Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

WANAHABARI, WATAFITI KUTOKA COSTECH WAZURU KABURI LA BABA WA TAIFA BUTIAMA MKOANI MARA

$
0
0
Wanahabari na Watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), waliokuwa katika ziara ya kuzungumza na wakulima wa mkoa wa Mwanza kuhusu changamoto za kulimo zinazo wakabili pamoja na matumizi ya bioteknolojia katika kilimo wakiwa mbele ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere walipozuru kaburi hilo hivi karibuni Kijiji cha Mwitongo Butiama mkoani Mara.
Watafiti na wanahabari hao wakiwa mbele ya makaburi ya wazazi wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknnolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (kushoto), na Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney wakiwa wamesimama ilipo sanamu ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Hapa ni picha ya pamoja katika sanamu ya Baba wa Taifa.
Mwendeshaji wa mtandao wa www. habari za jamii.com Dotto Mwaibale akivinjari katika moja ya jengo katika makazi ya Baba wa Taifa.
Matembezi yakiendelea katika makazi ya Baba wa Taifa.
Mratibu Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika, Daniel Otunge (kushoto) Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknnolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (katikati), na Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney wakiwa wamekaa katika kibanda alichokuwa akipenda kupumzika Hayati Nyerere wakati wa 
uhai wake.
Jamii inayofanya shughuli mbalimbali nyumbani kwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakionesha upendo kwa kunywa chai pamoja katika makazi ya Mwalimu Nyerere yaliyopo Kijiji cha Mwitongo, wilayani  Butiama mkoani Mara kama walivyonaswa na kamera yetu katika ziara hiyo.
Picha ya pamoja katika nyumba maalumu lilipo kaburi na Mwalimu Nyerere.
Dereva wa Msafara huo, Mr Stanley akiwa mbele ya gari na mtafiti Kutoka Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru cha jijini Mwanza, Isabela Msuya.
Mwendeshaji wa mtandao wa www. habari za jamii.com Dotto Mwaibale akiweka maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa.

MWENYEKITI WA CCM, RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AZINDUA RASMI JENGO LA OFISI YA CCM WILAYA YA KIBAHA MJINI MKOA WA PWANI

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete azindua rasmi jengo la Ofisi ya CCM, Wilaya ya Kibaha Mjini mkoa wa Pwani jana. Jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa fedha za familia ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Slyvester Koka (kulia).
Mbunge wa Kibaha Mjini Slyvester Koka akieleza kuhusu mradi wa ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha mjini mjini mkoa wa Pwani, kabla ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kuzindua jengo hilo




Viongozi wa CCM, Wilaya ya Kibaha mjini wakimkabidhi zawadi ya picha yake ya kuchorwa, Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, kabla ya kutoa vyeti kwa wana CCM mbalimbali walioshiriki kwa namna moja au nyingine kuimarisha Chama..



Zifuatazo ni mfululizo wa taswira mbalimbali alivyokuwa akionekana Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipohutubia wana CCM na wananchi kwa jumla baada ya kufungua Ofisi hiyo ya CCM Wilaya ya Kibaha mjini.


Kikwete alisisitiza umuhimu wa kuchukuliwa hatua waliookisaliti chama wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, lakini akaonya hatua kuchukuliwa kwa uangalifu ili wasije wakachukuliwa hatua kwa kupakaziwa wanachama au viongozi ambao kwa kuonekana ni wanaonekana tu kuwa kkwazo kwa wenaotaka nafasi katika uchaguzi ujao.

   Pia Mwekyekiti aliwataka WanaCCM kuzingatia ujenzi wa Uhai wa Chama kwa kuingiza wanachama wapya, kufanya vikao na pia kufanya maamuzi kwa busara.

  Aidha Kikwete akikana kuhusika kwa namna yoyote kutoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha, kuufuta uchaguzi uliopita. TAFADHALI>BOFYA HAPA

MKAZI WA MAFINGA APORWA NA WANAODAIWA MAJAMBAZI SH.MILIONI 12 DAR , WAWILI WAPOTEZA MAISHA

$
0
0
  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
 
MKAZI wa Mafinga,  David Isack ( 32) alivamiwa na majambazi na kuporwa sh.milioni 12 ambazo alikuwa akitaka kupeleka fedha hizo katika Benki ya  DTB na kuvamiwa na watu watano wanaotuhumiwa kuwa na majambazi wakiwa na usafiri wa pikipiki  mbili aina ya boxer.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo lilitokea Februari 12 mwaka huu katika eneo la uwanja , katika kurupushani za kutaka kuchukua fedha hizo walitokea askari na kuwazingira na kisha kuanza kukimbia na kuweza kudondosha bunduki aina ya SMG pamoja na risasi 24 ambazo zilitakiwa kutumika katika tukio hilo.
 
Amesema askari walipowakamata wananchi walikusanyika katika tukio hilo na kuanza kuwapiga watu wanaodaiwa kuwa majambazi mpaka kupoteza maisha kutokana kushambuliwa huko na wengine watatu waliweza kukimbia na kiasi hicho cha fedha .
 
Kamishina Sirro amesema Isac alikuwa akitokea benki ya NMB na kwenda kupeleka fedha hizo katika benki ya DTB iliyopo Quality Plaza.
 
Katika operesheni nyingine imefanikiwa kukamata bastola moja ambayo ilipatikana  Februari 19 mwaka huu maeneo ya Kiwalani Kwa Gude kutokana na polisi kupata taarifa juu ya watu kujificha katika kichaka kwa ajili ya kufanya uhalifu  na baada ya kugundua polisi wapo eneo hilo walikimbia na kuacha silaha hiyo na jeshi la polisi linafanyia kazi mmiliki wa silaha.
 
