Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

DK. KIGWANGALLA AUPA MIEZI SITA UONGOZI WA HOSPITALI YA RUFAA MOROGORO KUREKEBISHA MFUMO WA CHUMBA CHA UPASUAJI

$
0
0
kigwaDk. Kigwangalla akimsikiliza mtoa huduma kwa njia ya mtandao katika malipo (hayupo pichani) alipotembelea hospitalini hapo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro mapema jana Februari 16 na kubaini matatizo mbalimbali ikiwemo chumba cha upasuaji, mfumo wa malipo na ubovu wa vifaa vya maabara.

Dk. Kigwangalla ametoa siku 60 vifaa ndani ya chumba cha upasuaji ziwe zimerekebishwa huku akiagiza ndani ya miezi sita mfumo wa chumba cha upasuaji uwe umetengenezwa vizuri na endapo watashindwa basi atachukua hatua za kufungia vyumba hivyo vya upasuaji kwani vikiendelea kuachwa hivyo vitaendelea kusababisha matatizo Zaidi kwa wanaopaatiwa huduma.

Dk. Kigwangalla akiwa ameambatana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Ritha Lyamuya walitembelea vitengo kadhaa ikiwemo chumba cha upasuaji, jengo la maabara, pamoja na majengo mengine ikiwemo lile la wamama wajawazito na jengo maalum la daraja la kwanza (Grade A).

Hata hivyo ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kushughulikia mara moja mapungufu yaliyobanika. Katika jengo la kuhudumia wagonjwa wa daraja la kwanza, Dk. Kigwangalla alikuta hali ya uchafu na muonekano usiofaa kwa matumizi ya kuitwa daraja la kwanza.
Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, awali lawama nyingi zinatupiwa Wizara yake wakati ukweli ni kuwa Hospitali zipo chi ya Wizara ya TAMISEMI ambao wanashughulikia huku wao Wizara ya afya wakisimamia baadhi ya mambo ikiwemo ukaguzi, madawa, mashine na vifaa.
kigwangalla morogoroDk. Kigwangalla akiangalia namna ya mfumo wa ulipaji kwa kutumia mtandao unavyofanya kazi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro. Wengine ni uongozi wa Hospitali hiyo akiwamo Mganga Mfawidhi, Dk. Ritha Lyamuya.
kigwangalla moroDk. Kigwangalla akiangalia mfumo huo wa malipo kwa mtandao hospitalini hapo ambapo hata hivyo ameuagiza uongozi wa Hospitali kuhakikisha wanafunga mifumo ya ulipiaji karibu idara zote za malipo ilikuzuia upotevu wa fedha.
kigwamorozzNaibu Waziri wa Afya Dkt. Kigwangalla akimsisitizia jambo Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Ritha Lyamuya kuyafanyia kazi maagizo aliyoyatoa huku akimweleza kuwa atachukua hatua kali endap hayatatekelezwa ikiwemo kufungia huduma za upasuaji. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Morogoro).

HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA MKOANI RUVUMA YATUMBUA JIPU,YAMFUKUZA KAZI MHANDISI WA WILAYA HIYO

$
0
0
Halmashauri ya Wilaya ya SONGEA Mkoani RUVUMA imemfukuza kazi mhandisi wa Wilaya hiyo, Mhandisi DAUDI BASILIO kwa kosa la kutumia vibaya madaraka yake kwa kuidhinisha fedha za ujenzi wa barabara kutoka MBINGA MHALULE hadi MPITIMBI pamoja na ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao la MGAZINI kinyume cha taratibu na kusababisha hasara ya zaidi ya milioni 38. Story kamili hii hapa RUVUMA TV.

TAASISI YA TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) YAZINDUA KAMPENI YA UWIANO WA KIJINSIA

$
0
0
Rais wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) (TWA), Irene Kiwia (katikati ) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu uzinduzi wa kampeni ya uwiano wa kijinsia ambayo ni kauli mbiu kuelekea kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, kushoto kwake ni Balozi wa kampeni ya uwiano sawa kijinsia Inspk.Prisca Komba na kulia kwake ni Mwenyekiti wa TWA, Sadaka Gandi kwenye mkutano uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam. 
Mwenyekiti wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA), Sadaka Gandi akifafanua jambo kuhusu uzinduzi wa kampeni ya usawa wa kijinsia kwenye mkutano na waaandishi wa habari uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam. 
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Rais wa TWA Irene Kiwia kuhusu uzinduzi wa kampeni ya usawa wa kijinsia katika mkutano uliofanyika mapema leo Jijini Dar es salaam .


Dar es Salaam, Februari 17, 2016: Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) imetangaza uzinduzi wa kampeni ya uwiano wa kijinsia kwenye kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani ya Wanawake inayotoa wito kwa kila mtu kuchukua hatua za dhati kusaidia upatikanaji wa usawa wa jinsia kwa kasi zaidi ili kuwasaidia wanawake na wasichana kufikia malengo yao.

Hali kadhalika inatoa wito kwa jamii kuwa na uongozi ulio na usawa wa kijinsia, kuheshimu na kuthamini tofauti bainia ya jinsia, kuanzisha utamaduni jumuishi na kuondoa upendeleo kwenye sehemu za kazi. 

