mara baada ya wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es Salaam walipotembela mradi huo unaofadhiliwa na nchi ya India ambapo mbali na kujionea ujenzi wa tanki hilo pia walitembelea na kujionea ulazaji wa bomba litakayokuwa linasafirisha maji toka vyanzo vya maji vya Ruvu Chini na Ruvu Juu na kwenda kuifadhiwa katika tanki hilo tayari kwa kusambazwa katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake.

Hata hivyo Disemba 31, 2015 Serikali ya Tanzania na India zilisaini mkataba wa ufadhili wa Dola Millioni 59.3 ili kutekeleza mradi wa ulazji wa bomba la maji kutoka Mlandizi mpaka Kimara na kuishia Kinyerezi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa tanki hilo la Kibamba.

Mradi huo unatarajiwa kukamilika Marchi 31 mwaka huu ambapo mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 90 ili uanze kusambaza maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na viunga vyake.

Mkuu wa msafara wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es Salaam alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Said Meck Sadiq ambaye ndio mwenyekiti wa kamati hiyo amesema lengo la kamati hiyo ni kuona Jiji zima linakuwa na huduma ya maji safi na salama kwa matumizi mbalimbali na kuondokana na suala la maji ya mgao linalolikumba Jiji la Dar es salaam kwa miaka mingi.

“ Tatizo la maji litakuwa historia katika Jiji letu maana mradi huu ni mkubwa sana na utawezesha watu wengi kupata huduma ya maji safi na salama na tutaondokana na uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo na yale ambayo yalikuwa hayana kabisa huduma ya maji kwa kipindi kirefu sana yatapatiwa huduma hiyo”

“ Nawaomba wananchi na wafanyakazi wa Dawasco kutunza miundombinu hii kwani ni hazina kubwa si kwetu tu hata kwa vizazi vijavyo, na ni marufuku kwa watu kujenga nyumba katika eneo lilipopita bombala maji, alama maalum ziwekwe ili kuonesha kuwa sehemu hii bomba limepita ili kuzuia uharibifu wa miundombinu” Alisema Mushi.

Mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa tanki la Kibamba litakuwa na uwezo wa kusambaza maji katika maeneo yafuatayo; Ruvu, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Kimara, ubungo, Segerea, hadi kinyerezi ambapo bomba linatakuwa limeishia hapo na maeneo yote ambayo yanapata maji kupitia mtambo wa Ruvu Juu na Chini na wale amabao bado hawajaunganishwa na huduma ya maji wataunganishwa ili waweze kupata huduma hiyo kwa urahisi zaidi.

Aidha, mmoja kati ya wajumbe wa kamati ya ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam mbunge wa viti maalum Ilala (CHADEMA) Mhe. Anatropia Theonest amesema huduma ya maji ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yoyote, hivyo basi Serikali iliwekee uzito na kulitekeleza kwa nguvu zake zote na kuonya wale wanaohujumu miundombimu ya maji kuchukuliwa hatua za kisheria, iwe ni kwa wafanyakazi wa idara za maji au wananchi ili kuhakikisha huduma hiyo inawanufaisha wananchi.

Kamati ya ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam inaundwa na wakuu wa Wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam, Mameya wote, wabunge wa Mkoa wa kuchaguliwa, kuteuliwa au viti maalum na kamati hiyo inakuwa chini ya Uwenyekiti wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

SERIKALI YALITAKA DIRA YA MTANZANIA KUKANUSHA TUHUMA DHIDI YA BALOZI OMBENI SEFUE

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw.Assah Mwambene (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu taarifa za upotoshaji zilizotolewa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la tarehe 29/02/2016 kuhusu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Vyombo Habari, Bw.Jamal Zuberi na Mkurugenzi Msaidizi Habari Bw.Vicent Tiganya wote kutoka Idara ya Habari (MAELEZO).
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw.Assah Mwambane (ambaye hayupo katika picha) iliyokuwa ikiutaka uongozi wa Gazeti ya Dira Mtanzania kukanusha habari waliyoitoa hivi karibuni iliyokuwa na kichwa cha habari “Uchafu wa Ombeni Sefue Ikulu”.

