Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

DAWASCO KUZIMA MTAMBO WA MAJI WA RUVU CHINI.

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA
KUZIMWA KWA MTAMBO WA MAJI WA RUVU CHINI

SHIRIKA LA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAR-ES-SALAAM (DAWASCO), LINAWATANGAZIA WAKAZI WA JIJI LA DAR-ES-SALAAM NA MJI WA BAGAMOYO MKOANI PWANI KUWA, MTAMBO WA KUZALISHA MAJI WA RUVU CHINI UTAZIMWA KWA SAA 36 KWA SIKU YA ALHAMIS TAREHE 18.02.2016. 

UZIMWA KWA MTAMBO HUO KUMETOKANA NA MATENGENEZO KATIKA BOMBA KUU LENYE UKUBWA WA INCHI 54 LINALOSAFIRI MAJI KUTOKA BAGAMOYO MPAKA KWENYE MATENKI YA MAJI YALIYOPO CHUO KIKUU ARDHI . 

MATENGENEZO HAYO YATAFANYIKA ENEO LA LUGALO JESHINI NA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI YA TAREHE 18/02/2016

KWASABABU HIYO MAENEO YAFUATAYO YATAKOSA MAJI:

MJI WA BAGAMOYO, VIJIJI VYA MAPINGA, KEREGE NA MAPUNGA. BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.

MAENEO MENGINE NI MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, MANZESE, MABIBO, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO. 

WASILIANA NASI KUPITIA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022-2194800 AU 0800110064

DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU


“DAWASCO TUTAKUFIKIA”.

93.7 EFM RADIO KUTANGAZA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA LIVE.

$
0
0
Katika kuendelea kuwapa burudani ya michezo wasikilizaji wake, Efm Radio kituo pekee kinachochambua michezo kiundani zaidi kitarusha moja kwa moja mchezo waligi kuu ya soka Tanzania bara ikiwani Dar es Salaam dabi ambapo bingwa mtetezi wa ligi hiyoYanga akiwa mwenyeji wa wekundu wamsimbazi Simba, katika mchezo utakaochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa10:00 jioni siku ya jumamosi ya tarehe 20/02/2016. 


Mchezo huo ni wa roundi ya pili ya ligi kuu ya soka ya Tanzania bara ambapo roundi ya kwanza Yanga ili ibuka na ushindi wa magoli mawili kwa bila mchezo uliochezwa katika uwanja huo wa taifa wakati samba akiwa mwenyeji wa mchezo huo.

Kwasasa Simba inaongoza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwaimecheza michezo 19 nakujikusanyia pointi 45 wakati wapinzani waoYanga wakiwa nafasi ya pili kwa kucheza michezo 18 nakujikusanyia pointi 43.

Kurushwa live Kwa mchuano huu kumedhaminiwa Na Michuzi blog, 


Bado nafasi ipo, iwapo unataka kutangaza nasi wasiliana kwa namba 0712 430 220, idara ya masoko ya Efm. 

AMERI GROUP YA DUBAI KUZALISHA MEGAWATI 600 ZA UMEME

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo( kulia) akipata maelezo kutoka kwa Makamu wa Rais Mwandamizi wa kampuni ya PW Power Systems Charles Levey,( kushoto) ambayo ni wakandarasi wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha megawati mia 600 za umeme wa gesi asilia iliyogundulika nchini ambao Kampuni ya Ameri Group ya nchini Dubai imeyonesha nia ya kuwekeza.( wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ameri Group ya Dubai.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,akiwa kwenye mkutano na watendani wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na ujumbe wa kampuni ya Ameri Group kutoka Dubai walionesha nia ya kuzalisha megawati 600 za umeme wa gesi asilia iliyogunduliwa nchini, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Nishati na Madini jijini DSM

 Na Zuena Msuya, Dar Es Salaam.

Kampuni ya Ameri Group yenye makazi yake nchini Dubai imeonyesha nia ya kuwekeza katika sekta ndogo ya gesi asilia kwa kuzalisha umeme wa megawati  600 za umeme unaotokana na nishati hiyo iliyogundulika nchini.


Hayo yalibainishwa  jijini Dar Es Salaam wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na  ujumbe wa Kampuni hiyo ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ameri Group, Ziad Barakat aliyeambatana na Mkandarasi atakayetekeleza mradi huo na kampuni itakayofunga mashine za kufua umeme.


Barakat alisema Kampuni hiyo inatarajia kuzalisha umeme wa megawati 600 unaotokana na gesi asilia ambapo katika awamu ya kwanza wataanza na megawati 300.


Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliitaka kampuni hiyo kukaa pamoja na Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji( EWURA) ili kuona namna ambavyo kampuni hiyo itatekeleza mradi huo.


 Aidha, Prof. Muhongo alizitaka Taasisi hizo kujadiliana kwa kina kuhusu masuala ya bei ya umeme ambayo kampuni hiyo itaiuzia TANESCO pamoja na masuala mengine ili wafikie muafaka kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi.