Akizungumza leo kwenye mkutano wa waandishi wa habari kwenye ofisi za TWA jijini Dar es Salaam Rais wa TWA, Bi. Irene Kiwia alisema kuwa lengo la Kampeni ya Uwiano wa Kijinsia ni kutoa wito kwa wanawake na wanaume kuungana pamoja kusaidia wanawake kufikia hali ya usawa kwa idadi kubwa na kutambua mchango wao usio na ukomo wanaoutoa kwenye uchumi duniani kote kwa ujumla hususani nchini kwetu Tanzania.

“Kampeni ya Uwiano wa Kijinsia inamaanisha kutoa wito kwa wadau wote vikiwemo vyombo vya habari, watu binafsi, serikali na mashirika yote kutambua na kujenga uelewa kuhusu mianya inayozuia mchakato wa kuwepo usawa wa kijinsia na kutaka kuchukua hatua za dhati kuharakisha mabadiliko,” alisema Kiwia.

“Mwaka 2014 Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum -WEF) lilitabiri kuwa usawa wa jinsia duniani utafikiwa mwaka 2095. Lakini mwaka mmoja baadaye, yaani 2015 lilikadiria kuporomoka kwa hatua husika na kupunguza kasi ya kufikia uwiano kuwa pengo la kijinsia linaweza kuzibwa ifikapo mwaka 2133. Hii inamaanisha kusubiri kwa miaka 117 ambayo ni mingi sana. Kutokana na hali hiyo TWA inaungana na wito wa dunia wa kuitaka kila nchi kuliweka suala la jinsia kwenye ajenda zake na kuharakisha kasi ya kufikia lengo la usawa wa kijinsia .” alisema Kiwia.

Akitoa wito kwa watu binafsi, mashirika na wadau wengine kushiriki kwenye kampeni hiyo Mwenyekiti wa TWA Bi. Sadaka Gandi alisema Kampeni itahusisha matembezi ya kilomita sita asubuhi ya siku ya tarehe Tano mwezi March kuanzia kwenye `Viwanja vya Mbio za Mbuzi´ maarufu kama ‘Uwanja wa Farasi’ kupitia kwenye makutano ya Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), kuelekea Kanisa Katoliki la Mt. Petro na kupitia Ubalozi wa Kenya nchini na kurudia sehemu yalipoanzia.
 
Bi. Sadaka Gandi aliendelea kusema kuwa matembezi hayo yatafuatiwa na mkutano wa kusherehekea siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani ambao utafanyika Machi 6, 2016 kwenye Hoteli ya Regency Kilimanjaro.


Bibi Gandi alisema, “Mkutano huu utawakutanisha wanawake na wanaume kutoka sehemu tofauti ambao watashirikiana na kushawishiana kuungana na harakati hizi, vile vile tutaonyesha mafanikio yaliyopatikana mpaka sasa kutoka Mkutano wa Beijing miaka 21 iliyopita, na hali kadhalika ni kasoro gani ambazo bado zipo na ni kwa namna gani ushirikiano wa pamoja unaweza kuharakisha mabadiliko. Tunaamini mchango wako sio tu kwamba utachangia msingi wa maendeleo ya wanawake bali pia utaonesha ni jinsi gani kampuni yako inachangia kwenye upatikanani wa usawa wa kijinsia kwa ujumla”.


Bibi Gandi alisema kuwa mkutano huo utazungumzia masuala mbalimbali yanayomhusu mwanamke kwa kuzingatia elimu, afya, uongozi, haki na sheria na uchumi. “Usawa wa jinsia ni muhimu kwa sababu umefungamana na kukua kwa uchumi kwani maendeleo ya wanawake na uongozi ni nguzo ya ufanisi kwenye biashara na ustawi wa uchumi”, alihitimisha. 

Wakurugenzi 5 wa Halmashuri Wasimamishwa Kazi kupisha uchunguzi.

MADIWANI WAPITISHA MAPENDEKEZO YA KUBADILI MATUMIZI YA MIL.40 ZA VIBURUDISHO KUPELEKWA SEKONDARI ZA WASICHANA

$
0
0
Baadhi ya wakuu wa idara wa halmashauri ya wilaya ya Singida vijijini wakiwa katika mkutano wa kupitisha mapendekezo ya mwelekeo wa bajeti ya mwaka 2016/2017.
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida wakiwa katika mkutano wa kupitisha mapendekezo ya mwelekeo wa bajeti ya halmashauri hiyo ya Singida vijijini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Singida, Bwana Simon Mumbee akipitia taarifa zake anazotarajia kuwasilisha kwenye mkutano huo maalumu kwa ajili ya kupitisha mapendekezo ya mwelekeo wa bajeti ya 2016/2017.
Diwani Magreth Mangu (wa kwanza kutoka kulia) akibadilishana mawazo muda mfuppi baada aya kumalizika mkutano maalumu wa baraza la madiwani kupitissha mapendekezo ya mwelekeo wa bajeti ya Halmashauri hiyo ya mwaka 2016/2017.
(Picha zote Na, Jumbe Ismailly)

