Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 772 | 773 | (Page 774) | 775 | 776 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mungy
  Mkuu wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy.

  Ili kuhakikisha kunapungua kwa makosa ya uvunjifu wa sheria ya mtandao, Mkuu wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Innocent Mungy amewataka watumiaji wa mitandao kuzingatia kanuni na masharti ya mitandao.

  Mungy aliyasema hayo katika mahojiano maalumu na Mo Blogna kueleza kuwa moja ya sababu zinazopelekea watumiaji wa mitandao kufanya makosa ni kutokusoma masharti na kanuni za mitandao wanaoingia wakati wanapojisajili.“Wengine hawaelewi maana ya mitandao ya kijamii lakini kabla ya kuingia wanatakiwa kusoma masharti na vigezo wakati wanajisajili kuingiza kwenye mitandao hiyo,” alisema Mungy.

  Alisema makosa ya mitandao yalianza kujitokeza zaidi mwaka 2012 katika mitandao ya Facebook na Instagram na yaliongezeka zaidi baada ya kukua kwa mtandao wa Whatsapp na kuwataja waathirika wakubwa kuwa vijana na zaidi wa kike kati ya miaka 18 hadi 24.

  Mungy alieleza kuwa ili kupambana na makosa ya mtandao Watanzania wanatakiwa kubadilika na kutumia mitandao vizuri na kabla hawajaweka picha au kuandika maneno wahakikishe wanachokiweka mtandaoni hakina makosa.

  Aliongeza kuwa sheria zipo na watumiaji ambao wamekuwa wakivunja sheria wamekuwa wakifungwa, wengine wakitozwa faini na wengine bado wanafatiliwa na Jeshi la Polisi ili kuwatia hatiani kwa makosa ya kuvunja sheria ya makosa ya mtandaoni.

  “Watanzania wanatakiwa kufuata sheria kabla ya kuweka picha mtandaoni wanatakiwa kufikiria kwanza je kama nikiweka itakuwaje maana mtandaoni kila mtu anaona na hiyo taarifa itadumu milele,” alisema Mungy.Pia alizungumzia tukio lililotokea mtandaoni linalomhusu Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu la kuandikwa vibaya na Mungy kueleza kuwa walipokea taarifa za Hoyce na tayari wameshalikabidhi kwa Jeshi la Polisi na hatua zaidi zinaendelea kuchukuliwa na Polisi ili kuishughulikia kesi hiyo.

  Mungy alimaliza kwa kuwataka Watanzania kutumia mawasiliano kama njia ya kuleta maendeleo na sio kuvunja sheria ambayo serikali imeitunga kwa ajili ya kudhibiti makosa ya mtandaoni lakini pia kuutaja mtandao wa Mo Blog kama moja ya mtandao ambao umekuwa mstari wa mbele kukemea matumizi mabaya ya mtandao.

  0 0

  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki amemsimamisha  kazi aliyekuwa mkuu wa chuo cha Utumishi wa Umma Said Nassoro kutokana na kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake.
  Kairuki ametoa maamuzi hayo leo jijini Dar es Salaam  katika mkutano na waandishi  wa  habari katika moja ya kumbi zilizopo katika ofisi za Utumishi wa Umma.

  “Namsimamisha Bwana Said Nassoro aliyekuwa mkuu wa chuo hiki kwa kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake  na kupelekea suala zima la usimamizi wa shughuli za chuo hususani katika matawi yake mbalimbali yaliyoko mikoani kuathirika,” alisema Mhe. Kairuku.

   Kairuki aliongeza kwa kusema kuwa usimamizi  wa Bw. Nassoro  ambao haukuwa wa ufanisi umetoa mwanya kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya ubadhilifu wa mali za Umma ambapo mwaka  2011 na 2013 aliyekuwa mkurugenzi wa chuo upande wa tawi la Mtwara Silvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi.

  Aidha taarifa kutoka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na TAKUKURU zilithibitisha ubadhilifu huo lakini mkuu huyo wa chuo hakuweza kuchukua hatua yoyote badala yake alimuhamisha Bw. Ngata kwenda kwenye tawi la Tabora na kuendelea na wadhifa wake.

  Kutokana na ubadhilifu huo imempelekea  Kairuki  kumsimamisha kazi Bw. Ngata ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tabora na Bw. Joseph Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha za malipo ya ada kiasi cha shilingi bilioni moja ambazo zilikuwa zikilipwa na wanafunzi kwa mwaka wa fedha 2014/15.

