Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 773 | 774 | (Page 775) | 776 | 777 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Sehemu ya waombolezaji, walioshiriki Mazishi ya mwanahabari wakibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa  Mtangazaji wa  Redio Tumaini, marehemu Fred Mosha makaburi ya Kinondoni baada ya ibada katika Kanisa la Katoliki  la Chang'ombe Parokia ya Mtakatifu Francis Xavier, Temeke, Dar es Salaam 
  Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Fred Mosha likiwekwa sawa tayari kwa Mazishi.
  Ibada ya Mazishi ikiendelea kwenye Makaburi ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam jioni hii.

  0 0   Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa akiwapa pole wanawake na watoto wakati alipotembelea makazi ya dharura  waliyojengewa na serikali katika kijiji cha Kasanga  wanapohifadhiwa waathirika wa mafuriko yaliyozikumba tarafa za Pawaga na Idodi , Iringa Februari 22, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua baadhi ya nyumba za dharura wanazoishi wananchi wa katika kijiji cha Kasanga baada ya maeneo yao kukumbwa na mafuriko kwenye tarafa za Pawaga na Idodi, Iringa  Februari 22, 2016. Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipokea taarifa ya msaada  kutoka kwa meneja uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mangele katika mkutano wa kuwapa pole wananchi wa tarafa za Pawaga na Idodi uliohutubiwa na Waziri Mkuu katika Kijiji cha Kasanga, Iringa Februari 22, 2016. Mfuko huo umetoa mabati 200 na saruji mifuko 200 vyote vikiwa na thamani ya sh. 6,600,000/=.
    Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa akiwapa pole kinamama na watoto wakati alipotembelea makazi ya dharura  waliyojengewa na serikali katika kijiji cha Kasanga  wanapohifadhiwa waathirika wa mafuriko yaliyozikumba tarafa za Pawaga na Idodi , Iringa Februari 22, 2016.

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea misaada mbalimbali yenye thamani ya sh. milioni 85.88/- kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko kwenye vijiji vya kata ya Mlenge, tarafa ya Pawaga,  wilaya ya Iringa vijijini mkoa wa Iringa. 

  Misaada hiyo imetolewa na wadau mbalimbali kutokana na mafuriko ambayo yalibomoa nyumba 82 katika kitongoji cha Kilala, kijiji cha Kisanga na kuwaacha wananchi wake bila makazi. Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kasanga ambako alikwenda kukagua athari za mafuriko  na kuwapa pole wananchi hao leo mchana (Jumatatu, Februari 22, 2016), Waziri Mkuu aliwashukuru wadau wote waliojitolea kuwachangia watu waliopata maafa kutokana na mafuriko hayo.
  Wadau waliotoa misaada hiyo ni Benki ya NMB mabati 500, mifuko ya saruji 500, kilo 820 za maharage, kilo 750 za unga wa mahindi na lita 250 za mafuta ya kupikia vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 20/-. Wengine ni Mfuko wa Pensheni wa PPF uliotoa mabati 200 na mifuko ya saruji 200  vyenye thamani ya sh. milioni 6.6/-.
  Wengine ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) waliotoa mabati 200 na mifuko ya saruji 160 vyenye thamani ya sh. milioni 4.5/-; Kiwanda cha kusindika nyanya cha RedGold kimetoa mifuko ya saruji 100 na mabati 50 vyenye thamani ya sh. Milioni 3/-; mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya CHADEMA, Bi. Susan Chogisasa na wenzake wametoa mabati 150, mifuko 23 ya saruji, kilo 100 za  maharage, kilo 50 za chumvi na nguo mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 1.3/-.

  Madiwani wa Iringa Vijijini walitoa sh. 380,000/-, Wabunge wa Viti Maalum kupitia CCM walitoa vifaa vya sh. Milioni 1.7/-; ofisi ya CCM Mkoa wametoa vifaa vya sh. milioni 6.1/-, Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa,  Bw. Salim Abri aliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Iringa sh. milioni 5/- ili wanunue vyakula vya waliopatwa na maafa.

  Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mbunge wa Isimani, Bw. William Lukuvi alitoa fedha taslim sh. milioni  20/- kati ya hizo sh. milioni  15 zikiwa ni zake na milioni 5/- ni za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Bw. George Simbachawene.  Pia alikabidhi seti 251 za mashuka zenye thamani ya sh. milioni 4/- zikiwa ni mchango kutoka Benki ya CRDB.

  Waziri Lukuvi ambaye alishatoa mabati 250, aliahidi kuongeza mabati mengine 250 (yote yana thamani ya sh. milioni 8), pia alikabidhi sh. milioni 1.5/- kwa diwani wa Mlenge ili ziwasaidie kukodi gari la kukarabati barabara yao ambayo imeharibika sana kutokana na mafuriko hayo. 
  Mapema, akitoa taarifa ya maafa kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi. Amina Masenza alisema jumla ya kaya 82 zilikosa makazi kutokana na mvua zilizonyesha Februari 12 na kusababisha mafuriko. Kabla ya hapo, kaya nyingine 75 zenye wakazi 377ziliathirika kutokana na mvua zilizoanza Februari 3, mwaka huu. 

  Alisema miundombinu ya barabara na ya maji safi iliharibiwa vibaya na kusababisha hasara ya zaidi ya sh, milioni 250/-. Pia wakazi hao walikubwa na uginjwa wa kipindupindu kutokana na mto Mapogoro kufurika na kusomba baadhi ya vyoo vya wakazi hao. “Tangu Februari mosi, wamekkkwishapokea waginjwa wa kipindupinda 351 llakini walioko wodini hivi sasa ni wagonjwa 25 tu,“ alisema Mkuu huyo wa mkoa.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATATU, FEBRUARI 22, 2016.