Pamoja na mambo mengine, Prof. Muhongo alisema mara baada ya kampuni hiyo kujadiliana na TANESCO, EWURA pamoja na TPDC na kufikia makubalino; Serikali itaelekeza eneo ambalo kampuni hiyo itafua umeme wa gesi katika maeneo ambayo gesi asilia imegunduliwa kama ni Mtwara, Lindi, au Somangafungu.

CCM TAWI LA UINGEREZA WAPONGEZA SIKU 100 ZA UTENDAJI WA MAGUFULI

$
0
0

Tawi la Chama Cha Mapinduzi nchini Uingereza, wamepongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa uthubutu na kasi ya hali ya juu ya kurekebisha mfumo wa utendaji katika serikali ambapo umekuwa na uozo mwingi na wa muda mrefu uliopelekea wananchi hasa wa hali ya chini kukosa huduma za muhimu kutokana na watendaji wengi kufanya kazi kwa mazoea yaliyopelekea kuzorota kiufanisi.

WanaCCM hao wa Uingereza wamesema kuwa siku zote serikali ya CCM imekuwa ikipata lawama nyingi katika utendaji mbovu na hivyo kupelekea wananchi kukata tamaa na utendaji wa Serikali na Chama chenyewe ili hali ni baadhi tu ya watendaji wachache wabovu waliokuwa kwa makusudi mazima wanatenda kazi zao chini kiwango bila weledi ama kwa makusudi ili tu kuharibu sifa ya Chama Cha Mapinduzi.

REGIONAL WORKSHOP ON MAKING AN IMPACT WITH HUMAN DEVELOPMENT REPORTING STARTS

$
0
0
The host of the workshop, Executive Director of ESRF, Dr. Tausi Kida, presents a paper; The Tanzania human development report experience. The session highlighted the Tanzania report experience in producing the Tanzania human development report 2014/2017.
UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative in Tanzania, Mr.Alvaro Rodriguez, delivers his speech when opening a four-day regional workshop on making an impact with human development reporting at Ramada Resort in Dar es Salaam, February 16, 2016.

Delegate from UNDP-Mozambique, Manuel Filipe, makes his contribution following papers presentation.
A cross section of participants attend the morning session.
Executive Director of Economic and Social Research Foundation, ESRF, Dr.Tausi Kida congratulates the UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative in Tanzania, Mr.Alvaro Rodriguez, after he had delivered his opening remarks.
Rodgers Dhliwayo, Economics Adviser/Senior Economist UNDP Tanzania Country Office, presents a paper; Influence of the National Human Development Reports (NHDRs)-Why Produce NHDRs?, during the morning session of four-day regional workshop on making an impact with human development reporting at Ramada Resort in Dar es Salaam, February 16, 2016.
Head of the United Nations Development Programme (Human Development Reports Unit), in New York, Mr. John Hall, presents a paper; The Human Development Approach: An overview of the human development approach, 1990 onwards.
Ice breaker exercise, delegates knowing each other before the start of the crucial session.
UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative in Tanzania, Mr.Alvaro Rodriguez, (R), exchanges ideas with the, Head of the United Nations Development Programme (Human Development Reports Unit), in New York, Mr. John Hall, during the opening day of four-day regional workshop on making an impact with human development reporting at Ramada Resort in Dar es Salaam Tuesday February 16, 2016.
Mr.Alvaro Rodriguez (seated-R), ESRF Chief, Dr.Tausi Kida, (seated centre), and Rodgers Dhliwayo, in a group photo with some delegates.
UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative in Tanzania, Mr.Alvaro Rodriguez, (L), is being escorted by ESRF Executive Director, Dr. Tausi Kida, as he leaves the workshop venue.

JAMII YAASWA KUTUMIA FURSA YA UFUGAJI WA NYUKI NA UPANDAJI WA MITI KIBIASHARA.

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Gladyness Mkamba (katikati) akizungumza wakati akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Gen. Gaudence Milanzi katika ufunguzi wa Mkutano wa mapitio ya kukamilisha mradi wa Kitaifa wa Uendelezaji Misitu na Ufugaji Nyuki nchini (NFBKP II) unaofadhiliwa na Serikali ya Finland kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika Chuo cha Taifa cha Utalii Tawi la Bustani Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Februari, 2016. Kushoto ni Mshauri wa masuala ya Malisili kutoka Ubalozi wa Finland hapa nchini Bw. Mikko Leppanen.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na TAMISEMI. 
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii Tawi la Bustani Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Gladyness Mkamba akizungumza na Waandishi wa Habari katika chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Februari, 2016.
Mratibu Msaidizi wa mradi wa NFBKP II, Bi. Magdalena Muya (kulia) akiwasilisha mada ya jumla juu ya mradi huo ambao ulianza mwaka 2013 na kukamilika mwaka huu 2016.
Mshauri wa masuala ya Malisili kutoka Ubalozi wa Finland hapa nchini Bw. Mikko Leppanen akieleza jambo kwa waandishi wa habari.
Picha ya pamoja.
Na Hamza Temba, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii

JAMII hapa nchini imeaswa kutumia fursa iliyopo ya ufugaji wa nyuki na upandaji wa miti kibiashara kujikwamua kwenye lindi la umasikini.