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Singida limepitisha mapendekezo ya kufanyika kwa mabadiliko ya matumizi ya zaidi ya shilingi milioni 40 zilizotengwa kwa ajili ya kununua viburudisho na vitafuno wakati wa vikao mbali mbali vya Halmashauri hiyo na badala yake fedha hizo zielekezwe katika kutatua matatizo yaliyopo katika shule za sekondari za bweni kwa wasichana.
Diwani wa kata ya Ikhanoda,Hinga Mnyawi alitoa mapendekezo hayo kwenye mkutano maalumu wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo uliokutana kwa lengo la kupitisha mwelekeo wa mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
“Jingine mwenyekiti wakati afisa elimu sekondari akituaga amenikuna sana lakini sisi naye tuliangalie sana hili,tunatenga fedha kwa ajili ya viburudisho pamoja na vitafuno zaidi ya shilingi milioni arobaini nimesoma hapa,zile hela kwa nini badala ya kula hapa tuzielekeze ziende kuwasaidia watoto wa kike wanaosoma katika shule za bweni”alisisitiza Mnyawi.
Aidha diwani huyo alizitaja shule zitakazonufaika na kiasi hicho cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya viburudisho na vitafuno kuwa ni pamoja na Kijota,Ughandi,Msange,Ikhanoda na Mwanamwema zilizopo katika Halmashauri hiyo.
Hata hivyo Mnyawi alibainisha kuwa umefika wakati kwa Halmashauri hiyo kulipa deni la Kituo cha afya kilichojengwa katika Kijiji cha Ngimu kwa zaidi ya miaka saba sasa lakini bado halijaezekwa.  
Kwa mujibu wa diwani huyo wakati wa kuanza ujenzi wa kituo hicho wananchi walingia mkataba na mkandarasi kwa makubaliano ya kumlipa shilingi milioni arobaini mara ujenzi huo utakapokamilika,jambo ambalo wameshindwa kutekeleza.
“Kwenye ukurasa wa kumi inasema uwepo wa madeni katika miradi viporo nakumbuka kuna kituo cha afya kata ya Ngimu wananchi waliingia mkataba na mkandarasi kwa makubaliano ya shilingi milioni arobaini kazi itakapokamilika,lakini mpaka sasa bado hazijalipwa.”alibainisha Mnyawi.
Aidha diwani Mnyawi hata hivyo aliweka bayana kwamba katika kudhihirisha kwamba ujenzi wa zahanati hiyo umesahaulika aligundua kwamba hata kwenye kabrasha walilokabidhiwa kujadili mwelekeo wa mpango wa bajeti ya mwaka ujao wa fedha hakuna sehemu inayolitamka jengo hilo.
Wakichangia hoja ya mwelekeo wa mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017 baadhi ya madiwani wa Halmashauri hiyo walionyesha wasiwasi wao juu ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu ya barabara.
Kwa mujibu wa diwani wa kata ya Merya,Iddi Kijida kiasi cha shilingi milioni 39 zilizotengwa kwa ajili ya barabara yenye urefu wa zaidi ya kilomita 45 haziwezi kukamilisha matengenezo ya uhakika wa kuwawezesha wananchi wanaolima na kusafirisha mazao ya biashara kama vitunguu kwenda kuuza mazao yao kwenye soko la mjini Singida.
Naye diwani wa kata ya Itaja,Paul Himida aliweka bayana kwamba kutokana na Halmashauri hiyo kuwa na mahitaji makubwa ya fedha hivyo hawana budi kwenda kusimamia kwa karibu makusanyo ya ndani ili waweze kufanikisha kusaidia kwenye miradi viporo vilivyobakia katika mwaka wa fedha wa 2015/2016.
Akifungua mkutano huo maalumu wa Baraza la madiwani,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Singida,Elia Dgha alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi juu ya umuhimu wa kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha wakati huu kwa kulima mazao ya mzizi ikiwemo viazi na mihogo,mtama na uwele kwa mazao ya chakula na alzeti na vitunguu kwa biashara yatakayowasaidia endapo baa la njaa litawakumba kama ambavyo lilivyowakumba kwa mwaka wa 2015/2016.
Hata hivyo Digha ambaye pia ni diwani wa kata ya Msange aliishukuru serikali kwa kuipatia Halmashauri hiyo zaidi ya tani mia nne za chakula ambazo zimewasaidia wananchi wake kukabiliana na upungufu wa chakula uliokuwa ukiwakabili.

WAHAMIAJI HARAMU 15 WAKAMAATWA SINGIDA WAKISAFIRISHWA KUPELEKWA AFRIKA YA KUSINI.

$
0
0
 Afisa uhamiaji Mkoa wa Singida, Faith Ihano akitoa taarifa za kukamatwa kwa wahamiaji haraamu kutoka nchini Ethiopia waliokuwa wakisafirishwa kwenda Afrika ya kusini.
Watumishi wa idara ya uhamiaji Mkoa wa Singida waliofanikisha upatikanaji wa watu 15 ambao ni raia wa Ehiopia.
Wahamiaji haramu 15 waliokuwa wametoka Ethiopia wakisubiri katika nyumba moja ya mtaa wa mitunduruni kusafirishwa kwenda Afrika ya kusini.