  0 0

  Wananchi wa Eneo la Tegeta Nyuki Jijini Dar es Salaam wamelilalamikia Shirika la TANESCO kushindwa kutatua Kero ya Nguzo ambayo inahatarisha Maisha ya wakazi Hao katika eneo hilo kwa zaidi ya Miaka 8 hivi sasa, nguzo hiyo imesogelea Kibanda cha Biashara na kusababisha hali ya Sinto fahamu kufuatia usalama wao.

  Uzembe wa Nani?
  Wakizungumza na Mtandao huu wakazi wa Eneo hilo wamedai yakuwa Taarifa walisha peleka katika sehemu husika lakini Hadi leo hii ni mwaka wa Nane Bila ya Mafanikio.

  Uzembe wa Nani?
  Mwaka 2008 wakazi hao waliiandikia Tanesco Barua ya kufanya Marekebisho ya Kuomba Kuondoa Mstimu huo lakini hadi leo Mamlaka hiyo haijafanya hivyo, Ila Mwaka 2015 mwishoni Tanesco ilifika eneo la tukio na kuangalia tu na kuondoka bila ya kufanya Marekebisho yoyote.
  Uzembe wa Nani?
  Je kwa hali hii Tunangojea Maafa au Hasara Itokee Ndio tukimbilie? Tunaiomba Mamlaka Husika Iweze Kuchukua Hatua za Haraka kurekebisha hili kabla ya Maafa hayajaweza Kutokea.

  0 0

   
  1.Ina vyumba 3, kimoja master.
  2. Ipo Tabata Segerea stand hapohapo.
  3. Bei milioni  78 .

  WASILIANA NAMI KATIKA 0658772649 AU 0745216776.
  KUONA  ZAIDI  TEMBELEA baylimited.blogspot.com 

   
  1.Ni  sqm  1200.
  2. Ndani  kuna  kijumba kidogo.
  3. Ni  Dege  Kigamboni  karibu  na  maghorofa  ya mradi.
  4. Bei milioni  25  .
  WASILIANA NAMI KATIKA 0658 772 649 AU 0745 216 776.
   
  KUONA  ZAIDI  TEMBELEA baylimited.blogspot.com

  0 0


  MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA
  TANGAZO KWA UMMA
  MATUMIZI YA MASHINE ZA EFD KATIKA VITUO VYOTE VYA MAFUTA NCHINI:
  Kufuatia Tangazo kwa Umma lilitolewa kwenye vyombo vya Habari na kuchapishwa kwenye Magazeti, Uongozi wa Chama cha Wamiliki na Waendeshaji wa Vituo vya Mafuta Nchini (TAPSOA) ulikutana na Kaimu Kamishna Mkuu na kufanya majadiliano ya msingi kuhusu matumizi ya EFD na kufunga Mashine za EFD Maalum katika vituo vya mafuta kwa ajili ya kutolea risiti za mauzo. Makubaliano ya pamoja kutokana na majadiliano ni kwamba, agizo la Kaimu Kamishna Mkuu liendelee kutekelezwa katika utaratibu ufuatao;
  1. Wamiliki wote wenye vituo vya mafuta walio katika kundi la Makampuni makubwa wanaoagiza mafuta na kutumia Mawakala kusambaza/kuuza mafuta kwa wateja (CODO) wakamilishe kufunga Mashine za EFD katika vituo vyao vyote Nchini kama ilivyokubalika katika kikao hicho (yaani kufikia tarehe 15 Machi 2016).

  1. Wamiliki wote wenye vituo vya mafuta walio katika kundi la Makampuni wanaoagiza mafuta na kusambaza/ kuuza mafuta kwa wateja wao wenyewe (COCO) walioanza na wanaofunga Mashine za EFD kwenye pampu za vituo vyao waendelee kufanya hivyo wakati Mamlaka ya Mapato kwa kushirikiana na Wasambazaji na Uongozi wa TAPSOA wakiendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazojitokeza za kiufundi na gharama ya Mashine za EFD kwa ajili ya pampu husika.

  1. Wamiliki/Waendeshaji wote wenye vituo vya mafuta walio katika kundi la Makampuni ya watu binafsi wanaonunua mafuta kutoka kwa Makampuni mama na kusambaza/kuuza kwa wateja moja kwa moja (DODO) ambao hawajafunga Mashine za EFD kwenye pampu waendelee kutumia Mashine za EFD za kawaida (ETR) wakati changamoto za kiufundi, mtandao na bei za Mashine za EFD zikishughulikiwa.

  Mamlaka ya Mapato kwa kushirikiana na uongozi wa TAPSOA kwa pamoja tutaendelea kuhimiza Matumizi ya Mashine za EFD katika vituo vya mafuta vyote Nchini.
  Ni vyema kila Mfanyabiashara akatambua wajibu wake na kujenga utamaduni wa kutekeleza matakwa ya sheria kwa hiari bila kushurutishwa.

  Pamoja Tunajenga Taifa Letu  KAIMU KAMISHNA MKUU


  0 0


  Bendi maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band,ni bendi ya kwanza ya kiafrika iliyojiwekea nafasi ya pekee katika nyoyo za washabiki huko ughaibuni.