  Kairuki ameendelea kueleza kuwa  bado wanaendelea kuondoa watumishi wa Umma ambao hawafuati   mifumo na miongozo ya Utumishi wa Umma ili kuwabakiza  watumishi ambao wanaonyeshe taswira nzuri na kufuata mifumo na  miongozo  ya Utumishi wa Umma kwa ukamilifu wake.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya leo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga 
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Michael Mhando akizungumza Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya leo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza 
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Michael Mhando kushoto akiingia kwenye ukumbini wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya leo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza 
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Michael Mhando akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa mfuko huo wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya leo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza na wa mwisho kulia ni Meneja wa NHIF Mkoa wa Tanga,Ally Mwakababu.
  MKURUGENZI wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti akifuatilia kwa umakini hotuba ta mkuu wa mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya uliofanyika leo mjini Tanga. 
  MKURUGENZI wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti wa kwanza kushoto akiimba nyimbo ya solidarite na wafanyakazi wenzake wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya uliofanyika leo mjini Tanga.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakifuatilia mambo mbalimbali wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya uliofanyika leo mjini Tanga. 
  Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)wakiwa mkutanoni leo 
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya leo mara baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi kulia kwake ni Kaimu Mkuu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Michael Mhando,Picha na Tanga Raha Blog
  Kaimu Mkuu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Michael Mhando akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Picha na Tanga Raha Blog 

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangalla(kushoto)akitoa taarifa ya wiki kuhusu  ugonjwa kipindupindu nchini kwa waandishi wa habari ambao hawapo pichani. Katika taarifa hiyo ya wiki kuanzia Februari 15 hadi 21, mwaka huu jumla wagonjwa walioripotiwa kuugua ugonjwa huo ni 499, ambapo kati ya hao wagonjwa sita walipoteza maisha pia tangu ugonjwa huo ulipoanza Agosti mwaka huu hadi sasa jumla 16,352 wameugua ugonjwa huo, kati ya  hao 249 wamepoteza maisha.Picha na Magreth Kinabo-MAELEZO

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan  akizungumza na Ujumbe wa kampuni ya Gezhouba kutoka China kuhusu masuala ya uwekezaji. Kushoto ni kiongozi wa msafara huo Mhandisi Hu pend.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan  akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa kampuni ya Gezhouba kutoka China.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan  akizungumza na Mwenyekiti wa Shell Deepwater Tanzania BV Alex Knope walipokutana leo ofisini kwake Ikulu kwa ajili ya kumsalimia.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah  Kairuki amemsimamisha  kazi aliyekuwa mkuu wa chuo cha Utumishi wa Umma Said Nassoro kutokana na kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake
  Mhe. Kairuki ametoa maamuzi hayo leo jijini Dar es Salaam  katika mkutano na waandishi  wa  habari katika moja ya kumbi zilizopo katika ofisi za Utumishi wa Umma.
  “Namsimamisha Bwana Said Nassoro aliyekuwa mkuu wa chuo hiki kwa kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake  na kupelekea suala zima la usimamizi wa shughuli za chuo hususani katika matawi yake mbalimbali yaliyoko mikoani kuathirika,” alisema Mhe. Kairuki.
  Mhe. Kairuki aliongeza kwa kusema kuwa usimamizi  wa Bw. Nassoro  ambao haukuwa wa ufanisi umetoa mwanya kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya ubadhilifu wa mali za Umma ambapo mwaka  2011 na 2013 aliyekuwa mkurugenzi wa chuo upande wa tawi la Mtwara Silvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi.
  Aidha taarifa kutoka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na TAKUKURU zilithibitisha ubadhilifu huo lakini mkuu huyo wa chuo hakuweza kuchukua hatua yoyote badala yake alimuhamisha Bw. Ngata kwenda kwenye tawi la Tabora na kuendelea na wadhifa wake.
  Kutokana na ubadhilifu huo imempelekea Mhe. Kairuki  kumsimamisha kazi Bw. Ngata ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tabora na Bw. Joseph Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha za malipo ya ada kiasi cha shilingi bilioni moja ambazo zilikuwa zikilipwa na wanafunzi kwa mwaka wa fedha 2014/15.
  Mhe. Kairuki ameendelea kueleza kuwa  bado wanaendelea kuondoa watumishi wa Umma ambao hawafuati   mifumo na miongozo ya Utumishi wa Umma ili kuwabakiza  watumishi ambao wanaonyeshe taswira nzuri na kufuata mifumo na miongozo  ya Utumishi wa Umma kwa ukamilifu wake.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Pan African Energy Andy Hanna ( wa pili kutoka kulia) akielezea majukumu ya kampuni hiyo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Taasisi zilizopo chini yake.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akielezea fursa za uwekezaji katika sekta ya gesi nchini.
  Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Pan African Energy Andy Hanna akisisitiza jambo katika kikao hicho.
  Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Pan African Energy Andy Hanna (kushoto) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Pan African Energy Nchini Patrick Rutabanzibwa (kulia) wakinukuu maelekezo kutoka kwa Wiziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani)

  …………………………………………………
  Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) kufanya kazi katika mtindo wa kisasa ili nishati ya umeme iweze kuwa ya uhakika kwa maendeleo ya uchumi wa nchi.

  Profesa Muhongo aliyasema hayo katika kikao chake na Kampuni ya Pan African Energy kilichofanyika jijini Dar es Salaam kilichoshirikisha pia watendaji kutoka wizara ya nishati na madini, TANESCO, TPDC na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

  Alisema mahitaji ya gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme wa uhakika ni makubwa, hivyo hakuna sababu ya kuwepo kwa upungufu wa nishati ya umeme nchini wakati kuna gesi ya uhakika.