Hata hivyo Jedhi la Polisi Kanda Maalumu linawashikilia watu wane wanaodaiwa kuwa ni majambazi sugu waliowakamata eneo la  Buguruni kwa Mnyamani ambao ni Mohamed Hassan maarufu kwa jina Kidali (21)Mkazi wa Vingunguti Speco,Hamis Alli (20) Mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani, Adam Salum (23) Mkazi wa Buguruni  kwa Madenge, Bakari Hamis (19) Mkazi wa Buguruni.
 
Aidha amesema katika taarifa usalama Barabarani wameweza kukusanya zaidi ya Sh. Bilioni moja ya ni fedha iliyotokana na makosa ya magari kuanzia Januari 02 hadi Februari 22 mwaka huu.

BIBI ABIOLA DELUPE MWAKILISHI WA UBALOZI WA NIGERIA AITEMBELEA EFM

$
0
0
Mwakilishi wa ubalozi wa Nigeria, bibi Abiola Delupe aitembelea Efm Radio leo  katika vitengo tofauti na  kuona utendaji kazi wa radio. Huku akikutana na baadhi ya watangaziji  kujadili mambo tofauti tofauti na jinsi watakavyo weza kuendeleza kazi zoa nje ya mipaka ya Tanzania.
  Meneja mkuu Dennis Ssebbo akijadili mambo tofauti kuhusiana na ufanisi wa kazi katika radio hiyo.
Bibi Abiola Delupe (Kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi  wa Efm radio Francis Ciza. 
Baadhi ya viogozi wa Efm Radio katika mazungumzo na Bibi Abiola Delupe.
 Bibi Abiola Delupe akizungumza jambo na Mkurugenzi  wa Efm radio Francis Ciza.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA MABALOZI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Mhe. Alvaro Rodriguez kabla ya mazungumzo yao Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 23, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 23, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Yosemin Eralp kabla ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 23, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 23, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Switzerland nchini, Mhe. Florence Tinguely Mattli, Ofisini kwake Mkuu jijini Dar es salaam Februari 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MGAMBO WASIO WAADILIFU KUSHUGHULIKIWA.

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Kutokana na tabia ya baadhi ya mgambo katika Halmashauri za Jijini la Dar es Salaam kujipatia fedha kwa njia zisizo za halali, serikali kupitia Halmashauri zake imejipanga kuwachukulia hatua za kisheria migambo wote watakaobainika kujishirikisha na vitendo vya rushwa.

Akitoa ufafanuzi juu ya madai ya wanachi juu ya mgambo wanaochukua rushwa nje ya faini halali zinazistahili kutozwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Ilala, Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala Tabu Shabibu amesema kuwa zipo baadhi ya taarifa wamepewa na watawachukulia hatua kwa kuwasitishia mikataba wale wote watakaobainika kukiuka sheria na taratibu za kazi.

“ Wapo mgambo ambao watumia vitambulisho feki na kufanya vitendo vya rushwa bado hatujawakamata ila hatutawafumbia macho tutawachukulia hatua kali za kisheria kwa yoyote atakayekamatwa akipokea rushwa na hata wale watakaotoa rushwa”

“Napenda kuwaasa watanzania kuacha kuwapa fedha mgambo ili kukwepa kulipa faini halali hivyo basi nawaasa watu kutii Sheria bila shuruti kama umefanya kosa kwa mujibu wa Sheria lipa faini kwa mujibu wa Sheria lipa faini halali ili tuondoe vitendo vya rushwa na kuiongezea mapato Serikali ”Alisema Tabu.

Afisa Tabu amewaomba watanzania kutoa taarifa za mgambo wote wanaopokea rushwa na kusisitiza kuwa tabia hii inayoendelea ikome mara moja na mgambo wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa watasitishiwa mikataba yao ya kazi kwa kukiuka maadili ya kazi zao

Mgambo katika Jiji la Dar es Salaam wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuchukua rushwa kuanzia shilingi 5,000/= mpaka 10,000/= badala ya kutoza faini ya shilling 50,000/= inayostahili kutoza kwa wale wanaokiuka kanuni na taratibu za afya na mazingira katika Halmashauri mbalimbali.

Katika kupambana na suala la mgambo wasio waadilifu,Halmashauri zimejipanga kuwaajiri vijana walipitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliopata mafunzo yenye yenye kujenga uadili na uwajibikaji katika kazi ili kudhibiti suala la mmomonyoko wa maadili na utendaji kazi mbovu wa mgambo katika Halmashauri mbalimbali.

Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaendelea na Vikao kazi kwa Njia ya Video (Video Conference).

$
0
0
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Laurean Ndumbaro (picha ndogo kulia) akiongoza kikao kazi kwa njia ya video kilichohusisha Ofisi ya Rais-Utumishi,Ofisi ya Rais- TAMISEMI,Wizara ya Fedha,Wizara ya Viwanda, Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na ofisi za Sekretarieti za mikoa ya Iringa, Pwani, Mtwara, Dar es Salaam, Kagera,Kigoma.
 Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Ushauri na Uchambuzi Kazi Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi.Sakina Mwinyimkuu (kushoto) akiwasilisha mada kuhusu Uimarishaji wa Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini Serikalini kwenye kikao kazi kwa njia ya video kilichofanyika ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA).
 Washiriki wa kikao kazi kwa njia ya video wakimsikiliza mtoa mada.

CHF Mkombozi wa kweli kwa afya ya Jamii

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Ni jambo lisilopingika kokote duniani kuwa afya   bora ndio chanzo cha maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla.

Afya ikiwa bora binadamu anakuwa na uwezo wa kuwaza na kufanya mambo mbalimbali yenye tija kwake na kwa taifa lake.