Hayo yamesemwa jana na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Gladyness Mkamba akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam.

Bi. Mkamba alisema kuwa Tanzania ina fursa kubwa ya kuzalisha asali kwa wingi duniani ambayo ikitumiwa ipasavyo itasaidia kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

"Kwa sasa Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika ambapo inazalisha asali tani 34,000 kwa mwaka baada ya Ethiopia inayozalisha tani 56,000. Hata hivyo kiwango hicho ni kidogo kwa kuwa Tanzania ina uwezo wa kuzalisha asali tani 1,038,000 kwa mwaka" Alieleza.

Akizungumzia changamaoto kuu inayosababisha kiwango hicho kisifikiwe kirahisi, amesema ni utashi hafifu wa jamii kujishuulisha na kazi za ufugaji nyuki na uhifadhi wa mazingira ikiwemo upandaji wa miti.

Bi. Mkamba aliongeza kuwa Jamii ikihamasishwa vya kutosha juu ya faida za ufugaji nyuki na upandaji wa miti inaweza kutoa matokeo ya haraka kwa kuwa asali ina faida kubwa ikiwemo za kiafya na za kiuchumi.

Kwa upande wake Bi. Magdalena Muya ambaye ni Mratibu Msaidizi wa mradi wa Kitaifa wa Misitu na Ufugaji wa Nyuki nchini (NFBKP II) ameeleza kuwa changamoto zingine zinazokwamisha mafanikio katika sekta ya ufugaji nyuki nchini ni ukosefu wa teknolojia za kisasa za ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali pamoja na ukosefu wa mitaji ya kuanzisha miradi mikubwa ya ufugaji wa nyuki.

Nae mshauri wa masuala ya Malisili kutoka Ubalozi wa Finland hapa nchini Bw. Mikko Leppanen, ameeleza kuwa Misitu ya Tanzania inakabiliwa na changamoto ya uharibifu mkubwa unaosababishwa na shughuli za kibinadamu ambapo hupelekea ukame na kuathiri pia uzalishaji wa asali ambao hutegemea malighafi za misitu.

Mshauri huyo ameiasa jamii hapa nchini kutunza mazingira ya misitu, kupanda miti kibiashara na kuhifadhi mazingira ambayo yatasaidia kuweka mazingira bora ya kuishi ikiwa ni pamoja na kuwezesha ufugaji wa nyuki kibiashara na kuwainua watu kiuchumi.

Wakati huo huo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili Bi. Gladyness Mkamba akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Gen. Gaudence Milanzi wakati akifungua mkutano wa siku moja wa mapitio ya kukamilisha Mradi wa Kitaifa wa Misitu na Ufugaji wa Nyuki nchini (NFBKP II) ameishukuru Serikali ya Finland kwa kusaidia ufadhili wa mradi huo.

Ameeleza kuwa mradi huo ambao bajeti yake ni Euro Milioni 19.5 ambazo ni zaidi ya Tsh. Bilioni 47 kwasasa unafadhili mpango wa miaka minne wa Misitu binafsi katika Mikoa ya Iringa, Njombe na Morogoro kwa lengo la kuinua kipato cha wananchi wa vijijini katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania, Mikoa hiyo ni shemu ya Mikoa saba ya jumla inayofadhiliwa na mradi huo.

Amesema hayo yatafanyika kwa kuanzisha misitu ya uhakika yenye faida na kuongeza thamani ya mazao yake kwenye mtiririko wa uzalishaji kuanzia mbegu za miti hadi kwenye bidhaa bora za mbao.


Mradi huo ulianza Oktoba mwaka 2013 hadi Oktoba 2015 na kuongezewa muda wa ziada wa miezi minne ambapo unakamilika mwezi huu wa Februari 2016.

Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa nao wamo Tamasha la Pasaka

$
0
0
KAMATI ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka imewatangaza waimbaji wengine watakaopanda jukwaa la tamasha hilo linalotarajia kufanyika mikoa ya Geita, Mwanza na Wilaya ya Kahama ikiwa ni muendelezo  wa maandalizi ya kuelekea sikukuu hiyo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama wameongeza idadi ya waimbaji katika tamasha hilo ambao ni Christopher Mwahangila na Joshua Mlelwa.

Msama alisema wamepanga tamasha hilo litakaloanza Machi 26 mkoani Geita kwenye ukumbi wa Desire huku Machi 27 litafanyika jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba na Machi 28 litamalizia Uwanja wa Taifa ulioko Wilayani Kahama.

Msama alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha malengo ya tamasha hilo ambayo ni pamoja na kusaidia wenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu  na wajane.
Aidha Msama alisema mwaka huu kamati yake imejipanga kugawa baiskeli zaidi ya 100 kwa walemavu ikiwa ni sehemu ya tamasha hilo.