  Alifafanua kuwa haiwezekani shirika la TPDC likadai kuwa kuna gesi ya kutosha kwa ajili ya kuzalisha umeme, wakati kuna upungufu wa umeme nchini.

  Alisema serikali ina mpango wa kuhakikisha kuwa wananchi wote hasa waishio vijijini wanaunganishwa na umeme wa uhakika kupitia Wakala wa Nishati Nchini (REA) hivyo ni jukumu la mashirika hayo kuhakikisha yanabuni miradi na kukaribisha wawekezaji mbalimbali katika uzalishaji wa umeme wa uhakika ili wananchi wote waweze kuunganishwa na huduma ya umeme.

  Alisisitiza kuwa amekwishawaalika wawekezaji mbalimbali kwa ajili ya kuwekeza kwenye uzalishaji wa Megawati 1000 za umeme kwa ajili ya kuingizwa kwenye gridi ya taifa, hivyo ni vyema shirika la TPDC likahakikisha gesi ya uhakika inapatikana ili umeme uweze kuzalishwa mara moja.

  “ Lengo la serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025 Megawati 10,000 zinazalishwa, hivyo sekta ya nishati kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi na kutoka kwenye kundi la nchi masikini duniani na kuingia kwenye kundi la nchi za kipato cha kati, kama Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, inavyofafanua,”alisema Profesa Muhongo.

  Wakati huo huo, Profesa Muhongo aliitaka kampuni ya Pan Afrian Energy kuhakikisha inatatua changamoto zote inazozikabili kwa kipindi cha miezi mitatu kabla ya kukutana naye Juni 01 mwaka huu kwa ajili ya kupokea mapendekezo ya kampuni hiyo katika kuzalisha gesi ya uhakika.

  Alisisitiza kuwa kutakuwepo na utaratibu wa kukutana na kampuni hiyo kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya kujadili utendaji kazi wa kampuni hiyo, na serikali ipo tayari kutoa msaada pale kampuni itakapokwama.

  Aidha, Profesa Muhongo aliitaka kampuni hiyo kuweka utaratibu wa kuajiri vijana wa kitanzania wanaomaliza masomo ndani na nje ya nchi baada ya kupata ufadhili kutoka serikalini.

  “ Kwa sasa tuna vijana wengi waliohitimu mafunzo kwa ngazi ya shahada za uzamili katika masuala ya mafuta na gesi katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi kama Norway, Uingereza na China, hivyo ni vyema wakapata ajira katika kampuni ya Pan African Energy, ili nao waweze kufaidika na elimu na uwepo wa uwekezaji katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini,” alisisitiza Profesa Muhongo.

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Pan African Energy Andy Hanna, akielezea mafanikio ya uwekezaji kupitia kampuni yake, alieleza kuwa kampuni hiyo imefanikiwa kutoa ajira 87 kwa watanzania na kuboresha huduma za jamii kama vile kutoa huduma ya umeme bure katika eneo la Kilwa kilipo kituo chake za kuzalisha gesi.

  Aliendelea kusema kuwa kampuni ya Pan African Energy imejenga zahanati pamoja na kutoa mafunzo kwa waajiriwa wake lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inakuwa na wataalam wazawa.

  0 0


  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  BAADA ya Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Boniface Jacob kuhoji misaada mbalimbali inayotolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari za manispaa  hiyo ambao unasimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Ando Mwankuga amesema kuwa misaada  ujenzi wa shule hizo,unasimamiwa na manispaa chini ya Afisa Ugavi.

  Mwankuga ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya misaada inayotolewa na wadau mbalimbali juu ujenzi wa Shule za sekondari saba katika manispaa hiyo.

  Amesema kuwa  Desemaba mwaka jana baada ya kuonekana na upungufu wa vyumba vya madarasa katika manispaa hiyo ambapo wanafunzi 3000 wangeweza kukosa nafasi hiyo Mkuu wa Wilaya alianzisha mpango wa uchangiaji kwa wadau mbalimbali katika kuweza kufanikisha ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa.

  Kaimu Mkurugenzi ameongeza kuwa katika msaada wadau waliochangia ujenzi huo wameweza kupata mifuko ya saruji 3190 na bati 100 na vitakwenda kufanya kazi iliyopangwa baada ya kupata taarifa kwa maafisa mipango miji.

  Amesema  kuwa ni shule za kata mbili zinaendelea kujengwa kati  saba zenye mahitaji ya kuongeza vyumba vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi 3000 kupata nafasi ya kusoma na sio kubaki nyumbani.
  Aidha amesema katika ukusanyaji wa michango hiyo hakuna fedha iliyotolewa na wadau ,akaunti yake haina fedha yeyote na vitu vyote viko salama.

  0 0

  WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imetoa rai kwa   viongozi wa mikoa na wilaya, wataalamu na wanajamii kutoficha taarifa ya ugonjwa wa kipindupindu kwani kufanya hivyo kunakwamisha juhudi za kuudhibiti ugonjwa huo nchini.