Kwa kuonyesha kujali afya zetu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ilianzisha Mfuko wa Afya ya Jamii  ujulikanao kama CHF ambao ulianza kwa majaribio wilayani Igunga, Mkoa wa Tabora mwaka 1996 na kuanza rasmi 2001 baada ya bunge kupitisha muswada huo.

Chimbuko hasa la kuanzisha Mfuko wa Afya ya Jamii ni kupungua kwa rasilimali na vyanzo vya mapato vya kuhudumia sekta ya afya hivyo kusababisha kudorora kwa huduma hiyo ambapo inasababisha wananchi kutopata matibabu yanayotakiwa na wengine kuacha kabisa kwenda kupata huduma katika vituo vya afya kwa kuwa gharama za matibabu ni kubwa.

Mfuko wa Afya ya Jamii yaani CHF ni utaratibu wa hiari unaomuwezesha mtu binafsi,vikundi au kaya kupata huduma za matibabu kwa mwaka mzima kwa kuchangia kiasi cha shilingi 5000 hadi 20000 kwa kadri ya  uwezo wa mtu au jamii yenyewe kulingana na Halmashauri husika itakavyoamua.
 
Kiasi hiki cha kuchangia kwa mwaka kinaweza kupatikana hata kwa mtu mwenye kipato cha chini kwakua kiwango hiki ni sawa na bei ya kuku mmoja, uchangiaji huu ndiyo uliyomfanya aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe. Yahaya Nawanda kuja na kauli mbiu isemayo “Kuku mmoja, matibabu mwaka mzima”. Uhamasishaji huu ulisaidia sana watu wengi kujiunga na CHF katika wilaya hiyo.
 
Na kama iliwezekana katika Halmashauri ya Iramba kwa kuku mmoja kugharamia matibabu ya kaya kwa mwaka mzima, tunaamini kuwa kauli mbiu hiyo inaweza kufanya kazi pia katika Halmashauri nyingine iwapo kila kiongozi aliyekabidhiwa dhamana ya kusimamia maisha ya watu atadhamiria kuwapa wananchi huduma bora za matibabu kwa utaratibu wa kuchangia kabla ya kuugua.

Mfuko huu unatoa huduma za matibabu kwa jamii ambazo hazipo katika sekta isiyo rasmi wilayani, tarafani na katika kata na vijiji. Mtu akijiunga katika mfuko huu na kutoa fedha atahudumiwa yeye na kaya yake au familia kwa mwaka mzima bila ya nyongeza ya malipo ya ziada kwa huduma zilizopo katika eneo husika.

Uchangiaji wa CHF kwa ngazi ya kaya unajumuisha familia ambayo ni baba, mama na watoto wanne wasiozidi miaka kumi na nane.
 
Lengo hasa la kuanzisha Mfuko huu ni kunufaisha nchi nzima kwa huduma zote za afya ya msingi za kinga na tiba zitolewazo katika zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya kama vile:Huduma ya wagonjwa wa kutwa na kulazwa, vipimo vya maabara, huduma ya upasuaji kulingana na utaratibu uliowekwa na Halmashauri husika, wanachama wanapata huduma bora ya afya mwaka mzima pia Halmashauri zinazoendesha mifuko hii zinapata malipo toka Serikalini.
 
Ni agizo la Serikali kuwa asilimia 67 ya makusanyo ya michango na fedha zinazochangwa na Serikali yaani Tele kwa Tele zitumike kwa kununulia dawa ili kuhakikisha kuwa kila mwanachama anapata dawa wakati wote.

Idadi ya wanufaika wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) umeongezeka kwa kiasi kikubwa ambapo hadi Desemba 2015 idadi ya wananchi ilikua 6,677,241 ambayo ni sawa na  asilimia 15.3 ya watanzania wote.

Kuongezeka kwa idadi hiyo kunaashiria mabadiliko chanya yanayofanywa na CHF kwa kutekeleza matakwa ya wananchi yakiwemo ya kupunguza gharama za matibabu na kuboresha huduma za afya katika Halmashauri mbali mbali.

Jumla ya Halmashauri 144 zimejiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii na kwa mwaka huu wa 2016,Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unategemea kutoa elimu na kuhamasisha Halmashauri 54 kujiunga na CHF.

Kwa upande wa vifaa tiba, CHF imefanikiwa kusajili jumla ya maduka 560 ya kuuza dawa  yaliyofunguliwa katika halmashauri mbali mbali nchini ambayo kwa kiasi kikubwa imeondoa adha ya ukosefu wa dawa hivyo kupunguza sana idadi ya vifo kwa wananchi hasa waishio vijijini.

Fedha zinazopatikana kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii hazitumiki kwa manufaa ya wachache bali  zinatumika kwa kuboresha huduma za afya na kuhakikisha upatikanaji wa  dawa na vifaa tiba muhimu,uboreshaji wa miundo mbinu ya afya, kutoa ajira za muda panapokuwa na upungufu wa wataalamu wa kutoa huduma hizo, kusaidia ukarabati na ulinzi wa vituo vya afya.

Kila kituo cha matibabu kina Kamati ya Afya inayosimamia huduma za matibabu siku hadi siku na kuhakikisha kuwa dawa, vifaa tiba na mazingira ya kutolea huduma viko katika hali nzuri wakati wote.

Pia zimeundwa Kamati za usimamizi wa afya zilizo chini ya uongozi wa Halmashauri zinazofanya kazi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuwezesha kufanyika kwa vikao vya kisheria vinavyosimamia makusanyo na matumizi ya fedha za CHF.
 
