Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WAGONJWA WA KIPINDUPINDU WAONGEZEKA NA KUFIKIA 528.

$
0
0


Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii,Jinsia,Wazee na watoto, Ummy Mwalimu akizugumza na wandishi wa habari juu ya takwimu za wiki iliyopita zinaonyesha kuwa kuanzia Februari  8 hadi 15 mwaka huu, idadi ya wagonjwa walioripotiwa wiki hii imeongezeka kutoka 242 ya wiki iliyoishia ya February 7 hadi imefikia wagonjwa  528 ambapo ni sawa na ongezeko la 118%, kati yao watu 5 walipoteza maisha.leo jijini Dar es Salaam,kusoto ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii,Jinsia,Wazee na watoto,Dk.Mpoki Ulisubisya

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

UGONJWA wa kipindupindu hadi kufikia Februari 14 mwaka huu , jumla ya watu 15,853 wameugua ugonjwa huo, na kati yao watu 243 wamepoteza maisha. 

Akizungumza na waandishi wa Habari wa Jijini Dar es Salaam leo, Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii,Jinsia,Wazee na W    atoto, Ummy Mwalimu amesema takwimu za wiki iliyopita zinaonyesha kuwa kuanzia Februari  8 hadi 15 mwaka huu, idadi ya wagonjwa walioripotiwa wiki hii imeongezeka kutoka 242 ya wiki iliyoishia ya February 7 hadi imefikia wagonjwa  528 ambapo ni sawa naongezeko la 118%, kati yao watu 5 walipoteza maisha.

Amesema ongezeko hili limechangiwa zaidi na kuibuka tena kwa ugonjwa huu mkoani Iringa katika Halmashauri ya Iringa ambayo imeripoti jumla ya wagonjwa 199 kwa wiki iliyopita ikiwa ni sawa na 38% ya wagonjwa wote walioripotiwa kwa wiki husika.

Ummy amesema awali ya  Julai mwaka  jana , Mkoa wa Iringa uliwahi kuripoti wagonjwa 2 kwa siku moja tu, hata hivyo wagonjwa hao waliripotiwa katika halmashauri tofauti za Mufindi (1) na Iringa Mjini (1).

Amesema kwa Mkoa wa Dar Es Salaam ambapo ugonjwa ulidumu sana kwa muda wa miezi 4 na baadae kutoweka kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa umeanza tena kuripoti wagonjwa kwa  wiki iliyopita mkoani Dar es salaam waliripotiwa wagonjwa 6 ambao walitokea Manispaa ya Temeke.

Aidha amesema  mikoa ambayo imeripoti kuwa na wagonjwa kwa wiki iliyopita ni 11 ikiongozwa na Iringa 199 (Halmashauri ya Iringa Vijijini 199)  ikifuatiwa na Mkoa wa Mwanza 87 (Ilemela 31, Ukerewe 26, Nyamagana 15, Buchosya 11 na Sengerema 4), Mara 84 (Musoma mjini 36, Tarime vijijini 17, Musoma Vijijini 12, Butiama 10, Tarime Mjini 5 na Rorya 1). Mikoa mingine ni pamoja na Morogoro 54, Arusha 49, Simiyu 16, Dodoma 11, Mbeya 8, Kilimanjaro 8, Dar es salaam 6 na Manyara 6.


Wizara imekuwa ikikabiliana  na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na mwitikio mdogo wa jamii katika kudhibiti ugonjwa hasa kwenye suala la usafi wa mazingira na vyoo, pamoja utumiaji wa maji safi na salama. Hii ni pamoja na kufuata sheria ndogo ndogo zilizowekwa na jamii husika katika kuhakikisha suala zima la usafi.

Hata hivyo Ummy, amesema uelewa mdogo wa jamii kuhusu sababu zinazochangia kuwepo kwa ugonjwa wa kipindupindu pamoja na mila potofu zimekuwa ni changamoto katika swala zima la kumaliza ugonjwa huu, kama ilivyodhihirishwa huko Kyela mkoani Mbeya ambako mila potofu zimehusishwa na sababu za ugonjwa wa kipindupindu na kusababisha vifo kwa watu wasiokuwa na hatia.

Waziri huyo amesisitiza kuwa mikoa na halmashauri zote kutilia mkazo suala la uelimishaji jamii kwa kushirikisha viongozi mbalimbali ikiwa pamoja na ushirikishwaji wa walimu wa shule, viongozi wa dini, kimila  na viongozi wengine wanaokubalika na jamii husika katika kuelimisha na haswa swala la mila potofu.
  
Wizara imeendelea kuchukua hatua mbalimbali  za kudhibiti ugonjwa ikiwa ni  pamoja na kupeleka timu mbalimbali kutoka ngazi ya taifa katika mikoa ambayo bado kuna changamoto ikiwa ni pamoja na Morogoro, Simiyu, Mwanza, Mara, Mbeya na Manyara ili kuweza kushirikiana na mikoa hiyo katika kudhibiti Ugonjwa wa Kipindupindu.

Amesema kutokana na ongezeko la wagonjwa katika Halmashauri ya Iringa Wizara imetuma timu ya wataalamu kushirikiana na timu za mkoa na Halmashauri katika shughuli za kudhibiti ugonjwa huu.

Aidha Wizara ilikwishapeleka dawa na vifaa tiba na juhudi za kupata dawa na vifaa zaidi zinaendelea. Bado naendelea kusisitiza mapambano ya Kipindupindu yanahitaji ushirikishwaji wa ngazi zote mpaka katika ngazi ya kaya hivyo tukishirikiana kwa pamoja tutatokomeza Kipindupindu.

Amesema  kutokana na uzoefu kutoka mikoa ya Dar Es Salaam na Iringa kutoweka na kurudi tena kwa ugonjwa huu, na pia kutokana na ukweli kuwa ugonjwa upo pia katika nchi za jirani, Wizara inasisitiza Mikoa na Wilaya kuendelea kuimarisha mikakati ya kuzuia wa kipindupindu na kuifanya kuwa endelevu.


SOMA VICHWA VYA HABARI KUTOKA MAGAZETI MBALIMBALI ASUBUHI HII

BONAZA LA WAANDISHI DODOMA LAFANA

$
0
0
 Timu ya kuvuta kamba ya waandishi wa habari wanaume wa chama cha waandishi wa habari Dodoma(CPC) wakionyesha umahiri wao wa kuvuta kamba katika bonaza la kuaga na kuukaribisha mwaka 2016 lilodhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Tigo.
 Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima Hamida Ramadhani akishangilia baada ya kufanikiwa kumkamata kuku katika mchezo wa kufukuza kuku uliofanyika kwenye Bonaza hilo.

RAIS wa umoja wa vyama vya waandishi wa habari nchini, Deogratius Nsokolo amewaasa waandishi wa habari wasio na mikataba ya ajira kujiunga kwenye mifuko ya hifadhi ya Jamii ili kujiwekea akiba zitakazokuwa na faida hapo baadae.

Akizungumza katika bonanza la kuukaribisha  mwaka 2016 lililoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma (CPC) na kudhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mikononi ya Tigo, Nsokolo alisema asilimia 80 ya waandishi wa habari nchini hawajaajiriwa.

“Kila moja ana wajibu wa kuhakikisha anajiunga na mifuko ya hifadhi na hata kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (NHIF) ili kuwe na uhakika wa matibabu pale anapougua au familia yake’”alisema Nsokolo
Alitolea mfano katika Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Kigoma wameweza kila mwandishi kujiunga na Mfuko wa LAPF ambapo kiasi cha Sh. 20,000 kinapelekwa kila mwezi.