Na Anitha Jonas – MAELEZO

…………………………

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw.Assah Mwambene ameutaka uongozi wa Gazeti la Dira ya Mtanzania kukanusha haraka na kuiomba radhi Serikali na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kutokana na taarifa waliyoitoa katika toleo namba 404 la tarehe 29/02/2016 lenye kichwa cha habari “Uchafu wa Ombeni Sefue Ikulu.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi huyo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu taarifa kuwa hazikuwa na ukweli wowote kwani Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue hakuhusika katika uteuzi wa Mkurugenzi wa MSD wala kuhusika na kampuni ya CRJE katika utoaji wa tenda ya kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma Oktoba 2007 kwani katika kipindi hicho alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

“Serikali inautaka uongozi wa Gazeti la Dira ya Mtanzania ukanunushe taarifa hiyo kwa uzito ule uliyotumika kuchapisha habari hiyo na kama wanapinga wakidai wana ushahidi basi waupeleke mara moja kwenye vyombo vinavyohusika ikiwemo Sekretarieti ya Maadili na TAKUKURU”,alisema Bw.Mwambene.

Aidha, Bw.Mwambene amesema gazeti hilo liliandika kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipigia chapuo Kampuni ya “UGG” iliyowahi kuonyesha nia ya kujenga reli ya Kati nchini. Taaarifa hii pia siyo ya kweli na hakuna kampuni yenye jina la “UGG” ilishawahi kuonyesha nia ya kujenga reli hiyo.

Mkurugenzi aliendelea kusema kuwa gazeti hilo lilimtuhumu pia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue kuhusika na kumsafisha Bwana Eliakim Maswi wakati alichokifanya Balozi Sefue ilikuwa ni kusoma matokeo ya uchunguzi ambao hakuufanya yeye. Waliomsafisha ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Kamati ya Uchunguzi iliyoongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu kwani ndio waliiyofanya uchunguzi huo.

Hata hivyo serikali imewashauri wamiliki wa vyombo vya habari,wachapishaji,wahariri, na waandishi wa habari wajikite kwenye weledi na ukweli pia wafanye utafiti wa kina na kuandika mambo waliyo na uhakika nayo

Wataalamu TPRI wapelekwa Kilombero kufanya uchunguzi

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro imewapeleka wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Viuwatilifu ya Kitropiki (TPRI) wilayani Kilombero kufanya uchunguzi wa zao la mpunga linalosadikiwa kuharibiwa na dawa zilizomwagwa na Kampuni ya Kilombero Plantation (KPL) inayomiliki mashamba yanayopakana na mashamba ya wananchi.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mali Mkoa wa Morogoro Bw. Ernest Mkongo kuhusu uchunguzi unaoendelea kufanyika katika mashamba ya wananchi ili kutathmini athari zinazotokana na dawa hizo.

“Wataalamu kutoka TPRI wameshafanya uchunguzi wa awali na mpunga huo umeonekana kuwa na rangi ya njano isivyo kawaida, hivyo wamechukua sampuli za mpunga huo na kuzipeleka maabara kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kujua kama umeharibiwa na dawa za kuondoa magugu zilizomwagwa na Kampuni ya KPL” alisema Mkongo 

Aidha, Bw. Mkongo ameongeza kuwa, Taasisi ya TPRI ina wataalamu wa uhakika kwa hiyo anaamini watatoa majibu ya ukweli juu ya tatizo hilo.

TPRI ilianzishwa miaka ya 1940 ambapo kwa Tanzania ilirasimishwa rasmi katika Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Sheria Na. 18 ya mwaka 1979 kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa dawa zinazoathiri afya ya binadamu, wanyama na mazao.