  Bendi hiyo ambayo imetajwa kuwa ndio bendi ya kwanza ya kiafrika kutumia muziki wake kutoka uswahilini kama daraja la kuwafikia washabiki wake  katika kona zote duniani,pia imetajwa na vianzo vya habari vya kimataifa  kuwa  mdundo wa mziki wake umekuwa ni urimbo unao wanasa na kuwatia kiwewe washabiki, popote pale duniani.

  Bendi ya Ngoma Africa band aka FFU yenye maskani yake nchini Ujerumani ilianzishwa mwaka 1993 na mwanzilishi kwake mwanamziki Ebrahim Makunja almaarufu pia kwa majina kama Ras Makunja kamanda wa FFU,Mtawala wa himaya ya Anunnaki Empire "ambaye  pia ndiye mtunzi,mwimbaji na kiongozi wa bendi hiyo,bendi yenye utajili wa wanamziki wenye vipaji baadhi yao wakiwemo mpiga solo gitaa Christian Bakotessa aka Chris-B aka “Mshenzi” wa solo gitaa ambae pia yupo katika safu ya uimbaji,Wengine ni  Matondo Benda,Aj Mbongo na Saidi Jazbo Vuai wapiga bass gitaa ,Jonathan Sousa aka “Jo Jo” (Drum),wapo akina dada FrolaWilliam,Jessica Oyah ,bendi hiyo maarufu ina wanamziki takriban kumi ,bendi hiyo pia imezungukwa na wataalamu .

  Ngoma Africa band ni bendi iliyo pachikwa majina mengi mengi ya utani au usanii kama vile FFU, Mzimu wa Muziki, Wazee wa kukaanga mbuyu, majina ambayo bendi hiyo haiwezi kuyakwepa !  Jina lingine ambalo lilikua gumu kwao kulikubali ni  “Watoto wa Mbwa” bendi hiyo ilibandikwa jina hilo na baadhi ya wadau wa mziki, kuwa nyimbo zao ni sawa  vitisho vya mbwa wanao bwaka katika kila sekta na kugusa nyoyo za walio wengi !

  Ngoma Africa band imefanikiwa kufyatua CD nyingi ambazo nyimbo zilizomo katika santuri hizo zinatawala anga za redio za kimataifa..na kulitangaza kwa kasi kubwa jina la Tanzania kanji ya muziki , baadhi ya nyimbo zao ni pamoja “Rushwa ni adui wa haki” , Album “Mama Kimwaga”,Single CD “Apache wacha Pombe” , CD “Jakaya Kikwete 2010”,CD "Miaka 50 ya uhuru" na CD Bongo Tambarare na Uhuru wa habari, Single CD La Mgambo yenye nyimbo mbili za kumuaga rais JK, juzi kati waliachia singel CD mpya "Mapenzi Mpya" ambazo zote ni Utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja wa FFU,mjeshi wa ambaye kufanya nae kazi inataka uwe na tabia za ki FFU, yaani uwe tayari tayari wakati wowote kwenda kutumbuiza hata ikiwa katika nchi za vita ! Na mdundo anautaka yeye lazima uwe na mwendo wa kasi na magitaa Lazima yalie milio ya kushambulia mashabiki katika ulingo wa dansi, mdundo ambao umepewa jina “Extra Ordinary” Bongo Dance mdundo ambao umefanikiwa kuwateka , kuwanasa na kuwatia kiwewe watu wengi katika kila kona duniani.

  Wasikilize katika  website yao at www.ngoma-africa.com au pia http://www.itunes.apple.com/us/album/mama-kimwaga-sugar-mum/id947329929  ambayo mpenzi au mshabiki anaweza ku log in na kujumuika nao kama mwanachama wa bendi hiyo.

  Ngoma Africa band inaonekana kuwa na mfumo tofauti sana ! Kuwa washabiki wanasauti kubwa ya kuweza kulazimisha maonyesho kuliko uongozi wa bendi !? Mashabiki mara nyingi wamekua tishio hadi kwa maporomota na waandaaji wa maonyesho makubwa ya mziki…kama bendi ya Ngoma Africa haikualikwa au kupangwa katika ratiba ya onyesho
  Fulani basi wapo tayari kususia onyesho hilo…au pengine wakalivunja !

  Tena washabiki  hao wa umri wa lika na mataifa mbali mbali hawaoni wala hawasikii kitu kingine chochote mbele Bongo dansi la Ngoma Africa band aka FFU,ukipenda    waite  “Watoto wa Mbwa” au "Anunaki aliens" viumbe wa ajabu kutoka kutoka special Planet bongo land majina yote size yao !

  Maporomota au waandaaji wa maonyesho mengi ya mziki huko ughaibuni wanalazimika Kuandaa  ulinzi wa kutosha mara tu wanapoialika bendi hiyo   kushiriki katika maonesho yao....hapa ndipo vianzo vingi vya habari vya ndani na nje  ya nchi vinapofika katangaza kuwa FFU wa Ngoma Africa band “jino kwa           jino” au “Jicho kwa Jicho” na washabiki .
   wasikilize katika tovuti yao www.ngoma-africa.com 

  pia unaweza kuwasiliana nao at contact@ngoma-africa.com

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini (kushoto) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (kulia), kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Idara hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni. Wakwanza upande wa kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya, na wakwanza upande wa kushoto ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Victoria Lembeli.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akizungumza jambo katika kikao kazi alichokiitisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) kuzungumza na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara yake, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi ndani ya Idara hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni. Wakwanza upande wa kushoto ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Victoria Lembeli.
   Kaimu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli (wapili upande wa kushoto) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) kuhusu masuala mbalimbali ya kikazi ndani ya Idara yake katika Kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kilichoitishwa na Waziri Kitwanga na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, balozi Simba Yahya.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni (kulia meza kuu) wakifurahi jambo pamoja na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji (kushoto) na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (kulia), wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi ndani ya Idara hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya, na wakwanza upande wa kushoto ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imerejesha  huduma ya upatikanaji wa Maji katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu chini  jijini Dar es salaam, pamoja na maeneo ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na mtambo huo kuzimwa kwa wastani wa saa 36 kuanzia siku ya Alhamisi 18/02/201.