Na Jumbe Ismailly,Singida.
IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Singida imefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 45 raia wa kutoka nchi za Ethiopia, Demokrasia ya Jamuhuri ya watu wa Congo pamoja na Malawi kwa tuhuma za kuingia na kuishi nchini bila kuwa na vibali.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, Ofisa Uhamiaji huyo wa Mkoa wa Singida, DSIS, Faith Ihano alisema wahamiaji hao haramu raia wa nchini Ethiopia walikamatwa baada ya kukutwa wakiwa wamefichwa kwenye nyumba ya mtu binafsi iliyopo kwenye Mtaa wa Unyankindi, Manispaa ya Singida,mkabala na nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa(NHC).

Kwa mujibu wa Ihano wakati askari wa jeshi hilo wakiwa katika doria kwa lengo la kukomesha wimbi la wahamiaji haramu hao linaloendelea kujitokeza siku hadi siku,walikuwa wakisafirishwa kwenda nchini Afrika ya kusini,wakitokea Jamuhuri ya Demokrasia ya watu wa Kongo, Malawi pamoja na Ethiopia.

“Wahamiaji hawa haramu waliokamatwa idadi yao ni kumi na tano na hao ni raia wa Ethiopia na kwamba wahamiaji hawa walikamatwa na askari wa kikosi cha uhamiaji wakiwa katika doria na wahamiaji hawa walikuwa wamehifadhiwa katika nyumba moja ya mtu binafsi”alifafanua Ihano.

Hata hivyo kwa mujibu wa afisa uhamiaji huyo kwa sasa wanamshikilia mwenye nyumba waliyokuwa wamehifadhiwa wahamiaji hao haramu kwa mahojiano zaidi na pindi upelelezi wao utakapokamilika,hatua za kisheria zitaweza kuchukuliwa dhidi yake.

Ofisa huyo wa uhamiaji hata hivyo alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa watu wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu kuacha mara moja kwani idara ya uhamiaji inaendelea kufanya kila juhudi za kuwasaka wale wote wanaowasaidia kuwaingiza nchini kinyume cha sheria na kuhakikisha inawakamata na kuwachukulia hatua kali na za kisheria.

Ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (katikati) akielekezwa jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bw.Magid Hemed alipofanya ziara yake ya kutembelea Wilaya hiyo kwa kuangalia mradi wa ujenzi wa daraja la Ruvu chini na bandari ya Bagamoyo.
 Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (katikati) akionyeshwa ramani itakapojengwa bandari ya Bagamoyo kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa Upanuzi wa Bandari hiyo kutoka Mamlaka ya Bandari nchini Bw. Alexender Ndibalema (Kushoto) katika ziara yake ya kutembelea Wilaya ya Bagamoyo.
  Eneo ya Chuo cha Uvuvi cha Mbegani Wilayani Bagamoyo ambayo ipo katika mpango wa kubadilishwa na kuwa Bandari ya Bagamoyo.
 Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (kulia) akisalimiana na Mafundi wa kampuni ya Ujenzi ya ESTIM inayojenga daraja la Ruvu chini katika barabara ya Bagamoyo kwenda Msata katika ziara yake ya kutembelea Wilaya ya Bagamoyo.
 Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (kulia) akielekeza jambo wakati alipotembelea ujenzi wa daraja la Ruvu chini katika barabara ya Bagamoyo kwenda Msata , wanaongalia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Magid Hemed (katikati) na Kushoto ni Mbunge wa Bagamoyo Mhe. Shukuru kawambwa.

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (kushoto) akimsikiliza Mhandisi wa mradi wa ujenzi wa daraja la Ruvu chini Bw. Adam Makiba(Kulia) wakati wa ziara ya kutembelea Wilaya ya bagamoyo pamoja na miradi ya ujenzi wa Bandari na daraja .
 Ujenzi wa daraja la Ruvu chini unavyoonekana katika picha ambapo unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.
  Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (kushoto) akipata maelezo kuhusu ukarabati wa barabara ya Msata kutoka kwa Mhandisi wa mradi wa ujenzi huo Bw. Adam Makiba wakati wa ziara ya kutembelea Wilaya ya bagamoyo pamoja na miradi ya ujenzi wa Bandari na daraja la Ruvu chini.
Barabara ya Bagamoyo kwenda Msata inavyoonekana katika picha baada ya kubainika mapungufu yake hata hivyo Mkandarasi ameahidi kufanyia kazi mapungufu hayo.

(Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)

UFAFANUZI KUHUSU TAKWIMU ZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.

UFAFANUZI KUHUSU TAKWIMU ZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo miongozo inayosimamia ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko na miongozo hii imetolewa na kusambazwa katika mikoa na wilaya zote nchini. Mwongozo huu unafuata utaratibu wa mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ujulikanao kama “Integrated Disease Surveillance and Response (IDSR)”

Katika mwongozo huu, taarifa za magonjwa ya milipuko kama Kipindupindu pindi yanapotokea hutolewa taarifa mara moja kwa kutumia Ainisho sanifu yaani “Standard case definition”. Aidha maainisho haya ya utambuzi wa ugonjwa yapo kwa ajili ya jamii (Community case definition) na katika ngazi ya kituo cha Afya (Health facility Case Definition).