Hata hivyo alisema kwa upande wa afya, kila mwandishi anaweza kujiunga na mfuko wa Taifa ya bima ya afya kila kwa Sh. 76,800 ataweza kutibiwa yeye na kuwakatia kadi ya matibabu watu wanne.Aidha alisema UTPC inatarajia kuiwezesha Dodoma kuwa na Ofisi ya kisasa kwa ajili ya waandishi wa habari kufanya kazi zao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CPC, Habel Chidawali alisema changamoto kubwa ni waandishi wa habari kukosa ofisi ya kufanyia kazi kwani baadhi ya vyombo vya habari havina ofisi mkoani Dodoma.

NEWZ ALERT;MSANII WA BONGOFLEVA JONI WOKA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Maregehemu Michael Denis a.k.a Joni Woka enzi za uhai wake

Akiongea kwa simu kaka wa marehemu Omari Milay, amesema walipigiwa simu alfajiri ya leo na kujulishwa kuwa Michael Denis  aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa jina la Joni Woka amefariki katika hospitali ya Muhimbili, alipokuwa akipata matibabu ya ajali aliyopata siku ya jana.

Michael Denis a.k.a Joni Woka alipata ajali ya kugongwa na kitu kizito kwenye paji la uso, alipokuwa garage maeneo ya Sinza akitengeneza gari yake, kwa bahati mbaya mtungi wa gesi ukalipuka na moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani,

Tarifa za awali za madaktari zilisema wanahofia kipande hiko kimefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.

Mipango ya mazishi familia imesema inakutana kujadili na mara itakapokamilika watajulisha watu nini kinaendelea.

Msanii John Woka ambaye alikuwa kwenye kundi la Watukutu Family, alijipatia umaarufu kwa nyimbo zake za Sophia, baby gal na nyinginezo, ambazo aliziimba kwa mtindo wa ulevi.

MAGHEMBE APONGEZA JUHUDI ZA KURUDISHA MBWA MWITU SERENGETI.

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) akiongeawakati wa tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) akielekea katika boma la mbwa mwitu kwa ajili ya tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) akikata utepe kuruhusu kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kutoka nje kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.
Wanahabari wakichukua picha mbalimbali wakati mbwa mwitu walipokuwa wakitoka kwenye boma.Kundi la sita la mbwa mwitu 11 wakitoka katika boma maalum katika Hifadhi ya Serengeti.Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi akiongea na wanahabari mara baada ya tukio la kuachiwa kwa mbwa mwitu.Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (MB) akiwa katika picha ya pamoja na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (MB) akisalimiana na Mhifadhi Ashery Loishooki mara baada ya kuwasili katika eneo la Nyasirori, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita katika boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu.Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi (aliyesimama) akitoa neno la ukaribisho kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) katika tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu
.………………………………………………
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amepongeza jitihada zinazofanywa na watafiti kwa kurudisha mbwa mwitu katika Hifadhi ya Taifa Serengeti baada ya kutoweka katika miaka ya tisini. Waziri Maghembe alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki alipokuwa akiachia huru kundi la sita la mbwa 17 waliokuwa wamehifadhiwa katika boma maalum ili kurejea katika makazi yao ya asili.

Profesa Maghembe amesema serikali itaendelea kuwekeza katika eneo la utafiti ili kuwezesha sekta ya uhifadhi nchini kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa. Alisema mabadiliko ya tabia nchi yameathiri sekta nyingi ikiwemo ya uhifadhi na kuwa wanyama wamekuwa wakiathirika na mabadiliko hayo hivyo ni vema uwekezaji mkubwa ukafanyika katika eneo la utafiti ili kujua namna ambavyo uhifadhi unaweza kukabiliana na mabadiliko hayo.

Mradi wa uhifadhi wa mbwa mwitu unalenga kurudisha mbwa mwitu katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambao walitoweka kabisa tangu mwaka 1994 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaweza kubainika kisayansi. Mradi huu unasimamiwa na kuendeshwa na watafiti wa kitanzania.

Tangu kuanza kwa mradi huu mwaka 2011, jumla ya makundi sita ya mbwa mwitu wamesharudishwa ndani ya Hifadhi ya Serengeti. Makundi haya ni pamoja na Vodacom ambapo Kampuni hii ya simu ilifadhili gharama za mradi; Serengeti; Loliondo; Kikwete; Nyasirori na hili la mwisho ambalo lilipewa jina la Markus Borner, mwanasayansi kutoka nchini Ujerumani aliyetumia miaka 35 akifanya shughuli za uhifadhi katika hifadhi ya Serengeti.

Mradi wa mbwa mwitu Serengeti unaendeshwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, TANAPA na Chuo Kikuu cha Glasgow.

Dkt. Kigwangalla atembelea eneo la mafuriko Iringa Mjini.

$
0
0
 Baadhi ya   maeneo yaliyokumbwa na marufiko katika eneo la mashamba ya mbunga lijulikalo kwa jina la Nyalu
 Baadhi ya   maeneo yaliyokumbwa na marufiko katika eneo la mashamba ya mbunga lijulikalo kwa jina la Nyalu
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifyeka majani kwa ajili ya njia kuelea eneo lilikubwana mafuriko katika eneo la mashamba ya mbunga Nyalu.
 
 Rubani wa ndege ya Jeshi la Polisi, Flora Focas akimwokoa mama mjamzito na kumuingiza katika chopa iliyompeleka Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye aliamuru chopa hiyo imchuke mama huyo ili kuokoa miasha yake.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla  akitokea kwenye eneo la pori kwenye  mashamba ya mpunga ya Nyalu kwa ajili ya kuangalia watu waliozingirwa na maji ili wawezekuokolewa . Alikuwa amembatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela.
Akina mama wenye watoto wadogo mtoto wa wiki moja na  miezi miwili kuondoka katika eneo la marufiko katika mashamba ya Nyalu lililopo wilaya  ya Iringa Mjini.(Picha  na MAGRETH KINABO –MAELEZO)
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimwangalia mtoto aliyeugua ugonjwa wa kipindupidu katika kituo cha afya cha Mtakatifu Lucas (Kambi ya ugonjwa huo) kwenye eneo la Mboliboli kutokana na marufiko yaliyotokea katika kijiji cha Idodi, Iringa ambayo yalisomba nyumba na vyoo baada ya mto Ruaha kujaa maji kubadilisha mkondo wake.
Baadhi ya wagonjwa wakiendelea kunywa maji maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu baada ya kukumbwa na ugonjwa  huo katika kambi maalum ya ugonjwa huo   iliyopo katika kituo cha afya cha Mtakatifu Lucas.kwenye wilaya ya Iringa Mjini. 

PRODUCER WA FILAMU YA MPANGO MBAYA STAFORD KIHORE KUTUA NAIJERIA

$
0
0
MTAYARISHAJI na muongozaji wa filamu ambaye pia ni mwasisi wa Mtandao hu FC Staford Kihore anatarajia kutua nchini Naijeria kwa ajili ya kushuhudia utoaji wa tuza za African Magic Views Choice Awards tuzo hizo ambazo zinatarajia kutolewa mwezi March 2016, akiongea na FC Kihore amesema kuwa anatarajia kutoa Lagos tarehe 2 March. 2016.