Suala la Wananchi kujiunga na CHF liwe ni ajenda ya kudumu kwenye vikao vyote vya maamuzi  na kila kiongozi wa watu atolee taarifa ya utekelezaji wa mikakati hiyo ili lengo la kuwaondoa wananchi katika umaskini wa kukosa fedha za matibabu uishe kwa kuwa  CHF ndio mkombozi wa matibabu.

Ni wajibu wa kila mwananchi kuilinda afya yake ili iwe bora siku zote na hali ya afya inapobadilika mwananchi anapaswa kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya haraka ili kufanyiwa vipimo na kupewa dawa sahihi.

Ili kuepukana na kushindwa kumudu gharama za matibabu, kila mwananchi anashauriwa kujiunga na mifuko hii ya afya  ambayo itamsaidia kutibiwa kwa gharama nafuu tofauti na gharama za matibabu atakazojigharamia mtu ambaye hajajiunga na mifuko ya afya.

Mfuko wa afya ya jamii wa CHF ukitumiwa vizuri na wananchi hasa wale wa vijijini utakuwa ni chachu ya maendeleo na ni mkombozi wa kweli kwa sababu fedha nyingi zilizokua zikitumika kwa ajili ya kugharamia matibabu sasa zinaweza kufanya shughuli nyingine za kujenga Taifa. Hii inadhihirika katika usemi usemao, Taifa lenye watu wenye afya njema ni taifa lenye uchumi imara.
 

Jengo la posta lateketea kwa moto

$
0
0
JENGO Posta lililopo katika eneo la sabasaba katika Manispaa ya Dodoma jana limeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa.

Akizungumzia kutekeleza kwa jengo hilo Meneja wa Posta Mkoa wa Dodoma, Magreth Mlyomi alisema mpaka sasa kuna hasara kubwa kutokana na kutekeleza jengo hilo sambamba na vifaa vyote vya ofisi.Mlyomi alisema licha ya kuwa hakuna mfanyakazi hata mmoja aliyepoteza maisha katika jengo hilo lakini mpaka sasa kuna vitendea kazi vingi vya ofisi pamoja na mizigo ya wateja imeteketea.

“Kuna mizigo mingi pamoja na vifaa vya kazi vyote vimeteketezwa na moto na kwa taarifa nilizopata kulikuwa na mizigo ya watu, inaonesha kuwa chanzo cha moto ni umeme,” alieleza Meneja huyo.Akizungumzia kuhusu masuala ya miundombinu ya maeneo husika alisema ni mibovu na kutokana na changamoto hiyo suala hilo lipo katika mamlaka husika ya manispaa.

Kwa upande wake katibu wa wafanyabiashara katika soko la Sabasaba katika Manispaa ya Dodoma, Gergod Lugusi alisema jana saa nne asubuhi kulitokea moto mkali ambao uliunguza jengo hilo.


Alisema chanzo cha moto huo inasemakana kuwa ni tatizo la umeme na uongozi ulilazimika kutoa taarifa katika kikosi cha zima moto na bila kuchelewa walifika kwa wakati.Hata hivyo alisema licha ya kufika kwa wakati katika tukio bado kikosi hicho kilikutana na kikwazo kwa kutokana na miundombinu kuwa mibovu na migumu kupitika

MBUNGE WA ISMANI WILIAM LUKUVI ATOA MSAADA WA FEDHA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO IDODI

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi (kulia) akimpa maelekezo mwenyekiti wa kijiji cha Mapogolo baada ya kumkabidhi fedha kiasi cha Tsh milioni 2 za kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi watakaohamishiwa makazi mapya kutoka kitongoji cha Kitanewa Idodi ambao nyumba zao zilisombwa na mafuriko .
 
MKazi wa kitanewa Idodi akimpongeza mbunge wake Lukuvi kwa kuwajali wananchi 
 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela Katikati na kamati yake ya Ulinzi na usalama wakitazama daraja la Iringa -kuelekea hifadhi ya Ruaha ambalo awali lilikuwa halipitiki baada ya kusombwa na mafuriko na sasa linapitika

Wananchi wanaotakiwa kuhamishwa kwenda makazi mapya baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko wakimsikiliza kwa makini mbunge wao Lukuvi .


Na MatukiodaimaBlog 

MBUNGE wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi amewapa pole waathirika wa mafuriko wa kata ya Mapogolo tarafa ya Idodi wilaya ya Iringa mkoani Iringa kwa kuwakabidhi msaada wa pesa zaidi ya Tsh milioni 9 kwa ajili ya kusaidia mahitaji mbali mbali ikiwa ni pamoja na kurejesha miundo mbinu ya maji safi iliyoharibiwa na mafuriko.

Bw Lukuvi ambae pia ni waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi alikabidhi msaada huo jana baada ya kutembelea waathirika hao waliopo kambi ya Kitanewa pamoja na kutembelea eneo la barabara ya kutoka Iringa kuelekea hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo kwa sasa imekarabatiwa baada ya awali barabara hiyo kukatika kutokana na mafuriko hayo , alisema kuwa lengo lake kama mbunge wa jimbo hilo la Isimani na serikali ni kuona wananchi waliokumbwa na mafuriko wanaendelea kusaidiwa . 

Alisema kuwa awali aliomba msaada wa mahindi tani 100 kutoka serikali kwa ajili ya waathirika hao  wa mafuriko Idodi na Pawaga ikiwa ni pamoja na kuwasaidia msaada wa fedha kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 3 kwa ajili ya kuwawezesha waathirika hao wa mafuriko kupata mahitaji mengine kama mboga na pesa ya kusagia mahindi hayo . 