NAIBU WAZIRI DKT ABDALLAH POSSI ATEMBELEA SHULE ZA WATU WENYE ULEMAVU JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na watoto wenye ulemavu wa ngozi (albinism) katika ziara yake shule ya Arusha ikiwa ni moja ya kituo alichotembelea mkoani Arusha Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Arusha wakati wa ziara yake ya kuangalia hali ilivyo katika Vituo, Vyuo na shule zinazolea watoto wenye ulemavu Mkoani Arusha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na mwanafunzi wa shule ya msingi Themi mwenye tatizo la uoni Bi. Lissa Lucas wakati wa ziara yake shuleni hapo Februari 29, 2016
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Longido mkoani Arusha wakati wa ziara ya kutembelea watoto wenye ulemavu na mahitaji maalum mkoani hapo Februari 29, 2016. 

TFDA YAKAMATA KIWANDA BUBU CHA KUTENGENEZA PERFUMES BANDIA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa, Hiiti  Sillo akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kukamatwa kwa kiwanda bubu cha kutengeneza perfumes bandia  aina SAME.leo  jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti  Sillo akiwaonesha wandishi wahabari (hawapo  pichani) mitambo ya kutengenezea perfumes bandia zinazoitwa kwa jina la SAME   leo jijini Dar es Salaam. 
Wandishi wakimsilkiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa, Hiiti  Sillo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA), Hiiti  Sillo akiwaonesha wandishi wa habari perfumes bandia zinazoitwa kwa jina la SAME   leo jijini Dar es Salaam.


 Na Emmanuel Massaka wa Globul ya jamii

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ,Kanda ya Mashariki kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imekamata  vipodozi vya manukato ‘Perfume’  katika nyumba  inayomilikiwa na Mwanaidi iliyopo eneo la Tuangoma,  Wilayani Temeke Mkoani Dar es Salaam.

Akizungumzna na wandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo ,Mkurugenzi Mkuu wa TFDA,Hiiti Sillo amesema kuwa walipata taarifa juu ya utengenezaji wa mafuta ya manukato na ndipo wakafanyia kazi na kwenda kukamata.

 Amesema katika nyumba hiyo  ina vifaa vya kimaabara, malighafi na kemikali mbalimbali  za kutengeneza manukato yenye alama ya kibiashara  SAME huku mafuta yakionyeshwa stika kuwa inatengenezwa nchini Uturuki

Sillo amesema wangalizi wa nyumba hiyo Fatuma Selemani anashikiliwa na Jeshi la Polisi ili kusaidia upelelezi na jalada la Polisi na MBL/IR/1998/2016 limefunguliwa katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Mbagala, Temeke.

Amesema vielelezo vyote ikiwa ni chupa 5,350 za perfumes zilizokamatwa dukani pamoja na vifaa, malighafi, kemikali na stika mbalimbali zilizokamatwa dukani vinashikiliwa.

Sllo  amewaomba wananchi wote ambao wanazo majumbani kwao perfumes aina ya SAME waache kuzitumia na wazirudishe katika ofisi za TFDA zilizopo hapa nchini kwa sababu perfumes hizo hazijasajiliwa na TFDA na hivyo ubora na usalama wake haufahamiki.

Aidha amesema wananchi waendelee kutoa taarifa kuhusu mtu au makundi ya watu mbalimbali wanaojihusisha na biashara haramu za utengenezaji, uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba katika maduka au majumbani mwao.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWASILI MWANZA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , Magesa Mulongo baada ya kuwasili kwenye uwanja  wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo baada ya kuwasili  kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mwanza baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1,2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi, Angelina Mabulla baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimu wananchi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitazama ngoma  ya nyoka baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Magessa Mulongo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Rais Magufuli akutana na kuzungumza na Rais Museveni


Rais Magufuli akutana na kuzungumza na Rais Museveni

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na akifafanua jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha jijini Arusha leo Machi 1, 2016 mara tu baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.Pichani kulia ni Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni.
 Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni akiongea na wanahabari mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha jijini Arusha leo Machi 1, 2016 mara tu baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.Pichani shoto ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisikiliza kwa makini 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni wakifanya mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha jijini Arusha leo Machi 1, 2016 mara tu baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. 