"Tamasha la Pasaka linawajali wenye uhitaji maalum kama walemavu, yatima na wajane ambao wanapata misaada kupitia mapato ya mlangoni kupitia viingilio," alisema Msama.

Msama aliwataja waimbaji wengine waliothibitisha kushiriki tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Faustine Munishi, Anastazia Mukabwa na Jennifer Mgendi.

BEI YA MADAFU HII LEO.


GERMANY DONATE SURVEILLANCE AIRCRAFT TO SERENGETI NATIONAL PARK

$
0
0
 Germany Ambassador Hon. Egon Kochanke (2nd left) handing over a certificate of ownership of the Husky surveillance aircraft donated to Serengeti National Park to the Minister for Natural Resources and Tourism Pro. Jumanne Maghembe. Others in the picture are FZS Program Manager for Africa Gerald Bigurube, Acting Director General of TAWA Martin Loibooki, TANAPA Director General Allan Kijazi, Serengeti Chief Park Warden William Mwakilema and TANAPA Director of Tourism and Marketing Ibrahim Mussa.
  Germany Ambassador in Tanzania Egon Kochanke (2nd left) delivering his speech during the handing over event. Others in the picture from left are Serengeti Chief Park Warden William Mwakilema,  Minister for Natural Resources and Tourism Pro. Jumanne Maghembe and Director General of TANAPA Allan Kijazi. 
 Minister for Natural Resources and Tourism Prof. Jumanne Maghembe (right) receive Germany Ambassador in Tanzania Egon Kochanke during the handing over event of the Husky Surveillance aircraft to Serengeti National Park over the weekend.
 The Husky surveillance aircraft donated by Germany to Serengeti National Park to enhance patrol activities. 
 Minister for Natural Resources and Tourism Prof. Jumanne Maghembe greet Serengeti National Park Tourism Warden Godson Kimaro during the handing over event.



A Husky to help watch over the Serengeti

Seronera, 15 February 2016 – Today, the German Ambassador to Tanzania handed over an aircraft to the Tanzanian Minister of Natural Resources and Tourism. The Husky aircraft will be deployed by Frankfurt Zoological Society (FZS) for surveillance of the Serengeti National Park to support TANAPA’s fight against poaching.

„We are seeing the large mammals of our protected areas under a severe threat of local extinction because of poaching,“ said Minister Jumanne Maghembe on the occasion of the handover in Seronera. He thanked the German government for the support in countering the recent upsurge in poaching.

“Stringent law enforcement, community involvement and ecosystem management are key in the fight against poaching”, said the German Ambassador Egon Kochanke. “I am very proud to be able to hand this aircraft over to the Tanzanian authorities and FZS. This is an important cornerstone of our close and longstanding cooperation.”

Frankfurt Zoological Society will operate the aircraft in close cooperation with the Serengeti National Park Authority. With aerial support, poacher camps and illegal activities can be detected and the pilots can provide critical information to reaction forces on the ground.

Tanzanian wildlife authorities are faced with a dramatic upsurge of poaching threatening the country’s populations of elephants and rhinos. To counter this threat and to support wildlife and habitat monitoring, the German Government through the German Federal Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ) has provided funding for the acquisition of three aircraft.

The other two Husky A-1C Aircraft will be deployed in the Tanzanian Selous Game Reserve and the Zambian North Luangwa National Park. The Husky is well suited for monitoring and anti-poaching surveys as it operates at low heights and slow speeds.

This support is part of longer-term financial and technical development cooperation measures implemented by FZS, GIZ, KfW, in collaboration with Tanzania Wildlife Authority TAWA, Tanzania National Parks TANAPA, and the Zambian Department of National Parks and Wildlife DNPW.

   

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA UONGOZI WA SHIRIKISHO LA MICHEZO (SHIMMUTA) LEO

$
0
0



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Uongozi wa shirikisho la michezo la mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi (SHIMMUTA) ulioongozwa na Mwenyekiti wa shirikisho hilo Khamis Mkanachi, wakati ujumbe huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 17, 2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika Picha ya pamoja na uongozi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma Taasisi na Makampuni Binafsi wakati ujumbe huo ulipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Februari 17, 2016. (Picha na OMR)

Balozi Seif awasihi wananchi Zanzibar kutoshiriki katika vitendo vya uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi.

WAKUFUNZI WATATU WA ELIMU YA WATU WAZIMA WA MIKOA KUVULIWA MADARAKA.

$
0
0
Kamishina wa Elimu,Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa akizungumza na waandishi habari (Hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko akizungumza na waandishi habari (Hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishina wa Elimu,Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa.

Baadhi ya Waandishi habari wakimsikiliza Kamishina wa Elimu,Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam 

(Picha na Emmanuel Massaka wa Globul ya Jamii).