Mtayarishaji huyo ambaye pia ni muongozaji wa Tmt anakwenda kama mmoja ya watayarishaji wanaogombea tuzo huku yeye akipelekwa na filamu ya Mpango mbaya kazi bora kazi kutoka Swahilihood ikishirikisha wasanii nyota waliopikwa kutoka na mradi mkubwa kabisa wa Tanzania Movie Talent (TMT).

“Nitakuwepo kwa siku kadhaa nchini Naijeria kwa matukio makuu mawili au hata matatu kwanza kabisa ni kushudia utoaji wa tuzo nikishiriki kupitia filamu ya Mpango Mbaya, jambo la pili ni kuonana na kubadilishana mawazo na watengeneza filamu wakubwa kutoka sehemu mbalimbali za Afrika,”anasema Kihore.

Unapomuongelea Staford Kihore ana sifa ya kipekee kwani ndio Producer pekee aliyeweza kuwa mtayarishaji mkubwa wa filamu bila yeye kuwa mwigizaji kama historia ya watayarishaji wengi wa Swahilihood ambao wengi ni waigizaji mtayarishaji huyu amekuwa ndio mtayarishaji wa kwanza kutengeneza filamu za bajeti kubwa.

Na unapoongelea miradi mingi sana ya tasnia ya filamu Swahilihood hususani project za Filamucentral anahusika sana kama tuzo za BORA 2010, DAR FILAMU FESTIVAL (DFF 2013) ni mratibu na mwasisi pia sisi menejimenti ya FC tunajivuania mtu muhimu sana kwa maendeleo ya tasnia ya filamu Bongo.

Mwaka 2010 aliweza kutengenza filamu ya CPU kazi ambayo iliamsha ari kwa baadhi ya watengnezaji wa sinema kujiamini na kuazna kufuata nyayo zake kwani sinema hiyo iliweza kuonyeshwa katika majumba ya sinema na kushangiliwa sana na watazamaji, kila mara ukiongea Staford ni mtu anayependa mapinduzi katika tasnia ya filamu.

“Naweza kusema tasnia inapiga hatua na kila sehemu nayokwenda kwa safari za kikazi nafanya utafiti utakaoleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu na kuwa Industry kubwa Afika kila mtu awajibike alipo,”Kihore.

Ni matarajio yetu sisi kama wadau wakubwa wa tasnia ya filamu Swahilihood kuwa Kihore anapokkwenda Naijeria anarudi na ushindi mkubwa sambamba na tuzo FC inamtakia kila heri katika kupigania tasnia ya filamu Swahilihood.

WAZIRI MBARAWA ASISITIZA UKUSANYAJI WA MAPATO KATIKA SEKTA YA MIUNDOMBINU.

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na mkandarasi Nyanza Road Works anayejenga barabara ya Bulyamba-Kisolya yenye urefu wa Km 51. (Wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bw. Joshua Mirumbe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisolya kuhusu ujenzi wa mradi wa barabara ya Bulyamba-Kisolya yenye urefu wa Km 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Muonekano wa barabara ya Bulyamba-Kisolya yenye urefu wa Km 51 inayojengwa kwa kiwango cha lami ambayo ni sehemu ya barabara ya Nyamuswa-Bunda hadi Nansio Km 121.9.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Emmanuel Koroso (wa pili kulia) wakati akikagua daraja la Kyarano linalounganisha barabara ya Makutano-Nata- Mto wa Mbu yenye urefu wa Km 467.7.
Muonekano wa daraja la Kyarano linalounganisha barabara ya Makutano-Nata- Mto wa Mbu yenye urefu wa Km 467.7 likiwa katika hatua za ujenzi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na watumishi wa sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (hawapo pichani) kuhusu kufanya kazi kwa umoja na kuongeza mapato katika sekta zao, mkoani Mara.
Meneja wa uwanja wa ndege wa Musoma Bi. Bertha Bankwa akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika mkutano wa watumishi wa sekta zilizo chini ya Wizara hiyo.
Daraja la reli linaloingia baharini katika bandari ya Musoma kupokea na kupakia mizigo kwenye melikwa ajili ya kuisafirisha katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

…………………………………………………………………………………………………

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka watendaji walio chini ya Wizara yake kuongeza kasi ya kukusanya mapato ili kuwezesha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi kufikiwa kwa wakati.

Akizungumza na watumishi wa sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino mjini Musoma, Prof. Makame Mbarawa amesema kufanya kazi kwa umoja, uadilifu, uwazi na ubunifu kutasababisha kufikiwa kwa malengo hayo mapema.

“Kama mtu hawezi kufanya kazi kwa kasi na kwa malengo yanayotekelezeka na kupimika atupishe kabla hatujamuondoa, hatuta muonea mtu na hatutamvumilia mtu atakayeshindwa kuendana na kasi yetu”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema Serikali imetenga zaidi ya dola milioni 30 kwa ajili ya kukarabati uwanja wa ndege wa Musoma na kununua magari ya kisasa ya zimamoto ili kurudisha hadhi ya uwanja huo.

Aidha, amezitaka taasisi za Serikali zinazodaiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mkoani Mara kulipa madeni yao ili kuuwezesha wakala huo kufanya kazi kwa kasi na kufikia malengo yaliyowekwa.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Makutano-Nata-Mto wa Mbu yenye urefu wa km 467.7 inayojengwa na makandarasi wazalendo kumi na kutaka mkandarasi anayejenga kipande cha km50 kutoka Makutano hadi Sanzate kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa haraka ikiwemo daraja la kyarano ili kuiwezesha barabara hiyo kupitika wakati wote wa mwaka.

Amemwagiza Meneja Wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa Mara Eng. Emmanuel Koroso kuhakikisha makandarasi wanaojenga barabara mkoani humo wanarejea kazini kwa kuwa serikali imeanza kulipa madai yao.

Ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kutumia fedha zilizotumwa kutoka Mfuko wa Barabara (RFB) kutumika kwa miradi iliyokusudiwa ili kuingunisha wilaya hiyo mpya na wilaya nyingine mkoani Mara kwa barabara za lami.

Akiwa wilayani Bunda Prof. Mbarawa amemtaka mkandarasi Nyanza Road Works anayejenga barabara ya Buliamba-Kisolya Km 51 kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo kwa mujibu wa mkataba kwani serikali imeshalipa fedha shilingi bilioni 8.5 kwa ajili ya barabara hiyo ambayo ni sehemu ya barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisolya-Nansio yenye urefu wa Km 121.9.

Aidha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Mbarawa amewataka viongozi wa Wilaya za Magu, Bunda na Musoma kufanya kampeni kubwa ya kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kulinda Miundombinu ya Barabara, Reli na Mkongo wa taifa wa Mawasiliano ili isihujumiwe na kusababisha usumbufu kwa jamii na kuisababishia serikali hasara.

Naye, Mbunge wa Mwibara Mhe. Kangi Lugola amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa kukamilika kwa barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisolya hadi Nansio yenye urefu wa KM 121.9 itasaidia kukuza uchumi wa Wilaya ya Bunda na Ukerewe kwa kuwa eneo hilo lina shughuli nyingi za uchumi zinazotokana na kilimo, ufugaji na uvuvi wa Samaki.

Prof. Mbarawa amewataka makandarasi wote nchini kuhakikisha wanawapa wafanyakazi wao mikataba kulingana na sheria za nchi ili kuwezesha miradi ya barabara inayoendelea kujengwa kukamilika kwa wakati na kuondokana na hujuma zinazoweza kudhoofisha ujenzi wa barabara na miundombinu mingine.