MAGAZETINI LEO JUMATANO

$
0
0
Karibu katika magazeti ya leo 02 March 2016. Kama ukihitaji kusoma zaidi pitia katika meza za magazeti karibu nawe upate habari kwa kina


MKUTANO WA 10 WA KUTATHMINI SEKTA YA AFYA UNAOFANYIKA KILA MWAKA WAFUNGULIWA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Muhammed Jidawi akiwakaribisha washiriki wa Mkutano wa siku tatu wa kutathmini sekta ya Afya Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, Mazizini.
Kiongozi wa washirika wa maendeleo kutoaka Mashiriki ya Umoja wa Mataifa DKT. Kirsten Havemann akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini sekta ya Afya Zanzibar unaofanyika Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Baadhi ya washirika wa maendeleo na maafisa wa Wizara ya Afya Zanzibar wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifungua Mkutano wa 10 wa kutathmini maendeleo ya sekta ya Afya Zanzibar kwa niaba ya Rais wa Zanzibar katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akiteta jambo na kiongozi wa washirika wa maendeleo kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa Dkt. Kirsten Havemann wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kutathmini sekta ya Afya Zanzibar.
Mgeni rasmi Balozi Seif Ali Iddi na washiriki wa maendeleo na maafisa wa Wizara ya Afya Zanzibar mara baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku tatu wa kutathmini sekta ya Afya unaofanyika Zanzibar Beach Resort Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

NAPE ATEMBELEA MITAMBO YA KURUSHA MATANGAZO YA TBC ARUSHA

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo ya kutoka kwa Mkurgenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana (kushoto)mara baada ya kutembelea maeneo ya TBC yaliyopo Themi na Themi Hill mkoani Arusha na kujionea mitambo ya TBC na ile iliyokuwa ya Radio Tanzania .
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia mitambo iliyokuwa ya Radio Tanzania kwenye nyumba iliyokuwa ikitumika kurusha matangazo, Themi mkoani Arusha.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akionyeshwa moja ya eneo la TBC mkoani Arusha na Mkurgenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungunmza na Mkurgenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement Mshana mara baada ya kutembelea eneo la TBC lililopo Themi mkoani Arusha,katikati ni Mkuu wa Kanda wa Shirika la Utangazaji TBC Ndugu Christopher Mkama
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiangalia baadhi ya mitambo ya zamani ya kurushia matangazo iliyopo Themi Hill, Arusha.

President Magufuli and President Museveni agree on building oil pipeline frona Tanga to Uganda

$
0
0
The President of the United Republic of Tanzania Dr. John Pombe Magufuli who is The current chairman of the East African Community (EAC) has held talks with His Excellency Yoweri Kaguta Museveni, The President of the Republic of Uganda in which among other things the two leaders have agreed to the construction of an oil pipeline from the port of Tanga in Tanzania to Uganda.


President Museveni paid a visit to President Magufuli at the state lodge in Arusha this evening soon after arriving in the country from Uganda to attend the 17th East African Community Heads of State Summit to be held at Ngurudoto Hotel in Arusha tommorow.


Speaking after private talks between the two leaders, President Magufuli said they have agreed to implement the Tanga-Uganda oil pipeline project for the benefit of both countries and other East African countries.


He said the oil pipeline will be 1,120 kilometers long and that the project will create more than 15,000 jobs.


President Magufuli added that, apart from constructing the oil pipeline, they also discussed increasing trade within the East African countries, building factories and creating jobs through various productive sectors.


Furthermore, President Magufuli said during the summit, Partner States will also discuss about South Sudan joining the East Africa Community (EAC).


He said that South Sudan becoming a member of the EAC means the region will be able to trade in an area with approximately 150 million people and therefore benefiting greatly.


On his part, President Yoweri Kaguta Museveni besides concurring with President Magufuli, has congratulated his Tanzanian counterpart on his leadership performance so far, and he has said that it is his hope that EAC Partner States will be in position to match President Magufuli’s speed in bringing development.


Gerson Msigwa

Ag. Director for Presidential Communications,

Arusha

1 March 2016




Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images