  Aidha wizara hiyo imesema kwamba yenyewe ndiyo yenye jukumu la kutoa taarifa za ugonjwa huo,hivyo mtu mwingine kwa akitoa taarifa ni zake binafsi.

  Kauli hiyo imetolewa leo  na  Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangalla wakati akitoa taarifa ya wiki kuhusu  ugonjwa kipindupindu nchini kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.

  “Moja ya changamoto kubwa inayoendelea kujitokeza ni pale ambapo baadhi ya wataalamu wa ngazi mbalimbali pamoja na wanajamii wanapoficha wagonjwa na hivyo kutoa taarifa ya wagonjwa wachache kuliko uhalisia.

  “ Madhara yanayoambatana na hii ni kutokuwepo kwa taarifa za kutosha zitakazoongeza juhudi za kuzuia ugonjwa kutoka katika maeneo ambayo wagonjwa hawakutolewa  taarifa na hivyo kuongeza hatari ya ugonjwa kuendelea kusambaa kimnyakimnya na baadae kusababisha wagonjwa wengi kujitokeza katika maeneo hayo kwa maramoja,” alisema Dkt.Kigwangalla.

  Aidha Dkt.Kigwangalla alitoa rai kwa viongozi wa hususan ngazi za mikoa na wilaya kutokutoa kauli za kutaka kuwaadhibu watendaji na viongozi wa ngazi za chini kwa kigezo cha wagonjwa kuwepo katika maeneo yao kwani kwa kufanya hivyo wataongeza kasi ya kuficha wagonjwa na kumwamisha juhudi za kupambana na ugonjwa huo.

  “Sisi tutaendelea kutoa taarifa za ugonjwa huu, hata kama hawataki kukubali kama kuna kipindupindu, tunafanya hivyo kwa sababu tuna takwimu sahihi,kama  hawataki kutumbuliwa majipu sisi tutayatumbua,” alisema.

  Naibu Waziri huyo alifafanua hayo kufuatia baadhi ya viongozi kudai Jiji la Dar es Salaam halina mgonjwa wa kipindupindu  baada ya vyombo vya habari kuripoti jiji hilo lina  ugonjwa huo  na wagonjwa waliokuwepo ni  sita kwa mujibu wa taarifa za wizara hiyo za wiki iliyopita.

   Katika taarifa hiyo ya wiki kuanzia Februari 15 hadi 21, mwaka huu, Dkt. KIgwangalla alisema jumla wagonjwa walioripotiwa kuugua ugonjwa huo ni 499, ambapo kati ya hao wagonjwa sita (6) walipoteza maisha.

  Alisema   tangu ugonjwa huo ulipoanza  Agosti mwaka huu hadi sasa jumla 16,352 wameugua ugonjwa huo, kati ya  hao 249 wamepoteza maisha.

  Aliongeza kwamba  kwa kipindi cha wiki hiyo, jumla ya mikoa 11 imeripotiwa kuwa na ugonjwa huo, ambapo mkoa wa Iringa ndio unaongoza kuwa idadi kubwa ya  wagonjwa 143, Mwanza 94, Mara 87, Dodoma 66, Morogoro 42,Mbeya 30,Arusha 17,Dar es Salaam 14,Simiyu3,Kilimanjaro 2 na Manyara 1. 

  0 0

  Wadau wa filamu nchini tunaomba muendelee kuipigia kura filamu yetu ya Mpango Mbaya ilichezwa na washiriki wachanga kabisa ambao ni zao la Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Msimu wa Kwanza.

  Filamu ya Mpango Mbaya ni moja ya filamu nzuri na yenye ubora wa hali ya juu na ndio sababu kubwa iliyopelekea kuingia katika Kinyanganyiro cha African Magic Viewers Choice Awards 2016 katika kipengele cha BEST MOVIE - EAST AFRICA.

  Jinsi ya Kupiga Kura tembelea tovuti hii http://amvca2016 awards.dstv.com/nominees/best-movie-east-africa_2 


  Na kama hauna akaunti DSTV unachotakiwa ni kujisajili kupitia kiunganishi hiki http://africamagic.dstv.com/ halafu nenda sehemu ya AMVCA halafu pigia kura kipengele cha BEST MOVIE - EAST AFRICA chagua MPANGO MBAYA hapo utakuwa umeiwezesha filamu ya MPANGO MBAYA kuisaka nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania nchini Nigeria. Tuendelee Kupiga Kura Ili Tulete Heshima Nyumbani ni Zamu ya FIlamu sasa.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kulia akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya wa mikopo ya viwanja vinavyotolewa na taasisi yao katika maeneo sita ambayo ni Kilwa, Bagamoyo, Kigamboni, Chalinze, Kibaha na Morogoro. Kulia kwake ni Zahra Moore kutoka kwenye kampuni yao ya BlackWood na Mwanasheria wao Ntiiba Muganga. Picha na Story kwa Hisani ya Bayport Financial Services.


  TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, imezindua miradi sita mipya ya mikopo ya viwanja katika maeneo ya Kibaha, Bagamoyo, Chalinze, Temeke, Kilwa na Morogoro, ikiwa ni mwendelezo wa utoaji huduma bora za viwanja baada ya ule wa Vikuruti kuungwa mkono Watanzania wengi.

  Kuzinduliwa kwa huduma hizo mpya za viwanja huku wakiongozwa na Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Temeke, Martha Minga, kunatanua wigo wa urahisishaji wa maisha ya Watanzania, hususan katika suala la ardhi linalozidi kupanda thamani siku hadi siku, jambo linalohitaji juhudi za taasisi kama Bayport za kuwasaidia wananchi wake kupata maeneo ya makazi kwa utaratibu rahisi na nafuu.
  Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Temeke, Bi Martha Minga, aliyesimama akizungumza katika uzinduzi wa hudumaya viwanja inayotolewa na taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, leo mchana katika Ukumbi wa Ramada Encore, Posta, jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni mwanasheria wa Kampuni ya BlackWood, Ntiiba Muganga na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa BlackWood Zahra Moore.

  Akizungumza katika uzinduzi wa miradi hiyo mipya ya viwanja, Mkurugenzi Mkuu Bayport Financial Services, John Mbaha, alisema huduma zao zitakuwa na njia rahisi kwa ajili ya kuwawezesha wananchi wote kuchangamkia fursa ya upatikanaji wa viwanja hivyo.
  Meneja Masoko na Mawasilianowa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo kushoto akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Temeke, Bi Martha Minga.
  Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, Jonh Mbaga, akipiga picha ya pamoja na Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Faustine Ndugulile katika uzinduzi wa huduma ya mikopo ya viwanja, uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Temeke, Bi Martha Minga.
  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo akizungumza katika uzinduzi huo wa huduma ya mikopo ya viwanja.
  Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa taasisi yao John Mbaga kulia kwake wakati anazungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa huduma yao ya mikopo ya viwanja.

  Alisema njia hizo ni pamoja na ununuaji wa kiwanja kwa pesa taslimu ambapo mteja anatakiwa kulipia fedha zote za kiwanja kwenye akaunti ya Bayport, kukabidhi nakala za nyaraka za malipo hayo kwenye ofisi za Bayport na kusubiri ndani ya siku 90 ili akabidhiwe hati yake baada ya kukamilisha malipo yote.


  “Kwa wateja wa mkopo wa upande wa ujasiriamali na watumishi wa kampuni binafsi, wanatakiwa kulipia malipo ya awali ya mita za mraba walizochagua, huku Bayport ikikamilisha malipo yaliyosalia na wateja hao kupatiwa nyaraka zao baada ya kukamilisha mkopo wao, ambapo thamani ya viwanja hivyo vikianzia sh Sh 550,000,” Alisema Mbaga.


  Naye Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema watumishi wa umma hawatakuwa na gharama za awali, badala yake wakichagua maeneo watakayo, wataingizwa kwenye kundi la mkopo na kutakiwa kulipa mkopo huo kila mwezi kwa kipindi cha miaka mitatu, huku makato yakikadiliwa kuwa Sh 73,684.49 kila mwezi.


  “Bado tunaendelea kutanua wigo kwa watu wote kama vile watumishi wa umma, watumishi wa kampuni binafsi, bila kusahau kundi kubwa la wajasiriamali ambalo limeendelea kujumuishwa kwenye miradi yetu ya viwanja, tukiamini gharama ya makato ya kila mwezi ya Sh 102,855 ni rahisi na yanaweza kuwa mkombozi wa maisha ya watu wengi,” alisema Mndeme.


  Kwa mujibu wa Mndeme, huduma za viwanja zinapatikana katika maeneo ya Bagamoyo na mita moja za mraba zitauzwa kwa Sh 10,000 tu na (Boko Timiza) Kibaha mita moja za mraba itauzwa kwa Sh 9,000 na (Kibiki na Mpera) Chalinze mita moja za mraba zitauzwa Sh 4500, huku (Tundi Songani) Kigamboni mita moja ya mraba itanunuliwa kwa Sh 10,000 na (Msakasa) Kilwa mita ya mraba itapatikana kwa Sh 2000, bila kusahau (Kiegea) mita moja ya mraba Sh 3500 tu.


  Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba hakuna Mtanzania atakayelalamika kushindwa kujenga nyuumba, kama watafanyia kazi juhudi za taasisi yao yenye dhamira na malengo makubwa ya kuwakwamua watu wote ili wawe na vitu vya thamani kama vile nyumba na viwanja.