Aidha utambuzi huu wa ainisho la awali, huzingatia dalili za ugonjwa ili mgonjwa aweze kupatiwa huduma wakati taratibu za vipimo zinapofanyika. Vipimo huchukuliwa kwa wagonjwa 10 wa awali wanaohisiwa kuwa na ugonjwa wa Kipindupindu, na iwapo mmoja wao akithibitika kuwa na vimelea vya ugonjwa basi uwepo wa mlipuko wa ugonjwa husika hutangazwa.

Aidha kutokana na utaratibu huu, ni wagonjwa wa mwanzo tu ndio watakaochukuliwa vipimo, na wengine watakaoendelea kujitokeza huwa wanachukuliwa kuwa wana ugonjwa kwa kuwa wana mahusiano na ushirikiano na wagonjwa waliokwisha thibitika “epidemiological link”

Vipimo vya maabara huchukuliwa tena kwa baadhi ya wagonjwa watakaoendelea kuugua ili kuweza kuangalia mwenendo wa ugonjwa husika na pia kupima usikivu wa Dawa (Antimicrobial Sensitivity Test).

Wizara inaendelea kusisitiza mambo manne muhimu, 
1. Utoaji wa taarifa ya wagonjwa wapya wa Kipindupindu huzingatia Ainisho Sanifu yaani Standard case Definition bila ya kuwepo uthibitisho wa ugonjwa kimaabara

2. Pindi ugonjwa ukisha thibitishwa kwa wagonjwa wa awali kumi (10) katika Mkoa/Wilaya/Halmashauri husika tayari mlipuko wa ugonjwa huu unathibitishwa na kutangazwa.

3. Uthibishwaji wa ugonjwa kimaabara unafanyika tu kwa baadhi ya wagonjwa ili kuweza kuangalia mwenendo wa ugonjwa na pia kupima usikivu wa Dawa (Antimicrobial Sensitivity Test)

4. Baadhi ya watu wenye ugonjwa wanaweza kupimwa na kuonekana kutokuwa na vimelea vya ugonjwa husika mfano kipindupindu. Zipo sababu nyingi zinazoweza kupelekea kipimo kutoonyesha uwepo wa vimelea hivyo mojawapo ikiwemo wagonjwa kuanza kutumia dawa kabla ya kufika katika vituo vyetu vya tiba.

Kwa mfano katika Mkoa wa Dar es salaam kwa siku kumi zilizopita kuanzia tarehe 7 hadi 16 Februari wagonjwa 16 wa kipindupindu (Temeke 12 na Ilala 4) ambao walikidhi vigezo vya ainisho sanifu na kupata matibabu katika kambi ya kipindupindu ya Temeke kwa wagonjwa wa Temeke na Hospitali ya Amana kwa wagonjwa wa Ilala na hivyo kulazimu kutolewa taarifa kwa mujibu wa muongozo.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
17 FEBRUARI 2016.

WAZIRI KITWANGA AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI, AWATAKA WAPANGE MIKAKATI MIPYA YA KUPAMBANA NA WAHALIFU NCHINI

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Polisi nchini kabla ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Jeshi hilo, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa hao kutoka Mikoa yote nchini kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini. Watatu kulia meza kuu ni Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Ernest Mangu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akitoa hotuba yake kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi lake, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) kuzungumza na maafisa hao kutoka mikoa yote nchini na kuufungua Mkutano wao wa Mwaka unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga kabla ya kufungua mkutano huo, aliwataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB nchini, Ineke Bussemaker, mara baada ya kumkabidhi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (kulia), Shilingi Milioni 75 kwa ajili ya kuudhamini Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa yote nchini. Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri Kitwanga katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, na aliwataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini.

 Sehemu ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, wakimsikiliza mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alipokuwa anazungumza na maafisa hao katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam kabla ya waziri huyo kuufungua Mkutano huo wa Mwaka wao wa Mwaka kwa ajili ya kufanya tathimini ya utendaji wao pamoja na kuliboresha zaidi Jeshi hilo. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa hao kutoka Mikoa yote nchini kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akiyajibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari ambao walitaka kupata ufafanuzi zaidi kutokana na hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, unaofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kasi inayoandana na Serikali ya Awamu ya Tano, na pia wapange mikakati mipya ya kupambana na uhalifu nchini. Kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. 

Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kwaya mbili kusindikiza Tamasha la Pasaka.

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
KWAYA mbili za nyimbo za Injili zimethibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa kuanzia Machi 26 hadi 28.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama tamasha hilo linaanza Geita katika ukumbi wa Desire ambalo litafanyika Machi 26, Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba litafanyika Machi 27 na Kahama Machi 28 kwenye uwanja wa Taifa.