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. 
KAMISHINA wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko kuwavua madaraka Wakufunzi Wakazi Watatu (3), wa Elimu ya Watu Wazima kutokana na kukiuka utaratibu wa kuchagua wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza kuwaingiza katika Mfumo wa Elimu ya Watu Wazima. 



Profesa Eustella ameyasema hayo leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , amesema kuwa wakufunzi hao wamedanganya kutokana na kuingiza huo utaratibu wa kuwapata wanafunzi wa elimu ya watu wazima. 

Amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakishirikiana na Halmashauri baada ya kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wamefanya vizuri wao kuchukua wanafunzi waliofeli na kuwapeleka katika shule za serikali wakadai kuwa wanafunzi wamechaguliwa katika chaguo la pili. 

Amesema wazazi wamekuwa wanachanganywa na mkanganyiko huo baada ya kuchaguliwa wanafunzi hao wakifika shule wanadaiwa ada wakati serikali imesema bure. 

Wakufunzi waliopata na kadhia hiyo ni Wotugu Mganda (Dar es Salaam), Senorina Kateule (Dodoma),Steward Ndandu Geita na (Mwanza). 

Profesa Eustella amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakidandia matokeo ya kidato cha kwanza kwa kufanya upotoshaji kwa wazazi wakati wanafunzi wanaosoma katika elimu ya watu wazima ni hiari kutokana sera ya elimu. 

Wanafunzi ambao wamechaguliwa kwa mwaka huu wamekuwa wakidai ada ya sh. 80,000 hadi 250,000 na ndipo malalamiko yakaanza kwa wazazi baada ya kudaiwa ada hiyo. 

Profesa Eustella, amesema kuwa mmoja wanafunzi katika Mkoa wa Dar es Salaam aliambiwa amefaulu katika chaguo la pili katika shule ya sekondari ya Oasterbay na baada ya kufika wanafunzi wanakuta mambo tofauti kwa kudaiwa ada na kuambiwa awasiliane na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. 

Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko amesema kuwa watu hao wakivuliwa madaraka wanakuwa walimu wa kawaida wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na kukaimisha nafasi zao.

WAZIRI KITWANGA AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA ULAYA, WANANIA YA KUWEKEZA NCHINI, MAHUSUSI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimfafanulia jambo Mwekezaji kutoka Bara la Ulaya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje wa Kampuni ya Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan Schampheleer (kulia) na Rais wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk. Erick Gohl (wapili kulia), wakati wawekezaji hao walipomtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya uwekezaji nchini mahususi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Ujio wa wawekezaji hao umeratibiwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Daraja la Umoja kati ya Bara la Ulaya na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)-(ESSB). Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ESSB, Dk. Alawi Swabury, na wapili kushoto ni Mwakilishi wa TPSF ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Uraghibishaji wa Taasisi hiyo, Edward Furaha. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimsikiliza Mwekezaji kutoka Bara la Ulaya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje wa Kampuni ya Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan Schampheleer (kulia) wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa majukumu mbalimbali wanayoyafanya katika kampuni yake. Kulia kwake ni Rais wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk. Erick Gohl. Wawekezaji hao walipomtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya uwekezaji nchini mahususi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Ujio wa wawekezaji hao umeratibiwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Daraja la Umoja kati ya Bara la Ulaya na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)-(ESSB). Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa ESSB, Dk. Alawi Swabury. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji kutoka Bara la Ulaya, ambao ni Mkurugenzi wa Mauzo ya Nje wa Kampuni ya Vifaa vya Zimamoto nchini Ubeligiji, Jan Schampheleer (kulia), Rais wa Klabu ya Wafanyabiashara wa Ulaya, Dk. Erick Gohl (wapili kulia), Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Daraja la Umoja kati ya Bara la Ulaya na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc)-(ESSB), Dk. Alawi Swabury, na wapili kushoto ni Mwakilishi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sera na Uraghibishaji wa Taasisi hiyo, Edward Furaha. Wawekezaji hao walikutana katika ofisi ya Waziri Kitwanga, jijini Dar es Salaam leo.

 Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAMA JANETH MAGUFULI AAGA RASMI WALIMU WENZIE NA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI MBUYUNI, DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni alipowasili katika shule ya Msingi ya Mbuyuni, Oysterbay, jijini Dar es salaam kwa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo. 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongozana na mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela , Oysterbay, jijini Dar es salaam kabla ya kuanza kwa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo. 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa ameketi kwenye meza yake katika ofisi ya waalimu katika shule ya Msingi ya Mbuyuni, Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo. 

 Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Oysterbay, jijini Dar es salaam katika sherehe hiyo fupi ya Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo. 
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza maelezo ya utangulizi ya mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela , Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.

 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza maelezo ya utangulizi ya mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela , Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.