  Kwa upande serikali kwa kupitia mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Temeke, Martha Minga, aliitaka Bayport kushirikiana na serikali katika mambo yao hususan ya viwanja ili kuhakikisha kwamba wananchi wanafanikiwa kwa dhati na kuepusha migogoro hususan katika suala zima la hati ambalo ndio muhimu katika mambo yanayohusiana na ardhi.  Naye Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile alisema kwamba amefurahishwa mno na huduma ya viwanja vya Bayport sambamba na kuguswa kwa jimbo lake la Kigamboni, jambo linaloweza kuiweka eneo hilo katika nafasi za juu.
  Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Kampuni ya BlackWood Zahra Moore kushoto akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma ya viwanja ya Bayport Financial Services.
  Mwanasheria wa Kampuni ya BlackWood Ntiiba Mungana akizungumza jambo kwenye uzinduzi huo wa huduma ya mikopo ya viwanja.
  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, akipiga picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa kampuni ya BlackWood, Bi Zahra Moore.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Jeshi hilo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na wakwanza upande wa kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) akizungumza jambo katika kikao kazi alichokitisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) kuzungumza na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara yake, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Jeshi hilo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akizungumza jambo katika kikao kazi alichokitisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) kuzungumza na Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara yake, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Jeshi hilo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa Balozi Simba ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.Wakwanza upande wa kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) kuhusu masuala mbalimbali ya kikazi ndani ya Jeshi lake katika Kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kilichoitishwa na Waziri Kitwanga na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akifuatiwa na Naibu wake, Balozi Simba Yahya. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

   Mlalamikaji wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya ubunge jimbo la kigoma kusini David Kafulila akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama ya hakimu mfawidhi mkoa wa Kigoma baada ya Jaji kuhairisha kesi yake
   Wakili wa kafulila profesa safari akiongea na waandishi nje ya mahakama ya hakimu mfawidhi wa mkoa baada ya jaji kuhairisha kesi.
  Baadhi ya wananchi wa mkoa wa kigoma wakiwa nje ya viunga vya mahakama ya hakimu mfawidhi wa mkoa kwaajili ya kusikiliza kesi ya David Kafulila wa NCCR Mageuzi ya kupinga matokeo ya ubunge dhidi ya Hasna Mwilima wa CCM


  Na Editha Karlo wa blog ya jamii Kigoma

  KESI No. 2 ya mwaka 2015 ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma kusini iliyofunguliwa na mlalamikaji  David Kafulila dhidi ya mbunge Hasna Mwilima,Msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa serikali imeahirishwa leo na mahakama kuu kanda ya Tabora mpaka  marchi 9, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa tena.

  Kesi hiyo ambayo ilikuwa  ianze mapema leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kigoma,  Mbele ya Jaji Dr Wambari ambae pia ni Mkuu wa chuo cha sheria lushoto mkoani Tanga, imeahirishwa kwasababu mshatakiwa Hasna pamoja na wakili wake Kennedy Fungamtama pamoja na mawikili wa serikali kushindwa kufika mahakamani hapo, kwa madai ya kuchelewa kupata wito wa mahakama hyo, huku mlalamikaji David Kafulila akifika na wakili wake Prof Safari.

  Katika mazingira hayo Jaji Wambari aliagiza mawasiliano yafanyike kwa pande hizo ili kujua ni lini kwa hakika mawakili hao wataweza kushiriki katika kesi hiyo.

  Kutokufika kwa mlalamikiwa  na mawakili wake na wale wa upande wa serikali ilipelekea zoezi la kusikiliza kesi hiyo kusimama kwa saa mbili kutoka saa tano asubuhi  mpaka saa saba mchana na baada ya hapo hakimu mfawidhi wa Mkoa wa Kigoma kwa niaba ya Jaji silivesta Kahinda alisema  kuwa kesi itaendelea march 9 mwaka huu na kwamba kwakuwa tarehe hiyo imependekezwa na mawakili na pande zote mbili.

  Akiongea na mtandao huu mlalamikaji wa kesi hiyo David Kafulila alusema luwa anakubiana na uamuzi wa mahakama hivyo aliwataka wananchi wawe na subiri hadi hiyi tarehe 9 march mwaka huu.

  ""Jaji mkuu na Jaji kiongozi wamekuwa dhamira  kwa sasa kuwa kesi za uchaguzi zimalizike haraka na hivyo kufikia tarehe hiyo ya march 9,  kesi inatarajiwa kusikilizwa mfululizo hadi itakafik

  0 0   Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizindua Ofisi ya CCM Wilaya ya Kibaha mjini mkoani Pwani leo. Ofisi hiyo imejengwa na familia ya Mbunge wa Kibaha mjini Slyvester Koka (kulia). (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0


  Mwandishi wetu Lindi
  BARAZA la watoto mkoani  Mkoani Lindi  limefanya uchaguzi wa Viongozi wataliongoza  kwa muda wa miaka miwili kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 baada ya   viongozi waliokuwapo madarakani kumaliza muda wake kwa mujibu wa katiba.

  Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa  
   Uliofadhiliwa na  shirika lisilo la kiserikali la Save the Children International  ambapo nafasi zilizogombewa ni pamoja na  Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti,Katibu,Katibu Msaidizi  Mtunza Hazina wajumbe kamati ya utendaji na  kundi maalumu.