  Akizungumzia kurejea kwa huduma hiyo, Meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amesema kuwa huduma ya Maji katika jiji la Dar es salaam na miji ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa sasa yameanza kwenda kwa wananchi, na maeneo mengi ya jiji ambayo yalikosa huduma ya Maji kutokana na uzimwaji wa mtambo wa Ruvu chini.

  “Napenda kuwaambia wateja wetu kuwa huduma ya Maji kwa sasa imerejea kwenye maeneo mengi ya jiji baada ya matengenezo kukamilika na mtambo kuwashwa siku ya Jumapili saa 9:30 alasiri” alisema Bi. Lyaro.

  Alibainisha kuwa Kuna maeneo mengine yatachelewa kupata Maji kwani mara nyingi kwa kitaalamu huwa mtambo ukizimwa kwa zaidiya saa 24 ndani ya mabomba ya kupitisha Maji hujaa hewa hivyo baadhi ya maeneo kazi ya utoaji hewa kwenye mabomba unaendelea, hivyo tuwahakikishie wananchi kuwa huduma imerejea na wataipata ndani ya muda tuliotarajia.

  Awali, mtambo wa Ruvu Chini ulizimwa ili kuwaruhusu wakandarasi kutoka kampuni ya sino Hydro na mafundi kutoka DAWASCO kukarabati bomba la Maji lenye inchi 54 linalosafirisha Maji kutoka Bagamoyo mpaka matenki ya Chuo kikuu cha ardhi, Bomba lililokuwa likivuja maeneo ya Makongo Jeshini, na kusababisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kukosa huduma ya Maji, Mji wa Bagamoyo vijiji vya Zinga, Kerege na Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach na Kawe.

  Maeneo mengine ni pamoja na Maeneo ya Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City centre, Ilala,, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa Muhimbili, Buguruni, Chang’ombe na Keko.

  0 0

  BARABARA ya Kilwa, kipande cha Mtoni-Kwa Azizi Ali hadi Msikitini, kwa wale wenyeji wanajua maeneo hayo, imekuwa ni kama ile hadithi ya “Mfupa” uliomshinda Fisi.

  Barabara hiyo imekuwa ikifanyiwa ukarabati karibu kila siku jambo la kusikitisha hata pale palipofanyiwa ukarabati napo panaharibika baada ya mudamfupi.

  Ikumbukwe ya kwamba Waziri wa Ujenzi wakati huo, ambaye sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, alikataa kuipkea barabaar hiyo kutokana na kujengwa chini ya kiwango.

  Tanguwakati huo, imekuwa ikifanyiwa marekebisho ya “kisanii” hapa na pale bila ya kukamilika. Pichani leo hii asubuhi Februari 23, 2016, Bwana huyu akielekeza magari katika eneo la ukarabati wa mtaro wa maji taka ambao huo tu peke yake umeshafanyiwa ukarabati zaidi ya mara tatu, chini kidogo ya daraja inakopita reli ya Tazara. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)


  0 0

   Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  MKAZI wa Mafinga,  David Isack ( 32) alivamiwa na majambazi na kuporwa sh.milioni 12 ambazo alikuwa akipeleka katika Benki ya  DTB, ambapo alivamiwa na  watu  watano wanatuhumiwa kuwa ni majambazi wakiwa na usafiri wa pikipiki  mbili aina ya boxer.

  Akizungumza na waandishi wa habari ijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo lilitokea Februari 12 mwaka huu katika eneo la Uwanja Ndege , katika kurupushani za kutaka kuchukua fedha hizo walitokea askari na kuwazingira na kisha kuanza kukimbia na kuweza kudondosha bunduki aina ya SMG pamoja na risasi 24 ambazo zilitakiwa kutumika katika tukio hilo.

  Amesema askari walipowakamata wananchi walikusanyika katika tukio hilo na kuanza kuwapiga watu wanaodaiwa kuwa majambazi mpaka kupoteza maisha kutokana kushambuliwa huko na wengine watatu waliweza kukimbia na kiasi hicho cha fedha.

  Kamishna Sirro amesema Isac alikuwa akitokea benki ya NMB na kwenda kupeleka fedha hizo katika benki ya DTB iliyopo Quality Plaza.

  Katika operesheni nyingine imefanikiwa kukamata bastola moja ambayo ilipatikana  Februari 19 mwaka huu maeneo ya Kiwalani Kwa Gude kutokana na polisi kupata taarifa juu ya watu kujificha katika kichaka kwa ajili ya kufanya uhalifu  na baada ya kugundua polisi wapo eneo hilo walikimbia na kuacha silaha hiyo na jeshi la polisi linafanyia kazi mmiliki wa silaha.

  Hata hivyo Jedhi la Polisi Kanda Maalumu linawashikilia watu wane wanaodaiwa kuwa ni majambazi sugu waliowakamata eneo la  Buguruni kwa Mnyamani ambao ni Mohamed Hassan maarufu kwa jina Kidali (21)Mkazi wa Vingunguti Speco,Hamis Alli (20) Mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani, Adam Salum (23) Mkazi wa Buguruni  kwa Madenge, Bakari Hamis (19) Mkazi wa Buguruni.