Bw Lukuvi alisema kuwa kwa ajili ya kurejesha huduma ya maji kijijini hapo amewasaidia kiasi cha Tsh miliobni 4 ambazo wameomba kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu hiyo ,pia kiasi cha Tsh milioni 2 kwa ajili ya kukiwezesha kijiji kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi waliotoa ardhi yao kwa ajili ya wakazi wa kitongoji cha Kitanewa ambao wanapaswa kuhamishwa eneo hilo la mafuriko la kupewa makazi mapya.

" Waambieni watu wenye mashamba ambayo yatachukuliwa kwa ajili ya viwanja mwaka huu wavune mazao yao na baada ya hapo kila mmoja muweze kumlipa fidia ya Tsh 200,000 na baada ya hapo waitini wataalamu wa ardhi ili waweze kupima viwanja na mpanfgilio mzuri zaidi kwa ajili ya makazi mapya,pia nataka hata mashamba ya kawaida ya wananchi kupimwa ili kupata hati za ardhi zitakazowawezesha kutumia kupata mikopo ....ila nitawaletea mashine za kufyatulia tofari ambazo unaweza kuzijengea bila kuchoma " 

Alisema kuwa kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi wa nyumba bora mwananchi atakayekuwa wa kwanza  kupandisha jengo atamchangia bati japo kwa sasa amekwisha toa bati zaidi ya 300 kwa mkuu wa wilaya ya Iringa kwa ajili ya waathirika hao. 

Bw Lukuvi pia amewapongeza wadau mbali mbali zikiwemo taasisi za dini ,watu binafsi ,taasisi ya kifedha pamoja na mifuko ya hifadhi za jamii kwa kujitolea misaada mbali mbali kwa ajili ya waathirika wa mafuriko na wagonjwa wa Kipindupindu Pawaga . 

Pamoja na kuwashukuru wadau hao Lukuvi alimpongeza waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuwatembelea waathirika hao wa Mafuriko na wale wa Kipindupindu Pawaga . 

Hata hivyo Lukuvi alimpongeza mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela na viongozi wote akiwemo mkuu wa mkoa Amina Masenza kwa kusimamia shughuli mbali mbali ikiwemo ya urejeshaji wa miundo mbinu ya barabara iliyokuwa imekatika katika barabara ya Iringa - Ruaha . 

Katika hatua nyingine Bw Lukuvi aliagiza serikali ya kijiji cha Mapogolo kutowabagua wananchi katika kugawa chakula hicho cha msaada na kutaka hata ambao si waathirika wa mafuriko ambao wana njaa wapewe chakula hicho cha msaada kwa waathirika wa mafuriko . 

Wakati huo huo Waziri Lukuvi alisema kuwa serikali inakusudia kuijenga barabara ya Iringa- kuelekea hifadhi ya Ruaha kwa kiwango cha lami kama mbavyo Rais Dr John Magufuli alivyoahidi wakati wa kampeni kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM

Pia kwa ajili ya kuwafanya wananchi kunufaika watalii wanaotembelea hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa alisema tayari jitihada za kujenga viwanja vidogo vya ndege nje ya hifadhi ya Ruaha zimeanza na kuwa lengo la serikali ni kuwahamisha wafanyakazi wanaoishi ndani ya hifadhi hiyo na kujumuika na wananchi nje ya hifadhi ili waweze kupata mahitaji kama wananchi wengine. 





Lukuvi kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela katikati jana


Lukuvi akizungunza na waathirika wa mafuriko ambao kwa sasa wanaishi katika mahema



Mkazi wa Kitanewa akifurahia baada ya Lukuvi kuwapatia misaada mbali mbali







Mmoja kati ya wakazi wa KItanewa ambao walikubwa na mafuriko aliyepata kusoma na waziri Lukuvi darasa moja shule ya msingi akimsikiliza mbunge wake









Lukuvi akitoa maelekezo kwa wananchi wa Kitanewa Idodi







Mkazi wa Kitanewa akilalamika kunyimwa msaada wa mahindi ya msaada wakati yeye ni mlemavu japo si mlengwa wa msaada huo wa waathirika wa mafuriko







Lukuvi akielezwa jambo na mmoja kati ya waathirika wa mafuriko Idodi







Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimweleza jambo mbunge Lukuvi













Gari la watalii wa ndani likipita kuelekea hifadhi ya Ruaha baada ya daraja kurejeshwa ndani ya siku tano sasa













SOMA YALIYOJIRI MBELE NA NYUMA YA MAGAZETI YETU YA LEO

BASATA YAONYA WASANII DHIDI YA MATAPELI

$
0
0




Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linawataka wasanii wote kuwa makini na wakuzaji Sanaa (Mapromota) au baadhi ya wanaojiita wadau wa Sanaa ambao wamekuwa wakitumia njia za kiulaghai na utapeli katika kujipatia faida na manufaa kupitia mgongo wa Wasanii.Baraza linatoa angalizo hili kufuatia kuwepo kwa ongezeko la matukio ya baadhi ya watu wanaojiita wadau wa Sanaa ambao wamekuwa wakiwadanganya wasanii na kuwalaghai kwa kuwaahidi fursa mbalimbali kama za maonesho ya ndani na nje ya nchi ambazo hata hivyo zimekuwa zikiishia katika kuwaletea wasanii matatizo kiuchumi na kijamii.

Aidha, watu hao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi wa Serikali kuwatapaeli wasanii na kujipatia fedha isivyo halali.BASATA linapenda kuwakumbusha wasanii kwamba kabla hawajaingia makubaliano yoyote na mtu, asasi au kampuni yoyote wawasiliane na wanasheria au watoe taarifa Ofisi za Utamaduni za wilaya au manispaa zilizo karibu nao ili kuhakikisha wanaepuka ulaghai na udanganyifu kutoka kwa watu hao wasio waaminifu.