Msama alizitaja kwaya hizo zinazotarajia kupanda jukwaani katika mikoa hiyo ni pamoja na AIC Makongoro Vijana ya jijini Mwanza sambamba na Wakorintho Wapili ya Mafinga ya Iringa.

Msama alitoa wito kwa wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ambalo malengo yake ni kusaidia wenye uhitaji maalum ambao ni walemavu, yatima na wajane.

“Nawaomba wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi ili tuwasaidie wenzetu wenye uhitaji maalum ambao ili wafikie malengo wanahitaji kutoka kwetu,” alisema Msama.


Aidha Msama alisema bado wanaendelea kufanya mawasiliano na waimbaji mbalimbali wa Tanzania ambao kwa pamoja watafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.

BEI YA MADAFU HII LEO.

BENKI ya CRDB imelipa kodi ya sh. bilioni 107 kwa serikali hadi Desemba 31,2015.

$
0
0
Akizungumza na baadhi ya wakurugenzi na mameneja wa benki hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya miaka 20 ya utendaji wa benki hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Charles Kimei alisema wamefanikiwa kuifanya taasisi hiyo kuwa kinara wa kutoa huduma bora.

Alisema amana za wateja wa benki hiyo zimeongezeka zaidi ya mara 100 kutoka sh. bilioni 40 walizoanza nazo mwaka 1996 hadi sh. trilioni 4.2 iliyokuwepo Desemba 31 mwaka jana.“Safari ya miaka 20 ilikuwa na misukosuko ikiwemo kupata hasara y ash. bilioni 1.8 mwaka 1997 lakini tunajivunia kusema tumepita salama na sasa tumekuwa taasisi bora ya fedha hapa Tanzania.

“Idadi ya bidhaa zetu, wateja na hata thamani ya benki pia imeongezeka… tunao waajiriwa 2,682 wenye nidhamu,” alisema Dk. Kimei huku akibainisha kwamba katika kampeni hizo watawekeza zaidi kwenye elimu.Alisema maadhimisho ya kuelekea kilele cha miaka 20 ya CRDB yatakayohitimishwa Juni mwaka huu yamepewa kauli mbiu ya ‘Benki inayokua na kuboresha maisha ya watu.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafitti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sherehe za miaka 20 ya benki ya utendaji wa benki hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sherehe za miaka 20 ya benki hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo.
Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya mameneja na wakurugenzi wa beki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya mameneja na wakurugenzi wa beki ya CRDB wakiwa katika uzinduzi huo.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Dk. Charles Kimei (kushoto).
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakishuhudia uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 20 ya benki ya CRDB katika hoteli ya Ramada leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charls Kimei (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyopadhyay (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Esther Kitoka.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya Pamoja. 
Wakurugenzi wakiwa wamepozi kwa picha.
Wakurugenzi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mameneja wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.

katibu mkuu wizara ya habari,utamaduni,sanaa na michezo akutana na Bodi ya Wakurugenzi ya TSN.

$
0
0
Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper Ltd (TSN) wakimskiliza Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kuzungumzia changamoto mbali mbali za kampuni hiyo.kutoka kulia ni Dkt Consolatha Ishebabi,Dkt Evelyn Richard na Bw,Alfred Nchimbi.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akizungumza jambo na mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper Ltd (TSN) Bw.Prof Moses Warioba (kushoto).
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (wa kwanza kulia) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper Ltd (TSN) kuhusu changamoto mbalimbali za kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwa katibu mkuu ni Prof Moses Warioba ambaye ni mwenyekiti wa bodi hiyo.

Picha na Daudi Manongi-WHUSM.

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WADAU WA MICHEZO NCHINI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa michezo nchini kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Februari 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wapenzi na viongozi wa michezo nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza na wadau wa michezo nchini kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Februari 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipata maelezo kuhusu michoro ya viwanja vya ndani vinavyotarajiwa kujengwa pembeni mwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kutoka wa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ( watatu kulshoto) na katibu Mkuu wake Profesa Elisante Ole Gabriel (wapili kushoto) wakati alipozungumza na wadau wa michezo kwenye uwanja wa taifa Februari 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa michezo nchini baada ya kuzungumza ao kwenye uwanja wa taifa jijini dar es salaam Februari 17, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wadau wa michezo nchini baada ya kuzungumza nao kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Februari 17, 2016. 

WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU NA NAIBU WAKE WATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KUKAGUA

$
0
0
Tazama video ya tukio hilo hapa:
muhimbili waziri wa afya
Dk.Stanslaus Ntiyakunze (aliyenyoosha mkono) akiwaonyesha mawaziri namna jengo linavyokarabatiwa ikiwemo miundombinu yake inavyotakiwa kuwa pindi litakapokamilika ikiwemo suala la mfumo wa maji safi na maji taka. Kuliwa kwake ni Naibu Waziri wa Afya Dk Hamisi Kigwangalla wengine Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo ya Muhimbili, Prof. Laurance Masaru (kushoto) na Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu (katikati).

Mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli wameendelea kufanya kile ambacho wananchi wanataka ikiwemo suala la kutumikia wananchi ambapo mapema leo, Februari 17, Mawaziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu na Naibu wake, Dk. Hamisi Kigwangalla wameweza kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kukagua majengo likiwemo lile aliloagiza Rais kuwa litumike kuwa wodi ya akina mama.