  Aidha amesema katika taarifa usalama Barabarani wameweza kukusanya zaidi ya Sh. Bilioni moja ya ni fedha iliyotokana na makosa ya magari kuanzia Januari 02 hadi Februari 22 mwaka huu.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa sukari nchini, ofisini kwake jijini Dar es salaam leo, Februari 23, 2016. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Bango la matangazo la Kampuni ya EFTA LTD ilikiwa kwenye mzunguko wa Mnara wa Mwenge likiwakaribisha kwenye maonyesho ya siku tatu ya mashine na mikopo kama lilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha

  Mahmoud Ahmad Arusha.
  WAJASIAMALI kote nchini wakiwamo pia wakulima na wafugaji nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya mikopo ya vifaa ikiwemo trekta na mashine mbali mbali za kilimo na ufugaji sambamba na vifaa mbali mbali lengo likiwa ni kukuza kipato kwa wananchi.


  Akizungumza na waanahabari meneja mikopo wa kampuni ya Wasambazaji wa vifaa kutoa mikopo kwa wajasiriamali bila dhamana yeyote (EFTA)yenye makao makuu yake Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Peter Temu amesema kuwa wanawakaribisha wananchi kwenye maonyesho hayo ya siku tatu yakatayofanyika mkoani hapa.

  Amesema kuwa kwenye maonyesho hayo zaidi ya wauzaji na wasambazaji wa mashine 25 watakuwa wakionyesha bihdaa na mashine walizonazo kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wananchi watakaoudhuria ili wajue matumizi bora ya mashine aina,mashine halisi,waranti na mabo mengine mbali mbali bila ya kiingilio.

  Alisema kuwa mbali na maonyesho hayo ya EFTA pia wamejianda kuwafanya watembeleaji wa mabanda ya maonyesho hayo kuona na kupata mambo mengi ya ziada ikiwemo kupata semina na mafunzo kwa wajasiriamali toka kwa wataalamu mbali mbali bila malipo.

  “Mafunzo haya yatatolewa bure na wataalamu wenye uzoefu na masuala ya ujasiriamali na kilimo ili wakulima na wajasiriamali wapate faida ya shughili wanazofanya kama kuongeza thamani katika bidhaa wanazozalisha na vifungashio vya kilimo na viwandani”alisema Temu

  Alisema hiyo itakuwa fursa muhimu nay a kipekee kwa watanzania watakaobahatika kufika kwenye viwanja vya makumbusho kwa siku tatu kuanzia Alhamisi hadi yatakapofungwa jumamosi huku wakitarajia wakazi wengi kutoka mikoa ya kaskazini ikiwemo Kilimanjaro,Tanga,Arusha na Manyara kuchangamkia na kufika kukutana na wauzaji na was am,bazaji hawa huku wakijua kuwa EFTA LTD inafanya nn kwa ajili yao katika shughuli nzima ya utoaji wa mikopo bila dhamana na kutoa huduma ya mikopo moja kwa moja kwa wajasiriamali na wakulima wote watakaofika katika maonyesho hayo.

  “Tunaposema mashine za kila Aina tunamaanisha anazohitaji mteja na sio kuwa tunamchagulia mteja,mfano mashine na vifaa vya kilimo,mashine za kufyatulia matofali,mashine za kukamulia alizeti vifaa vya maabara mashine za kutengeneza chakula cha mifugo na kutotolea vifaranga pamoja kilimo cha umwagiliaji na green house na nyingine nyingi’’Alisema Temu

  0 0

   Mshindi wa droo ya pili wa promosheni ya Pasua  Anga na StarTimes, Bw. Johannes Maluli (kulia), akibonyeza kitufe cha kuchezesha droo ya kumpata mshindi wa tatu wa safari ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga. Wakishuhudia katikati ni Balozi wa kampuni hiyo kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda na Meneja Uhusiano wa Umma, Bw. Muddy Kimwery (kushoto).
  Balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda (katikati) akimwonyesha mshindi wa droo iliyopita (ya pili) ya kujishindia safari ya kwenda Ujerumani, Bw. Johannes Maluli (kulia) na waandishi wa habari (hawapo pichani) namna mshindi wa tatu wa promosheni ya Pasua Anga alivyopatikana. Akishuhudia droo hiyo kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo, Bw. Muddy Kimwery.
   Balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda (katikati) akizungumza kwa njia ya simu na mshindi wa tatu wa promosheni ya Pasua Anga ya kujishindia safari ya kwenda Ujerumani. Wakifuatilia kwa makini kulia ni mshindi wa droo iliyopita Bw. Johannes Maluli na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo, Bw. Muddy Kimwery .

  Balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda (kushoto) akimpongeza mshindi wa droo ya tatu, Johannes Maluli. 

  Na Dotto Mwaibale

  Bi Kisa Uswege (41) ambaye ni mfanyabiashara wa mchele mkoani Mbeya amebahatika kuibuka mshindi wa safari ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga katika promosheni iliyochezeshwa na kampuni ya StarTimes mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza kwa njia ya simu Bi. Uswege alisema kuwa amefurahi sana kupata taarifa hiyo kutoka kwa kampuni ya StarTimes kwani hakutarajia kama angebahatika kujipatia fursa hiyo.