Aidha, kwa wasanii walioko Dar es Salaam BASATA linawaelekeza kufika Ofisi zake zilizoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Slaam ili wapate msaada wa kisheria na kujiridhisha kama makubaliano yao ni halali na ya uhakika.


Mwisho kabisa, BASATA linapenda kuwakumbusha wasanii kwa ujumla kwamba, tangu Januari Mosi mwaka 2013 tasbia za muziki na filamu ni rasmi hivyo Wasanii wote hawana budi kusajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na wanafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za uendeshaji wa kazi za Sanaa nchini.


Aidha, kila msanii anawajibika kuhakikisha anafanya kazi na mtu, watu, asasi au kampuni iliyo na vibali halali vya kuendesha shughuli za Sanaa na si vinginevyo.


Sanaa ni Kazi, Tuitunze, Kuikuza na Kuithamini


Godfrey L. Mngereza


Katibu Mtendaji - BASATA

Taarifa ya Uteuzi wa MKurugenzi MKuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)

MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU AZINDUA MPANGO WA KUWAONGEZEA UWEZO WANAWAKE LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) ambayo itawajengea uwezo wanawake katika bodi za wakurugenzi wa taasisi na makampuni mbalimbali.

Uzinduzi huo uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency  jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuliwa na watu mbalimbali wakiwepo wakenya, waganda na watanzania na watu kutoka bara la Ulaya na Asia.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu amesema kuwa wanawake ni watendaji wazuri na wanamaamuzi mazuri katika uongozi na uendelezaji wa makamuni pamoja na Tasisi mbalimbali.

Mpango huo uliozinduliwa leo umefanywa wanachana chama cha  waajili Tanzania ambao unalenga kuwajengea uwezo wanawake ili kuongeza ufanisi katika biashara zao na kujenga mtandao ambao utaongeza juhudi na maarifa kwa wanawake.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati wa kuzindua Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) ambayo itawajengea uwezo wanawake katika bodi za wakurugenzi wa taasisi na makampuni mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Regency  jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Mwenyekiti wa kampuni ya ATE, Zuhura Muro akizungumza na wanawake kutoka kutoka makampuni mbalimbali leo wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua mpango malumu wa kuwafundisha wanawake ili waweze kuwa na uwezo wa kuleta mawazo yenye kuinua kampuni au taasisi mbalimbali kuwa kubwa.
Mtumbuizaji akitumbuiza katika uzinduzi wa mpango wa kuinua wanawake katika uongozi wa juu katika makampuni au taasisi mbalimbali, uzinduzi  huo umefanyika leo katika hoteli Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akitoa ushuhuda alioufanya katika taasisi hiyo ya fedha kwa maendeleo ya wanawake waliokusanyika leo ili kuzindua mpango wa kuwaundisha wanawake uongozi katika makampuni na Tasisi mbalimbali katika uzinduzi uliofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, sera na Uratibu wa bunge, Jenister Mhagama akizungumza leo katika uzinduzi wa Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) ambayo itawajengea uwezo wanawake katika bodi za wakurugenzi wa taasisi na makampuni mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency  jijini Dar es Salaam leo.
Wadau mbalimbali wakisikiliza shuhuda mbalimbali za wadau wa uongozi kwa wanawake kutoka hapa nchini, Uganda na Kenya leo katika uzinduzi wa Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) ambayo itawajengea uwezo wanawake katika bodi za wakurugenzi wa taasisi na makampuni mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency  jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiteta jambo na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, sera na Uratibu wa bunge, Jenister Mhagama leo katika uzinduzi wa Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) amayo itawajengea uwezo wanawake katika uongozi wa juu wa taasisi na makampuni mbalimbali katika uzinduzi uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency  jijini Dar es salaam leo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzindua Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam leo.

Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

BEI YA MADAFU HII LEO.


SHIRIKA LA ETIHAD LAZIDI KUKUA NCHINI INDIA BAADA YA KUVUNJA REKODI YA IDADI YA ABIRIA.

$
0
0
SHIRIKA  la Ndege la Etihad na mshirika wake Jet Airways wametangaza ongezeko la asilimia 63 la wasafiri wanaoenda na kuondoka nchini India. Ongezeko hilo limeipa nguvu mpya ushirikiano huo na kuimarisha azma yake ya kuwa moja kati ya ndege zenye soko kubwa.

Kwa pamoja, mashirika haya yameweka rekodi ya kuasafirisha abiria milioni 3.3 baina ya vituo vyake vya Abu Dhabi na India mwaka 2015, kwa kulinganisaha mashirika hayo yalisafirisha abiria  milioni 2 ndani ya miezi 12 iliyopita.

Etihad limekuwa shirika geni la kwanza lililowekeza katika shirika la Ndege la Kihindi chini ya Sheria ya Uwezekaji kutoka nje ya nchi ya India ambapo liliwekeza dola za Kimarekani milioni 750 katika Jet Airways ili kupata hisa asilimia 24 mwaka 2013. Shirika la Etihad leo lina ndege 175 kwenda miji 11 India kila wiki. Mitandao ya Etihad na Jet Airways kwa pamoja imewezesha safari za ndege 250 kila wiki katika ya Abu Dhabi na miji 15 ya India.

Pamoja, mashirika haya yanaongoza katika soko kwa usafiri kati ya India na UAE. Kwa kuangalia soko la kimataifa, wanasafirisha asilimia 20 ya abiria kutoka na kwenda India na hii inawakilisha hisa kubwa ya sekta usafiri wa anga nchini India.

Kwa kuongezea, Etihad inafanya operesheni ya uchukuzi mara 14 kila wiki kwenda miji 4 India na inaingiza na kutoa tani 120,000 za mizigo kila mwaka- hii inawakilisha asilimia 9 ya jumla ya soko la kimataifa.