“Lindeni miundombinu ili idumu kwa muda mrefu, barabara, reli na mkongo wa taifa ni miongoni mwa miundombinu inayojengwa kwa fedha nyingi na kuhujumiwa mara kwa mara hivyo kuisababishia Serikali hasara”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa yupo kwenye ziara ya kukagua Ujenzi wa miundombinu ya barabara, bandari na mkongo wa taifa wa mawasiliano katika mikoa ya kanda ya ziwa ambapo ametembelea Wilaya za Magu, Bunda, Butiama na Musoma

NHIF KIGOMA WAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI AFYA WANANCHI BURE.

$
0
0
Baadhi ya wakazi wa Kigoma wakijiandikisha tayari kwa upimaji afya zao bure katika viwanja vya mwanga center.

Mkazi wa Kigoma mjini akipimwa shinikizo la damu(BP) katika viwanja vya mwanga center zoezi linaloendeshwa bure na mfuko wa bima ya afya(NHIF).
Mkazi wa kigoma akichukuliwa vipimo kwaajili ya kupima ugonjwa kisukari
Meneja wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kigoma Elias Odhiambo akiongea na waandishi juu zoezi hilo la upimaji wa wananchi afya zao bure.

Na Editha Karlo,wa blog ya jamii Kigoma

WANANCHI wa MKoa wa Kigoma wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya mwanga center katika zoezi la upimaji wa afya bure, zoezi linaloratibiwa na ofisi ya mfuko wa bima ya afya Kigoma wakishirikiana na makao makuu ya mfuko huo. 

Meneja wa mfuko wa Bima ya afya Mkoa wa Kigoma Elias odhiambo alisema kuwa zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku tano na watapima maradhi mbalimbali ikiwemo shinikizo la damu(BP) sukari, urefu, uzito na ukimwi na watakao kuwa na matatizo watapatiwa ushauri wa kitaalam. 

Alisema zoezi hilo ni sehemu ya majukumu ya mfuko ya kuwahudumia wananchi lakini pia wanaendelea kuwahamasisha wananchi kujounga na mfuko huo ili wawe na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao. 

Alisema lengo lao ni kuwafikia wakazi mia saba katika maeneo ya mjini hivyo aliwataka wakazi wa Kigoma kujitokeza kwa wingi kupima afya zao. 

Naye mkazi wa eneo la. Majengo mjini hapa Faudhia Hamis aliupongeza uongozi wa mfuko huo lwa kuendesha zoezi hilo la kuwataka wananchi kutambua afya zao. 

"Kwa moyo wa dhati naupongeza sana uongozi wa mfuko wa Bima ya afya kwa zoezi hili wamefanya jambo zuri ninawaomba zoezi hili lisihishie hapa mjini waende na vijijini kule kuna changamoto sana za huduma ya afya

Ninawasihi wananchi wenzangu wajitokeze ili tuitumie fursa hii vizuri ya kujua afya zetu"alisema mwananchi huyo

WAZIRI MUHONGO AZITAKA TAASISI KUONGEZA KASI YA MIRADI YA UMEME NCHINI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Kibo Mining, Louis Coetzee ( wa pili kutoka kulia) akielezea mikakati ya kampuni hiyo katika uwekezaji wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia makaa ya mawe mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( kulia) akimweleza Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Kibo Mining, Louis Coetzee (kushoto) fursa za uwekezaji nchini kwenye sekta ya umeme.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo katika kikao hicho
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Kibo Mining, Louis Coetzee akifafanua jambo katika kikao hicho.
………………………
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amezitaka taasisi zinazosimamia miradi ya umeme nchini kuongeza kasi ya utendaji kazi ili Tanzania iweze kupata umeme wa uhakika.

Profesa Muhongo aliyasema hayo katika kikao chake kilichokutanisha Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Kibo Mining na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wizara ya Nishati na Madini.

Alisema kuwa ili nchi iweze kuwa na umeme wa uhakika unaozalishwa kwa wakati ni lazima taasisi zilizopo chini ya Wizara zikahakikisha zinaongeza kasi katika uwekezaji kwenye uzalishaji wa umeme kwa kushirikiana na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wenye vigezo ili uchumi wa nchi uweze kukua kwa kasi na kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025 ambayo ni kuhakikisha kuwa nchi inatoka katika kundi la nchi masikini duniani na kuingia katika kundi la nchi zenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Alisisitiza kuwa ili kufikia lengo hilo ni lazima taasisi zikaongeza kasi katika miradi yake ya umeme, kwa kushirikiana na wawekezaji mbalimbali na kuwataka kuondoa urasimu kwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye miradi ya uzalishaji wa umeme nchini.

Aliongeza kuwa nishati ni roho ya uchumi wa nchi na kusisitiza kuwa hakuna nchi yoyote duniani iliyopiga hatua bila kuwa na nishati ya umeme ya uhakika.

“ Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha kuwa sekta ya viwanda inakua kwa kasi na kutoa ajira hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo nishati ya umeme inahitajika sana; bila nishati ya uhakika uchumi hauwezi kukua kwa kasi inayotakiwa,’ alisisitiza Profesa Muhongo.

Waziri Muhongo aliendelea kusema kuwa nishati ya umeme ya uhakika itachangia ukuaji wa sekta za viwanda vidogo hasa maeneo ya vijijini, kilimo kukua kwa kasi na hivyo kunufaisha wananchi na pato la taifa kukua kwa kasi.

Aidha Profesa Muhongo alilitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kushirikiana kwa pamoja katika hatua zote za uwekezaji nchini ili kuondoa mkanganyiko unaoweza kujitokeza kati ya serikali na wawekezaji.

“TANESCO na EWURA naomba mshirikiane katika kila hatua, kwa kukaa meza moja na wawekezaji na kufikia mwafaka kabla hawajaanza kuwekeza”, alisema Profesa Muhongo

Awali Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Kibo Mining, Louis Coetzee akizungumza katika kikao hicho, alisema kuwa kampuni ya Kibo Mining ina mpango wa kuwekeza katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia makaa ya mawe ambapo itaanza na ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe wa Megawati 900 kwa awamu tofauti.

Alisema awamu ya kwanza ambayo ni ujenzi wa mtambo wa kuzalisha Megawati 300 utakaogharimu Dola za Marekani milioni 800 utakamilika ifikapo mwaka 2019.

Akielezea hatua iliyofikia ya maandalizi ya uwekezaji wa kampuni ya Kibo Mining Coetzee alisema kuwa kampuni hiyo iliyoanza maandalizi yake mwaka 2008 inakamilisha upembuzi yakinifu (feasibility study) katika mradi wake na kuongeza kuwa wana mpango wa kuanza ujenzi wa awamu ya kwanza mwaka 2017 baada ya taratibu zote kukamilika.

Alisema mara baada ya ujenzi wa mtambo wa kwanza kukamilika mwaka 2019, umeme utakaozalishwa mbali na kutumika viwandani utaongezwa kwenye gridi ya taifa na hivyo kupunguza changamoto ya ukosefu wa umeme nchini.

Wafanyakazi wa AICC wala kiapo cha Uadilifu

$
0
0
 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), ndugu Elishilia Kaaya akiongea na wafanyakazi kabla ya kuapa na kujaza fomu za  ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa Umma. Katikati ni Mkurugenzi wa Fedha na  Utawala wa AICC, ndugu Savo Mungóngó na kulia ni Afisa Maadili wa Sekretarieti  ya Maadili ya Viongozi Umma, ndugu Hendry Sawe.
 Wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) wakila kiapo  cha Uadilifu kabla ya kujaza fomu za ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa Umma.
 Afisa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Umma ndugu Hendry Sawe  akitoa mada juu ya Maadili kwa Viongozi wa Umma na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa Umma muda mfupi kabla ya wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kujaza fomu za ahadi ya uadilifu.



Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), ndugu Elishilia Kaaya akiweka saini fomu za ahadi ya uadilifu za baadhi ya Wafanyakazi wa AICC baada ya wafanyakazi hao kuapa na kuzijaza.

Marehemu Clara Pius Msekwa apumzishwa katika Nyumba yake ya Milele

$
0
0
Jeneza lenye mwili wa marehemu Clara Pius Msekwa likiwasili nyumbani kwa Mama yake mkubwa Kimara , Korogwe kabla ya ibada ya kumuombea marehemu na kupelekwa kuzikwa katika makaburi ya Mburahati Jijini Dar Es Salaam.
Ibada ya Kumuombea Marehemu Clara Pius Msekwa ikiendelea nyumbani Kwa mama mkubwa wa marehemu maeneo ya Kimara Korogwe kabla ya kwenda kupumzishwa katika nyumba yake ya Milele katika makaburi ya Mburahati jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mfanyakazi wa Proin Group, Emmanuel Mdinka akipita pembeni ya jeneza lenye mwili wa marehemu Clara Pius Msekwa Kwaajili ya kutoa heshima zake za mwisho kabla ya kupelekwa kupumzishwa katika nyumba yake ya Milele katika Makaburi ya Mburahati. 
Waliokuwa wafanyakazi wenzake na marehemu Clara Pius Msekwa wakitoa heshima zao za mwisho.

 
Mama mkubwa wa marehemu Clara Pius Msekwa akilia kwa uchungu mara baada ya kutoka kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu Clara Pius Msekwa
Ndugu, jamaa, marafiki na waliokuwa wafanyakazi wenzake na marehemu wakitoka kutoa heshima zao za mwisho katika jeneza lenye mwili wa marehemu Clara Pius Msekwa ambae alikua mfanyakazi wa Kampuni ya Proin Group Limited.
Baadhi ya wafanyakazi wenzie na marehemu Clara Pius Msekwa wakiwa na majonzi ya kuondokewa na Mfanyakazi mwenzao
 Jeneza lenye mwili wa marehemu Clara Pius Msekwa likiwasili katika Makaburi ya Mburahati tayari kwa kumpumzisha Marehemu Clara Pius Msekwa.
Sala ya kumuombea Marehemu Clara Pius Msekwa kabla ya kuzikwa ikiendelea
Jeneza lenye mwili wa marehemu Clara Pius Msekwa likiingizwa katika kaburi tayari kwa kuzikwa.
 Ndugu, marafiki pamoja na waliokuwa wafanyakazi wenzake na marehemu Clara Pius Msekwa wakiweka mashada ya maua juu ya kaburi ya marehemu Clara Pius Msekwa katika makaburi ya Mburahati.
Marehemu Clara Pius Msekwa alifariki dunia mnamo tarehe 11-02-2016 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili mara baada ya kuugua kwa muda, Marehemu Clara alikua akisumbuliwa na ugonjwa wa mapafu kujaa maji hali iliyopelekea kuteseka kwa muda akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi mpaka hapo mauti yalipomfika.
Marehemu Clara Pius Msekwa alikua mfanyakazi wa kampuni ya Proin Group limited ambapo aliwahi pia kufanya kazi katika kampuni ya Zantel na kabla aliwahi kuwa mwalimu wa shule ya awali. 
Kampuni ya Proin group inapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wote walioweza kushirikiana katika kuokoa maisha yake tokea alipokuwa mgonjwa lakini kwa bahati Mungu ameweza kumchukua Mja wake. 
Vilevile Proin inapenda kuwashukuru wale wote walioshirikiana nao katika msiba huu mzito ulioikimba familia yake, ofisi yake na hata marafiki zake kwa kuweza kuwa sehemu ya faraja kwetu.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Clara Pius Msekwa mahala pema peponi Amen

PROFESA NDALICHAKO ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI WA BODI YA MIKOPO, NA WATATU WASIMAMISHWA

$
0
0
WaziriwaElimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof.Joyce Ndalichako akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Tarishi Maimuna Kibenga. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Na CHalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mteandaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB), George Nyatage kutokana na kuwepo na ukiukaji wa utoaji wa mikopo pamoja na ucheleweshaji usio kuwa na sababu za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Profesa Ndalichako amesema kuwa bodi ya mikopo imekuwa na malalamiko  mengi kutoka kwa wanafunzi wanaostahili kupata mikopo ya kufanya kwao kuweza kupata mikopo mpaka waandamane wizarani kwa kusababishwa na watu wa wachache wa bodi hiyo.

Kutokana na udhaifu wa kiutendaji wa bodi hiyo baada ya kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji, watendaji watatu wa bodi hiyo wamesimamishwa kazi ambao ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji wa Mikopo, Juma Chagonja pamoja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo, Onesmo Laizer.

Profesa Ndalichako, amesema katika udhaifu wa utendaji huo ni pamoja ni ulipaji wa mikopo kwa wanafunzi 23 walilipwa katika vyuo viwili tofauti  kwa miaka mitatu mfululizo kwa chuo cha kwanza zililipwa zaidi ya sh.milioni 653 na chuo cha pili ni zaidi ya  sh. milioni 147.

Amesema baadhi ya wanafunzi ambao walikwenda kusoma nchini    Algeria wamekuwa wakiendelea kulipwa fedha wakati mkataba wao umekwisha kwa kipindi cha miaka saba.

Profesa Ndalichako amesema wanafunzi 169 walipata mikopo katika vyuo viwili tofauti kwa miaka mitatu mfululizo na kulipa chuo cha kwanza zaidi ya sh.milioni 658 na chuo cha pili zaidi ya sh. milioni 665 na wanafunzi 55 walioacha masomo walilipwa zaidi ya sh.milioni 136 huku wanafunzi 343 wasiokuwa na usajili kwenye vyuo husika walilipwa zaidi ya sh.milioni 342.

Aliongeza kuwa zaidi ya sh.milioni 159 zililipwa kwa wanafunzi 306 zaidi ya kiwango kilichobainishwa kutokana na muongozo wa upangaji na ukopeshaji wa mwaka 2008/2009 na 2009/2010.

Aidha amesema kuwa wanafunzi 77 walipatiwa mikopo kwenye vyuo vya ndani na nje ya nchi kwa wakati mmoja ambapo walilipwa zaidi ya sh.milioni 467 kwa vyuo nje na zaidi ya sh.milioni 123 kwa vyuo ndani pamoja na wanafunzi 19,348 walipata mikopo bila kupitiwa na kamati ya mikopo jambo ambalo ni kinyume na kanuni na 8ya kanuni za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Hata hivyo amesema wanafunzi 54,299 walipangiwa mikopo wakati hawakuwa wameomba ambapo walilipwa zaidi y ash.milioni 207 ambazo zilipelekwa kwenye vyuo sita.