  “Ninafuraha sana kupokea taarifa hii ya kuambiwa kuwa mimi ni mshindi wa droo ya bahati nasibu ya tatu ya wateja wanaotakiwa kwenda Ujerumani kushuhudia mechi ‘Live’. Nashukuru sana kwa ushindi huu kwa hakika nitaitumia hiyo fursa kwenda Ulaya kushuhudia mechi hiyo. Mimi ninaishi mkoani Mbeya na ninajishughulisha na shughuli za kuuza mchele, lakini fursa hii pia ninaimani itanifungulia mambo mengine.” Alielezea kwa furaha Bi. Uswege

  “Mimi ni mteja mzuri wa StarTimes na huwa ninajiunga kila mwezi ili kupata chaneli na vipindi ninavyovipendelea. Kila mwezi lazima nilipie ili nifurahie vipindi vyangu au wakati mwingine kwa ajili ya watoto wangu,” alisema na kumalizia Bi. Uswege kuwa, “Kwa mfano huwa naangalia chaneli za mipira, filamu za kihindi na kinaijeria. Watoto wangu wao wanapendelea sana chaneli na vipindi vya Kung Fu, StarTimes Swahili Bollywood na Novela E1. Kwa mfano hapa nyumbani huwa tunapenda sana chaneli ya Star Swahili Bollywood kwani filamu zake zimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na kutufanya tuelewe”

  Naye kwa upande wake Meneja Uhusiano wa kampuni ya StarTimes Tanzania aliongezea kwa kusema kuwa promosheni hiyo ni ya kweli na haina upendeleo wa aina yoyote ndiyo maana washindi wanatoka maeneo mbalimbali zilipo huduma za kampuni hiyo.

  “Wiki iliyopita tulishuhudia mshindi wa droo ya pili akitokea mkoani hapa Dar es Salaam lakini safari hii ni mama kutoka Mbeya. Promosheni hii inafanyika kwa kuhusisha wateja wetu wote nchini ukizingatia atumesambaza huduma zetu takribani mikoa 18 sasa. Ningependa kuwasihi wateja wetu wazidi kulipia vifurushi vya mwezi kwa kuanzia na kiasi cha shilingi 5000/- tu na kuendelea na wengine wajiunge nasi kwani kwa kufanya hivyo watakuwa waeunganishwa na droo hii moja kwa moja.” Alisema Bw. Kimwery

  Kwa kumalizia Meneja Uhusiano huyo wa StarTimes alisema, “Nawataka wateja na watanzania kufuatilia droo hiyo ya bahati nasibu kila mwishoni mwa wiki kwani yeyote anaweza kuwa mshindi. Na pia nawaomba simu zenu ziwe hewani au kupokea pindi mpigiwapo kwani mnaweza kupoteza bahati.”


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Jaap Frederiks Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Uholanzi hapa nchini Jaap Frederiks Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Nchini Burundi Bi Leontine Nzeyimana ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkururinza. Waziri huyo alifika Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo na Rais pamoja na kumueleza hali halisi ya nchini Burundi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Balozi wa Zambia hapa nchini Judith Kangoma Kapijimpanga Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Zambia hapa nchini Judith Kangoma Kapijimpanga Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Zambia hapa nchini Judith Kangoma Kapijimpanga Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi na ukarabati wa barabara za Halmashauri nchini unaotekelezwa kwa ushirikiano na shirika la Maendeleo la Japan ( JICA) mradi unaolenga kuwajengea uwezo wahandisi wa Halmashauri na Mikoa katika kusimamia na kukarabati barabara zilizopo katika maeneo yao kwa kushirikiana na wananchi.
  Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Godwin Mpinzile akieleza kwa waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara na ukarabati katika Halmashauri hiyo unaofadhiliwa na JICA ukilenga kuwashirikisha wananchi katika ujenzi na utunzaji wa barabara hizo ili ziweze kudumu.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe akimpongeza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la maendeleo la Japan (JICA) hapa nchini bw. Nagase Toshio kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Japan hali iliyochangia kufanikiwa miradi ya ujenzi wa barabara katika halmashauri mbalimbali hapa nchini inayofadhiliwa na shirika hilo.
  Muwakilishi Mkazi wa Shirika la maendeleo la Japan (JICA) bw. Nagase Toshio akifafanua kuhusu ushirikiano mzuri uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Japan katika kutekeleza mradi huo unaolenga kujenga uwezo kwa wahandisi wa Halmashauri hapa nchini ili waweze kuwashirikisha wananchi katika miradi ya barabara inayotekelezwa ili waweze kujiletea maendeleo .
  Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa bw. leopold Runji akitoa ushuhuda wa namna halmashauri hiyo ilivyonufaika na mradi wa ujenzi na ukarabati wa barabara unaotekelezwa katika halmashauri hiyo kwa ufadhili wa shirika la JICA.(Picha zote na frank Mvungi-Maelezo).

  ………………………

  Frank Mvungi-MAELEZO

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Mussa Iyombe amewataka wananchi kutunza barabara zinazojengwa na Serikali kwa kushirikiana na wafadhili katika Halmashauri zote hapa nchini.

  Akizungumza leo Jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kupokea ripoti ya utekelezaji wa mradi wa Ujenzi na ukarabati wa barabara za halmashauri nchini Iyombi amebainisha kuwa mradi huo umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) .

  “Mradi huu unatekelezwa katika Halmashauri za Iringa,Mufindi,Chamwino na Kondoa” alisisitiza Iyombe.

  Akifafanunua kuhusu utekelezaji wa mradi huo Iyombe amebainisha kuwa unadhamiria kujenga uwezo kwa wahandisi wa Mikoa na Halmashauri hapa nchini ili waweze kushirikiana na wananchi katika kujenga na kulinda miundo mbinu hiyo kwa maslahi ya Taifa.