 Waalimu wa Shule ya msingi ya Mbuyuni Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya Mama janeth Magufuli kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo. 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi toka kwa Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni katika Shule ya msingi ya Mbuyuni Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo. 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza risala toka kwa mwanafunzi wa shule ya Msingi ya Mbuyuni Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea risala toka kwa mwanafunzi wa shule ya Msingi ya Mbuyuni Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo. 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza maelezo ya utangulizi ya mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela , Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo. 
 Wanafunzi wakitumia simu za walimu wao katika Shule ya msingi ya Mbuyuni Oysterbay, jijini Dar es salaam kurekodia wa sherehe fupi ya Mama janeth Magufuli kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo. 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi ya saa toka kwa mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela , Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo. 


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wasiojiweza katika shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela , Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.

DKT KIGWANGALLA AUTAKA UONGOZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO KUREKEBISHA MAPUNGUFU YALIYOPO

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla alisamiliana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro(RAS) Elia Ntandu mara baada ya kuwasili mkoani humo jana jioni kwa ajili ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia mfumo wa makusanyao ya mapato kwa kutumia mtandao, ambao unafanya kazi sehemu ya usajili tu(mapokezi) kutokana na hali hiyo liagiza uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha unagunga mtandao huo kwenye maeneo yote ya malipo ili kuhakikisha mapato hayapotei.Aliyekaa katika kompyuta ni Mhudumu wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Asteria Mbele na kulia ni Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt Rita Lyiyamuya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia jana baadhi ya vifaa vya maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro .
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiangalia na kuhoji ni sababua zipi zinazosababisha mashine ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo ,figo na ini (BIOCHEMIST) ambayo haifanyi kazi mara baada ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Morogoro .Kushoto Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro(RAS) Elia Ntandu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimwaagiza kuhakikisha taa za vyumba vya upasuaji zinafanya kazi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro(RAS) Elia Ntandu ambapo alitoa muda wa siku 60 wakati alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Morogoro .Pia alitoa muda wa miezi sita wa kufanya marekebisho ya baadhi ya majengo.

BIOTEKNOLOJIA YA KILIMO NCHINI KUFANYIWA UTAFITI

$
0
0
Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndaro Kulwijila (katikati), akiwakaribisha mkoani humo watafiti wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha kabla ya kwenda kutoa mafunzo kwa watafiti, wakulima na wadau wa kilimo kuhusu matumimizi ya kilimo cha bioteknolojia ambacho kinafanyiwa utafiti na watafiti wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiruguru kilichopo jijini Mwanza, Dk.Evelyne Lukonge (wa pili kulia), akifurahi wakati akisalimiana na Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia, Dk.Emmarold Mneney alipo wasili na maofisa wenzake watafiti katika ofisi yake kujitambulisha kabla ya kutoa mafunzo kwa watafiti wa kituo hicho na wadau wa kilimo. Kulia ni Mtafiti Kiongozi kutoka Costech, Dk.Nicholaus Nyange na wa pili kushoto ni Mratibu Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika, Daniel Utunge kutoka nchini Kenya.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiruguru kilichopo jijini Mwanza, Dk.Evelyne Lukonge, akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mtafiti Kiongozi wa Costech, Dk.Nicholaus Nyange.
Mtafiti Kiongozi wa Costech, Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akisisitiza jambo kwenye mafunzo hayo ya matumizi ya bioteknolojia.
Mtafiti Mkuu kutoka Jukwaa la Bioteknolojia, Dk.Emmarold Mneney (kushoto), akifundisha kuhusu matumizi ya teknolojia mpya ya bioteknolojia katika semina hiyo iliyofanyika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiruguru cha jijini Mwanza.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Mratibu Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika, Daniel Utunge kutoka nchini Kenya (kushoto), akiwa kwenye semina hiyo. Wa pili kushoto ni Ofisa kutoka Costech, Mohamed Nyamka na kulia ni mshiriki wa semina hiyo.
Mafunzo yakiendelea.
Watafiti na washiriki wakiwa katika semina hiyo.
Washiriki wakifuatilia kwa karibu mafunzo hayo.
Mtafiti kutoka ARI -Ukiriguru, Maganga Joseph akiuliza swali katika semina hiyo.
Taswira ya ukumbi wa semina hiyo. 

Na Dotto Mwaibale, Mwanza

MTAFITI Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk.Ncholaus Nyange amesema Bioteknojia ya kilimo nchini itafanyiwa utafiti ili kukabiliana na changamoto ya mazao kuharibika.

Hayo aliyaelezwa jijini Mwanza katika semina ya siku moja ya Jukwaa la Bioteknojia iliyoandaliwa mahsusi kwa watafiti na wadau wa kilimo.Alisema ni muhimu bioteknojia ya kilimo kufanyiwa utafiti ili kwenda sanjari ya dunia ya kilimo ambayo inahitahi watafiti.

Katika hatua nyingine Dk. Nyange amewataka wananchi na wataalamu mbalimbali kuthamini tafiti za kilimo za bioteknolojia zinazofanywa na watafiti wetu wa ndani badala ya kusikiliza propoganda za nje kuwa hazifai."Bioteknolojia au uandisijemi ni teknolojia ambayo inakubalika lakini kuna taasisi kadhaa za nje hazilali usingizi zinaeneza propoganda kuwa haifai wakati wao wanaitumia" alisema Nyange.