Mawaziri hao wamefika Hospitali hiyo ya Taifa majira ya mchana na kisha kupokelewa na wenyeji wao akiwemo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Prof. Laurance Masaru na kisha kukagua moja ya majengo lililopo jengo la watoto ilikuona namna ya kuweza kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali hyo ya Taifa.

Mbali na kukagua majengo pia walipata kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji ikiwemo wodi maalum ya wagonjwa wa figo, wodi ya akina mama, wodi ya watoto na upasuaji mdogo pamoja na wodi ya watoto wa ugonjwa wa moyo na ile ya watoto wa ugonjwa wa kansa.

Aidha, Waziri Ummy Mwalimu ameeleza kuwa jengo ambalo Rais ameliagiza litumike kama wodi ya akina mama, amebainisha kuwa agizo hilo wameweza kulitekeleza ndani ya siku moja na awali wamefanikiwa kulaza wagonjwa zaidi ya 40 na hadi kufikia leo wameweza kufikisha wagonjwa 53.

Hata hivyo, Waziri Ummy Mwalimu amewataka wananchi na vyombo vya habari kuwa wavumilivu kwa kipindi cha sasa kwani tayari ukarabati unaendelea kuakikisha miundombinu inawekwa sawa na ndani ya wiki moja itakuwa imekamilika.

Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog
muhimbili2
Mkurugenzi wa ufundi, Gaudence Aksante akiwaongoza Mawaziri wa Wizara ya Afya kuelekea katika jengo hilo linalofanyiwa ukarabati ililitumike kwa matumizi zaidi ya wagonjwa kuondoa msongamano hospitali hiyo ya Muhimbili.
muhi
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akipata kuwafariji watoto wanaopatiwa matibabu katika wodi maalum ya matibabu ya kansa.
muimbiliWaziri wa Afya akimjulia hali mmoja wa wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika kitengo cha magonjwa maalum ikiwemo Figo. Mgonjwa huyo alipongeza mawaziri hao kwa kuweza kufika hospitalini hapo na kuwajulia hali.
muhimbili33
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati alipotembelea katika wodi ya wagonjwa wa Figo.
muhimbilin77
Waziri Ummy Mwalimu akiwa pamoja na watoto wanaopatiwa matibabu ya ugonjwa wa kansa katika hospitali hiyo ya Muhimbili katika jengo la Watoto.
muhimbili999
Naibu Waziri wa Afya Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na Muuguzi mkuu Bi. Praxeda Chenya, wengine ni Waziri Ummy Mwalimu wakati wakiondoka katika jengo hilo la watoto mapema leo Februari 17, 2016.
muhimbili
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Laurance Masaru akitoa maelezo namna ya walivyojipanga kuhakikisha wanasaidia wagonjwa wote wanaofika kutibiwa hospitalini hapo. wanaofuata ni Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla na Waziri Ummy Mwalimu pamoja na watendaji wa hospitali hiyo mchana wa leo Februari 17. 

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA NANE WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII AFRIKA MASHARIKI NA KATI.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi cheti katika Mkutano wa Nane wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika Mashariki na Kati. Makamu wa Rais amefungua rasmi mkutano huo leo katika Ukumbi wa Benki Kuu.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Kulia) akiteta jambo na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama katika ufunguzi wa Mkutano wa nane wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika Mashariki na Kati. Mkutano huo wa siku mbili umefunguliwa leo na unafanyika jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Vyombo mbalimbali vya Habari mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa nane wa Mifuko ya Jamii Afrika Mashariki na Kati. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika jijini Dar es Salaam.

SIMBA SPORT CLUB WAKUSOGEZEA KARIBU JEZI NA VIFAA VYA SIMBA MAHALI ULIPO

$
0
0
Upatikanaji wa jezi na vifaa vya Simba wasogezwa karibu


Klabu ya Simba leo imeanza rasmi utekelezaji wa kampeni yake ya uuzwaji wa jezi pamoja na vifaa mbalimbali venye chapa ya Simba, ikiwa na dhumuni la kukuza mapato kwa timu kwa kupitia wanachama na wadau wa Simba kununua bidhaa mbalimbali zenye chapa ya Simba, kupeleka huduma ya vifaa vinavyotolewa na duka rasmi la Simba karibu zaidi na wanachama na wapenzi wa Simba. Katika zoezi hili ambalo utaweza kununua jezi kwa Tsh. 15, 000/= ambapo yoyote atakaenunua atapata picha kubwa ya timu bure.



Kwenye mechi na watani wa jadi wetu Yanga siku ya Jumamosi, kikosi cha Simba kitavaa jezi nyeupe ambazo zitakuwa zikipatikana kwenye duka la Simba linalotembea katika mitaa mbalimbali yaani Mobile Shop.