   Msimamizi wa uchaguzi  Afisa maendeleo mkoa Lindi, Anna Maro alimtangaza Aziza Ahmad   kutoka wilaya Ruangwa kuwa Mwenyekiti  baada ya kupata  kura 9 na kuwashinda wapizani  wake Salamu Mwinja kutokaWilaya Kilwa aliyepata kura 6 na siwafu mpende kutoka Lindi aliyepata kura 5 huku Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikichukuliwa na Shaibu Peleu  kutoka wilaya Liwale badaa ya kupata kura 8 kati ya 18 zilizopigwa na kuwaacha wapizani  wake  wa wili  wakigawanya kura sita sita kila moja.

   Nafasi ya Katibu wa baraza hilo  ilichukuliwa na Abdul Selema kutoka wilaya ya kilwa  ambaye alipata kura 13 baada ya kumshinda mpizani wake Saidi Mohamedi kutoka Lindi mjini aliyepata kura 7 na  Katibu Msaidizi alipata  Swaumu Juma  aliyepata  kura 8 kati ya kura zote zilizopigwa.

  Anna maro  alimtangaza Sadamu Hamidu kutoka Kilwa  kuwa Mhazini wa baraza hilo ambaye alipata kura 9 wakati Siwatu mpende  kutoka Lindi Mjini alipata nafasi ya Mhazini Msaidizi kwa kupata kura 9

  kwenye Uchaguzi huyo  pia walichaguliwa wajumbe wawakilishi kundi maalumu wa baraza la Mkoa wa Lindi ambapo wajumbe   ambapoArkama Kihaku  kutoka wilaya ya Liwale alipata kura 17 na Nasoro isa kutoka Lindi Mjini alipata kura 2  

  Akizungumzia majukumu ya baraza la watoto Daudi Busweli Afisa Maendeleo ya jamii kutoka shirika lisilo la kiserikali la save the children  ambalo linafadhili mabaraza ya watoto mkoa wa Lindi  na shughuli za na kusimamia haki za watoto kwa kushirikiana na asasi za kijamii  za  Kingonet, Ropa na Lingonet  alisema kuwa baraza la watoto linajukumu la kutambua haki za watoto na kuzisimamia haki hizo na kutafuta njia za kuondoa changamoto zinazosababisha watoto kutotendewa haki zao na jamii.
   Akizungumza kwa niaba ya viongozi waliochaguliwa kwenye uchaguzi huyo Mwenyekiti wa baraza hilo  Aziza Ahmadi    amesema kuwa baraza la watoto wilaya humo aliwavumilia wazazi, walezi na wananchi atakaye nyanyasa na  kuvunja  haki ya mtoto ya kupata elimu , Kulindwa kwa kumsababishia Mtoto wa kike hasa wanafunzi akwa  kumpa ujauzito ,kushindwa kumpeleka  shule kwa visingizio visivyo vya msingi.

  Aidha Aziza Ahmadi  amewashauri watoto  hasa wa kike kuacha tamaa ambazo zinawaingiza kwenye matatizo yanayosababisha kupata mimba za utotoni ambazo zinaharibu malengo yao ,pia amewataka wazazi kuwalinda watoto wao ili wasiingie kwenye vishawishi hasa wanapokuwa shuleni kwani vishawishi hivyo ndivyo vinapelekea wao kushindwa kuendelea na masomo,

  Aziza  amevitaja vishawishi hivyo kuwa ni pamoja na simu za Mkononi ambazo zinajenga uhusiano wa karibu wa wanaume au wanawake wenye tabia za kuwaingiza watoto kwenye matendo yanayokwenda kinyume na haki za watoto na maadili

  Aidha ameiomba jamii kutoa ushirikiano kwa baraza la watoto ili liweze kufanya kazi yake bila vikwazo kwa maendeleo ya watoto ambao ni taifa tegemewa la kesho.

  0 0


  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo jinsi gazeti linavyotengenezwa kutoka kwa mchapaji msaidizi wa magazeti ya serikali (TSN) Bw.Paul Kasele alipofanya ziara katika shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.Na Shamimu Nyaki-WHUSM.


  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitembezwa kuonyeswa mazingira ya kampuni ya magazeti ya serikali(TSN) leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni mhariri mtendaji wa kampuni hiyo ya magazeti ya serikali Bw.Gabriel Nderumaki ambaye amesimamishwa kazi kutokana na utendaji usiorizisha na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Prof Moses Warioba. Picha na Daudi Manongi.Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mhe Nape Nnauye akiongea na vyombo vya Habari kuhusu maagizo aliyoyatoa kwa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya serikali TSN ikiwemo sababu za wafanyakazi wengi kuacha kazi katika shirika hilo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Prof Moses Warioba(wa kwanza kushoto) akitoa tamko la kumsimamisha kazi Mhariri mtendaji wa kampuni ya magazeti ya serikali Bw.Gabriel Nderumaki(hayupo pichani) kutokana na utendaji usiorizisha.Wengine pichani ni wajumbe wa Bodi hiyo Dkt Evelyn Richard na Bw.Alfred Nchimbi
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea kampuni ya magazeti ya serikali TSN leo jijini Dar es Salaam.