NRA kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar

$
0
0
  Katibu Mkuu Chama cha NRA Tanzania Bara Hassan Almasi Kisabya (wa pili kushoto) akitoa tamko la chama chake kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar March 20 ya waandishi wa Habari(Hawapo Pichani)leo Jijini Dare s salaam katika ukumbi wa Habari Maelezo.
Baaadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano ulioitishwa na Chama cha NRA kuelezea ushiriki wao katika uchaguzi wa marudio Zanzibar.
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO 

Na Nyakongo Manyama MAELEZO

Chama Cha National Reconstruction Alliance (NRA) kutoka Zanzibar kimethibitisha kushiriki uchaguzi wa marudio wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Machi 20, mwaka huu baada ya kikao kilichofanyika Februari 15.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Tanzania Bara Hassan Almasi Kisabya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa Chama hicho kitashiriki uchaguzi wa marudio na kusisitiza kuwa tamko lililotolewa na mgombea wao la kutoshiriki uchaguzi wa marudio lipuuzwe kwani ni tamko lake binafsi na sio msimamo wa chama.

“Tamko lililotolewa tarehe 14/02/2016 Si Tamko la chama cha NRA bali ni tamko binafsi na wale waliomuagiza kwani yeye hana mamlaka ya kukisemea chama wala wagombea wengine wa chama pasipo Baraka na vikao halali vya chama” alisema Kisabya.

Amesisitiza  kuwa maamuzi ya chama ni sharti yatoke katika chama na sio kwa mgombea na ikiwa yeye amejitoa anatakiwa afuate taratibu za kisheria katika kujitoa kama alivyofuata sheria katika kugombea nafasi hiyo.

Aidha, Chama kinatoa taarifa kwa wagombea wote Zanzibar kujiandaa na wapiga kura kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20, mwaka huu ili kutimiza haki yao kikatiba na kuchagua viongozi wao kwa kipindi cha miaka mitano ijayo

Chama cha NRA ni miongoni mwa vyama 14 vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa  Oktoba 25 mwaka jana katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofutwa kwa nafasi ya Rais.

BOMBA KUBWA LA KUSAMBAZIA MAJI KUTOKA CHANZO CHA MAJI CHA RUVU CHINI LAFIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mafundi wakiendelea na kazi ya kulaza mabomba ya Maji eneo la Mbezi Beach jijini Dar es salaam. Mabomba hayo ambayo sasa yamekamilika kwa urefu wa kilometa 54.8 kati ya 55.9 yatatumika kusafirisha maji kutoka mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini, Bagamoyo mkoani Pwani.

Mkurugenzi wa Usimamizi na Ufundi wa DAWASA, Romanus Mwang’ingo (katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya Mradi wa ujenzi  wa bomba hilo la kusafirishia Maji kutoka Ruvu Chini  kuelekea matangi ya kuhifadhia maji ya Chuo Kikuu cha Ardhi ambao umefika eneo la Mbezi Beach jijini Dar es salaam
Maneja wa Kampuni ya Gauff Consultants, Thorsten Seitz akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu maendeleo ya Mradi wa ujenzi  wa bomba hilo la kusafirishia Maji kutoka Ruvu Chini.

( Na. Aron Msigwa - Dar es salaam)

Huduma ya Usambazaji wa Maji Safi katika jiji la Dar es salaam inatarajiwa kuimarika kwa kuwafikia wananchi wengi zaidi mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu kufuatia kukamilika kwa kilometa 54.8 za mradi wa Ujenzi wa Bomba kubwa la kusambazia Maji kutoka chanzo cha Maji cha Ruvu Chini.



Mradi huo unajengwa na Kampuni ya JBG Gauff Ingenieure kwa gharama ya shilingi Bilioni 141 ambazo zimetolewa na Serikali ya Tanzania una jumla ya urefu wa kilometa 55.9. 


Akizungumzia mradi huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Usimamizi na Ufundi wa DAWASA, Romanus Mwang’ingo amesema kuwa mpaka sasa ujenzi wa bomba hilo kuelekea matangi ya kuhifadhia maji ya Chuo Kikuu cha Ardhi umefika eneo la Mbezi Beach jijini Dar es salaam na huku ikiwa imebakiza kilometa 1.1.

 Amesema ujenzi wa mradi huo kutoka mtambo wa Ruvu Chini ndiyo utakuwa suluhisho la tatizo la maji katika jiji la Dar es Salaam na maeneo ya mkoa wa Pwani na kuongeza kuwa utakapokamilika utazalisha lita milioni 270 kwa siku kutoka lita milioni 182 ambazo zote zitasukumwa kuja jijini Dar es salaam.

 Aidha, amesema kasi ya mkandarasi ya kulaza bomba hilo inaridhisha licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazochelewesha kazi hiyo zikiwemo za ufinyu wa eneo linapojengwa bomba hilo kuwezesha mitambo kufanya kazi vizuri katika eneo la mbezi Beach, mvua zinazoendelea kunyesha ,changamoto ya makazi ya watu kuwa ndani ya mradi ambapo kulikuwa na kesi 17 Mahakamani zikihusisha madai mbalimbali ya wananchi katika maeneo hayo.

“Ni kweli zipo changamoto zilizosababisha mradi kukawia kumalizika zikiwemo za wananchi kufungua kesi 17  Mahakama ya Ardhi, hadi sasa DAWASA tumeshinda kesi 14  ndiyo maana tumepata haki ya kutumia njia hii kukamilisha upanuzi wa mradi” Amesema Mwang’ingo.

Ameongeza kuwa lengo la mradi huu nikuongeza uzalishaji wa maji na kuboresha huduma kwa wakazi wa maeneo ya uwekezaji (EPZ) Bagamoyo, Chasimba, Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa wa Pwani. 

Maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huo kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Bunju, Wazo, Salasala, Madale na Kinzudi Mbezi Juu, Goba, Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani, Mikocheni, Mlalakua, Masaki, Sinza, Kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni, Kigogo na Vingunguti.

Kwa upande wake Meneja Mradi wa Kampuni inajenga bomba hilo nchini Muhandisi Eric Omuruli akizungumzia mradi huo amesema kuwa yeye kama Meneja mradi atahakikisha anashughulikia changamoto zilizopo ili kukamilisha kwa wakati.

Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika eneo la mradi hasa eneo la Mbezi Beach jijini Dar es salaam kampuni ya JBG Gauff Ingenieure inafanya kila linalowezekana ili mradi huo ukamilike mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.

“Tumejipanga kufanya kazi hadi usiku kupunguza muda,kazi iliyobaki ni ndogo, tunawahakikishia DAWASA tutaimaliza kazi hii mwishoni mwa mwezi huu” Amesisitiza.

UJENZI WA BARABARA YA MWENGE MPAKA MOROCCO WAENDELEA KWA KASI

$
0
0
Mafundi wakijengea bomba la maji eneo la Makumbusho kwa kuliwekea zege na nondo ili kulihakikishia usalama wake wakati wa ujenzi wa barabara ya Mwenge-Morocco inayotarajiwa kukamilika mapema mwezi Mei mwaka huu.
Sehemu ya Barabara ya Morocco kwenda Mwenge ikiwa katika hatua ya kutolewa tabaka ya udongo wa chini na kuwekwa tabaka ya udongo mpya kama inavyooenekana katika picha leo jijini Dar es Salaam .
Mafundi kutoka kampuni ya Ujenzi ya ESTIM wakiwa kazini katika hatua ya kutoa udongo wa chini kwa ajili ya kuweka udongo mpya ,ambapo ujnzi huo unatarajiwa kumalika mapema Mei mwaka huu.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

SHIRIKA LA KIMATAIFA LA DKT INTERNATIONAL LAZINDUA “FIESTA CONDOMS” NCHINI TANZANIA

$
0
0
Wanandoa mbalimbali wakishiriki kwenye michezo inayohamasiha upendo na mshikamano wakati wa maandalizi ya kusherekea siku ya wapendano ambayo iliambatana na uzinduzi rasmi wa chapa mpya za “Fiesta condoms” nchini Tanzania. Uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ledger Plaza, Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Mkurungezi wa shirika la DKT International Tanzania Raphael Da Silva akizungumza machache kwenye uzinduzi wa chapa mpya ya shirika hilo “Fiesta condoms” katika soko la Tanzania uliofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ledger Plaza, Kunduchi jijini Dar es salaam.
Meneja Masoko wa shirika la DKT International Tanzania Bw. Davis Kambi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa wa uzinduzi rasmi wa “Fiesta condoms” nchini Tanzania uliofanyika hoteli ya kitalii ya Ledger Plaza, Kunduchi jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.