Akizungumza na Simbasports.co.tz leo asubuhi wakati zoezi hili lilipoanza Rais wa Simba Evans Aveva alisema “ leo tunaanza rasmi zoezi letu la kutembea mtaa kwa mtaa kwenye kampeni yetu ya uuzwaji wa jezi pamoja na vifaa mbalimbali venye chapa ya Simba kwa kutumia duka linalotembea “Mobile Shop” zoezi hili ni maalumu kwa ajili ya kusogeza upatikanaji wa vifaa na jezi za Simba kwa karibu zaidi, lakini pia itahamasisha wanachama na wapenzi wa Simba kuchangia timu yao”



Tunatambua kwamba wanachama na wapenzi wa Simba waliopo mikoni wangependa zoezi hili lifike na mikoani  na punde tu tutakuwa na utaratibu wa jinsi Duka letu la Simba Sports Shop litakavyoweza kupeleka huduma katika mikoa mbalimbali Tanzania, aliongeza Rais wa Simba Evans Aveva.



Akizungumza mkurugenzi wa kampuni ya EAG Group Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya masoko ya klabu ya Simba alisema “zoezi hili litakuwa endelevu ambapo tutaendelea kubuni njia mbalimbali za kuwafikia watu waliopo mikoani nje ya Dar es Salaam ambapo kwa sasa wanaweza kupata jezi rasmi ya Simba kwenye duka mtandao la Simba kupitia Jumia www.jumia.co.tz na jezi zitawafikia popote walipo Tanzania”.


Simbasports.co.tz inaupongeza uongozi wa Simba SC pamoja na wasimamizi wa Duka la Simba Simba Sports Shop kwa ubunifu huu katika kuleta maendeleo ya klabu ya Simba.

UZINDUZI WA MRADI WA AFYA BORA YA MAMA NA MTOTO ZANZIBAR.

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Halima Maulid Salum akifungua warsha ya uzinduzi wa Mradi wa Afya bora ya mama na mtoto katika Hoteli ya Mzson Shangani Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi Idara ya Kinga na elimu ya afya Dkt. Mohd Dahoma akizungumza na washiriki waliohudhuria katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa Afya bora ya Mama na Mtoto katika ukumbi wa Hoteli ya mazson Shangani mjini Zanzibar.
 Meneja wa Mradi wa Afya bora ya mama na mtoto kutoka Shirika la kuhudumia watoto Tanzania Dkt. Bernard Mbwele akitoa maelezo juu ya mtazamo wa mradi huo kwa washiriki katika Hoteli ya Mazson Mjini Zanzibar.

  Meneja Msaidizi wa Shirika la kuhudumia watoto Dkt. Awrad Saleh akiwasilisha mada ya majukumu ya waangalizi na wakaguzi wa Mradi wa Afya bora ya mama na mtoto wakati wa uzinduzi wake.
  Daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt. Fadhil Mohd akitoa mchango wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Afya bora ya mama na mtoto katika Hoteli ya Mzson Shangani Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya washiriki katika uzinduzi wa Mradi wa Afya ya mama na mtoto uliofanyika Hoteli ya Mzson Shangani wakifuatilia uzinduzi huo.
PICHA NA ABDALLA OMARA/MAELEZO ZANZIBAR.

katibu mkuu wizara ya habari,utamaduni,sanaa na michezo akutana na Bodi ya Wakurugenzi ya TSN

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (wa kwanza kulia) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper Ltd (TSN)kuhusu changamoto mbalimbaliza kampuni hiyoleojijini Dar esSalaam. Kuliakwakatibumkuuni Prof Moses Warioba ambaye ni mwenyekiti wa bodi hiyo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akizungumza jambo na mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper Ltd (TSN) Bw.Prof Moses Warioba (kushoto).

Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper Ltd (TSN)wakimskiliza Katibu Mkuu kutokaWizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (hayupopichani)wakati wa kikao cha kuzungumzia changamoto mbalimbaliza kampuni hiyo.kutoka kulia niDktConsolathaIshebabi,Dkt Evelyn Richard na Bw,AlfredNchimbi.PichanaDaudiManongi-WHUSM

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA BAADHI YA MAKUNDI YALIYOSHIRIKI NAYE KWENYE KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2015

$
0
0
 Rais John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan  akisalimia katika mkutano wa Rais John Pombe Joseph Magufuli na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
 Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akisalimia katika mkutano wa Rais John Pombe Joseph Magufuli na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
 Rais John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
 
Baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016. 
 Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na kundi la sanaa la Tanzania One Theatre baada ya kuongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
 Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wataalamu wa TEHAMA baada ya  kuongea  na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
  Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wasanii wa Bongo Fleva  baada ya  kuongea  na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
 Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wasanii wa Bongo Movie   baada ya  kuongea  na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016
 Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na sehemu ya wanahabari  aliokuwa nao katika kampeni baada ya kuongea  na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
 Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na watendaji kutoka CCM Makao Makuu  baada ya  kuongea  na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
 Rais John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mhe January Makamba huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Nape Nnauye kabla ya kuongea  na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
Rais John Pombe Joseph Magufuli na Mama Janeth Magufuli wakiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  Mhe January Makamba huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Nape Nnauye wakielekea ukumbini kuongea  na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.PICHA NA IKULU
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images