  Aidha Iyombi amewata wakurugenzi wa Halmashauri ambazo mradi huo unatekelezwa kutunza barabara hizo ili zilete matokeo yaliyokusudiwa.

  Akizungumzia ushirikiano mzuri uliopo kati ya Japan na Tanzania Iyombe amesema kuwa maeneo ambayo Tanzania imekuwa ikipata ufadhili kutoka Japan ni Sekta ya Kilimo,Viwanda,Uimarishaji wa Utawala bora.

  Kwa upande wake mwakilishi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) bw. Nagase Toshio amesema kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

  Mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa barabara katika Halmashauri hapa nchini unatekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza imekamilika katika Halmashauri za Chamwino na Iringa na awamu ya pili imekamilika katika Halmashauri za Kondoa na Mufindi ambazo ripoti ya utekelezaji wake iliwasilishwa leo katika mkutano wa siku moja ulifanyika Jijini Dar es salaam ukilenga kufanya tathmini ya utekelezaji kabla ya kuanza kwa awamu ya tatu.

  0 0

  Na Nyakongo Manyama MAELEZO

  Dar es Salaam

  HALMASHAURI Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam katika mwaka kipindi cha 2016/17 imepanga kununua magari 40 yatakayotumika kwa ajili ya zoezi la ukusanyaji wa taka ngumu katika Kata na Mitaa ya Halmashauri hiyo.

  Hatua inaelezwa itasaidia kuondoa kero ya mlindukano wa taka ngumu ambazo huzagaa ovyo, kutokana na hushindwa kukusanywa kwa wakati na makampuni ya wakandarasi wa usafi katika Kata na Mitaa wa Halmashauri hiyo.

  Akizungumza na MAELEZO leo (Jumanne Februari 23, 2016), Afisa Habari wa Halmashauri hiyo Sebastian Mhowera alisema tayari ofisi hiyo pamoja na Halmashauri za Wilaya ya Ilala na Temeke zimewasilisha ombi maalum la kuomba kibali cha ununuzi wa magari hayo katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  Kwa mujibu wa Mhowera alisema Halmashauri hiyo huzalisha jumla tani 2020 za taka ngumu ambapo uwezo uliopo ni kuteketeza tani 1300 kwa siku, na hivyo kiasi kinachobaki huibua changamoto katika namna ya kukabiliana na ongezeko hilo.

  “Kiasi kikubwa cha taka zinazozalishwa nyingi hubakia mitaani na hazifiki barabarani ambapo ndipo hukusanywa kwa ajili ya kupelekwa dampo, kwani vitendea kazi katika maeneo hayo ni changamoto” alisema Mhowera.

  Alisema kwa mujibu wa Sera ya Usafi, Makampuni ya Wakandarasi wa Usafi yaliyopo katika Mitaa yana wajibu wa kukusanya taka zote kwani husimamiwa na wananchi wenyewe, ambapo hata hivyo makandarasi mengi yamekuwa hayana uwezo wa kufanya kazi hiyo.

  Aidha Mhowera alisema katika kufanikisha zoezi la usafi wa mazingira linalofanyika kila mwisho wa mwezi nchini, Halamshauri hiyo imetoa maelezo mbalimbali ya kiutendaji kwa Maaafisa Watendaji wa Mitaa na Kata.

  0 0

  Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi akielekeza jinsi ya kupiga simu wakati akiendesha mafunzo hayo kwa wakulima.
  Wakulima wakiwa kwenye mafunzo.

  Shamba la muhogo lililoshambuliwa na ugonjwa wa batobato lililopo jirani na jengo la Halmshauri ya Rorya ambapo wapo wataalamu wa kilimo.
  Mtafiti Kiongozi Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (katikati), akizungumza na wakulima wa Wilaya ya Rorya Mkoani Mara katika mafunzo ya siku moja kwa wakulima hao ya kutumia simu kupashana habari za kilimo na kujua changamoto zinazo wakabili. Kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel Otunge na kushoto ni Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney.
  Maofisa Ugani wa Wilaya ya Rorya wakiwa kwenye mafunzo hayo.
  Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Rorya, Dominick Ndentabura akizungumza na wakulima hao kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
  Wakulima wa Rorya wakiwa kwenye mafunzo hayo.
  Mkulima Sophia Charles kutoka Kijiji cha Roche akizungumzia changamoto ya ukosefu wa soko la zao la mhogo ambapo wanategemea zaidi soko nchini Kenya.

  Mkulima Charles Ruola akizungumzia changamoto ya kilimo cha mahindi.
  Mkulima wa Kijiji cha Kowaki kilichopo Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Elias Kaseno akizungumzia changamoto ya kilimo cha muhogo na mahindi mbele ya watafiti kutoka Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB) na Watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), waliopo wilayani humo jana kujua changamoto mbalimbali za wakulima na kutoa mafunzo ya matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo.
  Wakulima wakiwa mafunzo hayo.
  Wakulima wakiwa kwenye mafunzo hayo.
  Jengo la Halmshauri ya Wilaya ya Rorya.
  …………………………………………………………………………………
  Na Dotto Mwaibale
  KATIKA hali isiyotegemewa shamba lenye ukubwa wa ekari moja la zao la muhogo lililopo nyuma ya Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara ambapo ofisi ya wilaya ya kilimo ipo halipo katika matunzo ya kilaalamu ambapo mwandishi wa habari hii ambaye yupo katika ziara ya kilimo na watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) alitembelea.   Mwandishi wa habari hii alidhani kuwa shamba hilo la muhogo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia wakulima kuhusu ugonjwa unaoshambulia zao hilo ujulikanao kama batobato na athari zake kumbe ni shamba la mkulima ambalo limekosa huduma za ugani licha ya maofisa ugani kuwepo mita chache ya eneo hilo.