Alisema teknolojia hiyo inayotumika kwa kilimo cha pamba imeleta mafanikio makubwa katika nchi za Bakinafaso, India, Marekani na nyingine nyingi ambazo hivi sasa zimekuwa zikiongoza kwa utengenezaji wa nguo za kotoni duniani lakini nchi hizo zimekuwa mstari wa mbele kuzuia isitumike hapa nchini.

Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia, Dk.Emmarold Mneney alisema teknolojia hiyo mpya ambayo ina zaidi ya miaka 20 imesaidia kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi kutokana na kuwepo kwa ukame, magugu na wadudu waharibifu wa mazao na ndio maana wameamua kuipeleka kwa wakulima ili waijue.

"Tumeamua kuwafuata watafiti mikoani ili kuendesha mafunzo ya teknolojia hii mpya ambapo tumeanza hapa Mwanza na tutaenda Bunda na Butihama mkoani Mara na watu tuliowalenga ni watafiti wa kilimo, walimu ambao tunaamini wakiilewa nao watatoa elimu hiyo kwa makundi mengine" alisema Dk.Mneney.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiruguru, Dk. Evelyne Lukonge alisema katika ukanda huo wa ziwa changamoto kubwa waliyonayo ni magonjwa ya mazao ya pamba, ndizi, viazi na mihogo hivyo njia pekee ni kwa watafiti kutumia teknolojia hiyo ili kuwa komboa wakulima.

Dk. Lukonge alisema changamoto nyingine kubwa ni fedha za kusaidia kufanya tafiti hizo ambapo aliiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa karibu zaidi.

Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndaro Kulwijila akiwakaribisha mkoani humo watafiti hao kutoka Costech alisema hivi sasa duniani hakuna kilimo kitakachofanikiwa bila ya kuwa na watafiti hivyo aliiomba serikali kutenga fedha za kutoka ili kuwawezesha watafiti kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali za kilimo.

Kulwijila alisema mkoani humo changamoto kubwa waliyonayo ni kupanda kwa gharama kubwa ya kilimo cha pamba kwani bei yake imeendelea kuporomoka kutoka sh.1200 kwa kilo hadi kufikia sh. 800 hadi 700 jambo linalowakatisha tamaa wakulima.

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AFUNGA MACHIMBO YA MORAMU MOSHONO.

$
0
0
Picha kwa hisani ya maktaba

Na Woinde Shizza,Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu amesimamisha shughuli za uchimbaji katika machimbo ya moramu katika kata ya Moshono Mkoani Arusha kwa kipindi cha mwezi mmoja kupisha wakandarasi kuweka sawa machimbo hayo ambayo yanachimbwa bila kufuata utaalamu hali ambayo inadaiwa inaweza kuhatarisha uhai wa maisha yao.

Katika kipindi cha mwaka 2013 machimbo hayo yaliuwa wachimbaji 13 hali ambayo ilimfanya waziri mkuu mstaafu Peter Pinda kuyafunga mpaka yatakaporekebishwa ndiyo wachimbaji hao waendelee na uchimbaji ingawa inadaiwa wachimbaji hao hawakufuata maagizo mpaka hivi sasa kwani waliendelea na shughuli za uchimbaji.

Akizungumza wakati akifunga machimbo hayo mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhil Nkurlu alisema kuwa mazingira ya wachimbaji hao ni mabaya na yanahatarisha maisha yao kwa kiasi kikubwa na kwamba hawana utaalamu wa kutosha juu ya namna bora ya uchimbaji wa moramu hiyo mbali na kuchimba kinyemela toka kauli ya waziri mkuu kutamkwa.

Alisema kuwa ameamua kufunga machimbo hayo kutokana na oanagezeko kubwa la vifo linalosabibishwa na uchimbaji wa moramu usiozingatia sheria na kanuni .

Naye kamishina msaidizi wa madini kanda ya kaskazini Elias Kadabila alichukuwa fursa hiyo kuwaomba wananchi kufuata maelezo ya mkuu wa wilaya ili waweze kuchimba kuchimba kwa usala ambapo alisema kuwa pia iatawasaidia kuepukana na maafa au vifo vinavyotokana na uchimbaji holela.

Aidha pia aliuomba uongozi wa mtaa pamoja na wachimbaji hao kutoa ushirikiano ili kuweza kuwapisha wakandarasi kutengeneza machimbo hayo kwa muda wa mwezi mmoja .


Gazeti hili pia liliweza kuzungumza na baadhi ya wachimbaji hao ambapo walisema kuwa hawakubaliani na agizo hilo la mkuu huyo kwakuwa uchimbaji huo ndiyo ambao unawafanya kumudu gharama za maisha na kusomesha watoto na kwamba serikali iangalie namna nyingine.