Meneja Masoko wa shirika la DKT International Tanzania Bw. Davis Kambi (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa bahati nasibu iliyochezeshwa na shirika hilo wakati wa uzinduzi wa “Fiesta condoms” nchini Tanzania uliofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ledger Plaza jijini Dar es salaam. Washindi hao walijishindia safari za mapumziko kuelekea Zanzibar, Cape town na Dubai.


Shirika la kimataifa la DKT, linalojihusisha na elimu ya uzazi wa mpango pamoja na vita dhidi maambukizi ya VVU na UKIMWI, hivi leo limezindua kondomu za Fiesta katika soko la Tanzania.

Kondomu za Fiesta zimekuwa sokoni kwa zaidi ya miaka 20 na zinapatikana nchi zaidi ya 40 duniani kote. Uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Ledger Plaza maeneo ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huu umekuja kipindi kifupi kabla ya sikukuu ya wapendanao duniani ya Valentine ambayo pia ni siku ya kimataifa ya uelewa wa kondomu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, meneja masoko wa DKT International nchini Tanzania, Bwana Davis Kambi alisema anaamini ni muda muafaka kwa chapa hii kupatikana katika soko la Tanzania.

“Huu ndo utambulisho rasmi wa chapa hii Tanzania ikiwa kama njia ya kukabiliana na mahitaji ya wateja wetu na kuvutia watumiaji wapya” alisema wakati wa uzinduzi. Pia alisema uzinduzi huo utawapa wapendanao chapa wanayoweza kuiamini na itakayoboresha maisha yao. Wakiwa wameweka mikakati ya kuipa nguvu chapa hii kwa kutumia njia za mawasiliano na ushiriki katika nyanja mbalimbali ili kumrahisishia mtumiaji kuielewa na kuikubali chapa hii kama kitu poa kutumia.

“Kondomu za Fiesta ni mahususi kwa wapendanao ambao husaka raha na hisia kali zaidi. Fiesta ni sherehe yenye nakshi, Fiesta ni kwa ajili ya ukaribu zaidi. Fiesta ni chapa ya kisasa inayoshindana na chapa nyingine za kondomu kubwa kimataifa” alisema Kambi.

Fiesta ina zaidi ya ladha 55 tofauti na zaidi ya aina 60 lakini kwa sasa DKT International Tanzania imetambulisha aina nne tu; Fiesta Heat, Fiesta Ultra-thin, Fiesta Strawberry and Fiesta Max dotted. Aliongezea kwa kusema kuwa shirika linatazamia kuongeza aina tatu (3) zaidi kabla ya kufikia mwisho wa mwaka 2016.

Kambi alisema uzinduzi huu wa kondomu za Fiesta utatengeneza historia kwa kuunga mkono juhudi za kufikia lengo la kuzuia maambukizi ya VVU kabisa. Alisema katika kulinganisha tafiti za VVU ya mwaka 2007-08 na Malaria 2011-12 nchini Tanzania, wamebaini kuwa maambukizi ya VVU yamepungua kutoka asilimia 5.7 hadi asilimia 5.1 kati ya watu wenye miaka 15-49. Vivyo hivyo maambukizi yamepungua kwa wanawake kutoka asilimia 6.6 hadi 6.2 na kwa wanaume kutoka asilimia 4.6 hadi 3.8 na kama shirika linalopambana na VVU na UKIMWI katika dhana zote wanaendelea kuona haja ya kupunguza uenezaji wa gonjwa hili.

Aliwashauri watu wakumbuke kuwa kondomu husaidiaa kuzuia maambukizi ya VVU na hivyo ni muhimu kutumia. Aidha Kambi aliasa kuwa ni muhimu kondomu kupatikana kiurahisi na kwa bei poa ili kuvutia watumiaji wengi kitaifa.

Alielezea zaidi kwamba Fiesta zitapatikana kwa bei ya rejareja ya shilingi 1500 za Kitanzania ambayo ni kwa paketi ya kondomu tatu ambayo kiuhalisia ni bei rahisi kwa chapa ya kimataifa. Kwanzia mwezi huu zitapatikana maduka ya madawa, maduka makubwa ya rejareja, hoteli, gesti na klabu za usiku kubwa nchini kote. Alisema pia kwamba wanafanya kampeni maalum ya kuitambulisha zaidi Fiesta kwa soko la Tanzania.

Vyama vya Siasa Nchini Vyatakiwa Kuheshimu Katiba na Kanuni Zake

$
0
0

Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Mhe. JaJi Francis S.K. Mutungi amevitaka vyama vya Siasa nchini kuhakikisha kuwa Katiba na Kanuni za Vyama vya Siasa zinaheshimiwa na kufuatwa katika utendaji wa kila siku wa chama cha siasa ili kuepuka migogoro na migongano ndani ya vyama.  Hayo ameyabainisha kwenye barua yenye Kumb. Na. HA.322/362/01/103 aliyoiandikia vyama vya siasa mapema leo.

“Nimeona ni vyema nitumie fursa hii kuviasa Vyama vya Siasa kuhusu hali hii, kwani hali hii ya kufanya mambo kiholela pasipo kufuata Katiba na Kanuni kama itaachwa iendelee hivi ndani ya vyama kwa hakika italeta migogoro na mipasuko mikubwa ndani ya Vyama vya Siasa husika.”

“Wakati huu ambapo nchi yetu inasubiri marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, nimeandikiwa barua na pia kupata nakala za barua kutoka kwa baadhi ya Vyama vya Siasa kuhusu migongano ya wanachama na viongozi au viongozi wenyewe kwa wenyewe kuhusu suala la kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar. “alisema Jaji Mutungi
Barua hiyo ilibainisha  kuwa suala hilo la migongano limejitokeza pia kwa wingi kwenye Vyombo vya Habari, ambapo wanachama na viongozi au viongozi wenyewe kwa wenyewe wametofautiana na kupingana hadharani.

Jaji Mutungi amesema kwa mujibu wa Kanuni ya 3(1) ya kanuni za Usajili wa Vyama vya Siasa za mwaka 1992 (GN.No. 111) Vyama vya Siasa vinaposajiliwa vinapaswa kuwasilisha Katiba na Kanuni zake kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

“Ikumbukwe kwamba, suala la msingi hapa ni kwamba,sharti la kuwepo kwa Katiba na Kanuni katika chama, kimsingi ni mwendelezo wa kukuza na kudumisha dhana ya kuendesha Vyama kitaasisi kulingana na mwongozo uliokubalika na kuasisiwa kichama kwa mfumo wa Katiba na Kanuni za chama na si kuendesha chama kiholela kama inavyoelekea kuota mizizi kwa baadhi ya Vyama vya Siasa hivi sasa.”ameongeza Jaji Mutungi

 Jaji Mutungi amevisihi Vyama vyote vya Siasa, kuhakikisha kwamba matamko ya chama hususan yahusuyo msimamo wa chama kuhusu jambo zito la kisera, kitaifa n.k., mathalan kama lilivyo la uchaguzi huu wa Zanzibar basi yatolewe rasmi na mtu mwenye mamlaka ya kuongea kwa niaba ya chama. Na endapo kuna mwananchama au kiongozi ambaye ataenda kinyume achukuliwe hatua haraka iwezekanavyo na chama husika kwa kuzingatia   katiba na kanuni zake ili kuepusha sitofahamu inayokuwa imejitokeza katika jamii.