Takwimu hizi zinaonesha umuhimu wa Shirika hili katika soko la India - moja katika ya vyanzo vikubwa vya biashara kwa Etihad- kwa ushirikiano wake mkubwa na Jet Airways na kuimarisha mahusiano kati ya UAE na India.

Mahusiano kati ya nchi hizi mbili ndio yalikuwa kiini cha mazungumzo yaliyotokea Mumbai na Delhi wiki iliyopita ambayo yalileta makubaliano mapya katika sekta mbalimbali ili kukuza mikakati na biashara za kiuchumi.

Biashara kati ya nchi hizi imetabiriwa kukua kwa zaidi ya asilimia 60 ndani ya miaka 5 ijayo kutoka kiwango chake cha sasa cha dola za Kimarekani bilioni 60, katika uwezekaji na bidhaa za kuagiza na kuuza nje katika sekta mbalimbali, zikiwemo; nishati, ulinzi, viwanda, kutengeneza ndege, afya, elimu, utalii, sayansi na teknolojia. Hivi sasa UAE ni mwekezaji wa kigeni wa kumi kwa ukubwa India.

James Hogan, Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Etihad, alisema: “mahusiano kati ya UAE na India yanaendelea kukua kutokana na miaka mingi ya urafiki na dhamira ya kuimarisha uchumi, tamaduni na biashara. Etihad na Jet Airways wanatoa siti zaidi ya 44,000 kila wiki kati ya Abu Dhabi na India, sisi ni kati ya wachangiaji wakuu wa uchumi ya India. Kuna nafasi nyingi za ukuaji zaidi na tunatazamia kutumia fursa zilizopo kuendeleza operesheni zetu.

“Uwekezaji wetu katika Jet Airways ulilenga kuwa sehemu ya simulizi ya mafanikio ya India. Awali ya hili, Etihad ilikuwa inabeba asilimia 2 tu ya wasafiri wote wanaoingia na kutoka nchini India. Tumesaidia kuirudishia Jet Airways katika wigo la faida. Leo hii Jet Airways ni mshirika wetu wa kwanza kimapato huku wakichangia abiria kwa shirika la Etihad, wakati huo huo India ni chanzo cha kwanza cha abiria wa kimataifa kwenda Abu Dhabi.

Uwanja wa Kimataifa wa Abu Dhabi umekuwa kiunganishi cha msingi kwa usafiri wa anga kati ya India na dunia, wateja wameweza kusafiri kiurahisi na wana chaguo zaidi kupitia mizunguko mbalimbali kutoka India kwenda Abu Dhabi na kwingineko.

Tangu kuzindua safari kati ya Abu Dhabi na India kupitia Mumbai mwezi wa tisa mwaka 2004, shirika la Etihad limepanua uwepo wake India kwa kasi baada ya kuzindua njia nyingine kumi na kuongeza mizunguko katika sekta nyingi, zikiwemo safari 3 kwa siku katika njia saba. Kutoka Mei 1, Shirika litazindua operesheni kwenda Mumbai kwa kutumia Airbus A380.

Hivi sasa safari za ndege za Etihad kutoka Abu Dhabi zinafika sehemu zifuatazo India; Ahmedabad, Bengaluru, Chennai, Delhi, Hyderabad, Jaipur, Kochi, Kolkata, Kozhikode, Mumbai na Thiruvananthapuram. Jet Airways inaongeza vituo kwa kufika Pune, Lucknow, Goa na Mangalore pamoja na kuunganisha vituo vya ndani ya nchi.

Dhamira ya shirika la ndege la Etihad kwa India inaonekana katika ushiriki wake katika jumuiya ya biashara. Mwaka jana, shirika la Etihad lilikuwa mwanachama mwanzilishi wa Baraza la Biashara UAE huko India. Jumuiya hii inalenga kuhamasisha mahusiano kati ya vyombo vya biashara, kubadilishana mawazo na kukuza umoja wa kiuchumi kati ya UAE na India.


Akiongezea Bwana Hogan alisema: “India ni soko muhimu si tu kwa shirika letu bali pia kwa UAE yenyewe, hivyo tunaipokea fursa hii ya kuwa mwanachama mwanzilishi wa Baraza la Biashara la UAE nchini India. Ushirikiano huu wa kimkakati na Jet Airways unamaanisha wote tunaongeza wasafiri tutakaohudumia kati ya India na UAE. Tunatazamia kutumia ushirikiano huu ili uweze kuwa na mchango zaidi kwa Baraza la Biashara nchini India.”

“Kama shirika la usafiri wa anga, tuko katika nafasi nzuri kuwezesha biashara, na kuangalia fursa kubwa zilizopo kwa ajili ya uwekezaji India kutoka UAE, tunafurahia kuwa sehemu ya simulizi ya ukuaji wa India.”

Pamoja na hayo, Etihad na Jet Airways wanaingia kwenye mkataba wa pamoja wa kuwa washirika pekee na wadhamini wa Mumbai Indians, mabingwa wa ligi ya Pepsi Indian Premier (IPL) kwa mwaka jana. Mashirika haya yamedhamini matukio mengine ya kimichezo na kijumuiya, ikiwa ni pamoja na mara mbili kuleta kambi ya mafunzo ya Manchester City Football Club nchini India na kuwawezesha vijana wa chimbuko tofauti kupata mafunzo ya hali ya juu.