  Bodi ya wakurugenzi wa magazeti ya Serikali,(TSN) imemsimashisha kazi Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo Bw Gabrieli Nderumaki kupisha uchunguzi kutokana na utendaji usioridhisha ndani ya kampuni hiyo.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Prof Moses Warioba amesema hatua za kumsimamisha kazi Mhariri Mtendaji huyo umetokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambapo nafasi yake itachukuliwa na Naibu Mhariri Bi Tumma Abdalah.

  “Kumekuwa na mambo mengi yanayofanyika bila kufuata utaratibu ndani ya kampuni hii ikiwemo wafanyakazi kutoelewana na menejimenti katika kulipwa stahili zao, pamoja na wafanyakazi kupewa majukumu ambayo hawana uwezo wa kuyatekeleza”.Alisema Prof Warioba.

  Aidha Prof Warioba ametengua uteuzi wa Bw Felix Mushi aliyekuwa Meneja mauzo na masoko katika kiwanda cha uzalishaji kwa kukosa sifa na utendaji mbovu uliopelekea kampuni kushuka katika uzalishaji.

  Hatua hiyo ya kuwawajibisha watendaji hao imetokana na Ziara ya Mhe. Nape Nnauye Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika Kampuni hiyo ambapo pia hakuridhiswa na utendaji mbovu uliopelekea wafanyakazi 21 kuacha kazi.

  “Nataka Bodi itafakari juu ya malalamiko yaliopo kwa wafanyakazi na wachukue hatua kabla mimi sijakutana na wafanyakazi hao wiki ijayo ili kujua mapungufu yako wapi.”Alisema Mhe Nape.Hata hivyo Bodi hiyo ya wakurugenzi inaendelea kutafuta namna ya kuboresha utendaji ndani ya kampuni ili iendane na kasi iliyopo katika uzalisahaji wa magazeti kwa kiwango kikubwa.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bi. Dianna Melrose Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bi. Dianna Melrose Ikulu  jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Balozi Mteule wa Namibia hapa nchini Bi Theresia Samaria mara baada ya kupokea Hati ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa Namibia hapa nchini Bi Theresia Samaria mara baada ya kupokea Hati ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi Mteule wa Namibia hapa nchini Bi Theresia Samaria mara baada ya kupokea Hati ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Misri hapa nchini Mohamed Yasser El Shawaf Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Misri hapa nchini Mohamed Yasser El Shawaf Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Jean Pierre Mutamba Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Jean Pierre Mutamba Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini Thamsanqa Mseleku Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Picha na IKULU.

  0 0

   Naibu Mkazi Mkuu  wa Hesabu za Serikali , Idara  na Mashirika ya Umma,  Benjamin Mashauri, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu  ukaguzi  kwa Serikali Kuu, Mashirika ya mma na Serikali za Mitaa kwa mwaka 2014/15, Dar es Salaam, jana. Kulia ni  Sarah Reubeni, Msemaji wa ofisi ya  Taifa ya Ukaguzi. 

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  OFISI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),imesema kuwa ukaguzi wa mwaka 2014/2015  kwa serikali kuu haujakamilika hivyo kutumia rasimu hiyo ni makosa.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Naibu Mkaguzi wa Mashirika ya Umma, Benjamin Mashauri amesema kuwa taarifa ya mkaguzi inakamilika ni baada ya kuiwasilisha kwa Rais kwa mujibu wa katiba inatakiwa iwasilishwe mwishoni mwa machi mwaka huu.

  Mashauri amesema kuwa taarifa zinatolewa baadhi ya  vyombo vya habari na kunukuu ripoti ya CAG  kwa mwaka wa fedha 2014/2015 ni batili  kutokana na taarifa hiyo haijakamilika na wananchi wanatakiwa kupuuza taarifa hizo.

  Amesema rasmu hiyo inayotumika baadhi  vyombo vya habari wakati taarifa hiyo haijakamilika na kukamilika kwake ni mara ya kuwasilishwa kwa Rais na kupeleka katika bunge na hapo inakuwa imekamilika kwa kutumia kwa ajili ya wananchi juu ya fedha ya umma ilivyotumika.

  "Kuendelea kutumia rasmu hiyo wakati haijakamilika ni kupotosha watanzania na kukiuka maadili ya kiutendaji na taaluma yake kwa kuwapa taarifa zisizo na uhakika"amesema Mashauri.

  Amesema kuwa ofisi hiyo itaendelea na kutekeleza majukumu yake yote kwa kuzingatia misingi na uwazi na uwajibikaji usiokiuka taratibu za kisheria katika kukusanya na kutumia rasilimali za umma.

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na mdau wa filamu Bi.Khadija Seif (Didas) wakati alipomtembelea ofisini kwake kujadili jinsi gani ya kutunisha mfuko wa maendeleo ya filamu.Bi Khadija anategemea kuchangisha milioni 200 katika mfuko huo.mwingine pichani ni Bi.Joyce Fissoo ambae ni Katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania.

older | 1 | .... | 772 | 773 | (Page 774) | 775 | 776 | .... | 1898 | newer