“Ni vyema misimamo kama hiyo ya chama itokane pia na vikao halali vya chama na siyo matakwa ya kiongozi mmoja au mwanachama mmoja au wachache.  Vinginevyo kama tutapeleka na kufanya uendeshaji wa vyama kiholela tutachangia kuwachanganya wananchi na kupoteza kabisa imani na heshima ya Jamii iliyokuwa imeanza kujengeka kwa Vyama vya Siasa”. Amesisitiza Jaji Mutungi

Aidha vyama vvya Siasa vimeaswa kuchua hatua  ya haraka iwezekanavyo kwa mwanachama au kiongozi  wa chama anayefanya mawasiliano ama kutoa matamko bila idhini ya mamlaka na pia vyama  vimeonywa kutowajengea wananchi tashwira ya kwamba kuna makundi yanagombania madaraka  na kuendeleza maslahi binafsi  kwa sababu jambo hilo linashusha hadhi ya vyama vya Siasa nchini.

Muhongo ataka watendaji watangulize maslahi ya Taifa.

$
0
0
Wajumbe wa mkutano baina ya Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zilizo chini yake pamoja na muwekezaji, kampuni ya Mkonge Energy Systems (MeS) Ltd ya jijini Tanga. Mikutano baina ya wizara hiyo na wawekezaji wa uzalishaji umeme inaendelea chini ya uenyekiti wa Profesa Sospeter Muhongo.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao chake na muwekezaji kutoka kampuni ya Mkonge Energy Systems (MeS) Limited ya jijini Tanga. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Salum Shamte.
Wawakilishi kutoka kampuni ya Mkonge Energy Systems wakiagana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia). Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya MeS, Juma Shamte akifuatiwa na Mwenyekiti wa MeS, Salum Shamte.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewataka watendaji wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya Taifa.

Aliagiza hayo hivi karibuni katika kikao chake na wawekezaji wa kampuni ya Mkonge Energy Systems (MeS) Limited ya jijini Tanga kupitia kampuni tanzu ya Tanzania Masigira Power Limited (TMPL) ambao wameonesha nia ya kuzalisha umeme kiasi cha Megawati 71 wilayani Songea mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na kampuni ya China ya Sino Hydro Hong Kong Holding Limited (SHKHL) inayomilikiwa na Power China.

Katika kikao hicho Waziri Muhongo Alizitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha wanashirikiana katika majadiliano mbalimbali ya miradi ya umeme nchini ili kuharakisha utekelezaji wake.

“EWURA na TANESCO fanyeni kazi kwa pamoja ili miradi iende kwa kasi; tulipende Taifa letu na tufanye maamuzi kwa maslahi ya Taifa. Kaeni pamoja mjadiliane na sio kila mmoja kivyake,” alisisitiza.

Alisema kuwa Serikali haitokubali miradi ikwame kwa uzembe na hivyo aliagiza hadi kufikia tarehe 15 mwezi Machi mwaka huu majadiliano kuhusu miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme yawe yamekamilika. “Na ndani ya miezi mitatu ijayo lazima miradi mipya ya kuzalisha umeme iwe imejulikana na kuanza kutekelezwa,” alisema.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti wa Kampuni ya Mkonge Energy Systems (MeS), Salum Shamte alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 2008 baada ya Serikali kutangaza kuwa kampuni binafsi nazo zinaruhusiwa kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO.

Alisema awali kampuni hiyo ilikuwa inazalisha umeme wa maji kiasi cha kilowati 300 kwa matumizi yake ya kiwanda cha Mkonge na kufuatia tangazo hilo la Serikali, ndipo kampuni tanzu ya MeS ikaanzishwa.

Alisema kuwa tayari upembuzi yakinifu umekamilika na kwamba kupitia mradi huo wa Masigira, kampuni tanzu ya TMPL itajenga njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 33 ya kilomita 14 kutoka Mahanje hadi Madaba ambapo kutakuwa na kituo cha kupoozea umeme.

Aidha, mbali na mradi wa Masigira, Shamte alieleza kuwa wanayo miradi mingine midogo ya kuzalisha umeme ambayo ni mradi wa Kiwira wa Megawati 43.2 uliopo wilayani Tukuyu, Mkoani Mbeya ulio chini ya kampuni tanzu ya Kiwira Energy Limited (KEL) ya ubia wa MeS na kampuni ya Frontier Investment Management ya Denmark. 

Mradi mwingine ambao Shamte aliuzungumzia katika kikao hicho ni mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia mabaki ya mkonge kiasi cha megawati 11.2 ambao alisema upo chini ya kampuni mama ya MeS.


Mkutano huo ni moja kati ya mikutano inayoendelea kwa wiki hii baina ya Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake pamoja na wawekezaji lengo likiwa ni kuwawezesha kupata maelezo ya kina kuhusu fursa zilizopo nchini na pia kuiwezesha Wizara kupata maelezo kutoka kwa Wawekezaji hao kuhusu uwezo wao wa kutekeleza miradi wanayokusudia.

DC WA HAI,ANTHONY MTAKA AMALIZA MGOGORO WA MAJI KATI YA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA) NA WANANCHI KATIKA KIJIJI CHA SHIRI NJORO.

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akiongozana na baadhi ya wanakijiji cha Shiri Njoro wakitembelea chanzo cha maji cha Shiri.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony akiwa na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA pamoja na viongozi wa kijiji cha Shiri Njoro wakifanya maombi kabla ya kufanyika kwa kikao cha usuluhishi.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akimsikiliza mmoja wa viongozi wa kijiji cha Shiri .

DC Mtaka akizungumza jambo mara baada ya kumsikia malalamiko ya wanakijiji hao.


Mkuu wa wilaya akipitia rekodi ya kiwango cha maji ambacho kimekuwa kikirekodiwa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA).
Afisa kutoka bondde la Pangani,Brown Mwangoka akizungumza namna ambavyo mgawanyo wa maji katika chanzo cha Shiri unafanyika.
DC Mtaka akizungumza.
Mwenyekiti wa kijiji cha Shiri Njoro ,Clemence Nkya akimueleza jambo mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Shirimatunda Beda Massawe akizungumza jambo katika kikao hicho.
DC Mtaka akitoa ushauri katika kikao hicho ambacho wakulima walilalamika kupata maji pungufu kwa ajili ya kumwagilia mazao yao.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa MAzingira mjini Moshi,MUWSA Joyce Msiru akimuelekeza afisa uhusiano wa mamlaka hiyo,Flora Nguma kuchukua mambo mbalimbali yaliyotolewa katika kikao hicho.

Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza jambo katika eneo ambalo hugawanya maji kwenda katika mifereji mitatu inayotumiwa na wakulima katika kijiji cha Shiri.
Mwenyekiti wa kijiji cha Shiri Njoro,Clemence Nkya akishauri jambo kwa Mkurugenzi wa MUWSA,Joyce Msiru.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images