"kwakweli tunaomba serekali iangalie tena na tena swala hili kwani sisi wananachi ndio tunategemea maachimbo haya kwani ndio yanatusaidia tunaweza kula ,kusomesha watoto ,kujenga naweza sema kiujumla kuendesha maisha yetu"Alisema Lowayani Metili

Ipo haja ya wachimbaji hao kupisha marekebisho hayo yatakayofanywa na serikali kwa manufaa yao na uhai wao kwani kuendelea kuchimba wakati wanahatarisha maisha yao ni jambo la hatari Zaidi kwani wahenga wanamsemo usemao UHAI NI BORA KULIKO KIFO.

UAMUZI WA MATOKEO KUNDI C KUTOLEWA KAMATI YA NIDHAMU.

$
0
0
KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi ya Ligi (Kamati ya Saa 72) imekutana jana (Februari 16, 2016) kupitia taarifa za mechi mbili za Kundi C la Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya JKT Kanembwa na Geita Gold SC, na Polisi Tabora na JKT Oljoro ambapo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilisimamisha matokeo yake hadi taarifa hizo zitakapopitiwa.

JKT Kanembwa ilifungwa mabao 8-0 na Geita Gold SC katika mechi iliyofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, wakati Polisi Tabora ilishinda mabao 7-0 dhidi ya JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Baada ya kupitia taarifa hizo na vielelezo vingine, Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imeonyesha mashaka kutokana na kuwepo viashiria vya upangaji wa matokeo (match fixing).


Kwa vile suala hilo linahusisha masuala ya kinidhamu, na kwa kuzingatia Ibara ya 50(1) na (11) ya Katiba ya TFF na Ibara ya 69 ya Kanuni za Nidhamu za TFF, Kamati ya Saa 72 imemuelekeza Katibu Mkuu wa TFF apeleke suala kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa ajili ya uchunguzi na hatimaye kufanya uamuzi.

Article 4

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AFUNGA MACHIMBO YA MORAMU MOSHONO

$
0
0
picha kwa hisani ya maktaba

Na Woinde Shizza,Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu amesimamisha shughuli za uchimbaji katika machimbo ya moramu katika kata ya Moshono Mkoani Arusha kwa kipindi cha mwezi mmoja kupisha wakandarasi kuweka sawa machimbo hayo ambayo yanachimbwa bila kufuata utaalamu hali ambayo inadaiwa inaweza kuhatarisha uhai wa maisha yao.

Katika kipindi cha mwaka 2013 machimbo hayo yaliuwa wachimbaji 13 hali ambayo ilimfanya waziri mkuu mstaafu Peter Pinda kuyafunga mpaka yatakaporekebishwa ndiyo wachimbaji hao waendelee na uchimbaji ingawa inadaiwa wachimbaji hao hawakufuata maagizo mpaka hivi sasa kwani waliendelea na shughuli za uchimbaji.

Akizungumza wakati akifunga machimbo hayo mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhil Nkurlu alisema kuwa mazingira ya wachimbaji hao ni mabaya na yanahatarisha maisha yao kwa kiasi kikubwa na kwamba hawana utaalamu wa kutosha juu ya namna bora ya uchimbaji wa moramu hiyo mbali na kuchimba kinyemela toka kauli ya waziri mkuu kutamkwa.

Alisema kuwa ameamua kufunga machimbo hayo kutokana na oanagezeko kubwa la vifo linalosabibishwa na uchimbaji wa moramu usiozingatia sheria na kanuni .Naye kamishina msaidizi wa madini kanda ya kaskazini Elias Kadabila alichukuwa fursa hiyo kuwaomba wananchi kufuata maelezo ya mkuu wa wilaya ili waweze kuchimba kuchimba kwa usala ambapo alisema kuwa pia iatawasaidia kuepukana na maafa au vifo vinavyotokana na uchimbaji holela.

Aidha pia aliuomba uongozi wa mtaa pamoja na wachimbaji hao kutoa ushirikiano ili kuweza kuwapisha wakandarasi kutengeneza machimbo hayo kwa muda wa mwezi mmoja .Gazeti hili pia liliweza kuzungumza na baadhi ya wachimbaji hao ambapo walisema kuwa hawakubaliani na agizo hilo la mkuu huyo kwakuwa uchimbaji huo ndiyo ambao unawafanya kumudu gharama za maisha na kusomesha watoto na kwamba serikali iangalie namna nyingine.

"kwakweli tunaomba serekali iangalie tena na tena swala hili kwani sisi wananachi ndio tunategemea maachimbo haya kwani ndio yanatusaidia tunaweza kula ,kusomesha watoto ,kujenga naweza sema kiujumla kuendesha maisha yetu"Alisema Lowayani MetiliIpo haja ya wachimbaji hao kupisha marekebisho hayo yatakayofanywa na serikali kwa manufaa yao na uhai wao kwani kuendelea kuchimba wakati wanahatarisha maisha yao ni jambo la hatari Zaidi kwani wahenga wanamsemo usemao UHAI NI BORA KULIKO KIFO.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images