  Kutokana na hali hiyo inapaswa wakulima wa namna hiyo kupata huduma za kilimo kutoka maeneo mengine kutokana na maofisa ugani hao kushindwa kutoa elimu ambapo shamba hilo limekuwa ni chanzo cha kueneza ugonjwa huo katika maeneo mengine.


  Akizungumza katika mafunzo ya matumizi ya simu katika kilimo kwa wakulima wa wilaya ya Rorya Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi alisema mafunzo hayo ya siku moja yatawasaidia wakulima kupashana habari za kilimo na changamoto zao.


  “OFAB imeleta mafunzo haya kwa wakulima ambao ni wadau wetu ili waweze kupashana habari za kilimo, changamoto zinazo wakabili na kutafuta masoko ya mazao yao kwa njia ya simu badala ya kutumia simu hizo kupigiana kwa mambo ya kawaida” alisema Nyinondi.
  Alisema kupitia mafunzo hayo wakulima hao wataweza kushirikiana na mitandao mingine ya kijamii ili kutatua changamoto zao za kilimo zikiwemo za wadudu waharibifu wa mazao, ukame na nyinginezo.
  Alisema washiriki wa mafunzo hayo walikuwa ni 20 kutoka katika wilaya hiyo na kuwa shirikisha wataalamu wa kilimo.

  0 0  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  Description: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
  Simu: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425


  OFISI YA RAIS,
       IKULU,
  1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Rais wa Jamhuri ya Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunziza amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa hali ya Burundi ni shwari na kwamba tangu jana (Februari 22, 2016) nchi hiyo imepokea ugeni mkubwa wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki-moon na inatarajia kupokea marais watano kutoka nchi za Umoja wa Afrika tarehe 25 Februari, 2016.
  Ujumbe wa Rais Nkurunziza umewasilishwa na Mjumbe maalum ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi, Mheshimiwa Leontina Nzeyimana leo tarehe 23 Februari, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, alipokutana na Rais Magufuli na kufanya nae Mazungumzo.
  Pamoja na kumpa taarifa kuwa Burundi inaendelea vizuri, Mheshimiwa Nzeyimana pia amemueleza Rais Magufuli kuwa Burundi ipo tayari kupokea nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kwa Rwanda, ikiwa ni kwa mujibu wa Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaoelekeza kuwa  nchi inayofuata kutoa Katibu Mkuu baada ya Katibu Mkuu wa sasa kumaliza muda wake, ni Burundi.
  Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na kufanya Mazungumzo na Mabalozi watatu wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
  Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mheshimiwa Jaap Frederiks, amewasilisha salamu za Mfalme wa Uholanzi Mtukufu Willem-Alexander ambaye amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa alizoonesha katika mwanzo wa utawala wake, katika kusimamia Uadilifu serikalini na katika biashara na pia kuisaidia Mahakama. Amesema Uholanzi inaamini kuwa maeneo hayo ndio yamekuwa yakileta vikwazo vya maendeleo, biashara na uwekezaji.
  Balozi Jaap Frederiks amemhakikishia Rais Magufuli kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maendeleo kama ilivyofanya katika miaka 45 iliyopita, huku akitaja baadhi ya maeneo ya ushirikiano kuwa ni Kilimo na Nishati.
  Balozi wa India hapa nchini Mheshimiwa Sandeep Arya, amewasilisha salamu za Waziri Mkuu wa India Mheshimiwa Narendra Modi, ambaye pamoja na kuitaja Tanzania kuwa lango muhimu katika mpango wake wa ushirikiano na Afrika, amemhakikishia kuwa India itaendeleza uhusiano wake na Tanzania hususani katika biashara na uwekezaji ikiwemo kuunga mkono mpango wa ujenzi wa viwanda Tanzania.
  Nae Balozi wa Zambia hapa nchini Mheshimiwa Judith Kangoma Kapijimpanga ameelezea matumaini makubwa ya kuendelezwa kwa ushirikiano na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Zambia na amemuomba Rais Magufuli aimarishe maeneo kadhaa ya kiushirikiano yakiwemo Reli ya TAZARA, Bomba la Mafuta la TAZAMA na taratibu za usafirishaji wa Mizigo katika bandari ya Dar es salaam na Mpaka wa Tanzania na Zambia.
  Kwa upande wake Rais Magufuli amewahakikishia mabalozi hawa kuwa serikali yake ya awamu ya tano itaendeleza na kuimarisha zaidi mahusiano kati ya Tanzania na nchi hizo na kwamba atafurahi kuona mahusiano na ushirikiano huo unaleta manufaa kwa wananchi.
  Baadhi ya maeneo ambayo amezialika nchi hizo kuongeza ushirikiano na Tanzania ni katika ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge" kuwekeza katika viwanda vya kusindika mazao na kuzalisha bidhaa mbalimbali, Elimu na Afya.
  Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya Mazungumzo na Jaji Mkuu wa Mahakama hapa nchini, Mheshimiwa Mohamed Chande Othman, Ikulu Jijini Dar es salaam.

  Imetolewa;
  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  23 Februari, 2016  


  0 0

  Balozi wa Zambia  nchini Mhe Judith Kangoma-kapijimpanga akimsalimia kwa unyenyekevu wa wanawake wa Kiafrika Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam  Jumanne February 23, 2016

older | 1 | .... | 773 | 774 | (Page 775) | 776 | 777 | .... | 1897 | newer