Mwezi ujao, shirika la Etihad litashiriki katika mkutano wa usafiri wa anga wa mwaka 2016 nchini India, mjini Hyderabad, mkutano na maonesho kwa ajili ya sekta ya usafiri wa anga India. Ikiwa umeandaliwa na Wizara ya Usafiri wa Anga na Shirikisho la Biashara na Viwanda India, tukio hili litatoa nafasi kwa shirika la Etihad kuungana na watengeneza sera, wataalamu wa usafiri wa anga na wadau wengine wakubwa katika sekta ya usafiri wa anga India.

Mpaka kufika mwaka 2020, abiria wa kitaifa na kimataifa wanaopitia viwanja vya ndege vilivyopo India wanategemewa kufika milioni 450. Shirika la Utalii Duniani la Umoja wa Kimataifa linatabiri zaidi ya wahindi milioni 50 watasafiri nje ya nchi kufika mwaka 2020. Shirika la ndege la Etihad limedhamiria kuhudumia watalii kutoka nje na ndani ya nchi ilikutimiza mikakati yake ya ukuaji.

BENKI YA CRDB YATOA MILIONI 10 KUFANIKISHA MAONYESHO YA WAJASIRIAMALI WANAWAKE ZANZIBAR

$
0
0

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi ya shs. milioni 10 kwa Mwenyekiti wa Tanzania Informal Sector Foundation ajili ya Maonyesho ya Wajasiriamali Wanawake yatakayofanyika Zanzibar kuanzia Machi 5-8. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Dauda Salmini na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Masudi Maftah.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shs. milioni 10 kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Isiyorasmi Tanzania, Masudi Maftah kwa ajili ya Maonyesho ya Wajasiriamali Wanawake yatakayofanyika Zanzibar kuanzia Machi 5-8. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Mikopo wa CRDB Microfinance, Everson Temu, Mwenyekiti wa Umoja wa Wajasiriamali Wadogowadogo Zanzibar, Nuru Mohamed na Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Dauda Salmini.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wajasiriamali Wadogowadogo Zanzibar, Nuru Mohamed akizungumza baada ya kupokea hundi ya shs. milioni 10 kwa ajili ya ajili ya Maonyesho ya Wajasiriamali Wanawake yatakayofanyika Zanzibar kuanzia Machi 5-8.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wajasiriamali Wadogowadogo Zanzibar, Nuru Mohamed (wa pili kushoto) akipokea hundi ya shs. milioni 10 kwa ajili ya Maonyesho ya Wajasiriamali Wanawake yatakayofanyika Zanzibar kuanzia Machi 5-8kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
 Picha ya Pamoja.

RAIS WA ZANZIBAR AKUTANA BALOZI MTEULE WA KUWAIT.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait Mahadhi Juma Maalim leo alipofika Ikulu Mjini Unguja kujitambulisha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait Mahadhi Juma Maalim leo alipofika Ikulu Mjini Unguja kujitambulisha.
[Picha na Ikulu.]

TUME YA MIPANGO YATEMEBELEA SHIRIKA LA MAENDELEO YA VIWANDA VIDOGOVIDOGO (SIDO)

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO), Omar Jumanne Bakari (wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa timu ya wataalam kutoka Tume ya Mipango ikiongozwa na Bibi. Florence Mwanri Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kuhusu ufanisi wa mashine ya kutengenezea sabuni katika kiwanda kidogo cha sabuni ambazo soko lake linapatikana jijini Dar es Saalam na mikoa ya jirani.
  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri (wa tatu kulia) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Said Mjuli Mkurugenzi Mtendaji, kuhusu utengenezaji wa batiki katika moja ya viwanda vidogo vinavyofanya kazi chini ya mwamvuli wa SIDO. Wengine pamoja nae ni wataalam kutoka Tume ya Mipango na SIDO.
Kaimu Katibu Mtendaji,  Florence Mwanri pamoja na timu ya maofisa kutoka Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu Bw.George Buchafwe kuhusu utengenezaji wa mazulia kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini.
 Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango  Florence Mwanri,(wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Obedi Sylvester Musiba Mkurugenzi wa kampuni, (wa kwanza kushoto), kuhusu bidhaa wanazotengeneza kutokana na mimea na matunda. Wengine ni Bw. Omar Jumanne Bakari, Mkurugenzi Mkuu SIDO (wa pili kushoto), Bw. Omary Abdallah, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Mipango na Ufuatiliaji (wa tatu kushoto), pamoja na maofisa kutoka Tume ya Mipango.

 Viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa Bw. Abdallah Kayumbi (wa kwanza kulia) kuhusu uzalishaji wa vifaa vinavyotumika kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia upepo (wind Turbines).
 Viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango na SIDO wakiangalia mashine ya kuzalisha nyuzi kwa ajili ya kutengeneza nguo inavyofanya kazi katika kiwanda cha Fruitful Goshen, Matengenezo Textile. 
 Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango,  Florence Mwanri alipata pia fursa ya kutembelea kiwanda cha TEMSO Engineering kinachozalisha vifaa mbalimbali vya ujenzi kama vile mashine za kufyatulia matofali na matoroli (wheelbarrows).
Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Omar Jumanne Bakari, (aliyesimama), akitoa maelezo kwa viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango (waliokaa kushoto) kuhusu SIDO inavyofanya kazi katika kuwasaidia wazawa ili kukuza uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo. Waliokaa kulia ni wamiliki wa viwanda vidogovidogo wanaofanya shughuli zao chini ya SIDO. 
Na: Thomas Nyindo.



Tume ya Mipango.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkaribisha Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipomtembelea waziri Mkuu ofisini kwake Magogoni Dar es salaam kwamazungumzo ya kikazi 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiongea na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd alipofika ofisini kwa waziri Mkuu jijini Dar es salaam kwamazungumzo ya kikazi .
Picha na Chris Mfinanga
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images